Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kilichoendelea Leo Mahakamani Kuhusu Kesi Ya Tundu Lissu Kupinga Kuvuliwa Ubunge

$
0
0
Maombi namba 18/2019 yanayohusu shauri la kupinga kuvuliwa Ubunge Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, yameanza kusikilizwa Alhamis, Agosti 15, 2019 mbele ya Jaji Matupa, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dar es Salaam na kesi imeahirishwa hadi Agosti 23, mwaka huu.

Kupitia mawakili wanaomtetea Mhe. Lissu, wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala akiwa na mawakili wenzake, Freddy Kalonga, Jeremiah Mtobesya na Omary Msemo, upande huo umeiomba Mahakama Kuu

1. Kusimamisha uapishwaji wa mbunge mteule wa jimbo hilo, hadi shauri maombi hayo yatakaposikilizwa na kuamriwa.

2. Wameiomba Mahakama Kuu kulitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwasilisha barua rasmi yenye uamuzi wa Spika wa Bunge kufuta ubunge wa Mhe. Tundu Lissu.

3. Wameiomba Mahakama Kuu kutoa uamuzi haraka kabla mbunge huyo mteule hajaapishwa.

Aidha, upande wa mawakili wa mpeleka maombi, Tundu Lissu ambaye anawakilishwa na Ndugu Allute Mughwai, waliomba ombi la kuhusu kumtaka Spika wa Bunge asimwapishe mbunge mteule wa Jimbo la Singida Mashariki lisikilizwe leo hii.

Upande wa Jamhuri walitaka ombi hilo lisikilizwe wakati wao wakiwa wameshawasilisha majibu yao.

Katika ubishani huo wa kisheria, Jaji Matupa ameamuru yafuatayo:-

a) Maombi yote yatasikilizwa Agosti 23, mwaka huu.
b) Upande wa Jamhuri (wajibu maombi) walete majibu yao Agosti 21, 2019.
c) Upande wa wapeleka maombi walete majibu yao ya nyongeza Agosti 22, 2019.
d) Baada ya usikilizwaji wa Agosti 23, mwaka huu, ndipo uamuzi wa hoja/maombi yote ya wapeleka maombi utakapotolewa.

Jaji Matupa amesema amefanya "consultations" kwamba kabla ya Agosti 23, mwaka huu hakuna kikao cha Bunge na kwamba mbunge huyo mteule hatakuwa ameapishwa katika kipindi hiki.

Upande wa wajibu maombi (Jamhuri) waliongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Vincent Tangoh na mawakili wenzake, Lucas Malunde na Mark Mulwando.

Hivyo Jaji wa Mahakama Kuu Sirilius Matupa ameaihirisha kesi hiyo hadi Agosti 23 mwaka huu.

Wakati huo huo, kesi namba 112/2018 inayowakabili baadhi ya Viongozi Wakuu wa Chama na Wabunge 7 wa Chadema katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyokuwa iendelee leo, imeahirishwa hadi Jumatatu Agosti 19, mwaka huu. Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya Wakili Gaston Garubindi, kutoa taarifa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Simba, kwa niaba ya mawakili wanaowatetea washtakiwa katika shauri hilo kuwa, mawakili hao wako kwenye kesi nyingine mahakama ya juu, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuwakilisha upande wa wapeleka maombi (utetezi) katika maombi namba 18/2019 yanayohusu shauri lililofunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama, Mhe. Tundu Lissu dhidi ya Spika wa Bunge, kupinga kuvuliwa Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki.

Imetolewa leo, Alhamis, Agosti 15, 2019 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema

Okoa Ndoa Yako Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume Na Kisukari

$
0
0
Ni dawa zilizopimwa na mkemia na kupewa no 341/VOL,XV/36 na TFDA no 0127/F/F/1819/ MTINJETINJE ni dawa ya kisukari .....Hurudisha kongosho katika hali ya kawaidi hata kama limefeli haijalishi unatumia vidonge au sindano za insulin, itaifanya sukari kuwa normal

SUPER MAJINJA ni dawa inayotibu nguvu za kiume yani matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo na mwili kuchoka (2)kuwai kufika kabla ya  mwenzi wako (3)maumbile ya kiume kulegea na kusinyaa (4)maumbile ya kiume  kuingia ndani na kuwa mafupi kwa wale walio jichua (5)miuungurumo ya tumbo,ngiri,kukosa choo,kiuno kuuma

ACHA KUONGOPEWA SASA DAWA HIZI NI TOFAUTI NA ULIZOWAI KUTUMIA

NJOO OFISINI KWANGU MBAGALA KARIBU NA BENK YA KCB NA mwanza yupo wakala piga simu ya DR AGU whatsapp 0783185060. 0620113431

Je, Wewe ni Mwathirika wa Kujichua?... Soma Hapa

$
0
0
🔖Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.
------------------
🔖NINI CHANZO CHA HAYO?

📌Kupiga punyeto
,Ngiri,

Vidonda vya tumbo,

📌Korodani moja kuvimba,

📌 Msongo wa mawazo,

📌Presha, Magonjwa ya zinaa,

 📌Kufanyiwa tohara
ukiwa na umri mkubwa,

📌Kisukari.
------------------

💉DR. KHAFIZ Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.na maumbile mafupi
-------------------

💊MUJARABU :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka 
------------------
📌inazalisha homoni kwa mwingi na kuku fanya uwe nambegu nyingi zenye vimeleo vyauzazi vilivo koma
------------------
📌 itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa.
------------------
📌TIBA YA KUDUMU

 -----------------
📌TUMIALEO UWONE MAJABU YAKE

------------------
🌠Pia tunadawa za Kupandisha nyota , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono  na mvuto wa mpenzi.bishara na zindiko
--------------------
 💉DR.KHAFIZ ANAPATIKANA DAR-ES-SALAM SM 0716948950 kwa wale wa mikoani mingine huduma hii utaipata popote ulipo.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  0759208637   /  0620510598

Afrika Kusini Na Tanzania Kuongeza Nguvu Ya Mahusiano

$
0
0
Na Abraham Nyantori-MAELEZO
Wakati vikao tangulizi vya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) vinafikia ukingoni mwishoni mwa wiki na kutoa nafasi kwa Marais wa SADC kukutana katika Mkutano wao wa kilele Agost 17 na 18, wafanyabiashara wa Tanzania na ujumbe wa wafanyabiashara wa Afrika Kusini wamekutana wakiongozwa na Marais wao Cyril Ramaphosa na Dkt. John Magufuli. 

Mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar Es Salaam mbali  na kuwakutanisha sekta binafsi, umewaleta pamoja Mawaziri wa sekta mbalimbali nchini, taasisi za umma na binafsi za Tanzania na Afrika Kusini, ukiwa ni jukwaa la pili kwa nchi hizo kuongea kuhusu fursa za biashara, uwekezaji na ukuzaji wa uchumi kupitia sekta ya viwanda 

Huku kila upande ukionyesha ari ya kuongeza ushirikiano kwa mataifa haya, Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ameeleza mahusiano ya kibiashara baina ya Tanzania na Afrika Kusini, ambapo yanaonekana kukuwa kwa kasi, huku akitolea mfano miradi ya huduma na uuzaji wa bidhaa kwenda Afrika Kusini ulikuwa toka dola za kimarekani 108.2 milioni mwaka 2017 hadi dola 437.2 milioni kwa sasa.  

Rais Magufuli amesema wawekezaji toka Afrika Kusini wamefikia 228 na kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani 806.5 millioni na kushika nafasi ya 13 kwa ukubwa wa uwekezaji, ambapo Tanzania katika nchi za SADC, mahusiano yake kibiashara yako juu na Afrika Kusini ukilinganisha na nchi wanachama. 

Pamoja na Tanzania kujiimarisha katika kuboresha mihimili ya kujenga uchumi kama uboreshaji wa usafiri na usafirishaji; bandari, viwanja vya ndege, barabara na vivutio vya utalii, Dkt Magufuli amesema serikali yake inatambua sekta binafsi katika uwekezaji na hivyo imeboresha sheria mbalimbali na Mamlaka zinazohudumia wawekezaji na wafanyabiashara ili kufanikisha  

Wakati Tanzania inahimiza uwekezaji wa ujenzi wa viwanda nchini kwa wawekezaji wa nje na ndani, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anatambua hatua ambayo nchi yake imefikiwa kiuchumi, lakini anaona ipo haja kwa bara la Afrika kuona jinsi ya kujenga nafasi za kazi na kujenga uchumi wa mataifa hayo kwa maisha ya watu wake. 

Rais Ramaphosa anasisitiza watu wa Tanzania na Afrika Kusini kuendeleza mahusiano yao ya kihistoria kwa nchi zao katika kustawisha uchumi,huku jicho la pili likiangalia dunia kama sehemu ya kutegemeana. 

Pamoja na kuwepo uhusiano wa kihistoria uliotokana najitihada za Tanzania kushirikiana na nchi za Kusini mwa Afrika katika harakati za ukombozi wa Afrika, mahusiano yamekuwa yakipanda kutoka mahusiano ya kisiasa na kuona fursa za uwekezaji katika miradi mbalimbali na biashara baina ya mataifa haya mawili.
Mwisho.

Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa Asisitiza Dhamira ya Dira ya SADC

$
0
0
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.
Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) inatakiwa kukumbuka na kurejea kwenye Dira na Dhima za Jumuiya hiyo ili kuweza kuimarisha, kuongeza na kuwezesha ushirikiano wa nchi za kusini mwa Afrika kuwa katika lengo moja na  kusonga. 

Hayo yalisemwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa alipokuwa akizungumza leo katika mhadhara wa wajumbe na viongozi wa SADC katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.  

Rais Mkapa alisema kuwa katika kujenga uchumi ulioimara nchi hizo zinatakiwa kukumbuka Dira na Dhima ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ya nchi za Kusini mwa Afrika ili kuweza kuimarisha uchumi ulioendelevu; wenye kuwezesha wananchi kutoka nchi wanachma kuwa na maisha bora. 

“Naamini kuwa SADC imeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye muundo wa Maendeleo ya Bara la Afrika, na suala hili linapaswa kutangazwa ili ushirikiano huu uendelee kwa wananchi wanachama wa SADC, lakini haya yote yamesababishwa na kuwa na Dira na Dhima ambayo inaruhusu nchi hizi kuwaza na kutekeleza mawazo yao pamoja”, alisema Mkapa. 

Kiongozi huyo Mstaafu alisema kuwa SADC inatakiwa kukumbuka Dira ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ambayo ni kuunganisha na kuhusianisha Utumiaji wa rasrimali zilizoko nchi wanachama ili kuwezesha nchi hizo kujitegemea na kuimarisha uchumi wake pamoja na maisha ya watu wake. 

Mkapa alifafanua kuwa Dira hiyo inapaswa kutekelezwa huku nchi wanachama wakikumbuka waasisi wa SADC akiwemo Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere kuwa ilikuwa ni kuungana nakufanya kazi kwa pamoja ili kulinda rasrimali na kuwezesha wananchi kujitegemea kwa kuisha maisha yaliyobora. 

Aidha, Mkapa alisema kuwa SADC ina dhima kubwa ya kuendeleza uchumi endelevu na ulio sawa kwa nchi wanachama kupitia mifumo mizuri, utawala bora na kuongeza ushirikiano wa nchi hizo, na vitu hivyo vitawezesha upatikanaji wa amani na usalama kwa nchi wanachama pamoja na ujenzi wa miradi mbalimbali ya ushirikiano. 

“Dira ya SADC ni moja na nguzo muhimu katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ikiwemo miradi ya Nishati, Miundombinu ya usafarishaji na ujenzi wa viwanda hii yote ni utekelezaji wa kuifanya SADC kuwa katika uchumi ulio sawa ukanda huu wa nchi za kusini mwa Afrika”, alisema  

Aliongeza kuwa Miundombinu ya nchi za Afrika inatakiwa kuimarishwa kama mkakati wa nchi za SADC unavyoeleza, kwa sasa SADC inatakiwa ijikite katika ujenzi wa Viwanda na Nishati  ambapo vitu hivyo  vikitekelezwa SADC itasonga mbele. 

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Namibia, Natumbo Nandi Ndaitwah, alisema kuwa Jumuiya ya SADC inapaswa kuzingatia kumbukumbu ya kuasisiwa kwake ili kuweza kusonga mbele katika mashirikiano ya pamoja kwa nchi hizi. 

Waziri Ndaitwah alisema kuwa kumbukumbu ya Waasisi wa SADC itakumbukwa milele huku akiitaja Tanzania kuwa ni moja ya Taifa ambalo limeweza kusaidiwa kwa kiasi kikubwa katika ukombozi wa Afrika na kundwa kwa jumuiya hiyo. 

“Nchi wanachama wa SADC tunapaswa kujua kuwa Tanzania ni taifa ambalo limewezesha  kwa kiasi kikubwa kuzaliwa kwa Jumuiya hii, kwani Mwl. Nyerere aliwezesha nchi nyingi za upande wa Kusini mwa Afrika kukombolewa na alikuja na wazo la kuunda Jumuiya ya SADC ili nchi za kusini zipate kufanya kazi pamoja na kuimarisha maisha ya watu wao”, Naibu Waziri Mkuu, Ndaitwah. 

Waziri Ndaitwa alisema kuwa Mwl.Nyerere ni mfano wa kuigwa kwa nchi wanachama wa SADC na anapaswa kubaki katika kumbukumbu ili vizazi vijavyo viweze kukumbuka kuwa kuna Mwanzilishi na mkombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika. 

“Namshukuru Baba wa Taifa, Mwl.Julius Nyerere, aliyetangaza kuwa, Tanzania haiwezi kuwa huru kama Bara la Afrika halijakombolewa, nayasema haya ili tujue tulikotoka na nani alifanya kitu gani ili tuweze kusonga mbele katika Jumuiya hii ya Nchi za Kusini mwa Afrika”, Naibu Waziri Mkuu, Ndaitwah.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi 15 August

Rais Cyril Ramaphosa Wa Afrika Kusini Alivyowasili Nchini Kwa Ziara Rasmi Ya Siku Mbili

$
0
0
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameingia nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo Alhamisi Agosti 15,2019 kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, John Magufuli.

Ziara hiyo itawawezesha viongozi hao kujadili mambo yanayohusu nchi hizo, Bara la Afrika na mambo ya kimataifa na kujihakikishia wajibu wao katika ushirikiano wa karibu.

Ziara hiyo inakuja zikiwa zimebaki mbili kuelekea mkutano wa kawaida wa 39 wa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 17 na 18, 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Leo Alhamisi Agosti 15, 2019 saa 2: 00 atafanya mazungumzo Ikulu ya Dar es Salaam na mwenyeji wake Rais Magufuli na saa 5 hadi 8 mchana atakuwa ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kwenye Jukwaa la Biashara.

Ijumaa ya Agosti 16, 2019 saa 3 asubuhi, Rais Ramaphosa atatembelea kambi ya wapigania uhuru Mazimbu mkoani Morogoro.


Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusine akipokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini kwa Afrika SADC
 

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa 16 August

Waziri Jafo Aingilia Kati sakata la watumishi wa Hospitali kulipishwa mashine ya Ultrasound iliyoibiwa

$
0
0
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo ameingilia kata sakata la watumishi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi  na kuamruru wasichangishwe fedha kufidia mashine ya Ultrasound iliyoibwa hospitalini hapo.

Jafo ametoa kauli hiyo jana Alhamisi Agosti 15, kauli ambayo inamuunga mkono Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini ya kutaka watumishi hao wasilipishwe fedha kama walioamriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga  Jumatano Agosti 14.

Pamoja na mambo mengine, Jafo amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka kuunda tume ya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na wizi wa mashine hiyo.

“Kulikuwa na maelekezo kuwa wale watumishi 137 walipie ile mashine kwa kukatwa kwenye mshahara yao, nielekeze kwamba watumishi wetu hawa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, na tukumbuke hata tulipopata janga pale Morogoro watumishi wetu wa idara ya afya muda mwingi ndiyo walikuwa kimbilio kuwasaidia wananchi.

“Kitendo kama hiki ni kuwakatisha tamaa na kuwaweka katika ya sintofahamu lakini kumbe inawezekana kuna watu walihusika. Lengo hapa ni kuwatafuta waliohusika, wabainishwe ni kina nani wachukuliwe hatua lakini pia wahakikishe mashine hii inarudi.

“Kwa hiyo nitoe maelekezo kuwa watumishi hawa wasichangishwe fedha ya aina yoyote kwa sababu siyo jukumu lao, ni jukumu la ulinzi kwa hiyo Mkuu wa Mkoa namuelekeza kwanza aunde tume ya uchunguzi kuwabaini wahusika na watumishi hao waachwe wafanye kazi kwa sababu tunawategemea sana haipaswi kuwabebesha mzigo usiowahusu,” amesema Jafo.

Mashine hiyo inadaiwa kuibiwa pamoja na kifaa chake cha kudurufu picha (printer) ambapo ilikua maalumu kwa matumizi ya wodi mpya ya akina Mama wajawazito na iliibiwa ikiwa katika wodi hiyo.

Ajali ya Basi na Lori Yaua Watu Wanne Morogoro

$
0
0
Watu 4 wamefariki dunia na wengine 26,  wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyohusha basi la abiria na Lori  kugongana uso kwa uso katika eneo la nanenane Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo imehusisha basi la abiria lenye namba za usajili T212 DNU na Lori.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa,Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi ambaye alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua taadhari.

"Ni kweli usiku wa kuamkia leo Ijumaa August 16, saa saba na nusu usiku imetokea ajali eneo la Nanenane, Morogoro, basi mali ya kampuni ya Safari Njema ambayo ilikuwa inatokea DSM kwenda Dodoma imegongana kwa ubavu na lori mali ya Tumbaku Alliance, watu 4 wamefariki.

"Ingawa watu 4 wamefariki ila abiria wengine waliokuwa kwenye basi walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Morogoro sababu ya mshtuko na wengi wametibiwa na kuruhusiwa, wamebakia abiria 3 wanaendelea na matibabu, dereva wa lori ni miongoni mwa waliofariki.

"Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye aliovertake pasipo kuchukua tahadhari na kukutana na gari nyingine mbele kisha ajali ikatokea, dereva wa basi ametoweka na tunamtafuta, kama hatopatikana tutamkamata mmiliki wa basi ili atuoneshe dereva alipo". Amesema Mutafungwa

Tanzia: Mwanamuziki Mbalamwezi wa Kundi la The Mafik Afariki Dunia

$
0
0
Mwanamuziki Mbalamwezi ambaye ni mmoja wa Wasanii  wanaounda kundi la The Mafik amefariki dunia kutokana na majeraha ambayo yanahusishwa na kupigwa.

Baadhi ya ndugu wamesema taarifa za awali ni kwamba Mwili wake ulikutwa maeneo ya Africana Dar es salaam ukiwa hauna nguo ikiwa ni saa kadhaa zimepita toka msanii huyo atokomee bila kujulikana alipo. 

Msanii huyo ameshiriki katika kazi za kundi ambazo zimefanya vizuri kama Passenger, Sheba,Carola, Vuruga, na Dodo, pia ameshirikishwa katika nyimbo za Ruby na Ben Pol.


LIVE Kutoka Morogoro: Ziara Ya Rais Wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa....Tazama Hapa

$
0
0
Live Kutoka Morogoro: Ziara Ya Rais Wa Afrika Kusini  Mhe. Cyril Ramaphosa....Tazama Hapa

Mabalozi 42 watembelea mradi wa SGR.....Dr Wilibrod Slaa Ammwagia Sifa Rais Magufuli

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amewataka mabalozi wa Tanzania kushirikiana na shirika hilo ili kuweza kuleta maendeleo ya mradi inayoendelea hapa nchini na pia kulitangaza taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Mabalozi hao waliotembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge(SGR) unaendelea, Kadogosa amesema kuwa mpaka sasa ujenzi umefika asilimia 60.4 hivyo amewashukuru mabalozi waliokuja kuangalia mradi wa kimkakati kwani kutawawezesha kulitangaza taifa kwa mazuri yanayoendelea.

“Kama tunaweza kutekeleza miradi hii kwa pesa yetu, watu wa nje wanatuheshimu kwahiyo uwekezaji mkubwa kama huu unawagusa wawekezaji wa nje kwahiyo sisi tunawashukuru mabalozi kuja kuangalia miradi hii hivyo watakaporudi huko watawaelezea watu wa huko miradi hii walioyoiona kwa ukubwa wake,”amesema Kadogosa.

Aidha, Kadogosa amesema kuwa gharama za kutengeneza fensi katika ujenzi wa reli hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ni dola bilioni 1.2 kujumlisha na kodi na kutoka Morogoro kwenda Maktupola Singida ni dola bilioni 1.9 pamoja na kodi hivyo jumla ya gharama zitakazotumika ni takribani bilioni 3.1.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Swedeni, Wilibrod Slaa amewataka watanzania waweze kujivunia kumpata Rais mwenye kufanya maamuzi kwani wameona miradi mingi ikifanyika hapa nchini kwani hata nchi zilizoendelea wamekuwa wakifanya uwekezaji na ulipaji kodi ambazo zinasaidia kuibua miradi mbalimbali.

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Yatakiwa Kuwezesha Kampuni Nyingi Kuorodheshwa Soko La Hisa

$
0
0
 Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam
Serikali imeitaka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuhakikisha Kampuni nyingi zinaorodheshwa katika Soko la hisa ili kuweka uwazi zaidi katika utendaji wa kampuni hizo na hivyo kuwezesha Serikali kukusanya kodi stahiki na kuchangia katika ongezeko la mapato ya Serikali.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, alipofanya ziara katika Mamlaka hiyo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Dkt. Kazungu, alisema kuwa CMSA iendelee kusimamia masoko ya Mitaji ya Dhamana kwa kuorodhesha Kampuni nyingi zaidi katika soko hilo la hisa kwa kuzingatia masharti ya kuorodheshwa kampuni ili kuongeza uwazi, utawala bora na ufanisi wa kampuni hizo kwa kuweka mazingira mazuri ya uendeshaji na uwazi wa hesabu zao, hatua itakayochangia kukuza uwekezaji na mapato ya Serikali hususani katika eneo la kodi.

“Muendelee na kasi ya kutoa elimu kwa wananchi wengi ili waweze kujiunga na Masoko ya Hisa hususani kwa wananchi walio katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”, alieleza Dkt. Kazungu.

Alisema kuwa iwapo wananchi wengi watajiunga katika Masoko la Hisa kutawafanya kuongeza mapato yao lakini pia kushiriki katika umiliki wa uchumi wa nchi yao.

Dkt. Kazungu alisema kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa uchumi wa viwanda, uchumi unaotarajiwa kujengwa katika kipindi kifupi wakati wa kuelekea katika uchumi wa kati hivyo ni vema wawekezaji wakahimizwa kupata mitaji ya kuendeleza na kupanua uwekezaji kupitia masoko ya mitaji na kutoa fursa nyingi za uwekezaji kwa wananchi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Nicodemus Mkama, amesema Mamlaka yake imeweka mkakati wa kutoa elimu kwa umma na wawekezaji mbalimbali jinsi ya kutumia masoko ya mitaji kupata fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo.

“CMSA inaendelea kutoa elimu kwa umma na kwa makundi mbali mbali ya wanataaluma, wanafunzi wa elimu ya juu, watunga sera ikijumuisha Kamati za Bunge. Elimu hii inalenga kuelimisha umuhimu na fursa ya masoko ya mitaji katika kukuza uchumi na ushirikishwaji wa wananchi katika Sekta ya Fedha hususani masoko ya mitaji” alifafanua Bw. Mkama.

Alisema kutokana na jitihada hizo, kwa sasa uhitaji katika uwekezaji katika Soko ni mkubwa, hii inawafanya kuongeza bidhaa zinazokidhi matakwa ya wawekezaji ndani na nje ya nchi.

“Hii imejidhihirisha hivi karibuni kwa kuongezeka kwa kampuni nyingi katika sekta ya fedha kuorodhesha hatifungani ikiwa ni njia sahihi ya taasisi hizo kupata fedha za mahitaji mbalimbali ya utoaji mikopo na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Alisema elimu hiyo pia imeleta matokeo chanya na mwitikio wa matoleo ya hatifungani za Kampuni ya Kuendeleza Sekta ya Nyumba – TMRC, Benki ya Biashara ya DCB na Benki ya Biashara ya NMB na unaonyesha wazi kuwa kuna ongezeko kubwa la uelewa wa wananchi kushiriki katika uwekezaji kwenye masoko ya mitaji.

Toleo la hatifungani ya NMB Bank limeweka historia kubwa katika maendeleo ya masoko ya mitaji hapa nchini kwa kupata kiwango cha shilingi bilioni 83.3, ikiwa ni mafanikio ya asilimia 333 ikilinganishwa na shilingi bilioni 25 zilizotarajiwa kukusanywa.

Bw. Mkama alisema kuwa mauzo hayo yamekuwa na idadi na thamani kubwa kuliko mauzo yote ya hatifungani yaliyowahi kufanyika hapa nchini, ambapo jumla ya wawekezaji 2,264 wameweza kushiriki. Kati ya wawekezaji hao, asilimia 99.5 ni wawekezaji wadogo wadogo, na wawekezaji Kampuni ni asilimia 0.5.

“Tumeshatoa maelekezo kwa watendaji na washiriki (wanaotoa dhamana) katika Masoko ya Mitaji kuhakikisha wanakuja na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wawekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi watakao sababisha ongezeko la mapato yao na upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo jambo litakalochangia kushiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi”, alieleza Bw. Mkama.

Alisema kuwa katika utoaji wa elimu, CMSA inatumia mbinu mbalimbali za kibunifu ikiwa ni pamoja na kuweka mashindano kwenye Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania Bara na Visiwani kwa kuwezesha wanafunzi kujifunza elimu ya masoko ya mitaji kwa njia ya kujibu maswali na kuandika insha

Alibainisha kuwa, wanafunzi wanaofanikiwa kushinda nafasi ya kwanza hadi ya tatu wanapewa tuzo mbalimbali zikiwemo fedha taslimu kuanzia shilingi milioni moja hadi milioni 1.8 kama kivutio cha ushiriki huku wanafunzi walioshika nafasi 20 za juu wanazawadiwa shilingi laki 2 kila mmoja na kwamba washindi wa nafasi ya kwanza hadi ya tatu wa mwaka huu (2019) watapelekwa nchini Namibia kwa ziara ya mafunzo.

PICHA: Rais wa Shelisheli Danny Faure Awasili Nchini kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 39 wa SADC

$
0
0
Rais wa Shelisheli Danny Faure, amefika nchini na kupokelewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 39 wa SADC utakaofanyika kesho.

Rais Faure ni Rais wa pili kuja nchini baada ya kutanguliwa na Rais wa Afrika Kusini

#Kimataifa: Urusi kuchukua hatua kukabiliana na tishio linalotokana na Marekani kujitoa kwenye mkataba wa makombora ya masafa ya kati

$
0
0
Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema nchi yake itatumia makombora ya aina kadhaa kukabiliana na tishio linalotokana na Marekani kujitoa kwenye mkataba wa makombora ya masafa ya kati.

Rais Putin amesema hayo kwenye mkutano na wajumbe kadhaa wa kudumu wa baraza la usalama la shirikisho la Urusi, huku akisema Marekani imejitoa katika mkataba huo kwa kisingizio cha kufikiria na kuvunja mkataba huo wa kimsingi katika sekta ya udhibiti wa silaha. 

Hatua hiyo imeifanya hali ya dunia kuwa na utata zaidi na kuleta hatari kubwa kwa pande mbalimbali. Amesema Marekani inawajibika na hali hiyo.

Rais huyo ameamuru wizara ya ulinzi, wizara ya mambo ya nje na idara ya ujasusi kufuatilia hatua za Marekani katika utafiti, utengenezaji na upangaji wa makombora ya masafa ya kati na mafupi, na Urusi  itachukua hatua sawa kujibu hatua za Marekani.

#Kimataifa: Israel yawazuia wabunge wa kiislamu wa Marekani kuingia nchini humo

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Israel imetangaza kuwa waziri mkuu Bw. Benjamin Netanyahu amewazuia wabunge wanawake wawili wa kwanza wa kiislamu kuchaguliwa kuwa wabunge wa Marekani, Rashida Tlaib na Ilhan Omar, kuingia nchini mwake kwa madai kuwa wanapambana na Israel.

Uamuzi huo umekuja saa chache baada ya Rais Donald Trump kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Omar na Tlaib wanaichukia Israel na Wayahudi. 

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Bibi Nancy Pelosi amekosoa vikali hatua hiyo na kusema imeonyesha dalili ya udhaifu na kupunguza uadilifu wa Israel.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, viongozi hao wawili walikuwa na ziara ya kikazi Jumapili hii, ambayo pia ingelijumuisha wao kufika eneo tata la Temple Mount mjini Jerusalem, linalotambuliwa na Waislamu kama Haram al-Sharif.

Pia walikuwa na mpango wa kukutana na wanaharakati wa amani wa Israel na Palestina na kusafiri hadi ukingo wa Magharibi wa Jerusalem katika miji ya Bethlehem, Ramallah na Hebron.

Polisi Wazuia mkutano wa Zitto Kabwe....Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT- Wazalendo Achukuliwa Kwa Mahojiano

$
0
0
Katibu wa  Itikadi na Uenezi wa ACT- Wazalendo, Ado Shaibu  amechukuliwa  na Jeshi la Polisi kwa Mahojiano  alipokuwa katika Makao Makuu ya chama hicho, Kijitonyama jijini Dar es salaam  akiandaa mkutano wa kiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa ajili ya kuzungumza na waandishi habari.

Jeshi la Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam lilifika katika makao makuu ya chama hicho  na kuzuia  mkutano  huo ambao ulitarajiwa kufanyika leo Ijumaa Agosti 16,2019 saa 5 asubuhi.

Polisi waliwasili Makao Makuu ya chama hicho  na kumhitaji kiongozi yoyote wa chama baada ya kumkosa Zitto Kabwe.

"Ndugu waandishi huu mkutano usubiri kwanza, kwa hiyo ninawaomba mtawanyike mara moja," alisema askari mmoja.

Wakati waandishi wakitawanyika aliwasili Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu ambaye walimchukua  na kuondoka  naye kwa ajili ya mahojiano.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kuanza Kwa Vikao Vya Kamati Za Bunge

$
0
0
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kuanza vikao vya kamati za kudumu siku ya Jumatatu tarehe 19 Agosti hadi tarehe 02 Septemba 2019, Jijini Dodoma, kabla ya kuanza kwa mkutano wa kumi na sita wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 3 Septemba 2019.

Taarifa iliyotolewa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Bunge leo Ijumaa 16 septemba 2019 imesema pamoja na mambo mengine kamati tisa za sekta na kamati ya bajeti zitachambua taarifa za taasisi na wizara za Serikali kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali.

Mbali na kupokea taarifa mbalimbali za wizara/taasisi, kamati hizo zitachambua taarifa ya CAG.

Shughuli nyingine zitakazofanywa na kamati hizo ni pamoja na uchambuzi wa sheria ndogo, pamoja na uchambuzi wa taarifa za uwekezaji wa mitaji ya umma.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images