Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Waislamu Shinyanga washerehekea Eid Elhaj kwa kuwaombea Dua watu waliofariki dunia katika ajali ya moto mkoani Morogoro.

$
0
0
NA SALVATORY NTANDU
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamesherehekea sikukuu ya Eid Alhaj kwa kuwaombea watu wote walipoteza maisha na majeruhi katika ajali ya moto iliyohusisha lori la mafuta iliyotokea  agosti 10 mwaka huu mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 60.
                        
Swala hiyo imeongozwa na   mwakilishi wa jumuiya ya kisilamu ya Istiqama international wilayani humo Shekhe Ahmad Haroun Alnoob na kusema kuwa   taifa bado linaendelea kuomboleza vifo vya watanzania wenzetu ambao wamefariki dunia kutokana ajali hivyo ni budi kuendelea kuwaombea ili mwenyezi mungu ili awapunguzie adhabu ya kaburi.

Ametoa rai kwa  waumini wa kiisilamu  ambao wamejaliwa  nafasi kuendelea kuwapatia misaada mbalimbali majeruhi wa ajali hiyo ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili na ya mkoa wa morogoro ili kuwatia moyo waweze kupona haraka.

“Waisilamu tujifunze kwa tukio lililotokea mjini morogoro,ndugu zetu walitamani kula sikuuu ya Eid pamoja nasi lakini hawakuweza kutokana na ajari iliyokea,tukumbuke kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria  tunapoona gari la mafuta limeanguka nasio kuwaacha wananchi wakijichotea mafuta”Alisema Haroon.

Katika hatua nyingine Haroon amewataka waumini hao kuiombea nchi amani pamoja na viongozi wake akiwemo Rais Dk John Pombe Magufuli sanjari na kusherehekea sikukuu hiyo kwa amani kwa kuwatendea matendo mema ndugu jamaa na marafiki ambao wanauhitaji pamoja na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kumchukiza mwenyezi Mungu.

Ashura Hamisi na  Hawa Kasimu, ni miongoni mwa waumuni wa dini ya kiislamu wamewataka vijana kuacha mara moja tabia ya kuyavamia magari ya mafuta yaliyoanguka na kujichotea mafuta ili kuweza kuepukana na vifo visivyo vya lazima na badala yake wafanye kazi halali zitakazowaingizia kipato.

Katika siku kuu ya Eid  alhaj imeenda sambamba na Jumuiya hiyo ya kiislam ya Istiqmaa internation kutoa  mifungo mbalimbali zaidi ya 100 kwaajili ya kuchinjwa na kugawiwa waumini na watu wengine ambao waliswali siku kuu hiyo katika Msikiti wa Alwahab uliopo katika mtaa wa nyasubi.

Biteko:Siwezi kuwa na amani moyoni huku mnalia

$
0
0
Na Issa Mtuwa “WM” Nanyumbu Mtwara
Sikuzote katika sehemu ya maisha yangu nikiwa kama Waziri wa Madini, hakuna kitu kinachonisononesha na kunikosesha amani moyoni kama ninapofika mahali au kuona kwenye vyombo vya habari wananchi tena wanyonge wanalia na kunyanyasika kisa wanakosa  maeneo ya kuchimba, wanalilia leseni ama mwekezaji wana wanyanyasa wakati rasilimali hizo zinawazunguka kwenye maeneo yao. 



Haya yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko tarehe 12/08/2019 wakati akiongea na wananchi wa kata ya Michiga wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kufuatia ziara yake wilayani humo kukagua shuguli mbalimbali za sekta ya madini na kutatua wananchi wanamlilia na kumpigia magoti kuomba eneo baba chondechonde tunaomba tusaidie eneo lile tuchimbe. 


Katika ziara yake katika mikoa ya Lindi na Mtwara Biteko amekutana na kilio cha wananchi karibu kila mahali kukosa maeneo ya kuchimba madini huku raslimali hizo zikiwa zimewazunguka. 


“Mhe. Waziri kuja kwako leo tunakushukuru sana, Babaa kiliochetu sisi ni eneo la kuchimba baba tafadhali chondee tunaomba turuhusu tukachimbe, tupate riziki babaaaa, pale palipo fungiwa hata sisi tunaathirika kwa sababu palikuwa panatusaidia” alisema Mzee Faya Bozani Mussa  alipopata fursa ya kuongea mbele ya waziri Biteko. 


Kufuatia kilio hicho akiwaangalia kwa huruma na kwa kuonyesha kuguswa na wananchi hao waziri Biteko papo hapo hakutaka kuwa chukuwa muda kutatua kero hiyo alitoa kauli na iliyo geuza huzuni kuwa furaha ya wananchi walio kusanyika kwa wingi katani hapo. 


“Ndugu zangu, poleni sana, naumia sana moyoni kuwaona mnasononeka moyoni kwa ajili ya raslimali zinazo wazunguka. Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anawapenda sana na mimi ameniteuwa kumsaidia lakini kazi yangu aliyo nituma ni kuja kutatua kero za wananchi katika sekta ya madini na ndio maana nipo hapa Michiga siku ya leo.”  


“Mimi ni mtumishi wenu, nipo hapa kuwatumikia sipo teyari kuondoka hapa huku bado machozi yakiwa yanaendelea kutiririka. Sasa nisikilizeni. Moja, naagiza Tume ya Madini ifikapo ijumaa ijayo tarehe 16/08/2019 leseni ya lile eneo iwe imeshafika kwa Mkuu wa Wilaya ili yeye na afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mtwara waje wakabidhi hiyo leseni. Pili, safari yangu nimeambatana na Mkurugenzi Ukaguzi Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga yule pale, yeye atabaki hapa hataondoka japo kesho ilibidi aondoke kwa ajili ya majukumu mengine lakini hataondoka ili yule mwekezaji wenu Arafati Mrope  amsaidie kuandaa mpango kazi wa lile eneo ili ikifika leseni kazi ianze. Dkt. Utabaki hapaa” alisema Biteko. 


Maelezo hayo yaliibua shangwe, vigelegele, nderemo na vifijo kwa Wanamichiga na kusahau kilio chao. 


Kufuatia kauli hiyoo Mwenye (Chief) Njawala alisimama na kuishukuru serikali na kuipongeza huku akisema kauli ya waziri imeondoa minong’ono iliyokuwa imetanda ikiwatuhumu viongozi wa ngazi mbalimbali kuwa ndio waliokuwa wanawazuia wasichimbe wakati taratibu za kuchimba zilikuwa hazijazingatiwa. 


“Mhe. Waziri Mimi ni Chief wa eneo hili, nakushukuru kwa kutatua tatizo hili na umeleta amani maana awali viongi mbalimbali ndio walio kuwa wanatuhumiwa kwamba ndio wanaozuia, binafsi nakushukuru sana” alisema Chief Njalawa. 


Eneo  Michiga limezungukwa na madini ya Chuma eneo ambalo lilikuwa limechukuliwa na mwekezaji Arafati Omari Mrope aliekuwa anachimba na kununua madini hayo kutoka kwa wananchi na baadae eneo hilo kuzuiwa na serikali kwa kuwa waliokuwa wanafanya shuguli hizo walikuwa wanafanya kinyume cha sheria. 


Kwa upande mwingine Waziri Biteko alimshukuru na kumpongeza mwekezaji Arafati kwa kwa utii kwa serikali kwani hata alipo simamishwa asiendelee na kazi ya uchimbaji wa madini hayo mpaka afuate utaratibu kwa maana apate leseni alikubali na hakuendelea huku akilipa madeni ya zaidi ya Tsh. 35,000,000/= kwa wananchi waliokuwa wanachimba mchanga wa madini ya Chuma na kumuuzia mwekezaji huyooo. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali alimshukuru Waziri wa Madini Doto Biteko kwa kufanya ziara hiyo na kutatua kero hiyo papo hapo bila kusubiri. 

“Mhe. Waziri nakushukuru sana kwa ujio wako, na maamuzi ya papo kwa papo na hiyo ndio speed ya serikali ya awamu ya tano katika kutaatua kero za wananchi hasa katika kufanyaa maamuzi yanayogusa maisha ya wananchi  wetu moja kwa moja” alise Machali. 

Kabla ya mkutano huo Biteko alikutana na kufanya kikao cha ndani na viongozi wa Wilaya ya Nanyumbu wakiongozwa na mkuu wa wilaya Moses Machali ambapo alisomewa taarifa ya wilaya kuhusu hali ya sekta ya madini.

Sadc Yapania Kuimarisha Miundombinu Ya Usafirishaji

$
0
0
Na.Paschal Dotto-MAELEZO
SEKRITARIETI ya Miundombinu ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) inajikita katika kuimarisha na kuboresha miundombinu ya usafirishaji kwa kufanya ukarabari na kuhuisha sekta hiyo hususani sekta ya Bandari, Reli na Anga. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Wa Sekritarieti ya SADC Miundombinu Bi.Rosemary Makoena amesema kuwa hakuna Maendeleo pasipokuwa na uimarishwaji wa sekta hiyo, ili kuhakikisha kuwa nchi wanachama wanaunganishwa na sekta hiyo kufanya biashara katika ukanda wao. 

Ameongeza kuwa Miundombinu unayopigiwa chapuo kwenye utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka 5 ni pamoja na Miundombinu ya Usafirishaji ambayo imebeba dhamira kubwa kwenye kuimarisha mawasiliano ya kibiashara baina ya nchi wanachama. 

“Katika Mpango Mkakati wa 2015-2020 kwa nchi wanachama wa SADC tunaangalia zaidi kwenye utekelezaji na uangalizi wa miradi ya uimarishwaji wa miundombinu ya kusafirisha bidhaa.Mpango mkakati huo unalenga kuimarisha Sera mbalimbali ikiwemo ile ya uendelezwaji na ukarabati wa Bandari (SADC Corridors  of 2008) ya ukanda wetu wa kusini mwa Afrika”, Amesema Makoena. 

Aidha, mpango huo wa SADC unalenga zaidi kwenye kusaini, kutekeleza na kuendeleza Sheria itakayozileta pamoja nchi wanachama katika kuendeleza sehemu za lango la usafirishaji wa majini. Hii itawezesha wananchi kwenye nchi hizo kufanya biashara kwa urahisi bila vikwazo vyovyote. 

 Akisisitiza jambo hilo  amasema kuwa mpango huo unaendana na makubaliano ya wanachama  walioko katika lango ya bandari mbalimbali zilizoko katika ukanda huo wa kusisni mwa Afrika. Ikianzia bandari ya Mtwara, Dar es Salaam, Trans-Kalahari, Central Beira na Nacala ambapo wanachama wataweke kanuni kulingana na makubaliano yao ya usafirishaji yalifanyika chini ya Memorandum of Unederstanding For South-North amasema Makoena. 

Alisema kuwa katika kuimarisha sekta hiyo ya usafirishaji wa majini, nchi wanachama walioko kwenye lango la bandari wanaweka kanuni, lengo, katiba na namna ya kuungana katika kuendeleza miradi ya ujenzi na ukarabati wa bandari hizo, ili kuboresha na kuhakikishi zinakuwa imara zaidi kwa kupokea mzigo ya kutosha.

“katika kutekeleza na kuhakikisha kuwa sekta hii inaimarika azma kubwa tuliyonayo sisi kama Sekritarieti ya Miundombinu ni kuboresha na kuhuisha sekta hii ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi na uhakika zaidi. Sekritarieti inaendelea na mpango mkakati wa mwaka 2012-2021 na kuungwa mkono na Jumuiya ya Ulaya-EU ambao wako tayari kusaidia kuimarisha miundombinu katika nchi wanachama wa SADC”, Amesema Makoena. 

Katika Mpango mkakati huo Sekritarieti ya Miundombinu inalenga zaidi katika kuimarisha na kuweka kanuni  tisa (9) za pamoja kwa wanachama ikiwemo Udhibiti wa Uendeshaji wa magari ya mizigo barabarani, viwango na vipimo vya magari ya mizigo na mizani ya kupima magari yote, kwani kanuni hizo ni muhimu kwa usalama wa barabara na bidhaa. 

Pia, Machi mwaka 2018 SADC ialisaini makubaliano ya Sheria ya usafirishaji wa kuvuka mipaka miongoni mwa nchi wanachama inayojulikana kama Cross-Border Road Transporter-Regulator Forum (CBRT-RF). Ambayo inafanyakazi pamoja na Transport and Transit Facilitation Program (TTFP) yenye kazi ya kusimamia mambo ya usafirishaji yote hayo ni kuhakikisha Sekta ya usafirishaji inakuwa imara katika Jumuiya hiyo. 

Makoena aliongeza na kusema kuwa sekta ya usafirishaji kwa upande wa Anga inaimarishwa ili kuwezesha kuwepo na  ndege kubwa za mizigo katika ukanda huo wa kusini mwa afrika. Kwani usafiri wa anga ni moja wapo ya kichocheo muhimu katika kutekeleza ujenzi wa viwanda.  

Hivyo, Sekritarieti ya Miundombinu inatekeleza hilo kwa kuanzisha Taasisi ya masuala ya usalama wa usafiri wa Anga (SADC Aviation Safety Organization,SASO) inayoshughilikia masuala ya usafiri wa anga katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. 

Pamoja na hayo, SADC miundombinu inaendelea na utekelezaji wa ukarabati na ujenzi wa Reli katika Nchi wanachama ili kuimarisha na kulinda usalama wa barabara, kwani mizigo mizito itakuwa inasafarishwa kwa njia ya treni na kuepuka uharibu wa barabara. 

Akimalizaia Makoena alisema kuwa katika sekta ya Nishati SADC inajivunia utekelezwaji wa Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mto Rufiji nchini Tanzania,ambapo  wanachama wa SADc watafaidika na umeme  huo. 

“Tunajivunia mradi huu, siyo SADC tu haya Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC, na  tunakubaliana na kumuunga mkono kwa uongozi na mafanikio makubwa kwa Rais wa Sasa wa Tanzania katika utekelezaji wa mradi huo, tunahitaji kufanikisha hili kwa sababu tunahitaji Miundombinu hii. Amesema Makoena

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  0759208637   /  0620510598

Mkutano Wa SADC Ngazi Za Mawaziri Kuendelea Kesho

$
0
0
Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unatarajiwa kuanza kufanyika jumanne ya Agosti 12,2019 ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa ngazi za Mawaziri.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa pikipiki mpya zinazotarajiwa kutumiwa katika mapokezi ya viongozi na wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa SADC unaoendelea Jijini Dar Es Salaam,waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema serikali imekuwa ikiendelea na maandalizi mbalimbali ya mapokezi ya viongozi hao ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri ikiwemo magari na pikipiki achilia mbali hotel watakazofikia viongozi hao.

Aidha Prof. Kabudi kwa niaba ya serikali,ameeleza kuridhishwa na kufurahishwa kwa namna vyombo vya habari Nchini vinavyoripoti kizalendo Mkutano unaoendelea wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jambo ambalo limeongeza uelewa wa wananchi kuhusu SADC na kuvitaka kuendelea kufanya hivyo katika masuala yote yanayohusu maendeleo ya nchi.

Katika tukio jingine Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Denmark Nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet.

Katika mazungumzo yao Prof. kabudi amemkaribisha Balozi huyo mteule nchini na kumhakikishia kuwa Serikali ya Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha katika kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini huku Balozi Mteule Mette Norgaard Dissing-Spandet akiipongeza serikali kwa mageuzi ya haraka inayoyafanya ili kuleta maendeleo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya rushwa na kuongeza uwajibikaji serikalini.

Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini Kutua Dar Jumatano

$
0
0
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuwasili Nchini Jumatano ya August 14 kwa Mwaliko wa Ziara ya kitaifa (State Visit) ya siku mbili ambapo atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Ramaphosa atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere majira ya Saa Tano usiku na baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili ataendelea kubaki Nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkubwa wa Viongozi wa wakuu  wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika SADC.

Aidha RC Makonda amesema Maraisi wa Mataifa mengine wataendelea kuingia Nchini kuanzia Agosti 16, ambapo amewataka wananchi kuwa wakarimu kwa wageni na kutumia vizuri fursa ya ujio wa Viongozi hao

LIVE: Tukio la Utambuzi na Kuaga Waliofariki Morogoro Kwa Ajali ya Moto

$
0
0
LIVE:    Tukio la Utambuzi  na Kuaga  Waliofariki Morogoro Kwa Ajali ya Moto

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  0759208637   /  0620510598

LIVE: Tukio la Utambuzi na Kuaga Waliofariki Morogoro Kwa Ajali ya Moto

$
0
0
LIVE:    Tukio la Utambuzi  na Kuaga  Waliofariki Morogoro Kwa Ajali ya Moto

Kauli 12 Alizozitoa Waziri Mkuu Majaliwa Wakati wa Tukio la Kuwatambua Waliofariki kwa Moto Morogoro

$
0
0
1.Niko mbele yenu kumwakilisha Rais  Magufuli kuungana nanyi siku hii ya huzuni kubwa, Rais alipokea taarifa hii jana. Kwa taarifa mpaka sasa waliofariki ni 69, tumepata taarifa tukiwa hapa mwenzetu 1 aliyebebwa kwa Helikopta amekufa njiani.

2.Rais amepata taarifa hizi kwa masikito makubwa, ameendelea kuwaombea marehemu na majeruhi, amewaomba utulivu ndugu, jamaa, na marafiki mlioguswa na tukio hili, kwa uzito wa jambo hili amelitangazia taifa siku 3 za maombelezo kuanzia jana.

3.Yeye anaugeni mkubwa wa Marais 16 wanaoingia nchini kwa maandalizi ya mkutano wa SADC, kwa hiyo mtambue kwamba uzito wa kuwapokea wenzake pamoja na tatizo hili kubwa na kwa kuwa sisi wasaidizi wake tupo akaamua kunileta kwenu. 

4.Nimepita hapo hali si nzuri ndugu zetu wameungua sana, na iko hatari wengine tusiwafahamu kabisa, lakini hatutawanyima nafasi kuwatambua ndugu zetu, na kwa kuwa tulikuwa nao tangu jana asubuhi, tutawapa nafasi ya kuwatambua.

5.Kama una mashaka kuna ndugu yako humuoni tangu jana, tumekupa nafasi ya kuja kutoa taarifa, na tutakupima DNA, ili kutambua ndugu yake kwa sababu tumechukua vinasaba vya marehemu wote ili kuwatambua.

6.Nitaunda tume ianze kuchunguza kuanzia leo hadi Ijumaa, ichambue vizuri na hata kama mimi nitakuwa sijawajibika wanitaje, baada ya hapo serikali tutajua cha kufanya.

7.Manispaa kuna kitengo cha Fire, japo najua walikuja kwa kuzima, ila je walikuja baada ya muda gani? tumesisitiza umakini na uwajibikaji, nasikia tumeokoa mafuta sasa tumeokoa yakiwa yameisha? nitaunda tume wanijibu haya maswali madogo.

8.Hata kama mimi nimehusika wanitaje tu, hatuwezi likapita hivi. 

9.Ajali za aina hii Tanzania si mara ya kwanza ilitokea Mbeya niwasihi Watanzania ukiona gari limeanguka usilitumie kama fursa, ukawaokee binadamu walio pale. 

10. Je huu muda ambao walikutana hawa ndugu zetu waliotangulia mbele za haki kwa ajili kutoa mafuta, ni nani aliwazuia? mimi ninajua Trafiki huwa wanakuwa na haraka sana, ajali inapotokea, nani alihusika kuwazuia.? 

11.Vyombo vya habari mnaendelea kuhabarisha watanzania, kwenye vyombo vya habari tuelewane jambo moja kuhusu takwimu, jana zilikuwa zinachanganya msiseme suala la takwimu, anaeyeweza kusema ni Mkuu wa Mkoa. 

12.Naogopa msije mkaingia kwenye sheria ya takwimu, kuanzia sasa chukueni za Mkuu wa Mkoa, mlisababisha jana nikazungumza uongo nikiwa na wasomi wa Vyuo Vikuu, nikaona taarifa wako 100 ikaja nyingine 120, na mimi nikataja hiyo idadi.

 

 

 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne August 12

Naibu Waziri Kanyasu Aiagiza TFS Idhibiti Wachimbaji Wadogo Wa Madini Kupanua Maeneo Ya Uchimbaji Katika Shamba La Miti La Biharamulo-Chato

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kupitia Menejimenti ya Shamba la Miti la Biharamulo- Chato mkoani Geita idhibiti upanuzi wa Uchimbaji madini unaofanywa na Wachimbaji wadogo nje ya yale maeneo ambayo yanatambulika kwa shughuli hiyo katika Shamba hilo.

Aidha, Mhe.Kanyasu ameiagiza TFS idhibiti uanzishwaji wa makazi mapya pamoja na ukataji ovyo wa miti unaoendelea hadi pale Kamati ya Mawaziri nane itakapotoa ripoti iliyokuwa imeundwa na Rais John Pombe Magufuli kufuatia maombi yaliyokuwa yamewasilishwa na wilaya ya Chato kupitia Mbunge wao, Dkt. Medard Kalemani ya kuomba ardhi yenye ukubwa wa hekta 25 nje ya hifadhi hiyo ili kuwawezesha Wachimbaji hao kuanzisha makazi yao ya kudumu.

Hatua hiyo inakuja kufuatia uwepo wa leseni saba zilizotolewa na Wizara ya madini na kati ya hizo saba ni leseni moja tu ndo ambayo imeshalipiwa kibali cha kufanya shughuli hiyo ndani ya Shamba hilo

Agizo hilo amelitoa leo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wapatao 2000 katika eneo la Matabe ndani ya Shamba hilo, na kuwataka Wachimbaji hao wafuate sheria na taratibu zinazotakiwa za kuchimba madini ndani ya shamba hilo.

Katika shamba hilo Wachimbaji wadogo wamekutwa wakiendelea kuchimba dhahabu katika eneo la Matabe, Ilyamchele na Nyantimba ambapo wengi wao wakiwa hawana leseni wala kibali cha kuchimba kutoka TFS.

Amewataka Wachimbaji hao wajiunge katika vikundi visivyopungua watu watano ili waweze kukidhi vigezo vya kupewa leseni na badaye
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) itoe kibali cha kuwawezesha kufanya tathmini katika maeneo ya leseni hiyo.

Amesema kitendo cha Wachimbaji hao kukosa vibali vya kuchimba madini ndani yua Shamba hilo kunaikosesha serikali mapato kwa vile hawatambuliki.

Aidha, Mhe.Kanyasu amewaonya wachimbaji hao kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya shughuli za machimbo pasipo kuomba kibali kutoka TFS

” Tutakapokubaini unakata miti kwa ajili ya machimbo tutachukua sheria kali dhidi yako kwa kulipa faini au jela miaka miwili” alilisitiza Kanyasu.

Kwa upande wake Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Madini, Dkt.Medard Kalemani amewaeleza Wachimbaji hao kuwa nia ya serikali sio kutaka kuwafukuza ila inawataka wafuate sheria na taratibu ili waweze kutambulika na serikali

” Serikali inataka ninyi Wachimbaji wadogo mnufaike wakati huo huo Serikali nayo inufaike hivyo lazima mjiunge kwenye vikundi ili mtambulike kisheria.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhandisi.Mtemi Msafiri amewaonya Iponya Nybihabi wanaodai kuwa wao ndo wamiliki wa leseni waache kuwasumbua Wachimbaji wadogo kwani ofisi yake haiwatambui

Kufuatia malalamiko mengi kutoka Wachimbaji wadogo kuwalalamikia Wachimbaji hao Wakubwa, Mkuu wa wilaya hiyo alilazimika kumuamuru Mkuu wa Polisi kuwakamata Wachimbaji hao wakubwa na kisha kuondoka nao.

Naye ,Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo, Emanuel Juang amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa licha ya kusumbuliwa mara kwa mara na Wachimbaji Wakubwa katika eneo la Mataba lakini wapo tayari kufuata sheria na taratibu zinazotakiwa ikiwemo suala kununua miti kwa TFS kwa ajili ya uchimbaji madini.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Aagiza Wanaosambaza picha za marehemu Mitandaoni Wakamatwe

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata wanaosambaza picha za marehemu mitandaoni.

Masauni alitoa kauli hiyo jana mjini Morogoro mara baada ya swala ya Eid iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Mkoa huo.

Kiongozi huyo wa wizara alisema kusambaza mitandaoni picha za marehemu ni kuwadhalilisha wahusika na ni uvunjaji wa sheria za nchi.

"Ninaziagiza mamlaka na vyombo vinavyohusika vihakikishe vinafuatilia na kuchukua hatua kwa wale ambao wanakiuka sheria za nchi yetu kwa kusambaza mitandaoni picha za marehemu," aliagiza.

Masauni alisema siyo vema kuanza kutumia majanga ya kitaifa kama lililotokea Morogoro la watu zaidi ya 70 kufariki dunia ndani ya muda mfupi, kuanza kusambaza picha za waathirika mitandaoni kwa dhamira ya kudhalilisha.

"Watu hawa wamefariki dunia na mtu yeyote katika tukio lile angekufa, mimi au wewe, ndugu yako au jamaa yako, fikiria kama ni jambo limekukuta au ndugu yako halafu ukachukua picha na kuisambaza kwenye mitandao, katika mazingira kama yale," Masauni alisema.

Alisema  kufanya hivyo siyo tu kunavunja sheria za nchi, bali pia ni kinyume cha utamaduni wa Mtanzania.

PICHA: Waziri Kabudi Akabidhiwa Uenyekiti Wa Mawaziri Wa SADC

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo na Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah aliyemaliza muda wake ikiwa ni sehemu ya mkutano huo utakaohitimishwa na wakuu wa nchi wanachama Agosti 17 na 18, 2019.
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah (kulia) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi kijiti cha uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah akimpa maneno ya usia  kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea ngao ikiwa ni ishara ya kuupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea ngao ikiwa ni ishara ya kuupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akitoa hotuba yake mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja.

Takukuru Dodoma Yaokoa Zaidi Ya Tsh.milioni 135

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa[TAKUKURU] mkoa wa Dodoma imeokoa Jumla ya Tsh.Milioni 135,laki 9 ,48 elfu  na mia 193 kwa kipindi cha miezi 6.

Akizungumza na  Mtandao  Wa Mpekuzi Blog Mapema leo Agosti 13,2019  Ofisini  kwake jijini Dodoma,Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Dodoma ,Bw.Sosthenes Kibwengo amesema Fedha hizo zimeokolewa kwa kipindi cha Miezi 6 kuanzia  Mwezi Januari,hadi Juni ,2019.

Bw.Kibwengo amesema kwa kipindi cha miezi sita pia zimedhibibitiwa Jumla ya Tsh.Milioni 322,laki 3 ,48 elfu na mia 989.

Aidha,Bw.Kibwengo amebainisha kuwa katika kipindi hicho cha miezi 6 kuanzia Januari hadi Juni ,2019 TAKUKURU Mkoa wa Dodoma  imepokea jumla ya Malalamiko 231  ya vitendo vya rushwa .

Bw.Kibwengo amesema asilimia 28% ya Malalamiko hayo yanatoka Serikali za mitaa[TAMISEMI],Ardhi kwa asilimia 26.5%,Polisi 7% na mahakama   malalamiko kwa asilimia 6% na asilimia zilizobaki ni kwa sekta nyingine huku akitaja Wilaya iliyo na Malalamiko mengi ni Wilaya ya Dodoma Mjini.

Pia amesema kuanzia mwezi huu wa Agosti ,2019 wanatarajia kufungua ofisi za TAKUKURU Eneo la Chemba huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano na Taasisi hiyo na kuweza kuitumia namba ya bure 113 pindi wanapoona vitendo vya rushwa.

Acacia yaruhusiwa kuendelea kusafirisha Dhahabu kutoka mgodi wa North Mara

$
0
0
Kampuni ya Acacia imeruhusiwa kuendelea na utaratibu wa kusafirisha dhahabu baada ya kuzuiliwa kwa takribani mwezi mmoja na Tume ya Madini Tanzania

Taarifa iliyotolewa na Acacia inaeleza sasa wataanza kusafirisha madini kutoka North Mara baada ya kutimiza masharti

Hata hivyo, Tume ya Madini imesema inaamini baadhi ya vipengele vya kanuni ya madini ya mwaka 2010 vilikiukwa na imewataka kuwasilisha mpango wa uchimbaji na ripoti ya upembuzi yakinifu ifikapo Ijumaa ya wiki hii

Acacia imekuwa kwenye mvutano wa muda mrefu na Serikali baada ya kuzuiwa kusafirisha Makinikia nje ya nchi kwa madai ya kutolipa mrabaha stahiki

Serikali Yaagiza Mashamba Makubwa ya Tumbaku Yapimwe

$
0
0
Serikali  imeuagiza uongozi wa mkoa wa Tabora kuhakikisha mashamba makubwa ya tumbaku yanapimwa.

Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Tabora leo Jumanne Agosti 13, 2019, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, Angelina Mabula amesema kwa kutopimwa mashamba hayo ina maana Serikali  inakosa mapato.
 
Awali, mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amemweleza naibu waziri kuwa migogoro ya ardhi mkoani Tabora imepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na mkoa pamoja na wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya Ardhi kanda ya Magharibi.

Shehena ya malori ya dawa Yatua Muhimbili Kuwasaidia Majeruhi Ajali ya Moto Morogoro

$
0
0
Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi dawa na vifaa tiba kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi wa ajali ya moto waliohamishiwa hospitalini hapo kutoka mkoani Morogoro baada ya Kutokea kwa mlipuko wa mafuta Msamnvu Morogoro. 

Makabidhiano haya ya dawa ni mwitikio wa maombi ya dharura yaliyoombwa na Hospitali Muhimbili kwa ajili na majeruhi hao.

Meneja wa MSD, Kanda ya Dar es Salaam Bw. Celestine Haule amesema mpaka sasa jumla ya shehena ya malori matano yameshakabidhiwa Muhimbili zikiwemo dawa muhimu zinazotumika kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi hao.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images