Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mashambulizi mawili ya risasi Ohaio na Texas Nchini Marekani yaua watu 30

$
0
0
Watu kumi wameuawa kufuatia shambulizi la risasi katika mji wa Dayton, Ohio nchini Marekani. 

Polisi wamesema hayo mapema jana Jumapili na kuongeza kuwa mshambuliaj ni miongoni mwa waliouawa. 

Watu wasiopungua 16 wamejeruhiwa na wamepelekwa katika hospitali mbaimbali kwa matibabu. 

Shambulizi hilo linajiri katika muda wa saa 24, baada ya kutokea mkasa mwengine kama huo ambapo watu 20 waliuawa na 26 kujeruhiwa kwa kufyatuliwa risasi na mtu aliyekuwa na bunduki ndani ya duka moja kubwa eneo la El Paso, Texas. 

Polisi wamemkamata mwanaume anayeshukiwa kuhusika kwenye shambulizi la Texas mwenye umri miaka 21.

Msemaji wa polisi wa El Paso Robert Gomez ameeleza kuwa wengi wa wahanga katika kisa cha Texas walimiminiwa risasi katika duka la Walmart. 

Gomez ameongeza kuwa wakati wa tukio hilo kulikuwa na karibu wateja 3000 kwenye duka. 

Polisi wamesema huenda shambulizi hilo lilichochewa na chuki za ubaguzi wa rangi. 

Jumla ya watu 30 wameuawa kwenye mashambulizi hayo mawili.

Gari ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima Lapata Ajali Likidaiwa Kuendeshwa na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wa dereva

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki amesema gari la mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima limepata ajali jana Jumapili Agosti 4, 2019 likiwa linaendeshwa na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wa dereva wa mkuu huyo wa Mkoa.

Ndaki amesema ajali hiyo imetokea  jana saa 3 asubuhi na kwamba gari hilo lenye namba za usajili STL 5961 lilikuwa likiendeshwa na mtu ambaye taarifa za awali zinaeleza kuwa ni kijana wa dereva wa Malima.

"Mtoto na Baba yake wote wamelazwa Hospitali, Mtoto ana majeraha baada ya kupata ajali na gari ya Mkuu wa Mkoa na huyu baba ambaye ni Dereva wa Mkuu wa Mkoa alianguka kwa Presha tukamkimbiza Hospitali, maana alipata mshtuko bada ya kufika eneo la tukio na kuiona ajali"-Amesema

Rais Maguli Leo Atafungua Rasmi Maonesho ya 4 ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar

$
0
0
Rais Magufuli leo Jumatatu August 5, 2019  anatarajiwa kufungua rasmi Maonesho ya 4 ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Dar es Salaam.

Maonesho haya ni utangulizi wa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi zote 16 za SADC unaotarajiwa kufanyika hapa Dar es Salaam, Agosti 17-18.

LIVE: Rais Magufuli Katika Ufunguzi Wa Maonesho Ya SADC

$
0
0
LIVE: Rais Magufuli Katika Ufunguzi Wa Maonesho Ya SADC

Rosa Ree Ametuletea VIDEO Mpya Itazame Hapa...Wimbo Unaitwa Nguvu za Kiume

$
0
0
Rapper Rosa Ree anaendelea kushusha madude ni kijidhirisha kuwa ndio Rapper Bora kwa kipindi hichi, Usiku wa Leo ameachia Dude kali linaloitwa nguvu za kiume...

Serikali Kupitia Upya Sera ya kilimo Ili Kuwanufaisha Wakulima

$
0
0
Serikali imesema  sera iliyopo ya sekta ya kilimo inayotumika sasa,  ndiyo cha chanzo cha wakulima kuwa masikini kutokana na kuwatumikisha  wananchi kuilisha nchi na  matajiri, huku wakiwa wanakabiliwa na changamoto kubwa.

Kutokana na hali hiyo, imesema sera imepitwa na wakati ambapo wizara  imelazimika kuanza kuipitia upya  na kuondoa  changamoto  na vikwazo kwa wakulima.

Bashe ametoa kauli hiyo  Jumamosi Agosti 3, 2019 wakati akifungua maonesho ya Nanenane  Mikoa ya Kagera,  Geita na Mwanza yaliyofanyika viwanja vya Nyamhongoro jijini Mwanza ambapo aliwapiga marufuku wakuu wa wilaya na mikoa kuwazuia wakulima kuuza chakula chao kwa kuhofia uwepo wa njaa.

Alisema kila mkulima, anajua namna anavyotunza  na kuilisha familia yake hivyo  kama kuna kiongozi anahofia uwepo wa njaa ni vema  akanunua mazao hayo  kwa bei anayotaka mkulima na kuyatunza ili yaweze kusubiria dhana aliyoiweka kichwani kwake, kwamba kutakuwapo na uhaba wa chakula.

"Nataka niwaulize hata kama tumejaza mahindi hiki kiwanja chote kama hamna hela ya kuyanunua hayo mahindi yatawasaidia? Wakulima wanalima mazao ya kilimo, ya chakula na ya biashara ili kupata uwezo wa mifuko yao.”

"Hatuwezi kujenga viwanda wakati wakulima ni masikini, haiwezekani na ili wakulima waweze kupata fedha ni lazima tuwaruhusu kufanya biashara za mazao yao pale ambapo wanaweza kuuza mazao yao,” alisema Bashe

“Sera iliyopo imepitwa na wakati  kabisa,  inawaumiza wakulima   na kuwafanya kubaki  kila mwaka kuilisha nchi na matajiri huku wao wakibaki na umasikini wao  huku kukiwapo na utitiri wa taasisi nyingi ambazo ukichunguza zimeanzishwa kwa lengo la kuwakandamiza, hii haiwezekani kama wizara tumeanza kuangalia ni taasisi gani zinatakiwa  kufutwa na kubaki  chache.

“Fedha ambazo zilikuwa zikielekezwa kwenye utitiri wa taasisi hizo, zitaelekezwa katika mfuko maalum  ambo  wizara tunatarajia kuanzisha  na kazi ya mfuko huo ni kufidia mkulima pale inapotokea mtikisiko wa bei katika soko la dunia, kama serikali hatuna uwezo wa kuthibiti bei ya soko la dunia, mfuko huo ndio utakaokuwa na kazi ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuwafikia wakulima,”alisema.

Alisema Serikali ilikuwa ikipokea fedha nyingi kutoka mataifa ya nje ili kuendeleza kilimo, lakini zilikuwa zikishia katika semina mafunzo kwa  watendaji, huku  asilimia 50 ya fedha zilizokuwa zikipokelewa ndizo  zinafika kwa wakulima.

Mbaroni kwa Kumuua Mume Wake kwa BisiBisi

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MWAJUMA Omary Malembeka (28)anadaiwa kumuua mume wake Selemani Kondo (43) mkulima na mkazi wa Chamalale,kata ya Vihingo,Mzenga ,wilayani Kisarawe mkoani Pwani, kwa kumchoma na bisibisi kwenye bega  .
 
Akithibitisha kuhusu tukio hilo,kamanda wa polisi mkoani hapo, Wankyo Nyigesa alisema mwanamke huyo alifanya maamuzi hayo kutokana na wivu wa kimapenzi.
 
Alieleza, kulikuwa na mzozo baina yao ambapo Mwajuma alimtuhumu mume wake kuwa siyo mwaminifu katika ndoa yao.
 
“Selemani aliuawa kwa kuchomwa bisibisi katika bega lake la kushoto na sehemu ya juu na mke wake huyo”alifafanua.
 
Wankyo alisema, kujichukulia sheria mkononi sio jambo la msingi kwani inaweza kuleta madhara kama ya kujeruhi ama kusababisha kifo ,na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
 
Katika hatua nyingine, huko kijiji cha Lulenga, Ubena ,jimbo la Chalinze polisi walimkamata Kitenye Lumange ,mfugaji wa jamii ya kimasai (24) kwa kosa la wizi wa ng’ombe 13 wenye thamani ya sh.milioni 7.2 mali ya Arisen Hussein mkazi wa kijiji cha Visakazi .
 
Kamanda huyo alibainisha,wanawasaka watuhumiwa wengine walioshiriki kuiba mifugo hiyo.

Lugola Aaapa Kuendelea Kupambana na Polisi Wasiotii Maagizo Yake

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola mara baada ya kuteuliwa na Rais Dk John Joseph Pombe Magufuli kuiongoza Wizara hiyo, kazi ya kwanza aliyoifanya ni kulivunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na mabaraza yote ya ngazi ya Mkoa nchini.


Waziri Lugola alitangaza uamuzi huo Julai 5, 2018 jijini Mbeya alipozungumza na Wajumbe wa Baraza la usalama barabarani mkoani humo kutokana na changamoto mbalimbali zilizokua zinalikabili Baraza hilo, ikiwemo ongezeko la ajali, na askari wa usalama barabarani kujihusisha na matukio ya kuchukua rushwa.

Kutokana na uboreshaji wa baraza hilo, Lugola anaendelea kuhakikisha matrafiki wanafanya kazi kwa weledi kuepuka rushwa na kutonyanyasa madereva ambao wanafuata taratibu za usalama barabarani.

Licha ya baadhi ya madereva kutii sheria bila kushurutishwa lakini wapo ambao wanavunja sheria za usalama barabarani, Waziri Lugola anawaagiza Polisi nchini kuendelea kuwakamata na kuwapiga faini pamoja na kuwapeleka mahakamani wanaovunja sheria.

Lugola alisema kuna baadhi ya askari wa usalama barabarani wanajua sheria lakini wanafanya makusudi kwa lengo la kupata fedha za rushwa kwa madereva wanaofanya makosa au wana vyombo vya moto ambavyo ni vibovu.

Kutokana na changamoto hizo, Lugola akiwa katika ziara zake za kikazi zilizoambatana na mikutano ya hadhara, alizozifanya kuanzia mwezi Julai, 2019 mara baada ya kuteuliwa kuingoza Wizara hiyo, katika Mikoa ya Kigoma, Kagera, Arusha na Morogoro, licha ya kuzungumza mengi ya Wizara yake, lakini alijikita zaidi kusambaratisha kero za bodaboda nchini.

Lugola anasema yeye hawezi kufanikiwa peke yake bila Jeshi la Polisi hasa Kikosi cha Usalama Barabarani kumpa nguvu anapotoa maagizo yake kwa viongozi wa Jeshi ambapo lengo lake kuu si kubomoa bali kuboresha na kuwafanya madereva wa bodaboda waweze kupambana na hali ngumu ya maisha kupitia biashara ya bodaboda wanaoifanya.

“Lengo langu kuu ni kuwasaidia waendesha bodaboda waweze kufanya kazi zao kwa amani, bila bughudha kama walivyoahidiwa na mheshimiwa Rais Magufuli, hivyo maelekezo ninayotayoa kwa Jeshi lazima yafuatwe,” anasema Lugola.

Lugola amesema baadhi ya Wakuu wa Vikosi vya Usalama Barabarani (MaRTO) wanapuuza maagizo yake wakisema kuwa ni maagizo ya kisiasa hivyo wao wanafuata sheria, hali inayomfanya Waziri huyo kuchukizwa na kauli hizo ambazo zinavunja sheria za nchi na pia yeye Waziri anamamlaka ya kutoa agizo lolote ambalo lipo sahihi kwa mujibu wa sheria.

“Mimi ni Mwanasiasa nikiwa jimboni kwangu Mwibara, nje ya jimbo langu, mimi ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, hivyo ninapotoa maelekezo au maagizo ni kutokana na nafasi yangu na lazima yafuatwe ili nchi iweze kusonga mbele,” anasema Lugola.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara, uliofanyika Uwanja wa Stendi, Wilayani Malinyi, Mkoani Morogoro, ambao ulihudhuriwa na mamia ya wananchi Wilayani humo, Waziri Lugola anatoa ya moyoni jinsi baadhi ya viongozi matrafiki mikoa kuyapuuza maagizo yake anayoyatoa.

Lugola anasema yeye anajua sheria ya usalama barabarani, na yupo Wizarani kwa lengo la kumsaidia Rais katika mapambano ya kuondoa umaskini na nchi kuwa na uchumi wa kati, hivyo sekta ya bodaboda ni muhimu katika mapambano ya kuondoa umaskini.

“Sijawahi kutamka katika mikutano yangu yote ya ndani au ya hadhara, kuwa bodaboda wasikamatwe, bali nasema bodaboda lazima wapewe mazingira mazuri ya kufanya kazi yao bila bugudha, na pia kuyakamata hovyo bodaboda na kuzilundika vituoni kwa makosa ambayo yanapaswa kutozwa faini hilo nimelikataza,” anasema Lugola.

Anasema wapo baadhi ya wakuu wa matrafiki mikoa wanayapuuza maagizo yake na mmojawapo ni RTO Mkoa wa Arusha ambaye anatumia mikutano anayoalikwa kunipinga na kuyaaita maagizo yangu ninayoyatoa kwa maunfaa ya nchi ni yakisiasa.

Lugola kutokana na kumfuatilia RTO huyo kwa muda mrefu, kupitia mkutano wa hadhara wa Mji wa Malinyi, alitamka hadhara kumuondoa madarakani Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo, Charles Bukombe na kumuagiza Katibu Mkuu, pia kumchukulia hatua za kinidhamu ili iwe fundisho kwa matrafiki hao wa mikoa nchini.

Lugola amesema RTO huyo ameshuhudia katika video ambayo ilikua inasambaa mitandaoni akiwa katika mkutano jijini Arusha, akipinga maagizo yake na kuyaita ya kisiasa na pia kutokuyatekeleza.

“Sitoi maagizo ya kisiasa bali anatoa maagizo yatakayomsaidia rais kazi zake kwa wananchi wanyonge wanaopambana na umaskini na ajira, kutokana na kutokuwa na nidhamu kwa RTO huyu namuagiza katibu Mkuu achukue hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumuondoa u-RTO afanye shughuli zingine za kipolisi,” anasema Lugola.

Pia Lugola anatoa onyo kwa RTO wa Mikoa ya Morogoro na Mara, kujitathimini katika utendaji wao, na pia anawataka wakuu wa vikosi hao katika mikoa mbalimbali nchini kuyasimamia vema maagizo yake kwa kutowaonea wananchi, kuacha kuchukua rushwa barabarani.

Lugola anasema Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na haitaki kumnyanyasa mwananchi yeyote kupitia makosa ya trafiki wasiokuwa waaminifu.

Katika Mkutano huo, Lugola anaagiza kuwa, Jeshi katika vituo vya polisi nchini, bodaboda zinazotakiwa kuwepo vituoni ni zile zilizopo katika makundi matatu ambayo ni Bodaboda zilizohusika kwenye uhalifu, zilizotelekezwa au zilizookotwa na zilizohusika katika ajali.

“Ninasisitiza kwa mara nyingine, bodaboida hizo ndizo zinapaswa kuwepo vituoni, lakini kuziweka bodaboda ambazo hazipo katika makundi hayo, napiga marufuku na hii nataka Polisi nchi nzima munielewe,” anasema Lugola.

Katika kazi ya kuhakikisha madereva wa bodaboda na magari nchini wanafanya kazi zao kwa utulivu bila kunyanyaswa, Januari 2, 2019, akiwa mjini Bukoba, Mkoani Kagera, anatangaza kuwa, gari lolote litakalokamatwa na trafiki kwa kosa la bodi ya gari bovu, weipa haitoa maji, taa za breki haziwaki, mafuta yanavuja, hapo kosa ni moja tu, gari ni bovu na faini ni shilingi 30,000, na si sahihi kuwa kila tatizo la gari ni kosa linalojitegemea.

Huku wananchi wakimshangilia Waziri Lugola katika mkutano huo, aliendelea kusema kuwa, Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na haitaki kumnyanyasa mwananchi yeyote kupitia makosa ya trafiki wasiokuwa waaminifu.

“Kutokana na changamoto za barabarani, nawaagiza polisi wa usalama barabarani nchini, gari lolote litakalokamatwa kwa kosa la bodi ya gari bovu, weipa haitoa maji, taa za breki haziwaki, mafuta yanavuja, hapo kosa ni moja tu, gari ni bovu na faini ni shilingi 30,000, na si sahihi kuwa kila tatizo la gari ni kosa linalojitegemea,” anasema Lugola.

Akiwa Mkoani Arusha, mwezi Februari, 2019, katika Mkutano wake wa hadhara uliofanyika Jimbo la Arumeru, Waziri Lugola anapiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi hapa nchini kukamata pikipiki wakiwa hawana sare za Jeshi, anasema kwa kufanya hilo kunaleta kero kwa madereva na pia anayekamatwa anaweza akadhaniwa kuwa ni jambazi.

Lugola anaongeza hayo katika Mkutano huo wa hadhara uliofanyika uwanja wa Wilayani humo, akisisitiza kuwa, polisi wanapaswa kufuata utaratibu wa kijeshi hasa wanapokamata vyombo vya moto na siyo kuvunja utaratibu.

Lugola anafafanua kuwa, bodaboda zinazovunja sheria za usalama barabarani zinapaswa kukamatwa bila kuwaonea huruma, ila ni kosa Polisi kuwanyanyasa vijana hao ambao wanapata ridhiki kupitia biashara hiyo.

“Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” anasema Lugola.

Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda wa Wilaya ya Arumeru, jijini Arusha na Tanzania kwa ujumla wafuate sheria za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha vyombo hivyo vya moto wanapaswa kuwasha taa.

WaziriI Lugola licha ya kuzungumza hayo katika mikutano yake ya hadhara, pia anazungumza maneno hayo katika Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa, Wilaya na pia Mikutano yake na askari na watumishi raia wa Wizara yake waliopo mikoani.

Pia Waziri Lugola, anatangaza dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi.

Waziri Lugola anaendelea na ziara ya aina hiyo nchi nzima, na anatarajia Agosti 10, 2019 kuanza ziara Mkoa wa Rukwa ambapo anatarajia kuzitembelea Wilaya zote za Mkoa huo kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi, na pia kutangaza kazi nzuri zinazofanywa na Rais John Magufuli nchini.

Wananchi Wahimizwa Kuchangamkia Fursa Zilizopo SADC

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dk Stergomena Tax amewataka wafanyabiashara nchini Tanzania kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya kuanza kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika nchi wanachama.

Dk Stergomena  ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Agosti 5, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya bidhaa katika wiki ya Viwanda kwa Nchi 16 za SADC. Uzinduzi huo umefanywa na Rais John Magufuli katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) nchini Tanzania.

Katika hotuba yake, Dk Stergomena amewataka wafanyabiashara kutoa taarifa katika wizara ya viwanda pale wanapokutana na vikwazo wakati wa shughuli zao za kibiashara ndani ya jumuiya hiyo iliyoondoa vikwazo na baadhi ya tozo za kibiashara.

Alichokisema Rais Magufuli Wakati Akifungua Maonyesho Ya 4 Wiki Ya Viwanda Kwa Nchi Za SADC

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefungua maonesho ya viwanda ya nchi za Jumuiya ya SADC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki hiyo, Rais Magufuli amezitaka nchi hizo kupeana fursa wenyewe kwa wenyewe hasa linapofikia suala la biashara, ambapo ameziomba nchi hizo, kuangalia namna ya kushirikiana kwa manufaa ya uchumi wa viwanda.

"Tuweke kipaumbele kwenye utumiaji wa teknolojia ya viwanda kwenye Jumuiya yetu kabla ya kwenda mbali, tuuziane bidhaa kabla ya kwenda kwingine, kama Namibia wanahitaji mahindi tuwapelekee mahindi, hili soko la watu Mil. 300 wa SADC litakuza uchumi wetu." amesema Magufuli.

"Sekta ya viwanda imeanza kuleta mafanikio kwa nchi za SADC, hamasa ya ujenzi wa viwanda umeongezeka, kwa sisi Tanzania tumeweka mkazo wa kutumia malighafi zinazozalishwa hapa, kwa miaka 3 zaidi ya viwanda 4000 vimeanzishwa." Amesema Rais Magufuli.

Maonesho hayo ya viwanda yanatarajia kufanyika kwa wiki nzima kuanzia leo, Julai 05, ambapo mara baada ya kukamilika kwa maonesho hayo, utaanza mkutano wa Marais 19 wa nchi za Jumuiya ya SADC ambapo Rais Magufuli ni Mwenyekiti.

Mwanahabari Erick Kabendera Apandishwa Mahakamani na Kusomea Makosa Matatu ya Kuongoza Genge La Uhalifu,kukwepa Kodi Na Kutakatisha Fedha.

$
0
0
Mwanahabari Erick Kabendera amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 3 ikiwemo kujihusisha na genge la uhalifu,kukwepa kodi na kutakatisha fedha  Tsh.173.2 Milioni.

Hati ya mashtaka dhidi ya mshtakiwa Kabendera imesomwa na mawakili wawili  wakuu wa serikali, na mmoja Mwandamizi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile.

Mshtakiwa Kabendera anatetewa na mawakili wa kujitegemea, Gebra Kambore, John Mallya na Benedict inshabakaki.

Akisoma shtaka la kwanza, wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi amedai, mshtakiwa anadaiwa katika siku tofauti tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Kabendera alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Katika shtaka la pili lililosomwa na wakili Wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa  bila kuwa na sababu za msingi kisheria alishindwa kulipa kodi ya sh. 173, 247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Katika shtaka la utakatishaji fedha lililosomwa na wakili Wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon imedaiwa, kati ya Januari 2015 na Julai 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia kiasi hicho cha sh. Milioni 173.2 wakati akizipokea alijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kukwepa Kodi na kujihusisha na genge la uhalifu.

Hata hivyo, mshtakiwa Kabendera hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.

Mawakili wa utetezi wakiongozwa na wakili Kambore, wameomba upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka kwani kesi dhidi ya mteja wao haina dhamana. Hivyo katika terehe itakayokuja wangependa kujua upelelezi umefikia wapi.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 19 Mwaka huu, mshtakiwa amepelekwa rumande.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  0759208637   /  0620510598

Rais Magufuli ataka kufutwa utitiri wa Kodi SADC

$
0
0
Rais   Magufuli amehimiza sekta binfasi katika nchi za SADC kuendelea kuwa na ujasiri wa kufungua viwanda vingi hapa nchini kwa kuwa serikali inaendelea kuboresha mazingira  mazuri ya uwekezaji.

Rais Dkt.Magufuli ameyasema hayo wakati akifungua Maonesho ya nne ya wiki ya viwanda kwa nchi  za SADC jijini Dar Es Salaam na kusisitiza umuhimu wa kufungua viwanda vingi wakati huu mazingira ya uwekezaji yakiboreshwa ikiwemo ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Rufiji utakaosaidia kupunguza bei ya umeme pindi utakapokamilika.

Katika hotuba yake ya ufunguza Rais Dkt.Magufuli amendelea kuhimiza umuhimu wa kufutwa kwa utitiri mkubwa wa kodi kwa nchi za wanachama wa SADC kwa lengo la kuongeza hamasa ya uwekezaji wa viwanda vitavyosaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi kwa nchi za SADC.

Kadhalika Rais Dkt.Magufuli amehimiza uwekezaji pia katika viwanda vya madini kwa kuwa nchi nyingi za SADC zina rasilimali za kutosha za madini na kupongeza uwekezaji wa viwanda hapa  inayofikisha viwanda elfu nne kwa sasa.

Mwanamke Kaamua Kufunga Ndoa na Mbwa Baada ya Kutembea na Wanaume 221

$
0
0
Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Elizabeth Hoad raia wa Uingereza,  amefunga ndoa na Mbwa wake aitwaye Logan katika kipindi cha Television Nchini humo.

Baada ya kufunga ndoa, Mwanamke huyo ameeleza aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Wanaume 221, kati ya hao Wanne ndio walimvalisha pete ya uchumba lakini imeshindikana kuolewa.

Pia mwanamke huyo amesema ameamua kufunga ndoa na Mbwa wake "Logan", kwa sababu ya kuchoshwa na Tabia za Wanaume wazee kupenda Wanawake wadogo na Wanawake wadogo kupenda Wanaume wazee.

Aidha Elizabeth ameendelea kusema Mbwa huyo ana maana kubwa sana kwake kwa sababu wameshasaidiana kwa vitu vingi hasa wakati alipoumizwa na Wanaume ambao aliwahi kuwa nao, pia ana marafiki zake 10 ambao wameamua kufunga ndoa na Mbwa wao.

Akiweka kiapo katika sherehe ya kufunga ndoa hiyo Elizabeth aliahidi kuwa, "kwa mwili wake wote atatembea na Mbwa Logan, atamjali na kumpenda siku zote za maisha yake na kulala nae kitanda kimoja" amesema Elizabeth.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Lapiga Marufuku Bodaboda Kuingia Katikati ya Jiji

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam kupitia kwa  Lazaro Mambosasa  limesema limejipanga kuimarisha ulinzi wakati wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika jijini Dar es Salaam.

 Aidha katika kipindi hiki cha mkutano wa SADC Jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam linapiga marufuku mambo yafuatayo;

1.Marufuku pikipiki (Bodaboda )zote kuingia katikati ya Jiji kuanzia tarehe 06 August hadi 18 August, 2019 kutokana na sababu ya baadhi ya bodaboda kujihusisha na vitendo vya uhalifu

2. Marufuku kuweka taa za vimulimuli au za rangi rangi, taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye Magari ya kiraia au watu binafsi na pikipiki zote za kiraia

3. Marufuku kuingilia misafara ya wageni, wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu kipindi hiki cha ugeni mkubwa wa kimataifa.


“Katika kipindi hiki cha mkutano wa SADC Jeshi la polisi kanda maalum DSM linapiga marufuku pikipiki (Bodaboda )zote kuingia/kufika maeno yote ya katikati ya Jiji kuanzia August 06 hadi August 18,2019 kutokana baadhi ya bodaboda kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

“Polisi inapiga marufuku kuweka taa za vimulimuli au za rangi rangi, taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye magari ya kiraia au watu binafsi na pikipiki za kiraia, isipokuwa magari yanayotoa huduma za dharura tu na ya makampuni binafsi ya ulinzi” Amesema Mambosasa

Mkongo: Kibongo ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
********************************
SUPER MKONGO MPYA,
_______________________________
********************************
Ni dawa bora ya kutibu na kumaliza matatizo yote ya nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile,

- kuwahi kufika kileleni dakika moja ushakojoa
- maumbile kusinyaa na kulegea wakati wa tendo
- kukosa hamu ya tendo la ndoa
- kushindwa kurudia tendo la ndoa
- maumbile kusimama kwa kulegea
-  kulegea katikati ya tendo
- kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu
- kuishiwa nguvu kutokana na punyeto.

Epuka aibu hii leo kwa kutumia SUPER MCONGO MPYA, kiboko ya matatizo haya.
_______________________________
Kwanza fahamu sababu zinazopelekea kuwa na upungufu wa nguvu za kiume
_______________________________
(1) kujichua (punyeto) kwa muda mrefu maana hupelekea misuli ya uume kulegea.
(2) ngiri
(3) kuugua chango la uzazi kwa muda mrefu.
(4) kupungukiwa hormone za testosterone.
(5) ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho  vya kutosha.
(6) kutokufanya mazoezi na mwenendo wa maisha.
(7) kisukari.
(8) tumbo kuunguruma na kujaa gesi.
(9) maumivu ya kiuno nk.
_______________________________

WASILIANA NA:
DR. MCONGOMANI
SIMU NO:
📞0658816558
📞0682323682
Popote ulipo huduma hii inakufikia

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Rais Magufuli: Kipaumbele ni Kuhuisha Teknolojia ya Viwanda -SADC

$
0
0
Na.Paschal Dotto-MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amefungua maonesho ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC). 
 
Akizungumza katika hafla hiyo ya Wiki ya Viwanda ya SADC jana, Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kuwa ili kufikia uchumi wa kati viwanda ni kichochea muhimu katika sekta nyingi kwani uwepo wa viwanda utasababisha uhakika wa uzalishaji na uchakataji wa bidhaa na kufanyabiashara kwa nchi wananchama. 
 
Rais Magufuli amezitaka nchi wanachama wa SADC kuweka kipaumbele kwenye kuhuisha teknolojia katika viwanda vilivyoko ndani ya jumuiya ya Maendelea kusini mwa afrika (SADC) pamoja na kushughulikia kwa haraka zaidi vikwazo vinavyochelewesha ukuaji wa viwanda. 
 
“Viwanda ni Sekta muhimu katika kukuza uchumi wa nchi yeyote, kuondoa umasikini, kuongeza ajira na Sekta hii imeziletea Maendeleo makubwa nchi zilizoendelea, kwa hiyo mkutano huu ni dhahiri kuwa sasa nchi za SADC zimeanza kuchukua hatua madhubuti za kukuza sekta hii na ikiwa mkakati huu utatekelezwa utasaidia kukuza uchumi wa nchi zetu”, Rais Magufuli. 
 
Akielezea suala la teknolojia Rais Magufuli amesema kuwa ukuzaji wa teknolojia na ubunifu kwenye sekta ya viwanda ni silaha muhimu kwa nchi za SADC kuendelea na kutegemeana kwani utazalisha ajira, biashara kubwa, na kuepuka kuuza malighafi  kwa wingi nje ya Afrika kama ilivyosasa. 
 
Vilevile,  mchango wa sekta ya viwanda kwa nchi za SADC bado ni mdogo kwani Sekta hiyo inachangia wastani wa asilimia 10 ya pato la taifa na katika Jumuiya ya SADC sekta hiyo muhimu inachangia asilimia 11 tu. Amesema Rais Magufuli.  
 
Aidha Rais Magufuli alizitaka nchi wanachama wa SADC kujikita zaidi katika kukuza ubunifu na teknolojia rahisi kwenye sekta ya viwanda kwa kuwaendeleza vijana na kuimarisha viwanda vidogo vidogo vilivyoko kwenye jumuiya, kwa hiyo wiki ya viwanda ni fursa muhimu kwa nchi  zote wananchama. 
 
“Wiki ya Viwanda ya SADC ni fursa ya kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau kuhusu utekelezaji wa mikakati ya miaka 49 ya uendelezaji wa viwanda katika jumuiya yetu, bado tunasafari ndefu kuhakikisha sekta ya viwanda inazidi kukua na kuleta mageuzi ya kiuchumi katika nchi zetu”, Amesema Rais Magufuli 
 
Rais Magufuli amesisistiza kwa kusema kuwa katika kuimarisha mashirikiano ndani ya Jumuiya ya Maendeleo (SADC) ni lazima kuimarisha sekta ya uwekezaji kwani nchi hizo zina fursa nyingi kwenye uwekezaji ikiwemo  viwanda vya  madini, kilimo, uvuvi na ufugaji kwa hiyo wananchi kutoka SADC wanatakiwa kuchangamkia fursa kwenye soko la takribani watu milioni 344. 
 
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Innocent Bashungwa amesema kuwa uthubutu wa Rais Magufuli kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati wenye viwanda ni mkubwa na  matokea yake  yanaonekana sasa. Hivyo, maonesho haya ni moja ya njia muhimu ya kuimarisha sekta ya viwanda nchini. 
 
“Maonesho haya ya wiki ya viwanda yanawawezesha wanachama wa SADC kuona namna nchi wenyeji inavyotekeleza uwekezaji kwenye sekta ya Viwanda. Aidha,  tunaamini wazalishaji, wafanyabiashara, na wananchi kwa ujumla watachangamkia fursa mbalimbali zitazotokana na mkutano huu wa SADC.”, Waziri Bashungwa. 
 
Waziri Bashungwa alisema kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye biashara ndani ya SADC  kwani takwimu zinaonyesha kuwa mauzo ya Tanzania kwenda SADC mwaka 2018 yalikuwa dola za kimarekani milioni 999 ikilinganishwa na dola za kimarekani milioni 875 mwaka 2017 ikiwa na ongezeko la asilimia 12.16. 
 
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Ally amesema kuwa uthubutu wa Rais Magufuli wa kuendeleza ndoto ya Baba wa Taifa, Mwl . Julius Nyerere kwa kujenga bwawa Kubwa la kufua na kuzalisha umeme mto Rufiji ni hatua kubwa kwa maendeleo ya sekta ya viwanda. 
 
Balizo Amina alisema kuwa katika utekelezaji wa miradi yote inayofanywa na Serikali suala muhimu ni uwepo wa amani kwa Tanzania na ndiyo maana ikachaguliwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya SADC yakifuatiwa na Mkutano mkuu wa viongozi wakuu wa nchi za wanachama wa SADC.  
 
“Tanzania itaendelea kuwa kisiwa cha amani na kwa tukio hili itaendelea kudumisha amani na utilivu kwani mpaka sasa maonesho na mkutano mkuu unaofanyika hapa unaonesha kuwa tanzania ni nchi ya amani”, Waziri wa Viwanda Zanzibar, Amesema Balozi Amina Ally. 
 
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt.Stagomena Tax, amesema kuwa juhudi za Serikali ya Tanzania kutekeleza mradi mkubwa wa kufua na kuzalisha umeme mto Rufiji ni moja ya njia madhubuti katika kuimarisha na kukuza sekta ya viwanda kwa Jumuiya ya SADC. 
 
“Kutekelezwa kwa Mradi wa umeme mto rufiji tunaamini kuwa Tanzania itazalisha umeme wa kutosha, tunaomba ziada iweze kwenda kwenye nchi wanachama wa SADC kwani kumekuwa na changamoto ya kubwa mgawo wa umeme na uendeshwaji wa viwanda unahitaji mambo mengi ikiwemo umeme huwezi kuwa na viwanda bila kuwa na umeme unaozalishwa kwa urahisi, kwa hiyo Tanzania imechukuia maamuzi mazuri kuzalisha umeme mto Rufiji.”, Stagomena Tax, Katibu Mtendaji, SADC. 
 
Aidha Dkt.Stagomena aliwaomba watanzania kutumia fursa zilizopo nchi wanachama SADC kwa kuwa ni soko kubwa ambalo linajumuisha nchi 16, ambazo zinawatu wapatao milioni 344 na pato la taifa la pamoja la dola za Marekani milioni 2.5 hivyo ni muhimu kwa watanzania kuzijua fursa hizo na kuzitumia ipasavyo. 
 
Maonesho ya Wiki ya Viwanda yanayofanyika Tanzania kuanzia tarehe 05 mpaka 9 Agosti 2019 na kufatiwa na Mkutano wa wakuu wa nchi 16 wanachama utakaofanyika Agosti 17 na 18,  2019, katika Ukumbi wa Julius Nyerere Dar-es-salaam.
Mwisho

Waziri Wa Kilimo Autaka Uongozi Wa Mkoa Wa Simiyu Kuanza Haraka Utekelezaji Wa Bima Ya Mazao

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umetakiwa kuanza haraka utekelezaji wa mkakati kabambe uliozinduliwa leo tarehe 3 Agosti 2019 na Waziri wa Kilimo kuhusu Bima ya Mazao kwa wakulima.

Waziri Hasunga ameyasema hayo wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu na kuhudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kupokea maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kuhusu mustakali wa zao la Pamba.

Mhe Hasunga alisema kuwa kuanza haraka kwa utekelezaji wa uandikishaji wa wakulima kutaimarisha uwezekano wa kuboresha maisha ya wakulima ambao katika kipindi kirefu wameumia kupitia majanga mbalimbali wanayokumbana nayo ikiwemo mazao yao kuungua moto ama ukame.

Alisema kuwa uzinduzi wa Bima ya Mazao umefanyika katika mkoa wa Simiyu hivyo mkoa huo unapaswa kuanzisha haraka utekelezaji wake.

Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amempongeza Waziri wa Kilimo kwa kipindi cha muda mfupi ameweza kuonyesha dira na muelekeo chanya katika ukombozi wa sekta ya kilimo nchini.

Alisema kuwa maamuzi ya wizara ya kilimo inayosimamiwa na Mhe Hasunga ya kuanzisha Bima ya Afya, na Usajili wa wakulima ni miongoni mwa mambo muhimu yatakayoinua sekta ya kilimo nchini.

Muhimbili Yakanusha Uwepo wa Mgonjwa Mchawi Aliyejigeuza Kuwa Ndege

$
0
0
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekanusha juu ya taarifa inayosambaa mitandaoni ikimuonesha mwanamke mmoja mgonjwa anayedaiwa kujigeuza ndege usiku na kurudi kuwa binadamu asubuhi, aliyekamatwa na wagonjwa wenzake.

Taarifa hiyo ya Hospitali ya Muhimbili imesema kuwa imejiridhisha na uchunguzi uliofanyika na wamebaini kuwa picha na video hiyo hazihusiani na Hospitali ya Muhimbili kimazingira na katika takwimu zao hawana mgonjwa kama huyo.

"Kwanza hatuna mgonjwa huyo, pili, hatuna wodi zinazofanana na hiyo katika hospitali zetu (Upanga na Mloganzila), tatu, wauguzi wanaoonekana katika viso hiyo hawajavaa sare za hospitali yetu", imesema sehemu ya taarifa hiyo.

"Tunawaomba wananchi na watumiaji wa huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Upanga na Mloganzila) kutokuwa na hofu juu ya taarifa hizo kwani siyo za kweli", imeongeza taarifa hiyo.

Video inayosambaa mitanndaoni inamuonesha mwanamke huyo akiwa amezungukwa na wagonjwa, waangalizi wa wagonjwa na wauguzi kwenye wodi ya hospitali akikemewa na kutakiwa aondoke baada ya kukutwa na sintofahamu hiyo ya kujigeuza kutoka kuwa ndege hadi kuwa binadamu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images