Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TOUFIQ: Tanzania Kinara Katika Udahili Wa Wanafunzi Elimu Ya Awali Barani Afrika.

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni kinara katika suala la udahili wa wanafunzi katika elimu ya awali barani Afrika na hivyo kuifanya kupiga kubwa katika utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu(SDGs).  

Mafanikio hayo yanatokana na serikali kutoa elimu bure bila malipo ambao umechangia kuongeza udahili wa watoto wengi kupata fursa ya kupata elimu. 

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Viti maalum FATUMA TOUFIQ ambaye ni pia champion wa masuala ya SDGs bungeni wakati akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu mkutano aliohudhuriwa wa ‘High level political forum’ uliofanyika Umoja wa Mataifa(UN) hivi karibuni. 

Amesema katika mkutano huo waliwasilisha malengo 6 ya SDGs ambayo kwa ujumla wake Tanzania imefanya vizuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kutoa wito kwa serikali. 

TOUFIQ ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na wanawake na watoto(Wowap), amesema katika mkutano huo alipelekwa kwa ufadhili kutoka Shirika la Equal Measure 2030 la nchini Marekani  linalojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo hayo ili kuhakikisha kunakuwa kuna usawa kwenye mambo mbalimbali ikiwemo elimu. 

Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya utoaji taarifa jinsi nchi ilivyofanya katika utekelezaji wa SDGs na Tanzania ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kutoa ripoti yake iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Dk.Philipo Mpango.

CCM yashinda katika Uchaguzi wa Naibu Meya na Kaimu mwenyekiti wa Halmashauri mkoani Shinyanga

0
0
NA SALVATORY NTANDU
Diwani wa kata ya Igunda Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa Makamo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo katika Uchaguzi wa ndani wa  cha Chama cha Mapunduzi (CCM) kilichofanyika jana.

Uchaguzi huo umefanyika jana katika ofisi za CCM wilaya ya kahama ukiongozwa na Mwenyekiti wa uchaguzi huo Emmanuel Mbamange  ambaye pia ni katibu wa CCM wilaya ya Kahama na kusema kuwa mh, Katoto amepata kura 20 za ndio kutoka kwa madiwani wa Halmashauri hiyo waliohudhuria uchaguzi huo.

Amesema Halmashauri hiyo ina jumla ya madiwani 28 wa CCM lakini waliopiga kura ni 20 huku wengine wakiwa na udhuru mbalimbali na kusema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo Mh, Katoto amewashukuru madiwani wenzake na kuahidi kutoa ushirikiano kwao ili kuhakikisha Halmashauri ya Ushetu inapata maendeleo.

Katika Hatua nyingine  Diwani wa Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga John Kisandu (CCM) amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, na kumshinda mpinzani wake Zena Gulamu (Chadema).


Uchaguzi huo wa Naibu Meya umefanyika jana kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani wa kumchagua Naibu Meya pamoja na Kamati mbalimbali, ambazo zitasimamia utekelezaji wa maendeleo ya Manispaa hiyo, ikiwamo kamati ya fedha ya kudumu, uchumi, elimu na afya, miundombinu, ukimwi, maadili pamoja na Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT).

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, amesema John Kisandu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameibuka mshindi kwa kupata kura 15, dhidi ya mpinzani wake Zena Gulam kutoka Chadema ambaye amepata kura tano ,ambapo wajumbe waliopiga kura walikuwa 20.

Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo, Kisandu ameomba ushirikiano kutoka kwa madiwani hao na kuwa kitu kimoja katika kuisimamia halmashauri kwa maslahi mapana ya wananchi na kuwaletea maendeleo.

Aidha madiwani hao wameendelea kujadili ajenda mbalimbali zikiwamo za afya, elimu, maji, miundombinu, fedha, kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo.

LIVE: Rais Magufuli Akizindua Jengo La Tatu La Abiria Katika Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa Wa Julius Nyerere

0
0
Leo Agosti 01,2019 Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli anazindua rasmi Jengo la tatu la Abiria (Terminal III )katika Kiwanja cha ndege cha kimataifa  cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere


Tazama hapo chini

Hatima ya dhamana ya mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera Kujulikana Agost 5

0
0
Mahakama ya Kisutu imekataa na imeutaka upande wa Serikali kuwasilisha kiapo kinzani  kabla ya August 5, 2019 kujibu hoja kuhusu kukamatwa kwa Mwanahabari Erick Kabendera. 

Wakili wake  Shilinde Swedy amewasilisha maombi ya kutaka Kabendera afikishwe Mahakamani kwasababu anashikiliwa  kwa zaidi ya masaa 24 tangu July 29.

Upande wa Jamhuri ulitaka kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani  Agosti 7, mwaka huu, lakni Mahakama ikakataa.

Jamhuri wamekutana na kikwazo hicho leo Alhamisi saa tatu asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile anayesikiliza maombi hayo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai maombi hayo yaliwafikia jana na leo shauri linakuja kwa mara ya kwanza hivyo anaomba apewe muda wa kuwasilisha kiapo cha majibu kinzani Agosti 7 mwaka huu kwa sababu kesho atakuwa Mahakama Kuu katika kesi nyingine.

Wakili wa mwombaji, Shilinde Swedy alidai mteja wake yuko chini ya ulinzi kwa zaidi ya saa 24, hajapata uwakilishi wa aina yoyote hivyo aliomba kesi ije Jumatatu.
 
Hakimu Rwizile alisema kwa kuwa maombi yamekuja chini ya hati ya dharura, muda ulioombwa na Jamhuri ni mrefu, hivyo maombi hayo yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu.

“Maombi yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu siku ya Jumatatu saa saba mchana, wajibu maombi watajibu wakati wowote kabla ya muda huo,” amesema Hakimu Rwizile.

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro

0
0
Rais Magufuli leo August 01,ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kayombe Liyoba kutokana na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.

Taarifa hiyo imetolewa  leo Alhamisi Agosti 1, 2019, jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo wakati akiongea na waandishi wa habari.

Jafo amebainisha baadhi ya kasoro ambazo mkurugenzi huyo ameshindwa kusimamia  kuwa ni ujenzi wa hospitali ya wilaya ambapo Lioba alinunua dawa ya kupulizia mchwa katika majengo  kwa sh. milioni 66  ambazo ni zaidi ya matarajio ya matumizi ya fedha ya eneo hilo.

Kutokana na uamuzi huo, Waziri Jafo amesema Godfrey Mlowe ambaye ni meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) Morogoro vijijini atakaimu nafasi hiyo

Rais Magufuli amtaka Mo Dewji kujali maslahi ya wafanyakazi wake kama Anavyoijali Simba

0
0
Rais Magufuli amemtaka Mfanyabishara Mohamed Dewji (Mo Dewji), kuhakikisha anajali maslahi ya wafanyakazi wake kama anavyofanya katika Timu ya mpira wa miguu ya Simba Sports Club ambapo amemsihi kwamba wafanyakazi hao nao wanastahili kupata maslahi yao.

Ametoa ombi hilo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and Packaging, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, kinachomilikiwa na mfanyabiashara huyo.

“Mohamed Dewji ninakupongeza sana katika hili na ninakuomba uwajali wananchi wanaofanya kazi hapa hasa maslahi yao kwahiyo unapokuwa unaangalia maslahi ya Simba uangalie pia masilahi ya wafanyakazi wa 21st century food and packaging,” amesema.

Aidha ameiataka Kampuni ya Metl Group iliyopo chini ya mfanyabishara huyo kuachana na utaratibu walionao wa kuagiza ngano kutoka nje ya nchi na badala yake kuanza kulima ngano nchini kwani kwa kufanya hivyo itasawadia Watanzania wanaohitaji ajira.

“Ninatoa wito kwa Kampuni ya Metl Group chini ya Mohamed Dewji, nilipokuwa ninapewa maelekezo nmeambiwa mahindi yanatoka Tanzania ambayo yanatengenezwa tani 300 kwa siku lakini ngano inayotengeneza tani 1400 kwa siku inaagizwa kutoka nje hii tuibadilishe,” amesema.

“Katika maisha yangu nilikua ninafahamu kulikuwa na mashamba makubwa sana ya ngano kule Manyara lakini sasa hivi hayatumiki na kuna wakati wawekezaji wakijaribu wanachomewa moto sasa nitoe wito hata kwa Kampuni yako muanze kulima ngano kwani mtakuwa mmesaidia Watanzania wengi,” amesema.

Mo Dewji Ammwagia Sifa Rais Magufuli

0
0
Mkurugenzi wa Kampuni za Mohamed Enterprises Limited, Mohamed Dewji amempongeza Rais Magufuli kwa mageuzi makubwa kwa kipindi kifupi  cha uongozi wake.

Dewji ameyasema hayo leo akifungua kiwanda cha kusaga unga wa mahindi na ngano cha 21st Century Food Packaging kinachomilikiwa na Kampuni za Mohamed Enterprises Limited chenye uwezo wa kusaga tani 1,540 kwa siku

“Mheshimiwa Rais tunaamini kwamba wale wasiokuelewa leo watakuelewa baadae na wasioelewa lengo wataeleweshwa na matokeo ambayo tunaamini hayako mbali sana kwani mageuzi makubwa chini ya uongozi wako ndiyo yaliyotushawishi kuendelea kuwekeza nchini kama unavyoshuhudia leo hii,” amesema.

“Binafsi ninashuhudia kuimarika nidhamu kwa watumishi wa umma, mkazo mkubwa serikalini, kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo, kupungua kwa rushwa na kushughulikiwa kwa migogoro ya ardhi nchini pia tumeguswa na namna ulivyoshugulikia matatizo ya wafanyabishara,” amesema.

Aidha amesema kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda vikubwa na vya kisasa kinachojihusisha na uzalishaji wa unga wa ngano na wa mahindi nchini, na kwamba kampuni ilianza uwekezaji 2005 na ilianza na kiwanda chenye uwezo mdogo wa kusaga tani 240 kwa siku pamoja na uwezo wa kuhifadhi tani 20 tu za nafaka.

“Hivi sasa kiwanda kimeboreshwa kwa kuwekeza kwenye mitambo mikubwa iliyogharimu jumla ya Sh. bilioni 105 na inatumia teknolojia ya kisasa zaidi, uwekezaji huu umefanyika chini ya awamu ya tano, leo tunashuhudia kiwanda cha mahindi chenye uwezo wa kusaga tani 300 kwa siku, kiwanda cha ngano chenye uwezo wa kusaga tani 1240 kwa siku, mitambo yenye uwezo wa kupokea tani 600 kwa saa za nafaka na uwezo wa kuhifadhi nafaka hadi tani elfu 50,” amesema.

Baba Levo Ahukumiwa Kifungo cha Miezi Mitano Jela

0
0
Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Revokatus Kipando maarufu kwa jina la Baba Levo amehukumiwa kifungo cha miezi mitano kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani Mkoani Kigoma.

Inadaiwa kuwa  Baba Levo alimshambulia askari anayefahamika kwa jina la Msafiri Ponera, akiwa eneo lake la kazi eneo la Kwabela baada  ya  mtuhumiwa kulazimisha kupita kwa pikipiki wakati askari huyo akiwaruhusu watembea kwa miguu, na baada ya hapo Baba Levo aliamua kumshambulia askari huyo.

Rais Magufuli atoa Maagizo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara

0
0
Rais  Magufuli amemtaka Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa kusimamia wawekezaji wasisumbuliwe katika uwekezaji wa viwanda.

Rais Magufuli pia amewaomba Watendaji ndani ya Serikali kutowasumbua wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza nchini.

Ametoa tamko hilo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and Packaging, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, kinachomilikiwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo Dewji).

“Watendaji ndani ya serikali pamoja na Waziri wa vianda yuko hapa, tusiwaumize vichwa wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza katika nchi yetu, nimepata taarifa kuna baadhi ya wawekezaji wanawekewa masharti ya ajabu na wengine wanaombwa rushwa, sasa mnawazungusha kwanini hela ni yake haujamsaidia yeye anakuja kuwekeza ili watu wako wapate ajira,” amesema

“Waziri wa Biasha kama kuna watendaji wako ndani ya serikali bado hawajaona mwelekeo wa awamu ya tano wakae pembeni sisi tuendelee kwenda mbele kwani tunataka wawekezaji waje, akiwa na hela yake muoneshe eneo akajenge kiwanda chake na akishamaliza serikali itakusanya kodi, Tanesco watauza umeme, Dawasco watauza maji kwani hiyo ndiyo njia ya kuijenga nchi,”

“Waziri wewe ni kijana nenda ukafanye kazi kwa manufaa ya nchi, na mimi ninawaomba mkatangaze mema ya nchi yetu kwani serukali ya Tanzania ya awamu ya tano inapenda wawekezaji ndio maana tumefuta kodi zaidi ya 54 na sio rahisi kufanya hivyo lakini tunafanya kwa kuangali mbele,” amesema.

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Marekani yamuwekea vikwazo waziri wa mambo ya nje wa Iran

0
0
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema leo kuwa uamuzi wa Marekani kumuekea vikwazo Mohammed Javad Zarif inaonyesha kuwa Marekani inamuogopa mwanadiplomasia huyo mkuu.

Katika hotuba ya moja kwa moja ya televisheni, Rouhani amesema Marekani wanaogopa mahojiano yanayofanywa na waziri wa Iran wa mambo ya nchi za kigeni. Akimaanisha mahojiano ya karibuni aliyoyafanya Zarif na vyombo vya habari vya kigeni mjini New York.

Rouhani amesema wakati akiwa ziarani katika mji wa kaskazini magharibi wa Tabriz kuwa uamuzi huo wa Marekani ni wa "kitoto” na kizuizi kwa diplomasia. Utawala wa Trump umemuwekea vikwazo Javad Zarif, na hivyo kumfungia kabisa mlango mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran.

Vikwazo hivyo vinazuia mali zozote za Zarif nchini Marekani au zinazodhibitiwa na makampuni ya Marekani. Serikali ya Washington imesema hatua hiyo itadhibiti safari zake za kimataifa.

Taarifa ya Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin imesema kuwa Zarif anatekeleza ajenda hatari ya kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, na yeye ndiye msemaji mkuu wa utawala wa Iran kote duniani. Marekani inatuma ujumbe wa wazi kwa utawala wa Iran kuwa tabia yake ya karibuni haikubaliki kamwe.

Zarif alijibu maramoja akiandika kwenye Twitter kuwa Marekani inajaribu kumyanyamazisha kwenye jukwaa la kimataifa. Akasema vikwazo alivyowekewa havitakuwa na athari yoyote kwake wala familia yake kwa sababu hana mali wala maslahi yoyote nje ya Iran.

Lakini katika ujumbe mwingine wa kukanganya kwa Tehran, Marekani imerefusha kwa siku 90, msamaha wake kwa miradi mitatu ya nyuklia kwa matumizi ya kiraia ili kuepuka kuzikasirisha nchi nyingine zilizosaini makubaliano ya nyuklia ya 2015, ambazo ni China, Urusi, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza.

Akizungumza jana, Zarif alisema Iran iko tayari kupunguza ahadi zake za mkataba wa nyuklia, kama washirika wa Ulaya hawatoilinda dhidi ya vikwazo vya Marekani kwa kuhakikisha kuwa inaweza kuuza mafuta na kupokea mapato.

Mbali na kujaribu kutwaa mali zake, Marekani pia itauminya uwezo wa Zarif kusafiri kimataifa kama mwanadiplomasia. Anatarajiwa kuendelea kuzuru Umoja wa Mataifa mjini New York, ijapokuwa chini ya udhibiti mkali.

Rais Magufuli: Atayakuja ataweza Kuyamaliza Haya?

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amezindua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jengo la tatu (Terminal 3), jijini Dar es salaam mradi ambao unagharimu zaidi ya Bilioni 720.

Akizumgumza kwenye uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema licha ya Serikali yake kutekeleza mradi huo, lakini hadhani kama watakaofuata  kwenye nafasi hiyo ya Urais wataweza kuyatimiza anayoyafanya, kwa kile alichokieleza amekuwa akisemwa mara kwa mara.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.

Waziri Ummy Aagiza Waajiri Kote Nchini Kutoa Likizo Ya Kunyonyesha Akina Mama Ndani Ya Siku 84 Kama Ilivyo Kwa Mujibu Wa Sheria.

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa  Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ametoa agizo kwa waajiri kote nchini kuendelea kuwapa likizo ya kunyonyesha  ndani ya siku 84   akina mama   mara wanapojifungua kama ilivyo kwa mujibu wa Sheria. 

Waziri Ummy ametoa maagizo hayo leo Agosti 1,2019  jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya  wiki ya unyonyeshaji duniani  ambayo yameanza Agosti 1 hadi 7,2019. 

Mhe.Ummy amesema mama aliyejifungua ana haki ya kupewa likizo ya siku 84 hivyo ni wajibu wa kila mwajiri kutoa likizo kwa waajiri na mwajiri anayekiuka maagizo hayo ni mwajiri adui wa wanawake na watoto wa Tanzania na serikali haitasita kumchukulia hatua kali za kisheria. 

Aidha,Waziri Ummy amefafanua mchanganuo wa likizo ambapo amesema mama aliyejifungua mtoto mmoja anapaswa kupewa likizo ya siku 84 na aliyejifungua mapacha anastahili kupata likizo ya siku 100 ,baba mzazi ana haki ya likizo ya siku tano huku pia akitoa tahadhari ya kuifuta sheria kwa akina baba kwani baadhi yao wamekuwa wakitumia mwanya huo kushinda baa na vijiweni badala ya kumsaidia mama.

Waziri Ummy ameongeza kuwa kanuni za utumiaji wa Maziwa ya watoto  ya kopo,maelekezo yanatakiwa  kwa lugha zote mbili Kishwahili na kiingereza ili mtu wa kijijini aelewe namna ya matumizi. 

Pia waziri Ummy amesema asilimia 31% ya watoto waliochini ya miaka 5 wamedumaa  kutokana na kukosa maziwa ya mama huku akitaja baadhi ya faida za unyonyeshaji kuwa ni pamoja na hali ya lishe kwa watoto kuwa nzuri,kuondoa uwezekano wa saratani ya matiti na uzazi kwa akina mama,kupungua udumavu na utapiamlo kwa watoto .

Kwa upange wake ,Mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto Duniani  [UNICEF]hapa nchini,James Gitau amesema asasi za kiraia zinapaswa kuendelea kutengeneza mazingira ya Unyonyeshaji katika maeneo ya kazi  huku akiishukuru serikali ya Tanzania  kwa kuendelea kuwawezesha wazazi  kwa kuwatengenezea mazingira rafiki ya unyonyeshaji   .

Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 1 hadi 7 ya kila  mwaka na kaulimbiu mwaka huu ni “Wawezeshe wazazi kufanikisha unyonyeshaji”huku takwimu zikionesha kuwa asilimia 97% ya watoto walio chini ya umri wa miaka 2 wananyonyeshwa maziwa ya Mama  na hali ya unyonyeshaji Tanzania ikipungua kwa asilimia 1% ambapo sawa na watoto elfu 20 hawanyonyeshwi.

Tanzania Yajiandaa Kupokea Ugeni Wa Kutoka Jumuiya Ya Nchi Wanachama Kusini Mwa Afrika (SADC).

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara  Profesa Joseph Buchweishaija amewataka watanzania wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho na maonyesho ya nne ya wiki ya Viwanda ya Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC) . 

Maadhimisho na Maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 8 Agosti 2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC); Viwanja vya Karimjee na Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Profesa Bucheishaija amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inawaalika wananchi kufika kwa wingi kwani tunatarajia jumla ya nchi  15 wanachama wa SADC zitashiriki,

Aidha, ameongeza kuwa wiki hii ya SADC itawawezesha wananchi kuona fursa mbalimbali ikiwemo kuweza kupata malighafi za kilimo ambazo viwanda utumia kuzalisha bidhaa za viwandani. Miongoni mwa faida watakazozipata watanzania kupitia maonesho ya Viwanda kwa nchi za Kusini mwa Afrika  ni pamoja na kujifunza au kubadilishana uzoefu na nchi nyingine za SADC ambazo zitashiriki katika maonesho hayo pamoja na kuongeza wigo wa masoko ya ndani na nje ya nchi.  


Nafasi imetolewa kwa kila mtanzania kujisajiri bado ipo mpaka tarehe 2 August, 2019 na wale ambao watakuwa hawajajisajiri  wasiwe na wasiwasi maana nao watatembelea maeneo ya maonesho kama wengine na kuweza kuona bidhaa za nchi nyinyine, hivyo watu wote wanakaribishwa sana kwa ajili ya tukio la kihistoria ambalo kutokea tena mpaka ipite miaka kumi na mitano. 


Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda  na Biashara  ndugu Ludovick Nduhiye ametoa ufafanuzi kuwa lengo kuu ni kuweka utayari kwa wananchi hususani kwa Tanzania  kuweza kushiriki kwa wingi na kuweza kujionea fursa lukuki ambazo zitaonekana katika maoshesho hayo.  

Aidha bwana Nduhiye amewakaribisha wananchi kufika kwa wingi lengo likiwa ni   kuangailia fursa muhimu zitakazopatikana kwenye wiki hiyo ya viwanda ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa masoko pamoja na ubadilishaji wa mawazo namna ya kuanzisha viwanda mbalimbali pamoja na kupata fursa mbalimbali kwenye nchi hizo za SADC. 

 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya maonesho na maadhimisho ya Wiki ya Viwanda kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara bwana Ally Gugu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mtengamano na Biashara amewahimiza wananchi kujisajili kupitia anuani zinazopatikana katika tovuti ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo ni www.mit.go.tz na kisha kubofya katika  linki mbili za  haraka (quick link) ambazo ni Usajili Wiki ya Viwanda na Usajili Mkutano wa 39 wa SADC. 

Gugu aliongezea kuwa haya maonesho ya viwanda ni  fursa ya watanzania wote kuanzia wajasiriamali wadogo, wajasiriamali wa kati pamoja na wenye viwanda vikubwa ili tuweze kutimiza azima ya Serikali ya awamu ya tano inayosisitiza maendeleo kupitia uchumi wa Viwanda  ili Tanzania iweze kufikia uchumi wa kati.

Rais Magufuli apiga ‘push-up’ Tena Dar

0
0
Rais  wa Tanzania, John Magufuli leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019 amepiga ‘push-up’ tisa kabla ya kuzindua jengo jipya la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, ilikuwa ni kawaida kumshuhudia Rais Magufuli akipiga ‘push-up’ katika mikutano yake mbalimbali hali iliyotafsiriwa kuwa yuko imara kuwatumikia Watanzania.

Leo amerudia tena wakati akiongoza viongozi walioketi meza kuu kwenda kuwatunza waimbaji wa bendi ya Tanzania One Theatre (TOT).

Alipofika mbele ya wanenguaji wa bendi hiyo alisimama mbele yao kupiga  ‘push-up’ tisa na kunyanyuka hali iliyoibua shangwe kwa waliohudhuria uzinduzi huo.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo

0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  0759208637   /  0620510598

Rais Magufuli: Tanzania Tunao Uwezo Wa Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Maendeleo

0
0
RAIS Dkt. John Magufuli amesema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini pasipo na kutegemea fedha zenye masharti zinazotolewa kutoka kwa wafadhili na wadau wa kimataifa wa maendeleo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la 3 la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi (Agosti 1, 2019), Rais Magufuli alisema uzinduzi wa Jengo la Uwanja huo ni ushahidi wa wazi wa usimamizi na nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali zinazotokana na kodi ya wananchi.

Aliongeza Jengo la Uwanja huo limejengwa kwa asilimia 100 kutokana na kodi za Watanzania, na hivyo kuiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) kusimamia vyema miundombinu ya Uwanja huo kwa kuhakikisha kuwa inatunzwa ili kuakisi vyema taswira ya Jiji la Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema jengo hilo litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya abiria Milioni 6 kwa mwaka limeigharimu Serikali kiasi cha Tsh Bilioni 722 ambazo ni fedha zilizotolewa na Serikali, limeweza kuifanya Serikali kuaminika na kuwa na udhubutu wa kutekeleza miradi ya Maendeleo kupitia fedha za ndani.

“Ipo miradi mingi ya Maendeleo tunayoisimamia kwa fedha zetu za ndani ikiwemo Ujenzi wa reli ya kisasa, mradi wa kufua umeme Mto Rufiji, Barabara za Juu Ubungo, Daraja la Kigongo-Busisi, Daraja la Salender, Ujenzi na ukarabati wa Viwanja vya ndege 15, kujenga rada 4 katika Viwanja vya Ndege vya Dar Salaam, Mwanza, Mbeya na Kilimanjaro, huu ni ushahidi wa usimamizi imara wa fedha zetu za ndani” alisema Rais Magufuli.

Aidha   Rais Magufuli alisema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya sekta ya anga nchini, kwa kuwa sekta hiyo imekuwa kiungo muhimu katika maendeleo ya sekta ya Utalii, kwani kila siku takribani watu Milioni 12 duniani hutumia usafiri wa anga kutokana na kuwa njia ya haraka na ya uhakika kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutoa kipaumbele kwa makampuni ya kitanzania yanapewa nafasi katika maduka yatakayofunguliwa ndani ya Uwanja huo ili kuwawezesha kufaidi matunda ya kodi yao sambamba na kuweza kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale alisema tangu mwaka 2004-2011 Serikali imechukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya majengo ya Uwanja wa ndege vyaJulius Nyerere ikiwemo ujenzi wa Jengo jipya la tatu la abiria katika uwanja huo, kutokana na majengo ya sasa ya jengo la I na II kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  uwezo mdogo wa kuhudumia abiria.

Anaongeza kuwa ujenzi wa Jengo hilo la tatu la abiria lilisimama ujenzi wake mwaka 2016 kutokana na mkandarasi kudai Tsh Bilioni 29, ambapo awali alishapokea kiasi cha Tsh Bilioni 380 kati ya Tsh Bilioni 560 zilizohitajika kwa ajili ya ukamlishaji wa jengo hilo hapo awali, lakini mwaka 2017 Serikali ilitoa zabuni ya ujenzi wa mradi huo kwa mkandarasi mwingine kutokana mkandarasi aliyepita kuwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mfugale alisema kutokana na kasoro zilizojitokeza, shughuli za ujenzi wa jengo hilo zilipelekwa kwa kampuni ya TECU na mshauri mwelekezi kampuni ya Arab Contractor ambapo hadi kufikia Mei 29 mwaka huu zilikamilisha ujenzi wa jengo hilo na kusubiri kukabidhiwa kwa Serikali kwa ajili ya kuanza kutumika kwake.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama alisema hadi kufikia sasa jumla ya makampuni 18 kati ya 23 ya kimataifa tayari yamehamishia shughuli zao katika Uwanja huo  kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za usafiri kwa abiria wanaosafiri kwenda nje ya nchi.

Aliongeza kuwa katika kuimarisha usimamizi bora wa Jengo la Uwanja huo, Mamlaka hiyo pia imewapatia mafunzo watumishi wake kwa ajili ya kupata uelewa wa pamoja wa namna bora ya kulinda miundombinu ya Uwanja huo na hadi sasa imepokea Tsh Milioni 500 kutoka Serikalini ilizozilipa kwa mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Kuhudumia Abiria Mil.8 Kwa Mwaka

0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere umeongeza idadi ya abiria watakaokuwa wakihudumiwa na Uwanja huo kutoka abiria milioni 2 mpaka abiria milioni 8 kwa mwaka. Ongezeko hilo limetokana na kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja huo lenye uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6 kwa mwaka.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa jengo la tatu la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

"Mradi huu umekamilika na umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 720. Kukamilika kwa mradi huu kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya fedha za Serikali na nidhamu ya kutumia fedha hizo," amesema Rais Magufuli.

 Rais Magufuli amesema asilimia 100 ya fedha za ujenzi wa jengo hilo ni fedha za Watanzania ambapo asilimia 15 imelipwa fedha taslimu na asilimia 85 imekopwa na itarejeshwa kupitia kodi.

"Watanzania tunaweza, tunachotakiwa ni kujiamini na kuamua kufanya. Bila kuamua Tanzania tutaendelea kuwa wategemezi katika miradi ya maendeleo ya nchi yetu," amesema Rais Magufuli.

Aidha, ameitaja miradi mingine inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutumia fedha za ndani kuwa ni mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji wenye thamani ya shilingi trilioni 6.5, daraja la Selander lenye thamani ya shilingi bilioni 270, ujenzi wa viwanja vya ndege 15 nchini vyenye thamani ya shilingi ya trilioni 1.868, ujenzi wa vituo vya afya 352, zahanati 30, hospitali 67 na ukarabati wa hospitali za zamani 21 wenye gharama ya shilingi bilioni 321.6 pamoja na  ujenzi wa barabara wa nchi nzima wenye jumla ya kilomita 2105 yenye gharama ya shilingi trilioni 5.37.

Miradi mingine ni ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi katika ziwa Victoria, barabara ya njia ya nane kutoka Kimara Dar es Salaam hadi Kibaha, ununuzi wa rada, utanuzi wa bandari ya Dar es Salaam, ununuzi wa vifaa vya hospitali pamoja ukarabati wa shule kongwe.

Rais Magufuli amesema kuwa, heshima ya miradi yote hiyo iwaendee Watanzania na kuwataka Watanzania kulifuta kabisa neno la kujiita masikini kwani Tanzania ni nchi tajiri.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema Jengo la pili la abiria nalo linahitaji kukarabatiwa na kuongezwa uwezo wa kubeba abiria mara mbili ya sasa, ambapo kwa sasa lina uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama amesema taasisi yake imeshahamishia shughuli za uendeshaji wa ndege katika Jengo hilo kutoka Jengo la abiria la pili.

Vile vile amesema, jumla ya vijana 130 kati ya vijana 241 waliokuwa wanahitajika wameajiriwa, ambapo kwa sasa wapo katika mafunzo ya nafasi walizopangiwa kufanya kazi.

Vile vile Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Patric Mfugale amesema ujenzi wa jengo la abiria la kwanza ulijengwa mwaka 1956 ambapo unauwezo wa kuhudumia abiria laki 5 kwa mwaka. Mwaka 1984 ilikamilisha ujenzi wa jengo la tatu la abiria ambalo linauwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka.

Amesema baada ya kuonekana jengo la pili la abiria kutotosheleza abiria wanaohudumiwa uwanjani hapo, ndipo Serikali ilipoamua kuanza ujenzi wa jengo la tatu la abiria, ambalo ni jengo la kisasa zaidi ukilinganisha na majengo yote ya abiria hapa nchini.

Maadhimisho Na Maonesho Ya Nne Ya Wiki Ya Viwanda Ya Jumuiya Ya Maendeleo Ya Kusini Mwa Afrika (SADC)

Makusanyo Ya Kodi Kwa Kipindi Cha Mwaka Wa Fedha 2018/19

0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya TZS 15.9 trilioni kati ya lengo la TZS 18 trilion kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kuanzia tarehe 1 Julai 2018 hadi 30 Juni 2019. Aidha katika robo ya nne ya mwaka huo wa fedha yaani, mwezi Machi hadi Juni 2019, TRA ilikusanya TZS 1.1 trilioni, TZS 1.2 trilioni, na TZS 1.5 trilioni kwa mwezi Aprili, Mei, na Juni, mtawalia. Kwa namna ya kipekee kabisa, TRA inawashukuru walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kwa ushirikiano.

Ikumbukwe kwamba, katika mwaka huo wa fedha, Serikali ilianzisha Mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) ambao utekelezaji wake umefanyika kwa awamu mbili (2). Awamu ya kwanza, ilihusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na aina zote za vileo. Awamu hii ya kwanza iliyoanza kutekelezwa tarehe 15 Januari 2019 imeendelea vizuri na maandalizi ya awamu ya pili ya utekelezaji wa ETS inayojumuisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi, na CD/DVDs yamekamilika. Hivo mfumo huu wa ETS kwa awamu hii ya pili, unatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 1 Agosti, 2019.

Lengo kuu la kubandika stempu hizi za kielektroniki ni kuongeza usimamizi na ufanisi wa ukusanyaji wa Ushuru wa bidhaa ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi za uzalishaji viwandani ili kukusanya mapato stahiki.  

Ni matumaini ya TRA kuwa, wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, wauzaji wote wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa pamoja, na umma kwa ujumla wataendelea 
kutoa ushirikiano kwa TRA ili kufanikisha utekelezaji wa mfumo huu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Richard M. Kayombo
KAIMU MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images