Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Asilimia 74.4% Ya Vijana Hawana Uelewa Wa Kutosha Kuhusu Fedha Za Maendeleo Ya Vijana Nchini.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Tafiti zinaonesha asilimia 74.4 hawana uelewa wa kutosha kuhusu fedha za maendeleo ya vijana nchini. 


Kati ya vijana  6,265 waliohojiwa wakati wa utafiti ni vijana 4,659 sawa na 74.4 hawana uelewa wa kutosha kuhusu fedha za maendeleo ya vijana yanaonesha kuwa kuna kiwango kidogo cha uelewa. 


Mratibu msaidizi wa mradi wa Restless Development Denice Simeo ameyasema hayo Jana  Julai 26,2019   alipokua akizungumza na wandishi wa habari kwenye ukumbi Lawate jijini Dodoma. 

Aidha Denice Simeo ametoa mapendekezo kupitia matokeo ya utafiti huu, ambapo amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya vijana ,wawekeze katika utoaji wa elimu.

Pia Vijana wametakiwa kujenga utamaduni wa kuhakiki vyanzo vya taarifa kabla ya kuzifanyia kazi hasa zile zinazowekwa  katika mitandao ya kijamii  ambapo   Simeo amesema  kupitia matokeo ya utafiti uliosimamiwa na kuongozwa na vijana  umebaini  kuwa mara nyingi vijana hupokea taarifa  bila kufanya uhakiki wa taarifa hizo. 


Hivyo utafiti huo ulitoa   mapendekezo kwa vijana kuwa ,taarifa ambazo zinatolewa wanatakiwa kutengeneza mazingira ya kuhakikisha na kujiridhisha kuwa yana uhakika kiasi gani ili kuweza kuchukua maamuzi yaliyo sahihi.

Hata hivyo Bw.Simeo amesema kuwa serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kama mashirika binafsi wanapaswa kusaidia kuboresha mfumo wa utoaji wa upatikanaji wa taarifa kuhusu fedha za miradi ya maendeleo ya vijana kwa makundi yote ya vijana ili kuwezesha uwepo wa taarifa za kutosha kwa walengwa. 


Taasisi ya Restless Development ilifanya utafiti juu ya jitihada za serikali katika kumuwezesha kijana kiuchumi, kwa kuangalia fedha za maendeleo ya vijana  zinazotengwa iwapo zinawafikia walengwa.

Utafiti huo ulilenga  kutathmini  jitihada za uwezeshaji wa vijana kiuchumi kupitia fesha za maendeleo na kuhusisha  halmashauri  nne ikiwemo Manispaa ya kinondoni ,Kigamboni ,Morogoro huku ikiwafikia vijana zaidi ya elfu sita.

Katika hatua nyingine,baadhi ya vijana wamesema kuwa ,mwitikio mdogo  wa kuomba mikopo unasababishwa na sababu mbalimbali zikiwemo woga wa kufanya biashara pamoja na elimu hafifu kwa vijana hao hivyo  kuna uhitaji mkubwa wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana.

Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya waziri mkuu, kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu na halmashauri zote nchini inafanya jitihada kubwa ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kutenga fedha n akuweka mazingira  rafiki kwa vijana ili kunufaika na fedha hizo na kujikwamua kiuchumi.

Wamiliki wa Viwanda Nchini Watakiwa Kukuza Uzalishaji Kukidhi Mahitaji ya Soko la SADC

$
0
0
Na Mwandishi wetu- MAELEZO
Serikali yawahakikishia wamiliki wa Viwanda nchini kuwa itaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayoimarisha ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kuweka  mipango mahususi ya kuongeza uzalishaji ili kuendana na mahitaji ya Masoko katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). 

Akizungumza na wamailiki hao leo  Julai 28, 2019 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amesema kuwa wamiliki hao wanapaswa kuendelea kukuza uwezo wa uzalishaji bidhaa ili kuendana na soko lililopo katika jumuiya hizo. 

“Tunayo kila sababu ya kuhakikisha kuwa Serikali na wamiliki wa Viwanda tunaweka mikakati ya pamoja Ili kuweka mazingira wezeshi yatakayokuza sekta ya viwanda hapa nchini”. Alisisistiza Mhe Bashungwa. 

Akifafanua amesema kuwa sekta ya Viwanda inasaidia kuzalisha ajira na kuchangia katika kuwezesha maendeleo endelevu kwa kuimarisha viwanda vilivyopo na vipya kwa maendeleo ya nchi yetu. 

Akizungumzia changamoto za sekta hiyo Mhe Bashungwa amesema kuwa jukumu la Serikali ni kuchukua changamoto za wamiliki wa Viwanda na kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka ili dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda itimie kwa wakati kwa maslahi mapana ya Taifa na wamiliki wa viwanda hivyo. 

“Serikali ya Awamu ya Tano na Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli inatoa kipaumbele katika kuhakikisha  kuwa dhana ya ujenzi wa Viwanda inatekelezwa kwa vitendo kwa kujenga mazingira wezeshi katika sekta hii muhimu kwa ujenzi wa viwanda” Alisisitiza Mhe.   Bashungwa. 

Mkutano wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Bashungwa umelenga kuimarisha sekta ya viwanda hapa nchini  kwa kuweka mikakakati itakayowawezesha kumudu ushindani wa bidhaa  kutoka za nje.
 

Azim Dewji ,waandishi Watatu Wanusurika Ajalini

$
0
0
Mfanyabiashara, Azim Dewji, na waandishi watatu wa vituo vya televisheni vya ITV,  Channel Ten na Azam TV wamepata ajali jana, Julai 27, 2019, asubuhi baada ya gari lao kuacha njia wakati wakiwa njiani kuelekea Rufiji kwenye sherehe za uwekaji jiwe la msingi la mradi mkubwa wa umeme wa MW 2,115 wa Rufiji mkoani Pwani.

Kwa sasa Azim Dewji amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha  mifupa (MOI) akipatiwa matibabu baada ya mfupa wake mmoja wa uti wa mgongo kuvunjika ajalini. Watu wote waliokuwa kwenye gari hilo wametoka salama.

Waziri Lugola Ataka Viongozi Wa Taasisi Zake Kuacha Kuwanyanyasa Askari, Watumishi Raia

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Ifakara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara yake nchini, kuacha tabia ya kuwanyanyasa askari waliochini yao na wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha za likizo.

Lugola amesema kuna idadi kubwa ya askari wanaostahili kupandishwa vyeo na kurekibishiwa mishahara, kwa kuwa Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli askari hao wana haki kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Askari na Watumishi wa Wizara yake, mjini Ifakara, Wilaya Kilombero, Mkoani Morogoro, leo, Lugola alisema katika uongozi wake hataki kusikia askari wananyanyaswa na kiongozi yeyote wa Taasisi zake.

Lugola alisema, unyanyasaji, kutokupandisha vyeo, pamoja na kulipwa fedha zao za likizo, changamoto hizo zinapunguza nguvu ya utendaji kazi wa askari hao wanaofanya kazi ngumu.

Waziri Lugola aliongeza kuwa, alitoa agizo la askari wanaostahili kupandishwa cheo, kurekebishiwa mishahara yao, wanaodai kulipwa fedha za uhamisho pamoja na changamoto mbalimbali zingine alizozielekeza.

 “Kwanini bado hamjapanda vyeo na kubadilishiwa mishahara yenu mpaka sasa wakati nilishatoa maelekezo mpandishwe, nitahakikisha nalifuatilia hili mapema zaidi ili nijue tatizo ni nini, lakini naamini kila kitu kinaenda vizuri na ahadi niliyoitoa itakamilisha kwa wale askari ambao wanasifa watapewa vyeo hivi karibuni,” Alisema Lugola.

Pia Lugola alizungumzia kuhusu ukosefu wa nyumba za makazi ya askari, kuwa licha ya Rais Dkt. John Magufuli anatoa mchango mkubwa kwa kulisaidia Jeshi, lakini bado kuna upungufu mkubwa wa nyumba hizo.

“Pamoja na fedha kidogo tunazopata lakini bado tuna tatizo la ukosefu wa makazi wa nyumba za askari, lakini bado Serikali inatafuta fedha ili kuhakikisha changamoto hiyo inaisha,” alisema Lugola.

Pia Lugola alisema changamoto nyingine inayowakabili askari wa vyombo vyake ni kutopata fedha za kuhamishwa na atahakikisha madai yote ya askari hao yanafanyiwa kazi.

Lugola alisema jambo ambalo linamuumiza kichwa ni kuhusu madai ya askari na watumishi wa wizara yake ambayo anasema kama wafanyakazi hawatalipwa haki zao na utendaji wa kazi utapungua.

Waziri Lugola yupo Mkoani Morogoro kikazi na tayari amemaliza ziara yake Wilaya ya Kilombero, na anatarajia kufanya ziara hiyo katika Wilaya za Malinyi na Ulanga Mkoani humo.

Ulinzi Kuimarishwa Katika Viwanja Vya Ndege Hapa Nchini

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Wizara ya Mambo ya Ndani nchini, itaongeza askari watu na mbwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye viwanja vya Ndege nchini.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Hamad Masauni amesema hayo alipofanya ziara ya kikazi katika Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB3).

Masauni amesema serikali inatarajia kuongeza askari mbwa wengi wenye mafunzo na sifa, ili kuongeza ufanisi na ulinzi wa viwanja vyote vya ndege.

“Idadi ya mbwa inatakiwa iongezwe hasa inapokaribia kuhamia kwenye jengo jipya la tatu la abiria, ambalo litakuwa na idadi kubwa ya abiria na changamoto nyingi, pia kwa viwanja vingine navyo vitaangaliwa kwa suala la ulinzi,” alisema Masauni

Hatahivyo, amesema hatasita kukifuta kitengo cha mbwa endapo hakutakuwa na mbwa wa kukidhi mahitaji na wenye sifa zote, kwani kwa sasa askari binadamu ni wengi zaidi.

Ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kuhakikisha mfumo na ushiriki wa askari wake unaweza kuboreshwa na wale wanapelekwa viwanja vya ndege wawe na sifa na vigezo maalum vya kuweze kubaini vitu kama nyara za serikali, madini na madawa ya kulevyia.

“Hii itasaidia kwa kuwa na mfumo wa pamoja wa ushirikiano katika udhibiti, jingine ni kuhakikisha IGP analisimamia na kulitekeleza kwa haraka sana, kwani tumekuwa na askari mbwa waliopata mafunzo maalum ya kubaini vitu mbalimbali vinavyopitishwa kwenye viwanja vya ndege, hivyo maelekezo yangu kwake tuongeze idadi ya mbwa wenye sifa hapa JNIA ili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema Masauni.

Masauni amefanya ziara hiyo siku moja baada ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kushughudia makabidhiano ya kilo 35.267 za dhahabu zilizokamatwa Februari 15, 2019 katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 28 July

Waziri Hasunga Aagiza Kukamatwa Mfanyabiashara Aliyeuza Mbegu Feki Wilayani Mbozi

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Mbozi Mhr John Palingo kumkamata mfanyabiashara aliyewauzia wakulima mbegu feki katika wilaya hiyo hivyo kuathiri mavuno kwa wakulima.

Waziri Hasunga ameyasema hayo wakati wa mikutano yake katika kijiji cha Isalalo, Wasa na Malolo vilivyopo katika kata ya Wasa kadhalika akiwa katika kijiji cha Msia, Weru 1 na Iganduka vilivyopo katika kata ya Msia.

Waziri huyo wa Kilimo Mhe Hasunga amesema kuwa kitendo cha mtu kuuza pembejeo feki ni cha uhujumu wa Kilimo na uchumi na kwamba serikali haiwezi kuvumilia hali hiyo.

"Katika hili namwagiza mkuu wa wilaya kumkamata msambazaji wa mbegu hizo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa" alisema Hasunga.

Kauli hiyo ameitoa kufuatia swali la mkulima mmoja mkazi wa Kijiji cha Malolo Ndg Isaya Nyondo ambaye alitaka kujua hatua zipi zinachukuliwa na serikali kufuatia kuuziwa mbegu feki na hivyo kufanya washindwe kuvuna mwaka huu.

Mhe Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kuimarisha sekta ya Kilimo hivyo mfanyabiashara yeyote anayecheza na ufanisi wa wakulima atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Homa ya Dengue Yaua Watu 13

$
0
0
Serikali  imesema homa ya dengue imeua watu 13 nchini huku 6,677 wakiugua ugonjwa huo.

Takwimu hizo zimetolewa jana Jumamosi Julai 27, 2019 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa kupambana na mbu na wadudu wengineo katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Waziri Ummy alisema awali takwimu zilionyesha vifo sita  lakini Serikali ilifanya tathmini upya na kupata takwimu sahihi..

Alisema ugonjwa huo kwa sasa unapungua kwa maelezo kuwa Juni, 2019 kulikuwa na wagonjwa 536 na tangu kuanzia Julai hadi leo kuna wagonjwa sita pekee.

Mbatia Aipa Ushauri Serikali Kuhusu Uwekezaji na Mifumo ya Kikodi

$
0
0
Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia  ametoa tahadhali kwa Serikali akishauri hatua kadhaa zifanyike kabla ya kufanyika mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Mkutano huo utafanyika Tanzania Agosti 17 na 18 mwaka 2019 ukitanguliwa na mikutano mbalimbali pamoja na Maonyesho ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC chini ya kauli mbiu ya Mazingira Wezeshi ya Kibiashara kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu ya Viwanda.

Katika hotuba yake wakati wa Mkutano Mkuu wa NCCR Mageuzi kwa ajili ya kuchagua viongozi wapya wa chama hicho jana Jumamosi Julai 27,2019, Mbati ambaye ni Mbunge wa Vunjo aliitaka Serikali ifanye uchambuzi kwa kuangalia uamuzi wake katika maeneo mbalimbali yanayoonekana kuwa kikwazo katika mtangamano huo.

“Tanzania ni sehemu nzuri ya kujenga ubia, mazingira mazuri ya kibiashara lakini Serikali yetu waangalie namna ya kufanya uamuzi katika masuala ya kikodi, mifumo endelevu ya kikodi, kodi zinazotabirika, mazingira rafiki ya uwekezaji, mazingira ya kuvutia, mazingira yasiyo na vikwazo ili kuchochea ukuaji wa uchumi kulingana na kasi ya mabadiliko ya Kiuchumi duniani,” alisema Mbatia.

“Wakubali au wakatae, hata wangefunga masikio yao, sekta binafsi ndiyo msingi wa uchumi wa Taifa, huo ndiyo ukweli wa leo, tuwajenge mazingira rafiki, tusiwabeze.”

Mamia ya waandamanaji wakamatwa Urusi

$
0
0
Polisi mjini Moscow Urusi wamewakamata takriban watu 1000 waliokuwa wakiandamana kushinikiza uchaguzi wa mitaa ufanyike kwa njia ya uhuru na haki.

Takriban watu 3,500 walishiriki kwenye maandamano hayo ambayo hayakuruhusiwa na maafisa wa serikali.

Waandishi wa habari wa shirika la AFP waliokuwepo eneo hilo wamesema polisi walitumia vigongo na mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji.

Maandamano ya jana yalijiri, wiki moja tu baada ya maandamano makubwa kufanyika mjini Moscow ambapo waandamanaji 22,000 waliwataka maafisa kubadilisha uamuzi na wawaruhusu wanaharakati wa upinzani kugombea viti kwenye uchaguzi wa mji utakaofanyika mwezi Septemba.

Tangu uamuzi huo ulipotolewa, wachunguzi wamekuwa wakifanya msako majumbani na katika makao makuu ya wagombea waliokataliwa, huku mkosoaji mkubwa wa serikali Alexei Navalny akifungwa jela kwa siku 30 kwa kuitisha maandamano mapya.

Waombolezaji 23 wauawa na Boko Haram kwenye matanga

$
0
0
Wanamgambo wa Boko Haram, wamewaua waombolezaji 23 katika jimbo linalokumbwa na machafuko la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria. 

Wakaazi wamesema kuwa wanamgambo hao waliwashambulia waombolezaji waliohudhuria matanga katika eneo hilo. 

Kiongozi mmoja wa kundi la wanamgambo Bunu Bukar Mustapha, ameeleza kuwa washambulizi waliokuwa kwenye pikipiki waliwafyatulia risasi kundi la wanaume waliokuwa wakitembea wakitoka kwenye matanga wilaya ya Ngazai karibu na mji wa Maidiguri.

 Mustapha ameliambia shirika la habari la AFP kuwa walipata miili 23 kwenye eneo la mkasa huo uliotokea jana Jumamosi. 

Afisa wa wilaya ya Nganzai amethibitisha mkasa huo pamoja na idadi ya waliouawa.

Video Mpya ya MwanaFA - We Endelea Tu

$
0
0
Video Mpya ya  MwanaFA - We Endelea Tu

Spika Mstaafu Anne Makinda Atoa Ushauri kwa Madiwani Wanawake

$
0
0
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, amewataka wabunge na Mdiwani wa vitimaalum nchini kusimamia kikamilifu rasilimali za umma ili ziwanufaishe wananchi wote.

Akizungumza Jijini Mwanza katika semina ya kujenga uwezo kwa viongozi wanawake wa serikali za Mitaa (WASEMI) iliyoandaliwa na shirika la TGNP Mtandao, Makinda alisema kwamba, mchango wa wabunge na madiwani wa viti maalum umekuwa hauonekani vizuri au kutambuliwa na jamii kutokana na wao wenyewe kuwa na hofu au kutokujiamini kitu ambacho kimechangia kuwarudisha nyuma na kushindwa kuendelea mbele.

“Tatizo letu sisi viongozi Wanawake, tunajenga hofu, tunaogopa sana kujitokeza na kuwajibika vizuri kwa wananchi, eti kwa sababu ni viti maalum. Sisi tulianzia pia viti maalum , lakini tulipata nafasi ya kwenda jimboni kwasababu tulijiamini, tuliwajibika kikamilifu na tulihangakikisha uwezo wetu unaonekana na kila mmoja. Jitokeze, kwa wananchi, watumikie kwa uadilifu na watakuona na kutambua mchango wako” alisema Makinda

Makinda amewaasa wanawake viongozi wa serikali za Mitaa, kuhakikisha wanasimamia ubora wa huduma za jamii kwenye halmashauri zao na kuhakikisha kila kinachofanyika kwenye halmashauri wanakielewa vizuri na kutoa taarifa kwa wananchi wote.

Ufugaji wa nguruwe : Gharama na Faida Zake

$
0
0
 Utangulizi
Nguruwe ni mnyama amabaye hutumika kama chakula / mboga na pia ni zao la biashara kwa mfugaji, mjasirimali na mfanyabiashara.
 
NGURUWE HUTEGEMEA SANA MAMBO YAFATAYO
1 . Banda imara na rafiki kwake
2. Usafi ni muhimu sana katika banda la Nguruwe
3 Mchaganyo bora wa chakula
4. Tiba bora na kinga
5. Maji na Lishe ( access ya vyakula Muhimu kwake )
 
CHANGAMOTO
KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE KUNACHAGAMOTO ZAKE LAKINI ZAWEZA KUTATULIWA KWA KUFATA MAMBO KADHAA.
Katika ufugaji wa nguruwe kunachagamoto ya vifo vya nguruwe wachanga ambao hupunguza faida ya biashara ya nguruwe kwa kupunguza idadi ya nguruwe wazima wa kuuzwa lakini utunzaji mzuri wa nguruwe wachanga huepusha vifo vinavyotokana na shida kama:
 
Matatizo ya kupumua
Ni kifo kinachosababishwa na mama anapomlalia nguruwe mchanga.chagamoto hii inaweza kutatuliwa kwa kuwatenga au kuwa na mabanda makubwa ya kulelea watoto.
 
Baridi
Nguruwe wachanga huathiriwa na baridi haswa katika majuma mawili au matatu ya mwanzo. Hii ni kwa kuwa wana kiwango kidogo cha utando wa mafuta wa kuwakinga.
 
Unashuriwa kuwaweka katika hali ya joto, wape matandiko na utumie vipasha joto kama vile kuwasha globu za joto kama utakuwa umewaweka kwenye mabanda ya kuta au nyumba yenye sakafu baridi.
 
Namna bora utunzaji wa nguruwe wachanga
Nguruwe moja wa kike ana uwezo wa kuzaa watoto 12. Namna ifuatayo itasaidia kupunguza idadi ya vifo vya nguruwe wachanga:
1.Pale nguruwe awapo na kidonda nyunyizia dawa ya ayodini 5% kwenye kovu ili kuzuia kuambukizwa kwa magonjwa.
2.Wawekee matandiko (nyasi kavu au maganda ya miti) mahali pa mapumziko ili wapate joto au utumie globu za joto.
3Wadunge sindano ya madini ya chuma (iron) siku ya tatu baada ya kuzaliwa ili kuzuia upungufu wa damu.
3. Yalainishe meno ya vichaga kabla ya masaa 24 ili kuzuia uharibifu wa matiti wakati wanaponyonya.
4. Watie vibandiko au utoboe masikio ili uwatambue na uhifadhi rekodi zao kama kuna umuhimu kama vile wafanyavyo wafugaji wa ng’ombe.
5. Wapime uzani wanapozaliwa na uhifadhi rekodi hiyo itakusaidia kujua ukuaji wao na maendeleo yao
6. Wahasi wale wa kiume juma la tatu, wale ambao hawafai katika kuendeleza kizazi kwa kutumia mtindo wazi (open method) kama unaona inafaa.
7. Wapatie dawa ya kuzuia minyoo pia zipo dawa za asili kama unga wa mkaa na majivu pia zipo za kitaalamu, wasiliana na wataalamu wa mifugo
8.Waachishe kunyonya katika juma la nane au wafikapo kilo 14 hadi 20 hii itasaidia kujitegemea na kukua kwa haraka.
 
Nguruwe Walioachishwa Kunyonya
1.Walioachishwa kunyonya wawekwe makundi ya 10 hadi 12 kulingana na uzito au ukubwa wao kwenye eneo ambalo watajitosheleza.
2.Watenganishe wakubwa kwa wadogo ili kuzuia kupigana.
3.Wakati wa kuwaachisha kunyonya mwondoe mama yao kutoka kwa watoto ili kupunguza usumbufu.
4Watoto wa nguruwe wa mama tofauti wasiwekwe pamoja maana hii husababisha mapigano kati yao na
5.Unapowachanganya watoto wa mama tofauti wapake mafuta ya gari yaliyotumika kwenye ngozi yao au mafuta ya kula ili kuiondoa harufu ya kutambulika ili wasipigane
 
FAIDA YA UFUGAJI WA NGURUWE
Faida kuu ya nguruwe ni zao la chakula lakini pia ni zao la kukuongezea kipato ukiwa kama mjasirimali / mfanyabiashara.
Lengo langu nikueleza namna unavyoweza kufuga na kutupa faida, Steps zifatazo ni muhimu kuzigatia.
 
JIPE MTAJI WA MILLION 4 / 3.5 KWA NGURUWE 50
UANDAAJI WA BADA WEKA MAKADILIO YA LAKI TANO (800,000/=) .
Hapo nazugumzia banda lenye heru U yenye mstatili ikiwa na kitako kirefu
Eneo lenye ukubwa wa mita 50 kwa 50 litafaa zaidi ili kuhakikisha usalama wa nguruwe wako na ukuaji bora.
1. Tafuta mabati used kwa bei ya 5000 mfano mabati 20 ya futi 10 /10 = 100,000/=
2. Tafuta mabazi ya futi 10 kwa 2000 kila moja utapata mabazi pic 100 = 200,000/=
3. Tafuta miti ya nguzo na kechi ya 1000 na 2000 miti ya 1000*70 na 2000*3 = 120,000/=
4. Tafuta chagalawe / moramu trip 10*3000 =30000/=
5. Cement mifuko kwa ajiri ya sakafu na mashimo ya kulishia 5 *18000 = 90,000/=
6. Misumari ya aina 4, nch 6 kg5,nch 3 kg5 nch 5 kg10 na nch4 kg10, Bawaba na komeo =100,000/=
7. Malipo ya fundi 75000 fundi uashi na 75000 fundi seremala =150,000
JUMLA HAPO INAKUWA 790,000/= MAKADILIO INAKUWA 800,000/=
 
UNUNUZI WA NGURUWE WA KUANZIA .
Nguruwe wadogo wadogo ni vinzuri zaidi kuanza nao kwa sababu watakuzalia watoto wengi na kwa muda mrefu . Chukua mfano MILLION 2.5 . Nguruwe wadogo wa dogo wanauzwa 50000 au 40000 inategemeana na mahala na maelewano . Milioni 2.5 inakupa vitoto 50 au 55 . Hivyo unawexa kuwa na vitoto jike 50 na vidume 5. baadaye ukaongeza madume matano ya kuazima au kukondi kwa ajiri ya kupandishia
 
MAANDALIZI YA CHAKULA
Mchaganyiko wa chakula cha nguruwe na gharama zake tunaweza ukadilia kujitosheleza kwa laki tatu kwa mwenzi mmoja kwa nguruwe hao 50, kwa 300,000/= , ambapo itajumuisha tiba / kinga, lishe, vyakula vya nguruwe vinaweza kuwa pumba ya mpunga ile laini,pumba ya mahindi, mashundu, mabaki ya magada ya vianzi amba mabaki ya chakula yaliyosalama
 
MALIPO YA MSIMAMIZI NA ENEO LA KUWEKEZA
Katika kipengele hiki makadilio ya juu ama ya chini kwa msimamizi wa kazi yako waweza mlipa 100,000/= ama chini yake pia kwa mwenye eneo huwa nimaelewano tu aunaweza pata kwa fair au kukakodi kwa laki tatu, 300,000/= kwa mika miwili.
 
HIVYO JUMLA YOTE YA GHARAMA ZA UAZISHAJI UWEKEZAJI WA NGURUWE 50 ZITAKUGHARIMU MILLION 4 AMA MILLION 3.5 KWA MAANA KUWA HAPO JUU NIMETUMIA MAKADILIO YA JUU NA UKIINGIA KWENYE UHALISIA KAMA MJASIRIMALI LAZIMA IPUNGUE NA KUFIKIA 3.5

KIPATO AU FAIDA YA UFUGAJI NGURUWE
Nguruwe wanafaida ya haraka na nimradi wa uhakika kabisa, ukipitiia mchanganuo hapo juu wa nguruwe 50 utatupa faida kama ifatavyo
 
Nguruwe huzaa Mara mbili kwa mwaka na huzaa watoto zaidi ya watanoyaani huzaa watoto 12 ama nane .
Basi chukua nguruwe 50 * vitoto 5 yaani ufanye kuwa nguruwe wako 50 wakupatie vitoto vitano vya uhakika
Nguruwe 50*5 = 250 ukijumlisha na wale 50 wa mtaji umakuwa nao 300 . Chukua zao la nguruwe la 250 na uza kwa 200000 kwa kila nguruwe yaan bei ya kawaida kabisa. Utapata Million 50.

Hivyo zao la kwanza ndani ya robo tatu ya mwaka inakutegenezea million 50 pia na mienzi sita ijayo inakupa tena 50 na zaidi ili kukamilisha uzao wa pili hii inkupa uhakika wa kutegeneza million 100 za uakakika ndani ya mwaka mmoja na nusu ama miaka miwili ukijipa timeframe work lakini kumbuka hapo tumefanya kwa hesabu ya uzao wa chini kabisa ambapo tumeangalia na hasara ya vifo kama vifo visipotokea na uzao ukawa mkubwa utakuwa na uhakika wa kutegeneza million 150 kwa miaka miwili.

Kwenye hesabu ya kuwale unaweza kuwaza sana kuwa itaongezeka na kukughalimu sana jibu ni hapana mpka kufikia kuuza hawatokugharimu zaidi ya million 7 je million 7 kwenye million 150 ni kitu kisicho nafaida ?
 
NB . jambo lolote linahitaji umakini naa dhamira ya dhati pia kushirikisha wataalamu na wenye uzoefu ili kufikia leng Ewe ndugu kila kitu kinawezekana UTAYARI WAKO / UTHUBUTU WAKO, UAMINIFU .NA MAAMZI YAKO.
 

Waziri Mkuu Majaliwa Apokea Vifaa Vya Hospitali Na Shule Kutoka Taasisi Ya Helping Hand Na Benki Ya NMB

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa vifaa mbalimbali kutoka benki ya NMB vyenye thamani ya sh. milioni 25.

Vifaa hivyo ni fremu 46 za madirisha ya alminium na vioo vyake, milango 18, mabati 56, misumari na mbao, kompyuta 10, madaftari 4,050 vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 25/-.

Akipokea msaada huo leo mchana (Jumapili, Julai 28, 2019) kwenye zahanati ya Nandagala, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Waziri Mkuu amewashukuru viongozi wa benki hiyo kwa kuamua kuchangia vifaa hivyo.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nandagala, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, amesema mchango uliotolewa unamaanisha kazi ya kukamilisha jengo la wodi ya wagonjwa na vyumba vya madaktari ni lazima ifanyike haraka.

“Tunamshukuru Mkurugenzi Mkuu wa NMB kwa msaada huu mkubwa. Hii maana yake ni kwamba ni lazima tuharakishe kukamilisha jengohili ili tuanze kutoa huduma kwa wananchi wa Nandagala na wa vijiji vya jirani,” alisema.

“Tulianza na ujenzi wa zahanati kisha tukajenga jengo la upasuaji lenye wodi mbili. Moja ya wanaume na nyingine ya wanawake ambazo kila moja ina uwezo wa kulaza wagonjwa 20 kwa wakati mmoja.”

Jengo hili jipya ambalo tumelianza ujenzi wake, likikamilika litakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 60. Pia kuna jengo lenye vyumba vya madaktari, vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia.

Waziri Mkuu aliwataka wakazi hao wafikirie uwezekano wa kujenga wodi nyingine na pamoja na jiko ili wagonjwa watakaokuwa wanalazwa hapo, wapate mahali pa kupikiwa chakula.

Mapema, akitoa taarifa ya msaada huo, Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali katika benki ya NMB, Bi. Vicky Bishubo alisema kipaumbele cha benki hiyo kila mara ni kutatua changamoto za afya na elimu kwani sekta hizo ni nguzo kuu ya maendeleo kwa Taifa lolote.

“Vitu hivi (mabati, madirisha ya aluminium, kompyuta na madaftari) tunavyokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata,” alisema.

Alisema kwa mwaka huu, NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu. “Mpaka ninavyoongea leo, tayari tumetoa misaada yenye thamani ya zaidi ya millioni 600 kwa mwaka huu wa 2019 tu,” alisema.

Akielezea kuhusu programu ya WAJIBU, Bi. Bishubo alisema hadi sasa wameshawafikia vijana wasiopungua 42,000 katika shule za msingi na sekondari kwa kuwapa elimu ya fedha na kujifunza kuweka akiba katika umri mdogo kupitia programu yake ya ‘Jifunze, Jipange na Wajibika’ (WAJIBU).

“NMB imekuwa ikiwawezesha vijana kupata elimu ya fedha katika shule za msingi na sekondari Tanzania. Elimu hii ya fedha kwa vijana hutolewa na wafanyakazi wetu wa benki kwenye shule zilizopo karibu na benki ikilenga kuwafundisha vijana umuhimu wa kuweka akiba na mipango kwa ajili ya maendeleo yao na kukidhi mahitaji ya muhimu,” alisema.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Nandagala, Bw. Andrew Chikongwe aliishukuru benki hiyo kwa kuwasaidia vifaa hivyo ambavyo alisema vimefika kwa wakati muafaka. “Majengo yalikwishakamilika, yakabakia madirisha na milango, pamoja na vifaatiba, kwa hiyo sasa hivi tunaweza kuendelea na ujenzi,” alisema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Lugola Amtumbua Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), Charles Bukombe

$
0
0
Waziri  wa Mambo ya ndani Ya Nchi  Kangi Lugola amemuondoa madarakani Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), Charles Bukombe na ameagiza achukuliwe hatua kali za kisheria kwa kutokufuata maagizo anayoyatoa na kuyaita yakisiasa. Na pia ametoa onyo kali kwa Ma-RTO wa Mkoa wa Morogoro na Mara.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Julai 28, 2019 na ofisi ya mawasiliano ya wizara hiyo imeeleza kuwa licha ya kumuondoa katika nafasi hiyo,  Lugola amemuagiza katibu mkuu wa wizara yake, kumchukulia hatua  za kinidhamu  RTO huyo ili iwe fundisho kwa trafiki.

Lugola amesema amemshuhudia Bukombe katika video inayosambaa mitandaoni alipokuwa katika mkutano jijini Arusha, akipinga maagizo yake na kuyaita ya kisiasa na hakuyatekeleza.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Malinyi mkoani Morogoro leo Lugola amesema hatoi maagizo ya kisiasa, hutuo yanayomsaidia Rais John Magufuli katika kazi zake.

Uingereza yapendekeza jeshi la Ulaya katika Ghuba ya Uajemi

$
0
0
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema uwepo wa vikosi vya kigeni katika eneo hilo hautasaidia chochote bali hatua hiyo itasababisha mvutano. Rais Rouhani, ameongeza kusema kuwa Iran na Oman ndio zenye jukumu la msingi la kulinda eneo muhimu la pwani ya Hormuz.

Iran pia imesisitiza kuwa hali mbaya na mivutano ya sasa katika Mashariki ya Kati inatokana na kujiondoa kwa Marekani katika mpango wa nyuklia wa mwaka 2015 (JCPOA), uliofikiwa kati ya Iran na mataifa yenye nguvu.

Uingereza ilisema Jumatatu kuwa inajiandaa kuzindua kikosi kitakachoongozwa na nchi za Ulaya kujibu hatua ya Iran ya kuikamata meli ya mafuta iliyokuwa na bendera ya Uingereza mnamo Julai 19.

Kikosi maalum cha kijeshi cha Iran (IRGC) kiliikamata meli iitwayo Stena Impero katika bahari ya Hormuz baada ya kudai kwamba meli hiyo ilikaidi kujibu wito wa dharura na kuzima mawasiliano yake ya radio baada ya kuigonga mashua ya uvuvi.

Serikali ya Uingereza imekosolewa kwamba haikuchukua hatua madhubuti ya kulinda meli zake.

Ni wiki mbili sasa tangu kukamatwa meli ya Uingereza – ‘'Stena Impero'' ambapo hali hiyo imejitokeza baada ya kikosi cha wanamaji wa Uingereza kuitia nguvuni meli ya Iran ‘'Grace 1'' katika pwani ya Gibraltar kwa madai kwamba ilikuwa inasafirisha mafuta kwenda Syria hatua ambayo inakiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya.

Merikani imesema itaongeza uwepo wa majeshi yake katika eneo hilo ili kufuatilia shughuli za Iran. Lakini Iran imesema inaamini nchi za Mashariki ya Kati ndio zinapaswa kuhakikisha usalama wa meli zinazopita kwenye bahari ya Hormuz.

Mahusiano kati ya Iran na Marekani yanayumba tangu Rais Donald Trump aachane na mpango wa nyuklia wa mwaka 2015 na kuiwekea tena Iran vikwazo kwenye shughuli za usafirishaji wake wa mafuta.

Siku ya Jumapili, Wolfgang Ischinger, balozi wa zamani wa Ujerumani nchini Marekani ambaye sasa ni mkuu wa Mkutano wa Usalama wa Munich, amesema anataka jeshi la Ujerumani lihusike zaidi kwenye eneo la Ghuba. 

Ischinger amesema Ujerumani haifai kuangalia yanayotokea kutoka pemben na hasa ikiwa nchi zingine zinajadili kuhusu kuunda kikosi kujihami katika Ghuba.

Serikali ya Ujerumani bado haijaamua iwapo itashiriki. Waziri wa Ulinzi Annegret Kramp-Karrenbauer ametoa maoni kwamba Ujerumani inaweza kushiriki katika kuundwa kikosi cha jeshi kilichopendekezwa na Uingereza. 

Waziri wa Mambo ya nje Heiko Maas amesema hata hivyo mipango hiyo bado ipo kwenye hatua za mwanzoni.

Iran Yasema inania ya kuanzisha shughuli katika kinu cha nyuklia cha Arak.

$
0
0
Mkuu wa shirika la nishati ya Atomiki la Iran Ali Akbar Salehi amewaambia wabunge wa taifa hilo kwamba nchi hiyo, itaanzisha tena shughuli zake katika kinu cha nyuklia cha Arak. 

Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la habari la ISNA nchini humo. Shirika hilo lilimnukuu mbunge aliyekuwepo katika mkutano huo. Maji mazito yanaweza kutumika katika kinu hicho kuzalisha kemikali ya Pluto-nium inayotumika kutengeneza silaha za nyuklia. 

Mwezi Mei Iran ilitangaza kukiuka makubaliano ya nyuklia na mataifa makubwa duniani, kufuatia Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vipya. 

Mnamo Julai tarehe tatu rais wa Iran Hassan Rouhani alisema Iran itaongeza urutubishaji wa madini yake na kuanza kukifufua tena kinu chake cha nyuklia cha Arak Julai 7, iwapo mataifa yaliyotia saini mkataba wa nyuklia hayatolinda biashara na Iran kama yalivyosema makubaliano hayo.

Zitto kabwe Amtaka Waziri Jaffo Kusimamia Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Kwa Haki

$
0
0
Kiongozi wa Chama Cha ACT- wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh.Zitto Kabwe, amemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Mh.Selemani Jafo kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa mujibu na taratibu zilizowekwa pasipo kukiuka utaratibu ili wananchi waweze kumchagua kiongozi wao ambaye watamchagua.

"Natoa wito kwa Waziri wa Tamisemi, Jafo ahakikishe kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika kwa uhuru na haki. Tunataka wananchi wakachague viongozi wanaowataka na siyo kuvuruga uchaguzi, hilo hatutakubali," amesema Zitto.

Ameyasema hayo leo akiwa anafungua matawi 10 ya chama hicho akisindikizwa na mshaurii wa chama hicho Bw. Seif Sharif Hamad pamoja na viongozi wengine wa chama hicho katika kata ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa mkakati ambao wameupanga ni kuhakikisha masuala ya haki na uchumi unakuwa katika hali ya kuridhisha hapa nchini.

Aidha Zitto amesema kuwa lengo ni kuhakikisha kata ya Vingunguti kuongozwa na viongozi wa ACT-Wazalendo hivyo ameviomba vyama na visitumie mabavu katika Uchaguzi ujao ili kuweza kutenda haki kwa wapiga kura na wananchi kwa ujumla pasipo bughudha

Kwa upande wake, Maalim Seif amewataka vijana kusimama imara katika kutetea demokrasia hapa nchini kwa sababu wao ndiyo nguvu kazi ya Taifa hili na wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka.

Mwanasiasa huyo mkongwe amewataka vijana kufikiria kesho yao kwa kuleta mabadiliko chanya ambayo yataleta maendeleo katika Taifa hili. Amewataka wawe jasiri kupigania demokrasia na maendeleo ya nchi yao.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu 29 July

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images