Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli achangia Milioni 400 za ujenzi kituo cha afya Morogoro

$
0
0
Rais Magufuli ameahidi kutoa Sh400 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Kisaki kilichopo mkoani Morogoro huku akiwataka wakazi eneo hilo kuchapa kazi.

Magufuli ametoa ahadi  hiyo jana  Alhamisi Julai 25, 2019 wakati akizungumza na wananchi eneo la Kisaki lililopo katika halmashauri ya Morogoro vijijini huku akitoa agizo kwa mawaziri wake, Ummy Mwalimu (afya) na Seleman Jafo wa Tamisemi kuhakikisha wanasimamia ujenzi huo haraka.

Rais Magufuli alifikia uamuzi huo, baada ya wakazi hao kumweleza hawana kituo cha afya katika eneo hilo.

“Kwanini  hakuna kituo cha afya na kuna watu wengi hapa? Nataka kituo cha afya kianze kujengwe mara moja nitamuagiza Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) ashughulikie.”

“Nawapa siku saba tafuteni eneo, tujenge hospitali ambayo imejengwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk John Magufuli,” alisema Magufuli huku akishangaliwa na umati wa wakazi wa Kisaki waliojitokeza kumsikiliza.

LIVE: Rais Magufuli Akizindua Mradi Wa Stiglers Gorge

$
0
0
LIVE: Rais Magufuli Akizindua Mradi Wa Stiglers Gorge

Raia wa Hungary Afikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya

$
0
0
Raia wa Hungary Akos Berger (28), amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu  250  aina ya Amphetamine.

Berger amefikishwa mahakamani hapo  Juali 25,2019 na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Maira Kasonde.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai,  Julai 19 mwaka huu, eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu  Kasonde alimtaka mshitakiwa kutojibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya dawa za kulevya, isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa DPP

Upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilka na kesi iliahirishwa hadi Agosti 9 mwaka huu itakapotajwa.

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Mikanda miwili ya video yenye ushahidi yawasilishwa kesi ya Freeman Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea kielelezo cha Kamera ya kurekodia video na tepu mbili kwa ajili ya kutumika katika ushahidi wa kesi ya uchochezi inayowakabili Viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.

Hakimu Simba amesema kuwa Kifungu cha 18 cha sheria ya ushahidi wa kieletroniki kimeweka vigezo vya upokeaji wa vielelezo vya eletroniki ambavyo shahidi namba sita Koplo Charles alikidhi.

Kielelezo hicho kilitolewa na shahidi wa sita katika kesi hiyo, Koplo Charles.

Alidai saa 10 alasiri watu walianza kukusanyika katika Uwanja wa Buibui na mshereheshaji alitangaza kwamba viongozi wakuu wa chama wameshafika na baada ya muda wabunge na viongozi wakuu walipanda jukwaani na alimsikia Mbowe akitoa kauli za kufanya hamasa ya kuichukia Serikali.

Koplo Charles aliomba kutoa vifaa hivyo kama kielelezo, upande wa utetezi walipinga, lakini katika uamuzi wa mahakama vielelezo hivyo vimepokewa.
 
Mbali ya Mbowe, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, Katibu Mkuu, Vicent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa – Zanzibar, Salimu Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi na 16, mwaka huu wakiwa Kinondoni, Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama na wengine ambao hawapo mahakamani ya kutenda kosa la jinai, ikiwamo kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi wa uasi.

Masauni: Ni Aibu Kubwa Sana Madini Kutoroshwa Nchini na Kisha Kukamatwa na Nchi Jirani

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amesema ni aibu kusikia nyara za Serikali ikiwamo madini zinatoroshwa na kukamatiwa nchi za jirani na kuagiza ulinzi wa kutosha katika viwanja vya ndege nchini.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kupokea dhahabu kutoka Kenya, ambayo ilitoroshwa nchini kupitia viwanja vya ndege vya Mwanza na Kilimanjaro na kukamatiwa Nairobi, Kenya.

Akipokea dhahabu hiyo juzi, Rais Magufuli alisifu vyombo vya ulinzi vya Kenya huku akieleza kusikitishwa na vya Tanzania kushindwa kukamata.

Masauni jana mara baada ya kukagua usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, alisema kupokea madini ya dhahabu kutoka Kenya kumemuhuzunisha yeye na Rais Magufuli.

Alisema jambo hilo halitavumiliwa kuendelea, ni lazima jitihada za makusudi zichukuliwe na ndiyo maana ameanza kukagua usalama wa viwanja huku akiwataka Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Polisi wafanye kazi kwa pamoja.

“Hatua ya jana (juzi) ya Rais imeshtua sana na kuna haja ya kufanya kazi kwa muunganiko mkubwa kati ya Jeshi la Polisi, TRA, TAA ili kuhakikisha kunakuwa na usalama.

“Nimekagua kwa kuanza na huu uwanja mkubwa, nitaendelea katika viwanja vingine ili kuhakikisha naangalia maeneo ya usalama na hakuna mtu kupitisha dawa za kulevya, nyara za Serikali na vitu vingine visivyo halali,” alisema.

 Masauni alisema wataongeza kikosi cha askari wa kutosha na wenye sifa wenye mbwa kukagua mizigo na kubaini vitu ambavyo si halali ikiwemo dawa za kulevya.

Alisema ulinzi unatakiwa kuimarishwa, hasa kwa abiria wanaosafiri kwa kulinda mali zao, abiria wanaoingia nchini, mizigo na kuangalia usalama wa mali mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukamata wale wanaosafirisha dawa za kulevya na nyara za Serikali pia.

Mwakyembe: Serikali Itaendelea Kushirikiana Na Wadau Wa Sekta Ya Utangazaji

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
WAZIRI wa Habari, Utamadani, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewahakikishia wadau wa sekta ya utangazaji nchini ikiwemo waandaaji na wazalishaji wa vipindi vya televisheni vya maudhui ya ndani kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao na kuwajengea mazingira wezeshi ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao wa msingi katika  jamii na Watanzania kwa ujumla.

Akizungumza katika kikao maalum baina yake watayarishaji wa vipindi vya maudhui ya ndani jana Alhamisi (Julai 25, 2019) Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe amesema malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa tasnia ya habari inapiga hatua kubwa za maendeleo na kutoa mchango unaostahiki katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mwakyembe alisema Serikali inatambua wajibu na umuhimu wa tasnia ya habari nchini, na hivyo imetunga sheria na kanuni mbalimbali zinazoongoza vyombo vya habari ikiwemo televisheni, ambapo vimewekwa utaratibu wa kurusha na kuandaa vipindi mbalimbali kupitia miongozo inayotolewa mamlaka husika ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

“Tunatambua kuwa kuna baadhi ya vifungu vya kisheria vinavyoongoza maudhui ya vituo vya utangazaji vimekuwa changamoto, kwa kuwa Sheria hizi sio biblia au msahafu takatifu, tunaweza kuzifanyia marekebisho kila baada ya kipindi cha miaka 3-4 ili kuona ni namna gani inasaidia sekta ya utangazaji sambamba na kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza” alisema Waziri Mwakyembe.

Aidha Waziri Mwakyembe alisema Wizara yake ipo tayari kupokea aina yoyote ya ushauri, mapendekezo na maoni ya wadau wa wazalishaji na waandaji wa vipindi vya Televisheni hususani masuala yote ambayo yamekuwa yakiwaletea changamoto katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuhabarisha umma kupitia vipindi mbalimbali ambavyo vimekuwa daraja la kuwaunganisha Watanzania.

Akifafanua zaidi Dkt. Mwakyembe alisema Serikali itahakikisha kuwa waandishi wa vyombo vya habari kutoka sekta ya umma na binafsi ikiwemo waandaaji wa vipindi vya maudhui ya ndani wanajengewa uwezo ikiwemo kuwapatia mafunzo ya muda mfupi, ya kati na mrefu, hatua inayolenga kuwaongezea weledi, ujuzi na maarifa na hivyo kutimiza wajibu wao wa msingi katika jamii.

Dkt. Mwakyembe alisema katika mfumo uliopo sasa wa kutangaza maudhui ya ndani kumekuwepo na changamoto mbalimbali katika kanuni, sheria na taratibu ambazo zimekuwa zikileta malalamiko kutoka kwa wadau, na hivyo Serikali itahakikisha kuwa vipengele hivyo vinafanyiwa kazi kwa kuwa Serikali na vyombo vya habari vyote kwa pamoja vimekusudia kujenga msingi imara wa ushirikiano baina yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Matukio wa Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) Martha Swai amesema TBC imekuwa mstari wa pembe katika kutangaza vipindi vyake vya Televisheni katika maudhuo ya ndani, ambapo asilimia 82 vimegusa masuala ya elimu, biashara na kuburudisha, na asilimia 18 ikijikita katika masuala ya muziki.

Anaongeza kuwa Shirika hilo limekuwa likiatangaza matangazo yake ya Televisheni katika chaneli kubwa tatu ambazo ni  TBC 1,   TBC 2 na Tanzania Safari ambazo zote kwa pamoja vimekuwa na mchango mkubwa katika kutangaza habari na matukio ya vipindi mbalimbali vyenye kuakisi maudhui ya ndani.

Naye Meneja Vipindi wa Kampuni ya Tumaini Media, Paul Mabuga amesema kwa sasa kumekuwepo na changamoto kubwa ya ukosefu wa matangazo ya biashara katika vituo vya Televisheni kwani wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitumia zaidi mitandao ya kijamii ili kuweza kufikisha ujumbe wananchi kwa njia ya kisasa na haraka zaidi.

MWISHO

Waziri Mhagama: Serikali Kuendelea Kushirikiana Na Taasisi Za Dini Kujenga Ustawi Wa Taifa

$
0
0
Na. OWM, DAR ES SALAAM.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ameeleza kuwa serikali inatambua juhudi za taasisi za dini hapa nchini ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na utulivu, hivyo itaendelea kushirikiana na taasisi hizo katika kuunga juhudi za serkali za kujenga amani, umoja, upendo na mshikamano  na hatimaye  kuleta ustawi wa Taifa. 

“Napenda kuwahakikishia ushirikiano wa serikali katika kutekeleza majukumu yenu ya kiroho na ya huduma za kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya watanzania. Pale mtakapoona mchango wa serikali unahitajika msisite kuwasiliana nasi. Na iwapo mtaona kuna upungufu wowote semeni kwa viongozi wa wilaya, mkoa na wa kitaifa. Sisi ni wasikivu. Tuite tutawaitikia, tutatenda kwa lile ambalo lipo ndani ya uwezo wetu” amesisitiza Mhe. Mhagama.

Akiongea kwa niaba ya Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, katika Kongamano la maombi ya wanawake waombolezao, jijini Dar es salaam, tarehe 25 Julai, 2019, Mhe. Waziri Mhagama amefafanua kuwa waratibu wa Kongamano hilo wanapongezwa na viongozi wote serikalini,  akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwakuwa linachagiza maendeleo katika Taifa hili na ustawi wa watu wake.

“Viongozi wetu kwa pamoja ni shupavu, wanaoaminiwa na kutumainiwa na wananchi hasa wanyonge. Viongozi wanachukia na kupinga rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma kwa vitendo na Rais anayejipambanua kwa kufanya maamuzi magumu ya kulinda rasilimali za Taifa. Lakini haya yote yamewezekana kwa kuwa wamejikabidhi katika mikono ya Mungu na nyie mmekuwa mkiwaombea” amesema Mhe. Mhagama.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mhagama amewataka Wanawawake waombolezao waendelee kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa ambazo anaendelea kuzifanya tangu aliposhika hatamu ya uongozi,  kwa kuthubutu kutenda  na kuiletea nchi mafanikio makubwa.

“Kwa uchache kazi kubwa ambazo amezitekeleza Mhe. Rais, ni pamoja na kutoa elimu ya msingi bila malipo ambapo ameweza kuwagusa hata walewasiojiweza, kuongeza bajeti ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kujenga Hospitali na Vituo vya Afya vingi  ili watanzania wengi wapate huduma za Afya kwa karibu. Pia umeme kwa sasa umesambazwa vijijini kupitia mradi wa REA na sasa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Maji (Rufiji) umeanzishwa” amesisitiza Mhagama.

Awali wakiongea  katika Kongamano hilo, waratibu wa Kongamano hilo, Mchungaji Deborah Malassy na Askofu Dkt. Godfrey Malassy wamebainisha kuwa wameamua kuendesha Kongamano hilo kwa kuwa wanatambua kuwa viongozi wa dini kama walivyo wa serikali wanao wajibu  maalamu wa kulilea Taifa. Aidha wameongeza kuwa ushirikiano ukiwa imara watafanikiwa kuendeleza amani, umoja na mshikamano uliopo hapa nchini.

“Tutaendelea kutekeleza wajibu pekee wa kujenga uhai wa Taifa letu na watu wake. Tunampongeza Mhe.Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa uongozi wake bora uliokidhi kiu na kilio cha watanzania kwani tumeona jitihada anazofanya pamoja  na kutiwa moyo na kazi zake anazozifanya  na viongozi wote wa serikali ya awamu ya tano. Kwa hamasa hii tunapata nguvu ya kuendelea na wajibu huu mkubwa tuliopewa na Mungu kwa ajili ya kuendelea kuliombea Taifa letu” amesema, Mchungaji Deborah.

Kongamano hilo la kumi la Kihistoria hapa nchini liliohusisha Wanawake Waombolezao Kitaifa kutoka mikoa yote Tanzania  na Zanzibar, pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali, limebebwa  na maudhui ya  Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote. Kongamano hilo ni sehemu ya Maombi ya kila mwisho wa mwaka wa tarehe 31 Disemba ya kuliombea Taifa hili yajulikanayo kama MKESHA MKUBWA KITAIFA DUA MAALUM, ambayo yamekuwa yakifanyika katika viwanja vya wazi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Zanzibar.

MWISHO.

Jamii Yatakiwa Kutowatenga Watu Wenye Ulemavu.

$
0
0
NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI, KAGERA
Jamii mkoani Kagera imetakiwa kutowabagua wala kuwanyanyapaa  watoto wenye ulemavu  badala yake wapewe vipaumbele na  mahitaji  muhimu ili  wajione sawa na watu wengine. 

Kauli hiyo imetolewa  na mkuu wa taasisi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Kagera Bwana John Joseph wakati akiongea na Mwandishi wa kituo hiki ofisini kwake. 

Bwana Joseph amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwatenga, kuwabagua  watu wenye walemavu wakiwemo watoto jambo mbalo husababisha makundi hayo kujiona ni watu wa tofauti katika jamii 

 Amesema katika  ushiriki wa makundi ya vijana juu ya  mapambano dhidi ya Rushwa Taasisi  hiyo imefanikiwa kuyaelisha makundi ya wanafunzi kwa kuanzisha clabs za wapinga rushwa mashuleni 

Mkuu huyo amesema ili kulipa uzito suala hilo july 28 mwaka huu wanafunzi wa shule ya Sekondari Kahororo iliyoko mkoani Kagera  kwa kushirikiana na Taasisi hiyo watakwenda kutembelea  shule ya wanafunzi walemavu katika shule sekondari  Mgeza Mseto kwa ajili ya kuwapelekea mahitaji  mbali mbali mbali. 

Amesema  makundi ya watu wenye walemavu ni sehemu ya jamii na ili makundi hayo yatambue kuwa jamii haijawatenga kila mmoja ashiriki katika kuwatembelea kuwajali na kuwapa chochote walemavu waliopo katika maeneo yake. 

Hata hivyo ameongeza kuwa jamii iwafichuo na kuwaweka adharani wapate Elimu pamoja na mahitaji yao muhimu.

Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Korea Kusini kwamba ni vigumu kujilinda dhidi ya kombora lake jipya

$
0
0
Korea Kaskazini imesema hivi leo kwamba jaribio lake la makombora mapya linanuia kuwa onyo dhidi ya mipango ya silaha ya Korea Kusini na pia mipango ya kuandaa mazoezi ya kijeshi na Marekani. 

Kauli inakuja muda mchache baada ya kombora kurushwa kutoka Korea Kaskazini, ambapo jeshi la Korea Kusini limesema linafanana na kombora la masafa mafupi lililotengezwa Urusi.

Kombora hilo aina ya Iskander lenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia lina uwezo wa kufika popote Korea Kusini, ambako kuna wanajeshi 28,500 wa Marekani, na haliwezi kudunguliwa.

Wachambuzi wa mambo wanasema hatua hii ya Korea Kaskazini ni sehemu ya juhudi zake kuhakikisha inapata kile inachokitaka kwenye mazungumzo yake na Marekani, baada ya mkutano wa hivi karibuni kati ya Kim Jong Un na mwenzake Donald Trump.

Rais Magufuli aagiza pori la Selous kuwa Hifadhi ya Taifa......Mabilioni Dhahabu ya Kenya Aagiza Yakajenge Barabara ya Lami

$
0
0
Rais  Magufuli ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kukata eneo la ukanda wa juu wa pori la Selous na kulifanya kuwa Hifadhi ya Taifa na liitwe ‘Nyerere National Park’  ili kuenzi mawazo ya Hayati Baba wa Taifa .

Magufuli ametoa agizo hilo leo Ijumaa Julai 26, wakati akizindua ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Stieglers Gorge katika mto Rufiji mkoani ambapo amesema eneo litakalobaki waachiwe wawindaji waendelee na shughuli zao.

Amesema sababu ya kufanya hivyo ni kuongeza maeneo ya utalii hapa nchini ili kuendelea kukuza pato la taifa kutokana na fedha watakazolipa wataii.

“Kuna siri lazima niwaambie ndugu zangu,  kwenye pori la Selous kuna vituo vya uwindaji (hunting block) 47 vimeshachukuliwa, watu wanakuja na ndege hapa wanaua wanyama wanaondoka, bei yake ya chini kwa kituo ni Dola za Marekani 5, 000 ambazo ni sawa na Sh. milioni 10 za Tanzania kwa mwezi na ukilipa hiyo unaruhusiwa kuua hata nyati 10, kwa ujumla hii ‘Game Reserve’ haitupi faida.

“Kutokana na hali hii nataka  ‘Game Reserve’ ya Selous tuikate na iwe Hifadhi ya Taifa ili watalii wawe wanakuja hapa badala ya watu kuja kuwinda wanyama wetu, mataifa mengine hawafanyi sana hizi shughuli na uzuri Waziri wa Maliasili yuko hapa huu ndiyo ujumbe wako, kakae kwenye Wizara mkapunguze eneo la uwindaji, hilo limesemwa sana lakini utekelezaji umecheleshwa,” amesema Rais Magufuli.

Ameagiza pia fedha na dhahabu zilizorudishwa baada ya kuibiwa hapa nchini na kupatikana nchini Kenya zikatumike kujenga barabara ya lami kutoka lilipo pori la Selous hadi eneo la Fuga inakopita treni ya umeme ya Standard Gauge.

“Juzi nimepokea dhahabu zilizorudishwa kutoka Kenya nimepiga hesabu vizuri ni kama Sh bilioni nne au tano na fedha taslimu kama milioni 500, nataka hizo fedha zianze kutengeneza barabara ya lami kutoka hapa hadi eneo la Fuga ambazo ni kilometa 60 ili watu wakitoka Dar es Salaam kwa treni wakishuka pale Fuga wanatumia barabara hadi hapa kuja kutalii,” amesema.

Aidha ameagiza pia bwawa litakalojengwa kwa ajili ya mradi wa kuzalisha umeme lipewe jina la Mwalimu Nyerere kwani hayo yalikuwa mawazo yake na kufanya hivyo ni kumuenzi.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Maadhimisho Ya Siku Ya Homa Ya Ini Duniani

Watu 12 Kortini Kwa Kukwepa Kulipa Kodi na Kuisababishia TRA Hasara ya Mamilioni

$
0
0
Watu 12 wakazi wa sehemu tofauti jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la  kukwepa kodi na kusababisha hasara ya zaidi ya sh. Milioni 100.7/-

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Janet Magoha amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Rose Kerandi, Ally Abdul, Geoffrey Kayanza, Anwar Rubeya,  Khalid Kigoma, Joseph Marcelo, Samir Hussein, Matiku Mgaya Iddi Bogaboga, Edward Maguri, Alex Sanga, Said suleman, Lali Mohamed na Hamidu Abu.

Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally kuwa, Siku na mahali pasipo julikana, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la kukwepa kodi.

Katika shtaka la pili imedaiwa  February 21, 2019 ndani ya jiji la Dar es Salaam, washtakiwa walishindwa kulipa kodi ya sh. 100,739,873 ya mzigo wa ambao walikuwa wakiuingiza  nchini.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa, Siku na mahali hapo waliisababishia TRA hasara ya kiasi hicho cha fedha kwa nia ovu ya kutokulipa kodi ya bidhaa ya kontena la futi 40 lilolokuwa limebeba  mikoba.

Hata hivyo wakato wakisomewa mashtaka hayo, washtakiwa  Anwary Rubeya, Joseph Marcelo, Matiku Mgaya na Idd Bogobogo hawakuwepo mahakamani hapo na mahakama imetoa hati ya wa washtakiwa hao kukamatwa ili waweze kufika mahakamani hapo kujibu mashtaka yao.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu Uchumi na imeahirishwa hadi Agosti 6, mwaka huu.

Kwa mujibu wa upande wa utetezi, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, washtakiwa wote wamerudishwa rumande.

Rais Magufuli Aagiza Uchunguzi wa HARAKA wa Matumizi yz Bilioni 15 za TAZARA

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi 27 July


Jeshi la Polisi nchini latoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajali ya gari la polisi

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini limetoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajali ya gari la polisi iliyotokea mkoa wa Kipolisi Rufiji, Kijiji cha Kilimahewa.

Mahakama Yakwama kutazama mkanda wa video kesi ya viongozi 9 wa CHADEMA

$
0
0
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuangalia video inayowahusu viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kutokana na upande wa utetezi kuipinga.

Pingamizi hilo liliwasilishwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kuiomba mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba kuandaa mazingira wezeshi ya kuonesha maudhui ya video iliyochukuliwa wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni.

Upande wa mashitaka uliomba mahakama hiyo itumie Kituo cha Mafunzo cha Kisutu kuonesha maudhui hayo kwa sababu kina vifaa vinavyowezesha kuonekana kwa video hiyo vizuri.

Hata hivyo, Wakili Kibatala alidai upande wa mashitaka ulipaswa kuandika barua kwa uongozi wa mahakama kuomba kutumika kwa kituo cha mafunzo kuonesha maudhui hayo.

Pia amedai, walipaswa kuandaa vifaa vyote muhimu ikiwemo waya na projekta ambavyo vingewezesha kuonekana kwa video hiyo na sio wajibu wa mahakama kuandaa.

Kutokana na mvutano wa kisheria baina ya pande mbili, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi August 5, 6 na 7, 2019 kwa ajili ya kutoa uamuzi kama video itizamwe ama lah pamoja na kuisikiliza kesi hiyo.

Naibu Waziri Mavunde Awataka Vijana Kuenzi Mchango Wa Baba Wa Taifa

$
0
0
Na; Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) amewataka vijana kuenzi mchango wa Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa wazalendo na wenye mshikamano katika kujenga Taifa.

Mhe. Mavunde amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga vijana kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).

Alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa wazalendo kwa kuiga kivitendo yale yote yaliyotendwa na waasisi wa taifa hili, Mwl. Julius K. Nyerere na Hayati Mzee Abeid Karume kwa kuendelea kudumisha upendo, amani na mshikamo kwa mustakabali wa Taifa.

“Vijana waliowengi kipindi hiki wameweka pembeni uzalendo wa kulipenda taifa lao hali ambayo inatubidi tujitahmini na kuenzi falsafa walizokuwa nazo waasisi wetu ambao waliweka maslahi ya Taifa mbele wakati wote,” alisema Mavunde

Akitolea mfano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kuwatumikia wananchi kwa kutekeleza masuala mbalimbali ya kitaifa wakati wote ili nchi isonge mbele kimaendeleo.

Pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana waliopanda mlima huo awamu ya kwanza na awamu hii ya pili kwa kuonesha ushujaa na uzalendo kwa Taifa lao ikiwemo kuwa mabalozi wazuri katika kutangaza sekta ya utalii.

Aidha, Naibu Waziri Mavunde alitoa wito kwa vijana kuacha kukaa kwenye vijiwe na kujihusisha kwenye mambo yasio na tija, bali wajishughulishe kwenye miradi mbalimbali itakayo wawezesha kiuchumi na kusaidia kukua kimaendeleo, kwa kuwa waasisi wa taifa walikuwa wachapakazi, waadilifu na wabunifu ambao ni mfano mzuri wa kuigwa.

“Hakuna nchi yoyote dunia ambayo inaweza kuendelea pasipo kuhusisha nguvu kubwa ya vijana katika maendeleo ya taifa,” alieleza Mavunde

Aliongeza kuwa ili kufikia malengo kwenye uchumi wa viwanda ni lazima vijana wazingatie uzalendo, utaifa na bidii katika kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa kitendo cha vijana hao kushiriki katika kupanda Mlima huo ni jambo muhimu kwa taifa na inaashiria namna gani vijana wameanza kutambua historia ya waasisi wa taifa lao.

Naye, Kiongozi wa Vijana hao waliopanda Mlima Kilimanjaro Bw. Augustine Gusha aliunga mkono maelezo yaliyotolewa na Naibu Waziri na alitumia nafasi hiyo kuwasihi vijana kudumisha amani ya nchi wakati wote.

Katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana inaratibu shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Vijana 100 kwa ajili ya kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Awamu ya kwanza vijana walipanda mlima huo tarehe 26 Machi, 2019 na awamu ya pili 26 Julai, 2019. Awamu ya Tatu itakuwa mwezi Oktoba.

Baba Levo akutwa na kesi ya kujibu Mahakamani

$
0
0
Mahakama ya Mwanzo ya Mwandiga Mkoani Kigoma, imemkuta na kesi ya kujibu Diwani wa Kata ya Mwanga Revocatus Kipando (Baba Levo), baada ya kutuhumiwa kufanya shambulio kwa Askari wa usalama barabarani akiwa kazini July 15, 2019.

Uamuzi huo umekuja baada Hakimu wa Mahakama hiyo Frolence Ikorongo, kusikiliza upande wa mshitaki akiwa na mashahidi wawili ambao ni Mussa Lukomati na Karume Rashidi, ambao walieleza tukio hilo lilitokea July 15, majira ya saa 1 usiku.

Mashahidi wameeleza kuwa Baba Levo alimshambulia askari anayefahamika kwa jina la Msafiri Ponera, akiwa eneo lake la kazi eneo la Kwabela, na inadaiwa mtuhumiwa alilazimisha kupita kwa pikipiki wakati askari huyo akiwa waruhusu watembea kwa miguu, na baada ya hapo Baba Levo aliamua kumshambulia askari huyo.

Hakimu Ikorongo amesema kuwa, “kifungu cha 240 sura ya 16 kanuni ya adhabu chapisho la mwaka 2002, Mahakama imemkuta mshtakiwa Baba Levo na kesi ya kujibu baada ya kujiridhisha na ushahidi wa mshtaki”

Kesi hiyo imeahirishwa hadi July 30, 2019, ambapo kwa sasa mtuhumiwa Baba levo yuko nje kwa dhamana.

Waziri Mkuu Aagiza Walimu Wawili Wapelekwe Nanganga Keshokutwa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Afisa Elimu wa Wilaya ya Ruangwa anayeshughulikia elimu ya msingi, Bw. Selemani Mrope atafute walimu wawili kutoka Ruangwa na kuwahamishia kata ya Nanganga mara moja.

"Lazima kuna walimu wamejazana pale Ruangwa mjini, leo tukitoka hapa nenda kaandike barua za uhamisho. Kesho Jumapili, wahusika wapewe barua zao na Jumatatu waje kuripoti hapa Nanganga," amesema Waziri Mkuu na kuamsha shangwe miongoni mwa wakazi wa Nanganga.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2019) wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nanganga, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi alipopita kuwasalimia wakazi hao.

Waziri Mkuu ambaye amewasili Lindi leo kwa mapumziko mafupi, alipokea taarifa ya shule ya msingi Nanganga ambayo ilionesha kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 237 ina walimu sita tu. Kati ya hao, wavulana ni 124 na wasichana ni 113.

“Shule hii ina madarasa nane likiwemo darasa la awali, masomo yanayofundishwa ni tisa, mkibaki na walimu hawa sita, mzigo unakuwa mkubwa kwa walimu hawa waliopo. Afisa Elimu tafuta wawili walimu waje hapa Jumatatu, na Mkurugenzi wa Halmashauri atakupa gari ya kuwahamishia hapa,” amesema. Shule ya msingi Nanganga, iliyoko kata ya Nanganga, iko umbali wa km. 59 kutoka Ruangwa mjini.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa Ruangwa, amewataka wakazi wa kata hiyo wafikirie kuanza ujenzi wa shule ya sekondari yao ya kata ili kuwapunguzia safari wanafunzi wa kijiji hicho ambao kwa sasa wanalazimika kwenda kusoma Nangumbu, iliyoko umbali wa km. 10.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, Serikali imetoa sh. milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne ambayo yakikamilika walimu watapata ofisi pia.

Amesisitiza kwamba fedha hizo zitumike kujenga madarasa manne ambapo walimu pia watapata ofisi moja.

Pia amemwambia diwani wa kata ya Chinongwe, Bibi Maki Camillius kwamba katika bajeti ya mwaka huu, kata hiyo itapatiwa sh. milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba nne za walimu katika shule ya sekondari ya kata ya Chinongwe.

Mapema, akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Amiri Musa Kambona alisema madarasa mawili na ofisi moja ya walimu vilibomoka mwaka 2014 kutokana na mvua na upepo mkali na kusababisha upungufu wa madarsa na ofisi.

Akielezea changamoto nyingnea za  shule hiyo, Mwalimu Kambona alisema shule ina upungufu wa nyumba moja ya walimu, darasa moja, matundu mawili ya vyoo vya walimu, ofisi moja ya walimu na kukosekana kwa chanzo cha maji safi na salama kwa matumizi ya wanafunzi na walimu.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,      
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images