Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

UVCCM Taifa Yafanya Mafunzo Maalum Kwa Wasichana Mkoa Wa Dar Es Salaam

$
0
0
Makamo wa  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Vijana wa CCM Taifa *Ndg Tabia Mwita* amefungua mafunzo  Maalum kwa Wasichana kwa Mkoa wa Dar Es Salaam.

Mafunzo hayo Yaliyosimamiwa na kuratibiwa na *Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi *Ndg.Rose Robert Manumba* kwa Kushirikiana Taasisi ya Kijerumani FES kwa lengo la kuwaelimisha na kuwaongezea ujuzi na Maarifa yakiuongozi.

Pamoja na kufungua Mafunzo hayo Miongoni mwa waliyotoa na mada ni Ndg.Tabia Mwita na  amewasilisha Mada ya *Ushiriki wa wanawake katika siasa* ambavyo amesisitiza wanawake kuendelea kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa bila kuogopa. Amewasihi wanawake kujiamini na kutokukubali kukatishwa tamaa.

Makamu huyo  amesisitiza umuhimu wa kuwa na umoja na mshikamano ili kuendeleza kusaidia Serikali katika juhudi zinazofanyika kumuinua Mwanamke.

Aidha, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa *Rose Manumba* akiwa  amesisitiza kuwa ni muhimu sisi kama wasichana kuwa sehemu ya mabadiliko tunayotamani kuyaona katika nchi yetu na hata duniani kwa ujumla. Tuwe  tayari kutumikia nafasi zetu popote pale tulipo kuendelea kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dr. John pombe Magufuli anayepambana usiku na mchana kumuinua mwanamke wa kitanzania ili kuleta maendeleo katika Taifa letu.

Wameshiriki wakufunzi mbalimbali kama Dorris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation aliyewasilisha mada ya *Mchango wa asasi za kiraia katika kumuinua Mwanamke* Na Suma Mwaitenda ambaye ni Mkurugenzi wa FURSA, kutokea Clouds Media Digital aliyewasilisha mada ya;  *Namna gani msichana anaweza kuziona na kuzipata Fursa.*

 *Ndg. Japhary Kubecha* ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya UVCCM Taifa katika kufunga mafunzo hayo amesisitiza wanawake kujituma katika kazi na sio kuridhika na nafasi mbalimbali ambazo wanaweza kupata kwa kigezo kuwa ni wanawake.

Mafunzo haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali; Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni Lilian Rwebangira, Abdul-Rahman Killo na Mwanaidi ambao ni Maafisa kutoka UVCCM Makao Makuu.

January Makamba Akabidhi Ofisi Kwa George Simbachawene

$
0
0
Mbunge wa Bumbuli January Makamba leo amemkabidhi Waziri mpya katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano & Mazingira) George Simbachawene ambaye ameteuliwa na Rais Magufuli.

Rais Magufuli Avipongeza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa Kukamata Dhahabu na Fedha Zilizoibiwa Hapa Nchini

$
0
0
Rais Dk John Magufuli amevishangaa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushindwa kukamata na dhahabu na fedha zilizoibiwa hapa nchini hadi zikakamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya.

Magufuli amevihoji vyombo hivyo leo Jumatano Julai 24, wakati wa makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa nchini Kenya na kuwasilishwa  na Mjumbe Maalum wa Rais Kenyatta yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Wakupongezwa kwa hili ni vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya, najua wakuu wa vyombo Tanzania mpo hapa, lazima niwatandike hapa mbele za watu, kwasababu vitu vimetoka Mwanza vimekamatiwa Kenya, je zilipobebwa Mwanza na Kilimanjaro vyombo vyetu vilikuwa vinafanya nyinyi?

“Je vilishirikiana na huyu muhalifu au vilimuachia, je dhahabu ngapi zimesafirishwa bila watuhumiwa kushikwa? Hili nawaachia nyinyi, mnafanya kazi nzuri ila inawezekana kuna mahali hamfanyi kazi vizuri nahii inadhihirisha aibu kwa vyombo vyetu na niwaombe mshirikiane, kila mtu asifanye kivyake.

 “Na mimi nitaandika barua rasmi ya kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa niaba ya Watanzania kwasababu wamefanya kazi nzuri kama wasingezikamata hizi mali leo tusingekuwa hapa, askari walioshiriki katika hili nitafanya mango nione namna ya kuwazawadia wakiwa hukohuko Kenya,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli Ampigia Simu Rais Uhuru Kenyatta na Kumshukuru kwa Dhahabu Iliyorudishwa Nchini

$
0
0
Rais Magufuli amempigia simu Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kumpa ujumbe wa shukrani kwa kuwezesha urudishwaji wa dhahabu kilo 35.34 na fedha zilizoibiwa hapa nchini na kupatikana nchini Kenya.

Rais Magufuli amefanya hivyo leo Jumatano Julai 24, walipozungumza kwa njia ya simu wakati wa makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa nchini Kenya na kuwasilishwa  na Mjumbe Maalum wa Rais Kenyatta yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Ninakushukuru sana Mh Rais, Dada yangu Monica ameshashusha mzigo hapa na nimeuona ni wenyewe, fedha na dhahabu hizi tunazokusanya nilikuwa nawaambia Watanzania kama tungekuwa watu wabaya wasingeziona kabisa na ndiyo maana nawaambia Rais Kenyatta ni mzalendo sana na ndiyo sababu tumezitoa hadharani.

“Nataka uwapongeze sana vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwasababu hii mali haikushikwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania, nitatafuta zawadi ya kuwapa kwa niaba ya Watanzania na naomba kama wana mbinu nyingine wanatumia wawafundishe na wenzao wa Tanzania.

“Nashukuru sana ulivyomtuma Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Monica Juma mbali ya kuwa ni mzuri anachapa kazi na anaiwakilisha Kenya vizuri,” amesema Rais Magufuli huku akicheka.

Naye Rais Kenyatta akijibu ujumbe huo amesema wananchi wa Kenya na Tanzania waliwaamini na kuwapatia nafasi ya kuwaongoza hivyo watafanya kila linalowezekana kuilinda imani hiyo.

“Tulisema mali ya wananchi wetu lazima irudi kwa wananchi wetu, wametupatia imani yao na kutupatia uongozi hivyo kazi yetu ni kuhakikisha tunalinda mali zao wetu zikatumike kujenga barabara na shule ili kuunganisha wananchi na walaghai hawana nafasi tena katika nchi zetu,” amesema Rais Kenyatta.

Waziri Mhagama atoa neno kwa Baraza la Vyama vya Siasa nchini

$
0
0
Na. OWM, DODOMA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, amelitaka Baraza la Vyama vya siasa nchini kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu juu ya masuala yenye maslahi kwa Taifa kuhusiana na vyama vya siasa  pamoja na hali ya kisiasa nchini ili kuimarisha ustawi wa siasa na vyama vya siasa nchini.

Mhe. Waziri Mhagama ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha siku mbili cha Baraza hilo kilichoanza jana na kinafungwa leo, tarehe 24, Julai 2019, mjini Dodoma katika ukumbi wa Pius Msekwa, ambapo Mhe. Mhagama amesisitiza vyama hivyo kuendelea kushirikiana na kudumisha upendo na umoja wa kitaifa  katika kutekeleza majukumu yao ya kisiasa ili kuweza kuijenga Tanzania yenye umoja.

“Endeleeni kutumia fursa za vikao vya Baraza kutatua matatizo yenu na niwashauri  muunde kamati za Baraza na kutumia kamati hizo katika kutatua matatizo yenu, lakini pia tekelezeni majukumu yenu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu tulizonazo hapa nchini ili vyama viweze kuisaidia nchi na watanzania kuyafikia malengo yao kwa kuwajenga watanzania kuwa wamoja badala ya kuwagawanya” amesema Mhagama

Mhe. Waziri Mhagama amefafanua kuwa katika vikao vyao na serikali Baraza hilo walikuwa na matakwa yao ambayo walitaka serikali iyatekeleze kupitia ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini ambapo tayari serikali imeyatekeleza ikiwemo kuanzisha ofisi ya Naibu msajili wa vyama vya siasa Zanzibar.

“Serikali  ya awamu ya Tano chini ya  Rais, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, kupitia ofisi ya Waziri Mkuu, katika bajeti yake, ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, tayari imetenga bajeti ya kuiendesha Ofisi ya Naibu Msajili wa vyama vya siasa Zanzibar, lakini pia sisi serikalini tumeshakubaliana kuwashirikisha viongozi wa Baraza la vyama vya siasa katika matukio ya shughuli za maendeleo ya serikali ili viongozi nyie muweze kuelewa vyema mabadiliko ya utekelezaji yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano” Amesisitiza Mhe. Mhagama.

Aidha, Mhe. Mhagama ameeleza kuwa Wajumbe wa Baraza hilo watakuwa wakijengewa uwezo katika masuala ya siasa ili kuweza kuendelea kujenga msingi imara na ustawi wa demokrasia nchini.

Awali, akiongea katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza hilo, John Shibuda, ameeleza kuwa wanashukuru kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiupata kutoka serikalini kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ambapo ameomba kuendelea kushirikishwa ipasavyo ili waweze kuelewa vyema utekelezaji wa shughuli za maendeleo za serikali ya awam ya tano.

“Baraza tunamshukuru sana Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mhagama kwa ushirikianao ambao amekuwa akitupatia Baraza kimsingi hivi leo tunajivunia miaka miwili ya utendaji wa Baraza letu lakini msingi wa mafanikio hayo ni Waziri huyu amekuwa ufungua  ambao atufungulia milango kila jambo tunalotaka kulitekeleza kwa wakati ” amesema Shibuda.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini, Mhe. Jaji Francis Mutungi,  Naibu Msajili wa Vyama vya siasa, Mhe. Mohammed Ally Ahmed, pamoja na wajumbe wa Baraza hilo ambao ni vyama vyenye usajili wa kudumu. Baraza la Vyama vya Siasa limeanzishwa chini ya kifungu cha 21B cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 ikiwa ni jukwaa la viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kukutana mara kwa mara kujadiliana masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi na siasa hapa nchini kwetu. Baraza hilo limeundwa ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo, Wajumbe wa Baraza hilo hujumuisha viongozi wa kitaifa wawili wa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndio yenye jukumu la kisheria ya kuratibu shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa.

Majukumu ya Baraza hilo ni pamoja na kumshauri Msajili wa vyama vya siasa juu ya masuala yenye maslahi kwa Taifa kuhusiana na vyama vya siasa au kuhusiana na hali ya kisiasa nchini Siasa na sheria zingine zinazohusu masuala.

Mcheza Filamu Wa Mexico Atembelea Hifadhi Nne Za Taifa

$
0
0
MUIGIZAJI maarufu wa filamu kutoka Mexico, Bi. Leticia Calderon (51) amesifia rasilmali ya hifadhi za wanyama ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.

Muigizaji huyo ambaye amefanya kazi hiyo kwa miaka 36, na ameigiza sinema maarufu ya ESMERALDA, yuko nchini kwa mapumziko ya siku saba kwenye hifadhi za wanyama za ukanda wa Kaskazini.

Akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi, Bi. Calderon amesema amevutiwa na uzuri wa hifadhi za Tanzania na idadi kubwa ya wanyama aliowaona kwenye hifadhi za Taifa za Tarangire, Manyara na Ngorongoro.

“Kwa miaka mingi nilikuwa natamani sana kuja Tanzania kuona wanyama. Tuliyoyaona yametufurahisha mimi pamoja na wanangu. Nchi yenu ina uzuri wa kustaajabisha. Watu wenu ni wema na wakarimu,” alisema Bi. Calderon.

“Ninafurahi kwamba ndoto yangu imetimia. Tulienda Tarangire, Manyara na Ngorongoro ma sasa tunajiandaa kwenda Serengeti. Tulipokuwa Ngorongoro, tuliona simba wanne, majike wawili na madume wawili. Tumefurahi sana na nikirudi nyumbani, nitawaonyesha picha marafiki zangu na kuwaalika waje kutembelea Tanzania,” alisema.

Bi. Calderon ambaye amefuatana na wanaye wawili Luciano Collado (15) na Carlo Collado (14) alisema wakimaliza mapumziko yao huko Serengeti watakwenda Masai-Mara kwa siku tatu na kisha wataelekea Paris, Ufaransa kumtembelea rafiki yake ambaye waliigiza filamu pamoja huko nyuma.

Bi. Calderon pia ameigiza tamthilia ndefu (soap operas) 29 katika jiji la Mexico City ambalo ni mji mkuu wa Mexico. Mbali ya Esmeralda, filamu nyingine maarufu ambazo ameigiza ni En Nombre del Amor (In the Name of Love); Amor Bravia (Valiat Love) na La Indomable (The Taming of the Shrew).

Waziri Mkuu alimshukuru mwanamama huyo na wanaye kwa kuichagua Tanzania kwa mapumziko yao na akawatakia heri katika safari yao ya mbugani.

Akizungumza na wafanyakazi wa hoteli ya The Retreat at Ngorongoro iliyoko Karatu ambako muigizaji huyo alikuwa amefikia, Waziri Mkuu aliwataka wafanyakazi wa hoteli hiyo na wengine walioko kwenye hifadhi za Taifa, wafanye kazi kwa bidii ili huduma zao ziwavutie watalii wengi zaidi.

“Tunampongeza mwenye hoteli kwa uwekezaji huu mkubwa lakini niwasihi wafanyakazi mchape kazi ili wageni wengi zaidi waweze kuvutiwa na huduma zenu,” alisema Waziri Mkuu.

“Sasa hivi tunapata watalii wengi na watu maarufu kama hawa, wamechagua kuja kupumzika Tanzania. Mheshimiwa Rais Magufuli ameshanunua ndege sita, nyingine mbili zinakuja, moja itawasili Oktoba, na nyingine Januari, mwakani. Na tayari kuna ndege tatu nyingine zimeagizwa. Lengo lake ni kuimarisha usafiri wa ndani kwa kutumia ndege,” alisema.

“Zamani ilikuwa ni vigumu sana kuja Tanzania moja kwa moja. Ili mtalii afike, ilibidi apitie nchi nyingine na huko akidakwa anaondokea hukohuko. Sasa hivi, akitoka kwao ataweza kuja Tanzania moja kwa moja, akitua KIA anakuja Karatu au Serengeti moja kwa moja,” alisema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,       

Takukuru Dodoma Yawanasa Watu Wawili Akiwemo Mtendaji Wa Kata Kwa Kosa La Kupokea Rushwa Mil.nne[4].

$
0
0
Na.Faustine  Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na    kupambana Rushwa ,TAKUKURU  kwa Mkoa wa  Dodoma  inawashikilia watu wawili akiwemo mtendaji wa kata kwa kosa la kupokea hongo ya Tsh.Milioni nne. 

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Julai 24,2019  jijini Dodoma mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma  Bw.Sosthenes Kibwengo  amesema  mtendaji wa kata ya Mlowa Bwawani  wilaya ya Chamwino Bw.    Luis  Charles Pearson  na Mgambo  Bw.Josephat Ernest Msambili  wote wenye umri wa miaka [37]  walishikiliwa na TAKUKURU Kwa kosa la kushawishi  na kupokea hongo ya Tsh.Mil.4  kinyume  na kifungu cha  15[1]a  cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa  Na.11  Ya mwaka 2007. 

Watuhumiwa hao walimkamata na kumweka mahabusu ya kata  Bw.Samwel  Mabway   CHILULUMO ,mkazi wa kijiji cha WILIKO kilichopo kata ya MLOWA   BWAWANI Kutokana na ugomvi wa kifamilia . 

Wakati Chilulumo  akiwa yupo Mahabusu ndipo watuhumiwa   walipomtaka awape rushwa ya Tsh. Laki 6  ili wamwachie huru. 

Hata hivyo ,Bw.Chilulumo aliomba kupunguziwa  hadi kufikia Tsh.Laki nne na alipoomba atolewe mahabusu ili akatafute  fedha hizo watuhumiwa walikataa na kuamua kwenda kumtafuta mteja   wa mbuzi kumi[10] za Bw.Chilulumo zilizokuwa nyumbani kwake.

Aidha,Bw.Kibwengo  amesema uchunguzi wa TAKUKURU umethibitisha kuwa Mtuhumiwa Bw.Msambili alikwenda kutafuta mnunuzi wa Mbuzi hao na kumpeleka Mahabusu  alipokuwemo Bw.Chilulumo na baadaye kwenda nyumbani kuwakagua na akarudi tena mahabusu  ndipo walipokubaliana bei. 

Imethibitika kuwa mnunuzi huyo  alitoa  fedha hizo ambazo watuhumiwa walizipokea ndipo wakamtoa mahabusu na kumwachia huru  na TAKUKURU imekamilisha uchunguzi wa suala hilo na watuhumiwa wamefikishwa mahakamani leo . 

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma ametoa wito kwa watendaji wa kata,mitaa,vijiji kuenenda kulingana na maadili ya Kazi zao  na kujiepusha na  vitendo vya Rushwa  kwani havina nafasi katika serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe  Magufuli.

Halmashauri Ya Geita Mjini Yatoa Mkopo Wa Bilioni 1.6 Kwa Vijana, Wanawake Na Walemavu

$
0
0
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema Halmashauri ya mji wa Geita hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu tayari  imeshatoa mkopo wa Shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya wakinamama, vijana na walemavu  kwa lengo la kutimiza  adhima ya Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa  Rais John Pombe Magufuli.

Amesema lengo la kutoa mkopo huo  ni  kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na kuweza kuinua kipato cha wananchi kwa kunufaika na miradi mbalimbali na hatimae kuweza kujikwamua kiuchumi.

Hayo ameyasema kwenye mkutano wakati akizungumza na wananchi wake kuhusu ahadi mbalimbali alizozitekeleza ikiwemo ya kutoa mkopo wa shilingi bilioni 1.6   kwa vikundi mbalimbali  kwa lengo la kupunguza umasikini katika jamii katika mkutano huo  uliofanyika katika kata ya Ihanamiro wilaya ya Geita mkoani Geita.

Mhe.Kanyasu amewaeleza wananchi hao kuwa kutokana na uhusiano mzuri uliopo miongoni mwa madiwani katika Halmashauri hiyo wameweza kutoa mkopo huo. Hata hivyo amesema kuwa mikopo hiyo itasaidia katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo vitasaidia kutengeneza ajira na kukuza uchumi

Akizungumza katika mkutano huo,Mhe.Kanyasu amesema anajisika fahali ya  kutoa mikopo hiyo kwa vikundi ikiwa ni moja ahadi alizozitimiza za kuhakikisha mwananchi wake wanajihusisha kwenye shughuli za kiuchumi ili kupunguza umasikini kuanzia ngazi ya familia hadi taifa

Amesema kuwa kutokana na changamoto zilizoko  katika taasisi za fedha, ambazo hutoa mikopo kwa riba kubwa na kuhitaji dhamana ya nyumba na ardhi jambo ambalo linawakwamisha wakopaji hivyo serikali imeamua kutoa mikopo ya masharti nafuu.

Aidha amesema mikopo  hiyo itawasaidia makundi hayo kuweza  kuongeza mitaji na kutoa ajira ndani ya jamii.

Aidha, Mhe, Kanyasu amesema katika awamu ya pili ya utoaji mkopo  wataongeza viwango vya mikopo kwenye vikundi ambapo kila kikundi kitakuwa na uwezo wa kukopeshwa hadi kufikia shilingi milioni 20 tofauti na ilivyokuwa awali

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Ihanamiro,  Mhe. Joseph Lugaira amemueleza Mbunge huyo kuwa katika kata hiyo jumla ya vikundi 19 vimenufaika na mkopo huo kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi.

Amesema vikundi hivyo vimekuwa vikifanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo biashara pamoja na kilimo ambapo anaamini wataweza kupata faida pamoja na kurejesha mkopo huo na kukopa tena.

Naye Diwani wa viti maalum, Mhe. Suzana Mashala  amewahimiza wanawake wasiogope kukopa kwani hawawezi kujiendeleza kiuchumi pasipo kukopa.

Vile vile, Diwani huyo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanawake waliokopa wajitahidi kurejesha mikopo hiyo mapema ili mikopo hiyo iweze kuwasaidia watu wengine lengo likiwa ni kuondokana na umasikini.

Kwa upande wake, Emalio Nyangabo ambaye ni kiongozi wa Kikundi cha Tuinuane, amesema   walipokea mkopo ambao umewasaidia kuinuka  kiuchumi, na kuwawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuachana na kujihususha na vitendo visivyofaa katika jamii

Naye, Godson Maduka ambaye ni miongoni mwa vijana walionufaika wa mkopo huo amesema mkopo huo umewasaidia vijana wengi kujiepusha kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na unywaji wa pombe kupita kiasi.

NEC Yatangaza Uchaguzi Mdogo Kata 13 Za Tanzania Bara

$
0
0
Idara ya Habari-NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa Kata 13 ambao utafanyika tarehe 17 Agosti 2019.
Taarifa kwa umma iliyosomwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji (Rufaa) Mbarouk Salim Mbarouk Mjini Babati, Mkoani Manyara leo (tarehe 24.07.2019) imesema kwamba fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya tarehe 29 Julai mpaka tarehe 03 Agosti 2019.

Jaji Mbarouk amesema kwamba uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 03 Agosti 2019 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 04 Agosti 2019 mpaka tarehe 16 Agosti 2019.

Alizitaja kata zenye uchaguzi na halmashauri zake kwenye mabano kwamba ni pamoja na Laroi, Lemanyata na Likiding’a (Wilaya ya Arusha), Kimokouwa (Wilaya ya Longido), Kwembe (Manispaa ya Ubungo), Izigo (Wilaya ya Muleba), Mahida (Wilaya ya Rombo).

Nyingine ni pamoja na Makanya (Wilaya ya Same), Barikiwa (Wilaya ya Liwale), Kikeo (Wilaya ya Mvomero), Biro (Wilaya ya Malinyi), Myangayanga (Mji wa Mbinga) na Kapenta (Wilaya ya Sumbawanga).

Jaji Mbarouk amesema Tume imetangaza nafasi hizo kuwa wazi baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, ameitaarifu Tume  uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata Kumi na tatu (13) zilizopo katika Halmashauri Kumi na moja  (11) na Mikoa Nane (8) ya Tanzania Bara.

Amesema nafasi wazi za udiwani katika Kata hizo zimetokana na sababu mbalimbali zikiwemo Vifo, Kujiuzulu na Uamuzi wa Mahakama.

“Baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Tume ina utaarifu Umma kuhusu kuwepo kwa Uchaguzi mdogo katika Kata hizo Kumi na tatu (13),” Jaji Mbarouk alisema.

Kwa taarifa hiyo, Jaji Mbarouk amesema Tume inavialika Vyama vya Siasa, Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi kwa ujumla kushiriki katika Uchaguzi huo.

“Tume inachukua fursa hii kuviasa vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo,” alisema.

Rais Magufuli kuzindua mradi wa umeme Mto Rufiji Julai 26, 2019

$
0
0
Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dk Medard Kalemani amesema Rais wa Tanzania, John Magufuli keshokutwa Ijumaa Julai 26, 2019 ataweka jiwe la msingi katika Mradi wa  kufua umeme wa megawati 2115 wa Rufiji ‘Stigler's Gorge’ uliopo mikoani ya Pwani na Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Julai 24, 2019 Morogoro, Waziri Kalemani amesema tukio hilo kubwa la kihistoria kukamilika kwake kutawezesha Taifa Kuwa na umeme wa kutosha, wa uhakika, unaotabirika na hatimaye kuwa wa gharama nafuu kwa watumiaji.

Amesema wizara inawahakikishia Watanzania kuwa utekelezaji wa mradi huo ni wa kasi, weledi na nidhamu na hiyo ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali inayongozwa na Rais Magufuli.

Mradi huo mkubwa wa umeme utakapokamilika unatarajia kutumia kiasi cha Sh6.5 trilioni ambazo ni fedha za Serikali ya Tanzania.

Uhuru Kenyatta atengua uteuzi wa Waziri wa Fedha, amteua Waziri wa Kazi kushika nafasi yake

$
0
0
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametengua uteuzi wa Waziri wa Fedha Henry Rotich na kumteua Waziri wa Kazi, Ukur Yattan kushika nafasi yake.

Rais Kenyatta ametengua uteuzi huo leo Jumatano Julai 24, ikiwa ni siku moja tangu Rotich apandishwe kizimbani akikabiliwa na tuhuma za ufisadi kufuatia sakata la ujenzi wa mabwawa ya Kimwarer na Arror uliogharimu shilingi bilioni 19 za Kenya.

Rotich alikamatwa Julai 23, kufuatia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini humo, Noordin Haji, kutoa agizo la kumkamata pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Thugge Kamau na maafisa wengine wa Serikali kwa tuhuma za kufanya udanganyifu na kushindwa kutii muongozo wa unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi.

Ahukumiwa Miaka Miwili Jela Kwa Kumuua Mkewe Bila Kukusudia

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela Mhandisi, Novat Kaberwa baada ya kukiri kosa la kumuua mke wake, Clara Munisi bila kukusudia.

Kaberwa anadaiwa kumpiga mke wake na kumsababishia umauti baada ya kurudi nyumbani saa 3 usiku na kukuta watoto wameshinda njaa na mama yao (marehemu) kutokujulikana alipokwenda, kisha baadaye akarudi nyumbani akiwa amelewa kwa kutumia hela ya matumizi aliyoachiwa.

Hukumu imetolewa na Msajili wa mahakama, Pamela Mazengo, baada ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Justus Ndibalema na kukubali kuwa alimuua mke wake bila kukusudia.

Katika maelezo ya awali aliyosomewa anadaiwa mshitakiwa alikuwa anaishi na Mke wake Clara maeneo ya Keko mwanga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa Januari 13,2016 majira ya jioni Clara alitembelewa na dada yake Veronika Munishi nyumbani kwake .

Alidai, Clara  alimfahamisha dada yake huyo kuwa mume wake Kabelwa  kuwa majira ya mchana alimpiga wakati huo mshtakiwa hayupo hapo nyumbani.

Baada ya hapo Clara na Veronika walienda dukani kununua mafuta ya kupikia wakati wanarudi nyumbani walimkuta mshtakiwa amerudi  nyumbani ndipo ugomvi ulianza  baina yao.

Wakati ugomvi ukiendelea Veronika alifanikiwa kukimbia wakati mshtakiwa akiendelea kumpiga mdogo wake Clara huku akimburuza na kumtoa nje ya geti ndipo marehemu akapiga kelele na majirani wakaja.

Kabelwa alipowaona majirani hao alikimbia ambapo walimchukua Clara na kumpeleka kituo cha Polisi na baadaye walimkimbiza katika hospitali ya Rufaa ya Temeke.

Inaelezwa kuwa hali ya Clara iliendelea kuwa mbaya na ilipofika Januari 14,2016 alifariki na mwili wake ulipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi.

Januari 18,2016 uchunguzi wa mwili wa marehemu ulifanyika na ripoti ilionyesha sababu ya kifo chake damu ilivia tumboni.

Ilidaiwa kuwa, Januari 15,2016 Kabelwa alikamatwa eneo la Kilosa mkoani Morogoro na kuletwa kituo cha Polisi Chang’ombe.

Mhe Hasunga Aanza Ziara Ya Ukaguzi Wa Shughuli Za Maendeleo Jimboni Vwawa Mkoani Songwe

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameanza ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa.

Akiwa katika kata ya Iyula Mhe Hasunga amekagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na kuzungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Iyula ambapo pamoja na mambo mengine amewasisitiza wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kujikwamua katika wimbi la ujinga kadhalika kiuchumi.

Waziri Hasunga amewapongeza walimu wa shule hiyo kwa mshikamano na usimamizi madhubuti wa fedha za ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa ambavyo vimefikia katika hatua nzuri ya kuanza kutumika.

“Mna bahati sana kusoma katika shule ambayo imetoa waziri wa kilimo hivyo ili kuwa na viongozi wengi katika Taifa hili mnapaswa kusoma kwa bidii na kuongeza ufaulu katika Takwimu za mkoa wetu” Alisema Mhe Hasunga

Pamoja na kuchangia shughuli za maendeleo katika jimbo hilo la Vwawa lakini pia amewataka wanafunzi hao kutambua kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuimarisha elimu na imeanza na utoaji wa elimu bure kuanzia ngazi ya awali mpaka sekondari.

Alisema kuwa lengo la Rais Magufuli kuruhusu elimu kuwa bure ni kutaka kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa urahisi kwa wanafunzi wote nchini ili hata wale waliokosa fursa kutokana na kipato duni cha wazazi waweze kuelimika na kuwa msaada katika familia zao na Taifa kwa ujumla.

Mhe Hasunga amesema kuwa pamoja na vitabu kuwasaidia wanafunzi kuelimika lakini wazazi na walimu ni sehemu ya uimara wa mafanikio ya wanafunzi katika ufaulu wao.

“Mimi nawapongeza sana ninyi wanafunzi kwani mna bahati kubwa kusoma katika kata zenu mnazoishi maana sisi wakati tunasoma tulikuwa tukienda umbali mrefu kutafuta elimu jambo ambalo lilikuwa likitukatisha tamaa ya kusoma” Alikaririwa Mhe hasunga

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga atakuwa na ziara ya siku tano katika jimbo hilo ambapo pamoja na mambo mengine atashirikiana na wananchi katika shughuli za maendeleo.

Waitara awatolea uvivu wanaoihujumu CCM

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Naibu waziri wa ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi Mwita Waitara amewaonya wanaCCM wanaoendelea kukihujumu chama cha mapinduzi angali bado ni wanachama huku wakijua hawakitendei haki chama hicho.

Waitara akiwa mkoani Njombe amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wanachama wa aina hiyo kwa kuwa wamekuwa wakijaribu kurudisha nyuma jitihada za kuyafikia maendeleo ya chama hicho.

“Hauwezi kuwa mbunge wa chama cha mapinduzi,unaingia kwenye vikao vya CCM  vya chama halafu unapinga serikali huko nje na chama chake hauwezi kuwa,ukitaka ubaki salama kama wewe na maisha yako utakufa,wenzetu ulaya huwa wanaua nenda China kafanye mambo hayo”amesema Waitara

Waitara ameongeza kuwa
“Kwa hiyo huwezi kuwa mbunge wa chama cha mapinduzi,unakaa kwenye vikao vya chama,watu wanapanga mikakati halafu ukiwa mtaani unatoa yote,unatuhujumu ni kama tupo kwenye mtumbwi tunaogelea unatoboa inatakiwa tukuwahi ili uzame wewe tusizame wote ili tubaki salama”alisema Waitara

Akizungumzia upande wa watumishi wa umma waziri huyo ametoa wito kumuunga mkono rais Magufuli kutokana na juhudi kubwa anazozifanya kwa watanzania.

“Kwa mtu mstaarabu anayejua uongozi maana yake nini,siwezi kukubali uteuzi nikaenda nikala kiapo,nikapewa majukumu,nikapewa na gari nikapewa na posho nikapewa na mshahara halafu nikakaa  kwenye vijiwe nikamtukana Rais hivi unakuwa unaakili kweli,sasa watu ambao wanashangaa hivi watu wanaondolewa uongozi wewe hujui utaratibu”alisema tena Waitara

Rais Magufuli ateua Mkuu wa Wilaya usiku huu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Edward Mpogolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida.

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 24 Julai, 2019, Mpogolo anachukua nafasi ya Bw. Miraji Mtaturu ambaye amechaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mpogolo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, nafasi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma itajazwa baadaye.


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi 25 July

Taarifa muhimu kutoka Wizara ya Maji

Wananchi Wakumbushwa Kujiandikisha Daftari La Mkaazi Kwa Ajili Ya Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amewahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mkaazi ili kupata fursa ya kuchagua viongozi bora katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mhe Hasunga ametoa wito huo  jana tarehe 24 Julai 2019 kwa wananchi wakati wa mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kijiji cha Ipapa, Ipanzya na Mpela katika kata ya Ipunga sambamba na vijiji vya Maronji, Shilanga na Hanseketwa vilivyopo katika kata ya Ihanda.

Alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ajili ya kuchagua wajumbe na wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa ni muhimu kwani ndio sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaowahusisha Madiwani, Wabunge pamoja na Rais.

Hivyo umuhimu wa wananchi kujiandikisha ni sehemu ya kufanya maamuzi ya viongozi watakaowawakilisha katika kipindi cha miaka mitano kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili wananchi katika jimbo hilo ambazo kwa sehemu kubwa zimetajwa kuwa ni pamoja na uboreshaji wa barabara, Zahanati na upatikanaji wa maji, Mhe Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejikita katika dhamira ya utatuzi wa changamoto hizo kwa kipindi cha muda mfupi na malengo ya muda mrefu.

Mbele ya wananchi Mhe Hasunga amekiri kuwa kumekuwa na tatizo sugu na la muda mrefu kwenye sekta ya Kilimo la kuchlewa kwa pembejeo kuwafikia wakulima lakini tayari amekemea na kuagiza Taasisi zinazohusika kufikisha pembejeo kwa wakati.

Alisema kuwa Uongozi wa Taasisi itakayoshindwa kufikisha pembejeo kwa wakati na kukwamisha juhudi za serikali katika kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya wakulima utachukuliwa hatua za haraka ikiwemo kusimamishwa kazi.

Kadhalika Mhe Hasunga amepiga marufuku kuzuia kwa kufunga mipaka ya biashara ya Mazao badala yake wananchi wametakiwa kuuza popote watakapo.

MWISHO

Umoja Wa Wanafunzi Vyuo Vikuu Mkoa Wa Dodoma Wamwandikia Waraka Mzito Rais Magufuli

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
UMOJA wa vijana wanafunzi wazalendo wa Vyuo vikuu  Mkoa wa Dodoma,  wamemuandikia Walaka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, wakimpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya tangu alipoingia madarakani mwaka 2015.

Katika walaka huo uliouwasilishwa na msemaji wa umoja huo, ambaye ni Rais ya serikali ya wanafunzi wa chuo cha mtakatifu Yohana(st John univesity) Jerry Motela kwa mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.
 
Umoja Wa vijana hao wa vyuo vikuu umeeleza kuridhishwa na kazi kubwa anayoifanya Rais Magufuli  hasa katika kusimamia misingi ya uzalendo na kuwaamini vijana na kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi  hivyo ni jambo la kuigwa kwa viongozi wengine watakaofuata nyayo  zake.
 
“Kwanza kabisa tunapenda kukupongeza wewe binafsi na serikali yako ya awamu ya tano kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya katika nchi yetu, dhumuni la tamko hili ni kuunga mkono na kukutia moyo kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya”
 
“Tunapenda kusema kusema sisi kama vijana tunaimani kubwa sana na wewe binafsi pamoja na serikali yako unayoiongoza,  sisi umoja wa wanafunzi wazalendo wa vyuo vikuu vya Dodoma tumeamua kutoa tamko kwa yote uliyotufanyia vijana wa taifa hili kwa kuwachagua katika ngazi mbalimbali” amesema Motela.
 
Wamemuomba Rais kuwapuuza wale wote  ambao wanaonyesha dalili za viashiria vyovyote vya kutaka kukwamisha juhudi zako za kutuletea maendeleo katika nchi yetu.
 
Pia wamempongeza kwa kuboresha miondombinu ya elimu hapa nchini, ikiwamo kukarabati shule kongwe ili kuendana na hali ya sasa, sambamba na kutoa elimu bure kutoka elimu ya msingi hadi sekondari kidato cha nne.
 
Wamempongeza kwa kuongeza wigo udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini, kitendo kimetoa fulsa kubwa kwa wanafunzi wengi kuweza kujiunga na elimu ya juu.
 
Wamesema wamefurahishwa na suala la kuboresha mikopo suala ambalo hapo mwanzo lilikuwa sugu na kusababisha migomo ya mara kwa mara katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
 
“Mh Rais suala ambalo lilikuwa likionekana sugu na kusababisha migomo mingi katika vyuo vikuu vingi hapa nchini ni suala la ucheleweshaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo jambo umelipatia ufumbuzi, na sasa mikopo hiyo inapatikana tena kwa wakati” amesema.
 
Pia wamempongeza kwa kuboresha miondombinu mbali mbali ikiwamo, katika sekta ya Afya, usafiri wa aina zote na hasa kutengeneza reli ya kisasa na kununua ndege nane tena za kisasa na kurahisisha usafiri huo.
 
Nae mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi wakati akipokea walaka huo, ili kumfikishia Rais wa Tanzania, amewapongeza kwa jambo hilo kwa kusema ni  jambo la kizalendo na linatakiwa kuigwa na vijana wengine kwa sababu ni jambo la kizalendo.
 
“Kwanza niwapongeze kwa jambo hili ni jambo la kizalendo na linatakiwa kuigwa na vijana wengine kwa kuonesha uzalendo kwa kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu mzalendo” amesema.
 
Pia amewapongeza kwa kujikita katika kutoa pongezi kwa kazi kubwa inayofanywa na Rais wan chi,  tofauti na wengine ambao wamejikita katika kuwaponda watu wengine na kuwajibu wengine, lakini wao wamejikita kwa  pongezi.
 
Amesema serikali ya awamu hii ipo kazini kwa ajili  ya kutekeleza ilani ambayo ndiyo aliyoiombea kura kwa wananchi, na  suala kubwa kabisa ni la kukomesha suala lamigogoro na migomo iliyokuwa ikitokea mara kwa mara katika vyuo mbali mbali.
 
Pia amewataka wanafunzi hao  kuwa  mfano kwa jamii na kuiongelea vizuri serikali  hii ambayo imejikita katika kkutatua kero za wananchi, na amewataka kutokuishia hapo tu bali  waendee kuwaelimisha vijana na kusambaza  walaka huo na katika mitandao ya kijamii ili kujenga kizazi cha uzalendo.
 
Kwa upande wake mmoja wa waliokuwepo katika maandamano hayo Jamal Adam, ambaye ni spika wa bunge wa chuo cha serikali za mitaa cha Mipango, amesema wameamua kufanya hivyo ili kusherehesha kazi nzuri ambayo inafanywa na Rais dkt John Magufuli ili hata wale ambao hawaoni anayoyafanya nao wajue mambo makubwa yanayofanywa katika nchi yetu.
 
“ Lengo ni kuwaonesha wale ambao hawaoni kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu, na sisi kama vijana lazima tuoneshe uzalendo kwa kusherehesha yale mazuri ambayo yanafanywa na Rais wetu ili na watu wengine wayaone” amesema Adam.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma[PSSSF] Watumia Bilioni 122 Kulipa Kiinua Mgongo kwa Wastaafu

$
0
0
Na.Faustine  Gimu Galafoni,Dodoma.
Mfuko wa  Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma[PSSSF] kuanzia Juni 1 hadi Julai 24,2019   umelipa kiinua mgongo kwa wastaafu  elfu  mbili ,mia sita na hamsini[2,650] huku zikitumika Tsh.Bilioni 122.9  kulipa wastaafu hao.
 
Hayo yamesemwa Julai 24,2019 jijini Dodoma na Meneja kiongozi ,uhusiano wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii  kwa Watumishi wa Umma[PSSSF] Bi.Yunis Chiume wakati akitoa taarifa ya Maendeleo ya Mfuko huo kwa  vyombo vya habari.
 
Bi.Chiume amesema kuwa ,PSSSF  unaendelea na jukukumu lamsingi la   kulipa pensheni kwa wastaafu ambapo pia umelipa  pensheni ya Mwezi kwa wastaafu laki moja,ishirini na sita elfu na arobaini na tatu[126,043]  na kiasi kilichotumika ni  Tsh.Bilioni 92.7.
 
Aidha,Bi.Chiume amesema idadi ya wastaafu ambao  hawajalipwa mafao imepungua kutoka wastaafu 227  Mwezi Mei,2019 na kubaki wastaafu 119 hadi sasa na sababu zinazosababishwa kutolipwa kwa wastaafu hao ni pamoja na kukosa kwa viambatanisho ,pingamizi la waajiri juu ya vyeti feki,kupokea mshahara baada ya kustaafu,na kutofautiana kwa sababu ya kustaafu kati ya nyaraka halisi na mfumo wa utumishi huku juhudi zikiendelea kufanyika  ili kutatua mapungufu hayo    ili wanachama  waweze  kupata mafao  kwa mujibu wa sheria.
 
Bi.Chiume ameongeza kuwa baada ya mifuko ya PPF ,LAPF,GEPF,na PSPF kuunganishwa na kuundwa PSSSF tarehe 1,Agost,2019 serikali inafanya tathmini juu ya Mafao ya Uzazi  na tathmini hiyo ikikamilika taarifa itatolewa kwa umma .
 
Kuhusu mfumo wa  Malipo wa Government Electronic Payment Gatway[GePG]  Bi.Chiume amesema umeleta faida kwa mwajiri kujifanyia tathmini ya michango inayotolewa na PSSSF ,Kujitengenezea Ankara za malipo  ,kutengeneza control number,kuweka hesabu sawa,kuweza kupata risiti kwa wakati,kupunguza safari za kwenda kwenye ofisi za mfuko.
 
Na Faida kwa Mfuko ni kuongeza uwazi,ufanisi,kukusanya michango kwa wakati,mawasiliano rahisi na kutambua wanaowasilisha michango kwa wakati.
 
Pia ,Bi.Chiume amegusia juu ya suala la mfumo wa Majalada ya kielektroniki [Paperless  Work  Envinronment ]ambapo mfuko wa PSSSF Umeanza kutumia mfumo huo kwa kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali  na kuongeza ufanisi na kupunguza matumizi ya karatasi.
 
Sanjari na hayo ,katika kueneza elimu kwa umma,PSSSF imeshiriki katika maonesho 43 ya kimataifa ya  Dar Es Salaam na Jumla ya Wastaafu 381 na wanachama na wananchi wengine 1,040  walihudumiwa  huku mfuko huo wa PSSSF Ukitarajia kushiriki kutoa huduma na Elimu kwa wananchi kwenye maonyesho ya Wakulima Nanenane Agosti 1 hadi 8 ,2019 yatakayofanyika katika eneo la Nyakabindi ,Bariadi ,Simiyu  huku maonesho mengine ya PSSSF  yakitarajia kufanyika katika mikoa ya Ruvuma,Mbeya na Morogoro.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images