Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

January Makamba Kafunguka Tena Baada ya Mawaziri Wapya Kuapishwa

0
0
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumuamini na kumteua kushika wadhifa huo.

Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), uteuzi wake ulitenguliwa jana Jumapili Julai 21 na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter leo Julai 22, Makamba ameandika ujumbe wa kumshukuru Rais Magufuli saa chache baada ya kuwaapisha Waziri Simbachawene na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ambaye amechukua nafasi ya Innocent Bashungwa aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

“Neno la Mwisho kwenye hili:
Namshukuru Rais kwa kuniamini, Makamu wa Rais kwa kunielekeza, PM kwa kunisimamia, na Team ya VPO/NEMC na Mawaziri wote kwa ushirikiano. Nampongeza @HusseinBashe na Simbachawene kwa kuaminiwa. Nawatakia heri na kuwaahidi ushirikiano wangu wa dhati. 🙏🏾"
-Ameandika January Makamba

Jana Jumapili, Rais Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wa Makamba na kumrejesha tena Simbachawene aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), miaka miwili iliyopita.

Rais Magufuli aagiza kigogo aliyesimamishwa kazi mwaka 2016 arejeshwe kazini

0
0
Rais Magufuli ameagiza Dkt. James Mataragio  arejeshwe katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), baada ya kusimamishwa kazi tangu Agosti 2016.

Agizo hilo amelitoa leo Julai 22, 2019 kupitia taarifa ya Ikulu ambayo imeeleza kuwa Rais, ameitaka Wizara ya Nishati kumrejesha kazini Mkurugenzi huyo Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.

Rais Mstaafu Mwinyi Kasema Hajafurahishwa na Kitendo cha January Makamba Kuweka Picha Yake Baada ya Kutumbuliwa

0
0
Rais  Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi amesema hajafurahishwa na kitendo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba kutumia picha waliyopiga pamoja mitandaoni muda mfupi baada uteuzi wake kutenguliwa na Rais Magufuli.

Katika picha hiyo, ambayo January aliiweka muda mchache baada ya rais kutengua uteuzi wake ikimuonyesha yeye na Mwinyi wamekaa kwenye viti viwili tofauti, ambapo aliandika;
“Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo.”

Mwinyi amesema hakuona ubaya wa picha ile na wala hakuchukizwa nayo kwa sababu watu wengi wanaokwenda kumuona humuomba picha ya ukumbusho lakini kilichomshangaza ni kitendo cha kutumia picha hiyo katika kipindi hichi.

“Kwa kweli sikupenda kuona picha ya namna ile katika mazingira haya, ile ni picha ya kawaida maana watu wengi wanakuja kuniona na tukishamaliza kuzungumza wanasema tupate ukumbusho na tumefanya sana kwa mtu mmoja mmoja na kwa watu wengi sana kwahiyo nimestaajabu nilipoona imewekwa wakati huu.

“Kijana yule amendika kitabu na aliniomba nimsaidie kuandika dibaji, inawezekana alifanya kama kushukuru lakini silaumu wala sioni vibaya ila kwanini ikawe katika mazingira haya wakati maji yamekorogeka.

”Ile picha ni ya zamani lakini mambo yametokea leo na huko zamani tulikuwa na sababu ya kufanya hivyo kwasababu na mimi nilishika nafasi hii lakini pia kulikuwa na uhusiano wa kitabu chake alichokiandika maana si cha sasa hivi kiliandikwa zamani lakini kwanini ikawa sasa hivi hili kidogo limenishtua,” amesema Mwinyi. 


==> Msikilize hapo chini

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne 23 July

Waziri Mkuu Aagiza Eneo La Mnara Wa Zinjathropous Liboreshwe

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii isimamie uboreshaji wa eneo la mnara wa Zinjathropus ili paweze kuvutia zaidi.

Ametoa agizo hilo jana mchana (Jumatatu, Julai 22, 2019) wakati akizungumza na wananchi na viongozi waliohudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la Zinjathropus Bosei, eneo la bonde la Olduvai, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

Maadhimisho hayo yamefanyika ndani ya hifadhi ya Ngorongoro sambamba na uzinduzi wa makumbusho ya Dkt. Mary Leakey. Mnara wa Zinjathropus na Homo habilis umejengwa kwenye hifadhi ya Ngorongoro karibu na njia panda ya kuelekea bonde la Olduvai.

“Kwenye mnara wa Zinjathropus na Homo habilis pasiachwe kama palivyo. Pajengwe seng’eng’e kuzunguka eneo lile lakini pia paweke kibanda cha mlinzi ambaye pia atakuwa anatoa taarifa kwa wageni wanaopita hapo.”

“Mtafute vijana kadhaa ambao ni wenyeji wa eneo hili, wafundishwe historia kamili kisha wapewe ajira hizo. Kibanda kikijengwa kwa juu kiwe na vioo ili anayelinda aweze kuona pande zote na pia muweze kumkinga na vumbi na upepo mkali wa eneo lile.”

Waziri Mkuu pia alitembelea korongo la Frida Leakey, (mahali ambapo zinjathropous aligunduliwa) na kupata maelezo juu ya kugunduliwa kwa fuvu la mtu wa kale duniani yapata miaka milioni mbili iliyopita.

Akigusia kuhusu uhifadhi wa eneo hilo, Waziri Mkuu alisema nako pia pajengwe kibanda cha mlinzi mwenye uwezo wa kutoa taarifa kwa watalii na akasisitiza pia ajira hizo ziwahusu wenyeji wa eneo hilo.

“Kwenye korongo la Frida, pawekwe bango lenye maelezo ya Kiswahili, nako pia wapatikane vijana sita au nane, waeleweshwe hiyo historia, wakifuzu, Wizara iwawezeshe, wapangiane zamu ya kushinda hapo. Pia pajengwe kibanda cha wageni kupumzikia wakifika eneo hilo.

Kuhusu makumbusho ya Dkt. Leakey, Waziri Mkuu alisema makumbusho hayo ni lulu kwa Taifa. “Ninawapongeza viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Ngorongoro kwa kuendeleza na kutunza makumbusho haya.”

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah alisema kwa sasa dunia inatambua kuwa chimbuko la binadamu ni Afrika. “Hata kama tunatofautiana sura na rangi, watu wote duniani wana asili ya Afrika. “Kwetu sisi Tanzania, tunaadhimisha uvumbuzi huu kwa sababu fuvu la Zinjanthropus ni alama na nembo ya Tanzania na dunia.”

Alisema maadhimisho hayo yataendelea kwa kufanya maonesho ya fuvu la Zinjanthropus boisei na malikale zingine katika mikoa sita ya Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Mtwara na Dodoma.

Alisema wizara yake imebaini fursa zilizopo kwenye sekta ya urithi wa utamaduni yaani malikale au utamaduni tuli (static cultural heritage) na utamaduni hai (dynamic culture) ili  kuvutia watilii na hivyo kuongeza idadi yao na kuwafanya waongeze muda wa kukaa nchini (length of stay) na hatimaye kuongeza pato la Taifa litokanalo na utalii.

“Wizara yangu imeanza kuiboresha na kuendeleza sekta ya malikale na urithi wa utamaduni ili izalishe mazao ya utalii na kuvutia watalii kwa kuhamisha vituo vya Idara ya Mambo ya Kale na kuvipeleka TANAPA, TAWA, NCAA, TFS na Makumbusho ya Taifa ili viendelezwe na kuwa vivutio vya utalii.

“Pia tumehamishia Makumbusho ya Taifa kazi zote za uhifadhi wa urithi wa utamaduni tuli au malikale na kuanzisha tamasha la urithi wa utamaduni wa Mtanzania (Urithi Festival: Celebrating Our Heritage).  Tamasha hili litasherehekewa Septemba, kila mwaka.

Naye Balozi wa Marekani hapa nchini, Dk. Inmi Patterson ameipongeza Serikali kwa kukuza na kuendeleza utalii wa kitamaduni.

Pia alisifu utajiri wa rasilmali misitu na wa nyama ambao Tanzania imejaliwa kuwa nao. “Uamuzi wa Rais Magufuli wa kuanzisha hifadhi ya Burigi, unazidi kunogesha sifa ya Tanzania katika suala la hifadhi za maliasili na utalii na katika kukuza urithi na utajiri wa nchi,” alisema kwa Kiswahili fasaha.

Alisema maadhimisho hayo ni siku muhimu kwake kwani yamewakutanisha watu wa kaliba tofauti wakiwemo wanasiasa, wanasayansi, maprofesa kutoka Uingereza, Marekani na Ujerumani, wanafunzi kutoka shule za Tanzania na wenyeji wa Ngorongoro.

Rais Mstaafu Mwinyi Auponda Waraka wa Kinana na Makamba

0
0
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, amesema kitendo cha makatibu wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba kuandika waraka kuhusu hali ya kisiasa nchini, ni utoto.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa zimepita siku chache tangu viongozi hao walipoandika waraka kwenda Baraza la Viongozi Wastaafu na kuzua gumzo kwa viongozi na wananchi wa kada mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilieleza kuwa Mwinyi hakubaliani na jambo hilo.

“Kuhusu waraka ulioandikwa na makatibu wakuu wastaafu, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba kwenda kwa Baraza la Viongozi Wastaafu, ni utoto,” alisema Mwinyi.

Alipongeza majibu yaliyotolewa na Katibu wa Baraza hilo, Pius Msekwa na kusema walioandika waraka huo wameshindwa kufuata katiba na taratibu za chama.

“Viongozi wastaafu hawawezi kupoteza muda wao kwa masuala ya kitoto,” alisema.

Aliwataka Watanzania kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya za kuleta maendeleo kwa muda mfupi.

Alisema ukiondoa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, viongozi wengine waliofuata akiwemo yeye, wamefanya juhudi za kuipeleka nchi mbele, lakini kasi ya Rais Magufuli ni kubwa zaidi.

Rais Magufuli Atoa Agizo Kero Ucheleweshaiji Vibali NEMC Itatuliwe

0
0
Na: Frank Shija – MAELEZO
Rais John Pombe Magufuli metoa agizo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Goerge Simbachawene  kushughulikia kero ya ucheleweshwaji wa vibali kwa wawekezaji ili kuendana na kasi ya uchumi wa viwanda.

Amelitaka  Baraza la  la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kutochelewesha utoaji wa vibali kwa wawekezaji ili kuongeza ufanisi katika ukuaji wa uchumi wa viwanda.

“Pasiwe na ucheleweshwaji wa vibali vya NEMC kwa viwanda vyetu, sisi tunataka kuwa na viwanda vya kutosha na wawekezaji wasiwekewe vikwazo kwa visingizio vya NEMC, vibali hivi vitoke kwa sababu tunahitaji viwanda, ikiwezekana wawekeze kwanza vibali vya NEMC vitafuata baadae,”alisema Dkt. Magufuli.

Rais Magufuli amemtaka Simbachawene kusimamia kwa karibu suala hilo la ucheleweshwaji wa vibali vya Tathmini ya uharibifu wa Athari ya Mazingira vinavyotolewa na NEMC.

Rais Magufuli ameongeza kuwa fedha nyingi zinatolewa na wafadhili kwa ajili ya miradi ya mazingira lakini kumekuwa hakuna matokeo ya kuridhisha hivyo ametaka kuwepo usimamizi madhubuti wa rasilimali fedha inayoelekezwa katika miradi ya mazingira.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amempongeza Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Mohamed Bashe kwa uchambuzi mzuri wa masuala ya kilimo aliokuwa anaufanya akiwa bungeni na kuongeza kuwa hiyo ndiyo sababu ameamua kumteua ili akayatekeleze kwa vitendo kwa ajili  ya kukwamua kilimo.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Boniphace Simbachawene amesema kuwa shughuli zote za kiuchumi zinategemea sana mazingira  hivyo atashirikiana na wataalamu wa wa ofisi yake kumshauri vyema Makamu wa Rais katika namna bora ya kutatua changamoto zitokanazo na uharibifu wa mazingira.

Ameongeza kuwa fedha zinazotajwa kuingia katika nchi kwa ajili ya mazingira ni nyingi lakini zimekuwa zinatumika zaidi katika masuala ya kiutawala badala ya kuelekezwa katika miradi ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

“Nataka nikuhakikishie Mhe. Rais kuwa nitamsaidia Makamu wa Rais katika Ofisi yake, kwanza natambua lakini pili mimi kwa kushirikiana na wenzangu nitakaowakuta pamoja na walaalamu nitajitahidi kutoa mawazo yangu ili tuone ni namna gani tunaokoa mazingira,” alisema Simbachawene.

Akizungumzia masuala ya Muungano, Waziri Simbachawene amesema kuwa anafahamu kuwa msingi wa Muungano wetu siyo tu yaliyoandikwa katika Katiba na kufafanuliwa katika sheria bali ni wa kihistoria ambao unajengeka katika maelewano zaidi badala ya maandishi.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Mohamed Bashe amesema kuwa anafahamu changamoto zinazowakabili wakulima wa nchi hii hasa ukizingatia kuwa ndiyo sekta inayowagusa asilimia kati ya 60-70 ya watanzania wote, wengi wao ndiyo wanyonge ambao Rais Magufuli ndiye mtetezi wao.

Amesema kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kwa mamlaka atakayopewa kuhakikisha anamsaidia Mhe. Rais katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ili kukwamua sekta ya Kilimo nchini.

Hafla hii ya uapisho imefanyika kufuatia Mhe. Rais kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba na nafasi yake kuchukuliwa na Waziri George Simbachawene, huku Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Innocent Bashungwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara..

Mwisho.

Abiria sita wafariki dunia katika ajali ya Hice na Land Cruiser Kahama.

0
0
NA SALVATORY NTANDU.
Watu sita wamefariki dunia na wengine 24 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia jana  katika eneo la nyambula barabara ya kahama kakola  kata ya Ngogwa Wilayani  Kahama mkoani Shinyanga baada ya Magari mawili kugongana uso kwa uso aina ya Totoya hice yenye namba T 710  AZZ na Toyota  Land cruiser  yenye namba za usajili T 477 ATC.

Akizungumza na waandishi wa Habari  jana mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya kahama,DK George Masasi amekiri kupokea majeruhi hao ambao wanaenelea kupatiwa matibau  na miili ya watu sita  waliofariki dunia.

Amesema majeruhi watatu wamepewa rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali ya Bugando kutokana na hali zao kutokuwa nzuri huku majeruhi wengine 19 hali zao zinaendelea vizuri na ambao hali zao zitaimarika wataweza kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Nao baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo Salu Maige na Martine Marice wamesema dereva wa gari aina ya Hice alikuwa na mwendo kasi ambapo lilimshinda na kusababisha ajali hiyo huku barabara hiyo ikiwa na vumbi kubwa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kahama Anamringi Macha ameserikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kuwataka abiria kupaza sauti ili kudhibiti ajali.

Amesema wamebaini baadhi ya Madereva wa magari ya abiria  yaenda vijijini hawazingatii sheria za usalama kwa kuendekeza mwendo kasi huku magari mengine yakiwa ni mabovu hivyo watahakikisha wanasimamia usalama wa abiria kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.

Naye kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kuahidi kuwa wataanza ukaguzi maalum wa magari yanayoekea katika Halmashauri za Msalala na Ushetu baada ya kubaini uwepo wa taarifa za mwendo kasi kwa madereva.

Amewataja majina waliofariki ni pamoja na dereva wa Hice, Enock maganga(32),Buruan Yasini (32) Mwanamke mmoja na watoto wadogo wa kiume wa wawili na mmoja wa kike wenye umri wa miaka kati ya mitatu hadi mitano ambao majina yao hayajafahamika.

Kamanda Abwao ametoa rai kwa ndugu jamaa na marafiki kujitokeza kuwatambua ili waweze kukabithiwa ndugu zao kwaajili ya tararibu za mazishi.

Kubenea Ataka Wanaosambaza Mawasiliano ya Simu ya Nape, Makamba, Kinana Wachukuliwe Hatua

0
0
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini (TCRA) kutoa taarifa za waliohusika kudukua mawasiliano ya simu ya mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na watu wengine.
 

Wiki iliyopita sauti fupi za mazungumzo ya simu yanayomhusisha Nape, aliyekuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba na makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii

Akizungumza na vyombo vya habari  jana  Julai 22, Kubenea alisema kitendo kilichofanyika ni kinyume cha katiba na sheria za nchi ambazo zinatoa uhuru wa faragha kwa mtu.

“Hii ni hatari sana kama viongozi wanafanywa hivi kwa mambo ya faragha kutolewa si hata baadaye watu wanaweza kuvunja ndoa za watu, kama Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amezungumza na hawara kwa mfano ikatoka nje si jambo la hatari hili, kuna vitu ambavyo vinatakiwa kuwa na usiri kwa maana kama hawa ni viongozi tu je wananchi wa kawaida inakuaje..?


"Haya mambo hayawezi kufanyika katika nchi inayojali utu wa mtu. TCRA itoe taarifa, ni nani aliyefanya kazi hiyo chafu." Alisema

Wagunduzi wa umeme Njombe kusaidiwa mitambo ya kisasa

0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Waziri wa nishati dkt.Medard kalemani ametoa maelekezo kwa shirika la umeme Tanzania Tanesco kuhakikisha linafikisha baadhi ya mitambo ya kisasa kwa wagunduzi wa umeme walioibuliwa hivi karibuni mkoani Njombe ili kuweza kuongeza uzalishaji wa nishati  katika vyanzo vyao.

Waziri kalemani ametoa maelekezo hayo mkoani Njombe alipotembelea mitambo ya kuzalishia umeme kwa wagunduzi John fute (Mzee pwagu) wa Msete pamoja na bwana Lainery Ngailo wa Lugenge mjini Njombe mkoani humo.

“Mfano nilivyoiona haraka ile pressure ya maji hapa kwa mzee Fute ni kubwa sana sio ya kutumia tu kupata kilowati 28 tunaweza tukapata hata megawati moja,na megawati 1 inaweza ikahudumia wananchi zaidi ya 800 mpaka 1000 hata kata nne,ukiangalia Burundi wana megawati 45 za umeme na wanahudumia nchi nzima”amesema Kalemani

Waziri kalemani ameongeza kuwa

“Tanesco wanachotakiwa ni kushirikiana na huyu bwana ili kusudi waanze kujenga ile kingo,waweke transfoma tuone pa kuanzia kama mfano pamoja na kumsaidia Tabani,tunaweza kufanya kama project kwa mwaka mmoja lakini wakati huo mwaka mmoja wananchi majirani wa hapa wakatumia huo umeme bure ili kutazama hali itakavyo kuwa”amesema Kalemani

Awali wagunduzi hao akiwemo mzee John fute alisema,umeme anaouzalisha anautumia kwaajili ya matumizi yake nyumbani lakini hata hivyo amesimamisha huduma za usagaji  wa nafaka kutokana na kufunga tabani ndogo huku mzee Ngailo naye akishukuru kwa uamuzi wa waziri.

“mfano mimi nilikuwa nawasaidia hata majirani kusaga unga kwa shilingi mia tano,lakini kwa sasa nimefunga kutokana na kufunga tababani ndogo,na mimi hapa kwenye chanzo changu kuna kama kilowati 300 hivi ambazo kwa kuanzia ninaweza kuwasambazia kama watu 600 hivi lakini kwa sasa hivi ninazalisha chini ya kilowati 28”alisema Mzee pwagu

Hata hivyo licha ya wagunduzi hao kukabidhiwa fedha kiasi cha shilingi milioni 15 kila mmoja siku chache zilizopita  na shirika la umeme Tanzania tanesco kutokana na ahadi iliyotolewa mbele ya Rais Magufuli,shirika limeweza kusimika jumla ya Nguzo sabini,kurekebisha mashine,kufunga nyaya mpya pamoja na vikombe kutoka kwenye chanzo cha umeme cha mzee Ngailo na kughalimu takribani milioni 100.

Washitakiwa Wengine Watano Raia wa Kigeni Kuongezwa Kesi ya Kutekwa Mo Dewji

0
0
Upande wa mashtaka katika kesi ya kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa hati ya kuwakamata washtakiwa watano ili waunganishwe na mshtakiwa wa kwanza, Mousa Twaleb.

Walioongezwa ni raia wa Afrika Kusini, Phila Tshabalala na wenzake wanne raia wa Msumbiji ambao ni, Henrique Simbue, Daniel Berdardo Manchice, Issac Tomu na Zacarious Junior.

Mahakama imetoa hati hiyo leo Jumanne Julai 23,   mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuomba kufanya hivyo.

Washtakiwa hao wanatakiwa kuunganishwa katika shtaka la pili na shtaka la tatu ambapo shtaka la kwanza linamkabili Twaleb ambaye anadaiwa  kujihusisha na genge la uhalifu,  kati ya Mei mosi mwaka 2018 na Oktoba mwaka huo Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Johannesburg Afrika Kusini.

Inadaiwa shtaka la pili la kujihusisha na genge la uhalifu linamuhusu washtakiwa wote wanaosakwa ili wafikishwe mahakamani.

Shtaka la tatu washtakiwa wote wanadaiwa kuteka nyara, inadaiwa Oktoba 11 mwaka 2018 katika Hoteli ya Colleseum wilayani Kinondoni, akiwa pamoja na wenzake walimteka mfanyabiashara, Mohammed Dewji kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri kinyume cha sheria.

Mshtakiwa Twaleb katika shtaka la nne wanadaiwa kutakatisha fedha Sh milioni nane, inadaiwa Julai 10 mwaka jana maeneo ya Mbezi Beach alijipatia kiasi hicho cha fedha huku akijua fedha hizo ni mazalia ya genge la uhalifu. Kesi itatajwa Agosti 6 mwaka huu.

Jeshi la Polisi Laanza Uchunguzi wa Sauti Zinazodaiwa za Napee, Kinana na Makamba

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema wanafanya uchunguzi wa sauti zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii, zinazodaiwa ni za baadhi ya viongozi wa wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali.

Sauti hizo fupi za mazungumzo ya simu zinadaiwa kuwa za Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye; aliyekuwa waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), January Makamba; makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba pamoja na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Benard Membe.

 
IGP Simon Sirro amesema wameziona sauti hizo na wameanza kuzifanyia uchunguzi japo hajafahamu uchunguzi huo utakamilika baada ya muda gani na endapo itathibitika kuna makosa ya jinai, watuhumiwa watachukuliwa hatua za kisheria.

"Ni kweli hata sisi hizo sauti nimezisikia na tunafuatilia ili kujua ukweli wake, tukibaini kama kuna kesi ya jinai na kama yaliyokuwa yakitamkwa ni kweli basi tutachukua hatia za kisheria", amesema.

"Kuhusu uchunguzi utakuwa muda gani mimi sijui, inategemea shauri lenyewe", ameongeza IGP Sirro

Wakati huohuo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kupitia msemaji wake, Semu Mwakyanjala ameeleza kuwa suala hilo wamewaachia Jeshi la Polisi.

"Uhalifu wowote unaoripotiwa na TCRA watu wanaoshughulika na hilo ni Jeshi la Polisi, ila ninachosema kama kuna kosa la jinai, muhusika ashirikiane na Jeshi la Polisi ili ukweli ufahamike", amesema Mwakyanjala.

Jeshi La Polisi Dodoma Lanasa Mtu Mmoja Aliyetapeli Kwa Kujifanya Polisi.

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limemshikilia  RAJAB RAMADHAN[32] aliejifanya  askari polisi  Kwa     kutapeli  watu  mbalimbali. 

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dodoma Leo Julai 23,2019 Kamanda wa polisi mkoani hapa Gilles  Muroto amesema kwa muda Mrefu kijana huyo anayeishi eneo la Area A Mjini Dodoma amekuwa akijipatia huduma mbalimbali kwa udanganyifu akijifanya askari polisi na kutishia watu kwa silaha  bandia. 

Kamanda Muroto ametaja vifaa alivyokuwa navyo  mhalifu huyo kuwa ni sare ya polisi Jangle Green,pistol ya bandia na hoster yake,picha akiwa na sare za jeshi [JWTZ] huku uchunguzi wa awali ukionesha kuwa kijana huyo alishawahi kuhudhuria mafunzo ya JKT na Kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu. 

Katika hatua nyingine Kamanda Muroto amesema jeshi hilo limekamata  vifaa vya NIDA ambavyo ni kamera 12 ambapo mtumishi wa NIDA  Ezekiel Subugo [24] aliiba vifaa hivyo ofisini na kuwauzia watu  mitaani  na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. 

Hata hivyo,Jeshi hilo limemkamata Musa Pungu akiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin kiasi  cha kete 132 zilizofungashwa katika vinailoni ambapo Kamanda Muroto amesema kijana Musa ameharibu vijana wengi kwa madawa ya kulevya katika Mtaa wa Hazina  jijini Dodoma hivyo mtuhumiwa na wenzake wanne watafikishwa mahakamani. 

Kamanda  Muroto ametoa wito kwa jamii kujihadhari na Matapeli katika jiji la Dodoma na hakuna Fedha zinazokuja kiurahisi bila kufanya kazi halali. 

Sanjari na hayo,Kamanda Muroto ameipongeza Kampuni ya INNOMAX kwa kulikabidhi jeshi hilo pikipiki mbili mpya aina ya HAOJUE na HONGLOG  zenye thamani ya zaidi ya Tsh.Milioni 4 Kwa ajili ya kufanyia doria  huku akiwaasa Watanzania wengine kuwa na uzalendo wa kusaidia jeshi hilo.

Uingereza Yapata Waziri Mkuu Mpya

0
0
Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha Conservatives nchini humo atakayechukua mara moja nafasi ya Bi Theresa May.

Hii inamaanisha Boris Johnson sasa atakuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza baada ya May kutangaza kujiuzulu mwezi uliyopita.

Boris aliye na miaka 55 alimshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa wanachama wa chama cha conservatives hii leo.

Waziri huyo wa masuala ya kigeni wa zamani wa Uingereza ananatarajiwa kuchukua rasmi nafasi hiyo ya uwaziri Mkuu hapo kesho Jumatano (24.07.2019).

Dr. Bashiru: Wapuuzeni hao "Wapumbavu" Wanaotaka Kukivuruga Chama Chetu

0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Bashiru Ally,  leo Julai 23,  2019,   ametoa wito kwa wanachama wa chama hicho kuwapuuza wale aliowaita wapumbavu, yaani watu wanaoendeleza mjadala usiokuwa na tija ndani ya chama hicho, na akawahakikishia kwamba chama hicho kiko imara.

Dk. Bashiru  ameyasema hayo wakati akipongeza hatua ya wanaCCM Mkoa wa Dodoma, kutaka Kanal Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, makatibu wastaafu wa CCM kuchukuliwa hatua.

Ni baada ya makatibu hao wastaafu wiki iliyopita, kumwandikia barua Pius Msekwa, Katibu wa Baraza la Viongozi Wastaafu wa CCM wakilalamikia kuchafuliwa na Cryspian Musiba, anayejitambulisha kuwa mtetezi wa Rais John Magufuli.

Kwenye barua hiyo, Makamba na Kinana wamelalamika kuchafuliwa na kuzushiwa huku serikali ikishindwa kuchukua hatua. Hata hivyo, wamehoji ‘ulinzi’ anaopewa Mtu huyo  anayewachafua.

Akizungumza tamko lililotolewa na Halmashauri ya CCM Mkoa wa Dodoma jana, Dk. Bashiri amewataka makada wa chama hicho kuwapuuza ‘wapumbavu’ hao.

“Wapuuzeni hao wapumbavu, hatuogopi kukosolewa, lakini hatuko tayari kudharauliwa, kutukanwa na kubezwa na majina yaliyo na kebehi na watu wasio na shukrani. Hatujafunzwa hivyo, hatujazoea hivyo,” amesema Dk. Bashiri bila kutaja jina lolote.

Aidha, Dk. Bashiru amesema, uongozi wa CCM hautaruhusu malumbano ndani ya chama hicho, huku akieleza kwamba mwenyekiti wake, Dk. Magufuli yuko tayari kuwasamehe, ili kukijenga chama.

“Msijifanye majasiri wa kupambana na malumbano, hakuna ruksa hiyo kwenye chama chetu. Waacheni wabwabwaje kitoto toto watachoka wenyewe.


"Ole wake mwanaCCM yeyote atakayetaka kutumia fursa ya upumbavu wa wapumvavu wa mwaka kutafuta kiki, ya kisisasa ili achaguliwe kwenye seriali za mtaa, hapana msifanye hivyo.


 “Jifunzeni kutoka kwa kiongozi wetu ambaye wakati wote hana muda wa malumbano. Amevumilia, wanaomtusi wengine wana umri wa watoto wake amewavumilia na yuko tayari kuwasamehe pia.  Lakini kwa kufanya hivyo si kwamba ni muoga.

“Mwalimu Julius Nyerere alishatuhasa tujisahihishe, kujisahihisha ni kujiimarisha, tujikosoe, tukosoane kwa adabu kwa nidhamu tuache utoto. Kisiwe chama cha siasa za kipuuzi, sababu majira haya ni ya uchaguzi,” amesema Dk. Bashiru.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano 24 July

Jamal Malinzi na Katibu wake Selestine Mwesigwa Wakutwa na Kesi Ya Kujibu

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Jamal Malinzi na Katibu wake Selestine Mwesigwa katika mashtaka 20 kati ya 30 ikiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Wengine waliokutwa na kesi ya kujibu ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, na Karani Flora Rauya huku Meneja wa TFF, Mariam Zayumba akiachiwa huru.

Uamuzi huo umetolewa jana Jumanne Julai 23, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyotolewa na Jamhuri.

Hakimu Kasonde alisema mashtaka ambayo washtakiwa wameonakana hawana kesi ya kujibu, upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kama washtakiwa wana kesi ya kujitetea.

Mahakama iliwafahamisha haki zao washtakiwa kwamba wanaruhusiwa kujitetea wenyewe kwa kiapo ama kuita mtu yoyote kama mashahidi wao.

Pia walifahamishwa kwamba wanayohaki ya kunyamaza kimya lakini kwa kufanya hivyo mahakama itaamini kwamba ushahidi uliotolewa na Jamhuri ni sahihi.
 
Washtakiwa walikubali kujitetea kwa kiapo na watakuwa na mashahidi ambapo wataanza kujitetea Agosti 6 mwaka huu.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 20 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017. Ambapo Meneja wa Ofisi TFF, Miriam Zayumba ameachiwa huru.

 Kesi imeahirishwa hadi Agosti 6, mwaka huu kwa ajili ya kuanza kujitetea utetezi.

Mizengo Pinda Awaponda Wanaotapatapa Kusaka Urais 2020 Kupitia CCM

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amesema anasikia kuna mtu anatapatapa kutaka urais kwa tiketi ya CCM, kusisitiza kuwa kwa muundo wa chama hicho tawala ulivyo, jambo hilo haliwezekani.'

Pinda amesema kuwa watu wasiumize kichwa katika hilo maana amefanya kazi na marais wote waliopita na anaujua utaratibu wa chama ulivyo, hivyo Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli anatakiwa aachwe achape kazi kwani kibaya chajiuza na kibaya chajitembeza.

“Siku zote tunaambiwa chema chajiuza na kibaya kinajitembeza, sasa huyu bwana huyu mpende msimpende ni chema kinachojiuza.

"Kwamba 2020 kuna mtu anajitokeza wala msihangaishe kichwa, msihangaishe vichwa kwenye eneo hilo ana miaka mitano na ana miaka mingine mitano, mimi nimefanya na baba wa Taifa miaka 8, mzee mwinyi 10, Mkapa 10 kwa nafasi mbili na Kikwete miaka 10.

"Kwahiyo na mimi nimo nikisema  anamaliza miaka yake 10 nina  uhakika na sitashangaa akimaliza miaka 10 mkasema mzee huyu angendelea." Amesema Mizengo Pinda

LIVE: Rais Magufuli Anashuhudia Makabidhiano Ya Dhahabu Iliyokamatwa Nchini Kenya .....Inawasilishwa Na Mjumbe Maalumu Wa Rais Wa Kenya

0
0
LIVE: Makabidhiano Ya Dhahabu Iliyokamatwa Nchini Kenya ....Inawasilishwa Na Mjumbe Maalumu Wa Rais Wa Kenya

Waziri Mkuu Azionya Halmashauri Zilizolega Makusanyo Ya Kodi

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezionya Halmashauri za Wilaya na Manispaa zilizoshindwa kufikisha malengo ya makusanyo ya kodi na kuzitaka zijitathmini ni kwa nini hazijafikisha malengo hayo.

“Kuna Halmashauri zimetajwa hapa kwamba hazijafikisha malengo ya makusanyo ya ndani. Fanyeni tathmini, ni kwa nini hamjafikia malengo na mhakikishe kuwa mwakani hamji kutajwa tena kwenye mkutano kama huu,” alisema. Halmashauri hizo ni Kakonko, Buhigwe, Madaba, Kigoma, Momba na Songea.

Ametoa agizo hilo jana mchana (Jumanne, Julai 23, 2019) wakati akizungumza na washiriki wapatao 700 ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) unaoendelea jijini Mwanza.

Waziri Mkuu ambaye amefungua mkutano huo wa siku tatu kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka washiriki wa mkutano ambao ni Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Majiji, Miji na Manispaa, wasimamie makusanyo ya mapato kupitia vyanzo vyao ili waweze kupanga mipango ya maendeleo. “Lengo la Serikali ni kuwezesha kila Halmashauri zijitegemee kwa asilimia 80-100 ifikapo 2025,” amesema.

“Katika makusanyo hayo, hakikisheni kuwa mnatenga asilimia 40 kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Na hili ni tatizo kwa Halmashauri nyingi zikiwemo zile kubwa. Ukifuatilia kwa makini huoni miradi inayogusa maisha ya wananchi wa kawaida.”

“Ukichukulia Dar es Salaam au Arusha ambao wanakusanya kati ya shilingi bilioni tano na 10, ni mradi gani wa thamani kubwa uliojengwa kwa kutumia fedha zenu za ndani, ukiacha hii mikubwa ya stendi za mabasi au barabara za lami ambayo inajengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu?” alihoji.

“Hivi kuna Halmashauri ambayo imejenga kituo cha afya cha kisasa kwa kutumia fedha zake za makusanyo? Afadhali hawa wa Dodoma ambao wameanza kujenga stendi ya mabasi na hoteli mbili za kitega uchumi,” amesema.

“Uamuzi wa Mheshimiwa Rais Magufuli wa kukusanya fedha zote na kuziweka kwenye chanzo kimoja ulitokana na study ya muda mrefu iliyofanyika na kubaini kuwa fedha zinazokusanywa haziendi kwenye miradi inayogusa wananchi. Niwasihi sana, fanyeni miradi ambayo kila Mtanzania angependa kuiona kwenye Mamlaka zenu za Serikali za Mitaa,” amesisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba Serikali iliamua kumuondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa ALAT, Bw. Abraham Shamumoyo kwa sababu ya utendaji mbovu.

“Kuna maamuzi alikuwa akiyafanya bila kuishirikisha Kamatai ya Utendaji. Kuna mikataba ilikuwa ikifanyika na mingine inahusisha hadi mataifa ya nje. Kuna fedha zilitolewa, zikawekwa kwenye akaunti binafsi na siyo akaunti ya ALAT,” amesema.

Amesema ALAT ni taasisi kubwa ya Serikali ambayo inahitaji kuheshimiwa, na siyo ya kuancha iendeshwe na mtu mmoja kama atakavyo. “ALAT ni taasisi kubwana Serikali inaitegemea. Niwahakikishie kuwa Mheshimiwa Rais, anawathamini, anawapenda na anataka mchape kazi kuisaidia Serikali yenu,” amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Bw. Suleiman Jafo alisema Serikali inajivunia ujenzi wa shule za sekondari za kata ambazo mwaka huu zimefanya vizuri kwenye mitihani ya kuhitimu kidato cha sita.

“Kati ya shule bora 100, shule 64 ni za Serikali na kazi ya shule hizo 64, shule 54 ni za kata. Na kwenye matokeo ya masomo ya sanaa, kati wanafuzi bora 10 wa kiume, wanafunzi saba wanatoka kwenye shule za kata,” alisema.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imewekeza sana kwenye sekta ya elimu, ikiwemo ujenzi wa shule za sekondari na ukarabati wa shule kongwe za sekondari.

Alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa kutenga sh. bilioni 268.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi 38 ya kimkakati kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kama vile ujenzi wa masoko, machinjio na stendi za mabasi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images