Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Trump kuanza kuwafukuza watu wasio na vibali vya kuishi Marekani

$
0
0
Utawala wa rais Donald Trump unapanga kuanza utekelezaji wa operesheni ya nchi nzima inayolenga familia za wahamiaji, licha ya kupingwa vikali na Democrats. 

Operesheni hiyo inasemekana kwamba inaweza kuanza kutekelezwa mwishoni mwa juma hili, baada ya kuahirishwa na Trump mwishoni mwa mwezi uliopita. 

Inalenga kuwafuatilia watu walio na amri za mwisho za kurejea katika nchi zao, zikiwemo familia za wahamiaji ambazo kesi zao zilikuwa zikifutiliwa kwa haraka na majaji katika jumla ya miji 10 kama vile Chigaco, Los Angeles, New York na Miami. 

Hatua hizo zimeibua hasira na wasiwasi miongoni mwa wanaharakati wa haki za wahamiaji na wabunge. Operesheni hiyo ni sawa na ile iliyowahi kufanywa mwaka 2003 na kisha kuwakamata watu wengi wasio na vibali. 

Trump alitangaza kwenye Twitter mwezi uliopita kwamba operesheni hiyo itakuwa ni mwanzo wa kuwafukuza mamilioni ya watu wanaoishi Marekani kinyume cha sheria.

Uturuki yaanza kupokea mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Urusi

$
0
0
Uturuki imepokea shehena ya kwanza ya mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Urusi licha ya vitisho vya Marekani.

Uturuki ilipokea shehena hiyo katika uwanja wa ndege wa jeshi wa Murted jana Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara. 

Serikali ya Moscow imethibitisha habari hiyo ya kuanza kuikabidhi Uturuki mfumo huo na inasisitiza kwamba itaendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa makubaliano ya pande mbili.

Serikali ya Ankara imeanza kupokea mfumo huo wa makombora ya S-400 licha ya Rais Donald Trump wa Marekani kutahadharisha kuwa ataiwekea Ankara vikwazo vikali iwapo mfumo huo wa kujikinga na makombora wa S-400 kutoka Russia utawasili nchini Uturuki.

Mkataba wa mauzo ya ngao hiyo ya makombora kati ya Ankara na serikali ya Moscow ulitiwa saini Disemba mwaka 2017.
 
Jumatano iliyopita, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki alisema kuwa, iwapo nchi hiyo itashambuliwa na maadui, basi itatumia ngao hiyo ya makombora ya S-400 kujilinda.

Alisisitiza kuwa, Uturuki imeamua kununua ngao hiyo ya makombora kutoka Russia kwa ajili ya kujidhaminia usalama wake. 

Hata hivyo, maafisa wa Marekani hawataki kabisa ndege zao aina ya F-35 kuwa karibu na makombora ya S-400 - wakihofia wataalamu wa kirusi wataweza kung'amua mapungufu ya ndege hizo.

Marekani imeenda mbali kwa kutishia kuitoa Uturuki kwenye mpango wa kuendelea na manunuzi ya F-35 na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi.

Uturuki hata hivyo inasema mifumo hiyo ya Urusi na Marekani itawekwa kwenye maeneo tofauti.

Tafsiri 17 Kuhusu Kuota Ndoto Upo Shuleni Unasoma Au Upo Shuleni Unafanya Mtihani Wakati Ulishamaliza Shule Miaka Mingi Iliyopita

$
0
0
IMESIMULIWA  NA   Dokta  Mungwa  Kabili…………………………………0744 -  000  473.


Awali  ya  yote  ujumbe  katika  ndoto  yoyote  ile  huwa  unapatikana MWISHONI  mwa  ndoto  wakati  ndoto  inaisha  na  sio  MWANZONI  mwa  ndoto,

KUHUSU  KUOTA  UMERUDI UTOTONI AU  SHULENI  UNASOMA  WAKATI  SHULE  ULISHA  MALIZA  ZAMANI.

Hii  ni ndoto  ambayo  imekuwa  maarufu  sana  katika  siku  za  hivi  karibuni.  Siku  hizi  karibu  kila  mtu mzima   anaota  ndoto  hii.  Sio  mara  moja  wala  sio  mara  mbili  ni  mara  nyingi  nyingi.

Wapo  wanao  ota  ndoto  hii  walau  mara moja au mbili  kila mwezi, wengine  huota  mara  moja  kila  wiki  na  wengine  huota  karibu  kila  siku.   Wakati mwingine  mtu  anaweza  kuota  ndoto  hii Zaidi  ya mara  moja  ndani  ya  usiku  mmoja  na  hali  hiyo  inaweza  kujirudia   mfululizo, yani  mtu  amelala  tuseme  saa  nne  usiku , saa  sita  usiku  anaota  ndoto  hiyo, anastuka. Akilala  tena  anaiota  ndoto  hiyo hiyo.


NINI  MAANA  YA  NDOTO  HIZI  MBILI ; KUOTA  UPO  SHULENI  UNASOMA  AU  UPO  UTOTONI  NA  KUOTA  UPO  SHULE  UNAFANYA  MTIHANI  AMBAO  ULISHA  UFANYAGA  MIONGO  KADHAA  ILIYOPITA  AU  MIAKA  MINGI  ILIYOPITA  ?

Tuanze  na  ndoto  ya  kuota   UPO  SHULENI  UNASOMA  WAKATI  WEWE  ULISHAMALIZAGA  SHULE  MIAKA  MINGI  SANA  IMEPITA.

Ulimaliza  darasa  la  saba  mwaka  1994  na  kuendelea  na  masomo  ya  juu. Sasa  hivi  umeshakuwa  mtu  mzima mwenye  watoto  na  pengine  wajukuu  kabisa.   Lakini  unalala  usiku  unaota  ndoto  umerudi  shuleni  katika  darasa  hilo  hilo  la  saba  au  hata  chini  ya  hapo. Upo   katika  mazingira ya  shule  ulio  kuwa  unaisoma.  Katika  ndoto yako  hiyo  mazingira  ya  shule  yako  huwa  ni  yale  yale  yaliyo  kuwepo  kipindi  unasoma hata  kama  katika  ulimwengu  wa  nyama  yameshabadilishwa. Mfano  kulikuwaga  na  miti  mikubwa  labda  sasa  hivi  imeshakatwa.  Kulikuwa  na  sehemu  ya  wazi  na sasa  hivi  imejengwa  madarasa  mengine.  Wewe  katika  ndoto  yako  utakuwa  katika  mazingira  yale  yale  yaliyo  kuwepo  mwaka  huo  wa  94  wakati  bado  unasoma  katika  shule  hiyo.

JE   NDOTO  HII INA  MAANA  GANI  ?
Dhana  iliyo  jengeka  miongoni  mwa  watu wengi katika  jamii  ni  kwamba  ukiota  ndoto  hii  basi  maana  yake  ni  kwamba  kuna  watu  wanakurudisha  nyuma  kwa  kutumia  uchawi.  Yani  kwa  lugha  nyepesi  kuna  watu  wanakufunga  kichawi  ili  usipate  maendeleo. Uendelee  kubakia  hapo  hapo  ulipo  na  uzidi  kurudi  nyuma  kimaisha.

JE  TAFSIRI  HII  NI  SAHIHI  ?
Jibu  langu  ni  NDIO  na  HAPANA.  Ndio  kwa maana   ya  kwamba  ukiota  ndoto  umerudi  shuleni  inaweza  kuwa  ina  maanisha  kwamba  kuna  watu  wanakufunga kwa  lengo  la  kukurudisha  nyuma  kimaendeleo  lakini  HAPANA  kwa  maana  ya  kwamba  si  kila  unapo  ota  ndoto  umerudi  shuleni  basi  tafsiri  yake  ni  kwamba  kuna  watu  wanakuroga  kwa  lengo  la  kukufunga  ubaki  hapo  hapo  ulipo  na  kukurudisha   nyuma.

Ndoto  hii  ina  tafsiri  nyingi  sana. Kuipa  tafsiri  moja  tu  kama  watu  wengi  wanavyo  amini  ni  kuto  kuitendea  haki  ndoto  hii  na  ulimwengu  wa  ndoto  kwa   ujumla  wake.

Kama  nilivyo  dokeza  hapo  juu, ndoto  hii  ina  tafsiri  nyingi  sana.  Baadhi  ya  tafsiri  muhimu  kuhusu ndoto  hii  ni  kama  ifuatavyo ;

TAFSIRI NAMBA MOJA :       UNAPEWA  ONYO  KUHUSU  MWENENDO  NA TABIA  ZAKO  AMBAZO  ZINAKURUDISHA  NYUMA  KIMAENDELEO.

Ulevi, uzinzi  na  uasherati  pamoja  na  anasa  za  dunia  ni  miongoni  mwa  tabia  na  mienendo  ambayo  inarudisha  nyuma  maendeleo  ya  watu  wengi  sana . kama  wewe  unajihusisha  na  tabia  hizo  hapo  juu  halafu  ukawa  unaota  ndoto umerudi  utotoni basi ni ishara  kwamba  tabia  na  mwenendo  wako  vinakurudisha  nyuma  kimaendeleo.  Tabia  na  mwenendo  wako  ndio  mchawi  wako  namba  moja.

 2.TAFSIRI   NAMBA  MBILI :   NI  ISHARA  YA KUKUONDOA  HOFU  JUU  YA  JAMBO  ULILO  LIFANYA  AU  LILILO  KUTOKEA  AMBALO  LIMEKUFANYA  UWE  NA  HOFU  KUBWA  SANA  KATIKA  MAISHA  YAKO.

Mfano   umekutana  kimwili  na  mtu  bila  kutumia  kinga  halafu  baadae  ukasikia  mtu  huyo aliwahi  kuwa  na  mahusiano  ya  kimapenzi  na muathirika, jambo  hili  linaweza  kukupa  hofu  kubwa  sana  kwenye  nafsi  kiasi  cha  kukata  tamaa  ya  kuishi  duniani  kwa  kuamini  na  wewe  umeathirika  na  mwisho  wa siku  unaweza  kujiingiza  katika  tabia  za  hatari zaidi  kama  kuendelea  kufanya  ngono  nzembe  na watu  mbalimbali  huku  ukiamini  kwamba  wewe  ndio  unawasambazia . Matokeo  yake  basi  katika  mchakato  huo  wa  kuwaambukiza  na  kuwasambazia  watu  virusi, wewe  ndio  unaweza  ukajikuta  unaambukizwa.  Malaika  walinzi wako  kwa  sababu  wana  uwezo  wa  kusoma  nyota  yako  na  kujua  mambo  yatakayo  kutokea  mbeleni, wataanza  kukupa  ujumbe  wa  kukutoa  hofu  kwa  njia  ya  ndoto. Ukiwa  katika  hali  kama  hii  halafu  ukaanza  kuota  ndoto  umerudi  utotoni  basi  maana  yake  ni  kwamba  jambo  unalo  lihofia  halipo.  Yani  kwa  suala  la usalama  wa  damu  yako, damu  yako  ni  salama  kama ilivyo  kuwa  miaka  mingi  iliyo  pita  wakati  upo  utotoni.   Hapa  malaika  walinzi  wako wanakuwa  wameisoma  nafsi  yako  ambayo  inatamani  siku  zirudi  nyuma.  Hivyo wanakujibu  kwa  njia  ya  ndoto  kwa  kukurudisha  nyuma  kwa  njia  ya  ndoto.

Hapa  malaika  walinzi  wako  wakiona  huelewi  kwa  njia  ya  ndoto, wataanza  kukupa  ishara  nyingine  za  kawaida. Kwa  mfano  uta kuwa  unatembea  mjini  mara  unakutana  na  rafiki  yako  ambae  mlisoma  wote  shule  ya  msingi  na  kwa  mara  ya  mwisho  mlionana  miaka  kumi  iliyopita  ( kipindi  ambacho  hukuwa  na  hofu  kama  uliyo  nayo  leo hii ). Unatoka  hapo  unaenda  kupanda  kwenye  gari  unasikia  zinapigwa  nyimbo  za  miaka  25  iliyo  pita  wakati  upo  darasa  la  tatu  nakadhalila . ( Ukiona  hivyo  basi jua  unapewa  taarifa  kwamba  jambo  unalo  lihofia  halipo  wala  halijakutokea  kwa  hiyo usiwe  na  hofu  yoyote  kuhusu  jambo  hilo )

4.TAFSIRI  NAMBA  NNE :  UNAPEWA  ONYO  USIRUDIANE  NA  MTU  ULIE  KUWA  UMEACHANA  NAE.

Ulikuwa  na  mke, mume , mchumba  au  mpenzi  halafu mkatengana.  Baada  ya  muda  Fulani, mke, mume, mchumba  au  mpenzi  huyo  akakuomba  mrudiane.  Ukiwa  katika  mchakato  wa  kutaka  kurudiana  nae  unaanza  kuota  ndoto umerudi  shuleni  au  utotoni.  Tafsiri  ya  ndoto  hiyo  ni  kwamba  endapo  utarudiana  na  mke, mume, mchumba  au  mpenzi  huyo  basi  jambo  hilo  litakurudisha  nyuma  sana  kimaisha.  Malaika walinzi  wako  kwa  sababu  wana  uwezo  wa  kuona  mambo  yatakayo  kutokea  mbeleni  wanakupa  tahadhari  hiyo  kwa  njia ya  ndoto.

Sababu  zinaweza  kuwa  mke, mume, mpenzi, au  mchumba  huyo  ana  laana  na  vifungo  vya  kimasikini  vya  ukoo, familia  au  kijiji.  Ukifunga  nae  ndoa  au  ukiwa  nae  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  maana  yake  na  wewe  unakuwa  umeunganishwa  kwenye  laana  na  vifungo  vyake.

Vile  vile  sababu  zinaweza  kuwa  tabia  za  mwanaume  huyo zitakurudisha  nyuma  kimaendeleo.  Kwa  mfano  inawezekana  wewe  unafanya kazi  au  shughuli  inayo  kuingizia  kipato  ambacho  unakitumia  kukidhi  haja  zako  na  kuwasaidia  familia  yako halafu  huyo  mwanaume  yeye  hataki  kuoa  mwanamke   ambae  anafanya  kazi.  Yeye  akikuoa  atataka  uwe  mama  wa  nyumbani. Atakuachisha  kazi  na  hatotaka  ufanye  biashara  yoyote  na  anaweza  kutumia  fursa  hiyo  kukunyanyasa  pia  na  mwisho  wa  siku  utaishia  kuachana  nae  huku  ukiwa  umepoteza  muda  wako  mwingi  sana ukiwa  nae. NDIO  MAANA  UNAPEWA  ONYO  USIRUDIANE  NAE.


5. TAFSIRI NAMBA  TANO : NI  ISHARA  KWAMBA  MARADHI  YA  KICHAWI  YALIYO KUWA  YANAKUSUMBUA  YAMEPONA.

Kama  ulikuwa  umetupiwa  maradhi  ya  kichawi  na  yakakutesa  kwa  muda  mrefu  halafu  baadae  ukapata  tiba  ya  kuondosha  maradhi  hayo basi  kuna  uwezekano  mkubwa  sana  kuota  ndoto  umerudi  utotoni.

Hii  maana  yake  ni  kwamba, maradhi  yako  yote  yameondoshwa  na  sasa  umekuwa  mpya.  Umerudi  kwenye  upya.,  Kwa  hiyo  kama  upo  kwenye  kundi  hili  halafu  ukaota  ndoto  umerudi  utotoni  basi  maana  yake  ni  kwamba  wewe  umekuwa  mpya.

6.TAFSIRI NAMBA  SITA : NI ISHARA  KUWA  NYOTA  YAKO  ILIYO  KUWA  IMEIBIWA AU  KUCHAFULIWA SASA   IMERUDISHWA.

Kama  nyota  yako  ilikuwa  imechukuliwa  halafu  ikarudishwa  basi  kuna  uwezekano  mkubwa wa  wewe  kuota  ndoto  umerudi  utotoni.

 Hii  maana  yake  umekuwa  mpya. Nyota  yako  imekuwa  swafi  kama  ulivyo  kuwa  mtoto  mdogo.   Ukiachilia  mbali  kurogwa, nyota ya  mtu  huwa  ina  haribiwa  na  zinaa.  Unapo fanya  zinaa  una  haribu  nyota  yako  kwa  sababu  una unganisha  nafsi( nyota )  yako  na  nafsi ( nyota ) ya  mtu  unae  fanya  nae  zinaa.  Katika  ulimwengu wa  kiroho, watoto wadogo ni  alama  ya  nyota  inayo  ng’aa  ama  nyota  iliyo  kamilika, nyota  safi.

Sasa  kama  nyota  yako  ilikuwa  imechafuliwa, imekufa, imeshushwa, imefungwa  au  ime imechukuliwa ( imeibwa )  halafu ukarejesha  nyota  yako. Ukiota  ndoto  umerudi  utotoni  maana  yake  ni  kwamba  nyota  yako  iliyo  kuwa  imeibwa  sasa  imerudi.  Na  kama  wewe  ni  mwanamke  basi  tunasema  umerudi  kwenye  ubikira. Umekuwa  swafi.

7.  NI  ISHARA  KWAMBA  PESA  ULIYO  IPATA  HIVI  KARIBUNI  ITAISHA  YOTE  BILA  WEWE  KUFANYA  KITU  CHOCHOTE  CHA  MAANA :  Kama  umepata  pesa  nyingi  hivi karibuni  baada  ya  kusota  kwa  muda  mrefu  labda  kupitia  kilimo  au uchimbaji  madini  halafu  ukaanza  kuota  ndoto  umerudi utotoni  au  shuleni  basi  kuwa  makini  sana  na  matumizi  ya  pesa  zako  kwani  hiyo  ni  ishara  kwamba  pesa  zako  zitaisha  zote  hivi  karibuni  bila  wewe  kufanya jambo  lolote  la  maana. 

 Malaika  walinzi  wako  kwa  sababu  wana  uwezo  wa  kusoma  na  kuona  mambo  yatakayo  kutokea  katika siku  za  usoni, wanakupa  tahadhari  kwa njia  ya  ndoto. Kama  upo  katika  kundi  hili  hakikisha  unafanya  mambo  yote  ya  msingi  uliyo  kusudia  kuyafanya  hapo  mwanzoni  endapo  ungepata  pesa  ulizo  zipata. 

Kama  ulipanga  kununua, nyumba, ardhi, kufungua  kampuni, nakadhalika  basi fanya  hivyo  haraka sana  kwani  pesa zako zitaisha  zote  bila  kufanya  jambo  la  maana. 

Mara  nyingi  ndoto  hii  huwatokea  wale  wanao  pata  pesa  nyingi  na  kuingia  kwenye  maisha  ya  starehe  pamoja  na  wale  wanao pata  pesa  nyingi  halafu  wana  iacha  tu benki huku  wakisubiri  wapate  pesa  nyingine Zaidi  ndio wafanye  wanacho  taka  kukifanya.  

Sasa  hapa  Malaika  walinzi  wako  ambao  wana  uwezo  kuona  mambo  yatakayo  kutokea  mbeleni  wanajua  kuwa  pesa  hiyo  unayo  itaka  hutoipata  leo  wala  kesho. 

Itachukua  muda  mrefu  sana. Kwa hiyo  wanakutahadharisha  kuwa  pesa  yako  uliyo  weka  utaishia  kuitumia  kidogo  kidogo  hadi  itaisha  yote  hivyo  basi  kama  ulikuwa  na  biashara  unataka  kufanya  basi  anza  kufanya  sasa  kwa  pesa  hiyo  hiyo  uliyo  nayo.

8.TAFSIRI  NAMBA  NANE :  UNA TAHADHARISHWA  KUTOWEKEZA  PESA  ZAKO  KWENYE  BIASHARA  MPYA  AMBAYO  UNATAKA  KUIFANYA.

Umetoa  pesa  ya  mtaji  kutoka  kwenye  biashara  yako  moja  na  unataka  kuiweka  yote au  karibu  yote  kwenye  biashara  nyingine  halafu  ukaona  unaanza  kuota  ndoto upo  shuleni  au umerudi  utotoni  basi  tafsiri  yake  ni  kwamba,  endapo  utawekeza  pesa  zako  kwenye  biashara  hiyo  mpya  basi  pesa  zako  zitapotea  kwani  biashara  hiyo  haitokulipa.  

Ukiwa  katika  kundi  hili  na  ukawa  unaota  ndoto  hizo, nakushauri  ufanye  mambo  yafuatayo : Moja usiweke  pesa  zako  kwenye  biashara hiyo  kabisa, endelea  kufanya  biashara  yako  ambayo  umeizoea au  kwenye  hiyo  biashara  mpya  weka  pesa  kidogo  sana  ambayo  hata  kama  itapotea  basi  wewe  huto ijutia  sana.

9.TAFSIRI  NAMBA  TISA: NI ISHARA  KWAMBA  MPANGO  UNAO  TAKA  KUUFANYA  UTA KUSABABISHIA  HASARA  KUBWA  SANA  NA  UTAKURUDISHA  NYUMA  SANA.

Kama kuna  mpango  wowote  ambao  unataka  kuufanya  halafu  ukaanza  kuota  ndoto upo shuleni  au utotoni  basi  hiyo  ni  ishara  kwamba, mpango  huo  ambao  unataka  kuufanya  utakuletea  hasara  kubwa  sana  katika  maisha  yako  na  kukurudisha  nyuma  sana  kifedha  na  kimaisha.  Mpango unaweza  kuwa  wowote, mfano  kuacha  kazi  unayo  ifanya  na  kufanya  kitu  kingine, kuoa, kumroga  mtu  nakadhalika.

11. KWA  MTU  ALIE  BWETEKA  NA    KAZI  AU  SHUGHULI  ANAYO  IFANYA.

Anaweza kuota  ndoto  kama  ishara  kwamba kubweteka/kuridhika  kwake  kunamkwamisha  na  kumrudisha  nyuma  kimaisha na  kimaendeleo.

12. NI  ISHARA  KWAMBA  MUNGU  AMEKUFANYIA/ATAKUFANYIA  WEPESI KWENYE  JAMBO  UNALO  MUOMBA

Kama upo  kwenye  kipindi  kigumu  cha  maisha  na una muomba  Mwenyezi  Mungu  akufanyie  wepesi  kuhusu  magumu  unayo  yapitia  halafu  ukaota  ndoto  umerudi  utotoni basi  tafsiri  yake  ni  kwamba  Mungu  amejibu  maombi  na  dua  zako  na kwamba  mambo  yako  yatakuwa  mepesi  muda  si  mrefu.  

Mtoto  ni  kiumbe  ambae  maisha  yake  ni  mepesi  kwa  sababu  kila  kitu  anapata  kutoka  kwa wazazi  ama walezi  wake. Kwa  hiyo  kama  upo  kwenye  kundi  hili  basi  shukuru  kwa sababu  mambo  yako yanaenda  kufanyiwa  wepesi.

13.  NI  ISHARA  KWAMBA  TABIA  YAKO  YA  UZINZI  NA  UASHERATI  INAKURUDISHA  NYUMA   KIMAENDELEO

Hakuna  tendo  linalo  chafua  na  kuharibu  nyota  ya  mtu  kama uzinzi  na  uasherati. Nyota  ya  mtu  ikichafuka  na kuharibika  basi  na  mambo  yake  yatachafuka  na  kuharibika  pia.  Kama  unajihusisha  na  uzinzi  na  uasherati  halafu  ukaota  ndoto  umerudi  utotoni  basi  huo  ni ujumbe  kwamba, tabia  yako  ya  uzinzi  na  uasherati  inachafua  na  kuharibu  nyota  yako  na  inakurudisha  nyuma  kimaendeleo.  Kwa  hiyo  unatakiwa  kubadili  mwenendo  wako  haraka  iwezekanavyo.

14. NI  ISHARA  KWAMBA  KUNA  WATU  WANA IBA  MALI ZAKO  AU  MALI  ZAKO  ZINA  TEKETEA.

Kwa mfano  una  miliki  duka  au  maduka  na  kwenye  duka  au  maduka  yako umeweka  wafanyakazi  wa  kusimamia  duka  lako.  Ukiota  ndoto  umerudi  utotoni basi  ni  ishara  kwamba  kuna  watu  wanakuibia  mali  za duka  lako  na  hivyo  kukurudisha  nyuma.  Mfano  mwingine  ni  kama  una  lima  mashamba  au  unafuga mifugo  halafu  ukaota  ndoto  hii  ya  utotoni  basi jua  kuna  watu  wanakufanyia  hujuma  kwenye  mashamba  yako  au  mifugo  yako, hujuma  ambazo  zinakurudisha  nyuma  kimaendeleo.

Mfano  mwingine  ni  kama  upo  nje  ya  nchi  unayo  ishi  halafu  unatuma  pesa  kwa  ndugu, jamaa  au  rafiki zako waliopo  nchini  kwako  kwa  ajili  ya  kujenga  nyumba yako  na  kuisimamia, kununua  mashamba, mifugo  nakadhalika  halafu  ukawa  unaota  ndoto  ya  utotoni  basi  ni  ishara  kwamba nyumba  yako  haijengwi  na  ulio wapa  kazi  hiyo  wanakula  pesa  yako  tu.

17. KWA  MTU ALIYE  LISHWA  LIMBWATA  KWA  LENGO  LA  KUCHUNWA  PESA  NA  MALI  ZAKE : Anaweza  kuwa  anaota  ndoto  amerudi  shuleni  au  utotoni  ikiwa  ni  ishara  ya  kwamba  anarudishwa  nyuma  kimaisha  na  mtu  ambae  amemlisha  limbwata la  mapenzi.


Tafsiri zipo nyingi  sana  lakini  kwa  leo  hizi  zinatosha.

KUOTA   NDOTO UNAFANYA   MTIHANI   AMBAO  ULISHA  UFANYAGA  MIAKA  MINGI  IMEPITA .

Ndoto  hii  ni  tofauti  na  kuota  ndoto  umerudi shuleni. Ndoto  hii  ni tofauti kabisa  na  kuota  ndoto  umerudi  shule.

Ndoto hii  ina  maana  ifuatayo :  MAANA  YA  NDOTO  HII NI  KWAMBA  MTIHANI  WA  KIMAISHA  ULIO  PEWA, UMEUSHINDWA, KWA  HIYO  LAZIMA  UUFANYE  TENA  MTIHANI  HUO.  Na  usipo  ufanya  basi  utaendelea  kukuandama  katika  siku  zote  za  maisha  yako.

Kwa mfano wewe  ni  mwanaume, uliingia  kwenye  ndoa  halafu  baadae  ukagundua  kwamba  mke  wako  ni  mkorofi na sababu  hiyo  basi  ukaamua  kuachana  nae na  sasa  unatafuta  mwanamke  mwingine  ambae  sio  mkorofi.

Usicho  kijua  ni  kwamba  mwanamke  huyo  unae  muona  mkorofi  aliletwa  kwako  kama  mtihani  ambao  ulitakiwa  kuufaulu.  Mungu  aliuleta  mtihani  huo  kwako  ili  ujifunze  jinsi  ya  kuishi  na  mke  mkorofi . Sasa wewe  mtihani  huo  umeufeli, umemfukuza  mkeo  kwa  sababu  mkorofi. Ni  sawa  na  kuacha  kuandika  majibu  ya  mtihani  kwenye  chumba  cha  mtihani  kwa  sababu  maswali magumu. Kitatokea  nini? Utafeli  mtihani  huo. Na  ukifeli  mtihani  wa  kiroho  lazima  uurudie. Hakuna  mjadala  katika  hilo.

Sasa  basi  ukiwa  katika  mchakato  wa kutafuta  mke  mwingine  ambae  sio  ‘mkorofi’ kama  huyo  ulie muacha, halafu  ukawa  unaota  upo shule  unafanya  mtihani  ambao  uliufanyaga  miaka  mingi  imepita  basi  jua  kuwa  una fahamishwa  kwamba, unapoteza  muda  wako  kujaribu  kufanya  mtihani  ambao  ulishaufeli  kwa  sababu  hata  kwenye  mtihani  huo  utaenda  kufeli  pia.  

Hii  ni  kwa wote  wanawake  kwa  wanaume.

Ndio  maana  wapo  watu   ambao  hawatulii  kwenye  ndoa  moja.  Ndani  ya  miaka  kumi  mtu  ana  ndoa  tatu  na  zote  wameachana  kwa  sababu  zinazo  fanana.

Mifano  ipo  mingi  sana  ila huu  wa  ndoa  ni  mfano ambao  unaweza  kueleweka  kwa urahisi.

Ni  matumaini  yangu  kuwa  sasa  umejua  ni  kwanini  unaota  ndoto  ukiwa  umerudi  utotoni, upo  shuleni  unasoma  au   unafanya  mtihani  ambao  ulisha  ufanya  miaka  mingi  imepita.

IMESIMULIWA  NA   Dokta  Mungwa  Kabili…………………………………0744 -  000  473.

Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu Ataka Dhana Ya Afya Moja Kutekelezwa Kwa Wakati

$
0
0
Na; MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko amewataka waratibu wa dawati la Afya Moja kutekeleza dhana ya Afya Moja kwa wakati sambamba na kuweka mikakati mahususi itakayowaongoza katika utendaji wa dhana hiyo. 

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha wadau wa afya moja na wataalam kutoka sekta ya Afya, Mifungo, Wanyamapori na Mazingira kilichofanyika Julai 12, 2019, Jijini Dodoma.

Alieleza kuwa dhana ya afya moja inajumuisha wataalam na wadau mbalimbali kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa dhana hiyo ikiwemo kutoa fursa ya kushirikiana pamoja katika kukabiliana na madhara au magojwa hatarishi nchini.

“Nimepitia Sera ya Afya moja na kuona suala hili linatakiwa kusimamiwa vyema, ikiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mratibu wa Dawati la Afya moja kwa kushirikiana na Wizara, Taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo, katika kuhakikisha nchi yetu inakuwa mahala salama,” alieleza Mwaluko

Aliongeza kuwa, suala la kujenga uwezo kwa waratibu wa dawati la afya moja inatakiwa kuangalia ofisi kwa ujumla na si mjumbe mmoja tu ambaye atakuwa anasimamia masuala hayo ya Afya moja wakati wote.

“Mnatakiwa mtambue kuwa mkiwa kama wafanyakazi mna majukumu mengine ya kiofisi ambayo mnatakiwa kuyatekeleza, hivyo mtoe fursa kwa wafanyakazi wengine waliopo kwenye ofisi zenu kujifunza na kuelewa dhana hii ya afya moja,” alieleza Mwaluko.

Aidha, alitoa wito kwa waratibu wa dawati hilo kuelimisha umma kuhusu maana ya Afya Moja na dhana nzima ya Afya moja ili wananchi waweze kuwa na ufahamu wa suala hilo.

Pia, aliwahimiza washauri elekezi wa dawati hilo kutimiza majukumu yao kwa weledi na kutoa ushauri mapema kuhusu dhana ya Afya Moja.

Kwa upande wake, Prof. Robinson Mdegela ambaye ni Mtaalamu Mshauri wa Afya Moja alisema kuwa kukutana kwao katika kikao hiko ni kuonesha utayari wa kila mtaalamu katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuongeza msukumo juu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Afya Moja.

 

Utalii Wa Sokwemtu Kuanzishwa Katika Hifadhi Ya Taifa Rumanyika Na Ibanda Mkoani Kagera.

$
0
0
Na. Aron Msigwa – WMU
Serikali imesema itawapandikiza Sokwemtu katika hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu iliyoko wilayani Karagwe na Ibanda iliyoko Kyerwa, mkoani Kagera kwa kuwa hifadhi hizo zina Ikolojia na chakula cha kutosha kinachoruhusu kustawi kwa wanyamapori hao hatua itakayochangia kukuza shughuli za utalii wa Sokwemtu hapa nchini na kuongeza pato la Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa kauli hiyo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya Kikazi ya kukagua maendeleo ya shughuli za uhifadhi katika hifadhi hizo zilizotangazwa hivi karibuni kuwa hifadhi za Taifa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Kigwangalla amesema mpango huo umekuja kufuatia taarifa za kitaalam zinaonesha kwamba katika miaka mingi iliyopita kulikua na Sokwemtu katika maeneo hayo ya wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambayo watalaam wanasema ikolojia yake inaruhusu kustawi kwa wanyamapori hao kwa kuwa yana makazi mazuri na chakula cha kutosha.

Amesema mpango huo hautahusisha upandikizaji wa wanyamapori    

Waziri Mkuu Awasili Kigoma

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma kufungua Kongamano la Wananwake Kitaifa, kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Amandus Dismas Nzamba.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CCM Yagoma Kuwapokea Wabunge Watatu wa Upinzani

$
0
0
KATIBU Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally amepongeza Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya kuwa ni mbunge mahiri, makini na mchapakazi ndiyo sababu wakakubali kumpokea CCM kwani waliwakataa wabunge watatu wa vyama vya upinzani waliiomba kujiunga na CCM baada ya kubaini kuwa hawawezi kukidhi vigezo vya kuwa wabunge wa chama hicho. 

Dk Bashiru akizungumza Mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro kwenye ziara yake ya siku mbili Mkoani Manyara alisema Ole Millya ni miongoni mwa wabunge 10 mahiri waliokuwa upinzani wakakubaliwa kujiunga na CCM. 

Alisema kwenye mkoa wa Manyara waliwapokea viongozi wawili wa upinzani Ole Millya na Pauline Gekul wa jimbo la Babati Mjini ambaye alikuwa mwanafunzi wake chuo kikuu. 

Alisema CCM siyo chama cha kuchukua kila mtu ndiyo sababu wamewakataa hao ambao hakuwataja majina kwani wangewakubali kuwapokea wote upinzani ungemalizika. 

“Tumewakataa wabunge hao watatu waliotaka kuja kwetu kwani CCM siyo jalala kwani mtu aliyekata tamaa anaweza kujiumiza mwenyewe au kuumiza wenzake,” alisema Bashiru. 

Alisema siyo kweli kuwa wanafungua milango na kuchukua kila mtu kwani chama hicho cha CCM kina dhamira ya dhati na majukumu ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi. 

Akizungumza kwenye kikao hicho Ole Millya alisema miradi mingi ya maendeleo iliyofanyika Wilayani Simanjiro kupitia Rais John Magufuli ndiyo sababu yeye akajiuzulu Chadema na kujiunga na CCM. 

Ole Millya alisema hivi sasa hospitali ya Wilaya inajengwa, mradi mkubwa wa maji wa mto Ruvu, barabara ya lami itajengwa kutoka Arusha hadi Kongwa Mkoani Dodoma kupitia Simanjiro na Kiteto na ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani. 

Katika kikao hicho katibu mwenezi wa Chadema Wilayani Simanjiro na aliyegombea udiwani kata ya Orkesumet mwaka 2015, Zephania Kituyo alirudisha kadi ya Chadema na kujiunga CCM. 

Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara, Simon Lulu alisema hivi sasa majimbo yote saba ya mkoa huo yanaongozwa na wabunge wa CCM na Halmashauri zote saba zinaongozwa na wenyeviti kupitia CCM. 

Katibu wa CCM wa wilaya ya Simanjiro Ally Kidunda alisema wamejipanga kuhakikisha mbunge na madiwani wa CCM wanafanya mikutano na wananchi na kuwasikiliza kero zao na kuzungumza nao.

Rais Wa Uganda Museveni Alivyowasili Chato Mkoani Geita Na Kupokewa Na Rais Dkt. Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.


Watanzania na Wakenya ni miongoni mwa 26 waliouawa katika shambulizi Somalia

$
0
0
Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la kigaidi dhidi ya hoteli moja kusini mwa Somalia imeongezeka na kufikia watu 26. Awali Polisi ya Kismayo iliripoti kuwa waliouawa katika hujuma hiyo ya kigaidi ni watu saba.

Rais wa eneo lenye mamlaka ya ndani la Jubaland kusini mwa Somalia, Ahmed Mohamed amesema miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo la kigaidi la jana Ijumaa katika mji wa bandari wa Kismayo ni raia kadhaa wa Tanzania, Kenya, Marekani na Uingereza.

Vyombo vya usalama vinasema kuwa, gaidi mmoja aligongesha gari lililojaa mada za milipuko katika Hoteli ya Asasey katika mji wa Kismayo kabla ya washambuliaji hao kuvamia jengo hilo.

Msemaji wa operesheni za kijeshi wa kundi la wanamgambo wa al-Shabaab, Abdiasis Abu Mus'ab ametangaza kuwa, wanachama wa genge hilo ndio waliohusika na shambulizi hilo.

Shambulio hilo limefanyika siku moja baada ya kumalizika mkutano wa kupiga vita ugaidi uliofanyika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, ambapo mikakati ya kulitokomeza kundi hilo la ukufurishaji ilijadiliwa.

Akihutubu katika mkutano huo wa Pan African counter-terrorism, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alionya kuwa ugaidi unatishia amani ya bara la Afrika na kusisitiza kuwa, jinamizi hilo halipaswi kuruhusiwa kudhoofisha mwenendo wa ustawi katika bara hilo.

Hezbollah: Iran inaweza kuiangamiza Israel iwapo vita kati ya Marekani na Iran itatokea.

$
0
0
Mkuu wa kundi la Hezbollah Hassan Nasrallah amesema Iran, inao uwezo wa kuiangamiza Israel iwapo vita kati ya Marekani na Iran itatokea. 

Mkuu huyo wa Hezbollah amesema ni wazi Israel ambayo ni mshirika wa Marekani haiwezi kuacha kufungamana na upande wowote iwapo vita itatokea kati ya nchi hizo mbili. 

Nasrallah, ambaye kundi lake linaungwa mkono na Iran ameyasema hayo katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Al Manar wiki chache baada ya kuzidi kufukuta kwa mgogoro kati ya Marekani na Iran. 

Ameongeza kuwa, iwapo Marekani ingejua kuwa vita dhidi ya Iran vinaweza kuiangamiza Israel, ingejitafakari upya. 

Israel, imefanya mamia ya mashambulizi nchini Syria dhidi ya kile inachokiita maeneo yanayolengwa kijeshi ya Iran na Hezbollah. 

Hapo jana, baraza la wawakilishi la Marekani, lilipiga kura ya kudhibiti uwezo wa Rais Trump wa kuishambulia Iran likihofia sera zake zinazoelekea kuanzisha vita visivyo vya lazima.

Waziri Mkuu: Suala La Kuwaondoa Watumishi Wala Rushwa, Wazembe Ni Endelevu

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema suala la kuwaondoa kazini watumishi wa umma ambao ni wazembe, wala rushwa na wasiotimiza majukumu yao ipasavyo ni endelevu.

‘Serikali inahitaji watumishi wenye heshima na nidhamu ya kazi ili waweze kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote iwe wa kiuchumi, kidini au kikabila.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Julai 13, 2019) wakati akihutubia mwananchi katika kongamano la kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa utekelezaji wa ilani.

Kongamano hilo limeandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ili kumpongeza Rais Dkt. Magufuli lilifanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Amesema Serikali imejipanga vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, hivyo amewataka wananchi watoe taarifa iwapo watabaini uwepo wa watumishi wanaojihusisha na rushwa.

"Watumishi wa umma tunataka watambue kwamba wao ni watumishi wa wananchi, hivyo hawana budi kutambua wajibu wao ambao ni kuwatumikia mwananchi ipasavyo."

Amesema kuwa Serikali imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya rushwa ambapo kwa Afrika Tanzania inaongoza kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Transparency Internation.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi amesema kongamano hilo ni muendelezo wa makongamano mengine ya kumpongeza Rais yaliyofanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Unguja na Pemba.

Amesema viongozi hao wameonesha dhamira ya kweli ya kuwaletea wananchi maendeleo. "Tutaendelea kushirikiana na viongozi wetu na hatupo tayari kugawanyika."

Awali, Mawaziri na Manaibu Waziri mbalimbali walipata fursa ya kuelezea namna ilani ilivyotekelezwa katika maeneo mbalimbali kupitia wizara zao.

Katika kongamano hilo viongozi na wanachama wa vyama mbalimbali walivihama vyama vyao na kujiunga na CCM akiwemo na aliyekuwa Kalibu wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Maombi ya Kujiunga Vyuo Vikuu Kuanza Rasmi Jumatatu July 15.....Soma Hapa Taarifa Rasmi ya TCU

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa amezungumzia wahitimu wanaohitaji maombi ya Vyuo vya Elimu ya Juu kuzingatia umakini katika uombaji kwa sababu hakuna kubahatisha.

Prof.Kihampa amesema wanaoomba maombi hayo wanapaswa kuomba kupitia tovuti za Vyuo husika na yatafanyika kwa njia ya Elektroniki.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 14 July

Breaking News: Rais Magufuli Amemteua Julius Mtatiro Kuwa Mkuu Wa Wilaya Tunduru.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Yaipiga faini ya shilingi bilioni 1, Benki ya DTB kwa kosa la kutoanzisha kituoa cha data (Information Data Center).


BREAKING: Benki kuu ya Tanzania yasitisha uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya TIB Corporate.

Rais Magufuli Kuzindua Nyumba Za Polisi Geita

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewaomba wananchi wa mkoa wa Geita pamoja na maeneo jirani na mkoa huo kujitokeza kwa wingi siku ya jumatatu kwenye tukio la uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari, uzinduzi utakaofanyika katika eneo la magogo mkoani humo.

IGP Sirro amesema kuwa, katika tukio hilo ambalo litaongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, ambapo atazindua zaidi ya nyumba 114 zilizokwisha kamilika huku matarajio ya mradi huo ni kuwa na nyumba takribani 400 kwa nchi nzima.

Aidha, IGP Sirro amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha askari wanaishi kwenye mazingira mazuri jambo ambalo litachangia weledi na uwajibikaji hususan kulinda maisha ya raia na mali zao.

Chadema kutinga mahakamani Kupinga Tundu Lissu kuvuliwa ubunge

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kimesema  mapema wiki ijayo kinategemea kufika mahakamani kupinga utaratibu uliyotumika kumvua ubunge aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Antipas Lissu ambaye yupo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu baada  kushambuliwa na watu wasiojulikana mwaka jana katika eneo la eria D jijini Dodoma .

Hayo yamesemwa  na mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa chama hicho  John Mrema  wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili mkoani Njombe  akiwa ameambatana  viongozi mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa chama hicho freeman mbowe  ambaye amefanya mkutano wa ndani mjini humo.

Mrema amesema kuwa chama hicho kinaona kuwa utaratibu huo umekiuka sheria kwa sehemu kubwa kwakuwa utenguzi huo umefanyika wakati  mbunge huyo akiwa katika matibabu na kwamba kuhusu kujaza fomu za maadili na mali amesema asingeweza kujaza kwa kuwa hakuwa ndani ya nchi na asingeweza kusainiwa kwa mujibu wa sheria

 Amesema Agenda nyingine ambazo zinajadiliwa katika ziara hiyo katika kanda ya Nyasa ni pamoja uchaguzi wa serikali za mitaa,kuwashukuru viongozi na wanachama kwa kazi kubwa waliyofanya wakati  mbowe na viongozi wa chadema wakiwa mahabusu kwa zaidi ya miezi minne pamoja na kutoa ufafanuzi wa sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo imeonyesha kubadili kwa kiasi kikubwa utendaji wa vyama nchini.

Nao baadhi ya viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo Rose Mayemba kiongozi wa chadema msingi na Alatanga Nyagawa ambaye ni katibu wa mkoa chama wamesema wameanza kuandikisha wanachama katika daftari la maalumu la A3 kuanzia ngazi ya chini na kwamba watanzania wategemee chama hicho kupata ushindi mkubwa kwa kuwa kimejihimarisha katika utunzaji wa taarifa.

Katika ziara hiyo Mbowe  amekagua ujenzi wa jengo la ofisi za chama iliypo katika mtaa wa hagafilo ilyofikia asilimia 95 katika ujenzi wake

RPC Shinyanga athibitisha Tukio la kushambuliwa na kudhalilishwa kwa Mshiriki wa Miss Shinyanga 2019.

$
0
0
SALVATORY NTANDU
Jeshi la mkoani Shinyanga limethibitisha kuwepo kwa tukio la kushambuliwa kwa mwanamitindo, Nicole Emanuel (19) mshiriki wa Miss shinyanga 2019 kushambuliwa na waandaaji wa shindano hilo na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda wa Polisi mkoa humo, (ACP) Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea julai 11 mwaka huu katika hoteli ya Nedman iliyopo mjini Shinyanga.

Amewataja waliohusika kumshambulia na kumshalilisha  Nicole ni pamoja na mkurugenzi wa  Makumbusho  Entertainment, Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) mkoa wa Shinyanga na Meneja Mkuu wa Makumbusho Entertainment, George Foda.

Amesema watuhumiwa wanadaiwa kumshambulia kwa kupigwa ngumi, mateke, kuburuzwa na kisha kuchaniwa nguo zake jambo ambalo kumsababishia majeraha  maumivu makali baada ya Nicole kwenda kuwadai fedha za  nauli na gharama alizotumia katika shindano la miss Shinyanga.

Bei ya pamba nyuzi katika Soko la dunia yashuka Makampuni ya hofia kupata hasara Shinyanga

$
0
0
SALVATORY NTANDU
Kushuka kwa bei ya Pamba nyuzi katika Soko la dunia kumetajwa kuwa ndio chanzo cha makampuni ya ununuzi wa zao la Pamba  mkoani Shinyanga kushindwa kununua kwa kuogopa kupata hasara.

Hayo yamebainishwa na Amiri Mwinyimkuu Meneja Shughuli wa Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) wakati akizungumza na waandishi wa Habari mjini Kahama kuhusiana na hatua walizichukua ili kukabiliana na tatizo hilo.

Amesema kwa sasa Kampuni za ununuzi wa zao hilo zimeshindwa kwenda sokoni kununua pamba kutokana na kushuka bei ya Pamba nyuzi katika soko  la dunia hali ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kufunguliwa kwa soko la Pamba.

Amefafanua kuwa bei ya pamba nyuzi katika soko la dunia kwa sasa ni dola 1.39  ambayo ikibadilishwa kwa fedha za kitanzania ni shilingi 1,449 hivyo endapo watanunua pamba mbegu kwa shilingi 1,200 watapa hasara.

Ameongeza kuwa kampuni hizo zimeomba bei ya kununua kwa mkulima ishuke sokoni au serikali iwape kinga (guarantee) ya  kuwafidia hasara itakayopatika baada ya kuuza pamba katika soko la dunia  ambapo hadi sasa bado serikali haijatoa maekekezo yeyote.

Katika hatua nyingine Mwinyimkuu amesema  wakulima katika wilaya ya kahama wamelima pamba ekari 40,869 na wanatarajia kuvuna kilo zaidi ya milioni 400.

Makampuni yaliyopatiwa leseni za kununua pamba hizo ni Kahama Cotton Campuny Limited (KCCL) Kahama Oil Mill, Afriacian na kampuni ya Fresho ambapo mpaka sasa kampuni mbili ndio zimeweza kununua zao hilo ambazo ni Fresho na Kahama Oil Mills.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images