Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Waongezeka Hadi Asilimia 3.7% Kutoka Asilimia 3.5%.

0
0
Na.Faustine Gimu  Galafoni,Dodoma.
Mfumuko wa bei wa Taifa  kwa mwaka ulioishia Mwezi   Juni,2019   umeongezeka hadi asilimia 3.7%  kutoka asilimia 3. 5%   kwa mwaka  ulioishia   Mwezi  MEI,2019. 

Hayo  yamesema  leo    Julai 8,2019   jijini  Dodoma  na mkurugenzi wa  Takwimuza  Uchumi  Bw.Daniel Masolwa ambapo amesema  hali hiyo inamaanisha kuwa ,kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka  ulioishia mwezi  Juni ,2019 imeongezeka   ikilinganishwa na kasi ya iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mwezi  Mei,2019. 

Bw.Masolwa amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Taifa  kwa mwaka ulioishia  Mwezi Juni ,2019 kumechangiwa  kuongezeka  kwa bei za  baadhi ya bidhaa za  vyakula na bidhaa zisizo za  vyakula kwa kipindi kilichoishia Mwezi Juni,2019   Zikilinganishwa  na bei ya bidhaa za mwaka ulioishia mwezi Juni,2018. 

Baadhi  ya bidhaa za  vyakula zilizochangia kuongezeka  kwa  mfumuko wa bei   wa Mwezi Juni,2019 ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia  3.6%,unga wa ngano kwa  asilimia   4.4%,mtama kwa asilimia 4.9%,samaki wabichi kwa asilimia   27.3%,dagaa kwa   asilimia 16.5%,mafuta ya kupikia kwa asilimia 9.5%,maharagwe kwa asilimia 3.0%,mihogo kwa asilimia    16.6% na viazi mviringo kwa asilimia 18.8%. 

Aidha,Bw.Masolwa amevitaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei     wa Mwezi Juni,2019 ni pamoja na dizeli kwa asilimia 11.4%,petrol kwa asilimia 4.9,gharama za kulala kwenye nyumba za wageni kwa asilimia 5.8% na vitabu vya shule kwa asilimia 2.4%. 

Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Juni,2019 umeongezeka hadi asilimia 2.3kutoka asilimia 2.2% kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2019. 

Hata hivyo,Mkurugenzi huyo wa Takwimu za Uchumi Bw.Masolwa amezungumzia mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulkioishia Mwezi Juni,2019 ambapo nchini Uganda mfumuko wa bei     umeongezeka kwa asilimia   3.4% kwa mwaka ulioishia Mwezi     Juni,2019  Kutoka asilimia 3.3% kwa mwaka ulioishia Mwezi Mei,2019 na Kenya  mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Mwezi Juni,2019 umeongezeka  hadi asilimia 5.70% kutoka asilimia  5.49 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2019.  

Ikumbukwe kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu [NBS]ni Taasisi ya Umma  iliyoanzishwa kwa sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 pamoja na mapitio yake ya   mwaka 2018    na kwa mujibu wa sheria hiyo ,NBS imepewa mamlaka ya kutoa ,kusimamia na kuratibu upatikanaji wa taarifa za Takwimu hapa nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za mfumuko wa bei kwa ajili ya  matumizi ya serikali na wadau wa Takwimu.

Kigwangallah Ampa Makavu January Makamba...."Ni Dharau na Kujionesha tu"

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla ameonesha kutoridhishwa na kauli ya Waziri wa Mazingira, January Makamba akiieleza TANAPA kuwa hawawezi kuanza utaratibu wa kutumia magari maalumu ya umeme (Cable Cars), kwa ajili ya watalii wanaotembelea mlima Kilimanjaro.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri Kigwangalla amehoji baadhi ya maswali kwenda kwenye mamlaka ya mazingira, akieleza kuwa watu hao wamekuwa wakishiriki zaidi kwenye makongamano na si uhalisia wa kulinda mazingira.

"Watu wa mazingira wanataka kuingilia kati mradi wa cable cars KILIMANJARO. Lengo letu ni kukuza utalii, kuongeza mapato na kuboresha experience ya watalii wetu nchini. Tusipokuwa wabunifu tunatukanwa kutokutumia vizuri vivutio vyetu, tukiamka wanakuja ‘speed governors’.

"Hivi kuna nchi ngapi zimeweka Cable Cars kwenye milima yake?, hizi haziharibu mazingira?, Cable inapita juu inaharibu mazingira gani?. Zaidi ya hekari 350,000 za misitu zinapotea kila mwaka nchini, ipi ni hatari kubwa?, watu wa mazingira wamechukua hatua gani zaidi ya makongamano tu?", amesema Kigwangalla.

Hivi karibuni wakati TANAPA ilieleza mpango wake wa kuja na namna mpya ya usafiri kwa watalii wanaotaka kwenda kutembelea mlima Kilimanjaro, Waziri wa Mazingira, January Makamba akasema suala hilo haliwezi kufanyika mpaka pale NEMC watakapo thibitisha.

"Inabidi watu wa Mazingira tupitishe na kutoa cheti kwanza kabla hawajaanza. Na tutafanya 'studies' ili kujua madhara kwa mazingira na uthabiti wa 'mitigation measures", alisema Makamba

Vijana wapewa elimu kuhusu kuanzisha biashara ili kujikwamua na uchumi

0
0
Na.Mwandishi Wetu-DSM
Vijana wapewa elimu kuhusu kuanzisha biashara ili kujikwamua na uchumi kwa  kuchangamkia fursa zilizoko kwenye maeneo yao na kujua umuhimu wa kodi katika biashara ili kuwezesha taifa kupata mapato na wao kupata faida. 

Akizungumza katika Semina ya Vijana iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana Tanzania (TYVA), Afisa Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi kutoka TRA, Isihaka Sharifu alisema kuwa Serikali imerekebisha baadhi ya Sheria za kodi hususani kwa vijana wanaofungua kampuni au biashara mpya. 

Sharifu alisema kuwa kwa sasa Sheria ya kodi imejikita kuwasaidia vijana wanaoanzisha kampuni na biashara mpya kwani imeweza kugusa msamaha wa kodi kwa miezi sita tofauti na awali ambapo biashara mpya zilikuwa zinalipiwa kodi baada ya miezi mitatu. 

“ Kwa sasa Sheria inasema ukiwa unafungua biashara yako au kampuni mpya kwa sasa unatakiwa kulipa kodi baada ya miezi sita, kwa hiyo hii itawasaidia vijana wengi ambao wanania ya kuanzisha biashara, nawasihi vijana wenzangu tumieni Fursa hiyo kujikwamua kiuchumi”, Alisema Sharifu. 

Katika Semina hiyo ambayo kauli mbiu yake ilikuwa ‘Nguvu ya Kodi’ Sharifu alipaeleza kuwa TRA inatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwakwamua vijana hasa wajasiriamali wadogo ambao wanafanya biashara zao kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini. 

Alisema kuwa kodi inayotozwa kwa wafanya biashara wenye mauzo kuanzia milioni 0 hadi 100 imegawanyika katika makundi manne ambayo ni mauzo kuanzia 0 mpaka milioni 4 ambao hawatozwi kodi, mauzo ya milioni 4 mpaka 7.5 wanatozwa 100,000, milioni 7 mpaka 11 wanatozwa  250,000 na milioni 11 mpaka 14 wanatozwa 450,000 tofauti na hapo zamani ambapo walikuwa wanatozwa 546,000, kwa hiyo vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo. 

Kwa upande wake, Afisa Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Anna Marika alisema kuwa vijana wanatakiwa kuwa wazalendo kwa kutimiza wajibu wao kwenye suala la kulipa kodi kama Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli anavyoagiza. 

“Nimefurahi kwa Semina hii kwani watoa mada wamekuja na Mada nzuri zinazoelimisha ulipaji Kodi, wito wangu kwa vijana ni kwamba wanatakiwa kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kama Rais alivyoagiza kuchukua vitambulisho ili wasipate shida kwenye maeneo yao ya kufanyia Biashara”, Alisema Marika. 

Marika aliongeza kuwa kwa Wilaya ya Temeke wamejikita zaidi katika kuwasaidia vijana, wanawake na walemavu kujikwamua kimaisha kama Ofisi ya Rais –TAMISEMI ilivyoagiza kuwa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri ijikite kwenye kuwasaidia vijana, wanawake na walemavu. 

Alisema Wilaya ya Temeke imetanga asilimia nne kwa vijana, asilimia  nne kwa wanawake na asilimia mbili kwa walemavu, huku wakilenga kuboresha utoaji wa huduma kwa kutoa vifaa vya kazi kwa vikundi mbalimbali kama vile pikipiki, Chelehani,vifaa vya mziki na magari ya kuzoa takataka na kusomba matofali. 

Alitolea mfano wa kikundi cha wanawake waliopewa chelehani 50 na wataanza kurejesha mikopo baada ya miaka miwili na wakimaliza mkopo vifaa vile vinakuwa mali ya kikundi. 

“Niombe sasa kwa wale vijana ambao mnaisha Temeke, haijarishi unatoka Wilaya gani hapa Dar es Salaam au mkoani, mkirudi kwenu kachangamkieni fursa hii ili kuwawezesha kujikimu kimaisha na kupata faida kubwa ya kuendesha uchumi wenu”, Alisistiza Marika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne 9 July

Bunge la Tanzania kuwa mwenyeji wa vikao vya Kamati ya Uongozi na ya Bajeti za Chama cha Wabunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola–Kanda ya Afrika

0
0
Bunge la Tanzania linatarajia kuwa mwenyeji wa vikao vya Kamati ya Uongozi na ya Bajeti za Chama cha Wabunge wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola–Kanda ya Afrika (CPA-AFRICA REGION) vitakavyofanyika tarehe 9 hadi 14, Julai, 2019 katika Ofisi Ndogo za Bunge la Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

Kamati hizo zitakutanisha Wajumbe kutoka Mabunge zaidi ya Kumi (10) ya nchi za Afrika ambapo mbali na Wajumbe hao vikao hivyo pia vinatarajiwa kuhudhuriwa na Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi, Spika wa Bunge la Sierra Leone Mhe. Dkt. Abbas Bundu, Spika wa Bunge la Uganda Mhe. Rebbeca Kadaga na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Y. Ndugai ambaye ndiye mwenyeji wao.
 
Aidha, mbali na Maspika hao, vikao hivyo vitahudhuriwa na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon Mhe. Emilia Lifaka, Naibu Spika wa Bunge la Namibia, Mhe. Bernard Sibalatani na pia Mnadhimu Mkuu wa Bunge la Ghana Mhe. Dkt. Osei Mensah Bonsu.
 
Mbali na vikao vya Kamati, kutakuwa pia na kikao cha Bodi ya Chama cha Wabunge wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika ambacho kitafanyika tarehe 11 Julai, 2019.
 
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Y. Ndugai anatarajiwa kuhudhuria na kuongoza kikao cha Bodi ya Chama cha Wabunge wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola–Kanda ya Afrika na pia kutoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Uongozi wa chama hicho.
 
Wajumbe wengine ambao ni Waheshimiwa Wabunge wanaotarajiwa kuhudhuria katika vikao hivyo wanatoka katika Mabunge ya nchi za Malawi, Kenya, Nigeria, Ghana, Sierra Leone, Afrika kusini, Uganda, Namibia, Zambia, Lesotho, Mauritius na wenyeji Tanzania. Kwa hivi sasa Bunge la Tanzania ndiyo Sekretarieti ya Chama Chama cha Wabunge wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola–Kanda ya Afrika.
 
Imetolewa na;
KATIBU WA CPA-KANDA YA AFRIKA
8 Julai, 2019

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Ahudhiria Mkutano Wa 12 Wa Dharura Wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kuhusu Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,  ameshiriki katika Mkutano wa 12 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) unaofanyika jijini Niamey nchini Niger.
 
Makamu wa Rais Mhe. Samia ameipongeza Serikali ya Ghana kwa kuchaguliwa kuwa Makao Makuu ya Sekretarieti ya AfCFTA na kuisihi Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuharakisha ukamilishaji wa muundo, wa bajeti na mpango kazi  wa Sekretarieti hiyo ili ianze kufanya kazi haraka.
 
Mkutano huo wa Wakuu wa nchi na Serikali umepokea taarifa ya Mheshimiwa Mahamadou Issoufou, Rais wa Jamhuri ya Niger kuhusu utekelezaji wa AfCFTA ambayo imepokelewa na kupishwa na viongozi hao. Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) umeanza kazi rasmi tarehe 30 Mei, 2019 na unahusu uasili wa bidhaa zitakazouzwa katika soko la Afrika, kufungua biashara ya bidhaa kwa asilimia 97 na uanzishwaji wa Sekretarieti ya kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA.
 
Aidha, alimpongeza Mheshimiwa Mahamadou Issoufou, Rais wa Jamhuri ya Niger kwa jitihada zake za kuhakikisha azma ya Umoja wa Afrika ya kuanzisha Soko Huru la pamoja la Afrika inafikiwa. 

Makamu wa Rais pia alizipongeza nchi 27 wanachama wa Umoja huo zilizoridhia mkataba wa uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) kati ya nchi 54 zilizotia saini mkataba huo na kuahidi kwamba Tanzania itaungana nao baada ya kukamilisha taratibu za ndani.
 
Kwenye mkutano huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo alitoa salam za Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wakuu wa Nchi na Serikali waliohudhuria mkutano huo.
 
Wakati huo huo Waziri wa Fedha na Uchumi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa amesema kwa upande wa Afrika Mashariki  Tanzania imepiga hatua zaidi kutokana na kuwepo katika Jumuiya za Afrika Mashariki na SADC, hivyo Tanzania imefaidika sana kutokana na kupanuka kwa Soko hilo.
 
Nae Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro amesema Tanzania imenufaika na mkutano huo kutokana na kuendelea kujifunza zaidi kuhusiana na Biashara ya pamoja katika Afrika pamoja na kuweza kushiriki kuchagua Muwakilishi wa Bara la Afrika katika nafasi mbalimbali ndani ya Afrika na Duniani kote wakati Tanzania imepata nafasi moja ambapo Bethabina Seja Afisa wa Takukuru amechaguliwa katika Bodi ya kudhibiti Rushwa Barani Afrika.

Upandaji holela wa miti katika njia za umeme Kahama watajwa kusababisha nishati ya umeme kukatika.

0
0
NA SALVATORI NTANDU
Upandaji holela wa miti katika njia kuu za Umeme Wilayani kahama mkoani Shinyanga umetajwa kuchangia kusababisha Nishati hiyo kukatika mara kwa mara kutoka na miti hiyo kugusa nyanya za Umeme.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilayani Kahama Mhandisi King Fokanya wakati akizungumza na waandishii wa habari ofini kwake kuhusiana namna walivyojipanga kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme.

Amesema katika maeneo mengi wilayani humu wananchi wamepanda miti mikubwa katika karibu na nguzo za umeme jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa pindi nguzo zinapo anguka ama kuguswa na miti hiyo.

Amefafanua kuwa pindi Shirika hilo linapotaka kuikata baadhi yao wamekuwa wakilaumu juu ya ukataji wa miti hiyo katika njia za umeme na watumishi wake katika oparesheni za kuhakikisha miundombinu hiyo inakuwa salama.

Katika Hatua nyingine Mhandisi Fokanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 Ofisi yake imepokea shilingi milioni 847 kwa ajili ya kupeleka huduma ya nishati ya umeme kwenye kata 10 ambazo hazina umeme zilizopo Halmashauri ya Mji wa Kahama na Msalala.

Amefafanua kuwa  shilingi Milioni 847 zimegawanya katika makundi mawili ambapo shilingi milioni 402 zitatumika kupeleka huduma ya nishati ya umeme kwenye kata 10 msalala na kahama mjini huku Milioni 445 zinatumika kwenye mategenezo ya kubadilisha nguzo,vikombe, maboresho ya Transfoma na vifaa vilivyoharibika.

Kata ambazo zinapelekewa huduma hiyo ni pamoja  kata ya Muhungula, Nyakato, Mbulu, Mhongolo, Nyashimbi, Nyihogo sekondari, Kagongwa, Mwendakulima Isaka na Kakola.

Mwisho.

LIVE:Rais Magufuli anazindua Hifadhi mpya ya Taifa ya Burigi Chato

0
0
LIVE:Rais Magufuli anazindua Hifadhi mpya ya Taifa ya Burigi Chato

Uhusiano Kati Ya Punyeto Na Kusinyaa Kwa Maumbile Ya Kiume

0
0
Zipo sababu kuu 2 kwanini wanaume walio jihusisha na punyeto kwa muda mrefu maumbile yao husinyaa na kuwa kama ya mtoto.

SABABU YA KWANZA: Tendo la kujichua linapo fanyika kwa muda mrefu huathiri na kuharibu misuli ya uume na hivyo kusababisha kujengeka kwa mafuta na tishu zisizo vutika kwenye mishipa ya ATERI.

Kujengeka kwa mafuta na tishu zisizo vutika kwenye mishipa ya ateri husababisha mambo makuu mawili. Kwanza huzuia mishipa ya ateri kupanuka na kuongezeka.

KUPANUKA NA KUONGEZEKA KWA MISHIPA YA ATERI NI JAMBO MUHIMU SANA KATIKA UKUAJI WA MAUMBILE YA KIUME. Mishipa hii inapo shindwa kupanuka na kuongezeka huathiri ukuaji wa maumbile ya kiume na hivyo kusababisha maumbile ya mhusika kudumaa.

Lakini pili, kujengeka kwa mafuta na tishu zisizo vutika ndani ya mishipa ya ateri huzuia na kuathiri kutiririka kwa damu kwenye misuli ya uume. Mambo haya mawili yanapo tokea huathiri uzalishaji wa homoni zinazo husika na kuchochea ukuaji wa maumbile ya kiume. Homoni hizi hujulikana kitaalamu kama HGH na huzalishwa kwenye ini.

Hali hii inapo tokea basi maumbile ya kiume ya mhusika husinyaa na kudumaa kiasi cha kuyafanya yaonekane kama ya mtoto mdogo.

SABABU YA PILI: Upigaji wa punyeto huathiri utendaji wa ini. Na katika ini ndimo zinamo zalishwa homoni ziitwazo HGH ambazo hu husika na kufanya kazi ya kuchochea ukuaji wa maumbile ya kiume.

Kinacho fanya ini la mwanaume anae jihusisha na.punyeto lishindwe kuzalisha homoni za HGH ni mwili wa mhusika kukosa kiwango cha kutosha cha nishati kinacho hitajika katika uzalishaji wa homoni hizo. Nishati hii hupotea kwa wingi wakati wa tendo la upigaji punyeto.

Mwanaume anae piga punyeto hutumia nguvu, akili na nishati nyingi sana . Nishati hii ambayo inahitajika mwilini ili itumike katika kazi mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa homoni za HGH kwenye ini inatumika kwenye tendo la upigaji punyeto na hivyo kupotea bure.

Kibaya zaidi ni kwamba waathirika wengi wa punyeto huanza kujihusisha na punyeto wakati wa balehe. Na ni katika kipindi hiki hiki cha balehe ndio kipindi ambacho homoni za HGH huzalishwa kwa wingi na huhitajika kwa wingi mwilini katika kufanya kazi ya kuchochea ukuaji wa maumbile ya kiume.

Matokeo yake ini linashindwa kufanya kazi ya kuzalisha homoni hizo kwa sababu ya kukosa kiwango cha nishati kinacho hitajika ili kuweza kuzalishwa kwa homoni hizo.

Kukosekana kwa homoni hizo hupelekea maumbile ya kiume ya mhusika kushindwa kuongezeka ambako huenda sambamba na kusinyaa, kulegea na kunywea ndani kiasi cha kuyafanya yaonekane kama ya mtoto.

NINI SULUHISHO LA MAUMBILE YA KIUME YALIYO ATHIRIKA KWA PUNYETO: Mwanaume ambae maumbile yake ya kiume yame athiriwa na upigaji punyeto wa muda mrefu anatakiwa apate tiba maalumu ya asili ambayo INATIBU na KUPONYESHA kabisa tatizo la maumbile ya kiume ambayo yameathirika kwa punyeto. Tiba hii ya asili mbali na kufanya kazi ya KUREFUSHA na KUNENEPESHA maumbile ya kiume ambayo yamesinyaa kwa ajili ya punyeto lakini pia INATIBU na KUPONYESHA kabisa tatizo la ukosefu na upungufu wa nguvu za kiume linalo tokana na kufanya punyeto kwa muda mrefu.

JINSI  YA  KUPATA  DAWA  HII
Kupata  dwa  hii  fika  katika  duka  la  kuuza  dawa  za  asili. Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

kwa  wateja  wetu  waliopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  ambao  hawana nafasi  ya  kufika  dukani  kwetu  tunayo  huduma  ya  kuwapelekea dawa  mahali  walipo  (  HOME  &  OFFICE  DELIVERY)  na  kwa  wateja  wetu  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar Es  Salaam, tunatumia  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  mbalimbali.

WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA : 0693 005 189.

Tutembelee  kwenye  site  yetu :  www.neemaherbalist.blogspot.com

Tu  follow  Instagram kupitia :  www.instagram.com/Neema Herbalist  Official.

Katazo La Mifuko Ya Plastiki Nchini Limesaidia Kuweka Mazingira Safi.

0
0
Na Faidha Jumanne-Maelezo.
Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya mazingira imefanikiwa kuboresha upatikanaji wa mifuko bora mbadala kwa wananchi. 

Hii imetokama na jitihada za serikali za kupiga marufuku mifuko hiyo, kuanzia tarehe 01 Juni 2019 na kupelekea kupatikana kwa mifuko mbadala,  kwa wananchi inayoimarisha afya zao kuongeza ajira na kupunguza uchafuzi wa mazingira. 

Akihojiwa na Idara ya Habari - MAELEZO, Afisa Habari Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Lulu Musa, alianza kusifia juhudi zilizopatikana kwa muda mfupi, huku akirejea Siku ya Maazimisho ya Usafi Kitaifa Jijini Dodoma, yaliyofanyika Juni 5, 2019. 

``Tumetoa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwa wananchi, kazi hii inafanywa na Halmashauri za Serikali za Mitaa- TAMISEMI kwa kusimamia maeneo yao kwa kutotumia mifuko ya plastiki hakika wanastahili pongezi, nasema hongereni sana”. 

Uamuzi wa Serikali kuhusu kuondoa matumizi ya mifuko ya plastiki lengo lake ni kuboresha usafi wa mazingira na kuwaweka wananchi katika hali ya kuepuka magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na kuhara damu. 

“Lengo ni kuimarisha afya.  Kadhalika, mazingira salama ambapo, sote tunatambua umuhimu wa mtu kuwa na mazingira mazuri na yenye usalama kiafya kwa kushiriki katika shughuli za kijamii na za kitaifa”. Amesisitiza Lulu. 

Ameongeza  serikali itaendelea kuwa macho kufuatilia mwitikio mzuri wa wananchi kutoendelea kutumia mifuko ya plastiki, na kutotegemea watu wengine kusimamia mazingira ya Watanzania, kadhalika akasema bali iwe ni zoezi la kawaida kwa wananchi.  

Lulu akazidi kufafanua kuwa, serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kutunza mazingira kwa lengo  la kuboresha afya zao na kufahamu kwa kina mifuko ya plastiki kwa kiasi gani imeleta madhara na kusababisha magonjwa ya aina mbalimbali yakiwemo nyemelezi,  kuteketeza uhai wa viumbe kama vile samaki na mifugo. 

Aidha, Tanzania ni nchi miongoni mwa nchi zilizoonekana katika orodha ya matumii makubwa ya mifuko uya plastiki. Hii ilitokana na kuongezeka kwa kasi kwa matumizi hayo kadiri siku zilivyozidi kwenda, amesema Lulu.  

Imeelezwa pia, Serikali kwa kushilikiana na wadau kama Shirika la Viwango Tanzania -TBS limeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwenye sekta ya afya na mazingira yenye lengo la kuboresha matumizi ya mifuko mbadala na kuimalisha afya za wananchi. 

Mfano, TBS imeweka viwango vya ujazo kwenye mifuko ya plastiki ambayo bado inatumika kama vifungashio kuepusha kuzagaa kwa mifuko ya plastiki na kusababisha uchafuzi wa mazingira. Pia, imebainisha  viwango vya mifuko ambayo imeruhusiwa kwa kutumika kwa kufungashia chakula pamoja na madawa ya kilimo kwa kuangalia uzito/ujazo wa bidhaa, aina za bidhaa ambazo zitatumia mifuko hiyo ili kuweza kusaidia katika utunzaji wa mazingira. 

Vilevile,  Lulu aliongezea kuwa shirika la viwango, TBS litakua na uwezo wa kuwasiliana na wananchi kwa njia yoyote ile hata ikiwa kimtandao kwa kuwapa taarifa ya matumizi ya mifuko iliyo bora na yenye viwango  ili kuweza kusaidia kutoa huduma bora kwa wanainchi. 

Akielezea mfumo wa matumizi ya kidigitali Lulu amesema kuwa, Tanzania ilishaingia mfumo wa matumizi ya kidigitali katika utoaji huduma kwenye maeneo mengi, na imekuwa msaada mkubwa katika shirika la viwango TBS. 

Hata hivyo Tanzania imekua na matumizi mazuri ya mfumo wa kidigitali kwa kutoa mawasiliano kwa wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii na kuleta mafanikio chanya katika mwitikio wa jambo kama hili la katazo ya mifuko ya pllastiki, Lulu akasema, “Kupitia mfumo huu wa kutoa mawasiliano katika mitandao ya kijamii utasaidia kuongeza uwingi wa watu katika kupata taarifa kwa uharaka na sisi kutupelekea ufanyaji kazi wetu kutoa taarifa haraka kwa umma”.
`` … tutaendelea kuwa na utaalamu wa hali ya juu kwa kuhakikisha taarifa tutakazo zitoa zitakuwa taarifa sahihi zenye viwango sahihi kwa kutoa msaada mkubwa sana kwa kuwa hizi taarifa ni za muhimu sana kwa wananchi’’.   

Akiongea mmoja wa wananchi waliohojiwa,  Hashim Chikwaya ambaye ni mkulima amesema, “  Kutokana na kusitishwa  kwa mifuko ya plasiki,  hakika hili ni jambo jema sana kwa wananchi kwa kuwa wananchi walikuwa wakitumia mifuko hiyo kwa kuhifadhia chakula ambacho chakula hicho ni chenye joto” alisema Chikwaya.  

Akaendelea Chikwaya ambaye anaonekana kuwa na uzoefu wa kujua athari za mifuko, kuwa Kutokana na joto la kwenye mfuko linasababisha kutoa mvuke wenye majimaji ya tindikali ambayo imetumika kutengenezea mfuko huo na kuingia kwenye chakula, iwapo chakula hicho kikiliwa na mtu, hupata athari kubwa za kiafya.   

Vilevile, akielezea zaidi adhari za kiafya Chikwaya alisema “Kulikuwa na matumizi mengine yasiyokuwa ya lazima pale mtu anapochukua mfuko wa plastiki kwa matumizi ya kuwashia moto, hususani jiko la mkaa, kitendo hicho kinapofanyika mtu huyo anavuta hewa ya mfuko unaoyeyuka na kumsababishia madhara ya kupata ugonjwa wa kansa”. 

Akimalizia, Chikwaya alisema, mbali na uchafuzi wa mazingira mara nyingi, mfano hospitali madaktari walikuwa wakishauri kuepukana na matumizi ya vifaa vya plastiki kuhifadhia chakula chenye joto na kusema kuwa plastiki hizo huchubuka zipatapo joto na kusababisha athari ya upatikanaji wa magojwa pinde ulapo chakula hicho, akaongeza, “hata hivyo si rahisi kuona michubuko hiyo kwa macho”.  

Zoezi la katazo la Mifuko ya Plastiki limeanza Juni mosi, 2019 ambapo mpaka sasa kwa tafiti imeonyesha mafanikio, mfano katika Jiji la Dar-es-salaam wengi waliohojiwa mitaa ya Kariakoo wamesema mitaa yao inaonekana safi kwa kuondolewa mifuko hiyo na hivyo wanaishukulu serikali.      

Shirika la Reli Tanzania TRC kufunga Njia za Reli kwa saa 72 ili kukarabati Reli ya Kati

0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO
Shirika la Reli Tanzania TRC limeanza kukarabati njia ya Reli ya kati ya kutoka Dar Es Salaam mpaka Isaka iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga takribani kilomita 970 ili kuimarisha reli hiyo yenye kiwango cha Mitagauge zoezi ambalo lilianza Juni mwaka huu na kutarajia kukamilika mwaka 2020.

Katika Utakabati huo Shirika hilo linatarajia kufunga njia za reli hiyo kwa saa 72 kwa wiki ikiwa ni sawa na siku tatu kwa Wiki kwa muda wa miezi mitano kuanzia Julai hadi Novemba 2019, zoezi zoezi ambalo  kukamilika kwake kutaingiza faida mara dufu ya usafiri huo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Masanja Kadogosa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam na kubainisha kuwa kukamilika kwa Reli hiyo kutaongeza mapato ya usafirishaji wa Reli kwa asilimia mia moja.

“Waandishi wa Habari na Watanzania kwa ujumla, TRC sasa tunakuja kuimarisha miundombinu yenu ya Reli, tunafanya hivi kwa kuwa tunafahamu mnahitaji huduma hizi, tunaomba mtuvumilie kwa siku ambazo tutafunga njia hizi”alisema Kadogosa.

Alisema kwa treni za kawaida za mjini (Cummuter Train) za kutoka Kamata kwenda Ubungo na Pugu zitafanya kazi siku za jumatatu hadi Ijumaa huku Treni za kawaida (Ordinary Train) za kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma, Mwanza na Mpanda zitafanya kazi siku za Jumatatu na Jumatano saa tisa alasiri tu na treni za Deluxe ya kutoka Dar kwenda Kigoma zitakuwepo siku ya Jumanne pekee.

Alibainisha kuwa ukarabati mwingine wa njia ya Reli kutoka Tanga kwenda  Arusha ulianza mapema mwaka huu ambapo njia hiyo itaanza kutumika mwezi Desemba mwaka huu.

“Ndugu zangu wa mikoa ya Kaskazini mtaanza kunufaika na usafiri wa treni ya Abiria kuanzia Desemba mwaka huu, yaani Sikukuu zaKrismas na Mwaka mpya mtaenda nyumbani na Treni ya Abiria ya TRCälisema Kadogosa.

Akizungumzia ujenzi wa Reli ya Standard Gauge inayoendelea kujengwa Nchini Kadogosa alisema kwa awamu ya kwanza kutoka Dar Es Salaam kwenda Morogoro ujenzi huo umefikia asilimia 56.
 

TARURA Kuanza Kutumia Mfumo Mpya Wa Malipo Serikalini

0
0
Na. Geofrey Kazaula, TARURA, Morogoro
Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) umeanzishwa na wataalamu wa ndani ili kuunganisha mifumo mingine iliyopo, lengo likiwa ni kupunguza gharama na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za fedha.

Hayo yameelezwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Francis Mwakapalila, ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini- MUSE kwa wahasibu na wahandisi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini- TARURA mkoani Morogoro.

Bwana Mwakapalila alisema kuwa mfumo huo umetengenezwa na wataalam wa ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na utaanza kutumiwa na TARURA kisha kutumiwa na Taasisi zote za Serikali pamoja na Wizara baada ya kujiridhisha na ufanisi wake.

 “Nitoe wito kwa washiriki wote wa mafunzo haya kuhakikisha wanauelewa vizuri mfumo na kuwa tayari kuutumia mara tu baada ya mafunzo kukamilika kwa kuwa mfumo huu ni muhimu kutoka na mabadiliko ya teknolojia katika mifumo ya fedha duniani”, alisema Bw. Mwakapalila .

Naye Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff, amewataka wataalam wa Wakala huo wanaoshiriki mafunzo, kutokuwa na mtazamo hasi kuhusu mfumo na badala yake changamoto watakazo kutana nazo waziwasilishe mahali husika ili kuweza kutafutiwa ufumbuzi kwa kuwa mfumo huo ndio suluhisho la matumizi bora ya fedha za Serikali.

Aidha ameeleza kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imetoa wataalam wa kutosha ili kuhakikisha wahasibu wote wa TARURA wanapatiwa mafunzo na kuuelewa mfumo kwa kina.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, alieleza kuwa mfumo huo utaiwezesha Serikali kuangalia malipo yanayofanyika Katika Taasisi, Kampuni na wadau wengine wanaotoa huduma Serikalini .

Alisema kuwa mfumo huo ulianza baada ya kukusanya mahitaji kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi Ishirini za Serikali na kwamba Taasisi ya TARURA itakuwa ya kwanza kutumia mfumo huo kupitia wahasibu wake na wahandisi watakao kuwa wakiidhinisha malipo.

Bwana Sausi, alisema mafunzo hayo yanawahusisha wahasibu na wahandisi wa TARURA nchi nzima kuanzia ngazi ya Halmashauri lengo likiwa ni kumwezesha Mtendaji Mkuu wa TARURA kuona malipo yote yanayofanyika na Wakala huo katika sehemu mbalimbali kwa wakati.

Wizara ya Fedha na Mipango imekuwa ikitumia Mifumo ya Fedha tangu miaka ya Sitini na kutokana na ukuaji wa teknolojia imeamua kufanya maboresho ya mifumo hiyo ili kuendana na mahitaji ya sasa na kurahisisha kupata hesabu sahihi za fedha kwa wakati.

Mwisho

Tanzania Kuendelea Kunufaika Kiuchumi na SADC

0
0
Na Frank  Mvungi- MAELEZO- Morogoro
Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Mussa Uledi amesema kuwa Tanzania inanufaika kiuchumi  kama mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na jumuiya nyingine ambazo Tanzania ni mwanachama.
 
Akizungumza wakati akiwasilisha mada leo mjini Morogoro ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo  kwa waandishi  wa habari ya kuwajengea uwezo wa kuandika na  kuripoti   habari za SADC, Bw. Uledi amesema kuwa  nchi yetu imenufaika na utekelezaji wa miradi ya miundomnbinu,  biashara, uwekezaji  na viwanda.
 
“ Mkakati wa maendeleo wa SADC unafafanana kwa kiwango kikubwa na ule wa Tanzania ambao pia unazingatia haja ya utekelezaji wa viwanda na miundombinu hapa nchini hali itakayochangia katika kuimarisha maendeleo na kukuza uchuni na ustawi wa wananchi” Alisisitiza Bw. Uledi
 
Akifafanua amesema kuwa vipaumbele vya Tanzania vimejikita katika upanuzi wa Mauzo nje na uongezaji wa michepuo yake lengo likiwa ni kukuza na kuendeleza biashara hali inayowezesha uendelezaji wa viwanda vya kuongeza thamani katika malighafi za ndani hususan mazao ya kilimo na madini.
 
Aliongeza kuwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli  katika baadhi ya nchi wanachama wa SADC imeonesha kuwa Tanzania imejipanga vizuri kimkakati inaweza kuwa ghala la Chakula kwa kukuza zaidi uzalishaji kuendana na mahitaji katika soko la jumuiya hiyo na hata nje ya jumuiya.
 
 Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na  uendelezaji miundombinu kama barabara, reli, usafiri wa anga, uzalishaji na usambazaji huduma za umeme ambayo ni nyenzo muhimu sana katika kuyaunganisha masoko ya nchi wanachama wa SADC.
 
Aliongeza kuwa vipaumbele vingine ni utafutaji wa rasilimali na utekelezaji wa miradi ya Kikanda kwa kuundwa kwa kikosi kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya Fedha na uendelezaji miundombinu, Amani na Usalama umeendelea kuimarika ndani ya SADC.
 
Tanzania inatarajiwa kuleta msukumo mpya kwa nchi wanachama wa SADC katika utekelezaji wa miradi na program za maendeleo za Jumuiya hiyo kwa kuwa itakuwa na dhamana kubwa ya kukidhi matarajio makubwa ya nchi wanachama wakati wote wa uenyekiti wake.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Brigedi ya Magharibi ya Jeshi  la Ulinzi la  Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  Kanali Wilbert  Ibuge akiwasilisha mada katika mafunzo hayo amesema kuwa  Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa Barani Afrika zilizotoa mchango mkubwa na kuratibu kuanzishwa kwa mtangamano wa  SADC.
 
“Hadi sasa hali ya amani na usalama imeendelea kuimarika katika SADC kama inavyojidhihirisha kwa takribani nchi zote za SADC  ambapo nchi wanachama ziliazimia kusimamia maendeleo ya kiuchumi ya Kanda kwa kuzingatia malengo ikiwemo kukuza uchumi, kuondoa umasikini, kuboresha hali ya maisha ya wananchi.
 
Msingi wa SADC ni kusimamia malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii sambamba na yale ya ulinzi na usalama unabainishwa katika Ibara ya 2 ya mkataba wa SADC ( Article 2 of SADC Treaty).

Taasisi Za Kidini Na Jumuiza Kijamii Katika Mikoa Ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa Na Songwe Kuhakikiwa Kuanzia Tarehe 15 Julai, 2019

Waziri Lugola aagiza Polisi kuwakamata wanaowapa mimba Wanafunzi

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amelitaka Jeshi la Polisi  wilayani Bunda, mkoani Mara, kuwakamata wazazi wanaowatumia wanafunzi katika shughuli za kilimo na mifugo na kuwasababishia kukatisha masomo yao.

Pia Waziri Lugola amewaagiza Polisi hao kuwakamata watu wanaowarubuni wanafunzi wa kike na kuwasababishia kukatisha masomo kwa kuwapa mimba.

Waziri Lugola, ametoa kauli hiyo akiwa wilayani Bunda katika  ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ndani ya jimbo lake la Mwibara, ambapo amesema kuwa lazima Watoto waendelezwe kielimu ili iwaletee manufaa kwao na kwa taifa.

“Nina taarifa baadhi ya wazazi uwatumikisha Watoto wao kufanya shughuli za kilimo, kulima dengu, pamoja na kuwatumia katika kuchunga mifugo, hii haikubaliki, wazazi lazima muwajibike kwa kutowatendea vema watoto,” alisema Lugola na kufafanua;

“Kuvunja sheria za nchi kwa kutompa elimu mtoto ni kosa, hivyo, wazazi wanaotumikisha Watoto shughuli za uchumi wa wazazi hao,hakika tutawakamata, OCD (Kamanda wa Polisi Wilaya), akikisheni mnawakamata wazazi ambao wanawatumia Watoto katika shughuli zao binafsi na pia kusababisha utoro katika shule zetu.”

Pia Lugola aliwahoji wanafunzi wa Shule ya Msingi Karukekere, Kata ya Namuhura, Wilayani humo, kuwa wanataka Serikali iwafanyie nini wazazi wao ambao wanawakatisha masomo, hata hivyo,wanafunzi hao walisema wazazi wao washitakiwa kwa kutowapa haki zao za msingi.

Alisema ili kupunguza utoro ndani ya Jimbo hilo, aliwataka wazazi kufuatilia elimu ya watoto wao, kwa kuhakikishe wanakua na daftari ambalo wanafunzi hao wataenda nalo shuleni, na Mwalimu atasaini baada ya mwanafunzi huo kufika shuleni na pia atasaini kabla ya muda wa kuruhusiwa kwenda nyumbani, hatua hiyo itapunguza zaidi utoro katika jimbo lake.

Iran Yasema Italipa Kisasi kwa Uingereza

0
0
Mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Iran Meja Jenerali Mohammad Bagheri amesema leo kwamba, hatua ya Uingereza kuikamata meli yake ya mafuta nje ya eneo la Gibraltar haitapita bila majibu. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim Bagheri amesema kukamatwa kwa meli hiyo ya mafuta ya Iran chini ya misingi ya visingizio vya kutengenezwa, hakuta pita bila kujibiwa na itakapolazimika Tehran itatoa jibu sahihi. 

Jeshi la majini la Uingereza liliingia katika meli hiyo, Grace 1, nje ya pwani ya Gibraltar siku ya Alhamis na kuikamata kuhusiana na shutuma kwamba inavunja vikwazo kwa kupeleka mafuta nchini Syria. 

Iran imetaka kuachiwa mara moja kwa meli hiyo ya mafuta, wakati kamanda huyo wa jeshi la mapinduzi la Iran ametishia siku ya Ijumaa kukamata meli za Uingereza kwa kulipa kisasi.

Rais Magufuli .Ampongeza Faru Rajabu

0
0
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amempongeza faru Rajabu, ambaye ni mtoto wa Faru John, kwa juhudi zake za uzalishaji na kuzidi kuongeza idadi ya faru hadi kufikia faru140, katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Rais Magufuli ameyabainisha hayo leo Julai 9, wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi, iliyopatikana mara baada ya mapori matatu ya akiba kuunganishwa, likiwemo pori la Burigi, Biharamulo na Kimisi Wilayani Chato Mkoani Geita.



"Mwaka 2014 kulikuwa kuna tembo 43,330 lakini hivi sasa baada ya kuanzisha kikosi cha kupambana na ujangili wamefikia zaidi ya 60,000 faru hawakuwepo kabisa ila sasa wamefikia 163 ", amesema Magufuli.
 
''Hakuna budi kupongeza kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na faru rajabu, mtoto wa faru John naambiwa kwasasa amezalisha watoto 40, nadhani wajina wangu john alikuwa hajitumi vizuri'

Mwakyembe Atoa Onyo Kwa Wanaosambaza Picha za Ajali Mitandaoni

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewaonya watu wanaopiga picha kwa simu mara tu zinapotokea ajali na kusambaza mitandaoni.

Mwakyembe ametoa onyo hilo leo Jumanne Julai 9, wakati wa shughuli ya kuaga miili ya wafanyakazi wa Azam Media waliofariki jana Julai 8, katika ajali ya gari kati ya Shelui na Igunga na kuongeza kuwa Sheria ya Makosa ya Mitandao inazuia kufanya hivyo.

"Niwaombe Watanzania tuendeleze utamaduni wa utu ndugu zetu wanapopata ajali, niwaombeni acheni tabia ya kupiga picha na kurusha kwenye mitandao, sheria ya mitandao inakataza, hatutazungumza tena hili ni onyo la mwisho" - Waziri Mwakyembe

Rais Magufuli Aitaka Wizara ya Maliasili Iweke a mikakati kuongeza watalii

0
0
Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza watalii nchini ambao ametaja baadhi ya malalamiko ambayo amekuwa akiyapata kupitia ripoti ya robo mwaka na kiitaka wizara hiyo kuhakikisha inafanya kazi masuala hayo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 9, wilayani Chato mkoani Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi – Chato yenye ukubwa wa kilometa za mraba 4,702.

“Ninatoa wito kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kujipanga na kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza watalii nchini, miongozi mwa malalamiko ambayo nimekuwa nikiyapata ni pamoja na gharama za utalii kuwa juu, usafi kwenye hoteli na mengine mengi hivyo hamna budi kufuatilia mambo hayo,” amesema.

“Ninawasihi kuwa na utaratibu wa kufanya kaguzi mara kwa mara lakini pia wekeni mikakati ya kujenga uwezo wa waongoza watalii na kuhakikisha wote wanatambuliwa rasmi maana kuna wengine wanadanganya watalii, hakikisheni hifadhi zetu zinakuwa na mchanganyiko mzuri wa vivutio,” amesema.

Aidha amewataka watanzania kujega utamaduni wa kutembelea vivutio vya ndani hasa katika maeneo ya hifadhi zinazowazunguka ili kuiongezea nchi kipato na kukuza uchumi wa nchi ambapo ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuweka gharama nafuu kwa watalii wa ndani ili kuwezesha zoezi hilo.

“Ninahimiza Wizara kuendelea kuhamasisha utalii wa ndani ikiwemo kwa kuweka gharama za nafuu pia kwa watanzania ninawasihi kujenga utamaduni wa kutembelea vituo vyetu vya utalii pia tuanzisha hifadhi ndogo ndogo za kufuga wanyama pori,” amesema.

“Mimi ninafikiria kuanzisha hifadhi ndogo lakini nitafuga wale wanyama ambao ni wapole nisije nikajikuta nimekuwa kitoweo huko ndani, ninasisitiza Wizara hakikisheni mnaangalia gharama kwa wazawa zinakuwa chache,” amesema.

Serikali kujenga uwanja mkubwa wa mpira Chato

0
0
Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. 

Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images