Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Abiria saba wanusurika kifo kwa ajali ya basi kahama

0
0
NA SALVATORY NTANDU
Abiria saba Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamenusurika kifo baada lori la mizigo aina ya Fuso lenye T 322 ACC walilokuwa wakisafiria kugongana na basi  aina ya Scania lenye namba za usajili T 245 AJS Kwela Classic Mali ya Laurent Ncheye mkazi wa Kahama linalofanya safari za kahama kwenda mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanya Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa  ajali hiyo  na kusema kuwa  ajali hiyo leo asubuhi baada ya dereva wa basi hilo kuligonga lori hilo lilokuwa limebeba magunia 100 ya mahindi katika eneo hilo na kusababisha lori hilo kupinduka na kusababisha majeruhi wa ajali hiyo.

Amesema majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama na hali zao zinaendelea vizuri  na kuwataka madereva wote wilayani humu kuheshimu alama za barabarani husasni wanapotaka kuingia katika makutano ya barabara ili kuzuia ajali zinazoweza kuzuilika.

Kamanda Abwao amesema chanzo cha ajali hiyo ni Uzembe wa Dereva  wa basi hilo kutochukua tahadhari pindi anapongia katika makutano ya barabara kwa kuingia katika barabara hiyo kwa mwendo kasi na kusababisha ajali hiyo ambayo imeharibu miundo mbinu ya barabara na nyumba za watu zilizopo karibu na eneo hilo.

Amefafanua kuwa dereva wa basi hilo amejisalimisha katika kituo cha polisi kahama  na baada ya kuhojiwa   atafikishwa Mahakamani  kujibu tuhuma zinayomkabili.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama DK, George Masasi amesema amepokea majeruhi hao Saba na hali zao zinaendelea vizuri ambao ni pamoja na dereva wa lori hilo ambao wameumia katika sehemu mbalimbali za miili yao.

Mmoja wa shuhuda wa Tukio hilo   Amosi Joseph amesema ajali hiyo  imetokea leo majira ya saa 11 alfajiri baada ya dereva wa basi kupita katika eneo hilo kwa mwendo kasi kwa lengo la kuwahi abiria katika kituo kikuu cha mabasi kahama kwaajili ya kuanza safari na kusababisha abiria waliokuwepo katika lori hilo kujeruhiwa.

Mbali na Kamanda Abwao amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuchukua hatua kali kwa madereva wote wazembe ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani .

Mbunge Jaguar wa Kenya Aliyetishia Kuwatimua Watanzania Ndani ya Masaa 24 Akamatwa Mchana Huu

0
0
Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda waliopo jijini Nairobi.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo vinaripoti kuwa Charles Kanyi maarufu kama Jaguar amekamatwa mchana huu akiwa anatoka kwenye viwanja vya bunge.

Jana, June 25 Serikali ya Kenya ilitoa taarifa ya kuwahakikishia wafanyabiashara wa kigeni nchini humo usalama wakati wote huku ikisema Serikali haipo upande wa Mbunge wa Starehe, Charles Njagua maarufu Jaguar kuhusu kauli alizozitoa.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki kupitia mitandao ya kijamii jana Jumanne ilisambaa video yake akieleza kuwafukuza wafanyabiashara wa kigeni wakiwemo Watanzania ndani ya masaa 24 kurudi kwao la sivyo watawapiga na kuwarudisha nchini mwao..


Rosa Ree Atoa Wimbo Mpya Akimshirikisha Ruby -Champion

0
0
Rosa Ree Atoa Wimbo Mpya Akimshirikisha Ruby -Champion

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi June 27

Waziri Mhagama Apokea Msaada Wa Vifaa Saidizi Na Cherehani Kutoka Ubalozi Wa China

0
0
NA; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amepokea cherehani na vifaa siadizi kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ndogo za ubalozi huo zilizopo Jijini Dodoma, Waziri Mhagama alieleza kuwa Serikali inatambua haki za Watu wenye Ulemavu nchini hivyo imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao stahiki ikiwemo kuwapatia vifaa saidizi.

“Vifaa saidizi ni muhimu kwa kundi hilo maalumu kwa kuwa vinawawezesha kumudu mazingira yanayowazunguka na kuwasaidia kufanya shughuli zao za kila siku bila kukabiliana na changamoto,” alisema Mhe. Mhagama

Alieleza kuwa kutokana na vifaa hivyo kuwa ni ghali na upatikanaji wake umekuwa mgumu na kupelekea watu wenye ulemavu kushindwa kuvinunua, Serikali imeendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kununua vifaa hivyo.

Aliongeza kuwa, katika ujenzi wa uchumi wa viwanda Serikali kupitia Shirika la kuhudumia viwanda Vidogovidogo (SIDO) kushirikiana na wadau imejipanga kuimarisha utengeneza wa baadhi ya vifaa hivyo, vitakavyokuwa vinapatikana hapa nchini.

Aidha alitoa wito kwa jamii kubadili mtazamo na fikra potofu juu ya watu wenye ulemavu, bali watambue kundi hilo linaweza na linamchango mkubwa katika jamii na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tanzania, Bi. Wang Ke alisema kuwa Serikali ya China itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania katika nyanja mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya wenye uhitaji.

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa aliwataka wadau ndani na nje ya nchi kuendelea kujitokeza na kusaidia makundi yenye uhitaji maalumu, kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusaidia masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Katika hafla hiyo pia aliudhuria Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Toufiq na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza Mhe. Kemilembe Lwota.

Wazee Shinyanga waomba kupewa kipaumbele katika huduma za afya

0
0
SALVATORY NTANDU
Serikali Mkoani Shinyanga imewataka wakurugenzi wa Halmashauri sita za mkoa huo kuhakikisha wanaweka Madirisha maalumu ya kutolea huduma za afya kwa wazee katika Zahabati, Vituo vya afya na Hospitali za Wilaya  ili kuondoa malalamiko yanayotolewa  juu ya upatikanaji wa tiba.

Uamuzi huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Tellack katika mkutano wa hadhara na wananchi uliokuwa na lengo la kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi uliofanyika katika kata ya majengo mjini Kahama baada ya kupokea malalamiko ya wazee juu ya kukosa huduma za afya.

Amesema Wazee kupatiwa huduma za afya bure ni hitaji la  kisheria kwa wenye umri kuanzia miaka 60 ,hivyo wanapaswa kuhakikisha kila mzee mwenye umri huo anakuwa na kitambulisho maalumu kitakachomuwezesha kuapatiwa matibabu bure bula kusumbuliwa na wahudumu wa afya.

Amefafanua kuwa ni lazima wahakikishe wanapatiwa matibabu pamoja na dawa, pamoja na kuwepo kwa  wahuduma maalumu ambao watakuwa wakiwasiliza matatizo yao ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwao na kutowachanganya na makundi mengine ya wagonjwa.

Mbali na hilo Tellack amesema, serikali imetoa shilingi Bilioni 4.4 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 11 katika Halmashauri sita zilizopo katika mkoa wa Shinyanga  ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi na kupambana na vifo vya akinamama wajawazito na watoto.

Amesema jukumu la kupambana na vifo vya akinamama wajawazito na watoto ni jukumu la kila mmoja  hivyo ni budi  wanaume wakawahimiza wake zao kujifungulia katika zahanati na vituo vya ili kuzuia vifo visivyo vya lazima.

Amefafanua kuwa upatikanaji wa dawa katika Hospitali, zahanati na vituo vya afya katika Mkoa wa shinyanga zinapatikana kwa asilimia 95 nakudai kuwa dawa ambazo utazikosa katika zahanati zitapatikana katika vituo vya afya au Hospitali za Wilaya.

Madini ya Mamilioni ya Pesa Yakamatwa Yakitoroshwa Kuelekea Kenya

0
0
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekamata madini aina mbalimbali ambayo  yalikuwa yakitoroshwa kuelekea nchi jirani ya Kenya.


Madini hayo zaidi ya kilo 36 yamekamatwa jana Jumatano Juni 26, 2019 na askari maalum ya intelijensia baada ya kupata taarifa madini hayo kutoroshwa kutoka Arusha katika basi la Perfect trans ambalo hufanya safari kutoka Arusha hadi Nairobi nchini Kenya.

Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema madini hayo ikiwepo Tanzanite kilo tano, Ruby na Greentonaline  yalikuwa yanasafirishwa kwenye mfuko mkubwa yakiwa yamechanganywa na mchele.

Amesema dereva wa gari hilo na kondakta wake wanashikiliwa kwa mahojiano wakidai hawamjui mmiliki wa madini hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank James Mwaisumbe akishuhudia madini zaidi ya kg 36 zikiwemo 24 za Tanzanite yenye thamani ya mabilioni yaliyokamatwa hapo jana mpakani Namanga yakivushwa kwenda Kenya na dereva na kondakta wa basi la abiria la Perfect.

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Afikishwa Mahakamani Kwa Kuomba Rushwa

0
0
Askari  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT 77341 Johanes Kubambi, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kwa shtaka la kuomba rushwa ya Sh 700,000.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa, Wakili wa Takukuru, Vera Ndeoya, alidai kuwa katika ofisi za jeshi la akiba, Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa aliomba rushwa kwa Kelvin Fabian ili aweze kumpatia nafasi ya mafunzo ya jeshi.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Ndeoya alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo aliiomba mahakama kutaja tarehe nyingine.

Hata hivyo, Hakimu Kiliwa alisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao sio wanajeshi wala polisi na wawe na barua zinazotambulika kisheria, watakaotoa bondi ya Sh milioni 1 kila mmoja.

Mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Juni 28 kwa ajilii ya kutimiza masharti ya dhamana.

Daktari Feki Akamatwa Nyumbani Akitibu Watu

0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja Abdallah Bushiri Shija (42), mkazi wa Igodima Jijini Mbeya  kwa tuhuma za kufanya kazi za utabibu bila kuwa na taaluma ya utabibu hususani kwa magonjwa ya wanawake wenye matatizo ya uzazi.

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa hakuwa na kibali chochote cha kufanya shughuli hiyo wala cheti chenye taaluma hiyo na alikiri kuwatapeli wahanga hao pesa Tsh. 2,472,000 kwa madai kuwa atawasaidia.

Akizungumza na wandishi wa Habari jijini Mbeya , Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei amesema  mtuhumiwa alikamatwa Juni 24 mwaka huu nyumbani kwake.

Kamanda Matei amebainisha kuwa baada ya kupekuliwa nyumbani kwake, Daktari huyo feki alikutwa na vifaa tiba pamoja na dawa mbalimbali ambazo zinamilikiwa na Serikali zikiwa na nembo ya Bohari ya Dawa (MSD) pamoja a nembo inayoonyesha kuwa ni mali ya Serikali.

"Baada ya kumhoji tulibaini kuwa hana taaluma yoyote ya udaktari, lakini pia yuko na baadhi ya vifaa na dawa ambazo baadhi ni za Serikali, zina nembo ya MSD na GOT, lakini pia baadhi ya wananchi walikuja kulalamika kuwa mtu huyo alishachukua fedha zao zaidi ya 2,000,000," alisema Kamanda Matei.

Amesema  baadhi ya vitu alivyokutwa navyo mtuhumiwa huyo kuwa ni pamoja daftari 119 zenye taarifa za wagonjwa aliowahi kuwatibu, vipimo vya kupimia mkojo 15, dawa za kusafishia vidonda  kipimo cha Malaria ambacho kinapatikana MSD pamoja na vifaa vingine.
 

Matei amesema kuwa baada ya taratibu kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria huku akiwataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya kuendelea kutoa taarifa za uharifu na waharifu.

Zitto Kabwe Aipongeza Serikali...Chama Chake Chamkana, Chasema Siyo Yeye

0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa licha ya yeye kuwa mpinzani lakini ataendelea kuipongeza Serikali ya Rais Magufuli.

Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “ACT Wazalendo kimekuwa chama kinachohubiri Ujamaa lakini kwa kuingia huku kwa Maalim Seif ambaye kwenye chama chake cha CUF walikuwa wakitumia mfumo wa Kibepari inabidi tuhamie huko sasa kama tulivyokubaliana na kutakuwa na mabadiliko ya Kiuongozi.“.

“Ni kweli tumekuwa tukiikosoa Serikali kwa muda mrefu lakini lazima nikiri kuwa kuna mabadiliko makubwa sana yamefanywa na Serikali hii ya JPM. Japokuwa najua kuna baadhi ya viongozi aliowateua wanamuangusha kiuhalisia MAGUFULI amefanya mengi.” ameandika Zitto Kabwe na kusisitiza.

“Wapo ambao najua wataniita majina mengi ya ajabu kwa maamuzi yangu haya kama jinsi ambavyo wamekuwa wakimshambulia ndugu yangu @Nnauye_Nape kwa kutokuwa na misimamo thabiti lakini nataka niwaambie huo ndio msimamo wangu na sitaki kuyumbishwa kwani hata Wanakigoma wamefaidika.” amemaliza Zitto Kabwe.

Hata hivyo, Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa Tweets hizo sio za Zitto Kabwe kwani simu na laptop yake vipo mikononi mwa jeshi la polisi.

Baadhi ya Wabunge Kenya wamuunga mkono Jaguar....Wataka aachiwe huru

0
0
Matamshi ya mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles 'Jaguar' Kanyi kuhusu kuwatishia raia wa kigeni wakiwemo watanzania  wanaofanya kazi nchini Kenya yaliwasilishwa jana  mbele ya kikao cha bunge ili kujadiliwa.

Baadhi ya wabunge nchini humo  wakichangia mjadala huo wameunga mkono kauli ya Jaguar huku wakitaka aachiwe huru kwani alichosema ndio mtazamo wa Wakenya waliowengi.

Akichangia maoni bungeni jana Juni 26, 2019, Mbunge wa Garissa mjini, Aden Duale amesema Jaguar alifanya jambo la kizalendo kwani Taifa hilo linahitaji kuwalinda wananchi wao kwenye masuala ya kibiashara.

Mbunge mwingine ni Moses Kuria wa jimbo la Gatundu Kusini, Amesema kuwa kauli ya Jaguar sio ngeni kwani viongozi wengi wa nchi hiyo walishawahi kuongea kuhusu wageni kupora fursa za kibiashara nchini humo.

Jana Mbunge wa jimbo la Starehe, Jaguar alishikwa na maafisa polisi katika viunga vya bunge la nchi hiyo na mpaka sasa bado hajaachiwa.

==>.Wasikilize hapo chini

Watumishi MWAUWASA Wapewa Somo

0
0
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) wametakiwa kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao na kufanya kazi kwa uadilifu.

Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga alitoa wito huo hivi karibuni wakati wa mkutano na wafanyakazi wote uliofanyikia kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka kwenye jengo la Maji House ikiwa ni utaratibu aliyojiwekea wa kuzungumza na watumishi wote kila mwezi.

Mhandisi Sanga alisema ili kupata matokeo chanya, watumishi wote hawana budi kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na wanakuwa kitu kimoja na kwamba yampasa kila mtumishi kutambua na kuheshimu nafasi ya mwenzake kwenye utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

“Hakuna mtumishi aliyebora kumzidi mwenzake, sote tunahitajiana ili kutimiza majukumu yetu na ndiyo maana kukawa na mgawanyo wa majukumu. Yatupasa tufanye kazi kwa pamoja kwa kuzingatia umuhimu wa kila mmoja wetu,” alisema Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga aliwakumbusha watumishi hao jukumu lao kuu ambalo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji na aliwataka kuhakikisha wanatekeleza jukumu hilo kwa ufanisi na ubunifu mkubwa ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Alibainisha kwamba endapo kila mtumishi atatimiza majukumu yake kama inavyostahili, huduma itaboreka zaidi na maeneo mengi yatafikiwa hasa ikizingatiwa kwamba Jiji la Mwanza linakuwa kwa kasi.

“Tunapaswa kwenda na kasi ya ukuaji wa Jiji letu, hatupaswi kuachwa nyuma; kadri Jiji linavyozidi kutanuka nasi hatuna budi kutanua huduma zetu na busara zaidi ni kufika mbali zaidi kwa maana yakufika kwenye maeneo ambayo bado Jiji halijafika,” alisema Mhandisi Sanga.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Edith Mudogo aliwaasa watumishi wote kuwa wazalendo na aliwataka watumie nafasi walizonazo kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kama inavyostahili.

Alisema MWAUWASA inawatumishi wa kada mbalimbali na kwamba yampasa kila mtumishi kwa kada yake afikirie namna bora ya kuhakikisha huduma ya maji inaimarika na kuwafikia wananchi wengi zaidi hususan wale wa maeneo ya pembezoni.

“Hapa tuna watumishi wa kada mbalimbali, sasa itapendeza kila mtumishi kwa kada yake atazame ni vipi anaweza kuwa na mchango wa kusambaza huduma hii ya maji kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni,” alisema Mudogo.

Aliwahakikishia ushirikiano kutoka kwa Bodi ya Wakurugenzi hasa ikizingatiwa kwamba dhamira ya Bodi ni kuona wananchi wengi zaidi wanapata huduma ya maji bila kujali maeneo waliyopo.

“Sisi kama wajumbe wa Bodi matamanio yetu ni kuona wananchi wote wa Jiji la Mwanza wanapata huduma ya maji kutoka MWAUWASA; hatupo tayari kuona mnashindwa kutimiza majukumu yenu, tupo nanyi, tufanye kazi,” alisisitiza.

Aidha, mkutano huo ulitumika kutambua jitihada za watumishi waliofanya kazi MWAUWASA kwa miaka 15 ambapo watumishi sita walikabidhiwa tuzo za utumishi wa muda mrefu ikiwa ni ishara ya kutambua jitihada zao za muda mrefu katika kuwahudumia wananchi.

Tuzo hizo za utumishi wa muda mrefu hutolewa kila mwaka ambapo mtumishi anayetimiza miaka 15 hukabidhiwa ikiwa ni ishara ya kutambua utumishi wake kwa muda wote huo. 

Fahamu Chanzo Halisi cha Kupungukiwa Nguvu za Kiume

0
0
Unafahamu kwa kina tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na  maumbile ya kiume kusinyaa?

Wanaume wengi kwa sasa wanasumbuliwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile  kuwa mafupi na wengi wao huamua kutafuta tiba ili waweze kujilejeshea nguvu zao za asili bila kujua ni nini chazo cha hilo tatizo 

Tambua kuwa hakuna dawa ya kuongeza maumbile ya kiume  kama  ulikuwa mdogo  tangu unazaliwa, labda kama tatizo limeazia ukubwani kwa kujichua ( kupiga punyeto)  au kutokana na magonjwa 

Pia hakuna dawa ya kuongeza nguvu za kiume kama tatizo umezaliwa nalo bali zipo tiba za kutibu na ukapona matatizo hayo kama yameanzia  ukubwani kutokana na sababu zifatazo ;
1,Unene kupita kiasi 
2.Kuvaa nguo za kubana 
3.Magonjwa ya moyo,kisukar,presha,vidonda vya tumbo,ngiri,tumbo kuunguruma na kujaa gesi,kupiga punyeto,Msongo wa mawazo.

Haya ndo mambo makuu yanayosababisha tatizo hilo. kwa ushauri zaidi , piga simu 0683645920

Mbunge Jaguar wa Kenya aburuzwa mahakamani

0
0
Mbunge wa Starehe, nchini Kenya Charles Njagua maarufu Jaguar na amefikishwa mahakamani leo. Hata hivyo, ametupwa ndani hadi kesho mahakama itakapoamua iwapo ataachiliwa kwa dhamana.

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) yaomba Mbunge huyo azuiliwe kwa siku 14 kwa uchochezi na kutoa vitisho dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni.

Hapo jana Mbunge huyo alikamtwa nje ya majengo ya Bunge kufuatia kauli zake za ‘kibaguzi' akiwataka wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wanaoendesha shughuli zao katika masoko mjini Nairobi na miji mingineyo kuondoka nchini humo ndani ya saa 24

 
Mbunge huyo analionekana katika video fupi ambayo ilisambaa katika mitandao ya kijamii akizungumza na wafanyabiashara wa jijini humo na kuwaeleza kuwa hawatokubali watu wa nje waje kufanya biashara nchini mwao.

''Wakenya ni sharti wafanye biashara zao bila kushindana na watu kutoka mataifa mengine. Raia wa Pakistan wametawala biashara za kuuza magari nchini humu, Watanzania na Waganda wanatawala katika masoko yetu. Tunasema imetosha iwapo hawatarajeshwa nyumbani katika saa 24 tutawashika na kuwapiga na hatuogopi mtu yeyote,” alisisitiza mbunge huyo.

Majambazi yatelekeza Silaha aina ya Gobole Kahama baada ya kubaini kufuatiliwa na Jeshi la Polisi.

0
0
NA SALVATORY NTANDU
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linaendelea kuwatafuta Majambazi wawili waliotelekeza silaha aina ya Gobole iliyotengenezwa kienyeji,panga mmoja  pamoja na pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC 359 AZE baada ya kushindwa kutekeleza tukio la uporaji.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard  Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea jana katika mtaa wa shunu  saa tatu na nusu usiku ambapo walilenga kufanya uhalifu katika duka la M pesa  la Neema Byabato mkazi wa shunu wilayani Kahama.

Amesema wakati polisi wakiwa katika doria walipata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo kisha kuanza kuwafuatilia  Majambazi hao walipobaini kuwa wanatafutwa  walianza kukuimbia na katika harakati za kukimbia walidondosha silaha hizo na  kisha kuitelekeza pikipiki hiyo.

Amesema Majambazi hao walikuwa na lengo la kumpora fedha Neema baada ya kufunga duka lake lakini hawakuweza kufanikiwa baada ya njama yao kuharibiwa na jeshi la Polisi na Juhudi za kuwatafuta zinaendelea ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Pikipiki hiyo na silaha hizo zimehifadhiwa katika kituo cha polisi Wilaya ya kahama.

Nape Nnauye Akerwa Jina Lake Kutajwa Kwenye Tweets za Zitto Kabwe...."Hamuwezi kuendelea na maisha msiponitaja!"

0
0
Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye amezungumzia kuhusiana na kutajwa katika ujumbe uliochapishwa kwenye akaunti ya kijamii ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe.

Kupitia ukurasa wa twitter wa Zitto umechapishwa ujumbe unaodai kuwa kiongozi huyo wa ACT- Wazalendo ameunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano na kuwataka viongozi wengine wa upinzani kuipongeza serikali na sio kukosoa kila kitu.

Nape ameandikwa kuwa, "Nimeona tweets zinazodaiwa kuwa za Ndugu Zitto zikinitaja, amekakanusha sio zake. Kilichonishangaza ni uwezo mdogo wa kufikiri wa wadukuaji! Mnanyimwa usingizi na nini?? Hamuwezi kuendelea na maisha msiponitaja!", amemalizia kwa kucheka.

Moja ya ujumbe uliochapishwa ambao Zitto mwenyewe pamoja na chama chake wamekanusha ujumbe huo umesema kuwa, "Wapo ambao najua wataniita majina mengi ya ajabu kwa maamuzi yangu haya kama jinsi ambavyo wamekuwa wakimshambulia ndugu yangu Nape Nnauye kwa kutokuwa na misimamo thabiti lakini nataka niwaambie huo ndio msimamo wangu na sitaki kuyumbishwa kwani hata Wanakigoma wamefaidika".

 
Taarifa ya chama cha ACT-Wazalendo iliyotolewa na Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi imesema kuwa taarifa zinazowekwa hivi  sasa kwenye akaunti ya Twitter ya  Kiongozi wa Chama hicho Ndugu Zitto Kabwe si zake kwani simu na laptop yake vipo mikononi mwa Jeshi la Polisi.

Bashe Ageuka Mbogo Baada ya Kutajwa kwenye Tweets za Zitto Kabwe....."

0
0
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe ameonesha kutofurahishwa, baada ya yeye, Januari Makamba pamoja na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye, kutajwa kuwa miongoni mwa watu ambao washajiunga na chama cha ACT - Wazalendo na wanasubiri kipindi cha Ubunge kiishe.

Hussein Bashe ameonesha hali hiyo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya mtu anayedaiwa kudukua mawasiliamo ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuchapisha taarifa juu ya Wabunge hao kujiunga na ACT - Wazalendo muda wowote.

Mdukuzi ameandika kuwa "nawakaribisha pia Hussein Bashe na Nape Nnauye ambao tayari wameshachukua kadi za uanachama ACT - Wazalendo na wanachosubiri ni kuvunjwa tu kwa Bunge na bila kumsahau mdogo wangu Januari Makamba,"

Akijibu madai hayo Mbunge wa Nzega Hussein Bashe ameandika kuwa "wanaofahamu siasa za Tanzania na wanaonifahamu vizuri misimamo ama maamuzi yangu ya kisiasa, huwa sifanyi kwa njia za kificho ama za kichimvi, Siku nikiamua kuondoka CCM nitaondoka hadharani ,sitasubiri njia za kificho"

"Hili Genge la kihuni ambalo linaongozwa na wahuni wachache ipo siku nitawataja kwa majina, ila mpango wenu wakutaka kunifanya nione CCM si chama sahihi kwa mimi kuwatumikia wananchi wa Nzega na Tanzania hautafanikiwa,CCM bado nipo sana" amemaliza Bashe.

Wakulima mkoani Mbeya walalamikia mifugo kuingia mashambani

0
0
Na Amiri kilagalila
 Licha ya serikali  kukemea vitendo vya mapigano baina ya wafugaji na wakulima nchini, wakazi wa kijiji cha Ipwani wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwakamata wafugaji wanaoingiza mifugo ya ng’ombe kwenye mashamba ya mpunga wanayovuna hivi sasa, huku wafugaji hao wakituhumiwa kuwapiga na kuwapa ulemavu wa kudumu.

Kijiji cha Ipwani kinachopakana na wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe kinasifika kwa kulima zao la mpunga kwa wingi, hata hivyo hofu imewakumba wakazi wa kijiji hicho kilichopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya kutokana na vitendo vinavyofanywa na wafugaji kabila la wasukuma kuingiza idadi kubwa ya ng’ombe katika mashamba ya wakulima wa mpunga , kitendo ambacho   baadhi ya wakazi waliopigwa na kupata ulemavu wamekilaani kitendo hicho na  kuziomba mamlaka kuingilia kati.

“kuna siku niliondoka na kijana wangu kwenda shambani kupiga mpunga lakini wakatokea wafugaji hawa wa kabila la kisukuma wakawa wanataka kulisha mpunga na hizo ng’ombe zao nilivyojaribu kuwazuia wakaanza kunishambulia na kunivunja mkono”alisema Juliana Mkupala mmoja wa wakazi wa Ipwani

Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Ipwani  wamekiri kutokea mgogoro huo huku tangazo likitolewa na afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipwani kwa wafugaji kuepuka kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima na watatozwa faini ya shilingi laki moja mifugo ikipatikana mashambani

“Hii changamoto ipo,wafugaji wamekuwa wakileta ugomvi lakini kama ofisi ya kijiji huwa hatuna mamlaka ya kuweza kusuluhisha mfano jambo la kupigwa kwa hiyo huwa tunawaandikia barua ya kwenda ngazi za juu,kwenye kituo cha polisi ili washughulikiwe”alisema Yasinta Pugili afisa mtendaji wa kijiji.

Maamuzi Ya Kikao Cha Halmashauri Kuu Ya Taifa NEC Ya CCM Kilichoongozwa Na Mwenyekiti Rais Magufuli Leo

0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi leo Jijini Dar es Salaam chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni mkutano wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Kikao pamoja na mambo mengine kimefanya uchaguzi wa kujaza nafasi moja iliyokuwa wazi ya Mjumbe wa Kamati Kuu na kuteua wanachama wa CCM wanao omba dhamana ya uongozi katika Chama, Jumuia na Serikali.

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) kwa kauli moja kimeazimia kuwapongeza Wanachama wa CCM na Viongozi kwa kazi nzuri ya kufuatilia utekelezaji wa ilani kote nchini Tanzania.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza Serikali za CCM za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) inayo ongozwa na Ndugu Rais John Pombe Joseph Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na Ndugu Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani na unaokwenda na wakati huku tukiwa tumepata mafanikio makubwa ya kuimarisha kiwango cha ukuaji wa uchumi wa asilimia 7.1 na 7.3 mtawalia ambao ni jumuishi.

Kwa kauli moja wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) wamewapongeza viongozi wawakilishi wa wananchi wanaotokana na CCM kwa kuendelea kuwa daraja kati ya wananchi na Serikali ya CCM ambayo wananchi wameichagua. Kikao cha HKT pia kimewapongeza Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa CCM kwa kusimama kidete kujadili mipango na kupitisha bajeti za Serikali zenye mrengo wa kuwainua wananchi kutoka hali duni kwenda hali bora zaidi ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020.

Ikiwa ni sehemu ya kazi zake kikao cha HKT kimejadili na kupitisha kanuni za Chama Cha Mapinduzi katika maeneo ya;-

1.    Kanuni za Utumishi za wafanyakazi wa CCm na Jumuia zake Toleo la 2019
2.    Kanuni za Uteuzi wa Wagombea wa CCM katika vyombo vya Dola, Toleo la 2019
3.    Taratibu za Sehemu ya Wazee, Toleo la 2019
4.    Kanuni ya Jumuia ya Umoja wa Vijana wa CCM, kuhusu Idara na Uteuzi wa Wakuu wa Idara

Kikao cha HKT kimepokea na kuridhia kwa kauli moja pendekezo la Kamati Kuu la kumteua Ndg. Munde Tambwe kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT).

Halmashauri Kuu ya Taifa imewapendekeza ili wakashiriki katika uchaguzi katika ngazi husika wana CCM wanao omba dhamana za uongozi katika Chama na Jumuia kama ifuatavyo;-

Nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mkoa wa Kaskazini Pemba

Ndugu Omar Zubeir MBWANA
Ndugu Elizabeth Andrea MIHALE
Ndugu Abdulrahman Makame SHAKE


Nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mkoa wa Mkoa wa Kusini Unguja

Ndugu Makame Omar MAKAME
Ndugu Othman Ali MAULID
Ndugu Suleiman Ame VUAI (Kibeni)


Nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi, Mkoa wa Arusha

Ndugu Bakari Rahibu MSANGI
Ndugu Gerald Eliaika MUNISI
Ndugu Elipokea Wangael URIO


Nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi, Mkoa wa Arusha

Ndugu Fadhail Rajab MAGANYA
Ndugu Daud Ezron Daud MBISE
Ndugu Novai Megro MOLLEL


Nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Arusha

Ndugu Selemani Qassim MSUYA
Ndugu Lovety PHILLEMON
Ndugu Omary Bahati LUMATO


Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Amani, Mkoa wa Mjini Unguja

Ndugu Juma Khamis HAJI
Ndugu Stumai Mohamed MSIMBE
Ndugu Faida Daud ABDALLA


Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Pangani, Mkoa wa Tanga

Ndugu Abdallah Ally ABDI
Ndugu Pili Ally OMAR
Ndugu Rajab Abrahaman ABDALLAH


Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) kimepokea na kujadili taarifa ya Uhakiki wa Mali za Chama uliofanyika Zanzibar na kuelekeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuchukua hatua stahiki za kinidhamu kwa waliohusika na kupeleka mashauri yao kwa Kamati Ndogo ya Usalama, Maadili na Udhibiti wa Nidhamu kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kuhujumu mali za Chama.

Awali Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (HKT) imefanya uteuzi wa majina ya Wagombea wa nafasi za Umeya katika Manispaa za;-

Mtwara Mikindani, Mtwara
Ndugu Geofrey Isack MWANICHISYE

Ilala, Dar es Salaam
Ndugu Omary S. Kumbilamoto

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na,

HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images