Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali yakiri ‘udhaifu’ vitambulisho vya wajasiriamali....Yaahidi Kuandaa Waraka

0
0
Serikali imekiri ‘udhaifu’ katika utekelezaji wa vitambulisho vya wajasiriamali na  imesema itatoa waraka utakaoelekeza ni nani anatakiwa kutozwa kodi na nani anatakiwa kupata vitambulisho.
 
Hayo yameelezewa leo Jumanne Juni 25, 2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Bariadi (CCM), Andrew Chenge.

Katika swali lake Chenge amesema ni kwa nini Serikali isitoe waraka kueleza kodi zote zilizofutwa na Bunge la Tanzania pamoja na maelekezo ya wanaostahili kupewa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ili kuwe na usawa nchi nzima.

Akijibu swali hilo naibu Waziri wa Tamisemi, Waitara amesema, “Waraka kuhusu kukodi zote zilizofutwa ni jambo ambalo tumelipokea na tutautoa huo waraka na kugawa maeneo mbalimbali.”

“Kuhusu vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo kuanzia Julai 2019 tutatoa maelekezo ya nani anayepaswa kuwa na vitambulisho hivi.”

==>>Tazama hapo chini

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. 

Simu:  +255745495181 au 0682644040  

www.tumainitibaasili.co.tz

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Rais Magufuli: Uzeni Gesi Msiuze Mitungi

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara na wauzaji wa gesi nchini  kuuza bidhaa ya gesi tu na sio mitungi. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ghala la mitambo ya kuchakata gesi iliyoko Dar-es-salaam, Wilayani ya Kigamboni, Rais Magufuli amesema kuwa sekta binafsi ni muhimu katika ukuaji wa uchumi nchini na kuwahakikishia kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana nao. 

“Nimefurahi kuona Taifa Ges mmeanza kukarabati na kutengeneza mitungi yenu wenyewe hii itashusha bei ya mitungi na kuwawezesha wananchi wengi kutumia gesi, tena kwa hii ikiwezekana fanyeni kama makampuni ya soda na bia’’, Alisema Rais Magufuli. 

Akisisitiza jambo hili Rais Magufuli ametoa mfano wa Kampuni za Soda na Bia  ambapo ukinunua soda na bia maana yake hulipii creti ila unalipia soda hii itasaidia kupunguza bei ya gesi na kuwafanya wananchi wengi kutumia nishati hii 

Rais Magufuli amewataka  wananchi kutumia Nishati ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa, uharibifu wa mazingira, kulinda afya na kupunguza gharama ya maisha, kwani gunia mbili za mkaa ni sawa na 120,000, lakini ukitumia gesi gharama yake kwa mitungi miwili ni sawa na 94,000 kwa hiyo wananchi wakitumia gesi wataweza kuokoa shilingi 26,000. 

 “uwekezaji huu mkubwa uliofanywa na Taifa Gas Ltd ni uthibitisho, Serikali yetu inaipenda sekta Binafsi na ipo tayari kushirikiana na ninyi, kwa hiyo Sekta Binafsi endeleeni kujiamini, endelezeni kazi pamoja,  hapa Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji”, Rais Magufuli. 

Rais Magufuli alisema kuwa Tanzania inahitaji wawekezaji muda wote ili kuwekeza katika sekta ya nishati kama vile kuzalisha umeme utokanao na Makaa ya mawe, Maji, Upepo pamoja na Jua ili kuwezesha upatikanajiwa umeme wa kutosha na kwa bei nafuu. 

“Wawekezaji tuwahitaji leo, kesho, kesho kutwa na miaka yote, kwa sababu Tanzania ipo miaka yote, kwa hiyo wawekezaji  na ninyi tunawahitaji kwa sababu tutakusanya kodi na watanzania watapata ajira kama ambavyo Taifa Gas mmefanya”, Alisisitiza Rais Magufuli. 

Rais Magufuli pia aliwataka wananchi kutumia Nishati ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa, uharibifu wa mazingira, kulinda afya na kupunguza gharama ya maisha, kwani gunia mbili za mkaa ni sawa na 120,000, lakini ukitumia gesi gharama yake kwa mitungi miwili ni sawa na 94,000 kwa hiyo wananchi wakitumia gesi wataweza kuokoa shilingi 26,000. 

Naye Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani alisema kuwa biashara ya gesi sasa imeendelea kukua nchini tofauti na hapo zamani ambapo kwa sasa gesi inafika hadi vijijini. 

“Biashara hii ya gesi imekwenda hadi kwenye baadhi ya mikoa, naipongeza na kuishukuru kampuni ya Taifa ya gesi, ambayo kwa afrika ina maghala makubwa na kuhifadhi na kupokea gesi kwa Afrika  Mashariki na Kusini mwa Afrika, kwani wanahifadhi tani 7,650, wakifuatiwa na Afrika ya Kusini tani 5,200 huku Morocco wakihifadhi tani 5,077 kwa hiyo sisi ni namba moja”, Alisema Dkt.Kalemani. 

Aidha Dkt.Kalemani aliongeza kuwa kwa sasa bei ya gesi imeshuka kuliko nchi zote Afrika Mashariki, kwani kilo moja ya gesi inauzwa Shilingi 3,080, kenya 3,500 huku Uganda ikiuzwa kwa 4,001. 

Dkt.Kalemani alisema kuwa Sekta ya gesi imepunguza changamoto ya ajira kwa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 12,000 katika kampuni za gesi zilizowekeza nchini. 

Biashara ya gesi nchini ilianza mwaka 1965, huku kampuni ya gesi ya Tipper ilikuwa mshiriki mkuu wa biashara hiyo, ambapo gesi ilikuwa inatumika viwandani, Mashuleni, katika Taasisi za Serikali na Vyuoni.

Ajali yaua mmoja Njombe, 22 wajeruhiwa

0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Gari la Abiria (Ibbu Trans) lenye namba za usajili T 225 DGF, Mitsubish Rosa linalofanya safari zake kutoka Njombe kuelekea wilayani Ludewa limepata ajali katika eneo la daraja la muholo wilayani Ludewa na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe RPC Salumu Hamduni, amesema kuwa Ajali hiyo ilitokea Jana june 24/2019 majira ya saa Moja jioni, na Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Dereva aliyefahamika kwa jina moja la Chance ambae baada ya ajali alikimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Amesema kuwa uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambae alishindwa kulimiliki gari na kuacha njia kisha kugonga gema na Kusababisha kifo cha mtoto mwenye umri wa miezi minne aliyefahamika kwa jina la Alvin Yohana Mtitu na Abiria 22 wamejeruhiwa.

Siku chache zilizopita Gari la Kampuni hiyo  linalofanya safari  kutoka kijiji cha Luvuyo wilayani Ludewa kuelekea Njombe mjini, lilipata Ajali na kupinduka maeneo ya Uwemba lakini halikusababisha madhara yeyote kwa abiria.

Mganga mkuu wa hospital ya wilaya ya Ludewa, Stanley Mlai amesema kuwa Hospital hiyo imepokea jumla ya majeruhi 22 Wanaume 7 na wanawake 15 ambao kati ya hao watano tayari wameruhusiwa, wawili wamepewa rufaa huku wengine wanaendelea na matibabu katika hospital hiyo.

Kufuatia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ametoa wito kwa Madereva kuacha tabia ya kuendesha magari kwa spidi kali na kuwataka abiria na Jamii ya mkoa wa Njombe, kutoa ushirikiano pindi Madereva hao wanapokiuka sheria za usalama barabarani.

Wadaiwa sugu SIDO mkoani Njombe mali zao kutaifishwa

0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Shirika la kuhudumia viwanda vidogo mkoani Njombe SIDO limesema lipo hatarini kupoteza zaidi ya mil 100 ambazo zilikopeshwa kwa wajasiriamali, wabunifu na wamiliki wa viwanda vidogo ili kuongeza mitaji ya biashara zao kwa kuwa limebaini idadi kubwa ya wakopaji walikuwa wakitoa taarifa za uongo na kugushi nyaraka.

Akizungumzia changamoto hiyo meneja wa SIDO mkoani humo Isdori Kiyenze amesema mwaka uliopita shirika hilo lenye dhamana ya kuwainua kimitaji wajasiriamali na wamiliki wadogo wa viwanda lilitoa mikopo yenye thamani ya mil 250 ambapo katika kiwango hicho mil mia moja na laki nane hazijareshewa hadi sasa huku akidai katika uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kuwa wengi wao hawakuwa waaminifu kwa kuwa wamegushi nyaraka pamoja na dhamana zao,huku wengine wakishindwa kurejesha mikopo yao kwa kutumia pesa nje ya malengo ya mkopo.

Kutokana na hali hiyo inayokwamisha mpango wa serikali wa kuwainua kiuchumi na mitaji ya wajasiriamali na wamiliki wadogo wa viwanda nchini meneja huyo anataJa hatua ambazo shirika kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zimeanza kuchukuliwa dhidi ya wadaiwa sugu na kueleza jinsi hali hiyo inavyowakosesha haki ya kukopeshwa wahitaji wengine waaminifu.

"Tunaenda hatua kwa hatua,na itafikia mpaka kuuza zile dhamana zao na sasa yamekwishabandikwa matangazo, haya mfano hata huduma zingine usipo lipa maji unakatiwa na usipolipia umeme unakatiwa na usipolipa mkopo tutachukua dhamana zako ili hela ya serikali iludi na kuendelea kuwakopesha wengine"amesema Isdory kiyenze

Baadhi ya wajasiriamali akiwemo Joyce Chumi na Selini John wanasema vikwazo vinavyo likumba shirika la SIDO katika ukusaji wa fedh hiyo imesababishwa na uwepo wa mfumo mbovu wa utoaji wa mikopo hiyo huku wakidai kwamba imekuwa ikitolewa kisiasa zaidi.

"Watu waliopewa mikopo ya Sido walichukuliwa bila utaratibu mzuri,wengi waliopata hawakustahili,sasa unampa hela mtu asiyekuwa na mtaji unategemea nini?utakuta anachukua pesa anaenda kununua vitenge"amesema Joyce Chumi

Tayari mpango wa kuanza kuuza dhamana za wadaiwa sugu unategemewa kuanza ili kunusuru upotevu wa fedha hiyo ya serikali

Mbunge Ashauri Tozo Ya Pombe ,sigara Ipande Maradufu

0
0
Na.Faustine  Gimu Galafoni,
Ikiwa leo Juni 25,2019 Bunge la Tanzania likiwa lina piga kura  ya ndio au hapana ya  kuipitisha au kutoipitisha bajeti kuu ya serikali,wabunge wamekuwa wakitoa michango na maoni mbalimbali kuhusu bajeti hiyo ambapo mbunge wa Rujiji Mohamed  Mchengelwa ameishauri serikali kuongeza tozo kwenye Pombe na sigara . 

Mhe.Mchengelwa amesema kuongeza tozo kwenye pombe na sigara itasaidia kulinda afya za watu kwani watapungua kunywa pombe na sigara kutokana na gharama kubwa  ya  bidhaa hizo ambazo sio muhimu kwa maisha ya binadamu  kwani husababisha madhara kiafya pamoja ,uchumi kudumaa, migogoro kutokana na walevi  kuwa na fujo zisizo za msingi. 

Hivyo Mbunge huyo amesema serikali hutumia gharama kubwa katika matibabu kwa watu walioathirika na utumiaji wa pombe na sigara Mfano,TB, ili kupunguza gharama hizo na kuepusha madhara kwa watanzania ni wakati sasa umefika tozo  za pombe na Sigara zikawa kubwa maradufu. 

Katika hatua nyingine mbunge huyo ameishauri serikali kufanya tathmini ya Madhara ya Ukoloni  uliotokea na kubainisha hasara na madhara ya ukoloni ili Tanzania ifungue kesi ya kimataifa dhidi ya nchini zilizokuwa makoloni ya Tanzania ambazo ni Ujerumani na Uingereza ili ziweze kuipa fidia Tanzania kwani baadhi ya nchi za Afrika zilishawahi kufanya hivyo na kulipwa. 

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya miezi ya hivi  karibuni kuona clip ya video   ya  Bunge la Ujerumani ikishinikiza Taifa la Tanzania kusitisha utekelezaji wa mradi wa umeme wa  mto Rufiji wa Stieglers Gorge   wakidai kuwa wao ni koloni la Tanzania. 

Ikumbukwe kuwa mradi wa umeme wa Mto Rufiji Stieglers Gorge unagharimu  dola za kimarekani Bilioni 2.9  na ukikamilika utazalisha Megawati 2,100 na hatua hiyo ya utekelezaji  imekuja baada ya miaka 40  ya utafiti.

Ndugai ataka tamko la serikali kuhusu Watanzania Kupewa Masaa 24 Waondoke Kenya

0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameitaka serikali kutoa tamko kufuatia kauli yenye kuashiria ubaguzi aliyoitoa mmoja wa wabunge wa Kenya.

Amesema hayo kufuatia kusambaa kwa video mtandaoni ikimuonesha Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi 'Jaguar', akitishia usalama wa wageni mbalimbali wanaofanya kazi pamoja na biashara nchini humo.

Leo Jumanne, Juni 25, Mbunge wa Rufiji-CCM, Mohammed Mchengerwa amehoji bungeni juu ya umuhimu wa Serikali kutoa ulinzi kwa Watanzania wanaoishi, kufanya kazi pamoja na biashara nchini Kenya, ndipo Spika Ndugai alipotoa rai hiyo kwa serikali.

"Ninaiomba Serikali kutoa tamko hii leo kufuatia kitendo hiki", amesema Spika Ndugai.

Katika video hiyo inayosambaa kwa kasi, Mbunge Jaguar amesema, "hapa hatuwazungumzii wachina 6, tunawazungumzia mamia ya wageni wanaofanya kazi hapa. Ninaipa serikali masaa 24 kuwaondoa hawa wageni, endapo itashindwa, nikiwa kama mwakilishi wa eneo hili, tutakwenda katika maduka, tutawapiga na kuwafurusha hadi uwanja wa ndege ili warejeshwe walikotoka".

Kauli hiyo ya Jaguar imewalenga zaidi raia wa Tanzania na Uganda, ambao kwa madai yake ndiyo waliochukua fursa zao za kibiashara nchini humo.

Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Kauli Ya Serikali Bungeni Kuhusu Watanzania Kufukuzwa Kenya

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Kenya imesema kauli iliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Starehe nchini humo, Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar si kauli ya Serikali, hivyo amewataka Watanzania wawe watulivu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Juni 25, 2019) wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu kauli ya iliyotolewa na mbunge huyo ya kuwataka wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania waondoke nchini Kenya ndani ya saa 24.

Amesema baada ya mbunge huyo kutoa kauli hiyo, Serikali ilianza kulifanyiakazi jambo hilo ambapo ilimuita Balozi wa Kenya nchini Tanzania ili kujua kama huo ni msimamo wa Serikali yao ama la, ambapo balozi huyo alimesema ile si kauli ya Serikali ya Kenya wala wananchi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mbali na kuwasiliana na Balozi huyo, pia Serikali imewasiliana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya ili afuatilie kuhusu kauli ya Mbunge huyo, hivyo amewataka Watanzania waendelee kushirikiana na Wakenya.

“Si kauli nzuri na kauli hii iliyotolewa na mtu mmoja linajenga chuki baina ya mtu na mtu, nchi na nchi na tayari Serikali ya Kenya inalifanyia kazi suala hili na imetuomba Watanzania tuendelee kuwa wavumilivu.”

Waziri Mkuu amesema tamko lile linaweza kuibua chuki na vurugu miongoni mwa nchi mbalimbali zikiwemo za Afrika Mashariki na tayari Wabunge wa Bunge Afrika Mashariki wanaoendelea na kikao cha Bunge hilo jijini Arusha wamepinga na kulaani kauli hiyo.

Wamesema hawatoa nafasi kwa mtu yeyote kuvuruga nchi hizo.

Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania popote walipo waendelee kuishi vizuri na Wakenya kwa kuwa wao hawana chuki na Watanzania bali ni mtu binafsi. Pia amewatahadharisha wananchi wa Afrika Mashariki wawe makini na kauli zao ili kuepusha vurugu.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano June 26

Jeshi La Polisi Dodoma Lakamata Wahalifu 10 Wanaojihusisha Na Uhalifu Wa Simu Pamoja Na Wahamiaji Haramu Wanne

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limefanikiwa kuwakamata watu kumi (10) wanaojihusisha  na usajili line za simu kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine na kuzalisha line nyingi kwa kitambulisho kimoja bila ridhaa ya mwenye kitambulisho. 

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa line hizo  wamekuwa wakiuuza kwa wa halifu  na watu wasio na vitambulisho ambao ni wahalifu.

Aidha muroto ameongeza kuwa wamewakamata wahamiaji  wahamiaji haramu wanne ambao ni raia wa Ethiopia huku akisema raia hao wanne walikamatwa katika eneo la chipolo wilayani mpwapwa wakiwa wanasafirishwa katika basi Namba T.112 ATC SCANIA Bus la Kampuni ya Premere  line linalofanya safari  kutoka mwanza kwenda mbeya.

Hatahivyo, kamanda muroto amesema kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa yote wameanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo sasa wanasaidia jeshi la polisi kuwaibua wahalifu wote katika mitaa yao wanaohifadhi wahalifu pamoja na wapokeaji wa mali zinazotokana na uhalifu.

Katika hatua nyingine kamanda muroto amewataka Madereva kuheshimu sheria za usalama  barabarani huku akisema kuwa anayetembea kwa miguu ana haki ya kisheria kama dereva anaye endesha barabarani.

Methew Benjamini ni Mrakibu msaidizi,wa jeshi la polisi, Mkuu wa kitengo  cha usalama barabarani  mkoa wa Dodoma  amesema wameamua kujikita katika utoaji wa elimu zaidi  ya usalama  barabarani hasa katika vivuko vya waenda kwa miguu ambapo zaidi ya asilimia 76 ya ajali za barabarani hapa nchini husababishwa na makosa ya kibinadamuikiwa ni pamojana uzembe  wa madereva. 

Nao watembea kwa miguu wamesema kuwa walikuwa hawana elimu ya kutosha juu ya vivuko hivyo vya watembea kwa miguu huku wengine wakitoa ushauri kwa madereva kufuata sheria za barabarani

Rais Magufuli amtumbua Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa C. Juma kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Uteuzi wa Dkt. Mussa C. Juma umeanza June 25, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mussa C. Juma alikuwa Mkuu wa Idara ya Bima katika Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Dkt. Mussa C. Juma anachukua nafasi ya Dkt. Baghayo Abdallah Saqware ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Dirisha la Maombi ya mikopo elimu ya juu kufunguliwa Julai Mosi

0
0
Tunapenda kuwafahamisha waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kuwa dirisha la kuomba mkopo kwa njia ya mtandao litafunguliwa rasmi Jumatatu, Julai 1, 2019 na kufungwa Alhamisi, Agosti 15, 2019. Maombi yote yatafanywa kupitia mtandao utakaopatikana kupitia www.heslb.go.tz.
 
Kati ya leo (Jumanne, Juni 25) na Julai 1, 2019 wakati dirisha litakapofunguliwa, wanafunzi wanashauriwa kuhakikisha wanakamilisha nyaraka muhimu zinazotajwa katika ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa 2019/2020’ unaopatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz).
 
Nyaraka hizo na maelezo mengine ya ufafanuzi pia yanapatikana katika kitabu kidogo cha ‘Maswali na Majibu 26’ kuhusu uombaji mkopo kinachopatikana katika tovuti hiyohiyo.
 
Kwa ajili ya kumbukumbu, nyaraka muhimu ni pamoja na:
  1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mwombaji wa mkopo iliyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA);
  2. Nakala ya cheti cha kifo cha mzazi wa mwombaji mkopo iliyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA);
  3. Barua ya Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO), Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji, Wilaya, Manispaa au Jiji inayothibitisha ulemavu wa mwombaji mkopo au mzazi wake; na
  4. Barua kutoka kwa taasisi iliyofadhili masomo ya sekondari au stashahada ya mwombaji mkopo.
Ufafanuzi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na stashahada mwaka huu
Baada ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita au stashahada (diploma) wamekuwa wakiuliza maswali kadhaa kuhusu utaratibu wa ujazaji wa fomu za uombaji mkopo wakiwa katika kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na iwapo wanaweza kujaza fomu kabla matokeo ya mitihani hayajatoka.
 
Ufafanuzi ni kuwa HESLB inawasiliana na Makao Makuu ya JKT ili kuweka utaratibu bora kuwawezesha wanafunzi wahitaji waliopo katika kambi za JKT kuwasilisha maombi kwa njia ya mtandao.
 
Aidha, mfumo wa uombaji mikopo kwa njia ya mtandao utakaofunguliwa Julai 1 mwaka huu haumlazimishi mwombaji kuwa na matokeo ya kidato cha sita. Mwombaji atapaswa kuwa na namba ya mtihani wake wa kidato cha nne tu.
 
Wito
Waombaji wa mikopo watarajiwa wanashauriwa kusoma mwongozo uliotolewa na kuandaa nyaraka zote muhimu zinazohitajika kuthibitisha uhitaji wao kabla ya kuingia katika mfumo wa uombaji. Uzoefu unaonesha kuwa mwombaji mkopo anaweza kutumia dakika 30 kukamilisha maombi yake katika mfumo ikiwa ana nyaraka zote muhimu.
 
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Dar es salaam
Jumanne, Juni 25, 2019

Diamond Platnumz azindua Wasafi Festival 2019

0
0
Uongozi wa WCB pamoja na Wasafi Media kwa pamoja wamezindua rasmi Tamasha la Wasafi Festival 2019 ikiwa ni msimu mpya wa Mapinduzi ya Burudani nchini.

Msanii Diamond Platnumz ndiye ametangaza ujio wa Tamasha hilo ambalo litaanza Juluy 7 mwaka huu, Muleba.

Wasafi Festival litafanyika sanjari na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya kondom ili kujikinga kupata virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini(VVU) na Ukimwi.

Tume ya Kupambana na Ukimwi Tanzania (Tacaids) itatoa elimu hiyo na ni mmoja wa wadhamini wa tamasha hilo. Mkurugenzi wa lebo ya WCB Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, kuna uwezekano mikoa ikaongezeka kwa kuzingatia mwamko wa washiriki kwenye mikoa minane ya kwanza.

Tamasha hilo litaanza Julai 12 wilayani Muleba mkoani Kagera, kisha litahamia Tabora Julai 14, na Iringa Julai 20.

“Tumejipanga kupeleka burudani ya kutosha kwenye mikoa husika na tutaendelea kutoa taarifa ya wasanii wangapi watashiriki na wangapi watatoka nje ya nchi,” amesema Diamond.

Bunge laipitisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020

0
0
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2019/2020.

Bajeti hiyo ilipitishwa mjini Dodoma  jana baada wabunge kupiga kura ya wazi ya kuitwa mbunge mmoja mmoja.

Matokeo ya kura yalikuwa kama ifuatavyo: Wabunge waliopiga kura walikuwa 380 ambapo 12 hawakuwepo.

Waliosema ‘Ndiyo’ ni 297 sawa na asilimia 78.2 na waliosema ‘Hapana’ ni 83 sawa na asilimia 21.8 .

Hotuba ya Bajeti iliwasilishwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango na mjadala wa bajeti hiyo ulichukua siku saba kabla kuhitimishwa jana.

Awali, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mpango akijibu baadhi ya hoja za wabunge waliochangia, alisema kamwe saini yake haitoweza kutumika kusaini mikataba, itakayoiuza nchi hata kama atatukanwa vipi.

Alisema ataendelea na msimamo wake huo, ikiwamo kutosaini mikataba mitatu ya miradi mikubwa inayohusu Zanzibar ambayo wafadhili wake wameweka masharti magumu ya dhamana ikiwemo kutaka kutumia mali za jeshi, mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), malikale, mali za kihistoria na za ubalozi kama dhamana ya mkopo.

Rais Magufuli: Mradi wa majengo ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika eneo la Dege Beach Ni wa Kifisadi

0
0
Rais  Magufuli amesema mradi wa majengo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliopo wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam ni mradi bomu na wa kifi sadi.

Ameyasema hayo  jana wakati akizindua ghala na mitambo ya gesi ya Kampuni ya Taifa Gas iliyoko Vijibweni wilayani Kigamboni. 

Rais Magufuli alisema mradi huo ambao ni maarufu kwa jina la Dege, unapaswa kubadilishwa matumizi yake kwa kuwa majengo hayo hayaendelezwi kwa lolote.

“Yale majengo ya NSSF yamekaa kwa muda mrefu na ni mradi bomu, wa ovyo na wa kifisadi. Tumeshawaeleza haya NSSF pamoja na bodi washughulikie, watoe mawazo yao na nyie wananchi mtoe mawazo yenu tuone jinsi gani haya majengo tunaweza kuyatumia katika njia iliyo sahihi.

“‘Investment’ kubwa kama hiyo imekaa na wala hatutoi majibu. Kama ni kuyatoa yawe mabweni ya chuo au nyumba za wafanyakazi tusubiri uchambuzi utakaofanywa,” alisema Rais Magufuli.

Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia alitembelea mradi huo na kusikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaoendelea katika eneo hilo na kuagiza ulinzi uimarishwe.

Mkataba kati ya NSSF na AHEL ulisainiwa mwaka 2012 na kuanzisha kampuni hodhi ya ‘Hifadhi Builders’ ambapo AHEL ilikuwa na asilimia 55 na NSSF asilimia 45.

Katika asilimia 55 za AHEL, asilimia 20 ni ardhi iliyotoa katika mradi na asilimia 35 kampuni hiyo ingetakiwa kuweka fedha taslimu.

Mradi ulihusisha ujenzi wa nyumba 7,460 ambapo jumla ya gharama za mradi zilikadiriwa kuwa Dola za Marekani 653,436,675 ambazo kati yake ujenzi ungegharimu Dola 544,530,562 wakati gharama za ardhi zingekuwa Dola 108,906,113. Kwa fedha za Tanzania mradi pamoja na ardhi ungegharimu Sh trilioni 1.5.

Hadi kufikia Juni mwaka jana, NSSF walishailipa Kampuni ya Hifadhi Builders Dola 133,838,662.2 kama mchango wake katika ujenzi wa mradi huo ambazo ni sawa na Sh bilioni 305.8 wakati Kampuni ya Azimio ilitoa Dola 5,500,000 sawa na Sh bilioni 12.6 tu.

 
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli aliwahakikishia wananchi wa Kigamboni kuwa serikali inazifanyia kazi changamoto zao za kukatikakatika kwa umeme na ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo barabara ya Kibada-Kimbiji hadi Mji Mwema.

Amesema Mpango Mkuu (Master Plan) wa serikali ni kuifanya Kigamboni kuwa Mji wa Kisasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo uboreshaji na uimarishaji wa miundombinu mbalimbali ni sehemu ya mpango huo.

Ndugai Akerwa na Kiongozi wa Serikali Aliyesema Mbele ya Rais Kuwa Wabunge Wamewadhihaki Wachezaji wa Taifa Stars

0
0
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kiongozi mmoja wa Serikali aliyezungumza maneno yasiyofaa kuhusu Bunge la Tanzania na wabunge na kumdanganya hadharani Rais John Magufuli kuwa wawakilishi hao wa wananchi wamewadhihaki wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, hajitambui.

Spika ametoa kauli hiyo bungeni  jana Juni 25, baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, (ACT-Wazalendo), kuomba muongozo kwa kutumia kanuni ya 68 (7), kuhusu jambo lililotokea mapema bungeni.

Zitto alilazimika kuomba muongozo huo baada ya Spika Ndugai kutoa ufafanuzi kwamba hakuna mbunge yeyote aliyewadhihaki wachezaji wa Taifa Stars baada ya mchezo wake na Senegal.

“Mheshimiwa Spika, kwa kutumia kanuni 68 (7), kuhusu jambo lililotokea bungeni mapema, umeelezea jambo ambalo limetokea nje ya bunge kuwa mmoja ya viongozi wa serikali kuwabagaza wabunge waliokwenda Misri.

Mara baada ya mbunge huyo kuomba muongozo huo, Spika Ndugai, alijibu akisisitiza kuwaomba wabunge kutolikuza jambo hilo.

“Naomba tusilikuze jambo hili kabisa, kama wabunge tungekuwa na mawazo kama wachezaji wanamakosa isingewezekana wabunge wengine 30 kwenda Misri. Ni bahati mbaya sana, kwamba tuna viongozi wa serikali, wanadiriki kumdanganya Rais hadharani.

“Kiongozi wa serikali unapoongea mbele ya Rais, jipange, ongea ukweli mtupu mbele ya Mwenyenyezi Mungu na sisi hatutamani kusema, natamani kufunguka kidogo…inatosha..inatosha.

“Nasema wazi bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui, hajielewi kwa sababu ana nguvu aliyonayo ana makundi ya vijana kwenye mitandao ambao wanaweza kumtukana Spika, lakini tuache,”alisema.

Wananchi 13,234 Wapatiwa Elimu Ya Madhara Ya Mimba Za Utotoni

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Jumla ya wananchi 13,234  wamefikiwa na elimu ya madhara ya mimba za utotoni hapa nchini .

Hayo yamesemwa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya  jamii,jinsia wazee na watoto Dokta Faustine Ndugulie  wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Fatma Tafiq aliyehoji,ndoa  za utotoni ni tatizo kubwa katika jamii zetu  hususan katika jamii zenye umasikini ,je ,serikali haioni kuwa kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa umma hasa katika maeneo ya vijijini ili wananchi wafahamu athari za kuozesha watoto katika umri mdogo.
 
Katika majibu yake,Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na watoto Dokta Ndugulile amesema serikali ina tambua umuhimu wa elimu kwa umma katika kupambana na ndoa za utotoni ambazo zina madhara makubwa kwa watoto wa kike .
 
Hivyo amesema kupitia mbalimbali za mawasiliano ikiwemo TV,Radio,Magazeti na Majarida serikali imekuwa  ikitoa elimu kwa  kuandaa jumbe mbalimbali kuhusu madhara  ya mimba za utotoni sambamba na kusisitiza wazazi na walezi  na jamii kwa ujumla kutoozesha  watoto Mapema.
 
Aidha,Dokta Ndugulile ,amesema, Kwa kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka  ,2018,Jumla ya Wananchi 13,234  wamefikiwa na Elimu ya Madhara ya Mimba za utotoni .
 
Kati ya hao,wanafunzi  8,546,walimu  476,viongozi wa dini 110,wazee wa mila na watu Mashuhuri 90,ngariba 38,waendesha bodaboda 261,wazazi/walezi  3600 na watendaji wa vijiji 113.
 
Kampeni ya  kutokomeza mimba za utotoni ijulikanayo’mimi Msichana Najitambua ilizinduliwa mkoani  Mara mwaka 2017 ambayo tayari imefanyika katika mikoa ya Shinyanga,Mara,Tabora,Lindi,Dodoma,Tanga,Dar   es  Salaam na Katavi.
 
Mikoa 6 yenye  kiwango kikubwa cha mimba za utotoni hapa nchini Tanzania ni Shinyanga,Dodoma,Tabora,Mara,Katavi na Singida  na takwimu zinaonesha kuwa asilimia 27% ya mabinti walio chini ya miaka 18 wana  mimba au wamezaa.

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. 

Simu:  +255745495181 au 0682644040  

www.tumainitibaasili.co.tz

Serikali Kutoa tamko kuhusu ajira za madereva nchini

0
0
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Walemavu, Anthony Mavunde amesema kuanzia Julai Mosi, 2019 Serikali ya Tanzania itatoa tamko kuhusu ajira za madereva nchini humo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 26, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka aliyetaka kujua ni lini Serikali itatoa kauli kuhusu  malalamiko ya madereva wengi kutokuwa na mikataba ya ajira.

“Wamiliki wa malori walielezwa wazi wanapokwenda kusajili leseni Sumatra (Mamlaka ya Udhibiti, Usafiri wa Majini na Nchi Kavu) waende na mikataba ya ajira ya wafanyakazi, ila siku mbili zijazo Wizara ya Mambo ya Ndani na ofisi ya Waziri Mkuu wataeleza hatua ambazo zimechukuliwa. Kila dereva atakuwa na mkataba wa kazi na litatolewa tamko,” amesema Mavunde.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images