Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa Awataka waislamu kote nchini waendeleze utulivu, amani na uadilifu

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waislamu kote nchini waendeleze utulivu, amani na uadilifu waliouonesha katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kwa kufanya hivyo, watasaidia kukuza umoja wa kitaifa, uchumi na kuboresha huduma za jamii.

Amesema ni vema wakatambua kwamba uadilifu waliouonesha ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni silaha muhimu hususan katika kuimarisha maendeleo na kudumisha haki, umoja, usawa, upendo na utulivu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Juni 5, 2019)kwenye Baraza la Eid El Fitri, lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Tanga Beach Resort jijini Tanga.“Nawashi sana kuyaenzi mema yote mliyoyafanya kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan’’.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezipongeza taasisi za Kiislamu na imani nyingine ambazo zimejenga shule ili kuchangia maendeleo ya elimu kitaifa lakini amesisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongeza shule nyingine na vyuo zaidi pamoja na kuziboresha zile zilizopo ili kusaidia jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za jamii nchini

Amesema licha ya juhudi inazozichukua, Serikali peke yake haina uwezo wa kueneza huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji katika kila pembe ya nchi hivyo, inapotokea taasisi za Kiislamu au madhehebu mengine yakaweka mikakati ya kueneza huduma hizo, basi bila shaka Serikali ipo tayari kuunga mkono juhudi hizo na kuchangia ufanisi wake.

Wakati huo huo, ameitaka BAKWATA ichukue hatua za makusudi katika kuhakikisha huduma nyingi za maendeleo na za kijamii zinaifikia kwenye mikoa mingi zaidi ya pembezoni. “Huu ni wakati muafaka sasa wa kutafakari ni namna gani Watanzania wa maeneo mengine nao watanufaika na uwepo wa huduma mbalimbali kama vile elimu, afya na nyinginezo.“

Kwa upande wake,Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally ametumia fursa hiyo kuwataka waislam wote nchini wabadilike na waache mazoea ili waweze kusonga mbele kielimu na kiuchumi.

Sheikh Zubeir amesema ni vema kwa waislamu wakajiimarisha kiuchumi kwa sababu kutawaondolea changamoto za kuendesha shughuli zao mbalimbali na hivyo watakuwa wamejiletea maendeleo na kuboresha maisha yao.

Mbali na wito huo pia amewataka waislamu wote wahakikishe wanatii mamlaka yaliyo juu yao , viongozi waliopo madarakani wawe wa kiserikali na wa kidini kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa [TAKUKURU], Diwani Athuman amesema ili nchi iweze kuendelea kuwa na amani,  utulivu na usalama watanzania wote hawana budi kuungana pamoja katika kupiga vita vitendo vya rushwa.

"Rushwa ni dhambi kubwa na hukumu yake mbele ya Mwenyezi Mungu ni moto kwa sababu rushwa ni kipingamizi kikubwa cha maendeleo, hivyo tuungane pamoja kupinga rushwa ndani ya nchi yetu kama Rais Dkt. John Magufuli anavyotuongoza."

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Kuahirishwa Kwa Zoezi La Ajira Za Watumishi Wa Muda Kwa Ajili Ya Uboreshaji Wa Daftari La Kudumu La Wapiga Kura

0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa tarehe 30 Mei, 2019 iliwatangazia nafasi za kazi za muda kupitia tovuti yake ya www.nec.go.tz na kuwaalika watanzania wenye sifa zilizo ainishwa kwenye tangazo hilo kuomba nafasi hizo za kazi.
 
Hivyo, Tume inapenda kuwataarifu wananchi wote ya kwamba mchakato wa ajira za muda kwa ajili ya zoezi hilo umeahirishwa hadi hapo itakapotangazwa tena.
 
Aidha, Tume inapenda kutoa shukrani zake kwa wale wote walioleta maombi yao ya kazi na inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
 
Dkt. Athumani Kihamia
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Rais Magufuli Kukutana na Wafanyabiashara Watano Kutoka Kila Wilaya Kesho Ijumaa

0
0
Rais wa Tanzania, John Magufuli kesho Ijumaa Juni 7, 2019 atakutana na wafanyabiashara watano kutoka kila Wilaya kujadili mambo mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Juni 6, 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema mkutano huo utafanyikia Ikulu kuanzia saa 3.30 asubuhi.

Msigwa amesema wafanyabiashara hao watawawakilisha wenzao ambapo wataambatana na wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).

“Mkutano huu utaanza saa 3:30 asubuhi hivyo wajumbe wote wanatakiwa kuwasili katika ukumbi wa Kikwete kuanzia saa 2:00 hadi saa 2:30 asubuhi,”  amesema Msigwa

Mama Maria Nyerere alazwa hospitali baada ya kuugua ghafla akiwa Uganda

0
0
Mke wa baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere amelazwa katika Hospitali jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini jana Jumatano Juni 5, 2019 akitokea Kampala Uganda alipokuwa amelazwa baada ya kuugua ghafla.

Mtoto wake Makongoro Nyerere amesema, baada ya kuwasili nchini mama yake alipumzishwa kwa muda wakati madaktari wakiendelea na uchunguzi kabla ya kufikia uamuzi wa kumlaza.

Makongoro alisema alipelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam akitokea Kampala nchini Uganda alikokuwa amelazwa baada ya kuugua ghafla.
 
Mama Maria Nyerere alikuwa nchini Uganda kwa ajili ya ibada maalum ya kukumbuka mchango wa hayati Mwalimu juliasi Nyerere kwa Afrika na Ukristo.

Tangu mwaka 2009, waumini wa kanisa katoliki wamekuwa wakifanya ibada katika hekalu la Namugongo kwa ajili ya kumkumbuka mwalimu Nyerere.

Nyerere alitoa mchango mkubwa sana kwa ajili ya kuung'oa madarakani utawala wa rais Idi Amin..

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Patrick Ole Sosopi Akamatwa na Polisi

0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Patrick Ole Sosopi pamoja na wenzake wawili wamekamatwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kufanya shughuli za kisiasa ikiwemo kampeni za nyumba kwa nyumba. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa  amesema watu hao wamekama Ifaraka na wapo njiani kupelekwa kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro.

Umoja wa Afrika wasimamisha uanachama wa Sudan katika jumuiya hiyo

0
0
Umoja wa Afrika AU umechukua uamuzi wa kusimamisha uanachama wa Sudan katika jumuiya hiyo kubwa zaidi barani Afrika mpaka pale Baraza la Kijeshi litakapokabidhi madaraka ya nchi kwa utawala wa kiraia.

Umoja huo pia umesema unajadili suala la kuwawekea vikwazo maafisa wa jeshi la Sudan waliohusika na mashambulizi dhidi ya raia wa nchi hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa katika kikao cha dharura cha Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kinachokutana mjini Addis Ababa huko Ethiopia kwa ajili ya kutathmini hali ya mambo nchini Sudan. 

Katika kikao hicho pia Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limelaani tena mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Sudan na kupinga mabadiliko ya aina yoyote yasiyokuwa ya kikatiba.

Msimamo huo wa Umoja wa Afrika umechukuliwa huku Baraza la Kijeshi lililotwaa madaraka nchini Sudan likiendelea kukabiliwa na upinzani mkali wa wananchi na vyama na makundi ya upinzani yanayosisitiza kuwa yataendelea kufanya maandamano na migomo ya kijamii hadi pale wanajeshi watakapokabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia. 

 
Waziri wa afya nchini Sudan amesema kuwa ni watu 46 pekee waliofariki katika ghasia za hivi majuzi,  madai yanayopingwa na kamati ya madaktari nchini humo ambao wamesema kuwa idadi hiyo inafika watu zaidi ya 100.

Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika Caf akamatwa Ufaransa

0
0
Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad ametiwa mbaroni na mamlaka nchini Ufaransa ambako alikuwa akihudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Taarifa ya kukamatwa kwake imethibitishwa na FIFA lakini haijaweka wazi sababu zaidi ya kusema “Tuhuma zake zinahusiana na mamlaka yake akiwa Rais wa CAF”.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa “FIFA haijui kwa undani uchunguzi unaofanywa dhidi yake kwahiyo haiwezi kusema chochote”.

FIFA imeziomba mamlaka zinazohusika na sakata hilo nchini Ufaransa kutoa taarifa kwenye kamati yake ya maadili.

Ahmad ambaye ni waziri wa zamani wa Madagascar aliripotiwa kwa kamati ya maadili ya fifa kwa madai ya ufisadi na unyanyasaji na katibu mkuu wa Caf Amr Fahmy. Baadaye Fahmy alifutwa kazi.

Ahmad mwenye umri wa miaka 59, alichukuliwa katika hoteli yake, mjini Paris mapema mwendo wa alfajiri na kuhojiwa na maafisa wa polisi wa Ufaransa wanaokabiliana na uhalifu wa kifedha na Ufisadi, kulingana na vyombo vya habari vya Ufaransa.

Ahmad ambaye pia ni naibu rais wa Fifa alikuwa nchini Ufaransa katika mkutano wa Fifa siku ya Jumatano ambapo rais wake mpya Gianni Infantino alisema kuwa shirikisho hilo limeondoa picha mbaya iliokuwa nayo..

Urusi Yaionya Marekani dhidi ya kujiingiza kijeshi Venezuela

0
0
Rais Vladimir Putin wa Urusi ameonya dhidi ya Marekani kuivamia kijeshi Venezuela na kusema hilo litakuwa balaa kubwa. 

Rais Putin amekumbusha washirika wa Marekani hawaungi mkono jambo hilo. 

Akizungumza katika kongamano la kiuchumi la mjini St. Petersburg, Rais Putin amesema pia kwamba wataalam wa kiufundi wa Urusi wanasalia Venezuela ili kushughulikia mitambo ya kijeshi ya Urusi, jambo ambalo anasema wanalazimika kulifanya. 

Hata hivyo, anasema Moscow haifungui kituo chochote cha kijeshi nchini Venezuela.

Lugola Atangaza Kiama Kwa Polisi Wasiotii Maagizo yake

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuanzia Juni 15, 2019 ataanza ziara katika vituo mbalimbali vya polisi kukagua utekelezaji wa agizo lake kuhusu jeshi hilo kuzishikilia pikipiki (Bodaboda).

Aametoa kauli hiyo leo ambapo ameeleza kuwa atapita kila kituo kwa nyakati tofauti kuangalia utekelezaji wa agizo hilo, huku akisisitiza kuwa anataka suala hilo liishe ili tuondoe malalamiko ya muda mrefu ya vijana kuhusu bodaboda zao.

“Nawaambia nikikuta kituo chako kuna bodaboda  umezikamata tofauti  na makosa niliyoanisha ile kauli ya niliyoisema Bungeni itatimia siku hiyo,” anasema Lugola.

Utakumbuka May 20, 2019 akiwa Bungeni Lugola alitoa maagizo kwa polisi akitaka pikipiki zinazokamatwa na kuwekwa vituoni ni zile zilizohusika katika uhalifu, zilizoibiwa na zisizo na wenyewe badala ya kuziweka kituoni bodaboba zenye makosa ya kofia ngumu au kupakia abiria zaidi ya watatu.

Taifa Stars wakabidhiwa Bendera ya Taifa kuelekea AFCON Kesho

0
0
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amemkabidhi bendera Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta tayari kwa safari ambapo kikosi cha timu ya taifa kitaondoka kesho kwenda nchini Misri kuweka kambi ya wiki mbili kikijiandaa na AFCON.

TFF Watoa Ufafanuzi kuhusu Shomari Kapombe kuachwa AFCON

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa June 7

LIVE: Mazungumzo Ya Rais Magufuli Na Wafanya Biashara Wakubwa Kutoka Katika Wilaya Zote Nchini. Ikulu Dsm

0
0
Rais wa Tanzania, John Magufuli amekutana na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini na kuwataka wawe wazi kueleza changamoto zilizopo ili zipatiwe ufumbuzi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ijumaa Juni 7, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo ameanza kwa kuelezea mafanikio mbalimbali ya Serikali  anayoiongoza tangu iingie madarakani Novemba 5 mwaka 2015.

Amesema kikoa hicho kitasaidia kuboresha mazingira ya biashara na kwa kuona umuhimu wa kikao hicho, amewalika mawaziri na wakuu wa vyombo vya dola  kusikiliza yale yatakayosemwa na wafanyabiashara na hatua zianze kuchukuliwa.

Magufuli amesema kuzungumza na wafanyabiashara wa aina mbalimbali itawasaidia kuwa na lengo la aina moja na kuwataka kuzungumza ukweli ili kupata suluhisho.

 
Tazama hapo chini

Lugola Aunda Kamati ya Watu Wanne Kuchunguza Kifo Cha Anayedaiwa Kufia Mikononi Mwa Polisi

0
0
Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameunda kamati ya watu wanne kuchunguza kifo cha Isululu Kabote (85), mkazi wa Kijiji cha Buhungukila, Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, ambaye anadaiwa kuuawa akiwa mikononi mwa polisi.

Kamati hiyo imeundwa baada ya wananchi wa kijiji hicho kudai kabla ya Kabote kukumbwa na mauti, Mei 17 saa 8:00 usiku, alikamatwa na askari polisi na kupigwa akidaiwa hajatoa mchango wa maendeleo wa Sh 50,000 madai ambayo Jeshi la Polisi limekanusha.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa Maswa Mashariki (CCM), alisema kutokana na ukimya na polisi Mkoa wa Simiyu juu ya tukio hilo, aliiomba Serikali iundwe kamati hiyo ili kubaini ukweli wa tukio hilo.

Akiitambulisha kamati hiyo, Nyongo alisema kuna dalili za watu kulindana katika suala hilo kwa sababu tangu mzee huyo afariki, hakuna mtu aliyekamatwa.

“Kuna dalili za watu kulindana, wanafahamika waliosababisha kifo cha mzee wetu, lakini hatujasikia hata mtu mmoja ameshikiliwa na Jeshi la Polisi ili kusaidia uchunguzi, Polisi Mkoa wapo kimya, kwa kuundwa timu hii kila kitu kitajulikana,” alisema.

Alisema mwili wa marehemu umekaa siku 20 katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya uchunguzi wa kidaktari, taarifa ambayo itatumiwa na timu hiyo katika kubaini ukweli.

Nyongo alimtaja mwenyekiti wa timu hiyo ni Laifu Mella kutoka dawati la malalamiko Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Wengine ni daktari bingwa wa mifupa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Ibenze Ernest, Kefa Kaswamila kutoka Dawati la Malalamiko Kitengo cha Upelelezi Wizara ya Mambo ya Ndani na Mzee Mzee kutoka Ofisi ya Ofisa Usalama Mkoa wa Simiyu.

Wanaodaiwa kodi ya pango Waitwa Ofisini Kwa Lukuvi Bila Kukosa

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi atakutana na taasisi na mashirika ya umma 207 yanayodaiwa kodi ya pango la ardhi katika kikao maalumu ikiwa ni mkakati wa wizara hiyo kuhakikisha wadaiwa wa kodi hiyo wanalipa kwa mujibu wa sheria.

Wadaiwa watakaoshindwa kufika katika kikao hicho hatua za kufuta miliki zao na kuuza maeneo husika zitafuata kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Sura Namba 113 Kifungu cha 50.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika, Waziri atakutana na mashirika na taasisi hizo ukumbi wa Hazina Dodoma Juni 11, mwaka huu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, taasisi, mashirika na wenye viwanda na maeneo makubwa ya biashara ambao wana malimbikizo makubwa ya kodi ya pango la ardhi watatakiwa kufika katika kikao hicho maalum bila kukosa na nyaraka za umiliki na stakabadhi za malipo ya kodi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wadaiwa watakaoshindwa kufika katika kikao hatua za kufuta miliki zao na kuuza maeneo zitafuata.

Baadhi ya taasisi na mashirika yaliyopewa wito wa kuhudhuria kikao hicho ni Shirika la Ndege Tanzania (ATC), Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC), Bodi ya Pareto.

Nyingine ni Chuo cha Madini, Bodi ya Korosho, BP Tanzania Ltd, Puma Energy, Chuo cha Ushirika, CRDB, Mamlaka ya Maji Dodoma (DUWASA), Kahama Mining Corporation na Kituo cha Elimu Kibaha.

Mengine ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Shirika la Bima la Taifa (NIC), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Rubada-Wizara ya Kilimo, Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Pia zimo Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Capco Tanzania Ltd, Aga Khan Foundation, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Exim Bank Tanzania na Shirika la Masoko Kariakoo.

Uamuzi wa kukutana na wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi ni mwanzo wa jitihada za kuhakikisha wadaiwa wa kodi ya ardhi wanalipa kodi hiyo kabla ya Juni 30, mwaka huu. Baada ya hapo watakaokaidi watafikishwa katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya husika ambapo adhabu yake ni kufuta miliki na kuuza maeneo.

China na Urusi Zatiliana Saini ya Kupiga Marufuku ya Matumizi ya Dola ya Marekani

0
0
Rais Xi Jinping wa China ametangaza habari ya kutiwa saini mapatano ya kufutwa sarafu ya dola ya Marekani  katika miamala ya kibiashara ya nchi yake na Russia.

Rais amesema kwamba kwa mujibu wa mapatano ya nchi mbili hizi, dola itafutwa kabisa katika mabadilishano ya kibiashara ya nchi mbili na badala yake sarafu za mataifa hayo kuchukua nafasi ya dola katika mabadilishano hayo.

Sambamba na matamshi hayo ya Xi Jinping serikali ya Russia, kupitia tovuti rasmi ya serikali ya Moscow, imetoa amri ya kuanza kutekelezwa mapatano hayo ya mabadilishano ya kibiashara kwa kutumika sarafu za nchi hiyo na China.

Kwa mujibu wa mapatano hayo ambayo yanachukuliwa kuwa waraka rasmi wa serikali za China na Russia, malipo yote ya kifedha kuhusiana na mauzo na maagizo ya bidhaa kutoka nje, huduma na uwekezaji wa moja kwa moja baina ya mashirika ya kiuchumi ya nchi mbili yatafanyika kwa kutumika ruble, sarafu ya kitaifa ya Russia na yuan, sarafu ya kitaifa ya China. 

Mapatano hayo ambayo yametiwa saini katika safari ya Rais Xi Jinping mjini Moscow ni hatua muhimu ya nchi hizo katika kuimarisha thamani ya sarafi hizo mkabala wa dola ya Marekani.

Russia na China ambazo kwa sababu moja au nyingine zina mivutano ya kisiasa na kibiashara na Marekani, zimetumia njia ya kufuta dola katika miamala yao ya kibiashara na hivyo kupunguza makali ya chombo hicho muhimu ambacho kimekuwa kikitumiwa na viongozi wa Washinton kutoa mashinikizo dhidi ya nchi hizo.

Na hasa ikitiliwa maanani kwamba China hivi sasa iko katika mvutano mkubwa wa kiashara na kiuchumi na Marekani na hivyo kuwa katika mazingira ya kupata madhara makubwa kuliko Russia.

Hivyo uamuzi wa nchi mbili hizo kutumia sarafu zao za kitaifa katika mabadilishano ya kibiashara kati ya Moscow na Beijing ni hatua muhimu katika juhudi za kujaribu kupunguza mashinikizo ya Washington dhidi ya mataifa hayo.
 
Serikali ya Russia pia tokea wakati wa kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi mwaka 2014 imefanya juhudi kubwa za kuweka sarafu ya yuan ya China, ikiwa sarafu muhimu ya kigeni, katika akiba yake ya fedha za kigeni. 

Kuhusiana na suala hilo, Elvira Nabiullina, Gavana wa Benki Kuu ya Russia anasema: Sera ya kufuta kabisa dola katika akiba ya fedha za kigeni na miamala ya kimataifa, ni jambo ambalo limeikinga Russia kutokana na hatari za kiuchumi na kisiasa kutoka nje.

Tunapasa kuashirika hapa kwamba mbali na uamuzi wa Russia na China kutumia sarafu zao za kitaifa katika miamala ya biashara ya pande mbili, pia zimechukua uamuzi wa kutumia sarafu ya euro katika miamala hiyo na pia kijiwekea akiba katika hazina zao za fedha za kigeni.

Katika uwanja huo Mehdad Imadi, mtaalamu wa masuala ya kiuchumi anasema:  Kuchukuliwa euro kuwa sarafu ya kwanza muhimu katika akiba za benki kuu tofauti za dunia, kutapelekea kupungua kwa matumizi ya dola na hatimaye kupungua thamani yake.

Ni wazi kuwa uamuzi wa kufuta dola katika mzunguko wa kiuchumi wa kitaifa haujachukuliwa na nchi mbili za Russia na China pekee bali nchi nyingine kadhaa duniani zimechukua uamuzi kama huo na hivyo kudhoofisha kwa kiwango fulani thamani ya sarafu ya dola. 

Katika miezi kadhaa iliyopita nchi za Malaysia na Uturuki zimeanzisha mikakati ya kufuta matumizi ya dola katika mifumo yao ya uchumi.
 
Kuhusiana na hilo, katika ripoti yake ya hivi karibuni, Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF, limesema kuwa kiwango cha dola katika akiba za fedha za kigeni za nchi tofauti duniani kilipungua sana katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka uliopita wa 2018, na nchi hizo zimekuwa zikionyesha hamu ya kuongeza sarafu za euro, yuan na pauni ya Ungereza katika akiba zao.

Kwa mujibu wa tathmini ya shirika hilo la kimataifa, kupungua huko kwa dola katika akiba za fedha za kigeni za nchi tofauti ndiko kukubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Rais Magufuli: Nina orodha ya kampuni zaidi ya 17,000 zinazokwepa kodi

0
0
Rais Magufuli amesema ana taarifa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamejenga viwanda kama geresha tu, wanatumia viwanda hivyo kupokea au kutunzia bidhaa kutoka nje bila kulipa kodi stahiki

Ametoa kauli hiyo leo Juni 7, 2019  Ikulu jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na wafanyabiashara kutoka Wilaya zote nchini.

Amesema jambo hilo limejitokeza katika biashara ya sukari, mafuta ya kula na korosho.

“Baadhi yao wamekuwa wakitumia mbinu ya kukwepa kodi kwa kudai marejesho ya fedha ya ongezeko la thamani (VAT) wakati mauzo yaliyofanyika ni hewa ya biashara za nje na kwenye hili nataka niseme wazi nina orodha ya kampuni 17,446 ambazo zimehusika na tuhuma hizo,”

“Nitawapa copy (nakala) ya kampuni hizo hewa ili mkafanye uchambuzi wenu na kama yalikwepa kitu chochote yakajipange kulipa ndani ya siku 30,” amesema Rais Magufuli.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa miongoni mwa wanaofanya vitendo hivyo ni waliowahi kubinafsishiwa viwanda na Serikali, kupewa ardhi ili kuviendeleza, kwamba baadhi yao wameamua kuuza mitambo ya viwanda hivyo au kugeuza matumizi ya viwanda bila kufuata utaratibu.

“Wengine wametumia maeneo hayo kukopa fedha benki kwa ajili ya kazi hiyo na hawajafanya, hiyo ni dhambi na wengine najua mko hapa.”

“Baadhi ya wafanyabiashara wamejenga viwanda kama gelesha na kuvitumia kupokea bidhaa kutoka nje bila kulipa kodi stahiki kama vile bidhaa hizo zimetengenezwa nchini.” amesema

 

==>>Msikilize hapo chini

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Video Mpya: Nuh Mziwanda Ft. Dully Sykes - Machete

0
0
Video Mpya: Nuh Mziwanda Ft. Dully Sykes - Machete

Waziri Mkuu wa Ethiopia aelekea Sudan kupatanisha jeshi na raia

0
0
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed leo anatazamiwa kuitembelea Sudan kwa lengo la kujaribu kuwapatanisha watawala wa kijeshi na makundi ya raia kufuatia kuendelea mgoggoro nchini humo baada ya Omar al Bashir kuondolewa madarakani.

Taarifa zinasema Abiy Ahmed atatembelea Khartoum na kukutana na wakuu wa baraza la mpito la kijeshi na muungano wa kiraia wa upinzani unaojulikana kama Alliance for Freedom and Change. 

Taarifa zinasema Waziri Mkuu wa Ethiopia analenga kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Sudan katika mkutano wake na pande hasimu.  

Dkt. Abiy anatembelea Sudan baada ya uanachama wa nchi hiyo katika Umoja wa Afrika kusimaishwa hadi pale wanajeshi watakapowakabidhi raia madaraka.

Mgogoro wa nchi hiyo uliibuka Disemba mwaka jana baada ya wananchi kumiminika mabarabarani wakilalamikia hali mbaya ya kiuchumi ambapo kufuatia maandamano hayo, tarehe 11 Aprili mwaka huu jeshi la Sudan lilitangaza kumuondoa madarakani Rais Omar al-Bashir na kutwaa madaraka ya nchi hiyo. 

Baada ya hapo jeshi hilo liliunda Baraza la Kijeshi la Mpito ingawa wananchi wanalipinga na kulitaka liruhusu kuundwa serikali ya kiraia.


Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images