Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mfanyabiashara Aporwa Mil 55 Baada Ya Kudaiwa Kunyweshwa Sumu .

0
0
Watu wawili wa familia moja, wanashikiliwa na Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara wa ufuta Oswald Malambo na kupora kiasi cha shilingi milioni 55.

Watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Kata ya Ifumbo Wilayani Chunya, inasemekana waliweka kitu kinachodhaniwa ni sumu kwenye kinywaji alichotumia mfanyabiashara huo, wakati wakiwa kwenye hotel baada ya kufanikiwa kuuza ufuta.

Kamada wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.

Kamanda, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Raphael Walolile na Goliat Walolile.Amesema tukio hilo lilitokea Juni 2 mwaka huu na kwamba marehemu ndiye aliyetoa taarifa za kwamba alinyweshwa sumu na watuhumiwa lakini bado haijathibitishwa.

“Kwa sasa bado tunasubiri taarifa za daktari na kama itabainika ni sumu sheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa na kufunguliwa shitaka la mauaji,”

Aidha, akizungumzia hilo, Msemaji wa familia hiyo, Mhandisi Selemani Malambo, alisema ndugu yao alienda kuuza ufuta eneo la Mbalizi Halmashauri ya Mbeya, akiwa mzima lakini baada ya kuuza ufuta wakati akijiandaa kurudi aliombwa na watuhumiwa wakafanye mazungumzo.

Mhandisi Malambo amesema watuhumiwa walimtaka ndugu yao huyo wakazungumze naye kwenye moja ya bar zilizopo katika eneo la Kabwe Jijini Mbeya na alipofika katika eneo hilo, watuhumiwa hao, walimtaka awaache wadogo zake nje jambo lililofanyika.

Polisi Pwani Yawasaka Watu Wanne Wanaodaiwa Kupora Pikipiki

0
0
Mwamvua Mwinyi,Kibaha
JESHI la polisi mkoani Pwani,linawasaka watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao wanadaiwa kupora pikipiki eneo la Kidimu kata ya Pangani Kibaha Mjini .

Aidha jeshi hilo limewatahadhalisha madereva bodaboda kuacha kuamini abiria wanaokodisha pikipiki zao kwenda nje ya mji kwani sio wote ni abiria wema.

Akielezea juu ya tukio hilo,kamanda wa polisi mkoani Pwani Wankyo Nyigesa alisema kuwa ,watu hao wakiwa Kidimu kata ya Pangani,barabara ya Kibaha kupitia Mapinga kuelekea Bagamoyo walipora pikipiki ambayo mmoja wao aliikodi kutokea Mwanalugali Kibaha.

Wakiwa Kidimu walitumia gari Toyota IST rangi ya silver yenye namba za usajili T.355 DMA ambapo mmoja wao alikimbilia Mwanalugali na kukodisha pikipiki yenye namba MC 401 CDW aina ya hajoue ya bwana Amani Ambele.

Wankyo, anasema baada ya hapo jambazi huyo aliomba apelekwe Kidimu kwa sh.3,000 ambako Kidimu kulikuwa tayari na wenzie watatu wakiwa na gari yenyr namba T 355 DMA .

“Walipofika hapo abiria ambae ni anaedaiwa kuwa ni jambazi alimfunga kitambaa cheusi usoni na kumuingiza katika gari na kisha kuondoka na pikipiki”

“Bahati nzuri madereva boda wengine wa mjini Kibaha walipata taarifa na kuanza kulifukuzia gari hilo na walipolipata walilichoma moto na liliteketea huku majambazi hayo yakifanikiwa kukimbia”alifafanua Wankyo.

Wankyo alielezea kuwa, baada ya madereva bodaboda hao kuteketeza gari hilo kwa moto walitoa plate namba ,kadi ya gari na bima na kuwasilisha polisi.

Wakati huo huo kamanda huyo alisema jeshi hilo limejipanga kufanya misako ili kulinda raia na mali zao wakati wa sikukuu ya iddi el fitri.

Hata hivyo Wankyo,aliwaasa madereva kuacha kukiuka sheria za usalama barabarani wakati wa sikukuuu na kuacha kutumia vileo wakiwa wanaendesha.

Rais Magufuli azungumza na Makatibu Tawala Wilaya zote pamoja na Makatibu Tarafa Ikulu jijini Dar es Salaam

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano June 5

Urusi yakanusha kauli ya Trump kuhusu Venezuela

0
0
Ikulu ya Urusi mjini Moscow imekanusha kauli ya rais wa Marekani Donald Trump, kwamba inapanga kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Venezuela. 

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Trump aliandika jana kuwa amearifiwa na Urusi kuwa imewaondoa maafisa wake karibu wote kutoka Venezuela. 

Lakini msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov amesema hajui alichokimaanisha Trump, na kuongeza kuwa pengine kiongozi wa Marekani alikuwa akivinukuu vyanzo vya magazetini, kwa sababu Urusi haijatangaza kitu kama hicho. 

Alisema maafisa wa Urusi wanaendelea kuwepo nchini Venezuela, wakizifanyia matengenezo zana za kijeshi zilizoko huko. 

Mvutano umepanuka baina ya Marekani inayounga mkono kuangushwa kwa rais wa Venezuela Nicolas Maduro, na Urusi ambayo imeingilia kati kumkingia kifua kiongozi huo. Urusi imewapeleka maafisa wa jeshi wapatao 100 nchini Venezuela.

Waziri Mkuu: Tutumie Siku Ya Eid Kwa Kutenda Mema

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waislamu wote nchini watumie siku kuu ya Eid el Fitr kwa kutenda matendo mema pamoja na kuwakumbuka yatima na wajane.

“Leo ni siku kubwa na muhimu waislamu wanahitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, hivyo tuendeleze matendo mema.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 5, 2019) wakati aliposhiriki swala ya Eid El Fitr katika msikiti wa Anwar uliopo Msasani jinini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema wakati huu ni mzuri kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwenu na madhehebu mengine, hivyo hakikisheni mnayaendeleza mambo mema yote.

“Tumeona utulivu uliojitokeza katika mwezi mtukufu, na jambo hili limesisitizwa na viongozi wa dini. Tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikamano na tuvumiliane.”

Pia, Waziri Mkuu amewakumbusha wazazi na walezi kuwaongoza watoto kwa kuwapa mafundisho ya dini yatakayowawezesha kumjua Mwenyezi Mungu na kuwa raia wema.

Awali, Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mhina alisema waislamu wanatakiwa kuitumia siku ya leo kwa kuhamasisha Amani pamoja na kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo.

Pia amewasisitiza wayaendeleze mema yote waliyoyafanya katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu na kuwajali wazazi wao.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Wanne kizimbani kwa kuchapisha maudhui Youtube bila kibali

0
0
Serikali imewafikisha mahakamani watu wanne kujibu shtaka la kuchapisha maudhui katika mtandao wa YouTube bila kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Washtakiwa hao ni Charles Kombe (24) mkazi wa Mikocheni, John Chuwa (28), mkazi wa Baracuda, Amos Warema (27) na Raymond Mkoroka (30). Walipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Walisomewa mashtaka hayo mbele ya mahakimu mkazi wanne tofauti; Maira Kasonde, Janeth Mtega, Agustina Mbando na Augustine Rwizile.

Inadaiwa washtakiwa hao walichapisha mtandaoni maudhui hayo katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2018 na Mei mwaka huu, Dar es Salaam.

Mshtakiwa Kombe alisomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mbando ambapo Wakili wa Serikali, Elizabert Mkunde alidai alitenda kosa hilo kati ya Agosti mosi 2017 na Mei 21 mwaka huu katika maeneo tofauti Dar es Salaam.

Ilidaiwa alichapisha maudhui hayo kupitia mtandao wake wa YouTube  uitwao Charles Kombe bila kibali.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka na imedaiwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Kombe yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na wadhamini wawili waliosaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 5 kila mmoja. Kesi iliahirishwa hadi Julai 7, mwaka huu itakapotajwa.

Mshtakiwa Chuwa alisomewa shtaka mbele ya Hakimu Mkazi Kasonde na Wakili wa Serikali, Elizabert Mkunde.

Ilidaiwa alitenda kosa hilo katika terehe tofauti kati ya mwaka 2018 na Aprili 2019 Dar es Salaam.

Mshtakiwa anadaiwa kuchapisha maudhui kupitia mtandao wa Youtube uitwao John Film Entertainment bila kibali kutoka TCRA.

Alikiri kutenda kosa hilo na aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kujidhamini mwenyewe kwa dhamana ya maandishi ya  Sh milioni 5 pamoja na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya kiasi hicho cha fedha.

Kesi iliahirishwa hadi Juni 7 mwaka huu mshtakiwa atakaposomewa hoja za awali.

Mshtakiwa Warema ilidaiwa kuwa alitenda kosa hilo kati ya Novemba 2018 na Mei 17 mwaka huu katika maeneo tofauti Dar es Salaam.

Alisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mtega  na Wakili wa Serikali, Candid Nasua.

Anadaiwa alisambaza maudhui hayo kupitia mtandao wa Youtube uitwao Pro Media Tanzania bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Baada ya kusomewa, alikana shtaka hilo na aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kujidhamini na kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 3.

Kesi iliahirishwa hadi Julai 4, mwaka huu na upelelezi haujakamilika.

Mshtakiwa Mkoroka alisomewa shtaka na Wakili wa Serikali, Elia Athanas mbele ya Hakimu Mkazi Rwezile.

Ilidaiwa alitenda kosa hilo katika tarehe tofauti jijini Dar es Salaam na alikana shtaka.

Mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja na kujidhamini mwenyewe kwa kusaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 5. Kesi iliahirishwa hadi Julai 4 mwaka huu itakapotajwa.

Taarifa Ya Uteuzi Na Kupandishwa Vyeo Kwa Maafisa Waandamizi Wa Uhamiaji


Waziri Kigwangalla Aitaka Bodi Ya Utalii Tanzania Kutumia Njia Za Kisasa Za Mawasiliano

0
0
WMU - Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Dkt. Hamisi Kigwangalla ameitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iwekeze zaidi katika matumizi ya njia za kisasa za mawasiliano na mbinu rahisi zenye gharama nafuu kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.

Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Bodi hiyo iliyongezewa muda wa miaka 3 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Aprili 23 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuiongezea kipindi kingine cha miaka 3 na kuitaka bodi hiyo iendelee kubuni na kuongeza mbinu mpya za kutangaza utalii zitakazoleta tija na matokeo ya haraka.

Amewataka wajumbe wa Bodi hiyo kufanya kazi pamoja na kushirikiana na taasisi nyingine za Wizara ili kuongezea idadi ya watalii wanaoitembelea Tanzania akiweka msisitizo katika matumizi ya mifumo ya kisasa ya mawasiliano ili kupanua wigo wa kutangaza vivutio vya utalii kuliko ilivyo sasa.

“Bodi ya utalii mnapaswa kuona fursa zilizopo na kutimiza majukumu mliyopewa kwa tija na ufanisi zaidi, namna pekee ya kufikia malengo hayo ni lazima mtumie teknolojia na mbinu rahisi za mawasiliano  zenye gharama nafuu kutimiza majukumu yaleyale ya kutangaza vivutio vya utalii kisasa zaidi” Amesisitiza.

Ameipongeza bodi hiyo kwa kazi nzuri inayofanya ya kuendelea kuhamasisha shughuli za Utalii nchini na kuongeza kuwa kati ya vitu vilivyo iletea heshima sekta ya utalii Tanzania ni uwepo wa Kaulimbiu ya “TANZANIA UNFORGETTABLE” ambayo imekua chachu kwa taifa hasa katika kuitangaza sekta hiyo kitaifa na kimataifa.

Amesema kupitia kaulimbiu hiyo watalii wengi wanaoitembelea Tanzania wataendelea kukumbuka mambo mazuri na vivutio vizuri walivyoviona na kuendelea kuichagua Tanzania kuwa mahali pao pa kufanyia utalii.

Aidha, ametoa wito kwa Bodi hiyo kuendelea kuweka mazingira na kuongeza soko la bidhaa za utalii za Tanzania nje ya nchi kupitia maonesho ya kimataifa na kuwa na mkakati wa kulenga soko husika pamoja na kuonana na watu watakaouziwa bidhaa moja kwa lengo la kukamata soko katika maeneo kadhaa.

Pia ameitaka Bodi hiyo kuweka mkakati mahususi ya kukamata masoko mapya ya watalii kutoka nje ya nchi kutoka nchi za Marekani, Hispania, Urusi na nchi za Falme za Kiarabu zikiwemo za Dubai na Oman ambazo watu wake wakiwemo wasomi, wafanyabiashara, wanamichezo na watu maarufu wanapenda kwenda mapumziko ya muda mrefu na kutumia fedha nyingi kwa shughuli za utalii.

Katika hatua nyingine ameishauri Bodi hiyo kuwatumia watu maarufu na mashuhuri wakiwemo wasanii na wanamichezo watakaoalikwa mahususi kwa kazi maalum ya kutangaza utalii wa Tanzania.

“Licha ya changamoto ya ufinyu wa bajeti tunaweza kuweka mikakati ya kutangaza vivutio vyetu kwa tija na rahisi zaidi na kuifanya nchi yetu ijulikane na kuonekana na watu wengi , kuna mikakati tunaweza kuifanya mara moja tu ikadumu kwa muda mrefu, kama tukiwatumia watu mashuhuri wenye wafuasi wengi wakatembelea vivutio vyetu tuna uhakika watu wengi zaidi watafuatilia ziara zao na kufuata walichokichagua, lazima tuweke mikakati ya kuwaleta watu mashuhuri walau 5 kwa mwaka ambao sisi tutawaalika, tutapata mafanikio makubwa sana ndani ya muda mfupi” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constatine Kanyasu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo amemshukuru Rais kwa kuiongezea kipindi kingine cha miaka cha miaka 3.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka 3 imefanya kazi kubwa licha ya changamoto mbalimbali inazokabiliana nazo akisisitiza kwamba uwepo wa changamoto hizo ni uhalali wa kuwepo kwa bodi hiyo.

Amesema kuzinduliwa rasmi kwa bodi hiyo kutaifanya itekeleze majukumu yake kwa kasi kubwa zaidi akisisitiza kwamba kupitia bodi hiyo sekta ya Utalii Tanzania  itasonga mbele kwa kasi kubwa zaidi.

Mhe. Kanyasu ameitaka bodi hiyo iongeze juhudu ya kutangaza utalii na kupanua wigo wa kutangaza soko la utalii ndani na nje ya nchi akisitiza akisisitiza kwamba bado kuna mazao mengi ya utalii ambayo hayajavunwa na endapo bodi itafanya kazi yake ipasavyo Tanzania itapata mafanikio makubwa kiuchumi.

Naye Mwenyekiti wa Mwenyekiti  wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji (Mst) Thomas Mihayo akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa Bodi hiyo amemshukuru Rais hiyo nafasi nyingine akiahidi kwamba  bodi yake itafanya kazi kwa kasi na bidii zaidi ili kutimiza malengo ya kuitangaza Sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.

Jaji Mihayo amesema kuwa Bodi hiyo itaendelea kutekeleza majukumu yake chini ya uongozi wa Wizara na kuitangaza kikamilifu sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.

Bodi hiyo yenye wajumbe 6 iliongezewa muda wa kuhudumu wa miaka 3 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  Aprili 23, 2019.

MWISHO.

CAF Yathibitisha rasmi Tanzania kupeleka club nne michuano ya kimataifa 2019/2020

0
0
Shirikisho la soka Afrika CAF limetangaza rasmi kuwa Tanzania kuanzia msimu wa 2019/2020 itaanza kupeleka vilabu vinne katika michuano ya kimataifa inayoandaliwa na shirikisho hilo na sio timu mbili kama ilivyokuwa awali.

Tanzania imepata nafasi hiyo baada ya vilabu vyake kufanya vizuri kwa miaka ya hivi karibuni, kiasi cha kusababisha Tanzania kupata point nyingi zilizoiwezesha kupata nafasi hiyo, sasa katika michuano ya CAF Champions League itapeleka timu mbili msimu ujao na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika litapeleka timu mbili pia.

Suluhu Ya Tatizo La Ugumba Kwa Mwanamke Na Mwanaume ....Soma kwa Makini Makala Hii

0
0
Ugumba ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili (au kujamiana) bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12 na kutoweza kushika mimba au kupata ujauzito.

Kuna aina mbili za ugumba;
Ugumba wa asili (Primary infertility) - Hii ni pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi kutunguisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kujamiana au kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.

Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) - Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.

Asilimia 30-40 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.

Kwa wale wenye afya njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiana mara kwa mara kwa mwezi ni asilimia 25-30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini.

Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10.

Je mimba hutungwa vipi?
Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka katika moja ya viwanda vyake vya mayai ya kike yaani ovaries, kitendo hiki hujulikana kama ovulation.

Yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi inayojulikana kama mirija ya fallopian.

Mbegu moja ya kiume (sperm) ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea kwenye uterus.

Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo) hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kuwa kiumbe.

Tatizo la ugumba linaweza likawa ni la nwanaume au mwanamke pekee ingawa wakati mwingine wote wawili wanaweza kuwa na tatizo hili.

Ni sababu zipi zinazoleta tatizo la ugumba (infertility) ?

Kwa wanawake ;
Tatizo la ugumba linaweza kutokea wakati wa;
  1. Yai au kiumbe kilicho ndani ya mfuko (uterus) wa uzazi kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto.
  2. Mayai yaliyo ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining)
  3. Matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa uzazi (uterus).
  4.  Matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai (eggs).
Tatizo la ugumba kwa wanawake husababishwa na;
  1. Matatizo ya auto immune disorders kama antiphospholipid syndrome (APS)
  2.  Matatizo katika uterus na shingo ya kizazi (cervix) kama uvimbe (fibroids or myomas) na birth defects
  3.  Matatizo katika mfumo wa kuganda wa damu (clotting disorders).
  4. Mazoezi kupita kiasi (excessive exercise), afya iliyodhoofika (poor nutrition), matatizo ya kula (eating disoder).
  5.     Baadhi ya madawa au sumu.
  6.     Msongo wa mawazo (emotional stress)
  7.     Tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance)
  8.     Uzito uliopitiliza (obesity)
  9.     Unywaji pombe kupindukia (heavy alcohol intake)
  10.     Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari (diabetes)
  11.     Magonjwa ya kina mama (Pelvic inflammatory infection, PID)
  12.     Ovarian cysts and polycytic ovarian syndrome
  13.     Magonjwa ya zinaa (sexually transmitted disease, STD) au endometriosis
  14.     Saratani
  15.     Uvutaji sigara, madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk.
  16.     Matatizo ya hedhi - wanawake wanaopata hedhi bila kutoa mayai (anovulatory menstrual cycle)
  17.     Kuwepo kwa cervical antigens ambazo huua shahawa za mwanamume na hivyo kusababisha kwa mwanamke kutopata ujauzito.
Tatizo la ugumba - linaweza kutokea kwa mwanamume wakati wa;
  1.   Kupungua idadi ya mbegu za kiume  (decrease number of sperm)
  2.     Nguvu za kiume  kuzuiwa kutolewa (blockage of sperm)
  3.    Manii  ambazo hazifanyi kazi yake vizuri.

Kwa mwanamume, tatizo la ugumba husababishwa na;
  1.     Mazingira yaliyo na kemikali zinazoathiri uwezo wa mwanaume kumbebesha mimba mwanamke (environment pollutants)
  2.     Kukaa sehemu zenye joto kali sana kwa muda mrefu (exposure to high heat)
  3.     Matatizo kwenye mfumo wa viashiria vya asili (genetic abnormalities)
  4.     Unywaji pombe kupindukia, matumizi ya madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk, hupunguza idadi na kiwango (quality) cha shahawa .
  5.     Kuzeeka (older age)
  6.     Kutumia dawa za vichocheo vya mwilini (hormonal supplements) ama kukosekana kwa baadhi ya vichocheo mwilini (hormonal deficiency)
  7.     Kuasiliwa (impotance)
  8.     Magonjwa ya korodani (testicular infections) au kwenye mishipa ya korodani (epididymis)
  9.     Historia ya matumizi ya baadhi ya dawa za saratani
  10.     Magonjwa ya zinaa (STD), ajali (trauma) au upasuaji
  11.     Historia ya mionzi (radiation exposure)
  12.     Retrograde ejaculation (matatizo ya kukojoa au kutoa shahawa)
  13.     Msongo wa mawazo (emotional stress)
  14.     Uvutaji sigara
  15.     Matumizi ya baadhi ya dawa kama cimetidine, spironolactone, nitrofurantoin.
  16.     Varicocele
  17.     Mumps

Viashiria na vipimo vya ugumba (infertility)
Kwa wanaume;

  1.     Semen analysis - Kipimo hiki kinahusisha uchukuaji wa shahawa kutoka kwa mwanamume ambaye amekaa siku 2-3 bila kujamiana na kuzipima kujua wingi, kiwango chake, shepu zake, viscosity of semen, motility and swimming speed.
  2.     Testicular biopsy - Kipimo cha korodani

Kwa wanawake;
  1.  Kipimo cha kiwango cha vichocheo kwenye damu (blood hormone levels)
  2.  Cervical mucus detection - Kipimo cha kuangalia kamasi za kwenye shingo ya kizazi ili kupima jinsi zinavyovutika (stretch), na kama ni za majimaji (wet) wakati wa mzunguko wa hedhi, na kama zina utelezi ambao huusishwa na ovulatory phase
  3.  Kipimo cha kiwango cha joto mwilini (body basal temperature) - Kuongezeka kwa kiwango cha joto kwa 1 degree kutoka kiwango cha joto cha kawaida cha binadamu (37 C) kinahusishwa na ovulation ambapo mwanamke ana asilimia kubwa ya kushika ujauzito au yai limetolewa na ovaries.
  4.  Postcoital testing - Kupima kamasi za shingo ya kizazi (cervical mucus) zilizochukuliwa masaa 2-8 baada ya wapenzi kujamiana ili kuangalia mwiingiliano wa shahawa na kamasi za shingo ya kizazi.
  5.  Kipimo cha kichocheo aina ya progesterone kwenye damu (serum progesterone testing)
  6.  Kipimo cha ukuta wa uterus (biopsy of uterine lining or endometrium)
  7.  Kupima kichocheo aina ya Luteinizing hormone kwenye mkojo ili kuweza kutabiri lini yai litatolewa na ovaries ili kupangilia siku za kujamiana kwa wapenzi.
  8. Hysterosalpingography (HSG) - Kipimo cha X-ray kinachotumia dawa maalum (contrast dye) inayoonyesha njia ya shahawa kutoka kwenye shingo ya kizazi kupitia ndani ya mfuko wa kizazi (uterus) na kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes).
  9.     Laparascopy - Direct visualization of pelvic cavity
  10.     Progestin challenge
  11.     Pelvic exam-hufanywa na daktari.

Tiba ya tatizo la ugumba (infertility)
 
Tiba ni kama ifuatavyo;
1.Ushauri nasaha na kuwaelimisha wapenzi wawili - Matatizo mengi ya ugumba hutokea kutokana na uelewa au ufahamu mdogo wa elimu ya uzazi na ya kujamiana kwa wapenzi au wanandoa.

Kuna wanaume wengi ambao hufika kilele haraka wakati wa kujamiana na hivyo kutoa mbegu mapema (au kukojoa) kabla ya muda muafaka (premature ejaculation), hii husababisha kutopata ujauzito ambapo lawama zote hupelekwa kwa mwanamke pasipo mwanamume kugundua kuwa tatizo ni lake.

Ifahamike kwamba hakuna muda uliotengwa ambao ni muafaka wa kufika kilele au kukojoa kwa mwanamume lakini watafiti wa mambo ya kujamiana wanashauri angalau mwanamume afike au akojoe baada ya dakika 15 na kuendelea. Hivyo ni bora kwa wapenzi kujiandaa kisaikolojia mwanzo na kuchezeana kabla ya kuanza kujamiana ili kurefusha muda kwa mwanamume.
 
2.Tatizo jengine ni kutofahamu lini hasa ni muda muafaka wa kujamiana ili kushika mimba kwa urahisi. Kuna wanawake ambao hawajui hata mzunguko wao wa hedhi (yaani hawajui wanaanza na kumaliza hedhi lini na wakati wa hedhi wanatumika kwa muda wa siku ngapi). 

Ongeza nafasi yako ya kushika ujauzito kwa kujamiana angalau mara 3 kwa wiki kuelekea wakati wa ovulation au kujamiana wakati wa kipindi chote cha ovulation. Ovulation hutokea wiki 2 kabla ya mzunguko wako mwengine wa hedhi, kama una mzunguko wa hedhi wa siku 28 (yaani kila baada ya siku 28 unapata hedhi), ni vizuri kujamiana angalau kwa siku 3 kati ya siku ya 7-18 baada ya kupata hedhi.
 
3.Kupunguza kunywa pombe kupindukia, kuvuta sigara, kuacha matumizi ya bangi, kokeni nk.
4.Kupunguza kiwango cha mazoezi kwa wanawake.
5.Kupunguza unene uliopitiliza
6.Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu kwani kuwa na wapenzi wengi huongeza athari ya kupata magonjwa ya zinaa.
7.Kuacha tabia ya kuvaa nguo nzito au zenye kuleta joto kali sehemu za siri kwa wanaume kwani joto kali sana hupunguza kiwango na kuathiri utolewaji wa mbegu
8.Kula mlo kamili na wenye virutubisho vyote muhimu kwa afya njema.
9.Dawa za kutibu magonjwa kwenye mfumo wa uzazi, magonjwa ya zinaa nk.
10.Njia za kitaalamu za kupata ujauzito zijulikanazo kama in vitro fertilization na intrauterine fertilization.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

MAKALA: Mbinu Za Kupanga Jinsia Ya Mtoto Wakuzaa ( Mvulana Au Msichana ) Kabla Mkeo Hajashika Mimba

0
0
Mpendwa  msomaji  wetu, Maada  yetu  nyingine  ya  leo  ni  mbinu za kupanga  jinsia  ya  mtoto  wa  kuzaa  kabla  mkeo  hajashika  mimba....

Siku  hizi  ulimwengu  umeendelea  sana, matatizo  mengi  yanatibika  kwa  msaada  wa  wataalamu...Hakuna   tena  haja  ya  kupigana  na  kupeana  talaka  kisa  jinsia  ya  mtoto...

Somo letu   la  leo  litajikita  zaidi  katika  mbinu  za  kuzaa  mtoto  wa  kike. 


Ni vipi jinsia ya mtoto huainishwa?
Kinyume na wengi wanavyofikiria kwamba mwanamke au mwili wa mwanamke ndio wenye jukumu la kuainisha jinsia ya mtoto kwa kuwa yeye ndiye anayebeba mimba, uhakika wa mambo ni kuwa mwanamume ndie mwenye uwezo wa kuainisha jinsia.
 
Kila yai la mwanamke lina chromozomu mbili za X. Iwapo manii ya mwanamume au spemu(ambayo ina chromozomu X na Y) itakuwa na X na kurutubisha yai la mwanamke lenye X tupu, basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mwanamke.
 
Vilevile iwapo spemu ya mwanaume itakuwa na Y na kurutubisha yai la mwanamke lenye X, basi mtoto atakayezaliwaatakuwa mwanamume.
 
Hivyo kwa kufahamu suala hilo, ni matumaini yetu kuwa vile visa vya kinamama kuachwa eti kwa kuwa hawakuzaa watoto wa kiume au wa kike vitapungua katika jamii zetu. Mke wako asipozaa mtoto wa jinsia uitakayo, usifikiri kuwa yeye ndiomwenye makosa.
 
Wakati mwanamume anapomwaga mbegu, spemu kati ya milioni 200 hadi 400 humwagwa katika uke wa mwanamke. Baadhi ya spemu hizo huwa zina chromozomu X na baadhi zina chromozomu Y.
 
Hata hivyo, ni spemu moja tu ambayo hutakiwa kwa ajili ya kurutubisha yai la mwanamke nakuunda mimba.
 
Nadharia mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia kuchagua ni jinsia gani unaitaka awe nayo mwanao, zinategemea suala la kuandaa mazingira katika uke na mwili wa mwanamume na mwanamke,yatakayosaidia spemu ya baba yenye chromozomu inayotakiwa irutubishe yai la mama, na hivyo kutungwa mimba ya jinsia inayotakiwa.
 
Njia ya Dr. Shettles ya kuzaa mtoto wa kike
Njia hii imekuwa ikitumiwa na watu wengi kwa miaka mingi sana na imewasaidia kuweza kuzaa mtoto wa kike.
 
Wengi wanasema kuwa uwezekano wa kufanikiwa njia hii ni asilimia 90. Njia ya Dr. Shettles inategemea msingi kwamba, chromozomu Y (yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kiume) ni ndogo na yenye kwenda kwa kasi zaidi ikilinganishwa na chromozomu X(yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kike) ambayo ni kubwa na huenda polepole.
 
Pia kwa kutegemea kuwa chromozomu X inaishi muda mrefu zaidi kuliko ile ya Y.Hivyo Dr. Shettles anashauri kuwa iwapo unataka kuzaa mtoto wakike uhakikishe kuwa:
 
1.Unajamiiana siku 2 au 3 kabla ya Ovulation. Kinadharia spemu za kiume zitakuwa zimeshakufa hadi kufikia siku hasa ya Ovulation na kuziacha spemu za kike zikiwa hai tayari kurutubisha yai na kuunda mtotowa kike.
 
2.Anashauri pia wanawake wajizuie kufikia kileleni (orgasm) kwani hali hiyo itaufanya uke uwe na hali ya asidi ambayo ni kwa faida ya spemu ya kike yenye chromozomu X.
 
3.Pia anawashauri wazazi wanapojamiina wawe katika haliya mwanamke kulala chini na mwanamume juu au missionary position. Kwani anasema kuwa mtindo huo huziwezesha spemu zenye chromozamu X zimwagike karibu na mlango wa uke na kuwa na uwezekano mkubwa wa kuingia ukeni na kutungwa mimba.
 
Kuna wengine wanaamini kwamba baadhi ya lishe na vyakula vya aina mbalimbali husaidia kutunga mimba ya mtoto wa kike.
 
Kwa mfano kuna wanaoamini kuwa kula baadhi ya vyakula huufanya uke uwe na hali ya asidi ambayo husaidia Chromozomu Y ife katika uke.
 
Nadharia nyingineyo inayotumiwa katika kuchagua jinsia ya mtoto inasema kwamba,mwanamke anayetaka kubeba mimba ya mtoto wa kike ale vidonge vya virutubisho (supplements) vya Calcium na Magnessium mwezi mmoja kablaya kubebea mimba.
 
Iwapo unataka kutumia vidonge vya virutubisho ili uweze beba mimba ya mtoto wa kike, ni bora ushauriane na daktari wako kwanza.
 
Hii ni kwa sababu dawa hizo huweza kuingiliana na dawa nyinginezo za magonjwa mbalimbali.
 
Baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa vinasaidia katika kutunga mimba ya mtoto wa kike ni.
 
-->>>Mahindi, nyama, maharagwe, samaki, tunda damu, mayai na maini.
 
Vyakula hivyo ni vya asidi hivyo huifanya PH ya mwili wako hupungua na kuwa ya acidi. Hali hiyo husaidia kuua spemu za Y na hivyo kusaidia kuzifanya spemu za X ziwe na uwezekano mkubwa wa kurutubisha yai.
 
Hivyo mwanamke anayependelea kubebea mimba ya mtoto wa kike anashauriwa kutokula vyakula vyenye alikali ambavyo ni kama, ndizi, chokleti, juisi ya machungwa, viazi, tikiti maji na vinginevyo.

Wafanyabiashara Wa Viwanda Vya Kukoboa Na Kusaga Nafaka Ibinzamata Manispaa Ya Shinyanga Wamlilia Waziri Kalemani.

0
0
Wafanyabiasha wa viwanda 14 vya kusaga na kukoboa Nafaka  katika  eneo la Ibinzamata Katika manispaa ya shinyanga wakosa umeme kwa muda wa wiki mbili  na kusababisha kupata hasara huku Takribani wafanyakazi 30 waliokuwa wakifanyakazi zisisizo rasim kama vile mamalishe wakikosa ajira .

JOSEPHATI MICHAEL ni mmoja  wa wamiliki viwanda vidogo vya  kusanga na kukoboa nafaka, amesema kuwa katika kipindi hiki cha sikukuu ya idi wameshandwa kuzalisha Unga na mchele kutokana na kukosa huduma ya umeme kwa muda mrefu na kusbabisha bidhaa za mchele na unga kupanda bei.

Amesema Tatizo la kukatika kwa  umeme kwenye eneo hilo limekuwa ni sugu kwani limekuwa  likijitokeza mara kwa mara kutokana na uwezo mdogo wa mashine ya kupoza umeme(TRANSIFOMA) huku Shirika la umeme mkoa wa shinyanga likiwa halijalipatia ufumbuzi suala hilo.

Amefafanua kuwa  ,wamekuwa wakitoa taarifa mara kwa mara kwa uongozi wa Shirika la umeme Tanesco Mkoani Shinyanga,lakini hakuna ufumbuzi wa jambo hilo ambalo linakwamisha shughuli za uzalishaji mali kwa kuunga mkono kauli mbio ya Rais Magufu ya serikali ya viwanda.

Kwa upande wake  Kundi Malabari ambaye ni mmiliki wa kiwanda cha kukoboa mpunga amesema wameamua kupaza sauti kwa  waziri wa Nishati Dkt.Medadi Kalimani ili kuingilia kati ili kulipatia utatuzi suala hilo linalokwamisha ukuaji wa uchumi katika eneo hilo.

Amesema Wao wamefungua  viwanda kuumnga mkono Rais Magufuu katika sela ya viwanda,lakini wamekuwa wakikatishwa tamaa na tatizo la ukisefu wa umeme usio kidhi mahitaji yeto

Nae Diwani wa kata ya Ibinzamata DANIEL MATEM amesema kuwa, eneo hilo limekuwa sugu kwa umeme kukatika mara kwa mara na kuitaka shirika la umeme Tanzania kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo sugu ili kuendelea na shughuli za uzalishaji na kunusuru ajira za walialikwa.

Amefafanua kuwa , eneo hilo linamashine 14 ambazo zimetoa ajira rasmi na zisizo ramsi ambazo ni wakoboaji, wafanyabiashara wa chakula, wabeba mizigo, wamiliki wa viwanda nakudai kuwa makudni yote hayo kwasasa hayafanyi shuguli za uzalishaji.

Akijibu Malalamiko ya wafanyabiashara hao  Meneja wa Tanesco Mkoa wa Shinyanga FEDGRACE SHUMA amesema kuwa, kwasasa tatizo lililojitokeza ni mashine ya kupozea umeme kwenye eneo hilo kuharibika na juhudi za kutafuta mashine nyingine zinaendelea ili kuhakikisha huduma inarejea kama ilivyokuwa hapo awali.

Maafisa Usalama Feki (Batili) Wanaswa Kahama Wakitapeli Mfanyabiashara

0
0
JESHI la Polisi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawashikilia watu wawili kwa kujiwasilisha kuwa wao ni maafisa wa idara ya usalama wa Taifa (TSI) kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.

Watu hao ni Mrisho Zabroni (37) na Mgema Patrick (25) ambao walikwenda kwa mmoja wa wafanyabiashara wilayani hapa Abdallah Moro ambae ghala lake la kuhifadhia bidha ambalo lilifungwa na Mamala ya chakula na Dawa(TFDA)

Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kuwa,watuhumiwa hao walikamatwa juzi baada ya jeshi la polisi kuwawekea mtego na kufanikiwa kuwakamata.

Amefafanua kuwa , siku ya tukio watu hao walifika kwenye ghala ya mfanyabiashara huyo na kujitambulisha kwake kuwa ni maafisa usalama wa Taifa na kumwomba rushwa kiasi cha shilingi Milioni tatu ili waweze kumsaidia kufungua ghala lake ambalo lilifungwa na TFDA.

Kamanda ABWAO amesema MORO alitoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya watu hao walifika kwake na kujitambulisha  kuwa wao ni maafisa usalama wa Taifa na wanauwezo wa kumfungulia ghala ambao lililokuwa limefungwa na TFDA na kumuomba fedha hizo kama Rushwa ili kufanikisha zoezi hilo.

Sanjari na hilo kamanda ABWAO amewataka wananchi na wafanyabiashara wote kuwa makini na watu wanafika kwenye biashara zao hasa maafisa ukaguzi pindi wanapofungiwa maghala yao na kujiwasilisha kwao kuwa ni maafisa usalama wa Taifa waweze kutoa taarifa ili wachukulie hatua za kisheria.

Ameongeza kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ambao zinawakabili.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 6

Uteuzi Wa Wagombea Udiwani Katika Kata 32 Za Tanzania Bara

0
0
Tarehe 31 Mei, 2019, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza kuwa ni siku ya uteuzi wa wagombea katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata Thelathini  na mbili (32) za Tanzania Bara. Uteuzi huo ulifanyika kama ilivyopangwa.

Katika Kata hizo Thelathini na mbili (32), jumla ya wagombea 98 kutoka katika Vyama kumi na nne (14) vya Siasa walichukua Fomu za Uteuzi.  Vyama hivyo ni pamoja na AAFP, UMD, ADA – TADEA, CCK, CCM, CHADEMA, CUF, DEMOKRASIA MAKINI, NCCR - Mageuzi, NRA, SAU, TLP, UDP na UPDP.

Hadi muda wa mwisho wa uteuzi tarehe 31 Mei, 2019 saa 10: 00 jioni kati ya wanachama 98 waliochukua fomu za uteuzi, 41 walirejesha fomu hizo, kati ya hao 27 walikidhi vigezo na kuteuliwa kuwa wagombea. Wanachama wengine watano (5) hawakuteuliwa kuwa wagombea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kurejesha fomu za uteuzi nje ya muda, kukosa uthibitisho wa malipo ya dhamana na wagombea kuwa na idadi pungufu ya wadhamini. 

Jumla ya wagombea Watano (5) wa nafasi ya Udiwani waliwekewa pingamizi kwa Msimamizi wa Uchaguzi na hivyo kupelekea wagombea wawili (2) kuenguliwa kutoka katika orodha ya wagombea wa nafasi ya Udiwani.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Ipole iliyopo Halmashauri ya Wilaya Sikonge kupitia Chama cha Wananchi CUF, na malalamiko kutoka kwa wagombea wa CHADEMA na CUF katika Kata ya Murangi  iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Malalamiko yao ni dhidi ya maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi ya kuwaondoa kwenye orodha ya wagombea udiwani.

Tume katika kikao chake kilichofanyika leo tarehe 4 Juni, 2019 kimetoa maamuzi kama ifuatavyo:-

Kwanza, Tume imekubali rufaa moja ya mgombea Udiwani wa CUF katika Kata ya Ipole Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na hivyo kumrejesha kuendelea kuwa kugombea katika nafasi hiyo.

Pili, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi katika Kata ya Murangi  iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya kuwaondoa Wagombea wa CUF na CHADEMA katika orodha ya wagombea na hivyo Wagombea kuendelea kuenguliwa kugombea Udiwani.

Katika Uteuzi huu wa Udiwani katika Kata thelathini na mbili (32, jumla ya Wagombea udiwani katika Kata 29 wamepita bila kupingwa, na mgombea wa CUF kutoka Kata ya Kyaitoke Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na mgombea wa ACT –Wazalendo kutoka Kata ya Boma iliyopo katika Halmashauri ya Mji  Mafinga wamejitoa kwenye kinyang’anyiro hicho, hivyo Kata moja (1) ndio itakayofanya uchaguzi hapo tarehe 15 Juni, 2019, kata hiyo ni Ipole Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.

Kampeni za uchaguzi zimeshaanza kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi na zitaendelea hadi tarehe 14 Juni, 2019 ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya Uchaguzi.

Taarifa zaidi kuhusu walioteuliwa inapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya www.nec.go.tz na Ofisi za Tume Makao Makuu.

Imetolewa  tarehe 4 Juni, 2019.
Dr. Athumani Kihamia
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Lazaro Nyalandu: CHADEMA itashinda majimbo yote Singida Uchaguzi Mkuu wa Mwakani

0
0
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lazaro Nyalandu, amedai kuwa mwaka 2020, chama hicho kitarejesha majimbo yote ya Mkoa wa Singida ikiwamo jimbo alilokuwa akiliongoza la Singida Kaskazini.
 
Akizungumza katika Kijiji cha Ikungi mkoani Singida  wiki iliyopita, kada huyo alisema kutokana na kazi ya kujenga chama katika mkakati maalum unaofahamika katika chama hicho kama ‘Chadema ni msingi, chama hicho kitaibuka na ushindi katika majimbo yote ya mkoa wa Singida.

“Kama vile huu mkoa wa Singida ulivyokuwa na watu wawili maarufu yupo Tundu Lissu na yupo Nyalandu, sasa timu hii inacheza pamoja ,tutaichukua Singida Mashariki tena, tutaichukua Singida Kaskazini kwa mara ya kwanza ,tutashinda Singida Magharibi, majimbo yote mawili ya Iramba na Itigi”, Nyalandu alisema.

Kada huyo wa Chadema ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Singida Kaskazini na Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya awamu ya nne, hivi karibuni alikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wenzake wawili akituhumiwa kwa rushwa na mikutano iliyokatazwa na Serikali.

Kundi la IS ladai kuhusiaka na mashambulizi ya Msumbiji

0
0
Kundi linalojiita dola la Kiislam kwa mara ya kwanza limedai kuhusika na uasi nchini Msumbiji lakini wataalam wametilia shaka madai hayo na polisi ya Msumbiji imepuuza taarifa hiyo. 

Uasi wa makundi ya itikadi kali umekuwa ukiongezeka katika jimbo la kaskazini ya Msumbiji la Cabo Delgabo tangu mwaka 2017 ambapo zaidi ya watu 200 wameuwawa na vijiji kuchomwa moto. 

Kulingana na kampuni moja inayofuatilia shughuli za makundi ya itikadi kali, kundi la IS limelitoa taarifa yake hapo jana likidai kuhusika katika makabiliano ya bunduki na jeshi la Msumbuji yaliyotokea hivi karibuni katika jimbo la Cabo Delgado. 

Wapiganaji wa itikadi kali wamekuwa wakivishambulia vijiji na kuua watu mara kwa mara licha ya uwepo wa askari wengi wa polisi na jeshi katika jimbo hilo linalopakana na Tanzania. 

Polisi ya Msumbuji imepuuza madai hayo ya kundi la IS yaliyotolewa wakati Waislam duniani wanasherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Wanafunzi watano wazama ziwa Victoria Wakisoma

0
0
Wanafunzi watatu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Makurugusi iliyopo Chato mkoani Geita, wamepoteza maisha kwa kuzama katika Ziwa Victoria baada ya mtumbwi waliokuwa wamepanda kupinduka.

Walikuwa ziwani wakifanya mradi (project) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuhitimu kidato cha nne.

Mradi wao ulikuwa unahusu ongezeko la watu na athari za mazingira katika eneo la mwalo wa Matofali Kibunda, Kata ya Makurugusi, ambao waliuanza Mei mosi na walikuwa wawasilishe ripoti yao kesho.

Akitoa ufafanuzi juu ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo, aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Atha Gabriel (19), Manyencha Faustin (18) na Masalu Hamis (22).

Kamanda Mwabulambo alisema wanafunzi watano wakiwa kwenye mafunzo yao ya mradi, walitamani kutembelea mandhari ya ziwa hilo, wakaamua kukodi mtumbwi ili kufanya utalii wa ndani.

Alisema walipanda mtumbwi ambao dereva alikuwa Daud Thomas na wakati wakiwa umbali wa mita 120 kutoka ufukweni, mmoja wao, aliyejulikana kama  Samson Kano  alivua nguo na kutumbukia majini kwa nia ya kuogelea.

Kamanda Mwabulambo alisema kuwa mwanafunzi huyo alipotaka kurudi katika mtumbwi, alivuta ukingo wa mtumbwi huo na ndipo ulipoegemea upande huo na kupinduka.

 “Mtumbwi ulipopinduka wanafunzi wote walizama na kati yao watatu walizama  kabisa, huku wengine wawili wakifanikiwa kuogelea na kutoka,” alisema.

Kamanda Mponjoli aliwataja waliookolewa kuwa ni Abiana Fitina (19) ambaye pia alikunywa maji mengi na hali yake sio nzuri na mwingine ni Yohana Yamonda (19).

Alisema harakati za kuwaokoa zilifanyika chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mtemi Msafiri, Mkuu wa Polisi wa Wilaya na wananchi ambazo zilichukua siku nzima ya juzi hadi miili kupatikana saa 11 jioni.

Kamanda Mwabulambo aliwaonya wananchi watumiao vyombo vya majini kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni za usafiri huo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images