Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Wa Uingreza Theresa May Ajiuzulu

$
0
0
Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kuwa atajiuzulu Juni 7, 2019, baada ya kuliongoza taifa hilo kwa miaka 3. 

Kiongozi huyo ambaye ni mwanamke wa pili kushika wadhifa huo amekuwa akikumbana na upinzani mkali kuhusu makubaliano ya kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya (EU). 

Katika taarifa iliojaa hisia alioitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.

Amesema ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya

Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.

Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.

Video Mpya: Masanja Mkandamizaji – Short And Clear

$
0
0
Video Mpya: Masanja Mkandamizaji – Short And Clear

Video Mpya:Harmonize - Never Give Up

$
0
0
Video Mpya:Harmonize - Never Give Up

Sugu aitaka Serikali kupunguza tozo hotelini......Ashauri Hoteli Mpya Zipewe Miaka Miwili

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi (Chadema) maarufu Sugu ameitaka Serikali kupunguza tozo kwenye Hotel kwani zimekuwa zikiwarudisha nyuma wafanyabiashara.

Mbilinyi ametoa kauli hiyo leo Mei 24 bungeni wakati akichangia Mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2019-2020.

Mbilinyi amesema tozo zinazotozwa kwenye hotel nchini zimekuwa nyingi hivyo ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iziondoe ili wafanyabishara wenye biashara zao ziweze kukuwa.

“Kuhusu Tozo zimekuwa nyingi, umekaa tu mara wanapiga hodi anasema anatoka sehemu fulani,amefuata tozo, hotel mpya mzipe miaka miwili bila tozo ili wakuze biashara zao.Niiombe Serikali itoe hizo tozo zimejaa sana ndio maana biashara hazikuwi,”amesema Mbilinyi.

Dr. Mwakembye Avitaka Vyombo Vya Habari Kuweka Sera Madhubuti Katika Kutetea Na Kutangaza Mafanikio Ya Maendeleo Ya Afrika

$
0
0
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amevitaka vyombo ya habari vya Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kutangaza na kuandika habari za kweli ili kujitofautisha na vyombo vya Nje ya Bara hilo ambavyo upotosha na kubeza kwa makusudi mambo mazuri yanayotekelezwa na yaliyotekelezwa na Nchi za Afrika.

Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Mawasiliano Barani Afrika leo Ijumaa (Mei 24, 2019) Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe alisema vyombo vya Habari vya Afrika havina budi kuonyesha udhubuti kwa kuweka sera zinazoakisi maendeleo na kuyatangaza kwa Wananchi wake na wote waliopo nje ya Bara hilo.

Dkt. Mwakyembe alisema sehemu kubwa ya maudhui ya Vyombo vya Habari vilivyopo nje ya Bara la Afrika vinavyoongozwa na Wakoloni waliowahi kutawala katika Bara la Afrika hawapendi kuona Nchi za Afrika zinapiga hatua za Maendeleo kwa wananchi wake na badala yake hupenda kuripoti na kutangaza mambo mabaya yanayohusu Afrika ikiwemo njaa, magonjwa, vurugu za kisiasa, vita n.k.

Aidha Dkt. Mwakyembe alisema yapo mambo mazuri ya Maendeleo yanayofanyika katika Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambayo zimepiga katika kipindi cha miaka minne imepiga hatua kubwa katika Maendeleo ya kiuchumi, na miundombinu, jambo ambalo baadhi ya vyombo vya habari vya Mataifa ya Nje ya Afrika yamekuwa hayapendi kuyatangaza, hivyo ni wajibu wa vyombo  vya habari kutumia majukwaa yao kutetea na kutangaza mafanikio hayo.

“Wakati Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Kenneth Kaunda wa Zambia walipoamua kujenga Reli ya Tazara, walipingwa vikali sana Wakoloni waliotuwala na wengine waliita reli ile kuwa ni bamboo (mianzi) lakini ni taifa moja tu la Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China walitusaidia na leo hii reli ile ndiyo ndefu zaidi katika Bara la Afrika yenye urefu wa kilometa 1860” alisema Dkt. Mwakyembe.

Kwa mujibu wa Waziri Mwakyembe alisema Maendeleo ya Bara la Afrika yatatetewa na kupiganiwa na Wafrika wenyewe, hivyo ni wajibu wa vyombo vya habari vya Bara hilo kujitokeza na kutetea Maendeleo hayo na kamwe haitatokea siku moja chombo cha habari cha BBC au CNN vikatangaza mafanikio hayo kwani hawapendi kuona Mataifa waliyoyatawala yakifikia hatua kubwa za kimaendeleo.

Akifafanua zaidi Dkt. Mwakyembe aliwataka Vijana wa Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kujifunza historia ya Bara lao ili kuweza kufahamu wapi walipotoka na wapi wanapoelekea badala ya kupenda kulalamika pasipo na kuweka mikakati ya namna bora ya kupiga hatua za kujietea Maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi.

Waziri Mwakyembe alisema ni wajibu wa Taasisi mbalimbali za Habari na Mawasiliano zilizopo katika Bara la Afrika kujenga mifumo imara ya mawasiliano ikiwemo kutumia vyema mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuchapisha habari zinazohusu masuala ya maendeleo badala ya kutumia majukwaa hayo kuandika mambo yasiyo na faida wala tija kwa mataifa yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, alisema Serikali imeendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi za mawasiliano katika sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa wanajenga daraja moja katika kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo ya sekta ya habari na Mawasiliano nchini.

Naye Rais wa Chama cha Maafisa Uhusiano wa Sekta binafsi Tanzania (PRST) Loth Makuza alisema, taasisi hiyo ni jukwaa huru linalotoa fursa na nafasi ya kujadili masuala mbalimbali ya mawasiliano nchini ikiwemo changamoto na utatuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya habari na mawasiliano nchini.

Anaongeza kuwa Taasisi hiyo kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imeweza kutengeneza majukwaa mbalimbali yanayotangaza masuala mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofikiwa katika Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania, lengo likiwa ni kubadili mtazamo hasi wa Bara la Afrika katika nyanja za kiuchumi, kijamii kupitia ngazi ya kimataifa na duniani kwa ujumla.

Waziri Ummy Atoa Rai Kwa Viongozi Wa Dini Pamoja Na Wazazi Kushirikiana Na Serikali Kutoa Elimu Juu Ya Malezi Ya Watoto

$
0
0
 Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,jinsia Wazee na Watoto  Mhe.Ummy Mwalimu ametoa Rai kwa viongozi wa Dini,Taasisi pamoja na wazazi kushirikiana na Serikali  kutoa Elimu juu ya Malezi bora ya Watoto ili kupunguza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto vinavyofanywa na watu wa karibu ikiwa ni pamoja na ulawiti. 

Mhe.Ummy ametoa Rai hiyo,Leo Mei 24,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la  Nyongeza la Mbunge wa Rombo Joseph Selasini aliyehoji kuwa watoto wananyanyaswa kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kulawitiwa ni lini serikali itatembelea mashuleni ili kuweza kutoa elimu dhidi ya unyanyasaji na kulawitiana kwa watoto. 

Katika majibu yake,Waziri Ummy amesema pamoja na majukumu ya kila siku kwa wazazi wanatakiwa kuwakagua mara kwa mara watoto wao huku akiomba viongozi wa dini kusaidia kuhubiri kwani sheria peke yake haiwezi kumaliza tatizo hilo. 

Aidha ,Waziri Ummy amesema serikali imekuwa ikifanya mikakati mbalimbali katika kudhibiti vitendo vya  Ukatili kwa wanawake na watoto kwa kutoa elimu ambapo pia kuna namba ya bure ambayo ni 116 husaidia kwa watu wanaofanyiwa vitendo hivyo kuwasiliana na mamlaka husika na kuna zaidi ya madawati  ya kijinsia 350   hapa nchini. 

Hata hivyo,Waziri Ummy amesema kuanzia Tarehe 16 Juni,2019 ambayo ni siku Muhimu ya Mtoto wa Afrika serikali itazindua ajenda ya kitaifa kuhusu wajibu wa Mzazi katika Malezi ya Mtoto.

 

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

$
0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0757996194 au 0717339771

Serikali Kuwajengea Uwezo Mafundi Sanifu (Majengo) Na Mafundi Michundo Kupitia Miradi Inayotekelezwa Nchini.

$
0
0
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Serikali Kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imesema kuwa itaendelea kuwajengea uwezo na uzoefu mafundi sanifu na mafundi Michundo, ili waendelee kutekeleza kazi zao kwa ufanisi na kuongeza wataalam katika kada hiyo kwani fani hizo zina watu wachache. 

 Akizungumza  Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wasanifu Majengo na mafundi Michundo, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Dkt. Elius Mwakalinga alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imejikita katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa miundombinu unafanikiwa kwa kiasi kikubwa. 

“Serikali imedhamiria kujenga miundombinu ili kuwezesha ukuaji wa Sekta ya Viwanda nchini, hivyo Mafundi sanifu wanategemewa sana katika kuwezesha miundombinu hii, ili Tanzania iweze kufikia ndoto ya kuwa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda, na katika kutekeleza hilo mwaka wa Fedha 2019/2020, Wizara ya Ujenzi imejikita katika ajenda tatu ikiwemo kuwajengea uwezo wasanifu na wahandisi wote nchini”, Alisema Dkt. Mwakalinga. 

Dkt. Mwakalinga alisema kuwa Serikali inahakikisha watalaam chini ya Taaluma ya Uhandisi, Usanifu Majengo, Ukadiriaji Majenzi na kada zingine katika sekta ya ujenzi wanaongezeka kiidadi na kujengewa ujuzi mahsusi ili kuwa na uwezo na kumudu mahitaji ya nchi ya wataalam hao. 

Aidha, Dkt. Mwakalinga aliwathibitishia kuwa serikali inaendelea kushirikiana na bodi mbalimbali za taaluma za kihandisi kwa kutoa miradi inayotekelezwa nchini ili kuwawezesha watalaam hao kupata uzoefu na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kazi hiyo itaanza rasmi mwaka wa fedha 2019/2020, Julai Mosi. 

“Napenda niwadhihirishie kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya uongozi wa Rais Magufuli, inayo dhamira ya dhati ya kuendeleza fani ya usanifu kwa kutumia miradi yake inayotekelezwa, kama vile ujenzi wa Reli ya kisasa, SGR, Ujenzi wa Interchange Ubungo, Ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha umeme mto Rufiji, na ujenzi wa Daraja la Selander, kwa hiyo miradi hii itaweza kutoa uzoefu mkubwa kwa wataalum wetu”, alisema Dkt. Mwakalinga. 

Katika kuongeza uzoefu wa watalaam hao, Dkt Mwakalinga amesema ni lazima kuwepo na maarifa na vitendea kazi ambavyo kwa sasa ni uwepo wa miradi ya kimaendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali na sasa mafundi sanifu wanahitajika ili kuiwezesha miradi hii kutekelezwa pasipo gharama kubwa. 

Akaongeza kuwa Serikali inapoendelea na zoezi la kuwapa uwezo watalaam hao inawaomba wawe waadilifu, wenye kujituma na wenye weledi mkubwa maana kazi yao hiyo ni kubwa sana kuliko kazi zingine za kihandisi. 

“ Kama nilivyosema hapo awali tutaendelea kuwajengea uwezo watalaam wetu kwa kutumia miradi tuliyonayo, lakini kujenga uwezo kuna uhusiano mkubwa na masuala ya kujituma, kuijitoa kwa moyo kwa taifa, kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa, hii ndiyo itakuwa tiketi ya kupata kazi na tutachagua watalaam kulingana na vigezo hivyo,”Alisisitiza Mwakalinga. 

Akizungumzia kuhusu changamoto za uhaba wa wataalam hao, Dkt. Mwaklinga aliainisha kuwa, kwa takwimu za Shirika la kazi duniani, ILO, zinabaini kuwa Mhandisi mmoja anapaswa kufanya kazi na Mafundi Sanifu watano, na Mafundi Stadi 25, na kuongeza kuwa hiyo inaonyesha umuhimu wa wasanifu na mafundi stadi katika sekta ya ujenzi. 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Prof. Ninatubu Lema, alisema kuwa Wasanafi wanahitajika kijituma ili kuanzisha viwanda vidogovidogo vya kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuuzwa nchini. 

“Mnatakiwa Mafundi Sanifu kuwa wabunifu katika kujenga na kutengeneza uwezo kwa kufanya  wajasiriamali wa kujenga viwanda vidogovidogo, ili mtu mmoja aajiri watu watano, watu sita au watu 10 na kutengeneza vitu vidogovidogo vya kuuzwa hapa nchini, … tuko tayari kuratibu na kwenda kwenye nchi za wenzetu kama India, China kutazama hivyo viwanda vidogovidogo.”, Alisema, Prof.Lema.

Waziri Hasunga Awataka Watumishi Kupambana Na Rushwa Mahala Pa Kazi

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Awamu ya Tatu ya Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa (2017-2022 ina mtizamo mpya unaolenga kuhakikisha kuwa rushwa inaondolewa nchini kwa kutumia mbinu mpya na zinazotekelezeka kwa kuweka mkazo katika sekta zenye mazingira shawishi ya rushwa.

Utekelezaji wa Mkakati huo unalenga kupunguza na kudhibiti rushwa katika sekta/ maeneo muhimu ya kimkakati ambayo ni pamoja na manunuzi ya umma, ukusanyaji wa mapato, utoaji wa haki, maliasili na utalii, madini, nishati, mafuta na gesi, afya, elimu na ardhi.

Rushwa ni adui wa haki, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua  mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019 amekemea na kuwataka watumishi kupambana na rushwa katika sehemu za kazi.

Amewataka watumishi kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa kutoshiriki katika kutoa au kupokea rushwa. “Napenda kusisitiza kuwa yeyote atakayejihusisha na kubainika kupokea au kutoa rushwa hatua stahiki na kali zitachukuliwa dhidi yake” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri Hasunga amesema kuwa bado wizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake kutoa huduma kwa umma ikiwemo ukosefu wa rasilimali fedha na rasilimali watu wa kutosha, hali inayosababisha kutofikiwa kwa malengo. “Niwahakikishie kuwa, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua changamoto hizo. Ni matumaini yangu kuwa, mkiwa kama Wataalamu mtatumia uwezo wenu katika kuibua mikakati itayosaidia kuwezesha Kilimo kuwa chenye tija na cha kibiashara” Alisisitiza

Kadhalika, amewataka watumishi wote kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili katika Utumishi wa Umma.

Mhe Hasunga amesema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kwa Mtumishi yoyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na vitendo vinavyokiuka maadili ya Utumishi wa Umma.

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inayo dhamira ya dhati ya kuondoa uzembe na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma na hivyo mtumishi anaruhusiwa kudai haki zile za msingi kwa kuzingatia Kanuni, Sheria  na Taratibu za Utumishi wa umma wakati wa kutekeleza wajibu wake wa msingi kwa Mwajiri na kwa kutumia lugha ya staha.

Vilevile serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya Mwajiri na watumishi kwani pasipokuwa na ushirikiano wa pande hizo mbili, ni vigumu Taasisi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Umuhimu huu wa mashirikiano, umetiliwa mkazo kupitia Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia uendeshaji Taasisi za Umma.

Amesema kuwa ili kuweza kutafsiri dhana hiyo, ni muhimu pia kwa pande zote mbili kutambua haki na wajibu katika utekelezaji wa majukumu ya kazi, kwani umekuwepo utamaduni wa baadhi ya watumishi kudai haki bila kutimiza wajibu wao kwa Mwajiri.

Wahadhiri Wa Kigeni Nchini Wapungua Kutoka 502 Na Kubakia 151 Pekee.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
 Serikali imesema ,katika miaka 10 iliyopita  kati ya Mwaka 2008/2009 hadi 2018/2019  vyuo vikuu   17 vya umma 8 na binafsi 9  viliajiri wanataaluma wa kigeni 502. 

Hayo yamesemwa leo Mei 24,2019 bungeni jijini Dodoma na  Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.Mwita Waitara  kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,wakati akijibu Swali la mbunge wa Nkenge  Balozi Dkt.Diodorus Kamala  aliyehoji ,Kumekuwepo na utaratibu wa kuajiri wahadhiri toka nje ya nchi  kwa lengo la kukuza tafiti  na taaluma katika vyuo hivyo  je,katika miaka 10 iliyopita ,ni wahadhiri wangapi toka nje   wameajiriwa  katika vyuo vikuu Tanzania   na ni mafanikio gani kitaaluma  na kiutafiti  yameletwa na wahadhiri hao toka nje ya nchi. 

Katika Majibu yake,Mhe.Waitara amesema  vyuo vikuu vimekuwa vikiajiri wanataaluma  kutoka nje kwa malengo ya kuboresha hali ya Taaluma  na kujiimarisha  katika masuala ya kiutafiti  katika Nyanja mbalimbali  ambapo katika miaka 10 iliyopita  kati ya mwaka 2008/2009 hadi 2018/2019 ,vyuo vikuu 17 [vya umma 8 na binafsi 9] viliajiri wanataaluma wa kigeni 502. 

Aidha,Mhe.Waitara amesema kutokana na jitihada za serikali na vyuo vyenyewe  kuendeleza wataalam wa ndani, wanataaluma wa kigeni  wameendelea kupungua  kutoka 502 na kubaki  151 tu  hadi kufikia mwaka 2018/2019. 

Hata hivyo,Naibu Waziri Waitara amesema mafanikio yaliyopatikana baada ya kuajiri wataalam wa kigeni  ni pamoja na  kupata wataalam  wa fani ambazo nchi haijajitosheleza, kuanzishwa kwa Program mpya  katika vyuo mbalimbali , kuongeza ushirikiano kati ya vyuo vya ndani na nje,na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kisasa  vya kufundishia na kujifunzia ikiwa ni pamoja na vifaa vya maabara za utafiti. 

Katika hatua nyingine Mbunge Kamala ameishauri Serikali kuona namna ya kubadilisha sheria ya kustaafu kwa wahadhiri wasiwe wanastaafu mpaka achoke mwenyewe  ili kutatua upungufu wa Wasomi wahadhiri hapa nchini ambapo Naibu Waziri Waitara amesema maoni hayo Serikali imeyapokea  na yatafanyiwa kazi.

 

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Mnyika ahoji tatizo la umeme jimboni kwake......Naibu Waziri Mgalu Awataka Wananchi Wajiunge na Group la Whatsapp Kupata Taarifa

$
0
0
Na,Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu  Waziri wa Nishati,Mhe.Subira Mgalu amewataka wanachi wa Jiji la Dar Es Salaam Pamoja na Viunga Vyake kujiunga katika Group la mtandao wa kijamii wa Whatsaap ili kupata taarifa kwa uharaka juu ya katizo la Umeme . 
 
Mhe.Mgalu amesema hayo Leo ,Mei 24,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Ubungo Saidy Kubenea aliyehoji pamekuwepo na katizo la Umeme katika baadhi ya maeneo mbalimbali jijini Dar E s Salaam bila wananchi kupewa taarifa na kusababisha kupata hasara katika biashara zao,nini kauli ya Serikali. 

Katika Majibu Yake,Mhe.Mgalu amesema kuna Group Maalum la Whatsaap ambalo huwa linatoa taarifa kwa wakati pindi umeme unapokaribia kukatika hivyo amemtaka Mhe.Kubenea pamoja na Wananchi wake wajiorodheshe ili waunganishwe  kwani Yeye alishajiunga kwenye Group hilo. 

Awali,akiuliza swali la Msingi mbunge wa Kibamba John Mnyika  amehoji nini ufumbuzi wa kukatika umeme mara kwa mara ,maeneo gani  katika jimbo la kibamba mpaka sasa TANESCO haijafika na  mkakati gani wa kupunguza gharama za umeme. 

Katika Majibu yake ,Mhe.Subira Mgalu amesema  tatizo la kukatika umeme katika jimbo la kibamba linatokana na zoezi  la kuhamisha miundombinu  ya Umeme  ili kupisha upanuzi wa Barabara ya DSM-Morogoro hata hivyo tatizo hilo limepungua baada ya zoezi hilo kukamilika kwa asilimia 97 litakamilika mapema Mwezi Juni,2019. 

Hata hivyo,Serikali imetenga  Shilingi Bilioni 5 kwenye bajeti ya mwaka 2018/2019  kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupoza  umeme cha Mlonganzira [Luguruni ]chenye Uwezo wa  MVA 90. 

Aidha,Mhe.Mgalu amesema katika maeneo ya jimbo la Kibamba ambayo hayajapatiwa Umeme  ,bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/2019  TANESCO ilitenga 

Rais Magufuli Kawasili Salama Afrika Kusini

Lugola Awasimamisha Kazi Maofisa Watatu wa Jeshi la Polisi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewasimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita (OCD), Mkuu wa Kituo cha Polisi Geita(OCS) na Mkuu wa Upelelezi Wilaya hiyo (OC CID),kwa kosa la Mahabusu kutoroka Mahakamani. Na pia ameelekeza Askari 8 wa kituo hicho wawekwe Selo.

Mei 21, 2019 mahabusu 15 wanadaiwa kutoroka wakati wakisubiri kuitwa kwa ajili ya kesi zao.

Imeelezwa kuwa mahabusu hao walifungua mlango wa nyuma wakati askari wakiwa nje ya lango kuu la kuingia katika ukumbi walikokuwa wamewekwa. Hadi sasa mahabusu wanne wameshakamatwa.

Kigwangallah: Ni Marufuku Kusafirisha Wanyama Hai Nje ya Nchi

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema hakuna viumbe hai watakaosafirishwa nje ya Tanzania, hata iwe kunguni au chawa.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Mei 24, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara yake mwaka 2019/2020, kubainisha kuwa kitendo cha kusafirisha wanyama hakiungi mkono hivyo asingependa ifanyike akiwa katika wadhifa huo.

”Biashara ya wanyamapori hai haitafanyika nikiwa kama Waziri wa Maliasili na Utalii kwakuwa suala hilo lilishafungwa.

“Wizara imeamua kufunga mlango wa biashara hii, hata awe chawa au kunguni, atakayetaka kufuga afuge ili watanzania waende kwenye Zoo yake kuwatazama wanyama hao,” amesema Kingwangalla.

Ameongeza kuwa kuhusu suala la vipepeo kusafirishwa kwenda nje ya nchi wananchi ambao walikuwa wamechukuliwa vipepeo vyao ili viakuzwe watarudishiwa fedha zao na serikali.

Wakati huo huo Waziri huyo amesema kuwa Rais John Magufuli ameridhia hifadhi tatu mpya kuingizwa katika orodha ya Hifadhi za Taifa.

“Hapa nina hati kutoka kwa Rais, ameridhia hifadhi mpya tatu kuingia katika orodha ya hifadhi za taifa,” amesema Kigwangalla

Amezitaja hifadhi hizo mpya kuwa ni hifadhi ya Burigi, Chato, hifadhi ya Rumanyika, Karagwe na Ibanda, Kyerwa.

Serikali Yasema Itawafuta Kazi Viongozi Wataoshindwa Kuendana Na Kasi Ya Serikali Ya Awamu Ya Tano.

$
0
0
Na Salvatory Ntandu
Serikali kupitia Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma imesema itachukua hatua kali kwa Viongozi wa Umma ambao watabainika kukiuka sheria ya Maadili ya viongozi wa Umma kwa makusudi kwa kujinufaisha wao binafsi na kukwamisha malengo ya serikali ya awamu ya tano.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu katibu Msaidizi wa ofisi sekretarieti ya maadili ya umma kada ya Magharibi Tabora GERAD MWAITEBELE katika hafla ya siku mmoja ya mafunzo ya kwa viongozi wa Umma iliyojumisha viongozi wote wa Umma katika Halmashauri ya Mji wa kahama mkoani Shinyanga.

Amesema baadhia ya viongozi wa umma wanajisahau na kujikuta wanaingia katika vishawishi ikiwemo kupokea zawadi ambazo husababisha kushindwa kufanya maamuzi katika nafasi walizopewa na serikali hali ambayo inachangia kurudisha nyuma maendeleo na kuisababishia hasara serikali.

Amefafanua kuwa kwa sasa Ofisi yake inaendelea Kutoa elimu kwa viongozi wa umma ili kuwakumbusha majukumu yao,sheria,matamko na kanuni zilizowekwa na serikali katika kuhakikisha kila kiongozi wa umma anafanya kazi yake kwa usahihi bila kuvunja sheria.

Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya kahama Timoth Ndanya ambaye alikuwa mgeni rasm katika mafunzo hayo amewataka Viongozi wa umma kucha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wajitathimini kama wanafaa katika nafasi walizopewa jambo ambalo litaweza kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za Umma.

Naye mkuu wa Polisi Kahama (SSP) Sophia Jongo amesema viongozi wengi waumma wanashitakiwa kwa kukiuka sheria hiyo  na kuiomba serikali iweke mtaala wa sheria hii kwa gazi zote za elimu hapa nchini.

Fatma Karume: Hukumu ya kuzuia wakurugenzi wa serikali kusimamia chaguzi Tanzania, ni kuzuia ushindi wa goli la mkono

$
0
0
Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume amesema uamuzi wa Mahakama Kuu kuwaengua wakurugenzi wa halmashauri  kusimamia  chaguzi mbalimbali nchini ni sawa na kuzuia goli la mkono katika uchaguzi.

Fatma ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Mei 24, 2019 jijini Arusha katika kongamano la taasisi ya Change Tanzania, akibainisha kuhusu hukumu hiyo ya kesi iliyofunguliwa na Bob Wangwe kwamba ina maana kubwa katika demokrasia ya Tanzania.

Hukumu hiyo ilitolewa Mei 10, 2019  na kuwaengua wakurugenzi hao wa halmashauri za majiji, miji/wilaya na manispaa kusimamia uchaguzi. Hata hivyo, Serikali imetia nia ya kukata rufaa kuhusu hukumu hiyo.

Wakurugenzi hao ambao wamekuwa wakilalamikiwa na vyama vya upinzani kuwa baadhi yao ni makada wa CCM, ndio wasimamizi wa uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu cha 7(1).

Lakini, Mahakama Kuu katika hukumu yake pamoja na mambo mengine ilibatilisha kifungu hicho ikieleza kuwa kinakinzana na Katiba ya nchi Ibara za 21(1), (2) na ya 26(1), kuhusiana na ushiriki katika shughuli za uchaguzi na kutii na kufuata Katiba na sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa na jopo la majaji watatu; Dk Atuganile Ngala (kiongozi wa jopo), Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo kufuatia kesi ya kikatiba namba 17, ya mwaka 2018 iliyofunguliwa mahakamani hapo.

Akizungumzia hukumu hiyo leo,  Fatma amesema Watanzania wengi walikuwa wanajua jinsi wakurugenzi  wanavyovuruga uchaguzi lakini walikuwa kimya.

"Nimesaidia tumekwenda mahakamani tumeshinda kesi na hapa ndio tunaliondoa goli la mkono hivyo lazima tuungane" amesema.

Amesema ili kujua tatizo la wakurugenzi kusimamia uchaguzi ni vyema kutambua aliyewateua na sheria ya uchaguzi inasemaje.

"Kuna sheria ya Serikali za mitaa ambayo inazungumzia Rais kuteua wakurugenzi lakini kuna sheria ya uchaguzi ambayo inatambua hao wakurugenzi na kuwatumia.”

“Watu wanapenda kulalamika lakini hawachukui hatua ,tuige mfano wa Wangwe kwa kujitoa mhanga kufungua kesi hii,” amesema Fatma.

Kuhusu nia ya Serikali kukata rufaa, Fatma amesema kuna shinikizo la kisiasa tu na yeye kama wakili hana pingamizi kwani watakutana mahakamani.


Credit: Mwananchi

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya May 25

Korea Kaskazini yasema mazungumzo na Marekani hayatorejea karibuni

$
0
0
Korea Kaskazini imesema leo mazungumzo kuhusu mradi wake wa nyuklia na Marekani hayotaanza tena hadi utawala wa Rais Donald Trump utakapoachana na kile ilichokiita matwaka ya upande mmoja kwenye juhudi za kuuvunja mfumo wa nyuklia wa taifa hilo. 

Shirika la habari la Korea Kaskazini limenukuu maoni ya msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya nchi hiyo ambaye jina lake halikutajwa akiituhumu Marekani kwa kusababisha kwa makusudi kuvunjika mazungumzo ya mwezi Februari kati ya Rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un. 

Afisa huyo amesema mazungumzo hayo yaliyofanyika nchini Vietnam yalivunjika kwa sababu ya matakwa ya upande mmoja yasiyotekelezeka. 

Maafisa wa Marekani wamesema mara kadhaa kuwa mkutano wa Trump na Kim ulivunjika kwa sababu Korea Kaskazini ilitaka kupewa nafuu ya vikwazo vilivyopo lakini kwa kuchukua hatua ndogo kuelekea kuachana na mradi wake wa nyuklia. 

Kim amesema Marekani ina hadi mwisho wa mwaka huu kuja na matakwa yanayokubaliwa na pande zote ili kuyanusuru mazungumzo hayo.

Video Mpya Lulu Diva Ft. Country Boy - Mapopo

$
0
0
Video Mpya  Lulu Diva Ft. Country Boy - Mapopo
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images