Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mo Dewji Aipongeza Yanga...Amwaga Bodaboda Kwa Wachezaji Na Kutangaza Hatma Ya Kocha.

$
0
0
Na Bakari Chijumba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Timu ya SimbaSC , Mo Dewji amesema baada ya Kocha Mkuu wa Klabu hiyo,Patrick Aussems kutimiza malengo yaliyowekwa na Klabu,tayari bodi imepanga kukaa naye na kumuongezea mkataba mpya ili aendelee kuifundisha Simba SC.

Kuhusu ahadi ya Milioni 5 kwa kila mchezaji baada ya ubingwa, Mo Dewji amesema hakutoa ahadi hiyo bali alisema atatoa zawadi ya Pikipiki(Boxer) kwa kila mchezaji na tayari amewapa ili kuinua vipato vyao,MO amesema wakiweka watu wa kuziendesha zitawaingizia kipato.

Dewji amesema ameshaongea na viongozi wa klabu ya DC United ya Marekani na kuwaomba wakafanye maandalizi ya msimu ujao huko pia wacheze nao na timu nyingine za LMS au kwenda nchini Ureno ili wakacheze na timu za huko.

Katika hatua nyingine MO ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kuongeza ushindani kwenye Ligi.

"Naipongeza Yanga SC kwa kuleta ushindani mkubwa kwenye Ligi yetu na nichukue fursa hii kuwapongeza viongozi wapya wa Yanga SC na niwaombee wajipange ili waweze kufanikiwa, najua msimu ujao utakuwa mgumu sana"amesema Mo na kuongeza;

''Kwenye usajili tupo makini sana,leo tunapata ripoti ya kocha juu ya wachezaji wa nyumbani anaowataka,pia katika wachezaji 10 wa kigeni mpaka leo usiku kocha atatuambia anabaki na nani na nani waondoke..Simba itakuwa kwenye soko la kushindana na timu kama Mazembe na Al Ahly"

''Katika kusajili, kuna wachezaji wengine tutawatoa kwa mkopo lengo ni kutengeneza timu yenye ushindani zaidi na tutajitahidi usajili wetu uende sawa na vilabu vikubwa Afrika ili tukafanye vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa''

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi May 23

Marekani Kuongeza Wanajeshi Mashariki Ya Kati

$
0
0
Wizara ya ulinzi ya Marekani inaangazia ombi la jeshi la nchi hiyo la kupeleka wanajeshi 5,000 zaidi Mashariki ya Kati, wakati wasiwasi ukiongezeka kati yake na Iran. 

Kulingana na maafisa wawili waliozungumza na shirika la habari la Reuters kwa masharti ya kutotajwa majina, ombi hilo limewasilishwa na makao makuu ya jeshi la Marekani, lakini bado haiko wazi iwapo wizara hiyo italiidhinisha. 

Mmoja wa maafisa hao amesema wanajeshi hao wanapelekwa kwa ajili ya kujihami. 

Hili linatajwa kama ombi la karibuni zaidi la kuongezwa kwa wanajeshi katika kile ambacho Marekani inakitaja kama kitisho dhahiri kutoka kwa Iran dhidi Marekani na maslahi yake katika ukanda wa Mashariki ya Kati. 

Hata hivyo, wizara hiyo ilipoulizwa ilikataa kuzungumzia mipango yake ya usoni.

Uturuki kununua mfumo wa kujilinda wa Urusi

$
0
0
Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amesema nchi yake inajiandaa kwa vikwazo vya Marekani baada ya kuendelea na mpango wake wa kununua mfumo wa kujilinda na makombora kutoka Urusi. 

Kwenye taarifa iliyosambazwa jana Jumatano, Akar amesema wametuma watu wake nchini Urusi kupewa mafunzo ya kutumia mfumo huo wa S-400, yatakayoanza siku chache zijazo na kuendelea kwa miezi kadhaa. 

Ikulu ya White House ilitishia kuiwekea vikwazo Uturuki, chini ya sheria ya vikwazo inayozuia shughuli za kibiashara na sekta ya intelijensia na ulinzi ya Urusi. 

Marekani, inataraji kuiongezea mbinyo Uturuki, ambayo ni mshirika wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ili kununua mfumo wa Marekani, lakini Uturuki imekataa kuachana na ununuzi wa mfumo huo wa Urusi.

Kikwete Alia na Changamoto Ya Utawala Bora Afrika

$
0
0
Rais  mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, amesema kukosekana kwa umoja, utawala bora na uwepo wa umaskini ni miongoni mwa matatizo yanayozikandamiza nchi nyingi za Afrika, hivyo kuzikosesha maendeleo.

Akizungumza kwenye Tamasha la 11 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere,Kikwete alisema licha ya kufanikiwa kupata uhuru, nchi nyingi za Afrika ni maskini.

Alisema wakati viongozi kadhaa wa Afrika walipata nafasi ya kukutana kwenye nchi za Ulaya waliunganisha nguvu zao za kiharati katika kutetea Afrika, hatimaye kufanikiwa kusaidia kupatikana kwa uhuru kuanzia mwaka 1950 hadi 1964.

Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi kwenye tamasha hilo lililokusanya wasomi wa viwango mbalimbali kutoka katika nchi tofauti, alisema kuna nchi bado zinatawaliwa kijeshi, viongozi wengine wamekaa madarakani kwa muda mrefu.

Alisema kuna wakati viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) walianzisha utaratibu wa kujitathmini ambapo viongozi waliitwa na kupewa maoni ya kujisahihisha, wapo waliofanyia kazi na wengine waliyaweka.

Akizungumzia kuhusu umasikni Kikwete alisema katika nchi 30 maskini duniani 27 ni kutoka Afrika.

“Watu wetu wanakabiliwa na umaskini mkubwa sana, haya ndiyo mambo ambayo Afrika inatakiwa iungane kukabiliana nayo, tumetoka mbali na tulikuwa na mafanikio kwenye kujipatia uhuru, lakini licha ya jitihada tumeshindwa kujikomboa kutoka kwenye hali duni,” alisema.

Alisema hali ya uanaharakati iliyoanzishwa na waasisi wa nchi za Afrika kabla na baada ya uhuru, walibaini kuwapo kwa matatizo hayo walikubaliana kuyatatua kwa umoja, lakini hadi sasa harakati hazijafanikiwa.

Kikwete alisema katika nchi 54 zilizopo katika bara la Afrika, ni nchi moja pekee ndiyo inatajwa kuwa imeendelea nayo ni Mauritius wakati 27 kati ya hizo zipo katika uchumi wa kati.

Alibainisha kuwa nchi zimekosa umoja hata katika kujitafutia masoko ya bidhaa mbalimbali, kila moja inajitafutia binafsi, hivyo elimu inahitajika ili kuwezesha waafrika kupambana kuunganisha nguvu zao katika kujitafutia maendeleo.

Kamati ya Maadili ya Bunge Yapendekeza Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele Asimamishwe mikutano mitatu.....Ndugai Awaomba Wabunge Wamsamehe

$
0
0
Spika Ndugai amependekeza Mbunge wa Shinyanga Mjini, na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Stephen Masele asamehewe 

Awali Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza asimamishwe kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo Alhamisi Mei 23, 2019.

Mbunge Masele akijitetea Bungeni amesema;  “Nitumie nafasi hii kuomba radhi kwa Viongozi wangu wote waliopata usumbufu katika sakata hili akiwemo Rais Magufuli, sikuchonganisha mihimili bali nilikata rufaa baada ya Spika kuniandikia barua ya kunisimamisha bila hata ya kuniuliza lolote” 

Masele alihojiwa na kamati hiyo Jumatatu Mei 20 mwaka huu akituhumiwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba amekuwa na utovu wa nidhamu pamoja na kutoa maneno ya kugonganisha mihimili.

Spika Ndugai alilieleza Bunge Mei 16 mwaka huu kwamba kutokana na utovu huo wa nidhamu amesimamisha uwakilishi wa Masele katika Bunge la Afrika (PAP) lililokuwa likiendelea nchini Afrika Kusini na kuagiza mbunge huyo kurejea nchini.

IGP Sirro Afanya Ziara Ya Ukaguzi Kiwanja Cha Ndege Terminal |||

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (wapili kushoto), akiongozwa na Mhandisi Msimamizi wa Ujenzi wa jengo la kiwanja cha ndege Terminal III Barton Komba, wakati alipofanya ukaguzi wa kuona maendeleo ya mradi huo ambao hadi sasa umekamilika kwa asilimia 99. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akitoka kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege terminal III jijini Dar es salaam, ambapo IGP Sirro alisema Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha usalama kiwanjani hapo. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akikagua gwaride aliloandaliwa kwa ajili yake wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU Ukonga Dar es salaam, ambapo katika ukaguzi wake IGP Sirro alizungumza na maofisa na askari wa kikosi hicho. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akitoa maelekezo kwa maofisa wa Jeshi hilo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU Ukonga Dar es salaam, kulia ni kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas. Picha na Jeshi la Polisi.

Ujumbe wa Benki ya Dunia Waridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa ERPP

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameengoza kikao kazi cha majumuisho ya ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ufuatiliji wa utekelezaji wa Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga (Expanding Rice Production project), mradi ambao unatekelezwa Tanzania bara na Zanzibar.

Kikao hicho cha majumuisho kimefanyika jana Tarehe 22 Mei 2019 katika ukumbi wa ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo 1 Jijini Dar es salaam.

Ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Bi Sarah Simons umeeleza kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi katika utekelezaji wa kazi za mradi huo kulingana na malengo yaliyowekwa kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita.

Ujumbe huo ulianza kazi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mradi huo  wa ERPP tarehe 19-21 Mei 2019 ambapo walitembelea Tanzania bara na Zanzibar na walikutana katika wizara ya Kilimo (Bara)  na Wizara ya kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi (Zanzibar) na wameshukuru ushirikiano walioupata kwa watendaji wanaosimamia mradi huo.

Aidha ujumbe huo  pamoja na kusisitiza kasi ya  utekelezaji na ukamilishaji wa kazi za Mradi huo pia waliridhishwa na namna ambavyo mradi umekuwa ukiripoti kuongezeka kwa uzalishaji wa mpunga kwa hatua za awali baada ya wakulima kutumia mbegu bora katika mfumo wa  kilimo shadidi (SRI).

Pia maendeleo mazuri katika maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji na Maghala kwa kipindi cha miezi sita iliyopita na wamekuwa na matumaini kuwa Ujenzi wa miradi hiyo na kazi zingine zitakamilika kabla ya tarehe ya mwisho ya mradi huo.

Mhandisi Mtigumwe (Katibu Mkuu Kilimo Tanzania bara) ameushukuru ujumbe huo na kuwaeleza kuwa wataendelea kwa kasi kutekeleza shughuli zilizobaki za mradi huo ili tija kwa wakulima na nchi ionekane.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Bi Mansura Kassim aliushukuru Ujumbe huo kwa ufuatiliaji wao na kueleza kuwa Kwa upande wao wataendelea kukamilisha kazi zilizobakia katika mradi na kusimamia mradi huo ipasavyo.

Makamba Asisitiza Juni Mosi ndo mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kuanzia Juni Mosi mwaka huu itakuwa ndio mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki na Sheria kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo hayo.

Amesema hayo Mei 22 Jijini Dar es Salaam, kwenye kikao cha viongozi na watendaji mkoani hapo kilichokuwa kinahusu marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki.

Makamba Amesema, ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya Tamisemi watapita kwenye maduka na Magenge kwa ajili ya kukagua na kuangalia kama agizo linatekelezwa.

“Wazalishaji wa mifuko hiyo wakibainishwa bado wanazalisha faini itakuwa shilingi milioni 20 na kifungo, waingizaji katoka nje nao faini milioni 20, huku mtumiaji faini yake ikiwa ni 30,000.

Watanzania Wanaoishi Nje Ya Nchi Kupiga Kura Uchaguzi Mkuu wa Mwakani

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali inaangalia uwezekano wa watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweza kupiga kura katika uchaguzi ujao.

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 23 wakati akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni ambapo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Asha Abdalah Juma (CCM).

Katika swali lake Mbunge huyo ametaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwashirikisha watanzania wanaoishi nje kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

“Ilani ya Chama cha CCM imetekelezwa kwa kiasi kikubwa pamoja na mambo mazuri je serikali ina mpango gani wa kuwawezesha watanzania wanaoishi nje waweze kupiga kura mwaka 2020” amehoji

Akijibu swali hilo Majaliwa amesema suala hilo ni la kisera na kwa sasa serikali inalifanyia kazi kuona jinsi gani watanzania hao wataweza kupiga kura.

Amesema ni lazima kwanza kujua idadi ya watanzania hao waliopo nje na wanafanya nini

“Hili ni jambo la kisera lakini kwanza tujue idadi yao na wapo wapi na wanafanya nini kabla ya kuruhusu kupiga kura” amesema

Akizungumzia suala la miradi ya maji amesema ipo miradi ambayo imegundulika kuwa chini ya viwango na serikali imeshaanza kuchukua hatua na kuweka wasimamizi toka mikoani hadi ngazi ya halmashauri.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema pamoja na kuwepo kwa miradi mingi ya umwagiliaji lakini bado suala la kilimo cha umwagiliaji hakijatoa tija kwa taifa.

“Tayari tumeshavunja Tume ya umwagiliaji kwa sasa tunaipeleka kwenye wizara ya maji” amesema

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

$
0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0757996194 au 0717339771

Waziri Kalemani awataka wananchi kutunza miundo mbinu ya Umeme

$
0
0
Na Amiri kilagalila
Waziri wa Nishati Dkt.Medad Kalemani amewataka wananchi kutunza miundombinu ya Umeme inayopita katika vijiji vyao.

Akizungumza katika Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Masasi Jana,waziri kalemani amesema kuwa serikali inatumia  gharama kubwa kufikisha umeme na kuwataka wananchi wasifanye shughuli zitakazo athiri miundombinu ya Umeme ikiwemo kuwasha moto karibu na Nguzo na badala yake wahamasike kulipia huduma ya Umeme ili iweze kuwasaidia katika shughuli zao za kiuchumi

Akiwasha umeme katika vijiji vya Nanditi na Mombaka katika Wilaya ya Masasi Waziri amezitaka halmashauri za wilaya, kulipia gharama za Umeme za taasisi mbalimbali za kijamii ikiwemo Shule na zahanati na kudai umeme mara tu baada ya kulipia.

“Kabla ya kulalamika shule haina umeme na zahanati haina umeme, jiulize swali moja  tu umelipia?lipia kwanza ndo udai umeme, halmashaur zote za wilaya lipieni taasisi za umma, tunataka wananchi wapate umeme, na umeme pia ufike mashuleni, zahanati, na sehemu zote zinazotoa huduma” alisema Dkt.Kalemani  na kumtaka Mkandarasi kukamilisha  kuunganisha umeme katika vijiji 122vilivyobaki  katika kata ya Mndibwa, ndani ya siku 25.

Naye Mkuu wa wilaya ya Masasi,Mhe. Selemani Mzee ameiashukuru Serikali  kwa kufikisha Umeme Masasi na  kuwataka wananchi wote wa masasi kulipia Umeme.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Waziri Mkuu: Tozo Zinazokwamisha Biashara Nchini Kufutwa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanza jitihada za kufuta tozo zote ambazo zinakwamisha mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini zikiwemo za kwenye pembejeo ili kuwawezesha wafanyabiashara kuzifikisha hadi ngazi ya kijiji kwa wakulima.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 23, 2019) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Madaba, Kizito Mhagama katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu. Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kupunguza tozo kwa maduka yanayouza pembejeo ili kumwezesha mkulima kupata pembejeo.

Waziri Mkuu amesema Serikali imepokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo na wauzaji wa pembejeo juu ya tozo mbalimbali katika uendeshaji wa shughuli nzima wa biasharazao.

“Serikali imesikia vilio vyenu na sasa inafanya mapitio ya tozo hizo na itakapofikia hatua nzuri itawajulisha na kuwashirikisha kujua ni aina gani ya tozo ambayo itaondolewa au kuibadilisha ili muendelee kufanya biashara zenu katika mazingira rahisi.”

Waziri Mkuu amesema kazi kubwa inayofanywa na Serikali kwa sasa ni kufanya mapitio ya tozo zote kuanzia kwa wakulima hadi kwa wafanyabiashara na kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini, ikiwemo ya pembejeo ili kuzifikisha kiurahisi kwa wakulima.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwamba tayari Mawaziri wa kisekta wenye dhamana ambao wana tozo mbalimbali kwenye wizara zao zinazokwamisha ufanyaji biashara katika mazingira rafiki wameshakutana kwa ajili ya kujadili namna ya kulipatia ufumbuzi suala hilo.

“Hata juzi nilikuwa na mawaziri hao kupata taarifa zao kwa pamoja kuona maeneo yote waliyoyapitia na tozo zote zinazokusudiwa kupitiwa upya na kazi hiyo ikikamilika watakutana na Kamati ya Bajeti ya Bunge, Wizara ya Fedha ili kuona namna nzuri ya kuondoa tozo hizo. Lakini baadaye suala hilo litaenda kwenye mamlaka inayotoa ridhaa ya kuondoa au kupunguza tozo.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema miradi mingi ya maji ambayo inatekelezwa kwenye maeneo mbalimbali nchini baadhi yake haitekelezwi kwa viwango vilivyokusudiwa, hivyo haiwiani na thamani halisi ya kiasi cha fedha kinachotolewa.

Hata hivyo Waziri wa Maji wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2019/2020 alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya miradi yote ambayo haiwiani na kiasi cha fedha kilichotolewa pamoja na hatua zilizochukuliwa dhidi ya miradi yote.

“Moja kati ya hatua ambazo amezifanya ni pamoja na kuunda timu inayopita kukagua miradi yote nchini na kujiridhisha kama matengenezo yake yanakidhi thamani ya fedha iliyotolewa katika mradi huo na kama haukidhi hatua kali zinachukuliwa kwa wahusika.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Korogwe Mjini Mary Chatanda aliyetaka kujua Serikali kama ipo tayari kuchunguza na kuchukua hatua kwa watendaji walioshindwa kusimamia miradi ya maji na kuisababishia hasara pamoja na wananchi kukosa huduma waliyokusudiwa.

Waziri Mkuu Azungumza Na Mabalozi Wa Finland Na Switzerland Nchini

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Pekka Hukka na kumshukuru kwa jitihada za nchi hiyo kuisadia Tanzania kuondokana na umaskini.

“Tunaishukuru Serikali ya Finland kwa misaada ambayo imeendelea kuitoa kama njia ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania za kuondoa umaskini pamoja na kuongeza makusanyo ya mapato ili kukuza uchumi wa nchi yetu,” amesema Waziri Mkuu.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 23, 2019) alipokutana na Balozi huyo anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amemweleza balozi huyo kwamba Tanzania bado ina fursa za uwekezaji na kwamba Serikali inaendelea kutengeneza mazingira rafiki na bora kwa uwekezaji. “Sekta ambazo makampuni ya Finland yanaweza kuwekeza hapa nchini ni pamoja na TEHAMA, nishati, usafiri, uchakataji wa mazao ya kilimo na misitu,” amesema.

Waziri Mkuu alimtakia heri Balozi Hukka ambaye anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi huu kwenda Tunisia ambako ndiko kutakuwa na kituo chake kipya cha kazi.

Kwa upande wake, Balozi Hukka alisema ataondoka Tanzania akiwa na kumbukumbu nzuri ambazo atazienzi na anataraji kukutana na Watanzania wengine ili aendelee kukuza mahusiano yaliyokuwepo.

Alisema Serikali za Tanzania na Finland zilisaini mkataba wa programu iitwayo Forestry and Value Chain Programme (FORVAC) ambao unalenga kuongeza faida za kiuchumi na kijamii kwa kupitia sekta ya misitu pamoja na kupunguza ukataji wa miti. “Malengo hayo yatafikiwa kwa kukuza mnyororo wa thamani kwenye sekta ya misitu pamoja na kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji, sheria na sera katika sekta ya misitu,” alisema.

Finland inasaidia sekta ya misitu nchini Tanzania kupitia Programu ya Private Forestry Programme (PFP) ambayo ililenga kuongeza mapato kwa wakazi wa vijijini katika Halmashauri 10 za Njombe TC, Njombe DC, Makete, Ludewa, Kilombero, Mufindi, Kilolo, Madaba, Mbinga na Nyasa) kwa kusaidia upandaji wa miti na kuongeza thamani ya mazao ya misitu.

Programu hiyo imesaidia kujenga uwezo kwa wahusika wote katika mnyororo wa thamani wa biashara ya mazao ya misitu. Awamu ya kwanza ya programu hiyo imesaidia kuongeza kipato cha familia zaidi ya 9,000 kwenye wilaya hizo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekutana na Balozi wa Uswisi hapa nchini, Mhe. Florence Mattli ambaye pia alienda kumuaga ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu alimweleza balozi huyo dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kudumisha ushirikiano na Uswisi na kusisitiza kwamba iko tayari kufanya kazi na Balozi mpya wa Uswisi atakayekuja kwa manufaa ya pande zote mbili.

“Ni muhimu sana ushirikiano wa Tanzania na Uswisi ukadumishwa kwa kuzingatia pia masuala ya biashara na uwekezaji hususan kwenye sekta za afya, kilimo, elimu na teknolojia,” alisema Waziri Mkuu.

Alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Uswisi kwa misaada ambayo imeendelea kutolewa na nchi hiyo katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania za kuondoa umaskini hususan kwenye miradi ya afya, kilimo na uwekezaji katika elimu na biashara kwa ajili ya kukuza uchumi.

Kwa upande wake, Balozi Mattli alisema Serikali ya Uswisi imekuwa ikiunga mkono na kusaidia jitihada za kukuza uwazi na uwajibikaji kwa watendaji wa Serikali na wale wasiokuwa wa Serikali kuzingatia mazingira ya kitaasisi na kijamii yanayopiga vita masuala ya rushwa.

“Msaada huo wa kupambana na rushwa umechangia kuimarisha ufanisi wa uendeshaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kukuza uelewa wa kijamii kuhusu masuala ya rushwa,” alisema.

Alisema mwaka 2018, Serikali ya Uswisi ilitoa dola za Marekani milioni 24 kusaidia Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Ajira Tanzania, ambao ulianza kutekelezwa Agosti Mosi, 2018 kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

“Mpango huo unalenga kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa vitendo na kuimarisha mafunzo ya ufundi nchini. Hivyo, mpango huo umechangia kuboresha matarajio ya vijana kwa kuwapatia ujuzi katika kazi na ubunifu unaochangia kuondokana na suala la ukosefu wa ajira,” alisema.

Alisema Serikali ya Uswisi inasaidia maendeleo ya vijana kupitia Mpango wa Ajira ya Vijana (OYE) ambao unalenga kuimarisha maisha ya vijana wa kiume na wa kike kwa kuwafundisha fursa za ajira katika sekta za biashara, kilimo, nishati mbadala, usafi wa mazingira na kuboresha ujuzi.

Utauzi Mpya Uliofanywa na Rais Magufuli Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Onorius John Njole kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria (Chief Parliamentary Draftsman – CPD).

Uteuzi wa Njole umeanza leo May 23, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Njole alikuwa Mkurugenzi wa Sheria na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).

Njole anachukua nafasi ya Sara K. Barahomoka ambaye anastaafu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa May 24

Rais Magufuli Aondoka Nchini Kuelekea Afrika Kusinj

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2019 ameondoka nchini kwenda Afrika ya Kusini ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa.

Katika safari hiyo Rais Magufuli ameongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Philip Mangula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Wakizungumza kabla ya kuondoka Rais Mstaafu Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mangula wamesema Tanzania na Afrika ya Kusini zina uhusiano mkubwa na wa kihistoria na kwamba Serikali na chama zina kila sababu ya kudumisha uhusiano na ushirikiano huo.

Viongozi hao wameondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Afrika ya Kusini, Mhe. Rais Magufuli atafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Namibia ambako pia atazindua mtaa uliopewa jina la Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kutambua mchango mkubwa alioutoa katika ukombozi wa Taifa hilo.

Halmashauri Tatu Kupandishwa Hadhi na Kuwa Manispaa

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Kutoka Jijini Dodoma.

Bunge limeelezwa kuwa ,Serikali ipo katika mchakato wa kupandisha hadhi halmashauri 3 hapa nchini kutokana na kukidhi vigezo vya mapato kujitosheleza. 

Hayo yamesemwa leo Mei 24,2019 bungeni  jijini Dodoma na Waziri wa Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa TAMISEMI ,Mhe.Seleman Jafo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Msalala Kahama Ezekiel Maige aliyehoji,lini mji wa Kahama utapandisha kuwa hadhi kuwa Manispaa baada ya kutimiza vigezo vya mapato kujitosheleza  pamoja na Isaka kupandishwa hadhi ya Mji. 

Akijibu Swali hilo,Waziri wa TAMISEMI Mhe.Seleman Jafo amesema Serikali inatambua maeneo matatu hapa nchini ambayo serikali ipo katika mchakato wa kupandisha hadhi kuwa Manispaa kutokana na kukidhi vigezo vya kujitosheleza kimapato. 

Mhe.Jafo ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga,Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani na Halmashauri ya  mji wa Geita mkoani Geita na muda wowote kuanzia sasa maeneo hayo yatapandishwa hadhi kuwa Manispaa pindi mchakato utakapokamilika.

Wakaguzi wa mifuko ya plastiki hawaruhusiwi kuingia kwenye makazi ya watu, au kusimamisha magari, ili kutafuta mifuko ya plastiki.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images