Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yasema Bado Inaendelea Na Majadiliano Kuhusu Bandari Ya Bagamoyo

$
0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO
MKURUGENZI na Msemaji Mkuu wa, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali inaendelea na majadiliano kuhusu kuendelea na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani ili kuona kama inaweza kuwa na tija kiuchumi kwa upande wa Tanzania.

Dkt. Abbasi alisema Serikali ina uwezo wa kujenga bandari nyingi na kwa kuwa Tanzania ina ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari na kwamba bado majadiliano yenye tija kwa Taifa yanaendelea kufanywa baina ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji wa mradi huo.
 
“Serikali haijasema kuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni hatari, tunaendelea na majadiliano ya utekelezaji wa mradi huo, nchi yetu imejaliwa ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari kwa hiyo tuna uwezo wa kujenga Bandari nyingi tu, hii ya Bagamoyo si kweli kuwa imeachwa kuna mambo ya msingi tunayajadili na tusipofikia maamuzi tutaachana nayo” alisema Dkt Abbasi.
 
Kuhusu suala la uwekezaji wa vitu aliloulizwa kwenye kipindi hicho Dr Abbasi alisema Serikali haitaacha kuwekeza kwenye vitu kwa sababu vitu husaidia maendeleo ya watu, mfano afya, elimu na miundombinu mingine.
 
“Kwenye sekta ya madini tumekuachia fedha, dawa hospitalini tumeongeza na bei zimepungua, tumekuletea yote hayo lakini bado unasema huna pesa mfukoni, Serikali inafanya yote haya kuhakikisha kuwa uchumi wetu unaleta manufaa mapana kwa Taifa” alisema Dkt. Abbasi.
 
Kuhusu uhuru wa Habari na kufungia magazeti yasiyofuata sheria za uchapishaji Msemaji huyo wa Serikali alisema kuwa ofisi yake haikurupuki  kufungia magazeti, na kusema kuwa  ni magazeti  mitatu tu yalifungiwa kati ya 266 yaliyosajiliwa nchini na kuwataka wamiliki wa magazeti hayo kufuata sheria.
 
Kuhusu malamiko ya wafanyabiashara kwenye maeneo mbalimbali nchini ya kufunga biashara hizo kwa kisingizio cha kodi na tozo mbalimbali, Dkt. Abbasi alisema ni muhimu wakaelewa kwamba kwa sasa Serikali inapita katika kipindi cha mabadiliko na hakuna siku serikali haitadai kodi huku akieleza kuwa kodi nyingi zimepunguzwa hususan kwenye sekta za Kilimo, Mifugo na uvuvi.
 
“Kwanza tukubali tunapita kwenye kipindi cha mabadiliko, hakuna siku serikali haitadai kodi kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya nchi hii, kuna dhana ilijengeka kuwa unaweza kufanya biashara bila kulipa kodi hiyo sasa haipo, lazima tuangalie changamoto ambazo zinakumba sekta mbalimbali mfano sekta ya kilimo, miufgo na uvubvi kulikuwa na kodi zaidi ya 150, serikali imefuta zaidi ya kodi 80 hadi 100” alisema Dkt Abbasi.
 
Mwisho.




Waziri Mbarawa Ateua Wakurugenzi Watatu

$
0
0
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa,  Mei 16, 2019 amefanya uteuzi wa Wakurugenzi watendaji watatu wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira.

Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa Wizara hiyo Prof. Kitila Mkumbo imeeleza kuwa walioteuliwa ni Mhandisi Mbike Jones Lyimo ambaye atakuwa Mkurugenzi wa KUWASA mkoani Kigoma.

Mwingine ni Bi. Flaviana Kifizi, ambaye amekuwa mkurugenzi wa SHUWASA mkoa wa Shinyanga.

Wa tatu katika walioteuliwa ni Mhandisi Robert Lupoja ambaye anakuwa mkurugenzi wa MUWASA huko Musoma mkoani Mara.

Wagonjwa 1,901 wa Dengue wabainika

$
0
0
Jumla  ya wagonjwa 1,901 wamebainika kuwa na virusi vya  homa ya Dengue, tangu kuibuka kwa ugonjwa huo nchini, Januari mwaka huu.

Kati ya wagonjwa hao, 1,809 ni wakazi wa jiji la Dar es Salaam, 89 kutoka Tanga mmoja kutoka Singida, mmoja Kilimanjaro na mmoja kutoka mkoani Pwani.

Mganga Mkuu wa Serikali wa Wizara ya  Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Mohammed Kambi, ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya ugonjwa huo nchini

Amesema kwa mujibu wa taarifa ya siku tisa hadi jana, kuna ongezeko la wagonjwa 674 sawa wastani wa wagonjwa 75 kwa kila siku, ikiwa ni tofauti ya wastani wa wagonjwa 32 waliopatikana Aprili mwaka huu.

Amesema wagonjwa wawili waliopatikana katika mikoa ya Kilimanjaro na Pwani wametoka jijini Dar es Salaam.

"Ongezeko hili linatokana na kuongezeka kwa uelewa kuhusu ugonjwa huu kwa wananchi walio wengi wenye dalili na hivyo wanajitokeza kupata huduma za uchunguzi ambazo zimeendelea kupanuka kwenye vituo vyetu katika mkoa wa Dar es Salaam na Tanga," amesema Prof. Kambi.

Ametaja Idadi ya vituo vinavyopima ugonjwa huo imeongezeka hadi kufikia 19 tofauti na vituo saba vilivyokuwapo awali.

Makampuni Sita Yasaini mkataba wa awali Wa kununua korosho nchini

$
0
0
Serikali imesaini mkataba wa awali na kampuni sita ya kununua korosho kati ya zilizoomba kununua korosho hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 16, 2019 Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema baada ya Kampuni ya Indo Power ya nchini Kenya kushindwa kununua korosho wameendelea kusaini mikataba ya awali.

“Tumeendelea kusaini mikataba mingine na makampuni mengine, mikataba ambayo tumeisaini ni ya awali.

“Mpaka sasa   tumesaini na makampuni sita nisingependa kuyataja kwa majina kwa sababu tunajua hali halisi ya makampuni ya korosho watu wanafuatiliana, wanaharibiana biashara pamoja na majina.

“Lakini kuna kampuni moja tuliikaribisha wiki iliyopita imekuja kukagua maghala ya korosho wamejiridhisha kwamba korosho yetu ni safi na haijaharibika na tumepeleka kwenda kuhakiki TBS na wameenda kufanya uhakiki katika nchi yao na wamejihakikishia kwamba ni nzuri na wanajiandaa kulipa.

“Hawa mabwana wakilipa tunawakabidhi korosho mara moja,”alisema Waziri Kakunda.

Akitoa ripoti ya maagizo aliyoagizwa na Rais Dk. John Magufuli wakati akiapishwa, Novemba 12 mwaka jana ya kusimamia ununuzi wa korosho, Kakunda alisema tangu   Novemba 13 mwaka jana hadi Mei 15 mwaka huu zimeweza kukusanywa tani  225,000.

“Kati ya hizo tani 2,200 zinaendelea kubanguliwa na viwanda  vya ndani kwa mikataba maalum. Maana yake zinabaki tani 228,000 katika maghala."Alisema

Video Mpya: Bright - Aibu

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Bright anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya uitwao Aibu. Itazame hapa.

Serikali Yaanza mchakato wa kuanzisha BIma ya mazao

$
0
0
Serikali imeanza mchakato wa kuanzisha BIma ya mazao ili kuweza kukabiliana na changamoto za ukame, mafuriko, magonjwa na wadudu waharibifu.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo bungeni leo, Mei 17, waziri mwenye dhamana, Japheti Hasunga amelieleza Bunge kuwa mfumo huo utamwezesha mkulima kulipwa fidia pale anapopata hasara pamoja na kupata mkopo katika taasisi za fedha.

Amesema kwa kuanzia wizara imeanza kufanya vikao na wadau mbalimbali ili kufanya maandalizi ya awali kwa kuanza na maeneo machache.

“Maandalizi hayo yanaendelea kufanyika ili katika mwaka wa fedha 2019/2020 tuwe anglau na aina mbili za mifumo ya Bima ya mazao inayoweza kutumika nchini” alisema Waziri Hasunga.

Hata hivyo Hasunga alisema ili utaratibu huo uweze kufanikiwa kutahitajika takwimu sahihi za hali ya hewa pamoja na uzingatiaji wa kanuni bora za kilimo.

Hotuba Ya Waziri Wa Kilimo, Kuhusu Makadirio Ya Mapato Na Matumizi Ya Fedha Ya Wizara Ya Kilimo Kwa Mwaka 2019/2020

$
0
0

1.0  UTANGULIZI

1.  Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.  Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu lipitishe Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa Fedha 2019/2020.
2.   Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufikia siku ya leo tukiwa wazima wa afya njema na kuendelea kuijalia nchi yetu amani na mshikamano na kujadili bajeti hii inayolenga kusukuma mbele kasi ya maendeleo ya Sekta ya Kilimo na wakulima kwa ujumla wao.
3.  Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuniteua kuwa Waziri wa Kilimo. Pia, niwashukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu kwa kazi kubwa wanayofanya kusukuma maendeleo ya nchi hii, ikiwemo Sekta ya Kilimo. Napenda kuwaahidi kwamba nitafanya kazi ya kuongoza Wizara ya Kilimo kwa uaminifu, juhudi na maarifa ili kuhakikisha kuwa rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo zinawafikia walengwa ili kuongeza tija na kuinua kipato chao.
4.  Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwa hotuba  yake ambayo iligusa maeneo mengi ikiwemo Sekta ya Kilimo. Aidha, nimpongeze tena Mhe. Waziri Mkuu kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kuhamasisha na kusimamia kilimo pamoja na maendeleo ya Vyama vya Ushirika.
5.  Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe na Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb.) pamoja na Wenyeviti wa Bunge kwa jinsi mnavyoliongoza Bunge kwa umahiri mkubwa.
 Aidha, nitumie nafasi hii kuwapongeza Wabunge wote kwa umahiri wao mkubwa katika mijadala inayoendelea katika Bunge hili la Bajeti.
6.  Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kuwapongeza na kuwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji chini ya Uenyekiti wa Mhe. Mahmoud Mgimwa, Mbunge wa Mufindi Kaskazini na Makamu Mwenyekiti Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma (Mb). Kamati ilipata fursa ya kukutana na Wizara na kutembelea baadhi ya maeneo kuona utekelezaji wa kazi za kilimo na kushauri namna ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara, Bodi na Taasisi zake. Naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba, ushauri wao umezingatiwa na tutaendelea kushirikiana na Kamati ili kuleta mageuzi ya kilimo nchini.

2.0             MWELEKEO WA SEKTA YA KILIMO

7.  Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kubadilisha kilimo kutoka kuwa cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Aidha, Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo umesisitizia mapinduzi ya viwanda na umeitambua Sekta ya Kilimo kuwa mhimili imara kwa ajili ya upatikanaji wa malighafi za viwanda.  Miongozo hiyo ya Kitaifa, pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na Sera ya Kilimo ya mwaka 2013, inatekelezwa na Wizara kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ambayo inalenga kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo. Aidha, kwa kutambua umuhimu wa kuongeza mitaji, teknolojia na ubunifu, Sekta Binafsi inashirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa ASDP II.
8.  Mheshimiwa Spika, ASDP II iliyozinduliwa rasmi tarehe 4 Juni, 2018 na Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inalenga kubadilisha maisha ya mkulima kwa kufanya mageuzi makubwa kwenye kilimo kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele kulingana na ikolojia za kilimo. 

3.0             MCHANGO WA KILIMO KATIKA UCHUMI

9.  Mheshimiwa Spika, kilimo ni sekta kubwa na muhimu kwa maendeleo kutokana na mchango wake katika uchumi. Katika mwaka 2017, sekta hiyo imetoa ajira kwa Watanzania kwa asilimia 65.5, ikichangia takriban asilimia 28.7 ya Pato la Taifa ambapo sekta ndogo ya mazao ilichangia asilimia 16.58.  Vilevile, Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda. Takwimu zinaonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2018, ukuaji wa Sekta ya Kilimo ulifikia asilimia 7.1. Ukuaji huo ulichangiwa na jitihada za Serikali za kuhakikisha upatikanaji na matumizi ya  pembejeo bora, hali nzuri ya mvua na uboreshaji wa miundombinu ya uzalishaji.

3.1  Upatikanaji wa Chakula

10. Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa  chakula kwa mwaka 2018/2019 ulifikia tani milioni 16.89 zikiwemo tani milioni 9.53 za mazao ya nafaka na tani milioni 7.35 za mazao yasiyo nafaka. Kiwango hicho cha uzalishaji kimeiwezesha nchi kujitosheleza kwa mahitaji yake ya chakula ya tani milioni 13.56 na hivyo kuwa na ziada ya tani milioni 3.32 za chakula kwa kiwango cha utoshelevu cha asilimia 124. Niwahakikishie watanzania kwamba, tunacho chakula cha kutosha nchini.  Hata hivyo, tuendelee kuweka akiba katika kaya zetu hadi tutakapovuna tena kwani inaonekana kwamba huenda tusiwe na mavuno mazuri sana msimu huu kutokana na uhaba wa mvua kwenye maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kati na Kaskazini mwa nchi yetu.(Maelezo ya kina yanapatikana uk.5 wa kitabu cha Hotuba ya bajeti).

3.2   Umwagiliaji

11. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekamilisha mapitio ya Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji wa mwaka 2002 ili kubaini maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa kuzingatia Mipango Shirikishi ya Maendeleo ya Rasilimali za Maji. Katika mpango huo, hekta 560,880 zimepangwa kuendelezwa kwa lengo la kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 475,052 mwaka 2018/2019 hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2035. (Maelezo ya kina yanapatikana uk.6 wa kitabu cha Hotuba ya bajeti)

3.3   Maendeleo ya Ushirika

12. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika imeendelea kuimarisha Sekta ya Ushirika kwa kusimamia na kuhamasisha maendeleo yake. Vyama vya Ushirika vimeongezeka kutoka vyama 10,990 Desemba 2017 hadi vyama 11,331 kufikia Desemba 2018. Vilevile, idadi ya wanachama wa vyama vya ushirika imeongezeka kutoka 2,619,311 mwaka 2017 hadi 3,998,193 Februari, 2019 sawa na ongezeko la asilimia 53.
Hadi Desemba 2018, mikopo yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.3 imetolewa kwa wanachama ikilinganishwa na Shilingi bilioni 902 iliyotolewa kufikia Desemba 2017.
 Aidha, Akiba na Amana za wanachama katika SACCOS zimefikia Shilingi bilioni 575 na hisa Shilingi bilioni 79. (Maelezo ya kina yanapatikana uk.7 wa kitabu cha Hotuba ya bajeti)

4.0             UTEKELEZAJI WA MAENEO YA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2018/2019

13. Mheshimiwa Spika,  katika mwaka 2018/2019, Wizara imetekeleza  maeneo ya kipaumbele ya kuongeza tija kwa kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo, udhibiti wa visumbufu, matumizi ya zana bora za kilimo na huduma za ugani; ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji; ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi mazao ya kilimo na masoko; kufanya utafiti wa kilimo na kuzalisha teknolojia kwa mazao ya mahindi, muhogo, ngano, michikichi, ufuta, alizeti, pamba na mpunga.
14.  Mheshimiwa Spika, maeneo mengine ya kipaumbele ni kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora za mazao na kusambaza kwa wakulima; kuboresha maarifa na ujuzi kwa watafiti; kuimarisha huduma za upimaji wa matabaka na ubora wa udongo kuendana na mahitaji ya mazao ya kilimo ki-ikolojia; mafunzo na usambazaji taarifa za kilimo na sayansi shirikishi; kusajili na kuandaa kanzidata ya wakulima na kuimarisha ushirika. (masuala yote ya utekelezaji wa maeneo ya kipaubele yapo kwa kina kwenye ukurasa 10-61  katika kitabu cha Hotuba ya bajeti)
15. Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza vipaumbele hivyo, Shilingi bilioni 204.07 ziliidhinishwa na Bunge lako Tukufu. Kati ya fedha hizo, Fungu 43 – Wizara ya Kilimo iliidhinishiwa Shilingi bilioni 166.26zikiwemo Shilingi bilioni 68.14 za matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 98.12 za matumizi ya maendeleo; Tume ya Taifa ya Umwagiliaji - Fungu 05 iliidhinishiwa Shilingi bilioni 29.77 zikiwemo Shilingi bilioni 3.95 za matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 25.82fedha za maendeleo; na Tume ya Maendeleo ya Ushirika - Fungu 24 iliidhinishiwa Shilingi bilioni 8.05 zikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida.

4.1  Kuongeza Tija katika Kilimo

Upatikanaji wa mbegu bora za mazao
16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,  upatikanaji wa mbegu bora umefikia tani 49,040.66. Kati ya kiasi hicho, tani 38,507.87 zimezalishwa hapa nchini, tani 8,361.46 zimeagizwa toka nje ya nchi na tani 2,171.33 ni bakaa ya msimu wa 2017/2018. Vilevile, miche 1,507 ya miwa, vipando 121,805 vya muhogo na vikonyo 520,000 vya viazi lishe vimezalishwa. Aidha, aina mpya 13 za mbegu bora zimeidhinishwa na zitaanza kuzalishwa msimu wa 2019/2020.
Upatikanaji na udhibiti wa ubora wa Mbolea
17. Mheshimiwa Spika, hadi Machi 2019, upatikanaji na usambazaji wa mbolea nchini ulikuwa tani 492,394 ikilinganishwa na mahitaji ya tani 514,138 katika msimu wa 2018/2019. Aidha, Wizara kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imefanya ukaguzi kwa wauzaji wa mbolea 1,350 na wafanyabiashara 496 wapya wa mbolea  wamesajiliwa.
Upatikanaji wa Viuatilifu na Udhibiti wa Visumbufu
18. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara imenunua lita 296,000 na kilo 3,000 za viuatilifu vyenye thamani ya Shilingi bilioni tisa (9) kwa ajili ya kukabiliana na milipuko ya visumbufu vya mazao. Hadi kufikia Machi 2019, ndege waharibifu wa nafaka walidhibitiwa katika skimu za umwagiliaji za Kahe, Lekitatu na Misenyi kwa mazao ya mpunga na mtama.  Aidha, lita 119,000 kwa ajili ya kudhibiti Viwavijeshi Vamizi zimesambazwa katika Kanda ya Ziwa, Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Mashariki na kutoa mafunzo kwa maafisa ugani na wakulima 350.
Zana za Kilimo
19. Mheshimiwa Spika, takwimu zinaonesha kwamba wastani wa kitaifa wa matumizi ya zana bora za kilimo umeongezeka hadi kufikia asilimia 20 kwa matrekta na asilimia 27 kwa wanyama kazi ikilinganishwa na asilimia 14 ya  matrekta na asilimia 24 ya wanyama kazi mwaka 2013. Kutokana na ongezeko hilo, matumizi ya jembe la mkono yamepungua na kufikia asilimia 53 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na asilimia 62 kwa mwaka 2013.  Aidha, kupitia Mfuko wa Taifa wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) Wizara imendelea kutoa mikopo ya pembejeo na zana za kilimo. Katika kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019, mikopo 33 yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.50imetolewa.

4.2  Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji

20.  Mheshimiwa Spika, Tume ya Taifa ya Maendeleo ya Umwagiliaji imeendelea kusimamia utekelezaji wa Mradi wa  Skimu za Umwagiliaji za Wakulima Wadogo unaofadhiliwa na Serikali ya Japan. Mradi umekarabati skimu za umwagiliaji 129 katika Halmashauri 68 nchini pamoja na ununuzi wa mitambo ya ujenzi. 

4.3   Utafiti wa Kilimo na Uhaulishaji wa Teknolojia

21.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara kupitia TARI imegundua mbegu bora mpya aina nne (4) za mahindi. Mbegu hizo zina uwezo wa kutoa mavuno kwa wastani wa tani 5.8 kwa hekta kwenye mashamba ya wakulima katika ukanda wa chini na kati, zinahimili ukame na zina ukinzani wa magonjwa ya majani ya mahindi na michirizi na ukungu. Vilevile, kwa kushirikiana na kampuni binafsi, TARI imezalisha aina sita (6) ya miche ya mbegu bora ya migomba na kugundua aina 62 za  mbegu za mazao ya mikunde.

4.4  Maendeleo ya Mazao

22.  Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya  mazao mbalimbali  kwa kuimarisha huduma za utafiti, upatikanaji na utumiaji wa pembejeo na zana za kilimo, udhibiti wa visumbufu vya mazao, huduma za ugani, uongezaji wa thamani na upatikanaji wa masoko. Aidha, Wizara imeandaa mkakati wa miaka minne (2018/2019 – 2021/2022) wa  kuendeleza zao la michikichi.
Mazao Makuu ya Asili ya Biashara
23.  Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa mazao makuu ya biashara uliongezeka kutoka tani 901,641 msimu wa  2016/2017 hadi tani 967,184 msimu wa 2017/2018 ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.2. Katika msimu wa 2018/2019, Wizara ililenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara hadi kufikia tani 1,356,368 na hadi kufikia Machi 2019, tani 667,631.77 sawa na asilimia 49.2 ya lengo zilikuwa zimezalishwa na uzalishaji unaendelea.
Mazao ya Bustani
24. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018, uzalishaji wa mazao ya bustani ulikuwa tani milioni 5.33 na matarajio ya uzalishaji kwa mwaka 2018/2019 ni tani milioni 5.96. Hadi Machi 2019, uzalishaji umefikia tani milioni 4.36 sawa na asilimia 73.17 ya lengo na msimu wa uzalishaji unaendelea.

4.5  Ujenzi wa Miundombinu ya Kuhifadhi Mazao ya Kilimo na Masoko

Miundombinu ya Kuhifadhi Mazao ya Kilimo
25. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kutekeleza Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Nafaka. Hadi kufikia mwezi Machi 2019, asilimia 83 ya vifaa  vilikuwa vimeingizwa nchini kwa ajili ya ujenzi wa ghala katika vituo vya Makambako, Mbozi, Songea, Shinyanga na Dodoma.
Masoko ya Mazao ya Kilimo
26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara imeanzisha kitengo cha masoko ya mazao ya kilimo ambacho kinahusika na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi. Katika kutekeleza jukumu hilo, Wizara imeingia makubaliano ya Itifaki ya Usafi baina ya Tanzania na Serikali ya China kuwezesha kuuza muhogo nchini China ambapo hadi mwezi Machi 2019, kampuni tano zimesajiliwa kwa ajili ya kuuza zao hilo nchini China.
Hifadhi na Usalama wa Chakula
27. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, NFRA imenunua tani 46,236.035 za mahindi kwa ajili hifadhi na imeliuzia Shirika la Mpango wa Chakula Duniani tani 36,000 za mahindi zenye thamani ya Shilingi bilioni 21.  Aidha, Wizara imeanza kutekeleza Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu katika mazao unaolenga kudhibiti tatizo la sumukuvu katika mazao ya mahindi na karanga.

4.6  Huduma za Ushauri Kuhusu Utafiti, Mafunzo na Usambazaji Taarifa za Kilimo na Sayansi Shirikishi

Huduma za Ugani
28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara imeandaa rasimu ya  Mwongozo wa Utoaji na usimamizi wa huduma za ugani utakaotumiwa na Sekta ya Umma na Binafsi. Aidha, elimu kuhusu kanuni bora za uzalishaji wa mazao, kuongeza thamani mazao ya kilimo, upatikanaji wa masoko, mitaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo, pembejeo na zana bora za kilimo imetolewa kupitia maonesho na vyombo vya habari.
Vyuo na Vituo vya Mafunzo ya Kilimo
29. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara kupitia Vyuo vyake vya Kilimo  imedahili na kufundisha wanafunzi 2,389 ambapo wanafunzi 2,051 wamefadhiliwa na Serikali  na 338 wanajilipia wenyewe.  Kati ya  wanafunzi waliodahiliwa, wanafunzi 1,537 ni ngazi ya Astashahada na 852 ni  ngazi ya Stashahada. Jumla ya wanafunzi 1,026 wakiwemo 263 wa Stashahada na 763 wa Astashahada watahitimu masomo yao mwezi Juni, 2019.

4.7  Kuimarisha Ushirika

30. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Tume ya Maendeleo ya Ushirika kupitia Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limefanya ukaguzi wa nje kwa vyama vya ushirika 2,297. Kati ya Vyama vilivyokaguliwa, asilimia 4.6 vilipata hati inayoridhisha, asilimia 64.6 vilipata hati yenye shaka, asilimia 21.6 vilipata hati isiyoridhisha na asilimia 9.2 vilipata hati mbaya. Hali hiyo ya Vyama vya Ushirika siyo nzuri na hatuwezi kuifumbia macho. Natoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge katika maeneo yetu tuendelee kushirikiana na Halmashauri zetu kuvisaidia vyama hivi ambavyo ni mkombozi wa mkulima.

4.8   Usajili wa Wakulima

31. Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza usajili wakulima wote kwa mazao ambayo yanasimamiwa na Bodi.  Mazao hayo ni, kahawa, korosho, miwa, pamba, chai, mkonge, tumbaku na pareto. Hadi kufikia mwezi Machi 2019, wakulima 1,464,827 wametambuliwa na kusajiliwa katika maeneo mbalimbali nchini.

4.9  Masuala Mtambuka


32.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara imeendelea kuzingatia masuala mtambuka katika kutekeleza majukumu yake. Masuala hayo ni pamoja na ushiriki wa vijana katika kilimo, lishe, jinsia, hifadhi ya mazingira na VVU na UKIMWI.

5.0             MPANGO NA MAENEO YA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2019/2020

5.1  Kuongeza Tija katika Kilimo

    Upatikanaji wa mbegu bora za mazao
33.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi, imejipanga kuzalisha jumla ya tani 53,608.2 za mbegu mbalimbali. Wazalishaji hao ni pamoja na ASA, Vituo vya Utafiti, Magereza na Sekta binafsi. Vilevile, ASA itazalisha vipando bora vya mihogo pingili 7,000,000 na miche bora ya matunda 20,000. Ili kufikia malengo hayo, miundombinu ya umwagiliaji itaboreshwa katika mashamba yanayomilikiwa na ASA na eneo la uzalishaji wa mbegu litaongezwa hadi kufikia hekta 811 katika mashamba mbalimbali.
Upatikanaji na udhibiti wa ubora wa Mbolea
34. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itasimamia uagizaji na usambazaji wa tani 625,000 za mbolea zinazokadiriwa kutumika nchini. Aidha, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) itaongeza mauzo ya mbolea kutoka tani 10,000 hadi tani 100,000. Vilevile, ghala moja (1) lenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 za mbolea litakarabatiwa katika wilaya ya Tabora pamoja na kuanza ujenzi wa kiwanda cha kuchanganya mbolea kwa uwiano (blending plant) katika Mkoa wa Dar es Salaam. 
Upatikanaji wa Viuatilifu na Udhibiti wa Visumbufu
35. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itanunua na kusambaza lita 300,000 na kilo 3,000 za viuatilifu kwa ajili ya kukabiliana na milipuko ya visumbufu vya mazao.  Aidha, Wizara itaendelea kuimarisha kituo cha kudhibiti milipuko cha Kilimo Anga (Arusha) ili kutoa huduma bora. Vilevile, Wizara itaendelea kuvijengea uwezo na kukarabati vituo 10 kati ya 36 vya ukaguzi wa mazao mipakani.
Zana za Kilimo
36. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itaanzisha kituo kimoja (1) cha zana za kilimo kwa ajili ya kutoa huduma za kiufundi na mafunzo kwa watoa huduma binafsi  wamiliki na watumiaji wa zana za kilimo kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wakulima katika Kanda ya Ziwa. Vilevile, Wizara kupitia AGITF, imepanga kutoa mikopo 250 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.12.

5.2  Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji

37. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itafanya tathmini ya miradi ya umwagiliaji ambayo ujenzi wake haujakamilika ili miradi hiyo iweze kukamilishwa kwa awamu.
Aidha, kupitia Mradi wa Kuendeleza Skimu za Wamwagiliaji Wadogo, Wizara itakamilisha ujenzi wa skimu 16 za umwagiliaji katika maeneo mbalimbali.

5.3  Utafiti wa Kilimo na Uhaulishaji wa Teknolojia

38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia TARI imepanga kutafiti, kugundua na kusambaza aina 15 za mbegu bora za mazao ya nafaka, mizizi, mbegu za mafuta, mikunde, migomba na mazao ya bustani. Vilevile, Wizara itasafisha aina tisa (9) za mbegu ya mpunga na kuzalisha tani 10 za mbegu za awali katika Kituo cha Utafiti cha KATRINI. Aidha, kupitia kituo cha TARI Naliendele, Serikali itajenga kinu cha kubangua korosho chenye uwezo wa kubangua tani 1,800 kwa mwaka na kusindika tani 1,000 za mvinyo na sharubati (juice).

5.4  Maendeleo ya Mazao

39. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara imepanga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kipaumbele kwa kuendelea kuratibu utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya  mazao hayo ikiwemo kuimarisha utafiti, upatikanaji na utumiaji wa pembejeo na zana za kilimo, udhibiti wa visumbufu, huduma za ugani, kuongeza maeneo ya uzalishaji, uongezaji wa thamani na upatikanaji wa masoko.
Zao la Korosho
40. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Korosho itaendelea kutekeleza programu ya kuzalisha miche bora milioni 10 ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Aidha, Bodi kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango itahakiki na kulipa vikundi vya wazalisha miche ya mikorosho kwa msimu wa 2017/2018 ambao hawajalipwa katika mikoa saba (7). Vilevile, Wizara itaratibu upatikanaji na usambazaji wa tani 30,000 na lita 500,000 za salfa kwa ajili ya kudhibiti visumbufu vya zao la korosho.
Zao la Miwa na Uzalishaji wa Sukari
41. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Sukari itaratibu uzalishaji wa tani 403,786  za sukari kwa kuongeza eneo la uzalishaji wa kilimo cha miwa kutoka hekta 52,000 hadi hekta 97,000.  Wizara, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) itawezesha upatikanaji wa ardhi ya uwekezaji wa miradi mipya ya sukari katika Wilaya za Kasulu, Kibondo, Rufiji, Geita, Kilombero, Karagwe, Pangani, Bagamoyo na Morogoro. 
Zao la Kahawa
42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya kahawa itaongeza uzalishaji wa kahawa kutoka tani 65,000 hadi tani 80,000. Aidha Bodi imepanga kuzalisha na kusambaza miche milioni 10 ya kahawa katika Wilaya 42.
Zao la Mkonge
43. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Mkonge imepanga kuongeza uzalishaji wa mkonge kutoka tani 38,506 hadi tani 113,506 kwa kuongeza eneo la uzalishaji kutoka hekta 42,426.11 hadi 114,915.08, kusimamia uendeshaji wa mfumo wa kilimo cha wakulima wadogo cha mkataba na kuimarisha vyama vya ushirika na masoko ya mkonge.
Zao la Pamba
44. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Pamba imepanga kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka tani 222,000 hadi tani 700,000 na tija kutoka tani 300 hadi tani 600 kwa ekari. Aidha, upatikanaji wa mbegu za pamba utaongezeka kutoka tani 22,000 hadi 40,000 na upatikanaji wa viuatilifu utaongezeka kutoka lita milioni 7 hadi milioni 10.
Zao la Tumbaku
45. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Tumbaku imepanga kuongeza uzalishaji kutoka tani 55,000 hadi tani 60,000; kuimarisha vituo 1,972 vya kufungia na kuchambulia tumbaku; itaimarisha mfumo wa upatikanaji wa pembejeo za zao la tumbaku kwa kuwaunganisha watoa huduma wa pembejeo na Vyama vya Ushirika ili ziwafikie kwa wakati.
Zao la Chai
46. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Chai imepanga kuongeza uzalishaji wa chai kavu kutoka tani 34,000 hadi tani 40,000 ambazo ni sawa na tani 182,000 za majani mabichi ya chai. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF) itafufua kiwanda cha chai cha Mponde ili kuimarisha upatikanaji wa soko la majani mabichi ya chai kwa wakulima na kuongeza ajira.

5.5  Miundombinu ya Hifadhi na Uongezaji Thamani Mazao ya Kilimo

47. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia NFRA itakamilisha awamu ya kwanza ya Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi ambapo ujenzi wa maghala matano (5) yenye uwezo wa kuhifadhi tani 60,000 na vihenge  nane (8) vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 190,000 za nafaka utakamilika na hivyo kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000.

5.6  Vituo vya Utafiti huduma za Ugani na Mafunzo

Kuimarisha Vituo vya Utafiti
48. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itakarabati ofisi na kuvipatia vifaa muhimu vituo vya utafiti vya Ukiliguru, Ilonga na Tumbi. Aidha, miundombinu ya umwagiliaji ya vituo vya utafiti vya Ilonga, Naliendele, Ukiliguru na miundombinu ya uhifadhi wa mbegu katika vituo vya Uyole, Ilonga na Seliani itaboreshwa. 
Huduma za Ugani
49. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI na Sekta binafsi itakamilisha Mwongozo wa Utoaji na Usimamizi wa Huduma za Ugani Kilimo ili kuendana na mahitaji ya sasa ya utoaji wa huduma za ugani nchini.
Vyuo na Vituo vya Mafunzo ya Kilimo
50. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itadahili wanafunzi 2,500 ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa ufadhili wa Serikali. Vilevile, itakarabati miundombinu ikiwa ni pamoja na madarasa sita (6), ofisi 12, mabweni 12, maktaba sita (6) na mabwalo ya chakula sita (6) katika vyuo vya mafunzo ya kilimo vya Mtwara, Igurusi, HORTI Tengeru, Tumbi, Mlingano na Maruku.

5.7  Kuimarisha Ushirika

51. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Tume ya Maendeleo ya Ushirika itaimarisha udhibiti na usimamizi wa vyama vya ushirika; itahamasisha wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao kuanzisha SACCOS 1,500 kwenye maeneo yao; na itahuisha Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002 na kuipitia upya sheria za ushirika.

5.8  Uratibu, Takwimu, Ufuatiliaji na Tathmini

52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar itafanya Sensa ya kilimo. 

5.9  Masuala Mtambuka

53.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itaendelea kuzingatia masuala mtambuka yakiwemo ushiriki wa vijana katika kilimo, lishe, jinsia, VVU na UKIMWI na mazingira katika utekelezaji wa majukumu yake.

5.10     Maeneo Maalum ya Maboresho katika Kilimo

54. Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie maeneo machache ya kimkakati ambayo kama Wizara tumeona ni muhimu kuyafanyia maboresho ili kuimarisha usimamizi wa kilimo na kuwapatia wakulima huduma kwa urahisi zaidi. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:

 Mapitio ya Sera na Sheria 

55. Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza na itaendelea kuipitia Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 na sheria mbalimbali kwa lengo la kubaini maeneo ambayo yatapaswa kuhuishwa ili kwenda na hali halisi ya sasa na mwelekeo wa Serikali wa kubadili kilimo chetu kuwa kilimo cha kibiashara.  Mtazamo wa Wizara ni kuwa na Sheria moja itakayosimamia rasilimaliwatu, matumizi bora ya pembejeo, ardhi ya kilimo na maeneo mengine muhimu. 
Bima ya Mazao
56.  Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau imeanza mchakato wa kuanzisha Bima ya Mazao hapa nchini ili kumwezesha mkulima kulipwa fidia pale anapopata hasara. Maandalizi yanaendelea kufanyika ili katika mwaka 2019/2020 tuwe angalau na aina mbili za mifumo ya Bima ya mazao inayoweza kutumika hapa nchini. Hata hivyo, ili utaratibu huu uwezekane, kutahitajika takwimu sahihi za hali ya hewa pamoja na uzingatiaji wa kanuni bora za Kilimo.
Usajili wa wakulima
57.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itaimarisha kanzidata ya wakulima na kuendelea na usajili wa wakulima wa mazao mchanganyiko kwa kushirikiana kwa karibu sana na Vyama vya Ushirika na Taasisi nyingine kilele za wakulima kama vile Tanganyika Farmers Association (TFA). Ninawaomba Waheshimiwa Wabunge tusaidiane kuhamasisha wakulima katika maeneo yetu ili watakapofikiwa na zoezi la uandikishaji watoe ushirikiano na waelewe kwamba zoezi hili ni la kuwasaidia kupata huduma bora za Kilimo.
Masoko ya Mazao ya Kilimo
58.  Mheshimiwa Spika, Wizara imeamua kuimarisha utafutaji wa masoko ya mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi. Katika mwaka 2019/2020, Wizara itakiimarisha kitengo cha masoko kwa kukijengea uwezo wa kufanya uchambuzi na utafutaji wa masoko ndani na nje ya nchi.
 Aidha, elimu itaendelea kutolewa kwa wakulima ili wazalishe kulingana na mahitaji ya soko. Vilevile, tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi nyingine zinazohusika na masoko nchini ikiwemo TANTRADE na Soko la Bidhaa (TMX).
Mfumo wa upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo
59.  Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza zoezi la kupitia kwa kina mifumo iliyopo ya uzalishaji, uagizaji na usambazaji wa mbegu, mbolea na viuatilifu. Mifumo iliyopo kwa sasa inatofautiana kwani kuna baadhi ya Bodi za Mazao zinazojihusisha na uagizaji  na usambazaji wa pembejeo, wakati mwingine Vyama vya Ushirika vinaagiza na kusambaza pembejeo kwa wanachama wao, wakulima pia hununua pembejeo moja kwa moja kutoka kwa wafanyabiashara na pia mbolea kwa sasa inaagizwa kwa mfumo wa pamoja (Bulk Procurement).
60.  Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wa pembejeo za kilimo na tofuati ya mifumo hiyo, tumeamua kuipitia yote ili kuona mfumo bora unaoweza kutumika kuhakikisha pembejeo zenye ubora zinapatikana na kusambazwa kwa wakulima kwa wakati. Malengo yetu ni kukamilisha mapitio hayo na kupata majawabu ya mfumo bora ifikapo Juni 2019, ili mwaka 2019/2020 tuwe na mfumo madhubuti utakaokuwa na tija kwetu sote. Nina uhakika kwamba, mfumo mzuri wa upatikanaji na usambazaji wa pembejeo utawezesha uwepo wa pembejeo bora kwa bei nafuu na hivyo kuongeza matumizi kwa wakulima wetu.
61.  Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina ya hotuba yangu hususan mpango na maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2019/2020 yanapatikana ukurasa wa 61 hadi 91 katika kitabu cha hotuba cha Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2019/2020 kilichowasilishwa Bungeni.

6.0              SHUKRANI

62. Mheshimiwa Spika, kabla sijamaliza hotuba yangu naomba nitoe shukrani za dhati kwa watu, taasisi, makundi na wadau mbalimbali ambao tunashirikiana kuendeleza kilimo. Kwanza, nawashukuru sana, Naibu Mawaziri wa Kilimo, Mhe. Omary Tebweta Mgumba (Mb.) na Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.) kwa ushirikiano wanaonipatia katika kutekeleza majukumu yangu. Napenda pia, kuwashukuru  Katibu Mkuu, Mhandisi Mathew John Mtigumwe; Naibu Katibu Mkuu, Prof. Siza D. Tumbo; Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo; Taasisi na Asasi zilizo chini ya Wizara; watumishi wote wa Wizara; na wadau wa Sekta ya Kilimo kwa juhudi, ushirikiano na ushauri uliowezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Wizara kwa mwaka 2018/2019 pamoja na kuandaa Hotuba hii. Ni matarajio yangu kwamba, nitaendelea kupata ushirikiano wao katika mwaka 2019/2020.
63. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kuzishukuru Nchi na Mashirika mbalimbali ya Kimataifa ambayo yamesaidia Wizara katika juhudi za kuendeleza kilimo. Nachukua fursa hii kutaja baadhi yao kama ifuatavyo: Serikali za Japan, Marekani, Uingereza, Ireland, Malaysia, China, Indonesia, Korea ya Kusini, India, Misri, Israel, Ubelgiji, Ujerumani, Finland, Norway, Brazil, Uholanzi, Vietnam, Canada na Poland.  Ninayashukuru pia Mashirika na Taasisi za Kimataifa zifuatazo: Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, AU, IFAD, DFID, UNDP, FAO, JICA, EU, UNICEF, WFP, CIMMYT, ICRISAT, ASARECA, USAID, KOICA, ICRAF, IITA, IRRI, ILRI na CABI. Nyingine ni CFC, AVRDC, AGRA, CIP, CIAT/PABRA, UNEP, WARDA, Shirika la Kudhibiti Nzige wa Jangwani na HELVETAS.  Wadau wengine ni Shirika la Kudhibiti Nzige Wekundu, Bill and Melinda Gates Foundation, Gatsby TrustRockfeller Foundation, Aga Khan Foundation, Unilever na Asasi zisizo za kiserikali nyingi ambazo hatuwezi kuzitaja zote hapa.
64. Mheshimiwa Spika, natoa shukrani za pekee kwa wananchi wa Jimbo langu la Vwawa kwa ushirikiano wanaoendelea kunipa katika kipindi chote cha kuwawakilisha hapa Bungeni. Aidha, napenda kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya jimbo letu na Taifa kwa ujumla. Kwa umuhimu wa kipekee ninatoa shukrani za dhati, kwa wakulima wa nchi hii kwa kazi kubwa wanayofanya katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

7.0             MAOMBI YA FEDHA MWAKA 2019/2020

65.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara inaomba idhini ya kukusanya maduhuli ya Shilingi 3,472,515,000yatokanayo na vyanzo mbalimbali vya mapato.
66. Mheshimiwa Spika,  katika mwaka 2019/2020, Wizara ya Kilimo inaomba kutumia jumla ya Shilingi 253,856,943,970 kupitia Fungu 43, Fungu 05 na Fungu 24 kama ifuatavyo;
FUNGU 43 – Wizara ya Kilimo
67. Mheshimiwa Spika, jumla ya Shilingi 208,044,783,140zinaombwaKati ya fedha hizo, Shilingi 143,577,036,140 ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo Shilingi 82,000,000,000ni fedha za ndani na Shilingi 61,577,036,140 ni fedha za nje. Aidha, Shilingi 64,467,747,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapoShilingi 13,214,159,060 ni kwa ajili ya mishahara ya Wizara, Shilingi29,621,801,490 ni kwa ajili ya mishahara ya Bodi na Taasisi, Shilingi11,453,309,490 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo kwa Wizara naShilingi 10,178,476,510 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo kwa Bodi na Taasisi.
FUNGU 05 – Tume ya Umwagiliaji
68. Mheshimiwa Spika,  jumla ya Shilingi 37,485,090,830zinaombwaKati ya fedha hizo, Shilingi 32,501,462,613 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 3,000,000,000 ni fedha za ndani na Shilingi 29,501,462,613 ni fedha za nje.
 Aidha, Shilingi 4,983,628,217 zinaombwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo Shilingi 4,098,444,217 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Tume na Shilingi 885,184,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.
FUNGU 24 – TUME YA USHIRIKA
69. Mheshimiwa Spika,  jumla ya Shilingi 8,327,070,000 zinaombwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo Shilingi6,127,370,000 kwa ajili ya mishahara na Shilingi 2,199,700,000kwa ajili ya matumizi mengineyo.
Maelezo ya sehemu ya maombi ya fedha mwaka 2019/2020 kwa fungu 43, 65 na fungu 24 yanapatikana ukurasa wa 93 hadi 95 katika kitabu cha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo.

HITIMISHO

70. Mheshimiwa Spika, Pamoja na hotuba hii, vipo viambatisho vinavyotoa ufafanuzi wa baadhi ya maeneo.  Hotuba hii pia inapatikana katika tovuti ya Wizara ya Kilimo, www.kilimo.go.tz. Ninaomba kuhitimisha kwa kukushukuru wewe binafsi na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.
71. Mheshimiwa Spika,  NAOMBA KUTOA HOJA

Mchungaji Msigwa ahoji uhalali wa Spika Ndugai kumsimamisha Kuwasimamisha Uwakilishi wabunge wanaochaguliwa na Bunge kuwawakilisha katika mabunge mbalimbali

$
0
0
Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa amehoji bungeni uhalali wa uamuzi wa Spika Job Ndugai kusimamisha uwakilishi wa Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (CCM) katika Bunge la Afrika (PAP), bila Bunge la Tanzania kujadili

Jana Spika Job Ndugai alisema kuwa amemuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi wa Stehen Masele hadi Kamati ya Maadili itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.
 

"Katika uwakilishi wa Bunge la Afrika kumetokea matatizo makubwa hasa kwa Mhe.Steven Masele matatizo ya kinidhamu,Tumelazimika kumrudisha nyumbani kuanzia Jumatatu, badala yake amekuwa akionyesha kugoma, ni kiongozi ambaye anafanya mambo ya hovyo hovyo". Alisema Ndugai.

“Uhalali unatoka wapi na hawa hawakuteuliwa wamechaguliwa na nilitaka kujua anasimamishwa na kiti bila kujadili inatuchafua kama Taifa. Bunge litakuwa na nguvu gani ya kuwalinda hawa tunaowachagua,” amehoji Mchungaji Msigwa.

Akijibu mwongozo huo, Chenge amemtaka Mchungaji Msigwa kutowahisha hoja kwa maelezo kuwa tayari jana Alhamisi, Spika Job Ndugai alilitolea uamuzi kwa kuomba wabunge wasubiri taarifa itakapowasilishwa bungeni watakuwa na nafasi ya kujadili kwani milango haijafungwa.

Serikali kupitia upya mashamba yaliyofutwa na Rais Magufuli

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema wizara yake itapitia upya mashamba yote yaliyofutwa na Rais katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.

Lukuvi amesema hayo tarehe 16 Mei 2019 katika kata ya Chanzulu tarafa ya Kimamba Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata hiyo ili kutatua mgogoro wa Ardhi katika wilaya hiyo ikiwa ni jitihada za wizara kumaliza migogoro ya ardhi nchini.

Waziri Lukuvi amesema, katika maeneo mbalimbali yapo mashamba yaliyofutwa na Rais lakini hayajawekewa utaratibu  wa kuyatumia na hivyo kutoa fursa kwa wajanja wachache kujigawia na mengine kuyauza kwa wananchi bila kufuata utaratibu.

Amesema katika kuhakikisha mashamba yote yaliyofutwa na Rais katika wilaya ya Kilosa na kuzua mgogoro baina ya wananchi na wamiliki, Wizara yake imeamua kupeleka timu kutoka wizarani kwa ajili ya kuyafanyia uhakiki mashamba yote yaliyofutwa katika wilaya ya Kilosa.

"Tutayapitia mashamba yote yaliyofutwa na Rais na kujua kilichomo ndani yake na timu ya uhakiki niliyokuja nayo itanilitea mapendekezo ya namna ya kutumia mashamba na mengine watapewa wanaostahili na si kila mtu atapewa", amesema Lukuvi

Mashamba yenye mgogoro na wananchi katika wilaya ya Kilosa ni Noble Agriculture Enterprises, Magereza dhidi ya wananchi wa Mabane, Mbigiri na Mabwegere, Chadulu Estate, Shamba la Swai dhidi ya wananchi wa Ilonga na shamba la Mauzi Estate Malangali.

Kutana na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff  Mwenye UWEZO wakufanya dua mbali mbali  Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Adam shariff Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO   Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? . Adam shariff Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN  . Anatafsiri Ndoto. , KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na Biashara.


Mawasiliano: (+255 )715971688 au (+255  )756914036

Rais Magufuli Awataka Viongozi Anaowateua Washirikiane

$
0
0
Rais wa Tanzania John Magufuli amewataka viongozi wa kuteuliwa kuanzia ngazi ya ukuu wa mkoa mpaka ngazi za chini kujenga ushirikiano na uhusiano mzuri baina yao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao, vinginevyo hatasita kuchukua hatua.

Wito huo umetolewa kwa wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu tawala wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji.

Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo jana Mei 16, 2019 katika kikao kazi kati yake na viongozi hao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Amewaonya baadhi ya viongozi hao ambao wamekuwa na migogoro baina yao na hivyo kuathiri utendaji kazi na amesema endapo vitendo hivyo vitaendelea hatasita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja kuwaondoa katika nyadhifa zao.

Kujichua Kwa Muda Mrefu Husababisha Maumbile ya Kiume Kusinyaa na Kupungukiwa Nguvu za Kiume

$
0
0
Wanaume  wengi  waliofanya  mchezo wa  kujichua  kwa  muda  mrefu hupatwa  na  madhara  ya kuwa  na  kusinyaa  na  kudumaa  kwa  maumbile  yao  ya  kiume  ambayo  huenda  pamoja  na  tatizo  a  Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.

Tendo  la  kujichua  kwa  mwanaume  linapofanyika  kwa  kipindi  kirefu huathiri na  kuharibu mishipa  na  misuli  ya uume  na  hivyo  kusababisha  kujengeka  kwa mafuta na tishu zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri.  Jambo  hili  husababisha  makuu mawili; 1. Huzuia  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuongezeka jambo  linalotajwa  na  wanasayansi  kama jambo  muhimu  sana  katika  kukua  kwa  uume. 2. Huzuika  kutirika  kwa  damu  kuingia  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili  huathiri  sana  ukuaji  wa  maumbile ya kiume  kwa  sababu  yanapo tokea huathiri uzalishaji  wa  homoni  muhimu  zinazo  husika  na  ukuaji  wa  misuli  ya  uume na matokeo  yake husababisha  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa,kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama uume  wa  mtoto.
 
Hii ndio  sababu  kwanini watu  wengi  walio athirika  na  punyeto  hulalamika  kwamba  maumbile  yao  ya  kiume  hayajaongezeka  tangu  walipo anza  kujihusisha  na  punyeto  wakiwa  na  umri mdogo. 

Maumbile  yao  huonekana  kama  ya  watoto  kwa  sababu hayakupata  nafasi  ya  kupokea  vichochea  vya  kuyafanya  yakue  na  kuongezeka  tangu  walipo  anza  kujihusisha  na  punyeto.

Suluhisho  La  Tatizo La Maumbile  Ya  Kiume  Yaliyo  Sinyaa  Kwa  Sababu  Ya  Punyeto.
Kama  bado  unaendelea  kujihusisha  na punyeto  basi  jitahidi  uache  tabia  hiyo  mara  moja  kwani  inakuharibu. Inaweza  isiwe  rahisi  sana  kuacha  mara  moja  lakini  ukiweka  nia  thabiti  basi  unaweza  kuacha  kabisa  kama  walivyofanikiwa  kuacha  wengine  ambao  walikuwa  wametopea  kwenye  tabia  hiyo  lakini  wakajitahidi  kujilazimisha  na  hatimaye  wakafanikiwa  kuachana  kabisa  na  tabia  hiyo.

==>> Acha kuangalia video chafu za ngono.
Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie  punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. 


Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

==>>Epuka kukaa nyumbani peke yako;
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine. 


Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata kama vile misuli ya uume kulegea, kushindwa kurudia tendo uwapo na mwenzi wako, kuishiwa nguvu za kiume, maumbile kusinyaa, kurudi ndani na kuwa kama ya mtoto mdogo.

Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivyohivo, kama unaacha acha mara moja ili utunze heshima yako mbele ya mwenzi au mke wako.

Kama utaona  kuna  ugumu  wa  kuacha  tabia  hiyo  na tayari ushaapata madhara ya maumbile kusinyaa na kupungiwa nguvu za kiume, basi  wasiliana nasi kwa ushauri zaidi; Simu  0715741788 au 0754741788

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

$
0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0759208637 au 0620510598

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Serikali kuanzisha program maalum ya magonjwa yasiyoambukiza

$
0
0
Serikali iko mbioni kuanzisha program maalum ya magonjwa yasiyoambukiza kama ilivyo kwa magonjwa ya Ukimwi, TB na Marelia kwa kufikisha huduma ngazi ya zahanati.

Katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza wananchi wameshauriwa  kufanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki, kula mlo unaofaa, kutotumia tumbaku na pombe.

Hayo yameelezwa bungeni na Naibu waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile bungeni leo, Mei 17 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji (CCM).

Katika swali lake, Mwantum alitaka kujua serikali ina mpango gani kushughulikia magonjwa yasiyoambukiza kama vile, presha, kansa na kisukari.

Membe Amjibu Rostam Aziz Sakata La Kugombea Urais Mwakani

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe amemjibu mfanyabishara Rostam Aziz kuhusu suala la kugombea urais 2020 akimtaka hivi sasa ajikite kwenye masuala ya kitaifa yanayohusu uchumi.

Membe ametoa kauli hiyo akiwa nje ya jengo la Mahakama kuu ya Tanzania, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka kusikilizwa kwa kesi anayodai fidia dhidi ya mmiliki wa gazeti la Tanzanite Cyprian Musiba, ambapo aliulizwa swali kuhusiana na kauli inayodaiwa kutolewa na mfanyabiashara Rostam Aziz kuhusiana na uchaguzi wa mwakani.

Jana Mei 16, 2019, picha moja ya video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Rostam akizungumzia suala la urais 2020 na kumshauri Membe asijitokeze kuwania nafasi hiyo badala yake aachiwe Rais John Magufuli kwa awamu nyingine.

Membe amesema kuwa ; "Kuhusu kugombea mwakani napata kigugumizi kumjibu Rostam, lakini yeye ni mchumi na nitakutana naye nimshauri anafanya vizuri kwa Watanzania anapozungumzia masuala ya uchumi, inabidi azungumzie 'main issue' za nchi sio 'personal', hizi tunaachia watu wa chini."

"Kwa 'level' yetu ni kuzungumzia masuala ya kitaifa masuala ya kiuchumi, kwanini uchumi wetu upo hapa ulipo? kwanini wafanyabiashara wanafunga biashara zao, Rostam ni 'economist' namshauri ajiadress kwenye masuala ya kiuchumi, Rostam wewe ni mwenzetu sisi tumekatwa mkia." amesema Membe.

"Ukikatwa mkia hata ujitahidi vipi mkia wako ni mfupi tu, tunayoyazungumza ni vizuri tuwe 'consistency' mdomoni na dhamira yetu, Rostam ni mchumi mzuri sana, tuzungumzie masuala ya uchumi wa nchi yetu, kuliko kujaribu kuwa mtoto mzawa badala ya kukubali 'status' ..Rostam na mimi ni watoto wa kambo." alimalizia Membe.

Taarifa Mbalimbali Za Uhalifu Kutoka Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya

$
0
0
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANNE KWA TUHUMA ZA WIZI NA KUGHUSHI NYARAKA MBALIMBALI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne [04] ambao ni:-
1.     PILI OMARI [30] Mkazi wa Mbezi – Dar es Salaam
2.     HAMIS NGOWI [40] Mkazi wa Dar es salaama na
3.     OMARY MOHAMED [41] Mwalimu na Mkazi wa Nzovwe
4.     MARTHA KASMIRI [34] Mkazi wa Dar es salaam - Mbezi kwa tuhuma ya wizi katika Benki.

Mnamo tarehe 13.05.2019 saa 14:00 mchana huko katika Benki ya Posta tawi la Mwanjelwa iliyopo Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi kwa kushirikiana na maafisa wa benki hiyo waliwakamata PILI OMARI [30] na MARTHA KASMIRI [34] wote wakazi wa Dar es salaam - Mbezi wakiwa na nyaraka ‘salary slip’ zenye majina ya watu wengine ambao ni watumishi wa idara ya elimu, vitambulisho vya mpiga kura, fomu za utambulisho kutoka Jiji, fomu za mikopo kutoka benki ya Posta na barua za uthibitisho kutoka kwa mwajiri ambazo ni za kughushi.
Watuhumiwa wengine ambao ni HAMIS NGOWI [40] mfanyabiashara na mkazi wa Dar es salaama na OMARY MOHAMED [41] mwalimu na mkazi wa Nzovwe wamekamatwa wakati mtuhumiwa HAMIS NGOWI @ OPTATI NGOWI alipopekuliwa alikutwa na:-
1.     Mihuri 6 ya idara tofauti za serikali.
2.     Laini 10 za mitandao ya simu Vodacom, Tigo na Halotel,
3.     Picha ndogo 3 za watu tofauti ya jinsia ya kike,
4.     Funguo 2 za gari,
5.     Fomu za utambulisho kutoka Jiji,
6.     Fomu za mikopo kutoka benki ya Posta,
7.     ‘Salary slip’ pamoja na barua za uthibitisho kutoka kwa waajiri. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.
 
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WAWILI WANAOJIHUSISHA NA MATUKIO YA UNYANG’ANYI, WIZI NA UBAKAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia vijana wawili ambao ni:-
1.     NASIBU JUMA [20] Mkazi wa Nzovwe Mbeya
2.     BRIGHT THOMAS [19] Mkazi wa Mtaa wa Ndanyella Mbeya
Kwa tuhuma ya kujihusisha na matukio ya unyang’anyi, wizi na ubakaji katika maeneo ya Nzovwe, Iyunga na Iwambi Jijini Mbeya.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 14/05/2019 huko Iyunga katika Klabu cha Pombe cha London kilichopo Jijini Mbeya na katika upekuzi watuhumiwa walikutwa na :-
1.     Mapanga mawili [02]
2.     Mizula miwili [02]
3.     Makoti meusi mawili [02]
Katika mahojiana na watuhumiwa wamekiri kuhusika katika matukio mbalimbali kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 26/03/2019 saa 22:00 usiku huko Mtaa wa Inyala uliopo Kata ya Iyunga na Tarafa ya Iyunga ambapo walivamia nyumbani kwa Mwalimu wa Chuo MUST aitwaye WILLIAM MBATTA na kumjeruhi kwa mapanga sehemu ya kichwani na kisha kutoweka.
Mnamo tarehe 30/03/2019 saa 22:00 usiku katika viwanja vya MUST walimjeruhi ALLEN NYITTI kwa kumkata panga kichwani, kiunoni na tumboni na kupora simu aina ya Samsung Galaxy na pesa taslimu Shiling 21,000/=
Mnamo tarehe 05/04/2019 saa 02:00 usiku huko katika Mtaa wa Ndanyella, Kata ya Nzovwe, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya walimvamia FATUMA HAJI [21] walimbaka na kupora pesa taslimu shilingi 3,280,000/= pia waliiba TV aina ya LG na Redio Sub Woofer, Deck na simu ya mkononi aina ya Samsung J7. Mali zote zikiwa na thamani ya shilingi 4,120,000/=
Mnamo tarehe 04/05/2019 saa 02:45 usiku huko Kota za Tazara zilizopo Iyunga Mbeya walivamia nyumbani  kwa FRANK CHARLES na kumjeruhi kwa kumkata na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake yeye na mke wake aitwaye VICTORIA SAMWEL pamoja na kupora TV aina ya Boss yenye ukubwa wa inchi 55.

KUKAMATA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Mnamo tarehe 16/05/2019 saa 05:00 Alfajiri huko maeneo ya Block “T”, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, Askari Polisi wakiwa doria katika maeneo hayo waliliona gari lenye namba ya usajili T.937 CKD aina ya Toyota Mark II Blit na kulitilia mashaka na ndipo kukuta limebeba bidhaa mbalimbali zilizopigwa marufuku nchini ambazo:-
1.     Pombe kali aina ya PRINCE katoni sita @ chupa 20 sawa na chupa 120
2.     Pombe kali aina ya Officer”s Verve katoni 24 @ chupa 20 sawa na chupa 480
3.     Condom aina ya Ultimate Assured Protection katoni 63 ambazo zilitolewa na Serikali ya Marekani kwa nchi ya Zambia.
4.     Panga moja.
5.     Carolight 120ml pcs 36
6.     Citrolight 120ml pcs 84
7.     Coco Pulp 150mls pcs 24
8.     Coco Pulp 500mls pcs 06
9.     Coco Pulp 300mls pcs 36
10. Coco Pulp Lightening oil 50mls pcs 72
11. Coco Pulp 50g pcs 06
12. Carotone Crème ndogo 65mls pcs 24
13. Cocoderm pcs 06
14. Clinic Clear pcs 06
15. Extra Clair 120mls pcs 54
16. Elle 5 Crème pcs 3
17. Diproson tube 30g pcs 74
18. Diproson lotion 30mls pcs 48
19. Top Lemon Plus 170mls pcs 84
20. Carotone black spot corrector pcs 06
21. Dermotyl tube 15g pcs 10
22. Dermotyl lotion 30mls pcs 90
23. Dodo Crème ndogo pcs 06
24. Clairmen pcs 12
25. Bronz tone crème 125ml pcs 15
26. Miki Clair 160ml pcs 48
27. Movate Cream 30g pcs 50
28. Oranvate gel 30g pcs 50
29. Beaution Cream 330mls pcs 12
30. Miss Caroline 150mls pcs 12
31. Carolight Cream 120mls pcs 78
32. Diana lotion 30mls dozen 03 sawa na pcs 36
33. Teint Clair 150mls pcs 48
34. Betasol lotion 30mls pcs 36
35. Betasol tube 15g pcs 40
36. Perfect white cream 150mls pcs 12
37. Perfect white lotion 30mls pcs 06
38. Lemon vate cream 30g pcs 40
39. Mont Claire 30g pcs 10
40. Neoprosone Gel 30g pcs 10
41. Epiderm Creme 15g pcs 41
42. Epiderm Crème 30g pcs 24
Gari hilo lilikuwa likitokea Tunduma kuja Mbeya likiwa na bidhaa hizo. Gari pamoja na vielelezo vipo kituo cha Polisi. Msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa waliokuwa wakisafirisha bidhaa hizo unaendelea.

KUPATIKANA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Mnamo tarehe 13.05.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko maeneo ya Iwambi, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Polisi walimkamata kijana mmoja aitwaye ELIA MWAKALIKWE [25] Mkazi wa Iwambi akiwa na Pombe Kali zilizopigwa marufuku nchini aina ya Verve katoni 27 zikitokea nchini Zambia.

Imetolewa na;
[ULRICH O. MATEI – SACP]
   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kupewa vifaa na zana bora za kisasa.

$
0
0
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussen Mwinyi, amesema katika mwaka ujao wa fedha 2019/20, watalipa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vifaa na zana bora za kisasa.

Alisema sambamba na hilo, watatoa mafunzo kwa wanajeshi ili kuliongezea jeshi hilo uwezo na weledi wa kiutendaji, kiulinzi na kivita.

Akiwasilisha hotuba ya wizara hiyo bungeni jana, Dk. Mwinyi alisema pia wamepanga kuboresha mazingira ya kazi, kuimarisha upatikanaji wa huduma stahiki na mahitaji ya msingi kwa wanajeshi na watumishi wa umma.

Pia, kuwapatia vijana wa Tanzania mafunzo ya ukakamavu, umoja wa kitaifa, uzalendo na stadi za kazi.

Aidha waziri huyo alieleza kuwa wizara itaendeleza tafiti na uhaulishwaji wa teknolojia kwa kuimarisha na kuanzisha viwanda kwa madhumuni ya kuzalisha bidhaa na huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia.

Pia kuimarisha ushirikiano wa jumuiya za kimataifa, kikanda na nchi moja moja katika nyanja za kijeshi na kiulinzi.

Nyingine ni kufanya upimaji, uthamini na ulipaji fidia ya ardhi katika maeneo yaliyotwaliwa kwa matumizi ya jeshi.

Dk. Mwinyi aliongeza kuwa wataendelea kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kukabiliana na majanga na dharura pale inapohitajika.

“Kulipa stahili mbalimbali za maafisa, askari, vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa na watumishi wa umma.

“Kukamilisha sera ya ulinzi wa taifa, mwongozo wa viwanda jeshini na mpango wa maendeleo wa miaka 10, yaani 2018/29-2027/28 wa kuliimarisha Shirika la Nyumbu,” alisema.

Dk. Mwinyi pia alizungumzia hali ya usalama wa mipaka ya Tanzania kuwa ipo shwari licha ya kuwapo tishio kutoka kwenye vikundi vya kigaidi katika baadhi ya nchi jirani.

Waziri Mkuu Afungua Semina Ya Wanahisa Wa Benki Ya CRDB .....Autaka Uongozi Wa Benki Ya CRDB Uzidi Kuzingatia Misingi Ya Utawala Bora

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Benki ya CRDB uzidikuzingatia misingi ya utawala borana kuongeza juhudi katika utoaji wa huduma ili benki hiyo iendeleekuwa mfano wa mafanikio kwa taasisi zinazomilikiwa nakuendeshwa na wazalendo.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Mei 17, 2019) wakati akifungua semina ya wanahisa wa benki ya CRDB katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha. Semina hiyo inahudhuriwa na wanahisa 1,500.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeendelea kuimarisha misingi ya utawala bora ili kuleta matokeochanya, hivyo ni vema kwa uongozi wa benki hiyo ukaizingatia. 

“Serikali imeendelea kuhakikisha kwamba katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kunakuwepo na uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu, usawa, kuzingatia taratibu za kisheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Viongozi wakuu wa kitaifa.”

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kusisitiza misingi hiyo ya utawala bora ili kujiridhisha kuwa taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha zinaongozwa kwa kufuata misingi hiyo.

“Serikali imeendelea kusisitiza uwazi katikakuendesha shughuli za umma na makampuni yanayomilikiwa nawananchi bila usiri na kificho. Lengo ni kuwapa wananchi uwezo wakupima utendaji na uzingatiaji wa kanuni, taratibu na sheria.”

Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wa jinsia zote na makundi yote wanahusishwa katika kupanga nakufanya maamuzi ya mambo yanayowahusu ili kuwawezesha kujiletea maendeleo.
“Nyote ni mashahidi kuwa Serikali imeendelea kuhimiza utendaji unaozalisha matokeo  yanayokidhi lengo na matarajio ya watu na kuhakikisha taasisi za kifedha zinatimiza ndoto za wananchi katika kupata huduma nzuri ikiwemo upatikanaji wa mikopo na elimu ya matumizi bora ya fedha.”

Hivyo, Waziri Mkuu amesema ni vema benki hiyo kupitia kitengo chake cha elimu ihakikishe inatoa elimu kwa umma juu ya matumizi mazuri ya fedha zikiwemo za mikopo ili wananchi waweze kuitumia vizuri na kujiongezea tija.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Msekela alisema zaidi ya asilimia 80 ya hisa za benki hiyo zinamilikiwa na Watanzania ikiwemo Serikali, hivyo uongozi wa benki hiyo una jukumu kubwa la kuhakikisha wanatoa huduma bora.

Alisema wamejipanga kuboresha huduma zao ili wanahisa waweze kujivunia uwekezaji wao walioufanya kwenye benki hiyo. “Tupo tayari kuhakikisha benki ya CRDB inasonga mbele zaidi ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma kwa wateja.”

Mkurugenzi huyo alisema kuwa mbali na kuboresha huduma kwa wateja, pia wataongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na hatimaye waweze kutoa gawio kubwa kwa wanahisa wao. Benki ya CRDB inaongoza kwa kupata faida kubwa.

Kwa upande wake,Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kicheere ambaye alimuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango katika semina hiyo, alitumia fursa hiyo kuwashauri wananchi wajenge tabia ya kuwekeza kwenye hisa. Alisema mwamko wa  Watanzania katika kuwekeza kwenye hisa bado ni mdogo.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya May 18

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images