Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

DRC yafuta uchunguzi dhidi ya Moise Katumbi, huenda akarudi nyumbani

$
0
0
Waendesha Mashitaka wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefuta uchunguzi wa shitaka la jinai dhidi ya Moise Katumbi, mwanasiasa wa upinzani ambaye kwa sasa yuko uhamishoni.

Moise Katumbi alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuajiri askari mamluki wa kigeni wakiwemo askari kadhaa wa Kimarekani waliostaafu kwa lengo la kuangusha utawala uliopita wa Joseph Kabila.

Timothee Mukuntu, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Kijeshi wa DRC alitoa rasmi tangazo hilo jana Jumanne na kufafanua kuwa, "Kwa kuzingatia kuwa rais wa Jamhuri ametoa kipaumbele kwa suala la kupunguza taharuki za kisiasa, tumeona kuwa ni vyema tufutilie mbali uchunguzi huo."

Ingawaje waraka kuhusu tangazo hilo ulitiwa saini tarehe Mosi mwezi Machi, lakini uliwekwa hadharani kwa umma jana Jumanne. Wakili wa Katumbi amesema huu ni wakati mwafaka kwa mteja wake kurejea nyumbani. Hata hivyo Katumbi mwenyewe hajazungumza chochote kuhusu uamuzi huo. 
 
Septemba mwaka jana, Ofisi ya Mashtaka ya Umma nchini humo ilimzuia Moise Katumbi kuwania urais na kutishia kuwa angelikamatwa iwapo angelitia mguu wake nchini DRC, akikabiliwa na tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa. Felix Tshisekedi alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa urais wa Disemba mwaka jana 2018.

Meya huyo wa zamani wa Katanga mwenye umri wa miaka 54, alikimbilia uhamishoni mwezi Mei mwaka 2016 baada ya kuhitilafiana kisiasa na rais mstaafu Joseph Kabila.

Maduro alipongeza jeshi la Venezuela kwa kuzima jaribio la mapinduzi

$
0
0
Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amelipongeza jeshi la nchi hiyo kwa kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake, harakati ambazo anasema zinaungwa mkono na Marekani.

Maduro amesema Marekani ndiyo iliyochochea na kufadhili kwa hali na mali ghasia zilizoshuhudiwa jana katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini, lakini amesisitiza kuwa vyombo vya usalama vilifanikiwa kuzima ghasia hizo.

Amesema asilimia 80 ya askari waliotangaza jana kuliasi jeshi na kuyauga mkono maandamano ya wananchi walirubuniwa kufanya hivyo, lakini walipogundua kuwa hizo zilikuwa njama za vinara wa upinzani nchini humo Juan Guaidó na Leopoldo Lopez waliachana na njama hizo.

Vladimir Padrino López, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo sambamba na kupongeza juhudi za Rais Maduro kwa ajili ya kuimarisha usalama na demokrasia, amesema kuwa jeshi lingali linamuunga mkono kikamilifu rais wa nchi hiyo aliyeingia madarakani kwa kura za wananchi.
 
Hii leo waungaji mkono wa serikali ya mrengo wa kushoto ya Caracas wanatazamiwa kufanya maandamano makubwa na kuonyesha uungaji mkono wao kwa serikali ya Maduro, mkabala wa ubeberu na njama za Washington.

Mgogoro unaoshuhudiwa hivi sasa nchini Venezuela ulishtadi mwezi Januari mwaka huu baada ya Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani ambaye ni kibaraka wa Marekani na madola ya Magharibi, kujitangaza kuwa rais wa muda wa Venezuela, suala ambalo linakiuka katiba ya nchi hiyo.

Jana Jumanne, Guaido alitangaza kuwa ni siku ya kwanza ya duru ya mwisho ya 'harakati za ukombozi' za kumng'oa madarakani Rais Maduro.

Video Mpya: Gumbo ft Baba Diamond – Charanga

$
0
0
Wimbo mwingine ambao Baba Diamond Platnumz amesikika nao kwenye Bongo Fleva. Itazame hapa video yake.

Kikosi cha Taifa Stars cha AFCON chatajwa

$
0
0
Hiki ndicho kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoitwa kwaajili ya mashindano ya AFCON na CHAN.

Kujichua Kwa Muda Mrefu Husababisha Maumbile ya Kiume Kusinyaa na Kupungukiwa Nguvu za Kiume

$
0
0
Wanaume  wengi  waliofanya  mchezo wa  kujichua  kwa  muda  mrefu hupatwa  na  madhara  ya kuwa  na  kusinyaa  na  kudumaa  kwa  maumbile  yao  ya  kiume  ambayo  huenda  pamoja  na  tatizo  a  Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.

Tendo  la  kujichua  kwa  mwanaume  linapofanyika  kwa  kipindi  kirefu huathiri na  kuharibu mishipa  na  misuli  ya uume  na  hivyo  kusababisha  kujengeka  kwa mafuta na tishu zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri.  Jambo  hili  husababisha  makuu mawili; 1. Huzuia  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuongezeka jambo  linalotajwa  na  wanasayansi  kama jambo  muhimu  sana  katika  kukua  kwa  uume. 2. Huzuika  kutirika  kwa  damu  kuingia  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili  huathiri  sana  ukuaji  wa  maumbile ya kiume  kwa  sababu  yanapo tokea huathiri uzalishaji  wa  homoni  muhimu  zinazo  husika  na  ukuaji  wa  misuli  ya  uume na matokeo  yake husababisha  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa,kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama uume  wa  mtoto.
 
Hii ndio  sababu  kwanini watu  wengi  walio athirika  na  punyeto  hulalamika  kwamba  maumbile  yao  ya  kiume  hayajaongezeka  tangu  walipo anza  kujihusisha  na  punyeto  wakiwa  na  umri mdogo. 

Maumbile  yao  huonekana  kama  ya  watoto  kwa  sababu hayakupata  nafasi  ya  kupokea  vichochea  vya  kuyafanya  yakue  na  kuongezeka  tangu  walipo  anza  kujihusisha  na  punyeto.

Suluhisho  La  Tatizo La Maumbile  Ya  Kiume  Yaliyo  Sinyaa  Kwa  Sababu  Ya  Punyeto.
Kama  bado  unaendelea  kujihusisha  na punyeto  basi  jitahidi  uache  tabia  hiyo  mara  moja  kwani  inakuharibu. Inaweza  isiwe  rahisi  sana  kuacha  mara  moja  lakini  ukiweka  nia  thabiti  basi  unaweza  kuacha  kabisa  kama  walivyofanikiwa  kuacha  wengine  ambao  walikuwa  wametopea  kwenye  tabia  hiyo  lakini  wakajitahidi  kujilazimisha  na  hatimaye  wakafanikiwa  kuachana  kabisa  na  tabia  hiyo.

==>> Acha kuangalia video chafu za ngono.
Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie  punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. 


Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

==>>Epuka kukaa nyumbani peke yako;
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine. 


Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata kama vile misuli ya uume kulegea, kushindwa kurudia tendo uwapo na mwenzi wako, kuishiwa nguvu za kiume, maumbile kusinyaa, kurudi ndani na kuwa kama ya mtoto mdogo.

Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivyohivo, kama unaacha acha mara moja ili utunze heshima yako mbele ya mwenzi au mke wako.

Kama utaona  kuna  ugumu  wa  kuacha  tabia  hiyo  na tayari ushaapata madhara ya maumbile kusinyaa na kupungiwa nguvu za kiume, basi  wasiliana nasi kwa ushauri zaidi; Simu  0716-263605

Fisi Wazua Gumzo Na Kuwa Tishio Kahama

$
0
0
Kundi kubwa la  wanayama aina ya fisi limewajeruhi watu  watano  sehemu mbalimbali za miili yao katika  kata za  Nyandekwa na Kilago halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wakati wakijaribu kupambana na fisi hao waliovamia makazi ya watu.
 
Diwani wa Kata ya Kilago PETER EMANUEL amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia  April 28,2019  ambapo  majeruhi watatu hali zao bado hazijaimarika na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mji wa Kahama  na kwamba wananchi katika maeneo hayo amejawa na hali ya wasiwasi.
 
Wakizungumza wakiwa wamelazwa katika hospitali ya mji wa Kahama, baadhi ya  majeruhi wameiomba serikali  kuwadhibiti fisi hao kwani wanaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi na kwamba wamekuwa wakipambana nao mara kwa mara.
 
Afisa maliasiri  halmashauri ya mji wa Kahama, THOMAS MANUMBU amesema  tatizo la Fisi kuvamia makazi ya watu   bado lipo kwa wingi katika kata za pembezoni tangu mwezi wa pili mwaka huu  huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari wakati serikali inaendelea kupambana na    fisi hao.
 
Kwa upande wake Mhifadhi wa wanyanama Tanzania  (TAWA) wilaya ya Kahama, MAPANYA KARUTO  amewataka wananchi kutumia toshi nyakati za usiku na kwamba waondokane na imani za kishirikina  dhidi ya uwepo wa fisi hao.
 
 Credit;kahama Fm

Kesi Ya Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu Yakwama

$
0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na wenzake watano jana walishindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza shauri linalowakabili ikielezwa kuwa basi la Magereza limeharibika.
 
Maimu na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 100, likiwamo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni katika kesi ya uhujumu uchumi namba 7/2019.

Wakili  kutoka Takukuru, Leonard Swai  jana mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally alieleza kuwa, wamepewa taarifa na askari magereza kuwa basi linalowabeba washtakiwa hao kutoka gereza la Segerea kuelekea mahakamani hapo ni bovu.

Kutokana na hali hiyo Swai aliiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

Hakimu Ally baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 14 itakapotajwa tena.

Mbali na Maimu Washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni meneja biashara wa Nida, Aveln Momburi, mkurugenzi wa kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, ofisa usafirishaji, George Ntalima, mkurugenzi wa sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Kati ya mashtaka  yanayowakabili, 24 ni ya kutakatisha fedha,  23 ya kughushi,  43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la  kumdanganya mwajiri na matano ya  kuisababishia hasara mamlaka hiyo.

Mengine ni mawili ya kula njama ya kulaghai, mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Rais Magufuli awataka wafanyakazi kuwa wavumilivu kuhusu nyongeza ya mishahara

$
0
0
Rais Magufuli amesema kuwa hatoongeza mshahara mwaka huu, kwani ahadi yake ya kupandisha mishahara katika uongozi wake haijaisha kwa sababu bado hajamaliza muda wake madarakani.
 
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo May 1, 2019 mara baada ya hapo awali TUCTA kumuomba atimize  ahadi yake ya kuwaongeza wafanyakazi mishahara.

"Niwaambie ndugu zangu, Katibu mkuu TUCTA alinikumbusha kuhusu ahadi yangu, ninaikumbuka na ninasema muda wangu bado nipo madarakani, ninachoomba muwe na subira.

“Ni kweli kwenye sherehe kama hizi mwaka jana niliahidi kuwa nitaongeza mishahara ya wafanyakazi kabla sijaondoka madarakani, ndugu zangu tuvumilie tu sikutaka kuwadanganya hapa kuwa nimewaongezea mishahara halafu fedha mtakazozipata hazipo, nyinyi endeleeni kuvumilia tupo katika muelekeo mzuri wa suala hili”, Amesema Rais Magufuli na kuongeza;


“Ningeweza kuwaongezea elfu 5 au 10, kesho tu bidhaa zingeanza kupanda hivyo lazima kwanza tujenge uchumi imara. Mimi mwenyewe nilikuwa mwalimu na nikaenda kuoa mwalimu anayejua shida zetu Serikali inawapenda wafanyakazi.



Rais Magufuli Atoa Maagizo Bodi za Mishahara nchini

$
0
0
Rais Magufuli amesema haelewi sababu za bodi za mishahara nchini Tanzania kutokutana kwa maelezo kwani yeye hana tatizo na kuonya vikao vyao kutokuwa uchochoro wa kutumia fedha za Serikali vibaya.

Ameyasema hayo leo katika sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi, maadhimisho hayo kwa Tanzania yamefanyika  katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

“Kwangu mimi hata wakitaka kukutana leo sina shida, sina tatizo namuagiza waziri mwenye dhamana kuhakikisha bodi hizo zinakutana lakini vikao vyao visiwe vichochoro vya kutumia fedha za Serikali vibaya,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Lazima nitoe angalizo hilo maana unaweza kusikia wameenda kufanya vikao Dubai lakini suala la kukutana na kujadili masuala mbalimbali kati ya wafanyakazi na yale yanayopaswa kutatuliwa mapema nasema kwa dhati sina tatizo mkutane.”

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 2

BREAKING: Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi amefaiki dunia

$
0
0
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP , Dkt Reginald Abraham Mengi (75) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Dk Mengi amefariki dunia akiwa jijini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Dk Mengi alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa barani Afrika, ambapo sehemu ya utajir wake aliuelekeza kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes mwaka 2014, utajiri wa bilione huyo ulitajwa kuwa ni TZS trilioni 1.3 ($560 milioni).

Enzi za uwahi wake na katika shughuli zake aliweza kushinda tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa, pamoa na kuandika kitabu chake cha I Can, I Must, I will.

Mungu Ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi. Amina

Rais Magufuli Atuma Salamu za Pole Kufuatia Kifo cha Mzee Reginald Mengi

$
0
0
Rais Magufuli ametuma salamu za Pole kwa familia na Wafanyakazi wa IPP Media kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo.

 Mengi amefariki dunia usiku wa kuamkia Leo Mei 2, 2019 akiwa Dubai

"Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo ktk kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabishara. "Ameandika Rais Magufuli

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Ubalozi wa Marekani Wamlilia Mzee Reginald Mengi

$
0
0
Ubalozi wa Marekani nchini umesema kuwa umepokea kwa majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi kilichotokea huko Dubai falme za Kiarabu.

Mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange Ahukumiwa Jela Wiki 50

$
0
0
 Mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange, amehukumiwa hapo jana kwenda jela kwa wiki 50, kwa hatia ya kukiuka amri ya korti ya Uingereza miaka saba iliyopita.

Assange aliomba hifadhi katika ubalozi wa Equador mjini London, kuepuka kusafirishwa hadi Sweden alikokuwa akikabiliwa na tuhuma za ubakaji, ambayo anayakanusha.

Mfichuzi huyo wa nyaraka za siri ambaye alikamatwa Aprili mwaka huu baada ya kufukuzwa ubalozini alikokuwa akijificha, anakabiliwa pia na kitisho cha kupelekwa Marekani. 

Nchi ya Marekani inamtafuta kwa kuvujisha mamilioni ya nyaraka zake za siri. Kesi yake ya kwanza kuhusiana na ombi la Marekani, litasikilizwa leo Alhamis.

Wasanii nchini Wamlilia Mzee Reginald Mengi

$
0
0
Wasanii nchini wamezidi kutuma salamu za pole kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi kilichotokea usiku wa kuamkia leo. 


Chini ni baadhi ya  wasanii waliotuma salamu zao za pole kupitia mitandao.

Idris Sultan - Jana ilikuwa birthday ya Ruge na leo msiba wa Mengi. Another media tycoon is gone. Sina nafasi ya kuongezea kwenye huzini ambayo wote tunayo ila tukumbuke siku zake za mwisho na mkewe zilitupa wote furaha sanaaaa sio siri. It’s a life well lived. Innalillahi wainna ilaihi rajiun.
Vanessa Mdee - What a loss. Poleni sana kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na kila mmoja aliyeguswa na msiba huu hakika ni wengi. Thankyou for your time, brilliance and the constant motivation 🙏 prayers up kwa familia na watoto wote 🙏 Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mzee Mengi pahali pema. Praying for you sis J Mengi
Diamond Platnumz-  Dah! What a Sad news....May your Humbled Soul Rest in Paradise...🕯🙏🏻🕯
Mwijaku -  Binaaadamu hupimwa kwa mchango wake aliouacha kwenye jamii na sio umri alioishi kwenye jamii. Rest easy ,Reginald Mengi ,go and Dance with angels.Rest In Paradise. Pole J Mengi.

Chege Chigunda - Lala salama babaetu MENGI Mungu akuweke mahala pema peponi,poleni ndugu jamaa na marafiki wote mlo guswa na msiba huu mkubwa🙏 poleni sana wafanya kazi wa IPP Group Mipango ya Mungu haina makosa

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Wanasiasa na Viongozi Wengine Waombolea Kifo cha Reginald Mengi

$
0
0
 Watu mbalimbali wamezidi kutuma salamu za pole kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi kilichotokea usiku wa kuamkia leo. 

Chini ni baadhi ya  viongozi waliotuma salamu zao za pole kupitia mitandao.

Peter Msigwa: Haijalishi tunaishi muda gani hapa duniani, cha msingi unatoa mchango gani hapa duniani kabla ya kifo. Dr Mengi sio tu uliwavutia wengi ,bali uligusa sana maisha ya wengi , umetuonyesha kuziacha jamii zetu bora zaidi kuliko tulivyo zikuta. Is all about donation not duration. RIP 

Maria Sarungi: Rest in Peace @regmengi 🙏🏽 Your contribution to the growth of our industries in #Tanzania remain indelible. Pumzika kwa amani na Mungu awape faraja wanafamilia na marafiki katika kipindi hiki kigumu

Faustine Ndugalile: Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mzee Reginald Mengi. Hivi karibuni tulikutana na kuongea kuhusu kuanzisha huduma ya stem cell therapy hapa nchini. Nitakukumbuka kwa ubunifu, uthubutu na kutosita kujaribu mambo mapya. Natoa pole kwa familia na IPPMEDIA. RIP Mzee Mengi

Makamu wa Rais, Samia Suluhu: Moja ya vitu ulivyotuachia ni ule wepesi wako wa kusaidia masuala ya kijamii, daima tutakukumbuka. #RIPReginaldMengi

Zitto Kabwe: Msiba mkubwa kwa Taifa na haswa kwa Familia ya Mzee @regmengi . Pole sana @JNtuyabaliwe na Watoto, The twins. Poleni sana Regina, Abdiel na familia nzima ya Makampuni ya IPP. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi mahala pema anapostahili

Nape Nnauye - Umeacha alama kubwa! Nimejifunza mengi kwako, Rafiki, Mshikaji, Kiongozi na Mzazi! Ulinifundisha kuwa KUKATA TAMAA NI DHAMBI! {Msalimie Mzee Sitta, mkumbushe kile kikao chetu Cha mwisho nyumbani kwako}Pumzika kwa Amani Dr. R.A Mengi.

Godbless Lema - Watu wanagopa kifo,kimsingi tunacho ogopa ni kuwahi kufa kwani kifo hakizuiliki,ktk maisha ni vyema kuishi maisha ya baraka na watu wote,ili utakapo tangulia maisha yako yaweze kuwa na thamani.Nina mshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Dr R.Mengi,kwani alijua thamani ya ubinadamu

January Makamba - Pole kwa Jacqueline na Regina, Abdiel and the twins - na familia nzima ya IPP Group. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi peponi.

Makatibu Wakuu Tanzania Na Uganda Wahitimisha Mkutano Wa Mahusiano Na Kusaini Makubaliano

$
0
0
Na Munir Shemweta, BUKOBA
Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, Kiuchumi na Kimazingira umemalizika Bukoba mkoani Kagera kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot kusaini makubaliano yaliyofikiwa.

Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika juzi na kuwakutanisha Makatibu Wakuu wa nchi za Tanzania na Uganda kutoka Wizara zinazoshughulika na masuala ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mambo ya Nje, Mifugo na Uvuvi, Maji pamoja na Nishati.

Kabla ya mkutano huo, Wataalamu wa sekta zinazohusika kutoka nchi hizo mbili walikutana na kujadiliana namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda katika eneo la Mpaka na baadaye kuwasilisha mapendekezo kwa Makatibu Wakuu kwa lengo la kujadiliwa kwa manufaa ya nchi hizo.

Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda, Mpango Kabambe wa Utunzaji Mto Kagera na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera kati ya Tanzania na Uganda.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel alisema katika siku mbili za mkutano huo, nchi washiriki zilijadili namna bora ya kuendeleza mahusiano ya mipakani kwa lengo la kurahisisha mambo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira sambamba na kujadili jinsi ya kuboresha matumizi endelevu ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera ili ziweze kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Okidi Ollot alisema, mkutano huo ni njia sahihi ya kuonesha kuimarika kwa mahusiano ya Tanzania na Uganda na kusisitiza kuwa kilichofanyika ni kuonesha uhalisia wa ushirikiano kwa lengo la  kuwafanya wananchi wa pande zote kunufaika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alizishukuru pande zote mbili za nchi za Tanzania na Uganda kwa kufanikisha kufikiwa makubaliano aliyoyaeleza kuwa yana lengo la kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.

Kijiji Chapiga Marufuku Umbea ....Ukikamatwa Unapiga Umbea Faini Yake ni USD Dola 4 sawa na Tsh. 9200 pamoja na kufanya usafi masaa matatu

$
0
0
Binolonan ambacho ni  Kijiji kinachopatikana kaskazini mwa mji mkuu wa Ufilipino, Manila, kimepiga marufuku kufanya umbea.

Meya wa mji, Ramon Guico, amesema umbea ulisababisha ugomvi mkubwa utokee katika kijiji hicho kitu kilichopelekea vikao vya viongozi kuchukua tahadhari kwa kupiga marufuku kufanya umbea.

Guico alisema kuna umbea wa aina nyingi, lakini katika kijiji hicho kesi nyingi ni za umbea unaohusu mali, pesa na mahusiano. 

Sababu ya marufuku hio ni kukumbusha kwamba kila mtu na hasa wanaoishi katika kijiji hicho anawajibika kwa atakayoyasema. 

Pia wanataka kuonyesha watu wengine kwamba watu wa Binolonan ni watu wazuri na eneo hilo ni salama.

Guico, aliongeza kwamba hatua walizochukua zitaongeza ubora wa kijiji hicho.

Guico aliongeza kwamba maeneo ambayo watu wake hawafanyi umbea yana Baraka zaidi, kwa sababu yeye anaamini watu wana kazi za muhimu zaidi za kufanya badala ya kufanya umbea.

Kwa mujibu wa sheria atakayekutwa na hatia ya kufanya na kueneza umbea na maneno ya uongo atatozwa faini pesa taslimu peso 200 takribni dola za kimarekani 4. Pamoja na tozo hilo la pesa atapewa adhabu ya kukusanya takataka kwa masaa 3.

Atakayekutwa na hatia ya kufanya umbea kwa mara ya pili atatozwa faini ya pesa taslimu peso 1000 takriban dola 20, faini hiyo itaambatana na kupewa adhabu ya kutoa huduma kwa jamii kwa masaa 8.

Jaribio La Mapinduzi Lafeli Tena Venezuela....Urusi na Marekani Wachimbana Biti Kali

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi  Sergei Lavrov amelaani vikali uungaji mkono  wa Marekani kwa kinara wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido ambaye alikuwa amedai amepata uungaji mkono wa jeshi katika jaribio lililofeli la kumpindua Rais Nicolas Maduro.

Lavrov aliyasema hayo jana Jumatano wakati akizungumza kwa simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo ambapo amemfahamisha bayana kuwa, uingiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya Venezeula ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa.

Lavrov aidha amekosoa vitisho vya wakuu wa Marekani hasa Rais Donald Trump kuhusu kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Rais Maduro na kusema, utekelezwaji wa hatua kama hizo utakuwa na matokeo mabaya.


Jumanne April 30, Caracas, mji mkuu wa Venezuela ulipitia siku ngumu na iliyojaa mitihani. 

Kwa mujibu wa viongozi wa  Venezuela, Marekani na watu wanaodaiwa kuwa vibaraka wake wa ndani wanaoongozwa na Juan Guaido aliyejitangaza kuwa Rais na ambao wanaendesha vurugu na upinzani dhidi ya serikali  ya nchi hiyo walifanya jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali ya mrengo wa kushoto inayoongozwa na Nicolas Maduro, kwa kushirikiana na baadhi ya wanajeshi, lakini kwa mara nyingine tena Marekani ikawa imeshindwa katika jaribio lake hilo la mapinduzi nchini Venezuela.

Huku akisisitiza kuwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali halali ya nchi hiyo limefeli, Jorge Arreaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela amesema kwamba licha ya juhudi zote zinazofanywa na wapinzani na serikali ya Washington kwa ajili ya kuupindua mfumo wa kisiasa wa Venezuela, lakini bado Rais Nicolas Maduro anaidhibiti nchi kwa uungaji mkono wa wananchi na jeshi.

Akizungumza juzi akiwa katika uwanja wa ndege wa kikosi cha anga cha La Carlota katika viunga vya mji wa Caracas, Juan Guaido alidai kuwa jeshi haliko tena pamoja na Nicolas Maduro na hapo akatangaza rasmi kuanza kwa operesheni aliyoitaja kuwa ni ya  'kuikomboa Venezuela.' 

Licha ya matamshi hayo , wanajeshi watiifu kwa serikali halali ya Venezuela wangali wanamuunga mkono Rais Maduro pamoja na katiba ya nchi hiyo na wamefanikiwa kufelisha jaribio hilo la mapinduzi kwa ushirikiano wa wananchi. 

Baada ya kushindwa mapinduzi hayo, Vladimir Padrino López, Waziri wa Ulinzi wa Venezuela amesema: 'Wanajeshi wa nchi hii wamesimama imara kulinda katiba na serikali halali ya Venezuela.'
 
Hali ya hivi sasa ya Venezuela na hasa kushindwa kwa mapinduzi hayo kumeamsha hasira ya viongozi wa Washington kwa kadiri kwamba mara tu baada ya kushindwa mapinduzi hayo, John Bolton, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, alikariri misimamo ya chuki ya nchi hiyo dhidi ya Caracas na kutishia kwamba bado machaguo yote yako mezani dhidi ya Venezuela ikiwemo kuivamia kijeshi.

Maafisa wa Marekani pia wamedai kwamba uungaji mkono wa baadhi ya nchi za kigeni zikiwemo Urusi na Cuba kwa Venezuela ndio umepelekea kushindwa mapinduzi hayo. 

Marekani inadai kuwa kurejesha demokrasia Venezuela, kuboresha uchumi wa nchi hiyo na kupeleka huko misaada ya kiuchumi, chakula na madawa ndiko kumeifanya itake kuiondoa madarakani serikali halali ya Maduro, katika hali ambayo viongozi wa Caracas wanasema kuwa hali mbaya ya nchi hiyo imesababishwa na siasa za vikwazo za Washington na msimamo wake wa kuongeza mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi dhidi ya nchi hiyo.

Kwa mtazamo wa viongozi wa Venezuela, Marekani inafanya juhidi za kuhuisha nafasi yake ya zamani katika nchi za Amerika ya Latini na hasa nchini Venezuela ambayo ina utajiri mkubwa wa mafuta. 

Akizungumzia suala hilo, Igor Kostyukov, Mkuu wa Idara ya Intelijensia ya Jeshi la Russia GRU, huku akiashiria kwamba kila mwaka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani hutumia kwa uchache dola bilioni moja na nusu kwa ajili ya kuongeza ushawishi wake katika eneo la Amerika ya Latini, ameonya kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Marekani kutumia hivi karibuni 'mapinduzi ya njano' ambayo inayatekeleza sasa huko Venezuela kwa ajili ya kuziangusha serikali za Nicaragua na Cuba.
 
Hali ya hivi sasa ya Venezuela ni tata mno. Viongozi wa Venezuela wakiwemo wanajeshi wametangaza kwamba wanadhibiti hali ya mambo nchini humo na kwamba jaribio la mapinduzi limeshindwa. 

Kwa mara nyingine jeshi limetangaza utiifu wake kwa serikali ya Maduro na wananchi wameitikia kwa wingi mwito uliotolewa na chama cha Umoja wa Kisoshalisti kwa ajili ya kukusanyika mbele ya ikulu ya nchi hiyo.

Katika upande wa pili, Juan Guaido ambaye anaungwa mkono kwa hali na mali na utawala wa Washington amewataka wafuasi wake waingie mitaani. 

Viongozi wa Washington wamekerwa sana na jinsi mambo yalivyobadilika kinyume na matarajio yao na wanafuatilia kwa karibu mno matukio ya Venezuela. 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images