Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ujenzi Wa Mradi Wa Maji Magu Wafikia Asilimia 85

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga amesema ujenzi wa mradi wa maji katika Mji wa Magu, Mkoani Mwanza umefikia asilimia 85 za ujenzi wake.

Mhandisi Sanga alisema hayo alipofanya ziara kwenye mradi huo Aprili 24 kwa lengo la kujionea na kujiridhisha hatua iliyofikiwa ya ujenzi wake ambao unasimamiwa na MWAUWASA kwa niaba ya Wizara ya Maji.

Mhandisi Sanga alisema utekelezaji wa jumla wa mradi umefikia asilimia 85 na ulazaji wa bomba kwa ajili ya kuunganisha wananchi imefikia asilimia 95.

Alibainisha kwamba mradi una uwezo wa kuzalisha lita 7,250,000 ambayo ni mahitaji ya Mji wa Magu kwa miaka 20 ijayo. “Mradi huu ni mkubwa sana hata kama wananchi wa Magu wataongezeka mara mbili zaidi bado utaweza kuwahudumia,” alisema Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga alisema kukamilika kwa miradi inayotekelezwa chini ya ufadhili wa Serikali kupitia mpango wa Uboreshaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria, miji yote mikuu ya Mkoa wa Mwanza itakua imepata huduma ya majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria.

“Mradi ukikamilika miji yote mikuu ya Mkoa wa Mwanza itakua imepata huduma ya maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria kwani tumepeleka Nansio, Sengerema, Ngudu, Magu na Misungwi,” alisema.

Mhandisi Sanga aliupongeza uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wa Wilaya ya Magu kwa ushirikiano mkubwa wanaotoa kwenye shughuli mbalimbali za utekelezaji wa mradi.

Aidha, aliwapongeza wananchi kwa ushirikiano wanaoutoa hususan wa ulinzi wa miundombinu ya maji inayotumika kwenye ujenzi wa mradi huo.

Waziri Mkuu: Kesho Ni Siku Ya Mapumziko

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kesho tarehe 26 Aprili, 2019 ni siku ya mapumziko na hakutakuwa na shamrashamra za sherehe.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dodoma leo (Alhamisi, Aprili 25, 2019), Waziri Mkuu amesema kesho ni siku ya mapumziko kitaifa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini hakutakuwa na sherehe.

Amesema jumla ya sh. milioni 988.9 ambazo zilikuwa zimepangwa kwa ajili ya sherehe hizo, zimeokolewa na zitapangiwa shughuli nyingine.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 26

Nape Afunguka Tena Tukio la Kutishiwa Bastola

$
0
0
Mbunge wa Mtama,Nape Nnauye amezungumzia kwa mara ya kwanza tukio lake la kutishiwa bastola miaka miwili iliyopita.

Katika maelezo yake, Nape amsema wakati anatishiwa kwa bastola miaka miwili iliyopita  walikuwapo watu mbalimbali akiwamo Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD)pamoja na Kamanda wa polisi wa Mkoa (RPC).

Pamoja na hayo alishangaa tukio lake hilo kutotolewa ufafanuzi wowote na Serikali wakati inalijua vizuri.

Nape aliyasema haya bungeni wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi kujadili bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Aidha Nape aliitaka Serikali ijitenge na matukio ya kihalifu kama ya tukio lake kwa kuwa anaamini aliyemtishia hakutumwa na Serikali ingawa anamfahamu vizuri.

Serikali Yasitisha Uhamisho wa Walimu

$
0
0
Serikali imezuia uhamisho wa walimu nchi nzima ikieleza kuwa sababu za kuomba hivyo nyingi ni za uongo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi,  Mwita Waitara amesema hayo bungeni jana  Alhamisi Aprili 25,  akieleza kuwa kuanzia sasa uhamisho utatolewa kwa kibali maalumu na masharti muhimu kutoka serikalini.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mrimba (Chadema), Suzan Kiwanga ambaye amehoji kuhusu upungufu wa walimu hasa wa kike katika wilaya ya Kilombero.

"Suala la kuhamisha walimu kwa uhamisho wa ndani liko chini ya mkurugenzi na hapa ninaagiza kufanyika marekebisho hayo mara moja tena ndani ya miezi miwili au wiki mbili ili kupata walimu kwa jinsia zote," amesema.

Waitara amesema Serikali imefikia hatua ya kuzuia uhamisho kutokana walimu wengi kusingizia kuwa wanawafuata wenza wao na kugundulika kuwa sababu nyingi ni za uongo.

Katika swali la msingi, Mbunge Viti Maalum (CCM), Ferister Bura alitaka kujua ni lini Serikali itaajiri walimu 527 wa masomo ya sayansi katika mkoa wa Dodoma.

Akijibu, Waitara alisema ni kweli Dodoma ina upungufu wa walimu lakini Serikali imeshatoa kibali cha kuajiri walimu 4,549 wakiwamo walimu wa sayansi na hisabati.

Kangi Lugola: Sijawahi Ona Mtu Muongo Tanzania Kama CAG

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema hajawahi kumuona mtu muongo katika nchi hii kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad.

Amesema kwamba taarifa iliyotolewa na CAG katika ukaguzi wake kwamba Jeshi la Polisi liliagiza sare hewa za polisi haina ukweli wowote kwa kuwa sare hizo zipo na ziko kwenye makontena katika ghala  kuu la polisi.

Ili kuthibitisha kauli yake,Waziri Kangi alisema yuko tayari kwenda kutembelea ghala hilo na kama sare hizo hazitakuwemo, uwaziri wake ana uweka rehani.

“Sijawahi kuona mtu muongo kama CAG, Jeshi la Polisi hakuna sare hewa. Ninaomba maofisa wa ofisi ya CAG twende nao stoo wakaone sare mpya za jeshi la polisi. Kama nasema uongo nitajivua nguo na ninaweka uwaziri wangu rehani” Alisema  Kangi Lugola   jana bungeni   alipokuwa akihitimisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Pamoja na hayo,Waziri Kangi aliwataka wabunge wamuogope Mungu na kwamba wasipende kushabikia mambo yasiyokuwa na ukweli wowote na kwamba watu wasiokuwa wakweli waogopwe kama ukoma

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

$
0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0763172670/ 0715172670

Bunge la Uingereza latahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea vita vya silaha za nyuklia duniani

$
0
0
Kamati ya Mahusiano ya Kimataifa ya Bunge la Uingereza imetoa taarifa inayoonya juu ya uwezekano wa kutokea vita vya silaha za nyuklia kati ya nchi zenye silaha hizo.

Kamati hiyo imeeleza kwamba kutokana na kushindikana ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi zenye silaha za nyuklia na kadhalika kuendelea kustawishwa kila siku teknolojia na uwezo mpya katika uwanja huo, kumeongeza hatari ya kutokea vita vya silaha za nyuklia dunia. 

David Howell, Mkuu wa Kamati hiyo ameitaka serikali ya nchi hiyo kuupa umuhimu wasiwasi wa wawakilishi wa bunge hilo. 

Aidha Howell ametaka kuongezwa kiwango cha mazungumzo kati ya nchi zenye kumiliki silaha hizo za maangamizi. 

Ripoti ya kamati hiyo juu ya uwezekano wa kutokea vita vya silaha za nyuklia imetolewa ikiwa ni miezi michache imepita baada ya kutolewa ripoti iliyosema kuwa, Marekani na Russia ambazo ni wamiliki wakubwa wa silaha za nyuklia, zimesimamisha makubaliano muhimu ya silaha baina yao.
 
Mwezi Februari mwaka huu, serikali ya Marekani kwa kisingizio cha kuwa eti Russia imekiuka mkataba wa makombora kati ya nchi mbili, ilitangaza kwamba imesimamisha Mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati maarufu kwa kifupi kama INF kuanzia tarehe pili Februari na kuanza kutekeleza hatua za kujiondoa kwenye mkataba huo ambazo zitadumu kwa kipindi cha miezi sita. Kufuatia hatua hiyo, Rais Vladmir Putin wa Russia alisisitiza kuwa hatua hiyo haitakosa jibu na kwamba serikali ya Moscow nayo imesimamisha mkataba huo.

Serikali Yaanzisha mfumo wa kielektroniki ambao mwekezaji anaweza kuomba kuwekeza nchini akiwa popote duniani.

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ofisi yake imeanzisha mfumo wa kielektroniki ambao mwekezaji anaweza kuomba kuwekeza nchini akiwa popote duniani.

Kauli hiyo aliitoa jana bungeni wakati akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Jasmine Tiisekwa (CCM).

Dk. Tiisekwa alisema kwa kuwa dira ya maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025 ni kufikia uchumi wa kati na uchumi wa viwanda ni kigezo kimojawapo.

“Na kwa kuwa Serikali ya awamu ya tano imejielekeza kwenye uchumi wa viwanda na imejitahidi kutengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji ili waweze kuja kuwekeza, hata hivyo wawekezaji wengi wanakwamishwa na kusumbuliwa sana.

“Je, nini kauli ya Serikali kuhusu suala hili?” aliuliza Dk. Tiisekwa.

Akijibu, Waziri Mkuu alisema ofisi yake imeanzisha mfumo mpya wa kielektroniki ambao mwekezaji anaweza kuomba kuwekeza nchini akiwa popote duniani.

“Ofisi ya Waziri Mkuu tumeanzisha mfumo wa kielektroniki ambao sasa mwekezaji anaweza kuomba kutoka popote alipo.

“Tunatambua wawekezaji wako nje ya nchi, haimlazimishi yeye kuja moja kwa moja Tanzania kuanza kujaza makaratasi, anajaza huko huko Marekani kuomba nafasi ya kupata ardhi, kupata ithibati ya uwekezaji hapa nchini,” alisema Majaliwa.

Alisema Serikali imetengeneza haya yote kurahisisha mfumo wa uwekezaji kwa lengo la kupanua wigo wa uchumi hapa nchini kupitia viwanda.

“Lakini pia kufungua kupitia kilimo, kupitia madini lakini eneo maalumu mwekezaji anataka kuwekeza, sasa Tanzania imefungua fursa na kutengeneza mazingira rahisi ya uwekezaji,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa wito kwa wawekezaji kuja  kuwekeza Tanzania, ambako alidai fursa ipo na ardhi ipo.

“Na fursa hizi sasa tumezikaribisha katika mikoa na wilaya, tunayo ardhi kwa ajili ya kukaribisha wawekezaji ili kuendelea kuongeza mapato ya halmashauri yenyewe, mikoa yenyewe na taifa kwa ujumla,” alisema.

Wimbo Mpya: Lava Lava - Hatuachani

$
0
0
Wimbo Mpya: Lava Lava - Hatuachani

Video Mpya: Chege Ft. Vanessa - Manjegeka

$
0
0
Video Mpya:  Chege Ft. Vanessa - Manjegeka

Video: Nay wa Mitego ft. Mtafya & Nini - Nishaachaga

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya uitwao Nishaachaga...Itazame hapa.

Rais Magufuli Ateua Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Moses Mpogole Kusiluka kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).

Rais Magufuli Atoa Msamaha Kwa Wafungwa 3530

$
0
0
Katika kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Aprili 26, 2019, Rais Magufuli kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa  msamaha kwa wafungwa ambapo kati ya waliopewa msamaha ni pamoja na wafungwa walioingia gerezani kabla ya machi 15, 2019.

Rais Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,530  ambapo wafungwa 722 wataachiliwa huru siku ya leo April 26, 2019.

Taarifa iliyotolewa na Meja Jenerali Jacob G Kingu, imeeleza kwamba wafungwa 2808  watabaki gerezani kumalizia kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huo.

Wafungwa wengine waliobahatika msamaha huo ni pamoja na na wale wanaougua magonjwa kama Ukimwi, Kansa na Kifua kikuu ambapo watathibitishwa na Jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu Mkoa au Wilaya.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Tatizo la Kutokwa na usaha Wakati wa Kukojoa

$
0
0
Bila shaka wapo wengi ambao wana tatizo kama hili. Naomba tuwe pamoja kwenye makala hii ili ujifunze kuhusu tatizo la mtu kutokwa usaha wakati wa kukojoa.

Tatizo la Kuwepo kwa chembechembe za usaha au usaha kwenye mkojo hujulikana kama pyuria ambapo linaweza kuonekana kwa kutumia hadubini (microscope) au kama tatizo ni kubwa linaweza kuonekana kwa macho.

Visababishi vya tatizo la Kutokwa Usaha Wakati wa Kukojoa ni nini?

Visababishi vya tatizo hili ni kama vifuatavyo;
  1. Ugonjwa wa mfumo wa mkojo (UTI)-Maambukizi kwenye figo, kwenye mrija wa mkojo na kwenye kibofu cha mkojo (cystitis- amabayo huonekana sana)
  2. Magonjwa ya Zinaa-Kama ugonjwa wa kisonono au ‘’gono’’ kama wengi wanavyoita, ugonjwa wa Chlamydia na Trichomoniasis
  3. Sumu inayotokana na kemikali (Chemical poisoning) kama 4-Aminodiphenyl inayotumika kwenye maabara na kwa ajili ya tafiti
  4. Tatizo linajulikana kama Reiter’s syndrome
  5. Pyelonephritis-Maambukizi ya bakteria kwenye sehemu za figo zinazojulikana kama calyces, renal pelvis na tishu za figo
  6. Madhara ya pyelonephritis ambayo husabababisha ugonjwa unaojulikana kama renal abscess
  7. Maambukizi kwenye tezi dume-Prostatitis (Kwa wanaume)
  8. Upungufu wa kinga mwilini
  9. Mcharuko (Inflammation) kutokana kuwa na mawe kwenye kibofu cha mkojo au kwenye figo
  10. Mzio (Allergy) au kuota uvimbe sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo
Viashiria vya tatizo hili ni;
  1. Maumivu makali ya kuchoma (Painful burning sensation) wakati wa kukojoa
  2. Maumivu chini ya kitovu
  3. Homa
  4. Kutapika
Tatizo hii likidumu kwa muda mrefu husababisha kupungua uzito kwa mgonjwa

Vipimo vya uchunguzi
  1. Urinalysis – Kipimo cha mkojo
  2. Urine for culture and sensitivity - Kipimo cha kuangalia bakteria kwenye mkojo
  3. Complete blood count – Kipimo cha kuangalia wingi wa damu na chembechembe za damu (husaidia  kuonyesha kama kuna maambukizi kwenye mwili)
  4. Blood culture - Kuangalia kama kuna maambukizi kwenye damu
  5. Prostate –Specific Antigen (PSA) Test-Kipimo cha tezi dume
  6. Kipimo cha mionzi ya X-ray - Huonyesha kama tatizo ni kubwa sana
  7.  Kipimo cha ultrasound
  8. Kipimo cha CT scan au MRI - Husaidia kuonyesha kama tatizo hili lipo ndani ya tishu za figo  (Intra-renal abscess) au nje ya tishu za figo (Extra-renal abscess)
Vichagizi vya Tatizo la Kutokwa Usaha Wakati wa  Kukojoa (Predisposing Factors)

Vichagizi vya tatizo hili ni;
  1. Kutosafisha vizuri sehemu za siri baada ya kujisaidia haja ndogo
  2. Kujamiana na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wowote wa zinaa
  3. Ugonjwa wa kisukari
  4. Madhara yanayotokana na kutumia mpira wa mkojo - Kwa wale wote waliowekewa mpira huu wa mkojo (catheter)
  5. Saratani ya kwenye mfumo wa mkojo au sehemu za siri
  6. Matumizi ya dawa za jamii aina ya Non-steoridal anti-inflammatory drugs (NSAIDS) au madawa yanayopunguza kinga mwilini (Immuno-suppressant medications) kwa muda mrefu
  7.  Kuvimba kwa tezi dume
Matibabu
  1. Tiba hutegemea na chanzo cha tatizo hili
  2. Dawa za kutibu vimelea (antibiotics)
  3. Matibabu ya mawe kwenye kibofu cha mkojo au kwenye figo
  4. Kunywa maji kwa wingi mara kwa mara ili kusaidia kutoa chembechembe za usaha kupitia njia ya haja ndogo-Ikumbukwe ya kwamba maji sio tiba
Angalizo:-mgonjwa Atahitaji Kumuona Daktari Ili Apate Tiba Stahiki  Kulingana Na Chanzo Cha Tatizo La Kutoka  Usaha  Wakati Wa Kukojoa

Mahakama: Ni Marufuku Kuchora Vibonzo Vya Kumkejeli Rais wa Rwanda

$
0
0
Mahakama Kuu nchini Rwanda imetupilia mbali mashtaka yaliyokuwa yametolewa na baadhi ya wanasheria nchini kupinga sheria iliyoanzishwa mwaka jana kuwa ni kosa la jinai kuchora vibonzo vinavyomkejeli Rais wa nchi hiyo.

Wanasheria hao walifungua kesi kulipinga hilo huku wakisema hiyo ilikuwa ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo. 

Hata hivyo mahakama hiyo imeamua kuwa viongozi wengine waandamizi serikalini na viongozi wakuu wa kidini halitakuwa kosa la jinai kuwachora kwenye vibonzo.

Viwanja vinauzwa Bunju na Mapinga

$
0
0
Viwanja vinauzwa Bunju na Mapinga

Kwa Mapinga, vipo viwanja vya ukubwa wa sqm 400, 600, 800, 1000, 1200, 1600, 2000 na 2400 na bei ya sqm moja ni tshs 12,000

Viwanja hivi viko umbali wa km 2 tu kutoka main road (Dar to Bagamoyo). Huduma za umeme na maji zipo na luksa kulipa kwa awamu 2/3, ukilipa kwa awamu moja tu bei inapungua.

Kwa Bunju (dsm), vipo viwanja ukubwa wa sqm 600, sqm 1200 na sqm 1700 na bei ya kila sqm ni tshs 30,000 na viwanja hivi viko umbali wa km 1 kutoka main road.

Biashara hii haina dalali/udalali.
CALL 0758603077, WHATSAP 0757489709
Ukipata ujumbe huu, share na rafiki/ndugu/jamaa

Sugu: Rais Magufuli Nina Kuunga Mkono Kwa Asilimia 100

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi amesema yeye ni miongoni mwa Wabunge ambao wanamuunga mkono Rais Magufuli licha ya kutohama chama na amedai ataendelea kumuunga mkono hadi mwisho.

Mbunge Sugu ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ruanda, Nzovwe jijini Mbeya leo Aprili 26, 2019.

"Mimi ni katika watu tunaokuunga mkono bila kuhama chama, na nitaendelea kukuunga mkono mpaka mwisho, wanasema kuna watu wamepanga kufanya fujo, haiwezekani watu na akili zao wapange kumfanyia fujo Rais," amesema Mbunge Sugu.

Akizungumzia changamoto ya maji katika jiji la Mbeya, Mbunge huyo alisema Sh70 bilioni zinahitajika ili kumaliza tatizo la maji huku chanzo chake ikiwa ni Mto Kiwila.

Amesema kwa mujibu wa wataalamu njia hiyo itakuwa ni tiba ya shida ya maji katika jiji la Mbeya na hata mkoa jirani wa Songwe.

Rais Magufuli Atoa Maagizo TCRA Kuhusu Zoezi la Kusajili Upya Line za Simu

$
0
0
Rais Magufuli, ameitaka Mamlaka y Mawasiliano nchini, TCRA, kutowabughudhi watu ambao hawana vitambulisho vya taifa, katika zoezi ambalo limepanga kuanza tarehe 01, Mei mwaka huu.

Rais ametoa kauli hiyo leo wakati, akizungumza na wananchi wa Mbeya ambapo amesema kwamba zoezi hilo haliwezi kufanyika kama ilivyopangwa na TCRA kwa kuwa sio watu wote wanaomiliki simu wana Vitambulisho vya Taifa.

"TCRA wamesema watu wasajili simu kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa kwa 'logic' ya kawaida Watanzania waliopata vitambulisho ni milioni 14, ukisema mpaka vitambusho vya Taifa ndo wapate usajili ni kuwaeleza watanzania milioni 24 wasiwe  na simu. Hicho ni kitu ambacho hakiwezekani", amesema JPM.

Rais amezitaka Mamlaka zinazohusika kuendelea na usajili wa laini kwa watu wenye vitambulisho tu, huku NIDA wakiendelea kusajili Wananchi ili kuwapatia Vitambulisho vya Taifa.

"Ninawaambia TCRA na Wizara inayohusika jambo wanalolifanya ni zuri sana lakini waanze na wale milioni 14 walio na vitambulisho vya Taifa na zoezi la kusajili liende mpaka Desemba, ili liendane sawa na utoaji wa vitambulisho vya taifa", ameoongeza.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images