Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Data na MB za Bonus Hadi Mara Mbili Kutoka Vodacom

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom, Linda Liwa (katikati) akiongea na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo.

KAMPUNI ya Vodacom  imezindua promosheni ya Data Datani inayompatia mteja Bonus za MB (Internet) hadi mara mbili ya bando  kila anaponunua kifurushi cha Internet kwa bei ileile.

Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom, Linda Liwa.

Bonus hizo za MB zinamwezeha mteja wa Vodacom kuangalia video kupitia Youtube, kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii (WhatsApp, Facebook na Instagram).

Wateja wakijiunga na bando kujishindia simu za Smartphone.Liwa amesema wameanzisha promosheni ya ubunifu na kuwaelimisha wateja jinsi ya kutumia bando baada ya malalamiko mbalimbali kutoka kwa wateja kupoteza MB zao kutoka kwenye mtandao Supa wa Vodacom wa 4G na na kwamba hawana mpinzani kwenye promosheni hiyo ya Data Datani.

Katika hafla hiyo pia zimetolewa zawadi za simu aina ya Smartphone kwa wateja wa Vodacom waliokuwepo katika uzinduzi huo kwa kuwauliza maswali mbalimbali ya jinsi ya kujiunga na bando kutoka Vodacom.

Uzinduzi huo ulifanyika sambamba na burudani mbalimbali.

Kwa mujibu wa promosheni hiyo, fursa zilizopo ni pamoja na mtu kumnunulia rafiki yake vifurushi vya internet na kufurahia Bonus za Data Datani. Pia mteja anaweza kupata Bonus kwa kujiunga/kununua vifurushi vya internet kwa njia zifuatazo:
  1.     Piga *149*01# chagua Internet>bando za internet/masaa 24, siku 7 au siku 30
  2.     Piga *150*00# chagua nunua kifurushi/muda wa maongezi >Nunua vifurushi>internet/bando za internet
  3.     My Vodacom App
  4.     M-PESA APP
  5.     Tovuti ya Vodacom (www.vodacom.co.tz)
Kwa Vodacom: Kila kitu ni mwendo wa kudata datani na Vodacom kwa kupata Bonus za MB hadi mara mbili ambapo mteja anachotakiwa ni kupiga *149*01# na kuchagua Intaneti na anunue kifurushi akipendacho ili kujipatia bonus papo hapo.

Tahadhari Ya Kimbunga Yatolewa Mtwara...Wafanyakazi Na Wanafunzi Waagizwa Kusalia Majumbani.

$
0
0
Na Bakari Chijumba, Mtwara.
Kufuatia Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania(TMA),kutoa angalizo la uwezekano wa kutokea Kimbunga katika  pwani ya kusini mwa Tanzania kesho Alhamisi  25/04/2019, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ameagiza watumishi wote wasiende makazini kesho,pia wanafunzi ngazi zote wasiende mashuleni na vyuoni.

Bakyanwa amesema taarifa zinaonesha kuanzia asubuhi saa mbili hadi tatu zitaanza mvua za kawaida,ila baadae utafuata upepo mkali,radi na mvua kubwa zinazoweza sababisha Mafuriko na kimbunga na kwamba  licha ya kwamba ni utabiri lazima tahadhari ichukuliwe.

"Tumepata angalizo la kutokea Kimbunga..Kamati ya usalama wa mkoa tumekubaliana,kesho watu wote wanaoishi mabondeni watoke na wakae sehemu zenye miinuko,Pia watu wasiende makazini,mashuleni wala Vyuoni,kwa ajili ya kuangalia hali itakavyokuwa" amesema Byakanwa na kuongeza kwamba;

"Tumepata angalizo la kutokea Kimbunga..Kamati ya usalama wa mkoa tumekubaliana,kesho watu wote wanaoishi mabondeni watoke na wakae sehemu zenye miinuko,Pia watu wasiende makazini,mashuleni wala Vyuoni,kwa ajili ya kuangalia hali itakavyokuwa"

Kwa upande wake Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Mtwara Mikindani imewataka wananchi wanaoishi maeneo hatarishi kama Chuno,Miseti,Skoya,Reli,Kiyangu,kiyangu,Mtepwezi,Mikindani &maeneo yaliyopo pembezoni mwa Bahari kuondoka na kwenda kujihifadhi katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujihifadhi.

"Wananchi wametakiwa kuwa na Akiba ya Chakula cha kutosha siku ya Kesho Maeneo yaliyotengwa ili kujihifadhi ni shule ya msingi Majengo,Shule ya Msingi Tandika,Sekondari ya sabasaba,uwanja wa ndege,Naliendele Jeshini na Mitengo  na Sabodo Secondary" imesema taarifa hiyo kutoka ofisi ya Mkurugenzi.

NIDA, TCRA na Makampuni ya Simu nchini kuwezesha zoezi la uandikishaji wa watumiaji wa simu kwa kutumia Namba za Utambulisho wa Taifa

$
0
0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Makampuni ya Simu nchini, itawezesha zoezi la uandikishaji wa watumiaji wa simu nchini kwa kutumia Namba za Utambulisho wa Taifa au Kitambulisho cha Taifa.  

Zoezi la Uandikishaji wa laini za simu linatarajia kufanyika kuanzia tarehe 01-Mei-2019. Mazoezi ya majaribio ya zoezi hili yamefanyika katika baadhi ya Mikoa na Taasisi na kuonyesha mafanikio.

NIDA tayari imesajili asilimia 88 ya watu wote wanaostahili kusajiliwa kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa nchi nzima. 

Zoezi la Utambuzi na usajili ni endelevu, hivyo asilimia 12 ya lengo la usajili lililobaki linaendelea kutekelezwa katika wilaya zote nchini kwa kusajili watu ambao hawakusajiliwa kwenye zoezi la usajili wa umma (Mass Registration) na ambao wamekisha umri wa miaka 18, ambacho ni kigezo cha kisheria kinachoruhusu mwananchi kusajiliwa kwa ajili ya Utambulisho wa Taifa.  

Vile vile usajili wa umma unafanywa tena katika mikoa ambayo watu wengi hawakusajiliwa katika usajili wa awali. Mikoa hiyo ni pamoja na Dar es salaam, Tanga, Pwani na Kigoma.

NIDA tayari imetengeneza Namba za Utambulisho wa Taifa Milioni 12, sawa na asilimia na 59 ya usajili uliofanyika. Zoezi la uhakiki, kuchakata na kutengeneza Namba za Utambulisho wa Taifa linaendelea kutekelezwa kwa kasi usiku na mchana. 

Aidha tunatoa rai kwa wale wote ambao wamejulishwa kuwa vitambulisho vyao vipo tayari wafike Ofisi za NIDA au Ofisi za Serikali za Mitaa walipo jiandikishia kuvichukua. Vitambulisho vya Taifa vinaendelea kuzalishwa na kusambazwa kwa wananchi. Namba za Utambulisho wa Taifa zitatumika katika usajili wa Namba za simu na matumizi mengine. Hivyo wale ambao tayari wana Namba za Utambulisho wa Taifa wazitumie kujisajili wakati vitambulisho vinazalishwa.

Wananchi mnaweza kupata Namba ya Utambulisho wa Taifa na huduma zingine zitolewazo na NIDA kwa njia zifuatazo:-
a. Kupiga namba * 152 *00#; chagua Ajira na Utambuzi; Chagua NIDA
b. Kupakua nakala ya Kitambulisho cha Taifa kwa kutembelea tovuti: https://services.nida.go.tz/nidportal/NID_Copy.aspx au tovuti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.
c. Kupiga simu huduma wateja; 0673 333444, 0743 202020, 0743 201020,
d. 0759 102010, 0765 201020.
e. Kufika ofisi za NIDA ya Wilaya ilyopo karibu.

Ni Muhimu kwa Wananchi wote wenye sifa za kusajiliwa kwa ajili ya Utambulisho wa Taifa kufanya hivyo sasa pasipo kusubiri mpaka wanapokuwa na hitaji la haraka kwani uhakiki wa taarifa zako lazima ufanyike kabla ya utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Taifa na baadae kitambulisho cha Taifa.

“Utambulisho wa Taifa kwa Maendeleo na Ustawi wa Nchi Yetu”

Imetolewa na
MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA
23 APRILI, 2019.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 25

Waziri Ummy Azitaka Halmashauri Kote Nchini Kuhakikisha Zinatenga Bajeti Maalum Kwa Ajili Ya Kutekeleza Mikakati Ya Kupambana Na Malaria

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Ikiwa leo ni   Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo huadhimishwa April 25 ya kila mwaka  , Waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu  amesema kuwa ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha kuwa wanatenga bajeti  maalumu  kwa ajili ya kutekeleza mikakati mbalimbali ya kupamba na malaria.

Waziri Ummy ametoa rai hiyo   April 24 ,jijini  Dodoma alipotembelea  katika kituo cha afya cha Makole Mkoani  Dodoma   kwa ajili ya  kukabidhi vyandarua vyenye dawa viuatilifu katika kutekeleza   adhma ya serikali ya kuwakinga akina mama wajawazito pamoja watoto dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Aidha, waziri  ummy amesema kuwa kati magonjwa ambayo yanaongoza  kuua watanzania ni ugonjwa wa malaria lakini  habari njema ni kwamba toka serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  aingie madarakani wameweza kutekeleza mikakati mbalimbali ya kutokomeza  malaria nchini Tanzania.

Mbali na hilo amesema kuwa akina mama wajawazito wanatakiwa kuhudhuria kliniki mara tu wanapo gundua kuwa ni wajawazito   huku akibainisha  mikakati mbalimbali wanayo itekeleza kama serikali kupitia wizara ya afya kwaajili ya kutokomeza malaria .

Kwa upande wake Fransis Bujiku   ambaye pia Kaimu Mganga  Mkuu wa Mkoa  lakini pia anaratibu kitendo cha udhibiti wa Malaria mkoa wa Dodoma  , amesema kuwa kwa mwaka 2015 kulikuwa na kiwango cha maambukizi kwa asilimia moja  na kwa  kiwango hicho wameweza kukishusha mpaka asilimia 0.6 hivyo ni mafaniko makubwa.

Akizungumza kwa niaba  ya akina mama waliopokea msaada huo , mmoja wa  akina mama hao, Amina Alphonce ameishukuru wizara ya afya kwa kuwapatia vyandarua hivyo kwani vitawasaidia katika kujikinga na ugonjwa wa malaria pamoja na kutoa ushauri kwa  wakina  mama wenzake kuwa na tabia ya kuhudhuria  vituo vya afya.

Kauli mbiu ya  Maadhimisho ya Malaria mwaka huu 2019 ni  ‘’ Zero Malaria inaanza na Mimi’’.

Lukuvi Atatua Mgogoro Wa Wafugaji Wa Kimasai Na Wawekezaji Monduli

$
0
0
MONDULI, ARUSHA: Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemaliza mgogoro uliodumukwa muda mrefu baina ya wananchi wa vijiji vya Lengiloriti na Naalarami vilivyopo wilayani Monduli mkoani Arusha na wawekezaji wa mashamba yanayomilikiwa na TANFOAM na SLUIS kwa kuamua kumega sehemu za mashamba na kuwapatia wananchi wa vijiji hivyo.

Lukuvi alifikia umauzi huo baada ya kukutana na pande zote mbili  tarehe 23 Aprili 2019 wilayani humo na kujadiliana kwa kina kwa takriban saa tano kwa lengo la kupata suluhu ya mgogoro huo ambao umeleta sintofahamu kati ya wananchi wa vijiji hivyo na wawekezaji wa mashamba.

Katika makubaliano hayo iliamuliwa ekari kati ya 850 hadi 900 zimegwe kutoka kwa muwekezaji TANFOAM na kugawiwa kwa kijiji cha Lengiloriti  wilayani Monduli  kutoka shamba namba 44 lenye ukubwa wa  ekari 3098. Aidha, upande wa muwekezaji SLUIS jumla ya ekari 2000 za muwekezaji zimetolewa kwa kijiji cha Naaralami, NAFCO, Lokisari na Tukusi ambapo sasa muwekezaji atabaki na aekari 2217 badala ya 4,217 alizokuwa nazo awali.

Kwa mujibu wa Lukuvi, ardhi iliyomegwa na kurudishwa katika vijiji hivyo itakuwa chini ya mamlaka ya kijiji ambacho ndicho kitakuwa na jukumu la kuigawa upya kwa wananchi wa vijiji husika na baadaye kupangwa matumizi bora ya ardhi.

Akizungumzia kijiji cha Lengiloriti, Waziri wa Ardhi aliwataka wananchi wenye Maboma yaliyokuwa ndani ya eneo la shamba la muwekezaji TANFOAM kuhamia eneo jipya walilotengewa katika kipindi cha miezi mitatu ili kupisha muwekezaji kuendelea na shughuli za kilimo na kutotekelezwa kwa aina yoyote agizo hilo kutaifanya serikali kuchukua hatua.

Aidha, ameagiza kuanzia wiki hii timu ya upimaji ardhi mkoani Arusha iende ktika eneo hilo kwa ajili ya kuweka mipaka/alama za kudumu  ili kuepuka uvamizi mwingine unaoweza kutokea na kuagiza wawekezaji na wananchi wa vijiji vilivyopatiwa ekari hizo kuchangia fedha kwa ajili ya upimaji ambapo muwekezaji na wananchi walikubali kutoa milioni tano kwa ajili ya upimaji.

Kuhusu mgogoro wa muwekezaji SLUIS, Lukuvi alisema muwekezaji huyo amekubali  kutoa ekari 520 kwa kijiji cha Naaralami pamoja na ekari 300 kwa ajili ya kupitishia mifugo ya wananchi wa kijiji hicho huku ekari 513 zikitolewa kwa NAFCO, 366 kwa Lokisari na ekari 301 kwa kijiji cha Tukusi.

Lukuvi alisema serikali inawaeshimu sana wawekezaji wa sekta ya ardhi kwa kuwa wanalipa kodi inayosadia utoaji wa huduma za jamii huku wananchi nao wakipata ajira na kusisisitiza kuwa wawekezaji wanaomiliki mashamba kisheria serikali itawalinda na kuonya baadhi ya viongozi wa vijiji kujigawia maeneo bila ya kushirikisha wananchi wa vijiji husika.

‘’Nimekuja kusuluhisha mgogoro siyo kunyanganya wawekezaji mashamba, wawekezaji wamekubali kupunguza mashamba yao na hayo mashamba siyo mali ya wananchi wanaoishi katika maboma yaliyohamishwa bali ni mali ya kijiji ambacho kitakuwa na jukumu la kugawa maeneo hayo’’ alisema Lukuvi

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa, baada ya makubaliano ya pande zote mbili anategemea kila upande utaheshimu maamuzi yaliyotolewa na mtu yoyote atakayekiuka basi serikali ya mkoa itachukua hatua kali dhidi yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanfoam Riaz Lemtula amepongeza jitihada iliyofanywa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi mpaka kufikia muafaka wa suala hilo na kuahidi kutekeleza makubaliano waliyoafikiana kwa lengo la kuleta maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Lengiroliti Baraka Lemai alimshukuru Waziri wa Ardhi kwa niaba ya Kijiji chake kwa kazi anayoifanya ya kutatua migogoro ya ardhi na kuahidi kushirikiana na wawekezaji waiokubali kumega maeneo yao kwa ajili ya kijiji.

Wawekezaji wanaomili mashamba katika vijiji hivyo wamekuwa wakiendesha mashamba yao katika shughuli za kilimo ambapo hulima mazoa ya Maharage, Mtama, Ngwara na mahindi na kusafirisha mazo hao katika nchi za Sweden, Canada na Uholanzi.

Serikali Imesema Halmashauri Ambayo Haina Uwezo Kujiendesha Kimapato Ikiwa Ni Pamoja Na Uwezo Wa Kulipa Posho Za Madiwani

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imesema kuwa halmashauri ambayo haina uwezo wa kujiendesha  kimapato ikiwa ni pamoja na uwezo wa kulipa posho za Madiwani haina sifa ya kuwa Halmashauri kwa mujibu wa     Sheria  na inapaswa kufutwa.
 
Hayo yamesemwa jana April 24,2019  bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais na Serikali Mitaa ,TAMISEMI,Mwita Waitara wakati akijibu swali la  Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe,Flatei Grigory Massay aliyehoji kwa baadhi ya halmashauri kushindwa kulipa posho za Madiwani ,je,serikali ina mpango gani wa kubadilisha mfumo wa kuwalipa posho Madiwani kupitia hazina kama watumishi wengine huku pia akihoji mpango  wa serikali kuanza kuwalipa posho Wenyeviti wa vijiji na mitaa kutokana na kazi kubwa wanayofanya.
 
Katika majibu yake Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara amesema halmashauri ambayo haina uwezo wa kujiendesha kimapato kwa mujibu wa Sheria inapaswa kufutwa na ametoa maelekezo kwa wakurugenzi kote nchini kuhakikisha wanalipa posho kwa madiwani huku akisema  kuwa kila asilimia 20 ya Mapato ya ndani ya halmashauri inatakiwa irejeshwe vijijini ama mitaani hali itakayowezesha kulipwa  wenyeviti wa mitaa na vijiji.

Hata hivyo Waitara amesema serikali inatambua kazi kubwa zinazofanywa na Madiwani ambapo mwaka 2012/2013  posho za madiwani zilipandishwa kutoka  Tsh.laki moja na nusu[1,50,000]   kwa mwezi hadi  Tsh.laki mbili na nusu [2,50,000]  kwa mwezi, kwa waraka wa mwaka 2012  sawa na ongezeko la asilimia 108.3%.
 
Mwaka 2014/2015 serikali ilipandisha posho za madiwani kupitia waraka wa mwaka 2014  kutoka  Tsh.laki mbili na nusu[2,50,000] hadi Tsh. laki tatu na nusu [3,50,000] kwa mwezi  sawa na ongezeko la asilimia arobaini[40%].
 
Vilevile Serikali inalipa posho ya madaraka kwa wenyeviti wa kamati  Tsh.elfu themanini[80,000] kwa mwezi  na posho ya kikao Tsh.elfu arobaini[40,000] kwa mujibu wa waraka wa mwaka 2007  na kigezo kinachotumika kupandisha posho za madiwani ni uwezo wa halmashauri kukusanya mapato.

Tahadhari Kutoka Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji Nchini Kuhusu Kimbunga Kenneth

$
0
0
 Kutokana na utabiri uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuhusu kutokea kwa Kimbunga kikali (KENNETH) na mvua kubwa leo tarehe 25 Aprili 2019 kitakachoathiri maeneo ya Pwani ya Kusini mwa nchi na kusababisha madhara mbalimbali. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatoa rai kwa Wananchi wote waishio katika maeneo hatarishi, maeneo yaliyopo pembezoni mwa bahari na kandokando ya Mito, kuchukua tahadhari katika kipindi hiki kwa kuyahama maeneo hayo haraka.

Wananchi wanatahadharishwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki na kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania na kusikiliza vyombo vya habari pamoja na kuzingatia tahadhari zinazotolewa, ushauri na miongozo ya kitaalam ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Tuchukue tahadhari kwa kuepuka kukaa au kuegesha vyombo vya Usafiri na Usafirishaji chini ya miti mikubwa, maana matawi au mti vyaweza kuangukia chombo na kusababisha uharibifu mkubwa wa Mali hata kudhuru Maisha.

Kutokana na Kimbunga hiki kikali kinachoambatana na mvua kubwa kuna uwezekano wa mawe makubwa au udongo kuporomoka kutoka milimani au miti kuanguka na kuziba barabara, hivyo madereva wanapaswa kuwa makini kwa kuendesha vyombo kwa mwendo unaokubalika ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limejipanga na liko imara kuhakikisha linatoa huduma bora, sahihi na kwa wakati.

Imetolewa na;
Billy Mwakatage
Kamishna wa Operesheni
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Video Mpya ya Lady Jaydee - I Don't Care

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Lady Jaydee anakukaribisha kutazama video ya  wimbo wake mpya uitwao I Don't Care. Itazame hapa.

Vladimir Putin na Kim Jong-un Wakutana na kufanya mazungumzo kwa mara ya kwanza

$
0
0
Jumatano Kim Jong-un Kiongozi wa Korea Kaskazini aliwasili nchini Russia kwa lengo la kukutana na kufanya mazungumzo kwa mara ya kwanza na Rais Vladmir Putin wa nchi hiyo.

Baada ya kuwasili mji wa Vladivostok wa mashariki mwa Russia Jong-un amekutana na kufanya mazungumzo ya kufana na Rais Putin. 

Kabla ya kuanza safari hiyo Kim Jong-un alisema kuwa, alitaraji kwamba katika mazungumzo na rais huyo wa Russia wangeweza kujadili masuala muhimu kuhusiana na mgogoro wa Rasi ya Korea na kustawishwa mahusiano kati ya Moscow na Pyongyang. 

Ukweli ni kwamba safari ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini nchini Russia kwa ajili ya mazungumzo ya kistratijia na rais wa nchi hiyo, na ambayo imekuja baada ya kuvunjika kwa duru mbili za mazungumzo kati yake na Rais Donald Trump wa Marekani nchini Singapore na Vietnam na katika muda ulio chini ya mwaka mmoja uliopita, imetoa ujumbe kwa White House kwamba sasa Pyongyang inaelekea upande wa kustawisha uhusiano wake na Russia. 

Hii ni katika hali ambayo kwa kuingia katika mazungumzo na Korea Kaskazini, Trump alitaraji kwamba angeweza kuishawishi Pyongyang ifuate siasa na sera za Washington, jambo ambalo halikufanikiwa. 

Kutofikiwa mwafaka kwenye duru mbili za mazungumzo kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong-un, kumeifanya Korea Kaskazini ifikie natija hii kwamba, Marekani ni nchi isiyoaminika na isiyo na itibari, ambayo licha ya Pyongyang kutekeleza makubaliano ya kusimamisha majaribio yake ya makombora na silaha za nyuklia, lakini haikuweza kutekeleza hata sehemu ndogo tu ya mapatano yao.

Rais wa China Akerwa na siasa za kimabavu za Marekani dhidi ya mataifa mengine

$
0
0
Rais Xi Jinping wa China amesema kuwa, anapinga siasa za kibabe, utumiaji mabavu za baadhi ya madola makubwa dhidi ya mataifa mengine.

Rais Xi Jinping amesema hayo alipokutana na makamanda wa kigeni wa majeshi ya majini walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 70 ya kuasisiwa jeshi la majini la China katika bandari wa Qingdao ya mashariki mwa nchi hiyo na kuongeza kuwa, mataifa ya dunia hayapaswi kutumia wenzo wa mabavu kwa ajili ya kuzitisha nchi nyingine.

 Rais wa China amesisitiza kuwa, mataifa yote yanapaswa kufungamana na suala la kuboresha mahusiano wakati wa migogoro na kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na kieneo kama ambavyo yanapaswa pia kudhamini suala la kutatua hitilafu na mivutano inayohusiana na bahari. 

Rais Xi Jinping amesema bayana kwamba, usalama na utulivu wa bahari una uhusiano na usalama na maslahi ya mataifa ya dunia na ili kudhamini usalama wa bahari kunahitajika kuweko ulinzi wa pamoja. 

Matamshi ya Rais wa China ya kukosoa siasa za kibabe na utumiaji mabavu za Marekani katika kukabiliana na nchi nyingine aliyoyatoa katika maadhimisho ya mwaka wa 70 wa kuasisiwa jeshi la majini la China ni ishara ya wazi ya kupinga siasa za Marekani za kuingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine ambazo zinakwenda sambamba na ubabe wake huko katika eneo la majini la kusini mwa China.
 
Siasa za kibabe na utumiaji mabavu za Marekani katika uga wa kimataifa hususan tangu aingie madarakani Rais Donald Trump zinaonekana kuchukua kasi na wigo mpana zaidi. 

Hatua ya upande mmoja ya Marekani ya kujiondoa katika makublaiano ya nyuklia ya JCPOA ambayo yaliungwa mkono na azimio 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na madola makubwa duniani, ni sehemu ya utendaji mbovu wa Washington wa kupenda makuu ambao ni mfano wa wazi wa siasa za kimabavu za White House katika uga wa kimataifa ambazo zimekabiliwa na ukosoaji mkubwa wa jamii ya kimataifa.

Kuingilia masuala ya ndani ya Venezuela na kufanya njama za kutaka kuipundua serikali halali ya Rais Nicolas Maduro na hata kutoa vitisho vya kutaka kuishambulia kijershi nchi hiyo ya Amerika ya Latini na kisha kuweka madarakani serikali kibaraka sambamba na kutambua rasmi umiliki wa utawala haramu wa Israel kwa miinuko ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo vamizi, hatua ambayo inakiuka wazi maazimio ya Umoja wa Mataifa, ni mifano mingine ya wazi ya kushadidi siasa za kibabe na utumiaji mabavu za Marekani katika uga wa kimataifa. 

Hatua hizo za Marekani zimeibua wasiwasi na malalamiko ya jamii ya kimataifa dhidi ya siasa za kuchupa mipaka za Rais Donald Trump.
 
Kujiondoa Marekani katika mikataba ya kimataifa kama vile mkataba wa Biashara Huru ya Amerika ya Kaskazini (NAFTA), mkataba wa biashara katika ukanda wa Pasifiki na mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris, Ufaransa ni mifano mingine ya wazi inayodhihirisha siasa za kimabavu za Washington zenye lengo la kuyatwisha mataifa mengine matakwa yake.

Hata hivyo, mwendelezo  wa vikwazo vya kidhalimu dhidi ya mataifa mengine hususan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umekuwa na madhara makubwa zaidi kwa wananchi wa nchi zilizowekewa vikwazo hivyo. Huu nao ni upande mwingine wa utumiaji mabavu kwa ajili ya kukabiliana na nchi na tawala ambazo haziko tayari kufuata siasa za Marekani.

Credit:Pars

Zimbabwe yatoa tahadhari ya athari za kimbunga Kenneth...Kwa sasa Kimeshatua visiwani Comoro

$
0
0
Taarifa ya wizara ya habari Zimbabawe imeeleza kwamba Kimbunga Kenneth kinachotarajiwa kutua Msumbiji Malawi na baadhi ya maeneo ya Zimbabawe, kimeshuhudiwa visiwani Comoros.

Imeeleza kwamba kutokana na uzoefu wa mkasa na athari ya kimbunga Idai mwezi uliopita, watu wote wanaoishi katika maeneo yalio katika hatari ya kukumbwa na mafuriko kama Mbire Muzarabani na maeneo ya chini ya jimbo la Masvingo na kwingineko, wanapaswa kujihadhari pakubwa.

Kimbunga hicho kimefika daraja la nne kikiambatana na upepo wa kasi ya 130 mph karibu na eneo la kati na kinaarifiwa kuelekea Msumbiji katika jimbo la Cabo Delgado.

Mtendaji Mkuu Wa Bodi Ya Filamu Atenguliwa

$
0
0
KATIBU MKUU wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan Mlawi ameagizwa ampangie kazi nyingine Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, Bi. Joyce Fisoo na ateue mtu mwingine kushika nafasi hiyo.

Agizo hilo lilitolewa jana jioni (Jumatano, Aprili 24, 2019) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akihitimisha kikao chake na wasanii zaidi ya 100 kutoka Shirikisho la Filamu Tanzania kilichofanyika Ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma.

Shirikisho la Filamu Tanzania linajumuisha vyama 11, ambapo 10 vimesajiliwa na kimoja hakijakamilisha usajili. Vyama hivyo ni vya waigizaji, waongozaji, watayarishaji, wahariri, wachekeshaji na wapigapicha. Wengine ni waandishi wa miswada (script writers), watafutaji mandhari, wasambazaji wa filamu, walimu na chama cha wanawake wa tasnia ya filamu ambacho bado kiko kwenye mchakato wa usajili.

Kikao hicho ambacho kilidumu kwa zaidi ya saa saba, kilihudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bodi ya Filamu Tanzania pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakiongozwa na Naibu Waziri wa Habari, Bibi Juliana Shonza.

“Katibu Mkuu mtafutie eneo jingine la kufanya kazi. Hana tuhuma zaidi ya mahusiano mabaya na wadau wake, ana historia nzuri, lakini tatizo ni mahusiano. Mpeleke idara nyingine na hapa mlete mtu mwingine,” alisema Waziri Mkuu.

“Mama Fisoo wewe uko clean, sina tatizo na utendaji wako lakini ukikaa hapa hutaweza kwenda mbele na wala hawa wote hawatakuja kufanya kazi na wewe. Tunataka hii tasnia iende mbele, tunataka maendeleo kwenye tasnia ya filamu,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Alimuagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania, Profesa Frowin Nyoni ajipange upya na Bodi yake na kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa wasanii kama ambavyo imeainishwa kwenye sheria ya kuanzishwa kwa Bodi hiyo.

“Bodi yako inao wajibu wa kutoa elimu kwa makundi tofauti ya wasanii. Sheria yenu imeainisha kuwa mnapaswa kutoa elimu. Wapeni refresher courses ili waongeze ujuzi na wakienda huko wanatoa uzoefu walionao kwa wanachuo, nao pia wanakuwa wamejifunza,” alisema.

“Nimeangalia makundi ya wasanii na kukuta kuna wachoraji na wachongaji; wasanii wa filamu, wasanii wa maigizo, wabunifu wa mitindo na wote hawa wana Bodi zao. Timizeni majukumu yenu. Bodi pia mna kazi ya kupromote brand kwa kutumia wasanii wetu,” alisema.

Kuhusu utitiri wa tozo ambao umelalamikiwa na wasanii hao, Waziri Mkuu alisema kuna haja ya kulinda soko la ndani la kazi za wasanii wa Kitanzania tofauti na hali ilivyo sasa ambapo wazawa wanatumia gharama kubwa kutengeneza kazi zao lakini wanapata shida kuziuza ilhali wageni wanapata faida zaidi kwa kazi kama hizo.

“Wasanii wamesema kuna tozo 11 lakini Mtendaji Mkuu kataja tozo chache tu. Hebu Waziri aitishe kikao baina yenu, Waziri wa Fedha, Waziri wa Viwanda na Biashara, Kamishna wa TRA, Bodi ya Filamu na TCRA, mkutane mara moja na kuziangalia upya hizi tozo ili zipunguzwe kama tulivyofanya kwingine. Lazima tulinde soko la ndani,” alisisitiza.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaonya wasanii juu ya fukuto linaloendelea ndani kwa ndani baina ya vyama tofauti, baina ya vyama na shirikisho na baina ya shirikisho na taasisi nyingine za kiutendaji.

Kuhusu maudhui ya filamu zinazotengenezwa na wasanii wa Tanzania, Waziri Mkuu alisema inashangaza kuona masuala ya mapenzi yanaongoza kwenye filamu za Kitanzania kwa kushika nafasi ya kwanza ikiwa ni sawa na asilimia 68, ikifuatiwa na vichekesho ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa sawa na asilimia 12.

“Je, wote ni lazima muigize masuala la mapenzi kwenye filamu zenu au huwa mnaambiana mtoe maudhui yanayohusu mapenzi. Je, ni kweli kwamba Watanzania wengi wanapenda kuangalia mambo ya mapenzi?”

“Ni lazima muangalie maudhui yenu na mpanue wigo. Kwa kuwa mna shirikisho, ni vema mkagawana maeneo ya kuigiza ili kupanua soko na mkiingiza filamu zenu sokoni, zote zipate mashabiki.”

Alisema nafasi ya tatu kwenye maudhui imechukuliwa na filamu za masuala ya utamaduni na mambo ya uchawi ambayo ni sawa na asilimia 10 huku nafasi ya nne ikichukuliwana na filamu zinazohusu mapigano ambazo ni sawa na asilimia saba. “Hizi ni chache kwa sababu zinahitaji mtaji mkubwa wakati wa kuzitengeneza na pia ni risky,” alisema.

Wakitoa maoni yao ni kwa nini tasnia ya filamu imedidimia, wasanii hao ambao waliwakilisha wenzao kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Katavi na Rukwa, walidai kwamba Bodi ya Filamu imeua tasnia hiyo kwa hiyo hawana imani na Bodi na hawako tayari kufanya nayo kazi.

Waliomba pia kuwe na taratibu za kuvutia wawekezaji kwenye tasnia hiyo, uwekwe mkakati wa haraka wa kuinua soko la filamu kupitia lugha ya Kiswahili ambayo walisema ni bidhaa adimu. Pia waliomba sera ya filamu nchini ikamilishwe haraka ili iweze kulinda maslahi ya wasanii wa filamu.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Spika Ndugai Aruhusu hotuba za Kambi rasmi za Upinzani Bungeni Zisomwe Kama Zilivyo

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameruhusu kuanza kusomwa kwa hotuba za Kambi rasmi za Upinzani Bungeni  bila kuhaririwa kufuatia kambi hizo kugoma  kusoma hotuba zao mara mbili mfululizo  kwa kile kilichoelezwa waandaji kuwa wamekuwa wakitumia maneno ambayo yanaonekana kuwa na ukakasi.
 
Maamuzi hayo ya Spika yamekuja ikiwa ni siku chache baada ya wasemaji wa Kambi hizo  kugoma kusoma hotuba zao mara mbili mfululilo katika Wizara za Habari pamoja na Mambo ya Ndani kupitia Wabunge, Joseph Mbilinyi pamoja na Mchungaji Petter Msigwa.

Akizungumza wakati wa muendelezo wa vikao vya Bunge jijini Dodoma, Spika Ndugai amesema kuwa, “naomba nizungumzie jambo moja ambalo lilijitokeza jana na siku za nyuma, hotuba za wenzetu wa upinzani kuna shida kidogo katika uandishi na wakati mwingine zinaleta matatizo makubwa, shida  wanaandika nje na hawazisomi wao wanafika na kusaini tu”.

April 18, 2019 Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson aliagiza hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, iliyokuwa ikisomwa na Mbuge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, kutohifadhiwa kwenye kumbukumbu za Bunge baada ya Mbunge huyo kugoma kuisoma.

Spika Ndugai Kasema Zitto Kabwe Ni Muongo

$
0
0
Spika wa Bunge Job Ndugai,amesema Mbunge wa Kigoma Mjini,Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) anawadanganya wananchi.

Ndugai alisema uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), unaofanywa na Zitto unalenga kuwaaminisha wananchi kwamba kila kilichomo kwenye ripoti hiyo ni cha kweli.

Alisema kwa upande wake humuungi mkono kwa kuwa ukweli wa ripoti hiyo hudhihirishwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni kamati ya PAC na LAAC.

Spika Ndugai aliyasema hayo bungeni leo mchana muda mfupi kabla hajaahirisha Bunge hadi jioni.

Pamoja na hayo Spika alisema Zitto anatumia muda wake mwingi kuichambua ripoti hiyo kwa kuwa anataka awe Mwenyekiti wa Kamati ya PAC kinyemela.

“Kama nilivyosema wakati fulani zile ni hoja, lakini watu wanawaaminisha Watanzania kuwa kila kichoandikwa na CAG mle ni ukweli asilimia mia moja. Yapo mambo mle si kweli hata kidogo tena mengi tu.

“Mengine utakuta kiambatanisho tu hakipo na mifano ipo mingi, yaani kitabu huchambuliwa na wakati mwingine zinabaki hoja chache ndio tunawapa Serikali au polisi kama zinahusu huko. Anachokitaka Zitto ni kuendelea kuwa mwenyekiti wa PAC kinyemelela.” Amesema

Taarifa ya mwenendo wa Kimbunga "Kenneth" Mchana Huu

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imetoa taarifa mpya juu ya mwenendo wa kimbunga Kenneth na kusema kuwa kinatarajiwa kutua kesho Ijumaa alfajiri au asubuhi.

Katika Taarifa ya video iliyopakiwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt Agness Kijazi amesema kufikia saa tia mchana wa leo kimbunga kitakuwa umbali wa kilomita 177 kutoka pwani ya Mtwara kikiwa na kasi ya kilometa 140 kwa saa.

Kutokana na kasi hiyo kimbunga kinatarajiwa kutua nchini Msumbiji kuanzia Alfajiri ya Ijumaa kikiwa na kasi kilomita 100 kwa saa.

Hata hivyo, kitakapotua kimbunga hicho ni karibu na mpaka wa Tanzania kwa kilomita 230, na athari zake zinatarajiwa kukumba maeneo yaliyo ndani ya kilomita 600.

"Nchini mwetu, maeneo ya mpaka Lindi na Ruvuma yataathirika sana," amesema Kijazi na kuongeza, "wakazi hususani wa Mtwara kwa sasa wanaweza wakaona tu kuna mvua zinanyesha lakini waendelee kuchukua tahadhari. Kadri muda unavyosidi kusonga ndiyo kimbunga kinazidi kukaribia nchi kavu."

==>>Msikilize hapo chini

Waziri Mkuu Akutana Na Mabalozi Wa Kenya, Kuwait ....Asisitiza Uwekezaji Kwenye Ujenzi Wa Viwanda

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na mabalozi wa Kenya na Kuwait na kuwasisitizia kwamba Tanzania inakaribisha wawekezaji kutoka kwenye nchi zao na hasa eneo la ujenzi wa viwanda.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 25, 2019) alipokutana kwa nyakati tofauti na Balozi wa Kenya nchini, Bw. Dan Kazungu na Balozi wa Kuwait nchini, Bw. Mubarak Alsehaijan ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda, tutafurahi tukipata wawekezaji kutoka Kenya ili waje wawekeze kwenye viwanda kwani tunajua Kenya ilianza mapema kujihusisha na ujenzi wa viwanda wakati sisi tukiwa bado na mfumo wa ujamaa,” amesema.

Waziri Mkuu alimweleza Balozi Kazungu kuwa anatambua kwamba miongoni mwa nchi za Afrika, Kenya inaongoza kwa uwekezaji hapa nchini lakini kwa fursa ambazo Tanzania inazo, bado wanayo nafasi ya kuja kuwekeza.

“Kwa kuzingatia kuwa Mheshimiwa Rais ameleta Waziri, Katibu Mkuu na TIC kwenye ofisi yangu, hii maana yake ninapaswa nisimamie suala la uwekezaji kwa karibu zaidi. Tumetengeneza blueprint, tumeweka taasisi 11 pale TIC za kurahisisha usajili na hivi sasa mwekezaji siyo lazima aje Tanzania, anaweza kujisajili mtandaoni hukohuko aliko,” amesema.

Pia alisisitiiza suala la kulinda amani katika nchi hizo mbili na hasa ulinzi wa mipakani. “Wenzetu mmepata mitisikiko ya ugaidi hivi karibuni, lakini ulinzi wa uhakika wa pamoja ni jambo linalojadilika na linalowezekana. Sisi tuko tayari kuwaunga mkono katika vita dhidi ya ugaidi, uharamia, na usafirishaji wa dawa za kulevya,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Balozi Kazungu amemshukuru Waziri Mkuu kwa ushirikiano ambao Serikali ya Kenya imekuwa ikiupata kutoka Tanzania na kuahidi kudumisha udugu ambao umekuwepo kwa miaka mingi.

“Sisi ni ndugu, tena ni majirani na mtu huwezi kuchagua jirani yako awe nani. Tunahitaji tuwe karibukaribu na kama ni biashara, basi watu wetu wawe wanafanya biashara kama majirani,” alisema Balozi Kazungu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemshukuru Balozi wa Kuwait kwa misaada ambayo nchi hiyo imekuwa ikiipatia Tanzania kupitia taasisi zake za kijamii.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu amesema Serikali ya nchi hiyo kupitia Kuwait Fund, imesaidia ujenzi wa barabara ya Chaya-Nyahua (Tabora), mradi wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe na ukarabati wa hospitali ya Mnazi Mmoja huko Zanzibar.

Amesisitiza kuwa bado Tanzania na Kuwait zinahitaji kuimarisha mahusiano yao katika maeneo mengine ya kiuchumi.

Naye Balozi Alsehaijan wa Kuwait amemshukuru Waziri Mkuu na kuahidi kuwa nchi yake iko tayari kuendelea kutoa misaada na huduma za kijamii.

Alisema kupitia taasisi za kujitolea, kuna mashirika manne (charity groups) ambayo yamejenga vituo vya watoto yatima Singida na Mwanza lakini kwa Mwanza, pia wameanza kuwahudumia na watu wenye ulemavu. “Pia wanajenga hospitali huko Zanzibar,” alisema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Wakuu wa Mikoa na Wilaya Watakiwa Kutoa Elimu ya Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo

$
0
0
Na Lilian Lundo  – MAELEZO, Dodoma.        
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa Mikoa na Wilaya kutoa elimu ya Vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo nchini.

Agizo hilo limetolewa leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Mhe. Pascal Haonga kuhusu watu waliolengwa kulipia vitambulisho hivyo kutokana na wajasiriamali hao kuwa na viwango tofauti tofauti vya mitaji.

“Serikali imeweka utaratibu mzuri wa kuwafanya wajasiriamali wadogo kuweza kuchangia Pato la Taifa, Mhe. Rais alibuni njia nzuri ambayo inawatambulisha wajasiriamali. Hata hivyo wajasiriamali hao tumewaweka kwa madaraja yao wako  wadogo, wakati na wakubwa. Mhe Rais na Serikali iliwalenga Wajasiriamali wadogo ambao kipato chao hakizidi shilingi milioni Nne kwa mwaka,” amesema Waziri Mkuu.

Amesema kuwa lengo ni wajasiriamali hao kuchangia pato la Taifa na pia kuwaondolea usumbufu katika maeneo wanakofanyia biashara zao kwa kutozwa ushuru wa shilingi 200 au 500 kila siku ambayo  imekuwa ikiwapunguzia mapato wanayopata kwa mwaka.

Ameendelea kusema, vitambulisho vingi hutolewa kwa Wakuu wa Wilaya, na anatambua kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo hutoa vitambulisho kwa kuwalazimisha watu badala ya kuwaelimisha namna ya kupata vitambulisho hivyo. Vile vile, yapo maeneo yanatoa vitambulisho kwa wajasiriamali wakubwa ambao pato lao ni zaidi ya milioni 4 kwa mwaka ambao wanatakiwa kuchangia TRA moja kwa moja.

“Maelekezo tunayoyatoa tena kwa Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya watumie  muda wao kuelimisha nani anapaswa kuwa na kitambulisho badala ya kutumia nguvu au kwenda kulazimisha au kuwapa wajasiriamali wakubwa wenye mapato zaidi ya milioni  4 na kuondoa maana ya uwepo wa vitambulisho,” amesema Waziri Mkuu.

Ameeleza kuwa, Mhe. Rais aliwalenga wafanyabiashara kama wauza maandazi, watembeza mahindi vituo vya mabasi  ili na wao waone uchangiaji wa uchumi na pato la nchi ni sehemu yao lakini waendelee kufanya biashara zao bila kusumbuliwa katika halmashauri zao.

Wakati huo huo  ameeleza kuwa Serikali ina mkakati wa kupunguza maambukizi ya ukimwi kupitia kampeni mbalimbali za kupambana na maambuki ya UKIMWI zinazoendeshwa na TACAIDS, Taasisi inayosimamiwa na  Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wizara ya Afya.

Amesema lengo la Serikali ni kila Mtanzania awe amepima na kujua afya yake ifikapo mwaka 2020. Vile vile wale waliopima na kugundulika na UKIMWI wawe ameanza kutumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI ifikapo 2020.

Serikali imekuwa ikitoa huduma za Upimaji wa UKIMWI katika kila eneo ambalo wanakutana zaidi ya wananchi 100 ili kutoa fursa ya Watanzania kupima na kujua Afya zao.

Serikali kupandisha vyeo watumishi wa Umma Mei mosi

$
0
0
Leo April 25, 2019 Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya utumishi na utawala bora George Mkuchika imesema mara baada ya kukamilika kwa upandishaji vyeo watumishi wa umma wapatao 113,520,imewaelekeza waajiri kuendelea na upandishaji vyeo kwa watumishi 193,166 waliokasimiwa katika ikama na Bajeti ya mishahara kwa mwaka 2017/18 kuanzia tarehe 01 Mei 2019.
 
Amesema upandishwaji vyeo kwa watumishi waliokasimiwa katika Ikama na bajeti ya mishahara ya mwaka 2015/16 uliahirishwa Mei 2016 kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi hewa.

Ameelekeza kipaumbele cha kwanza kitolewe kwa utendaji mzuri ambao wanatarajia kustaafu hivi karibuni ili waweze kushughulikiwa mapema iwezekanavyo kabla ya kustaafu
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images