Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 21


Sri Lanka: Watu 156 wauawa katika milipuko ya Bomu Wakati wa Sala ya Pasaka

$
0
0
Takribani watu 156 wanaripotiwa kufariki dunia na mamia kujeruhiwa kufuatia milipuko iliyotokea katika makanisa na hoteli nchini Sri Lanka.

Milipuko sita imeripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali nchini humo wakati raia wa nchi hiyo wakisherehekea sikukuu ya Pasaka.

Katika milipuko hiyo sita iliyotokea, milipuko mitatu imetokea katika makanisa, huku mingine mitatu ikitokea katika hoteli tatu tofauti.

Makanisa ambamo milipuko imetokea ni Kochchikade, Negombo na Batticaloa huku hoteli zilizokumbwa na milipuko zikiwa ni, The Shangri La, Cinnamon Grand na Kingsbury.

Picha mbalimbali katika mitandao ya kijamii zinaonesha hali ilivyo katika baadhi ya maeneo ambamo milipuko hiyo imetokea. Majengo yanaonekana yameharibika, pamoja na damu za watu kutapaa chini, huku vyombo vya huduma ya kwanza na Polisi wakitoa misaada.

Rais Maithripala Sirisena amewataka wananchi kuwa watulivu wakati wa kipindi hiki kigumu, na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi ili kufanikisha uchunguzi.

Viongozi wengine nchini humo wamelaani mauaji hayo ambayo yanayoonekana kuwa yalikuwa yamepangwa, na kugharimu uhai wa watu wasio na hatia.

Kwa muda kumekuwapo na vitisho vya kundi la kigaidi la ISIS nchini humo. Lakini hadi sasa hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulio hilo.

VIDEO: Kassim Mganga – Solemba

$
0
0
VIDEO: Kassim Mganga – Solemba

Wimbo Mpya: Kassim Mganga Ft. Mbosso - SALIMA

$
0
0
Wimbo Mpya: Kassim Mganga Ft. Mbosso - SALIMA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni Amvaa Katibu wa Tume ya Dawa za Kulevya Zanzibar

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amemtaja Katibu wa Tume ya Dawa za Kulevya Zanzibar, Heriyangu Mgeni kuwa ni mmoja wa wanaokwamisha juhudi za serikali katika kupambana na dawa hizo nchini.

Akizungumza na wanahabari, April 20 viziwani Zanzibar, Naibu Waziri Masauni amesema kuwa atatoa mapendekezo kwa mamlaka inayohusika na mapambano ya dawa hizo kumwondoa katika nafasi yake kutokana na uzembe anaoufanya.

"Mimi nikiwa na dhamana, mara kadhaa nimekuwa nikimwita Katibu nikishauriana naye kwa kuwa suala la dawa za kulevya linaniumiza roho, ni mpaka leo Kisiwa cha Zanzibar chenye watu milioni 1.3 kinashindwa kupambana matatizo ya dawa za kulevya kwa kiwango kinachostahili", amesema Masauni.

"Maazimio ya kikao ilikuwa ni kushughulika na watu hao ambao Katibu alisema anawafahamu kuwa wanamkwamisha. Nilimweleza mbele ya kikao kuwa nataka unipatie data nikashughulike, naacha Bunge nakwenda Zanzibar kwa shughuli hii, siwezi kusubiri Rais John Magufuli anitumbue mimi kwasababu ya uzembe wa watu wachache", ameongeza.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema kuwa haoni kama Zanzibar ina nia ya dhati ya kupambana na dawa za kulevya kwa aina ya Katibu huyo aliyedai anakwamisha juhudi za serikali.

Hata hivyo amegundua kuna mapungufu ya baadhi ya askari kwa kuwa wapo wanaoharibu kesi za dawa za kulevya makusudi kwa kuchukua rushwa kutoka kwa wauzaji wa dawa hizo wanaojulikana na kuwaachia mitaani na amemwelekeza Katibu wa Wizara hiyo kuunda tume maalumu itakayokuja kufanya kazi Zanzibar kuwabaini askari wanaozorotosha jambo hilo na hatua za haraka zichukuliwe.

China Kusaidia Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Taifa kilichopo Kunduchi Dar

$
0
0
Serikali ya China kupitia Jeshi la Ukombozi la China, kikosi cha Anga limetoa msaada wa ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Taifa kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam unaogharimu Shilingi Bilioni 56.

Ujenzi huo wa awamu ya pili ya chuo hicho utakifanya kuwa cha kisasa na miundombinu rafiki na kukiwezesha chuo hicho kudahili zaidi ya wanafunzi 100 kwa wakati mmoja baada ya ule wa awamu ya kwanza uliofanyika 2013 na kumalizika 2015. 

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, aliishukuru Serikali ya China kupitia jeshi la ukombozi la watu wa China kwa msaada huo kwani utasaidia kuongeza kozi na idadi kubwa ya wanafunzi.
 
Alisema mafunzo yanatolewa katika chuo hicho yanalenga ulinzi wa taifa na kimataifa kwa sasa na baadaye kiuchumi, kisiasa, kijeshi na kisayansi katika mikakati ya maendeleo ya taifa.

Dk Mwinyi pia alisema mbali na ujenzi wa chuo hicho pia wamejenga kituo maalumu kwa mafunzo maalum ambacho kipo Mapinga Bagamoyo, Pwani na hivi karibuni wataanza ujenzi wa makao makuu ya jeshi mkoani Dodoma eneo la Kikombo. 

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

$
0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0763172670/ 0715172670

Haji Manara Ataja Tofauti Ya Kocha wa Simba na Yanga

$
0
0
Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ametaja utofauti wa makocha Mwinyi Zahera wa Yanga na Patrick Aussems wa Simba.

"Tofauti ya kocha wa mpira na kocha wa Sunsumia au kibao kata unafungwa unawapongeza wa shindi na kukubali mapungufu yako angekuwa yeye!!!

Waamuzi wanatuonea mimi nimefundisha ulaya mika Arobaini (Ukigogle huoni timu alizo fundisha zaidi ya kufundisha kucheza Ndombolo na Mayenda) oooh Simba inabebwa leo Fei Toto hawakuvaa boksa na hawajala toka juzi!!!

"Ila akishinda sasa ninafuu kupiga gitaa kuliko Diblo na ile fasi ya putuluu imekuja na Ndege na ndio mana sisi wa Congo tunapendwa na madada wa kibongo .

Kocha mzuri huzungumzia vitu Technical na sio Riwaya kwa mahawala wako wanao tumia mkorogo wa buku" ameandika Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Waziri Kairuki Atoa Wito Kwa Wawekezaji Wazawa Kuchangamkia Fursa Za Uwekezaji Zilizopo Na Kusajili Miradi Ya Uwekezaji

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe.  Angela Kairuki ametoa wito kwa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato  Tanzania (ATAPE) na wawekezaji wengine wazawa kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini na kusajili miradi  yao ya Uwekezaji katika Tume ya uwekezaji ya Taifa (TIC).

Kairuki ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano wa 20 wa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato  Tanzania (ATAPE) Mjini Bariadi, ambapo amebainisha kuwa kwa mwaka huu 2019 wawekezaji wazawa zaidi ya asilimia 72 wamesajili miradi yao ya uwekezaji TIC.

“ Kwa mwaka huu peke yake tumepata wawekezaji wazawa waliosajili miradi yao ya uwekezaji TIC zaidi ya asilimia 72, hii inanipa faraja sana kama waziri wa nchi ninayesimamia uwekezaji ninapoona Watanzania wenzangu wanachangamkia fursa”

"Naomba mchangamkie fursa hizo kwa sababu wawekezaji wa nje tunapenda waje tu endapo watakuja kuungana nasi kwenye mtaji, kubadilishana nasi ujuzi na uzoefu " alisema Kairuki.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara, uwekezaji na kuweka vipaumbele kwa ajili ya kuvutia wawekezaji katika sekta ambazo zitakuwana athari na tija kubwa kiuchumi kwa wananchi, ili kuimarisha minyororo ya thamani katika kilimo,uvuvi, na mifugo ambayo ni maeneo yanayoajiri Watanzania wengi zaidi.

Aidha, Waziri Kairuki amezitaja sekta nyingine za kipaumbele kuwa ni  uzalishaji wa mafuta ya kula kwa kutumia mbegu zinazozalishwa nchini, uzalishaji wa sukari, uzalishaji wa dawa za binadamu, vifaa tiba na kemikali, ujenzi wa miundombinu ya uvuvi wa kisasa, viwanda vya kuchakata samaki, kusindika nyama, viwanda vya kubangua korosho, viwanda vitakavyotumia pamba na viwanda vya  pembejeo na mbolea.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ameipongeza ATAPE kwa jinsi  inavyoshirikiana na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji pamoja na huduma nyingine.

Kairuki amesema serikali pekee  haiwezi kutatua changamoto zote hivyo  kwa kushirikiana na wadau ikiwemo taasisi za dini wanaweza kuwahudumia wananchi na kuleta mabadiliko chanya ikiwa ni pamoja na  kuhubiri amani, huku akisisitiza kuwa masomo ya ujasiriamali yanayotolewa kwa wana ATAPE wayatumie kwa manufaa ya kanisa na jamii kwa ujumla.

Awali akimkatibisha waziri Kairuki, mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkutano huo umewasaidia  watu wa  Simiyu  kukutana na watu wa maeneo mengine hatua iliyopelekea kubadilishana uzoefu  sambamba na kuongeza na kupata masoko mapya .

‘’watu wetu wameongeza wigo wa masoko, mmebadilishana uzoefu ....huu ni mkoa wa kibiashara na ni mkoa wenye fursa nyingi;  tunajenga tawi la chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) hivyo ninawaalika wafanyabiashara na Watanzania wote kuja kuwekeza ujenzi wa hosteli eneo lile linalojengwa tawi hilo"alisisitiza Mtaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ATAPE Freddie Manento amesema kwa miaka mitatu ATAPE imewekeza miradi ya bilioni 1.2 katika miradi yenye manufaa kwa kanisa, wanajamii na wana ATAPE.

Alisema wamewekeza kwenye miradi ya maji kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa, miradi ya miti ya matund), korosho na miradi ya mashamba ya mihogo kwa kutengeneza ajira na faida katika vijiji walivyolima mashamba yao.

‘’Wana ATAPE wamejitoa kwelikweli na wameitikia dhana yetu ya kutumia vipaji na rasilimali zetu kwa ajili ya kazi ya MUNGU, hii iko katika mathayo 28;19, 20…hii ndio dhana yao’’ alisema Manento.

Mkutano wa Wanataaluma na Wajasiriamali (ATAPE) kutoka kanisa la Waadventista Wasabato umefanyika mkoani Simiyu kwa muda wa siku sita ambapo umehudhuriwa na wananchama zaidi ya 1500.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Ugonjwa wa Zinaa wa Kaswende (Syphilis) : Dalili Zake, Madhara Yake Na Jinsi Ya Kujikinga

$
0
0
Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum. Ugonjwa wa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara mengi. 

Maambukizi ya kaswende wakati wa ujauzito huleta madhara mengi sana kama kujifungua kiumbe mbacho kimeshakufa, mtoto kuathirika na ugonjwa huu wakati wa kuzaliwa, mtoto kupata matatizo wakati wa ukuaji wake, degedege na kuongezeka kwa vifo vya watoto wachanga nchini. 

Ugonjwa wa kaswende huathiri zaidi ya mimba millioni moja duniani kote kila mwaka na huchangia theluthi mbili ya vifo vya watoto wale wanaozaliwa tayari wameshakufa katika nchi za maeneo ya jangwa la sahara. 
 
 Asilimia 30 ya mimba zinazoathiriwa na kaswende huishia watoto kufariki wakati wa kuzaliwa. Asilimia nyengine 30 ya mimba zinazoathiriwa na kaswende husababisha watoto kuzaliwa na ugonjwa huu wa  kaswende, kupata matatizo ya ukuaji wao, degedege na kuongeza vifo vya watoto kwa asilimia 50. 
 
Ugonjwa wa ukimwi na kaswende mara nyingi huambatana pamoja. Ugonjwa wa kaswende huongeza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa ukimwi.

Visababishi vya ugonjwa wa kaswende

Kama tulivyosema awali, kaswende husababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum. Njia za maambukizi za ugonjwa huu ni kama zifuatavyo;
  • Kupitia kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeambukizwa kaswende
  • Kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kujamiana kupitia njia ya mdomoni (oral sex)
  • Mama aliyepata ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.
  • Kuambukizwa kupitia michibuko au mipasuko kwenye ngozi wakati wa kujamiana au wakati mwengine wowote pale mtu anapogusana na mtu mwenye kaswende ikiwa wote wawili wana mipasuko kwenye sehemu mbalimbali za ngozi zao. Sio rahisi mtu kutambua kama ana michibuko au la kwenye ngozi kwani mengine inakuwa midogo sana isipokuwa ile ambayo inaweza kuonekana kwa macho.
Dalili na Viashiria vya ugonjwa wa kaswende
Dalili na viashiria vya ugonjwa wa kaswende hutegemea na aina ya ugonjwa wa kaswende wenyewe. Kuna aina tano za ugonjwa wa kaswende ambazo ni;
  • Ugonjwa wa kaswende wa awali (Primary syphilis)
  • Ugonjwa wa kaswende wa pili (Secondary syphillis)
  • Kaswende iliyojificha (Latent syphilis)
  • Kaswende ya baadae (Tertiary syphilis)
  • Kaswende ya kurithi (Congenital syphilis)
Kaswende ya awali (primary syphilis)
Dalili ya kwanza ya aina hii ya kaswende ni kutokea kwa kidonda kidogo cha mviringo (chancre kama kinavyojulikana kitaalamu) katika sehemu ambayo bakteria wameingilia na hutokea kati ya siku 10 hadi miezi mitatu (kwa kawaida kuanzia wiki 2 hadi 6) baada ya mtu kupata maambukizi ya kaswende. Kidonda hiki kinaweza kutokea kwenye sehemu ya haja kubwa, shingo ya kizazi kwa wanawake (cervix), mdomoni (lips), uume (penis), ulimi, vulva, tupu ya mwanamke (vagina) na sehemu nyengine mwilini. Tezi (lymph nodes) ambazo zipo karibu na sehemu iliyotokea kidonda hiki kawaida huwa zinavimba baada ya siku 7 hadi 10. 


Kidonda hiki hakiambatani na maumivu na kwa kuwa kinaweza kutokea katika sehemu zilizojificha kama kwenye shingo ya kizazi, sio rahisi mtu kutambua kama na aina hii ya kaswende. Kidonda hiki kinaweza kuwepo kwa muda wa wiki 3 hadi 6 kama mtu hatapata tiba na kinatoweka chenyewe bila tiba au baada ya kupata tiba. 

Robo tatu ya wale ambao hawapati tiba huishia kuingia kwenye kundi la kaswende ya aina ya pili (Secondary syphilis).
 
Kaswende aina ya pili (Secondary syphilis)
Aina hii hutokea wiki 4 hadi 10 baada ya mtu kupata kaswende ya awali. Dalili za aina hii ya kaswende ni;
  • Vipele ambavyo haviwashi katika viganja vya mikono au nyayo za miguu. Vipele hivi pia vinaweza kutokea mwili mzima au sehemu mbalimbali za mwili.
  • Uchovu
  • Kuumwa kichwa
  • Homa (fever)
  • Kunyofoka nywele
  • Vidonda vya koo (sore throat)
  • Kuvimba kwa matezi mwili mzima
  • Maumivu ya mifupa (joint pain)
  • Kupungua uzito
Kaswende ya aina hii inakuwepo kwa wiki kadhaa na hupotea hata bila kupata tiba kwa mtu aliyeathirika. Pia inaweza kujirudia rudia katika kipindi cha mwaka mmoja hadi miwili na mtu huingia kwenye kundi la aina ya tatu ya ugonjwa wa kaswende (latent syphilis) baada ya miaka miwili.
 
Kaswende iliyojificha (Latent syphilis)
Hii inajulikana kama kaswende ambayo inaweza kuthibika tu kwa kutumia vipimo vya maabara (serological test). Imegawanyika katika makundi mawili:
i. Early latent syphilis (kaswende iliyojificha ya awali) – Hii ni ile ambayo hutokea ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya muathirika kuugua kaswende aina ya pili (secondary syphilis). Aina hii huwa na dalili zinazojirudia kama za kaswende ya pili (secondary syphilis)
ii. Late latent syphilis (kaswende iliyojificha ya kuchelewa) – Hii hutokea baada ya mwaka mmoja wa kuugua kaswende ya aina ya pili (secondary syphilis). Wakati wa kuugua aina hii, muathirika anakuwa hana dalili wala viashiria vyovyote vile na uwezo wake wa kuambukiza mtu mwengine unakuwa chini au hawezi kabisa kumuambukiza kaswende mtu mwengine.

 
Kaswende ya baadae (Tertiary syphilis)
Asilimia 30 ya wagonjwa wa kaswende ambao hawakupata tiba hapo awali huingia kwenye kundi hili na hutokea miaka 15 – 30 baada ya maambukizi ya kaswende hapo awali. 


Aina hii inaweza kuathiri viungo kama macho, ubongo, mishipa ya fahamu (Neurosyphilis), jointi au viunganishi vya mifupa, uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu na hivyo kusababisha madhara makubwa kama;
  • Upofu
  • Magonjwa ya moyo – Aortic dissection type B, syphilitic aortitis
  • Magonjwa ya akili
  • Magonjwa ya mishipa ya fahamu
  • Mtu kuwa kiziwi
  • Kupungukiwa na kumbukumbu (Memory loss)
  • Kifo
Pia aina hii ya kaswende inaweza kuathiri mfumo wa chakula (abdominal organs), mfumo wa kupumua (respiratory system) na mfumo wa uzazi (reproductive system).
 
Kaswende ya kurithi (Congenital syphilis)
Aina hii hutokea wakati wa ujauzito au baada ya mtoto kuzaliwa. Robo mbili ya wototo wanaozaliwa hawaonyeshi dalili zozote. Nusu ya watoto wenye maambukizi ya kaswende hufariki muda mfupi kabla ya kuzaliwa au baada ya kuzaliwa. Dalili za aina hii ya kaswende kwa mtoto mchanga zinaweza kutokea baada ya kuzaliwa au wiki 2 hadi miezi 3 baada ya kuzaliwa;
  • Kutoongezeka uzito au kushindwa kukua
  • Homa
  • Kukasirika haraka (irritability)
  • Kutochongoka kwa pua, pua inakuwa bapa (no bridge to nose or saddle nose)
  • Vipele kwenye viganja vya mikono na kwenye nyayo
  • Vipele vya rangi ya madini ya shaba kwenye uso, viganja vya mikono na nyayo
  • Vipele kwenye mdomo, sehemu za siri na sehemu ya haja kubwa
  • Kutokwa na majimaji puani
  • Kuongezeka ukubwa wa ini na bandama (hepatosplenomegally)
  • Ngozi kuwa ya njano (jaundice)
  • Upungufu wa damu mwilini (anemia)
Dalili kwa mtoto mkubwa
  • Kuathirika meno (Hutchinson teeth)
  • Maumivu ya mifupa
  • Upofu
  • Kupungua uwezo wa kusikia au mtoto kuwa kiziwi
  • Ukungu kwenye mboni za macho (Clouding of cornea)
  • Vidonda rangi ya kijivu kwenye sehemu ya haja kubwa na kwenye tupu ya mwanamke (vagina)
  • Ngozi kuwa na mabaka meusi kwenye mdomo, sehemu za siri na sehemu za haja kubwa
  • Maumivu kwenye mikono na miguu
  • Kuvimba jointi za mifupa
Ugunduzi wa ugonjwa wa kaswende
Ugunduzi wa ugonjwa wa kaswende huusisha utambuzi wa dalili na viashiria vya ugonjwa huu (hii hufanywa na daktari) kupitia historia ya mgonjwa, vipimo vya damu na vipimo vya kugundua bakteria aina ya Treponema pallidum. 

 
a. Utambuzi wa dalili na viashiria vya ugonjwa wa kaswende
  1. Hufanywa na daktari
  2. Huusisha historia ya mgonjwa
b. Vipimo vya damu
Vipimo hivi vinahusisha utambuzi wa chechembe za antibodies dhidhi ya bakteria Treponema pallidum. Majibu yanaweza kuwa false positive (Wale ambao vipimo vimeonyesha wana kaswende lakini hawana ugonjwa huu,hii hutokea kwa wale ambao waliugua kaswende awali na hali hii inaweza kuwepo hadi miezi mitatu baada ya kupona ugonjwa huu au wale wenye ugonjwa wa kifua kikuu, malaria, wajawazito, measles, endocarditis, connective tissue disease nk.) au false negative (Wale ambao wameathirika na kaswende lakini vipimo vinaonyesha hawana kaswende). Mara nyingi ni vigumu sana kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huu, hivyo vipimo hurudiwa ili kupata uthibitisho.
  • RPR (Rapid plasma reagin) test
  • VDRL (Veneral Disease Research Laboratory)
  • The microhemagglutination assay [MHA-TP] Hufanywa kuthibitisha ugonjwa wa kaswende
  • Fluorescent-treponemal-antibody absorption [FTA-ABS, enzyme-linked immunosorbent assay ELISA]) Hufanywa kuthibitisha ugonjwa wa kaswende
  • PCR (Polymerase Chain Reaction) – Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) vya Treponema pallidum.
  • Complete Blood Count - Kipimo cha kuangalia wingi wa damu na aina tofauti za chembechembe za damu
c. Vipimo vya kugundua bakteria
Hufanywa kwa kutumia hadubini ( Dark field microscopy).
d. Vipimo kwa wale wenye madhara ya kaswende
  • Picha ya X-ray ya kifua, uti wa mgongo
  • Vipimo vya moyo – ECG, transesophageal echocardiogram,aortic angiography, doppler ultrasonography, chest MRI, cardiac CT scan (contrast), CT angiography.
  • CT scan ya kichwa, mfumo wa chakula (abdominal CT)
  • MRI ya kichwa, uti wa mgongo, brainstem
  • Bone scan (Vipimo vya mifupa)
  • Vipimo vya macho
  • Vipimo vya masikio
  • Lumbar puncture – Kipimo cha kuangalia bakteria kwenye maji ya uti wa mgongo
  • Cerebral angiogram – Kipimo cha kuangalia mishipa ya damu kwenye ubongo
  • Nerve conduction tests
Tiba ya ugonjwa wa kaswende
Tiba ya ugonjwa wa kaswende inahusisha matumizi ya dawa za antibiotic za kundi la penicillin. Dawa nyengine ni aina ya polyketides antibiotics (doxycyline nk.) lakini hizi hazitumikia kwa wajawazito. Kwa wale ambao wanapata madhara baada ya kutumia penicillin ni bora kumjulisha daktari mapema. 


Tiba kwa wale wenye kaswende iliyoathiri mishipa ya fahamu ni penicillin inayotolewa kupitia kwenye mishipa ya damu na wanahitaji kulazwa hospitali kwa matibabu zaidi. Wale ambao wameathiriwa na kaswende kwenye viungo vya mwili, madhara hayo sio rahisi kurekebishika na mengine hayarekebishiki.
 
Tiba ya upasuaji
Tiba ya upasuaji kwa wale wenye madhara ya ugonjwa wa kaswende kama kwenye moyo na nk.
Wagonjwa wa syphilitic aortitis wanaweza kutibiwa kwa angiography/angioplasty lakini kama wana magonjwa mengine ya moyo kama coronary heart disease basi tiba hii haifanyiki. 

 
Madhara ya ugonjwa wa kaswende
  • Magonjwa ya moyo
  • Magonjwa ya akili
  • Mtu kuwa kiziwi
  • Upofu
  • Magonjwa ya mishipa ya fahamu
  • Kupungukiwa kumbukumbu (memory loss)
  • Upungufu wa damu mwilini
  • Mimba kutoka wakati wa ujauzito
  • Kuzaa mtoto ambae ameshafariki
  • Madhara kwenye mifupa
  • Vifo vya watoto
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa kaswende
  1. Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu, njia sahihi ni kuepuka kabisa ngono
  2. Wale walioathirika kuacha kufanya ngono na wenza wao hata kama wameanza tiba mpaka vidonda vipone
  3. Kwa wajawazito, kuhudhuria kliniki mapema ili kama ukigundulika kuwa na kaswende hivyo kupata tiba haraka.
  4. Epuka kugusana na majimaji yoyote yanayotoka kwa mtu aliyeathirika kwa ugonjwa huu.

Ugonjwa wa Zinaa wa Kisonono (gonorrhea) : Dalili Zake, Madhara Yake Na Jinsi Ya Kujikinga

$
0
0
Kati ya magonjwa yanayoathiri watu wengi sana duniani ni magonjwa ya zinaa. Haya ni magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vitendo vya ngono. 

Vitendo hivi vya ngono vinaweza kuwa kujamiana, kupiga denda (kissing), vitendo vya ngono kwa kutumia mdomo (oral genital sex), kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) iwe kwa mwanamume na mwanamke au kati ya wanaume wenyewe na hata wale wanaotumia vifaa vya kufanyia ngono (vibrators). 

Magonjwa ya zinaa huathiri sana watu walio katika umri wa miaka 15 – 24 lakini hata kwa watu wengine ambao wana umri chini au zaidi ya huu niliotaja pia yanaonekana kwa wingi.

Kuna magonjwa ya zinaa zaidi ya ishirini yanayotambulika duniani, baadhi ya magonjwa ya zinaa ni
  1.  Kisonono (Gonorrhoea – “Gono” kama wengi wanavyopenda kuita kwa kifupi).
  2.     Chlamydia
  3.     Kaswende (Syphillis)
  4.     Human papilloma virus (HPV)
  5.     HIV/AIDS (Ukimwi/Upungufu wa kinga mwilini)
  6.     Hepatitis B, C, A
  7.     Herpes virus
  8.     Trichomoniasis
  9.     Bacteria Vaginosis
  10.     Pubic lice (chawa kwenye nywele za kinena)
  11.     Chancroid
Magonjwa mengi ya zinaa yanatibika lakini kuna baadhi ambayo hayana tiba ya uhakika kama HPV, Hepatitis B na C, na HIV. Mengine yameanza kuwa sugu kutokana na matumizi ya dawa za antibiotics bila mpangilio, magonjwa hayo ni kama gono (gonorrhoea) na nk.
 
Visababishi vya magonjwa ya zinaa
  1. Vitendo vya ngono kama nilivyoeleza hapo awali
  2. Kuanza vitendo vya ngono mapema au wakati wa umri mdogo
  3. Kuwa na wapenzi wengi
  4. Kufanya mapenzi ambao sio salama
  5. Maambukizi kupitia michibuko au sehemu zilizokatika kwenye ngozi kwa kugusana na majimaji ya aina yoyote yanayotoka kwa mtu mwenye ugonjwa wa zinaa kama damu, shahawa nk. Hii inaweza kutokea bila mtu kujua kwani mara nyingi dalili za magonjwa ya zinaa zinakuwa hazionekani kwa wanawake na hata baadhi ya wanaume.
Watu wengi huhisi kitendo cha kula denda (kissing) ni salama lakini si kama wanavyofikiria kwani baadhi ya magonjwa kama kaswende, herpes nk, yanaweza kuambukizwa kupitia njia hii. 

Soma pia:Tatizo la Kutokwa na usaha Wakati wa Kukojoa 

Kondomu husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama gono, Chlamydia lakini sio kinga muafaka dhidhi ya magonjwa ya zinaa kama kaswende, genital herpes, genital warts, na magonjwa ya upungufu wa kinga mwilini (AIDS).

Kisonono (gonorrhea) ni nini?
Kisonono ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao hukuwa na kuzaliana kwa haraka katika sehemu zenye unyevunyevu na joto mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa wanawake (cervix), mirija ya kupitisha mkojo au shahawa (urethra), mdomoni na kwenye puru. Maambukizi mengi kwa wanawake hutokea kwenye shingo ya kizazi (cervix). 

Asilimia 75 ya ugonjwa wa gono hutokea kwa watu wenye umri wa miaka 15 – 29, wanawake walio katika umri wa miaka 15 -19 na wanaume walio katika umri wa miaka 20 – 24 wako kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
 
Ugonjwa huu huambukizwa vipi?
Ugonjwa huu huambukizwa kupitia vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex). Ugonjwa unaweza kujitokeza kwenye sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na kwenye puru (rectum). 

Soma Pia: Ugonjwa wa Zinaa wa Kaswende (Syphilis) : Dalili Zake, Madhara Yake Na Jinsi Ya Kujikinga 

Ugonjwa wa gono huonekana sana kwa vijana, watu wenye maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi mijini, watu weusi na watumiaji madawa ya kulevya.
 
Dalili za ugonjwa wa kisonono
Dalili za ugonjwa wa kisonono huanza kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7 baada ya mtu kupata maambukizi na huweza kuchelewa kwa wanawake. Dalili ni kama zifuatazo

Kwa wanaume
  1. Kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa (burning sensation)
  2. Kutokwa na majimaji ya njano au meupe au ya kijani kutoka kwenye uume yanayoambatana na maumivu makali sana
  3. Wakati mwengine maumivu au kuvimba kwa korodani (swollen testicles)
  4. Maambukizi yakiwa kwenye puru (rectum) huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuwashwa sehemu za haja kubwa, na hata haja kubwa inaweza kutoka ikiambatana na damu, hii inatokea kwa wanaume na wanawake.
Kwa wanawake
Dalili kwa wanawake huwa si nyingi lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili zozote
  1. Maumivu au kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa
  2. Kuongezeka kwa kutoka majimaji kutoka kwenye tupu ya mwanamke ambayo ni ya njano au yamechanganyika na damu
  3. Kutokwa na damu kupitia tupu ya mwanamke kabla ya hedhi kufika.
  4. Kutokwa na damu baada ya kujamiana au baada ya tendo la ndoa
  5. Kichefuchefu
  6. Homa (fever)
  7. Kutapika
Vipimo vya ugonjwa wa kisonono
  1. Swab for culture – Kipimo hiki hufanyika maabara kwa kupandikiza bakteria baada ya kufuta sehemu za siri kwa kutumia swab ili kuona kama kuna bakteria wanaosababisha gono.
  2. Polymerase Chain Reaction (PCR)– Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya bakteria, ni ghali sana.
Tiba ya ugonjwa wa kisonono ni nini?
Tiba ya gono inahusisha na tiba ya ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi magonjwa haya huambatana kwa pamoja.Tiba hutegemea na umri wa mgonjwa na kama mtu ni mjamzito au la. 

Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra na puru, dawa zinazotumika ni aina za cephalosporin dozi moja pamoja na dawa za aina ya macrolide antibiotics (mfano azithromycin) na za jamii ya penicillin (mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa chlamydia. Mara nyingi kwa wale chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano.

Soma Pia: Saratani ya tezi dume : Madhara Yake, Dalili Zake, Chanzo na Tiba Yake

Fuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi kwani dawa nyingi zina madhara kwa wajawazito (mfano doxycyclin). Ushauri nasaha hutolewa kwa wapenzi wote wawili na ni vizuri wapenzi wote wawili kutibiwa hata kama mmoja hana dalili za ugonjwa huu.
 
Madhara ya ugonjwa wa kisonono
  1. Kutoweza kuzaa kwa mwanamke (tasa) au kutoweza kutungisha mimba kwa mwanamume (infertility)
  2. Huweza kuathiri moyo (heart valves), ubongo,ngozi nk ambayo ni hatari sana kwa mtu yoyote.
  3. Madhara kwenye sehemu za maungio au jointi (joint inflammation)
  4. Kwa wanawake wale ambao hawajatibiwa wanaweza kupata ugonjwa wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) ambao huongeza asilimia ya mwanamke kuwa tasa.
  5. Wale wanawake ambao ni wajawazito na wameambukizwa gono wako kwenye hatari ya mimba kutoka au kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza umri wake (preterm labor).
  6. Kwa wale wanaoambukizwa gono kipindi cha kukaribia kujifungua, wanaweza kuwaambukiza watoto wao na hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), kuwa kipofu (blindness), homa ya mapafu (pneumonia) na ugonjwa wa mifupa (septic arthritis).
Kinga ya kisonono
  1. Kutumia kondomu wakati wa kujamiana
  2. Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
  3. Kuacha vitendo vya ngono kama matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa wanawake mfano vibrators nk.
  4. Kwa wanawake wajawazito – Hakikisha unahudhuria kliniki mapema ili upate kuchunguzwa na kupatiwa tiba muafaka kama utagundulika na ugonjwa wa gono au ugonjwa mwengine wowote.
  5. Wanawake wajawazito wanashauriwa kujifungulia hospitali ili kama mtoto ameathirika na gono apate matibabu ya haraka baada ya kuzaliwa kuepusha kuwa kipofu.
  6. Epuka kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa gono.

Wafugaji Waaswa Kubadilika Kifikra Na Kufuata Sheria

$
0
0
Na. Edward Kondela
SERIKALI imewataka wafugaji nchini kubadili fikra zao na kutambua umuhimu wa kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi ili kujiepusha na mkono wa sheria pindi wanapoingiza mifugo yao katika hifadhi na mapori ya akiba.

Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika Wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amesema baadhi ya wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika hifadhi na mapori ya akiba, hivyo kusababisha kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kati yao na wahifadhi kwa madai ya kuonewa ilhali wahifadhi hao wanatakeleza sheria za nchi.

“Tunatamani fikra za wafugaji wote nchini zibadilike na zianze kutambua umuhimu wa kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo msingi wa mafaniko. Niwaombe wafugaji wote nchini watambue kwamba Wizara ya Mifugo na Uvuvi itapenda wafugaji wafuate sheria, taratibu na kanuni, tukifanya hivyo tutakuwa marafiki wa wizara unapokuwa mhalifu unakuwa tena siyo mfugaji bali unakuwa mhalifu.” Alisema Prof. Gabriel.

Katibu mkuu huyo amelazimika kukutana na wafugaji hao kutokana na hivi karibuni ng’ombe kukamatwa katika Pori la Akiba la Maswa ambapo wamiliki wa ng’ombe hao wamekiri kufanya kosa na kulipa faini waliyotozwa na mahakama mara baada ya kukiri kosa na kutiwa hatiani.

“Hivi karibuni ng’ombe walikamatwa katika Pori la Akiba la Maswa, ndipo busara ikatumika kuona jambo hilo linafikia tamati ambapo wahusika wamekabidhiwa ng’ombe zao kwa kuwa busara imetumika na siyo kwamba wao wameshinda, kwa mujibu wa sheria wenzetu wa hifadhi wanachofanya ni kusimamia Sheria Namba Tano ya Mwaka 2009 ya Hifadhi ya Wanyamapori kwamba mifugo ikikamatwa inaweza kutaifishwa.” Alifafanua Prof. Gabriel.

Awali akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kabla ya kuzungumza na wafugaji hao, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amewashukuru madiwani wa halmshauri hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mhe. Juma Issack Mpina kwa uelewa wa hali ya juu baada ya Meneja wa Pori la Akiba la Maswa Bw. Lusato Masinde kutoa elimu na sheria iliyotumika na maamuzi yaliyotolewa na mahakama kwa wafugaji waliyoingiza mifugo katika Pori la Akiba la Maswa.

Aidha amebainisha kuwa kunapaswa kuwepo kwa mawasiliano mazuri kati ya viongozi na jamii ya wafugaji katika maeneo yote nchini ili kujenga mahusiano mazuri na kuelewa majukumu ya wasimamizi wa hifadhi na mapori ya akiba ambao wamekuwa wakisimamia sheria na kwamba hawapo kwa ajili ya kumuonea mtu yeyote.

Katika kikao na wafugaji Prof. Gabriel amewataka pia wasijichukulie sheria mkononi hata wanapokuwa wamepishana kauli na wasimamizi wa sheria kama ambavyo imekuwa ikijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini ambapo amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo ni kosa kubwa kisheria, huku akiwapongeza wafugaji wa Wilaya ya Meatu kwa kuwa watulivu na kuonesha ushirikiano kwa maafisa wa Pori la Akiba la Maswa baada ya kuingiza mifugo yao katika pori hilo kinyume na sheria na kutii hatua za kisheria zilizochukuliwa dhidi yao.

Akizungumza na wafugaji Katika kuhakikisha sekta ya ufugaji inaboreka katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wizara inahakikisha kwa juhudi zote inaboresha sekta ya ufugaji nchini yakiwemo malisho bora kwa kuwepo kwa shamba darasa katika wilaya hiyo na maeneo mengine.

Pia Prof. Gabriel amewataka wafugaji kufuga kisasa kwa kuwa na ng’ombe wanaopatikana kwa njia ya uhimilishaji ambao wamekuwa na matokeo mazuri kwa kuwa na nyama nyingi na maziwa mengi yenye ubora.

“Ukifuga kisasa ng’ombe wanaopatikana kwa njia ya uhimilishaji hautajivunia idadi ya ng’ombe ulionao bali kwa kilo na wingi wa maziwa ambao ng’ombe hao wanatoa, ambapo ng’ombe mmoja anafikia hadi kilogram 800 na tumehakikisha kama wizara wafugaji wanapata mbegu za ng’ombe bora kwa bei isiyozidi Shilingi Elfu Tano.” Alisema Prof. Gabriel

Kwa upande wake Meneja wa Pori la Akiba la Maswa Bw. Lusato Masinde amesema wapo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi na kwamba wataendelea kusimamia sheria.

“Sisi tutaendelea kutoa elimu ili wananchi wafahamu umuhimu wa sheria zilizopo nchini ikiwemo inayohusu maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba ili wananchi wasifanye shughuli zinazokatazwa katika maeneo hayo.” Alisema Bw. Masinde.

Amefafanua wao kama maafisa wanaolinda Pori la Akiba la Maswa wanahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi hususan wafugaji wa Wilaya ya Meatu ili kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuwatia hatiani kwa kukiuka sheria za nchi ambazo wamepewa kuzisimamia.

Nao baadhi ya wafugaji walioshiriki kikao cha Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel wameomba kupata elimu zaidi juu ya uhimilishaji ili waweze kufuga ng’ombe kisasa na wenye tija kiuchumi.

Pamoja na hilo wamewaomba pia wafugaji wenzao kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi na kuwa karibu na viongozi wa wilaya hiyo ili waweze kufanya shughuli zao kwa kufuata maelekezo yao na kuwa na mawasiliano mazuri ambayo yatawaepusha kutojiingiza na ukiukwaji wa sheria kwa kuingiza mifugo kwenye maeneo wasiyoruhusiwa.

SIDO Yawataka Wananchi Mkoani Dodoma Kuchangamkia Fursa Za Ndani

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni ,Dodoma.
Wananchi mkoani Dodoma wameaswa kutumia fursa za ndani ikiwa ni pamoja na kushiriki katika mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi ili kufikia Tanzania ya viwanda.

Wito huo umetolewa na Kaimu meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda Vidogo SIDO Mkoa wa Dodoma Stephano Martin Ndunguru wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,ambapo amesema wananchi waache kuwakimbia wageni wanaohamia jijini Dodoma na wao kwenda mbali na mji bali watumie fursa za ndani kuingiza kipato ambacho kitakidhi mahitaji.

Aidha amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwasiliana na SIDO ili kuwa mshirika wa karibu na kujua fursa mbalimbali zinazo tolewa na shirika hilo, huku akiwataka wananchi kushiriki katika mafunzo ya usindikaji wa mazao mbalimbali ili kufikia Tanzania ya viwanda.

Mbali na hilo amesema kuwa bidhaa inayotengenezwa na ngozi ni imara katika matumizi sababu imetengenezwa na wataalamu ambao wamepata mafunzo bora huku wengine wakiwa wamejiajiri kutengeneza bidhaa hizo.

Hata hivyo ndunguru amesema kuwa SIDO wapo tayari kutoa huduma muhimu kwa watengenezaji wa mifuko mubadala ya Rambo kwa kutoa mafunzo,fedha, na kutafuta masoko kwa wakati.

Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Shekinah Presbyterian Akemea Rushwa na Wanasiasa Wanaovuruga Amani

$
0
0
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Shekinah Presbyterian lililoko Madale, jijini Dar es salaam Mch. Daniel John Seni amekemea vikali vitendo vya baadhi ya viongozi kuwaaminisha uongo watu wengine kwa manufaa yao binafsi. 

Akihubiri katika ibada ya kuadhimisha sikukuu ya Pasaka kwa mwaka 2019 alidai kuwa “watu waliokuwa wakipiga kelele kwamba Yesu asulubiwe waliaminishwa kwamba Yesu ni mtu mbaya na hafai, na ndiyo maana walianza kupiga kelele kwamba “na asulubiwe”. Lakini ukweli ni kwamba wale wakuu wa makuhani waliwashawishi makutano kwa ajili ya kutetea maslahi yao ambayo yalikuwa yanahatarishwa na Yesu ambaye aliwaambia ukweli mkavu kwa matendo waliyokuwa wakifanya. 

Aliendelea kusema kwamba “hivi wanasiasa wengi wamekuwa wakiwatumia watu wasiojua chochote kuandamana pasipo hata kujua kwa nini wanaandamana!” Watenda mema katika jamii yetu wameanza kuonekana ni wabaya kwa sababu ya nguvu ya ushawishi ya watenda mabaya, ni lazima mambo haya tuyakemee katika jamii zetu. Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunapata ukweli katika kila jambo, ili tusije tukadanganywa kwa kuaminishwa kwamba fulani ni mbaya kumbe sivyo.

Vile vile aliongelea kitendo cha Wakuu wa Makuhani kujaribu kuuaminisha umma kwamba Yesu Kristo hakufufuka kutoka wafu. 

Alielezea kuwa “Wakuu wa Makuhani baada ya kuona kwamba ushawishi wao wa kwanza umegonga mwamba, waligeukia upande wa pili kwa kuwahonga askari wao ili kuuaminisha umma maneno ya uongo. 

Hata hivyo alikemea vikali vitendo vya rushwa katika jamii kwa madai kwamba “kitendo cha wale askari waliokuwa wakilinda kaburi la Yesu kukubali kupokea rushwa ili kufunika ukweli kilikuwa ni kitendo cha aibu sana kwao. 

Askari hawa waliamua kuisaliti kazi yao kwa kudanganya kwamba walikuwa wamelala! Ni mlinzi gani anayeweza kusema kwamba nimeibiwa kwa sababu nilikuwa nimelala? Kazi ya askari ni kazi inayohitaji uaminifu mkubwa lakini hawa askari walijishushia heshima kwa kupokea kitita cha pesa ili wazibwa midomo yao.

Akiwageukia watu wanaopenda kutoa rushwa ili kuziba ukweli kwa faida yao binafsi mchungaji huyu alisema kuwa “ni jambo la aibu kwa viongozi kutoa rushwa ili kuziba midomo ya watu, tunajua kwamba rushwa huziba ukweli na hupotosha macho ya watu.” 

Aliongeza kwamba” tumekaribia kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa, watu wa Mungu kataeni rushwa, kataeni kufunikwa macho yenu, msikubali kuchagua viongozi ambao hawafai eti kwa kisingizio cha kwamba amekupa chochote.”

Mchungaji huyu aliendelea kusema kwamba “katika maisha yetu ya kila siku tunahitaji kutumia pesa, lakini lazima tujue kwamba pesa tuliyo nayo imepatikana kwa njia gani? Askari hawa alipata pesa kubwa kwa ajili ya kufunika ukweli kwamba Yesu Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. 

Inawezekana katika jamii zao walianza kuheshimiwa kwa kuwa na pesa, lakini je pesa hizo zilikuwa ni pesa halali? Epuka pesa ya rushwa na acha kutoa rushwa, ni lazima tuwe wakweli ili nchi yetu iendelee mbele.

Ibada hii ilijumuisha kushiriki Meza ya Bwana, tendo ambalo Bwana Yesu aliliagiza kwa wanafunzi wake kwamba wafanya hivyo kwa ajili ya kukumbuka mateso yake, na ni tendo ambalo hupokelewa kwa Imani na Wakristo ulimwenguni.
HERI YA PASAKA, 2019
________________________
Imetolewa na ofisi ya Mchungaji,
Shekinah Presbyterian Church Tanzania
0769080629 au spctanzania@gmail.com

PICHA: Magari Mawili Ya Mashindano Yagongana Na Kuua Arusha

$
0
0
Ajali  imetokea leo Aprili 21, 2019 baada ya magari mawili ya mashindano kugongana eneo la Oldonyosambu, Arumeru jijini, Arusha na kuua na kujeruhi baadhi ya watu waliokuwa nje ya barabara.

Kati ya magari hayo mawili yaliyopata ajali, moja lilikuwa linaendeshwa na Mkenya na lingine Mtanzania.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shanna akiongea  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema atatoa taarifa kamili baada ya saa moja.


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya April 22

Askofu Shoo: Kuna watu wanaotumia nguvu nyingi kuuficha ukweli bila kujua kuwa ukweli una asili ya kutofichika.

$
0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, (KKKT) Dkt Fredrick Shoo, amesema siku hizi duniani kuna watu wanaotumia nguvu nyingi kuuficha ukweli, bila kujua kuwa ukweli una asili ya kutofichika.
 
Askofu Dkt. Shoo, alitoa kauli hiyo jana wakati akihubiri kwenye ibada ya Pasaka iliyosherekewa duniani kote jana. 

"Tunaweza kusema tunaipenda nchi yetu, lakini swali kubwa kwetu ni je tunao ujasiri wa kujitoa kweli kweli hata kiasi cha kutoogopa vikwazo vya hatari?" Alihoji Askofu Shoo.
 
Alisema ujasiri peke yake bila upendo unaotoka moyoni, huzaa ukatili na ujasiri usiokuwa na upendo huzaa hofu, na inapotokea kusimama kwa ajili ya wengine kwa manufaa ya wengine upendo bila ujasiri unabakia kuwa upendo wa mdomoni tu.
 
Aliongeza kuwa imefika hatua baadhi ya Wakristo wanaweza kusema wanampenda Yesu, lakini inapokuja saa ya kusimama kama shahidi wa Kristo, kuitetea familia yake, Kanisa na hata nchi yao, watu wanaingia mitini.
 
"Akina mama wale hawakusaliti, walisimama kweli kweli, na upendo wao huu wa dhati,î alisema Askofu Shoo. Aliongeza kuwa; "Ujasiri wa kujitoa kwa ajili ya wengine na familia, Kanisa na nchi unahitaji watu kama hawa wenye upendo wenye ujasiri na upendo wa kujitoa kwa ajili ya wengine"
 
Aliongeza kuwa wakati wa Yesu, askari waliokuwa wakilinda kaburi, walipewa pesa nyingi ili kuuficha ukweli, lakini haikuwezekana na leo wapo watu ambao wanajaribu kuwazuia Wakristo kutangaza habari za Yesu na kulizuia kanisa kufanya kazi ya Kitume, bila kujua kuwa tendo hilo ni la Mungu mwenyewe.
 
"Kulifanyika jitihada nyingi kwa ajili ya kuficha ukweli wa Yesu
kufufuka, askari walioshuhudia lile tetemeko na kushuhudia Yesu kufufuka walikuwa na hofu kubwa, walipewa pesa nyingi na wale wakuu wao, ili eti waseme Yesu hakufufuka, bali wanafunzi wake walikuja kumuiba usiku wakiwa wamelala."
 
"Lakini haikuwezekana kuuficha ukweli huo, habari za kufufuka kwa Yesu zikaenea na tena mbaya zaidi hata habari kwamba wakuu waliwapa pesa wale askari ili wanyamaze nazo zikaenea.

Waziri Kalemani asisitiza Taasisi za Umma vijijini ziwekewe umeme

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchi nzima, kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha kuunganisha umeme kwa taasisi zote za umma zilizo katika maeneo yao.

Alitoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti wiki iliyopita akiwa katika ziara ya kazi wilayani Chamwino, Mkoa wa Dodoma, ambapo aliviwashia umeme vijiji vya Buigiri na Mwigamwile.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Buigiri pamoja na wananchi, Waziri alisisitiza kwamba, kitendo cha kuwasha umeme katika shule hiyo kinalenga kutoa hamasa katika utekelezaji wa maagizo ya serikali kuwa taasisi zote za umma ni lazima zipelekewe umeme.

“Niwaombe viongozi wa Halmashauri za Vijiji na Wilaya nchini kote, kuhakikisha taasisi za umma katika maeneo yenu zinalipia gharama ya kuunganishiwa umeme ambayo ni shilingi 27,000 tu kwa ninyi mlioko vijijini, ili taasisi hizo zote ziunganishiwe umeme,” alisisitiza.

Aidha, kuhusu suala hilo la kulipia gharama za kuunganishiwa umeme, Waziri alilazimika kutoa msisitizo kwa viongozi na wananchi kwani alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu kulalamika kuwa hawajaunganishiwa umeme lakini baada ya kufuatilia sababu iliyobainika ni kuwa wanakuwa hawajalipia huduma hiyo.

“Lipieni umeme. Msibaki kulalamika tu. Mlalamike mkiwa mmelipia.”

Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani aliwataka wanafunzi wa Shule hiyo ya Buigiri kuongeza jitihada katika masomo kwani tayari wamepelekewa umeme ili kuongeza kiwango cha ufaulu shuleni hapo.

Awali, akizungumza wakati wa tukio hilo la uwashaji umeme, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga alimweleza Waziri kuwa, Shule husika imekuwa na kiwango duni cha ufaulu kutokana na sababu mbalimbali, mojawapo ikiwa ni ukosefu wa umeme tangu ilipoanzishwa mwaka 2007.

Akiwa katika kijiji cha Mwigamwile, Waziri Kalemani aliwasha umeme katika Ofisi mpya ya Serikali ya Kijiji, ili kuendelea kutoa msisitizo wa azma ya serikali kuhakikisha taasisi za umma zinaunganishiwa umeme.
 
Aidha, ili kuonesha msisitizo zaidi, Waziri Kalemani, alilazimika kulipa yeyé mwenyewe shilingi 27,000 ikiwa ni gharama za kuunganisha umeme katika kisima cha maji kilichoko kijijini Ikoa, Kata ya Ikoa ambacho pamoja na kuwa kimekamilika kwa muda mrefu hakijaanza kufanya kazi kutokana na kutokuwa na umeme.

Waziri aliwaagiza wataalamu wa TANESCO kuunganishia kisima hicho umeme kabla ya Jumanne  Aprili 23 mwaka huu.

Katika maeneo yote ya Wilaya hiyo ambayo Waziri alipita kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, alimsisitiza Mkandarasi kuongeza kasi ya kuunganisha umeme ambapo alimtaka kufikia Desemba mwaka huu, awe amekamilisha kazi ya kuviunganishia umeme vijiji na vitongoji vyote vya Jimbo la Chilonwa.

Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye alifuatana na Waziri katika ziara hiyo, Joel Mwaka, alimwambia kuwa vijiji 20 vya jimbo hilo kati ya 47 vilivyopo, havijafikiwa na umeme.

“Pamoja na kuwa mkataba unaonesha kazi hii ya kuunganisha umeme kupitia mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA III, Phase I) inatakiwa ifikie tamati Juni mwakani, lakini nakuagiza wewe mkandarasi ukamilishe kazi hii ifikapo Desemba,” alisisitiza Waziri.

Mbali na kuwasha umeme katika vijiji vya Buigiri na Mwegamile, Waziri pia alikagua utekelezaji wa miradi ya umeme katika vijiji vya Ikoa (Kata ya Ikoa), Nguga (Kata ya Msamalo) na Mlebe (Kata ya Msamalo).

Viongozi wengine walioshiriki ziara hiyo ni pamoja na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga, Kaimu Meneja wa TANESCO, Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Tumaini Nyari, pamoja na wahandisi wasimamizi wa miradi ya umeme vijijini kutoka wizarani na REA.


Serikali mbioni kuanza Mpango wa Uagizaji wa Gesi ya Mitungi (LPG) Kwa Pamoja

$
0
0
Serikali imesema iko katika hatua za awali za kuandaa mpango  wa uagizaji wa gesi ya mitungi (LPG) kwa pamoja kama ilivyo kwa mafuta ya Petroli hali itakayosaidia kudhibiti masuala mbalimbali ikiwemo  bei ya gesi hiyo .

Akizungumza wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dodoma, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, wananchi katika maeneo yote nchini wanafikiwa na huduma hiyo, hivyo Serikali itaratibu usambazaji wa gesi hiyo badala ya kuwaachia wauzaji wenyewe kuamua maeneo  wanayotaka kupeleka gesi.

‘’ Serikali ikitangaza bei elekezi kulingana na soko, itawafanya wauzaji wafuate bei hiyo badala ya wao kujipangia, hii itasaidia wananchi kuuziwa gesi kwa gharama inayofanana katika maeneo mbalimbali ambapo gesi hiyo itauzwa.”alisema Dkt. Kalemani.

Alieleza kuwa, suala la sasa la kila muuzaji kujiamulia sehemu anayotaka kupeleka gesi inafanya maeneo mengine kukosa kabisa nishati hiyo hivyo sasa Serikali itaweza kuwadhibiti wauzaji na kuhakikisha kuwa maeneo yote nchini yanafikishiwa gesi.

Aliongeza kuwa, utaratibu wa kuagiza gesi inayotumika  majumbani kwa pamoja utasaidia Taifa kutambua kiwango halisi cha gesi kinachohitajika nchini na kiasi cha gesi kinachoingizwa nchini na hivyo kusaidia pia katika shughuli za ukusanyaji wa mapato.

Awali, akitoa taarifa kwa Wajumbe wa Kamati hiyo, Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja  (PBPA), Erasto Simon  alisema kuwa, Wakala huo kwa sasa unafanya tathmini ya namna bora ya kuanza uagizaji wa pamoja wa gesi ya mitungi (LPG) kwa kuzingatia maoni kutoka kwa  wadau mbalimbali.

Akizungumzia faida mbalimbali zinazotokana na uagizaji wa mafuta wa pamoja, Simon alisema kuwa, ni kuweka mazingira sawa ya kibiashara kwani gharama za uagizaji wa mafuta ziko sawa kwa makampuni yote na kuondoa mianya ya rushwa katika uagizaji wa mafuta kwani ufunguzi wa zabuni hufanyika kwa uwazi na washiriki wote huridhika na matokeo ya zabuni.

Alitaja faida nyingine kuwa ni, Taifa kuwa na uhakika wa usalama wa upatikanaji wa mafuta kwa muda wote na kuwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za mafuta zinazosaidia katika ukusanyaji wa mapato na kupanga bei elekezi ya mafuta.

Aliongeza kuwa, mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja umewezesha nchi kudhibiti ubora wa mafuta yanayoingia nchini na pia kuongezeka kwa sehemu za kupokelea mafuta kama  bandari ya Tanga na Mtwara, tofauti na ilivyokuwa awali kwani Bandari ya Dar es Salaam ndiyo ilikuwa ikitumika kwa shughuli hizo.

Kutokana na hilo, alisema kuwa, nchi mbalimbali barani Afrika kama vile Malawi, Zambia na Msumbiji wamekuja kujifunza kuhusu mfumo huo wa uagizaji  mafuta ili waweze kuutumia katika nchi zao.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images