Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Tume Ya Taifa Uchaguzi Yakusudia Kutoa Elimu Kwa Watu Wenye Ulemavu. Kabla ya Uchaguzi mkuu 2020

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020,Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu  inatarajia kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu  nchi nzima namna ya kushiriki kupiga kura .
 
Pia Tume hiyo itaandaa mfumo wa karatasi Nundu kupata   fursa  kwa walemavu kuchagua viongozi wa ngazi zote tofauti  na chaguzi za nyuma ambapo walipata fursa kupitia mfumo huo kuchagua Rais Pekee.
 
Hayo yamesemwa jana April 18 ,bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri wa Kazi,Ajira ,vijana na watu wenye Ulemavu Mhe.Antony Mavunde wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti Maalum ,Suzan Chogisasi Mgonokulima aliyehoji serikali imetoa elimu kwa kiasi gani kwa watu wasioona ili waweze kupata mwongozo mzuri pindi wanapofika kwenye vituo vya kupigia kura.
 
Katika majibu yake,Mhe,Mavunde amesema tume ya taifa ya Taifa ya uchaguzi ina mkakati wa kutoa elimu kwa walemavu na kuongeza kuwa mwaka 2020 walemavu wote wa macho  watapata nafasi ya kuchagua viongozi wa ngazi zote kupitia mfumo wa maalum wa karatasi nundu tofauti ilivyokuwa mwaka 2015 ambapo walipata nafasi ya kuchagua nafasi ya Urais pekee kupitia mfumo huo.

Ikumbukwe kuwa , kifungu cha  61 ,kifungu kidogo cha 3[b] cha sheria ya Taifa ya uchaguzi  sura ya 343  na kifungu cha 62 [h]cha sheria za uchaguzi  serikali za mitaa sura ya 292 kinafafanua kuwa ikiwa mpiga kura ni mlemavu wa macho au mlemavu wa viungo ,mikono au hajui kusoma na kuandika  anaweza kumchagua mtu anayemwamini  ili aweze kumsaidia  kupiga kura.
 
Hivyo mtu huyo anapaswa kuwa msimamizi mkuu,msaidizi wa kituo cha kupigia kura au awe wakala wa chama cha siasa.
 
Vilevile kanuni ya 53 ya kanuni za uchaguzi wa wabunge na Rais mwaka 2015 na kanuni ya 46 ya chaguzi za serikali za mitaa ,madiwani  imeelekeza iwapo mpiga kura ni mlemavu wa macho ataomba karatasi za Nukta nundu ili aweze kupiga kura na msimamizi atawajibika kumpatia .

Mwanzinga: Agizo La Rais Magufuli Kukamilishwa Kituo Cha Mabasi Njombe Mjini Ndani Ya Siku 30 Haliwezi Kufanikiwa

0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa  Njombe Edwirn Mwanzinga amesema kuwa maendeleo ya ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha Njombe mjini yanaashiria kuwa kituo hicho hakita weza kukamilika kwa asilimia 100 ndani ya muda walioagizwa na Rais Magufuli.

Mwanzinga amesema hayo jana ikiwa ni Wiki moja imepita tangu Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John pombe Magufuli kuagiza kituo cha mabasi kinachoendelea kujengwa mkoani Njombe kukamamilika ndani ya siku 30 tangu april 10  mpaka mei 10 mwaka huu.

itakumbukwa kwamba kutokana na ujenzi kutumia muda mrefu bila kukamilika,akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani njombe tarehe 9 mpaka tarehe 11 Rais Magufuli aliagiza wizara ya ujenzi  kwa kushirikiana na halmashauri ya mji wa njombe kukamilisha ujenzi ndani ya siku 30.

Akizungumza na Mpekuzi Blog mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa njombe Edwirn mwanzinga amesema kuwa baadhi ya shuguli zinazoendelea katika kituo hicho cha mabasi haziwezi kuwa zimekamilika ndani ya muda huo wa siku thelathini  kutokana na ukubwa wa kazi huku  hali ya hewa ikiwemo mvua pia ikiathiri kazi hiyo.

"Tuna kazi mbili pale katika kituo cha mabasi kipya tunachoendelea kujenga, ni ujenzi katika eneo la kupaki magari madogo ambapo mkandarasi alikuwa anashindwa kutandika peving bloks kutokana na tope linalotokana na mvua nyingi’’alisema mwenyekiti halmashauri ya mji njombe

Amezitaja baadhi ya kazi ambazo zinaendelea katika kituo hicho kuwa ni pamoja na utoaji wa kifusi,ujenzi wa parking za maeneo ya kukatia tiketi,pamoja na maeneo ya kupumzika abiria ambayo yanahitaji kumiminwa kwa zege na ufungaji wa milango na mageti.

Mwanzinga aliongeza kuwa licha kazi kubwa ya ujenzi kukamilka mpaka kufikia mei 10,2019 lakini  kituo hicho hakitaanza kutumika  ili kuwezesha shughuli zote kukamilika ambapo amesema halmashauri inatarajia kuanza kukitumia kituo hicho rasmi mapema julai ,2019 utakapo anza mwaka wa fedha.

‘’Hata kama mkandarasi akikamalisha kazi zote ndani ya muda tuliopangiwa na mh Rais lakini hatutaweza kuruhusu kituo kuanza kutumika kwa sababu maduka yaliyopo pale yatakuwa bado kuanza kutumika kwa kuwa bado hatuja pata wafanyabiashara katika vibanda ‘’ aliongeza Mwanzinga

Ujenzi wa kituo hicho cha mabasi unatarajia Kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 9 na ulianza kujengwa  tangu mwaka 2013 huku ukijengwa kwa awamu tatu ambapo katika awamu ya mwisho unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 5.7

Wananchi Wa Ihanga’na Mkoani Njombe Walalamika Kukosa Umeme Wa REA

0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Wananchi wa kijiji cha Ihanga’na kata ya Lupembe wilayani Njombe mkoani Njombe wameiomba serikali kupitia shirika la umeme Tanesco  kufikisha huduma ya umeme katika kitongoji A ambacho licha ya kupitiwa na miundombinu lakini hakijaunganishwa na huduma hiyo.

Kitongoji hicho chenye kaya zaidi ya 100 zenye uhitaji wa umeme kimedaiwa kushindwa kuendelea kiuchumi ikilinganishwa na maeneo mengine ya kata hiyo kwa sababu ya kukosa nishati hiyo muhimu kwa maendeleo ya uchumi na biashara.

Wakizungumzia changamoto hiyo wakazi hao wamesema wanashangazwa na kitendo cha miundombinu ya  umeme kupita katika  makazi yao lakini hawanufaiki nayo licha ya viongozi wa serikali akiwemo waziri wa nishati kuhimiza vijiji vinavyopitiwa kuunganishwa na nishati hiyo.

“Tunaumia sana na tunauhitaji na umeme sana hata mheshimiwa Rais kwenye vyombo vya habari  tulimuona umeme huu ni nyumba kwa nyumba hata kama nyumba iwe ya nyasi sasa tunashanga huu umeme umefika tunasikia unaishia huko juu na wanasema huu umeme utaishia kilomita kadhaa tu sisi tunajiuliza ni akina nani mpaka tukose,na sisi tunatamani tuonje huu umeme kwani sisi sio watanzania”walisema baadhi ya wananchi

Wakazi hao ambao wanategemea zaidi kilimo cha chai na parachichi wanadai wanashindwa kuongeza thamani ya mazao yao.

Mpekuzi blog imezungumza na Kaimu meneja wa Tanesco mkoa wa Njombe mhandisi  Yusuph Salimu ambapo amesema kuwa serikali itasambaza umeme katika kaya zote za vijijini kupitia miradi ya REA  mzunguko wa tatu.

“Kwa sasa hivi kijiji cha Ihanang’ana B tayari wananchi watapata umeme mpaka kwenye mashule lakini Ihang’ana A kutokana na umbali tayari tumewaingiza kwenye Rea tatu mzunguko wa pili kwa hiyo ni mategemeo baada ya  mwaka wa bajeti kuanza maana yake utekelezaji wa maeneo hayo pia utafuata”alisema mhandisi Yusuph

Kangi Lugola: Watumishi Kitengo cha Malalamiko tekelezeni wajibu wenu

0
0
NA VERONICA MWAFISI, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa wito kwa watumishi wa Wizara hiyo kitengo cha kushughulikia malalamiko ya wananchi, kutekeleza wajibu wao wa kufuatilia na kuyapatia ufumbuzi wa haraka malalamiko wanayopokea. 

Lugola aliyasema hayo jijini Dodoma juzi katika kikao kazi kilichoshirikisha watumishi wa kitengo hicho.

Aliwataka wafuatilie malalamiko yanayotolewa na wananchi dhidi ya taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). “Hakikisheni malalamiko mnayoletewa, mnayapatia ufumbuzi wa haraka bila kufika ngazi ya juu, tekelezeni wajibu wenu kwa ufanisi ili kujenga imani kwa wananchi (walalamikaji).

“Kama wananchi watajiridhisha kuwa kitengo hiki ni msaada mkubwa kwao, mtakuwa mmejijenga uaminifu na kuifanya Wizara ijitegemee kushughulikia malalamiko,” alisema. Lugola alisisitiza umuhimu wa viongozi wanaoshughulikia malalamiko yanayotolewa na wananchi kuchukuliwa hatua kama itabainika wameshindwa kutimiza wajibu wao.

Alisisitiza umuhimu wa kubadili mfumo wa kushughulikia malalamiko akisema yanapofikishwa katika kitengo hicho yachunguzwe hapo hapo wizarani.
 
“Malalamiko yasirudishwe kwenye taasisi zinazolalamikiwa kama Polisi, Uhamiaji, Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na NIDA…pia walalamikiwa waitwe na kuhojiwa.

“Lengo ni kupata suluhisho la malalamiko yanayotolewa ili kuleta uhuru, malalamiko yajibiwe kwa haraka na uwazikwa njia ya barua ama simu, malalamiko ambayo yataonekana hayana ukweli walalamikaji wapewe taarifa,” alisisitiza Lugola. Aliongeza kuwa, malalamiko mengine hayapaswi kuchukua muda mrefu ili kutatuliwa akitolea mfano malalamiko ambayo aliyapokea kwa wananchi na kuyapatia ufumbuzi wa haraka kwenye ziara alizofanya katika mikoa mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, alitumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa kitengo hicho kwa kuyafuatilia malalamiko yanayotolewa na wananchi pamoja na kuyafanyia kazi kwa haraka. Alisema kitendo cha kupokelewa, kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi ndani ya muda mchache, kitawezekana kama kila mtumishi anayeshughulikia malalamiko atawajibika ipasavyo ili kupunguza mrundikano wa malalamiko yanayotolewa.

Alitoa wito kwa watumishi wa kitengo hicho kwenda maeneo mbalimbali ambayo yana malalamiko ili kupata usahihi wa taarifa, kuzifanyia kazi na kutoa maamuzi. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo na kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji, NIDA na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Mara Wataka Kamati Za Maafa Ngazi Ya Kijiji Hadi Mkoa

0
0
Na. OWM, MUSOMA.
Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Maafa Mkoani Mara wameiomba ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa maafa kuwajengea uwezo wa  kuunda kamati za Usimamizi wa Maafa mkoani humo. Wajumbe hao wamebainisha kuwa wanataka kamati hizo ziundwe kuanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi ya mkoa ili mkoa huo uwe na uwezo wa kujiandaa, kuzuia, kukabili na kurejesha hali kama maafa yatatokea.

Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha  majukumu ya  kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja na  Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji  wilaya au mkoa. Pia kutoa taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika, hivyo kila mkoa hauna budi kuwa na kamati hizi.

Akiongea wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi wa Maafa mjini Musoma, tarehe 18 Aprili, 2019, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, amesema kuwa yeye na wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya mkoa wameamua kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu Maafa, ili wawejengee uwezo utakao wawezesha kuanzisha kamati hizo kuanzia ngazi ya Kijiji, ili  Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya mkoa ambayo  ilianzishwa rasmi kisheria kwa ajili ya  kumshauri Mkuu wa mkoa masuala ya Usimamizi wa maafa iweze kumshauri kwa weledi na  kwa wakati.

“Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu Maafa ikishatujengea uwezo sisi jukumu letu ni moja tu, ni kuhakiksha tunajiimarisha juu ya usimamizi wa maafa kuanzia ngazi ya kijiji ili haya majanga ya Upepo mkali, Ukame, Ajali za vyombo vya usafiri wa majini na nchi kavu, moto, Uharibifu wa mazao unaofanywa na tembo, tuwe na uwezo wa kuyazuia au kupunguza madhara yake  pindi yanapotokea  mkoani hapa na hatutapata vifo, uharibu wa mali na ulemavu wa kudumu kwa wananchi” Amesisitiza Malima.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amefafanua kuwa ili kamati hizo ziwe na ufanisi katika usimamizi wa shughuli za maafa zinapaswa  kuandaa Mkakati wa Kupunguza madhara  ya maafa pamoja na Mpango wa kujiandaa na kukabili maafa.

“Ofisi ya waziri Mkuu tutaendelea kuendesha mafunzo haya  ili kuzijengea uwezo kamati hizi ambazo ni chombo cha kisheria hapa nchini kwa ajili ya kutathimini na kutekeleza masuala ya kitaalam kuhusu usimamizi wa maafa, kuzuia na kupunguza madhara ya majanga ya aina zote katika mkoa lakini mkishapata mafunzo haya hakikisheni mnaweka masuala y amaafakatika mipango yenu ya maendeleo.”

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa shughuli za maafa, yamehudhuriwa na wajumbe wote wa Kamati ya Usimamizi wa maafa wa mkoa pamoja  kwa kuzingatia Kifungu cha 13 cha sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya mwaka 2015,  pamoja na baadhi ya wananchi wa kawaida walioalikwa katika kikao  mafunzo hayo. . 

Rai Yatolewa Kwa Jamii Kutowanyanyapaa Au Kuwabagua Wagonjwa Wa Afya Ya Akili Kwa Imani Za Kishirikina

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Rai imetolewa kwa jamii kutowanyanyapaa au  kuwabagua wagonjwa wa akili kwa imani za kishirikina na badala yake wapewe huduma stahiki za kibinadamu pindi wanapokutwa wakizagaa  na kuzurura mitaani.
 
Rai hiyo imetolewa jana  April 18,2019 ,Bungeni  jijini Dodoma Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dokta. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la mbunge wa Njombe mjini , Mhe.Edward  Frans Mwalongo liliohoji serikali ina mpango gani wa kuwahudumia wagonjwa wa akili wanaozurura mitaani katika mavazi ,matibabu na makazi huku mbunge wa Rombo ,Joseph Selasini akihoji juu ya kufufua vituo vya ushauri nasaha kwa wagonjwa wa akili.

Katika majibu yake , Dokta.Ndugulile amesema  magonjwa ya akili yanatibika na huduma hizo zinatolewa bure hivyo ameiasa jamii kuacha tabia ya kuwanyanyapaa na kuwabagua kwa imani za kishirikina na badala yake wawaibue pindi wanapowaona na kuwapeleka katika vituo vya Afya.

Hata hivyo,Naibu waziri Ndugulile ameezea jinsi wizara ilivyojipanga kutoa huduma za Afya huku akizungumzia juu ya sheria ya Afya ya akili ya mwaka  2008  sehemu ya 3 kifungu cha sheria No.9 Kifungu kidogo cha kwanza hadi cha tatu kinaeleza wazi juu ya jukumu la maafisa polisi,maafisa usalama,maafisa ustawi wa jamii ,viongozi wa dini,maafisa watendaji wa kata na vijiji  jukumu la kumchukua mtu yeyote anayerandaranda  na kumfikisha sehemu ya uchunguzi wa magonjwa ya akili na ikithibitika taratibu za matibabu huanza mara moja .

Dokta Ndugulile anavitaja visababishi vya magonjwa ya  afya ya akili ikiwa ni pamoja na kurithi,matumizi ya dawa za kulevya,  na hali ya maisha ambayo hupelekea msongo wa mawazo ambapo kwa sasa kuna wimbi la ugonjwa wa Sonona.
 
Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro ni miongoni mwa Wilaya zenye magonjwa ya akili kwa wingi hususan ugonjwa wa kifafa huku wizara ya Afya  ikiendelea kufanya utafiti juu ya tatizo hilo na Watafiti wasema mmoja kati ya wagonjwa 10 wa maradhi ya akili ni kutokana na kuvuta bangi.

Dereva wa gari dogo aina ya Nissan March Afariki dunia baada ya gari hilo kugongana na Basi la Mwendokasi Dar

0
0
Dereva wa gari dogo aina ya Nissan March lenye namba za usajili T968 DNZ amefariki dunia baada ya gari hilo kugongana na Basi la Mwendokasi eneo la Magomeni Mapipa leo mchana.
 
Dereva wa gari dogo alikuwa anakata kona kutoka Magomeni kwenda Kariakoo, katika taa za kuongoza magari za Magomeni Mapipa ambazo hazikuwa zinawaka. Ndipo gari dogo likachelewa kupita, na kukutwa katikati ya barabara na Basi la Mwendokasi lililokuwa likielekea Kimara.
 

Baada ya kumpitia, Basi ka Mwendokasi likaichana gari katikati na dereva kufariki pale pale

Waziri Mbarawa Aagiza Mkandarasi wa Maji Akamatwe

0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, ameagiza kukamatwa ndani kwa Mkandarasi wa Kampuni ya ukandarasi PET CO Operation, inayojenga mradi wa chujio la Maswa katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Tryphone Elias, kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo kwa wakati.

Mradi huo unaogharimu kiasi cha Sh bilioni 3.5,  ulitakiwa kujengwa kwa muda wa miezi minane lakini umetimiza miaka minne tangu mwaka 2015 bila ya kukamilika ujezi wake.

Jana usiku Waziri huyo alifanya ziara ya ghafla kukagua ujenzi unavyoendelea kabla ya kutoa maagizo hayo Waziri huyo alisema kuwa mkadarasi huyo amepewa miradi 15 kwenye maeneo mbalimbali nchini, ambayo yote imeshindwa kukamilika kwa wakati.

“Pale Wizarani ulitumia njia za rushwa ukapewa hii miradi, haiwezekani miradi yote 15 mtu mmoja na yote imemshinda, hakuna mradi ambao umekamilisha ujenzi wake, umeendelea kukatili wakazi wa Mji wa Maswa kutumia maji yenye tope,” amesema Waziri Mbarawa.

Baada ya kusema hayo, aliwataka Kamanda wa Polisi Wilaya ya Maswa na Mkuu wa Wilaya kusimamia Mkandarasi huyu akamatwe na kuwekwa ndani kwa saa mbili na muda huo ukiisha aandike maelezo ndani ya siku 11 awe amekamilisha akishindwa kuandika hayo maelezo vizuri asitoke.

Bodi ya Filamu Tanzania Wailaan Kauli ya Mbunge Joseph Musukuma

0
0
Bodi Filamu amesema kauli iliyotolewa na Mbunge Joseph Musukuma inadhalilisha bodi hiyo na wasanii.

Jana Bungeni Musukuma alisema, 'Tasnia ya filamu nchini ipo hoi taabani. Wasanii wa Bongo Movie hawana kitu, wanategemea michango ya misiba, kufungua madanguro na kuwa makuwadi wa wanaume'.

Jeshi la Zimamoto Tanzania latoa tahadhari Sikukuu ya Pasaka

0
0
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania limesema limejipanga vyema kupambana na majanga katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka huku likitoa wito kwa Watanzania kuchukua tahadhari katika matumizi ya vifaa vya kielektroniki.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Aprili 19, 2019 inaeleza kuwa jeshi hilo litakuwa imara kushirikiana na watoa huduma wengine katika mikoa yote ya nchi.

“Tunapoelekea kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Zimamoto na uokoaji katika mikoa yote linawahakikishia wananchi limejipanga kikamilifu kuhakikisha sikukuu hii inasherehekewa bila kuwa na majanga ya moto yanayoweza kuathiri maisha na mali za Watanzania,” inaeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema jeshi lipo imara na litaendelea kuelimisha umma kuzingatia kinga na tahadhari dhidi ya moto ili kuhakikisha maisha na mali za Watanzania zinakuwa salama.

“Tunatoa rai kwa Watanzania kuchukua tahadhari hasa katika matumizi ya vifaa vya kielektroniki kwa sasa vinatumika mpaka ngazi ya familia. Janga la moto huzuka endapo kitapatikana chakula cha moto, joto la kutosha na hewa ya oksijeni,” inasema taarifa hiyo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya April 20

Mgombea Wa CCM Jimbo La Arumeru Mashariki Apita Bila Kupingwa.

0
0
Msimamizi wa uchaguzi Emmanuel Mkongo amemtangaza mgombea Ubunge (CCM) Dkt.John Danielson Pallangyo kuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa kupita bila kupingwa baada ya Wagombea wenzake 10 kukosa sifa.

Mkongo amesema jumla ya wagombea 11 walichukua fomu na kati yao, watatu hawakurudisha na saba fomu zao zimebainika kutokidhi vigezo.

Amesema wapo ambao hawajalipa fedha ya dhamana ya kugombea ubunge  ya Sh50,000, kukosa wadhamini na kurejesha fomu ya kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.

Sugu agoma kusoma hotuba ya upinzani bungeni

0
0
Msemaji wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni katika Wizara ya Habari Joseph Mbilinyi (Sugu) amegoma kuendelea kusoma hotuba yake Bungeni kwa madai kuwa zaidi ya 80% ya maneno yameondolewa katika hotuba yake kuhusu bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Sugu amelazimika kuchukua uamuzi huo leo Alhamisi Aprili 18, bungeni jijini Dodoma, baada ya  Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kumtaka asisome baadhi ya maeneo yaliyoko katika hotuba yake.
 

Kwa mujibu wa Dk. Tulia, hotuba aliyotaka kusoma Sugu ilikuwa na mambo yaliyoondolewa baada ya kuonekana yanakiuka kanuni za kudumu za Bunge.
 

Kabla ya Sugu kuchukua uamuzi huo, alianza kusoma hotuba kupitia katika kitabu alichokuwa nacho lakini baada ya muda mfupi tangu alipoanza kusoma, Dk Tulia alimtaka asiisome bali asome kupitia kitabu kipya cha hotuba yake ambacho wabunge wote walikuwa wamegawiwa.

 Kutokana na maelekezo hayo,Sugu alisema hawezi kufanya hivyo kwani kitabu kipya hakina maoni ya kambi yake na hivyo kulazimika kuondoka mbele ya Bunge na kurudi katika kiti chake.

Baada ya kusema hayo Naibu Spika aliruhusu mjadala wa bajeti hiyo uanze huku akisema hotuba ya Sugu isiingizwe katika kumbukumbu za Bunge kwa kuwa Sugu hakusema kama anataka iingizwe katika kumbukumbu hiyo.

Marekani yamuunga mkono mbabe wa kivita Libya

0
0
Rais Donald Trump amezungumza kwa simu na mbabe wa kivita wa Libya, Jenerali Khalifa Haftar, akimuahidi kumuunga mkono, licha ya jitihada za Umoja wa Mataifa kusitisha mapigano ya kuwania udhibiti wa Tripoli.

Katika mazungumzo hayo ya jana, Trump na Haftar walijadiliana hatua za kupambana na ugaidi na haja ya kufikia amani na utangamano nchini Libya, kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani.

Taarifa ya Ikulu hiyo inasema kwamba Trump alilitambuwa jukumu muhimu la Jenerali Haftar katika kupambana na ugaidi na kulinda rasilimali ya mafuta ya Libya.

Marekani inaungana sasa na Misri, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu katika kumuunga mkono mbabe huyo wa kivita, ambaye mapambano yake ya kutwaa madaraka yanatishia kuirejesha tena Libya kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Ikulu ya Marekani haikusema kwa nini ilichelewa kutoa taarifa ya mazungumzo hayo ya simu kati ya Trump na Haftar, lakini wachunguzi wanasema uamuzi wa Trump kumsifia Haftar ni ushahidi wa kwa nini jenerali huyo muasi amekuwa na dhamira ya kuutwaa mji mkuu, Tripoli, unaodhibitiwa na serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj, anayetambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Kamanda huyo wa kijeshi anaunga mkono serikali hasimu ya Libya yenye makaazi yake mashariki mwa nchi hiyo na amekataa kuyatambua mamlaka ya serikali iliyo mjini Tripoli.

Siku ya Alhamis (Aprili 18), Urusi na Marekani zilipinga rasimu ya azimio la Uingereza ambalo lilikuwa likiungwa mkono na Ufaransa na Ujerumani kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka usitishwaji mapigano nchini Libya.

Urusi ilisisitiza kutokuwepo ukosowaji wowote dhidi ya Haftar kwenye rasimu ya azimio hilo, huku Marekani ikitaka ipewe muda zaid kufikiria hali ilivyo.

-DW

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Ufugaji wa nguruwe : Gharama na Faida Zake

0
0
 Utangulizi
Nguruwe ni mnyama amabaye hutumika kama chakula / mboga na pia ni zao la biashara kwa mfugaji, mjasirimali na mfanyabiashara.
 
NGURUWE HUTEGEMEA SANA MAMBO YAFATAYO
1 . Banda imara na rafiki kwake
2. Usafi ni muhimu sana katika banda la Nguruwe
3 Mchaganyo bora wa chakula
4. Tiba bora na kinga
5. Maji na Lishe ( access ya vyakula Muhimu kwake )
 
CHANGAMOTO
KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE KUNACHAGAMOTO ZAKE LAKINI ZAWEZA KUTATULIWA KWA KUFATA MAMBO KADHAA.
Katika ufugaji wa nguruwe kunachagamoto ya vifo vya nguruwe wachanga ambao hupunguza faida ya biashara ya nguruwe kwa kupunguza idadi ya nguruwe wazima wa kuuzwa lakini utunzaji mzuri wa nguruwe wachanga huepusha vifo vinavyotokana na shida kama:
 
Matatizo ya kupumua
Ni kifo kinachosababishwa na mama anapomlalia nguruwe mchanga.chagamoto hii inaweza kutatuliwa kwa kuwatenga au kuwa na mabanda makubwa ya kulelea watoto.
 
Baridi
Nguruwe wachanga huathiriwa na baridi haswa katika majuma mawili au matatu ya mwanzo. Hii ni kwa kuwa wana kiwango kidogo cha utando wa mafuta wa kuwakinga.
 
Unashuriwa kuwaweka katika hali ya joto, wape matandiko na utumie vipasha joto kama vile kuwasha globu za joto kama utakuwa umewaweka kwenye mabanda ya kuta au nyumba yenye sakafu baridi.
 
Namna bora utunzaji wa nguruwe wachanga
Nguruwe moja wa kike ana uwezo wa kuzaa watoto 12. Namna ifuatayo itasaidia kupunguza idadi ya vifo vya nguruwe wachanga:
1.Pale nguruwe awapo na kidonda nyunyizia dawa ya ayodini 5% kwenye kovu ili kuzuia kuambukizwa kwa magonjwa.
2.Wawekee matandiko (nyasi kavu au maganda ya miti) mahali pa mapumziko ili wapate joto au utumie globu za joto.
3Wadunge sindano ya madini ya chuma (iron) siku ya tatu baada ya kuzaliwa ili kuzuia upungufu wa damu.
3. Yalainishe meno ya vichaga kabla ya masaa 24 ili kuzuia uharibifu wa matiti wakati wanaponyonya.
4. Watie vibandiko au utoboe masikio ili uwatambue na uhifadhi rekodi zao kama kuna umuhimu kama vile wafanyavyo wafugaji wa ng’ombe.
5. Wapime uzani wanapozaliwa na uhifadhi rekodi hiyo itakusaidia kujua ukuaji wao na maendeleo yao
6. Wahasi wale wa kiume juma la tatu, wale ambao hawafai katika kuendeleza kizazi kwa kutumia mtindo wazi (open method) kama unaona inafaa.
7. Wapatie dawa ya kuzuia minyoo pia zipo dawa za asili kama unga wa mkaa na majivu pia zipo za kitaalamu, wasiliana na wataalamu wa mifugo
8.Waachishe kunyonya katika juma la nane au wafikapo kilo 14 hadi 20 hii itasaidia kujitegemea na kukua kwa haraka.
 
Nguruwe Walioachishwa Kunyonya
1.Walioachishwa kunyonya wawekwe makundi ya 10 hadi 12 kulingana na uzito au ukubwa wao kwenye eneo ambalo watajitosheleza.
2.Watenganishe wakubwa kwa wadogo ili kuzuia kupigana.
3.Wakati wa kuwaachisha kunyonya mwondoe mama yao kutoka kwa watoto ili kupunguza usumbufu.
4Watoto wa nguruwe wa mama tofauti wasiwekwe pamoja maana hii husababisha mapigano kati yao na
5.Unapowachanganya watoto wa mama tofauti wapake mafuta ya gari yaliyotumika kwenye ngozi yao au mafuta ya kula ili kuiondoa harufu ya kutambulika ili wasipigane
 
FAIDA YA UFUGAJI WA NGURUWE
Faida kuu ya nguruwe ni zao la chakula lakini pia ni zao la kukuongezea kipato ukiwa kama mjasirimali / mfanyabiashara.
Lengo langu nikueleza namna unavyoweza kufuga na kutupa faida, Steps zifatazo ni muhimu kuzigatia.
 
JIPE MTAJI WA MILLION 4 / 3.5 KWA NGURUWE 50
UANDAAJI WA BADA WEKA MAKADILIO YA LAKI TANO (800,000/=) .
Hapo nazugumzia banda lenye heru U yenye mstatili ikiwa na kitako kirefu
Eneo lenye ukubwa wa mita 50 kwa 50 litafaa zaidi ili kuhakikisha usalama wa nguruwe wako na ukuaji bora.
1. Tafuta mabati used kwa bei ya 5000 mfano mabati 20 ya futi 10 /10 = 100,000/=
2. Tafuta mabazi ya futi 10 kwa 2000 kila moja utapata mabazi pic 100 = 200,000/=
3. Tafuta miti ya nguzo na kechi ya 1000 na 2000 miti ya 1000*70 na 2000*3 = 120,000/=
4. Tafuta chagalawe / moramu trip 10*3000 =30000/=
5. Cement mifuko kwa ajiri ya sakafu na mashimo ya kulishia 5 *18000 = 90,000/=
6. Misumari ya aina 4, nch 6 kg5,nch 3 kg5 nch 5 kg10 na nch4 kg10, Bawaba na komeo =100,000/=
7. Malipo ya fundi 75000 fundi uashi na 75000 fundi seremala =150,000
JUMLA HAPO INAKUWA 790,000/= MAKADILIO INAKUWA 800,000/=
 
UNUNUZI WA NGURUWE WA KUANZIA .
Nguruwe wadogo wadogo ni vinzuri zaidi kuanza nao kwa sababu watakuzalia watoto wengi na kwa muda mrefu . Chukua mfano MILLION 2.5 . Nguruwe wadogo wa dogo wanauzwa 50000 au 40000 inategemeana na mahala na maelewano . Milioni 2.5 inakupa vitoto 50 au 55 . Hivyo unawexa kuwa na vitoto jike 50 na vidume 5. baadaye ukaongeza madume matano ya kuazima au kukondi kwa ajiri ya kupandishia
 
MAANDALIZI YA CHAKULA
Mchaganyiko wa chakula cha nguruwe na gharama zake tunaweza ukadilia kujitosheleza kwa laki tatu kwa mwenzi mmoja kwa nguruwe hao 50, kwa 300,000/= , ambapo itajumuisha tiba / kinga, lishe, vyakula vya nguruwe vinaweza kuwa pumba ya mpunga ile laini,pumba ya mahindi, mashundu, mabaki ya magada ya vianzi amba mabaki ya chakula yaliyosalama
 
MALIPO YA MSIMAMIZI NA ENEO LA KUWEKEZA
Katika kipengele hiki makadilio ya juu ama ya chini kwa msimamizi wa kazi yako waweza mlipa 100,000/= ama chini yake pia kwa mwenye eneo huwa nimaelewano tu aunaweza pata kwa fair au kukakodi kwa laki tatu, 300,000/= kwa mika miwili.
 
HIVYO JUMLA YOTE YA GHARAMA ZA UAZISHAJI UWEKEZAJI WA NGURUWE 50 ZITAKUGHARIMU MILLION 4 AMA MILLION 3.5 KWA MAANA KUWA HAPO JUU NIMETUMIA MAKADILIO YA JUU NA UKIINGIA KWENYE UHALISIA KAMA MJASIRIMALI LAZIMA IPUNGUE NA KUFIKIA 3.5

KIPATO AU FAIDA YA UFUGAJI NGURUWE
Nguruwe wanafaida ya haraka na nimradi wa uhakika kabisa, ukipitiia mchanganuo hapo juu wa nguruwe 50 utatupa faida kama ifatavyo
 
Nguruwe huzaa Mara mbili kwa mwaka na huzaa watoto zaidi ya watanoyaani huzaa watoto 12 ama nane .
Basi chukua nguruwe 50 * vitoto 5 yaani ufanye kuwa nguruwe wako 50 wakupatie vitoto vitano vya uhakika
Nguruwe 50*5 = 250 ukijumlisha na wale 50 wa mtaji umakuwa nao 300 . Chukua zao la nguruwe la 250 na uza kwa 200000 kwa kila nguruwe yaan bei ya kawaida kabisa. Utapata Million 50.

Hivyo zao la kwanza ndani ya robo tatu ya mwaka inakutegenezea million 50 pia na mienzi sita ijayo inakupa tena 50 na zaidi ili kukamilisha uzao wa pili hii inkupa uhakika wa kutegeneza million 100 za uakakika ndani ya mwaka mmoja na nusu ama miaka miwili ukijipa timeframe work lakini kumbuka hapo tumefanya kwa hesabu ya uzao wa chini kabisa ambapo tumeangalia na hasara ya vifo kama vifo visipotokea na uzao ukawa mkubwa utakuwa na uhakika wa kutegeneza million 150 kwa miaka miwili.

Kwenye hesabu ya kuwale unaweza kuwaza sana kuwa itaongezeka na kukughalimu sana jibu ni hapana mpka kufikia kuuza hawatokugharimu zaidi ya million 7 je million 7 kwenye million 150 ni kitu kisicho nafaida ?
 
NB . jambo lolote linahitaji umakini naa dhamira ya dhati pia kushirikisha wataalamu na wenye uzoefu ili kufikia leng Ewe ndugu kila kitu kinawezekana UTAYARI WAKO / UTHUBUTU WAKO, UAMINIFU .NA MAAMZI YAKO.
 

Ufafanuzi Kuhusu Habari Inayohusu ujenzi wa Stendi ya Mabasi Njombe

0
0
Mpendwa Msomaji wetu, Jana Ijumaa April 19,2019 tulichapisha Habari  inayohusu  ujenzi wa Stendi ya Mabasi Njombe iliyokuwa na kichwa cha habari; "Mwanzinga:  Agizo La Rais Magufuli Kukamilishwa Kituo Cha Mabasi Njombe Mjini Ndani Ya Siku 30 Haliwezi Kufanikiwa."

Habari  hiyo ilinukuu mahojiano kati ya mwandishi wetu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa  Njombe Ndg. Edwin Mwanzinga  kuhusu  maendeleo ya ujenzi wa stendi mpya ya Njombe na namna walivyojipanga kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dr. John pombe Magufuli  ambaye  April 10, 2019 aliagiza  ujenzi wa kituo hicho  ukamilike ndani ya siku 30.

Hata hivyo, katika mahojiano hayo, pamoja na  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa  Njombe Ndg. Edwin Mwanzinga kuelezea maendeleo ya mradi huo, lakini alinukuliwa vibaya kwamba ujenzi huo unaweza usikamilike kwa  asilimia 100 ndani ya muda walioagizwa na Rais Magufuli.

Tunaomba radhi  kwa makosa hayo ya kiufundi yaliyojitokeza.

Uhalisia wake ni kwamba, Ndg. Edwin Mwanzinga  alifafanua kuwa stendi hiyo itakamilika kwa mujibu wa tarehe ya mkataba ambayo ni 30/04/2019 na shughuli zitakazosalia za ukamilishaji zitafanyika ndani ya siku zilizoongezwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kama alivyoagiza kwenye ziara yake ya kikazi tarehe 10 Aprili akiwa Mkoani Njombe ambapo ni kufikia tarehe 10, Mei 2019.

Ujenzi wa kituo hicho cha mabasi unaotarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 9  ulianza kujengwa  tangu mwaka 2013.

Naibu Waziri Kanyasu Atoa Onyo Kwa Wahifadhi Nchini Kuhusu Wananchi

0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amezionya na kuzitaka Taasisi za Uhifadhi kuacha tabia ya kuwabughudhi wananchi wanaoishi katika vijiji na vitongoji 366 vilivyokutwa ndani ya Hifadhi katika maeneo mbalimbali nchini mpaka hapo maamuzi ya Kamati ya Mawaziri saba iliyoundwa kushughulikia suala hilo itakapokamilisha kazi iliyopewa na kuwasilisha ripoti  kwa Mhe. Rais.

Hatua hiyo ni kufuatia  malalamiko kutoka  kwa baadhi ya  wananchi wakiwemo wakulima na wafugaji  wanaoishi katika vijiji na vitongoji hivyo kudai kuwa wamekuwa wakisumbuliwa  na mifugo yao kukamatwa mara mara kwa madai ya kukutwa imeingia ndani ya Hifadhi.

 Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko ambacho ni miongoni mwa vijiji vilivyomo ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Mhe. Kanyasu amezitaka taasisi hizo kufuata na kuzingatia  maelekezo yaliyotolewa na Serikali kuhusu wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.

 Aidha, Mhe. Kanyasu ametumia fursa hiyo kuwaonya wananchi  ambao wamekuwa wakivamia maeneo mapya ya Hifadhi  kwa kisingizio cha kauli aliyoitoa Mhe. Rais kuacha mara moja na kwamba yeyote  atakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

" Wananchi ninao walenga ni wale tu ambao walikuwa wakiishi Hifadhini  kabla ya kauli ya Rais aliyoitoa mwanzoni mwa mwaka huu" Alisisitiza.

Hata hivyo, Mhe Kanyasu amebainisha kuwa Kamati ya Mawaziri saba iliyoundwa na kuzunguka nchi nchi nzima imebaini kuwa kuna zaidi ya vijiji 820 ambavyo vimo ndani ya Hifadhi mbali ya vile 365 vilivyobainishwa awali na kuwasihi wananchi  wasiendelee kuvamia maeneo mengine.

Mhe.Kanyasu  ameowanya baadhi ya askari wa wanyamapori  wanaoomba rushwa Kutoka kwa wafugaji pindi wanapokamata  mifugo yao ili waweze kuiachia waache mara moja tabia hiyo akisisitiza kwamba  askari yeyote atakayethibitika atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria za utumishi wa Umma.

Mkuu wa wilaya ya Kondoa, Mhe. Sezaria Makota  amewataka wananchi hao kuendelea kuwa walinzi wa maeneo hayo huku wakisubili hatma ya taarifa ya kamati ya Mawaziri saba itakayotolewa hivi karibuni.

" Baada ya taarifa hiyo  mtajua hatma yenu na kama hapa mtabaki au mtahamishwa na kama mtahamishwa tutajua tutawapeleka eneo gani kwa ajili ya malisho na kilimo." Alisema.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi, Mwenyekiti wa kijiji cha Kisondoko, Ismail Said amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa baadhi ya askari wa wanyamapori wamekuwa wakikamata mifugo yao na kuomba rushwa na pale makubaliano yanaposhindikana huondoka na mifugo yao.

Amesisitiza kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikichochea chuki baina ya wananchi na askari hao jambo linalorudisha nyuma jitihada za Uhifadhi nchini.

Mkutano wa Urusi Vladimir Putin, Kim Jong Un waikera Marekani

0
0
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anatarajiwa kutembelea nchini Urusi mwezi huu ambako atakuwa na mazungumzo na Rais Vladimir Putin, huku hatua hiyo ikitajwa kuwa imewaudhi viongozi wa Serikali ya Marekani, ambao wako kwenye mnyukano mkubwa na Korea Kaskazini kutokana na mikutano yao kushindwa kupata suluhisho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Kremlin ya Urusi kwenda kwa vyombo vya habari juzi, mkutano kati ya Putin na Kim haujapangiwa tarehe rasmi, lakini unatarajiwa kuwakutanisha viongozi hao.

Mkutano huo umepangwa muda mfupi baada ya Korea Kaskazini kutoa mapendekezo kwa Serikali ya Marekani kumwondoa waziri wao wa mambo ya nje, Mike Pompeo kwenye Kamati ya majadiliano kati ya nchi hizo mbili.

Pia, Korea Kaskazini imeeleza kuwa imefanikiwa kufanya majaribio ya silaha mpya za kivita za kinyuklia. Hatua hiyo imetajwa kuwa pigo dhidi ya kiongozi wa Kamati ya Majadiliano ya Marekani, Pompeo.

Mkutano wa Kim na Putin utakuwa wa kwanza  kuwakutanisha viongozi hao, ambapo utafanyika mjini Moscow nchini Urusi. Ikulu ya Kremlin imesema imemwalika Kim Jong Un kwenye mkutano huo, ambao utafanyika katika kipindi cha pili cha mwezi Aprili, lakini hakukuwa na taarifa nyingine zaidi.

Maofisa wawili wa Serikali ya Marekani, mshauri wa rais, Fiona Hill na Balozi maalumu Stephen Biegun nao walikuwa mjini Moscow kufanya mazungumzo na maofisa wa serikali ya Urusi.

Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa na uhusiano wa mashaka wa kidiplomasia tangu kuvunjika kwa mkutano wa Kim na Trump mwanzoni mwa mwaka huu. Korea Kaskazini imemtaja Mike Pompeo kuwa kiongozi anayetakiwa kuondolewa kwenye wadhifa wake.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images