Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Msukuma Ataka Adhabu Mbadala Kwa Wafungwa Wenye Makosa Madogomadogo

$
0
0
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) ameitaka Wizara ya Katiba na Sheria kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazoonekana hazina manufaa kwa mazingira ya sasa.

Musukuma ametoa kauli hiyo katika vikao vya Bunge kwenye mjadala wa Wizara ya Katiba na Sheria ambapo kupitia Waziri wa Katiba na Sheria, Agustino Mahiga aliwasilisha makadirio ya bajeti yake.

"Niseme tu kiukweli ni vizuri mkaangalia mkarekebisha sheria, hasa kwenye makosa madogodogo ambayo yamepelekea magereza mengi kujaa mahabusu ambayo kwa kweli mengine yanastahili makofi tu mtu akaenda nyumbani", amesema.

Musukuma ameongeza kuwa, "nashauri sana hizi sheria zilizotungwa tukiwa milioni 20, leo tuko milioni 55 mtu anawekwa wiki 2 kwa kesi ya kuiba kuku, ni vitu ambavyo tufikirie adhabu ili kupunguza mrundikano wa mahabusu kule ndani."

"Nilisoma kwenye kitabu cha Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusiana na uteuzi wa Majaji, inampa mamlaka Rais kuteua na anakuwa jopo la kumshauri ninawataka tu wenzangu wamuachie Rais akafanya majukumu yake." amemalizia Musukuma.

Askari Polisi waenda kuangalia mpira na kuacha kituo bila ulinzi.....Wezi Wavamia na Kuiba Bunduki 3 na Risasi 20

$
0
0
Wezi wamevunja kituo cha polisi cha Kamorwon kilichopo kaunti ya Nandi nchini Kenya, na kuiba baadhi ya silaha zilikuwepo katika kituo hicho.

Ripoti za polisi zinaonesha kuwa, watu wasiojulikana waliingia katika kituo hicho siku ya Jumanne, Aprili 16, wakati maafisa wa polisi waliokuwa wameshika doria waliondoka na kwenda kutazama mechi  eneo  jirani na kituo hicho

Waliporejea  baadaye usiku, maafisa hao walipigwa na butwa baada ya kugundua kuwa chumba kilichotumika kuhifadhi silaha hizo kimevunjwa huku bunduki tatu na risasi 20 zikiwa hazionekani. Silaha hizo zilikuwa zimefungwa ndani ya gazeti.

"Maafisa wote wa polisi walikuwa wameondoka kutazama mechi ya UEFA katika kituo cha kibiashara  na waliporudi  usiku, waligundua kuwa ofisi iliyotumika kuhifadhi silaha imevunjwa. Isitoshe bunduki 3 na risasi 20 zilikuwa zimeibwa," ripoti ya polisi ilisema.

Hata hivyo, magazeti mengine yaliyokuwa na risasi 17 na 20 yalikuwa hayajaguswa kulinga na ripoti zaidi za polisi wa kituo hicho.

Mamlaka ya usalama ikiongozwa na kamanda wa polisi wa kituo cha polisi cha Nandi kusini walizuru eneo la kisa hicho na kuwahamasisha maafisa wa polisi kuchukua hatua haraka iwezekanavyo.

Kwa sasa msako dhidi ya wahalifu hao unafanywa ili kuzuia uhalifu ambao huenda ukatekelezwa kwa kutumia silaha hizo.

ATAPE Kuwekeza Kwenye Miradi Ya Maji, Ujenzi Wa Hosteli Simiyu

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE), kinakusudia kuwekeza katika ujenzi wa mradi wa maji kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi  na ujenzi wa hosteli ili kutoa huduma za malazi katika Mkoa wa Simiyu.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Freddie Manento,  Aprili 17, 2019 wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi, ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho kwa takribani siku saba ambao umeanza Aprili 16 na utahitimishwa Aprili 21, 2019.

Manento amesema  ATAPE imedhamiria kuwekeza kwenye miradi itakayokuwa na tija kwa Watanzania wote kwa ujumla huku akieleza kuwa timu ya wataalam wa uwekezaji wa chama hicho inaendelea kufanya utafiti, ili kubaini eneo litakalofaa kuchimba kisima cha maji na kujenga hosteli mkoani Simiyu.

“Tumedhamiria kuacha alama katika Mkoa wa Simiyu kupitia mkutano wetu wa 20 wa ATAPE, tumepewa fursa ya kiwanja kwa ajili ya kujenga hosteli katika kukabiliana na changamoto ya malazi, lakini pia wataalam wetu wanaendelea na utafiti kubaini mahali tutakapochimba kisima kwa ajili ya huduma ya maji kwa Wanasimiyu” alisema Manento

Pamoja na miradi hiyo inayotarajiwa kutekelezwa mkoani Simiyu, Manento amesema ATAPE imewekeza katika kilimo kwenye mashamba ya miti, miwa, mikorosho, miti ya maparachichi ambayo kwa ujumla yana ukubwa wa ekari 10,000 na ekari zaidi 3500 ambazo zinatarajiwa kufanyiwa uwekezaji mwingine.

Amesema  hadi sasa ni takribani shilingi bilioni 1.039 imewekezwa katika miradi hiyo ambayo pia imechangia kutoa ajira za kudumu na za msimu kwa Watanzania walio katika maeneo yenye miradi hiyo, huku akibainisha kuwa katika baadhi ya maeneo hayo ATAPE imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii husika.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa ATAPE ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu hususani Bariadi kutumia mkutano huo kama fursa kiuchumi kupitia biashara ya bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo usafiri wa kuwatoa na kuwapeleka wajumbe katika eneo la mkutano

Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu wamesema Mkutano wa ATAPE umekuwa fursa kwao kwa kuwa utawasaidia kujiingizia kipato na kupata ujuzi mpya kupitia huduma na bidhaa zitakazouzwa kwenye mkutano huo.

“ Binafsi ninashukuru uwepo wa mkutano huu, mimi kama mjasiriamali nimepata pesa, nimepata ujuzi mpya kutoka kwa wenzetu waliotoka nje ya Simiyu, hivyo ninaendelea kuwaomba viongozi wetu waendelee kutuletea matukio kama haya ili tupate pesa zaidi” alisema Bw. John Bubinza mjasiriamali kutoka Bariadi.

Nao wajasirimali wanaoshiriki katika mkutano huo kutoka nje ya mkoa wa Simiyu wametoa wito kwa Wananchi mkoani Simiyu kufika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kusekwa Memorial kujifunza na kujionea kazi mbalimbali za ujasirimali ili waweze kupata ujuzi na maarifa mapya ya kufanya kazi za ujasiriamali kwa ufanisi na kununua bidhaa mbalimbali.

“ Binafsi nawakaribisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu kufika katika viwanja hivi waje wajionee, wakifika hapa watapata bidhaa kwa bei za jumla na rejareja, laikini pia nawasisitiza wanawake wainuke waje waone maana ujasiriamali unatuinua sana wanawake” alisema Mjasiriamali Esther Jichogo kutoka Jijini Dar es salaam.

Wanachama zaidi ya 1500 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE) wanaendelea na mkutano wao wa 20 mkoani Simiyu, ukiwa na Kauli mbiu “KUSONGA MBELE NA MUNGU” ambao utachukua takribani siku saba kuanzia tarehe  16/04/2019 hadi 21/04/2019.

MWISHO

Tundu Lissu Azungumzia Maendeleo Ya Afya Yake na Muda Atakaorudi Tanzania

$
0
0
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki amesema muda wowote atareja nchini kutokea matibabuni nchini Ubelgiji.

Lissu  amesema kuwa tayari  madaktari wake wamemueleza ni siku gani atakuwa tayari kurejea nchini.

Hata hivyo Lissu ameeleza kuwa wanahitaji kushauriana na wadau mbali mbali kuhusu tarehe halisi na namna bora zaidi ya kurudi kwake nyumbani.

"Tarehe 2 ya mwezi huu nilikutana na madaktari wangu kwa appointment ya kwanza tangu operesheni za tarehe 20 Februari.

"Taarifa yao ni kwamba mfupa wote wa mguu wa kulia umepona vizuri. Sehemu iliyowekewa 'kiraka' cha mfupa na kupigwa 'ribiti' ya chuma juu kidogo ya goti; na sehemu ya kwenye paja iliyotakiwa kuota mfupa mpya, zote ziko vizuri.

"Sasa kazi kubwa iliyobaki ni kukunja goti na kujifunza kutembea tena. Naomba mniamini nikisema kujifunza kutembea tena, baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa kulala kitandani, ni kazi ngumu sana!!!!

"Nafikiri sina tofauti sana na mtoto mdogo anayejifunza kupiga hatua zake za kwanza. Lakini pole pole nitafika inshaallah.

"Tarehe 14 ya mwezi ujao nitapimwa urefu wa miguu ili nitengenezewe kiatu au soli maalum kwa ajili ya mguu wa kulia.

"Kwa sababu ya majeraha makubwa niliyopata, mguu huo ni mfupi kwa sentimita kadhaa. Bila kiatu au soli maalum nitakuwa 'langara' sana na madaktari wamesema hiyo sio sawa sawa.

"Kwa kumalizia, sasa nina tarehe ambayo madaktari wangu wamesema nitakuwa 'fiti' kurudi nyumbani.

"Msiniambie niiseme kwa wakati huu. Tunahitaji kushauriana na wadau mbali mbali kuhusu tarehe halisi na namna bora zaidi ya kurudi kwangu nyumbani.

"Tukumbuke tu kwamba waliotaka kuniua mchana kweupe katikati ya mji wa Dodoma bado wanaitwa 'watu wasiojulikana.' Itabidi tupate 'security guarantees' kutoka kwa wahusika,  kwamba nitakuwa salama nikirudi." Amesema Tundu Lissu katika waraka wake aliouweka mtandaoni

Jeshi Lililompindua Rais Omar Al- Bashir Latoa Maagizo Kwa Benki Kuu Ya Sudan

$
0
0
Baraza la Kijeshi linaloongoza serikali ya mpito nchini Sudan limeiamuru Benki Kuu ya nchi hiyo, kuchunguza shughuli zote za uhamishaji wa fedha zilizofanyika kuanzia Aprili 1, na kushikilia fedha zote zinazotiliwa shaka. Hayo yameripotiwa leo na shirika la habari la Sudan, SUNA. 

Baraza hilo pia limeamuru kusimamishwa kwa shughuli ya kubadilishwa umiliki wa hisa, hadi itakapotangazwa vinginevyo. 

Benki Kuu vile vile imeamuliwa kuripoti kwa mamlaka husika, juu ya kufanyika mchakato wowote wa uhamishaji mkubwa, au unaotiliwa shaka ya hisa pamoja na umiliki wa makampuni.

Bibi Anayetuhumiwa Kuua Mwanafunzi Auawa na Wanachi Wenye Hasira

$
0
0
Tukio lisilo la kawaida limetokea Wilayani Muleba Kata ya Kishanda Mkoani Kagera ambapo mtoto mwenye miaka saba Ismail Hamisi ambaye alipotea tangu April 5 akitokea shule na jana usiku amekutwa kwenye shamba la bibi mmoja akiwa amefukiwa kwenye shimo tayari ameshapoteza maisha.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi wa maeneo hayo kukata migomba ya bibi huyo na kumuua kwa kumchomo moto akiwa ndani ya nyumba yake

Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mtoto huyo alitoweka April 5 mwaka huu alipoondoka nyumbani kwenda shule, lakini hakuonekana tena hadi  mwili wake ulipogundulika umezikwa katika shamba la bibi huyo, akiwa na sare zake za shule.

Aidha Kamanda Revocatus amesema Taratibu za kiuchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zinaendelea kufanyika.

Sugu agoma kusoma hotuba ya upinzani bungeni

$
0
0
Msemaji wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni katika Wizara ya Habari Joseph Mbilinyi (Sugu) amegoma kuendelea kusoma hotuba yake Bungeni kwa madai kuwa zaidi ya 80% ya maneno yameondolewa katika hotuba yake kuhusu bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Sugu amelazimika kuchukua uamuzi huo leo Alhamisi Aprili 18, bungeni jijini Dodoma, baada ya  Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kumtaka asisome baadhi ya maeneo yaliyoko katika hotuba yake.
 

Kwa mujibu wa Dk. Tulia, hotuba aliyotaka kusoma Sugu ilikuwa na mambo yaliyoondolewa baada ya kuonekana yanakiuka kanuni za kudumu za Bunge.
 

Kabla ya Sugu kuchukua uamuzi huo, alianza kusoma hotuba kupitia katika kitabu alichokuwa nacho lakini baada ya muda mfupi tangu alipoanza kusoma, Dk Tulia alimtaka asiisome bali asome kupitia kitabu kipya cha hotuba yake ambacho wabunge wote walikuwa wamegawiwa.

 Kutokana na maelekezo hayo,Sugu alisema hawezi kufanya hivyo kwani kitabu kipya hakina maoni ya kambi yake na hivyo kulazimika kuondoka mbele ya Bunge na kurudi katika kiti chake.

Baada ya kusema hayo Naibu Spika aliruhusu mjadala wa bajeti hiyo uanze huku akisema hotuba ya Sugu isiingizwe katika kumbukumbu za Bunge kwa kuwa Sugu hakusema kama anataka iingizwe katika kumbukumbu hiyo.

Kampuni zilizoingia mikataba na Marehemu Steven Kanumba Pamoja na Mzee Majuto Zaanza Kuzilipa Familia zao

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Wasimamizi wa mirathi ya wasanii Steven Kanumba na King Majuto wamelipwa Tsh. Milioni 45 baada ya serikali kupitia upya mikataba yao.

Ameyasema hayo leo Bungeni akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo ameeleza hayo ni mafanikio ya kama iliyoundwa na Serikali kufanya kazi ya kupitia upya mikataba hiyo.

Amesema kampuni ya Steps Entertainment imeshamkabidhi Mama wa  muigizaji marehemu, Steven Kanumba malipo ya ziada ya Sh milioni 15 baada ya kugundulika kuwa iliingia mkataba mbovu na msanii huyo.

Pia kampuni hiyo imeahidi kushirikiana na mama yake Marehemu Kanumba, kuandaa filamu ya maisha ya mwanawe huyo.


 Waziri Mwakyembe amesema Pamoja na malipo hayo Kampuni ya Pan African Enterprises Ltd na Ivori Iringa, zimeshaingiza kwenye akaunti maalum Sh milioni 30 kwa kazi alizotekeleza muigizaji marehemu Amri Athuman maarufu King Majuto.

Pia amesema  Kampuni ya Azam SSB imeandaa malipo ya ziada ya sh milioni 20 na Kampuni ya Tanfoam ya Arusha imeandaa Sh milioni 15 yatakayowasilishwa kwa msimamizi wa mirathi ya marehemu King Majuto

Kupiga Punyeto Kwa Muda Mrefu Husababisha Maumbile ya Kiume Kusinyaa na Kupungukiwa Nguvu za Kiume

$
0
0
Wanaume  wengi  waliofanya  mchezo wa  kujichua  kwa  muda  mrefu hupatwa  na  madhara  ya kuwa  na  kusinyaa  na  kudumaa  kwa  maumbile  yao  ya  kiume  ambayo  huenda  pamoja  na  tatizo  a  Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.

Tendo  la  kujichua  kwa  mwanaume  linapofanyika  kwa  kipindi  kirefu huathiri na  kuharibu mishipa  na  misuli  ya uume  na  hivyo  kusababisha  kujengeka  kwa mafuta na tishu zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri.  Jambo  hili  husababisha  makuu mawili; 1. Huzuia  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuongezeka jambo  linalotajwa  na  wanasayansi  kama jambo  muhimu  sana  katika  kukua  kwa  uume. 2. Huzuika  kutirika  kwa  damu  kuingia  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili  huathiri  sana  ukuaji  wa  maumbile ya kiume  kwa  sababu  yanapo tokea huathiri uzalishaji  wa  homoni  muhimu  zinazo  husika  na  ukuaji  wa  misuli  ya  uume na matokeo  yake husababisha  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa,kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama uume  wa  mtoto.
 
Hii ndio  sababu  kwanini watu  wengi  walio athirika  na  punyeto  hulalamika  kwamba  maumbile  yao  ya  kiume  hayajaongezeka  tangu  walipo anza  kujihusisha  na  punyeto  wakiwa  na  umri mdogo. 

Maumbile  yao  huonekana  kama  ya  watoto  kwa  sababu hayakupata  nafasi  ya  kupokea  vichochea  vya  kuyafanya  yakue  na  kuongezeka  tangu  walipo  anza  kujihusisha  na  punyeto.

Suluhisho  La  Tatizo La Maumbile  Ya  Kiume  Yaliyo  Sinyaa  Kwa  Sababu  Ya  Punyeto.
Kama  bado  unaendelea  kujihusisha  na punyeto  basi  jitahidi  uache  tabia  hiyo  mara  moja  kwani  inakuharibu. Inaweza  isiwe  rahisi  sana  kuacha  mara  moja  lakini  ukiweka  nia  thabiti  basi  unaweza  kuacha  kabisa  kama  walivyofanikiwa  kuacha  wengine  ambao  walikuwa  wametopea  kwenye  tabia  hiyo  lakini  wakajitahidi  kujilazimisha  na  hatimaye  wakafanikiwa  kuachana  kabisa  na  tabia  hiyo.

==>> Acha kuangalia video chafu za ngono.
Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie  punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. 


Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

==>>Epuka kukaa nyumbani peke yako;
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine. 


Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata kama vile misuli ya uume kulegea, kushindwa kurudia tendo uwapo na mwenzi wako, kuishiwa nguvu za kiume, maumbile kusinyaa, kurudi ndani na kuwa kama ya mtoto mdogo.

Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivyohivo, kama unaacha acha mara moja ili utunze heshima yako mbele ya mwenzi au mke wako.

Kama utaona  kuna  ugumu  wa  kuacha  tabia  hiyo  na tayari ushaapata madhara ya maumbile kusinyaa na kupungiwa nguvu za kiume, basi  wasiliana nasi kwa ushauri zaidi; Simu  0744040721

Upendo Peneza Amvaa Polepole....Ni Baada ya Kusema Wabunge Viti Maalumu CHADEMA Wamepatikana Baada ya Kutembea na Mbowe

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Upendo Peneza amemvaa Katibu Mwenezi wa CCM, Humphery Polepole, kuwa amewadhalilisha wabunge wa viti maalumu wanaotokana na chama chake kuwa wamepata nafasi hizo baada ya  kufanya ngono na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Peneza ameyasema hayo jana Jumatano Aprili 17, 2019   akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema wabunge wa viti maalumu wapo kwa mujibu wa Katiba lakini kuna kitu kibaya kilianza kutokea ndani ya Bunge na kwamba, viongozi wa Bunge wanapokaa kuendesha Bunge wamekuwa wakikemea tabia hiyo aliyoita ni ya kipuuzi.

"..Mwenyetiti na viongozi wengine wa Bunge walikemea tabia hii ya "kipuuzi", lakini sasa imefika huko nje ambapo ndugu, Humphrey Polepole amesema wabunge wa viti maalum wa CHADEMA wanapatikana mpaka "wapitiwe" na Mwenyekiti wao, huu ni udhalilishaji.

“Sasa kama hata hatambui haki za kikatiba ni aibu kwa Chama cha Mapinduzi kuwa na mwenezi anayedhalilisha wanawake… lakini ifike mahali nafasi walizonazo na vyeo walivyonavyo viheshimiwe,” amesema.

Amesema ni aibu kwa kiongozi kusimama na kusema kuwa nafasi ya mwanamke kisiasa inatokana na ngono.

"Ni aibu kwa kiongozi wa nchi hii kusimama na kusema kwamba mafanikio ya mwanamke ya kisiasa yanatokana na shughuli za kingono, tunawajengea watoto wetu fikra mbaya ndani ya kichwa chao" Amesema Peneza

Waziri Mkuu Aitaka PSSSF Iongeze Makusanyo

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka menejimenti ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ijizatiti na kuweka mbinu mpya za kuongeza makusanyo.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Alhamisi, Aprili 18, 2019) wakati alipokutana na menejimenti ya mfuko huo kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa PSSSF jijini Dodoma.

Waziri Mkuu ambaye aliamua kutembelea ofisi za mfuko huo ili afahamiane na menejimenti hiyo, amesema amepokea taarifa ya Mkurugenzi Mkuu na kubaini kuwa ukusanyaji wa michango hauridhishi.

“Mfuko huu ni wa tofauti na wa NSSF kwa sababu umeunganisha mifuko mingine ya GEPF, PSPF, LAPF na PPF. Mifuko yote hii ilikuwa na malengo na majukumu yake ya awali, lakini sasa imeunganishwa kwa hiyo jukumu letu ni moja,” amesema.

“Natambua mna kazi kubwa ya kusajili wanachama wapya lakini pia tunayo kazi ya kuwafikia wanachama wa zamani ambao tumewachukua kutoka mifuko mingine na kuhakikisha kuwa wanaingizwa katika mfuko mpya,” amesisitiza.

“Napenda kusisitiza kuwa jukumu la kukusanya michango ni la muhimu sana. Ni lazima mjue wastani wa makusanyo kwa mwezi ni kiasi gani, na kama zimepungua, ni kwa kiasi gani na pia mtafute ni kwa nini zimepungua,” amesema.

Ameitaka menejimenti hiyo pia ijiridhishe juu ya uhakiki wa mali walizorithi kutoka mifuko mingine na izitambue ziko katika hali gani. “Menejimenti peke yenu hamuwezi kufuatilia mali zote, kwa hiyo wapeni hiyo kazi wajumbe wa Bodi, wagawane maeneo ili waende kuzitathmini hizo mali na kisha nipate hiyo taarifa,” amesema.

Mapema, akiwasilisha taarifa ya utendaji wa mfuko huo kuanzia Agosti Mosi 2018 hadi Machi 31, 2019, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba alimweleza Waziri Mkuu kwamba majukumu makuu wa mfuko huo ni kusajili wanachama, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao kwa wanachama.

Alisema baada ya kuunganishwa kwa mifuko, uandikishwaji wa wanachama uliendelea ambapo hadi kufikia Machi 2019, jumla ya wanachama wapya 7,575 walikuwa wamesajiliwa.


“Hapo awali mfuko ulikuwa na wanachama 962,871. Kati ya hao, wanachama 279,564 wanatoka sekta binafsi ambao wamehamishiwa NSSF. Hadi kufikia Machi 31, 2019, mfuko ulikuwa na jumla ya wanachama 750,943 ambao ni watumishi wa umma ikijumuisha na wanachama 67,636 waliohamia kutoka NSSF,” alisema.

Kuhusu ukusanyaji wa michango, Bw. Kashimba alisema moja ya jukumu la mfuko ni kukusanya michango na tangu Agosti 2018 hadi Machi 2019, mfuko huo ulikuwa umekusanya jumla ya sh. bilioni 928.31 ikilinganishwa na lengo la lililowekwa la kukusanya sh. trilioni 1.05 sawa na asilimia 88.62.

Kuhusu malipo ya mafao, Bw. Kashimba alisema katika kipindi kilichoishia Machi 31, 2019, mfuko huo umelipa mafao ya jumla ya sh. trilioni 1.65.

Alisema mfuko huo hivi sasa una wafanyakazi 839 ambao kati yao, wanaume ni 470 na wanawake ni 369.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, (OWM – Sera, Uratibu, Bunge na wenye Ulemavu), Bibi Jenista Mhagama.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 19

Wenyeviti 13 wa Chadema jimbo la Freeman Mbowe watimkia CCM

$
0
0
Wenyeviti 13 wa Vitongoji katika Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro ambalo linaongozwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema), wameitikisa tena ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini, baada ya kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi.

Kundi hilo la wenyeviti hao wa vitongoji, linaivuruga ngome hiyo, huku ikiwa imepita miezi saba tangu Wenyeviti wa Serikali za Vijiji 19 katika Halmashauri ya Wilaya hiyo ambao wanatoka na Chadema, kubwaga manyanga na kujiunga na CCM, Septemba 6 mwaka jana.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kupokea barua za kujiuzulu kwa wenyeviti hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Yohana Sintoo alithibitisha kupokea barua za kujiuzulu kwa wenyeviti hao 13 jana asubuhi.

Aliwataja wenyeviti waliojiuzulu na vitongoji vyao kwenye mabano kuwa ni Gladson Swai (Bomani), Ruyandumi Kimaro (Makiweru-Uswaa), Beda Msofe (Lembeni B-Rundugai), Ndemael Massawe (Nure-Ng’uni), Leonard Urassa (Njoro Chini-Shirinjoro) na Raymond Mushi (Nkwelengy-Nronga).

Wengine ni Filbert Usiri (Nkwamandaa-Nronga), Eliatosha Lema (Maaseni-Nronga), Majisia Paul (Ngulujuu-Chemka), Nimkaza Mhando (Kikuletwa-Chemka), Gasper Mwasha (Boma Kati-Kware), Walter Swai (Masamu-Uswaa) na Majinsi Nyange (Lembeni A-Rundugai).

Watuhumiwa Wanne Wafikishwa Mahakamani kwa kutumia j jina la Mama Janeth Magufuli Kutapeli

$
0
0
Watuhumiwa wanne wa Dar es saalam wamefikishwa katika mahakama ya Kisutu wakituhumiwa kwa makosa manne ya matumizi mabaya ya mtandao ikiwemo kutapeli wananchi kupitia ukarasa wao wa Facebook kuwa wanatoa mikopo kupitia Taasisi waliyoitaja kuwa ni ya Mama Janeth Magufuli.

Pia washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la kutakatisha fedha kiasi cha Sh4.5 milioni,Washtakiwa hao ni  Saada Uledi, Maftaha Shabani, Heshima Ally na Shamba Baila.

Akisoma hati ya mashtaka jana Alhamisi Aprili 18, wakili wa Serikali Batilda Mushi alidai washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 30/2019.

Alidai shtaka la kwanza ambalo ni kula njama, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Januari 2017 na Machi 2019 katika jiji la Dar Es Salaam walichapisha taarifa za uongo kupitia akaunti yao ya mtandao wa kijamiii wa Facebook.

Shtaka la pili, washtakiwa wanadaiwa siku na eneo hilo walichapisha machapisho katika akaunti yao ya mtandao wa kijamii wa Facebook, wakionyesha Janeth Magufuli ambaye ni mke wa Rais  Magufuli ameunda taasisi ya kutoa mikopo kwa watu mbalimbali ikiwa na masharti ya kuweka fedha kabla ya kupewa mkopo kama ni kinga ya mkopo huku wakijua kuwa ni uongo.

Shtaka la tatu, wanadaiwa Machi 2 na 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam, wakiwa kama waendeshaji wa akaunti hiyo ya Facebook, walisajili akaunti hiyo kwa jina la Janeth Magufuli kwa nia ya kudanganya na kujipatia Sh4,487,000 kutoka kwa Paul Kunambi kama kinga  ya mkopo wakati wakijua kuwa siyo kweli.

Mushi ameendelea kudai katika shtaka nne ambalo ni utakatishaji wa fedha, washtakiwa kwa pamoja kati ya Machi 2 na 8 mwaka huu katika jiji hilo, walijipatia Sh 4, 487,000 huku wakijua kuwa fedha ni zao la  fedha haramu zilizotokana kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka yanayowakabili, Hakimu Kasonde alisema hawatakiwi kusema chochote mahakamani hapo kutokana na kesi inayowakabili kuwa ni uhujumu uchumi.
 
Upande wa mashtaka ulieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Kasonde aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 2 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na kesi inayowakabili kutokuwa na dhamana.

Fadhili Mahenge ( Mzee wa Ile Pesa tuma kwenye Namba Hii ) Anaswa Akiwa na Laini 629

$
0
0
Fadhil Mahenge (27) ambaye ni mfanyabiashara wa mtandao  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na makosa matano ikiwemo utakatishaji fedha wa Mil.123 kwa kutumia line za simu 629.

Fadhil ambaye ni miongoni mwa ‘Wazee wa Ile Pesa tuma kwenye Namba Hii’ amesomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi, Wanjah Hamza na Wakili wa Serikali, Batilda Mushi.

Wakili Mushi amedai kuwa mshitakiwa anakabiliwa na makosa matano ambapo la kwanza anadaiwa kuchapisha taarifa za uongo katika tarehe tofauti kati ya Januari 2017 na Machi 2019 katika mkoa wa Dar es Salaam, Rukwa, Songwe na mikoa mingine.

Inadaiwa alisamba taarifa kwa kusema ‘Tuma Pesa kwenye namba hii’ bila idhini ya aliowatumia.

Kosa jingine ni kusambaza ujumbe bila ridhaa ambapo inadaiwa kati ya Januari 2017 na Machi 2019 ndani ya jiji la Dar es Salaam, Rukwa, Songwe na mikoa mingine alisambaza ujumbe bila ridhaa kwa watu tofauti tofauti kwa kutumia Line ya simu 629 za mitandao tofauti tofauti.

Katika kosa la utakatishaji fedha inadaiwa alilitenda kati ya tarehe na mikoa hiyo ambapo alijipatia Mil.123 wakati akijua ni zao la fedha haramu.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo,mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana na Mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpatia.

Upelelezi wa kesi haujakamilika, kesi imeahirishwa hadi Mei 2, 2019.

Wawili Wafikishwa Mahakamani Kwa Kuchapisha Habari Mtandaoni Bila kuwa na Leseni ya TCRA

$
0
0
Wafanyabiashara wawili ambao ni wakazi wa Kigamboni wamepandishwa mahakamani hapo kujibu shtaka la kuchapisha habari katika mtando bila kuwa na leseni.

Washitakiwa hao ni Obadia Kwitega na Stella Ommary ambao wamesomewa shtaka lao  na  Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwezile.

Wakili Kakula alidai kuwa washitakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Januari 29 na Machi 29, 2019 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam ambapo kupitia runinga ya mtandaoni ikijulikana kama Habari Mpya TV walichapisha taarifa bila kibali cha Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Washtakiwa baada ya kusomewa mashitaka hayo, walikana kutenda kosa hilo.

Wakili Kakula alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Rwezile alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa hao ambapo kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya maneno ya Sh5milioni. Pia kila mshtakiwa anatakiwa kusaini dhamana ya maneno ya  Sh5milioni.

Hata hivyo, mshitakiwa Stella ndiye aliyeweza kutimiza masharti na kuachiwa kwa dhamana, huku mwenzie akirudishwa rumande.

Hakimu Hamza aliahirisha kesi hiyo hadi  Aprili 30, 2019, itakapotajwa.

Mahakama ya juu ya Uganda yamsafishia njia Museveni

$
0
0
Mahakama ya Juu nchini Uganda imekubaliana na uamuzi wa kuondosha ukomo wa umri wa mgombea urais, na hivyo kumsafishia njia Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 74 kuwania kwa muhula mwengine wa sita. 

Mahakama hiyo ilitupilia mbali zuio la wapinzani, ambao waliukatia rufaa uamuzi wa mahakama ya katiba ulioridhia mabadiliko ya katiba yaliyofanywa na bunge. 

Katika uamuzi wake hapo jana, Jaji Mkuu Bart Katureebe alitangaza kwamba rufaa hiyo imeshindwa, baada ya majaji wanne kuitupilia mbali dhidi ya watatu walioiunga mkono.

Mwezi Disemba 2017, Rais Museveni - ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 - aliusaini muswaada wa sheria kuondosha ukomo wa umri kwa wagombea urais, na hivyo kuashiria kuwa angeliwania tena mwaka 2021. 

Uamuzi huo ulizusha ukosoaji mkubwa kutoka kwa wapinzani, ambao wanamtuhumu kiongozi huyo kutaka kuwa rais wa maisha.

Ripoti: Urusi ilijaribu kuingilia Uchaguzi wa mwaka 2016 lakini Trump hana hatia

$
0
0
Ripoti ya kurasa 448 kuhusu uchunguzi maalum kubaini iwapo Urusi iliingia Uchaguzi wa urais nchini Marekani mwaka 2016  imewekwa wazi baada ya uchunguzi wa miaka miwili kumalizika.

Uchunguzi huo uliongozwa na Robert Mueller aliyewahi kuwa mkuu wa FBI na imebaini kuwa ni kweli Urusi ilijaribu kuingilia Uchaguzi huo.

Hata hivyo, katika ripoti hiyo, haikubainika iwapo kampeni ya rais wa sasa Donald Trump ilishirikiana na Urusi au raia yeyote wa Marekani.

'Baada ya uchunguzi wa miaka miwili, maelfu ya watu kujitokeza na mamia kutoa ushahidi, imebainika kuwa ni kweli Urusi ilijaribu kuingilia Uchaguzi wa Marekani lakini wale waliomsaidia Trump kufanya kampeni hawakuhusika," amesema Mwanasheria Mkuu William Barr.

Mawakili wa Trump wamesema kuwa ripoti hiyo ni ushindi mkubwa kwa upande wao baada ya kushtumiwa hapo awali kuwa, Trump alisaidiwa na Urusi kuingia madarakani.

Pamoja na hilo, ripoti hiyo imeeleza kuwa rais Trump alijaribu kushawishi kufutwa kazi kwa Mueller aliyekuwa anaongoza uchunguzi huo.

Trump amekuwa akisema kuwa hakuwahi kushirikiana na Urusi, kushinda Uchaguzi wa mwaka 2016.

Ufaransa yakanusha madai ya kumuunga mkono mpinzani wa serikali ya Libya

$
0
0
Ufaransa imekanusha vikali madai ya Libya kuwa, inamuunga mkono Kamanda wa kijeshi Khalifa Haftar, anayeongoza vikosi vyake kujaribu kuliteka jiji kuu, Tripoli.

Waziri wa Mambo ya ndani wa Libya Fathi Bach Agha ametangaza kusitishwa kwa mahusiano kati ya serikali yake na ile ya Ufaransa kwa madai ya kuwaunga maadui wake.

Wakari uo huo, wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa wameanza majadiliano kuhusu  namna ya kuwezesha pande zote mbili kusitisha mapigano.

Wiki iliyopita, Kanali Mohamad Gnounou, msemaji wa vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa (GNA) alishtumu vikosi vya Jenerali Khalifa, kuweza kuingia sehemu ya mji na kupiga picha na baadae kuondoka na kurudi kwenye ngome zao.

Hata hivyo mapigano bado yanaendelea pembezoni mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli. Baadhi ya raia wa maeneo hayo wametoroka makaazi yao.

Shirika la msalaba mwekundu liimeripoti kuuawa kwa mamia ya watu na wengine kujeruhiwa.

Nafasi Ya Ajira Katika Sekretarieti Ya Jumuiya Ya Ukanda Wa Maziwa Makuu (ICGLR).

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inawahamasisha Watanzania wenye sifa, kuomba nafasi ya ajira katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR).

Ajira hiyo ni Mtaalam wa Uhakiki wa Nyaraka. Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hiyo ya ajira zinapatikana kwa kupitia tovuti www.icglr.org.

Maombi yote yatumwe kwenda katika barua pepe jobs@icglr.org na nakala itumwe katika barua pepe gerard.nayuburundi@icglr.org  yakiwa na kichwa cha habari Maombi ya nafasi ya Mtaalam wa Uhakiki wa Nyaraka.

Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi hiyo ni  tarehe 25 Aprili, 2019.

    Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
      Dodoma.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images