Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Imeanza Mazungumzo Na Nchi Za Misri Na Algeria Kuandaa Makubaliano Ya Kuuza Tumbaku Ya Tanzania

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeanzisha mazungumzo na nchi wanachama wa COMESA na nchi kama Misri na Algeria kupitia balozi zake ili kuandaa Makubaliano Maalum (Bilateral Agreement) yatakayoiwezesha Tanzania kupeleka tumbaku kwa kodi nafuu.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mhe Edwin Amandus Ngonyani Mbunge wa Namtumbo aliyetaka kufahamu Wizara ya Kilimo inashirikianaje na Wizara nyingine zinazohusika na uwekezaji wa mambo ya nje kutafuta soko la tumbaku nchini Misri badala ya kulazimika kutumia nchi za Uganda na Kenya pekee.

Mazungumzo hayo yamefikia hatua nzuri na matarajio ni kufungua milango ya soko hilo na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima na taifa kwa ujumla. Aidha, Makubaliano hayo yakikamilika Tanzania inaweza pia kuuza chai nchini Misri na Algeria kwa faida kuliko ilivyo hivi sasa au badala ya kuuza chai kupitia mnada wa Mombasa nchini Kenya.

Mhe Bashungwa alisema kuwa mwaka 2014/2015 uzalishaji wa tumbaku ya moshi (Dark Fire Cured Tobacco – DFC) ulisimama mkoani Ruvuma kutokana na kukosa soko.

Hata hivyo, Jitihada za Serikali ikawezesha Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited (PATL) kuonesha nia ya kununua tumbaku hiyo ya DFC ambayo nchini Tanzania huzalishwa katika Wilaya ya Namtumbo na Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.

Alisema Kampuni hiyo ilieleza kuwa lipo soko kubwa la tumbaku aina ya DFC nchini Misri na Algeria lakini tumbaku ya Tanzania inauzwa kwa bei ya juu kutokana na kodi inayotozwa ikilinganishwa na aina hiyo ya tumbaku kutoka nchi za Uganda na Kenya kwa kuwa nchi hizo (Uganda, Kenya, Algeria na Misri) ni wanachama wa jumuiya ya COMESA na kwa hiyo kodi za kuingiza tumbaku, chai na bidhaa nchini Algeria na Misri kutoka Uganda na Kenya ni za chini.

Mhe Bashungwa alisisitiza kuwa, ili Tanzania iuze tumbaku, chai na bidhaa nyingine katika nchi za Algeria na Misri kwa faida, inatumia nchi zilizo kwenye jumuiya hiyo kama Uganda na Kenya.

Kadhalika, Mhe Bashungwa alisema kuwa Wizara ya Kilimo inaendelea kuimarisha masoko ya mazao mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo tayari soko la mahindi limepatiwa ufumbuzi kwa Wizara kuingia mkataba wa mauziano na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuingia mikataba ya masoko ya uhakika kwenye mazao ya kimkakati na mazao mchanganyiko.


Waziri Ummy Azindua Bodi Ya Uratibu Ya Asasi Za Kiraia[NGO’s]huku Akiwataka Viongozi Kufanya Kazi Kwa Ueledi

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mh Ummy Mwalimu amezindua  Bodi ya  uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali  katika ukumbi wa Ofisi  ya Taifa ya Takwimu (NBS) Jijini Dodoma.
 
Akizungumza jijini Hapa waziri Ummy amesema kuwa  Bodi ina jukumu la kutoa miongozo ya kisera pamoja na kuchunguza na kuhoji ili kuhakikisha uzingatiaji wa katiba za mashirika yasiyo ya kiserikali.
 
Aidha, Waziri ummy ameongeza kuwa ni wajibu wa bodi  hiyo kujielekeza  katika kuhakikisha sekta hiyo inajiendesha kwa misingi ya uwazi na uwajibikaji ndani ya serikali , ndani ya mashirika yasiyo ya kiserikali na kwenye sekta binafsi.
 
Mbali na hilo waziri Ummy amesema bodi hiyo itafanya kazi kwa kuzingatia sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali lakini pia kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni zilizoko.
 
Rukia masasi ni mwenyekiti  Bodi ya mashirika yasiyo ya kiserikali aliyemaliza muda wake amesema kuwa  bodi  ni chombo muhimu kwasababu  inabeba  NGO’s na  ni mwakilishi wa  asasi za kiraia ,NGO’s na pia ni  mwakilishi wa serikali hivyo ni kama kiungo kwani  serikali na  asasi za kiraia,NGO’s  ni wadau wanaoshirikiana katika maendeleo .
 
Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto anayeshughulikia idara kuu ya maendeleo  ya jamii, Dkt John Jingu amesema  sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali ni sekta ambayo inamchanganyiko wa kipekee kwani ni sekta kubwa na nipana.
 
Naye Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo  Richard  Sambaiga amesema jukumu lao kubwa ni kuwezesha uratibu na utendaji kazi wa sekta hiyo ili uweze kustawi kwa maslahi ya umma wa Tanzania.
 
Hatahivyo, Waziri ummy amesema  asasi za kiraia ,NGO’s  ni sekta kubwa na nimuhimu katika kujenga na kushiriki  katika Maendeleo ya kiuchumi,kisiasa ,kijamii na kiutamaduni.

Moto Mkubwa Ulivyotikisa Jengo la Mfanyabiashara Dodoma

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jana April 16, 2019 ajali  kubwa ya Moto ilitokea katika jengo la  mfanyabiashara Jijini Dodoma , Franscis  Maiko Shio lililo mkabala na Bahi Hotel jirani na  Nyerere Square  hali iliyolazimu jeshi la zimamoto mkoa wa Dodoma kufika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuokoa mali mbalimbali.
 
Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Dodoma A.C.F  Fikiri  Salehe Salla amesema walizipokea taarifa za ajali hiyo ya moto  jana majira saa 2:16 asubuhi na wakatuma gari la kwanza saa 2:19 asubuhi.
 
Amefafanua kuwa  baada ya kuona tukio la ajali ya moto ni kubwa waliongeza magari matatu ya zimamoto na askari 14  na maafisa watano ambao walifanikiwa kuuzima moto huo baada ya robo saa.
 
Aidha ,amesema chanzo cha ajali ya moto huo ni hitilafu ya umeme huku uchunguzi ukiwa unaendelea zaidi.
 
Kamanda Salla ametoa wito kwa wananchi kuitumia namba ya bure 114 pindi wanapopatwa na mikasa ya ajali ya moto huku akitahadharisha kila nyumba kuwa na vifaa  vidogovidogo vya kuzimia moto pamoja na kujenga nyumba zenye mpangilio maalum ili kuruhusu miundombinu kufikika haraka jeshi hilo pindi panapotokea ajali.
 
Vilevile  Kamanda Salla amelishukuru Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kwa kuweza kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha mali zilizokuwa zinaokolewa haziibiwi.
 
Mali zilizookolewa kutokana na ajali ya moto huo ni TV Screen kadhaa,Nguo,Kabati,viatu na vingine vingi huku hakuna majeruhi au vifo vyovyote vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo na uchunguzi unaendelea juu ya samani au fedha zilizoharibika au kupotea kutokana na ajali hiyo ya moto.

Ajali Za Majini 300 Hutokea Kila Mwaka Mkoani Mwanza

$
0
0
Na. OWM, MWANZA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amebainisha kuwa takribani ajali za majini  zaidi ya mia tatu huripotiwa kuwa zimetokea mkoani humo. Ajali hizo ni zile ambazo huripotiwa rasmi  tu  katika mamlaka husika , aidha inasadikika zipo ajali nyingi ambazo hutokea lakini huwa haziripitiwi  kutokana na jiografia ya mkoa huo. Mkoa wa Mwanza una visiwa zaidi ya 162 ambapo kati ya Visiwa hivyo vipo ambavyo watu wanayo makazi ya kudumu na vingine watu huishi kwa muda mfupi.

Akiongea wakati  akifungua Mafunzo kwa Kamati  ya  Usimamizi wa maafa  ya mkoa huo,  yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa shughulii za maafa Leo, tarehe 17 Aprili, 2019, jiijini Mwanza, Mongella amefafanua kuwa ajali za vyombo vya usafiri hasa vya majini zinaweza kupunguzwa sana kama wamiliki na waendeshaji wa vyombo hivyo watazingatia sheria na Kanuni  zinazotawala uendeshaji wa vyombo hivyo.

“Suala muhimu la Kuzingatia ni kuhakikisha mamlaka zetu za serikali za mitaa zinaimarisha utawala bora unaotoa nafasi kwa  jamii kushiriki katika kuzuia na Kupunguza madhara ya majanga, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali baada ya maafa kutokea ikiwa ni pamoja na kutoa elimu, taarifa za tahadhari ya awali kwa wakati muafaka na kuandaa rasilimali zinazohiotajika , Ni wajibu wetu kuhakikisha sheria zinasimamiwa kikamilifu ili kuepuka maafa“ alisisitiza Mongella.

Naye Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe, ameitaka Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya mkoa huo  kuandaa Mkakati wa Kupunguza madhara  ya maafa pamoja na Mpango wa kujiandaa na kukabili maafa, Aidha, ameeleza kuwa  Ofisi ya waziri Mkuu imeendesha mafunzo hayo  ili kuijengea uwezo kamati hiyo ambayo ni chombo cha kisheria hapa nchini kwa ajili ya kutathimini na kutekeleza masuala ya kitaalam kuhusu usimamizi wa maafa, kuzuia na kupunguza madhara ya majanga ya aina zote katika mkoa.

“Upunguzaji wa madhara ya maafa ni suala mtambuka linalohusika katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii sekta zote. Suala la usimamizi wa maafa linahitaji utashi wa kisiasa na kuwajibika kitaalam, kisheria, uelewa wa umma, elimu ya kisayansi, mipango makini ya maendeleo, ufanisi wa utekelezaji wa sera, mifumo ya tahadhari inayojibu matakwa ya jamii” alisema  Kanali., Matamwe.

Mwaka jana, Mwezi Septemba, mkoa wa Mwanza ulipata maafa makubwa baada ya Kivuko cha MV. Nyerere kuzama na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200 na wengine 40 waliokolewa. Kufuatia maafa hayo Mkoa huo umeendelea na jitihada za kuzijengea uwezo kamati za Usimamizi wa Maafa za mkoa huo

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa shughuli za maafa, yamehudhuriwa na wajumbe wote wa Kamati ya Usimamizi wa maafa kwa kuzingatia Kifungu cha 13 cha sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya mwaka 2015.

 

Shilingi Milioni 5 Ya Rambi Rambi Iliyotolewa Na Rais Magufuli Mkoani Njombe Yakabidhiwa

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amekabidhi fedha ya rambi rambi kiasi cha shilingi milioni tano zilizotolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John pombe Magufuli  kwa familia tano zilizokumbwa na mauaji ya watoto yaliyotokea kuanzia mwezi wa kumi na moja mwaka jana.

Olesendeka amesema Rais Magufuli kwa niaba serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania amekabidhi fedha hiyo ya pole kwa familia zilizoondokewa na watoto kutokana na ahadi yake aliyoitoa wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani humo.

“Mheshimiwa Rais alipokuwa mkoani hapa kwa siku tatu hakuonyesha kuficha hasira zake na alionyesha kufedheheshwa na kukasilishwa kwa vitendo  vilivyokuwa vimefanyika kati ya mwezi wa kumi na moja na mwezi wa pili mwaka huu ambapo tulipoteza watoto wetu takribani watoto nane,lakini Rais amenielekeza nifike kwenye familia hizi na kuwashika mkono wa pole kwa niaba yake kwa kuongozana na kamati ya ulinzi na usalama”alisema Olesendeka

Aidha Olesendeka amewasisitiza viongozi wote wa wilaya ya Njombe na mkoa kwa ujumla kuhakikisha vitendo vya aina hiyo havirudiwi kwa mara nyingine.

“Nichukue nafasi kuwataka viongozi wa wilaya hii ya Njombe na katika mkoa wetu kwa ujumla wake hakuna mtu au mtoto yeyote atakayepoteza maisha yake kwa vitendo kama hivyo au kwa visingizio vyovyote vile”aliongeza Olesendeka 

Miongoni mwa familia zilizotembelewa ni pamoja na familia ya Bw.Daloti Nahala walioondokewa na mtoto Oliver Nahala,wameishukuru serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na wananchi kwa ujumla kuyaona matatizo hayo na kuyachukulia uzito.

“Mimi niwashukuru wa Tanzania na serikali nzima ya Tanzania kwa kuliona hili na kulichukulia uzito ili liweze kutulia na nchi yetu ibaki kuwa na amani” alisema Nahala mmoja wa wazazi waliondokewa na watoto

Familia tano zilizokumbwa na matatizo hayo zimekabidhiwa kiasi cha shilingi milioni moja kila familia kama pole iliyotolewa na Rais Mgufuli mkoani Njombe.

Serikali Yafunguka Kuhusu Elimu ya Msingi Kuishia Darasa la Sita

$
0
0
Serikali imesema kwa sasa hakuna haja ya kubadilisha muda wa kuhitimu elimu ya msingi kwa sababu imebaini muda wa miaka saba unaotumika si kitu kibaya.

Hayo yamebaisnishwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha leo Aprili 17 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi ambalo limehoji, serikali inazunhgumziaje kuhusu kutotekelezwa kwa sera ya elimu ya kuishia darasa la sita badala ya darasa la saba.

Akijibu swali hilo, Ole Nasha amesema sera siyo msahafu na serikali inaweza kuibadilisha wakati wowote kadri itakavyoona inafaa kwa wakati husika, “Kwa wakati huu tumeona elimu kuanzia darasa la kwanza hadi la saba siyo kitu kibaya. Hatuna haja ya kubadili ndiyo maana tumebakia na mfumo wa zamani”, amesema Ole Nasha.

Amesema kwa hatua hiyo Serikali haijavunja sheria na kwa sasa ipo katika mapitio kwa mambo mapya yaliyoko katika sera ya elimu ambayo wanaona hawataweza kutekeleza.

Amesema Serikali inazingatia ubora wa elimu ndiyo maana kumetokea mabadiliko makubwa katika idara ya udhibiti wa elimu.


Ameongeza kuwa, wameanza utaratibu mpya wa udhibiti ubora wa elimu kwa ushirikishwaji ambao unawaleta wadau wote kwa pamoja, pia wanahakikisha waratibu wa elimu wanapata vifaa na ofisi ili kusimamia vizuri kuhakikisha elimu inakuwa bora.

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Dodoma Mjini Aliyekihama Chama Hicho Apokelewa Rasmi CCM

$
0
0
Yona Kusaja  ambaye alikuwa ni Diwani wa Kata ya Kikombo na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini,  amejivua uanachama wa Chama Chadema na vyeo vyake vyote ndani ya Chama hicho na kujiunga na CCM

Bwana Yona Kusaja amepokelewa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi akiwa katika Semina ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu ya CCM -  Dodoma.

Imetolewa na
IDARA YA ITIKADI  NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI

Serikali Yashusha Gharama Za Urasimishaji

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANNM
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuanzia sasa gharama za urasimishaji haitazidi shilingi 150,000 badala ya 250,000 iliyopangwa awali na makampuni yatakayoenda kinyume yatachukuliwa hatua ikiwemo kufutwa.

Lukuvi alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Makampuni ya Upangaji na Upimaji yanayofanya kazi ya urasimishaji katika mitaa mbalimbali nchini pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, baada ya Wizara yake kuona zoezi la urasimishaji linasuasua wamegundua asilimia 30 pekee ndiyo iliyorasimishwa tangu kuanza zoezi hilo na hali hiyo imechangiwa na uwezo mdogo wa wananchi wengi kumudu gharama za urasimishaji.

Waziri Lukuvi alisema, alichotegemea kwa makampuni yaliyopewa kazi ya urasimishaji ni kuwa na uzalendo kwa kushusha gharama lakini yameshindwa kupunguza gharama jambo lililoifanya serikali kuona haja ya kupitia upya gharama hizo na kubaini gharama za msingi ili  kumuwezesha mwananchi kupata hati na kusisitiza punguzo hilo halitawahusu waliolipia  gharama za urasimishaji.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameyataka makampuni yanaoyoendesha zoezi la urasimishaji kuhakikisha kiasi cha fedha inachowatoza wananchi kinaishia hatua ya Hati na gharama itakayolipwa na mwananchi baada ya kurasimishwa ni kodi ya ardhi na kuyatahadharisha kutochukua muda mrefu kukamilisha zoezi hilo.

Amewataka wananchi wote wanaoishi kwenye maeneo yasiyo rasmi kuhakikisha wanaingia katika zoezi la urasimishaji ili kupata hati itakayowawezesha kiuchumi na kusisitiza kuwa suala hilo linafanyika kwa nia njema kwa nia ya kuwaongezea mtaji wananchi kwa kupatiwa nyaraka itakayowasiadia kukopa fedha benki.

Akigeukia suala la Leseni za Makazi, Waziri Lukuvi alisema zoezi hilo linaendelea vizuri katika jiji la dar es Salaama kwa gharama ya shilingi elfu tano hadi hatua ya upatiwaji leseni ya makazi na kusisitiza kuwa leseni hiyo siyo ya kudumu bali itakuwa kwa miaka mitano na kuwataka wananchi walio katika maeneo ya urasimishaji kuendelea na zoezi hilo kwa kuwa wizara inayo kanzi data itakayotunza takwimu za mazoezi yote mawili.

‘’Tunataka kuwa na database ya nani anamiliki ardhi kiasi gani na kila mwananchi lazima awe na leseni ya makazi au hati kwa lengo la kushiriki kulipa kodi’’ alisema Lukuvi

Hata hivyo, Lukuvi alisikitishwa na baadhi ya Makampuni ya urasimishaji kushindwa kutoa takwimu wakati wa zoezi la upimaji zinazoendana na miongozo ya wizara na kuyataka yote yaliyoenda kinyume kurudia zoezi  na kuongeza kuwa kuna makampuni 34 yaliyotuma takwimu ambazo ni chafu na kuyapongeza makampuni mawili ya Visible Planners na Afro Max  kwa kufuata taratibu zote za urasimishaji.

Lukuvi alionya baadhi ya makapuni ya urasimishaji kuacha kuwalaghai wananchi kwa kuwapatia leseni za makazi badala ya hati kwa gharama za urasimishaji na kusema kufanya hivyo ni kosa la uhujumu uchumi na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Vile vile Lukuvi amewataka watendaji wa serikali ambao wana makampuni yanayofanya kazi ya urasimishaji kuchagua jambo moja la kuitumikia serikali ama makampuni yao kwa kuwa wanatumia muda mwingi kufanya kazi katika makampuni yao badala ya kuitumikia serikali.

‘’Ninyi watendaji wa serikali badhi yenu mna makampuni ya urasimishaji na ndiyo mnaoharibu zoezi mnataka squatters ziendelee ili mnufaike na mnapima halafu michoro mnapitisha ninyi hii ni conflict of interest’’ alisema Likuvi.

Serikali yaviandikia barua vyombo vya habari vilivyoripoti uchambuzi wa Zitto Kabwe Kuhusu ripoti ya CAG

$
0
0
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas amekiri kuwa ni kweli vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) uliofanywa na Mbunge Zitto Kabwe vimeandikiwa barua.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dk. Abbas ameandika akimuonya kiongozi huyo wa Chama cha ACT Wazalendo kuacha kile alichokiita ni upotoshaji, na kuleta siasa katika taaluma ambayo haielewi.

Awali Zitto Kabwe aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa magazeti yote yaliyoandika uchambuzi huo yaliandikiwa barua na kutakiwa kujieleza kwa kukiuka sheria

 "Msemaji Mkuu kaandikia barua magazeti yote yaliyoandika habari ya uchambuzi wa Ripoti ya CAG uliofanywa na @ACTwazalendo. Amewataka wajieleze kwa kuvunja sheria. Sasa Msemaji wa Serikali amekuwa Mhariri Mkuu wa Taifa. Vyombo vya Habari vinatishwa kuandika Habari kutoka upinzani "


Katika maelezo yake Dkt Abbas amemtaka mbunge huyo kutoleta siasa kwenye taaluma asiyoielewa na kwamba walioandikiwa barua wameelewa na/au wamekiri kosa.
 
 "Usilete siasa katika taaluma ambayo bahati mbaya huijui misingi yake. Walioandikiwa wamejua/kukiri kosa lao."

Hata hivyo msemaji huyo hakuweka wazi kuwa ni kosa gari vyombo hivyo hivyo vimekiri au wameomba msamaha kwa kosa gani.

Lakini aliendelea kusema kwamba, kama vyombo hivyo vimeandikiwa barua kisha vikaenda kuripoti kwake (Zitto), basi hilo linadhihirisha kuwa yeye ndiye amekuwa akivipotosha kila mara.

  "Kama waliandikiwa, wakaripoti kwako sasa tumejua wewe ndie Mhariri Mkuu unaewapotosha kila siku. Acha. "

Viongozi waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa klabu ya Yanga utakaofanyika mwezi Mei.

Omar al-Bashiri apelekwa Gerezani

$
0
0
Rais aliyeondolewa kwa nguvu madarakani nchini Sudan Omar al-Bashir amehamishiwa katika jela ya Kobar iliyopo kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum. Taarifa hiyo imetolewa na familia ya Bashir

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Bashir alikuwa akishikiliwa chini ya ulinzi mkali katika makaazi ya rais baada ya kuondolewa kwake madarakani na jeshi Aprili 11.

Wakati huohuo waandamanaji bado wanaendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi wakitowa mwito wa kuundwa serikali ya kiraia na jeshi kujayakabidhi madaraka kwa amani.

Rais wa TFF ajibu tuhuma za kupokea rusha ya Tsh. Milioni 46 kutoka kwa Rais wa CAF.

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Wallece Karia amekanusha taarifa zilizoenea kwenye mitandao kuanzia jana kuwa alipokea rushwa ya Tsh. Milioni 46 kutoka kwa rais wa shirikisho la soka barani Afrika kwa hivi sasa, Ahmed Ahmed ili aweze kumuunga mkono katika uchaguzi wa shirikisho hilo.

Karia akizungumza kwa njia ya simu na Television ya taifa (TBC) amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote kwasababu yeye hakuwepo madarakani wakati uchaguzi wa CAF unafanyika na kumuweka Ahmed kwenye kiti cha urais.

“Kwanza kwenye mitandao hiyo ambayo ina-trend haijataja jina langu imesema Tanzanian FA president, lakini watu wamitandao ya Tanzania wamebadilisha wameweka jina langu, lakini kipindi hicho wakati Ahmed Ahmed anaingia kwenye uchaguzi mimi sikuwa rais, na nna uhakika pia kwasasabu ukisoma ule mtandao unasema huyo rais wa shirikisho hakupata hiyo hela’’ amesema Karia.

Aidha, Karia ameongeza kuwa kilichopelekea jina lake kutajwa kwenye sakata hilo ni chuki binafsi za watu wanaopingana na utendaji wake wa kazi ndani ya Shirikisho hilo.

TCRA Yaziagiza Kampuni Za Simu Kuzuia Meseji Za Matapel

$
0
0
NA FAUSTINE GIMU GALAFONI,DODOMA
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kanda ya kati imeziagiza kampuni za mawasiliano kuzuiya meseji za matapeli zinazotumwa kwa watu kabla hazijafika kwa wananchi ili kudhibiti matukio ya namna hiyo.

Pia mamlaka hiyo imesema ili kukabiliana na makoa ya mtandao watapambana na kampuni za mawasiliano nchini pindi watakapobaini mtu anatumia line bila kusajiliwa kwa mfumo wa alama za vidole.

Mkuu wa TCRA kanda ya kati Dodoma Antonio Manyanda ameyasema  hayo jijini hapa  wakati wa mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano mkoani hapa ulioandaliwa na maamlaka hiyo kwa lengo la kujadili changamoto zilizopo pamoja na kuangalia namna ya kukabaliana nazo.

Akifungua mkutano huo kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema wahalifu hao wana mtandao mkubwa hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini ili kuepuka kutapeliwa huku akisema wapo ambao wanatuma meseji wakitumia majina ya viongozi wakubwa ili kutapeli.

Muroto ametumia nafasi hiyo kuwatahadharisha wale wote wanaojihusisha na utapeli kupitia mitandao ya mawasiliano kuwa pindi watakapokamatwa watashughulikiwa bila kigugumizi.

Amesema wanaangalia namna ya kupunguza kama si kumaliza kabisa makosa ya mtandao kwani kwa sasa uhalifu umehamia kwenye mitandao ya mawasiliano na kuwa wamejipanga ukabiliana na watu wa aina hiyo.

Watumishi Wizara Ya Fedha Na Mipango Watakiwa Kuboresha Zaidi Mifumo Ya Ukusanyaji Mapato Ya Serikali

$
0
0
Na Farida Ramadhani & Josephine Majura. WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji , amewataka  Watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato ya ndani na kupanua wigo wa walipakodi pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, wizarani hapo.

Alisema Wizara ya Fedha na Mipango imebeba majukumu ya  kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali na matumizi ya rasilimali fedha yanasimamiwa kikamilifu.

 “Watendaji na watumishi wote wa Wizara wanawajibu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha na ufuatiliaji wa matumizi ili kuhakikisha rasilimali fedha zilizopo zinatumika kwa ufanisi” ,alisema Dkt. Kijaji.

Alisema ni jukumu la Watumishi wa Wizara kugawa rasilimali fedha kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016-2021)  wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu.

Aliwataka Watumishi  kufanyakazi kwa ushirikiano, umoja , mshikamano, ufanisi  na uadilifu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyopo.

“Ni wajibu wetu pia kutumia busara na hekima, hususan pale tunaposhughulikia maslahi ya watumishi na wananchi kwa ujumla”, alisisitiza Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Doto James, amemhakikishia Dkt. Kijaji kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa haraka na ukamilifu kwa maendeleo ya nchi kwa kuwa Wizara hiyo ni nguzo ya kusimamia uchumi wa nchi.

Alisema uzoefu unaonesha kwamba vikao vya Baraza la wafanyakazi vimekua na umuhimu mkubwa mahala pa kazi na kwa kuzingatia umuhimu huo Wizara ya Fedha na Mipango imehakikisha kuwa vikao vya Baraza vinafanyika kila mwaka kulingana na Mkataba kati ya Wizara na Chama cha Wafanyakazi cha Serikali na Afya (TUGHE).

Alisema kupitia Baraza la wafanyakazi Wizara imefanikiwa kuongeza mshikamano kati ya Wafanyakazi hivyo kuamsha ari kwa watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali.

Aliongeza kuwa hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwenye Baraza zimeboresha huduma kwa watumishi, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo kuwapatia watumishi vitendea kazi pamoja na kuwelimisha watumishi kuhusu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu (BP), Kifua kikuu, HIV na UKIMWI.

Ofisa oparesheni mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Atoa Ushahidi Kesi ya Freeman Mbowe na Wenzake

$
0
0
Ofisa oparesheni mkoa wa kipolisi wa Kinondoni ambaye  ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Gerald Ngiichi ameieleza mahakama hiyo kuwa aliamuru askari kupiga risasi hewani kwa ajili ya kutawanya maandamano ya viongozi na wafuasi CHADEMA.

Ushahidi huo ambao wa kwanza kutolewa katika kesi hiyo, SSP Ngiichi alidai kuwa aliamuru risasi zipigwe kwa sababu njia ya kutumia mabomu ya Moshi ‘Machozi’ ilishindikana kuwatanya.


"Nililazimika kutumia njia ya mwisho ya kutumia silaha za moto kupigwa hewani kutoka na waandamanaji kutotii ilani tatu nilizozitoa katika umati huo wa waandamanaji kwa kutumia kingo'ra nikiwa katika gari la  polisi," alidai Ngichi.

Alidai kabla ya kutumia njia ya mwisho ya kuamuru askari wake wa vikosi vya doria kupiga risasi juu, aliamuru kikosi cha askari walikiwapo katika eneo hilo kupiga mabomu ya moshi kwa ajili ya kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wanaongozwa na viongozi wa chama hicho.

Alidai wakati askari wake wakiendelea kurusha mabomu ya moshi kwa waandamanaji hao, hawakufanikiwa vizuri kutokana na moshi wa mabomu hayo kuelekea  upande walipo askari hao.

"Zoezi la  kupiga  mabomu waandamanaji hao lilikuwa  hafifu kutokana na moshi kuelekea  upande walipo askari badala ya kwenda kwa  waandamanaji kutokana na  upepo uliokuwapo eneo hilo hali iliyopelekea waandamanaji kutosambaratika" alidai Ngichi.

Alidai katika harakati za kurusha mabomu kwa waandamanaji hao,  askari polisi wawili ambao ni PC Fikiri na Koplo Rahim waliokuwapo eneo la tukio walijeruhiwa kwa mawe na kuanguka chini.

"Baada ya kuanguka chini askari hao niliamuru askari wengine watoe msaada kwa majeruhi hao kwa kuwaondoa katika eneo hilo na niliamuru kikosi cha mabomu kirudi  nyuma na kikosi cha risasi kisonge mbele ili kukabiliana na waandamanaji hao," alidai.

Alidai askari wenye silaha walisogea mbele na kupiga  risasi hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliokiwa wanataka kuchukua silaha baada ya askari wake wawili kujeruhiwa na kuanguka chini.

"Risasi zilivyopigwa hewani kishindo kulikiwa  kikubwa hali iliyopelekea watu wengi kukimbia akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, sikujua  kama mheshimiwa Mbowe anajua kukimbia namna hiyo," alidai Ngichi

Pia amedai, baada ya waandamanaji kusambaratika, alifanya tathmini na kubaini kuna majeruhi wawili ambapo alikuwepo Akwilina aliyewahishwa Hospitali ya Mwananyamala na baadae kuripotiwa kuwa amefariki.

Ngiichi ambaye ni Ofisa Operesheni wa Kipolisi Kinondoni, na shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa chama hicho ameyaeleza hayo wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 13, 14 na 15, 2019 kwa ya kuendelea kusikilizwa.

Rais Magufuli atoa wiki moja kwa Wizara ya Ardhi

$
0
0
Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wiki 1 kwa Wizara ya Ardhi, na Wizara ya Viwanda na Biashara kukamilisha taratibu za uwekezaji kwa kampuni Sugar Investment Trust (SIT) ya Mauritius ambayo imecheleweshwa kuwekeza katika uzalishaji wa sukari tangu mwaka 2017.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 17 Aprili, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw. Gansam Boodram aliyeongozana na Balozi wa Mauritius hapa nchini Mhe. Jean Pierre Jhumun.

Katika mazungumzo hayo Bw. Boodram ameeleza kuwa yupo tayari kulima ekari 25,000 za mashamba ya miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari na kwamba uwekezaji huo utawezesha kuzalishwa kwa tani 125,000 za sukari, ajira za kudumu 3,000 na ajira za muda 5,000 lakini amekwama kuendelea kutokana na kusubiri majibu ya Serikali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu upatikanaji wa eneo la uzalishaji wa miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari.

Ameagiza ufanyike uchambuzi wa haraka katika maeneo ya Bonde la Mto Rufiji Mkoani Pwani, Eneo la shamba la Mkulazi Mkoani Morogoro na eneo la Kibondo Mkoani Kigoma ili mwekezaji huyo apatiwe na kuanza mara moja uwekezaji kwa kuwa nchi inahitaji kuongeza uzalishaji wa sukari utakaomaliza upungufu wa tani zaidi ya 100,000 ambazo kwa sasa zinaagizwa kutoka nje ya nchi.

Aidha Rais Magufuli amemuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Edward Mhede kufuatilia makubaliano ya ushirikiano katika uvuvi kati ya Tanzania na Mauritius ambayo hayajatiwa saini tangu mwaka 2017 licha ya wawekezaji wa Mauritius kuonesha nia ya kutaka kuwekeza katika uvuvi na viwanda vya samaki.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 18

Suala La Wafungwa Wajawazito Lazua Gumzo Bungeni....Serikali Yasema Inawajali Pamoja Na Watoto Wanaozaliwa Magerezani.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imesema itaendelea kuwajali wanawake , wafungwa wajawazito kwa kuwapatia huduma zote  anazopaswa kupatiwa mama mjamzito.
 
Hayo yamesemwa  April 17 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe.Kangi Lugola wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum mhe.Angelina Adam Malembeka aliyehoji ,baadhi ya akina mama wajawazito huingia gerezani  wakiwa wajawazito na kujifungulia gerezani  je,ni huduma gani hupata ili kuhakikisha anajifungua salama.
 
Katika majibu yake Mhe.Lugola amesema jeshi la Magereza limekuwa likitoa huduma za afya ,chanjo na kuhakikisha wanahudhuria kliniki ya akina mama wajawazito katika vituo vya afya vya magereza.

Aidha amesema jeshi la magereza limekuwa likiwapatia wafungwa wajawazito vyakula vinavyohitajika kiafya kwa kuzingatia maelekezo  na ushauri wa madaktari wa  Magereza.
 
Katika swali lake la nyongeza Mhe.Malembeka   amehoji ,Serikali inawasaidiaje watoto wanaozaliwa magerezani kisaiklojia  na kielimu na kwanini pasiruhusiwe vifungo vya nje  kwa akina mama wajawazito na wenye watoto ili waweze kulea watoto wao vizuri.

Akijibu Swali hilo,mhe.Lugola amesema kuna utaratibu watoto wanaozaliwa Magerezani  wamekuwa wakisoma shule za awali zilizoko magerezani  na wanawake wafungwa wenye vifungo  chini ya miaka mitatu kuna sheria ya “Probation for Offender  “pamoja na sheria ya “Community Services “ ambapo pia huwa na utaratibu wa kuwaondoa wafungwa wajawazito na wenye watoto  ili wawe na vifungo mbadala.
 
Hata hivyo watoto wanaoishi Magerezani wanapokuwa wakubwa na kufikia umri wa kuishi bila mama zao ,ndugu zao wamekuwa wakishirikishwa ili waweze  kutoa malezi kwa watoto ambao mama zao wako magerezani.
 
Katika hatua nyingine Waziri Lugola amesema sheria,taratibu na mila za kitanzania ,Serikali haiwezi kuruhusu wafungwa walio katika ndoa kufanya mapenzi magerezani.

Mke wa Kisena kuunganishwa na mumewe kesi ya uhujumu uchumi

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Aprili 23 kumuunganisha, Florencia Membe mke wa Robert Kisena katika kesi ya  uhujumu uchumi inayomkabili mumewe na wenzake watatu.

Membe ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Zenon Oil Gas Limited, anakabiliwa na mashtaka saba
ikiwamo uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha zaidi ya Bilioni 2.4.

Alifikishwa mahakamani hapo wiki iliyopita, akikabiliwa na mashtaka  hayo.

Kuunganishwa kwa Kisena na mkewe kulielezwa jana na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili Wankyo alieleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa lakini washitakiwa wawili ambao ni Kulwa Kisena na Charles Seleman hawajafika wanaumwa

Pia ameeleza kuwa upelelezi shauri hilo haujakamilika, kwa sababu baadhi ya washitakiwa wanatafutwa na mmoja ambaye ni Mke wa Kisena amepatikana na watamuunganisha na mumewe.

"Upelelezi bado haujakamilika kwa sababu bado tunaendelea kutafuta washtakiwa wengine na niseme tu tumeshampata mmoja ambaye ni Florencia Membe, hivyo tunaomba tarehe ijayo aunganishwe katika kesi hii ya uhujumu uchumi namba 11/2019 inayomkabili mumewe na wenzake watatu," alieleza Simon.

Hakimu Simba alikubaliana na ombi la  upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Aprili 23 itakapotajwa.


Kisena na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka 19 likiwemo la utakatishaji fedha na kuusababishia Mradi wa UDART hasara ya zaidi ya Sh.Bil 2.41

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kulwa Kisena(33), Charles Newe(47) na raia wa China, Cheni Shi (32).

Serikali Imeajiri Watumishi Wa Afya 52 Katika Hospitali Ya Rufaa Mkoa Wa Singida.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali kupitia wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kwa kushirikiana na ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora kwa mwaka wa fedha 2018/2019 imeajiri watumishi wa kada mbalimba za afya 52 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida hivyo kupunguza tatizo la upungufu wa watumishi na kufikia asilimia 45.

Kauli hiyo imetolewa April 17 ,2019  bungeni jijini Dodoma na naibu wa ziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto dkt faustine ndugulile wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu AishaRose ndogoli matembe lililohoji serikali inampango gani wa kuipatia hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida watumishi wa kutosha hasa ikizingatiwa hospitali hiyo ni tegemeo la watu wengi hususani kina mama wajawazito.

Dkt ndugulile amesema kwa mwaka wa fedha 2019/2020 wizara inategemea kuomba kibali cha kuajiri watumishi 197 wa kada mbalimbali za afya kwaajili ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida.

Katika swali lake la nyongeza mbunge matembe amehoji kwa kuwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida inahudumia zaidi ya wagonjwa 300 kwa siku na inatoa huduma katika maeneo mawili tofauti ambayo ni hospitali ya zamani iliyopo kata ya ipembe na hospitali mpya ya rufaa iliyopo kata ya mandewa je serikali inampango gani wa kuhakikisha inapeleka fedha za kutosha ili kumaliza ujenzi katika hospitali mpya ya rufaa ya mandewa.

Akijibu maswali hayo ya nyongeza dk ndugulile amesema wao kama serikali wamezipokea hospitali hizo za rufaa za mikoa na kusudio lao ni kuhakikisha wanaziboresha ili ziweze kutoa huduma za kibingwa kama ilivyokusudiwa.

Katika hatua nyingine naibu waziri ndugulile amemuelekeza mganga mkuu wa mkoa wa geita kuhakikisha wataalamu wote wa afya waliopelekwa na serikali ambao hawapo katika kituo cha kazi ilihali wapo mjini kuhakikisha wanafika mara moja katika hospitali ya nzela wilayani geita kuanza kutoa huduma kwa wananchi
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images