Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Ataka Tatizo La Taasisi Kuingiliana Majukumu Litatuliwe

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bibi Jenista Mhagama akutane na mawaziri wa sekta nyingine na watafute namna ya kuondoa mkanganyiko uliopo kwenye vyombo vya udhibiti hapa nchini.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Jumanne, Aprili 9, 2019) Bungeni jijini Dodoma, kwenye mkutano wa 15 wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2019/2020.

Alikuwa akitoa ufafanuzi juu ya masuala yaliyogusa vyombo vya udhibiti kama vile Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka nyingine za udhibiti pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), OSHA, BRELLA na Taasisi ya Mionzi ambayo yaligusiwa na Waheshimiwa Wabunge.

Alisema licha ya Serikali kujenga mazingira wezeshi na rahisi ya kufanya biashara na uwekezaji, bado kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara na wawekezaji kama walivyoeleza Waheshimiwa Wabunge wakati wa kuchangia hoja hiyo.

“Changamoto nyingine ambayo imeonekana kuwa kikwazo cha biashara na uwekezaji ni muingiliano wa majukumu ya taasisi hizo. Kwa mfano, uwepo wa majukumu yenye kufanana kwa TFDA, TBS, Mkemia Mkuu wa Serikali, Bodi ya Maziwa, Bodi ya Nyama, Baraza la Mifugo, EWURA, SUMATRA na TANROADS ni kikwazo kikubwa katika kurahisisha mazingira ya kufanya biashara,” alisema.

Alisema Serikali imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu mamlaka hizi na namna ya utendaji kazi wake. Miongoni mwa kero hizo ni mchakato wa muda mrefu wa kupata leseni za biashara; gharama za usajili wa bidhaa zinazotozwa na TFDA; suala la viwango vya TBS; madai ya kuwepo kwa unyanyasaji unaofanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kushirikiana na polisi dhidi ya wafanyabiashara.

Pia walibainisha changamoto nyingine kuwa ni umbali wa kutoka makao makuu na maabara za taasisi ya mionzi hadi eneo wanalofanyia kazi kama vile bandari na viwanja vya ndege.

“Tayari nimeshatoa maelekezo na yameanza kufanyiwa kazi na Waheshimiwa Mawaziri wa sekta husika chini ya uratibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) kwamba wakae pamoja kupitia sheria na mgawanyo wa majukumu wa taasisi za udhibiti ili kuondoa mkanganyiko uliopo sasa” alisema.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza mawaziri husika wahakikishe kuwa wakuu wa Mamlaka ya Mapato na taasisi zake, wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia sheria bila kuwabughudhi wafanyabiashara na wawekezaji.

Wakati wa mjadala huu, wabunge 142 walichangia hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo kati ya hao, wabunge 98 walichangia kwa kuzungumza moja kwa moja bungeni na wabunge 44 walichangia kwa njia ya maandishi.

Bunge lilikubali kupitisha sh. 148,886,523,581/- kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2019/2020. Kati ya hizo, sh. 86,290,355,000/- ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 62,596,168,581/- ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Vilevile, Bunge liliidhinisha sh. 124,182,537,600 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo kati ya hizo sh. 116,573,026,000/- ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 7,609,511,600/- ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Mbarawa Amtumbua Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Mtwara

Serikali Kuimarisha Kitengo cha Watu Wenye Ulemavu

$
0
0
NA.MWANDISHI WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha kitengo kinachoshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu ili kuendana na mahitaji halisi nchini.

Ameyasema hayo hii leo Aprili 09, 2019 alipokuwa akijibu hoja Bungeni Dodoma ikiwa ni moja ya hoja iliyotolewa kuhusu uboreshwaji wa kitengo hicho ili kuendelea kuongeza nguvu katika kushughulikia mahitaji ya kundi hilo.

Naibu Waziri alieleza kuwa Ofisi yake imejipanga kuhakikisha inaboresha kitengo hicho kwa kuendelea kuwajengea uwezo watumishi na kuongeza watumishi watakaohudumia makundi hayo.

“Serikali imeoa ipo haja ya kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hiki wanaosimamia na kuratibu masuala ya watu wenye ulemavu ili kuongeza nguvu na kuboresha utendaji,”alisema Ikupa

Aliongezea kuwa, umuhimu wa kuongeza watumishi utasaidia kuendana na mahitaji halisi ya kundi hilo na kupunguza changamoto zilizopo kwa sasa.

Katika kuendelea kuboresha utekelezaji wa masuala hayo Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kuandaa mazingira wezeshi ikiwemo kuanzishwa kwa Mfuko wa Taifa kwa Watu Wenye Ulemavu utakaosaidia kushughulikia masuala  ya ruzuku za vyama vya watu wenye ulemavu, kuwezesha programu za elimu na mafunzo, kuwezesha huduma za utengamavu kwa watu wenye ulemavu pamoja na kutumika katika tafiti mbalimbali.

“Kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 jumla ya shilingi Milioni 103 zimetengwa kwa ajili ya Mfuko huo ambazo zitakuwa ni mbegu kwa mfuko hivyo ni vyema sasa kukawa na wadau wataochangia kutunisha mfuko huu,”alisisitiza Ikupa

Aidha, Serikali imeendelea kutoa elimu kwa mamlaka mbalimbali kuhusu ujenzi wa miundombinu rafiki inayoendana na makundi ya watu wenye mahitaji maalum nchini ili kuondokana na changamoto za uwepo wa miundombinu isiyoendana na mahitaji halisi kwa kundi hilo.

”Suala la Miundombinu ni la kila mtu hivyo basi ni vyema tukahakikisha kunakuwa na ujenzi unaozingatia uhitaji wa wenye ulemavu ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza”, alisisitiza Ikupa

Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuwasilishwa rasmi Bungeni leo

$
0
0
Leo Jumatano Aprili 10, 2019 Bunge la Tanzania litawasilishiwa hati ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Orodha ya shughuli za Bunge leo Jumatano, Aprili 10 inaonyesha taarifa hiyo ya fedha ya mwaka wa fedha 2017/18 itawasilisha bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisa ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ikiwa ni siku ya saba tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Aprili 2, 2019. Hata hivyo orodha hiyo inaweza kubadilika.

Wakati taarifa hiyo ikiwasilishwa, jana Jumanne, Aprili 9 jioni ofisi ya CAG ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa leo Profesa Assad atakuwa na mkutano na waandishi kueleza yaliyomo katika taarifa yake ya ukaguzi.

“Nawakaribisha katika ukumbi wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (Naot) ghorofa ya pili. Jengo lipo nyuma ya jengo la hazina (Dodoma). Karibuni nyote msihofu,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ya mwaliko..

Shahidi: Nyama Na Nywele Sehemu Za Siri Zilithibitisha Uhusiano Wa Mwanafunzi Humphrey Makundi Na Wazazi Wake.

$
0
0
Na Dixon Busagaga
Mkemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ,Hadija Mwema ameieleza mahakama kuu kanda ya Moshi  kuwa Vinasaba (DNA) vya sampuli zilizochukuliwa katika mwili wa anayetajwa kama Humphrey Makundi vimeshabihiana na Vinasaba (DNA)  vya Joyce na Jackson Makundi ambao wanatajwa kama wazazi wa marehemu .

Dkt Mwema ambaye ni shahidi wa 12 katika shauri la mauji ya kukusudia ya Mwanafunzi Humphrey Makundi aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scholastica aliieleza makama kuwa sehemu iliyotoa majibu ya vipimo vya DNA ilikuwa ni Nyama na Nywele katika sehemu ya uume vilivyolinganishwa na Ute wa mate pamoja na Damu vya Joyce na Jackson Makundi.

Eneo la sehemu ya nyama na Nywele katika eneo la uume ni miongoni mwa sampuli zilizotumika kwa ajili ya vipimo kati ya sampuli 15 ambazo 10 kati ya hizo zilichukuliwa mwilini huku nyingine zikiwa ni viatu na nguo.

Baadhi ya sampuli nyingine zilizotajwa mahakamani hapo katika ripoti ya vipimo vya DNA,ni pamoja na Ngozi ya Kisigino,Mfupa wa Paja,Mfupa wa Kifua ,kipande cha nyama ya tako,viatua jozi mbili ,maji mazito yanayopatikana katikati ya mfupa vyote hivi vikiwa ni vya marehemu.

Mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu,Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi,Dar Es Salaam ,Firmin Matogoro ,shahidi huyo aliiomba mahakama kuu kanda ya Moshi kupokea Ripoti ya Vipimo vya Vinasaba (DNA) iwe sehemu ya kielelezo katika ushahidi wake ambacho kilipokelewa na kupewa namba nne.

Akiongozwa na Wakili wa serikali Mwandamizi ,Abdalah Chavula ,Mwema alieza kuwa baada ya kufanya vipimo vya Sampuli mbalimbali matokeo yaliyoonesha zilichukuliwa katika mwili wa Binadamu.

Mapema Shahidi wa 11 katika shauri hilo linalovuta hisia za watu ,Jackson Daudi aliyejitamburisha kama mbebaji wa mizigo katika kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Moshi Ciment aliwasilisha Panga mahakamani hapo lipokelewe kama kielelezo katika ushahidi wake.

Akiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Joseph Pande ,Daudi ambaye wakati huo alikuwa akifanya shughuli ya ulinzi katika shule ya sekondari ya Scholastica iliyopo Himo katika wilaya ya Moshi ambako alikuwa akisoma mwanafunzi Humphrey Makundi.

Alieleza kuwa Novemba 9 mwaka 2017 alifika katika shule hiyo akitokea Kahama ,mkoani Shinyanga ambako alifanya kazi ya ulinzi katika kampuni ya Solex Security Ltd kabla ya kukutana na mtu aliyemtaja kama mtoto wa Edward Shayo ambaye alimuunganisha kwenda kufanya kazi katika shule hiyo.

Daudi aliileza Mahakama sababu za kuacha kazi katika kampuni yake hiyo ya awali ilikuwa ni kutofautiana na muajiri wake baada ya kushindwa kumlipa mshahara wa mwezi mmoja ndipo alipoamua kuchukua vitu katika kampuni yake na kuvipeleka kituo cha Polisi.

“Baada ya kuelewana na mwajiri wangu na kunipa pesa na kutoka kituoni ,nilikutana na mtoto wa Edward Shayo anaye ishi wilaya ya Kahama ,ni Traffic ,akaniambia atanipeleka kufanya kazi kwenye shule ya baba yake”alieleza Daudi.

Alieleza kuwa Novemba 10,2017  ikiwa ni siku ya pili tangu kufika shuleni hapo alikutana na  Edward Shayo  aliyewauliza kama walielewana bei ya kufanya kazi na majibu yake yalikuwa ni hapana.

“Alituuliza ,Mlitaka mlipwe shilingi ngapi ? tukamjibu  shilingi laki mbili “alieleza Daudi huku Wakili Pande akitaka kujua walikuwa wangapi ndipo akaeleza kuwa walikuwa wawili yeye na mwenzake aliyemtaja kwa jina moja na Thomas.

Alieleza kuwa Edward Shayo aneyatajwa kama mmiliki wa shule hiyo aliwawambia kuwa atawalipa shilingi laki moja na wao walimueleza kuwa awalipe kiasi cha sh laki moja na ishirini kiwango ambacho alikubaliana nacho na kutoa maelekezo ya kumuona mtu aliyeitwa Chacha.

“Chacha alikuwa n mlinzi ,baada ya kumuona tukaambiwa nendeni mkapumzike mida ya saa 12 twende tuakaonyeshwe eneo la kazi ,tulikabidhiwa nguo za kazi “alieleza Daudi.

Daudi ambye mkewe anafanya kazi ya usafi katika shule ya sekondari ya Scholastica alieleza kuwa utaratibu waliopewa haukuwa wa kulinda wezi na kwamba walilinda wanafunzi wa shule na kwamba hata wangeingia wezi wangepambana nao.

“Thomas rafiki yangu alibaki pale getini,mimi na Chacha tukaanza kuzunguka maeneo ya shule ,sikuwa na kitu chochote ,Chacha alikuwa akitumia Panga na Rungu “alieleza Shahidi huyo.

Alieleza kuwa Novemba 17,2017 baada ya kutoka eneo lao la kazi walienda kupumzika na Chacha  na baadae mtu aliyemtaja kwa jina la Mcha Mungu aliyekuwa mlinzi wa getini  alifika na kuwaita bila ya kuaeleza kuwa wanaitwa na nani.

“Tuliendelea kulala,Mchamungu akatuaita mara ya pili ,akaita tena Chacha Chacha mnaitwa ,tukaulizwa tunaitwa na nani? Akatuambia mnaitwa na maaskari ,tukaenda getini tukakuta askari wa kike “trafiki “ “alieleza Daudi .

Shahidi huyo alieleza kuwa baada ya kufika yule Askari aliuliza anaitwa nani ndipo alipomtajia majina yake ya Jackson Evarlist Daudi na kueleza kuwasio yeye huku akiluza Chacha ni nani.

“Alipouliza Chacha nikamnyooshea kidole huyo hapo,akauliza na Mchamungu? Nikamnyooshea kidole huyo hapo na siku hiyo ilikuwa ni zamu ya Mchamungu kukaa getini” alieleza Daudi.

Mnamo Novemba 18 ,2017 majira ya saa mbili za usiku ,Daudi alieleza kuwa ilifika gari aina ya Landcruser ikiwa na vioo vyeusi ndipo alipofungua mlango mdogo katika geti la kuingia shuleni hapo ndipo aliposikia sauti ikimueleza kuwa hawaingii ndani.

“Walikuwa ni maaskari wakafungua mlango wa gari, wakamtoa Chacha,Chacha akawaongoza maaskari mpaka pale Panga lilipokuwa ,Panga lilikuwa kwenye kabati ndani ya Chumba cha Mlinzi ,kilichopo geti kuu lakuingia shuleni”alieleza Daudi.

“Walivyokuta Panga askari wakaniuliza tangu nifike hapo sijawahi kulishika hilo Panga au kulikamata nikasema hapana,nikaulizwa Panga la nani? Chacha mwenyewe kwa kinywa chake akakili Panga la kwangu”aliongeza Daudi.

Alieleza kuwa kuna Rungu lilikuwa juu ya meza ambapo pia askari walitaka kujua endapo nimewahi kulishika na majibu yalikuw ani hapana na kwamba baada ya hapo walipiga picha Panga na Rungu kisha wakaongozana na Chacha wakiwa na vitu hivyo.

Daudi alieleza muonekano wa Panga ulikuwa wa rangi nyeusi huku likiwa imemeguka kidogo huku akiionesha mahakama Panga hilo na baadae kuiomba mahakama itoe adhabu kutokana na Panga hilo.

Baada ya kutoa maelezo hayo Wakili Mkuu wa Serikali ,Pande aliwasilisha ombi mbele ya mahakama kupokea Panga hilo liwe sehemu ya kielelezo katika ushaidi wa Daudi jambo ambalo lilizua mabishano ya kisheria kwa pande zote mbili.

Wakili wa kujitegemea ,Gwakisa Sambo akiwasilisha ombi kwa Jaji,Mfawidhi,Matogoro alieleza kupinga ombi hilo akieleza sababu ya kuwa Wakili Pande si shahidi wa kutoa kielelezo hicho.

“Maombi yetu kwa upande wa prosecutor ,ni mahakama hii na mahakama zetu nchini ni shahidi pekee yake ambaye anaweza kuleta ombi hilo ,hivyo basi tunaomba ombi lake likataliwe.

Baadae alisimama wakili Pande na kuunga mkono hoja ya Wakili Sambo huku akileza kuwa ni kweli anayetoa kielelezo ni shahidi lakini anayeomba kielelezo kipokelewe ni upande wa Jamhuri na kwamba hivyo ni vitu viwili tofauti.

Shauri hilo linaendelea katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi,ambapo mashahidi wa upande wa jamhuri wameendelea kuwasilisha ushahidi wao.

Shauri la mauaji  ya mwanafunzi  Humphrey Makundi aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika  sekondari ya Scolastika imeanza kusikilizwa mfululuzo  likimkabili mmiliki wa shule hiyo ,Edward Shayo,Mwalimu wa nidhamu Labani  Nabiswa  na mlinzi wa shule ,Hamis Chacha.

 Upande wa Jamhuri katika Shauri hilo unawakilishwa na Wakili wa serikali Mkuu ,Joseph Pande,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Abdala Chavula,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Omary Kibwana  na Wakili wa serikali Lucy Kiusa.

Upande wa utetezi unawakilishwa na Wakili wa kujitegemea Elikunda Kipoko na Gwakisa Sambo wanaomtetea  mshtakiwa wa pili ,Wakili wa kijitegemea David Shilatu anayemtetea mshitakiwa wa kwanza na Patrick Paul anaye mtetea mshtakiwa wa tatu.

Mwisho.

Bofya Hapa Kuisoma Ripoti yote ya Mwaka 2017/2018 ya CAG Prof. Assad.....Imetolewa Leo

$
0
0
Leo Jumatano,  April 10, 2019 Tovuti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imechapisha Ripoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Juu ya Taarifa za Fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Bonyeza Hapo chini kuisoma


《《RIPOTI YA CAG MWAKA 2017/2018》》

Rais Magufuli Aibua Kashfa ya Stampu Hewa za Bilioni 10 TRA

$
0
0
Rais Magufuli amesema Wahujumu uchumi wamewahi kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutengeneza stampu hewa za Bilioni 10.

Amesema stampu hizo baada ya kutengenezwa zilisambazwa katika viwanda nchini kupitia ushirikiano wa baadhi ya wafanyakazi wa TRA.

Kauli hiyo ameitoa jana Jumanne Aprili 9, 2019 akifungua kiwanda cha majani ya Chai katika kijiji cha Kabambe mkoani Njombe, ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye mikoa mbalimbali nchini.


“Kwenye suala hili la kodi hasa kwenye vinywaji kama vile bia, konyagi na spirit (vinywaji vikali) nyingine hili kidogo ni very complex (linachanganya) ndio maana Mwenyekiti hakuzungumza tulikuwa tunakusanya kiasi gani, angezungumza hilo tungekuwa tunagonga stampu tungekuwa tunakusanya ngapi, tungepata jibu vizuri.

“Hatukusanyi kitu katika eneo ambalo tumepigwa sana ni hilo la vinywaji, kwa hiyo Serikali inakosa pesa hakuna mahali tulipata pesa, lazima sasa tutafute utaratibu mzuri ili hawa wenye viwanda vya vinywaji tusipoteze pesa zaidi” Alisema Rais Magufuli

Rais Magufuli atoa Milioni 10 kukamilisha ujenzi wa Wodi ya wakina Mama

$
0
0
Na. Amiri kilagalila, Njombe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhi fedha kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa Wodi ya kina mama katika kituo cha afya kifanya kilichopo  halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe.

Rais Magufuli  ametoa fedha hiyo mara baada ya kusikia changamoto ya afya inayowakabili wakazi wa kata hiyo, wakati akipokewa huku akitokea mkoani Ruvuma

"Hapa sasa hivi mmenieleza mmejenga kituo chenu cha afya na mmejenga wodi ya akina mama mmeshaezeka ila haijakamilika,mmenifurahisha kwa kuwa mmeanza vizuri hiyo wodi na mimi nawachangia milioni kumi ila zitumike vizuri,nitatuma watu wa kuja kuchunguza hizo milioni kumi zilivyoenda na atakayezila" alisema Magufuli

Aidha Rais Magufuli amesema anahitaji wodi hiyo ikajengwe kwa milioni kumi inatosha jengo hilo la akina mama huku akiagiza Tamisemi namna ya kuwapeleka manesi na madaktari mapema litakapokamilika jengo hilo.

Naye Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini, Edward France Mwalongo ameahidi kutoa mifuko 100 ya simenti huku diwani wa kata ya kifanya Nolasco Mtewele akiahidi Kuchangia mifuko mifuko 50 ya saruji kumuunga mkono Rais Magufuli katika kukamilisha ujenzi huo.

Awali Mbunge wa Njombe mjini Edward mwalongo alisema kuwa wananchi hao kwa kushirikiana na halmashauri walijitahidi kuchangia kituo hicho cha afya lakini bado hakijakamilika

"Mh Rais wananchi hawa kwa kushirikiana na halmashauri wamejitahidi sana kuchangia kituo cha afya na kituo chao kinatumika lakini hakijakamilika,wamejenga jengo la upasuaji limeshaezekwa  ndio tunaendelea nalo,wamechanga  milioni 30 na halmashauri kwa mapato ya ndani wamechangia milioni 30" alisema Mwalongo

Rais Magufuli: Muwekezaji anayetaka kujenga asihangaike, ukipata ardhi hata kesho anza kujenga

$
0
0
Na. Amiri kilagalila, Njombe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli ametoa wito kwa wawekezaji wanaohitaji kujenga kiwanda, kuanza muda wowote pindi watakapopata ardhi bila kusubili huku mambo mengine yakifuata.

Rais ametoa wito huo Mkoani Njombe wakati akizungumza na wananchi Mkoani Njombe mara baada ya kuzindua kiwanda cha kuchakata majani mabichi ya chai cha kabambe kilichopo Lwangu Halmashauri ya Mji wa Njombe Mkoani humo.

“Mtu anapotaka kuja kuwekeza muda mwingine anapata shida masharti ni ya ajabu ajabu na mimi nakubaliana na hilo baadhi ya watendaji wetu wamekuwa ni tatizo katika uwekezaji,wanamuona muwekezaji kama adui badala ya kumuona kama rafiki niwaombe watendaji wangu ndani ya serikali wabadilike,wapo wawekezaji ambao wamekuja hapa wakawekewa mikwara mpaka wakaenda nchi za jirani na wengine wakaombwa rushwa,wengine mara wanafuatwa na Nemc mara kuna Osha vimashariti vya hovyo vimekuwa vingi tunajichelewesha wenyewe”alisema Magufuli

“Sasa nikuombe mheshimiwa waziri na viongozi wengine tubadilike tunatakiwa twende speed nilishazungumza siku moja nilikuwa mkoa wa pwani narudia hapa muwekezaji yeyote anyetaka kujenga chochote asihangaike na mambo mengine yoyote wewe ukishapata eneo hata kesho anza yale mengine yaje baadaye”aliongeza Magufuli

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda,  Joseph Kakunda amesema kuwa kiwanda hicho cha chai kilichozinduliwa hii leo ni miongoni mwa viwanda 36 vya chai nchini ambapo kati ya hivyo viwanda 25 ni vya kusindika majani ya chai na viwanda 11 ni vya kuchanganya majani ya chai kwenye vikasha tayari kwa matumizi.

“Kiwanda hiki cha chai cha kabambe cha uniliver hapa Njombe  ni miongoni mwa viwanda 36 hapa Nchini na kati ya viwanda hivyo ni kiwanda kimoja tu cha Luponde huko Lushoto ambacho hakifanyi kazi tangu mwaka 2013 na tayari tumekirejesha serikalini tumekikabidhi juzi kwa pssf kwa ajili ya kukifufua”alisema Kakunda

Miongoni mwa watu wa waliofanikisha ujenzi wa kiwanda hicho ni pamoja na Rais wa wood foundation Iron wood amesema kuwa jitihada zao za kujenga kiwanda hicho ni pamoja na kuwasaidia wakulima wadogo ambapo mpaka sasa wameweza kuwasaidia wakulima wapatao 3000 wanaoweza kufikisha majani yao ya chai katika kiwanda hicho.

Mabasi 58 ya Mwendokasi yaondolewa barabarani,

$
0
0
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), imesema kuna uhaba wa mabasi yanayotoa huduma na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa usafiri huo.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano Aprili 10, 2019 kwa vyombo vya habari  na Meneja Uhusiano wa Umma wa Dart, William Gatambi imesema uhaba huo unatokana na mabasi hayo kupata hitilafu mbalimbali.

“Idadi ya mabasi yanayotoa huduma leo katika mfumo wa Dart ni 85, huku 58 yakifanyiwa matengenezo makubwa na madogo.

“Tunawaomba wateja wetu kuwa na subira wakati mabasi hayo yakifanyiwa matengenezo. Tunawaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza,”amesema Gatambi.

TAKUKURU Yamshitaki Mke wa Kisena wa UDART Florensi Mashauri Kwa Makosa Ya Uhujumu Uchumi na Utakatishaji Fedha

$
0
0
Mfanyabiashara, Florencia Mashauri ambaye ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil and Gas Limited amefikishwa Mahakamani leo na TAKUKURU kwa kujibu mashtaka ya wizi, uhujumu uchumi, ukiukwaji wa sheria ya mafuta juu ya ujengaji wa kituo cha uuzaji wa mafuta kwa UDART pamoja na makosa ya utakatishaji wa fedha haramu ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.2.

Mashauri ni mke wa mfanyabiashara Robert Kisena ambaye naye ana kesi ya uhujumu uchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi Takukuru, Kassim Ephrahim amewaeleza waandishi wa habari leo Aprili 10, 2019 kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jana.

Amesema katika uchunguzi wa Takukuru imebainika kuwa licha ya kampuni hiyo kusajiliwa kuingiza mafuta kwa wingi, haikuwahi kuagiza mafuta hayo na badala yake ilikuwa ikijihusisha na uuzaji wa petroli na dizeli kwa rejareja kwa kampuni ya Udart.

Ripoti ya CAG: Mapungufu Yaliyobainika katika Ukaguzi wa Vyama vya Siasa

$
0
0
==>>Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyobainika katika ukaguzi wa Vyama vya Siasa.
 
(a) Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilinunua gari jipya aina ya Nissan Patrol kwa Dola za Marekani 63,720 (sawa na shilingi milioni 147.76) ambalo lilisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya jina la Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA. 

Pia, gari hilo  lilioneshwa kwenye taarifa za fedha kama mkopo kwa mwanachama huyo bila kuwa na makubaliano ya mkopo yaliyosainiwa kati ya mwanachama na Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA.
 
(b) Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakikuwasilisha michango ya kila mwezi kwenda Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Hadi kufikia Mei, 2018 chama hicho kilikuwa na deni la shilingi bilioni 3.74 ambalo linajumuisha adhabu ya shilingi bilioni 2.73 iliyotokana na ucheleweshwaji wa uwasilishaji wa michango hiyo.
 
(c) Aidha, nilibaini kuwapo kwa tatizo la uendelevu wa biashara (Going concern) katika Kampuni ya Uchapishaji ya Uhuru inayomilikiwa na CCM. Pia, hati za ardhi za nyumba 199 zinazomilikiwa na CCM Zanzibar zilionekana hazijasajiliwa kwa jina la Bodi ya Wadhamini bali zimesajiliwa kwa majina ya maofisa wa Chama.
 
(d) Vyama saba vilifanya matumizi ya jumla ya shilingi milioni 777.91 bila ya kuwa na nyaraka toshelevu na hivyo nilishindwa kuthibitisha iwapo malipo hayo yalikuwa halali; na iwapo yalihusiana na shughuli za vyama hivyo. Vyama hivyo vimeainishwa katika Jedwali Na. 11
==>Mapendekezo kwa Serikali Kuu na Vyama vya Siasa
Ili kurekebisha kasoro nilizozibainisha, ninashauri yafuatayo:
(i) Serikali ifanye juhudi za makusudi kuziwezesha Mamlaka za Rufaa za Kodi ili kuhakikisha mashauri ya kodi yanashughulikiwa kwa wakati ili kupunguza mrundikano wa mashauri.


(ii) Serikali idhibiti mifumo ya ukusanyaji wa tozo za huduma za usafiri kwenye viwanja vya ndege na bandari. Pia, Serikali iimaishe udhibiti wa mafuta na bidhaa zinazoingia nchini kwa matumizi ya ndani, na zinazopita kwenda nchi nyingine ili kuhakikisha kuwa zinalipiwa kodi stahiki.


(iii) Serikali iimarishe udhibiti wa ndani katika kuhakiki mikopo iliyopokelewa na taasisi nufaika kabla ya kuingiza kumbukumbu za madeni kwenye mfumo ili kuondoa mapungufu katika usahihi wa taarifa.


(iv) Kupitia Maofisa Masuuli, Serikali iimarishe udhibiti na utaratibu wa kufanya mapitio ya uandaaji wa mafao ili kuhakikisha kuwa kanuni na vigezo vya ukokotoaji na sheria vinazingatiwa ili kuepuka ucheleweshaji wa mafao ya hitimisho la kazi na hasara kwa Serikali.


(v) Serikali itoe kwa wakati fedha za utekelezaji wa miradi ya barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania kama ilivyoidhinishwa na bunge ili kuepuka malipo ya ziada yanayotokana na riba.


(vi) Kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali ihamishe mali na madeni yote yanayohusiana na miradi ya barabara kwenda Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini; na Ofisi ya Rais - TAMISEMI inapaswa kufuatilia utekelezaji huo.


(vii) Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa iharakishe zoezi la usajili na utengenezaji wa vitambulisho vya Taifa. Pia, itathmini utendaji kazi wa mkandarasi ili kuweza kuamua iwapo imuongezee muda wa mkataba au iingie makubaliano na mkandarasi mwingine. 


(viii)Serikali kupitia Taasisi zake iepuke kufanya manunuzi toka chanzo kimoja au kushindanisha vyanzo vichache endapo bidhaa au huduma zinazotakiwa haziendani na zile zilizotajwa katika Kanuni ya 159 ya Kanuni za Manunuzi ya Umma za Mwaka 2013. Hii itasaidia kuwa na usawa na uwazi katika manunuzi ya Umma. Pia, ihakikishe kuwa manunuzi yote yanapata vibali vya Bodi za Zabuni kabla ya kufanyika kwa manunuzi ili kuhakikisha uwepo wa thamani ya fedha katika manunuzi.

(ix) Serikali ihakikishe malipo yote yanafanyika kwa mujibu wa mikataba iliyosainiwa baina ya Taasisi za Serikali na watoa huduma. Vilevile, Taasisi za Serikali zihakikishe zinadai na kupatiwa stakabadhi za kielektroniki pindi zinapowalipa wazabuni ili kuzuia ukwepaji wa kodi.


(x) Uongozi wa Vyama vya Siasa uhakikishe kuwa udhibiti unaanzishwa na kuimarishwa, hasa kwenye malipo, ili malipo yote yawe na vielelezo na nyaraka toshelezi, zikiwamo risiti za kielektroniki.

Ripoti ya CAG: Matokeo ya Ukaguzi wa Serikali Kuu

$
0
0
3.1 Utangulizi
Sura hii inawasilisha matokeo ya ukaguzi wa Serikali Kuu. Taasisi na Maeneo yaliyohusika na Ukaguzi ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania; Usimamizi wa Deni la Serikali; Udhaifu katika Malipo ya Mafao; na Ukaguzi wa Wizara, Idara, Wakala wa Serikali, Mifuko Maalumu, na Taasisi nyingine. Aidha, Sura hii inatoa mapendekezo kwa Serikali Kuu na Vyama vya Siasa.

3.2 Matokeo ya Ukaguzi wa Serikali Kuu
Ndugu Waandishi wa Habari,
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyojitokeza katika Ukaguzi wa Serikali Kuu. 

3.2.1 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Usimamizi wa Mapato Yatokanayo na Kodi
Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikusanya shilingi trilioni 15.38 ikilinganishwa na malengo yaliyowekwa ya kukusanya shilingi trilioni 17.31; hivyo kuwa na nakisi ya makusanyo kwa shilingi trilioni 1.93 ambazo ni sawa na asilimia 11 ya malengo. Jumla ya makusanyo hayo haikujumlisha shilingi bilioni 18.95 ambazo ni Vocha za Misamaha ya Kodi kutoka Hazina. Hivyo, makusanyo halisi ya mwaka 2017/18 ni shilingi trilioni 15.40 yakijumuisha na Vocha za Misamaha ya Kodi kutoka Hazina.

Kodi Zilizoshikiliwa katika Kesi za Muda Mrefu kwenye Mamlaka za Rufaa za Kodi
Mamlaka ya Mapato Tanzania ina Mashauri ya Kodi ya Thamani ya shilingi trilioni 382.6 kwenye Mamlaka za Rufaa za Kodi ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi trilioni 378.2 (asilimia 8595) ikilinganishwa na shilingi trilioni 4.4 kwa mwaka wa fedha 2016/17. Ongezeko hili limechangiwa kwa kiasi kikubwa na Mashauri manne yenye thamani ya shilingi trilioni 374.7 yanayoihusu Kampuni ya Uchimbaji Madini ya ACACIA.

Kutokukusanywa kwa Mapato Yatokanayo na Kodi ya Kiasi cha Shilingi Bilioni 46.81 na Dola za Marekani Milioni 2.74 
Ukaguzi wangu ulibaini kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ilishindwa kukusanya mapato zaidi ya shilingi bilioni 46.81 kutoka kwa walipakodi mbalimbali. Jedwali Na. 6 linabainisha taasisi, aina za kodi, na kiasi cha fedha ambacho hakikukusanywa.

Jedwali Na. 6: Taasisi ambazo Hazikukusanya Mapato Yatokanayo na Kodi 

Udhibiti Usioridhisha wa Bidhaa Zinazopitia Nchini na Zinazosafirishwa Nje ya Nchi

Ndugu Waandishi wa Habari,
Wakati wa uhakiki wa bidhaa zinazoingizwa Nchini na Nchi jirani ili zisafirishwe kwenda Nchi nyingine, Mamlaka ya Mapato Tanzania ilishindwa kunipatia ushahidi kuthibitisha kuwa kodi ya shilingi bilioni 57.09 ililipwa.

Aidha, nilibaini kuwa bidhaa zilizosafirishwa kutoka Nchini kwenda Nchi nyingine zilizopaswa kutozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani ya shilingi milioni 649.45 ziliruhusiwa kwenda nje ya Nchi bila kukamilisha taratibu za Forodha. Mamlaka ya Mapato Tanzania ilishindwa kutoa ushahidi wa nyaraka za kuthibitisha kuwa kodi stahiki zilikusanywa. 

3.2.2 Usimamizi wa Deni la Serikali
Kufikia tarehe 30 Juni, 2018, Deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni 50.92, ambapo Deni la ndani lilikuwa shilingi trilioni 14.73 na Deni la nje shilingi trilioni 36.19; kiasi hiki ni ongezeko la shilingi trilioni 4.84 sawa na asilimia 10.5 ikilinganishwa na Deni la shilingi trilioni 46.08 lililoripotiwa tarehe 30 Juni, 2017.

Katika ukaguzi wangu, nilibaini masuala ya msingi yafuatayo kuhusu Deni la Serikali na usimamizi wake:
(a) Mapungufu katika usahihi wa taarifa kutokana na udhibiti wa ndani usiojitosheleza katika kuweka kumbukumbu na kutoa taarifa za Deni la Serikali.

(b) Serikali kuchelewa kulipa madeni ya Benki Kuu ya kiasi cha shilingi bilioni 212.7. Kati ya hizo, shilingi bilioni 199.79  zinatokana na riba ya nakisi ya Serikali, na shilingi bilioni 12.9 ikiwa ni sehemu ya Serikali ya gharama za kudhibiti ukwasi kuanzia mwaka 2015/16 hadi 2017/18.

(c) Kutokuwapo kwa uwianishaji wa taarifa za mfumo wa malipo (Epicor) na Mfumo wa Utunzaji wa Taarifa za Deni la Taifa wa Jumuiya ya Madola (Common Wealth Secretariat-Debt Record Management System – (CS-DRMS)). Hii inasababisha taarifa za fedha kutowiana na vyanzo vyake, hivyo kuhatarisha uadilifu wa taarifa za Deni la Serikali.

3.2.3 Udhaifu katika Malipo ya Mafao
Ndugu Waandishi wa Habari,
Katika mwaka wa fedha 2017/2018, nilikagua Majalada 2,868, ambapo Majalada 2,814 yenye jumla ya shilingi bilioni 165.44 niliyaidhinisha kwa ajili ya malipo lakini Majalada 54 niliyahoji na kuyarudisha kwa Maofisa Masuuli husika kwa ajili ya masahihisho.
 
Kati ya Majalada 2,868 yaliyokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2017/18, Mafao ya Wastaafu 295 (10.5%) yalibainika kukokotolewa kimakosa. Kati ya hayo, Majalada 172 yamebainika kuwa na ziada ya malipo ya shilingi milioni 577.32 huku Majalada 123 yakiwa na upungufu wa malipo wa shilingi milioni 294.35.

Aidha, nilibaini ucheleweshaji mkubwa wa waajiri katika maandalizi na uwasilishaji wa Majalada ya wanufaika wa mafao kwa ajili ya Ukaguzi. Ucheleweshaji huo unatokana na waajiri kutotoa kipaumbele kwenye usimamizi wa uandaaji wa mafao hivyo kuwanyima wastaafu haki yao ya kupata mafao kwa wakati.

3.2.4 Ukaguzi wa Wizara, Idara na Wakala wa Serikali, Mifuko maalumu, na Taasisi nyingine

Ndugu Waandishi wa Habari,
Nilifanya ukaguzi katika wizara na idara za Serikali 65; wakala za Serikali 33, mifuko maalumu ya fedha 16, na taasisi nyingine za Serikali 42. Nilikagua pia vyama vya siasa 14, balozi za Tanzania 41, bodi za mabonde ya maji 14 na hesabu jumuifu za taifa. Katika ukaguzi wangu, nilibaini mapungufu yafuatayo:

Udhaifu Uliobainika katika Wakala za Serikali
(a) Wakala za Serikali hazikupeleka kiasi cha shilingi bilioni 9.26 kwenda Mfuko Mkuu wa Hazina kama inavyotakiwa na Kifungu cha 11 (3) cha Sheria ya Fedha ya Mwaka 2001 (kama iliyorekebishwa 2016);

(b) Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) unadaiwa kiasi cha shilingi bilioni 57.09 ikiwa ni riba ya ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi wa ujenzi na washauri wa miradi; 

(c) Kasi ndogo ya Wakala wa Majengo Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa majengo yenye thamani ya shilingi bilioni 24.06. Jedwali Na. 7 linaainisha miradi hiyo

Jedwali Na. 7: Miradi ya TBA iliyochelewa kukamilika
(d) Baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kushindwa kuhamisha fedha zilizokuwa za tozo za wakandarasi na fedha za kodi ya zuio za kazi zenye jumla ya shilingi bilioni 6.65 kwenda Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Udhaifu katika Utengenezaji wa Vitambulisho vya Taifa Kupitia Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa (NIDA)

Ndugu Waandishi wa Habari,
Katika ukaguzi wa Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa nilibaini kuwa kati ya watu 19,662,105 waliosajiliwa, ni vitambulisho 4,511,809 tu ndivyo vilivyotengenezwa, sawa na asilimia 23 ya idadi ya watu walioandikishwa.

Aidha, nilibaini kuwa Kampuni ya IRIS Corporation Berhad ya Malaysia (Mkandarasi) imesimamisha shughuli zote za kutengeneza vitambulisho kuanzia tarehe 14 Machi 2018. Sababu za kusimamisha zinajumuisha kutolipwa deni la mkandarasi lenye thamani ya Dola za Marekani milioni 30.18 (Shilingi bilioni 69.98), na kutoongezwa kwa muda wa mkataba kwa kipindi cha miezi kumi (10) tangu kwisha kwa muda wa mkataba wa awali, tarehe 14 Machi 2018.

Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba
Ndugu Waandishi wa Habari,
Katika mapitio ya taratibu za manunuzi na usimamizi wa mikataba kwenye taasisi mbalimbali za Serikali, nilibaini mambo yafuatayo ambayo yanaleta shaka katika kufikia thamani ya fedha.
(a) Kiasi cha shilingi bilioni 4.61 kilitumika kununua bidhaa, huduma, ushauri wa kitaalamu, na kazi za ujenzi ndani ya wizara, idara, na sekretarieti za mikoa pasipo kutumia taratibu za kushindanisha wazabuni kinyume na Kanuni za 163 na 164 za Kanuni za Manunuzi ya Umma za Mwaka 2013.  

(b) Taasisi saba (7) zilifanya manunuzi yenye thamani ya shilingi bilioni 5.37 bila kupata vibali vya Bodi za Zabuni kinyume na Kifungu cha 35 (3) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011, na Kanuni 55 ya Kanuni za Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013.  Taasisi hizo ni:
(i) Sekretarieti ya Mkoa wa Iringa;
(ii) Sekretarieti ya Mkoa wa Geita;
(iii) Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga;
(iv) Wizara ya Katiba na Sheria;
(v) Jeshi la Polisi;
(vi) Jeshi la Wananchi Tanzania; na
(vii) Ofisi ya Rais - Idara ya Kumbukumbu na Utunzaji wa Taarifa

(c) Taasisi tano (5) zilifanya manunuzi ya bidhaa, huduma, na kazi za kiasi cha shilingi bilioni 1.17 bila kuwapo kwa makubaliano ya Kimkataba na Wazabuni. Hii ni kinyume na Kanuni Namba 10 (4) ya Kanuni za Manunuzi ya Umma za Mwaka 2013. Taasisi hizo ni kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 8

Jedwali Na. 8: Taasisi zilizofanya manunuzi bila kuwapo na Mikataba na Wazabuni.
Udhaifu katika Usimamizi wa Matumizi
Ndugu Waandishi wa Habari,
Katika mapitio ya taarifa za matumizi ya fedha za umma, nilibaini dosari mbalimbali katika udhibiti wa ndani kama ifuatavyo; 
(a) Matumizi ya shilingi bilioni 4.66 yalifanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda kampuni binafsi za huduma za kisheria bila kufuata makubaliano ya mikataba; na

(b) Taasisi 20 za Serikali Kuu ziliwalipa watoa huduma mbalimbali kiasi cha shilingi bilioni 1.43 pasipo kudai stakabadhi za kielektroniki. 

Taasisi hizo ni:
1. Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe;
2. Sekretarieti ya Mkoa wa Katavi;
3. Idara ya Uhamiaji;
4. Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia;
5. Ofisi ya Waziri Mkuu-Ofisi Binafsi;
6. Idara ya Huduma za Magereza;
7. Ofisi ya Waziri Mkuu;
8. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Mawasiliano;
9. Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga;
10. Mahakama ya Tanzania;
11. Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga;
12. Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi;
13. Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi – Hospitali ya Rufaa Sokoine;
14. Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani;
15. Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro;
16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi;
17. Tume ya Maendeleo ya Usharika Tanzania;
18. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto;
19. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; na
20. Wizara ya Kilimo;

(c) Malipo yalifanyika kimakosa katika vifungu visivyostahili ya kiasi cha shilingi bilioni 885.99 kinyume na Kanuni ya 42(2) ya Kanuni za Fedha za Umma za Mwaka 2001. Jedwali Na. 9 linaonesha taasisi zilizofanya malipo kimakosa kwenye vifungu visivyostahili.

Jedwali Na. 9: Malipo Yaliyofanyika Kimakosa kwenye Vifungu Visivyostahili

Shilingi Bilioni 2.54 za Mapato Yasiyotokana na Kodi ambayo Hayakuwasilishwa Mfuko Mkuu

Ndugu Waandishi wa Habari,
Ukaguzi ulibaini kuwa kiasi cha shilingi bilioni 2.54 kilichokusanywa na Balozi 7 za Tanzania katika mwaka wa fedha 2017/18 hakikuwasilishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina kinyume na Kifungu cha 11 cha Sheria ya Usimamizi wa Fedha ya Mwaka 2001. Badala yake, kiasi hicho cha fedha kilibakizwa katika akaunti za fedha za Balozi husika. Jedwali Na. 10 linaonesha makusanyo yaliyofanywa na Balozi, ambayo hayakuwasilishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina.

Jedwali Na. 10: Mapato Yasiyotokana na Kodi ambayo Hayakuwasilishwa Mfuko Mkuu

Ripoti ya CAG: Matokeo ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma

$
0
0
5.1 Utangulizi
Sura hii inawasilisha matokeo ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma. Maeneo yaliyokaguliwa ni Mwenendo wa Kifedha na Uwezo wa Kuendelea kutoa Huduma; Usimamizi wa Mapato katika Mashirika ya Umma; Ongezeko la Madeni ya Wafanyakazi katika Taasisi za Elimu ya Juu; Ukamilishaji wa Miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa; Hali ya Mali za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya; Ukusanyaji wa Madeni ya Wateja wa Mamlaka za Maji; na Usimamizi wa Mikataba na Manunuzi katika Mashirika ya Umma.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Ukaguzi wa Mashirika ya Umma ulibaini masuala mbalimbali ambayo, Serikali inapaswa kuyafanyia kazi ili kuboresha usimamizi wa Rasilimali za Umma kama ifuatavyo. 

5.2 Udhaifu katika Mwenendo wa Kifedha na Uwezo wa Kuendelea kutoa Huduma 

Ndugu Waandishi wa Habari,
Katika ukaguzi wangu, nilibaini kuwepo kwa Mashirika ya Umma 14 yenye matatizo makubwa ya kifedha pamoja na kupata hasara hadi kusababisha madeni kuwa zaidi ya mitaji yao kwa zaidi ya asilimia 100. Aidha, kati ya Mashirika hayo, Mashirika 11 yana ukwasi hasi kwa maana yanajiendesha kwa hasara kwa zaidi ya miaka 2 sasa. Kufuatia hali hii, ni dhahiri kuwa Mashirika hayo hayawezi kujiendesha bila kutegemea msaada kutoka Serikali Kuu. Hivyo, ipo hatari ya kushindwa kuendelea kutoa huduma kwa jamii. Jedwali Na. 14 linaainisha Taasisi zenye hali mbaya kifedha.
 
Jedwali Na. 14: Taasisi Zenye Hali Mbaya Kifedha

5.3 Udhaifu wa Usimamizi wa Mapato katika Mashirika ya Umma 

Ndugu Waandishi wa Habari, 
Katika mapitio ya usimamizi wa mapato katika Mashirika ya Umma mbalimbali, nilibaini dosari zikiwemo;   

5.3.1 Udhaifu katika ufuatiliaji wa marejesho ya kiasi cha shilingi trilioni 1.46 cha mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu 

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeshindwa kufahamu walipo wakopaji wa mikopo ya elimu ya juu yenye thamani ya shilingi trilioni 1.46. Kiasi hiki cha fedha ni kikubwa sana ikizingatiwa kuwa Kifungu cha 4(h) cha Sheria ya Bodi kinaitaka Bodi kutengeneza mtandao na kushirikiana na Taasisi na Mashirika mbalimbali ili kuwatambua wadaiwa na kuwezesha kupata marejesho ya mikopo hiyo.

5.3.2 Changamoto katika ukusanyaji wa tozo za maegesho ya meli

Mamlaka ya Mapato Tanzania inakusanya tozo za maegesho ya meli kwa niaba ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na kila mwisho wa mwezi Mamlaka ya Bandari Tanzania inafanya uwianishaji wa kibenki. 

Hata hivyo, wakati wa ukaguzi wa mapato ya maegesho niligundua utofauti wa shilingi bilioni 42.5 katika kumbukumbu za Mamlaka ya Bandari Tanzania na zile za Mamlaka ya Mapato Tanzania. Hali hii inatokana na ukosefu wa ushirikiano wa kutosha kati ya Mamlaka hizi mbili katika uwianishaji wa taarifa pindi inapotokea tofauti. 

5.2.1 Udhaifu wa utawala bora katika mashirika ya umma
Kwenye taarifa zangu za ukaguzi kwa miaka ya fedha 2015/16 na 2016/17 niliripoti kuwa Mashirika ya Umma 18 na 20, mtawalia, yalikuwa yakijiendesha bila kuwa na Bodi za Wakurugenzi kwa muda mrefu. 

Nilishauri Mamlaka za Uteuzi kuchukua hatua za makusudi kuteua Wakurugenzi ili kuboresha Utawala Bora na Udhibiti wa Ndani wa Taasisi husika. Katika ukaguzi wangu wa mwaka 2017/18 nimebaini kuwa Mashirika 24 hayakuwa na Bodi za Wakurugenzi. Kati ya Mashirika haya, saba (7) yanafanya kazi bila ya kuwa na bodi kwa zaidi ya mwaka mmoja, huku Mashirika manne (4) yakiwa na zaidi ya miaka miwili.
 
5.4 Ongezeko la Madeni ya Wafanyakazi katika Taasisi za Elimu ya Juu 

Ndugu Waandishi wa Habari,
Kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2017/18, madeni yanayohusiana na malipo ya posho ya majukumu kwa wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya Mzumbe na Ardhi yameongezeka. Katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, madeni yameongezeka kutoka shilingi bilioni 1.49 hadi shilingi bilioni 3.41, na kwa Chuo Kikuu cha Ardhi, madeni yameongezeka kutoka shilingi bilioni 1.48 hadi bilioni 2.26. 

Aidha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Mzumbe vilikuwa na madeni ya kiinua mgongo ya shilingi bilioni 5.59 na shilingi milioni 525, mtawalia kwa wafanyakazi ambao wamemaliza mikataba yao. 

Vilevile, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kilikuwa na madeni ya shilingi bilioni 6.78 ikiwa ni posho za nyumba na madeni mengineyo ya wafanyakazi tangu Juni 2017. Hali hii inaweza kusababisha kushuka kwa kiwango cha elimu ya juu kutokana na wahadhiri kukosa morali ya kazi. 

5.5 Ucheleweshaji wa Ukamilishaji wa Miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa 

Ndugu Waandishi wa Habari, 
Shirika la Nyumba la Taifa lilianzisha Mradi wa Nyumba wa Golden Premier Residence (711-2) uliopo Kawe, Kitalu Na. 711/2 mnamo tarehe 16 Oktoba, 2013. 

Katika mapitio yangu, nilibaini mradi huo ulisimama tangu mwanzo wa mwaka 2017 kutokana na ukosefu wa fedha. Hadi unasimama, mradi ulikuwa umekamilika kwa asilimia 30 na umetumia jumla ya shilingi bilioni 34.87, ambapo vyanzo vya ndani vilichangia kiasi cha shilingi bilioni 11.64 na mkopo kutoka Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) ulikuwa ni shilingi bilioni 23.23. 

Shirika la Nyumba la Taifa lilitakiwa kuanza kulipa marejesho ya Mkopo kuanzia Julai 2018. Hivyo, Shirika linatumia fedha kutoka vyanzo vingine kulipa mkopo huo huku mradi ukiwa haujakamilika. 

Ikiwa Shirika la Nyumba la Taifa halitapata kibali cha kukopa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango kutokana na kufikia ukomo wake wa kukopa, litapaswa kuwalipa wakandarasi jumla ya shilingi bilioni 99.99 kwa kuvunja mikataba. 

Pia, litatakiwa kurejesha jumla ya shilingi bilioni 2.6 kwa wateja waliokwishaanza kulipia malipo ya awali ya ununuzi wa nyumba hizo. 

5.6 Kupungua kwa Mali za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

Ndugu Waandishi wa Habari,
Japokuwa makusanyo ya mwaka yanaendelea kuwa makubwa zaidi ya malipo ya huduma za bima ya afya, kwa sasa malipo ya huduma za afya yanakua kwa uwiano mkubwa mwaka hadi mwaka zaidi ya uwiano wa kukua kwa mapato. Kutokana na hali hii, makisio ya madai ya huduma za bima ya afya pekee ifikapo mwaka wa fedha utakaoishia Juni 2024 yatakuwa ni asilimia 99.2 ya jumla ya makusanyo yote. Uwiano huu unakisiwa kuongezeka zaidi hadi kufikia asilimia 104.8 katika mwaka unaofuata. 

Hali hii inamaanisha kwamba madai ya huduma za bima ya afya yanaendelea kuongezeka, na itafikia kipindi ambapo makusanyo na mapato kutoka katika uwekezaji hayataweza kukidhi madai na hivyo itaulazimu Mfuko kuchukua hatua za dharura kama kuuza mali zake.

5.7 Udhaifu katika Ukusanyaji wa Shilingi Bilioni 97.58 za Madeni ya Wateja wa Mamlaka za Maji 

Nilibaini kuwepo kwa kiwango kidogo cha kukusanya marejesho ya madeni ndani ya Mamlaka za Maji, kwa kuwa mapato mengi yalikuwa hayajakusanywa na yamezidi muda uliowekwa kwenye Sera ya Mikopo ya Mamlaka husika. 

Katika jumla ya deni hilo la shilingi bilioni 97.58, nilibaini kuwa shilingi bilioni 39.59 (sawa na asilimia 41) ni Madeni ya Serikali, na shilingi bilioni 57.99 (sawa na asilimia 59) ni madeni ya wateja wengine. Ongezeko hili la madeni limesababishwa na ufuatiliaji hafifu wa wadeni na kutokufuata Sera ya Mamlaka za Maji ya kukata huduma za maji kwa wateja wanaokiuka taratibu. 
  
Udhaifu katika Usimamizi wa Mikataba na Manunuzi katika Mashirika ya Umma
Kampuni Hodhi ya Kusimamia Rasilimali za Shirika la Reli (RAHCO) ilifanya malipo ya awali ya kiasi cha Dola za Marekani 500,000 ikiwa ni sawa na shilingi bilioni 1.07 mwaka 2015 kwa mhandisi mshauri kwa kazi ya kutoa huduma ya ushauri ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge). Hata hivyo, huduma hiyo haikutolewa hadi kufikia Februari 2019, ikiwa ni miaka mitatu tangu malipo yalipofanyika. Mkataba ulikuwa wa miezi 12 kuanzia tarehe ya kusaini mkataba ambayo ilikuwa tarehe 20 Mei, 2015. 

Aidha, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) kiliingia mkataba na Kampuni ya SUMSANG C & T Corporation tarehe 16 Desemba, 2014 kwa ajili ya kuleta na kufunga mfumo unaojulikana kama “OCS 121 System Viewer”. Mfumo huu ulifungwa tarehe 26 Julai, 2017 kwa mkataba wa Dola za Marekani milioni 1.41. Hadi kufikia wakati wa ukaguzi, mfumo huo ulikuwa haujaanza kutumika kwa kuwa ulikuwa haujakidhi vigezo vilivyokuwa vimeainishwa kwenye mkataba.  

5.8 Mapendekezo 
Ndugu Waandishi wa Habari,

Ili kurekebisha kasoro zilizobainishwa katika ripoti hii, ninaishauri Serikali ihakikishe: 
(i) Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inashirikiana na Taasisi zingine na vyanzo vingine vya taarifa ili kuiongezea nguvu kanzidata yake na kuweza kuwatambua wakopaji ambao hawajulikani walipo.

(ii) Mamlaka ya Bandari Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania zinaboresha uwianishaji wa kibenki katika eneo la tozo za maegesho ya meli ili kuhakikisha unafanyika kwa ufanisi na usahihi na tofauti za kimahesabu zinamalizwa kwa wakati.

(iii) Inaangalia upya muda wa uhakiki wa madeni ya wafanyakazi kwani kuendelea kuchelewesha malipo hayo kunazidisha ongezeko la madai na hivyo kuongeza mzigo kwa Serikali.

(iv) Kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iangalie namna bora ya kuepusha hasara inayoweza kupatikana kutokana na kutokukamilika kwa mradi wa Nyumba wa Golden Premier Residence. 

(v) Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) kinafanya ufuatiliaji wa karibu ili mzabuni akamilishe vigezo vya mfumo ambavyo bado havijapatikana ili mfumo uanze kufanya kazi. 

Ripoti ya CAG: Matokeo Ya Ukaguzi wa Miradi Ya Maendeleo

$
0
0
6.1 Utangulizi
Sura hii inawasilisha matokeo ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo. Maeneo yaliyohusika na Ukaguzi ni Kutorejeshwa kwa Fedha za Miradi zilizokopwa; Kodi ya Ongezeko la Thamani kulipwa kinyume na makubaliano ya Miradi; na Uchangiaji usioridhisha wa Serikali kwenye Miradi kinyume na makubaliano na Wadau wa Maendeleo. 


Maeneo mengine ya Ukaguzi ni Utekelezaji Hafifu wa Usambazaji wa Umeme Vijijini kupitia Mradi wa Wakala wa Nishati Vijijini; Kasi ndogo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mradi wa Uboreshaji wa Makazi; Ucheleweshaji wa kukamilika kwa Ujenzi wa Miradi ya Maji; na kutotumika kwa Mradi wa Dampo uliokamilika. 

Ndugu Waandishi wa Habari,
Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo umebaini masuala mbalimbali ambayo Serikali inapaswa kuyafanyia kazi ili kuboresha usimamizi wa rasilimali za umma. Masuala hayo yameainishwa kwa kina katika Ripoti ya Miradi ya Maendeleo, ambayo nimeiwasilisha kwako leo na muhtasari wake ni kama ifuatavyo;

6.2 Kutorejeshwa kwa Fedha za Mradi Shilingi Milioni 939.92 Zilizokopwa 

Ukaguzi wangu ulibaini kuwa Maofisa Masuuli wa miradi saba walikopa fedha za miradi jumla ya shilingi milioni 939.92 kwa ajili ya kugharimia matumizi ya kawaida kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2018. Fedha hizi hazikurejeshwa kwenye miradi husika na hivyo kuathiri utekelezaji wa shughuli za miradi zilizopangwa.

6.3 Kodi ya Ongezeko la Thamani ya Shilingi Bilioni 12.16 Iliyolipwa Kinyume na Makubaliano ya Miradi 

Ukaguzi wangu ulibaini kuwa malipo ya kodi ya ongezeko la thamani kiasi cha shilingi bilioni 12.16 yalifanywa na watekelezaji wa miradi 45 kinyume na makubaliano ya mikataba ya utekelezaji wa miradi husika. 
 
6.4 Uchangiaji wa Serikali Usioridhisha kwenye Miradi kiasi cha Shilingi Bilioni 111.01 Kinyume na Makubaliano na Wadau wa Maendeleo 

Ukaguzi wangu wa miradi mbalimbali kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2018 ulibaini kuwa miradi kumi ambayo Serikali ilitakiwa kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 118.44, ilichangia shilingi bilioni 7.43, sawa na asilimia sita tu. Hali hii ilisababisha upungufu wa kiasi cha shilingi bilioni 111.01 kinyume na makubaliano na wadau wa Maendeleo. Serikali kushindwa kuchangia miradi hii kwa kiasi kikubwa kumeathiri utekelezaji wa miradi husika na kudhoofisha juhudi za kufikia malengo yaliyokusudiwa.

6.5 Utekelezaji Hafifu wa Wakala wa Nishati Vijijini Kusambaza Umeme Vijijini 

Ukaguzi wa Miradi ya Nishati ulibaini kuwa Wakala wa Nishati Vijijini ilipanga kusambaza umeme kwenye vijiji vya Tanzania Bara vinavyokadiriwa kufikia 12,268 kuanzia mwaka 2013 hadi kufikia mwaka 2021. Hata hivyo, kufikia tarehe 30 Juni, 2018, mradi huo ulikuwa umefikisha umeme kwenye vijiji 4,395 tu, sawa na asilimia 36 kwa kipindi cha miaka mitano. Hali hii inaondoa uwezekano wa kufikia lengo la kusambaza umeme kwenye vijiji 7,873 vilivyobaki katika kipindi cha miaka mitatu iliyosalia hadi 2021. 

6.6 Kasi Ndogo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mradi wa Uboreshaji Makazi 

Mradi wa uboreshaji wa makazi unatarajiwa kukamilika mnamo tarehe 28 Juni, 2019. Hata hivyo, ukaguzi ulibaini kuwepo kwa kiasi kikubwa cha fedha ambacho hakijatumika cha Dola za Marekani milioni 36.25 sawa na shilingi bilioni 81.80. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 60 ya fedha za mkopo wa Dola za Marekani milioni 60 zilizotolewa kwa ajili ya mradi huu. Kuwepo kwa kiasi kikubwa cha fedha za mradi ambazo hazijatumika kumesababishwa na kasi ndogo ya utoaji wa mikopo na mchakato mrefu wa manunuzi. Hivyo, kuna uwezekano mdogo wa fedha hizi kutumika kufikia mwishoni mwa mwezi Juni 2019.

6.7 Kuchelewa Kukamilika kwa Ujenzi wa Miradi ya Maji

Ukaguzi wa miradi ya maji ulibaini kuwa miradi ya maji 65 inayotekelezwa na Halmashauri 22 za Mamlaka za Serikali za Mitaa yenye thamani ya shilingi bilioni 63.7 ilichelewa kukamilika kwa kipindi cha kati ya miezi 3 hadi 48. Uchelewaji huu ulitokana na uwepo wa wakandarasi wasio na uwezo; ucheleweshaji wa fedha kutoka Serikalini, changamoto za usanifu wa michoro; na mapungufu yatokanayo na manunuzi.

6.8 Kutotumika kwa Mradi wa Dampo Uliokamilika Wenye Thamani ya Shilingi Bilioni 2.96

Ukaguzi wangu ulibaini uwepo wa Mradi wa Dampo wa thamani ya shilingi bilioni 2.96 mjini Kigoma Ujiji, ambao licha ya ujenzi wake kukamilika, Dampo hilo halikuwa limeanza kutumika. Hali hii ilitokana na Ujenzi wa Shule ya Msingi karibu na mradi huo na hivyo kutumika kwa dampo lile kunaweza kuleta athari za Kimazingira kwa Wanafunzi na Miundombinu ya Shule. 

6.9 Mapendekezo

Ndugu Waandishi wa Habari, 
Ili kurekebisha kasoro nilizozibainisha katika ripoti yangu, ninaishauri Serikali ihakikishe:
(i) Fedha zilizolipwa kama kodi ya ongezeko la thamani kwenye miradi 45 iliyosamehewa kodi zinarejeshwa ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo husika. Aidha, ninashauri watekelezaji wa miradi kuzingatia mikataba ya makubaliano na wadau wa miradi ya maendeleo kwa kuhakikisha kuwa miradi iliyosamehewa kodi hailipi kodi hizo ili kusaidia kukamilika kwa wakati miradi hiyo.

(ii) Inaweka utaratibu wa uwajibikaji ili kuhakikisha fedha za miradi zinapelekwa kwa wakati na kulingana na bajeti iliyoidhinishwa ili kutokuathiri utekelezaji kwa ufanisi wa miradi hiyo.

(iii) Inaanzisha ofisi itakayokuwa na jukumu la kuratibu utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo nchini.


Ripoti ya CAG: Matokeo Ya Ukaguzi Wa Mifumo Ya Teknolojia Ya Habari Na Mawasiliano

$
0
0
7.1 Utangulizi
Sura hii inatoa muhtasari wa matokeo ya ukaguzi wa mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA). Masuala yaliyobainika wakati wa ukaguzi ni pamoja na kuwepo kwa mgawanyo hafifu wa kazi ambazo hazitakiwi kufanywa na mtu mmoja kwenye mifumo; mifumo ya TEHAMA kutokuwa tangamani; Maofisa Masuuli kuidhinisha maombi ya malipo Nje ya Mfumo; na kutohakiki Bidhaa na Mizigo inayopita Nchini kwenda Nchi zingine kwenye Mfumo wa Pamoja wa Forodha (TANCIS). 

Masuala mengine yaliyobainika ni ufuatiliaji hafifu wa Makato ya asilimia moja (1.1%) kwa watoa huduma wa simu za mkononi kutoka kwenye Mfumo wa Serikali wa Malipo ya Kielektroniki; Watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kutojengewa uwezo wa kusimamia Mfumo wa Usajili kupitia Mtandao; na Mifumo tofauti ya TEHAMA kufanya kazi moja.

Ndugu Waandishi wa Habari
Serikali kwa muda mrefu sasa imekua ikiwekeza katika mifumo ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi katika shughuli zake zikiwamo ukusanyaji wa mapato na utoaji huduma kwa jamii. Kwa kutambua umuhimu wa mifumo hiyo na vihatarishi katika uunganishaji wa mifumo mipya, Ofisi yangu imejikita katika kuhakikisha ninakagua mifumo hiyo kwa umakini mkubwa na kutoa ripoti zitakazowezesha uboreshaji wa utendaji wa mifumo hiyo.
  
Katika mwaka wa fedha 2017/18, nimekagua mifumo mikubwa mitatu, ambayo ni Epicor kwa TAMISEMI; Mfumo wa Usimamizi wa Rasilimali-watu (HCMIS - Lawson) katika Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma;  na Mfumo wa Serikali wa Malipo ya Kielektroniki (GePG) katika Wizara ya Fedha na Mipango. Aidha, nimekagua mifumo ya udhibiti wa ndani ya TEHAMA kwa mashirika mbalimbali ya umma na wizara, pamoja na usimamizi wa miradi ya TEHAMA. Ukaguzi wangu ulibaini mapungufu yafuatayo.

7.2 Mgawanyo hafifu wa Kazi zisizotakiwa kufanywa na Mtu Mmoja kwenye Mifumo

7.2.1 Udhibiti hafifu katika mfumo wa Epicor katika Mamlaka za Serikali za mitaa

Ndugu Waandishi wa Habari,
Tathmini ya mfumo wa Epicor katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ilibaini kuwepo kwa mapungufu katika mgawanyo wa kazi zisizotakiwa kufanywa na mtu mmoja. Aidha, nilibaini kuwa watunza hazina wa Halmashauri mbalimbali walikuwa na uwezo wa kuingiza taarifa za bajeti, kufanya mgawanyo wa fedha, kuanzisha malipo, kuandaa hati za malipo, na kuidhinisha malipo hayo. Majukumu haya yakifanywa na mtu mmoja yanaweza kusababisha ubadhirifu wa fedha kwani mfumo wa udhibiti unakuwa dhaifu. 

7.2.2 Udhibiti hafifu katika Mifumo ya Makusanyo ya Mapato ya Kiuhasibu katika Taasisi za Umma  

Ukaguzi wangu ulibaini uwepo wa mifumo dhaifu ya Makusanyo ya Mapato ya Kiuhasibu katika Mashirika ya Umma. Mathalani, Mfumo wa Kiuhasibu katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) haujawekwa katika mazingira ya kumzuia mtumiaji kuidhinisha miamala ya kifedha, ambayo ameianzisha mwenyewe. Ukaguzi wangu ulibaini kuwa kati ya hati 44,280 za malipo ambazo zilitengenezwa kutoka kwenye mfumo wa malipo ya kielektroniki wa Shirika, hati 192 zilianzishwa, kuidhinishwa, na kuthibitishwa na mtu mmoja.   

Vilevile, mapitio niliyoyafanya katika mfumo wa SURLIS wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini (SUMATRA) yalibaini kuwa hatua zote tatu za kutoa leseni zinafanywa na mtu mmoja, ambaye ana uwezo wa kuingiza taarifa za magari, kuthibitisha taarifa hizo, kuidhinisha, na kutoa hati za madai. 

Hali-kadhalika, katika mapitio ya mfumo wa MIS pamoja na vyeti vya usajili wa bidhaa za chakula na dawa katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) nilibaini kuwa kati ya maombi 2,782 yaliyopokelewa, maombi 286 yalifanyiwa tahmini, kukaguliwa, na kuidhinishwa na mtu mmoja. 

7.2.3 Udhaifu katika udhibiti wa Mfumo wa Serikali wa Malipo ya Kielektroniki 

Mapitio ya Mfumo wa Serikali wa Malipo ya Kielektroniki yalibaini kuwa mtumiaji wa mfumo mwenye jukumu la umeneja ana uwezo wa kuweka tarehe ya ukomo wa malipo ya ankara bila kuidhinishwa hali inayopelekea mazingira ya udanganyifu. Aidha, nilibaini kuwa meneja anaweza kutengeneza ankara ya malipo na kupata namba ya kumbukumbu ya malipo kutoka kwenye mfumo. Pia, mfumo hauna hatua ya ziada ya kuidhinishwa kwa ankara hivyo inaweza kupelekea meneja kukadiria kiasi cha chini ikilinganishwa na kiwango halisi kinachotakiwa kulipwa. 
 
7.3 Mifumo ya TEHAMA kutokuwa Tangamani 

Ndugu Waandishi wa Habari,
Mapitio zaidi ya mifumo ya TEHAMA yalibaini kuwa mifumo hiyo haijaunganishwa na hivyo kuathiri utendaji wa pamoja wa shughuli za Serikali.

7.3.1 Kutounganishwa Mfumo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Epicor na TISS

Ukaguzi ulibaini kuwa Mfumo wa Epicor wa Mamlaka za Serikali za Mitaa hauna ushirikiano wa moja kwa moja na mfumo wa TISS, na hivyo kusababisha uwezekano kufanya malipo mara mbili. 

7.3.2 Kutounganishwa Mfumo wa Epicor na Mfumo wa Akaunti Moja ya Hazina

Mfumo wa Epicor wa Mamlaka za Serikali za Mitaa haujaunganishwa na mfumo wa Akaunti Moja ya Hazina. Hivyo, katika mapitio ya uhamishaji wa fedha za Serikali za Mitaa kutoka benki za biashara kwenda Benki Kuu nimebaini mapungufu ya udhibiti katika kuhakikisha kuwa kiasi cha fedha kinachoonekana kwenye mfumo wa Epicor kinalingana na kiasi halisi cha fedha kilichotumwa kutoka benki za biashara kwenda Benki Kuu. 

7.3.3 Kutokuunganishwa Mfumo wa Usimamizi wa Rasilimali-Watu (HCMIS - Lawson), “Ajira Portal”, na Mfumo wa Epicor 

Ndugu Waandishi wa Habari,
Ukaguzi wangu wa mifumo ya TEHAMA umebaini pia kuwa Mfumo wa Usimamizi wa Rasilimali-Watu (HCMIS - Lawson) haujaunganishwa na Mfumo wa Epicor, na “Ajira Portal”. Hali hii inaweka uwezekano wa kuwapo kwa wafanyakazi hewa katika mfumo wa HCMIS - Lawson. 

Mifumo hii mitatu ingekuwa imeunganishwa, ingeweza kuondoa uwezekano wa kuwapo wafanyakazi hewa kwa sababu mfumo wa “Ajira Portal” ulianzishwa ili kusimamia mchakato wa ajira kuanzia hatua ya maombi ya kazi, usaili, hadi uajiri. 

Mfumo huu una uwezo wa kutengeneza namba ya utambulisho ya kipekee kwa mtu anayeajiriwa ambayo inatumika kama namba ya mwajiriwa mpya kwenye mfumo wa HCMIS - Lawson. Vilevile, kutounganishwa kwa Mfumo wa Epicor na Mfumo wa HCMIS - Lawson kumepelekea kutengeneza bajeti ya rasilimali-watu nje ya mfumo wa HCMIS - Lawson. Hii inaweza kusababisha hatari ya kufanya matumizi ya Rasilimali-Watu zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa. 

7.3.4 Kutokuunganishwa kwa Mifumo ya Kiuhasibu “Accounting software” na Mifumo ya Makusanyo ya Mapato   

Ukaguzi wa mifumo ulibaini kuwa Mfumo wa Kiuhasibu na mfumo wa makusanyo ya mapato haijaunganishwa. Ukaguzi ulibaini pia kuwa Mfumo wa Leseni na Maombi (LOIS) wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA); Mfumo wa Udhibiti wa Uchambuzi wa Usanifu wa Kiuhandisi (EDAMS) wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira, Dar es Salaam (DAWASCO), na Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi, Dar es Salaam (DART) haijaunganishwa na Mfumo wa Uhasibu. Hali hii inasababisha taarifa za mapato yaliyokusanywa na Taasisi hizi kuingizwa kwenye Mfumo wa Kiuhasibu na mtumiaji wa mfumo husika ambapo inaweza kupelekea kutokea kwa makosa ya kibinadamu na kusababisha kutowiana kwa taarifa zilizo kwenye mfumo wa mapato wa Taasisi na Mfumo wa Uhasibu. 

7.3.5 Maofisa Masuuli Kuidhinisha Maombi ya Malipo Nje ya Mfumo 

Mapitio ya Mifumo ya Kiuhasibu na Mifumo inayoendesha kazi za Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na Mashirika ya Umma yameonesha kuwa Maofisa Masuuli wanaidhinisha nyaraka zilizochapishwa nje ya mfumo badala ya kuidhinisha kwenye nyaraka za ndani ya mfumo. 

Hii imesababishwa na mifumo kutotengenezwa kwa namna inayowawezesha Maofisa Masuuli kuingia kwenye mfumo na kuidhinisha. Badala yake, maofisa wa chini huingiza taarifa kwenye mfumo ambazo zimeshaidhinishwa na Maofisa Masuuli kwenye nyaraka. 

7.4 Bidhaa na Mizigo inayopita Nchini kwenda Nchi zingine kutohakikiwa kwenye Mfumo Jumuishi wa Forodha (TANCIS) 

Ndugu Waandishi wa Habari,
Ukaguzi wangu ulibaini kuwa bidhaa na mizigo inayopita nchini kwenda nchi zingine hupita bila kuhakikiwa kwenye Mfumo wa TANCIS. Mapitio ya taarifa za TANCIS kuhusu bidhaa zinazosafirishwa kupitia mipaka ya Kabanga, Rusumo, Mutukula, Tunduma, na Kasumulu yalibaini kuwa miamala 599 ya bidhaa zilipita nchini kwenda nchi zingine pasipo kuhakikiwa kwenye mfumo wa TANCIS.

7.5 Ufuatiliaji hafifu wa Makato ya Asilimia 1.1 kutoka kwa Watoa huduma za Simu za Mkononi kutoka Mfumo wa Serikali wa Malipo ya Kielektroniki 

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliingia mkataba na watoa huduma za simu za mkononi kuwezesha mwingiliano wa Mfumo wa Serikali wa Malipo ya Kielektroniki kwa makato ya asilimia 1.1 ambayo itatozwa kwa kila malipo yanayofanywa na mteja. Kupitia ukaguzi wangu, nimebaini kuwa hakuna mfumo mzuri wa kuhakiki makato ya asilimia 1.1 kama yanatekelezwa. Ilibainika kuwa ukaguzi wa kushtukiza unafanyika mara mojamoja, ambapo ukaguzi huo si wa ufanisi na haujitoshelezi.  

7.6 Watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Kutokujengewa Uwezo wa Kusimamia Mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao  

Katika mapitio ya mradi wa BRELA wa Kubuni, Kuunda, Kusanidi, na Utekelezaji wa Mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao, nilibaini kuwa BRELA inamtegemea mkandarasi wa mfumo huo kutokana na kutokuwajengea uwezo wafanyakazi wake kusimamia na kuendesha mfumo huo baada ya kukabidhiwa. Hali hii inasababisha gharama kubwa za uendeshaji kwa BRELA.  

Ripoti ya CAG: Matokeo Ya Kaguzi Maalumu

$
0
0
8.1 Utangulizi
Sura hii inawasilisha matokeo ya ukaguzi maalumu uliofanywa na Ofisi yangu. Ukaguzi ulifanyika kuhusiana na Ununuzi wa Mfumo usiofanya kazi katika Shirika la Bima la Taifa; Malipo Hewa kwa Mzabuni yaliyofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya;
Udanganyifu katika Malipo ya shilingi milioni 267.89 kwenye Akaunti ya Matumizi Mengine katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo; na Malipo Hewa katika Kandarasi za Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’. Maeneo mengine ambayo Ukaguzi Maalumu ulifanyika ni Ununuzi wa Mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole (AFIS) katika Jeshi la Polisi Tanzania; ujenzi wa Uwanja wa Ndege Songwe; na Ununuzi wa Sare za Askari Polisi uliofanywa na Jeshi la Polisi Tanzania.

Ndugu Waandishi wa Habari, 
Ofisi yangu ilifanikiwa kufanya kaguzi maalumu katika Taasisi mbalimbali za Umma. Yafuatayo ni baadhi ya mapungufu niliyoyabaini. 

8.2 Shirika la Bima la Taifa kuwa na Mfumo usiofanya kazi ulionunuliwa kwa Gharama ya Dola za Marekani Milioni 3.59  

Shirika la Bima la Taifa liliingia mkataba wa kununua mfumo wa ‘Genisys’ tarehe 18 Juni, 2012 kwa ajili ya kufungamanisha kazi kuu tatu za Shirika ambazo ni Bima ya Maisha, Bima zisizo za Maisha, na Uhasibu. Shirika liliukubali na kuupokea mfumo na kulipa Dola za Marekani milioni 3.59. Hata hivyo, ukaguzi wangu umebaini kuwa mfumo huo haufanyi kazi kikamilifu, hivyo kusababisha Shirika kutumia mfumo mwingine uitwao UNISYS. Kutokana na changamoto hizi, thamani ya fedha zilizotumika katika kununua mfumo huu haijaweza kupatikana kwani malengo ya kununuliwa kwake hayakufikiwa.   

8.3 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kufanya Malipo Hewa ya Shilingi Bilioni 2.61 kwa Mzabuni 

Katika uchunguzi wa vitabu vya fedha, taarifa za benki, na hati za malipo za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nilibaini kuwepo kwa malipo ya kiasi cha shilingi bilioni 3, kati ya malipo hayo shilingi bilioni 2.61 yalikuwa malipo hewa; shilingi milioni 350.87 ni malipo ambayo walipwaji walishindwa kubainika; na shilingi milioni 42.6 hazikuweza kuthibitika kupokelewa na walipwaji. Malipo haya yalitakiwa kulipwa watoa huduma za afya kwa kutumia hundi zilizofungwa lakini yalifanywa kwa fedha taslimu kinyume na Kanuni za Fedha za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

8.4 Udanganyifu katika Malipo ya Shilingi Milioni 267.89 kwenye Akaunti ya Matumizi Mengine katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Ndugu Waandishi wa Habari,
Nilikagua malipo mbalimbali katika Akaunti ya Matumizi Mengine na nilibaini kuwa kwa nyakati tofauti kuna watumishi walianzisha, kupitisha, na kufanya malipo ya ya shilingi milioni 267.89 ambayo hayakuwa na viambatisho husika na mengine yalikuwa na viambatisho vyenye shaka. 

8.5 Upotevu wa Mapato ya Zaidi ya Shilingi Bilioni 3.4 katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’

Mapitio ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani yalibaini mapungufu mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Hanang kushindwa kuwasilisha vitabu 425 vya kukusanyia mapato. Mambo mengine yaliyobainika ni pamoja na:
(a) Upotevu wa mapato ya ndani ya Halmashauri ya jumla ya shilingi bilioni 1.04 yaliyokuwa yanakusanywa na mawakala; na 

(b) Kutopatikana kwa nyaraka muhimu za makampuni ya mawakala wa ukusanyaji wa mapato kwa mikataba yenye thamani ya shilingi bilioni 2.36

8.6 Malipo Hewa ya Shilingi Milioni 73.45 katika Kandarasi za Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’

Ukaguzi maalumu umebaini kuwa fedha kiasi cha shilingi milioni 73.45 za Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji zililipwa kwa wakandarasi kama dharura bila kuwepo kazi za dharura. Ukaguzi umebaini kutokuwepo kwa ushahidi wowote wa kufanyika kwa kazi hiyo, na hivyo kudhihirika kuwa matumizi hayo ni hewa. 

8.7 Ununuzi wa Mashine za Mfumo wa Kidigitali wa Usajili wa Wapiga kura (BVR) Uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi 

Nilibaini kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilinunua mashine za BVR 8,000 kwa ajili ya usajili wa wapiga kura, ambapo kati ya hizo, mashine 5,000 hazikukidhi vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba hivyo kusababisha kutolandana kimatumizi na vile vilivyonunuliwa hapo awali na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Taifa wa Usajili, Ufilisi, na Udhamini (RITA). Kutolandana huku kumeisababishia Serikali hasara ya shilingi milioni 862.08 zilizotumiwa na NIDA kununulia leseni mpya za “Windows” na “Biometric Algorithms” ili kubadilisha mashine 5,000 zilizopokelewa kutoka NEC ziweze kufanya kazi na mfumo wa BVR wa NIDA.

Aidha, nilibaini kuwa mzabuni alilipwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 72.30 badala ya Dola milioni 72.15, kiasi ambacho kilikuwa bei ya mkataba hivyo kuwa na ongezeko la Dola za Marekani 148,243.73. Pia, mafunzo kwa maofisa 15 wa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hayakufanyika licha ya mzabuni kulipwa Dola za Marekani 358,650 kwa ajili ya mafunzo hayo.

8.8 Ununuzi wa Mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole (AFIS) Uliofanywa na Jeshi la Polisi Tanzania 

Ndugu Waandishi wa Habari,
Ukaguzi maalumu wa Mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole (AFIS) ulibaini mambo yafuatayo: 
(a) Mahitaji ya kitaalamu kutoka idara inayotumia mfumo huo hayakuzingatiwa wakati wa kutathmini na kutoa zabuni. 

(b) Malipo ya shilingi bilioni 3.30 yalifanyika kwa mzabuni kwa ajili ya huduma ya matengenezo na msaada wa kitaalamu wa Mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole kwenye mikoa nane ya Kipolisi ya Temeke, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Kigoma, Geita, na Kinondoni lakini Jeshi la Polisi lilishindwa kuthibitisha kuwa matengenezo hayo na msaada wa kitaalamu ulifanyika. 

(c) Vifaa vya Utambuzi wa Alama za Vidole vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.73 havikufungwa kwenye magereza 35 yaliyoainishwa. Badala yake vilihifadhiwa katika Ofisi ya Upelelezi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. 

(d) Malipo ya shilingi milioni 604.39 kwa ajili ya mafunzo kwa wataalamu 30 hayakufanyika. 

(e) Jeshi la Polisi lilishindwa kuionesha timu yangu ya ukaguzi zilizo monita 58 za kompyuta aina ya Dell zenye thamani ya shilingi milioni 159.16 zilizopelekwa kwenye Kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi cha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi (Forensic Unit). Pia, monita 213 za kompyuta aina ya Dell zililipiwa kiasi cha shilingi milioni 195.22 kwa mzabuni Lugumi Enterprises Limited lakini mzabuni hakuzileta. 

8.9 Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Songwe

Ndugu Waandishi wa Habari,
Katika ukaguzi maalumu wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Songwe, Mbeya nilibaini mambo yafuatayo: 
(a) Malipo ya jumla ya shilingi bilioni 1.43 yalifanyika mara mbili kwa udanganyifu kupitia maofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA). Aidha, jumla ya shilingi bilioni 1.95 zililipwa bila ya kuwepo kwa jedwali la vipimo na hati za madai zilizoidhinishwa na mhandisi mshauri. 

(b) Kati ya malipo ya awali ya shilingi bilioni 1.70 alizolipwa mkandarasi kwa ajili ya kuanza shughuli za ujenzi, ni shilingi milioni 176.56 tu ndizo zilizorejeshwa. Hivyo, bakaa ya shilingi bilioni 1.52 haikurejeshwa hadi ukaguzi huu unafanyika. 

(c) Shilingi milioni 570.50 zililipwa zaidi ya gharama zilizoidhinishwa na mhandisi mshauri. 

(d) Jumla ya shilingi bilioni 5.48 zililipwa kwa mkandarasi bila ya kuidhinishwa na mhandisi mshauri. 

8.10 Ununuzi wa Sare za Askari Polisi Uliofanywa na Jeshi la Polisi Tanzania

Katika ukaguzi huu maalumu, nilibaini kuwa Jeshi la Polisi Tanzania lililipa jumla ya shilingi bilioni 16.66 bila ya kuwapo na ushahidi wa uagizaji na upokeaji wa Sare za Askari Polisi kwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Polisi. 

Pia, nilibaini maoni ya Kisheria ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanayohusu uwasilishaji wa Kiapo cha Nguvu ya Kisheria (Power of Attorney) na leseni halali ya biashara hayakuzingatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani wakati wa kusaini Mkataba Na. ME.014/PF/2015/2016/G/30 Lot 2 uliohusu ununuzi wa sare za askari polisi. 

8.11 Mapendekezo 

Ndugu Waandishi wa Habari,
Kutokana na matokeo ya ukaguzi maalumu nilioufanya katika maeneo yaliyoelezwa, ninaishauri Serikali:
(i) Kuchukua hatua stahiki za kisheria na kinidhamu dhidi ya maofisa waliohusika katika ubadhilifu wa Mali za Umma.  Pia, Mamlaka husika zihakikishe kuwa mianya yote niliyobainisha wakati wa ukaguzi inayopelekea upotevu wa Mali za Umma inazibwa.

(ii) Kupitia Shirika la Bima la Taifa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, iwasiliane na wazabuni ili kuhakikisha kwamba masuala yote yaliyobaki kama ilivyooneshwa katika Hati za Mahitaji ya Kazi za Mifumo yanatatuliwa na kwamba mifumo hiyo inafanya kazi kikamilifu kama ilivyotarajiwa.

(iii) Kupitia Jeshi la Polisi Tanzania, ihakikishe kuwa vifaa vya Utambuzi wa Alama za Vidole vinafungwa katika maeneo husika na kuanza kutumika kama ilivyokusudiwa 

Serikali Yafafanua Katazo La Matumizi Ya Mifuko Ya Plastiki

$
0
0
Serikali imejipanga kuhakisha kuwa mifuko mbadala wa plastiki inapatikana kwa wingi ili kukidhi mahitaji. 
 
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika hii leo Jijini Dodoma na kusisitiza kuwa katazo la Mifuko ya Plastiki lililotolewa jana na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa linakuwa na nguvu kisheria kwa kuandika kanuni za katazo ya mifuko ya plastiki zitakazotangazwa katika gazeti la Serikali chini ya Sheria ya Mazingira na kutoa adhabu kwa kila mtu atakaekiuka utaratibu uliowekwa.  
 
“Kabla ya Serikali kutangaza hatua ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki, ulifanyika utafiti na maandalizi ya mifuko mbadala. Uwezo wa kuzalisha upo na mifuko ya karatasi inayotumika Kenya na Rwanda inatumia malighafi inayozalishwa Mgololo-Iringa,Tanzania.” Makamba alisistiza
 
Waziri Makamba ameainisha kuwa kuna vifungashio ambavyo havitapigwa marufuku ambavyo ni pamoja na vifungashio vya dawa za hospitalini, vifungashio katika sekta ya kilimo na ujenzi pia vile vya kuhifadhi maziwa na kutolea mfano wa vifungashio vya maziwa ya ASAS na Tanga Fresh, hata hivyo utaratibu maalumu utawekwa kwa wamiliki wa kukusanya vifungashio hivyo mara baada ya matumizi yake. 
 
Akizungumzia juu ya ushirikishwaji, Waziri Makamba amesema kuwa zoezi hili limekuwa ni shirikishi na hatua iliyotangazwa na Waziri Mkuu sio ya kushtukiza kwa kuwa Ofisi yake iliratibu mikutano katika maeneo kadhaa nchini kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu zuio la mifuko ya plastiki.
 
Katika kukamilisha utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Waziri Makamba amesema Ofisi yake imeunda kikosi kazi cha kusimamia katazo hilo kikihusisha wajumbe kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Shirika la Viwango Tanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Wengine ni Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
Katika hatua nyingine Waziri Makamba amesema kuwa mapema wiki ijayo ataitisha mkutano wa wawekezaji wa mifuko mbadala kote nchini na kujadili kwa kina namna bora ya kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala rafiki wa mazingira.
 
Serikali imetangaza kuanzia Juni Mosi 2019 kuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake.

Waziri Mkuu Aagiza Eneo La Kumbukumbu Ya Sokoine Liboreshwe Haraka

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa mkoa wa Morogoro uhakikishe unaboresha eneo la kumbukumbu ya Sokoine lililoko Wami-Dakawa, wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Amewataka Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Steven Kebwe, Mkuu wa Wilaya ya Mvovero, Bw. Mohammed Utali na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bw. Florent Kyombo wasimamie haraka uendelezaji na utunzaji wa eneo hilo ili kila mwaka pawe panafanyika shughuli ya kumbukumbu.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Aprili 10, 2019) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa na watumishi wa wilaya ya Mvomero mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya Sokoine Memorial High School na kutembelea eneo alipopata ajali Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Moringe Sokoine, Aprili 12, 1984.

“Hili eneo ni maalum. Tulikubaliana ndani ya Serikali liwe sehemu ya kumbukumbu ya Mheshimiwa Edward Moringe Sokoine, na keshokutwa ni miaka 35 ya kumbukumbu yake lakini hakuna chochote ambacho kimeandaliwa hapa kwa ajili hiyo,” amesema.

“Eneo hili liko jirani kabisa na makao makuu ya Halmashauri ya Mvomero. Mngekuwa mmepaendeleza tangu Halmashauri ilipoanza, hata bustani mnayosema mnataka kuiweka ingekuwepo hapa.”

Amesema anashangaa kuona eneo hilo limetelekezwa wakati Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya wapo. “Hili eneo kama lingeendelezwa, naamini hata mbio za kumbukumbu yake zilizofanyika Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita, zingefanyika hapa. Hata wanafamilia wangekuwa wanapita hapa kwa ajili ya kumbukumbu hiyo,” amesema.

“Mkurugenzi wa Halmashauri hapa ni lazima pasafishwe, huku mbele pawe na bustani na hii miti ya mbele iachwe ili papendeze. Mkuu wa Wilaya una Kamati yako ya Ulinzi na Usalama, tumia watu wako ili zoezi hili likamilike,” amesisitiza

Wakati huohuo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema lengo la kuanzisha shule ya Sokoine Memorial High School lilikuwa ni kuweka kumbukumbu yake ili iwe ya kudumu. Amewapongeza kwa kutenga chumba maalum kwenye shule hiyo, ambacho kitatunza kumbukumbu zake.

Ameutaka uongozi wa mkoa na wilaya usimamie ujenzi huo ili yapatikane majengo ya kuanzia kutoa elimu na hatua nyingine zitakamilishhwa wakati wanafunzi wakiwa shuleni.

Shule hiyo ambayo ilianza kujengwa Juni 2017, kwa mfumo wa Force Account, hadi sasa ujenzi wake umeshatumia sh. bilioni 1.7. Ujenzi wa shule hiyo ulisimama Mei, 2018 kutokana na uhaba wa upatikanaji wa fedha.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bw. Florent Kyombo inaonesha kuwa hadi sasa madarasa 16, vyoo matundu 16 na ofisi nne za walimu vimejengwa kwa gharama ya sh. 396,988,359 ambapo hadi sasa wanakamilisha uchomeaji wa madirisha pamoja na skiming kuta za ndani na nje.

Taarifa hiyo inaonesha pia kiasi cha sh. 899, 381,643 kimetumika kwa ajili ya ujenzi wa bweni lenye uezo wa kuchukua wanafunzi 256, ambayo hatua iliyofikiwa ni ujenzi wa kuta za ghorofa ya kwanza.

Kazi nyingine ambazo zimefanyika ni ujenzi wa bwalo la chakula (sh. 218,068,299) na ujenzi wa nyumba mkuu wa shule pamoja na nyumba mbili za walimu za two-in-one kwa gharama ya sh. 178,583,000.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Rais Magufuli Atoa Siku 30 Kwa Tamisemi Kukamilisha Ujenzi Wa Kituo Stendi Kuu Ya Mabasi Ya Mkoa Wa Njombe

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 30 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kukamilisha ujenzi wa stendi Kuu ya Mabasi katika Mkoa wa Njombe ambayo ujenzi wake imechukua muda wa miaka 5 bila kukamilika.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara na Wananchi Mkoani humo leo Jumatano (April 10, 2019), Rais Magufuli alisema mradi huo ni haki ya wananchi kutokana na tozo ya kodi mbalimbali wanazokatwa hivyo anashangwa na kitendo cha stendi hiyo kutokamilika licha ya mkandarasi wa mradi huo kulipwa fedha zote na Serikali.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema Serikali haipo tayari kuwavumilia wakandarasi wazembe na kutoa maelekezo kwa mkandarasi wa awali wa mradi huo ambayo ni kampuni ya Masasi Construction kuchunguzwa haraka na iwapo atabainika na makosa achukuliwe haraka hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Aliongeza kuwa katika Serikali anayoiongoza hatoruhusu viongozi na watendaji wabaishaji na badala yake aliwaomba kuwajibika katika maeneo yao bila ya kufuatwa na Rais kwa kuwa majukumu aliyonayo ni mengi hivyo kuwataka kuwatumikia wananchi kwani wamechelewesha maendeleo yao kwa kipindi kirefu.

“Ipo miradi mingi ambayo imechelewa kwa kipindi kirefu tu ukiwemo huu wa stendi ya Mabasi katika Mkoa wa Njombe, tumechezewa vya kutosha na nyingi Viongozi na watendaji nawaagiza uamuzi usisubiri Rais mpya nina wawakilishi wangu ambao ni nyinyi timizeni wajibu wenu” alisema Rais Magufuli.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema anashangwa na mradi huo uliogharimu kiasi cha Tsh Bilioni 9 kushindwa kukamilika kwa wakati huku baadhi ya miradi kama hiyo ikitekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini, hivyo kitendo kilichofanywa na mkandarasi wa mradi huo ni cha ubabaishaji na kupongeza hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa Mkoa kwa kusimamisha haraka ujenzi wa stendi hiyo.

Rais Magufuli alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kutimiza ahadi zote ilizoahidi kwa wananchi wake, na hivyo hawatakubali kuona Mtendaji au Kiongozi yoyote anakwamisha jitihada hizo, kwani hayupo tayari kusema uongo mbele ya wananchi kwa kuwa ni dhambi.

Aliongeza kuwa katika mradi wa Stendi hiyo Serikali imetumia kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni fedha za wananchi maskini na hivyo aliitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuwa thamani halisi ya fedha ya mradi huo inapatikana  na mradi huo unakamilika kwa muda na wakati uliopangwa.

Akitoa taarifa ya Mradi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Njombe Mji, Bi Illuminata Mwenda alisema mradi huo unaotekelezwa kwa ujenzi awamu tatu ulianza mwaka 2013, ambapo mkandarasi wa kampuni ya Masasi Construction amelipwa fedha zote na Serikali lakini halmashauri hiyo imesitisha mkataba wake kutokana mkandarasi huyo kushindwa kuikamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Awali akitoa taarifa ya hali ya Maji katika Mkoa wa Njombe kwa Rais Magufuli, Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa alisema Serikali imeongeza kiwango cha upatikanaji wa maji katika Mkoa huo kutoka asilimia 39 mwaka 2015 hadi asilimia 67 kwa sasa, hatua iliyotokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa maji katika miji ya Njombe Mji na Njombe Mjini wenye wenye gharama ya Tsh Bilioni 12.5

Aidha alisema pamoja na mradi huo, Serikali pia imepata ufadhili kutoka Serikali ya India kupitia mradi wa maji utakaotekelezwa katika  miji 28 nchini ikiwemo mji wa Njombe na Njombe wenye gharama ya Tsh Bilioni 32 ambao mwezi Septemba mwaka huu mkandarasi anatarajiwa kukamilisha nyaraka mbalimbali za zabuni.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali imeendelea kuimarisha na kuboresha utoaji wa huduma ya afya Mkoani Njombe ikiwemo Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo ambayo ujenzi umegharimu kiasi cha Tsh Bilioni 3.5.

Aliongeza kuwa katika kuimarisha mfumo wa utoaji huduma katika hospitali hiyo ambapo Serikali imepanga kuiwezesha hospitali hiyo vifaa tiba na wataalamu wakiwemo Madaktari Bingwa wa magonjwa yote yakiwemo ya uzazi, upasuaji na mipasuko ya ajali.

Alisema hadi kufikia sasa Serikali inasomesha jumla ya Madaktari Bingwa 301 katia vyuo mbalimbali nchini, hatua inayolenga kuhakikisha kuwa hospitali, vituo vya afya na Zahanati zote nchini zinakuwa na watalaamu wa kutosha na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania ikiwemo vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images