Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Polisi Wazuia Mkutano wa Zitto Kabwe Tanga

0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga  limezuia mkutano wa ndani wa Kiongozi wa Chama wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe wa uzinduzi wa matawi kutokana na kuwapo   vurugu.

Hatua hiyo ilitokana na taarifa za  intelijensia ambazo zilidai kutokea   vurugu ambazo ziliratibiwa na wanachama na wafuasi wa Chama cha CUF.

Akizungumza hali hiyo jana, Kiongozi wa   ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema   vitendo vinavyofanywa na vyombo vya dola vya kuzuia shughuli za chama hicho vinaonyesha namna ambavyo kinahofiwa kwa kuwa na nguvu kubwa kwa umma.

Alisema zuio hilo linaonyesha namna wanavyoingizwa kwenye mitego ya wanachama wao waonekane wanafanya vurugu.

Ziito alidai   kumekuwa na mazuio ya kila mara kwa chama hicho   kinapojaribu kufanya shughuli zake kama vile mikutano ya ndani ya kuimarisha uhai wa chama .

Hata hivyo kiongozi huyo alishangazwa na jeshi hilo kuruhusu vyama vingine kama CUF na CCM kuendelea kufanya mikutano ya ndani na hadhara bila ya vizuizi vya aina yoyote ile.

Alisema   mpaka jana Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga, lilikuwa limetoa kibali kwa chama hicho kuendelea kufanya shughuli zake ikiwamo kupokea wanachama wapya na mikutano ya ndani kabla ya kuzuia shughuli hizo.

Akizungumzia hali zuio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, alisema   taarifa za  intelejensia zinaonyesha   iwapo chama hicho kitaruhusiwa kufanya shughuli zake kunaweza kutokea uvunjifu wa amani.

Alisema   kutokana na uchunguzi wao walibaini  baada ya kuwapo   mivutano ya  siasa baina ya chama hicho na CUF  kutokana na kunyang’anyana ofisi na kuharibu baadhi ya thamani za ofisi hizo jambo linaloweza kusababisha kutokea   vurugu na amani kutoweka.

LIVE: Rais Magufuli akizindua barabara Mkoani Ruvuma yenye Kilometa 193

0
0
LIVE: Rais Magufuli akizindua barabara Mkoani Ruvuma yenye Kilometa 193

Spika Ndugai Afafanua Kuwazuia Waandishi Kuwahoji Wabunge wa Upinzani Wanaotoka Nje

0
0
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefafanua sababu ya kuwazuia waandishi wa habari kufanya mahojiano na wabunge wa upinzani kwa kusema wabunge hao wamekuwa na utaratibu wa kutoka nje mara kwa mara.
 
Spika Ndugai ametoa ufafanuzi huo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kauli yake aliyoitoa ya kuwazuia waandishi wa habari kufanya mahojiano na wabunge wa upinzani ambao waliamua kutoka nje ya Bunge baada Mbunge Arusha Mjini kusimamishwa mikutano 3 ya Bunge.

"Hatukusema sasa waandishi msiwe mnaongea na wabunge huko nje, lakini waandishi mkiacha kuwafuatilia wataacha wakitoka saa saba si Bunge limeahirishwa wakasema wanayotaka, wakitoka wanaleta mtafaruku na kusababisha mijadala muhimu ya ndani ya Bunge isiwe na waandishi." amesema Spika Ndugai

Kuhusiana na hatma ya Mbunge Lema, Spika Ndugai amesema, "kuna watu wana madeni makubwa zaidi ya hayo lakini hayawachanganyi, na sisi Bunge next time niwepo au nisiwepo tutawalisisha watakaokuwepo tusiruhusu tena Bunge kudhamini wabunge kuingia kwenye madeni makubwa".

"Wanaotetea lazima watetee kwa sababu hawajui hali halisi ni nini, lakini mwisho wa siku hela yenu ndiyo inayotumika wale waliotimuliwa nane (wabunge wa CUF) inadaiwa zaidi ya bilioni 1 na hawana uwezo wowote wa kulipa, kama watakazia wale jamaa na kuna some how kodi yenu inaweza kutumika" amesema Spika Ndugai

Serikali ya Tanzania yashinda kesi ya madai ya dola 55,099,171.66 nchini Marekani

0
0
Mnamo tarehe 12 Februari, 2018 familia ya marehemu Vipula Valambhia ilifungua kesi ya Madai Na. 1:18-CV-370 (TSC) dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mahakama ya District Court of Columbia nchini Marekani. Walalamikiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Walalamikaji katika Shauri hili ni Bi. Vipula D. Valambhia, Priscilla D. Valambhia, Bhavna D. Valambhia, Punita D. Valambhia na Krishnakant D. Valambhia ambao ni Mjane na Watoto wanne wa Marehemu Vipula Valambhia aliyefariki mwaka 2005 nchini Marekani. Walalamikaji wote ni raia wa Marekani na wakati wakifungua kesi hii, walikuwa wanaishi Houston, Texas Marekani.

Katika kesi hii, walalamikaji waliwakilishwa na Wakili kutoka Meredith B. Parenti wa Parenti Law PLLC, kutoka Taxes, Marekani. Kwenye mdai yao, Walalamikaji waliiomba Mahakama ya Marekani kupitia Sheria ya Marekani iitwayo Uniform Foreign- Country Money Judgments Recognition Act,DC Codes, . §§ 15-361- 15-371 iweze kutambua na kutoa amri ya kukazia malipo ya fedha Kiasi cha Dola za Marekani 55,099,171.66 zilizoamuriwa na Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka, 2003.

Walalamikaji walidai kuwa, kiasi hicho cha fedha kilipaswa kilipwe tokea tarehe 4, Juni 2001, pamoja na riba ya 7% kila mwaka. Hivyo, wakati wa kufungua shauri hilo, yaani tarehe 19 Februari, 2018, deni halisi lilikuwa ni Dola za Marekani 64,500,750.87.

Madai katika shauri hili yalitokana na Mkataba wa ununuzi wa vifaa vya kijeshi kati ya Kampuni ya Transport Equipment Ltd (TEL) ya Marehemu Vipula Valambhia na Serikali ya Tanzania. Mkataba huo uliokuwa unahusu ununuzi wa vifaa vya jeshi uliingiwa miaka ya 1980 na Kampuni ya TEL ilikuwa ikidai kwamba haijakamilishiwa malipo yote ya fedha zitokanazo na Mkataba huo. Hivyo, Kampuni hiyo iliamua kufungua Kesi Na. 210 ya mwaka 1989 iliyotolewa uamuzi na Mahakama za Tanzania.

Serikali ya Tanzania ilishawasilisha utetezi wake kupinga shauri hilo tarehe 13 Julai, 2018. Katika utetezi huo, Serikali ya Tanzania ilipinga madai hayo ya familia ya Valambhia kwa kuwa yalifunguliwa kinyume cha Sheria na taratibu za Sheria ya Marekani inayotambua na kuruhusu kukazia hukumu za kimahakama zitokanazo na Mahakama za nchi nyingine (Recognisation and Enforcement of Foreign Judgments) nchini Marekani. Serikali ya Tanzania ilieleza kuwa, ina kinga ya kisheria kama Nchi kufunguliwa Madai ya kukazia hukumu za kimahakama nchini Marekani (sovereign immunity), kinga hiyo ambayo inatambulika chini ya Sheria ya Marekani iitwayo “Foreign Sovereign Immunities Act, 28 U.SC. §§ 1602”. (“FSIA” or “Act”).

Mnamo tarehe 31 Machi, 2019, Mahakama ya District Court of Columbia, nchini Marekani chaini ya Mhe. Jaji Tanya S. Chutkan ilitoa uamuzi wake na kuona kuamua kuwa, madai yaliyowasilishwa na familia ya Valambhia hayakukuhusisha shughuli za kibiashara zilizofanyika nchini Marekani kama ambavyo Sheria ya Marekani ya “Uniform Foreign-Country Money Judgments Recognition Act,” inavyotaka.

Walalamikaji walikiri kupitia maelezo yaliyowaslishwa Mahakamani hapo kuwa, Shauri hilo linahusisha suala lililofanyika nje ya Marekani baina ya Kampuni ambayo sio ya Kimarekani na Serikali ya Tanzania.

Katika mazingira hayo, Mahakama iliafikiana na hoja za upande wa Serikali ya Tanzania kuwa, madai ya Familia ya Marehemu Valambia hayana msingi kisheria na kuwa Walalamikaji hawakustaili kufunguliwa kesi ya namna hiyo nchini Marekani. Hivyo, Kesi hiyo ilifutwa Mahakamani hapo kwa ushindi upande wa Tanzania.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI

RC Makonda Kuwakutani Wadau wa Michezo 1000 Hotel ya Serena Kwa Ajili ya Kuichangia Taifa Stars

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi kwa timu za Taifa ameandaa hafla maalumu ya chakula cha jioni itakayoshirikisha wadau wa michezo wenye uzalendo na Timu yao ya taifa itakayofanyika  katika Hotel ya Serena na kushirikisha wadau zaidi ya 1,000.

Makonda amesema hafla hiyo itahusisha zaidi ya Kampuni 50 ambazo zimeomba kushiriki kama sehemu ya kuiwezesha Timu ya Taifa ambapo kila kampuni itatakiwa kuchangia kiasi cha shilingi Milioni 10 kwa meza moja zitakazotumika kuiwezesha Taifa Stars katika fainali za AFCON nchini Misri.

Aidha RC Makonda amesema hafla hiyo itarushwa Mubashara (LIVE) kupitia vyombo mbalimbali vya habari vilivyojitoa kuiwezesha Taifa stars huku akiwaomba wananchi kuendeleza uzalendo walioonyesha juzi.

Katika hatua nyingine RC Makonda kwa niaba ya kamati amewashukuru Wananchi,Wachezaji,wadau wa michezo,vyombo vya habari, watu mashuhuri na wamiliki wa Mahotel na Bar kwa umoja wa kitaifa walioonyesha katika mechi kati ya Taifa stars dhidi ya Uganda jambo lililowezesha Taifa Star kushinda na kufuzu AFCON.

Mhe. Makonda pia amewaomba wananchi na wadau kuonyeha uzalendo katika mashindono ya AFCON kwa vijana wenye umri chini ya Miaka 17 yanayotarajia kuanza April 14 jijini Dar es salaam Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo pamoja na kuishangilia Timu ya Wanawake ya Twiga Stars inayotaraji kucheza April 05.

Pamoja na hayo RC Makonda amemkabidhi kiasi cha Shilingi Milioni Moja kijana mzalendo kutoka Manyara aliesafiri kwa tabu kutoka Manyara hadi Dar es salaam akihamasisha wananchi kuwa wazalendo na Timu yao ya Taifa ambapo amewataka vijana wengine kuiga moyo huo.

Harambee ya Jokate Mwegelo Yakusanya Milioni 915

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo, ameeleza kuwa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana wilayani humo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya Sh.milioni 915 kati ya Sh.Bilioni 1.3 ambazo zinahitajika kufanikisha ujenzi huo.

Uchangiaji wa shule hiyo ya sekondari ambayo itajengwa katika Kata ya Kibuta ,ni muendelezo wa kampeni ya tokomeza ziro wilayani Kisarawe iliyoanzishwa na Jocate kwa kushirikiana na viongozi wengine.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mwegelo amesema baada ya kuzindua harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi huo wameamua  kutoa mrejesho kwa Watanzania wa nini ambacho kimepatikana.

"Tumefanikiwa kupata Sh 915,174,000 kati ya Sh 1.38 bilioni ambazo zilikuwa ndio lengo letu katika harambee iliyofanyika kwetu ni mafanikio makubwa yanayowezesha kuanza ujenzi" amesema Jokate na kuongeza kuwa  fedha hizo zinajumuisha ahadi,vifaa vilivyotolewa pamoja na fedha taslimu Sh 80,641,000 .

"Ziko ahadi nyingi zilizotolewa ikiwamo madarasa sita ambayo ni sawa na Sh 120 milioni, mabweni mamwili sawa na Sh160 milioni, maabara, mifuko 1,890 ya simenti, mbao pamoja na mabati," amesema

Amesema anawashukuru wananchi wa Tanzania na wadau wa maendeleo waliojetokeza kuchangia kampeni hiyo ya kuwakomboa watoto wa kike kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kupata elimu, ingawa kwa siku za usoni watajenga na ya watoto wa kiume kwani kupanga ni kuchagua.

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Waziri Mkuu: Serikali Itaendelea Kushirikiana Na CPA

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itatoa ushirikiano kwa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA – Africa)wanaotarajia kufanya mkutano wao Novemba 2019, nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Aprili 4, 2019) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Madola Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Emilia Monjolwa Lifaka.

Waziri Mkuu alisema Bunge na Serikali nchini wanafanya kazi kwa kushirikiana, hivyo amemuhakikishia Mhe. Emilia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Cameroon kuwa Serikali itatoa ushirikiano unaohitajika kwa CPA ili kufanikisha malengo tarajiwa

Pia, Waziri Mkuu alisema Serikali inaushukuru uongozi wa CPA kwa kutoa ushirikiano stahiki kwa wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni wanachama wa CPA

Kwa upande wake, Mhe. Emilia aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na kutoa fursa kwa wanawake katika nafasi za uongozi ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya wabunge wanawake kufikia asilimia zaidi ya 30 ya wabunge wote.

Kadhalika, Mwenyekiti huyo alisema Maspika wa CPA – Afrikawanaotarajia kufanya mkutano Novemba 2019, katika jiji la Arusha nchini Tanzania wameridhika sana kwa ahadi ya Serikali ya Tanzania kuhusu ushirikiano na maandalizi mazuri.

Mkutano huo wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika utajadili ajenda mbalimbali pamoja na kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Taarifa kwa Umma: Kuanza kutumika kwa Sheria ya Marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya Mwaka 2019

Marekani Yamfutia viza ya kuingia nchini humo Mwendesha mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda

0
0
Marekani imekifuta kibali cha kuingia nchini humo cha mwendesha mashitaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, Fatou Bensouda baada ya mwanasheria huyo kuanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa vikosi vya Marekani kufanya uhalifu wa kivita nchini Afghanistan. 

Wataalamu wa haki za binadaamu wa Umoja wa Mataifa wameiita hatua hiyo kuwa ni uingiliaji usiofaa kwa mahakama hiyo ya kudumu ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita. 

Hata hivyo wamesema wanajua hatua hiyo haitaathiri uwezekano wa Bensouda kuingia Marekani kufanya majukumu yake katika Umoja wa Mataifa. 

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo mwezi uliopita alielezea uwezekano wa Marekani kuchukua hatua hiyo kwa watumishi wa ICC wanaochunguza madai kama hayo dhidi ya Marekani na washirika wake.

Rais Magufuli: Hatuna Mpango Wa Kuongeza Mikoa Mpiya

0
0
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo ya utawala ikiwemo kuanzisha mikoa mipya na badala yake imejipanga kuimarisha huduma na mahitaji ya miundombinu iliyopo ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru yenye urefu wa kilometa 193 leo (Ijumaa April 5, 2019), Rais Magufuli alisema Serikali imekusudia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, maji, elimu n.k katika maeneo waliopo.

Aliongeza kuwa katika awamu yake yake ya Uongozi, suala la kuongeza maeneo ya utawala halipo na badala yake kuwataka Viongozi wa maeneo hayo wajipange katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya fedha zilizopo kwenda katika kujenga ofisi mpya za Wakuu wa Mikoa mipya na kuwalipa mishahara viongozi hao.

“Tumepanga kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wetu, tumechelewa kuleta Maendeleo hususani kwa wananchi wetu wa mikoa ya kusini, Serikali ninayoiongoza haina mpango wa kuanzisha mikoa mipya , badala yake pesa hizo tutazielekeza katika ununuzi wa madawa na kuboresha miundombinu ya barabara, elimu na nishati’ alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema bado yapo baadhi ya maeneo mengi nchini yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo barabara za lami, hivyo Serikali haitoweza kuleta Maendeleo katika sehemu moja kwa kuwa fedha hizo hazipo kwa kuwa ina na mahitaji makubwa katika kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa huduma muhimu na za msingi kwa Maendeleo ya wananchi zinapewa kipaumbele ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati, kwa kuwa kukamilika kwake kutasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo katika miaka ya nyuma vimekuwa vikisababisha vifo vya makundi hayo ya kijamii.

Akizumgumzia kuhusu Sekta ya Maji, Rais Magufuli alimtaka Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa kuwasimamia wakandarasi wa miradi ya maji nchini, kwani Serikali imekuwa ikitenga kiasi kikubwa cha cha fedha katika miradi ya Maendeleo pasipo na kupata matokeo yaliyotarajiwa, na hivyo kuisababishia hasara Serikali.

“Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Fedha na Mipango, miradi mingi ya maji imekuwa ikitumia fedha nyingi pasipo na kupata matokeo yoyote na wataalamu wetu hasa wakandarasi wamekuwa wazito kutoa tafsiri za nadharia za utaalamu na kuzileta katika nadharia halisi, na mataifa ya nje yanashangwa tunaposhindwa kuvitumia vyanzo tulivyonazo ili kuweza kuzalisha maji ya kutosha’ alisema Rais Magufuli.

Awali akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema kujengwa kwa barabara hiyo kutaimarisha mawasiliano katika ukanda wa kusini unaojumuisha Mtwara, Mingoyo, Masasi, Mangaka, Tunduru hadi Mbamba Bay na hivyo kuzidi kufungua fursa za kiuchumi nanchi jirani za Malawi na Msumbiji.

Alisema hadi kukamilika kwake barabara hiyo imegharimu kiasi cha Tsh Bilioni 173, ambapo Shirika la Misaada la Japan limetoa asilima 23.24, Benki ya Maendeleo ya Afrika asilimia63.32 na Serikali ya Tanzania asilimia 13.35 ikiwemo kodi na kulipa fidia kwa wananchi wanaostahili kwa mujibu wa sheria ya barabara ya mwaka 2007.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania, Shinichi Goto alisema Serikali ya Japan imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru na itaendelea kusaidia miradi mingine ili kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa umaskini kwa wananchi wake yanafikiwa.

Rais Magufuli Kufanya Ziara Ya Siku Mbili Mkoani Njombe

0
0
Na Amiri kilagalila
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John pombe Magufuli,anatarajia kufanya ziara ya siku mbili mkoani Njombe baada ya kutokea mkoani Ruvuma na kukagua baadhi ya miradi mikubwa ikiwemo ya barabara na hospital.

Akizungumza na vyombo vya habari ofini kwake, mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amesema Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli atafanya ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 09-10/04/2019.

Olesendeka amesema kuwa katika Ziara hiyo atatembelea na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo na kuongea na wananchi.

“Mheshimiwa Rais siku ya kwanza atapokelewa na viongozi wa serikali, chama pamoja na wananchi katika mpaka wa mkoa wa Njombe na mkoa wa Ruvuma na baada ya hapo atakwenda kuweka mawe ya msingi katika miradi mikubwa miwili,mradi wa kwanza itakuwa ni kuweka jiwe la msingi kwenye hospital ya Rufaa ya mkoa,awamu ya kwanza imekamilika kwa upande wa huduma za wagonjwa wa Nje (OPD) na imegharimu kiasi cha Tshs.Bilioni 3.6”alisema Olesendeka.

Aidha ataweka jiwe la Msingi katika barabara ya Njombe-Moronga-Makete  inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya takribani Tshs.Bilioni 217 ikiwa ni moja kati ya miradi ya barabara za lami na zege zinazojengwa mkoani Njombe yenye thamani ya zaidi ya Tshs.Bilioni 480 pamoja na kufanya mazungumzo na wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Ramadhani.

Katika hatua nyingine Olesendeka amesema kuwa  siku ya pili ya ziara ya Rais Magufuli atafungua kiwanda cha chai cha UNILIVER (kabambe factory)

“Siku inayofuata tarehe 10 ya mwezi wa 4 mheshimiwa Rais atafanya kazi ya kukaguwa miradi mikubwa miwili,mradi wa kwanza utakuwa ni wa kiwanda cha kabambe Tea factory inayomilikiwa na kampuni ya Uniliver  Plc ya London nchini Uingereza  kwa pamoja na kampuni ya Uniliver  nv ya Roturdam nchini Netheland, mchana atapata fursa ya kufungua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mafinga-Makambako-Igawa eneo la mpaka wa Makambako na wilaya ya Wanging’ombe ambao ni kilometa 64.6 uliojengwa kwa kiwango cha lami ya kisasa na kugharimu Tshs.Bilioni 103,432,947,407.64 na baadaye katika viwanja vya makambako  atapata fursa ya kuzungumza na wananchi wa Makambako na Njombe kwa ujumla”alisema Olesendeka

Kutokana na umuhimu wa ziara hiyo Olesendeka ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa jirani ya Mbeya na Iringa kujitokeza kwa wingi katika maeneo ambayo miradi itazinduliwa pamoja na mikutano ya hadhara ili kumlaki na kumsikiliza Rais na kiongozi huyo wa kitaifa.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

0
0
Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Magonjwa yanayoababisha Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Ni Kama Vile, Kisukari ,presha, Ngiri Ya Kupanda Na Kushuka, Kiuno, Maumivu Ya Mgongo, Tumbo Kuuma Chini Ya Kitovu, Tumbo Kujaa Gesi. Yote Matatizo Yote Haya husababisha Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Kushindwa Kufanya Kazi Kwa Mwenza Wako  .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa Dar anapatikana mbagala Zakhem.  Songea ,bombambili, Shinyanga, Kahama ,mjini, Kwa ,maelezo, Zaidi , Piga Simu 0763172670/ 0715172670,/ ,Sema ,haloo, Dr Sitta... Wote  mnakalibishwa. 

Rais Magufuli: Bila Mkapa Nisingekuwa Waziri, na Urais Yawezekana Msingeniona

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema hatajali maneno ya watu ambao watasema kuwa yeye anajenga miundombinu kwenye Mkoa anaotoka Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa, kwa kuwa anajua alipomtoa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Mtwara kwenye uznduzi wa Kituo cha Afya Mbonde kilichopo Masasi ambapo

“Watu watasema ninamjengea Mkapa, ndio ni kweli ninamjengea Mkapa kwasababu bila yeye nisingekuwa waziri na inawezekana hata urais nisingepata kwahiyo kumjengea kabarabara tu nishindwe

“Ninafahamu Mkapa alinitoa wapi, yako maeneo ya barabara hii kilomita 40 mimi nimeyajua kuliko watu wa Mkoa huu kwasababu Mkapa alikuwa ananituma kwenda kufanya kazi.

"Tulipomaliza ujenzi wa daraja la Mkapa tulimwambia tunalipa jina lake akakataa lakini siku anaenda kulizindua alikuta tumeandika jina lake sasa hivi ana miaka karibu 80 haiwezekani kila anapokwenda mahali walipozikwa wazazi wake tushindwe kutengeneza barabara"

Kuhusiana na Waziri wa awamu ya tatu kupewa kiwanda cha korosho lakini hakiendelezi Rais Magufuli amesema; "kuna kiwanda naambiwa ni cha Waziri wa awamu ya tatu mumnyang'anye, akikataa shikeni pelekeni mahakamani hata kama alikuwa Waziri, tukibembelezana hatutafika ndugu zangu, tubembelezane mimi nikishamaliza muda wangu."

"Nitoe wito kwa waliouziwa viwanda vya kubangua Korosho na Serikali, ni lazima waanze kubangua Korosho na wazinunue, wakishindwa wavirudidhe viwanda, mfano yule wa Newala kiwanda hakifanyi kazi kabisa Waziri wa Kilimo mnyanganye hata kama ni leo." amemalizia Rais Magufuli

Hqbari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 6


Taarifa Kutoka NIDA:Viambatisho Vinavyohitajika Kwenye Usajili wa Vitambulisho vya Taifa

Madereva wa vyombo vya moto Mkoani Arusha watakiwa kutotumia vilevi wakati wawapo barabarani

0
0
Kampeni ya unywaji wa kistarabu inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imezinduliwa rasmi Mkoani Arusha huku madereva wa vyombo vya moto wakihimizwa kuzingatia sheria za barabarani ikiwamo kutotumia vilevi wakati wa kazi. 
 
Kampeni hiyo maarufu kama ‘Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto’ imeenda sambamba na ugawaji wa makoti ya usalama (Reflectors) kwa madereva bodaboda mkoani humo ikiwa ni mkakati wa kuhimiza matumizi ya vifaa hivyo kwa usalama wa watumiaji wa barabara. 
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika leo katika Makao Makuu ya Traffic jijini hapa, Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha amesema kampeni hiyo imelenga kutoa elimu kwa wateja wake nchini ili kupunguza matukio yanayoepukika kama ajali zitokanazo na unywaji wa pombe kupindukia. 
 
“Pombe isipotumika kiistarabu inaweza kuleta madhara katika jamii na mojawapo ya madhara ni pale mtu anapokunywa pombe na akaendesha chombo cha moto ikasababisha ajali jambo ambalo ni hatari kwa madereva na pia ni hasara kwa Taifa,” alisema 
 
Kampeni hiyo inashirikisha wadau mbalimbali ikiwamo Jeshi la Polisi-Kikosi cha usalama barabarani, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), madereva bodaboda pamoja na jamii kwa ujumla ikilenga katika kupunguza ajali zitokanazo na ulevi wa kupindukia nchini. 
 
Kwa upande wake,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha  (RTO)  Joseph Bukombe  alisema kampeni hiyo itasaidia katika kupunguza ajali zinazosababishwa na ulevi huku akiwataka madereva kuzingatia  kuacha kutumia vilevi ili kujihakikishia usalama wawapo barabarani. 
 
 “Unywaji wa pombe kiistarabu ni suala la muhimu sana kwa madereva kwasababu madereva wakiwa kwenye hali ya ulevi ni moja ya chanzo cha ajali za barabarani hivyo tunaipa kipaumbele kampeni hii hapa mkoani Arusha na tutaendelea kutilia mkazo suala hili,” alisema 
 
Aliipongeza SBL kwa kuona umuhimu wa kuwalinda watumiaji wa barabara kwa kutoa elimu hiyo kwa madereva na umma kwa ujumla. 
 
“Pamoja na kuwa wao (Serengeti) ni watengenezaji wa pombe lakini wameona wajibu wao wa kumlinda na kuleta usalama wa madereva na watumiaji wengine wa barabara,” alisema   
 
Kwa mujibu wa ripoti za Jeshi la Polisi-Kikosi cha Usalama barabarani kwa mwaka 2018, jumla ya ajali 876 za bodaboda ziliripotiwa kutokea na kusababisha vifo 366 na majeruhi 694. Ripoti zinaonyesha kupungua kwa ajali hizo ambapo kwa mwaka 2017 zilikuwa 1,459 zilizosababisha vifo 728.
 
  MWISHO 
 
Kuhusu SBL:
 Ikiwa imeanzishwa kama Associated Breweries mwaka 1988, Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) ni moja ya kampuni kubwa za bia nchini Tanzania, ambapo aina zake za bia zinachangia zaidi ya asilimia 20 ya bidhaa hizo katika soko.
SBL  inaendesha viwanda vitatu vilivyopo  Dar es Salaam, Mwanza na Moshi. 
 
Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara yake imekua na kuimarika  zaidi  na  asilimia 51 ya hisa  mwaka 2010 zilizochukuliwa na Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) zimeshuhudia  ongezeko la uwekezaji katika  kukua zaidi na hivyo kusababisha kuongezeka kwa fursa zaidi za ajira kwa watu wa Tanzania.   
 
 Aina za bia zinazozalishwa na SBL  ambazo zimepata tuzo kadhaa za kimataifa  ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick. 
 
SBL pia ni wazalishaji  vinywaji vikali vinavyofahamika duniani  kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum  na Baileys Irish Cream. 
 
 Kwa habari zaidi wasiliana na:
John Wanyancha,
 Mkurugenzi wa Mawasiliano, SBL
Simu: 0692148857
Barua pepe: john.wanyancha@diageo.com   &  Imani Lwinga:Meneja wa Mawasiliano, SBL Tel: 0785428282 Email: Imani.lwinga@diageo.com

Sakata la Makinikia Lamuibua Abdallah Bulembo Bungeni

0
0
Sakata kuhusu mchanga wa makinikia, ubaguzi wa kiitikadi na kufungwa kwa maduka ya fedha jana yaliibuka bungeni wakati wa mjadala hotuba ya bajeti ya Ofisi ya waziri Mkuu, wakati wabunge walipotaka masuala hayo yaangaliwe upya.

Jana, mbunge wa kuteuliwa na Rais, Abdallah Bulembo aliishauri Serikali kuruhusu watu kusafirisha mchanga huo badala ya kuendelea kuwazuia.

Bulembo alisema kuwazuia kusafirisha nje kunasababisha Serikali ikose mapato na pia kuathiri wachimbaji ambao hawana madoa.
 
Wakati Bulembo akiibuka na makinikia, mbunge wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Jaku Hashim Ayub aliitaka Serikali kuweka masharti yenye uwiano katika biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni.

Rais Magufuli Awataka Waziri Mbarawa na Stella Manyanya Wajitathimini Utendaji Wao

0
0
Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Viwanda, Stella Manyanya wajitathmini katika utendaji wao wa kazi.

Katika hotuba yake jana,  Rais alimtaka Profesa Mbarawa akae na wataalamu wake kwa sababu wamekuwa wakifanya vibaya na miradi mingi ya maji haikamiliki .

“Nilikupeleka Wizara ya Maji ukafanye mabadiliko, lakini bado unashindwa kuwachukulia hatua wahandisi wa maji ambao hawasimamii kikamilifu miradi ya maji,” alisema Rais Magufuli jana wakati akizungumza na wananchi wa Tunduru mkoani Ruvuma katika ziara yake ya kikazi.

“Haifurahishi kuona wananchi wanalalamikia ukosefu wa maji, ni uzembe. Wafukuze wakandarasi wa maji na chukua hatua kwa mainjinia wa maji ambao wanafanya vibaya, ukiwa mpole miradi haitakamilika.” Alisema Rais Magufuliania na Msumbiji ambao ni Mto Ruvuma usiokauka.”

Rais Magufuli pia alionesha kukerwa na  Naibu Waziri Manyanya kwa kushindwa kufuatilia kiwanda cha kubangua korosho kilichopo Tunduru ambacho kilikuwa na uwezo wa kubangua tani 5,000 hadi 15,000 lakini mwaka jana kilibangua tani 3,500.

“Naibu Waziri wa Viwanda upo hapa na hili limekushinda kufuatilia, na hapa ni nyumbani kwako umeshindwa kusimamia hiki (kiwanda) kilichokuwa cha Serikali na kimebinafsishwa kwa kwa bei ya kutupwa milioni 75 wakati ni cha mabilioni, utaweza kusimamia viwanda vya Dar es Salaam? Unasubiri mimi ndio nifuatilie?” alihoji.

Rais Magufuli Awatangazia Kiama Majangili

0
0
Rais Magufuli amewatangazia kiama wauaji wa tembo ndani na nje ya nchi na kumtaka Mkuu wa Hifadhi ya Selous kujipanga vizuri.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana, wakati akizindua barabara ya kilomita 193 ya Namtumbo, Kilimasera, Matemanga hadi Tunduru, katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

 “Washtakiwa wa eneo hili wengi ni wanaoua tembo, unakuta Watanzania wanashirikiana na majangili wa nchi jirani, wakiua tembo huku wanawapeleka kule na wakiua tembo kule wanawaleta huku.

“Mtandao wote tumeshaujua, mkae mwendo wa mchakamchaka, wapo wengine wanashirikiana na viongozi, ninafahamu circle.

 “Tunataka Selous iwepo, sasa anayehusika na Hifadhi ya Selous ajipange vizuri, wengine wanaoshirikiana na kutengeneza mtandao ni watendaji kazi wa Selous,” alisema.

Akizungumzia barabara hiyo, Rais Magufuli alisema ujenzi wa kilomita 193 si kazi ndogo na umetumia zaidi ya Sh bilioni 173.3.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images