Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Lugola Asema Mkoa Wa Dar Es Salaam Unaongoza Kwa Biashara Haramu Ya Binadamu Nchini.

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA, Zanzibar
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza nchini kwa kufanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu huku akitoa onyo kali kwa wanaojihusisha na biashara hiyo.

Akizungumza kabla ya kufungua mafunzo ya siku tano ya Watekelezaji wa sheria ya kuzuia biashara hiyo haramu, katika hoteli ya Ngalawa, mjini Unguja, Zanzibar, Lugola amesema wanaofanya kazi hiyo waiache mara moja maana Serikali itawashughulikia.

“Tatizo hili, linaweza onekana likawa dogo, lakini ukweli ni kwamba sote tunafahamu ni kubwa na limeendelea kukua kila mwaka. Uzoefu wa kiutendaji kutoka Sekretareti hususani kutokana na wahanga wanaookolewa unaonyesha kwamba biashara hii inafanyika sana Mkoa wa Dar es Salaam Tanga, Mwanza, Kigoma, Geita, Dodoma, Singida, Arusha, Manyara, Shinyanga na Tanzania Zanzibar,” alisema Lugola.

Lugola alisema licha ya changamoto hizo, lakini Serikali katika kipindi cha kuanzia Januari mpaka Disemba 2018 imefanikiwa kuwaokoa jumla ya Watanzania 147 waliokuwa wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji binadamu. Kati ya wahanga 141walikuwa wakitumikishwa katika mikoa mbalimbali nchini.

Pia Lugola alisema wahanga 6 walikuwa wakitumikishwa nje ya nchi ambapo watano walikuokolewa kutoka Thailand na mhanga mmoja kutoka Malasia, na Mhanga mmoja aliokolewa hapa nchini alipokuwa akitumikishwa na taratibu za kumrudisha kwao Msumbiji bado zinafanyika.

“Napenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa hatutamuacha salama mtu yeyote, wanaojihusisha na biashara hii waiache mara moja kabla mkono wa sheria haujawafikia,” alisema Lugola.

Aidha, Lugola alisema Serikali ya Tanzania, haijaikataza Watanzania kufanya kazi nje ya nchi, bali imeweka taratibu zenye lengo za kumlinda Mtanzania na madhara yatokanayo na biashara hiyo haramu.

Kwa upande wake, Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara hiyo Haramu kutoka Wizara hiyo, Separatus Fella, alisema zaidi ya washiriki 80 wameshafika katika mkutano wa mafunzo hayo, na matarajio yake makubwa washiriki watapata elimu nzuri kwa ajili ya kupambana na biashara hiyo haramu.

“Mafunzo haya yanatolewa kwa wadau wanaotekeleza sheria ya kuzuia na kupambana na Biashara hiyo, Maafisa Polisi, Uhamiaji, waendesha mashtaka, Mahakimu, Maafisa Ustawi Jamii na Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGO’s) yaliyopo Zanzibar,” alisema Lugola.

Fella alifafanua kuwa, mafunzo hayo yanafanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Marekani linalojihusisha na Masuala ya Utafiti (RTI).

Wimbo Mpya: Banana Zorro Ft Ashura Kitenge – Aiyaya

$
0
0
Wimbo Mpya: Banana Zorro Ft Ashura Kitenge – Aiyaya

Video Mpya ya Ommy Dimpoz - You Are The Best

$
0
0
Video Mpya ya Ommy Dimpoz - You Are The Best

Ufafanuzi Kuhusu Habari Iliyochapishwa Katika Gazeti La Nipashe Kwamba Magereza Yakiri Tatizo Wafungwa Kuingiliana Kinyume Na Maumbile

$
0
0
Katika Gazeti la Nipashe ISSN 0856 NA. 0579874 la tarehe 25 Machi, 2019 ukurasa wake wa kwanza ilichapishwa habari kwamba “MAGEREZA YAKIRI TATIZO WAFUNGWA KUINGILIANA”. 

Aidha, katika ukurasa wa pili (02) wa gazeti hilo, imeelezwa kuwa wafungwa wa kiume katika Gereza la Mkoa wa Shinyanga (Mhumbu), wamedaiwa kufanya ngono kinyume na maumbile, hali iliyoelezwa kuchangia maambukizi ya magonjwa ikiwemo virusi vya UKIMWI.

Jeshi la Magereza linakanusha habari hiyo kwamba wafungwa wa kiume wanaingiliana kimwili katika Gereza Shinyanga na kwamba taarifa hiyo siyo ya kweli. 

Ieleweke kuwa aliyenukuliwa kutoa taarifa hiyo, Ofisa wa Dawati la Jinsia la Magereza Mkoa wa Shinyanga, Victoria Kizito siyo Msemaji wa Jeshi la Magereza na hana mamlaka ya kutoa wala kuthibitisha habari/taarifa kwa niaba ya Jeshi.

Aidha, Sheria za nchi ikiwemo Sheria na kanuni za Jeshi la Magereza zinakataza vitendo vya aina hiyo kwa vile ni kosa la jinai. 

Vitendo hivyo vinadhibitiwa ndani ya magereza kwa kuwaelimisha wafungwa madhara yake na pindi kunapotokea jaribio la mfungwa kujihusisha na vitendo hivyo, Mhusika huchukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za Jeshi ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Vyombo vya habari na waandishi mnakumbushwa kuwa taarifa zinazolihusu Jeshi la Magereza hutolewa au kuthibitishwa na Kamishna Jenerali wa Magereza au Msemaji wa Jeshi. Hivyo taarifa zozote zinazotolewa nje ya utaratibu huo zisipokelewe.

Imetolewa na;

P.M. Kasike, 
ndc KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA

Msajili wa Vyama vya Siasa Atishia Kukifuta chama cha ACT- Wazalendo

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, ametishia kukifutia usajili Chama cha ACT-Wazalendo, kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa ikiwamo kuchoma moto bendera ya Chama cha Wananchi (CUF).

Mtungi kupitia barua yake kwa ACT Wazalendo, ametoa siku 14 kwa chama hicho kuwasilisha maelezo ya maandishi kuwa ni kwanini usajili wake wa kudumu usifutwe kutokana na kukosa sifa kukiuka Sheria za Vyama vya Siasa na kutowasilisha ripoti ya ukaguzi kuanzia mwaka 2013-17.

Taarifa iliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa jana Jumatatu Machi 25, imesema kutowasilisha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha 2013/14, chama hicho kinakuwa bado hakijakidhi matakwa ya Msajili wa Vyama vya Siasa na hivyo chama hicho pia kinakuwa kimekiuka Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258.

“Aidha, baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa kesi Na. 23 ya mwaka 2016, iliyokuwa inahojiuhalali wa Profesa Ibrahimu Lipumba, Machi 18, 2019, kumekuwa na matukio ya uvunjifu wa sheria ikiwemo kuchoma moto bendera za CUF, uliofanya na watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, wanadai sasa ni wanachama wa ACT. Kitendo cha kuchoma bendera ya chama cha siasa ni kukiuka kifungu cha 11C, cha sheria ya vyama vya siasa.

“Vile vile katika mitandao ya kijamii imeonekana video watu wakipandisha bendera ya ACT kwa kutumia tamko takatifu la dini ya kiislamu (Takbir), kitendo hiki pia ni kukiuka kifungu cha (9) (1) (c) cha Sheria ya Vyama vya Siasa inayokataza kuwa na ubaguzi wa kidini kwa wanachama wake na kifungu cha (9) (2) (a), kinachokataza katiba, sera au vitendo vya chama cha siasa kuhamasisha au kueneza dini fulani,” imesema taarifa hiyo ya msajili.

Pamoja na mambo mengine, msajili amekumbushia onyo lake la Machi 18 mwaka huu akikemea kitendo cha wananchi wa chama hicho huku akionyesha mshangao kwa chama hicho kutochukua hatua ya kukemea suala hilo akisema chama hicho kimeafiki au kilitoa maelekezo kufanyika kwa vitendo hivyo.

“Kutokana na maelezo hayo, vitendo hivyo vinaakisi ukiukwaji wa dhahiri wa Sheria ya Vyama vya Siasa ambao pia unasababisha chama chenu kupoteza sifa za usajili wa kudumu.

“Hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa anatumia fursa hii kukufahamisha wewe na wanachama wa ACT-Wazalendo nia yake ya kufuta usajili wa kudumu wa chama chenu kwa sababu hizo zilizotajwa,” amesema Msajili katika taarifa yake.

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)......Amteua Julius Ndyamukama Kujaza Nafasi Hiyo

$
0
0
Rais Magufuli amemteua Julius Ndyamukama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuchukua nafasi ya Richard Mayongela ambae uteuzi wake umetenguliwa na anatakiwa kuripoti Wizara ya Ujenzi kupangiwa kazi nyingine.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yatangaza Kuanza Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura

$
0
0
Na Margareth Chambiri
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kufanya zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura kwa majaribio katika Kata mbili za Kibuta iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani na Kihonda katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkoani Morogoro.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne Tarehe 26. 03. 2019) imesema Uandikishaji huo wa Majaribio utakaoanza Machi 29, hadi Aprili 04, 2019 utafanyika katika vituo 20 vya kuandikisha Wapiga Kura ikiwa ni vituo 10 katika kila Kata.  

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uandikishaji huo unalenga katika kuvifanyia majaribio vifaa na mfumo wa Uandikishaji Wapiga Kura ili kubaini changamoto kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo.

Imezitaja sifa za watu watakaoandikishwa katika uandikishaji huo kuwa ni raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 au atakayetimiza umri wa miaka 18 siku ya Uchaguzi  Mkuu ujao.
Aidha uandikishaji huo hautawahusu raia walio chini ya kiapo cha utii wa nchi nyingine, aliyebainika kuwa hana akili timamu au yuko kizuizini kama mhalifu mwenye ugonjwa wa akili au yuko kizuizini kwa ridhaa ya Rais.

Taarifa hiyo imeendelea kutaja watu ambao hawatahusika katika majaribio hayo ya uboreshaji kuwa ni mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama au anatumikia kifungo kinachozidi miezi sita pamoja na mtu aliyepoteza sifa za kuandikishwa kuwa Mpiga Kura chini ya Sheria za Uchaguzi au Sheria nyingine yoyote inayohusu makosa ya uchaguzi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawajulisha wakazi wa Kata hizo zinazofanya Uandikishaji wa Majaribio na ambao walijiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 kuwa wanaweza kutumia fursa hiyo kuhakiki taarifa zao katika vituo walivyojiandikishia.

Wakati huo huo Tume inatoa fursa kwa Vyama vya Siasa kuweka Wakala mmoja  katika kila kituo cha Kuandikishia Wapiga Kura kwa lengo la kushuhudia na kujiridhisha juu ya taratibu zitakazotumika pamoja na changamoto zitakazojitokeza ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kabla ya zoezi rasmi la Uandikishaji.

Tume imevitaka Vyama vyenye nia ya kuweka Mawakala katika uandikishaji huu wa Majaribio kuwasilisha orodha ya majina ya Mawakala na vituo walivyopangiwa kwa Maafisa Waandikishaji wa Halmashauri za Kisarawe na Manispaa ya Morogoro.

Kadhalika Vyama vimetakiwa kuwasilisha nakala mbili za barua za utambulisho zikiwa na picha mbili na nakala mojawapo kati ya Kitambulisho cha Taifa au Kadi ya Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria au Leseni ya Udereva na kwamba kila Chama kitagharamia Wakala wake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo wakati wa uandikishaji huo wa majaribio Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatumia runinga, redio, mitandao ya kijamii na magari ya matangazo kwa ajili ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika zoezi hilo.

Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Kaijage kupitia taarifa hiyo amewaomba wakazi wa Kata za Kibuta na Kihonda kujitokeza kwa wingi katika Uandikishaji huo wa majaribio na kutoa ushirikiano kwa Tume wakati wote wa utekelezaji wa jukumu hilo muhimu kwa mustakabali wa demokrasia ya Taifa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi hufanya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoipa Tume mamlaka ya kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano pamoja na Madiwani kwa Tanzania Bara.

Tume kwa mujibu wa Kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya Uchaguzi Mkuu mmoja na unaofuata. 

Taarifa ya Kiongozi wa Chama Ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto Kuhusu Tishio la Msajili wa Vyama vya Siasa Kukifutia Usajili Chama cha ACT Wazalendo

$
0
0
1. Utangulizi
Jana tarehe 25 Machi 2019, tulipokea barua kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa yenye kumbukumbu Na. HA. 322/362/20/98 ambayo; pamoja na mambo mengine, ilieleza juu ya kusudio la serikali kutaka kukifuta Chama cha ACT Wazalendo.

Barua hiyo ilieleza kuhusu mambo matatu yaliyosababisha Ofisi ya Msajili itangaze kusudio hilo ovu juu yetu. Kwanza ilizungumza kuhusu hoja zinazohusiana na ukaguzi wa hesabu za chama uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), pili kuhusu vitendo vya kuchomwa hadharani kwa bendera na kadi za chama cha CUF na tatu matumizi ya neno takbira kama yalivyoonekana katika baadhi ya video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii.

Naomba niwaeleze kwa kina kuhusu hoja moja baada ya nyingine kabla ya kutoa maoni yetu na mwelekeo wa chama baada ya kupata barua hii.

1. Kuhusu Ukaguzi wa CAG

Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa inadai kwamba ACT imekiuka Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kutopeleka kwake hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kama sheria inavyotaka.

Tuhuma hizi hazina ukweli wowote. ACT Wazalendo ilianzishwa na kupewa Usajili wa Kudumu tarehe 5 Mei, 2014 na kwa hivyo, kwa mwaka huo wa fedha (2013/14) Chama chetu kilikuwa na miezi miwili tu ya kukaguliwa. Kazi yetu ACT Wazalendo kama chama cha siasa ni kuwasilisha ripoti kwa ajili ya kukaguliwa na CAG. Ripoti ya hesabu za 2013/14 imewasilishwa kwa CAG kwa barua.

Kwa kutumia Kanuni za Kimataifa za Kihasibu na kwa ushauri wa CAG, chama chetu kilielezwa kinaweza kuunganisha hesabu za mwaka 2013/2014 na 2014/2015 katika ripoti moja, wakieleza kuwa hilo jambo la kawaida kabisa katika kanuni za uhasibu kwani inaruhusiwa kuunganisha hadi miezi 18. Kwa kuunganisha huku hesabu, ACT ilikuwa na miezi 14 tu.

Kabla ya kuchukua uamuzi wa kukubali ushauri huu wa kuunganisha hesabu kutoka Ofisi ya CAG, Chama chetu kilimwandikia Msajili wa Vyama vya Siasa (Kwa barua mbili zenye kumbukumbu namba AC/HQ/MSJ/2015/006 na AC/HQ/MSJ/2015/008 za tarehe za tarehe 22 na 29 Januari 2015) naye akajibu na kuridhia hesabu za miezi miwili ya mwaka 2013/2014 kuunganishwa kwenye mwaka wa fedha 2014/2015 (kwa barua yenye kumbukumbu Na. KA/ 322/20/60 ya tarehe 16 Februari 2015).

Taarifa zote hizi ziko wazi kwa kwake mwenyewe Msajili na kwenye Ofisi ya CAG, kuanzia barua za kutaarifiwa Juu ya kukusanywa kwa pamoja kwa taarifa ya Ukaguzi wa Mahesabu ya ACT Wazalendo kwa miezi 14 ya mwanzoni (miezi miwili ya mwaka 2013/14 na miezi 12 ya mwaka 2014/15), mpaka ripoti husika ya Ukaguzi kutoka kwa CAG. Tumeshangaa sana anaposema ana nia ya kutufuta kwa kutokupeleka ripoti ambayo tayari anayo Ofisini kwake.

ACT Wazalendo tunajua kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haina utaalam wa Masuala ya Ukaguzi wa Fedha na Matumizi ya Vyama. Hivyo tunajua kuwa upo uwezekano kuwa wameshindwa kuisoma, kuichambua na kuielewa ripoti hiyo ya Ukaguzi wa Hesabu za ACT Wazalendo kwa mwaka wa Fedha wa 2014/15, hatuwalaumu kwa jambo hilo. Ndio maana kisheria kazi hiyo ya ukaguzi amepewa CAG.

Lakini Msajili wa Vyama vya Siasa nchini angekuwa na nia njema, angeweza tu kuomba ufafanuzi au uchambuzi wa taarifa husika kutoka kwa CAG au hata kwetu ACT Wazalendo, Chama chenye uzoefu wa kuchambua hizo ripoti za CAG, na angepewa taarifa husika. Taharuki hii aliyoisababisha haikuwa na sababu yeyote, ni suala la uelewa tu.

Tunawaahidi wanachama wa ACT Wazalendo kuwa sisi Viongozi wao tutajibu barua hii ya msajili kwa kumuelewesha. Zaidi tunaishauri Ofisi ya Msajili kuwa ni vyema basi wakishindwa kuzielewa taarifa tunazowapelekea warudi kwanza kwa CAG ama kwetu kuomba ufafanuzi na uchambuzi kabla ya kuandika hizi barua za kutishia kutufuta.

2. Kuhusu Kuchoma bendera na kadi

Barua yenyewe ya Msajili iliyotufikia inasema kwamba imeona picha zinazoonyesha “wanaodaiwa” kuwa wanachama wa ACT Wazalendo wakichoma bendera na kadi za chama cha CUF. Katika hili, Msajili mwenyewe anaonyesha kwamba hana uhakika kama kweli wahusika ni wanachama wa ACT.

Si ilibidi Msajili ajiridhishe kwanza kuwa wale ni Wanachama wa ACT Wazalendo? Kama hajaridhisha anawezaje kutangaza NIA ya kutaka kufuta Usajili wa Chama chetu kwa jambo hilo? Watanzania waone Ofisi ya Msajili ilivyo na NIA Mbaya na Chama chetu, Watanzania waone namna Ofisi ya Msajili, inayoongozwa na Jaji inavyotoa tuhuma pamoja na kutoa hukumu bila hata ya kuwa na Ushahidi.

Chama chetu HAKIHUSIKI kabisa na uchomaji wa bendera wala kadi za Chama chochote. Kihistoria sisi ni Chama cha Masuala, tunaojikita juu ya Utetezi wa Wakulima wa Korosho, Mahindi, Giligilani, Karafuu, Mkonge na Mbaazi wanaokosa masoko ya bidhaa zao. Sisi tumezoeleka kuwa ni wapaza Sauti za Wafuagaji wanaotaifishiwa Mifugo yao na Wavuvi wanaonyang’anywa nyavu zao.

ACT Wazalendo tunatambulika kwa Uchambuzi wa Bajeti na kupinga Sera za mbaya za kuongoza Uchumi zinazowafanya wananchi waishi maisha magumu. Matumaini ya wananchi kwetu ni kwa sababu wamezoea kutuona tukichambua ripoti za CAG na kuhoji kutokuonekana kwa TZS 1.5 Trilioni na kusimamia uwajibikaji wa Serikali. Chama chetu utambulisho wake ni utetezi wa wanyonge wanaoonewa popote pale duniani, iwe ni Sahara Magharibi, Palestine au MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji). Rekodi zetu zinatutambulisha hivyo.

Tumesikitika sana Ofisi ya Msajili hata kuwaza tu kuwa Chama cha Masuala cha namna hiyo kinaweza kuhusika na mambo ya Uchomaji wa bendera na kadi za vyama vingine. Tumesikitika sana.

3. Kuhusu "Takbir"

Barua hiyo ya Msajili inaeleza pia kwamba chama chetu kimevunja sheria ya vyama vya siasa kwa sababu “wanaodaiwa kuwa wanachama wetu” wametumia maneno takbira kwenye shughuli za kichama na kwamba maneno hayo yana udini. Majibu ya hili ni kama kwenye suala la kudaiwa kuchoma kadi na bendera. Msajili hajaainisha hao wanaodaiwa kuwa ni wanachama wetu wana kadi namba ngapi za uanachama na ni kutoka tawi gani la chama chetu.

ACT Wazalendo ni chama cha siasa cha watu wa matabaka na dini zote na hata wale wasio na dini. Katika Katiba yetu ya chama tumeonyesha wazi kwamba hatufungamani na dini yoyote na ndiyo sababu tumeruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa.

Tuna ushauri tu kwa Ofisi ya Msajili, katika nchi ambayo Viongozi karibu wote wa Serikali wanaanza hotuba zao kwa salamu za kidini za “Bwana Yesu Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo na Assalaam Aleykum” ni rahisi kwa “wanaodaiwa kuwa wanachama wa ACT Wazalendo” kutumia kaulimbiu za Dini zao kama wanavyofanya Viongozi wa Serikali.


4. Mtazamo Wetu

Barua ya Msajili haina nia njema kwa ACT Wazalendo na wapenda demokrasia wote hapa nchini. Kukosekana kwa nia njema kulionekana mapema kabisa baada ya barua iliyotakiwa kutumwa kwetu kusambazwa kwanza katika mitandao ya kijamii kabla hata haijatufikia ofisini. Taswira tunayopata ni kwamba ilivujishwa makusudi na ofisi ya msajili kutimiza dhamira ovu waliyonayo dhidi yetu.

Serikali na Chama cha CCM vimepata mchecheto na ufuasi mkubwa wa chama chetu, hasa baada ya Maalim Seif Sharif Hamad na waliokuwa Viongozi wenzake kutoka chama cha CUF kuhamia ACT Wazalendo. Wameogopa zaidi kuwa sasa ACT Wazalendo ndio kimbilio la Wazanzibari wote waliomchagua Maalim Seif kuwa Rais wao kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Ushauri tu kwa CCM na Serikali yake, hata wasiwaze tu kuifuta ACT Wazalendo, hatua mbaya ya namna hiyo ya kionevu itawanyima fursa karibu theluthi moja ya Watanzania ya kufanya siasa kwa njia halali za kisheria. Watu hawa wakinyimwa fursa hii kionevu kupitia ACT Wazalendo watatumia njia nyengine zinazoweza hata kuleta mpasuko kwa Taifa letu. Ikifika hatua hiyo, sisi Viongozi wa ACT Wazalendo hatutakuwa na sauti ya kuwakataza watu hawa watakaodhulumiwa fursa ya kufanya siasa kwa njia halali za kisheria.

Tunachukua nafasi hii pia kuzitaka Taasisi za Dini, Asasi za Kiraia, Nchi marafiki na wahisani kupaza sauti juu ya jambo hili. Wasikae kimya wanapoona uonevu unataka kufanyika.

5. HATURUDI NYUMA

Kwa wanachama wa ACT Wazalendo, wafuasi na watanzania kwa ujumla, barua hii ya Msajili haijatutisha wala kututikisa. Na tutaazima busara za mwanachama wetu mwandamizi, Maalim Seif, kuwa TUSICHOKOZEKE. Na hatutachokozeka.!

Tamko langu hili kwenu liwe ni ishara kwenu kuwa Chama kiko salama na imara, na kwamba barua hii ya Msajili itajibiwa kwa hoja, na ushahidi wa hoja kabla ya hizo siku 14 alizozitoa. Ulinzi wa chama hichi ni wajibu wenu, sisi Viongozi wenu tuko hapa kutoa dira na mwongozo.

Endeleeni kugawa kadi na shughuli nyengine za uenezi wa Chama chetu, ziara zetu sisi Viongozi kuja kukagua shughuli zenu ziko kama ilivyo ratiba yetu. Huko mliko mtembee kwa fahari mkijua kuwa wapinzani wetu sasa wanatuogopa, hawataki tena kusubiri uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, wanataka kutufuta kwa hila. Tunajua hawataweza.

Mungu yupamoja nasi.
Nawashukuru sana.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
Machi 26, 2019
Dar es salaam

Zitto Kabwe amtangaza Juma Duni Haji ‘Babu duni’ Kuwa Naibu Kiongozi wa ACT-Wazalendo

$
0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ametangaza kumteua Juma Duni Haji maarufu kama Babu Duni kuwa naibu kiongozi wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya ACT-Wazalendo, Kijitonyama, Dar es Salaam leo Machi 26, 2019, Zitto amesema kuwa kwenye kikao cha uongozi wa chama, wameridhia Duni kuwa naibu kiongozi wa chama hicho.

"Nimepewa mamlaka na katiba ya chama kumteua, nikawasilisha kwa uongozi na wameridhia na ataanza kesho kutumikia nafasi hiyo", amesema Zitto.

Duni anashika wadhifa huo ikiwa ni siku chache zimepita tangu alipokabidhiwa kadi ya uanachama ya ACT akiwa pamoja na viongozi wengine kutoka CUF akiwamo Maalim Seif Sharif Hamad.

Katika uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2015, Duni alihamia CHADEMA na kupitishwa kuwa mgombea mwenza wa urais kupitia CHADEMA ikiungwa mkono na vyama washirika vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vya NCCR-Mageuzi, NLD na CUF. Baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Duni alirejea katika chama chake za zamani cha CUF.

Jeshi La Polisi Mbeya Linawashikilia Watu 21 Kwa Tuhuma Mbalimbali Ikiwa Ni Pamoja Na Kufanya Shughuli Za Uganga Bila Kibali

$
0
0
KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO YA WIZI.
Mnamo tarehe 23.03.2019 saa 14:39 mchana huko eneo na Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata JOSEPH MGAYA [27] Mkazi wa Ilomba akiwa na Pikipiki MC 395 BYN aina ya Kinglion ambayo mtuhumiwa amekiri kuiiba Pikipiki hiyo huko Kijiji cha Lupatingatinga Wilaya ya Chunya. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.

KUFANYA SHUGHULI ZA UGANGA BILA KIBALI.
Mnamo tarehe 25.03.2019 saa 00:10 usiku huko katika Kitongoji cha Mapinduzi ‘B’ kilichopo katika Kijiji cha Idunda, Kata ya Itewe, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata PASCHAL PATRICE [30] Mkazi wa Kijiji cha Idunda na wenzake 19 wakifanya shughuli ya uganga bila kibali.

Watuhumiwa wote wakiwemo wanawake 03 walikutwa wakiwa kwenye nyumba ya mtu aliyefahamika kwa jina moja la MWARABU mkazi wa Dar es salaam. Pia katika nyumba hiyo wamekutwa watu watatu wote wanaume waliokuwa wamekwenda kutibiwa hapo. Upekuzi umefanywa ndani ya nyumba hiyo na kufanikiwa kupata begi ambalo ndani yake likiwa na kibuyu kimoja, chupa mbili za plastiki zenye unga unaodhaniwa kuwa ni dawa za kienyeji, kikopo cha plastiki cha njano chenye unga unaodhaniwa kuwa dawa za kienyeji zinazotumiwa na waganga kutolea tiba pamoja na ngoma moja. Upelelezi unaendelea.

Gari aina ya FUSO lililokuwa likisafirisha magunia ya Mahindi kwenda nchini Malawi kwa njia ya magendo.

KUSAFIRISHA BIDHAA NJE YA NCHI BILA KIBALI.
Mnamo tarehe 24.03.2019 saa 12:15 mchana huko Kitongoji cha Mwambuluko, Kijiji cha Isaki, Kata ya Katumbasongwe, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa mbeya. Askari Polisi walikamata gari moja lenye namba T. 268 BNH aina ya Mitsubishi Fuso truck likiwa limebeba magunia yenye nafaka mahindi makavu yapatao magunia 88 mali ya mtu mmoja aitwaye DORIN KAONGA [35] Mmalawi, Mfanyabiashara na Mkazi wa Kalonga – Malawi na GLORY KAFWILA [32] Mmalawi, Mfanyabiashara na Mkazi wa Kalonga – Malawi.

Dereva wa gari hilo alikimbia kusikojulikana na msako mkali wa kumtafuta unaendelea. Gari hilo lilikua likielekea kivuko haramu cha Nyasa katika mto Songwe mpakani mwa nchi ya Tanzania na Malawi kwa ajili ya kuyavusha magunia hayo ya mahindi kwa mitumbwi kuelekea nchi hiyo jirani ya Malawi.

Gari hilo lililotumika kubeba magunia hayo ya mahindi ni mali ya mtu mmoja aitwaye SHABAN ADIL KAJUNI wa huko Wilaya ya Rungwe. Vielelezo gari hilo na magunia hayo ya mahindi vimekabidhiwa mamlaka ya mapato idara ya forodha Kasumulu na hatua zaidi za kisheria. Upelelezi unaendelea.

Waziri Mkuu: Wizi wa Mitihani Unalivunjia Taifa Heshima

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa onyo kali kwa baadhi ya Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya wanaoshirikiana na waliamu kujihusisha na wizi, udanganyifu na uvujaji wa mitihani waache mara moja tabia hiyo na mwenendo huo kwa sababu unalivunjia heshima na hadhi Taifa.

“Kamati za Mitihani za Mikoa na Wilaya ziendelee kusimamia sheria, kanuni na taratibu bila ya woga, upendeleo na tusiyumbishwe na hatua za kinidhamu na kiutumishi kwa mujibu wa sheria.Hatua ziendelee kuchukuliwa dhidi ya wote wanaobainika kukiuka sheria, taratibu na miongozo inayotolewa”.

Waziri Mkuuametoa onyo hilo leo (Jumanne, Machi 26, 2019) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Umoja wa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya(REDEOA), uliofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma. Kauli mbiu ya mkutano huo inasema “Elimu Bora Itatufikisha Katika Uchumi wa Kati Ifikapo 2025”

AmesemaBaraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ni chombo ambacho kwa muda mrefu kimejijengea sifa kubwa sana nchini na barani Afrika, ambapo Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha rasilimali ili kukifanya chombo hiko kuwa imara na cha kisasa.

Waziri Mkuu amesema hali hiyo imezifanya nchi mbalimbali kuja nchini kujifunza masuala ya upimaji na uendeshaji wa mitihani. “Nimejulilishwa pia hivi sasa hapa nchini wapo Viongozi wa Mabaraza ya mitihani kutoka nchi za Afrika Mashariki”.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema suala la tatizo la nidhamu mbaya ya wanafunzi ni jukumu la walimu wote, hivyo wanatakiwa watekeleze majukumu yao ya kufundisha, kulea, kuwaongoza na kuwaendeleza wanafunzi kimwili, kiakili na kiroho kwa uadilifu na kuzingatia sheria.

Waziri Mkuu amesema Serikali imesikitishwa sana na matukio ya hivi karibuni ya athari ya viboko kwa wanafunzi shuleni ikiwemo kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu pamoja na tukio la kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius wa shule ya msingi Kibeta Mkoani Kagera.

“Ninatambua si kusudio la walimu kuwadhuru wanafunzi lakini tukubaliane kuwa kuna udhaifu katika utaratibu wa utoaji na usimamizi wa adhabu ya viboko shuleni. Maafisa Elimu kawakumbusheni walimu wote nchini wazingatie mwongozo wa kutoa adhabu shuleni chini ya kifungu cha 61 cha sheria ya Elimu sura 353 pamoja na kanuni zake”.

“Adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhamu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima. Na adhabu hii itatolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi. Nina hakika tukisimamia utaratibu, matukio haya yaliyoanza kuonekana yatakoma”.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya hao kwa sababu wanafanya kazi kubwa ambayo imechangia kupandisha ufaulu wa kidato cha sita na cha nne nchini. Amewasisitiza waendelee kufanya kazi kwa bidii.

Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka maafisa hao wawe wanatoa taarifa sahihi kuhusu idadi ya wanafunzi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.

Awali, Mwenyekiti wa REDEOA, Germana Mung’aho amesema umoja wao unatekeleza majukumu yao ya kusimamia elimu kikamilifu nchini, lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli, ambaye anasisitiza watu wafanye kazi.

Amesema umoja huo una wanachama zaidi ya 400 na ulianzishwa ili kusimamia utoaji wa elimu nchini. Katika mkutano huo wanatarajia kujadiliana changamoto mbalimbali za sera ya elimu na namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Kadhalika, Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali iwapatie magari maafisa hao watakayoyatumia kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya elimu kwenye maeneo yao ya kazi, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Dereva aieleza mahakama alivyokuwa akichukua fedha kwa mhasibu kumpelekea Malinzi

$
0
0
Aliyekuwa dereva wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, Steven John, ameileza mahakama alikuwa anachukua fedha kutoka kwa aliyekuwa mhasibu wa shirikisho hilo, Hellen Ndaro na kumpelekea Malinzi.

Aidha, dereva huyo ambaye ni shahidi katika kesi hiyo ya utakatishaji fedha inayomkabili Malinzi na wenzake, baada ya kujitambulisha alishindwa kuongea akawa anatiririka machozi.

Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alimuita shahidi huyo lakini alinyamaza kimya huku akifuta machozi.

“Macho yameaanza kuuma au una tatizo gani shahidi? alihoji hakimu wakati shahidi anafuta machozi.

Dereva huyo amedai hajawahi kumchukulia fedha Malinzi mara mbili kwa siku moja na kwamba wakati anachukua fedha hizo alikuwa akisaini fedha lakini wakati akimkabidhi Malinzi hakuwa anasaini.

Shahidi huyo akiongozwa na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, amedai Septemba 26 mwaka 2016, alimpelekea Malinzi Dola za Marekani 28,650 na Dola 24,000.

Septemba 26 mwaka 2016 alimpelekea Sh milioni nne na kwamba yeye ndiyo alikuwa akisaini hati za malipo kwa niaba ya Malinzi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF,  Nsiande Mwanga, Meneja wa Ofisi TFF, Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja  wanakabiliwa na mashitaka 30 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za Marekani 173,335.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wanaendelea kusota rumande kwa sababu wanakabiliwa na mashitaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Hussein Bashe: Sitatumia tena salamu ya ‘Assalaam Alykum’ wala ‘Bwana Yesu Asifiwe’

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Hussein  Bashe amesema kuwa hatotumia tena salamu za kidini katika mikutano ya hadhara ili kutokiletea chama chake matatizo ya kisheria.

Ameyasema hayo mara baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kukionya na kukitaka kujieleza Chama Cha ACT- Wazalendo baada ya kutumia salamu za kidini kinyume na sheria ya vyama vya siasa nchini.

Amesema kuwa hatotumia tena salamu hizo ambazo zitapelekea chama cha Mapinduzi (CCM) kuonekana kwamba kinabagua wasio na dini.

“Kuanzia leo nikienda kwenye mikutano ya hadhara situmii salaam kama “Assalaam Alykum” or “Bwana Yesu Asifiwe” nisije nikakiletea matatizo chama chetu CCM nakuonekana kinabagua wasiokua na dini. “tafakuri yangu tahadhari kabla ya mauti”. ameandika Bashe kwenye ukurasa wake wa kijamii.

Aidha, tafakuri hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Fransic Mutungi kutishia kukifuta Chama Cha ACT- Wazalendo kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa ikiwamo kuchoma moto bendera ya Chama cha Wananchi (CUF) huku wakitumia maneno ya kidini.

Hata hivyo, sehemu ya taarifa ya msajili wa siasa ilisema kwamba, “vile vile katika mitandao ya kijamii imeonekana video watu wakipandisha bendera ya ACT kwa kutumia tamko takatifu la dini ya kiislamu (Takbir), kitendo hiki pia ni kukiuka kifungu cha (9) (1) (c) cha Sheria ya Vyama vya Siasa inayokataza kuwa na ubaguzi wa kidini kwa wanachama wake na kifungu cha (9) (2) (a), kinachokataza katiba, sera au vitendo vya chama cha siasa kuhamasisha au kueneza dini fulani”

Rais Wa TFF Wallace Karia Awashukuru Watanzania Kuiunga Mkono Taifa Stars......Aomba hamasa Hiyo Iendelee kwa Twiga Stars na Serengeti

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) ametoa shukrani za dhati kwa Serikali,Taasisi Mbalimbali,Vyombo vya Habari,Vyombo vya Usalama na kila Mtanzania kwa kuiunga mkono Timu ya Taifa “Taifa Stars”.
 
Amesema TFF inaamini kila mmoja alihamasika kuiunga mkono Taifa Stars hasa kutokana na kiu ya kila mmoja kuona  inacheza AFCON.
 
“Hakika ilikuwa hamasa kubwa na Uzalendo wa hali ya juu ambao unapaswa kupongezwa kwa namna ambavyo kila mmoja alijitoa kwa nafasi yake kwaajili ya timu yake ya Taifa” Amesema Rais wa TFF Ndugu Karia.
 
Uungwaji mkono uliofanyika kwa Taifa Stars ni sehemu kubwa ya morali kwa wachezaji na TFF inaamini Watanzania wataendelea kuziunga mkono timu za Taifa na Wawakilishi wa Tanzania wanaokabiliwa na mashindano ya Kimataifa.
 
Kwasasa timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” ipo Kambini ikijiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Olympic dhidi ya DR Congo utakaochezwa April 5,2019,Pia timu ya Vijana U17 “Serengeti Boys” ipo Kambini ikijiandaa na mashindano ya AFCON ya Vijana U17 yatakayofanyika Tanzania April 14-28,2019.
 
Karia amewaomba Watanzania waziunge mkono timu hizo kwa kujitokeza kwa wingi ili kuwa sehemu ya hamasa ya kufanya vizuri kwa timu zetu.
 
TFF itaendelea kuhakikisha timu hizi zinapata maandalizi mazuri ili kupata matokeo chanya katika mashindano yanayowakabili.
 
Ni Imani ya TFF kuwa Watanzania wataendelea kujitokeza kwa wingi Uwanjani kuziunga mkono timu zetu kama ilivyokua kwa Taifa Stars.
 
Vyombo vya Habari ambao ni moja ya Wadau wakubwa tunaamini tutaendelea kushirikiana katika kuhamasisha pia kwa timu zilizopo Kambini

TAKUKURU Yazirejesha Sh. Bilioni 14.9 Kutoka Kwa Mafisadi.....Yatangaza Kumsaka Mwanamke Mmoja Ambaye Ametoroka

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inamtafuta mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Magreth Kobelo mkazi wa Kinondoni jijini Dar es salaam, kwa makosa ya utakatishaji fedha na kujipatia mali, kupitia kampuni  iliyokuwa ikifanya kazi bila kulipa kodi.

Akizungumza leo Jumanne Machi 26, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna wa Polisi, Athuman Diwani, amesema wakati uchunguzi ukiendelea mtuhumiwa huyo alitoroka nchini.

Amesema mtuhumiwa huyo kwa kutumia fedha ambazo ni zao la ukwepaji kodi alinunua viwanja vitatu vilivyoko ufukweni katika Manispaa ya Temeke na nyumba tatu za kifahari zilizoko Tegeta Manispaa ya Kinondoni.

“Tumeamua kutangaza kutafutwa kwake kabla ya kutaifisha mali alizojipatia kwa rushwa.

“Asiporudi nchini kwenye kesi inayomkabili madhara yake ni makubwa sana kwake binafsi na familia yake kwa kuwa mali zitataifishwa na kurudishwa serikalini kwa mujibu wa sheria,” amesema Kamishna Diwani.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna wa Polisi, Athuman Diwani amesema wamefanikiwa kuzirejesha fedha mali ya Uma zaidi ya Sh14.9 bilioni, na kutaifisha nyumba saba na magari manne kutoka kwa mafisadi.

“Kuanzia mwaka 2016 hadi sasa, Takukuru imefanikiwa kurejesha zaidi ya Sh14.9 bilioni na kutaifisha nyumba saba na magari manne kutoka kwa mafisadi.

“Tumeweka zuio la mali ikiwamo akaunti za fedha zaidi ya Sh20 bilioni, nyumba 26, viwanja 47, magari 61 na mashamba 13.”Amesema

Amesema Takukuru ina mamlaka ya kufuata sheria ya kutafuta, kushikilia na kutaifisha mali kupitia tangazo la kutafutwa.

CUF Wafanikiwa Kuirejesha Ofisi yao Ya Makao Makuu Zanzibar

$
0
0
Hatimae Chama cha wananchi CUF leo Jumanne March 26,2019 kimefanikiwa kudhibiti Makao makuu ya chama hicho yaliopo Mtendeni mjini Unguja na kupachika bendera zoezi ambalo lilisimamiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi.

Zoezi hilo limeongozwa na mjumbe wa bodi ya wadhamini, Mussa Haji Kombo pamoja na wanachama wengine wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kombo amesema wamelazimika kuweka bendera wakifahamu kuwa ofisi hiyo ni miongoni mwa mali za chama hicho.

CUF Yafungua Kesi Mahakamani Dhidi ya Waliochoma Moto Bendera zao na Kubadilisha rangi za ofisi ya chama hicho

$
0
0
Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Khalifa Suleiman Khalifa amesema wamefungua kesi ya kiraia mahakama kuu ya Vuga visiwani Zanzibar dhidi ya wote waliofanya vitendo vya kijinai kwa kuchoma moto bendera na kubadilisha rangi za ofisi ya chama hicho.

Katibu mkuu huyo ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua walizochukua kwa wanachama wa chama hicho waliohamia ACT Wazalendo kwa kuharibu mali za CUF ikiwemo bendera na ofisi za chama hicho.

Amesema takribani ofisi 100 za chama cha CUF zimepakwa rangi ya ACT Wazalendo hivyo hawawezi kufumbia macho hujuma hizo dhidi ya chama chao.

Katika hatua nyingine khalifa amesema wabunge wa CUF waliokuwa wanamuunga mokono maalim Seif Sharif Hamad wanatakiwa kushirikiana na chama hicho pekee na wale watakaobainika kuimarisha vyama vingine hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Kesi hiyo ya kiraia namba 19 ya mwaka 2019,imefunguliwa dhidi ya waliokuwa wanachama wa chama hicho kwa kuchoma bendera pamoja na kubadilisha rangi za ofisi za chama cha CUF visiwani Zanzibar,baada ya kuhamia chama cha ACT Wazalendo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 27

Tazama Video ya Wimbo Mpya wa Rosa Ree Feat G Nako -Dip n Whine it

$
0
0
Rapper Rosa ree ameachia Video ya wimbo wake mpya unaitwa Dip n Whine ambao amemshirikisha Mwanamuziki G Nako kutoka kundi la Weusi...

Tazama Video Hapa Chini:

Video Mpya: Harmonize - Niteke

$
0
0
Video Mpya:  Harmonize - Niteke
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images