Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

CCM Yazungumzia Maalim Seif Kuhamia ACT-Wazalendo

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema uamuzi uliofanywa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo umeonyesha na kuthibitisha kwamba utawala uliopo unaozingatia misingi ya Katiba ambayo CCM imeutekeleza.

CCM ilitoa kauli hiyo jana Jumatatu Machi 18, 2019 kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole   baada ya Maalim Seif kutangaza kuhamia ACT- Wazalendo baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa hukumu yake kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF.
 
“Huu ni Utawala wa sheria unaoruhusu mihimili ya dola kufanya kazi pasina kuingiliwa, watu wanazo haki kufanya uamuzi wa kisiasa kwa kujiunga na chama chochote.

“Hili ni fundisho kwa wale ambao wanasema mtu kujiunga na chama kingine maanake kanunuliwa, hii imedhihirisha ni uhuru wao wa kisiasa,” alisema Polepole

Koffi Olomide ahukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la unyanyasaji wanawake kingono

$
0
0
Msanii wa muziki mkongwe nchini DR Congo, Koffi Olomidé, amehukumiwa miaka miwili jela au kulipa faini ya Euro 5,000 baada ya kukutwa na hatia ya unyanyasaji kingono, moja ya waliokuwa Dancers wake miaka 15 iliyopita.

Hukumu hiyo imetolewa jana na mahakama ya Nanterre mjini Paris, Ufaransa.

Hata hivyo, wakati wa hukumu hiyo inasomwa, Koffi Olomide hakuwepo mahakamani hapo.

Olomidé, mwenye umri wa miaka 62, ametakiwa alipe Euro 5,000 kwa madhara aliyomsababishia mwanamke huyo.

Wakili wa Olomidé amepongeza uamuzi huo na kuutaja kuwa ushindi, akiwaarifu waandishi wa  habari kwamba uamuzi huo utachangia kuondolewa waranti ya kimataifa ya kumkamata.

Koffi Olomidé ni nyota wa muziki wa mtindo wa rumba na soukous ambao ni maarufu sana barani Afrika.

Mwaka 2012, Olomidé alishtakiwa kwa mara ya kwanza kwa makosa ya ubakaji na unyanyasaji kingono, lakini alikana makosa yote.

Awali, wanenguaji wanne aliokuwa akifanya nao kazi waliiambia mahakama kwamba mwanamuziki huyo, aliwanyanyasa kingono mara kadhaa kati ya mwaka 2002 na mwaka 2006. Walieleza kuwa unyanyasaji huo ulifanyika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Ufaransa.

Pia wanawake hao walieleza kwamba walizuiwa katika nyumba moja nje ya mji wa Paris na walifanikiwa kutoroka usiku wa Juni 2006, lakini hawakurudi DR Congo kutokana na kuogopa kutafutwa na kulipiziwa kisasi.

Maalim Seif akabidhiwa Rasmi Kadi ya ACT-Wazalendo

$
0
0
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe  amemkabidhi maalim Seif Hamad kadi namba moja ya ACT Wazalendo ambayo imeshalipiwa kwa kipindi cha miaka 10.

"Mimi nina kadi namba  nane.. Kadi namba moja kuna mtu aliiwahi na kwa heshima kadi hii imekwenda kwa Maalim Seif"Amesema Zitto.


Shughuli ya kukabidhi kadi hizo inaendelea kufanyika leo Machi 19, 2019, makao makuu ya ACT- Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine ambao wamekabidhiwa kazi ni Ismail Jussa, Mbalala Maharangande na Sheweji Mketo,

Katika makabidhiano hayo, Zitto amesema hiyo namba kumi ambayo amekabidhiwa Duni ni kama mchezaji wa timu ya Liverpool.

''Kadi maalumu zimekuwa nyingi kweli kweli maana tumepokea watu muhimu mpaka ilibidi tunyang'anyane lakini namba 1, 6, 10 na 17 zote zimekwenda kwa viongozi walioambatana na Maalim'.

''Naomba tusiingie kwenye mtego wa msajili, hivyo tutakwenda kusajili kadi zetu kwenye matawi yetu ili tusije kuulizwa kama makao makuu kuna tawi'' Amesema Zitto Kabwe.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Maalim Seif amesema yeye ni mara ya kwanza kukanyaga ofisi za ACT- Wazalendo lakini anajiona ni mwenyeji.

Lipumba Atoa Onyo Kwa Wanaopora Mali za CUF na Kuhama nazo ACT- Wazalendo

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema chama hicho hakitawavumilia wanaopora mali za chama hicho na kuzihamishia Chama cha ACT Wazalendo.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Jumanne Machi 19, Jijini Dar es Salaam, Profesa Lipumba amesema hatua hiyo ni utapeli na wizi wa wazi, hivyo chama chake kitafuata utaratibu wa kisheria kuzirejesha.

“Hili ni jambo la kisheria, mali za chama zitaendelea kuwa za chama, hao wanaobadili rangi majengo ya chama ninawaambia, akili za Maalim Seif wachanganye na zao, kwa sababu jinai itawahusu wao binafsi na huyu maalim hatakuwa nao,” amesema Profesa Lipumba.

Aidha, Profesa Lipumba amesema kuna watu wenye fikra nzuri ambao walikuwa wanaungana na Maalim Seif lakini hawawezi kubadilisha maamuzi yao na kumfuata ACT.

“Nataka kuwambia wale wote ambao mlikuwa sambamba na Maalim Seif wenyeviti, madiwani, wabunge na wanachama wa CUF tujumuike na tuwe pamoja katika kukijenga chama chetu,” amesema.

Mamia ya wanachama CUF Kutoka Kata 27 na Matawi 96 Tanga wahamia ACT-Wazalendo Kuungana na Maalim Seif

$
0
0
Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) jijini Tanga, kutoka kata 27 na matawi 96, wamemfuata aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif, ACT- Wazalendo na kukabidhiwa kadi za uanachama.

Wakati wanachama hao wakifanya uamuzi huo, leo Jumanne Machi 19, jijini Dar es Salaam, Maalim Seif amekabidhiwa rasmi kadi namba moja ya ACT-Wazalendo iliyolipiwa ada ya miaka 10.

Wanachama hao pia, wamechoma kadi zao za zamani na bendera za CUF, kuashiria kwamba wamejivua uanachama wa chama hicho na sasa wao ni rasmi wanachama wa ACT-Wazalendo.

Wamesema wameamua kumuunga mkono maalimu Seif kujiunga ACT Wazalendo kwani ndio chama makini kinachoweza kuwafikisha kwenye azma yao ya kuiondoa CCM madarakani.

Serikali Ya Tanzania Yatoa Misaada Ya Madawa Na Chakula Kwa Malawi, Msumbiji Na Zimbabwe Zilizokumbwa Na Mafuriko

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakagua madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakagua madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakagua madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakipokea misaada ya madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakagua madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika
 Sehemu ya misaada iliyotolewa na serikali ya Tanzania na madawa na chakula ikiwa tayari kupelekwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba
 Askari wa Jeshi la Ulinzi wakishusha misaada ya madawa na chakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika.
 Askari wa Jeshi la Ulinzi wakishusha misaada ya madawa na chakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika.
 Askari wa Jeshi la Ulinzi wakishusha misaada ya madawa na chakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika baada ya kuwakabidhi misaada ya madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika.
Brigedia General Francis Mushi wa kikosi cha anga cha JWTZ akiongea na wanahabari baada ya kukabidhiwa misaada ya madawa na chakula ili kuipeleka nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba

Mbunge Katani: Wapiga Kura Wangu Wataamua Kama Nitamfata Maalim Seif Ama Laah!.

$
0
0
Na Bakari Chijumba, Mtwara.
Mbunge wa CUF anayewakilisha Jimbo la Tandahimba Mkoani Mtwara, Katani Ahmed Katani, amesema kwa sasa hawezi kusema kama anaunga mkono maamuzi ya maalim Seif Ama Laah! Hadi pale atakapopata ushauri kutoka kwa wapiga kura wake.

Akizungumza mapema leo Asubuhi kupitia Pride Fm Radio (Mtwara), Katani ambaye ni mmoja ya wabunge waliokuwa wanaiunga mkono CUF ya Maalim Seif, amesema wapiga kura wake ndio waliompa dhamana hivyo wana nafasi kubwa ya kumpa muelekeo.

"Ukiona mbuzi kapanda juu,kuna aliyempandisha,Mimi nafasi ya ubunge sikufika tu,wapo wana Tandahimba walionipandisha..Kwahiyo kwa sasa siwezi sema naunga mkono alichokifanya Maalim Seif Sharif Hamad bila kurudi kwa wapiga kura wangu ili wanipe muelekeo" amesema Mbunge Katani na Kuongeza ;

"Napenda sana ushauri wa wapiga kura wangu,siwezi fanya maamuzi bila kurudi kwa walionipa dhamana, watakachonielekeza ndicho nitakachofanya..Hata wakisema Katani kwa tulipofika pumzika siasa ufanye vitu vingine nitaacha,sikuzaliwa nikiwa Mbunge"

Tayari hii Leo 19 March 2019, Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe  amemkabidhi maalim Seif Hamad kadi namba moja ya ACT Wazalendo ambayo imeshalipiwa kwa kipindi cha miaka 10.

"Mimi nina kadi namba  nane.. Kadi namba moja kuna mtu aliiwahi na kwa heshima kadi hii imekwenda kwa Maalim Seif" amesema Zitto.

Shughuli ya kukabidhi kadi hizo imefanyika, makao makuu ya ACT- Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine ambao wamekabidhiwa kazi ni Ismail Jussa, Mbalala Maharangande na Sheweji Mketo.

Maalim Seif ambaye Alikuwa katibu Mkuu CUF Taifa, alitangaza rasmi kujiunga chama cha ACT Wazalendo,pamoja na wafuasi wake jana 18 March 2019, muda mfupi baada ya Mahakama,kukubaliana na maamuzi ya msajili ya kumtambua Prof. Lipumba kama Mwenyekiti halali CUF.

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali Ambaye Awali Alikuwa Upande wa Maalim Seif Atangaza Kumuunga Mkono Profesa Lipumba

$
0
0
Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali ambaye awali alikuwa akimuunga mkono Maalim Seif Sharif Hamad  ndani ya CUF, sasa ametangaza kumuunga mkono  mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Bobali ametangaza uamuzi wa kumuunga mkono Profesa Lipumba leo Jumanne Machi 19, 2019 wakati akizungumza na wanahabari katika ofisi za makao makuu ya Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Amesema wapo wengi watakaorudi kuungana na Profesa Lipumba na kusema hivi sasa ni wakati wa kukijenga chama hicho na walioondoka kwenda sehemu nyingine ni utashi wao.

"Nimerudi nyumbani baada ya msuguano uliodumu kwa miaka mitatu ndani ya CUF na uliokidhoofisha chama, nawaomba mnisamehe kwa yaliyotokea.

“Natoa rai kwa wabunge wenzangu, madiwani na wenyeviti tusikimbie chama chetu, natoa wito tuungane turudi nyumbani tuje tujenge chama chetu huko kwingine kunakoendewa hakuna mwelekeo wowote utakapopatikana,“

"Najua kuna wenzangu wanataka kurudi lakini wanashindwa wataanzia wapi, nawaambia mimi nimeonyesha njia waje wasiogope wakati ndio huu," amesema .

Kwa upande wake, Profesa Lipumba amesema hawana nia ya kuwafukuza uanachama wabunge hao bali wanataka nidhamu ndani ya CUF .

Bobali amechukua uamuzi huo wakati leo Jumanne Maalim Seif pamoja na viongozi mbalimbali waliokuwa CUF wamekabidhiwa kadi za uanachama wa ACT- Wazalendo.

Waziri Mkuu: Sekta Ya Kilimo Kuleta Mageuzi Ya Kiuchumi

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema sekta ya kilimo ina nafasi kubwa ya kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini iwapo changamoto zinazoikabili kama za upatikanaji wa pembejeo, mbinu na miundombinu duni ya uzalishaji, usafirishaji, uchakataji wa mazao na masokozitafanyiwa kazi kwa wakati.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Machi 19, 2019) wakati akifungua ofisi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa Kanda ya Ziwa. Ameutaka uongozi wa benki hiyo ushirikiane na wadau wengine kutatua changamoto za kilimo nchini ili ndoto ya kuwa nchi ya uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025 itimie.

Waziri Mkuu amesema bado sekta za kilimo, mifugo na uvuvi zimeendelea kukabiliwa na changamoto nyingi ambazo kwa kiasi kikubwa zimesababisha ufinyu wa tija hususan kwa wakulima wadogo, hivyo amewaagiza viongozi wa TADB waendelee na kasi ya utoaji huduma ili kuwafikia wakulima na wafuaji wengi zaidi nchini.

“Endeleeni kufanya kazi na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuweka na kutekeleza mipango ya utatuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima, wafugaji na wavuvi nchini. Pia panueni zaidi wigo wa huduma hususan utoaji wa mikopo katika kuendeleza miradi ya miundombinu ya kilimo, ufugaji na uvuvi na kutoa mafunzo kwa wakulima wadogo kwa lengo la kuinua uzalishaji”.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema kwa kuwa Benki Kuu ndiyomdhibiti mkuu wa mabenki nchini inao wajibu wa kutambua umuhimu wa kuandaa kanuni mbadala na sera za fedha ambazo ni rafiki kwa benki za mandeleo ya kilimo na ujasiriamali.

Amesema lengo ni kurahisisha utoaji wa huduma ya mikopo ya kibiashara tena yenye kuvutia kwenye sekta ya kilimo, hivyo ameitaka Benki Kuu iangalie namna ya kushirikiana na wadau hususan wa kilimo kuandaa kanuni maalumu za usimamizi angalifu wa fedha ambazo zitazingatia mazingira halisi ya kilimo na changamoto zake.

“Sambamba na kushughulikia sera au kanuni ambazo zinarahisisha kufanya biashara katika kilimo, Benki Kuu, pia inatakiwa kuendesha zoezi hilo bila kuhatarisha utulivu wa kifedha na kujihami na madhara na hatari zinazoambatana na ukopeshaji”.

Nae, Naibu Waziri wa Kilimo, ….Bashingwa amesema ufunguzi wa benki hiyo kwa Kanda ya Ziwa ni hatua nzuri ambayo inakwenda kuwasogezea huduma wakulima, hivyo ameutaka uongozi wa benki hiyo uandae utaratibu wakuwafundisha wakulima namna ya kuandika maandiko kwa ajili ya kuomba mikopo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine amesema hadi kufikia Februari 28, mwaka huu benki ya TADB imefanikiwa kukuza mtaji wake na kufikia kiasi cha sh. bilioni 68 ikiwa ni ongezeko la asilimia 13 kutoka mtaji wa sh. bilioni 60 uliotolewa na Serikali mwaka 2015.

Mkurugenzi huyo amesema ukuaji wa mtaji wa benki hiyo umechangiwa na malimbikizo ya faida iliyotengenezwa katika kila mwaka wa fedha tangu kuanzishwa kwa benki hiyo mwaka 2015, kutokana na utoaji wa mikopo ya kimkakati inayotolewa kwa wateja wao.

“Kilimo ‘kinabenkika’ kwani katika msimu wa pamba wa mwaka 2018 TADB ilitoa mkopo wa gharama nafuu ili kufanikisha ununuzi na usambazaji wa viuatilifu vya zao la pamba kwa wakulima katika mikoa 17 ikiwemo yote ya Kongani ya Kanda ya Ziwa na wilaya 49 nchini”.

Amesema mkopo huo ulichangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la uzalishaji, ambapo kwa msimu wa pamba wa mwaka 2018, mavuno ya pamba yaliongezeka na kufikia tani 221,600 ikiwa ni ongezeko la asilimia 67 ikilinganishwa na tani 133,000 zilizozalishwa msimu wa mwaka 2017.

Baada ya kufungua ofisi hiyo ya TADB kwa Kanda ya Ziwa, Waziri Mkuu alikabidhi matrekta 16 aina ya URSUS kwa vyama vya msingi, ambapo viongozi wa vyama hivyo wameishukuru Sekali kwa uamuzi wake wa kuwajali wakulima kwa kuwapatia huduma muhimu zikiwemo  pembejeo.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Mkuu Aagiza Msako Kwa Waliomuibia Mkandarasi Misungwi

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Mwanza ihakikishe inafanya msako wa watu wote waliohusika na wizi wa fedha na vifaa katika eneo la ujenzi wa mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Misungwi mkoani Mwanza.

Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Machi 19, 2019) wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira uliopo wilayani Misungwi, ambapo ametumia fursa hiyo kuiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza iimarishe ulinzi katika eneo la mradi huo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya kuwepo kwa vitendo vya uvamizi wa mara kwa mara kwenye eneo hilo la mradi wa maji unaojengwa katika kijiji cha Nyahiti wilayani Misungwi, Mwanza.

“Hawa waliofanya tukio hilo la uvamizi katika eneo la mradi si tu wanamuhujumu mkandarasi na kampuni yake, bali wanahujumu jitihada za Serikali ili miradi ya maendeleo kwa wananchi isikamilike hatutakubali, wananchi tushirikiane katika kuwabaini wote waliohusika.”

Ujenzi wa mradi wa maji katika mji wa Misungwi ni utekelezaji wa Sera ya Maji pamoja na Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 inayoelekeza Serikali kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 95 wakazi waishio mijini na waishio vijijini asilimia 85 ifikapo 2020.

Awali,Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa mradi wa maji katika mji wa Misungwi unatekelezwa kupitia Mpango wa Uboreshaji wa Huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Ziwa Viktoria, ambao unatekelezwa katika miji ya Mwanza, Musoma, Bukoba, Magu, Misungwi na Lamadi kwa gharama ya Euro milioni 104.5 sawa na wastani wa sh. bilioni 276.

Amesema katika kiasi hicho cha fedha, Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) zinachangia Euro milioni 90 sawa na sh. bilioni 238 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu, ambapo Serikali ya Tanzania inachangia Euro milioni 14.5 sawa na sh. bilioni 38.

Profesa Mbarawa amesema mradi wa maji na usafi wa mazingira katika mji wa Misungwi unagharimu kiasi cha Euro milioni 4.85 ambazo ni sawa na wastani wa sh. bilioni 12.85 ambazo zinatumika katika ujenzi wa kituo cha uzalishaji na kutibu maji, ulazaji wa mabomba kwa umbali wa kilomita 53.7.

Pia, fedha hizo zitatumika kwenye ujenzi wa matenki mawili ya kuhifadhia maji yenye ukubwa wa lita 600,000 na lita 300,000, ujenzi wa kituo cha kutibu majitaka, ununuzi wa magari mawili moja la kunyonya majitaka na Toyota pick up na pikipiki mbili pamoja na ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Maji na nyumba mbili za watumishi katika kituo cha uzalishaji.

Waziri Profesa Mbarawa amesema mbali na ujenzi huo pia watajenga maabara ya kupima ubora wa maji na karakana ya matengenezo. Mradi huo pia utaunganisha kaya 2,158 katika mfumo wa maji pamoja na kuwafungia mita za maji na ujenzi wa vituo 13 vya kuchotea maji.

Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya M/S China Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) ya China chini ya Mhandisi Mshauri Kampuni ya Egis ya Ufaransa na unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Jijini Mwanza (MWAUWASA) ulianza Mei, 2017 na unatarajiwa kukamilika Mei mwaka huu.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Amteua Bw. Hassan Abeid Mwang’ombe kuwa PostaMasta Mkuu.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Hassan Abeid Mwang’ombe kuwa PostaMasta Mkuu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mwang’ombe umeanza tarehe 12 Machi, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Mwang’ombe alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Msajili wa Vyama vya Siasa Alaani Kitendo cha Kuchoma Moto Bendera za Chama cha CUF

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amelaani  kitendo cha kuchomwa moto bendera za Chama cha Wananchi (CUF), kilichofanywa na baadhi ya waliokuwa wanachama wa chama hicho na baadaye kuhamia ACT-wazalendo

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano March 20

Waziri Mkuu Azindua Mradi Wa Ujenzi Wa Kituo Cha Afya Koromije

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua mradi wa ujenzi na ukarabati mkubwa wa kituo cha afya cha kata ya Koromije wilayani Misungwi na amewahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga vizuri kuboresha huduma za afya.

Amesema uboreshaji huo unahusisha ujenzi wa chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, wodi ya mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti.Uboreshaji huo unagharimu sh. milioni 500.

Waziri Mkuu alifungua mradi huo jana (Jumanne, Machi 19, 2019) akiwa ziarani Misungwi, ambapo aliwataka wananchi waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.

“Hapa zamani kulikuwa na zahanati yenye jengo moja, tumeamua kuboresha na kupandisha hadhi na kuwa kituo cha afya. Rais Dkt. John Magufuli anataka wananchi wapatiwe huduma muhimu zikiwemo za afya karibu na makazi yao”.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema hakuna kijiji chochote nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA), vikiwemo na vya wilaya ya Misungwi tena kwa gharama nafuu.

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya yenu hii ya Misungwi. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

Waziri Mkuu aliongeza kwamba lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi ya taifa vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Lugola atoa onyo kali kwa wanaoingiza wahamiaji haramu nchini

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa onyo kali kwa baadhi ya Watanzania ambao wanafanya biashara ya kuwaingiza wahamiaji haramu nchini huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.

Kutokana na changamoto hiyo, Waziri Lugola amesema Idara ya Uhamiaji itashirikiana na Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwakamata watu hao na kuwafungulia mashtaka.

Akizungumza mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kumaliza kukagua eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji, jijini Dodoma, leo, Lugola alikiri uwepo wa wahamiaji haramu nchini, na akasisitiza kuwa tatizo la uwepo wa wahamiaji haramu litamalizika.

“Naomba muwafikishie salamu watu ambao wanatabia hiyo ya kuwaingiza wahamiaji haramu nchini, Serikali ipo na pia inafanya kazi, kama wapo basi wajue tutawakamata tu,” alisema Lugola.

Alisema Jeshi la Polisi litashirikiana na Uhamiaji kuwatafuta popote wahamiaji hao walipo, na watakapokamatwa watafikisha ujumbe kwa wenzao wenye nia ya kuja nchini kwa njia isiyo halali.

Aidha, Lugola aliwataka Suma JKT wanaojenga jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji wafanye kazi kwa weledi mpaka jengo hilo litakapo kamilika, na pia mara kwa mara viongozi wa Wizara yake akiwemo yeye mwenyewe atakuwa anatembelea eneo hilo la ujenzi.

“Sitasubiri mpaka Mheshimiwa Rais haje hapa kukagua, litalifuatilia mwanzo mwisho ujenzi huu, na pia mlisema pale Magereza Ukonga mbele ya Rais, kuwa Jeshi halishindwi, nami ninaamini nyie Suma JKT, ujenzi huu utakamilika bila kuwa na matatizo,” alisema Lugola.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, alisema ujenzi huo unatarajiwa kwenda vizuri na pia endapo watapata changamoto zozote wawe huru wajenzi hao kuja kumuona kwasababu ofisi za Wizara zipo jirani na eneo la ujenzi huo na pia naye atakua anautembelea mradi huo.

Naye Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, alisema ujenzi wa jengo hilo kubwa wa ghorofa nane kwenda juu na moja kuja chini, ukikamilika litakua la kisasa, na ukubwa wa jengo hilo utawasaidia kufanya kazi zao kwa utulivu zaidi. 

Kesi ya Maimu wa NIDA Sasa kuhamishiwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

$
0
0
Kesi  ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na wenzake watano iko katika mchakato wa kuhamishiwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Hayo yalidaiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally wakati kesi hiyo ilipokuwa inatajwa.

“Mheshimiwa Hakimu, Jamhuri tupo kwenye mchakato wa kuwasilisha taarifa za kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi,” alidai Wakili wa Serikali, Estazia Wilson.

Wakili Estazia alidai bado hawajawasilisha taarifa katika mahakama hiyo ili waweze kupewa vijalada na kuwezesha kusomwa kwa maelezo ya mashahidi.

Hakimu Ally aliutaka upande wa mashtaka kuharakisha mchakato huo ili tarehe ijayo waje na maelezo tofauti.

Kutokana na hali hiyo, Estazia aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo ambapo Mahakama ilipanga Aprilii 4 mwaka huu.

Mbali na Maimu, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Meneja Biashara wa NIDA, Aveln Momburi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Katika kesi hiyo, wanakabiliwa na mashtaka 100 yakiwamo 24 ya kutakatisha fedha, kughushi 23, kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri 43 na matano ya kuisababishia hasara NIDA.

Pia, yapo mashtaka mawili ya kula njama ya kulaghai, mawili ya matumizi mabaya ya madaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka lipo moja ambalo linawakabili Maimu na Sabina.

Halmashauri 31 Zatakiwa Kujieleza Kwa Waziri Kwa Kutokutenga Fedha Za Lishe

$
0
0
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa, Seleman Jafo, ameagiza ndani ya siku kumi na nne kwa Halmashauri therathini na moja, ambazo zilishindwa kuwasilisha fedha zilizotengwa kwa ajiri ya lishe katika halmashauri zao kujieleza kwanini hazikufanya hivyo.

Waziri Jafo  ameagizo hayo leo Jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua kikao kilichowakutanisha wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, waganga wakuuwa mikoa, wawakilishi toka taasisi ya chakula na wadau wa maendeleo,waliokutana kutathmini hali ya lishe hapa Nchini na mahali walipofikia katika mpango wa kwanza wa lishe wa august 2018 hapa Nchini.

Waziri Jafo amesema kuna halmashauri therathini na moja hazikutoa fedha zilizotengwa kwa ajiri ya kutekeleza hali ya lishe katika maeneo hayo hali iliyosababisha kushindwa kutekelezwa kwa malengo ya lishe ndani ya halmashauri hizo.

“Ni agize ndani ya siku kumi na nne halmashauri ishirini na moja zitoe maelezo ya kina kwa wakuu wao wa mikoa kwanini hazikutoa fedha zilizotengwa ndani ya halmashauri hizo kwa ajiri ya lishe kwanini hazikufika”

“Na ninyi wakuu wa mikoa baada ya siku hizo kumi na nne baada ya hapo nipate maelezo ya kwanini zilishindwa kutekeleza mikataba hiyo wakati halmashauri nyingine zaidi ya mia mija zimetekeleza” alisema Jafo

Kwa upande mwingine Waziri Jafo amekemea vikali tabia ya wakuu wa idara ambao hawafiki kwenye semina zinazohusu lishe na kuwaagiza watumishi wengine ambao hawana uelewa katika sekta hizo na kusababisha elimu hiyo kutokufikia mahala husika kwa uzembe wa wakuu wa idara hizo.

“Kuna tabia ya wakuu wa idara kushindwa kuhudhuria semina, hawahudhurii au wana waagiza watumishi wengine ambao hawana uelewa juu wa mambo ya lishe na  hii inasababisha kuwa na gepu kubwa la maamuzi  na ninaomba wakuu wa mikoa muwe wakali kwenye mambo kama haya” alisema.

Waziri Jafo pia ameagiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanatoa elimu ya lishe kwa akina mama wajawazito wanapofika kliniki kabla ya kujifungua na watengeneze vipeperushi ambavyo  vitasaidia kupeleka elimu kwa jamii na kuchukua hatua.

Nae muwakilishi wa wakuu wa wilaya Daniel Chongolo, ambae ni mkuu wa wilaya ya kinondoni, amewaomba wadau wa maenendeleo kupelekwa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa wa lishe ili kujenga kizazi imara cha baadaye.

Alisema endapo tusipokabiliana na changamoto hii kuna wakati tutakuta kuna sehemu kuna kizazi ambacho hakina uelewa kabisa kwenye maswala ya kielimu kwa sababu ya kutopata lishe bora.

Kwa upande wake muwakilishi kutoka shilika  la GAIN linalijihusisha na elimu ya lishe, Archard Ngamela  amesema, changamoto kubwa kwenye lishe ni wasindikaji wadogowadogo hawaweki virutubisho katika bidhaa za vyakula na kusababisha kuenea kwa tatizo la lishe.

“Changamoto kubwa tunayokutana nayo ni  tabia ya hawa wajasiliamali wadogo au hawa wasindikaji wa viwanda vidogovidogo hawaweki virutubisho kwenye bidhaa zao na hii ni changamotokatika lishe hapa nchini.

Wimbo Mpya: Enock Bella - Walifuata Jina

$
0
0
Wimbo Mpya: Enock Bella - Walifuata Jina

Maalim Seif amjibu Msajili wa Vyama vya Siasa

$
0
0
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, amesema sheria aliyotumia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuwaonya waliokuwa wanachama wa chama hicho waliochoma bendera na kadi za chama hicho, haipo.

Maalim Seif amesema hayo leo Jumatano Machi 20, wakati akihojiwa na Maria Sarungi katika mtandao wa Kwanza TV, akirejea tamko la Jaji Mutungi alilolitoa jana akiwaonya wanachama hao waliohamia Chama cha ACT-Wazalendo, pamoja Maalim Seif.

“Msajili anasema tumevunja sheria, sheria ipi, tunavyojua kuna sheria iliyopitishwa lakini hadi sasa hatuna hakika kama rais ameweka saini maana utaratibu ni kwamba kama amesaini ingewekwa kwenye gazeti la serikali lakini hadi sasa hakuna gazeti la serikali lililochapisha sheria hiyo.

“Sasa msajili anatumia sheria ipi ambayo ameirejea kifungu chake au anayo yeye peke yake?” amehoji Maalim Seif.

Aidha, Maalim Seif amesema ni kama vile dola inawatega wananchi wake kwa sababu haiwezekani kutumia sheria ambayo wananchi wake hawaijui.

“Kwanza tunauliza ni sheria ipi labda anayosema kwenye kupandisha bendera kuna maneno wanayatamka, wanasema Alah Akbar maana yake Mungu Mkubwa, lakini kwa upande wa wakristo wangekuwa wanapandisha bendera wanasema Bwana Asifiwe, angeuliza?

“Lakini isitoshe katika baadhi ya mikutano ya CCM (Chama Cha Mapinduzi), wanaanza kwa kusoma Quraan, sasa hii inakuja kwa ajili ya Cuf tu au vyama vingine, mimi namuomba msajili sana awe ‘fair’ maana unapokuwa na mamlaka ya kuamua uache mapenzi na chuki,” amesema Maalim Seif.

Joshua Nassari Amfungulia Mashtaka Spika, Mahakama Yazuia Uchaguzi Kufanyika

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari,  amefungua shauri la madai dhidi ya Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma chini ya hati ya dharura kuomba kibali cha mahakama ili kufungua shauri la kufuta na kutengua uamuzi  wa Spika wa kumvua ubunge kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya bunge.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Dayness Lyimo, amesema kesi hiyo namba 22 ya mwaka 2019 inasikilizwa na Jaji Latifa Mansoor ambapo wajibu maombi ambao ni Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamepewa siku saba kupeleka kiapo kinzani cha maombi hayo.

Nassari ambaye alikuwapo mahakamani hapo asubuhi anawakilishwa na mawakili watatu ambao ni Hekima Mwasipe, Jonathan Mndeme na Fred Kalonga. Upande wa walalamikiwa unawakilishwa na wakili wa Serikali, Masunga Kawahanda. Kesi hiyo itakwenda tena mahakamani Machi 27 kwa ajili ya kusikilizwa.

Aidha, mahakama hiyo imezuia kufanyika kwa uchaguzi katika jimbo la Arumeru Mashariki hadi kesi ya maombi madogo ya kufungua kesi ya msingi ya kuomba kutengua uamuzi wa Spika wa kumfutia ubunge Joshua Nassari itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images