Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kortini Kwa Kukutwa na Bangi na Wizi wa Simu

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam imempandisha kizimbani Mohamed Hamisi (24) kwa shtaka la kukutwa na bangi yenye uzito wa kilo 0.57.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Bonifasi Lihamwike, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Veronika Mtafia alidai kuwa Januari 10, mwaka huu eneo la Sinza Kwa Mori, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam mshtakiwa alikutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya huku akijua ni kinyume cha sheria.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Alihamwike alisema hatampa mshtakiwa dhamana kutokana na kurudishwa mara nne mahakamani kwa shtaka hilo moja.

“Kutokana na mtuhumiwa kurudishwa mara nne mahakamani kwa wakati tofauti kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya, mahakama imeamua kutompa dhamana kwa kesi hiyo mpaka hukumu itakapotolewa,” alidai Lihamwike.

Mshtakiwa alirudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa tena Machi 25, mwaka huu.

Wakati huo huo, mahakama imempadisha kizimbani Emmanuel Mushi (34) Mkazi wa Sinza, Wilaya ya Kinondoni kwa shtaka la wizi.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa, Wakili wa Serikali, Neema Mushi alidai mnamo Novemba 15, mwaka jana eneo la Kibamba, Wilaya ya Ubungo, aliiba simu aina ya Samsung yenye thamani ya Sh 360,000, pesa taslimu Sh 5,000,000 na pochi moja yenye vitambulisho mali ya Imani Kisiwa.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hata hivyo, Hakimu Kiliwa alisema kuwa dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh milioni 2.7.

Mshtakiwa aliachiwa hadi Aprili 3, mwaka huu kesi yake itakaposomwa baada ya kukidhi masharti ya dhamana.

Naibu Wa Ardhi ahimiza upimaji vijiji kuondoa migogoro ya ardhi

$
0
0
Na Munir Shemweta, KATORO
Serikali imehimiza  halmashauri nchini kupima maeneo ya vijiji ili kuwamilikisha wananchi ardhi kwa nia ya kuwapatia hati za kimila na wakati huo kupanga matumizi bora ya ardhi katika maeneo hayo kwa lengo la kuepuka migogoro ya ardhi na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 12 Februari 2019 na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa kutoa hati 21 kwa wananchi wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro uliopo wilaya ya Geita mkoa wa Geita pamoja na kutoa Ramani za Urasimishaji kwenye wilaya za Chato na Geita wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.

Alisema suala  la kupima vijiji ni la lazima na halmashauri zinapaswa kuchukua  hatua za kuwapimia wananchi kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi lakini pia kuleta salama ya miliki ya maeneo yao kwa kuwa kutofanya hivyo kutasababisha kuwepo migogoro ya mipaka pamoja na kiwanja kimoja kumilikishwa kwa watu wawili    (double allocation).

Akigeukia suala la urasimishaji, Dkt Mabula alizitaka halmashauri za wilaya ya Geita kuhakikisha zinarasimisha maeneo yaliyojengwa kiholela na kusisistiza kuwa salama ya eneo la mtu haliishii kuwekewa vigingi bali kinachotakiwa ni mtu kumilikishwa ili aweze kuitumia ardhi hiyo kujiinua kiuchumi kwa kuwa anaweza kuitumia hati yake kwa ajili ya kukopea fedha benki,

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  alikabidhi ramani za urasimishaji kwa wakurugenzi wa halmashauri  mbili za wilaya ya Geita pamoja na ile ya Chato kwa nia ya kuendesha zoezi la urasimishaji katika maeneo ya halmashauri hizo.

Sambamba na hilo Dkt Mabula alishuhudia utiaji saini  makubailiano ya kupatiwa kiasi cha shilingi milioni 180 kwa halmashauri ya wilaya ya Geita kwa ajili ya kutwaa maeneo mapya ya halmashauri hiyo ambapo alieleza kiasi hicho cha fedha kitumike  kuepuka kero wakati wa kutwaa maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  fedha zilizosainiwa ni kama mkopo na halmashauri husika inatakiwa kuuza viwanja na kurejesha fedha hizo ndani ya miezi mitatu na kubainisha kuwa Wizara imetengewa  shilingi bilioni 7 kwa ajili ya kuzikopesha halmashauri mbalimbali nchini ili kutwaa maeneo.

Alisisitiza kuwa ni marufuku kuchukua eneo la mtu bila kulipa fidia na kubainisha kuwa sheria ya mwaka 2016 inaweka wazi kuwa ukitwaa eneo ndani ya miaka miwili kama hujalipa fidia basi mwenye eneo anaruhusiwa kubaki na eneo lake na kiasi cha riba kinaongezeka kila baada ya miezi sita.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ally Kidwaka alisema pamoja na Halmashauri yake kuwa na miji midogo yenye wakazi 50,000 lakini Mji Mdogo wa Katoro ndiyo unaokuwa kwa kasi na sasa umefikia wakazi wapatao laki moja. Alisema kutokana na mji huo kukuwa kwa kasi wataalamu wa upimaji wanatakiwa kuongezwa katika mji huo ili kuepuka changamoto za urasimishaji maeneo ya mji huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Geita Elisha Lupuga alisema Mji wa Katoro pamoja na kukuwa kwa kasi kwa muda mrefu lakini  ulichelewa kupatiwa mamlaka ya Mji  jambo lililochelewesha maendeleo katika mji huo. Hata hivyo, alisema  pamoja na wananchi wa Mji wa Katoro kuwa na uwezo wa fedha na nyumba nzuri lakini wamekuwa wazito kutoa fedha kwa ajili ya kupimiwa maeneo yao jambo linalosababisha mji kutopangika vizuri.

Wimbo Mpya:Gigy Money Ft Tushynne - Changanya

$
0
0
Wimbo Mpya:Gigy Money Ft Tushynne - Changanya

Serikali Yapiga Marufuku Kutangaza Magonjwa ya Mifugo

$
0
0
Serikali  imeogesha mifugo milioni 32, sawa na asilimia 56 ya mifugo milioni 57 iliyopo nchini, katika kipindi cha miezi mitatu, tangu kuzinduliwa kwa kampeni ya kitaifa ya uogeshaji mifugo.

Pia, imepiga marufuku mtu yeyote kutangaza kuwepo magonjwa ya mifugo, isipokuwa yule aliyepewa mamlaka hayo kwa mujibu wa Sheria.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, wakati akizungumzia tathmini ya kampeni ya uogeshaji kitaifa, iliyofanyika kwenye josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge, lililojengwa mwaka 1905 wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Alisema Sheria za Kimataifa na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Namba 17 ya mwaka 2003, inazuia kufanya hivyo.

Mpina alisema shabaha ya kuzuiwa kufanya hivyo kwa sababu baadhi ya watu wanaweza kujitokeza kupeleka hofu kwa wananchi na kusababisha kuharibu biashara hiyo.

Hivyo, alisema Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) ndiye aliyepewa dhamana ya kutangaza ugonjwa wowote wa mifugo kwa niaba ya Watanzania na wala sio mtendaji yeyote yule wa serikali.

“Ndugu zangu vyombo vya habari msije mkaingia kwenye mgogoro wa serikali, mambo ya chakula ni sensitive (nyeti) tukifanya hivyo tutakuwa tunapeleka maneno ya taharuki kwa wananchi, tumuachie aliyepewa jukumu hilo, hivyo sitegemei tena kama watu wengine wataendelea kufanya hivyo,” alisema Mpina.

Alisema nchi imejipanga vizuri kudhibiti magonjwa ya mifugo na ndio maana inazo kanda nane za uchunguzi wa magonjwa ya mifugo, hivyo Watanzania wako salama Tanzania iko huru na magonjwa.

Alisema kwa sasa Tanzania inazalisha chanjo nane na kufikia Septemba hadi mwakani, kutakuwa na chanjo 11 ili mifugo ichanjwe isipatwe tena na magonjwa.

Mpina alisema ifikapo Julai mosi mwaka huu wizara yake itakuwa imeshatoa kanuni za namna ya uendeshaji wa kazi ya uogeshaji ili kila mmoja afahamu wajibu wake.

Alisisitiza agizo lake la ukarabati wa majosho na ifikapo Julai Mosi mwaka huu, halmashauri ambayo itakuwa haijakarabati majosho, itazuiliwa kukusanya mapato huku akizindikia barua za kusudio la kuzizuia kukusanya mapato halmashauri hizo.

Majosho 132 kati ya majosho mabovu 1,124 yameshakarabatiwa. Hivyo, asilimia 11 ya agizo hilo limetekelezwa, ikiwa ni miezi mitatu tangu limetolewa.

Aliupongeza Mkoa wa Kagera kwa kukarabati majosho 34, Mkoa wa Mwanza wamekarabati majosho 19, Mkoa wa Arusha majosho 11, Mkoa wa Dodoma majosho mawili tu na wengine hawajafanya hivyo.

Mpina alisema halmashauri zote nchini zinakusanya zaidi ya Sh bilioni 30 kwa mwaka kutokana na sekta ya mifugo, lakini halmashauri zinatenga fedha kidogo za kusaidia mifugo.

Wafikishwa Kizimbani kwa Meno ya Tembo ya Bilioni 1

$
0
0
Wakazi wawili wa Chanika Kwa Zoo, Dar es Salaam, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za  kukutwa na vipande 47 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni moja.

Washtakiwa hao, Abdallah Hamis (30) na Adam Kawàmbwa (35), walipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwezile.

Wakili wa Serikali, Candid Nasua alidai washtakiwa walitenda makosa hayo Februari 11, mwaka huu eneo la Chanika Kwa Zoo, Ilala Dar es Salaam.

Alidai kuwa katika shtaka la kwanza, washtakiwa hao walikutwa wakimiliki vipande 47 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh 1,081,357,500 mali ya Serikali bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori nchini.

Ilidaiwa kwamba katika shtaka la pili washtakiwa walitakatisha fedha hizo wakati wakijua zimetokana na kosa la ujangili.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwakuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Wakili Nasua alidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kesi iliahirishwa hadi Machi 25, mwaka huu itakapotajwa.

Serikali Yatoa Onyo Kwa Gazeti la Mwananchi, Citizen

$
0
0
Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetoa onyo kwa magazeti ya Mwananchi na The Citizen kwa kuyataka yajitafakari kwa kile ilichoeleza kuwa wameandika habari za “uongo wa karne”.

Akitoa onyo hilo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi Hassani kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema kuwa magazeti hayo kwenye matoleo yake ya mtandaoni yalichapisha habari za uongo, huku wakitumia takwimu zisizo rasmi.

Dr Abbasi ameandika; Ufafanuzi: Jana magazeti ya the Citizen na Mwananchi matoleo ya mitandaoni yalibeba habari iliyodai wahisani wametoa 6.7% tu kwenye bajeti. Habari hii ni uongo wa karne. Takwimu zilizowekwa hata kwenye viambatishi vya hotuba ya Waziri zinaonesha imetolewa 69% kufikia Jan., 2019.

Kwa makosa haya yanayojirudiarudia na yenye nia ovu (kwa kuwa hawakutaka hata ufafanuzi wa Serikali au nyaraka), Serikali inayapa nafasi ya mwisho magazeti ya Mwananchi na the Citizen kujitafakari tena kama yana sababu, nia na dhamira ya kuendelea na kazi hii.

Dkt. H.A.

Mgombea Uenyekiti CUF Ajifananisha na Lipumba Akiomba Kura

$
0
0
Mgombea uenyekiti wa Taifa katika Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Diana Simba, amesema si kwamba Lipumba ndiye msomi pekee  kwani hata yeye ana Stashahada ya Maendeleo ya Jamii hivyo anaamini anaweza kukiongoza chama hicho.

Diana ambaye ni mwanamke pekee anayegombea nafasi hiyo amejikuta katika wakati mgumu wakati wa kujinadi na kuomba kura kutokana na aina ya maswali aliyokuwa akiulizwa.

Elimu, uzoefu ndani ya chama na nchi alizowahi kutembelea ni kati ya maswali yaliyoelekezwa kwa mgombea huyo na alipokuwa akijibu baadhi ya wajumbe walisikika wakimkejeli hatua iliyosababisha msimamizi kuchukua kipaza sauti mara kwa mara kuwasihi watulie wamsikilize mgombea.

“Nilijiunga na chama mwaka 2017 na nimetembelea Kenya na Uganda, msifikiri Profesa Lipumba ndiye msomi peke yake hata mimi ni msomi. Nina Diploma ya Maendeleo ya Jamii hivyo nina uwezo wa kuwaongoza,” amesema Diana.

Awali, akizungumza kwenye mkutano huo leo Jumatano Machi 13, 2019 Profesa Lipumba alisema kwa sababu ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti hawezi kuwa mwenyekiti wa kikao hicho.

Alisema kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu za chama hicho kikao kipendekeze mwenyekiti wa muda.

Aliwauliza wanachama kwa ujumla wao wanamtaka nani awe mwenyekiti wa muda wakajibu. ‘Milambo Yusuph Kamili’ hivyo akamtangaza kuwa ndiyo mwenyekiti wa muda wa kikao hicho.
 
Lipumba alitoa ufafanuzi wa uchaguzi utakavyofanyika kuwa wataanza na kumchagua mwenyekiti wa taifa, akifuatia makamu mwenyekiti Zanzibar na kumalizia na makamu mwenyekiti Tanzania Bara.

Pamoja na Profesa Lipumba wengine kwenye kinyang’anyiro hicho ni Diana Daudi Simba na Zuberi Mwinyi Hamisi. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe 798.

Tangazo la Nafasi za masomo na ajira Toka Wizara ya Mambo ya Nje

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwahimiza Watanzania wenye sifa kuomba fursa za masomo na ajira zinazotolewa na wadau mbalimbali duniani. Fursa zilizopokelewa mwezi Machi 2019 ni kama ifuatavyo:

i. Mafunzo ya Shahada ya Uzamili yanayotolewa na Chuo Kikuu cha British nchini Misri (British University – Egypt) kwa kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2020. Fursa hizi zinaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na maombi yanafanyika kwa njia ya  mtandao kupitia tovuti, http://www.bue.edu.eg/;

ii.Mafunzo ya Shahada ya Kwanza na Uzamili yanayotolewa na Taasisi ya Elimu ya Urusi (Russian Education Institute)                                               kwa kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2020 na 2020/2021. Fursa hizi zinaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Maelezo ya namna ya kuomba fursa hizo yanapatikana katika Wizara zinazoratibu mafunzo hayo. Mwisho wa kufanya maombi kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ni tarehe 25 Machi 2019 na tarehe 25 Juni 2020 kwa mwaka wa masomo 2020/2021;

iii. Mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya Usuluhisihi katika Mchakato wa kutafuta Amani (Mediation in Peace Processes) yatakayotolewa nchini Ujerumani katika kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2021.  Fursa hizi zinaratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, na maombi yanafanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti, http://www.mas-mediation.ethz.ch/.  Mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 21 Aprili 2019;
NAFASI ZA AJIRA
iv. Nafasi ya ajira ya Afisa Tathmini (Evaluation Officer, P-3) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Kudhibiti Matumizi ya Silaha za Kemikali (The Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons-OPCW). Maelezo ya jinsi ya kuomba yanapatikana katika tovuti, https://opcw-career.talent-soft.com/job/job-officer-industry-p-3_11.aspx. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 Machi 2019; na

v.    Nafasi ya ajira ya Afisa Usalama wa Masuala ya Habari (Information Security Officer, P – 3) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Kudhibiti Matumizi ya Silaha za Kemikali (The Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons-OPCW). Maelezo ya jinsi ya kuomba yanapatikana katika tovuti, https://opcw-career.talent-soft.com/job/job-information- security-officer-industry-p-3_18.aspx. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 26 Machi 2019.
        
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
13 Machi 2019

Balozi wa Canada atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

$
0
0
Bw. Jestas A. Nyamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Pamela O’Donnell tarehe 11 Machi 2019.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salam yamelenga kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Canada. Mataifa haya mawili, kwa kipindi kirefu yamekuwa yakishirikiana kwenye masuala ya afya, elimu, ukuzaji wa uchumi, Utawala Bora pamoja na biashara na uwekezaji.

Katika mazungumzo hayo, Balozi wa Canada amemhakikishia Kaimu Mkurugenzi kuwa, Serikali ya Canada inaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika kuleta Maendeleo na kuondoa umaskini na kwamba Canada itatekeleza kwa ufanisi miradi iliyopo inayotekelezwa kupitia Serikali , Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Asasi zisizo za Kiserikali(NGOs).

Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi alimkaribisha Balozi huyo mpya nchini na kuishukuru Serikali ya Canada kwa ushirikiano mzuri na wakihistoria uliodumu baina ya Tanzania na Canada .

Aidha, aliishukuru Serikali ya Canada kwa kuisaidia Tanzania katika miradi muhimu na ya kipaumbele hususan miradi ya afya, elimu na ukuzaji wa uchumi. Alimhakikishia ushirikiano thabiti wa Wizara na Serikali kwa jumla katika kuhakikisha miradi iliyopo inatekelezwa kwa ufanisi na mingine mipya inaibuliwa.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
13 Machi 2019

Waziri Wa Kilimo Afanya Mazungumzo Na Mkurugenzi Wa Shirika La Kimataifa La Nguvu Za Atomiki Prof Shaukat Abdulrazak

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 13 Machi 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof Shaukat Abdulrazak.

Katika Mkutano huo uliotuama kwa masaa kadhaa katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma Waziri Hasunga amemueleza Prf Shaukat kuwa serikali ya Tanzania inaendelea na mchakato wa kubaini wafanyabiashara wanaouza mbegu feki kwa wakulima kwani wanasababisha hasara kwa wananchi na Taifa kwa ujumla wake.
 
Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi Duniani ambazo wananchi wake wa wamekuwa wakiuziwa mbegu feki jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt john Pombe Magufuli imetilia mkazo kadhia hiyo na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
 
Kadhalika, Waziri Hasunga alisema kuwa pamoja na Wizara ya Kilimo kuendelea na mchakato wa kuboresha kilimo kwa kutumia teknolojia mpya lakini bado inakabiliwa na uuzwaji wa viuatilifu feki jambo ambalo limefifihisha juhudi za wakulima kwa muda mrefu.
 
“Wananchi wetu wanajitahidi kulima kwa kiasi kikubwa lakini kumekuwepo na changamoto kubwa ya Viuatilifu na Mbegu feki jambo hili hatuwezi kuliacha kamwe hivyo hivi karibuni nimetangaza kiama na wafanyabiashara wanaosambaza tutakapowabaini tutawachukulia hatua kali sana” Alikaririwa Mhe Hasunga
 
Katika hatua nyingine alieleza kuwa wakulima wengi nchini wamekuwa wakitumia mazao yao kama mbegu badala ya kutumia mbegu mpya jambo hili linapunguza kwa kiasi kikubwa ufanisi katika uzalishaji wa mazao.
 
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof Shaukat Abdulrazak alisema kuwa kukutana na waziri wa Kilimo nchini Tanzania kumeimarisha maradufu ushirikiano ambao umeanzishwa kwa muda mrefu na shirika hilo.
 
Alisema kuwa mradi wa nguvu za Atomiki Duniani katika Kanda ya Afrika unahusisha nchi 45 ambapo unajikita katika uhusiano wa ushirikiano katika mazao mbalimbali yanayozalishwa.
 
Alisema katika Visiwa vya Zanzibar Shirika hilo limesaidia kutatua changamoto kwa kuteketeza magonjwa yote yanayoambukizwa na Mbung’o.
 
MWISHO

Prof. Kabudi Akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb)  amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Mikhail Bogdanov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi katika Ofisi Ndogo ya Wizara Jijini Dar es Salaam.
 
Katika mazungumzo hayo, Waheshimiwa Mawaziri wamezungumzia masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya mataifa haya mawili, hususan, katika Nyanja ya kidiplomasia, nishati, biashara na uwekezaji. Naibu Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku  mbili.

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Naibu Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Urusi Mikhail Bogdanov Ikulu Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov kabla ya kuanza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov ambaye aliambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Waziri Kairuki Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Balozi Wa Uingereza Nchini

$
0
0
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke mapema hii leo Machi 13, 2019 katika ofisi zake Jijini Dodoma

Lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kujadili maeneo muhimu yanayohusu masuala  ya uwekezaji ambapo Waziri Kairuki alieleza vipaumbele muhimu vya uwekezaji  vitakavyochangia adhma ya Serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda ikiwemo kuwekeza katika maeneo ya kilimo, elimu, afya, viwanda vya nguo pamoja na ujenzi wa Miundombinu ya barabara.

“Ninafarijika kwa ujio wako na ni ishara nzuri ya mahusiano mazuri yaliyopo  baina ya nchi hizi mbili naamini yatasaidia katika fursa za uwekezaji hasa kwa namna Uingereza ilivyochangia katika maeneo muhimu nchini ikiwemo elimu,”alisema Kairuki

Waziri aliongezea kuwa, Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kwa kuzingatia mchango unaotokana  na wawekezaji hasa katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo nchini.

Waziri Kairuki alieleza kuwa, kuwepo kwa Idara ya uwekezaji katika Ofisi ya Waziri Mkuu ni hatua muhimu kwani itasaidia kuongeza nguvu ya ufuatiliaji na utekelezaji wa masuala hayo na kuendelea kuleta mabadiliko katika kutatua changamoto zilizozikabili sekta hiyo.

Aidha alimshukuru balozi huyo kwa hatua ya mazungumzo yenye tija pamoja na kuendelea kuunga mkono nchi ya Tanzania na kuwataka kuendeleza urafiki huo kwa kuwekeza zaidi katika maeneo aliyoyaainisha ikiweko yale ya vipaumbele.

Naye Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Sarah Cooke aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na sera zinazovutia wawekezaji pamoja na maboresho yanayofanywa kuwavutia wawekezaji nchini ikiwemo maeneo ya ulipaji wa kodi.

“Tunaelewa kuwa Serikali inafanya jitihada kubwa katika kuboresha mazingira ya biashara ikiwa ni pamoja na mazingira ya ulipaji wa kodi tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuwa na mchango katika maendeleo ya nchi pamoja na kuimarisha mahusiano yaliyopo,”alisisitiza Cooke.

Rais Magufuli Aonyeshwa Uwanja Wa Mpira Wa Kisasa Utakaojengwa Jijini Dodoma

$
0
0
Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu wa Tanzania na Misri wanaoshughulikia ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI.

Balozi wa Morocco hapa nchini aliyeongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco Abdelilah Benryane amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocoo wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco hapa nchini mwaka 2016 ikiwemo ujenzi wa Msikiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Jijini DSM na kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema uwanja huo utajengwa eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma – Morogoro, utajengwa kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 85,000 na 100,005.

TRA Yawahimiza Wafanyabiashara, Wamiliki Wa Majengo Kulipa Kodi Kwa Wakati

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewahimiza wafanyabiashara na wamiliki wa majengo kote nchini kulipa kodi kwa wakati hususani Kodi ya Mapato awamu ya kwanza, Kodi ya Majengo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambapo huu ndio muda muafaka wa kulipa kodi hizo. 

Akizungumza na walipakodi katika Ofisi za TRA Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema kodi ya ongezeko la thamani inatakiwa kulipwa ifikapo Machi 20 mwaka huu, kodi ya mapato inatakiwa kulipwa kabla ya tarehe 30 Machi, 2019 wakati mwisho wa kulipa kodi ya majengo ni mwezi Juni, 2019.

“Ninachukua fursa hii kuwahimiza wafanyabiashara na wamiliki wa majengo mliopo hapa na wale watakaosikia taarifa hii kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwahi kulipa kodi hizi kwa wakati ili kuepuka usumbufu na hatimaye kujikuta mnatozwa faini na riba," alisema Kayombo.

Amesema kuwa, viwango vya kodi ya majengo ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida, shilingi 50,000 kwa kila sakafu ya ghorofa na shilingi 20,000 kwa nyumba za ghorafa zilizoko vijijini.

"Tunaona serikali imepunguza kiwango cha kodi ya majengo, hivyo hakuna sababu ya watu kuchelewesha na kusubiri dakika za mwisho, tulifanye suala la ulipaji kodi kuwa utamaduni wetu kwa lengo la kuleta maendeleo ya nchi yetu,” alisisitiza Kayombo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Kayombo amewatahadharisha walipakodi kuhusu uwepo wa watu wanaotumia jina la mamlaka hiyo kufanya utapeli kwa kujitambulisha kuwa ni maofisa wa TRA wakidai kwenda kukagua ulipaji wao wa kodi.

“TRA ina utaratibu wake wa kuwasiliana na wafanyabiashara na kuwajulisha siku rasmi ambazo maofisa wetu watakwenda kufanya ukaguzi na unafanyika kwa uwazi bila vitisho na si kwa taratibu nyinginezo,”alisema Kayombo

Ameongeza kuwa, "kama  mtu atapigiwa simu au kama una mtu una wasiwasi nae tafadhali toa taarifa kwa ofisi zetu zilizopo karibu nawe au toa taarifa Kituo cha Huduma kwa Wateja  namba 0800 780 078 au 0800 750 075 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku na utupe namba ya mhusika ili tuweze kufuatilia.

“Pia kuna namba ya Whatsapp ambayo unaweza kutoa taarifa au kuuliza chochote kupitia namba 0744 233 333 ambayo ni maalum kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi na kuwawezesha kulipa kodi kwa wakati,” alisema Kayombo.

Richard Kayombo amesema kuwa, tangu mwezi Desemba mwaka jana, TRA imekuwa ikipata malalamiko kutoka kwa watu tofauti tofauti ambao wamekuwa wakitapeliwa fedha na maofisa feki wanaodai kufanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Rais Magufuli Amshukuru Rais wa Urusi Vladimir Putin

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Urusi ulioongozwa na Mjumbe Maalum wa Rais wa Urusi katika masuala ya Afrika ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mikhail Bogdanov, Ikulu Jijini DSM.

Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa ushirikiano na uhusiano mzuri kati ya Tanzania na nchi hiyo na amemhakikishia kuwa Serikali anayoiongoza inatambua umuhimu wa uhusiano huo na kwamba itauendeleza na kuukuza zaidi hususani katika masuala ya biashara, uwekezaji, utalii na utoaji wa huduma za kijamii kama vile afya, elimu na miundombinu.

“Naomba ufikishe ujumbe wangu kwa Rais Putin kuwa Watanzania wanaipenda Urusi na tunamkaribisha kuja kutembelea nchi yetu pamoja na wananchi wengine wa Urusi, tunawakaribisha pia wawekezaji waje wawekeza katika fursa mbalimbali zilizopo hapa Tanzania kwa manufaa yetu sote” Rais Magufuli

Kwa upande wake Bogdanov ambaye amewahi kutembelea Tanzania miaka 8 iliyopita ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kasi nzuri ya maendeleo iliyoyapata katika kipindi kifupi na amebainisha kuwa Urusi imedhamiria kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania.

Bogdanov amesema Urusi inao mpango mahususi wa kushirikiana na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika kuongeza kasi ya maendeleo na kwamba hivi karibu Tanzania na Urusi zitatiliana saini makubaliano ya kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano (Joint Permanent Commission – JPC) katika biashara, uwekezaji na uchumi ili rasilimali na fursa zilizopo katika pande zote zitumike kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Prof. Palamagamba Kabudi amesema mazungumzo hayo yamekwenda vizuri na kwamba Tanzania inatarajia tume ya pamoja ya ushirikiano ya Tanzania na Urusi itasaidia kukuza uchumi kupitia madini, gesi na utalii hasa wakati huu ambapo Urusi imeitangaza Tanzania kuwa nchi yenye vivutio bora vya utalii duniani.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi Tanzania nchi Urusi  Mej Jen. Mstaafu Simon Mumwi na Balozi wa Urusi nchini Tanzania Yuri Popov.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya March 14

Majanga Yazidi Kumwandama Mbowe.....DC Lengai Ole Sabaya Ampokonya Kiwanja Chake

$
0
0
Siku chache baada ya kutoka mahabusu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amekumbana na pigo lingine baada ya uongozi wa Wilaya ya Hai kutangaza nia ya kupoka kiwanja chake.
 
Jana, uongozi wa wilaya hiyo ulitangaza kuwa tayari umeshawasilisha kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ilani ya ubatilisho wa umiliki wa wamiliki 34 wa viwanja vilivyoko eneo la maendelezo ya viwanda la Weruweru wilayani Hai.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, alidai wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na wamiliki wa viwanja hivyo kudaiwa kodi ya pango la ardhi.
Kwa mujibu wa Ole Sabaya, wamiliki hao wa viwanja 34, kwa pamoja wanadaiwa kodi ya pango la ardhi inayofikia Sh. 1,828,166,096.

Mbali na Mbowe, orodha ya wadaiwa hao iliyotolewa Ole Sabaya jana, pia ina majina ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Cynthia Ngoye, Kiwanda cha Kutengeneza Vipuri cha Kilimanjaro Mashine Tools Manufacturing Company Ltd kilichoko chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na wafanyabiashara maarufu wa Mji wa Moshi wanaomiliki shule binafsi na kampuni za utalii.

Akitangaza orodha hiyo jana, wakati wa mkutano wa siku mbili wa kusikiliza kero, malalamiko na migogoro ya ardhi wilayani mwake, Ole Sabaya alisema watu hao wamo kwenye orodha ndefu ya wamiliki ambao viwanja vyao vimeombewa kibali cha kufutwa.

Kwa mujibu wa Ole Sabaya, Kiwanda cha Mashine Tools kina deni la Sh. milioni 315.721 ambalo kinadaiwa kati ya mwaka 2010 na 2018.
 
“Huko nyuma, watu walipewa viwanja 52 vikubwa, wakaambiwa waendeleze kwa sababu ni eneo la viwanda, wana miaka mingapi? Ofisa Ardhi yuko wapi? Njoo, nini kimetokea pale?" Ole Sabaya alihoji.

“Sasa sikilizeni huo muziki, unapewa shamba (eneo la kiwanja) mwaka 1984, mmesikia? Kabla mimi sijazaliwa, hajawahi kufanya lolote, akapewa na halmashauri ili waendeleze kujenga viwanda.

"Sasa Ofisa Ardhi ameshaandika barua ya kubatilisha hivyo viwanja. Niwaambie hapahapa, wako watu mnaowaheshimu na hawalipi kodi na leo nitawataja humu.”

Katika mkutano huo, Ole Sabaya alipokea malalamiko 266 yanayohusu ardhi na kuahidi kuwa ndani ya siku mbili, yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi.

Kabla ya kutaja majina ya wadaiwa hao, Ofisa Ardhi Mteule Wilaya ya Hai, Jacob Muhumba, alisema: "Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya, wengi waliopewa vile viwanja, wengine walipewa tangu mwaka 1984, wengine mwaka 2001, wa mwisho kabisa ni mwaka 2004. Wengi hawajaendeleza, lakini pia hawalipi kodi ya ardhi."

Kwenye orodha hiyo ya wadaiwa wa pango la ardhi ambayo imedaiwa kutumwa kwa Waziri Lukuvi, jina la Mbowe ni la 17 akidaiwa kumiliki kiwanja/shamba Na. 51.

Inadaiwa kuwa kiongozi huyo wa kisiasa ana deni la Sh. milioni 28.284 ambalo hajalilipa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2018, wakati Hilda Ngoye anadaiwa Sh. milioni 18.688.

Credit:Nipashe

Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Kabudi kushiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika

$
0
0
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 14 Machi, 2019 kuelekea Windhoek, Namibia kwa lengo la kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya  ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia tarehe 15 hadi 17 Machi 2019.

Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mawaziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Mawaziri wa Fedha pamoja na Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wote wa SADC. Mkutano huu utatanguliwa na Kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 14 Machi 2019 ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe anashiriki.

Aidha, mkutano huu utajadili  masuala mbalimbali ikiwemo: Taarifa ya utekelezaji wa mipango na mikakati ya SADC; Taarifa ya Kamati ya Fedha na Kamati ya Usimamizi wa Rasilimali watu; Hatua zilizofikiwa katika mchakato wa Visiwa vya Comoro kujiunga na SADC na Mpango wa Kuanzisha Chuo cha Uhawilishwaji cha SADC (SADC University of Transformation).

Masuala mengine yatakayojadiliwa ni; Utekelezaji wa Mkakati wa Kanda wa Mawasiliano; Mabadiliko ya Kitaasisi katika Umoja wa Afrika; na Majadiliano ya Ubia Mpya Baina ya Nchi za Kundi la Afrika, Carribean na Pasifiki (ACP) na Umoja wa Ulaya (EU) baada ya mkataba wa sasa wa Cotonou kumalizika mwaka 2020.

Mhe. Prof. Kabudi ambaye ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo, atatumia fursa hiyo kuendelea kusisitiza umuhimu wa kuimarisha utangamano na ushirikiano katika Kanda na kufanya Jumuiya ya SADC kuwa chanzo muhimu cha maendeleo kwa wananchi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 13 Machi 2019.

Shirika la chakula Duniani WFP waungana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kusafirisha chakula nje ya nchi

$
0
0
👉*Kwa mwaka huu wamejipanga kununua zaidi ya tani laki 1 za mahindi

👉*JPM atoa Bil 5/- kukarabati mabehewa 200, WFP kukarabati 40 kwa Bil 1.1/-

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele amesema hawezi kuwa tayari kuona baadhi ya masuala yana shindwa kufanikiwa katika taasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kisingizio cha kubanwa na sheria.

Alisema hayo jana wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kutengeneza mabehewa 40 kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Mpango wa Chaakulaa Duniani (WFP) kwenye karakana ya treni jijini Dar es Salaam jana.

Mhandisi Kamwele alisema, uwiano wa mizigo inayosafirishwa hailingani na uwezo wa maamlaka ya bandari na TRC kutokana na uwekezaji mkubwa uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano na fursa ya kupakana na nchi zisizo na bahari.

“TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania), TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) na TRC zinakwamisha uwezo wa bandari yetu kupakua na kupakia mizigo. Tutafanya hiki kwa pamoja maaana nimebaini tatizo kubwa lipo TRA,” alisema Mhandisi Kamwele na kuongezaa:

“Nimeshamwandikia baruaa Waziri wa Fedha na Mipango tukutane kwa ajili ya maazungumzo, maana sheria za fedha zipo lakini kama zinatukwamisha tuzifanyie marekebisho. Kwa mfano Uganda inazalisha tani laki 7.5 kwa mwaka lakini uwezo wa bandari yetu hadi sasa ni tani laki tatu kwa mwaka, tunakwama wapi. Tutatajana nani anakwamisha kupata hii mizigo.”

Aidha, katika hafla hiyo TRC na WFP walikubaliana kusafirisha mizigo ya chakula kutoka shirika hilo la kimataifa linalosambaza chakulaa ndani na nje ya nchi.

Ambapo katika kuimarisha uhusano wao WFP wameamua kutoa kiasi cha Dola za Kimarekani 600,000 sawa na Sh Bilioni 1.1 kwa ajili ya kukarabati mabehewa 40 ya shirika hilo. 

“Napenda kutumia furssa hii kuwashukuru WFP kwa msaada huu ambao utaenda kukuza uwezo wa shirika la reli katika kuhudumia mizigo hususan unaopita bandari ya Dar es Salaam kwenda mikoa mingine na nchi jirani kama Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia, Rwanda na Burundi. Tunashukuru WFP kwa kuunga mkono juhudi za serikali iliyojielekeza kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini kwa kukuza biashara na kujenga uchumi wa viwanda,” alisema Mhandisi Kamwele.

Katika kuimarisha shirika hilo, hivi karibuni Rais Dk. John Magufuli alitoa kiasi cha Bil 4 kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa ya mizigo, ambapo lengo ni kukarabati mabehewa 200 hadi kufikia sasa TRC wameshakarabati mabehewa 40.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema kwa kiasi kikubwa mabadiliko yametokea ndani ya shirika hilo tangu kuingia madarakani Rais Magufuli, ambaye aliapa kuinua uchumi wa watanzania kupitia viwanda na miundombinu imara.

“Miaka 15 iliyopita TRC ilikuwa na uwezo wa kusafirisha hadi tani milioni 1.4 kwa mwaka, lakini katikati tulipata misukosuko tukapoteza uwezo wetu. Tulipolibinafsisha tulizifunga njia nyingi katika reli ya kati na ya Tazara.

“Tunafanya ukarabati mkubwa katika reli ya kati, tunakarabati kilomita 970. Tayari kipande cha Tanga hadi Mombo kimeshakamilika viwanda vya saruji vimeanza kusafirisha mizigo yao kwa njia ya reli,” alisema Kadogosa.

Alibainisha, uhusiano wao na WFP unafikia mwaka mmoja sasa na kwa kuwa hilo ni shirika la kimataifa kuna uwezekano mkubwa wakapata wateja wengi zaidi kwa kuwa vigezo wanavyotumia kutaka kusafirisha mizigo hadi vimekubaliwa maana yake TRC wanaweza kufanya kazi na shirika lolote duniani.

“Mkakati huu wa kukarabati mabehewa una lengo la kukarabati mabehewa zaidi ya 500, kwa sasa tunaanza na haya 200 kwa fedha iliyotolewa na Rais Magufuli. Tunafanya kazi usiku na mchana ili tumalize mapema, mpango huu utasaidia kutoa ajira za moja kwa moja 30 na za muda mfupi 32,” alisema Kadogosa.

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa WFP, Michael Dunford alisema walianza kutoa kazi za muda mfupi ili kuangalia uwezo wa TRC lakini ndani ya kipindi kifupi wamevutiwa na uwezo wao na ndiyo maana wameamua kufanya nao makubaliano.

“Mpango wa chakula kazi yake si lishe tu bali kusafirisha mizigo pia, tangu mwaka 2010 katika ardhi ya Tanzania tumenunua kiasi cha tani 500,000 za chakula, kwa mwaka jana 2018 tumenunua zaidi yaa tani laki moja na  mwaka huu tuna mpango wa kununua zaidi ya tani laki moja na nusu, hii mizigo yote inahitaji kusafirishwa.

“Ndiyo maana tukaamua kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa 40 yatakayosaidia kusafirisha mizigo yetu ndani na nje ya nchi kwenda DRC, Uganda hadi Sudan. Si tu tutaongeza ajira lakini pia tutachangamsha uchumi kwa masuala mbalimbali ya usafirishaji na miundombinu,” alisema
Dunford.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedith Kakoko ambaye pia alihudhuria hafla hiyo alisema kuimarika kwa shirika la reli kuna faida kubwa kwa TPA kwa sababu kazi zao zinategemeana.

“Hakuna reli bila bandari na hakuna bandari bila reli, lazima kazi zetu tuzifanye kwa pamoja. Nafikiria pia TPA tuingie mkataba kama huu na WFP kwa sababu ya kurahiisisha kuvusha mizigo mipakani. Na TRA vilevile wanahitaji kuhusishwa kwa kuwa yapo mambo mengi yanakwama au kuchelwa kwa kukosa maelewani,” alisema Kakoko.

Ushirikiano huu utakuwa na tija kwa wakulima na wafanyakazi wa kubeba na kupakua mizigo kuanzia bandarini hadi kwenye maeneo ya reli, kwa kuwa WFP wamepanga kuwa watanunuaa chakula kutoka Tanzania ambayo ni faida kwa wakulima na watasafirisha kwa kutumia miundombinu ya reli na wakifika maeneo ya maziwa makuu watavusha kwa kutumia Ziwa Victoria kwenda nchi jirani.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images