Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Kufungua Soko la Dhahabu Geita

$
0
0
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajia kufungua soko la dhahabu mkoani Geita, Alhamisi Machi 14, 2019  mwaka huu likiwa ni soko la kwanza nchini katika madini ya dhahabu na la tatu kwa ukubwa barani Afrika.

Mkuu wa mkoa wa Geita, Robert Gabriel akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu Machi 11, 2019 amesema mkoa huo unaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu kwa zaidi ya asilimia 40 ya dhahabu yote inayozalishwa nchini.

Amesema soko kuu la dhahabu litakalokuwa eneo la soko kuu mjini hapa litakuwa na wadau wote walio kwenye mnyororo wa biashara ya madini wakiwemo wanunuzi, wauzaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Madini, benki na mamlaka ya serikali za mitaa.

Amesema kuwepo kwa wadau wote eneo moja kutaondoa urasimu na kurahisisha kufanyika biashara.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 12

Mpina Azindua Mpango wa Kuendeleza Mifugo Nchini

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, amezindua Mpango Kambambe wa Kuendeleza Sekta ya Mifugo nchini (Tanzania Livestock Master Plan-TLMP) huku akimtaka Katibu Mkuu Mifugo kuandaa mpango wa utekelezaji wa mkakati huo ndani ya siku 30 ili utekelezaji uanze mara moja.

Akizindua mpango huo jijini Dar es Salaam, Waziri Mpina alisema, ni lazima mpango mkakati wa utekelezaji uwasilishwe ofisini kwake ndani ya kipindi hicho ili kuondoa dhana iliyojengeka ya mipango mingi kuandaliwa kwa muda mrefu na gharama kubwa, lakini usimamizi na utekelezaji wake kuwa dhaifu na kushindwa kuleta matokeo yaliyotarajiwa.

Alisema Tanzania ina mifugo mingi, ikiwa na asilimia 1.4 ya ng'ombe duniani na asilimia 11 ya ng'ombe Bara la Afrika wako Tanzania huku ikiwa ya pili barani Afrika baada ya Ethiopia.

Waziri Mpina alisema fursa na changamoto zimefanikisha kuandaliwa kwa mpango huo ili kuondoa vikwazo na kuweka mazingira wezeshi ya ufugaji, biashara na uwekezaji.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa malisho na maji, wafugaji kufukuzwa kila mahali, ukosefu wa dawa na chanjo za mifugo, ongezeko la bidhaa za mazao ya mifugo kutoka nje ya nchi, uwekezaji wa kusuasua, ukosefu wa bei nzuri, soko la uhakika na mitaji na ukosefu wa mifugo iliyoboreshwa na huduma za utafiti.

Aliwataka wadau wa maendeleo waliofadhili mpango huo Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) na Taasisi ya Bill & Melinda Gate Foundation, kutoishia kufadhili uandaaji wa mpango huo badala yake washiriki moja kwa moja kwenye utekelezaji wake.

Pia aliwataka watendaji wote wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa kujipanga na kushiriki katika utekelezaji wa mpango huo ili kuleta matokeo ya haraka.

Waziri Mpina pia aliitaka sekta binafsi, wafugaji, jumuiya za wafugaji, wafanyabiashara, wawekezaji, taasisi za fedha kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki kutekeleza mpango huo.

Kufuatia mpango huo, serikali italazimika kufanya marekebisho ya sera na sheria pamoja na kuanzisha mikakati na miongozo mipya ili kufanikisha utekelezaji wa mpango huo kwa ufanisi mkubwa.

Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema kuzinduliwa kwa mpango huo kumeiwezesha wizara yake kupanga matumizi bora ya ardhi ili kufanikisha utekelezaji wa mpango huo.

"Ardhi yangu haina maana kama haitumiki vizuri, mimi nafurahi sasa mmejipanga na mmetengeneza mpango mzuri ambao utasaidia hata kunipa kazi ya kupanga matumizi ya kufanikisha mpango wenu, nataka nikuhakikishie mheshimiwa Mpina tuko pamoja najua mahitaji yenu,” alisema Lukuvi.

Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel, alisema mpango huo ulianza kuandaliwa miaka mingi iliyopita, lakini sasa umekamilika na kuzinduliwa huku akimhakikishia Waziri Mpina kuwa atasimamia kikamilifu utekelezaji wake ili kuleta matokeo ya haraka yanayotakiwa na Watanzania.

Vikao vya kamati za Bunge Kuanza Leo Jumanne Machi 12

$
0
0
Vikao vya kamati za Bunge kwa ajili ya mkutano wa 15 wa Bunge la Bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020  unaanza leo Jumanne Machi 12, 2019 huku kesho wabunge wote wakipokea mapendekezo ya Serikali ya mpango na kiwango cha ukomo wa bajeti ya mwaka huo wa fedha.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana Jumatatu na Ofisi ya Bunge jijini Dodoma, vikao hivyo vinaanza kuanzia leo hadi Machi 30, 2019 kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge la bajeti Aprili 2, 2019.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kesho  Jumatano Machi 13,2019 kamati hizo za sekta zitaanza ziara za kutembelea na kukagua miradi mbalimbali na ziara za kufuatilia uwekezaji pamoja na thamani halisi ya matumizi ya fedha za umma.

Machi 22 hadi 24, 2019, Kamati za Sekta zitaanza uchambuzi wa taarifa za utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(2).

Waziri Biteko Ateta Na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya kuwekeza katika sekta ya madini.

Dkt. Gollmer amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini hususan katika masuala ya utafiti na uchimbaji wa madini kutokana na ushawishi unaofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi  ambaye amekuwa akihamasisha watu wa mataifa mbalimbali nchini humo kuwekeza nchini.

Pia, ameeleza kwamba, kampuni hizo hazina shaka ya kuwekeza Tanzania kutokana na mazingira tulivu ya kisisasa yaliyopo nchini pamoja na utajiri wa rasilimali madini ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao hicho ni muhimu na kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara inaratajia kukutana na kampuni hizo.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugeni wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa Waziri Kungulu Kasongi.

Kagame Afunguka Chanzo cha Mgogoro Kati Ya Rwanda na Uganda

$
0
0
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameelezea kuwa chimbuko la mgogoro baina ya nchi yake na nchi ya Uganda ni la tangu miaka 20 iliyopita nchi ya Uganda ikitaka kuangusha utawala wake.

Akihutubia mkutano wa kitaifa Rais Kagame amesema mgogoro huo ulishika kasi mnamo miaka ya hivi karibuni kutokana na serikali ya Uganda kuunga mkono kundi la RNC linalopinga Rwanda na ambalo linatumiwa na Uganda kuwanyanyasa raia wa Rwanda wanaotembelea au wanaoishi nchini Uganda.

Akihutubia mkutano wa kitaifa unaomkutanisha na viongozi wengine kuanzia ngazi ya mashinani,rais Paul Kagame amezungumzia kwa kirefu mgogoro baina ya Rwanda na nchi ya Uganda na kusema mgogoro huo ni wa tangu miaka 20 iliyopita.

Akifafanua mgogoro huo Rais Kagame amerejelea kitabu kinachoitwa 'From Genocied to continental War'' ambacho kiliandikwa na Gerard Prunier mwanishi wa vitabu kutoka Mfaransa.

Rais Kagame amesema kwamba mwandishi huyo aliandika kwamba alikutana na waziri wa zamani wa mambo ya ndani marehemu Seth Sendashonga mwaka 1998 pmaoja na maafisa wakuu wa jeshi la Uganda na kuzungumzia mipango ya kumsaidia Sendashonga ili kuangusha utawala wa Kagame.Mwandishi huyo katika kitabu chake kulingana na maelezo ya rais Kagame, Uganda ilikuwa imemuahidi kumsaidia kijeshi.

''Sababu ya mimi kurejelea kuzungumza haya nimetaka kuwaonyesha mfululizo wa jinsi mambo yalivyokwenda mnamo miaka 20 iliyopita.Tulijaribu kufanya mikutano ya hapa na pale ili kutafuta suluhu.lakini matatizo hayo hayaishi.Ukweli ni kwamba Seth Sendashonga alifariki dunia kwa kuwa alivuka mstari mwekundu.Sifurahii kusema hivyo lakini pia sijutii kifo chake''

Seth Sendashonga aliuawa katika mazingira ya kutatanisha mwaka 1998 mjini Nairobi alipokuwa uhamishoni baada ya kutofautiana na utawala wa Rwanda.

Rais Kagame amesema mgogoro huo ulishika kasi hivi karibuni kufwatia wananchi wa Rwanda wanaoingia nchini Uganda au kufanyia kazi nchini humo kushikwa na kuzuiliwa sehemu ambazo hazijulikani na kufanyiwa vitendo vya mateso huku akishtumu utawala wa Uganda kutoa nafasi ya ushirikiano kwa kundi la Rwanda National Congress linaloongozwa na mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda jenerali Kayumba Nyamwasa:

''RNC wanafanya kazi kwa ushirikiano na vyombo vya usalama vya Uganda.kilicho wazi ni kwamba Wanachokifanya ni kunyanyasa wanyarwanda ambao hawataki kuungana nao huku wakiwasingizia  kwamba wametumwa na utawala wa Kigali kuhujumu usalama wa Uganda na kuuwa wanyarwanda wa upinzani.Ni madai yasiyo na msingi,lakini haya yote yanaonyesha ushirikiano wa dhati uliyopo baina ya serikali ya Uganda na kundi la RNC.''
 
Uganda imekuwa ikiishutumu Rwanda kuwatuma majasusi na kufanyia vitendo vya ujasusi kwenye ardhi yake,shutuma ambazo Rwanda inakanusha.

Rais Kagame amesisitiza kwamba mara kadhaa mwenyewe aliwasilisha malalamiko hayo kwa mwenzake Yoweri Museveni na kwamba hakuonyesha utashi wowote wa kuyatatua.

Wiki iliyopita serikali ya Rwanda ilikataza wananchi wake kwenda nchini Uganda na kusababisha mkwamo wa biashara.Rwanda inasema inatoa kipaumbele kwa maiasha ya raia wake zaidi kuliko biashara baina ya nchi mbili. 

Credit: BBC

Anusurika Kufa Baada ya Sehemu zake za Siri Kukatwa

$
0
0
Mtu mmoja mkazi wa Marangu mkoani Kilimanjaro amenusirika kufa baada ya vijana kumkamata na kuzikatia chini sehemu zake za siri.
 
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 53 amesema, tukio hilo lilimtokea juzi wakati akitoka katika shughuli zake za kila siku ndipo alikutana na vijana wawili ambao walianza kumpiga.
 
"Nilitoka kazini muda wa saa tatu usiku nikiwa napandisha nyumbani,  nikakutana na vijana, mmoja akanipiga na chuma mgongoni nikaanguka chini, mwingine akachomoa sime akachana suruali nliyokuwa nimevaa na kunikata sehemu zangu,"alisema.
 
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, Hamisi Issah alisema, tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Marera lole Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani hapa.
 
Alisema kuwa, mtu huyo alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kwa kukatwa sehemu za siri akiwa maeneo ya karibu na nyumbani kwake.
 
Alisema kuwa , waliomjeruhi ni Inocent Rubi mwenye umri wa miaka 18 na mwingine anayeitwa Gift Olmekei ambaye ni mtoto wa kike ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiri na kusema wote wameshikiliwa na Jeshi la Polisi huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.
 
Aliendelea kusema kuwa, mara baada upelelezi utakapokamilika shauri hilo litapelekwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake ili waweze kujua mtu huyo alitoka wapi na watoto wadogo ambao ni wanafunzi.

Tanzania Yaingia Makubaliano Na Brazil Kuinua Kilimo Cha Pamba

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Tanzania na Brazil zimeingia makubaliano ya kuinua kilimo cha Pamba ili kiwe na tija kwa wakulima nchini.

Makubaliano hayo yamejili wakati ambapo Brazil ipo katika hatua kubwa za kimageuzi ya kilimo huku ikiwa na mafanikio makubwa katika sekta hiyo ambapo unatekelezwa katika nchi tatu za Burundi, Kenya na Tanzania.

Mradi wa kuinua kilimo cha Pamba unaotekelezwa na Brazil nchini Tanzania utajikita Zaidi hasa katika kuhakikisha wakulima nchini wanapata Pamba mbegu bora na uzinduzi wa utafiti utamfikia mkulima ili aweze kuongeza tija.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa ameyasema hayo jana tarehe 11 Machi 2019 mara baada ya kutembelea na kukagua mashamba ya mfano wa kilimo cha Pamba katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza.

Mhe Bashungwa amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa kauli moja kuimarisha sekta ya kilimo huku katika zao la Pamba imejipanga kuhakikisha inazalisha mbegu vipara za Pamba zitakazotosheleza kwa wakulima wote nchini na kuondokana na utumiaji wa pamba manyoya ambayo imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko Pamba Manyonya.

Alisema Wizara ya kilimo itakuwa na jukumu la kushawishi wawezaji ili kuwekeza kwenye viwanda vya Pamba nyuzi pamoja na viwanda vya nguo na kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza vyema maelekezo yaliyoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yam waka 2015-2020.

Aidha, alisema kuwa Serikali pia imejipanga kupanua maabara za utafiti wa zao la Pamba ili kuimarisha ufanisi na tija ya zao hilo kwani mafanikio ya kilimo yanategemea zaidi katika utafiti.

Mhe Bashungwa ameishukuru serikali ya Brazil kwa utekelezaji wa mradi huo nchini Tanzania ambao unatokana na mahusiano mazuri katika nchi hizo mbili inayoakisi katika kufungamanisha kilimo na uchumi wa viwanda.

Kadhalika alisema serikali tayari imeanzisha vituo viwili vya kuzalisha Pamba mbegu vipara katika mkoa wa Simiyu pamoja na Mkoa wa Tabora

Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi Ya Msajili Wa Jumuiya Za Kijamii

Polisi wazuia mkutano CUF upande wa Lipumba ......, Wenyewe wagoma, Waendelea na mkutano

$
0
0
Mkutano Mkuu wa saba wa Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, umeingia dosari baada ya Jeshi la Polisi kuingilia kati na kusema kuna zuio la mahakama.

Mkutano huo unaofanyika leo Jumanne Machi 12, Buguruni jirani na ofisi za chama hicho umeanza asubuhi kwa wajumbe kutoka maeneo mbalimbali nchini kuwasili na wakati zoezi la uhakiki likiendelea, polisi walifika na kuwataka kutoendelea na mkutano huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Zuberi Chembera, ambaye aliongozana na maofisa kadhaa wa polisi alifika katika ukumbi unakofanyika mkutano huo na kuzungumza na viongozi wa chama hicho wakiwemo Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Abdul Kambaya na kuwataka kutoendelea na mkutano.

“Sisi tumeleta taarifa kwamba mkutano una zuio,” alisema Chembera.

Hata hivyo viongozi hao wa Cuf walisema wataendelea na mkutano kwa sababu hawajaona nakala ya maandishi ya zuio hilo.

“Mkutano hauna zuio, je kuna ‘document’ umekuja nayo kamanda….ungekuja nayo tungekuelewa, sisi tunaendelea na mkutano wetu,” alisikika mmoja wa viongozi wa Cuf.

Mkutano huo ambao waandishi wa habari hawaruhusiwi kuingia ukumbini umefunguliwa na Naibu Msajili, Sisty Nyahoza .

Katika hotuba yake, Nyahoza amesema mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndio maana umetambuliwa na Ofisi yake.

Amewapongeza kwa kile alichosema wamehimili mapito ya mahakama na wameendelea kukilinda chama.

Vilevile amewapongeza kwa kuteua bodi mpya ya wadhamini na kuwakumbusha wajibu wao wa kutunza Mali na fedha.

Amewataka pia kuzingatia mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa.

Nyahoza pia amesema sheria ya sasa ya vyama vya siasa hairuhusu vyama kuwa na vikundi vya ulinzi.

Viwanja Vikubwa Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab Sec)

$
0
0
Viwanja Vikubwa Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab Sec)
Viwanja vipo mtaa wa Kimele, Kata Mapinga, km 2 tu kutoka Shule ya secondary Baobab (main road ya Dar to Bagamoyo).
Viwanja vimepangwa vizuri, vina miundombinu ya maji na umeme. 


Viwanja viko vya size na bei tofauti kuanzia mita 20/25 kwa bei ya tsh 6 milion, mita 20/30 kwa bei ya tsh 8 milion, mita 20/40 kwa bei ya tsh 10 milion, mita 30/50 kwa bei ya tsh 18 milion, mita 40/50 kwa bei ya tsh 24 milion, mita 40/60 kwa bei ya tsh 30 milion,

Pia ipo nyumba pagala (haijapauliwa) na ina vyumba 3, kimoja master, sebure, dining, public toilet, kitchen etc na bei yake ni tsh 23,000 (kiwanja chake ni sqm 400 au 20/20 mita)

Na pia, kwa Bunju sokoni, kipo kiwanja cha sqm 1800 kinauzwa tsh 54 milion.

Luksa kulipa kwa awamu (anza na 75%, maliza na 25%)
Ukipata ujumbe huu mjulishe ndugu/jamaa/rafiki yako.
Biashara hii haina dalali, mpigie mhusika: 0758603077, whatsap 0757489709

Waziri Biteko azitaka nchi za Maziwa Makuu Kudhibiti Raslimali Ardhi

$
0
0
Na Issa Mtuwa Dodoma
Nchi Wanachama wa Maziwa Makuu zimetakiwa kushikamana kuunganisha nguvu katika kulinda na kusimamia matumizi ya raslimali ardhi ikiwemo madini ili kunufaisha nchi hizo. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akifungua mkutano wa Kimataifa    wa nchi Wanachama wa Maziwa Makuu (International Conference on the Great Lakes Region - ICGLR) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 11-12 Machi 2019 katika Hotel ya Morena jijini Dodoma.  

Biteko amezitaka nchi hizo kuunganisha nguvu ya pamoja katika kudhibiti raslimali ardhi ikiwemo madini na kujiwekea utaratibu utakao dhibiti shughuli za uzalishaji na biashara ya madini ili raslimali hizo zinufaishe mataifa yao na zisitumike vibaya. 

“Unganisheni nguvu kwa pamoja, wekeni utaratibu utakao wafanya nchi wanachama kunufaika na raslimali ardhi/madini. Jitahidini kuhakikisha raslimali hizo hazitumiki vibaya kama ilivyo kubaliwa kwenye itifaki, hivyo lazima kuwe na utaratibu na sheria kwa kila nchi namna ya kudhibiti uzalishaji na biashara ya madini,” amesema Biteko. 

Naye, Mtaalam kutoka Wizara ya Madini, Mhandisi Assah Mwakilembe amesema Mkutano huo unalenga kujadili na kupitia mfumo wa udhibitisho wa mnyororo wa madini kwa lengo la kudhibiti uzalishaji na biashara ya madini katika nchi za maziwa makuu kufuatia kuwepo tetesi zilizo kuwa zinahusisha raslimali ardhi (Madini) na ufadhili wa vita katika nchi za aaziwa makuu. (Region Certification Manual) 

Akizungumza mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu marekebisho ya Sheria Madini ya Mwaka 2017 Mkurugenzi wa Idara ya Sheria kutoka Wizara ya Madini, Edwin Igenge amesema kwa upande wa Tanzania, imetekeleza itifaki ya pamoja ya nchi wanachama wa Maziwa Makuu kama ilivyo kubaliwa. 

Ameongeza kuwa, utekelezaji wa itifaki kwa Tanzania ni pamoja na marekebisho ya sheria ya Madini ya Mwaka 2017 yaliyopelekea kuundwa kwa Tume ya Madini ambapo shuguli zote za usimamizi wa raslimali madini zimepewa Tume ya Madini ambapo kabla ya hapo shuguli hizo zilikuwa chini ya Kamishna wa Madini. 

Igenge amesema kuanzishwa kwa itifaki katika nchi za maziwa makuu kulitokana na tetesi za uwepo wa matumizi mabaya ya raslimali ardhi ikiwemo madini ambapo kipato cha raslimali hizo inasadikika kuwa zilikuwa zinatumika kufadhili shuguli za za kivita katika nchi za maziwa makuu, hivyo kupelekea kuanzishwa kwa itifaki ya pamoja kwa lengo la kudhibiti.  

Mkutano huo wa kimataaifa unahudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania, Burundi, Rwanda na wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretariati ya nchi wanachama wa Maziwa Makuu. Kwa upande wa  Tanzania inawakilishwa na Wizara ya Madini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Shirikisho la Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Chama cha Wanunuzi  na Wauzaji wa  Madini Tanzania  (TAMIDA), Tume ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa  Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST).  

Katika mkutano huo, Waziri Biteko aliambatana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Kamishna wa Madini Mhandisi Daivid Mulabwa, Mkurugenzi wa Sheria kutoka Wizara ya Madini Edwin Igenge na baadhi ya maafisa kutoka wizara ya Madini. 

Mbowe, Matiko Wakaribishwa Bungeni

$
0
0
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemkaribisha Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kuendelea na shughuli za kibunge huku akisema kwa lugha ya kibunge walikuwa Mtera.

Mbali na Mbowe mwingine ni mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko ambao kwa pamoja walikuwa mahabusu katika gereza la Segerea baada ya kufutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hata hivyo, Machi 7, 2019 Mahakam Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliwarejeshea dhamana yao, baada ya kushinda rufaa waliyoikata wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu.

Baada ya kutoka, wawili hao leo Machi 12, 2019 wamekwenda bungeni kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango anawasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango, Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Kabla Waziri Mpango hajaanza kuwasilisha taarifa yake katika ukumbi wa Pius Msekwa, Spika Ndugai alisema, "Kwanza nianze kwa kumkaribisha kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni (Mbowe) na mheshimiwa Esther Matiko kwa lugha ya kibunge tunasema walikuwa Mtera," amesema.

Hata Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya kuanza kuongea naye aliwakaribisha bungeni na kusema ni matumaini yake Mungu atasaidia wahudhurie kwa kadri inavyotakiwa.

Polisi Kigoma Yaua Majambazi Watatu

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kuua majambazi watatu kati ya watano waliofanya tukio la unyanganyi wa kutumia silaha za jadi kwa kuteka gari aina ya Land Cruiser linalohudumia wakimbizi katika Kijiji cha Nyarulanga Kata ya Busunzu Wilayani Kibondo.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP Martin Otieno amesema majambazi hao waliteka gari hilo linalomilikiwa na Shirika la Good Neighbour na kupora mali mbalimbali ikwemo laptop, simu na fedha ambapo thamani ya vitu vilivyoporwa ni zaidi ya laki tatu.

Maelezo Ya Waziri Wa Fedha Na Mipango, Dkt. Philip I. Mpango Akiwasilisha Mapendekezo Ya Serikali Ya Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa 2019/20

$
0
0

Maelezo Ya Waziri Wa Fedha Na Mipango,  Dkt. Philip I. Mpango  Akiwasilisha Mapendekezo YaSerikali Ya Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa Na Ya Kiwango Na Ukomo Wa Bajeti Ya Serikali Kwa Mwaka 2019/20

 

UTANGULIZI


1.           Mheshimiwa Mwenyekiti,awali ya yotenapenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha wabunge wote kukutana tena hapa Jijini Dodoma, kupokea mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kwa mujibu wa Kanuni ya 97 fasili ya (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016. Aidha, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuijalia nchi yetu umoja na amani.

2.           Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kutumia fursa hii kuwapongeza Mheshimiwa Angellah Jasmine Kairuki (Mb), Mheshimiwa Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb), Mheshimiwa Prof. Palamagamba Aidan Kabudi (Mb), Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko (Mb), Mheshimiwa Joseph George Kakunda (Mb) na Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mawaziri ili kuongoza wizara mbalimbali. Ni matumaini yangu  kuwa Waheshimiwa Mawaziri mlioteuliwa na Waheshimiwa Wabunge wote mtaendelea kunipatia ushirikiano katika kuijenga nchi yetu kwa manufaa ya Watanzania wote.

3.           Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa hii inawasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na ukomo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2019/20 ambayo imegawanyika katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza ni tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi. Sehemu ya pili ni Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2018/19 na Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2019/20. Sehemu ya tatu ni tathmini ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2018/19 na mapendekezo ya kiwango na ukomo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/20.

SEHEMU YA KWANZA

TATHMINI YA MWENENDO WA HALI UCHUMI

4.           Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kuiandaa nchi kuelekea uchumi wa kipato cha kati, uchumi umeendelea kuimarika. Pato la Taifa  kwa kutumia mwaka wa kizio 2015 linaonesha kuwa katika robo ya tatu (Julai hadi Septemba) ya mwaka 2018, Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 5.0 kipindi kama hicho mwaka 2017. Shughuli za kiuchumi zilizokuwa kwa kasi kubwa ya ukuaji ni afya (asilimia 13.2), usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia 12.4); Maji (asilimia 10.7); Ujenzi (asilimia 7.4); Habari na Mawasiliano (asilimia 7.3); viwanda (asilimia 7.3); na Biashara na Matengenezo (asilimia 7.3).

5.           Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2018, mwenendo wa mfumuko wa bei nchini uliendelea kuwa tulivu katika wigo wa tarakimu moja kutokana na kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini na nchi jirani pamoja na usimamizi madhubuti wa sera za fedha na bajeti za Serikali. Mfumuko wa bei ulipungua kutoka wastani wa asilimia 4.0 Januari 2018, hadi kufikia asilimia 3.4 Juni 2018 na kuendelea kupungua zaidi hadi asilimia 3.0 Januari 2019.

6.           Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka unaoishia Januari 2019 thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nchi za nje ilikuwa dola za Marekani milioni 8,300.0 na thamani ya bidhaa na huduma zilizonunuliwa kutoka nje ilikuwa dola za Marekani milioni 10,462.6. Kwa upande wa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho wa mali nchi za nje ilikuwa dola za Marekani milioni 2,982.2 kutokana na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa za mitaji zilizoagizwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya miradi mikubwa ya maendeleo. Kwa matokeo hayo akiba ya fedha za kigeni ni Dola za Marekani milioni 4,884.4 Januari 2019, kiasi kinachotosheleza kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha takribani miezi 4.8. Kiwango hiki ni zaidi ya lengo la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki la miezi 4.5.

7.           Mheshimiwa Mwenyekiti, Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) uliongezeka kwa wastani wa asilimia 6.6 katika mwaka 2018 ikilinganishwa na ongezeko la wastani wa asilimia 5.5 katika kipindi cha mwaka 2017. Mwenendo huo ulichangiwa na kuimarika kwa ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi kulikotokana na jitihada za Serikali kupitia Benki Kuu katika kuchochea ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi. Riba za dhamana za muda mfupi za Serikali zilipungua hadi wastani wa asilimia 6.4 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 11.1 mwaka 2017. Vile vile, riba za mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi zimeendelea kupungua kutoka wastani wa asilimia 17.8 mwaka 2017 hadi wastani wa asilimia 17.4 mwaka 2018.

8.           Mheshimiwa Mwenyekiti,Mikopo kwa sekta binafsi iliendelea kuimarika kufuatia utekelezaji wa sera ya kuongeza ukwasi kwenye uchumi pamoja na jitihada zilizochukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu katika kuchochea ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi. Kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi imeendelea kuongezeka ambapo Januari 2019 ilikuwa asilimia 7.3 ikilinganishwa na asilimia 2.1 Januari 2018. Sehemu kubwa ya mikopo kwa sekta binafsi imeendelea kuelekezwa katika shughuli binafsi (asilimia 27.9 ya mikopo yote) ikifuatiwa na shughuli za biashara zilizopata asilimia 18.4, uzalishaji viwandani (asilimia 11.6) na kilimo (asilimia 7.8).

9.           Mheshimiwa Mwenyekiti, mwenendo wa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani umeendelea kuwa tulivu ambapo katika mwaka 2018, Dola moja ya Marekani ilinunuliwa kwa wastani wa Shilingi 2,263.8. Hii ni kutokana na utekelezaji madhubuti wa sera za fedha, usimamizi thabiti wa mapato na matumizi ya Serikali, matumizi ya gesi asilia na umeme wa maji badala ya mafuta katika kuzalisha umeme na baadhi ya viwanda nchini kuzalisha bidhaa ambazo awali zilikua zikiagizwa kwa wingi kutoka nje.

10.       Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Tano, itaendelea kutekeleza sera madhubuti za fedha na bajeti ili kuhakikisha uchumi wa nchi yetu unaendelea kuimarika.

SEHEMU YA PILI

TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MWAKA 2018/19 NA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA MWAKA 2019/20

A.           TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MWAKA 2018/19

11.       Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2018/19, Serikali ilitenga Shilingi bilioni 12,007.3 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, zikijumuisha Shilingi bilioni 9,876.4 fedha za ndani na Shilingi bilioni 2,130.9 fedha za nje. Hadi Januari 2019, jumla ya Shilingi bilioni 2,788.5 zilitolewa kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Aidha, Shilingi bilioni 144 zilipokelewa kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na kupelekwa moja kwa moja kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Wizara, Taasisi na Wakala za Serikali, Sekretaieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Vile vile, Shilingi bilioni 3,803.4 zimetumika kulipa mikopo iliyotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Serikali imeshatenga na inatarajia kutoa kiasi cha Shilingi bilioni 1,433.8 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo, ukiwemo mradi wa kufua umeme kwa kutumia nguvu ya maji Mto Rufiji (MW 2,115).

12.       Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo katika mwaka 2018/19 ni kama ifuatavyo:

(i)           Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Standard Gauge: Ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300) unaendelea vizuri kama ilivyopangwa, ambapo shughuli zinazoendelea ni ujenzi wa madaraja, makalavati, daraja lenye urefu wa km 2.54 katikati ya jiji la Dar es Salaam, ukataji wa miinuko, ujazaji wa mabonde na utandikaji wa reli. Katika kipande cha Morogoro – Makutupora (km 422), kazi zinazoendelea ni pamoja na ukataji wa miinuko na ujazaji wa mabonde, usanifu wa njia na ujenzi wa kambi za Kilosa na Ihumwa. Kwa upande wa kipande cha Isaka – Rusumo (km 371), hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa njia ya reli. Aidha, taratibu za ununuzi wa mabehewa, injini na mitambo itakayotumika kutoa huduma ya usafiri kwenye reli ya Standard Gauge zipo katika hatua za mwisho.

Katika miradi inayogharamiwa na mfuko wa reli, shughuli zilizofanyika ni: kununua vichwa 11 vya treni kwa ajili reli ya kati; kuendelea na ukarabati wa reli ya Tanga - Arusha (km 439) ambapo kipande cha Tanga – Mombo (km 129) kimeanza kufanya kazi ya kusafirisha mizigo na ukarabati wa vipande vya Mombo – Same (km124) na Same – Arusha (km 186) unaendelea. Aidha, kazi ya ukarabati wa mabehewa inaendelea ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati wa mabehewa 15.

(ii)         Mradi wa Kufua Umeme wa Maji Rufiji - MW 2,115: Hatua iliyofikiwa ni: kupatikana kwa mkandarasi wa mradi wa kufua umeme utokanao na nguvu ya maji katika Mto Rufiji ambaye ni Kampuni ya Ubia kati ya Arab Contractors na Elsewedy Electric S.A.E kutoka Misri ambapo mkataba wa ujenzi umesainiwa na mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi mwezi Februari 2019. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu wezeshi ikijumuisha njia ya umeme wa msongo wa kV 33 kutoka Msamvu hadi eneo la mradi; mifumo ya huduma ya maji na ya mawasiliano ya simu; kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 10 na kuendelea na ukarabati wa nyumba 28 za iliyokuwa kambi ya RUBADA; ujenzi wa barabara za Kibiti - Mloka – Mtemere – Matambwe Junction – Mto Rufiji (km 210) na Ubena Zomozi – Mvuha – Kisaki – Mtemere Junction (km 178.39) zimekamilika.

(iii)       Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania: Hatua iliyofikiwa ni: kuwasili kwa ndege nyingine tatu, moja ikiwa ni aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na mbili zikiwa ni Airbus A220-300, na hivyo kufanya idadi ya ndege zilizonunuliwa kuwa sita; kulipa sehemu ya gharama za ununuzi wa ndege moja aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na Bombadier Q400 zinazotarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa mwaka 2019. Kufuatia hatua hiyo, ATCL itaanzisha safari za ndege kwenda nchini China na India ambazo kimkakati ndizo masoko mapya ya utalii.

(iv)        Miradi ya Umeme: Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa njia ya kusafirisha umeme yenye urefu wa km 250 ya msongo wa kV 220 Makambako – Songea pamoja na vituo vitatu vya kupoza umeme vya Makambako, Madaba na Songea, hivyo kuwezesha mikoa ya Njombe na Ruvuma kuunganishwa katika Gridi ya Taifa; kuendelea na mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 wa Singida – Arusha – Namanga wenye urefu wa km 414; kuendelea na miradi ya kusafirisha umeme ya Geita – Nyakanazi (kV 220), Rusumo – Nyakanazi (kV 220) na Bulyankulu – Geita (kV 220); kuendelea na utekelezaji wa mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini na Makao Makuu ya Wilaya ambapo vijiji 1,782 na wateja 96,832 wameunganishiwa umeme hivyo kufikia jumla ya vijiji 1,039 vilivyounganishwa na umeme; kukamilisha utengenezaji wa mitambo minne ya kufua umeme na kupelekwa mitambo miwili ya kufua umeme katika eneo la mradi wa Kinyerezi I Extension – MW 185; Mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo MW 80: Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa barabara za kuingia eneo la mradi; kukamilika kwa ujenzi wa kikinga maji; kuanza kazi ya kuchimba handaki la kupitisha maji; kuendelea na uchimbaji wa eneo itakapofungwa mitambo; na kukamilika kwa ujenzi wa nyumba mbili kati ya tano za wafanyakazi.

(v)         Huduma zaMaji Mijini na Vijijini: miradi 65 imekamilika na kufanya jumla ya miradi yote iliyokamilika kufikia 1,659 na vituo vya kuchotea maji kuongezeka hadi 131,370 na kuhudumia wananchi 25,359,290. Upatikanaji wa huduma za maji Jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 85, katika mikoa mingine asilimia 80, miji midogo asilimia 64 na vijijini asilimia 64.8. Aidha, utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo mengine unaendelea katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa maji wa Ziwa Victoria – Igunga - Nzega na Tabora, mradi wa maji katika jiji la Arusha na Same – Mwanga - Korogwe. Vile vile, utekelezaji wa mradi wa maji katika miji 28 wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 465 upo katika hatua za kumpata Mtaalamu Mwelekezi na Mkandarasi wa mradi.


(vi)        Miradi ya Afya: Serikali imeendelea kuimarisha huduma za afya kwa kuongeza upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa asilimia 96. Hatua nyingine zilizofikiwa ni pamoja na: kukamilika kwa ujenzi wa jengo la vifaa vya uchunguzi (X–Ray Building)  na kununua vifaa vya tiba ya mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya; na kuongeza utoaji wa chanjo kufikia asilimia 97. Aidha, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya afya katika ngazi zote ikijumuisha ujenzi na ukarabati wa hospitali za rufaa za mikoa, kanda na kitaifa; ujenzi wa hospitali za halmashauri 67; ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya 352; kuajiriwa kwa watumishi wa sekta ya afya 7,680; ujenzi wa nyumba 310 za watumishi wa afya; ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati. Serikali imeendelea kuimarisha huduma za matibabu ya kibingwa kwa kuboresha miundombinu ya kutolea huduma, ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa na hivyo kupunguza rufaa za wagonjwa nje ya nchi katika hospitali za Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Mifupa (MOI),  hospitali ya Benjamin Mkapa na Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi – Mloganzila.

(vii)      Miradi ya Elimu: Serikali imeendelea kugharamia elimumsingi bila ada ambapo kila mwezi kiasi cha shilingi bilioni 24.4 kinatumika. Hatua nyingine zilizofikiwa ni: ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia ikijumuisha madarasa 870, matundu ya vyoo 1,958, mabweni 210, mabwalo 79; ukarabati wa shule kongwe; ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vya ualimu Ndala, Shinyanga, Patandi, Mpuguso na Murutunguru; kukamilisha maboma ya madarasa, mabweni na nyumba za walimu 39; ukarabati wa vyuo vya kati 20 kati ya 54 vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs), nyumba za walimu 39; kukamilika na kuzinduliwa kwa Maktaba ya Kimataifa yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,600 kwa wakati mmoja katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; ujenzi wa mabweni katika Chuo Kikuu cha Mzumbe yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000; ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vikuu vya Sokoine na Dar es Saaalm; na mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu 119,214; uimarishaji wa vyuo 10 vipya vya VETA na kukuza ujuzi kwa vijana; na ujenzi wa shule kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika chuo cha Ualimu Patandi.

(viii)    Kilimo: Utoshelevu wa Chakula kwa mwaka 2018/19 umefikia asilimia 124. Aidha, Serikali imeanza utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II) na mkazo umewekwa katika kuendeleza mazao ya kimkakati yakiwemo Kahawa, Pamba, Chai, Korosho, Tumbaku, Alizeti, Michikichi, Mpunga na Mahindi. Ili kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo, Serikali inaendelea kuimarisha shughuli za ushirika, ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 250,000 katika kanda saba, kuongeza uzalishaji wa mbegu za mafuta hususan alizeti na michikichi, kuimarisha shughuli za utafiti wa mazao, kuongeza thamani ya mazao ya kilimo kwa kufufua vinu vya kusindika mazao ya nafaka na mafuta, kudhibiti visumbufu vya mazao, kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo na kuimarisha mifumo ya masoko ya mazao. Vile vile, Serikali imeanza kuboresha mifumo ya takwimu za kilimo kwa kuanza usajili wa Wakulima.

(ix)        Mifugo: Hatua iliyofikiwa ni kuendelea kuimarisha vituo 3 vya kuzalisha vifaranga vya samaki vya Kingolwira (Morogoro), Mwampuli (Igunga) na Ruhila (Songea) kwa kuzalisha na kusambaza vifaranga vya samaki kwa wafugaji wa  samaki wakiwemo vijana. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na sekta Binafsi imeweza kuzalisha jumla ya vifaranga 17,301,076 kama ifuatavyo: kambamiti 11,080,000, sato 5,072,800 na kambale 1,148,276. Vile vile, jumla ya wananchi 6,995 wamepatiwa elimu ya ugani katika ukuzaji wa viumbe maji.

(x)         Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania): Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa tathmini ya athari za mazingira na jamii kwa upande wa Tanzania; kukamilika kwa tafiti za kijiolojia katika eneo la Chongoleani; kukamilika kwa tathmini za Kijiolojia na Kijiofizikia katika eneo la mkuza wa bomba; na kutwaa ardhi eneo la Bandari – Tanga (Chongoleani) kutakapojengwa miundombinu ya kuhifadhi mafuta.

(xi)        Miradi ya Viwanda:Kiwanda cha Kuunganisha Matrekta (TAMCO, Kibaha): Hatua iliyofikiwa ni: kuingiza matrekta 822 aina ya URSUS (semi knocked down) ambapo matrekta 571 yameunganishwa na matrekta 339 yameuzwa; Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini – CAMARTEC: kutengeneza zana zikijumuisha mashine 64 za kupandia mbegu za pamba, kusaga karanga, kukausha mbogamboga na kukata majani pamoja na  ujenzi wa mitambo 55 ya biogas; SIDO: kuendelea na ujenzi wa majengo ya viwanda 11 katika Mikoa ya Dodoma, Geita, Kagera, Katavi, Manyara, Mtwara na Simiyu na ujenzi wa ofisi za SIDO katika mikoa mipya ya Geita na Katavi.
(xii)      Miundombinu ya Biashara ya Madini: Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kuboresha mazingira ya biashara kwenye sekta ya madini ikihusisha: vituo vya umahiri katika mikoa saba, vituo vitatu vya mfano, jengo la taaluma la madini katika chuo cha madini, One Stop centreMirerani, Brokers house Mirerani, uanzishwaji wa masoko ya madini mikoani, na uwekaji wa mfumo wa ulinzi wa kidigitali Mirerani, ununuzi wa mtambo wa uchorongaji miamba kwa ajili ya kusaidia wachimbaji wadogo kupitia STAMICO.

(xiii)    Ardhi na Makazi: Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kuandaliwa na kusajiliwa kwa Hati Milki 110,000 na Hati za Kimila 133,000; kuandaliwa kwa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 263 katika Wilaya 45; kuandaliwa kwa Mipango Kabambe ya miji mikuu ya mikoa ya Arusha, Mwanza, Mtwara, Mara, Singida, Iringa na Pwani, Ruvuma, Tabora na Simiyu; kuendelea na hatua za maandalizi ya Mipango Kabambe ya miji mikuu ya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Rukwa, Shinyanga, Manyara, Dodoma, Tanga, Mbeya, Kagera, Kigoma, Katavi, Lindi, Kilimanjaro, Njombe na Geita; kuanzishwa kwa Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi; na kuongezeka kwa idadi ya benki na taasisi za fedha zinazotoa mikopo ya nyumba kufikia 31 na kuwanufaisha wananchi 4,174. Aidha, Mfuko wa Mikopo Midogo Midogo ya Nyumba ulio chini ya Benki Kuu umeongezewa mtaji wa dola za Marekani milioni 18 ambapo taasisi za fedha tano (5) zimepatiwa mtaji wa shilingi bilioni 13.87 kwa ajili ya kukopesha wananchi wa kipato cha chini kwa masharti nafuu.

(xiv)     Ujenzi wa Barabara Dar es Salaam: Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya TAZARA (Mfugale flyover); kuendelea na ujenzi wa barabara za muingiliano Ubungo; mradi wa kuendeleza Jiji la Dar es Salaam km 210 za barabara kwa kiwango cha lami; na kuendelea na ujenzi wa barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara – Kibaha (km 19) kwa njia nane.

(xv)      Ujenzi wa Meli: Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na Ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo katika ziwa Victoria; kufikia asilimia 82 ya ujenzi wa meli moja mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na mizigo tani 200 za mizigo katika ziwa Nyasa; na kukamilika kwa ujenzi wa matishari mawili katika Ziwa Nyasa. Kwa upande wa Ziwa Tanganyika, Ujenzi wa Meli Mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo, ambapo uandaaji wa mikataba kwa ajili ya ujenzi wa meli hiyo pamoja na ukarabati wa meli ya MV Liemba umekamilika. Miradi mingine ni kukamilika kwa ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo – Busisi; kukamilika kwa ukarabati wa kivuko cha MV Pangani II; kuendelea kukarabati vivuko vya MV Sengerema, MV Kigamboni na MV Misungwi.

(xvi)     Viwanja vya Ndege: Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa asilimia 90.7 ya ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal III) katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere; kuendelea na upanuzi wa maegesho ya ndege, ujenzi wa jengo la mizigo, uzio wa kiwanja, maegesho ya ndege za mizigo na jengo la kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Mwanza. Aidha, ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege vya mikoa vikiwemo vya Sumbawanga, Kigoma, Shinyanga, Mtwara, Songea, Mara, Songwe, Mbeya, Mwanza, Kigoma, Tabora na Iringa unaendelea.

(xvii)   Mawasiliano: Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo vituo vitatu (3) vya Mkongo katika maeneo ya Tukuyu, Kibaha na Kahama vimejengwa na kuvipa nguvu vituo vitatu (3) vya mkongo (Optical Line Amplifier (OLA) katika maeneo ya Ifakara, Kidatu na Mafinga; na kuendelea kutekeleza mradi wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi umetekelezwa kwa kubandika vibao vya namba za nyumba katika Halmashauri 12. Vile vile, Mfumo wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) umekabidhiwa rasmi kutoka kwa Mkandarasi SGS/GVG ambapo katika kipindi cha Julai, 2018 hadi Februari, 2019 jumla ya miamala 2,004,196,139 imepita katika mitandao ya simu na wastani wa fedha zilizopita ni Shilingi bilioni 12,202.7.

(xviii)Uendelezaji wa Bandari:Bandari ya Dar es Salaam: Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi na kuanza kutumika kwa gati Na.1; na kuendelea na ujenzi wa sakafu ngumu katika gati la kupakua na kupakia magari; Bandari ya Tanga: ukarabati wa miundombinu ya barabara kuelekea lango Na. 2 umekamilika; Bandari ya Mtwara: ujenzi wa gati la mita 300 la kuhudumia shehena mchanganyiko unaendelea. Aidha, ujenzi wa Bandari katika Maziwa Makuu (Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa) unaendelea.

(xix)     Ujenzi wa Barabara na Madaraja Makubwa: kazi zilizofanyika ni kujengwa kilomita 140.42 za barabara kuu na kilomita 12.43 za barabara za mikoa kwa kiwango cha lami. Aidha, kwa upande wa madaraja hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa Daraja la Mlalakuwa (Dar es Salaam); kuendelea na ujenzi wa madaraja ya Momba (Rukwa) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 94, Sibiti (Singida) asilimia 88.35, Mara (Mara) asilimia 85; na Ruhuhu (Ruvuma) asilimia 76; na kuanza ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 5.2.


(xx)      Ufungaji wa rada nne za kuongozea ndege za kiraia JNIA, KIA, Mwanza na Songwe: Hatua iliyofikiwa ni: JNIA: Kukamilika kwa asilimia 95 ya miundombinu ya rada. Mwanza: Ujenzi wa miundombinu  ya rada unaendelea vizuri. KIA: Ujenzi wa miundombinu  ya rada unaendelea na umefikia asilimia 90. Songwe: taratibu za ujenzi wa miundombinu zinaendelea. Aidha, mitambo itafungwa miundombinu itakapokamilika.

(xxi)     Miradi ya Mahakama: Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa Mahakama za Wilaya za Bukombe, Chato, Ruangwa, Geita na Kilwa; kukamilika kwa ujenzi wa Mahakama za Mwanzo za Magoma (Korogwe) na Mlowo (Mbozi); kuendelea na ujenzi wa Mahakama za mikoa ya Njombe, Katavi, Lindi na Simiyu; kuendelea na ujenzi wa Mahakama za Wilaya za Kasulu, Sikonge, Kilindi, Bunda, Longido, Kondoa, Njombe, Rungwe, Chunya, Wanging’ombe, na Makete; kuendelea na ujenzi wa Mahakama Kuu Kigoma na Mara ambao umefikia asilimia 80; ujenzi wa Mahakama za Mwanzo za Mkunya (Newala), Uyole (Mbeya), Ngerengere, Mlimba na Mang’ula (Morogoro); ukarabati mkubwa wa nyumba tatu za kufikia Majaji Mtwara; na kukamilika kwa uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji takwimu na kusajili mashauri, kuingiza taarifa muhimu za wadaawa ikiwa ni pamoja na kutuma taarifa kwa ujumbe mfupi (sms) kwa wadaawa kuhusu mwenendo wa mashauri. Aidha, imeanzishwa huduma ya mahakama zinazotembea (mobile court, kwa kuanzia na mikoa ya Dar es salaam na Mwanza, magari ambayo yamezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mwezi Februari 2019.

(xxii)   Miradi ya Kimkakati ya kuongeza mapato katika Halmashauri: Hatua iliyofikiwa niutekelezaji wa miradi ya kimkakati 37 ya kuongeza mapato ya halmashauri na kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali ikijumuisha Soko la kisasa – manispaa ya Morogoro, soko la kisasa – halmashauri ya mji Kibaha, Pwani, ghala la kisasa – halmshauri ya wilaya ya Ruangwa, kituo cha mabasi Mbezi Louis – Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, soko la Mburahati – manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam, ujenzi na upanuzi wa kiwanda cha kutengeneza chaki na kiwanda cha vifungashio – halmashauri ya wilaya ya Maswa, Simiyu, stendi ya mabasi Korogwe. Miradi hii inatekelezwa katika halmashauri 29 na ipo katika hatua mbalimbali.

(xxiii)Uwekezaji: Sekta ya Uwekezaji imeendelea kukua ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo ripoti mbalimbali za uwekezaji duniani zinaonesha Tanzania imeongoza kwa kuvutia uwekezaji kati ya nchi za Afrika Mashariki. Kwa mfano, Ripoti ya Uwekezaji ya Dunia ya mwaka 2018 inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) inaonesha kuwa Tanzania imevutia uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 1,180, ikifuatiwa na Uganda Dola za Kimarekani milioni 700 na Kenya Dola za Kimarekani milioni 672. Aidha, ripoti ya “Where to Invest in Africa” ya mwaka 2018 inayojulikana kama RMB’s Investment Attractiveness Index inayoonesha nchi zinazovutia zaidi kwa uwekezaji barani Afrika, Tanzania imeendelea kuwa katika kumi bora kwa kushika nafasi ya saba (7) kati ya nchi 52 ikipanda kutoka nafasi ya 9 mwaka 2017.

Aidha, jitihada za Serikali kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini zimewezesha kuongezeka mitaji katika viwanda mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, mtaji uliowekezwa chini ya Mamlaka ya EPZ umeongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.422 mwaka 2016 hadi Dola za Marekani bilioni 2.23 hapo Novemba, 2018, ikiwa ni ongezeko la Dola za Marekani milioni 808 (sawa na ongezeko la asilimia 56.8). Mwenendo wa mauzo ya bidhaa za viwanda hivyo nje ya nchi yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia Dola za Marekani bilioni 2.194 hapo Novemba 2018, kutoka Dola za Marekani bilioni 1.1 mwaka 2016, ikiwa ni ongezeko la asilimia 99.45. Mtaji mkubwa umewekezwa katika viwanda vya kuongeza thamani mazao (agro processing) ambapo ina asilimia 38 ya mtaji wote; zikifuatiwa na viwanda vya kuunganisha mitambo (assembling & engineering) asilimia 31 ya mtaji, mavazi na nguo asilimia 21 ya mtaji na uchakataji madini asilimia 10 ya mtaji. Aidha, viwanda 71 ni vya makampuni ya kigeni, viwanda 58 ni vya makampuni ya ubia na viwanda 45 ni vya makampuni ya ndani.

(xxiv)  Kuhamishia Utekelezaji wa Majukumu ya Serikali Makao Makuu Dodoma: Serikali imetekeleza azma yake ya kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Dodoma ambapo mpaka hivi sasa Wizara zote zimeshahamia Dodoma na jumla ya Watumishi 8,883 wanatekeleza majukumu yao wakiwa hapa Dodoma (Watumishi hao ni kutoka Ofisi/Wizara na Vyombo vya Ulinzi na Usalama). Vile vile, Mheshimiwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Naibu Mawaziri pia wameshamia Dodoma. Uendelezaji wa eneo la Mji wa Serikali – Ihumwa umeanza na jumla ya majengo 22 ya Ofisi za Wizara na Mwanasheria Mkuu wa Serikali yako katika hatua za mwisho za ujenzi.

(xxv)   Mfuko wa Maendeleo ya Vijana: Serikali imeendelea kuwawezesha Vijana kiuchumi ili waweze kujiajiri katika nyanja za uzalishaji mali na kutoa huduma ambapo hatua iliyofikiwa ni: kutolewa kwa mikopo nafuu yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.74 kwa vikundi vya vijana 523, vyenye wanachama 3,661 katika Halmashauri 128 za Tanzania Bara; na kuanzishwa kwa SACCOS 127 za Vijana kati ya 184 zinazotarajiwa kuanzishwa hadi kufikia mwaka 2020.

(xxvi)  Mafanikio mengine ni kuendelea kuimarika kwaAmani, utulivu na usalama nchini hivyo, kuwezesha kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii. Katika kutimiza jukumu hilo, Jeshi la Polisi limeendelea kuweka juhudi katika kudhibiti uhalifu sanjari na kuendelea kutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali ili jamii ibadilike na kuachana na matukio ya uhalifu.

(xxvii)                Mazingira:Serikali imetekeleza hughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa ikolojia ili kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, kujenga uwezo w taasisi na jamii kuhimili changamoto za mazingira na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuboresha kanuni za kutoa leseni za tathmini ya mazingira kwa kuanzisha utaratibu wa kutoa leseni za muda kabla ya kuanza mradi.

(xxviii)              Miradi ya Sekta Binafsi:Sekta hii imeendelea kushiriki katika ujenzi wa viwanda ambapo katika kipindi cha 2015 hadi 2018, jumla ya viwanda 3,530 vilijengwa na kuanza uzalishaji.

B.           MPANGO WA MAENDELEO WA MWAKA 2019/20

13.       Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2019/20 ni wa nne katika mfululizo wa mipango ya kila mwaka ya kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21, wenye dhima ya Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya Watu. Maandalizi ya Mpango huu yamezingatia azma ya kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; na Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

14.       Mheshimiwa Mwenyekiti,Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 yanatekeleza vipaumbele vilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 ambavyo ni:

(i)           Viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda: Miradi itakayotekelezwa katika eneo hili ni ile yenye lengo la kujenga viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini hususan kilimo, madini na gesi asilia. Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia, Uanzishwaji na Uendelezaji wa Kanda Maalamu za Kiuchumi na Kongane za Viwanda, viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, kuongeza thamani ya madini na usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu;

(ii)          Kufungamanisha Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu: Miradi itakayotekelezwa katika eneo hili ni ile yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, elimu na ujuzi, upatikanaji wa chakula na lishe bora na huduma za maji safi na salama. Shughuli zitakazotiliwa mkazo ni pamoja na kugharamia utoaji wa elimu msingi bila ada, kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi, utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu), ujenzi na ukarabati wa vyuo vya ufundi stadi nchini, kuboresha huduma za maji vijijini; 

(iii)       Uboreshaji wa Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji Biashara na Uwekezaji: Miradi itakayotekelezwa katika eneo hili ni ile yenye lengo la kuendeleza ujenzi na ukarabati wa miundombinu (reli, bandari, nishati, viwanja vya ndege, barabara). Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Kufua Umeme wa Maji Rufiji MW 2,115; Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania; Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Standard Gauge; na kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara na Uwekezaji. Aidha, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 umeweka msukumo katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwekeza ikiwemo kupitia upya mfumo wa kitaasisi, kisera na kisheria pamoja na kanuni zake ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo; na

(iv)        Kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa Mpango: Miradi inayotekelezwa katika eneo hili inalenga kuimarisha mifumo na taasisi za utekelezaji wa Mpango, kuweka mfumo utakaowezesha upatikanaji wa uhakika wa rasilimali fedha na kuweka vigezo vya upimaji  wa mafanikio ya utekelezaji.

SEHEMU YA TATU

TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2018/19 NA MAPENDEKEZO YA KIWANGO NA UKOMO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2019/20

A.           TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2018/19

15.       Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2018/19, Serikali ilipanga kukusanya na kutumia  jumla ya shilingi bilioni 32,476.0. Kiasi hicho kinajumuisha: mapato ya ndani shilingi bilioni 20,894.6; misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo shilingi bilioni 2,676.6; na mikopo yenye masharti ya kibiashara kutoka vyanzo vya ndani na nje shilingi bilioni 8,904.7. Aidha, matumizi ya kawaida yalikadiriwa kuwa shilingi bilioni 20,468.7 na matumizi ya maendeleo shilingi bilioni 12,007.3.

16.       Mheshimiwa Mwenyekiti, kipindi cha Julai 2018 hadi Januari 2019, mapato ya kodi yalikuwa shilingi bilioni 9,111.9, mapato yasiyo ya kodi shilingi bilioni 1,522.9 na mapato yaliyokusanywa na Halmashauri yalikuwa shilingi bilioni 371.7.

17.       Mheshimiwa Mwenyekiti,Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji kama ilivyoainishwa ndani ya Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara na Uwekezaji (Blueprint) kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza mapato ya Serikali. Hatua hizo ni pamoja na: Kupunguza kodi kwa wachimbaji wadogo wa madini; Ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo wadogo; Kupunguza kiwango cha ushuru wa bidhaa unaotozwa kwenye pombe kali zinazotengenezwa nchini kwa kutumia zabibu zinazozalishwa nchini; Kuweka utaratibu mpya wa ukusanyaji wa kodi ya majengo; Kuboresha mifumo ya TEHAMA ya kukusanya kodi na maduhuli ikiwemo Electronic Fiscal Device Management System (EFDMS) ambao hupokea na kutunza kumbukumbu za utoaji wa risiti za mauzo.

18.       Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi Januari 2019, Washirika wa Maendeleo walitoa jumla ya shilingi bilioni 1,034.8. Kati ya kiasi kilichotolewa, misaada na mikopo nafuu ya Kibajeti ilikuwa shilingi bilioni 125.4 na miradi ya maendeleo shilingi bilioni 782.0. Mifuko ya Kisekta ilipokea shilingi bilioni 127.4.

19.       Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha Julai 2018 hadi Januari 2019, Serikali ilikopa shilingi bilioni 2,025.0 kutoka soko la ndani. Aidha, katika kipindi hicho, Serikali ilifanya majadiliano na taasisi mbalimbali za kifedha za kimataifa na kupata shilingi bilioni 458.6 kutoka Benki ya Credit Suisse mwezi Februari 2019 na shilingi bilioni 247.7 zinatarajiwa kupatikana kutoka benki ya HSBC hivi karibuni. Vile vile, Serikali ipo katika hatua za mwisho za majadiliano na baadhi ya wakopeshaji walioonesha nia ya kuikopesha Serikali kwa mwaka 2018/19.

20.       Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha Julai 2018 hadi Januari 2019, Serikali ilitoa ridhaa ya matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 13,750.6. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 10,962.1 zilitolewa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na shilingi bilioni 2,788.5 zilitolewa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Mahitaji yaliyopewa kipaumbele katika utoaji wa fedha ni pamoja na: Ulipaji wa deni la Serikali ikijumuisha michango ya mwajiri katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii shilingi bilioni 5,465.9 ambapo Shilingi bilioni 3,803.4 zimetumika kulipa mikopo iliyotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo; na mishahara ya watumishi wa Serikali shilingi bilioni 3,890.0. Serikali imeshatenga na inatarajia kutoa kiasi cha Shilingi bilioni 1,433.8 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo, ukiwemo mradi wa kufua umeme kwa kutumia nguvu ya maji Mto Rufiji (MW 2,115).

21.       Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuongeza mapato na kuimarisha usimamizi wa matumizi ili kufikia malengo ya bajeti ya mwaka 2018/19. Miongoni mwa mikakati hiyo ni: Kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari kupitia vipindi mbalimbali vya elimu kwa umma; Kutekeleza mwongozo wa ushirikiano baina ya Serikali na Washirika wa Maendeleo; Kuendelea kusisitiza nidhamu ya matumizi katika utekelezaji wa bajeti kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015; kulipa  madai yote yaliyohakikiwa ya makandarasi; Kuanza kutumika kwa Mfumo wa Kielektroniki wa Stampu za kodi (ETS) ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi; na Kutekeleza Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Mapato ya Ndani (IDRAS) ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa makusanyo ya kodi za ndani.

B.           SERA ZA MAPATO NA MATUMIZI  KWA MWAKA 2019/20

22.       Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera za mapato kwa mwaka 2019/20 zitalenga: Kuboresha mazingira ya kufanya biashara ili kuvutia uwekezaji, ukuaji wa biashara ndogondogo na za kati pamoja na ukuaji wa uchumi endelevu; Kuboresha mazingira ya ulipaji kodi kwa hiari, upanuzi wa wigo wa kodi na matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika usimamizi wa kodi; Kuimarisha usimamizi wa sheria za kodi ili kutatua changamoto za ukwepaji kodi na kupunguza upotevu wa mapato; Kuwianisha na kupunguza tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na Wakala za Serikali na Mamlaka za Udhibiti; na Kuwajengea uwezo maafisa wa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala na Halmashauri ili kuimarisha uwezo wa ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi.

23.       Mheshimiwa Mwenyekiti,uboreshaji wa mazingira haya utawezesha kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa uwekezaji, uzalishaji, ajira na miamala ya biashara ambayo kwa ujumla itachangia kuongezeka kwa vyanzo vya mapato. Aidha, kwa upande wa misaada na mikopo nafuu, Serikali itaendelea kuimarisha mahusiano kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Ushirikiano na Washirika wa Maendeleo.

24.       Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2019/20, Serikali itaendelea kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti, SURA 439. Lengo kuu ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za umma na kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye miradi mikubwa ya miundombinu na miradi mingine muhimu. Aidha, Serikali itaendelea kugharamia matumizi ya maendeleo yenye vyanzo mahsusi kwa ajili ya uwekezaji katika maeneo maalum yenye maslahi mapana kwa Taifa kama vile Mfuko wa Barabara, Mfuko wa Reli, Mfuko wa Nishati Vijijini na Mfuko wa Maji. Vile vile, Serikali itaendelea kuhakiki, kulipa na kuzuia ongezeko la madeni ya Serikali.

C.           Kiwango na Ukomo wa Bajeti kwa Mwaka 2019/20

25.       Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa kuzingatia sera za bajeti kwa mwaka 2019/20, Sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla ya Shilingi bilioni 33,105.4 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika ambapo mapato ya ndani, yakijumuisha mapato ya halmashauri, yanatarajiwa kuwa Shilingi bilioni 23,045.3. Mikopo ya ndani inakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 4,960.0, mikopo ya nje yenye masharti ya kibiashara shilingi bilioni 2,316.4 na misaada na mikopo yenye masharti nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo Shilingi bilioni 2,783.7.

26.       Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2019/20 Serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 33,105.4 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 20,856.8 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida; matumizi haya yanajumuisha gharama za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020. Matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa shilingi bilioni 12,248.6, ambapo shilingi bilioni 9,737.7 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 2,510.9 ni fedha za nje.

27.       Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia maelezo hayo, kiwango na ukomo wa  bajeti kwa mwaka 2019/20 ni kama ilivyo katika Jedwali lifuatalo:

 ........
HITIMISHO

28.       Mheshimiwa Mwenyekiti,Mpango na Bajeti ya mwaka 2019/20 unazingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini na uongozi thabiti wa Mheshimwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya kujenga uchumi wa viwanda na  kuboresha ustawi wa jamii. Aidha, Serikali itaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kudhibiti mianya ya ukwepaji wa kodi. Vile vile, Serikali  itaendelea kuweka mkazo katika usimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha za umma ili zitumike katika uwekezaji wa miundombinu ya umma na uboreshaji wa huduma za kijamii kwa lengo la kuleta maendeleo ya haraka. Hivyo, napenda kuwahimiza Watanzania tuwajibike kulipa kodi na kuhakikisha tunatoa na kudai risiti  kulingana na muamala uliofanyika.

29.       Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendeleza mapambano dhidi ya rushwa, kuimarisha ulinzi wa rasilimali za umma na kudhibiti matumizi ya fedha za umma. Serikali pia itaongeza msukumo katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara na Uwekezaji. Mpango huu, pamoja na mambo mengine, unakusudia kuhuisha na kurahisisha taratibu za kulipa kodi, tozo na ada mbalimbali.

30.       Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuwasilisha.

Polisi, 'CUF Lipumba' waendelea Kuvutana

$
0
0
Mkutano Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, umesimama baada ya kutokea kutoelewana baina ya viongozi wa chama hicho na Jeshi la Polisi.

Kwa mara ya pili jeshi la polisi limefika katika ukumbi wa Lekam unakofanyika mkutano huo na kuwazuia kuendelea likisisitiza kuna zuio la mahakama.

Difenda mbili zikiwa na askari polisi na gari moja ya maji ya kuwasha zilifika kisha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Buguruni (OCD), Adam Maro, alionekana akizungumza na viongozi wa chama hicho.

“Hata kama umekuja na zuio la mahakama sisi hatulipokei kwa sababu wewe huna mamlaka ya kulileta na hapa hatuondoki mkitaka mtuue wote,” alisikika mmoja wa viongozi wa Cuf akimweleza OCD huyo.

Baada ya muda OCD huyo alitoka nje ya geti kisha alirudi tena akiwa ameongozana na askari wengine na kuingia ndani ukumbini.

Hata hivyo baada ya kuingia tu wafuasi wa Cuf walimtoa nje na kusababisha wajumbe wengine waliokuwa ndani kutoka.

Muda mfupi baadaye Profesa Lipumba alitoka ukumbini na kwenda kuzungumza na polisi hao kisha alionekana akiongea na simu huku akirudi ndani..


Baada simu hiyo, magari ya polisi yaliondoka eneo la mkutano. 

Alipoulizwa kuhusu simu aliyokuwa akipiga Profesa Lipumba amesema: "Niliongea na jamaa ninaowafahamu. Mimi ni mtu mzito siwezi kukwambia nimeongea na nani. Wewe unapopiga simu nakuuliza yakhe uliongea na nani?

Viwanja Vikubwa Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab Sec)

$
0
0
Viwanja Vikubwa Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab Sec)
Viwanja vipo mtaa wa Kimele, Kata Mapinga, km 2 tu kutoka Shule ya secondary Baobab (main road ya Dar to Bagamoyo).
Viwanja vimepangwa vizuri, vina miundombinu ya maji na umeme. 


Viwanja viko vya size na bei tofauti kuanzia mita 20/25 kwa bei ya tsh 6 milion, mita 20/30 kwa bei ya tsh 8 milion, mita 20/40 kwa bei ya tsh 10 milion, mita 30/50 kwa bei ya tsh 18 milion, mita 40/50 kwa bei ya tsh 24 milion, mita 40/60 kwa bei ya tsh 30 milion,

Pia ipo nyumba pagala (haijapauliwa) na ina vyumba 3, kimoja master, sebure, dining, public toilet, kitchen etc na bei yake ni tsh 23,000 (kiwanja chake ni sqm 400 au 20/20 mita)

Na pia, kwa Bunju sokoni, kipo kiwanja cha sqm 1800 kinauzwa tsh 54 milion.

Luksa kulipa kwa awamu (anza na 75%, maliza na 25%)
Ukipata ujumbe huu mjulishe ndugu/jamaa/rafiki yako.
Biashara hii haina dalali, mpigie mhusika: 0758603077, whatsap 0757489709

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 13

Naibu Waziri Aagiza Wafungwa Watumike Ujenzi wa Chuo cha Polisi Kurasini

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ameliekeza Jeshi la Polisi Tanzania kuwatumia wafungwa katika shughuli za ujenzi wa chuo cha polisi ili kupunguza gharama.

Masauni ametoa agizo hilo jana Jumanne Machi 12, 2019 alipotembelea majengo chakavu ya Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa kutengenezwa mabweni na vyumba vya madarasa.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imeeleza kuwa Masauni amekwenda chuoni hapo kuangalia hatua za awali kabla ya kuanza kwa ujenzi huo na kupata mchanganuo wa kiasi cha Sh700 milioni zilizotolewa na Rais John Magufuli zitakavyotumika.

Kiasi hicho cha fedha kilichotolewa kwa polisi Machi 7, 2019 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Magufuli aliyoitoa mwishoni mwa mwaka jana wakati wa mahafali ya kuhitimisha Mafunzo ya Kozi za Uofisa na Ukaguzi Msaidizi.

Masauni ameelekeza wafungwa wakitumika upo uwezekano wa kuokoa kiasi cha Sh200 milioni fedha ambazo zinaweza kutumika kwa matumizi mengine.

“Wizara ina taasisi ya magereza ambayo ina nguvu kazi ya kutosha, na Rais alishaagiza wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji, sioni sababu ya kutumia kiasi hicho cha pesa kuwalipa vibarua wa nje,” amesema. 

“Naagiza muwasiliane na Jeshi la Magereza na kikosi cha ufundi kilichopo ndani ya Jeshi la Polisi ili muweze kuona ni vipi mnaokoa kiasi hicho,” amesema Masauni.

Waziri wa Kilimo Asisitiza Kuwepo Matokeo Chanya Katika Utekelezaji Wa Mradi Wa SUMUKUVU (TAIPAC)

$
0
0
Na Mathias canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Watekelezaji wote wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania- (Tanzania Initiatives for Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC) wametakiwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na matokeo chanya katika jamii katika utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha kuwa umasikini unapungua (Poverty reduction), na kujikita kutazama utekelezaji wa matokeo ya kama yatalingana na thamani ya fedha itakayotumika (Value for Money).

Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo Tarehe 12 machi, 2019 wakati akizindua mradi wa kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), katika ukumbi wa Kambarage uliopo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango (HAZINA) Jijini Dodoma.

Alisema kuwa, Mwezi Juni, 2018 Serikali ilizindua Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili au kwa kifupi ASDP II.  Programu ya ASDP II inalenga kuongeza tija katika uzalishaji, kukifanya kilimo kiwe cha biashara na kuongeza pato la mkulima ili kuboresha maisha, uhakika wa chakula pamoja na lishe.  Program hii inatekelezwa kikamilifu kupitia miradi mbalimbali ili kufikia malengo iliyojiwekea.

Mradi wa TANIPAC unatekelezwa chini ya vipengele (Component) Na. 2 na 3 ambavyo vinalenga kuongeza tija katika uzalishaji na kuongeza thamani ya mazao.  Thamani ya mazao ni pamoja na chakula salama ambacho kinaenda kuuzwa kwa walaji ndani na nje ya nchi.  Na kwa kuwa ASDP II inalenga kukifanya Kilimo kuwa cha kibiashara, ni dhahiri mazao yanayotakiwa kuuzwa ni yale yaliyo salama.

Alisema, utekelezaji wa mradi huo utasaidia katika kutimiza malengo ya ASDP II ambayo yana Kaulimbiu inayosema: Chakula ni Uhai. Tafsiri ya Kaulimbiu hii ni: - chakula salama ni msingi wa maisha, hivyo hapana budi kuimarisha mfumo wa uzalishaji wa chakula salama.

Waziri Hasunga alisema kuwa Suala la kuimarisha  biashara na masoko pamoja na uhakika wa chakula na lishe pia ni vipaumbele muhimu katika utekelezaji wa mpango wa uwekezaji na usalama wa chakula katika sekta ya Kilimo (Tanzania Agricultural and Food Security Investment Plan -TAFSIP) na Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Bara la Afrika (Comprehensive African Agriculture Development Program – CAADP) kama ilivyoelekezwa kwenye Azimio la Malabo.

Kadhalika, suala la usalama wa chakula ni hitaji la lazima katika kufikia Malengo Endelevu ya Dunia (Sustainable Development Goals, SDGs), hususani Lengo Na.2.1, 3.2 na 2.3 ambayo kwa ujumla yamelenga kukomesha njaa, kuhakikisha kuwa kuna usalama wa chakula na lishe, kilimo endelevu, kuimarisha afya na siha za watu nakupunguza upotevu wa chakula kwa kiwango cha asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

“Ili tuweze kuelewana vizuri nataka tutofautishe dhana ya usalama wa chakula (food security) na chakula salama (food safety).  Mradi tunaozindua leo ni wa kuhakikisha chakula tunachozalisha, tunachouza na tunachokula ni salama kwa maana ya kutokuwa na sumu inayoweza kuathiri afya za watumiaji.  Usalama wa chakula ni hali ya kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha na chenye viini lishe vya kutosha katika ngazi ya kaya na Taifa” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

“Ni muhimu tukafahamu kuwa, suala la chakula salama (food safety) ni tatizo Duniani kote na huathiri mataifa yote, hasa yale yanayoendelea kama Tanzania na nchi nyingine za dunia ya tatu. Hii inatokana na kutokuwa na mifumo imara ya usimamizi katika nyanja za uzalishaji wa chakula, uhifadhi na ugavi”

Mhe Hasunga alieleza kuwa Changamoto hiyo ya chakula salama inachangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha afya za Walaji, wakati mwingine vifo na athari nyingine nyingi zikiwemo za kiuchumi.

Tatizo la sumukuvu si geni katika Ukanda wa Afrika Mashariki Kwa mfano, tatizo hilo limekuwa likijitokeza mara kadhaa katika nchi ya Kenya ambapo mwaka 2004 watu zaidi ya 300 walipata ugonjwa wa Aflatoxicosis utokanao na sumukuvu na kusababisha vifo vya Watu 125 baada ya kula chakula kilichokuwa na kiwango kikubwa cha sumukuvu.

Tatizo kama hilo liliwahi kutokea nchini mwaka 2016 ambapo zaidi ya watu 60 katika Halmashauri za Bahi, Chemba, Kiteto na Kondoa waliugua baada ya kula chakula chenye kiwango kikubwa cha sumukuvu na watu 19 kufariki kwa tatizo hilo.

Mradi wa TANIPAC ambao umezinduliwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga unalengo la kupunguza sumukuvu (aflatoxin) katika mazao ya mahindi na karanga.

Aidha, Taarifa zinaonesha kuwa tatizo la Sumukuvu ni kubwa kwani inakadiriwa kuwa asilimia 25 ya mazao yote yanayozalishwa duniani yanaathiriwa na Sumukuvu.

Tafiti za kiafya zinabainisha kwamba, sumukuvu huchangia zaidi ya aina 25 za saratani na kipekee inachangia asilimia 30 ya saratani ya ini.  Pamoja na kuchangia saratani, kuna ushahidi wa kisayansi unaoonesha kwamba sumu hiyo huchangia udumavu kwa watoto ambapo  yanaathiri ukuaji wa mtoto kimaumbile pamoja na kuchangia kudumaa kwa akili.  Vilevile, tatizo la sumukuvu huathiri biashara ya mazao ya chakula katika soko la Kimataifa ambapo kwa Bara la Afrika linapoteza zaidi ya Dola za Marekani Milioni 670 ambayo ni sawa na asilimia 40 ya mauzo yote ya nje yanayokataliwa kila mwaka.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images