Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Viongozi Wawili CHADEMA Wavuliwa Uanachama .....Wanne Wapewa Onyo

0
0
Na Amiri kilagalila Njombe
Chama cha Demokrasia na maendeleo chadema jimbo la Njombe mjini kimewavua uanachama na kuwafutia haki zao ndani ya chama hicho viongozi na wanachama wawili huku wanne wakipewa onyo.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Njombe katibu wa chadema jimbo ambaye pia ni diwani wa kata ya Ramadhani GEORGE MENSON SANGA amesema kuwa chama kimefikia uamuzi huo kutokana na ukiukwaji  wa katiba na miongozo ya chama.

Amesema mnamo march 8 2018 kamati ya jimbo la Njombe mjini ilikutana kwa minajili ya kujadili shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupokea na kujadili taarifa za kiutendaji za wenyeviti wa serikali za mitaa na madiwani ndani ya halmashauri ya mji wa Njombe na kufikia uamuzi huo.

“Kataika hatua moja chama kimetoa onyo kwa wenyeviti wanne (4) ambao hatutawataja kutokana na kukiri kwao na kuahidi kuongeza ufanisi katika kuwatumikia wananchi”alisema George Sanga

Katika hatua nyingine alisema  chama kinamsimamisha uanachama mwanachama JOSEPHINE MABENA wa tawi la Itulike shuleni kata ya Ramadhani amabye pia alikuwa ni mjumbe wa serikali ya mtaa huo.

“Ndugu waandishi wa habari,huyu alikuwa mjumbe wa serikali ya mtaa huo  kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014 na chama kimefikia uamuzi huu kutokana na mwanachama huyo kupoteza sifa za uanachama kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kama mwanachama na kiongozi anayetokana na CHADEMA” alisema katibu wa jimbo

Ameongeza kuwa uamuzi wa kumvua uanachama ndugu ERICK J MSIGWA aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Melinze kata ya mji mwema kutokana na kuhusika kwake katika tuhuma mbali mbali zinazomkabili.

“Chama kimeamua kumfuta uanachama pamoja na haki zake zote mwanachama Erick Msigwa ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa melinze jimbo la Njombe mjini baada ya kujiridhisha pasipo mashaka kuhusika kwake katika tuhuma mbali mbali zilizokuwa zikimkabili  ikiwa ni pamoja na  kukaidi maelekezo ya chama kama ulivyo wajibu wake katika katiba ya chama na sheria ya serikali za mitaa pia na mwenendo mbovu wa kimaadili kama mtumishi wa wananchi”alisema Sanga

Hata hivyo Sanga amesema chama kinatambua kuwa wanachama hao walikuwa na nafasi katika uongozi wa uwakilishi wa wananchi lakini kwa kukosa kwao sifa ya kuwa wanachama tayari chama kimevikumbusha vyombo vinavyohusika kutimiza wajibu wake kwa hatua za ziada ikiwa ni pamoja na kutangaza nafasi wazi ya uenyekiti katika mtaa wa Melinze.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa chama na kwamba maoni yao juu ya utendaji kazi wa viongozi waliowachagua wayawasilishe bila hofu yoyote na chama hicho kitaendelea kutimiza wajibu wake kwa kuchukua hatua za kinidhamu inapothibitika ukweli katika tuhuma.

Serikali Yahakikisha Vyanzo Vya Maji Vinalindwa Kufanikisha Mradi Wa Rufiji Hydro Power Project

0
0
Na Lulu Mussa, Morogoro
Serikali imesema itahakikisha kuwa vyanzo vya maji vinavyopeleka maji Mto Rufiji havivamiwi kwa shughuli za kilimo na kibinadamu ili Mradi Mkubwa wa kufua umeme katika bonde la Mto Rufiji uweze kutekelezeka. 
 
Hayo yamesemwa  mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima mara baada ya kukamilisha ziara yake katika Mikoa sita hapa nchini kwa lengo la kukagua maeneo yenye changamoto za kimazingira pamoja na kutafuta ufumbuzi kwenye ikolojia ya vyanzo vya maji vinavyo changia maji katika bonde la Rufiji.

Akiwa katika eneo la mradi litakapojengwa bwawa la kufua umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji Naibu Waziri Sima amesema amefanya ziara ya kukagua vyanzo vya maji vya Bonde la Rufiji ambavyo vinahusisha matawi matatu ya mito ambayo ni Mto Ruaha Mkuu, Kilombero, Luegu, na kutoa wito kwa wananchi kutoharibu vyanzo hivyo ili kuwa na maji ya kutosha kutekeleza mradi huo mkubwa.

“Ziara yangu imeanzia Lindi, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Iringa na Kilombero kote huko nimelenga kujione vyanzo hivi vikuu. Mito hii ya Ruaha Mkuu, Kilombero na Luegu inapoungana ndio inatengeneza Mto Rufiji ambako ndiko kuna maporomoko ya “Stiglers Gorge”. Na nimeridhishwa na hatua za watendaji katika ngazi zote za Serikali kwa kuwa mstari wa mbele kukahikisha kuwa vyanzo vya maji vinalindwa na kuhifadhiwa.” Sima alisisitiza.

Katika ziara yake Naibu Waziri Sima ameweza kutoa miongozo muhimu yenye kukuza, kulinda na kusimamia mazingira kwa namna endelevu husunan Ikolojia ya Vyanzo vya maji katika Mikoa aliyopita. Naibu Waziri Sima amesema Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa kufua umeme wa Maji wa Rufiji Hydro Power Project ambapo zaidi ya MW 2100 za umeme zitazalishwa, hivyo kulingana na ukubwa wa mradi huu ni wazi uhifadhi wa Mazingira katika vyanzo hivyo ni muhimu ukatiliwa mkazo.

“Uhifadhi wa Mazingira katika Bonde la Rufiji ni wafaida kwa pande zote hasa ustawi wa wananchi. Wananchi ndio walinzi na wahifadhi wa kwanza katika kutunza Mazingira, aidha Sheria ya Mazingira, 2004 kifungu cha 6 kimetamka wajibu wa kila mwananchi kutunza Mazingira kwamba; Mtu yeyote anayeishi Tanzania atakuwa mdau na atawajibika kutunza na kuendeleza Mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu shughuli au jambo lolote ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kuathiri mazingira. Hivyo kupitia sheria hii si jukumu la Serikali pekee kusimamia uhifadhi wa Mazingira, wananchi nao wana wajibu wa moja kwa moja wa  kutunza Mazingira”. Sima alisisitiza.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini Dkt. Samuel Gwamaka alieambatana na Naibu Waziri Sima katika ziara hiyo amesema kuwa Baraza limedhamiria kufungua Ofisi katika eneo hilo la mradi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya kila siku za Baraza.
 
Bonde la Rufiji lina ukubwa wa KM2 177,420 ambazo ni sawa na  asilimia 20 ya Tanzania na linapita katika mikoa 11 ya Tanzania na Wilaya 32 za Tanzania, Bonde hili ni Mashuhuri kwa Kilimo, ufungaji, uvuvi na uzalishaji wa umeme katika vituo vya Mtera na Kihansi.

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Lazima Inunue Mazao Ya Kutosha Kwa Wakulima

0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umetakiwa kununua mahindi mengi kwa wakulima kwani kufanya hivyo kutaongeza wigo wa masoko kwa wakulima wa mazao mbalimbali ya nafaka nchini.

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Wasa vilevile katika kijiji cha Ibebwa kilichopo katika kata ya Msia akiwa katika ziara jimboni humo kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye miradi ya maendeleo.

Mhe Hasunga alisema kuwa NFRA inapaswa kubadili dhana ya kununua mahindi kwa ajili ya hifadhi pekee badala yake wanapaswa kununua mahindi kwa ajili ya kuyauza ili kuongeza ufanisi wa soko kwa wakulima nchini.

Katika hatua nyingine alisema kuwa tayari NFRA imeanza kutekeleza maelekezo ya serikali kwa kununua na kuuza mahindi kupitia mkataba na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) utakaopelekea kurejea sokoni kununua mahindi kwa wakulima.

Alisema NFRA pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko zinapaswa kutekeleza wajibu wake katika ufanyaji biashara ya mazao.

Pamoja na mambo mengine Mhe Hasunga ameshiriki shughuli za Maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Sekondari Msia sambamba na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, nyumba moja ya mwalimu na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Masangula iliyopo katika kata ya Nyimbili.

Vilevile akiwa katika ibada maalumu kwenye kanisa la FPCT Ilolo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha kuwa vikundi mbalimbali vya ufugaji nyuki vinasajiliwa.

Aidha, alichangia jumla ya Shilingi 1,000,000 kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za ufugaji nyuki katika vikundi vya ufugaji nyuki kwenye kanisa la FPCT Ilolo sambamba na kuchangia kwaya kwa ajili ya kuendelea kuhubiri injili.

Aliongeza kuwa watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii huku akisisitiza kuishi katika matendo mema na kutobaguana katika shughuli za Maendeleo.

Kuhusu changamoto za upungufu wa walimu katika shule mbalimbali Waziri Hasunga alisema kuwa serikali imejipanga kutatua changamoto hizo na kwa kuanza tayari imetoa kibali cha kuajiri waalimu zaidi ya 4000 huku juhudi zingine ikiwa ni pamoja na kuwahamisha walimu kwenye shule ambazo zina walimu wa ziada.

Akiwa katika kata ya Nyimbili Mhe Hasunga amechangia Shilingi 1,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa barabara korofi ya kijiji cha Nyanyi

Naibu Waziri Maliasili Asisitiza Mahusiano Mema Kati Ya Wananchi Na Askari Wa Wanyamapori

0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amewataka  wananchi kuwachukulia askari wa Wanyamapori na Misitu  kama rafiki wa umma na watendaji waliotumwa na Serikali kulinda rasilimali hizo kwa niaba yao.

Akifunga kikao cha 26 cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Mwanza, Mhe. Kanyasu amesema Askari hao waliopewa dhamana ya kulinda maeneo ya  hifadhi nchini  wanafanya kazi nzuri ya kuifanya Tanzania iendelee kuwa na maeneo mazuri yaliyohifadhiwa.

Amesema Askari hao wameajiriwa kwa mujibu wa sheria hivyo hutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi zao na pale wanapokiuka sheria mamlaka zinazohusika huwachukulia hatua.

“Sisi kama Wizara tunaamini kwamba askari wetu na wahifadhi wetu wanafanya kazi nzuri, pale ambapo wamekuwa wakilaumiwa kwa kuwapiga na kuwanyanyasa watu kwa namna yoyote ile tumetuma Tume maalum kuchunguza na kuchukua hatua” Amesema

Mhe, Kanyasu amesema uchunguzi  unapofanyika na ikathibitika kuwa tukio lililofanyika halikuongozwa na matumizi ya sheria na kuwepo kwa haki wizara imekua ikichukua hatua.

Ameeeleza kuwa askari wanaolinda Hifadhi nchini wanategemewa na bila wao hakuna uhifadhi unaoweza kuendelea nchini akibainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipinga juhudi za uhifadhi kwa kuwatetea watu wanaovunja sheria.

“Watu hawafahamu tu, tukiwaondoa askari wetu wote katika maeneo ya hifadhi na tukawaondoa  Maafisa ukaguzi wa mazao ya Misitu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) barabarani, katika kipindi cha miezi 6 nchi hii itageuka kuwa jangwa”  Amesisitiza Mhe. Kanyasu.

Amesema yapo madhara makubwa yanayoweza kutokea kama hakutakuwa na uhifadhi imara ikiwemo maeneo mengi ya nchi kugeuka kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa misitu, ukosefu wa mvua, ukosefu wa maji, chakula na ukosefu wa hewa safi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa kumekuwa na tuhuma za vitendo vya ukatili dhidi ya raia vinavyofanywa na baadhi ya askari wa Hifadhi nchini na kutoa wito kwa wananchi wote wenye ushahidi na taarifa juu ya vitendo hivyo kuziwasilisha ili hatua stahiki zichukuliwe.

Amesisitiza kuwa Serikali hairuhusu askari kufanya vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya raia badala yake imekua ikiwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali zinazowazunguka.

Amewatahadharisha na kuwataka wananchi wawe makini dhidi ya kampeni zenye nia ovu zinazoendeshwa na baadhi ya watu zenye lengo la kuwavunja moyo askari wanaojitolea maisha yao kulinda rasilimali za taifa akieleza kuwa wapo askari waliopata madhara makubwa na kupoteza maisha kwa kushambuliwa na majangili kwa kuchomwa mishale yenye sumu na kukatwa vidole wakati wakitimiza wajibu wao.

Prof. Mkenda amesema kuwa wizara itaendelea kulinda hadhi ya vijana hao waliojitolea maisha yao kulinda rasilimali za Taifa akibainisha kuwa Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watakaokiuka kanuni na taratibu za kazi kazi ili iwe fundisho kwa wengine.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo amesema kuwa watumishi 23 wa wanyamapori na misitu wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa katika matukio tofauti yaliyotokea wakati wakipambana na majangili.

Amesema matukio hayo yametokea mwaka 2018/2019 na hifadhi inayoongoza kwa matukio hayo ni Sengereti,  Prof. Mkenda amesema kuwa watumishi hao waliofariki na wengine kujeruhiwa walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi hivyo Wizara inaangalia namna ya kuwaenzi kutokana na mchango wao.

Ndege ya Ethiopia yapata ajali ikielekea Nairobi....Watu 157 Wahofiwa Kufariki

0
0
Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi.

Taarifa ya Shirika la ndege la Ethiopia- Ethiopian Airlines inasema walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adi Ababa.

Takriban wasafiri 149 na wahudumu 8 wanahofiwa kufariki dunia.

Kampuni hiyo inasema imeanzisha kituo cha kupata taarifa kuhusu familia na marafiki za watu waliliokuwemo ndani ya ndege hiyo.

Waziri mkuu wa Ethiopia ameandika katika ukurasa wake wa Twitta leo Jumapili,10.03.2019 ujumbe wa kutoa pole kwa familia za waliofiwa kufuatia ajali hiyo mbaya.Ingawa pia ujumbe huo haukutoa maelezo zaidi.Ujumbe umesema-

''Ofisi ya waziri mkuu kwa niaba ya serikali na wananchi wa Ethiopia tungependa kutowa pole zetu kwa familia zilizopoiteza wapendwa wao waliokuwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikielekea Nairobi Kenya asubuhi ya leo''

RC Mnyeti Ampa Onyo Mbunge CCM

0
0
Mbunge wa Babati Vijijini, Vrajlal Jituson amejikuta akikemewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na kuambiwa kuwa atachukuliwa hatua kwa kile alichodaiwa kuwa anahamasisha vitendo vya uvunjifu wa sheria.

Vrajlal Jituson amejikuta kwenye hali hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliyomuhisisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti na baadhi ya wafugaji kwa ajili ya kutatua mgogoro wa ukamatwaji wa ng'ombe wa baadhi ya wafugaji hao.

Akizungumza kwenye mkutano, Mnyeti amesema kuwa, “nataka nikwambie mbunge kwamba nakuheshimu sana, sitaki uendelee kuchochea migogoro, na mimi mtu akivunja sheria simkamati aliyevunja, namkamata aliyemtuma kuvunja, sitaki mtu aje kunipapasa sharubu,”

“Anakuja mwanasiasa kwa njaa ya kura za mwakani anadanganya watu halafu wakipigana na kuuana anakimbilia Dodoma hilo sitalikubali litokee Manyara,” ameongeza Mnyeti.

Hata hivyo, Jituson alikanusha madai hayo ya uchochezi na kueleza kuwa hakuwahi kufanya hivyo.

Alisema migogoro ya ardhi katika jimbo la Babati Vijijini ilikuwapo miaka mingi hata kabla hajawa mbunge na eneo hilo lina mgogoro wa zaidi ya miaka 10.

Vanessa Mdee Apangua Tuhuma za Kutohudhuria Misibani

0
0
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Mdee, amejibu tuhuma za kutoonekana misibani hivi karibuni, baada ya kudai kuwa amechoshwa na tuhuma hizo zisiszo na msingi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vanessa amejibu tuhuma hizo na kudai kuwa amekuwa akihudhuria lakini kimya kimya kwani misiba na mazishi ni ibada na hakuna umuhimu kujionesha.

“Niliona nipotezee lakini naomba niseme once and for all. Misiba na mazishi ni kama ibada, ukishiriki sio habari ya kutangaza kama tamasha. Nimeona watu wanataka kunishikilia bango kama mtu asiyehudhuria au asiyeshiriki katika ibada hizi. 

"Kama unataka kufaham nilikuwepo katika misiba yote ya hivi karibuni lakini sikupenda kutangaza uwepo wangu kutokana na kupitia misiba mizito katika maisha yangu kama watu wengine wengi. 

"Siku ya kesho itakuwa miaka 12 tangu nimpoteze baba yangu mzazi na mwaka huu ni miaka miwili tangu nimpoteze Dada yangu ( mtoto wa kwanza wa baba) i bet you didn’t even know, why? Because I prefer to silently pray for the family and loved ones, I’ve found that only God can bring some relief in these situations. “ameeleza Vanessa Mdee na kufafanua.

“Mtu akifiwa anapitia mambo mengi na anahitaji faraja. Nadhani nimeeleweka. Asanteni na Mungu awatunze wote na familia zenu.“

Itakumbukwa kuwa Tanzania imekumbwa na misiba ya watu maarufu kwenye tasnia ya habari na burudani kwa wiki tatu mfululizo ikiwemo msiba wa Rapper Godzilla, Mtangazaji wa clouds FM, Ephraem Kibonde na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya March 11


Waziri Lugola Aagiza Polisi Kuwakamata Wapinzani Wanaomtukana Rais Kupitia Mikutano Ya Ndani...... Asisitiza Mikutano Ya Siasa Ya Hadhara Marufuku

0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewaagiza Makamanda wa Polisi nchini washirikiane na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuchunguza na kuwakamata wapinzani wanaomtukana Rais pamoja na Serikali kwa ujumla kupitia vikao vyao vya ndani vya siasa.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mjini Kilosa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kilosa Town, Wilayani humo, juzi, Lugola amesema ana taarifa kuna baadhi ya wapinzani ambao wanafanya vikao vyao vya ndani huku wakitukana, kubeza pamoja na kuwachonganisha wananchi na Serikali yao ambayo inaongozwa na Rais Dkt John Magufuli.

Kutokana na wapinzani hao kuvunja agizo lililowekwa, amewaagiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wilaya nchini kuwachunguza viongozi wa siasa kwa kina kupitia vikao vyao, na watakaowabaini wanavunja utaraibu huo wawakamate haraka iwezekanavyo.

Lugola ameendelea kusisitiza kwa kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano ya siasa ya hadhara mpaka hapo kampeni zitakapoanza rasmi kwa uchaguzi ujao.

“Mimi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sitakubaliana na kiongozi wa chama chochote kuvunja agizo tulilolitoa nchi nzima kwa kutokuruhusu kufanyika mikutano ya hadhara ya siasa, na pia kupitia mikutano ya ndani ambayo inafanyika, ambapo baadhi ya wanasiasa wahuni wanamtukana Mheshimiwa Rais ambaye ndio kiongozi mkuu wa nchi, mimi sitakubaliana na hilo,” alisema Lugola.

Lugola amewataka wapinzani kuwa wasikivu kwa kufuata sheria za nchi na pia kutambua kuwa, Rais wa nchi hii ambaye kipenzi cha wananchi anapewa heshima yake kwa kuiletea maendeleo nchi.

Lugola alisema Rais Magufuli ni kiongozi ambaye kwa muda mfupi ameiletea mabadiliko makubwa nchi, na pia mipango mikubwa ya maendeleo inakuja katika uongozi wake.



Lugola alifanya mikutano miwili ya hadhara wilayani Kilosa, ambapo mkutano mmoja ulifanyika mjini Kilosa na mwingine ulifanyika Tarafa ya Kimamba wilayani humo, ambapo alizungumza na wananchi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi wilayani humo kupitia kutoa nafasi kwa wananchi kutoa kero zao.

Aidha, Lugola aliwataka polisi nchini kuwa makini kwa kutenda haki wakati wanaletewa kesi za ardhi zenye jinai hasa katika Mkoa wa Morogoro ambao unakabiliwa na migogoro ya aina hiyo.

“Nimepata malalamiko ya baadhi ya polisi hapa Kilosa kutokutenda haki katika ukamataji wa watuhumiwa, polisi amepewa taarifa ya mtuhumiwa lakini hamkamati, sasa polisi ambaye ametajwa hapa mkutanoni hakumkamata mtuhumiwa huku uthibitisho ukionyesha kabisa mtuhumiwa amekosa na anapaswa kuwepo kituoni, naagiza polisi huyo akamatwe awekwe mahabusu,” alisema Lugola.

Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa za wahamiaji haramu katika mkoa huo ili Uhamiaji iweze kuwakamata na kuwafungulia kesi wahamiaji hao kutokana mataifa mbalimbali wanaoingia nchini bila kufuata taratibu za nchi.

“Wakazi wa Kilosa, endeleeni kuchapa kazi, moto wa Magufuli mnauona, sasa hakuna uonevu, hakuna kauli ‘unanijua mimi nani’, nchi imetulia, maendeleo ya kasi mnayaona, huyu Magufuli hakika ameletwa na Mungu,” alisema Lugola.

Lugola amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani humo akitembelea Wilaya za Morogoro, Mvomero na Kilosa, akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.

Lugola mwaka jana mara alipoteuliwa kuiongoza Wizara hiyo, alitoa maagizo mbalimbali kwa Makamanda wa Polisi Mikoa nchini ambayo ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe.

Makamu Wa Rais Anaondoka Nchini Leo Kuhudhuria Mkutano Wa Africa Now Summit 2019 Utakaofanyika Kampala - Uganda

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kuelekea Kampala, Uganda kushiriki kwenye Mkutano wa mwaka 2019 wa ‘Africa Now Summit’unaotarajiwa kufanyika tarehe12 na 13 Machi.Mhe. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huu. Mkutano utakuwa na mada mbalimbali ikiwemo ya Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika, mada hii itatolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA) Mhe. Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto; na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Ahmed Abiy. Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya Uongozi katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika.

Mkutano utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Makamu wa Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.

Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
11/03/2019

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Akemea Waajiri Sekta Binafsi Wanaofukuza Kazi Wanawake Pindi Wapatapo Mimba

0
0
Serikali imeagiza taarifa za waajiri wote hasa sekta binafsi waliowafukuza wanawake kazi au kuwashusha vyeo kwa sababu ya kupata ujauzito wakiwa kazini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alitoa agizo hilo jijini hapa wakati akizungumza na wanawake na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Aliitaka jamii katika maeneo ya kazi kuondokana na rushwa za ngono jambo alilosema ni tatizo katika upatikanaji wa haki za wanawake.

Kadhalika aliwataka waajiri wa sekta binafsi kuzingatia utu na haki za wanawake wafanyakazi.

"Mwanamke kupata mimba ni haki yake ya asili kutokana na uumbaji wa Mungu hivyo ni marufuku kuwafukuza kazi wanawake wafanyakazi hasa sekta binafsi kisa kuwa na ujauzito," alionya.

Aliongeza kuwa suala la usawa wa kijinsia ni muhimu kwa wanaume kushiriki kwa kuwa wao pia ni wahusika wakuu wa kuwapo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Waziri Ummy alisema kama waziri mwenye dhamana ya masuala ya wanawake atahakikisha wanawake wanapata fursa sawa katika masuala muhimu kwa manufaa ya haki na ustawi wao.

Aliagiza kutekelezwa kwa haki ya mwanamke kunyonyesha baada ya kumaliza likizo zao za uzazi, kwa kuwa ni jambo muhimu kwa mtoto kupata maziwa ya mama katika ukuaji wake kwenye umri wa miezi ya awali.

Waziri Ummy alikemea vitendo vya rushwa ya ngono na kuipongeza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kwa kuliona suala hilo kuwa moja kati ya vitendo vya kikatili afanyiwavyo mwanamke na kumnyima haki yake.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Philis Nyimbi, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, alisema mkoa unatekeleza mikakati mbalimbali katika kumwezesha mwanamke na mtoto wa kike kwa kumuweka mbali na vitendo vya ukatili dhidi yao ili kuwawezesha kupata fursa zitakazowezesha kufikia usawa wa kijinsia.

Naye Mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, alisema kuwa Umoja wa Mataifa unataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kunakuwapo na usawa wa kijinsia na kuondoa vikwazo vyote vinavyosababisha kutokuwapo kwa usawa wa kijinsia kama vile mimba na ndoa za utotoni ambazo zimekuwa zikiwanyima fursa watoto wa kike kutimiza ndoto zao.

Alisema kuwa mapambano ya usawa wa kijinsia yatafanikiwa pale yatakaposhirikisha wanaume na wavulana katika kuhakikisha wasichana na wanawake wanapata fursa sawa katika kutimiza ndoto zao.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women, Hodan Addou, alisema kuwa shirika hilo linashirikiana na serikali na mashirika ya kitaifa kuhakikisha elimu inatolewa na usawa wa kijinsia inakuwa suala la kipaumbele katika jamii.

Kiama Chaja kwa Waliolipa kodi ya pango la ardhi ya nyumba

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ameanzisha kampeni maalumu ya kuwasaka wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi ya nyumba kwa nyumba na wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi ambao hawajalipa hadi mwaka huu.

Kampeni hiyo ambayo aliizindua mwishoni mwa wiki wilayani Karatu mkoani Arusha, alipokuwa akisikiliza na kutatua migogoro ya ardhi ya wakazi wa wilaya hiyo katika kampeni ya Funguka kwa Waziri, amewaagiza watendaji wote wa wilaya na kanda nchini kuanza kuwasaka nyumba kwa nyumba wadaiwa wa kodi ya ardhi.

“Naagiza mikoa yote ya Tanzania Bara kuanza kampeni rasmi ya kuwasaka wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi ya nyumba kwa nyumba na msiwaonee huruma hata kama ni waziri na anadaiwa kodi ya ardhi peleka mahakamani hata kama ni kiongozi yeyote, hata kama Mkuu wa Wilaya mfuate na peleka mahakamani," alisema Waziri Lukuvi.

Aliwataka wamiliki wote wa ardhi kujitathmini na kukagua taarifa zao kama wamelipa kodi ya ardhi na kuanza kulipa haraka kabla kampeni hiyo haijamfikia mdaiwa.

Aliwataka watendaji wake wasiwe na huruma na mtu yeyote anayedaiwa kodi kwa sababu fedha za kodi ndizo zinazosaidia katika ujenzi wa miundombinu na utoaji huduma kwa wananchi na ndizo zinazosaidia uendeshaji wa serikali kwa kiasi kikubwa.

Alisema kila mtu aliyemilikishwa ardhi kwa matumizi yoyote lazima alipe kodi kwa wakati isipokuwa tu wale ambao wamesamehewa kuanzia mwaka huu wa fedha na Rais na Bunge limeridhia kwamba maeneo ya kuabudu na maeneo ya kutolea huduma bila biashara kama vile shule, zahanati, misikiti na makanisa na taasisi zisizofanya biashara zisilipe kodi hiyo.

Waziri Lukuvi pia aliwaagiza wenyeviti wote wa mabaraza ya ardhi na nyumba ambao wanahusika na hukumu za masuala ya ardhi, kusimamia na kuzipa kipaumbele kesi zote za watu wanaoshtakiwa kwa kutokulipa kodi ya pango la ardhi na kuzichukulia kwamba ni kesi kubwa katika kipindi hiki.

Alitaka kesi zote za wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi zitolewe hukumu kwa siku moja na mtu atozwe faini siku hiyo hiyo na akishindwa kulipa, hati yake ibatilishwe au kupigwa mnada kwa nyumba au mali yake kufidia kodi anayodaiwa.

Aidha, Waziri Lukuvi aliwaagiza maofisa ardhi wote kupekua mashamba yote ambayo yanatumika kwa biashara yanayolimwa na yenye hati yalipe kodi na kama hawatolipa basi watafutiwa hati zao kwa kuwa kigezo kikubwa cha kufutiwa hati ni kutokulipa kodi.

VIDEO: Harmonize Ft Diamond Platnumz & Burna Boy – Kainama

0
0
VIDEO: Harmonize Ft Diamond Platnumz & Burna Boy – Kainama

China Yatangaza kusitisha safari za ndege zake zenye chapa ya Boeing 737 Max 8

0
0
Kufuatia ajali ya ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Ethiopia iliyokuwa ikitoka Addis Ababa kwenda Nairobi na kuua watu 157, Mamlaka ya Udhibiti wa Safiri za Anga ya nchini China imetangaza maamuzi magumu.

Mamlaka hiyo imesema mapema Jumatatu, Februari 11 kuwa imeliagiza Shirika la Ndege la China kusitisha matumizi ya ndege za Boeing 737 hadi hapo itakapotoa taarifa zaidi kuhusu kurejea kwa safari zake.

Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia aina ya 737 MAX 8 ilipata ajali dakika chache baada ya kuruka katika Uwanja wa Ndege wa Addis Ababa Jumapili, March 10.

Hiyo ni ajali ya pili ya ndege hizo ambazo ni toleo jipya la kampuni ya Boeing lililotolewa mwaka 2017, ambapo mnamo Oktoba mwaka 2018, ndege ya Shirika la Ndege la Indonesia iliyokuwa ikifanya safari za ndani ilianguka dakika 13 baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Jarkata na kuua abiria 189 pamoja na wahudumu wa ndege.

Shirika la Ndege la China linamiliki jumla ya ndege 96 aina ya Boeng 737 MAX, ambapo imesema imeona mfululizo wa vyanzo vya ajali za ndege hizo zinafanana.

Lakini msemaji wa Shirika la Ndege la Boeing ameuambia mtandao wa Reuters akikanusha tuhuma hizo za China, akisema kuwa hana uhakika na taarifa ambazo nchi hiyo inazitumia.

UVCCM Wasema Wamemsamehe Lowassa Baada ya Kukiri Makosa na Kuahidi Kujirekebisha

0
0
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umesema wamesahau na kumsamehe Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya kukiri makosa na kujirekebisha.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Machi 11, 2019 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa umoja huo , Kheri James  wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuwa kama akitokea mtu akahoji kwa nini Lowassa amesamehewa na kukubaliwa na CCM anyooshe mkono kwamba yeye hana dhambi.

Amehoji waliobainika kuhusika katika ripoti ya ukaguzi wa mali za CCM kama yupo aliyepelekwa mahakamani kwa makosa na kwamba anayekiri makosa yake na kujirekebisha husamehewa.

Lowassa  alihamia CHADEMA  Julai 28, 2015 lakini  March Mosi, 2019 alitangaza kurejea chama chake cha zamani cha CCM.

Serikali imeimarisha usimamizi matumizi salama ya nyuklia nchini

0
0
Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imefanikiwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia nchini. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekenolojia Mheshimiwa William Ole Nasha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 46 wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki ( IAEA ) unaofanyika jijini Arusha.

Naibu waziri Ole Nasha amesema Shirika hilo linafadhili miradi mingi katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo sekta ya afya ambapo imewezesha kupatikana kwa vifaa mbali mbali vya uchunguzi wa tiba na maradhi ya saratani ambavyo vimefungwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando jijini Mwanza na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.

Pamoja na vifaa vya uchunguzi katika hospitali hizo mbili, pia taasisi nyingine mbalimbali zimepata vifaa vya maabara ambapo kwa ujumla wake vifaa vyote vina thamani ya kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 6.2 na pia kutoa mafunzo kwa wataalamu katika eneo la matumizi ya mionzi na Teknolojia ya Nyuklia mpango ambao uligharimu Shilingi za Tanzania Bilioni 3.3.

Mh Ole Nasha amelishukuru na kulipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa wanachama hususan kwa utaratibu wake wa kuwa na mikutano inayowezesha kubadilishana uzoefu baina ya wanachama. Amewataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha wanafanya majadiliano yenye tija kwa lengo la kusaidia nchi zao kwenye udhibiti na matumizi salama ya teknolojia ya nyukulia. “ majadiliano yenu yalenge katika kuhakikisha mionzi na teknoljia ya Nyuklia katika Afrika inatumika vizuri kwa maendeleo”.Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA ) Profesa Shaukat Abdulrazak amesema wataendeela kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia ya Nyukilia kwenye sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya , Kilimo,Mifugo,Maji ,Viwanda na Ujenzi.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Nguzu za Atomiki Tanzania , Profesa Lazaro Busagara amesema taasisis yake imeendelea udhibiti na kuwachukulia hatua za kuwafungia taasisi zinazokiuka taratibu za matumizi salama ya Mionzi na Teknolojia ya Nyuklia hapa nchini ikiwemo kutokuwa na leseni, kutokuwa na wafanyakazi wenye utaalamu wa matumizi ya mionzi na teknolojia ya Nyuklia na Mionzi.

Akitoa mfano wa Hospitali amesema mwaka 2018 walifungia hospitali 112 zilizoshindwa kufuata masharti hayo, katika hizi tayari hospitali 40 zimekidhi na kufunguliwa huku hospitali 72 zikiwa bado zimefungiwa kutumia vifaa vinavyotumia mionzi .
Mkutano huo wa Siku tano utamalizika tarehe 15 , Machi 2019.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC)
11/ 3/2019
Arusha, Tanzania

Mahakama Yaombwa Kutumia Nguvu Kesi ya 'Mpemba wa Magufuli'

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeombwa kutumia nguvu katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ na wenzake watano kwa sababu shauri hilo lipo tangu mwaka 2016.

Yusuf na wenzake watano, wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwemo la kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh.Mil 785.6.

Maombi hayo yametolewa na upande wa utetezi baada ya Wakili wa Serikali, Candid Nasua mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilka.

Wakili wa Utetezi Neemia Nnkoko amedai rekodi zinaonyesha tangu mwaka 2017 kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo wameshangazwa kusikia upande wa mashtaka kuwa upelelezi bado haujakamilika ambapo wanaiomba mahakama itumie nguvu.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba alisema rekodi zinaonyesha kuwa Oktoba 23,2018 upande wa mashtaka ulidai upelelezi umekamilka hivyo anawataka upande wa mashtaka wamueleze wakili wa Serikali Mkuu Mchimbi kuhusu kukamilisha kwa upelelezi huo.

Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi March 25, 2019 itakapotajwa tena na washtakiwa wote wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yao hayana dhamana.

Kesi ya Zitto Kabwe Yakwama Kuendelea......Wadhamini Wake Waitwa Mahakamani, Shahidi Kapewa Onyo

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam imewaita wadhamini na mshtakiwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe anayekabiliwa na kesi ya uchochezi kufika Mahakamani kujieleza kwanini hawakufika kwenye kesi mapema leo.

Kadhalika imemuonya shahidi wa kwanza Mrakibu Msaidizi (ASP), Shamila Mkoma kufika mahakamani hapo Aprili 9,mwaka huu kutoa ushahidi dhidi ya Zitto.

Amri hiyo imetolewa leo na Mahakama hiyo iliyokuwa chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Wakili wa Serikaki Wankyo Simon amedai kuwa kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikiliza ushahidi na Jamhuri imeita shahidi mmoja ASP Mkoma.

Hata hivyo, amedai kuwa mshtakiwa hayupo mahakamani, Wakili wa utetezi, Steven Mwakibolwa amedai kuwa amepata taarifa kutoka kwa shemeji wa mshtakiwa Vicent Kasala kwamba Zitto ni mgonjwa lakini hafahamu mahali alipo.

"Kasala amenieleza kwamba mkewe Zitto kampigia kumfahamisha kwamba ni mgonjwa lakini hajui yuko wapi" amedai Nwakibolwa.

Hakimu amehoji wakili amepewa taarifa kwamba mshtakiwa ni mgonjwa lakini hana uhakika.

"Umepewa taarifa kwamba mshtakiwa anaumwa lakini huna uhakika, tusitafutane maneno hapa, siku ya kesi wadhamini na mshtakiwa waje hapa mahakamani kujieleza kwanini hawakufika mahakamani" amesema Hakimu Shaidi.

Amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri Aprili 9, mwaka huu na shahidi afike siku hiyo.

Vyama Vya Ushirika Vyatakiwa Kuwa Na Mipango Yenye Tija

0
0
Na Amiri kilagalila
Shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania (TFC) limesema kuwepo kwa mipango yenye kuleta tija katika vyama vya msingi vya ushirika nchini, ndiyo sababu mojawapo itakayowajengea imani na matumaini wananchi ya kujiunga na ushirika hivi sasa.

Meneja wa elimu na mafunzo kutoka shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania, FROLIAN HAULE ametoa kauli hiyo  baada ya kutembelea Kiwanda cha kusindika unga wa Sembe cha chama kikuu cha ushirika mkoa wa Njombe (NJORECU) akiwa ameongozana na ujumbe wa shirikisho hilo na kusema kuwa mfano mzuri uliofanywa na Njorecu unapaswa kuigwa na vyama vingine.

Chama Kikuu cha ushirika Mkoani Njombe (NJORECU) kimeanzisha kiwanda cha kusindika unga wa sembe unaotokana na malighafi ya mahindi ambapo shirikisho la vyama vya ushirika nchini limetoa wito kwa vyama vingine kuzingatia ushauri na elimu wanayokuwa wakiitoa katika mafunzo na kuvitaka vyama vikuu kuwa na viwanda vitakavyosaidia kujiendesha na kupata faida kubwa.

“Tayari kuna baadhi ya vyama vimekwisha chukua hatua za kuanza kufanya maswala ya uwekezaji hii inatia faraja na kwa msingi huo tunakuwa na darasa kwa vyama vingine kuja kujifunza kuwa uwekezaji kwa vyama vya ushirika unawezekana”alisema FROLIAN HAULE meneja wa mafunzo na elimu

Mwenyekiti wa chama kikuu mkoa wa Njombe NJORECU CLEMENT MALEKELA anasema kiwanda cha kuchakata unga wa sembe kilichogharimu kiasi cha shilingi Milioni 75 kimeleta faraja kwa wanachama hivi sasa ambao wameonyesha nia ya kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na viongozi, ikiwemo   kuanza kupata soko la kuuza unga wa sembe katika nchi jirani.

“Soko la nje tayali tumelifanyia utafiti kwa mfano tumetembelea Lwanda tukitafuta soko la Sembe ilionekana kikwazo kikubwa ni swala la ubora lakini kwa ujumla tunakwenda vizuri”alisema Malekela

Pamoja na vyama vya msingi vya ushirika kuanzisha viwanda vya kusaidia kujiendesha JOAN KIRWAY ambaye ni msimamizi wa kitengo cha bima za mikopo kwenye shirikisho hilo anasisitiza umuhimu kwa vyama vya ushirika kuwa na bima za mikopo ili kusaidia kuepukana na majanga ya aina mbalimbali.

“Lakini changamoto kubwa vyama vya ushirika mpaka sasa hawajui nini maana ya bima mfano unakuta wana viwanda lakini mpaka sasa havijakatiwa bima wakati ni kitu pekee na cha msingi katika usalama wa mali zao”alisema JOAN KIRWAY

Naye afisa ushirika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe, EXVERY SAPALI amesema sheria namba sita ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 haina makali sana ya kuwabana wabadhirifu wa mali ndio maana wengi wamekuwa wakikiuka utaratibu na sheria za ushirika.

Mahakama Yatoa Neno Kesi ya Vigogo UDART

0
0
Upande wa mashtaka umetakiwa kuhakikisha upelelezi unakamilika kwa wakati katika kesi inayowakabili Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart), Robert Kisena (46) na wenzake watatu .

Kisena na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 19 likiwemo la utakatishaji fedha na kuusababishia Mradi wa Udart hasara ya zaidi ya Sh2.41 bilioni.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kulwa Kisena (33), Charles Newe (47) na raia wa China, Cheni Shi (32).

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Pendo Temba kudai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amewataka upande wa mashtaka kuhakikisha shauri hilo wanalifuatilia ili upelelezi ukamilike kwa wakati.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 25 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa hao wamerudishwa rumande.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images