Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Atoa Pole Kwa Familia Ya Mtangazaji Wa Clouds Fm, Efraim Kibonde

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kifo cha aliyekuwa Mtangazaji Muandamizi wa kituo cha redio cha Clouds, Ephraim Kibonde ni pengo kubwa kwa Taifa, Clouds Media Group na tasnia ya habari kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 8, 2019) alipokwenda kuhani msiba wa Mtangazaji Muandamizi kituo cha redio Clouds, Kibonde kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mbezi Beach Dar es Salaam.Kibonde alifariki dunia jana alfajiri Machi 7, 2019 jijini Mwanza.

“Msiba huu umetushtua sana na ni tukio ambalo hatukulitarajia ila ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Hivi karibuni sote tulimshuhudia akiongoza ratiba ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na alienda hadi Kagera kumzika.”

Waziri Mkuu amesema marehemuKibonde enzi za uhai wake ameshirikiana vizuri na Serikali katika shughuli mbalimbali, hivyo amewaomba wananchi waendelee kushikamana na kuifariji familia. “Tumuombee marehemu apumzike kwa amani.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.


 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Mwakyembe Aomboleza Kifo Cha Mtangazaji Ephraim Kibonde

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mtangazaji Mahiri wa Clouds Media Group, Bw. Ephraim Samson Kibonde kilichotokea jana Jijini Mwanza.

“Msiba huu ni pigo kubwa  kwetu wanatasnia wa habari nchini, tupo pamoja na  wenzetu wa Clouds Media Group katika kipindi hiki kigumu cha majonzi” amesema Dkt. Mwakyembe.

Enzi za uhai wake Marehemu Kibonde alikuwa Mtangazaji wa Redio ya Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, pia alijihusisha na shughuli ambalimbali za kijamii zikiwemo uandaaji wa  vipindi vya kuelimisha Umma katika masuala ya Makazi na Afya.

Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, uongozi na wafanyakazi wote wa Clouds Media Group pamoja na wadau wa habari nchini.

Imetolewa na

Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

08/03/2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya March 9

Mfumuko wa bei nchini wabaki asilimia 3.0 ya mwaka jana

$
0
0
Na Amiri kilagalila
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii  Ephraim Kwesigabo amesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia  mwezi Februari,2019 umebaki kuwa asilimia 3.0 kama ilivyokuwa mwaka ulioisha  mwezi Januari ,2019.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma , kwesigabo amesema hali hiyo  inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi februari , 2019 imebaki kuwa sawa  na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi januari 2019.

Aidha, kwesigabo ameongeza kuwa mfumuko wa bei wa mwezi Februari ,2019 kubaki kuwa sawa kama ilivyokuwa mwezi januari, 2019  umechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi februari ,2019 zikilinganishwa  na bei  za februari ,2018 .

Katika hatua nyingine kwesigabo amesema kuwa baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula ziliongezeka kwa asilimia 2.7,mkaa kwa asilimia 10.1,majokofu  kwa asilimia 2.1 na gharama za kumuona daktari hospitali za binafsi ni asilimia 4.6.

Mbali na hilo kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi  kwa mwezi  februari ,2019 umepungunga hadi asilimia 0.5 kutoka asilimia 0.7 ilivyokuwa mwezi januari mwaka ,2019

Hata hivyo, Kwesigabo amesema hali ya mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki ,Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi februari ,2019 umeongezeka hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 2.7 kwa mwaka ulioishia mwezi januari,2019 huku nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi februari ,2019 umepungua kidogo asilimia 4.14 kutoka asilimia 4.70 kwa mwaka ulioishia mwezi januari ,2019.

CHADEMA Wamkana Khamis Mgeja

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Shinyanga kimemkana aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja kuwa hakuwa mwanachama wa chama hicho ila alikuwa kama mshenga wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana  Ijumaa Machi 8, 2019 Katibu wa Chadema mkoa wa Shinyanga, Zakaria Obadi alisema Mgeja hakuwa mwanachama wa Chadema ila alikuwa mshenga tu wa Lowassa hivyo walishangaa kuona anatangaza kwa waandishi wa habari anahama Chadema na kuhamia CCM.

Obadi alisema Mgeja ametangaza akisema alihamia mwaka 2015 lakini chama kinajua alikuja kama mshenga kwa sababu hakukabidhiwa hata kadi ya Chadema hivyo chama kilikuwa hakimtambui kama ni mwanachama.

Alisema wao kama viongozi wa mkoa wana haki ya kumjibu Mgeja kwani hastahili kujibiwa makao makuu, kwa sababu hakuwepo hata kwenye taarifa za chama hata kuvaa mavazi ya Chadema hajawahi, wao wanawatambua wanachama.
 
Mgeja alitangaza kuhamia Chadema mwaka 2015 mara baada ya Lowassa kufanya hivyo Julai 28, 2015 lakini hivi karibuni, Lowassa alitangaza kurudi CCM na sasa Mgeja naye amechukua uamuzi kama wa Lowassa.

Halima Mdee: Sikuona Haja ya Kumzungumzia Lowassa, Najua Nafsi Yake Inavuja Damu ya Usaliti

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee amesema kwamba hakutoa neno lolote baada ya Lowassa kurudi kwenye Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa anatambua changamoto anazozipitia kiongozi huyo kwa sasa.

Mdee amefunguka hayo wakati akijibu swali kuhusu maoni yake kufuatia aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mgombea huyo wa Urais mwaka 2015 kwa mwamvuli wa Ukawa,kurudi CCM

"Natambua changamoto nyingi anazopitia za kifamilia na kibiashara, akalazimika kuomba po! sikuona haja ya kusema chochote nikiheshimu uamuzi wake. Najua nafsi yake inavuja damu ya usaliti kwa waliompa heshima na ‘kumrudishia uhai’" Ameandika Halima  Mdee.

Edward Lowassa alirejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, ya wiki iliyopita  na kupokelewa na uongozi wa juu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti, Dk. John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli Awamwagia Sia Wanawake....Awataka Watembee Kifua Mbele

$
0
0
Rais wa Tanzania, John Magufuli amewapongeza kina mama nchini kwa jitihada mbalimbali wanazozifanya na kwamba waendelee kutembea kifua mbele kwa kuwa Serikali inawathamini.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana  Ijumaa Machi 8, 2019 katika uwanja wa ndege wa zamani wa Julius Nyerere ikiwa ni muda mfupi baada ya kuagana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame aliyekuwa nchini kwa ziara ya siku mbili.

“Nawapongeza wananchi wote waliojitokeza kumsindikiza Rais Kagame, mmeonyesha ukarimu wenu kwa Watanzania. Nimefurahi sana kuona kina mama mpo wengi na leo ni siku yenu.

“Mungu awabariki mnafanya kazi nzuri sana, endeleeni kuimarisha umoja kwa Watanzania wote, Serikali ninayoiongoza inathamini sana kazi nzuri zinazofanywa na kina mama. Endeleeni kutembea kifua mbele na Mungu atawatunza na mimi sasa hivi nakwenda kumuona mama yangu hospitalini,” alisema Rais Magufuli huku akishangilia na kina mama waliokuwa uwanjani hapo.

Mbali na hilo, Rais Magufuli alivikabidhi Sh1 milioni vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza uwanjani hapo wakati wa hafla ya kuagana na Rais Kagame.

“Hiki kidogo mtakwenda kunywa chai. Nawapongeza sana mmekuwa mkionyesha ukarimu kwa wageni wanaokuja na kupokelewa vizuri,”alisema Rais Magufuli.

Rita yasajili Bodi ya CUF inayomuunga mkono Lipumba

$
0
0
Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, imepata usajili baada ya kukidhi vigezo vya kisheria.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu CUF, Magdalena Sakaya, alisema bodi hiyo imepata usajili baada ya kurekebisha kasoro mbalimbali zilizoelezwa na Mahakama Kuu, Februari 18 mwaka huu, jambo lililosababisha awali kushindwa kusajiliwa.
 
Akisoma barua ya Kaimu Katibu Ofi sa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufilisi na Udhamini (Rita), Emmy Hudson, kwenda kwa chama hicho, Sakaya alisema:
 
“Baada ya wakala huo kupitia nyaraka zilizowasilishwa na chama hicho kwa kuzingatia sheria ya usajili wa wadhamini sura 318, marejeo ya 202 kifungu cha 17 (1B) cha sheria ya Vyama vya Siasa na marekebisho yake.
 
“…pamoja na ofisi  ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuonyesha ushiriki katika kikao cha kuzingatia maelekezo ya hukumu, Mahakama Kuu ya mislenia civil case namba 13n ya 2017 mbele ya Jaji Masoud J., hivyo nimeridhika na nyaraka hizo baada ya kuonekana kuwa sahihi na zimehifadhiwa katika kumbukumbu za ofisi,” alisema Sakaya akisoma barua hiyo.
 
Aliwataja wajumbe tisa wanaounda Bodi hiyo kuwa ni pamoja na Peter Malebo, Hadra Silia, Aziz Dagesh, Abdul Magomba,
Amina Msham, Asha Suleiman, Mussa Kombo, Salha Mohamed na Suleiman Makame Issah.
 
“Nichukue fursa hii sasa kuwajulisha wananchi wote, wanachama wote wapenzi wote wa CUF popote walipo Bodi ya Wadhamini imesajiliwa na muda wowote kuanzia sasa Bodi itakaa kuweza kumchagua mwenyekiti wao ambaye ataongoza Bodi.
 
“Baada ya hapo wataweza kuangalia mambo yote ya chama kwa sababu kikatiba mambo mengi ya chama yanasimamiwa na bodi, ikiwamo kuangalia kesi zilizopo mahakamani, chama kimekwisha kuwa na bodi na anayeshtakiwa ni bodi, si mtu binafsi,” alisema.
 
Kutokana na hatua hiyo, Sakaya aliwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kuachana na kile alichokiita kuwa ni ‘blabla’ zinazoandikwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa lengo ya kuichafua CUF.
 

Kikosi cha Timu ya Taifa ( Taifa Stars) Kitakachocheza Dhidi ya Uganda

$
0
0
Kocha mkuu wa Timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Emmanuel Amunike amekitaja kikosi cha wachezaji 25 kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Uganda. Stars inajiandaa na mchezo dhidi ya Uganda wa kufuzu mashindano ya Afrika, mchezo utakaopigwa 24 March katika uwanja wa Taifa.

Katika kikosi hiko Amunike amefanya mabadiliko kwa kuwatoa nyota waliokuwa katika kikosi hiko na kuingiza wengine.

Amunike amemuondoa kikosini Beno Kakolanya ambaye yupo nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana kuwa katika sintofahamu na klabu yake, lakini pia amemuondoa Abdi Banda, Ibrahim Ajib na Erasto Nyoni anayesumbuliwa na majeraha.

Katika nafasi hizo amewaongeza Aaron Kalambo(Tanzania Prison),Metacha Mnata (Mbao) na Suleman Salula (Malindi Fc Zanzibar). Huku katika upande wa mabeki akiwaongeza Vicent Philipo (Mbao Fc) na Kennedy Wilson (Singida Utd).

Askofu Pengo: Chuo cha Mtakatifu Joseph (SJUIT) hakimlazimishi mtu kufuata misingi ya kikatoliki

$
0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka  watu wasiogope kwenda au kuwapeleka wengine kusoma katika Chuo cha Mtakatifu Joseph (SJUIT)  kwa kuogopa  watalazimishwa kufuata imani ya chuo hicho kinachoongozwa kwa  misingi ya dini ya kikatoliki.

Askofu Pengo amesema hayo jana Ijumaa Machi 8, katika mkutano wa kulitangaza Baraza jipya la chuo lililotangazwa na Mkuu wa Chuo hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema licha ya chuo kuwa na malengo ya kikatoliki ambayo yana dini ndani yake na kuna maeneo ambayo lazima yatabaki hivyo, haimaanishi kila mwanafunzi anapaswa kubadili na kuwa mkatoliki.

“Mimi nikija katika chuo hiki ntaingia kama Askofu na kama mkatoliki ambaye ninaamini Yesu ni mwana wa Mungu, lakini hii haimaanishi kila anayekuja kusoma hapa lazima afate misimamo yangu, kila mtu ana imani tofauti na ana haki ya kuwa na imani tofauti.

“Jambo la msingi ni kuwa na misimamo ya kidini ambayo inaongoza maisha ya binadamu, na nitaendelea kusisitiza kuwa kila binadamu aliumbwa na Mungu na maelekezo na maadili yote yanafundishwa kuhusu Mungu mmoja, haijalishi ni dhehebu gani ila tunapaswa kujua Mungu huja kabla ya kila kitu,” alisema Askofu Pengo.

Awali akisoma majina ya baraza hilo jipya Mkuu wa Chuo hicho, Padri Arul Raj aliwataka wajumbe wateule kufanya kazi zao kwa umakini wa hali ya juu ili kukisaidia chuo kutoa elimu itakayozalisha wanafunzi bora ambao wataisaidia nchi kukua katika nyanja mbalimbali hasa ya viwanda ili kuendana na sera ya serikali ya ‘Tanzania ya Viwanda’.

“Lengo la mwanzilishi wa chuo hiki ni kutoa wanafunzi wenye taaluma za Sayansi na Teknolojia, hivyo sisi tumepewa dhamana ya kuhakikisha jambo hili linatimia, hivyo basi inatupasa kuweka nguvu na akili zetu katika kuzalisha wanafunzi watakao isaidia nchi ya Tanzania kukua hasa katika sekta ya viwanda na uhandisi,”alisema.

Ephraim Kibonde Kuzikwa Leo Makaburi ya Kinondoni Dar

$
0
0
Mtangazaji  maarufu wa Clouds Media Group (CMG), Ephraim Kibonde, anatarajia kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, sehemu ambayo alizikwa mke wake, Sarah, aliyefariki dunia Julai, mwaka jana.

Kibonde alifariki dunia juzi jijini Mwanza kwa shinikizo la damu wakati jitihada za kumhamishia Hospitali ya Rufani ya Kanda ya Bugando kutoka Hospitali ya Uhuru zikifanyika.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana, mtangazaji huyo ataagwa leo nyumbani kwa wazazi wake, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na baadaye saa 10:00 jioni atazikwa makaburi ya Kinondoni.

Kibonde alianza kujisikia vibaya kabla ya kuzikwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa CMG, Ruge Mutahaba, Bukoba mkoani Kagera na kupelekwa Hospitali ya rufani ya Mkoa wa Kagera ya Bukoba na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Uhuru. Wakati akipelekewa Bugando, ndipo umauti ulipomkuta alfajiri ya kuamkia juzi.

Alichokisema Mtoto Wa Lowassa, Fred Lowassa Wakati wa Mapokezi ya Baba Yake Arusha

$
0
0
Mamia ya wakazi wa Arusha wamekusanyika uwanja mdogo wa Arusha kumsubiri Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa aliyetimkia Chadema akitokea CCM ambako alipitishwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Mei mosi, 2019 alitangaza kurudi CCM na leo Jumamosi Mei 9, 2019 anarejea nyumbani kwake, Monduli mkoani Arusha.

Watu hao wakiwepo familia ya Lowassa, wakiongozwa na mtoto wake, Fred Lowassa wamesema wamerejea nyumbani CCM na Lowassa.

Fred ambaye naye alijiunga na Chadema baada ya baba yake kutimkia Chadema Julai 28, 2015, amesema familia yote ya Lowassa imerejea nyumbani CCM.

"Kama alivyosema mzee amerudi nyumbani na sisi kama familia tumerudi kumuunga mkono" amesema Fred leo Jumamosi Machi 9, 2019 jijini Arusha.

Amesema anajisikia vizuri kurudi nyumbani kuendelea kushirikiana na rafiki zake ambao aliwaacha CCM na ambao bado wapo Chadema.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Apangua Tuhuma za Zitto Kabwe

$
0
0
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini kuwa mkweli katika kutoa takwimu za vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi tofauti na takwimu anazozitoa.
 
Waziri Ummy amelazimika kumjibu Mbunge huyo baada ya kubandika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti ACT - Wanawake, Chiku Abwao ambaye katika maadhimisho ya siku Wanawake jana alisema kwamba mwaka 2019 idadi ya wanawake wanaofariki kwa uzazi imeongezeka mpaka 11,000 kwa mwaka.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa imeeleza kwamba kipaumbele cha Serikali ya CCM kimekuwa ni kuongeza idadi ya wanawake wanaofariki kwa uzazi badala ya kupunguza jambo ambalo limetafsiriwa kama aibu kubwa kwa taifa.

Akijibu Tuhuma hizo, Waziri Ummy ameandika yafuatayo;"Kaka yangu, kwa nini husemi ukweli kuwa Takwimu hizi ni za TDHS 2015/16. Na kwamba survey nyingine itafanyika 2019/20 ambapo sina shaka kabisa kuwa vifo vitokanavyo na uzazi vitakuwa vimepungua kwa zaidi ya asilimia 50! Sema ukweli tafadhali,".

"Si kweli. Narudia tena kusisitiza TDHS ni ya 2015/16, takwimu hizi zilikusanywa 2015. hakuna Utafiti mwingine wa kitaifa uliofanyika na kutoa MMR. Hivyo tusubiri utafiti mwingine wa 2019/20 na hapo ndio mnaweza kusema ni jinsi gani Serikali imefanikiwa ktk kupunguza Vifo hivi" Amesisitiza Waziri Ummy

Pamoja na majibu ya Waziri Zitto amemsisitizia waziri kwamba matokeo ya utafiti ambayo bado haujafanyika si sahihi huku akihoji kama anapingana na tafiti zilipo sasa.

"Vikipungua tutamshukuru sana Mungu. Lakini takwimu za sasa kuwa wanawake 556/100,000 Sawa na wanawake 11,000 kwa Mwaka kufariki unazipinga? Kwamba wanawake 30 wanafariki dunia kila siku sababu ya uzazi unapinga? Matokeo ya survey itakayofanyika sidhani kama ni sahihi kujadili" Amesisitiza Zitto Kabwe .

PICHA: Rais Mstaafu Kikwete, Waziri Mwakyembe Wakiwa Msibani kwa Ephraim Kibonde

$
0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumamosi amewaongoza mamia ya wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media Group Ephraim Kibonde, nyumbani kwa wazazi wake Mbezi Africana jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine waliofika kuaga mwili wa Kibonde ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Dk Harrison Mwakyembe (Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo), Dotto Biteko (Waziri wa Madini), William Lukuvi (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na Nape Nnauye (Mbunge wa Mtama).

Wengine ni Manaibu Mawaziri, Katibu Mkuu wizara ya Habari, Wabunge na Wakuu wa Wilaya.

Ephraim Kibonde alifariki  Machi 6, 2019, asubuhi saa kumi na mbili na nusu katika Hospitali ya Uhuru jijini Mwanza. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Jumamosi saa kumi jioni  katika Makaburi ya Kinondoni.

Lowassa Apokelewa Kifalme Monduli

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu,Edward Lowassa ametua wilayani Monduli na kupokewa kwa shangwe na wafuasi wa CCM ambao wamekusanyika viwanja vya CCM Monduli.

Lowassa alifika Monduli majira ya saa 7:34 na kushuka kwenye gari na kupokewa na mbunge wa jimbo la Monduli, Julius Kalanga.

Baada ya kushuka kwenye gari, Lowassa aliwapungia mkono wafuasi wa CCM ambao walilipuka kwa shangwe na vigelegele.

Lowassa baada ya kushuka alikwenda moja kwa moja ofisi za CCM wilayani Monduli ambapo hadi sasa kikao kinaendelea ambacho anashiriki pia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole.

Baada ya kikao hicho ambacho kinajumuisha wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Monduli, Lowassa atakabidhiwa kadi ya CCM.

Waziri Mkuu: Aga Khan Fanyeni Mapitio Ya Gharalama Zenu

$
0
0
SERIKALI imeutaka Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), ufanye mapitio ya gharama za afya katika hospitali ya Aga Khan ili wananchi wa kawaida waweze kumudu na kunufaika na huduma za tiba wanazozitoa.

Imeelezwa kuwa pamoja na jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya, pia inatambua mchango unaotolewa na taasisi zisizo za Kiserikali ikiwemo Hospitali ya Aga Khan katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kisasa.

Hayo yamesemwa leo (Jumamosi, Machi 9, 2019) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Amesema upanuzi wa hospitali hiyo ni miongoni mwa jitihada za kuwafikishia Watanzania huduma za afya katika maeneo yao na kwa ngazi zote na kwa gharama nafuu, hivyo amewataka watoa huduma wote nchini waangalie upya gharama zinazotozwa katika huduma mbalimbali hususan za matibabu.

“Mtakubaliana nami kuwa gharama zikiwa kubwa hazitawanufaisha wananchi hususan wa kipato cha chini na wananchi hawataona unafuu wa kutibiwa nchini na nje ya nchi, hivyo fanyeni mapitio ya gharama hizo.”

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua gharama kubwa za uwekezaji na uendeshaji wa shughuli za afya nchini hususan kwa sekta binafsi. “Lengo la Serikali kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali kama Aga Khan ni kuwezesha huduma zinazotolewa kuwa nafuu.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeanzisha na kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na mwitikio wa ni mkubwa na lengo lake ni kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya matibabu tena kwa uhakika.

“Nitoe wito kwa taasisi zote zisizo za Serikali kuunga mkono jitihada hizi za Serikali na kuhakikisha wananchi wote wananufaika na huduma zenu kupitia mfumo huu bila kubaguliwa.”

Pia ameutaka uongozi wa Hospitali ya Aga Khan na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakamilishe majadiliano yao katika matumizi ya NHIF kwenye hospitali hiyo ya rufaa. “Dr. Konga Mkurugenzi Mkuu wa NHIF upo hapa kamilisheni mjadala.”

Amesema nia ya Serikali ni kuona wananchi wanakwenda hapo kwenye jengo hilo zuri na wanapata huduma kupitia bima ya afya. “Ni matumaini yangu kwamba jambo hili litafanyiwa kazi kwa kuzingatia maslahi mapana ya pande zote mbili.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji, kuimarisha amani na utulivu, ambapo ametoa rai kwa sekta binafsi ziendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo nchini kwa kuzingatia sheria za nchi, utamaduni na mila za Watanzania.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma katika jengo hilo ikiwemo maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya watoto, wodi ya wazazi. Ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu sh. bilioni 192, kati yake sh. bilioni 134 ni mkopo wa muda mrefu wenye masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameupongeza Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan kwa upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwani unakwenda kuboresha huduma za afya nchini.

Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kutolea huduma za afya ambapo kwa sasa imeanzisha ushirikiano na sekta ya umma na binafsi kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.

Naye Balozi wa Ufaransa nchini, Balozi Frederic Claiver amesema awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali hiyo utasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya Tanzania.

Pia Balozi huyo amesema Ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha inatimiza mkakati wake wa kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Ephraim Kibonde azikwa makaburi ya Kinondoni

$
0
0
Aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds Media Group (CMG), Ephraim Kibonde amezikwa leo Machi 10 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam majira ya sa Kumi jioni.
 
Amezikwa na maelfu ya watu ambao ni ndugu, jamaa na marafiki aliokuwa akifanya nao shughuli mbalimbali enzi za uhai wake na wengine waliomjua kupitia kazi yake ya utangazaji.

Kibonde amefariki dunia Machi 7 mwaka huu baada ya kuugua Presha kwa muda mfupi katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza.


Ameacha watoto wa nne wakike wawili na mmoja wakiume.

Lowassa Aishukuru CHADEMA....Ataka Waliompigia Kura Wamuunge Mkono Rais Magufuli

$
0
0
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amekishukuru Chama cha Demokrasia na Maendeleo, huku akiwaomba wafuasi wa chama hicho wasimuwekee maneno mdomoni.

Akizungumza leo Monduli, Jijini Arusha kwa mara ya kwanza tangu aliporejea ndani ya Chama Cha Mapinduzi wiki mbili zilizopita amesema amerudi CCM kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Rais John Pombe Magufuli na kasi.

"Nimerudi CCM kwa kuwa nimeshawishiwa na Kazi nzuri inayofanywa na Rais pamoja na mawaziri wake nchi nzima. Nimekuja kuwaombeni tumuunge mkono. Kwa CHADEMA nawashukuruni sana. Msiniwekee maneno mdomoni."

Edward Lowassa leo amewasili nyumbani kwake Monduli Arusha kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza kujiondoa kama Mwanachama wa CHADEMA, chama alichojiunga nacho 2015 ambapo alikuwa mgombea wa kiti cha uraisi.


“Kwenye uchaguzi nilipata kura zaidi ya milioni sita si haba, naomba wote walionipigia kura tumuunge mkono Rais John Magufuli.”-Lowassa

Mwanasiasa huyo Mkongwe nchini Tanzania, Edward Lowassa, mnamo mwaka 2015 alitangaza kujiengua ndani ya CCM na kujiunga na CHADEMA huku akiipeperusha Bendera ya  Chama hicho katika nafasi ya Urais na kushindwa na Mpinzani wake Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 10

Waziri Mkuu Awataka Agha Khan Wabadilishe Skeli Ya Mishahara.....Asema lengo ni kuondoa manung’uniko kwa watumishi wa taaluma moja

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, ameutaka uongozi wa Hospitali ya Aga Khan uandae skeli ya mishahara inayofanana kwa watumishi wenye taaluma zinazofafana ili kuondoa manung’uniko baina ya wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Ameyasema hayo kutokana na malalamiko ya watumishi wa taasisi hiyo ambao wanadai kuwepo kwa tofauti ya mishahara kwa watumishi licha ya kuwa na taaluma moja na kufanyakazi kwenye kituo kimoja.

Hayo yalisemwa jana (Jumamosi, Machi 9, 2019) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Waziri Mkuu alisema suala la maslahi kwa watumishi ni muhimu na linatiliwa mkazo na serikali hivyo uongozi wa Hospitali ya Aga Khan fanyeni mapitio ya mishahara hasa kwa watu walio katika taaluma zinazofanana.

“Serikali imeunda Tume ya Mishahara na Motisha inayofanya mapitio ya ngazi za mishahara ili kuondoa utofauti wa mishahara kwa watumishi waliosoma ngazi moja, wenye taaluma moja wanaofanyakazi kwenye kituo kimoja.”

Waziri Mkuu aliongeza kuwa suala la uwiano wa mishahara kwa watumishi wenye taaluma zinazofanana ni muhimu na linapaswa lifanywe kwa watumishi wote bila ya kujali kama mtumishi huyo ni Mtanzania au anatoka nje ya Tanzania.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma katika jengo hilo ikiwemo maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya watoto, wodi ya wazazi. Ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu sh. bilioni 192, kati yake sh. bilioni 134 ni mkopo wa muda mrefu wenye masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images