Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ruge Mutahaba Amezikwa Kishujaa Kijijini Kwao Kiziri, Bukoka

0
0
Aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amezikwa kishujaa na idadi kubwa ya watu wakiwemo viongozi wa serikali ngazi mbalimbali, wasanii, taasisis binafsi na watu wenye vipawa tofauti kutoka ndani ya mkoa wa Kagera na nje ya mkoa huo.

Mazishi hayo yamefanyika leo Machi 4 huko kijijini kwao Kiziru, Bukoba huku mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akiahidi kuendeleza mazuri yaliyoachwa na Ruge Mutahaba.

Ameyasema hayo katika viwanja vya Gymkhana Bukoba wakati wakiaga mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba na kisha kupumzishwa katika makao yake ya milele katika makaburi ya familia yaliyopo karibu na nyumba ya baba yake.

“Ruge alikuwa kinara wa mambo mengi mazuri alikuwa na talanta kubwa ya utunzi wa vipindi mbalimbali, Malkia wa nguvu, Kipepeo pamoja na Fursa ni baadhi ya vitu tutakavyo vienzi na kuviendeleza,” amesema Kusaga.

Mutahaba amefariki dunia Februari 26 Mwaka huu nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kusumbuliwa na figo kwa muda. Ameacha watoto watano wanne wa kiume na mmoja wa Kike.


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya March 5

Makamu wa Rais Awapongeza Wakulima Shinyanga

0
0
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wakulima wa mkoa wa Shinyanga kwa kuzalisha mazao ya biashara na chakula  kwa wingi na kufanya mkoa kuwa na chakula cha akiba kulinganisha na mikoa mingine.

Samia aliyabainisha hayo jana wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wilayani Kahama na kuelezea kufurahishwa kuona wakulima wengi mkoani Shinyanga wamejitokeza na kulima kwa wingi mazao ya chakula na biashara.

 Alisema mkoa wa Shinyanga kwa msimu wa kilimo uliopita, ulizalisha mazao ya biashara na chakula zaidi ya tani 500,000 na kuufanya kuwa na akiba ya chakula kingi cha kutosha.

Makamu wa Rais aliwataka wakulima mkoani hapa kuendelea kulima kwa wingi na kuuza mazao yao katika nchi za jirani na kuongeza kilimo kimekuwa kikiwanufaisha wakulima wengi na kimekuwa kikiingizia nchi fedha nyingi za kigeni.

Mbali na uzalishaji huo, aliwataka kukata bima za afya kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa pindi wanapouza mazao yao na kupata fedha. Alisema hali hiyo itawafanya kumudu gharama za matibabu na kusababisha hospitali kuwa na dawa za kutosha, kwa kuwa fedha za bima ya afya zinatumika kununuliwa dawa na vifaa tiba.

  Alisema kuwa, Wilaya ya Kahama ina zaidi ya kaya 49,437 kati ya hizo ni 9,000 pekee ndizo zilizokata bima ya afya ya CHF, huku kundi kubwa likibaki likitumia gharama kubwa za matibabu.

 "Ndugu zangu wakulima, kateni bima za afya ili kumudu gharama za matibabu pindi mnapofika hospitalini kupatiwa huduma. Kumbukeni mnakunywa bia ngapi? Ni kiasi gani cha fedha mnapeleka nyumba ndogo na kwa nini mnashindwa kukata bima za afya? Alihoji Samia.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Inocent Bashungwa, alisema kutokana na mkoa wa Shinyanga kulima mazao mengi ya kibiashara, serikali ina mkakati wa kujenga kiwanda kikubwa  cha usindikaji wa mazao Kanda ya Ziwa ili nchi za jirani za Rwanda, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrassi ya Congo zifike Kahama kununua mazao.

Alisema serikali imekuwa ikiwajali wakulima kwa kuwapelekea pembejeo kwa muda mwafaka ikiwa ni pamoja na kuwatafutia masoko ya kuuza mazao yao na kwamba kila mkulima ana wajibu wa kuuza mazao yake katika nchi za jirani ili kujiongezea kipato.

Serikali Kuendelea Kudhibiti Matumizi Ya Kemikali Nchini

0
0
Serikali itaendelea kusimamia na kudhibiti matumizi ya kemikali ili kuhakikisha hazileti madhara kwa afya za wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo alipokuwa kwenye mkutano na wadau wa kemikali kujadili namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ya kemikali nchini.

“Kemikali zisipodhibitiwa vizuri zinaweza kuleta madhara katika afya, mazingira pamoja na kuhatarisha usalama wa nchini, ipo haja ya kuweka mazingira mazuri ya kusimamia na kudhibiti uingizaji na matumizi ya kemikali nchini ili zisilete madhara” amesema Waziri Ummy.

Hata hivyo takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2014 zinaonyesha vifo milioni 12.6 vilitokana na mazingira duni ya kuishi, mojawapo ya kichocheo ni athari za kemikali ambazo zimekuwa zikisababisha magonjwa na vifo.

Waziri Ummy amesema kuwa kemikali zimekuwa na athari kubwa kwa binadamu kwa kusababisha magonjwa zaidi ya 100 huku akiyataja magonjwa ya moyo, saratani, ngozi, athari katika mifumo ya fahamu, upumaji pamoja na chakula kuathiri zaidi wananchi wengi.

“Tukubali kuwa kemikali zina madhara kwa wananchi lakini sasa tuwe na mazingira mazuri ya kuzidhibiti” amesema Waziri Ummy na kuendelea kusema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira mazuri kwa wafanya biashara ya kemikali nchini.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amezitaka Taasisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) kuangalia upya tozo wanazotoza kwa wafanyabiashara za kemikali nchini pamoja na kupunguza urasimu usiokuwa na ulazima ili kuwawekea mazingira rafiki wafanya biashara za kemikali.

“Msiwe ni kikwazo kwa uwekezaji na biashara, kikwazo cha kushamiri na kukua kwa uwekezaji nchini, nataka muwe mawakala wa kukuza biashara na uchumi nchini” amesema Waziri Ummy.

Awali akisoma taarifa yake Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema Sheria ya Kemikali ya mwaka 2003 imekuwa na mchango mkubwa katika udhibiti wa matumizi ya kemikali nchini.

“Kabla ya kutungwa kwa sheria hii, kemikali zilikuwa zikiingizwa nchini kiholela na kutumika bila ya kuwa na ufatiliaji au udhibiti wowote” alisema Dkt. Mafumiko.

Dkt. Mafumiko amesema Sheria ya kemikali imewawezesha kudhibiti usafirishaji, utumiaji pamoja uteketezaji wa taka zinazotokana na kemikali.

“Ofisi ya Mkemia inasimamia kwa ukaribu matumizi ya kemikali zote zinazoingizwa nchini kuanzia zinapoingia, mahali zinapokwenda pamoja na matumizi yaliyokusudiwa” alisema Dkt. Mafumiko.

Naye Katibu Mkuu wa Mawakala wa Forodha Tanzania Mhandisi Anthony Swai amesema tozo zimekuwa nyingi kiasi cha kuwaumiza wafanyabiashara wa kemikali huku urasimu pia ukisababisha wafanyabiashara kutumia muda mwingi kufuatilia vibali vya uingiza wa kemikali nchini.

Aidha Mhandisi Swai ameiomba Serikali kuainisha mipaka ya taasisi za umma pamoja na tozo wanatostahili kulipa kwani kumekuwa na mwingiliano wa majumuku baina ya taasisi za Serikali ambazo amezijata kuwa ni GCLA, TDFA na TBS (Shirika la Viwango Tanzania)

Lazaro Nyalandu: Sikuletwa CHADEMA na MAFURIKO

0
0
Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kurudi CCM akitokea Chadema, Mbunge wa zamani wa Singida Kaskazini ambaye kwa sasa ni kada wa Chadema, Lazaro Nyalandu amesema hakuletwa kwenye chama hicho na mafuriko.


Lowassa aliyerejea CCM wiki iliyopita alijiunga na Chadema Julai 28, 2015 na kupitishwa kugombea urais kupitia chama hicho akiwakilisha pia vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akiwa na kundi kubwa la wana CCM waliohama naye wakifahamika kama mafuriko.

Hata hivyo, Nyalandu aliyejitoa CCM Oktoba 30, 2017 na baadaye kujiunga na Chadema jana alitumia akaunti yake ya Twitter kuandika ujumbe unaoelezea  hatima yake ndani ya Chadema.

“Naamini katika kushiriki kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania kupitia upinzani. Tusikate tamaa. Kesho ni nzuri kuliko jana,” alisema Nyalandu katika ujumbe huo.

Watatu Wapandishwa kizimbani kwa unyang’anyi wa kutumia silaha

0
0
Watu wanne wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.
 
Waliopandishwa kortini ni Hamisi Mohamed (30), Mohamed Said (45), Alex Kyandarula (28) na Hamza Mohamed (24) wote wakazi wa Mbagala, Dar es Salaam.
 
Wakisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Frank Moshi, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Abudi Yusuph alidai kuwa Januari 29, mwaka huu eneo la Mbezi Makabe, Wilaya ya Ubungo, washtakiwa waliiba runinga moja aina ya Hisence yenye thamani ya Sh 2,300,000 mali ya Sayana Juma ambaye kabla na baada ya kuiba walimtishia kwa panga ili kuijipatia mali hiyo.
 
Aidha mahakama hiyo imemsomea shtaka la pili mtuhumiwa wa nne la kukutwa na mali ya wizi.
 
Akisoma shtaka hilo, mwendesha mashtaka alidai kuwa Februari 2, mwaka huu eneo la Mbagala Rangi Tatu, Wilaya ya Temeke, mshtakiwa alikutwa na runinga aina ya Hisence mali ya Sayana Juma ambayo ndiyo iliyoibwa huko Makabe.
 
Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa.
 
Hakimu Moshi alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa namba nne aliyetakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria ambao watatoa bondi ya Sh 500,000.
 
Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuachiwa huku washtakiwa watatu wakirudishwa rumande kutokana na shtaka lao kutokuwa na dhamana hadi kesi yao itakaposomwa tena Machi 18, mwaka huu.

Ahukumiwa Miaka 30 Jela kwa wizi wa kutumia silaha.

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Sande Teu mkazi wa Mtaa wa Mjimpya Kata ya Mpwapwa mjini ambaye ni mdogo wa Mbunge wa zamani wa Mpwapwa, Gregory Teu kwa kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha.
 
Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Mpwapwa, Pascal Mayumba na kuendeshwa na mwendesha mashitaka wa polisi, Stephen Masawa.
 
Hakimu Mayumba aliieleza mahakama kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa hilo siku ya Desemba 27, 2018 katika Kijiji cha Vighawe alimshambulia Bwana Meshack kwa kumpiga na vitu vizito kichwani ikiwemo nondo na rungu.
 
Hivyo kumsababishia majereha na maumivu mwilini mwake ikiwemo kichwani mikononi na miguuni na kumpora pikipiki.
 
Aidha, Hakimu Mayumba alisema bila halali mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na Sheria namba 287 (A) namba 16 ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
 
Pia alisema kesi hiyo iliyopewa nguvu na mashahidi wanane na vielelezo vilivyopelekwa mahakanani bila kuacha shaka yeyote mtuhumiwa alipatikana na hatia.
 
Katika utetezi wake mtuhuhumiwa alisema mambo yote yaliyozungumzwa mbele yake sio kweli.
 
Pia aliomba mahamakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana familia ya mke na watoto wanamtegemea.
 
Mwendesha mashitaka wa polisi, Stephen Masawa aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa kutokana na madhara ya wanayoyapata wahangawa wizi wa kutumia silaha na kuwataka vijana kupenda kufanya kazi kuliko kutegemea vitu vya wizi na utajiri wa haraka haraka.
 
Hakimu Mayumba aliambia mahakama kuwa,mtuhumiwa atafungwa kifungo cha miaka 30 jela kutokana na kupatikana na hatia na kutokana na ushahidi na vielelezo vilivyo wasilishwa mahakanani.
 
Alisema kwa yeyote ambaye hajaridhishwa na hukumu hiyo ana haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30.

Basi La BM Coach Lapinduka Likijaribu Kukikwepa Kichwa Cha Tren

0
0
Basi la Kampuni ya BM Coach limepata ajali ya kupinduka jana Jumatatu, Machi 4, 2019 majira ya alasiri wakati likijaribu kukwepa Kichwa cha Treni (Kiberenge) maeneo ya Chekelei wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akielezea kuwa dereva wa Basi la BM Coach, akitoka Arusha kuelekea Morogogo alishindwa kusimama katika kivuko cha Treni eneo la Chekelei Mombo, barabara kuu ya Segera/Same.

Ameongeza kuwa, wakati kichwa cha Treni kikikaribia eneo hilo na ndipo basi hilo likagongwa na kulala ubavu huku kichwa hicho cha Garimoshi kikiendelea na safari bila kusimama.

Hakuna taarifa ya vifo kwa sasa isipokuwa abiria kadhaa wamejeruhiwa akiwemo dereva wa BM Coach ambaye ameumia sana.

Tangaza Biashara Yako Au Bidhaa Yako Kwenye Mtandao huu Kwa BEI NZURI Kabisa

0
0

Tunakaribisha  matangazo  ya  aina  zote( Bishara, Viwanja, Bidhaa, matangazo ya Vyuo na mengine mengi)  .Bei  zetu  ni  nzuri  sana  na  kamwe  hutajuta  kutangaza  biashara  yako  kupitia  mtandao  huu....

Kwa Siku tunafunga na Pageviews zaidi  ya  laki tano kama graph  inavyoonyesha  hapo  chini
Kama  una  tangazo, basi  wasiliana  nasi   sasa.

Email  yetu:  mpekuziblog@gmail.com
Simu:     +255682493833 

Waziri wa Kilimo: Tumejipanga Kuimarisha Usambazaji Wa Pembejeo, Mbegu Bora Na Viuatilifu

0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mbeya
Uimarishaji wa mitandao ya usambazaji mbegu na viuatilifu ni muhimu katika kuhakikisha tija inaongezeka katika Uzalishaji wa mazao yote hususani nafaka, matunda mbogamboga na mbegu za mafuta.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 5 Machi 2019 wakati akizindua Mpango wa kuimarisha Mitandao ya Usambazaji wa Mbegu na Viuatilifu, Mpango unaotekelezwa na Mradi wa NAFAKA na Kampuni ya Kimataifa ya CORTEVA katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini nchini Tanzania.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Usungilo Hoteli Jijini Mbeya Mhe Hasunga alisema kuwa kuimarisha usambazaji mbegu na viuatilifu utamsaidia mkulima kuwa na uhakika wa chakula na kuongeza pato lake hivyo kuchangia katika kuipeleka Tanzania kufikia Uchumi wa Kati kama inavyoeleza sera ya Serikali ya awamu ya tano inayongozwa na Mhe Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Alisema wakulima nchini Tanzania wanategemea Sekta ya kilimo kuchangia katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi, kwa kuwa inatoa ajira kwa asilimia 65 ya wananchi, ina uwezo wa kutoa malighafi ya viwanda kwa asilimia 66 na inachangia asilimia 100 ya chakula kinachopatikana.

Alisema kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hiyo, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya II yaani Agricultural Sector Development Program - ASDP II inaolenga kuleta Mapinduzi katika sekta ya kilimo.

Programu hiyo ya miaka kumi (10) imeanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2018 na inafanyia kazi maeneo ya Usimamizi endelevu wa ardhi na maji, Kuongeza Tija (kuongeza matumizi ya pembejeo), Kuongeza masoko na kuongeza thamani ya mazao, Kuboresha mazingira ya uwekezaji katika kilimo. Hivyo, Uimarishaji wa Mpango wa Kusambaza Pembejeo na Viuatilifu ni moja ya shughuli muhimu katika Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo -ASDP 11 katika kuongeza tija.

“Ni Imani yangu kuwa, kufanikiwa kwa kazi hii ya Mradi wa Nafaka ni kufanikiwa katika utekelezaji wa sehemu ya Programu ya Kuendeleza Kilimo nchini ASDP II. Mradi huu pia utaendelea kuimarisha mahusiano yaliyopo baina na Serikali na Sekta nafsi katika kuendeleza kilimo nchini” Alisema

Kadhalika, Hasunga alisema Serikali inatambua mchango unaotolewa na Shirika la Misaada la Marekani USAID katika miradi mbalimbali husasani katika sekta ya kilimo. Mradi wa NAFAKA ni moja ya michango ya Shirika la USAID katika kuongeza tija kupitia Mashamba darasa, Uendeshaji wa Vikundi na vyama vya wakulima, Kuongeza thamani kwenye usindikaji wa Mahindi kwa njia ya virutubishi kwenye unga, Kuunganisha wakulima na huduma za kifedha Masoko na Bima ya Mazao yaani “Crop Insurance”.

Alisema kuwa Shughuli hizo zinazotekelezwa na Mradi wa NAFAKA kwa kushirikiana na CORTEVA  unaenda sambamba na jitihada za Wizara ya Kilimo katika kuendeleza kilimo. Moja ya maeneo ya kipaumbele yanayotekelezwa na Wizara ni kuongeza tija katika uzalishaji kwa kuimarisha upatikanaji wa pembejeo, na kuimarisha huduma za ugani.

Maeneo mengine ya Kipaumbele ya Wizara ya Kilimo ni Kutungwa kwa sheria ya kilimo ili kusimamia kilimo, Kuandikisha wakulima wote, Kuongeza uzalishaji wa sukari kuondoa upungufu wa sukari nchini, Kufungamanisha uzalishaji na mahitaji ya viwanda ili kutoa mali ghafi ya viwanda kwa kuongeza uzalishaji, Kuongeza uzalishaji wa mazao ya mafuta, Kuanzisha scheme za umwagiliaji ili kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji, Wakulima kuwa na bima ya mazao, na Kuongeza fursa za upatakanaji wa fedha kwa wakulima.

“Ni jambo la faraja kuona sekta binafsi sasa zinatoa mchango katika jitihada za Serikali katika kutoa mafunzo kwa wakulima kwa kuanzisha mashamba darasa, kutoa mafunzo kwa maafisa ugani, kusimamia na kuhimiza matumizi ya mbegu bora na viuatilifu pamoja na kufanya kazi na mawakala wa pembejeo wa daraja la kati na wadogo waliopo vijijini wapatao” Alikariirwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

“Ni jambo la kutia moyo kuwa mpango huu utasaidia usambazaji na upatikanaji wa viuatilifu vya kupambana na visumbufu vya mlipuko vikiwemo viwavi jeshi vamizi “Fall Army Worms” katika maeneo yaliyovamiwa kwenye Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini nchini mwetu”

Aidha, alisema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika kilimo ikiwa ni pamoja na kufanya mapitio katika taratibu zilizowekwa katika uzalishaji, usambazaji na uingizaji wa mbegu ili kurahisisha upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima nchini.

Katika suala la soko la mahindi Serikali imesharekebisha suala hil0 na itaendelea kutoa taarifa za hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha taratibu za masoko ya mazao ili wakulima, wafanyabiashara na wadau waweze kunufaika na uwekezaji katika sekta ya kilimo.

Sambamba na hayo pia Waziri Hasunga alisema kuwa serikali itaweka msisitizo katika sekta ndogo ya ardhi ili wakulima kuona umuhimu wake na kuondokana na kilimo kinachotegemea mvua.

MWISHO

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yaongeza Vituo Vipya 858 Vya Kupigia Kura

0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imeongeza vituo vya kupigia kura 858 kutoka 36,549 vya mwaka 2015  ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage  ameyasema hayo leo Jumanne Machi 5,2019 alipokuwa akizungumza na wawakilishi wa vyama vya siasa.

Mbali na kuongeza idadi ya vituo, Jaji Kaijage amesema vituo 6,208 vimebadilishwa majina na vituo 817 vimehamishwa kutoka kijiji/mtaa mmoja kwenda mwingine.

Kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura, Jaji Kaijage amesema mchakato wa kupata vifaa vya kukarabati machine za BVR umekamilika.

Rufaa ya Mbowe na Ester Matiko Kusikilizwa Kesho

0
0
Mahakama Kuu ya Tanzania kesho Machi 6,2019 inatarajia kuanza kusikiliza rufaa ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ya kupinga kufutiwa dhamana na Mahakama ya Kisutu.

Hatua hiyo inakuja baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kutupilia mbali pingamizi za Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ya kupinga mahakama hiyo kusikiliza rufaa hiyo, Machi 1, 2019.

Rufaa hiyo inatarajiwa kusikilizwa kesho mbele ya Jaji Sam Rumanyika ambapo alisimamisha kusikiliza rufaa hiyo kutokana na rufaa ya DPP.

Serikali Yapata Mkopo Wa Masharti Nafuu Kiasi Cha Shilingi Bilioni 589.26 Kutoka Benki Ya Maendeleo Ya Afrika (AfDB)

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James kulia akisaini mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wenye thamani ya Shilingi bilioni 589.26 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyowakilishwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini Dkt. Alex Mubiru (kushoto akisaini) katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) hapa nchini Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kutiliana saini mikataba miwili ya  mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Shilingi bilioni 589.26 itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.

TAKUKURU Yaomba Kumhoji Jamal Malinz

0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa mara ya pili, kumhoji aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa.

Ombi hilo limewasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali wa TAKUKURU, Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, baada ya shahidi wa 11 katika kesi hiyo kumaliza kutoa ushahidi wake.

Swai amedai kuwa Januari 16, 2019 waliomba kuwahoji washtakiwa hao, lakini hawakuweza kwa sababu walitoa sababu zao kuwa wahojiwe siku nyingine.

“Tunaomba tena kwenda kuwahoji washtakiwa, kwa sababu tayari Mahakama ilishatoa oda hiyo Januari 16, mwaka huu” Swai

Baada ya Swai kumaliza kuwasilisha, Hakimu Kasonde alikubaliana na ombi hilo na kutoa ruhusa kwa TAKUKURU kuwachukua kwa ajili ya mahojiano

Hakimu Kasonde alisema washtakiwa hao watahojiwa Machi 8, 2019 na kesi itaendelea kusikilizwa Machi 19,2019.

Mbali ya Malinzi na Mwesigwa, mshtakiwa mwingine ni Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga, Meneja wa ofisi ya TFF, Miriam Zayumba na Karani Flora Rauya, ambapo wanakabiliwa na mashtaka 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni USD, 375,418.

Taarifa: Kamati za Kudumu za Bunge Kuanza kukutana Jumatatu tarehe 11 hadi 31 Machi, 2019 Mjini Dodoma

0
0
Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza kukutana Jumatatu tarehe 11 hadi 31 Machi, 2019 Mjini Dodoma kutekeleza majukumu ya kibunge kabla ya Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 02 Aprili, 2019.  Kwa mujibu wa Ratiba ya Shughuli za Kamati, Waheshimiwa Wabunge wote wanapaswa kuwasili Mjini Dodoma Jumapili tarehe 10 Machi, 2019 tayari kwa ajili ya kuanza kwa vikao vya Kamati.

Shughuli zitakazotekelezwa na Kamati hizo ni pamoja na:

KUPOKEA WASILISHO LA SERIKALI KUHUSU KIWANGO CHA UKOMO WA BAJETI

Katika kipindi hicho cha vikao vya Kamati za Bunge, siku ya tarehe 12 Machi 2019, Wabunge watapokea Wasilisho la Mapendekezo ya Serikali kuhusu Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa mujibu wa Kanuni ya 97 ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016.

KUFANYA ZIARA ZA UKAGUZI WA MIRADI
Kamati zitafanya ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016. Kamati zitakagua miradi ya uwekezaji liyotekelezwa na Serikali kupitia Mashirika ya Umma.  Aidha, Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zitafanya ziara za ukaguzi wa miradi mingine iliyotekelezwa na Serikali ili kulinganisha matokeo ya utekelezaji na thamani halisi ya fedha za Umma zilizotumika katika miradi hiyo.

KUFANYA UCHAMBUZI WA BAJETI
Katika vikao hivyo pia Kamati zitafanya uchambuzi wa Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti za Wizara inazozisimamia kwa Mwaka wa Fedha unaoishia 2018/2019 kwa ajili ya kufanya ulinganisho kuhusu makadirio ya matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.

KUFANYA UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA UWEKEZAJI
Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) itafanya uchambuzi wa Taarifa za Uwekezaji uliofanywa na Serikali kupitia Mashirika ya Umma kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016.

UCHAMBUZI WA SHERIA NDOGO
Kamati ya Sheria Ndogo itafanya uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa Kumi na Nne Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 11 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016

Ratiba zote za Shughuli za Kamati za Bunge ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo Kamati hizo zitafanya ziara zinapatikana katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz. mara baada ya Kamati hizo kuanza kazi.

Imetolewa na:     Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa.

Ofisi ya Bunge
DODOMA
05 Machi, 2019

Waziri Mkuu Aongoza Mazishi Ya Imamu Wa Msikiti Wa Mtoro

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Machi 5, 2019) amewaongoza wakazi wa jijini la Dar es Salaam katika mazishi ya Imamu wa Msikiti wa Mtoro Sheikh Zubeir Yahya Mussa yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu.

Sheikh Zubeir ambaye ni miongoni mwa masheikh maarufu jijini Dar es salaam alifahamika sana kutokana na kuwa Imamu wa msikiti huo, ambao ni miongoni mwa misikiti mikubwa na maarufu zaidi hapa nchini, alifariki dunia jana usiku.

Pamoja na Uimamu wake, Sheikh Zubeir aliwavutia watu wengi sana kutokana na darasa zake alizokuwa akiziendesha kwa ufundi mkubwa katika msikiti huo wa Mtoro na maeneo mengine.

Sheikh Zubeir alikuwa miongoni mwa masheikh waliojiweka karibu sana na jamii na kuwa na uhusiano mzuri na masheikh wenzake kutoka taasisi mbalimbali.

Sheikh Zubeir alipata elimu yake ya juu katika chuo kikuu cha Madina, (Ummul- Quraa) akiwa pamoja na Sheikh Juma Omar Poli, Sheikh Muharram Juma Doga, Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir na wengineo.

 Baadhi ya viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba.

Wengine ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Abuu Jumaa, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Wafungwa na Mahabusu 340 Wakutwa na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi

0
0
Jumla ya wafungwa na mahabusu 15,250 nchini wamepima Virusi vya Ukimwi huku 340 wakikutwa na maambukizi baada ya Jeshi la Magereza wakishikiana na Wizara ya  Afya  kutoa elimu ya Upimaji katika Magereza mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akiwasilisha Taarifa Kuhusu Hali ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Upatikanaji wa Tiba ya Magonjwa Nyemelezi na Udhibiti wa Biashara na Matumizi ya Dawa za Kulevya Magerezani kwa mwaka ulioisha.

Akisoma taarifa  hiyo  mbele  ya  Kamati  ya  Kudumu  ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI iliyofika katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira mkoani Morogoro, Naibu Waziri Masauni alisema kati ya mahabusu na wafungwa waliopima wanaume waliokutwa na maambukizi ni 292 na wanawake ni 48

“Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Afya wanahakikisha huduma za afya zinaboreka magerezani ikiwemo lishe nzuri kwa  wanaothibitika wana maambukizi huku jumla ya wafungwa na mahabusu wanaotumia dawa za kufubaza  makali wakiwa 1,496” alisema Naibu Waziri Masauni

“.. elimu ya kifua kikuu na upimaji inatolewa kila siku Magerezani kwa wafungwa na mahabusu, kwa mwaka jana jumla ya waliopima ni 12,870 huku waliobainika na maambukizi ni 167 na tunashirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kwa kuandaa Mpango Mkakati wa UKIMWI na kifua Kikuu kwa miaka mitano.” Aliongeza Masauni

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kuwatembelea wafungwa katika Gereza la Kingolwira  Wajumbe wa  Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI , walilipongeza Jeshi la Magereza kwa kuwahudumia mahabusu na wafungwa wanaoishi na maambukizi magerezani huku wakitoa wito kwa wafungwa walioathirika kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao kuhusiana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Akizungumza mbele ya kamati hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Afya na Lishe wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Dkt.Hassan Mkwiche alisema magereza yana utaratibu wa kupima afya za mahabusu au wafungwa siku ya kwanza tu anayoingia gerezani  ikiwemo ujauzito, Ukimwi, kifua kikuu na magonjwa mengine ili waweze kuhudumia kila mfungwa na mahitaji yake.

“Mfungwa anapoingia humu anaenda kukutana na kazi mbalimbali kwahiyo ni muhimu kujua afya ya kila mmoja tangu siku ya kwanza anaingia ili kuweza kumpangia majukumu kulingana na afya yake lakini pia aina ya mlo anaotakiwa ale akiwa kifungoni” alisema Dkt. Mkwiche.

Juhudi mbalimbali za kuboresha afya za wafungwa magerezani  zinaendelea huku Wizara ikiendelea  kuboresha vituo vya kutoa huduma za afya ambapo mwaka 2018 zahanati ya Gereza Mahabusu mkoani Morogoro ilikamilika na imeshaanza kufanya kazi huku gharama za ujenzi zikiwa ni fedha za ndani za serikali.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano March 6

Viwanja vinauzwa Mapinga (Baobab Sec)........Surveyed plots for sale: Mapinga (Baobab)

0
0
Surveyed plots for sale: Mapinga (Baobab)
Viwanja vinauzwa Mapinga (Baobab Sec), viko umbali wa km 2 kutoka main road (Dar to Bagamoyo Road). Viwanja vina miundombinu yote ya barabara za uhakika, maji na umeme.
 
Bei ya kila sqm ni tsh 13,000 na vipo viwanja vya sqm 500 kwa bei ya tsh 6,500,000/=, sqm 600 bei yake tsh 7,800,000/=, sqm 800 bei yake tsh 10,400,000/=, Nusu eka (sqm 2000) bei yake milion 24 na eka nzima (sqm 4000) bei yake milion 48

Viwanja vyote vinafaa kwa Makazi, Biashara na Ufugaji.
Luksa kulipa kwa awamu 2, awamu ya kwanza ni 75% na awamu ya pili ni 25% ambayo inalipwa baada/ndani ya miezi 3 (mitatu).
 
Ukipata ujumbe huu mjulishe Ndugu/jamaa/rafiki mwenye uhitaji wa Viwanja.
 
Mhusika anaitwa mr. H. Kajumulo, mpigie 0758603077 whatsap 0757489709

Taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu gharama za leseni kwa wasafirishaji wa vifurushi, vipeto na nyaraka.

0
0
Taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu gharama za leseni kwa wasafirishaji wa vifurushi, vipeto na nyaraka.

Jana Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Atashasta Nditiye alipiga marufuku magari yote ya abiria kusafirisha vifurushi vya aina yoyote ile, pasi na kuwa kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA). 

Katika kudhibiti vitendo hivyo, waziri huyo ameagiza SUMATRA kuendesha operesheni kubaini wanaokaidi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images