Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

PICHA: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mke Wake Wafika Nyumbani kwa Ruge Mutahaba Kutoa Pole na kuwafariji wafiwa.

$
0
0
Rais Mstaafu Dr. Jakaya Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete leo wamefika nyumbani kwa Prof. Mutahaba ambaye ni baba mzazi wa Ruge Mutahaba aliyekuwa mkurugenzi wa uzalishaji vipindi wa Clouds Media Group kutoa pole na kuwafariji wafiwa.

Ruge Mutahaba Alifariki dunia Juzi nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu ya figo zilizoanza kumsumbua mwaka jana.


BREAKING: Mkutano wa Trump na Kim Jong Un wavunjika, Hakuna Makubaliano Yoyote Yaliyofikiwa

$
0
0
Katika hali ambayo haikutegemewa, Mkutano kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un umevunjika.

Mkutano wa siku mbili kati ya viongozi hao waliokutana nchini Vietnam umelazimika kuahirishwa baada ya kutofautiana katika masuala ya msingi, hivyo hawakufikia lengo la kutia saini nyaraka zozote.

Waandishi wa habari walishangazwa na taarifa ya kuahirishwa kwa chakula cha mchana kati ya viongozi hao ambacho walitarajia kushiriki kuchukua matukio.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema  kwamba alitoka kwenye mkutano huo kwasababu ya masharti yasiyowezekana ya kiongozi hiyo ya kutaka nchi yake iondolewe vikwazo ilivyowekewa kwa uchochezi wa Marekani.

“Ndoto yetu na ndoto yao havikushabihiana. Wao walitaka kuondolewa vikwazo katika maeneo yote, na hatukuweza,” alisema Trump.

“Hatujakata tamaa, kuna uwezekano. Anataka kuachana na silaha za nyuklia, [Kim] anataka kufanya kwenye maeneo ambayo yana umuhimu kidogo kuliko tunavyotaka. Wakati mwingine inabidi kuondoka na wakati huo ulikuwa leo,” aliongeza.

Hata hivyo, Trump amemuelezea Kim kama kiongozi mzuri na kwamba anaamini wakati mwingine watafikia muafaka. Amesema ingawa mkutano huo haukuzaa matunda yaliyotarajiwa, kuna hatua ambazo zimepigwa kulinganisha na ilivyokuwa awali.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amewaambia waandishi wa habari kuwa katika makubaliano ya awali walibaini kuwa hakukuwa na kitu ambacho kingeifaidisha ipasavyo Marekani.

Amesema timu ya nchi hizo mbili itakutana tena kuendelea kujadiliana kwa mara nyingine ili wafikie muafaka.

Serikali Yatangaza Ajira Mpya 4,549 Za Walimu

$
0
0
Na.Alex Sonna/Fullshangwe
Serikali  imetangaza  nafasi za ajira 4,549 za walimu wa shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2018/19 ili kupunguza uhaba wa walimu ulipo nchini.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,amesema Serikali inajua kuwa kuna changamoto nyingi katika sekta ya elimu nchini hasa uhaba wa walimu hivyo itaajiri walimu ili kupunguza uhaba uliopo.
 
Hata hivyo Jafo amesema kuwa  ajira hizo mpya  kwa waombaji zinapaswa kuombwa kwa njia ya mtandao na mwisho wa kupokea maombi utakuwa Machi 15, mwaka huu.

”Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli inaendelea kuongeza idadi ya watumishi katika sekta ya umma kwa kutoa nafasi mbalimbali za ajira kwa vijana wa kitanzania katika sekta ya Elimu”amesema Jafo
 
Waziri Jafo amesema kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi inawatangazia walimu wenye sifa hizo kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao (Online Teacher Employment Application System-OTEAS).
 
Jafo amesema kuwa  kwa walimu wa shule za msingi wanaotakiwa kutuma maombi ni wenye sifa za kitaaluma Daraja la IIIA wenye Astashahada ya ualimu, na wenye daraja la IIIB wenye Stashada (Diploma ya ualimu katika masomo ya Kingereza, Uraia, Historia, Jiografia na kiswahili.
 
Aliongeza kuwa walimu  wenye sifa ya Daraja la IIIC wenye shahada ya ualimu kwa masomo ya Kingereza,Uraia,somo la ziada,Historia,Geographia na Kiswahili.
 
Jafo ametangaza  kundi jingine lenye sifa ni Mwalimu mwenye Daraja la IIIC na mwenye mahitaji maalum aliyehitimu Shahada kwa masomo ya English,Uraia,somo la ziada,Historia,Geographia na kiswahili.
 
Kwa walimu wa sekondari  Waziri Jafo amesema kuwa wao  wanaotakiwa kufanya maombi ni Mwalimu wenye Daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu aliyesomea Elimu maalum.
 
Jafo amesema wengine ni wenye Daraja la IIIB wenye Stashahada (Diploma) ya ualimu waliosomea Elimu maalum na mwalimu Daraja la IIIB mwenye Stashahada ya ualimu somo la Mathematics, Biology, Physics,na Chemistry.
 
Amesema wengine wenye sifa za kuomba ni mwalimu daraja la IIIC mwenye shahada ya ualimu somo la Agriculture Science, na mwalimu wa Daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu somo la Home Economics na mwalimu Daraja IIIC mwenye Shahada ya ualimu somo la Physics, Mathematics, Chemistry na Biology.
 
Aidha Jafo ameongeza  kuwa walimu wengine ni  wa Daraja IIIC wenye shahada ya ualimu somo la Book keeping, Commerce, Accounts na Economics na mwalimu daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu somo la English, Civics na General Studies.
 
Hata hivyo Jafo amesisitiza kuwa waombaji wenye sifa zote hizo wanatakiwa kuwa watanzania, wawe wamehitimu kati ya mwaka 2014 hadi 2017 isipokuwa kwa kundi maalum la wahitimu wa elimu ya ualaimu wa masomo ya Fizikia na Hisabati.
 
Jafo amesema kuwa sifa nyingine ya jumla kwa muombaji asiwe na umri zaidi ya miaka 45, na wakati wa kutuma maombi walimu ambao waliwahi kutuma na hawajaajiriwa wanapaswa kutuma upya.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Maduka Ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa kawaida wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni jijini Dar es Salaam na kubaini kwamba maduka mengi yanaendesha biashara hiyo pasipo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni.

Kufuatia ukaguzi huo, Benki Kuu ya Tanzania imeanza utaratibu wa kufuta leseni za maduka yote yaliyokutwa yanaendesha biashara hiyo bila kuzingatia masharti ya leseni. Zoezi hili linaendelea.

Mnamo mwezi Desemba mwaka 2018, Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni nchini kote na kubaini kuwa mengi hayakidhi matakwa ya kisheria ya biashara hiyo. Hivyo, iliyaandikia maduka hayo kuyataka kutoa maelezo kwa nini yasifutiwe leseni kutokana na ukiukaji huo. Hatua zilizochukuliwa jana zinatokana na tathmini ya taarifa ambazo Benki Kuu ya Tanzania ilizipokea kutoka kwa waendeshaji wa maduka hayo.

Aidha, kama ilivyoelezwa katika taarifa za Benki Kuu ya Tanzania za mwezi Novemba 2018 na tarehe 31 Januari 2019, huduma za kubadilisha fedha za kigeni zinaendelea kupatikana katika mabenki na taasisi za fedha nchini kote pamoja na maduka ya fedha za kigeni ya Shirika la Posta Tanzania (TPC).

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutahadharisha umma kutotumia huduma zisizo rasmi za ubadilishaji wa fedha za kigeni kutokana na hatari mbalimbali, ikiwemo kuibiwa au kupewa fedha bandia. Aidha, utumiaji wa huduma zisizo rasmi ni kinyume cha sheria za nchi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watoaji na watumiaji wa huduma zisizo halali (black-market).

=================

Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Kijaji Ashitukia Gharama Za Mradi Wa Ukarabati Wa Shule Ya Sekondari Mzumbe Mkoani Morogoro

$
0
0
Na Peter Haule, WFM, Morogoro
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amuagiza uongozi wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuuchunguza mkataba wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya Wavulana-Mzumbe, ulioingiwa kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Shirika la Nyumba la Taifa-NHC ili kujiridhisha kuhusu gharama halisi za mradi baada ya kubaini kiasi kinachodaiwa kutumika kukarabati shule hiyo kinatofautiana na fedha halisi zilizotolewa na Serikali

Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo alipotembelea na kufanya ukaguzi wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya wavulana ya Mzumbe iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro na kuelezwa na viongozi wa wilaya hiyo akiwemoo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kutokuwa na taarifa zozote kuhusu mradi huo.

Dkt. Kijaji alishangazwa na utofauti wa kiwango cha fedha kilichoainishwa katika taarifa ya gharama ya ukarabati wa shule hiyo kwamba ilikuwa shilingi milioni 999.7 wakati kiasi cha fedha kilichotolewa na Serikali ni zaidi ya shilingi bilioni 1.

Alitoa wito kwa wakuu wa wilaya kote nchini kufuatilia kwa karibu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili kujiridhisha kuhusu fedha zinazotumika kwenye miradi hiyo, kukagua thamani ya fedha kwenye miadi husika, pamoja na mikataba yote inayohusika ili kujua mawanda (scope) ya miradi hiyo

"Kila anayekuja kutekeleza miradi katika Wilaya ni vema akaulizwa amekuja kufanya nini na kwa namna gani kwa kuwa lengo ni kuwasaidia wananchi wa maeneo husika na Taifa kwa ujumla na hakuna siri kwenye miradi hiyo kwa hiyo ni lazima muijue kwa undani" alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa,  Shule Kongwe ya Mzumbe imekarabatiwa na mabadiliko yanaonekana lakini ni vigumu kujua ilitakiwa kukarabatiwa kwa kiwango kipi na maeneo gani kwa kuwa wahusika wakiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na Mkuu wa Shule hiyo hawafahamu mawanda ya mradi huo.

"Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero hakikisheni mnapata mkataba wa ukarabati wa shule hii ili kupata uhakika wa nini kilitakiwa kifanyike kwa kuwa bado maeneo mengi hayajakarabatiwa na Mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa lakini tayari amekabidhi kazi" alisisitiza Dkt Kijaji.

“Dhamana ya Wizara ya Fedha na Mipango ni kutafuta fedha, kupeleka maeneo husika kwa ajili kubadili maisha ya watanzania na kukagua matumizi yake, hivyo hali hiyo iliyojitokeza inaenda kufanyiwa kazi kwa lengo la kuongeza ushirikiano”, alieleza Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kyombo, aliishauri Serikali kuona namna bora ya kuboresha ushirikiano wakati wa utekelezaji wa miradi kama hiyo kuanzia kwenye upembuzi yakinifu wa majengo yanayokarabatiwa, nini kikarabatiwe, wakati gani, na kuwahusisha wataalam wa wilaya wakati wa kukagua na kutathimini kazi iliyofanyika kabla ya mkandarasi kulipwa

Naye Mkuu wa Shule hiyo Kongwe ya Mzumbe Bw.Wal Kihongosi, aliishukuru Serikali kwa hatua yake ya kuboresha shule hiyo ya vipaji maalum kwa kuwa hapo awali mazingira yake yalikua hayasadifu hadhi ya kuwa na wanafunzi wenye vipaji.

Pia akaiomba Serikali kusaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi, kuongeza vifaa vya maabara kwa kuwa havitoshi, kujengewa jengo moja jipya kwa ajili ya ofisi ya taaluma pamoja na idara zake tisa  na pia kuongeza idadi ya watumishi wakiwemo wapishi na walinzi walioajiriwa wa muda mrefu badala ya waliopo ambao ni wa mkataba wa mda mfupi ambao udhibiti wake kulingana na unyeti wa kazi hizo ni mgumu.

Mwisho

Kaburi la Ruge Mutahaba Laanza Kuandaliwa

$
0
0
Maandalizi ya kumzika marehemu Ruge Mutahaba katika kijiji cha Kiziru Wilaya ya Bukoba yamepamba moto na ujenzi wa kaburi umeanza leo.
 

Siperatus Mbeikya ambaye ni mmoja wa wanafamilia amesema taratibu zinaendelea ikiwa ni pamoja na kupokea wageni kutokana maeneo mbalimbali.

Pia, amesema maandalizi hayo yamekwenda sambamba na kukubaliana na kikosi cha usalama barabarani sehemu utakapopita msafara wenye mwili wa marehemu Ruge.

Pilikapilika zimeongezeka katika eneo la msiba ikiwa ni pamoja na kumwaga vifusi kwenye maeneo korofi.


Marehemu Ruge anatarajiwa kuzikwa Jumatatu, wakati  mwili wake utawasili Dar es Salaam kesho Ijumaa na kuagwa Jumamosi.

Watu 7 Wafikishwa Mahakamani Mauaji ya Watoto Njombe

$
0
0
Na Amiri kilagalila Njombe
Watu saba wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe  kwa tuhuma za mauaji ya watoto mkoani Njombe yanayohusishwa na imani za kishirikina.

Mmoja wa watuhumiwa hao ni David Kasila ambaye alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe februari 18 mwaka huu akituhumiwa kuwaua watoto watatu ambao ni Oliver Ng’ahala(5),Goodluck Mfugale(5)Meshack Myonga(4) wote ni wakazi wa wilaya ya Njombe.

Watuhumiwa wengine ni Mariano Malekela,Edwini Malekela,kalistus Costa wakazi kijiji cha Matembwe tarafa ya Lupembe walifikishwa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe mnamo februari 19 mwaka huu kwa tuhuma za kumuua mtoto wao Rachel Malekela(7) februari moja mwaka huu ambapo mwili wake ulikutwa mita 50 kutoka nyumbani kwao akiwa amechinjwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Renata Mzinga,alisema kati ya watuhumiwa 49 waliokuwa wakishikiliwa na jeshi la polisi baada upelelezi watuhumiwa saba pekee ndio walikutwa na hatia na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo.

‘’Hata hivyo oparesheni zetu ziliendelea hadi tulipofika mikoa jirani ya Mbeya,Iringa na hata Songea ambako tuliweza kuwapata watu mbalimbali pamoja na msako wetu tuliendelea kuwakamata waganga wa jadi na hasa wale wapiga ramli chonganishi ambao waliweza kuchochea chuki katika mkoa wetu’’alisema Renata.

Alisema jeshi la Polisi  limewafikisha mahakamani watu saba,watatu kwa tukio la mauaji ya watoto watatu kijiji cha Ikando,mtuhumiwa mmoja kwa mauaji ya watoto watatu mjini Njombe,na watuhumiwa watatu kwa mauaji ya mtoto mmoja kijiji cha Matembwe.

Alisema kutokakana na oparesheni iliyofanyika wanaendelea kuwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za mtu yoyote atakaebainika na kuwa na dalili zozote za kujihusisha kwenye mauaji hayo.

‘’Tunaomba wananchi waendelee kutuletea taarifa ambazo ni za kweli. taarifa ambazo zitaweza kutusaidia sio taarifa za fitina au za kukomoa watu wakidai kuwa wanajihusisha na matukio haya kwa mfano wananchi wanaotuletea taarifa za maandishi wakieleza kuwa kuna matumizi ya gari namba zimehifadhiwa,kuna watu walioshuhudia majina yamehifadhiwa kuna gereji zinazotumika kuficha waalifu jina la gereji limehifadhiwa hapo itatuletea ugumu  sisi polisi kukamilisha upelelezi wetu’’alisema.

‘’Tunaomba taarifa za kueleweka ili kuweza kukomesha mauaji haya moja kwa moja sio taarifa ambazo zinaeleza majina yamehifadhiwa,sisi tunazichukulia kama taarifa za majungu ambazo hazina utafiti wowote na haziwezi kutuletea mafanikio.pia wananchi waendelee kutuletea taarifa za waganga wa jadi hasa wale wapiga ramli chonganishi ili tuwakamate na kuwafikisha mahakamani’’alisema Renata.

Pia Kamanda huyo amewataka wazazi na walimu kuendelea kushirikiana kuwalea watoto sambamba na kuwaasa wananchi waache kuamini imani za kishirikina na badala yake wafanye shughuli halali ili waweze kuhakikisha jamii inakuwa salama.

Kamanda Mzinga alisema wananchi wazingatie taratibu za kisheria kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi na wafuate taratibu za mirathi ili kuepuka kufanya mgawanyo wa mali kwa kutumia ubabe na visasi.

Aidha jeshi la polisi  mkoa wa Njombe linaendelea na upelelezi juu ya mtoto Gaudes Kihombo(7) mkazi wa kijiji cha Ikando kata ya Kichiwa aliyepotea tangu Januari sita ambaye hadi sasa hajapatikana.

Mpaka sasa watuhumiwa saba wamefikishwa mahakama ya hakimu mkoa wa Njombe kwa matukio ya mauaji ya watoto nane wakiwemo wa familia moja.

Waziri Mwakyembe Amlilia Ruge Mutahaba


Waziri Mkuu Atembelea Hispitali ya Rufaa Temeke na Mwananyamala....Wananchi Waimwagia Sifa Serikali

$
0
0
WANANCHI wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwabana watumishi wa umma, kwa sababu uamuzi huo umezaa matunda na sasa hali ya utoaji wa huduma katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya hospitali yameimarika.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumatano, Februari 27, 2019) na wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hospitali hapo.

“Huduma zimeimarishwa dawa tunapata, hakuna lugha chafu wala kuombwa rushwa. Tunahudumiwa vizuri na kuna wakati hadi tunabembelezwa kunywa dawa mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo, hivyo tunaishikuru Serikali.”

Mmoja wa wagonjwa hao ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi hospitalini hapo baada ya kujifungua, Mwajuma Mohammed amesema baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani na kuwabana watumishi wa umma sasa kuna mabadiliko makubwa sana ya kiutendaji.

Amesema zamani baadhi ya wauguzi hususani wanaofanyakazi kwenye wodi ya wazazi hawakuwa na lugha nzuri walikuwa wakiwatukana na kuwakashifu jambo ambalo kwa sasa halipo, kwani wakifika wapokelewa vizuri.

Mama mwingine aliyelazwa kwenye wodi hiyo, Crista Moyo amemuomba Waziri Mkuu kuisadia hospitali hiyo kwa kuiongezea watumishi kwa kuwa walipo ni wachache ukilinganisha na idadi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kila siku.

Crista ameishauri Serikali ikiwezekana iajiri hata watu wasiokuwa na taaluma ya udaktari au uuguzi ili wakafanyekazi ambazo hazihitaji ujuzi kama za  kuwasaidia wagojwa kutoka eneo moja kwenda lingine.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amezishauri Halmashauri jijini Dar es Salaam zihakikishe zinaendelea kuimarisha vituo vya afya na kuongeza vingine ili utoaji kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa.

Pia ameshauri ianzishwe miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika hospitali hizo kwa lengo ya kuwezesha utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za dharura kwa wakati.

“Rais Dkt. Magufuli anataka wananchi wapate huduma za afya karibu na  makazi yao ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo. Ndio maana tunajenga vituo vya afya vilivyokamilika vinavyotoa huduma zote muhimu kama maabara, upasuaji na mama na mtoto.”

Waziri Mkuu amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua utoaji wa huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hizo na kubaini kama kuna changamoto ili Serikali iweze kuzitambua na kuzitafutia ufumbuzi.

“Tumesikia changamoto zinazowakabili madaktari, tumezichukua na tutazifanyia kazi ikiwepo ya upungufu wa watumishi mbalimbali kama madaktari na wauguzi ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wananchi.”

Waziri Mkuu amesema dhamira ya dhati ya Serikali kwao ni ya kuwatumikia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote, hivyo waendelee kuwa wazalendo na washirikiane na Serikali yao. Wafanye kazi kwa bidii.

Naye,Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Amaani Malima amesema hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa nje 1,800 hadi 2,000 kwa siku na wagonjwa wa ndani 250 hadi 300. Wagonjwa hao watoka wilaya mbalimbali.

Dkt. Malima amesema hospitali hiyo ina jumla ya watumishi 439 kati yao madaktari bingwa ni 16, madaktari 76 na wauguzi 209 na watumishi wengine 138. “Idadi hii ni ndogo kulingana na mahitaji ya hospitali kwani tuna upungufu wa watumishi 278 sawa na asilimia 39.”

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa  dawa muhimu kwenye hospitali hiyo, Dkt. Malima amesema kwa kipindi cha Januari upatikanaji ulikuwa wa kuridhisha kwa asilimia 85 ya kiasi cha dawa na vifaa tiba vilivyohitajika.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala ambapo alikagua mradi wa ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa mashuhuri ambalo lilianza tangu mwaka 2014 na bado halijakamilika.

Hivyo, ameishauri Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuangalia namna ya kuweza kusaidia ujenzi wa jengo hilo ili mradi huo uweze kukamilika na hatimaye huduma zilizokusudiwa kutolewa katika jengo ziweze kufanyika.

Pia, Waziri Mkuu amewataka Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Daniel Nkungu na Kiongozi wa Wauguzi, Wambura wahakikishe wanaimarisha ushirikiano wao na hata wanapotoa maagizo kwa wasaidizi wao wawe wanataarifiana.

Kwa upande wa watumishi wanaofanya kazi katika idara za maabara amewataka wawe wanawahi kutoa huduma kwa sababu kuna malalamiko ya ucheleweshwaji wa huduma katika eneo hilo.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watumishi wanaofanya kazi katika kitengo cha radiolojia kwenye hospitali za Rufaa za Mkoa za Mwananyamala na Temeke jijini Dar es Salaam waache urasimu na wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 1

Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) Lasitisha usajili wa Msanii Godfrey Tumaini (Dudubaya)

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) limesitisha usajili wa Msanii Godfrey Tumaini(Dudubaya),kuanzia jana Alhamisi, 28 Feb 2019 . 

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya msanii huyo kukamatwa na jeshi la polisi, kutokana na kutoa kauli zisizofaa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Ruge

Waziri Mkuu Akutana Na Wafanyabiashara Dar Es Salaam ....Awataka Wasikubali Kutoa Rushwa Kwa Chombo Chochote

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa kati na wadogo wa Kariakoo ambapo amewataka wasikubali kutoa rushwa kwa chombo chochote.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inapiga vita vitendo vya rushwa, hivyo wakiona kuna mazingira ya rushwa watoe taarifa kwani rushwa ni adui wa haki.

Waziri Mkuu amekutana na wafanyabiashara hao JANA (Alhamisi, Februari 28, 2019) katika ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es Salaam. Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imepata mafanikio makubwa baada ya kupiga vita rushwa.

“Rushwa si sehemu ya mkakati wa Serikali, hivyo vita dhidi ya rushwa lazima iendelezwe na watu wote. Mafanikio tuliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa huduma za afya ni matokeo ya kupiga vita rushwa.”

Pia, Waziri Mkuu amewataka watumishi wawe na tabia ya kuwatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao na kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzitafutia ufumbuzi.

“Kila mtendaji katika eneo lake atekeleze majukumu yake kikamilifu Urasimu, dharau, lugha za ajabu zimeshamiri kwenye maeneo ya kutolea huduma jambo ambalo si sahihi. Badilikeni.”

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali imepanga mpango wa kulibadilisha utaratibu wa kufanya biashara katika eneo la Kariakoo ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa saa 24 kama yalivyo masoko makubwa duniani.

Waziri Mkuu amesema lengo la madiliko hayo ni kukuza uchumi wa Taifa na wa wafanyabiashara kwa ujumla. “Nchi yetu ina usalama na ulinzi wa kutosha hivyo hatuwezi kushindwa kufanya biasahara wakati wote.

Katika mkutano huo alioutisha kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao, Waziri Mkuu amesema kesho atakutana na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam ili kupanga namna ya kutekeleza mpango huo.

Waziri Mkuu amesema jiji la  Dar es Salaam ndio jiji la kibiashara nchini, hivyo Serikali inataka kuhakikisha mwenendo wa biashara unaboreshwa pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kufanyabiashara zao wakati wote.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu  amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsiia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuhusu ziunganisha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Waziri Mkuu amesema TFDA na TBS zinafanya kazi ambazo zinafafa hivyo Mawaziri hao wakutane na wafanye mapitio ya kazi za mamlaka hizo na waandae muswada kuunganisha mamlaka hizo na kuuwasilisha bungeni.

Amesema mamlaka hizo zikiunganishwa zitaweza kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakilalamikia kuwepo kwa tozo nyingi na urasimu unasababisha Taifa kupoteza makundi makubwa ya wafanyabiashara na wateja.

Waziri Mkuu amesema mamlaka hizo zimekuwa zikitumia muda mrefu kwa ajili ya kupima bidhaa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara. “Sijui mnatumia kemikali gani ambazo zinachelewesha majibu. Na sasa TBS napima hadi stuli na mashati na mnapoona havina ubora hamuwarudishii wenyewe.”

Amesema kuna mwananchi mmoja aliagiza madirisha na bidhaa nyingine kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake akaamiwa havina ubora. Kila taasisi ifanyekazi yake kwa mujibu wa sheria na waache uonevu na kuomba rushwa.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Mkuu Aridhishwa Na Hatua Za Ujenzi Wa Teminarl III katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.
 
Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo jana (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.

Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha  taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95.

Mhandisi huyo alisema tayari wamefanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa mbalimbali na kwamba mkandarasi anatarajia kukabidhi mradi huo Mei 31 mwaka huu. Jengo hilo linauwezo kubeba abiria milioni sita.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao. 

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari. 

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume. 

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa. 

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo nchi 3-8 na unene cm 2-5,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji :Hii ni tiba tofauti kabisa nazile ambazo umekwisha wahi kutumia. 

Pia tunadawa za , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono pamoja na mvuto wa mpenzi.

 DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Akabidhi Kompyuta 25 Ludewa Kuongeza Kiwango Cha Ufaulu Shule Za Sekondari

$
0
0
Na Amiri Kilagalila
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amegawa kompyuta 25 kwa shule za sekondari za Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe zenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kujifunzia na waalimu kufundishia, kuongeza uelewa na kupata maarifa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuunganisha kompyuta hizo na mtandao wa intaneti ili kuwawezesha wanafunzi wa Wilaya hiyo kuongeza kiwango cha ufaulu

Nditiye amekabidhi kompyuta hizo kwa Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Ludewa ili ziweze kutumika kwenye shule mbali mbali zilizopo Wilayani humo

“Nimeleta kompyuta 25 ili zigawiwe kwenye shule mbalimbali ili watoto wajifunze kutumia TEHAMA pamoja na waalimu waliopewa mafunzo ya TEHAMA na taasisi yetu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)”, amesema Nditiye. 

Kompyuta hizo zimetolewa na UCSAF ambayo inahusika na ufikishaji wa huduma za mawasiliano vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara

Nditiye ameongeza kuwa Wilaya ya Ludewa inafahamika katika kipindi cha miaka ya nyuma kwa kuwa moja ya Wilaya saba nchini ambapo wanafunzi wake wana kipaji cha akili ukilinganisha na Wilaya nyingine zilizopo nchini ambapo ameona ni vema kuwapatia wanafunzi wa shule za Wilaya hiyo kompyuta hizo ili waweze kuongeza ufaulu, kujenga uelewa na kupata maarifa ili waweze kuwa wanafunzi vinara kama iliivyokuwa imezoeleka katika kipindi cha miaka ya nyuma. Pia, amesema kuwa Tanzania inaongoza katika matumizi ya TEHAMA katika Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mara baada ya kupokea kompyuta hizo kwa niaba ya wananchi, Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere kuwa, kuwe na kituo kimoja cha kutunga mitihani Ludewa ili waalimu watunge mtihani wa aina moja na waweze kumaliza kufundisha masomo ya kiada na ziada kama walivyopanga kwa muhula husika wa masomo ili waweze kuwapima wanafunzi wote kwa pamoja

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Andrea Tsere alimueleza Nditiye kuwa wataweka intaneti kwenye kompyuta hizo ili waalimu na wanafunzi waweze kupata notisi. Pia, amesema kuwa kompyuta hizo zitatumika kuinua kiwango cha elimu na zimefika muda muafaka

“Mmetusaidia sana, umeingia kwenye akili yangu ya kuinua kiwango cha elimu Ludewa,” amesisitiza Tsere wakati akimshukuru Nditiye kwa kuzipatia shule za Wilaya yake kompyuta 25. Tsere amewataka waalimu wakuu wa shule kuzitunza kompyuta hizo na kuzifanyia matengenezo pindi inapohitajika badala ya kuacha ziharibike na pasipo kuzipanga vizuri kwa sababu ni vifaa vya Serikali badala yake wanapanga lini wavichukue badala ya kuzitunza vizuri ili zisaidie wanafunzi wengi na kwa muda mrefu. Aidha, amesisitiza kwa waalimu hao kuwa kompyuta zikipotea na wao wapotee

Katika hatua nyingine, Nditiye amewaeleza wananchi hao kuwa, Wizara yake ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia UCSAF imetoa ruzuku kwa kampuni ya simu ya Halotel na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ili wajenge minara 11 kwenye maeneo ya mwambao kwa wananchi waishio Wilayani Ludewa kwa kuwa hawana mawasiliano.

“Tunahitaji Ludewa iwasiliane na dunia,” amesisitiza Nditye. Amefafanua kuwa minara tisa imejengwa na kampuni ya Halotel na miwili ni ya TTCL

Vile vile, ameongeza kuwa, ujenzi wa meli ya abiria waishio Ludewa kwa ajili ya usafiri wa Ziwa Nyasa umekamilika ambapo kwa sasa meli hiyo inafanyiwa majaribio kabla ya kuanza safari zake na Serikali inakamilisha ujenzi wa gati za kushusha na kupakia abiria kwenye mwambao wa ziwa hilo kwenye maeneo ya Manda, Lupingu, Nsele, Yiga na Nkanda ambapo meli hiyo inatarajiwa kuanza safari zake za kutoka Ludewa, Njombe hadi Kyela, Mbeya mwezi Aprili mwaka huu

“Tunataka Lupingu hadi Matema watu wapite kwa lami,” amefafanua Nditiye. Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Ludewa mjini na kuwaeleza kuwa  azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa barabara ya Lusitu – Mawengi yenye urefu wa kilomita 50 inajengwa kwa kiwango cha zege kwa gharama ya shilingi bilioni 159 ambapo tayari mkandarasi wa kutoka nchi ya Korea yupo na anaendelea na ujenzi wa barabara hiyo ili iweze kupitisha madini ya Mchuchuma na Liganga

Ngalawa amewaeleza wananchi kuwa anamshukuru Nditiye kwa kuwa alifanya ziara kutoka Lupingu hadi Manda mwaka jana mwezi wa tatu akiwa na miezi minne tu tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri na kushuhudia ukosefu wa mawasiliano kwa wananchi waishio mwambao na sasa minara 11 imejengwa ambapo tayari minara mitatu ya Nkanda, Mawengi na Mahong’olo imewashawa na meli ya abiria pia itaanza safari zake

Tsere alimshukuru Ngalawa kwa kumleta Nditiye ambapo alisafiri na boti siku nzima Ziwani mwaka jana mwezi wa Machi na kushuhudia ukosefu wa mawasiliano kwa kuwa tangu dunia iumbwe wananchi wa mwambao hawajawahi kupata mawasiliano na sasa wanawasiliana.

Benki Ya Maendeleo Ya Afrika-AfDB Yaahidi Kuipatia Tanzania Mikopo Nafuu Kutekeleza Miradi Ya Maendeleo

$
0
0
Na Farida Ramadhani,  WFM, Abidjan
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maedeleo ikiwemo mindombinu ya barabara, umeme na ujenzi wa viwanja vya ndege hususan Kiwanja cha Msalato mkoani Dodoma.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na  Rais wa AfDB, Dkt. Akinwumi Adesina, wakati wa  Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa nchi za Afrika Mashariki, uliofanyika Abidjan nchini Ivory Coast.

Dkt. Mpango,  ambaye pia ni Gavana wa Benki ya Maendelo ya Afrika (AfDB), alisema Rais wa Benki hiyo amekubali ombi la Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli la kuipatia Tanzania mkopo nafuu ili kuwezesha kuanza ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Msalato mkoani Dodoma.

"Benki hii imekuwa ni ya msaada mkubwa sana na yapo maeneo mengi ambayo Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika amekubali kuendelea kushirikiana na nchi yetu",  alisema Mhe. Mpango.

Mhe. Mpango alieleza kuwa Dkt. Adesina ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Magufuli, kwa juhudi zake za kupiga vita rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma kwa vitendo, kufanya maamuzi magumu ya kulinda rasilimali za Taifa hususan madini, kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima Serikalini, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kudhibiti ukwepaji kodi.

Alisema kuwa Dkt. Adesina ameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ambazo zimesababisha Tanzania kupata mafanikio makubwa katika maendeleo kwa kipindi kifupi.

Akizungumza wakati wa  Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa nchi za Afrika Mashariki, Mhe. Mpango aliishukuru  Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kuendelea kuipatia mikopo nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Katika mkutano huo wa Mawaziri, Mhe. Mpango aliuomba  uongozi wa Benki kuharakisha maandalizi ya miradi inayotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2019 ikiwemo: Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato (USD milini 200); Ujenzi wa Barabara ya Kuzunguka Jiji la Dodoma (USD  milioni 180).

Miradi mingine ni Mradi wa Kufua Umeme wa Maji (87 MW) wa Kakono (USD milioni 350); Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Tanga/Lungalunga-Mombasa-Malindi (USD milioni 158.2); na Awamu ya Pili ya Mpango wa Kuendeleza Utawala Bora na Maendeleo ya Sekta Binafsi (USD milioni 56).

Benki ya Maendeleo ya Afrika imeahidi kuiwezesha Tanzania kupata mikopo nafuu ili miradi hiyo iweze kuanza kutekelezwa mapema. Aidha, iliahidi kuwa mkataba wa Dola za Marekani milioni 256 kwa ajili ya ujenzi ya barabara ya Kabingo-Kasulu-Manyovu (km 260) kwa kiwango cha lami utasainiwa mapema mwanzoni mwa mwezi machi, 2019.

Kwa upande mwingine,  Mawaziri wa  Fedha wa nchi za Afrika Mashariki waliohudhuria mkutano huo, walimuahidi Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kuwa wataendelea kuunga mkono kusudio la Benki hiyo la kuongeza mtaji ili kuziwezesha nchi wanachama kupata mikopo nafuu kwa ajili kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mwisho.

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (CHADEMA) Alazwa ICU

$
0
0
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (CHADEMA) amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, ambapo alifikishwa Februari 27 mwaka huu. Mbunge huyo anasumbuliwa na shinikizo la damu.

Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro Basili Lema  amethibitisha kulazwa kwa Mbunge huyo.

Super Mbushi Power:ni Maalum Kwa Wenye Matatizo Ya Upungu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Wanaume wengi wamekuwa na upungufu wa Nguvu za kiume na kuwa na maumbile madogo ya kiume .

Magonjwa kama Kisukari,Presha,Ngiri ya kupanda na kushuka,Tumbo kuunguruma chini ya kitovu,Kutokupata choo vizuri,Tumbo kujaa gesi,Unywaji wa pombe kupita kiasi Pamoja na msongo wa mawazo huchangia kwa kiasi kikubwa upotevu wa nguvu za kiume

Tumia dawa za mitishamba ambayo haina madhara kwa mtumiaji hata awe na miaka 70-85 inatibu na kumaliza matatizo hayo kwa mda mfupi tu.

SUPER MBUSHI POWER:Hii ni dawa yenye uwezo mkubwa wa kuongeza nguvu za kiume mara dufu; huanza kufanya kazi ndani ya dk kumi na tano(15)toka uitumie.
(1)Itakufanya uwe na NGUVU za ajabu ukiwa unafanya tendo la ndoa
(2)Inaongeza hamu ya kurudia tendo la ndoa bila kuchoka.(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 27 kwa tendo la pili nakuendelea bila kuchoka.

NKINDA:INAREFUSHA NA KUNENEPESHA MAUMBILE YA KIUME SAIZI INAYOKUBARIKA KIAFYA KUANZIA nch 3-71/2 NA UNENE CM 2-4.
(4)Itaimalisha mishipa ya uume uliolegea
(5)Inasaidia kusafisha mishipa ya kwenye uume na hivyo kuongeza kasi ya msukumo wa damu ndani yauume,na inasidia kuzarisha HORMONES ZA CETROGEN,Vile vile inazalisha kwa wingi mbegu za kiume yaani(manii)

NGUMO: Ni dawa inayotibu Kisukari kwa mda wa wiki mbili(14)tu nakuwa  nomo.

NGITO:Ni kwale waliochwa na mpenz,mke,hata kwa wewe unayetafuta mchumba majibu ni ndani ya masaa kumi na mbili(12)tu.

WASILIANA NA DR.SEMEKA 

TEL 0753-459433 -ANAPATIKANA MAGOMENI MAPIPA.

Kwanini Uhangaike Na Magonjwa Yanayowezekana Kupona?..........Tiba Sahihi Imewasili

$
0
0
Asilimia 60- 80 ya wanaume wameathilika kisaikologia baada ya kujiona wako tofaut na wengine kimaumbile na kupungukiwa nguvu za kiume , mwanaume aliekamilika kimaumbile anatakiwa awe na maumbile yasiyo pungua nchi 6-8 tofautina hapo anaupungufu ,

zipo sababu nyingi zinazosababisha mapungufu hayo ambazo ni :- upigaji wa punyeto ( mastervation) ,ngili,KISUKARI,vidonda vya tumbo,maumivu ya mgongo ama kiuno,unene(kitambi) tumbo kuunguluma na kujaa ges, matatizo haya huchangia kwa kiasi kikubwa sama kukosa nguvu za kiume vilevile maumbile kuwa madogo na kiingia ndani (kunywea)

GALIMBO 3 POWER :- hii nidawa kiboko kwa matatizo ya nguvu za KIUME,ni dawa ya Asili tuliyo jaaliwa na mwenyezi MUNGU huimarisha misuli ya uume wakati wa tendo la ndoa na kuzalisha viini vya uzazi (manii) vilevile utaludia tendo zaidi ya mara tatu bila ham kuisha pamoja na kuchelewa kufika kilele takiriban dk 20 - 45 kwatendo moja.

SUNUPER :- hii nidawa ya Asili Hurefusha na kune nepesha maumbire madogo ya UUME , hurefusha urefu wa nchi (6-8 )na unene wa sm( 3-4) huanza kufanya kazi masaa machache baada ya kuanza kuitumia,( tiba niyakudumu ikishakutibu,

Nina dawa ya kutokomeza KISUKARI na kupona kabisa hata kama kimekusumbua kwa mda mrefu mpaka ukajikatia tamaa  tiba ipo na utatumia vyakula vyote bila tatizo baada ya kupona ,

Pia ninadawa ya Vidonda vya tumbo,Ngiri, miguu kuwaka moto, mvuto wa mapenz ( kumvuta mke /mme/mpenzi/hawara/ama yoyote unaemuhitaji) dawa za biashara, uzazi kwa akina mama na akina baba (pande zote) pata dawa ya bawasili bila kufanyiwa upasuaji,

KWAMAELEZO NA MSAADA WASILIANA NA DR SILIMBA NAPATIKANA DAR ES SALAAM

 SM O620510598 / 0743543944

Nb km huna nafasi huduma hii inakufikia popote ulipo kwaware wa mikoani tunatuma kwa njia ya mabasi

Mrisho Mpoto Avunja Ukimya......Amtaka Diamond Ahudhurie Msiba wa Ruge Mutahaba

$
0
0
Msanii wa muziki wa asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto, maarufu kama ‘Mjomba’ amemtaka msanii mwenzake, Diamond Platnumz asikae kimya na badala yake  ahudhurie katika msiba wa  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba

Mrisho Mpoto kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kwa majonzi akisema;“@diamondplatnumz Nasib Abdul nimekwita jina lako la kuzaliwa mimi kama kaka yako unaeniheshimu na kunisikiliza nakwambia. RUGE MUTAHABA AMEFARIKI nakuomba NJOO UMZIKE… Nimemaliza.”

Msanii Diamond  amekuwa kimya mpaka sasa, si kuposti mitadaoni au kufika msibani jambo ambalo limeibua maneno.

Hivi karibuni, ilidaiwa kuwa Diamond na Lebo yake ya WCB waliingia kwenye bifu zito  na Ruge Mutahaba kwa madai ya kutofautiana katika mambo yao ya sanaa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images