Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wabunge wawili wa Chadema, Peter Lijualikali na Susan Kiwanga Wafikishwa Mahakamani

$
0
0
Wabunge wawili wa Chadema, Peter Lijualikali (Kilombero) na Susan Kiwanga wa Mlimba na wenzao saba wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada ya kukamatwa na polisi.

Kwa mujibu wa  Kaimu Katibu wa Vijana Chadema mkoa wa Morogoro, Jackson Malisa, Wabunge hao walikamatwa Jumatano iliyopita ya Februari 20, 2019 wakiwa Kijiji cha Sofi wilaya ya Malinyi na kukaa rumande hadi leo Jumatatu Februari 25, 2019.

Bado haijafahamika wabunge hao na wenzao wana tuhuma gani, lakini wiki iliyopita Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema jeshi hilo  lilikuwa linawasaka wabunge hao pamoja na wanachama 11 wa Chadema walioachiwa huru na mahakama mkoani humo Januari  2019.

Waliachiwa huru kupitia kifungu cha Sheria namba 225 cha mwenendo wa makosa ya jinai baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili, ikiwa ni pamoja na kuchoma moto ofisi ya Sekondari ya kijiji cha Sofi Wilaya ya Malinyi.

Mutafungwa  alisema kuwa  jeshi la Polisi hivi sasa wamejipanga kwa kuwa na ushahidi na vielelezo vya kutosha vya kuwatia hatiani watuhumiwa hao waliokuwa  wameachiwa huru na Mahakama.

BREAKING: Jamhuri Yaiomba Mahakama Ifute Dhamana ya Tundu Lissu na Itoe Hati ya Kumkamata

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeombwa kumfutia dhamana na kutolewa hati ya kukamatwa kwa mwanasiasa wa upinzani nchini, Tundu Lissu, kufuatia kushindwa kwake kufika mahakamani.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amewasilisha maombi hayo leo Jumatatu Februari 25, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Wankyo amedai mshtakiwa anaonekana akizunguka nchi mbalimbali akitoa mihadhara na huko Ubelgiji anakodaiwa yuko Hospitali haijaelezwa yuko hospitali gani.

“Kama itafaa Mahakama iamuru mshtakiwa Lissu akamatwe maana hayupo hospitali kama inavyodaiwa hapa mahakamani,” amedai.

Hata hivyo, Hakimu Simba amekataa kutekeleza ombi hilo na kusema mahakama haiwezi kuitikia wito huo kwa kuwa kutekeleza kwake, ni kinyume na utu wa kibinadamu. 


Badala yake, Hakimu Simba amewaonya wadhamini na kuwataka  kukumbuka majukumu yao ya kuhudhuria mahakamani na kutoa taarifa za washtakiwa.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Lissu na wenzake Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob, wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Je Kwanini Baadhi Ya Wanaume Wengi Wana Ukosefu Ama Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
JE KWANINI BAADHI YA WANAUME WENGI WANA UKOSEFU AMA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO ???

Pata sululisho la matatizo haya na  magonjwa mengine utapona kwa mda mfupi sana hatakama ulihangaika mpaka ukakata tamaaa 

GALIMBO 3 MIX  ni dawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa aina mbili ili kukidhi mahitaji ya mtumiaji, imetengenezwa kwa muundo wa vidonge pamoja na unga kwaajili ya kuponesha tatizo moja kwa moja , huimalisha misuli ya uume iliyolegea wakato wa tendo la mdoa ,na kukufanya ucherewe kufika kileleni kwa mda wa dk ( 20 - 45 ) itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu nira hamu kuisha wara kuhisi kuchoka vilivile huzalisha viini vya uzazi ( manii ) 

YOLAN  hurefusha na kunenepesha  maumbile madogo ya uume na kuwa na uume kuanzia nchi (6-8) tiba kwa mda mfupi sana

Zipo sananu nyingi sana zinazosababisha matatizo hayo  km vile -:punyeto, kisukali,ngili,chango,vidonda vya tumbo,  tumbo kuunguluma na kujaa gesi maumivu ya mgongo ama kiume ,kolodani moja kuvimba ama kuingia ndani  presha nk 

Matatizo haya yote sio mageni, kigeni ni tiba sahihi ya kuponesha matatizo hayo

SUPER MBUKE -:  nidawa ya kuponesha tatizo la kisukali kwa mda mfupi sana , usihangaike wara kuteseka tumia dawa ya mitishamba kwaajili ya tatizo hili na upone kabisa

NTINJIWA  nidawa ya mvuto wa biashara,kazi, kupandishwa cheo,kumfanya mfanyakazi apendwe na bos wake

Pia ninadawa za kumvuta mme , mke,mchumba,hawara, au mtu yoyote unaemuhitaji katika maisha yako hata km yupo mbali na atatulia na kukutimizia cjovjote utakacho na kumfunga asiwe na mtu mwingime ,

Pata tiba za magonjwa mbalimbali ikiwemo miguu kuwaka moto, mgongo,bawasili ,kaswende ,gono na mengine mengi

KWAUSHAULI NA TIBA WASILIANA NA DR CHIKAGO    0759 208 637

Km huna nafasi ya kufika ofisini hudumahii utaletewa hapo ulipo , kwa wale wa mikoani natuma kwanjia ya basi

Serikali Yaagiza Msako Kwa Waliowapa Mimba Wanafunzi Siha

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza viongozi na wazazi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro washirikiane kuhakikisha watu wote waliowapa mimba wanafunzi wanasakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana jumla ya wanafunzi wa kike 57 walikatishwa masomo baada ya kupata mimba na hadi sasa kesi zilizofunguliwa ni sita tu.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Februari 24, 2019) alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Isanja, Sanya Juu wilayani Siha wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro.

“Jambo hili halipendezi, kesi sita tu ndio zimefikishwa mahakamani. Hakikisheni wahusika wote waliowapa mimba wanafunzi wanatafutwa popote walipo, wakamatwe na wachukuliwe hatua kali za kisheria.”

Waziri Mkuu alisema Serikali imeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike lengo ni kumuwezesha amalize masomo yake ili aweze kujikwamua kiuchumi na aondokane na utegemezi, hivyo ni marufuku kuwakatisha masomo.

Watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na Serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako, katika nyumba ya wageni.

“Tukikukuta na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria. Ole wenu vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela, sasa tafakari kabla ya kutenda.”

Waziri Mkuu alisema kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto wa kike ambao bado ni wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

“Kuna taarifa nimezipata kuwa baada ya watoto kupewa mimba wazazi au walezi mnamalizana na wahusika kwa kupeana ng’ombe. Sasa tukikukamata unamalizana na mtu aliyempa mimba mwanafunzi na wewe tunakufunga.”

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wote hususani wa kike wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao na wasikubali kushawishika kwa sababu watashindwa kuendelea na masomo yao.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Serikali Kuweka Mazingira Wezeshi Kutekeleza Mradi Wa Uendelezaji Na Upatikanaji Wa Mbegu Za Mazao Jamii Ya Mikunde Na Nafaka Afrika (Avisa)

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya kilimo-Arusha
Serikali imeeleza kuwa imejipanga kuweka mazingira wezeshi katika kutekeleza Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (The Accelerated Varietal Improvement and Seed Delivery of Legumes and Cereals in Africa project-AVISA).utakaosimamiwa na kutekelezwa kwa ukamilifu nchini Tanzania.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 25 Februari 2019 wakati akifungua mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha.

Katika ufunguzi huo wa mkutano wa siku tatu, Mhe Hasunga alisema kuwa ana mategemeo makubwa kuwa katika mradi huo msukumo mkubwa utawekwa katika uhaulishaji wa teknolojia kupitia uimarishaji wa mashirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili matokeo ya mradi yaweze kuonekana kwa walengwa.

Alisema, Kilimo kimeendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi katika nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania. “Kwa mfano, hapa Tanzania kilimo kinachangia asilimia 29.1 katika pato la taifa na karibia asilimia 65.5 ya nguvu kazi inategemea kilimo”

“Hata hivyo, kwa Afrika kilimo kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukame, upungufu kwa rutuba katika udongo, kuongezeka kwa magonjwa na wadudu wa mazao vipando, miundombinu hafifu, kipato kidogo kwa wakulima, upokeaji mdogo wa teknolojia, soko lisilokuwa la uhakika na bei ndogo za mazao, kutegemea kilimo cha jembe la kutumia mkono na mifumo hafifu ya uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora. Hivyo, hali hii inasababisha uzalishaji mdogo, ubora mdogo wa mazao na kuwafanya wakulima kubakia kuwa wadogo na kulima kwa kujikimu tu sio kibiashara” Alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema kuwa, ana matumaini makubwa kuwa Mradi huo utaimarisha mafanikio yaliyopatikana kutoka kwenye miradi ya utafiti iliyotangulia ya Mikunde (Tropical Legumes -TL), Uendelezaji wa Tija katika Mazao ya Mtama na Ulezi (Harnessing Opportunities for Productivity Enhancement for Sorghum and Millets - HOPE) na Harvest Plus ambayo ilifadhiliwa na Shirika la Bill & Melinda Gates Foundation (BMGF) –  kwa ajili ya kuendeleza uzalishaji wa mbegu na usambazaji wake.

Aidha, BMGF imekuwa ikifadhili miradi hiyo katika nchi saba (7) za Afrika zikiwemo Tanzania, Uganda, Ethiopia, Burkina Faso, Ghana, Mali na Nigeria katika utafiti wa  dengu, karanga, maharagwe, kunde, mtama na ulezi. Hivyo, Mradi huo wa AVISA utaendeleza na kuimarisha mashirikiano kati ya Vituo vya  Kimataifa vya Utafiti wa Kilimo (CGIAR) na Mifumo ya Kitaifa ya Utafiti wa Kilimo katika nchi za Afrika (NARS) katika kuendeleza uzalishaji na usambazaji wa mbegu za aina ya nafaka na mikunde zinazohimili maeneo ya ikologia ya ukame.

Manufaa mengine ni kuimarisha na kuongeza madini ya chuma na zinki katika mazao ya maharagwe na ulezi katika mradi wa HarvestPlus unaofadhiliwa na BMGF kupitia CIAT (Maharage) na ICRISAT (Ulezi). Hivyo, kuwekeza Miradi miwili ya TL-III na HOPE ambapo itaongeza tija kwenye mazao husika na  kujenga uwezo wa utafiti kwenye nchi zetu za Afrika.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Daqarro, Wawakilishi Shirika la Bill & Mellinda Gates, likiongozwa na Dkt Jeff Ehlers, Mkurugenzi Mkuu ICRISAT: Dkt Peter Carberry, Wakurugenzi wa Taasisi za Utafiti za Kanda: CIAT, ICRISAT and IITA, Wawakilishi wa Shirika laSyngenta, Wakurugenzi Wakuu, Taasisi za Utafiti wa Kilimo kutoka: Uganda, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Mali and Tanzania,Wakurugenzi wa Wizara ya Kilimo na Wakuu wa Taasisi zake Wawakilishi wa Makampuni ya Mbegu, Wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya Serikali pamoja na Wawakilishi wa Vyama vya Wakulima.

MWISHO

Serikali Yakarabati Shule Zake Kongwe Za Serikali Ili Kuboresha Elimu

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Kibaha
Serikali imetoa zaidi ya  sh. bilioni 42 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Sekondari 42 kati ya shule 88 kongwe zilizopo nchini kote ikiwemo shule ya Sekondari Ruvu iliyoko Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Akizungumza mara baada ya kukagua ukarabati wa shule hiyo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa shule zote Kongwe ambazo zinahistoria kubwa ya kutoa viongozi wengi na wataalam mbalimbali nchini, zinakuwa na hadhi na kuwa kimbilio la wananchi.

Ametoa wito kwa uongozi wa shule hiyo ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ili thamani ya uwekezaji mkubwa wa Serikali unaofikia zaidi ya shilingi bilioni 990 uweze kuonekana

"Dhamira yetu ni kuona watoto wetu wanasoma kwenye mazingira sahihi na ufaulu wao unaongeeaka kwa sababu tunawaandaa wataalam wa kesho wa Taifa letu" Aliosisitiza Dkt. Kijaji

Alisema amejionea ukarabati uliofanyika shuleni hapo ambapo pamoja na shilingi milioni 992 kutumika katika ukarabati huo, bado nyumba 6 za walimu hazijakarabatiwa pamoja na kutonunuliwa kwa samani za shule vikiwemo vitanda na kuahidi kuifanyia kazi changamoto hiyo wakati wa huu wa mchakato wa bajeti mpya

Kwa upande wao, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Juma na Mkuu wa Shule hiyo, Juliana Chimazi, wameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha shule hiyo na kuomba wapatiwe fedha kwa ajili ya kununulia samani hasa vitanda kwa ajili ya wanafunzi ili kwenda sambamba na uboreshaji mkubwa wa majengo uliofanyika shuleni hapo.

Mkuu wa shule hiyo Mwl. Juliana Chimazi alimweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji kwamba shule hiyo inahitaji vitanda vipya kwa kuwa vilivyopo vimedumu zaidi ya miaka 50 pamoja na kuomba fedha kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa nyumba sita za walimu.

Miongoni mwa miundombinu iliyoboreshwa katika shule hiyo ya Sekondari ya washichana Ruvu ni pamoja na mifumo ya maji taka, madarasa, vyoo, mabweni, nyumba za walimu na Ofisi.

Naibu Waziri Dkt. Kijaji anaendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali iliyopewa fedha na Serikali ikiwemo ya kimkakati inayolenga kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kujitekemea kwa mapato.

Mwisho

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan awataka Wananchi Tabora kuboresha usafi na kutokata miti hovyo

$
0
0
Makamu wa rais Samia Suluhu amefanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa mazingira Mkoani Tabora, ambapo amewataka kuboresha usafi na kuacha kukata miti kutokana na matumizi ya mkaa na kuni kuchangia uharibifu wa mazingira mkoani humo kwa kiasi kikubwa.

Ameyasema hayo leo Februari 25, mwaka huu katika kongamano la kujadili mustakabali wa mazingira mkoani humo ambapo amewataka wazazi kuwafundisha watoto na vijana juu ya utunzaji wa mazingira ili waweze kusaidia kupambana na uharibifu huo.

“Fursa mliyo nayo ni wingi wa watu hapa nimeona kuna vijana na watoto wengi sana na wanakuwa hivyo tusipowafundisha jinsi ya kutunza na kuhifadhi mazingira tutaiweka nchi yetu katika hali ambayo sio nzuri, tuangalie ni kazi gani tunawapangia ili wanavyozidi kukua waweze kujua wanatunza vipi mazingira yao,” amesema.

Aidha amesema kuwa mazao yanayolimwa mkoani humo ni ya uchumi wa viwanda na uchumi huo unahitaji umeme ili viwanda viweze kufanya kazi vizuri hivyo amesisitiza utunzaji wa mazingira ili bwawa liweze kujazwa na kuwe na umeme wa kutosha.

“Makundi ya ng’ombe yakikanyaga ardhi wanaharibu mfuko wa ikolojia na kinyesi cha wanyama kinafanya ardhi inakuwa ngumu na kupasuka hivyo jaribuni kutumia utajiri huo mlio nao vizuri kwaajili ya kuleta maendeleo,” amesema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya February 26

Mkurugenzi UDART na wenzake wawili kwenda kuhojiwa TAKUKURU

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhoji Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) Robert Kisena (46) na wenzake wawili.

Kisena ambaye jana hakufika Mahakamani kwa sababu anaumwa na wenzake watatu ambao ni Kulwa Kisena(33) na Charles Newe(47) wanakabiliwa na mashtaka 19 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kuusababishia Mradi wa UDART hasara ya zaidi ya Bilioni. 2.41.

Maombi hayo yaliwasilishwa Mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Simon alidai kuwa wanawaomba washtakiwa hao kwenda kuhojiwa kwa siku moja TAKUKURU kisha kurudishwa na kubainisha kuwa mshtakiwa wa kwanza Kisena ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa sababu ni mgonjwa.

Hata hivyo mahakama hiyo imeridhia washtakiwa hao kuhojiwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 11, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa hao na mwenzao mmoja ambaye ni raia wa China, Cheni Shi (32) walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 11, 2019 na kusomewa mashtaka 19 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kuusababisha mradi huo hasara ya zaidi ya Bilioni. 2.41.

Katika mashtaka hayo, lipo shtaka moja la kuongoza uhalifu, lingine moja la kujenga kituo cha mafuta bila kibali, la kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa pamoja na shtaka la wizi wakiwa Wakurugenzi.

Pia wanakabiliwa na mashtaka manne ya utakatishaji fedha, ya kughushi manne, kutoa nyaraka za uongo manne, mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la kuisababishia mradi huo hasara.

Waziri wa Fedha Dokta Mpango Azionya Taasisi Za Serikali Zisizotumia Mfumo Wa Kieletroniki Kukusanya Mapato

$
0
0
Na Josephine Majura na Ramadhani Kissimba, WFM, Arusha.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango amezitaka Taasisi zote za Serikali kutumia kikamilifu mfumo wa malipo wa Serikali wa kielektroniki (GePG), ili kutimiza azma ya Serikali ya kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za Umma.

Dkt. Mpango ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kikao cha wafanyabiashara wa sekta ya madini, utalii, mahotel na viwanda wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Akijibu hoja na kutolea ufafanunuzi wa kero mbalimbali zilizowasilishwa na Wafanyabiashara hao, Dkt. Mpango alisema Serikali ilishatoa maagizo kwa Taasisi zote za Serikali kuwa malipo yote yafanyike kwa kutumia mfumo wa malipo ya Serikali, na endapo itatokea Taasisi yoyote itashindwa kufanya hivyo itachukuliwa hatua za kisheria.

“Serikali iliziagiza Taasisi zote kuanza kutumia mfumo wa malipo ya Serikali ifikapo mwezi Juni, 2019, na nina agiza kuanzia leo mwananchi yeyote asikubali kulipa malipo yoyote yasiyotumia mfumo huu” alisisitiza Dkt. Mpango.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia  Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki alisema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba inaboresha mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini.

Mkutano huo uliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, kwa lengo la kutatua kero mbalimbali za Wafanyabiashara wa Mkoa huo, na kuhudhuriwa na  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe. Kangi Lugola, Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu ya Rais Mazingira Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Isack Kamwele,  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu, na Naibu Waziri wa Vijana, Kazi na Ajira, Mhe.Anthony Mavunde.

Mwisho

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 25

Mvua Kubwa ya Upepo Yaua Wawili Ukerewe na Kubomoa Nyumba 16

$
0
0
Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia huku watu 77 wakazi wa kijiji cha Mibungonanakwekwe wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wakikosa makazi baada ya nyumba zao 16 kubomolewa kwa mvua iliyoambatana na upepo mkali.

Watoto waliokufa katika tukio hilo baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba walimokuwa wamelala wametambuliwa kuwa ni Nelson Benedictor (3) na Daison Benedictor mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Mulilo Jumanne Mulio amesema tukio hilo lilitokea jana saa 9:00 usiku wa kuamkia Februari 25.

Alisema watu wengine wa familia hiyo, Mektrida Benedictor (30) na Eric Benedictor (7) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu wa shule ya msingi Namakwekwe wamelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo mjini Nansio kwa matibabu.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Ukerewe, Dk Revocatus Cleophace alisema majeruhi katika tukio hilo wanaendelea vema na miili ya watoto waliopoteza maisha imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitalini hapo.

Naibu Waziri Ikupa: Kilimo Si Shughuli Ya Wazee

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe.  Stella  Ikupa  amewashauri Vijana nchini, kuondokana na dhana ya kuwa shughuli za kilimo ni za Wazee na badala yake watumie vitalu nyumba kujifunza kilimo chenye tija na hatimaye waweze kujikwamua  kiuchumi.

Ikupa ametoa ushauri huo wilayani Maswa wakati alipowatembelea  Vijana katika kitalu nyumba katika kata ya Binza  akiwa katika ziara yake wilayani humo Mkoani Simiyu Februari 25, 2019.

IKUPA amesema Vijana wanapaswa  kuachana na dhana potofu kuwa kilimo ni shughuli inayopaswa kufanywa na Wazee, badala yake watumie fursa za mafunzo ya kilimo na wakawe mabalozi ndani ya jamii kuwa kilimo kinaweza kuwapatia ajira na kipato.

“ Kilimo kinaweza kuwatoa vijana kutoka mahali fulani kikawapeleka mahali pengine tena wakawa na uwezo mzuri kifedha kuliko hata wale walioajiriwa katika kazi za maofisini, niwashauri vijana muione fursa kupitia vitalu nyumba ondoeni dhana kwamba eti kilimo ni kazi ya wazee si kweli” alisema.

Ameongeza kuwa vijana wanayo nafasi ya kupata mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Halmashauri zao hivyo wachangamkie fursa hiyo kupata mikopo itakayowawezesha kuendeleza shughuli zao za uzalishaji ikiwemo kilimo kupitia vitalu nyumba.

Katika hatua nyingine Mhe. Ikupa amesema ni vema Halmashauri zikazingatia masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango ya bajeti zao ili ziweze kusaidia katika utatuzi wa baadhi ya changamoto za watu wenye ulemavu.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwatumia wakalimani wa lugha ya alama ili waweze kusaidia mawasiliano kati ya walemavu wa kusikia na makundi mbalimbali ya watu ikiwemo viongozi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amekiri kupokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Naibu Waziri Ikupa na kumhakikishia kuwa watu wenye ulemavu watalindwa, watashirikishwa katika fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa Kitalu nyumba.

Nao baadhi ya vijana wanaojihusisha na utekelzaji wa mradi wa Kitalu nyumba katika Kata ya Sola wameishukuru Serikali na kuomba ipanue wigo wa kuwafikia vijana kupitia mradi huu ili vijana wengi waweze kufikiwa mpaka ngazi ya Kata.

“ Mimi ninaishukuru Serikali yetu kwa kutuletea mradi wa kitalu nyumba, tumeshajifunza namna ya kutengeneza vitalu nyumba, kilimo bora chenye tija kupitia mradi huu, tunaomba mradi upelekwe mpaka ngazi ya kata ili vijana wengi waweze kunufaika  zaidi” alisema Rachel Paulo mkazi wa Sola Maswa.

Naibu Waziri Ikupa, anaendelea na ziara yake Mkoani Simiyu ambayo itahitimishwa tarehe 27 Februari 2019, akiwa wilayani Maswa Naibu waziri ametembelea kitalu nyumba kilichopo Sola na kuzungumza na viongozi wa Serikali na watu wenye ulemavu.

Mahakama Yaibana Serikali Kesi ya Mpemba

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewataka upande wa mashtaka kuja na maelezo ya kutosha kuhusu kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Yusuf Ali maarufu ‘Mpemba wa Magufuli' na wenzake watano upelelezi wake umefikia hatua gani.

Yusuf na wenzake wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwamo la kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh785.6 milioni.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Candid Nasua kuieleza Mahakama hiyo, jana Jumatatu Februari 25,2019 kuwa imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

"Wakili wa Serikali aliyekuwa anaendesha shauri hilo hayupo hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," alidai Nasua.

Hakimu Simba alisema, “kesi hiyo ipo mikononi mwenu tangu mwaka 2016, hatutaendelea kuwavumilia mnatakiwa kumfikishia ujumbe wakili  wa serikali huyo kuwa siku tutakapokutana tena mje na majibu sahihi.

Hakimu Simba aliliahirisha shauri hilo hadi Machi 11, 2019 itakapotajwa tena na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa.

Katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, 2016 wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh392.8 milioni bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Tiba ya Tatizo la Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote.

Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-

☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.

Kwa kutumia mimea na matunda  Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-

1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza  size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=

2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6 hadi 7  @130,000/=

3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @130,000/=

4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @250,000/=

5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130,000/=

BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA NI SALAMA KIAFYA

    Wasiliana nasi Popote

  ulipo duniani kwa (+255)

      Whatsap     0653 074067 )

             0752 92 34 61

Kwanini Uhangaike Na Magonjwa Yanayowezekana Kupona?..........Tiba Sahihi Imewasili

$
0
0
Asilimia 60- 80 ya wanaume wameathilika kisaikologia baada ya kujiona wako tofaut na wengine kimaumbile na kupungukiwa nguvu za kiume , mwanaume aliekamilika kimaumbile anatakiwa awe na maumbile yasiyo pungua nchi 6-8 tofautina hapo anaupungufu ,

zipo sababu nyingi zinazosababisha mapungufu hayo ambazo ni :- upigaji wa punyeto ( mastervation) ,ngili,KISUKARI,vidonda vya tumbo,maumivu ya mgongo ama kiuno,unene(kitambi) tumbo kuunguluma na kujaa ges, matatizo haya huchangia kwa kiasi kikubwa sama kukosa nguvu za kiume vilevile maumbile kuwa madogo na kiingia ndani (kunywea)

GALIMBO 3 POWER :- hii nidawa kiboko kwa matatizo ya nguvu za KIUME,ni dawa ya Asili tuliyo jaaliwa na mwenyezi MUNGU huimarisha misuli ya uume wakati wa tendo la ndoa na kuzalisha viini vya uzazi (manii) vilevile utaludia tendo zaidi ya mara tatu bila ham kuisha pamoja na kuchelewa kufika kilele takiriban dk 20 - 45 kwatendo moja.

SUNUPER :- hii nidawa ya Asili Hurefusha na kune nepesha maumbire madogo ya UUME , hurefusha urefu wa nchi (6-8 )na unene wa sm( 3-4) huanza kufanya kazi masaa machache baada ya kuanza kuitumia,( tiba niyakudumu ikishakutibu,

Nina dawa ya kutokomeza KISUKARI na kupona kabisa hata kama kimekusumbua kwa mda mrefu mpaka ukajikatia tamaa  tiba ipo na utatumia vyakula vyote bila tatizo baada ya kupona ,

Pia ninadawa ya Vidonda vya tumbo,Ngiri, miguu kuwaka moto, mvuto wa mapenz ( kumvuta mke /mme/mpenzi/hawara/ama yoyote unaemuhitaji) dawa za biashara, uzazi kwa akina mama na akina baba (pande zote) pata dawa ya bawasili bila kufanyiwa upasuaji,

KWAMAELEZO NA MSAADA WASILIANA NA DR SILIMBA NAPATIKANA DAR ES SALAAM

 SM O620510598 / 0743543944

Nb km huna nafasi huduma hii inakufikia popote ulipo kwaware wa mikoani tunatuma kwa njia ya mabasi

Naibu Waziri Kanyasu Atoa Mbinu Ya Kuzibana Halmashauri Kupanda Miti Milioni 1.5

$
0
0
NA LUSUNGU HELELA-WMU
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameshauri itungwe sheria ya  kuhakikisha kila  Halmashauri nchini inapanda  miti milioni 1.5 kila mwaka ili kukabiliana na tatizo la  uharibifu wa mazingira nchini
 
Hatua hiyo inakuja baada ya agizo la Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan  alilolitoa wakati alipokuwa akizindua kampeni ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani mwezi  Disemba 2018  kuwa kila Halmashauri ihakikishe inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka.
 
Amesema hata hivyo tangu agizo hilo lilipotolewa hakuna Halmashauri hata moja iliyoweza kulitekeleza agizo hilo badala yake Halmashauri zilizo nyingi zimekuwa zikitaja takwimu za uongo.

Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye  kongamano la kulinda Mazingira lililofanyika kitaifa mkoani Tabora, Mhe.Kanyasu ameshauri itungwe sheria itakayowabana Wakurugenzi kutekeleza agizo hilo.
 
Amesema endapo agizo hilo likapitishwa na bunge na baadaye kuwa sheria Wakurugenzi watalazimika kupanda idadi hiyo ya miti badala ya ilivyo sasa kila Mkurugenzi kutekeleza agizo hilo kama hiyari.
 
Ameeleza kuwa Halmashauri zilizo nyingi zimekuwa zikitaja takwimu kubwa za miti iliyopandwa lakini anapokwenda kwa ajili ya kuiona  wmiti hiyo imekuwa haionekani na huku  wengine wamekuwa wakiibuka na visingizio kwa vile hakuna idadi hiyo ya miti waliyoipanda.
 
Amesema idadi ya miti ambayo imekuwa ikitajwa na Halmashauri kupandwa imekuwa ya vitabuni isiyo na uhalisia wa aina  yoyote.
 
Ameongeza kuwa hata zile Halmashauri ambazo zimekuwa zikijaribu kupanda zimekuwa hazifikishi idadi hiyo hata zikishapanda zimekuwa hazijishughulishi na kufuatia maendeleo ya miti hiyo.
 
Amesema hali hiyo imepelekea miti iliyo mingi kufa kwa kukosa uangalizi huku mengine kuliwa na mifugo wakati  Halmashauri hizo zimekuwa zikibaki na takwimu zile zile za miti waliyoipanda.
 
Akizungumza Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassani amesema agizo lake lililenga  kila Halmashauri ipande miti milioni 1.5 ikiwa ni lazima na sio hiyari kama Halmashauri zinavyotekeleza.
 
Hata hivyo, Mhe. Samia ameeleza kuwa katika agizo hilo lilikuwa wazi liikitaka kila Halmashauri  ihakikishe inapanda  miti ya aina yoyote ile akitolea mfano mizabibu, miti ya matunda ili mradi tu uwe mti bila kujali miti ya aina gani.
 
Ameongeza kuwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea nchini, Ofisi yake itahakikisha taratibu zinafuatwa za kulifanya agizo hilo liwe sheria.

Benki ya NMB Yamwaga Milioni 500 Kusaidia Wakulima na Wafugaji

$
0
0
Benki ya NMB imetoa Sh. bilioni 500 kwa ajili ya kusaidia wakulima na wafugaji wa viwanda vidogo na vikubwa ili kuinua uzalishaji wa maziwa nchini ikiwamo sekta ya kilimo.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa sekta hizo, Meneja Mwandamizi katika Idara ya Mikopo na Kilimo, Isack Nyangaro, alisema lengo la kufanya hivyo ni pamoja na kwenda na sera ya awamu ya tano ya kutaka nchi ya viwanda, ndio maana wametoa fedha hizo.

Alifafanua kuwa mpaka sasa wametoa Sh.trilioni 2.7 kwa jamii hiyo na kwa sekta ya kilimo wametoa Sh. bilioni 148, kupitia dirisha la watalaam la kilimo hadi kufikia 2019.

Alisema lengo lao ifikapo mwaka 2020 wawe wametoa fedha hizo kwa wafugaji na wakulima ili kuhakikisha wanainua sekta hiyo.

Kwa upande wa Serikali, Waziri wa Mifugo, Luhaga Mpina, alisema anashangazwa kuona Tanzania inazidiwa na Kenya katika uzalishaji wa maziwa ilhali nchi ina malisho bora kuliko nchi hiyo.

Alisema Kenya hivi sasa inazalisha maziwa lita bilioni 5.2, huku Tanzania ikizalisha lita bilioni 2.4, wakati ina malisho bora kuliko nchi nyingine.

Mpina alisema hakuna sababu ya Tanzania kuzidiwa uzalishaji na Kenya wakati kuna kila kitu, huku akiwataka kuhakikisha wanafikia uzalisha kama ilivyo Kenya, ikiwamo kusimamia suala la soko.

Alisema wao kama Serikali wako pamoja katika kuhakikisha mifugo yote inakua salama ili iweze kutoa maziwa mengi kama ilivyo kwa nchi nyingine za Ethiopia na Kenya.

Alisema wamefunga mitambo ya kupima na kugundua magonjwa ya mifugo na wameanza kubaini na kuzuia mlipuko wa magonjwa.

Alisema wanazalisha madawa na chanjo huku akisema wanaagiza dawa kwa mfumo ambao si wa gharama kubwa ambao hauwezi kuleta athari yoyote nchini.

"Tunadhibiti kuhakikisha hakuna chanjo isiyo salama kwa mifugo yetu lengo ni kusonga mbele katika ufugaji," alisema Mpina.

Alisema gharama za chanjo haziwezi kuwa kubwa huku akiwataka wafugaji kujitokeza kwa sababu watapata dawa kwa bei nafuu ikiwamo chanjo sahihi.

Alifafanua zaidi kuwa ndani ya mwaka mmoja watahakikisha chanjo zote 11 zinapatikana hapa nchini ili kuwarahisishia wafugaji kufuga kisasa zaidi bila wasiwasi wa magonjwa.

Aidha, alisisitiza benki kutoa mikopo kwa wafugaji ili kuhakikisha wanakwenda sawa katika uzalishaji wa maziwa hapa nchini.

Waziri Mhagama; Vijana Tumieni Fursa Zilizopo Nchini Kuanzisha Vijiwe Vya Kiuchumi

$
0
0
Na; OWM (KVAU) - SONGWE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao kwa kuanzisha vijiwe vya kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa na Waziri Mhagama wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo na miradi ya vijana iliyopo katika Kituo cha Maendeleo ya Vijana, Sasanda kilichopo Kata ya Nyimbili, Mkoani Songwe.

Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Mhagama alieleza kuwa, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imeendelea kutimiza azima yake ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, hivyo vijana watumie fursa hiyo kujifunza mambo muhimu na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawafanya wabadilishe vijiwe wanavyokaa kuwa vya kiuchumi.

“Tunataka kuona vijana watakapo jifunza kilimo bora, ufugaji wa ng’ombe au nyuki wataweza kuboresha thamani mazao na bidhaa kwa kuanzisha viwanda vidogo ndani ya Mkoa wa Songwe, mkakati wetu katika kituo hiki ni kutoa mafunzo yatakayowawezesha vijana kuongeza thamani ya mazao na bidhaa watakazozalisha ambazo zitakuwa ni kichocheo muhimu katika kufikia maendeleo yao” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa, Takribani vijana 500 kwenye kituo hicho wamejifunza stadi za maisha, ufundi na elimu mbalimbali zinazotolewa kwenye kituo ambazo zitawawezesha kujipatia kipato.

Sambamba na hilo, Mhe. Mhagama aliwahimiza Viongozi wa Mkoa kushirikiana na Ofisi yake ili waweze kuwasaidia vijana ambao wamekwisha anzisha viwanda vidogo vidogo ndani ya mkoa huo kwa kuwawezesha kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuwatafutia soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Aidha, Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kujiunga kwenye vikundi ambavyo ni endelevu na vyenye muelekeo  wa kuanzisha viwanda  vidogo vitakavyowawezesha kujiajiri na kuajiri wenzao na pelekea kufikia uchumi wa kati kama mpango wa maendeleo wa taifa unavyoelekeza.

Pia, aliwaelezea juu ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zitafanyika katika Mkoa huo na kuwataka vijana na wanawake kutumia fursa hiyo kuutangaza vyema mkoa wa Songwe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi alieleza kuwa kituo cha Maendeleo ya Vijana cha Sasanda kimewawezesha vijana kujitambua na kujiwekea malengo ya maisha na kuyatekeleza kwa faida yao, jamii na taifa kwa ujumla.

“Tunatarajia kuanzisha mafunzo na programu zitakazowaelekeza vijana masuala ya kilimo biashara ambacho kitasaidia upatikanaji wa malighafi zitakazokuwa zinahitajika kwenye viwanda vilivyopo nchini,” alisema Kajugusi

Naye Bw. Silia Kibona ambaye ni mnufaika kupitia kituo hicho, aliishukuru Serikali kwa kuwajengea mazingira ya kujifunzia ambayo yamewasaidia kupata mafunzo muhimu na aliwahamasisha vijana wenzie kuhudhuria mafunzo yanayotolewa kwenye kituo hicho.

Kituo cha Maendeleo ya Vijana – Sasanda kilianzishwa mwaka 1979 kwa ushirikiano wa Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni wa Taifa, Vijana na Michezo iliyopo wakati huo pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Uanzishaji wa Kituo hicho ulifuatia kuanzishwa kwa mpango wa kuunda vikundi vya vijana vya uzalishaji mali, uliolenga kuwawezesha vijana wasio na ajira kuweza kujiunga na kufanya kazi za kujitegemea hasa katika sekta ya kilimo.

MWISHO
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images