Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kilicho mkuta Adriunus baada kuvamia msafara wa Rais

$
0
0
Adriunus Landnam (34), mkaazi wa Mkunazini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuingilia msafara wa Rais wa Zanzibar.

Adriunus ambae ni Mfaransa wa Swedzan House akiwa dereva wa gari yenye namba za usajili Z 724 FF  private  akitokea mjini kueleka shamba alipatikana akitenda  kosa hilo huko Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.

Akisoma shitaka hilo Mwendesha Mashitaka wa serikali Asma Juma Khamis, mbele ya hakimu Rauhiya Hassan Bakari, alidai kuwa mtuhumiwa  huyo alipatikana na kosa hilo  siku ya Jumatano ya Febuari 20, mwaka huu mnamo majira ya saa 03:30 asubuhi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwendesha mashtaka alidai kuwa kuingilia msafara wa Rais ni kosa kinyume na kifungu  128 (2) (3) cha sheria namba 7 sheria za Zanzibar.

Video Mpya ya Shilole Ft. Aslay - Ukintekenya

$
0
0
Video Mpya ya Shilole Ft. Aslay - Ukintekenya

Bastola ya Profesa yatoa uhai wa mwanafunzi Kidato cha Nne

$
0
0
Mtu  mmoja aliyetambulika  kwa jina la Jasmini Ngoye (18), mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Lupanga iliyopo manispaa ya Morogoro,  amekutwa amukufa baada ya kujipiga risasi ya kicha huku chanzo cha kifo hicho kikidaiwa kuwa ni msongo wa mawazo. .

Tukio hilo limetokea Jumanne Februari 19, 2019 eneo la Kola B mtaa wa Bogwa na mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa ukiwa na bastola pembeni aina ya Bereta ikiwa na magazini moja na ganda la risasi.

Akizungumzia tukio hilo leo Alhamisi Februari 21, 2019 Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema muda mfupi baada ya tukio hilo, shemeji wa binti huyo, Profesa Hamisi Mahigi alijitokeza na kueleza kuwa bastola hiyo ni yake na anaimiliki kihalali.

Kamanda huyo amesema binti huyo aliacha ujumbe aliouandika katika kitabu chake cha kumbukumbu kabla ya kujipiga risasi, alimkabidhi rafiki yake aliyekuwa akisoma naye darasa moja, Imelda Milanzi.

Katika kitabu hicho mwandishi huyo ameandika; “Ni mtoto asiye na wazazi wake na asiyejua kazaliwa wapi? Mtoto huyu anatamani kukiona kifo chake wakati wowote, mtu yeyote atakayesoma dayari (diary) hii ndiye atakayeandika siku ya kifo chake.”

Amesema profesa huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano. Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Tanzania na Umoja wa Ulaya waazimia kuimarisha Uhusiano

$
0
0
Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuimarisha uhusiano na ushirikiano kwa kufanya majadiliano ya mara kwa mara yatakayojengwa katika misingi ya kuaminiana, usawa, uwazi na kuheshimiana ili kujenga uelewa wa pamoja katika maeneo mbali mbali yenye changamoto kwa manufaa  mapana ya watu wa pande zote mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) na Mkurugenzi wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki, Huduma za Nje katika Umoja wa Ulaya, Bw. Patrick Simonnet wakati wa ziara yake iliyofanyika nchini kuanzia tarehe 17 hadi 20 Februari 2019.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliushukuru Umoja wa Ulaya kwa misaada ambayo umekuwa ukiipatia Tanzania kwa ajili ya utekelezji wa miradi mbalimbali ya maendelea katika sekta za kilimo, nishati na ujenzi wa miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege. 
 
“Umoja wa Ulaya ni mbia muhimu wa Tanzania katika shuguli za maendeleo tokea mahusiano rasmi ya kidiplomasia yalipoanzishwa mwaka 1975; baada ya kusainiwa kwa mkataba wa kwanza wa Rome baina ya kundi la nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (ACP) na nchi wanachaama wa Umoja wa Ulaya”; alisema Mhe. Mahiga.

Viongozi hao walihitimisha mazungumzo yao kwa kuazimia kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya pande mbili hizi katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, ushirikiano wa maendeleo na usalama wa majini, hususan katika pwani ya Bahari ya Hindi. 

Aidha, walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kimataiafa ikiwa ni pamoja na kusaidia juhudi za kudumisha na kuimarisha hali ya amani, usalama na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
21 Februari 2019

Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu' Aachiwa kwa Dhamana

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Mhe. Joseph Mbilinyi 'Sugu' ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi jioni hii 

Mbunge huyo alishikiliwa tangu majira ya saa 1 asubuhi ya leo  Alhamisi tarehe 21 Februari, 2019  kwa tuhuma za kutoa/kutumia maneno ya uchochezi akiwa anazungumza na wafanyabiashara wadogo wadogo. 

Kwamba vitambulisho vya wajasiliamali vimetolewa bila elimu na ni sawa na kunawa mikono kasha kwenda kujisaidia.

Kwa mujibu wa RPC Mbeya Urich Matei ni kwamba Mhe. Mbilinyi ameonekana katika moja ya clip ya video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii akisikiliza hoja na malalamiko ya wananchi na kuyatolea ufafanuzi na ndipo alipoongea kwa kutoa msimamo wake kuhusu zoezi la ugawagi wa vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogo ndogo @ wamachinga na kusema havifai vinastahili kuchomwa moto.

RPC Matei amesema Mhe.Mbilinyi alisikika akitumia maneno ya kashfa dhidi ya mamlaka iliyotoa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogo ndogo pia kutumia lugha zinazopinga zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao.

Sugu ametakiwa kuripoti tena kesho asubuhi

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya February 22

Waziri Mkuu Awaonya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Tuhuma za Ushirikina

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wende Ng’ahara wamalize tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais Dkt. John Magufuli kufanya maamuzi mengine.

Amesema kitendo cha viongozi hao kutoelewana kinaonesha mfano mbaya kwa watumishi walio chini yao, hivyo amewataka wajirekebishe mara moja kwani wameaminiwa na Serikali kuliongoza eneo hilo na si kuwachanganya wananchi.

Waziri Mkuu ametoa kalipio hilo jana (Jumatano, Februari 20, 2019) wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Nyakanazi, kijiji cha Nyakanazi, Biharamuko mkoani Kagera.

Amesema kutokuelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana kufanyiana vitendo vya kishirikina kumesababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika wilaya. “Mliletwa hapa kuiwakilisha Serikali na kusimamia maendeleo ya wananchi nyie mnagombana.”

Awali, Waziri Waziri Mkuu akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera alitembelea kambi ya Nyanza Roads inayojenga barabara ya Nyakanazi-Kabingo, inayounganisha mikoa ya Kigoma na Kagera na kusema kuwa hajaridhishwa na kasi ya mkandarasi huyo.

Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami inaurefu wa kilomita 50 na ilianza kujengwa 2014 ilitarajiwa kukamilika 2016, ambapo kwa sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 60.

“Sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hii, mkandarasi na mhandisi mshauri wote wanaonekana hawapo makini katika kufanya kazi hii. Hii ni aibu kwa wakandarasi wa ndani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia kutokupewa kazi kumbe hawako makini.”

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Dodoma Kupambana na Vifo vya Akina Mama na Watoto Wachanga

$
0
0
Na Adelina Johnbosco, MAELEZO- Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge amezindua rasmi kampeni ya ‘JIONGEZE! TUWAVUSHE SALAMA’ jijini Dodoma, kampeni ambayo imelenga kumsaidia mama mjamzito kujifungua salama.Katika hotuba yake Mhe.Mahenge, amewataka viongozi wote kuwa washiriki na watendaji wa kampeni hii, ili kuhakikisha mama anakuwa salama kwa kutoa elimu ya uzazi popote kwa wananchi.

Aidha, amesema lengo la tamko hili ni kuongeza kasi ya uwajibikaji katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga nchi nzima.

‘’Tumeamua kuchukua kuchukua hatua hii muhimu kwa sababu, kifo cha mama mjamzito au anayejifungua au aliyejifungua na kifo cha mtoto mchanga aliyezaliwa havikubaliki,’’ alisema Dkt. Mahenge.

Hata hivyo, amezitaja sababu kuu zinazosababisha vifo hivi kwa kina mama kuwa ni pamoja na kutokwa na damu nyingi kabla na baada ya kujifungua, kifafa cha mimba, kuchanika kizazi, upungufu mkubwa wa damu, kondo la nyuma kushindwa kutoka, matatizo yatokanayo na ugonjwa wa UKIMWI, uchungu pingamizi, matumizi ya dawa za miti shamba zinazoaminika kuongeza uchungu wa kujifungua na matatizo yatokanayo na kuharibika kwa mimba kwa njia yoyote ile.

Dkt. Mahenge amesema kuwa sababu za vifo vya watoto wachanga ni pamoja na kushindwa kupumua kwa mtoto akiwa tumboni na mara baada ya mama kujifungua, matatizo yatokanayo na kuzaliwa njiti na matatizo ya ulemavu wa kuzaliwa nao (Congenital abnormalities).

Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Tanzania kwa mwaka 2017, vifo vya wanawake wajawazito 556 kwa kila vizazi hai 100,000 vilitokea, na lengo la Serikali ni kupunguza vifo hivi hadi kufikia 292 kwa vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2020.

Ameongeza kuwa kwa mwaka 2017, vifo vya watoto wachanga ni 25 kwa kila vizazi hai 1,000 na lengo ni kupunguza hadi kufikia vifo 16 kwa kila vizazi hai 1,000 ifikapo mwaka 2020.

“Kwa Mkoa wetu wa Dodoma, takwimu za miaka mitano mfululizo zinaonesha bado tunayo kazi kubwa ya kufanya ili kukabiliana na matatizo yanayojitokeza wakati wa ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua hasa unapoangalia namba halisi ya kinamama na watoto wanaofariki. Jumla ya wajawazito 309 walifariki, ambao ni sawa na mabasi 5 ya abairia 62 au waumini wa kanisa/msikiti mzima,’’ amebainisha Dkt. Mahenge

Katika kuhakikisha huduma inaimarika, amesema tayari serikali imejenga na kukarabati kwa awamu miundombinu ya afya katika jumla ya vituo vya afya 22, kufadhili ujenzi wa hospitali tatu za wilaya katika Halmashauri ya Chemba, Chamwino na Bahi ambazo hazikuwa na Hospitali za Wilaya.

Pia Serikali imeongeza bajeti ya dawa ambapo katika mkoa wa Dodoma bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi milioni 900 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 4.3 mwaka 2018/19.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamis Mkunda, amesema amepokea kwa furaha kampeni hii na yuko tayari kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi katika kuhakikisha elimu inamfikia kila mmoja ili tahadhari ichukuliwe kwa kipindi cha ujauzito.

Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. James Charles Kiologwe amesisitiza akina baba kuwa na ushirikiano na wake zao kipindi cha ujauzito, ikiwemo kuhudhuria kliniki, na kuwa waangalizi wao muda wote ili kuwasaidia inapotokea hali ya tofauti kiafya.

Vile vile, ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Dodoma kutoa ushirikiano wa kuyachunguza magari ya kubebea wagonjwa na kuhakikisha yanafanya kazi inayopaswa, hii itasaidia wagonjwa ikiwemo kina mama kufikishwa hospitalini mapema.

Dkt. Kiologwe amewataka wataalamu wa afya kufanya uchunguzi yakinifu ili kubaini mapema dalili zozote za hatari na kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za chanjo, ubora wa matibabu ya utotoni, ushauri kuhusu lishe bora, ikiwemo kutoa lugha nzuri kwa akinamama.

Huu ni mwendelezo wa mapambano dhidi vifo vinavyotokea kwa akina mama wakati na baada ya kujifungua, pamoja na watoto wao, kwani serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa Afya ya Uzazi na Mtoto, ilizindua kampeni hii mnamo tarehe 06 Novemba, 2018 hapa Jijini Dodoma, ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa kusaini tamko la ahadi mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

NIDA: Usajili na Utambuzi wa Wanchi ni Bure

$
0
0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwakumbusha wananchi wote kuwa Huduma ya Usajili na Utambuzi wa Watu kwa ajili ya kupatiwa Kitam- bulisho cha Taifa inatolewa BURE. Mwananchi anatakiwa kufika katika ofisi za NIDA akiwa na nakala (Photocopies) za viambatisho vyake muhimu.

Waombaji wote wa Vitambulisho vya Taifa mnakumbushwa kuwa “Rushwa ni Adui wa Haki. Usikubali kudai, kutoa wala kupokea Rushwa.” Kitambulisho cha Taifa ni haki yako ya msingi na hakiuzwi.

Hakikisha unahudumiwa katika Ofisi au Vituo rasmi vya Usajili vya NIDA na Afisa wa NIDA na sio Vishoka wanaojipenyeza kwenye zoezi.

Ukiombwa Rushwa Toa Taarifa kwa Mawasiliano :-

Simu: 0800758888 au 0673 333 444 au 0759102010 au 0765201020, Barua: S.L.P 12324 Dar es Salaam, Barua pepe (email): nida.tanzania@nida.go.tz. Tembelea tovuti yetu: www.nida.go.tz, Facebook nidatanzania, twitter @nidaTanzania au twitter.com/nidatanzania

Imetolewa na:- Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Dawa Lishe Ya Asili Ya Kunenepesha Na Kuongeza Mwili.

$
0
0
Je umekonda  na  kudhoofu  mwili  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile msongo  wa  mawazo  na  kuugua  maradhi  mbalimbali kama  vile  kisukari nakadhalika ?

Unahitaji  kurejesha  mwili  wako  katika  hali  yake  ya  kawaida ?  Unahitaji kuongeza mwili na uzito wako ?

Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi  HII  NI  HABARI NJEMA  SANA  KWAKO.

Neema  Herbalist  ni  duka  la  kuuza  dawa  mbalimbali  za  asili.  Tunayo   DAWA  LISHE  YA  ASILI  ambayo inanenepa  mwili  kwa watu  walio  dhoofu  na  kukonda  kwa  sababu  mbalimbali.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa  wateja  wetu  wa  jijini  DAR  ES  SALAAM  ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu  tunayo  huduma  ya  HOME & OFFICE  DELIVERY

Na  kwa  wateja  wetu  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  DAR ES  SALAAM  tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  mbalimbali  kama  vile  MABUS  au  BOTI kwa  wateja  wetu wa  ZANZIBAR.

Wasiliana  nasi  kwa  SIMU NAMBA : 0693  005 189


Watumishi Wa Serikali Wanaodaiwa Kodi Ya Ardhi Kushtakiwa

$
0
0
Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Dkt. Angeline Mabula ameagiza kuanza mchakato wa kuwaorodhesha watumishi wa umma ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi hadi sasa ili wafikishwe katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba.

Dkt. Mabula ameyasema hayo alipofanya ziara katika Wilaya ya Bunda na Serengeti mkoani Mara na wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wakati wa ziara yake inayoendelea ya kuhamasisha malipo ya kodi ya pango la ardhi  katika kanda ya ziwa.

“Nyinyi watumishi wa Serikali mnatakiwa kuwa wa mfano katika kulipa kodi za serikali kwa sababu hatuwezi kwenda kudai wengine wakati sisi wenyewe hatujalipa kodi ya pango la ardhi, na kokote ntakapopita nataka majina ya watumishi ambao hawajalipa ili wafikishwe katika mabaraza” alisisitiza Dkt. Mabula.

“Mheshimiwa Rais anasimamia miradi mikubwa hapa nchini kama ule wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa Mto Rufiji, Stiegler's Gorge na uimarishaji wa Shirika la Ndege la Tanzania ambayo miradi hii yote inategemea kodi na mapato ya ndani, hivyo ni lazima tumuunge mkono katika kulipa kodi hizi” aliongeza Dkt. Mabula.

Wakati akiwa Wilayani Ukerewe alipokea taarifa ya afisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Ndugu Tewe Shaban kuwa hadi sasa halmashauri yake imeshakusanya jumla ya Tsh 41,288,175 wakati lengo ni 100,000,000 kwa mwaka wa fedha 2018/2019, ambayo ni sawa na 41.2% iliyokusanywa.

Afisa huyo alimueleza Dkt. Mabula kuwa hadi sasa jumla ya ilani 131 zenye thamani ya Tshs 54,446,550 za madai ya kodi ya ardhi zimesambazwa kwa wadaiwa kodi ya ardhi ambao wameanza kupunguza madeni yao na mpaka sasa wameshalipa Tshs. 3,100,700 na kubaki Tshs. 51,345,850.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Dkt. Mabula alishangazwa na ukusanyaji huo hafifu wa maduhuli ya Serikali na alimuagiza Afisa huyo kuwafikisha mahakamani wadaiwa sugu wa kodi ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo, na aanze na watumishi wote wa Serikali katika halmashauri ya wilaya ya Ukerewe.

Katika kuhakikisha linatekelezwa hilo Dkt. Mabula akaagiza kuwepo kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi atakayesimamia kesi hizo na kuzitolea hukumu kwa wadaiwa sugu waweze kulipa kwa wakati na kama hawatotekeleza basi milki zao zitauzwa ili kulipwa deni hilo.

Akiwa wilayani Bunda Dkt. Mabula alimuagiza afisa ardhi mteule kumfikishia majina ya maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Bunda ambao wanadaiwa kodi ya pango la ardhi na hawajalipa hadi sasa wakati muda wa kulipa kwa hiari ushaisha tangu tarehe 31 januari 2018.

Vivyohivyo Dkt. Mabula akiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Serengeti amamuagiza Afisa Ardhi Mteule kukabidhi majina ya watumishi wa umma ambao wadaiwa wa kodi ya ardhi kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili waweze kufikishwa katika baraza ardhi iwapo watakuwa hawajalipa.

Nkoma: Tiba Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
NKOMA
_________________________
NKOMA Ni dawa bora ya nguvu za kiume  yenye mchanganyiko wa mitishamba (7) yenye maajabu yafuatayo/

🔖 (1) inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimalisha misuli ya uume uliolengea wakati wa tendo la ndoa/
🔖 (2) Kurefusha maumbile ya kiume yaliyorudi ndani kuazia nchi 5 - 9/
🔖 (3) kunenepesha uume cm 5 ya upana itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15 - 20 kwa tendo la kwanza na utakuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya 2-4 bila hamu kuisha/

📌 Na inatibu kabisa, unashauriwa uitumie dawa hii kama kinga ya magonjwa sugu./
 📌 Haijalishi umri hata kama una miaka 85 itumie huanza kufanya kazi dk 50 tu na haina madhara yoyote kwa mtumiaji/

📍📍📍📍📍📍📍📍📍
            MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA.
_________________________
🔖 (1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖 (2)Choo kama cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(4)Kaswende/
🔖(5)Gono/

📌Haya yote husababisha kuishiwa nguvu za kiume na kuwa na uume mdogo/
📌 Itumie leo, bado hujachelewa ni tofauti na nyingine.
_________________________
DR MAKOBA ANAPATIKANA DAR ES SALAAM, PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO.
___________________________
WASILIANA NA
Dr MAKOBA SIMU.
📞0754832349
📞0683490600
____________________________
*****************************

Wachimbaji madini watakiwa kuwa na Mpango wa Ufungaji Mgodi

$
0
0
Na Greyson Mwase, Pwani
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amewataka wachimbaji wa madini  ya ujenzi aina ya kokoto katika mkoa wa Pwani kuwa na Mpango wa Ufungaji Mgodi utakaotumika kama mwongozo wa kuhakikisha mazingira yanaachwa yakiwa katika hali salama mara baada ya kumalizika kwa shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

Profesa Kikula aliyasema hayo jana tarehe 21 Februari, 2019 katika nyakati tofauti alipofanya ziara yake katika migodi  inayojishughulisha na shughuli za uchimbaji wa madini ujenzi aina ya kokoto iliyopo katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani yenye lengo la kutembelea wachimbaji wa madini hayo pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Profesa Kikula katika ziara hiyo akiwa ameambatana na Kamishna – Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, wataalam kutoka Makao Makuu ya Tume ya Madini jijini Dodoma, Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi wa Lugoba pamoja na waandishi wa habari, Profesa Kikula alitembelea migodi ya Sisti Mganga, Gulf Concrete Company Limited na  Yaate Company Limited iliyopo katika Wilaya ya Bagamoyo.

Akizungumza katika nyakati tofauti mara baada ya kutembelea migodi hiyo, Profesa Kikula aliwataka wamiliki wa migodi kuhakikisha wanakuwa na mipango ya ufungaji migodi mapema badala ya kusubiri mpaka shughuli za uchimbaji madini zinapomalizika hivyo kufanya zoezi la ufungaji wa migodi kuwa gumu huku wakiacha mazingira yakiwa hatarishi.

“Ninapenda kuwakumbusha kuwa suala la kuwa na Mpango wa Ufungaji wa Migodi ni la lazima kulingana na Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake, hivyo ninawataka kuhakikisha mnakuwa na mpango ili kuhakikisha mashimo hayaachwi wazi,” alisema Profesa Kikula.

Awali akiwa katika mgodi unaomilikiwa na Sisti Mganga Profesa Kikula  alielezwa mafanikio ya mgodi huo ikiwa ni pamoja na kokoto za mgodi huo kutumika katika ujenzi wa daraja la Mto Wami uliopo mkoani Pwani,  reli ya kisasa ya standard gauge na utengenezaji wa marumaru kwa ajili ya soko la ndani ya nchi.

Katika hatua nyingine Mganga alitaja changamoto zinazoukumba mgodi huo kuwa ni pamoja na tozo kubwa kutoka katika halmashauri na tozo nyingine zinazotozwa na kijiji cha Kihangaiko  pasipo kuwa na risiti pamoja na ukosefu wa vifaa vya kisasa.

Profesa Kikula alisema kuwa, suala la tozo litafanyiwa kazi kwa kuliwasilisha mamlaka za juu kwa ajili ya kufanyiwa kazi na kusisitiza kuwa nia ya Serikali kupitia Tume ya Madini, ni kuhakikisha wachimbaji wa madini hususan wadogo wanafanya kazi katika mazingira mazuri yenye faida kubwa huku wakilipa kodi mbalimbali Serikalini pasipo vikwazo vyovyote.

Wakati huo huo, akiwa katika mgodi wa uzalishaji wa kokoto wa Gulf  Concrete Limited Profesa Kikula alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa mgodi huo kuhakikisha wanarekebisha kasoro ya mazingira kwa kuhakikisha vumbi linalotoka wakati wa shughuli za uchimbaji wa kokoto halisambai kwani linaathiri wananchi  wa vijiji vya jirani katika mgodi huo.

Alisema ni vyema wakazingatia Sheria ya Mazingira kwani vumbi mbali na kuathiri wananchi wanaoishi katika vijiji vya jirani linaweza kuathiri wafanyakazi wa mgodi huo.

Aidha, alituaka mgodi huo kuendelea kuhakikisha unatoa huduma kwa jamii inayozunguka mgodi huo na kutumia huduma za ndani ya nchi kama vile bidhaa pamoja na ajira kwa wazawa.

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula akiwa katika mgodi wa kuzalisha kokoto wa Yaate Co. Limited, mbali na kuupongeza mgodi kwa kuaminiwa na kupewa kazi ya kusambaza kokoto kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge unaotelekezwa na kampuni ya Yapi  Merkezi na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii inayouzunguka mgodi huo pamoja na ajira, aliutaka mgodi huo kuendelea kununua bidhaa/huduma kutoka kwa wananchi.

“Kutoa huduma bora kwa wananchi wanaozunguka mgodi kunaboresha mahusiano na kupunguza migogoro ya mara kwa mara inayoweza kujitokeza.

Awali akielezea mafanikio ya mgodi, Mkurugenzi Mtendaji wa Yaate Co. Limited, Eugen Mikongoti alisema  mradi umenufaisha watanzania wengi kwa kuchangia maendeleo ikiwa ni pamoja na ulipaji wa zaidi ya shilingi bilioni 1.31 ambazo zimelipwa kama ushuru wa madini  kati ya kipindi cha mwezi Juni, 2018 hadi Januari, 2019 na shilingi milioni 338.8 zilizolipwa kama mrabaha.

Alieleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na utoaji wa fursa za ajira kwa watanzania hususan vijana wanaozunguka mgodi na kuziwezesha kampuni zinazomilikiwa na wazawa kushiriki katika miradi mikubwa  hivyo kuzijengea uwezo wa kitaalam na kupata fursa.

Mikongoti alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kuwezesha maendeleo ya wanachi wanoishi karibu na mgodi kupitia huduma za jamii ambapo mpaka  sasa mgodi huo unaendelea na ujenzi wa nyumba za watumishi na kuhudumia wananchi katika zahanati iliyopo mgodini.

Katika hatua nyingine Mikongoti alipongeza kazi kubwa zinazofanywa na Tume ya Madini chini ya Mwenyekiti wake Profesa Kikula ikiwa ni pamoja na kuwatembelea, kuwapa elimu na kutatua changamoto mbalimbali.

Ujenzi Wa Viwanda Vya Dawa Kuokoa Mabilion Ya Shilingi Nchini

$
0
0
Na WAMJW – PWANI
WAZIRI Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amefanya ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa kiwanda vya Dawa cha Vista Pharma Ltd na Kairuki Pharmaceutical Ltd  vinavyoendelea kujengwa kwa kasi katika Mkoa wa Pwani.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy alilenga kujionea na kutatua Changamoto zinazowakumba Wawekezaji nchini hususani katika Viwanda vya Dawa ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachoendelea kupotea kutokana na kuagiza Dawa nje ya nchi.

Waziri Ummy amesema kuwa katika kila Shilingi 100 ambayo Serkkali inatumia kununua Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba, Shilingi 94 inapotea nje ya nchi, ambapo kumalizika kwa Viwanda hivi kutasaidia pesa hiyo kubaki ndani ya nchi na kutumika katika shughuli nyingine za  Maendeleo kwa Wananchi.

“Katika kila Shilingi 100 ambayo Serikali inatumia kununua Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba, Shilingi 94 tunaipeleka nje ya nchi kununua Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba, na ndiomaana nimefanya ziara hii pamoja na viongozi wa Mkoa na kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Kituo cha uwekezaji ili kuokoa fedha hiyo inayopotea nje ya nchi” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendele kusema kuwa kumalizika kwa Viwanda hivi kutasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa Dawa za kutosha na kwa bei rahisi, jambo litalosaidia kuimarika kwa huduma za Afya nchini.

 ”Dawa kupatikana kwa wingi na kwa bei rahisi na kwa haraka zaidi, kwasababu kuagiza Dawa nje ya nchi MSD anatumia mpaka miezi 6  mpaka ifike Tanzania” alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewaagiza Tanesco ndani ya Mkoa kuhakikisha wanaleta huduma ya umeme ndani ya wiki moja ili hatua za mwanzo za ufungaji wa mashine katika Viwanda hivyo uanze Mara moja.

Pia, Waziri Ummy amewaagiza Mamlaka ya Maji Mkoani Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaleta huduma ya maji ndani ya Machi 15 katika eneo hilo la Viwanda ili kuharakisha shughuli za ujenzi.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amewashukuru wawekezaji hao wa Ndani kwa maamuzi mazuri aliyochukua ya kuwekeza katika Viwanda vya Dawa ili kuisaidia Jamii ya Watanzania ambao Dawa bado imekuwa ni changamoto licha ya Jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali katika kukabikiana na changamoto hiyo.

#TunaboreshaAfya

Kwanini Uhangaike Na Magonjwa Yanayowezekana Kupona?..........Tiba Sahihi Imewasili

$
0
0
Asilimia 60- 80 ya wanaume wameathilika kisaikologia baada ya kujiona wako tofaut na wengine kimaumbile na kupungukiwa nguvu za kiume , mwanaume aliekamilika kimaumbile anatakiwa awe na maumbile yasiyo pungua nchi 6-8 tofautina hapo anaupungufu ,

zipo sababu nyingi zinazosababisha mapungufu hayo ambazo ni :- upigaji wa punyeto ( mastervation) ,ngili,KISUKARI,vidonda vya tumbo,maumivu ya mgongo ama kiuno,unene(kitambi) tumbo kuunguluma na kujaa ges, matatizo haya huchangia kwa kiasi kikubwa sama kukosa nguvu za kiume vilevile maumbile kuwa madogo na kiingia ndani (kunywea)

SUPER KAMULI  :- hii nidawa kiboko kwa matatizo ya nguvu za KIUME,ni dawa ya Asili tuliyo jaaliwa na mwenyezi MUNGU huimarisha misuli ya uume wakati wa tendo la ndoa na kuzalisha viini vya uzazi (manii) vilevile utaludia tendo zaidi ya mara tatu bila ham kuisha pamoja na kuchelewa kufika kilele takiriban dk 20 - 45 kwatendo moja.

GEMBE 2 MIX :- hii nidawa ya Asili Hurefusha na kune nepesha maumbire madogo ya UUME , hurefusha urefu wa nchi (6-8 )na unene wa sm( 3-4) huanza kufanya kazi masaa machache baada ya kuanza kuitumia,( tiba niyakudumu ikishakutibu,

Nina dawa ya kutokomeza KISUKARI na kupona kabisa hata kama kimekusumbua kwa mda mrefu mpaka ukajikatia tamaa  tiba ipo na utatumia vyakula vyote bila tatizo baada ya kupona ,

Pia ninadawa ya Vidonda vya tumbo,Ngiri, miguu kuwaka moto, mvuto wa mapenz ( kumvuta mke /mme/mpenzi/hawara/ama yoyote unaemuhitaji) dawa za biashara, uzazi kwa akina mama na akina baba (pande zote) pata dawa ya bawasili bila kufanyiwa upasuaji,

KWAMAELEZO NA MSAADA WASILIANA NA DR SILIMBA NAPATIKANA DAR ES SALAAM

 SM O620510598 / 0743543944

Nb km huna nafasi huduma hii inakufikia popote ulipo kwaware wa mikoani tunatuma kwa njia ya mabasi

Waziri Wa Kilimo Abainisha Jitihada Za Serrikali Kwenye Mapinduzi Ya Kilimo Nchini

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuweka mazingira bora ya kuleta mapinduzi katika kilimo.

Japokuwa Kilimo kinachangia karibu asilimia 30 ya Pato la Taifa, ukuaji wa Sekta ya Kilimo bado hauridhishi kutokana na changamoto zilizopo, japo kumekuwepo na mwelekeo chanya katika siku za karibuni. Kulingana na taarifa zilizopo za hivi karibuni ukuaji wa sekta ya kilimo umefikia asilimia 7.1

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo jana tarehe 21 Februari 2019 wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa asasi zinazotoa huduma ndogo za fedha vijijini kwa Wajasiriamali Wadogo (TAMFI) katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania – Dar es salaam.

Alisema kuwa kwa kutambua hilo, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara za Sekta ya Kilimo (ASLMs) kwa kushirikiana na wadau wa sekta inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Programme Phase Two-ASDPII).
 
Lengo kuu la ASDP II ni kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo (mazao, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha na usalama wa chakula na lishe.
 
Alisema kuwa Utekelezaji wa lengo hilo ni kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula; kuimarisha uchumi; kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda; na kuongeza ajira. Ili kufikia malengo haya; Utekelezaji wa ASDP II utazingatia mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
 
Alizitaja jitihada zingine katika kuleta mapinduzi ya kilimo ambazo ni Kuanzishwa kwa eneo maalum la kuboresha mnyororo wa thamani kwa mazao mbalimbali (yaani The Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT), Kuanzishwa kwa Program ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (yaani Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance Support Programme –MIVARF) ambao lengo lake kuu ni kusaidia nyanja mbalimbali muhimu katika kuendeleza kilimo cha kisasa nchini na Kuanzishwa kwa Benki ya Kilimo (yaani TADB) ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wakulima na shughuli za kilimo nchini.
 
Alisema kuwa Jitihada za dhati zinahitajika kuwashawishi vijana kwa njia mbalimbali ili nao waingie katika biashara ya kilimo hasa katika uboreshaji wa mnyororo wa thamani kutokea shambani hadi kwa mlaji.

Kuwepo kwa huduma kama bima ya afya kwa wakulima na makazi bora kunaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kuwafanya watu wengi zaidi haswa vijana kujihusisha na kilimo kwa njia za kisasa zaidi na usalama wa afya zao na makazi yao pia.

Allisema kuwa hiyo itakuwa njia bora ya kutatua mahitaji yao na kuwasaidia wakulima vijana kufanya shughuli za kilimo pamoja na kilimo biashara kwa ufanisi. “Umefika wakati sasa tuhamasishe kuwa na Kilimo cha mashamba makubwa na ya kati yatakayopelekea kuzalisha kwa wingi na kwa tija” Alikaririwa Mhe Hasunga
 
Mkutano huo utafanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 21 Februari 2019 mpaka kesho tarehe 22 Februari 2019 ukiwa na lengo la kujadili namna bora ya kuwajengea wakulima uwezo wa kustahimili matukio mbalimbali kwa kutumia huduma za fedha vijijini, namna ya kuwanufaisha wakulima na huduma za hifadhi ya jamii, bima ya afya, matumizi ya teknologia rafiki ya kuwafikishia huduma za fedha vijijini, makazi bora kwa wakulima pamoja na elimu ya fedha vijijini.

Mkutano huo umewajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo maafisa kutoka serikalini, watoa huduma za kifedha vijijini, wataalam wa mambo ya kifedha, wakulima, na wawakilishi wa mashirika.

MWISHO

Video Mpya: Nini - Usiniendeshe

$
0
0
 Video Mpya: Nini - Usiniendeshe

Video Mpya: Lyyn Ft Shetta - Chomeka

$
0
0
Video Mpya: Lyyn Ft Shetta - Chomeka

Atiwa Mbaroni Kwa Kuwalisha Wananchi Nyama ya Mbwa Huku Akiwadanganya ni ya Mbuzi

$
0
0
Mkazi wa kijiji cha Mitonji,kata ya Mbuyuni wilayani Masasi Mkoani Mtwara,Dismasi Malikitu maarufu kizito,anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuwauzia wananchi nyama ya mbwa huku akiwadanganya ni nyama ya mbuzi.

Mtendaji wa Kijiji cha Mitonji,Yunisi Makolo amethibitisha kuhusu tukio hilo.

==>>Sikiliza hapo chini

Mahakama Kuamua Hatima ya Lipumba na Maalim Seif CUF Leo

$
0
0
Siku chache baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kutengua Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Prof. Ibrahim Lipumba, leo mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi mwingine kuhusu hatima ya uenyekiti wake.

Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Shauri hilo namba 23 la mwaka 2016, lililofunguliwa na chama hicho upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, linatarajiwa kutolewa uamuzi leo mbele ya Jaji Benhajj Masoud wa Mahakama Kuu, baada ya awali kushindwa kusikilizwa na Jaji Wilfred Dyansobera aliyehamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara.

Profesa Lipumba alitangaza kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho Agosti 2015, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa madai kuwa haungi mkono makubaliano yaliyofikiwa na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Prof. Lipumba alichukua uamuzi huo baada ya vyama hivyo kumkaribisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuwa mgombea wao wa urais.

Hata hivyo, mwaka mmoja baadaye Prof. Lipumba alimwandikia barua Katibu Mkuu, Maalim Seif, akiomba kurudi katika nafasi yake.

“Nimemwandikia Katibu Mkuu (Maalim Seif Sharif Hamad) kutengua barua yangu niliyoandika tarehe 5 Agosti, mwaka 2015. Sasa nasubiri majibu kutoka kwa Katibu Mkuu baada ya barua yangu kujadiliwa na ngazi husika za chama,” alisema Lipumba kwenye barua yake ya wakati huo.

Ombi hilo la Prof. Lipumba lilikataliwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho hasa wanaomuunga mkono Maalim Seif, hivyo kusababisha mgawanyiko kati ya wanachama wanaomuunga mkono profesa huyo wa uchumi na wale wanaomuunga mkono Maalim Seif.

Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alitangaza kumtambua Prof. Lipumba kama mwenyekiti halali wa (CUF), jambo lililopingwa vikali na baadhi ya wanachama wa chama hicho wakiongozwa na Katibu Mkuu.

Mtafaruku huo ndio uliosababisha kufunguliwa kwa kesi ya kikatiba na kambi ya Maalim Seif kupinga uenyekiti wa Prof. Lipumba.
 
Tangu kurejea kwake kama mwenyekiti wa chama hicho, kumekuwa na mgawanyiko na mivutano baina ya viongozi na wanachama wa chama hicho.

Hali hiyo ilisababisha hata baadhi ya wabunge wa chama hicho kujiuzulu na wengine kutenguliwa ubunge wao baada ya mwenyekiti huyo kuteua wabunge wapya wa kambi yake.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images