Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yainyang'anya Manispaa ya Ilala Bilioni Tatu Za Mradi Wa Kimkakati Wa Machinjio Ya Vingunguti

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
SERIKALI imeinyang'anya Manispaa ya Ilala, mkoani Dar es Salaam shilingi bilioni 3 ilizoipatia kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Kimkakati wa Machinjio ya Kisasa wa Vingunguti, baada ya Manispaa hiyo kushindwa kutekeleza kwa wakati mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.5.

Hatua hiyo imechukuliwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo wa Kimkakati katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar ers Salaam.

Alisema kuwa Serikali ilitoa kiasi cha Sh. bilioni 3 kati ya Sh. bilioni 8.5 za kukamilisha mradi wa Machinjio ya Vingukuti kuanzia mwezi Mei, 2018, chakushangaza hadi sasa fedha hizo hazijatumika hata senti moja.

"Fedha haziwezi kukaa kwa mwaka mzima bila matumizi ilihali kuna maeneo mengine ambako fedha hizo zinahitajika  kwa ajili ya utekelezaji wa miradi, hivyo tunazichukua fedha hizi na Manispaa ya Ilala mtalazimika kuomba upya mtakapokuwa mmejipanga" Alieleza Dkt. Kijaji.

Alibainisha kuwa kwa mujibu wa taratibu za fedha za Serikali zinazopelekwa kwenye miradi zinatakiwa zianze kutumika ndani ya miezi mitatu lakini Manispaa ya Ilala haijazitumia fedha hizo huku karibu Mwaka wa Fedha ukikaribia kumalizika.

"Tunaiangusha dhamira njema ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwahudumia Watanzania waliosubiri kuhudumiwa kwa upeekee ndo maana tukaanzisha miradi hii ya kimkakati ya kuongeza mapatio ya halmashauri na mkaleta maandiko yenu Serikali ikatoa fedha kumbe hamko tayari na mnatukwamisha kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi" Alisema

"Tumewapatia fedha Mmeshindwa!, kwahiyo wana Ilala na WanaVingunguti, kwamba Serikali yao ina dhamira njema lakini wapo watu wanaotuangusha kwahiyo tutazichukua fedha hizi mpaka hapo Manispaa ya Ilala watakapo leta mpango kazi unaotekelezeka na siyo huu ambao hawakujiandaa" alisisitiza Dkt Kijaji

Dkt. Kijaji alisema kuwa kabla ya kuomba fedha za miradi ya kimkakati ni lazima masuala yote ya upembuzi yakinifu yawe yamefanyika na kama hayakufanyika basi Manispaa ilimdanganya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wazifri wa Fedha ambaye aliridhia Manispaa ya Ilala ipewe fedha hizo.

Naye Naibu Kamishna wa Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja, alieleza kuwa Manispaa ya Ilala, imekiuka mkataba ama makubaliano ya kupewa ruzuku ya sh. bil 8.5 kwa ajili ya mradi huo na ni lazima sheria ya fedha ichukue mkondo wake kwa uzirejesha fedha hizo kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina hadi hapo watakapo kuwa tayari.

"Mhe. Naibu Waziri, kuna dosari kubwa katika utekelezaji wa mradi huu na kwa kuzingatia malengo ya miradi kama hii tukienda namna hii, hatuwezi kufanikiwa, sisi tulidhani walipoleta maombi ya mradi huu walikuwa wamejiandaa kumbe sivyo" aliongeza Dkt. Mwamwaja

Kwa upande wake Afisa Mipango wa Manispaa ya Ilala Bw. Ando Mwankuga, alikiri kuwa kulikuwa na ucheleweshaji wa kuanza kutekeleza mradi huo kwa kile alichodai ni kuchelewa kwa mchakato wa kufanya ununuzi na mabadiliko ya mara kwa mara ya  kiufundi kutoka kwa mtaalam mshauri wa mradi huo.

"Ucheleweshaji huu si wa makusudi bali ilikuwa ni kuhakikisha tunafuata  taratibu zote za ununuzi na kuhakikisha kuwa mradi utakaojengwa uwe na ubora unaotakiwa na unaolingana na thamani ya fedha na tunatarajia kuanza kuutekeleza Machi 10, 2019" aliongeza Bw. Mwankuga

Manisapaa ya Ilala, ilikuwa miongoni mwa Halmashauri na Manispaa 17 nchini zilizopatiwa ruzuku na Serikali kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 147 katika awamu ya kwanza katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati itakayochochea upatikanaji wa mapato ya ndani na kuzijengea uwezo Serikali hizo za Mitaa na miradi hiyo inatakiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 18 kuanzi Mwezi Mei, 2018.

Mwisho

RC Makonda Atimiza Ahadi Ya Kumpatia Mtaji Wa Milioni 5 Mama Mzazi Wa Marehemu Msanii Godzilla

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  ametimiza ahadi aliyotoa ya kumpatia Mama Mzazi wa Marehemu Msanii Godzilla kiasi cha shilingi milioni 5 kama mtaji wa kufungua duka la kisasa la kuuza dawa za binadamu (pharmacy) itakayowezesha familia kujikwamua kiuchumi.

February 16 wakati wa maziko ya Msanii Godzilla,mama yake alisema Godzilla alikuwa na ndoto ya kumpatia  mtaji wa shilingi milioni 5 kwaajili ya kufungua Pharmacy itakayomsaidia kuendesha maisha na tayari alikuwa ameshamkabidhi milioni 4 lakini baada ya Marehemu Godzilla kuugua ghafla Mama huyo alisema alilazimika kutumia fedha hizo kumuuguza mwanae na kusababisha fedha kuisha. 

Baada ya kusikia hilo, RC Makonda alimfuta machozi mama huyo na kumuahidi kumkabidhi Fid Q pesa hiyo ili mama atimize ndoto yake kitu ambacho amekitekeleza jana

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Agoma Kukagua Ukarabati Wa Shule Ya Sekondari Pugu

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amelazimika kuahirisha kagua ukarabati wa Shule Kongwe ya Sekondari Pugu, Jijini Dar es Salaam baada ya uongozi wa mkoa na Manispaa ya Ilala kueleza kuwa hawajui lolote kuhusu ukarabati huo unao gharimu zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa madai kuwa hawajashirikishwa.

Dkt. Kijaji amechukua uamuzi huo baada ya Kaimu Katibu Tawala  wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Yokobeth Malisa, Afisa Mipango Manispaa ya Ilala Bw. Ando Mwankuga, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Dar es Salaam Mwl. George Lukoa  na Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Mwl. Jovinus Mutabuzi, wote kwa pamoja, kuukana mradi huo.

Mradi huo unatekelezwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania-TEA chini ya ukandarasi wa Shirika la Nyumba Tanzania- NHC, lakini Mkataba wake pamoja na mawanda ya kazi inayotakiwa kufanyika haijulikani mkoani, Manispaa ya Ilala pamoja na uongozi wa shule.

"Mradi huu una changamoto kubwa, hatujawahi kuona mkataba wake kuanzia mkoani hadi Manispaa ya Ilala pamoja na uongozi wa shule, kwahiyo hatujui umegharimu kiasi gani na ni vitu gani viko kwenye Mkataba huo jambo linalotuwia vigumu kuuelezea" Alisema Bw. Ando Mwankuga

Bw. Mwankuga alieleza kuwa yeye ndiye mwenye taarifa ya miradi yote inayotekelezwa katika ngazi ya Manispaa ambayo kwa mujibu wa taratibu na kanuni hupitishwa kwenye vikao mbalimbali ikiwemo Kamati ya Ushauri ya Manispaa na Baraza la Madiwani, na kwamba mradi huo wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu haujawahi kujadiliwa

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Jovenus Mutabuzi alieleza kuwa taarifa alizonazo ni za kuambiwa kwamba mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 900, lakini hajawahi kushirikishwa kikamilifu kuhusu ukarabati huo na yeye amekuwa akiwaona mafundi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa wakiingia kufanyakazi na kutoka shuleni hapo.

"Mhe. Naibu Waziri mimi naona tatizo kubwa hapa ni mawasiliano hafifu kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mamlaka ya Elimu Tanzania na Halmashauri Manispaa ya Ilala, ndio maana haya yote yamejitokeza" alisisitiza Mwl. Mutabuzi

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Yokobath Malisa, aliahidi kupeleka taarifa kwa Katibu Tawala wa mkoa huo ili aitishe vikao vya wadau wanaohusika ili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

Alieleza kuwa yeye binafsi akiwa miongozi mwa wasimamizi wa masuala ya miradi ya maendeleo ya mkoa wa Dar es Salaam hakuwa na taarifa ya uwepo wa mradi huo na haujawahi kuripotiwa mahali popote kwenye vikao.

Kwa upande wake Dkt. Kijaji ameelezea kushangazwa na hali hiyo kwamba mradi kama huo wenye thamani kubwa, utaratibu wake wa ushirikishanaji miongoni mwa wadau wanaohusika haujakaa vizuri jambo lililomfanya kuamua kusitisha zoezi la kukagua ukarabati wa shule hiyo.

"Kama hali ndiyo iko hivi! kila kiongozi hapa kuanzia mkoa, Manispaa hadi uongozi wa Shule mmeukana mradi huu kwamba hamuujui, wakati Mwalimu wa Takwimu wa Manispaa anasema anaufahamu pia juujuu, sasa mimi nitakagua nini? Tuondoke!" alielezea kwa masikitiko Dkt. Kijaji na kuahidi kulifanyiakazi suala hilo

Serikali imetoa zaidi ya  sh. bilioni 42 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Sekondari 42 kati ya shule 88 kongwe zilizopo nchini kote zikiwemo shule sita za Sekondari mkoani Dar es Salaam za Jangwani,  Azania, Tambaza, Zanaki, na Pugu.

Mwisho

Watu 34 washikiliwa na Polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma mbalimbali

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 34 kwa tuhuma mbalimbali katika misako iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Mbeya kama ifuatavyo:-

KUINGIA NCHINI BILA KIBALI @ WAHAMIAJI HARAMU.
Mnamo tarehe 16.02.2019 majira ya saa 18:30 jioni huko eneo la mpakani, Kata ya Igawa, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Polisi walifanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wawili raia wa nchini Ethiopia ambao ni DANIEL HARAM [29] na SADACK DADAGO [22] wakiwa wameingia nchini bila kibali. Taratibu za kisheria zinafanyika na upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA POMBE MOSHI [GONGO]
Mnamo tarehe 17.02.2019 majira ya saa 11:30 asubuhi huko eneo na Kata ya Nkuyu, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa doria walimkamata JOHN MWASEBA [31] Mkazi wa Nkuyu Wilayani Kyela akiwa na Pombe Haramu ya Moshi @ Gongo ujazo wa lita 13. Uchunguzi unaonyesha kuwa mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa Pombe hiyo. Upelelezi unaendelea.

KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
Mnamo tarehe 16.02.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Mwakapangala, Kata ya Nsalala, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakifanya upekuzi katika magari mbalimbali walimkamata PRISCA PETER [32] mfanyabiashara, mkazi wa Uyole akiwa na:-
  1.     Pombe aina ya Prince chupa 20,
  2.     Kinywaji aina Power asili chupa 60,
  3.     Maziwa aina ya Super shake chupa 12,
  4.     Biscuits aina chiko dazan 2
Bidhaa hizo zote hazikulipiwa ushuru akiwa anazisafirisha kwa kutumia coaster ya abiria kutoka tunduma kuja Mbeya. Chanzo cha tukio hili ni kujipatia kipato kikubwa kwa kukwepa kulipa kodi ya mapato.

Mbinu iliyotumika ni kununua bidhaa hizo huko eneo la Black nchini Zambia katika duka la mtu mmoja raia wa Zambia [Jina linahifadhiwa] na kuvusha kwa njia za panya kwa kumtumia bodaboda ambaye husafirisha bidhaa hizo mpaka eneo la Sogea Stand alafu hupakia bidhaa hizo katika gari za abiria aina ya coaster na kuzipeleka wanakopanga kuzipeleka kwa wateja mbalimbali.

Mtuhumiwa amehojiwa na kukiri kufanya biashara hiyo. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa Mahakamani.

KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
Mnamo tarehe 16.02.2019 majira ya saa 13:00 mchana huko eneo la Kalumbulu, Kata ya Kyela, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika msako walimkamata STEWART NTULO akiwa amebeba:-
  1.     Mafuta aina ya Cook well lita 60 (sitini),
  2.     Kilo 60 (sitini) za sukari
Bidhaa hizo zilikamatwa zikiwa zinaingizwa nchini toka nchi jirani ya Malawi bila kuwa na kibali. Upelelezi unaendelea.

KUJERUHI.
Mnamo tarehe 15.02.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Galijembe, Kata ya Tembela, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya. MAJUTO MASHOWE [32] mkazi wa Ifiga alijeruhiwa kwa kukatwa kwa kitu butu kichwani na watu waliojichukulia sheria mkononi.

Chanzo cha tukio hilo ni kwamba mhanga ambaye anaishi Ifiga alienda kumchukua mtoto wake aitwaye BERNADETA MAJUTO [05] mwanafunzi wa Chekechea Shule ya Msingi Ngonde, mtoto ambaye huwa anampeleka shuleni hapo kila jumatatu na kwa sababu kuna umbali toka anakoishi hadi shuleni mtoto huyo huwa anabaki kwa mama yake mkubwa JOYCE BAHATI na huwa anamfuata kila ijumaa nakumleta jumatatu hivyo ijumaa alipoonekana akiwa amembeba mtoto huyo na raia wa pale standi bila kuuliza walihisi kuwa amemwiba mtoto huyo hivyo kumshambulia.

Mhanga amepatiwa PF3 na amelazwa wodi namba 2 katika Hospitali ya Rufaa Mbeya na hali yake inaendelea kuimarika. Msako mkali wa kuwakamata watuhumiwa waliohusika na tukio hilo unaendelea na mara baada ya kuwakamata, watafikishwa katika vyombo vya sheria.

KUFANYA MKUSANYIKO USIO HALALI KWA NIA YA KUFANYA VITENDO VYA KISHIRIKINA.
Mnamo tarehe 16.02.2019 majira ya saa 17:40 jioni huko maeneo na Kata ya Itagano, Tarafa ya Sisimba ndani ya Jiji na Mkoa wa mbeya.  Askari Polisi waliwakamata watu kumi na nane [18] wakifanya mkusanyiko usio halali. Watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na:-
  1.     JASSON SHONYELA [56]
  2.     NELSON MPESYA [48]
  3.     MICHAEL LABSON [32]
  4.     NELSON LEO [56]
  5.     JACKSON MWANDEMBA [60]
  6.      SIMON WALENJELA [65]
  7.      SAMSON MWANDEMBA [56]
  8.      MANFREDY MLAWIZI [60]
  9.      ARON MWANANYENE [48]
  10.      AMSHA NDELE [29]
  11.     ONESMO MAMBOLEO [45]
  12.     RASHID DAMSON [26]
  13.     TAZARA MWASHETWA [24]
  14.     MARIA SAMSON [60]
  15.     BALONGO WALENJELA [70]
  16.     SHIDA DAIMON [35]
  17.     FRANK JUMA [28]
  18.     DANIEL MWAMBIZA [78]
Wote wakazi wa Idimi Mkoani Mbeya. Watuhumiwa hao walikamatwa wakifanya mkusanyiko usio halali kwa nia ya kufanya vitendo vya kishirikina kwa kuwaleta waganga wa jadi (lambalamba) kwa kusadikiwa kuwa wanatoa uchawi kwa baadhi ya wananchi wa eneo hili wanaowatuhumu kuwa ni wachawi kitendo ambacho ni kinyume cha sheria. Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa.  Upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA MALI ZIDHANIWAZO KUWA ZA WIZI.
Mnamo tarehe 16.02.2019 majira ya saa 00:15 usiku huko mtaa wa Sae – Pipeline, Kata ya Ituha, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata JOSHUA FRANK MWAKILEMA [32] mkazi wa Sae Pipeline akiwa na mali zinazodhaniwa kuwa za wizi ambazo ni:-
  1.     Printer mbili kubwa aina ya Epson,
  2.     Laptop mbili aina ya Accer na Fujistu,
  3.     UPS tano,
  4.     Polaroid Cd micro System moja,
  5.     Radio moja aina ya Polaroid,
  6.     Subwoofer mbili aina ya Sea Peano na Pioneer,
  7.     Radio aina ya Lasonic,
  8.     Feni moja aina ya Dolphin,
  9.     Dvd deck mbili pamoja,
  10.     Wino wa printer Pcs 29,
Mali zote hizo zinadhaniwa kuwa ni za wizi. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika, Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.

Maimu wa NIDA Augua....Ashindwa Kufika Mahakamani

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Vitambulisho (Nida), Dickson Maimu, ambaye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisabishia Serikali hasara ya Sh1.16 bilioni ni mgonjwa.

Mbali na Maimu mshtakiwa mwenzake mwingine katika kesi hiyo, Astery Ndege, ambaye ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  pia ni mgonjwa.

Kutokana na kuugua  kwa washtakiwa hao ambao wote wako mahabusu, jana walishindwa kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi yao, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu.

Kesi hiyo ambayo inasikiizwa na Hakimu Mkazi Mkuu Salum Ally jana Jumanne, Februari 19, 2019 ilitarajiwa washtakiwa  kusomewa maelezo ya mashahidi baada ya upelelezi kukamilikaa.

Hata hivyo mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliieleza mahakama kuwa kwa taarifa alizopewa na askari Magereza washtakiwa hao hawakuweza kufikishwa mahakamani kwa kuwa wanaumwa.

Kutokana na hali hiyo Swai aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia maendeleo ya afya ya wagonjwa hao.

Hakimu Ally amepanga kesi hiyo itajwe tena mahakamani hapo Machi 5 mwaka huu ili kuangalia maendeleo ya afya ya washtakiwa hao kabla ya kupangiwa tarehe nyingine ya kuendelea na hatua  ya  kesi hiyo kwa washtakiwa hao kusomewa maelezo ya mashahidi.

Mbali na Maimu na Ndege washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Avelin Momburi, aliyekuwa Meneja Biashara wa Nida; Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani; Ofisa Usafirishaji,  George Ntalima; Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Wanakabiliwa na mashtaka 100 kati ya hayo, 24 yakiwa ni ya utakatishaji fedha zaidi ya Sh1.1 bilioni, 23ya kughushi nyaraka, 43 ya nyaraka za uwongo ili kumdanganya mwajiri wao, na mashataka matano ya kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh1.3 bilioni.

Mashtaka mengin ni ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu (mawili), shtaka moja la matumiz mabaya ya madaraka na mashtaka mawili ya kula njama.

Manispaa ya Iringa yaongoza kwa ukusanyaji mapato

$
0
0
 Na Amiri kilagalila
MADIWANI  wa  halamshauri ya Manispaa ya  Iringa  mkoani  Iringa  wameipongeza  halmashauri  hiyo  kwa  kuendelea  kuongoza  kitaifa  katika ukusanyaji  wa mapato  kwa kundi la  Halmashauri za  Manispaa nchini .

Madiwani hao  walitoa  pongezi hizo jana  mara  baada ya  taarifa ya  mstahiki meya  wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe  kutoa taarifa  rasmi katika  kikao hicho kuhusu  Manispaa ya  Iringa  kuongoza  kwa  ukusanyaji wa mapato kwa  mwezi Januari .

Diwani  wa kata ya Mwangata Edward  Chengula  alisema  kuwa  ni hatua  ya  kujipongeza kwa  halmashauri  hiyo ya  Manispaa ya Iringa  kuendelea  kufanya  vizuri  katika  ukusanyaji wa mapato  na kuwa kinachoendelea ni uwajibikaji mzuri wa  watendaji wa halmashauri hiyo  chini ya mkurugenzi  wake Hamid Njovu pamoja  na  madiwani .

Alisema  pamoja na  kufanya  vizuri katika  ukusanyaji wa mapato , Manispaa ya  Iringa  ni  moja kati ya Halmashauri  ambazo zimefanya  vizuri katika  zoezi la  ujenzi wa vyumba vya madarasa na  kufanikiwa  kupeleka wanafunzi wote  waliofaulu  mtihani wa darasa la  saba  kujiunga na  sekondari .

" Ushirikiano  uliopo  ndio ambao  umepelekea  Halmashauri  yetu  kuendelea  kuwa  wamoja na  kuwatumikia  wananchi kwa  nguvu ya  umoja  bila kuwepo mivutano  ya kisiasa  hadi  sasa mfano kata  yangu ya Mwangata  najivunia  kuona  watoto  waliofaulu kujiunga na elimu ya  sekondari  wote  wanakwenda  shule  ila  pia  kuna  maendeleo makubwa  yanayofanywa katika kata ya Mwangata " alisema Chengula

Naibu  meya wa Manispaa ya  Iringa Joseph Lyata  alisema  kuwa  kuongoza kwa  Manispaa hiyo  katika  ukusanyaji  kodi ni ishara  nzuri  kuwa  wananchi  wa Manispaa ya  Iringa  wameitikia wito wa  serikali ya  awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt  John Magufuli ya  kila mmoja  kulipa  kodi kwa maendeleo ya  Taifa .

Naye Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa, Ritta Kabati (CCM) na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa, Suzana Mgonakulima (Chadema) wamesema kuwa mbali na kuipongeza manispaa yao kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ila wanapongeza kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vimepelekea watoto wote kwenda shule . .

Serikali Yakerwa Na Mauaji, Unyang’anyi Mipakani.....Waziri Mkuu Aviagiza Vyombo Vya Ulinzi Viongeze Ulinzi Na Doria

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza ulinzi na doria katika maeneo ya mipaka kutokana na ongezeko la vitendo vya mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha na vitisho kwa wananchi.

Pia, Waziri Mkuu ameagiza wakimbizi wote watakaobainika kutoroka kwenye makambi wanayohifadhiwa na kuingia uraiani wakamatwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za Tanzania, kwani wanachokifanya ni ukiukwaji wa sheria.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumanne, Februari 19, 2019) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wilayani Kibondo wakati akihitimisha ziara yake mkoani Kigoma.

Alisema maeneo yaliyo katika hali mbaya ni Kibondo, Buhigwe, Kasulu, Ngara, Biharamulo, Uvinza, Kakonko na Kigoma Vijijini, ambako wananchi hususani wafanyabiashara wameingiwa na hofu kutokana na vitendo hivyo.

Waziri Mkuu alisema pamoja na undugu waliokuwanao na nchi jirani, lakini kila nchi ina sheria na taratibu zake, hivyo ni lazima zifuatwe na ni marufuku kuingia katika nchi yoyote bila ya kufuata sheria na taratibu za nchi husika.

“Kulinda usalama wa nchi ni jukumu letu sote na si la vyombo vya ulinzi na usalama pekee, kila mmoja anapaswa kushiriki. Kwa upande wa majirani zetu wanaotaka kuja nchini ni lazima wafuate taratibu kwa kuomba vibali.”

Alisema watu wote wanaoingia bila ya kufuata sheria na taratibu ndio hao wanashiriki katika vitendo vya uhalifu yakiwemo mauaji ya raia wasiokuwa na hatia, unyang’ani wa kutumia silaha za kivita pamoja na utekaji wa watoto.

Waziri Mkuu alisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama viendelee kulinda mipaka yetu na watu wote watakaobainika wameingia nchini bila vibali wakamatwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.

Aliongeza kuwa wakimbizi wanaohifadhiwa katika maeneo mbalimbali nchini hawaruhusiwi kutoka nje ya kambi hizo kwa sababu huduma zote wanazostahili zikiwemo za afya, elimu  na chakula zinapatikana kambini.

Pia, Waziri Mkuu aliitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iwasimamie vizuri watumishi wake wanaofanya kazi kwenye kambi hizo na kuchukua hatua kwa watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Mbali na agizo hilo kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, pia Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa wizara hiyo ufanye mazungumzo na Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) ili litekeleze majukumu yake bila kukiuka sheria za nchi.

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaonya wananchi kuacha tabia ya kuwachukua raia wa nchi jirani na kuwaleta nchini kwa ajili ya kuja kufanya kazi za vibarua katika mashamba yao bila ya kuwa na vibali.

“Tabia ya kuwachukua watu kutoka nchi jirani kwa ajili ya kulima mashamba bila ya kuwaandikisha ni makosa kisheria. Anayetaka kupata vibarua kutoka huko aende kuomba vibali huku akieleza idadi ya anaowataka na siku watakazokaa.”

Waziri Mkuu alisema lengo la kufanya hivyo ni kulinda usalama kwa sababu wengine wanawafanyisha kazi na wakimaliza hawawalipi wanawatishia kuwashitaki kwa kuingia nchi bila ya kibali jambo linalochangia kuwepo kwa migogoro na visasi.

Pia, Waziri Mkuu alisema hata kama wakiwalipa hakuna anayefuatilia kama kweli baada ya kumaliza vibarua hivyo wanarudi makwao kwani wengi wao wanaendelea kubaki nchini huku baadhi wakijihusisha na vitendo vya kihalifu.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao. 

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari. 

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume. 

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa. 

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo nchi 3-8 na unene cm 2-5,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji :Hii ni tiba tofauti kabisa nazile ambazo umekwisha wahi kutumia. 

Pia tunadawa za , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono pamoja na mvuto wa mpenzi.

 DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Kakakuona 2: Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume

$
0
0
_________________________
'DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME KAKAKUONA 2''.
_________________________                                     Inakadiriwa 75% ya Wanaume katika Nchi Za Jangwa la Sahara wanakabiliwa na Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume. SABABU KUU ni:
 🔖 (i) Mfadhaiko wa Mawazo pindi anapotaka kufanya Tendo la Ndoa hupelekea msukumo wa Damu na Mapigo ya Moyo kwenda Kasi kulingana na Hofu ya Kumudu Tendo la Ndoa/
🔖 (ii) Mwili kupatwa na Magonjwa ya Mara kwa Mara (Body Disorder dieses) kama vile KISUKARI, MAGONJWA YA ZINAA, MALARIA SUGU, BP, VIDONDA VYA TUMBO, BAWASIRI, NGIRI, ( hernia) , Matatizo ya Mgongo na Kiuno/
🔖(iii) Magonjwa Sugu kama Cancer, Kisukari , Bp, Ukimwi, Kifua Kikuu, Tambazi, BAWASIRI na Vidonda Tumbo. Hupelekea kupungua kwa Hormones za vichocheo/
🔖 (Iv) Constipation ni kuaharibika kwa Mfumo wa Ulaji wa Chakuala na Mmeng'enyo wa Chakula Mwilini na kupelekea kupata choo kigumu na Tumbo kuunguruma na kujaa gesi/
📎Hii hupelekea mwanaume kuwahi kufika kileleni na kushindwa kurudia Tendo la Ndoa📎
________________________
TIBA YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME KWA DAWA ZA ASILI.
📍KAKAKUONA 2 Ni dawa ya Bora zaidi inayotibu na kuponya kabisa Tatizo la upungufu wa Nguvu za Kiume , hukufanaya urudie Tendo la Ndoa zaidi ya 4 _kwa siku.
📍Pia KAKAKUONA 1 Hurefusha na Kunenepesha Maumbile ya umme kwa siku 5 tu./
📌Dawa hizi hutumika kwa umri zaidi ya 18 tu.pia Tunatibu Matatizo ya:
🔖Uzazi/,
🔖Muwasho Sehemu Za siri/
🔖Fungus/
🔖Kisukari/
🔖BAWASIRI/
🔖Mgongo/
🔖Kiuno kuuma/
🔖Tumbo kujaa gesi/
🔖Maumivu ya Misuli ,Miguu ,Bp, Mwili kukosa Nguvu nk.
_________________________
Fika kwa KAKAKUONA HERBAL CLINIC.
SIMU NO:
📞0713 29 39 88  na
📞0758 07 82 80
DR THOMAS NAPATIKANA MBAGALA RANGI TATU __________________________

Mahakama ya Afrika Yaipa Serikali ya Tanzania Siku 45 za Kujitetea

$
0
0
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCPHR), imetoa siku 45 kwa Serikali ya Tanzania, ikiitaka itoe utetezi kuhusu maombi yaliyofunguliwa mahakamani hapo kutaka matokeo ya uchaguzi ya Rais yapingwe mahakamani.

Kwa mujibu wa barua ya Msajili wa AfCPHR, Dk. Robert Eno, amri hiyo inafuatia ombi namba 018/2018 lililofunguliwa mahakamani hapo na mlalamikaji Jebra Kambole dhidi ya mlalamikiwa ambaye ni Serikali ya Tanzania.

Katika barua yake ya Februari 14, mwaka huu, yenye kumbukumbu namba AfCHPR/Reg./APPL/018/2018/008, Msajili Dk. Eno, amemtaka malalamikiwa kutoa utetezi wake ndani ya siku 45.

“Mlalamikiwa anajulishwa na mahakama hii, kwa mujibu wa maslahi ya haki, kuendelea na kutoa hukumu kwa mujibu wa maombi yaliyowasilishwa iwapo haitapokea utetezi wowote ndani ya siku 45 baada ya kupokea barua hii.

“Msajili anakutaarifu (mlalamikiwa) kwamba mlalamikaji ameomba kutolewa uamuzi kuhusu kushindwa kwako (mlalamikiwa), kutoa utetezi wa shauri alilofungua kwa mujibu wa kanuni 55(1) ya Kanuni za Mahakama hiyo.

“Pale ambao upande mmoja unashindwa kuonekana mahakamani au unashindwa kutetea kesi yake, mahakama inaweza kwa kuzingatia maombi yaliyowasilishwa na upande mwingine, kupitisha hukumu/uamuzi baada ya kujiridhisha kwamba upande ulioshindwa kufanya hivyo, ulipelekewa hati ya maombi ya shauri husika pamoja na nyaraka zake zote kwa ajili ya mwenendo wa shauri hilo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Kwanini Uhangaike Na Magonjwa Yanayowezekana Kupona?..........Tiba Sahihi Imewasili

$
0
0
Asilimia 60- 80 ya wanaume wameathilika kisaikologia baada ya kujiona wako tofaut na wengine kimaumbile na kupungukiwa nguvu za kiume , mwanaume aliekamilika kimaumbile anatakiwa awe na maumbile yasiyo pungua nchi 6-8 tofautina hapo anaupungufu ,

zipo sababu nyingi zinazosababisha mapungufu hayo ambazo ni :- upigaji wa punyeto ( mastervation) ,ngili,KISUKARI,vidonda vya tumbo,maumivu ya mgongo ama kiuno,unene(kitambi) tumbo kuunguluma na kujaa ges, matatizo haya huchangia kwa kiasi kikubwa sama kukosa nguvu za kiume vilevile maumbile kuwa madogo na kiingia ndani (kunywea)

SUPER KAMULI  :- hii nidawa kiboko kwa matatizo ya nguvu za KIUME,ni dawa ya Asili tuliyo jaaliwa na mwenyezi MUNGU huimarisha misuli ya uume wakati wa tendo la ndoa na kuzalisha viini vya uzazi (manii) vilevile utaludia tendo zaidi ya mara tatu bila ham kuisha pamoja na kuchelewa kufika kilele takiriban dk 20 - 45 kwatendo moja.

GEMBE 2 MIX :- hii nidawa ya Asili Hurefusha na kune nepesha maumbire madogo ya UUME , hurefusha urefu wa nchi (6-8 )na unene wa sm( 3-4) huanza kufanya kazi masaa machache baada ya kuanza kuitumia,( tiba niyakudumu ikishakutibu,

Nina dawa ya kutokomeza KISUKARI na kupona kabisa hata kama kimekusumbua kwa mda mrefu mpaka ukajikatia tamaa  tiba ipo na utatumia vyakula vyote bila tatizo baada ya kupona ,

Pia ninadawa ya Vidonda vya tumbo,Ngiri, miguu kuwaka moto, mvuto wa mapenz ( kumvuta mke /mme/mpenzi/hawara/ama yoyote unaemuhitaji) dawa za biashara, uzazi kwa akina mama na akina baba (pande zote) pata dawa ya bawasili bila kufanyiwa upasuaji,

KWAMAELEZO NA MSAADA WASILIANA NA DR SILIMBA NAPATIKANA DAR ES SALAAM

 SM O620510598 / 0743543944

Nb km huna nafasi huduma hii inakufikia popote ulipo kwaware wa mikoani tunatuma kwa njia ya mabasi

Wamiliki wa Shule Binafsi Wakutana Dodoma

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,DODOMA.
Mdhibiti mkuu wa Ubora wa Elimu Kanda kati ,Bw.Sospeter Magina    Jana Februari  19,2019  amefanya kikao na wamiliki wa Taasisi binafsi za Elimu  mkoani Dodoma  na kujadili Masuala mbalimbali ya kielimu ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuzingatia maadili katika taasisi zao.
 
Akizungumza  Katika  kikao hicho kilichofanyika shule ya sekondari Dodoma ambacho kimekutanisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwamo maafisa elimu msingi na sekondari jiji la Dodoma,Bw.Magina alisema  suala la maadili ni la tangu zamani hivyo ni vyema  kila Shule ikazingatia kusimamia maadili ya wanafunzi na walimu.
 
“Suala la maadili halijawahi kubadilika  tangu nyaraka za miaka iliyopita tatizo ni usimamizi wa nyaraka hizo kuhusiana maadili ya  wanafunzi na walimu sio mzuri hivyo mnatakiwa kuzingatia kusimamia maadili ipasavyo”
 
Aidha ,Bw.Magina alizungumzia juu ya  suala la ufundishaji shuleni kwa kuzingatia Mtaala wa elimu  uliopo wakati mchakato wa  vitabu ukiandaliwa .
 
“Suala la mitaala ieleweke  wazi kuwa kulikuwa na shida ya vitabu  fulani vilivyokuwa vinaingia mashuleni  ,serikali  imechukua jitihada  kuhakikisha ya kwamba vitabu vipya vinaandaliwa .Taarifa nilizonazo kwa sasa karibu vinatoka ,muda wowote vinatoka .Walimu wanatakiwa kufundisha kwa kuzingatia syllabus wakati vitabu vipya vikiandaliwa.”
 
Hata hivyo Mdhibiti huyo wa ubora wa elimu kanda ya kati Dodoma alisema kuwa haiingii akilini shule za Dodoma haziingii kwenye kumi bora kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa hivyo kuna haja ya kufanya mabadiliko sasa ili mkoa huo ujipambanue vyema  na kufanya vizuri  katika masuala ya kielimu.
MWISHO.

CHADEMA Wamvaa Polepole

$
0
0
Siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, kudai hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya mikutano ya hadhara ni ukorofi na uvunjifu wa sheria, uongozi wa chama hicho cha upinzani umemjibu, ukidai kauli yake hiyo ni ya watu  wasiopenda kufikiri.

Wiki iliyopita, Chadema kupitia Katibu Mkuu wake, Dk. Vicent Mashinji, ilitangaza kuwa inatarajia kuanza mikutano ya hadhara baada ya kukamilisha mambo yake ya ndani.

Chama hicho kilieleza kuwa kinatambua kuwapo kwa zuio la serikali kufanya maandamano na mikutano ya siasa nchini, lakini kitaendesha mikutano hiyo kwa kuwa iko kisheria na kwamba CCM wamekuwa wakiifanya bila kuchukuliwa hatua.

Baada ya Chadema kutangaza uamuzi huo huku wakiitaja CCM kukiuka agizo la Rais John Magufuli la Juni 23, 2016, ya kuzuia mikutano ya siasa na maandamano, Polepole alizungumza na gazeti la Nipashe kuhusu kauli hiyo na kudai chama hicho cha upinzani kutangaza kufanya mikutano nchi nzima, ni ukorofi na uvunjifu wa sheria.


Akijibu kauli hiyo ya Polepole jana, Dk. Mashinji, alidai kauli ya Polepole ni ya mtu mvuvi ambaye anapinga kitu bila ya kuwa na hoja.


"Hiyo ni kauli ya watu wavivu ambao hawapendi kuzihangaisha akili zao kupinga hoja zinazotolewa," Dk. Mashinji alisema, "kufanya mikutano ni uvunjifu wa sheria? Hebu atuambie ni sheria au kanuni ipi anayozungumzia hapo ambayo inakataza mikutano.


"Hawa ndiyo vijana wa CCM ambao wamepewa nafasi bila kuandaliwa, hawajui wazungumze nini. Sisi tutaendelea na programu zetu za mikutano kama tulivyoeleza awali.

"Polisi wetu hawana shida, tunawaandikia barua kuwataarifu kuhusu mikutano yetu, wanakuja wanatulinda, hawana shida na sisi. Sasa huyu Polepole anazungumzia sheria ipi au kuna kanuni ipi inayozuia mikutano?"

Lipumba, Maalim Seif Waendelea Kunyukana....Pande Zote Mbili Zatangaza Kuteua Wajumbe Wapya wa Bodi

$
0
0
Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, umesema unatarajia kuitisha kikao cha kamati kuu ya chama hicho  waweze kuitisha kikao cha Baraza Kuu ambacho kitateua wajumbe wapya wa bodi ya wadhamini.

Kauli hiyo imetolewa siku moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Saalam, kutengua uteuzi wa bodi ya wadhamini wa chama hicho kwa upande wa Lipumba na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kwa madai kuwa hawana sifa ya kuwa wajumbe wa bodi.

Wakati upande wa Profesa Lipumba ukisema hivyo, upande wa  Katibu Mkuu wa chama hicho kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad  nao umesema utateua wajumbe wengine ili kujaza nafasi hizo.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho, upande wa Lipumba, Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya alisema  wamekubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu na   wapo kwenye mchakato wa vikao vya juu vya taifa  waweze kufanya uamuzi ikiwamo kuteua wajumbe kama mahakama ilivyoagiza.

“Tupo kwenye mchakato wa kuitisha kikao cha Baraza Kuu ambako muda siyo mrefu tutateua majina ya bodi ya wadhamini na kuwapitisha.

“Kikao hicho pia kitashirikisha viongozi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kama sheria inavyotutaka  tuweze kuwa na bodi bora itakayosimamia shughuli za chama,” alisema Kambaya.

Mkurugenzi huyo wa Habari   upande wa Lipumba, alisema   katika kipindi hiki ambacho wako kwenye uchaguzi wa ndani wa chama hicho, watahakikisha wanapata bodi mpya mapema iwezekanavyo jambo ambalo linaweza kusaidia shughuli nyingine za chama kuendelea.

Alisema kwa mujibu wa uamuzi wa juzi, bodi zote mbili za Lipumba na Katibu Mkuu wa chama, Maalim Seif Sharif Hamad,  hazitambuliki katika sheria, hivyo basi kufanyika haraka kwa mchakato huo ni muhimu   chama kiweze kuwa na bodi ya wadhamini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama hicho,  Maalim Seif alisema uamuzi huo wa mahakama umewapa nguvu wanachama wao waliokuwa wakishuhudia mvutano uliozaa makundi ndani ya chama hicho.

“Tutafanya uteuzi mpya wa wajumbe wa bodi kwa kufuata vifungu vyote vya sheria na tutavipeleka Rita (Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi) ili isajiliwe. Ni matarajio yetu Rita itafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria

“Rita ni chombo muhimu katika nchi, tuna imani ya kuwa imejifunza mengi kutokana na hukumu ya jana (juzi) na italinda credibility (weledi),” alisema Maalim Seif.

Alisema uamuzi huo wa mahakama ni ushahidi tosha kuwa msajili wa Rita hakufanya kazi kwa ufanisi na kwamba hilo ni funzo kwa taasisi nyingine za Serikali katika kutekeleza majukumu yake bila kufuata msukumo.

Aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kuwa makini katika kufuata vipengele vyote vya kisheria katika utendaji kazi badala ya kufanya kwa mazoea huku akisisitiza kuwa uamuzi wa mahakama ulikuwa sahihi.

Kutokana na uamuzi huo wa mahakama, Maalim alisema ni wakati muafaka sasa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya uchunguzi wa kina kuhusu fedha za ruzuku akidai kwamba masuala ya fedha yalifanywa na bodi hiyo kinyume na sheria.

Tumia Vunja Kero 3 Power: Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
VUNJA KERO 3 POWER ni dawa Bora ya vidoge asilia hutibu tatizo la nguvu za kiume na huanza kufanya kazi baada y dk 30 
(1)Huongeza nguvu za kiume Mara dufu 
( 2) Huimarisha misuli ya uume iliyolegea na kusinyaa  pia dawa hii itakufanya ufurahie tendo la ndoa zaidi ya Mara ( 4) nne bila kuchoka
 ( 3) Hunenepesha na kurefusha uume kwa saizi uipendayo kuanzia nchi (6-7) 

Pia dawa hii hutibu maumivu ya mgongo ,kiuno tumbo kujaa gesi na kuunguruma ,kutopata choo vizuri ,ngiri na busha bila kupasuliwa         

Dr saidi anauwezo mkumbwa aliyojaliwa wa kumvuta na kumrudisha mmeo  ama mpenzi wako alikuacha au aliyembali nawe au hakutimizii shida zako

Pia Dr saidi anadawa ya kutibu kisukali,vidonda vya tumbo na miguu kuwaka Moto.  

DR SAID ANAPATIKANA DAR ES SALAAM BUGULUNI ROZANA  KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NO 0758 199338 Au 0786243789

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

PICHA:Rais Magufuli Akutana Na Afisa Mwendeshaji Mkuu Wa Kampuni Ya Barrick Gold Corporation (Africa Na Mashariki Ya Kati) Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Bw. Willem Jacobs baada ya  kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 20, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga katika picha ya pamoja  na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Bw. Willem Jacobs na ujumbe wake baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 20, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga wakiwa katika   mazungumzo na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Bw. Willem Jacobs na ujumbe wake walipokutana Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 20, 2019
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Bw. Willem Jacobs alipokutana naye kwa   mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 20, 2019

PICHA NA IKULU

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Majizo Ajitoa Muhanga Sakata la Matibabu ya Ruge Mutahaba

$
0
0
Mkurugenzi wa EFM na E-TV, Majizo ameunda kamati ambayo itaratibu namna ya kukusanya fedha za kusaidia mtibabu ya mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu.

Akihojiwa leo Jumatano Februari 20, 2019 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Clouds TV, Majizo amesema tayari kamati ya kufanikisha uchangishaji wa matibabu hayo imeundwa na imeanza kukutana jana.

Amesema Watanzania watarajie kamati hiyo itafanikisha walilokusudia na kuwaomba wasiache kuwapa ushirikiano pale watakapowafuata kueleza walichoamua kufanya katika kufanikisha matibabu hayo.

"Undugu, urafiki na ukaribu wetu hauwezi kufa kwa sababu ya kazi zetu kwani ukitaka kuwa mfanya biashara mzuri hutakiwi kuchukulia vitu personal kwenye kazi huwa tunafanya kazi, na ili ukae muda mrefu kwenye biashara hutakiwi kuchukulia vitu personal na ukichukulia personal lazima upotee”

“Kabla sijafungua redio nilimwambia Ruge nataka kufungua redio akaniambia kwa sababu unaweza vitu vingi fungua, nilitaka kumfanyia surprise na nilivyofungua nikamwambia tayari nimefungua. Alinipongeza kwa furaha karibu kwenye game.”

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa zake za kuumwa na kwa nafasi yangu nitaonyesha jinsi gani nimeguswa tutajitoa kwa namna yoyote kupitia vyombo vyangu vya habari au hata mimi personal, ili kuweza kusaidia hili kikubwa ni tuungane kwa pamoja”

‘Kamati ilikutana jana kwa bahati mbaya sikuwepo nilikuwa kwenye kamati zingine mipango haikuwa vibaya imekamilika, kamati yetu italeta mafanikio makubwa lengo letu ni kutaka Ruge arudi akiwa mzima, kikubwa ni ushirikiano pindi tukirudi kwenu wananchi’’

“Baada ya kupata taarifa za Ruge kuumwa, nilitamani miujiza ya haraka na nilikuwa najaribu kuweka karibu mawasiliano, na nilipata ushirikiano kutoka kwa watu wa hapa mjengoni na kunipa taarifa kuhusu hali yake”

“Kuna vitu vingi ambavyo tumepanga kuvifanya kwenye kamati yetu ya kihakikisha Ruge anarudi kwenye game na mwenyikiti wa kamati atakuja kuongea mengi ambayo tumeyapanga na mimi na vituo vyangu ( #TvE na #Efm) tutashiriki kwa pamoja” Amesema Majizo

Tundu Lissu Kufanyiwa Upasuaji wa 23 Leo

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu leo anafanyiwa upasuaji wa 23 na wa mwisho katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg nchini Ubelgiji.

Lissu amesema baada ya upasuaji huo utakaofanywa kwenye goti la mguu wake wa kulia atakuwa tayari kurejea nyumbani mwaka huu.

Tundu Lissu yupo nje ya nchi tangu Septemba 7 mwaka juzi aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa maeneo ya nyumbani kwake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria Mkutano wa Bunge.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images