Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ugonjwa wa Surua ..... Dalili zake, Tiba na Kinga

0
0
Utangulizi
Surua ni mojawapo ya magonjwa ya kuambukiza yanayotisha kwa binadamu. Huu ni ugonjwa ulio na kiwango cha juu cha karibu asilimia 100 cha mashambulizi pindi mtu apatapo vimelea vya ugonjwa huu.

Pamoja na kuwepo chanjo ya ugonjwa huu, bado surua ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vingi vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 katika baadhi ya maeneo duniani hasa kwa nchi zinazoendelea. Ugonjwa huu ambao ulitoweka katika baadhi ya nchi, umeanza kuonekana tena hivi karibuni miongoni mwa watu ambao hawakupata chanjo katika nchi za Uingereza na nyingine za Ulaya.
 
Surua husababishwa na nini?
Surua huenezwa na aina ya virusi jamii ya paramyxovirus. Jamii hii ya virusi hupatikana katika mfumo wa njia ya hewa. Hukaa katika kamasi na majimaji yaliyopo katika mfumo wa hewa. Kwa sababu hii basi virusi hawa huenezwa kwa njia ya upumuaji.

Virusi hawa wanaweza kuishi hewani kwa muda wa hadi saa moja baada ya kutolewa kwa kupiga chafya au kukohoa au hata mazungumzo na mgonjwa. Hii ina maana kuwa, ili kuambukizwa surua, si lazima mtu akutane uso kwa uso na mgonjwa.

Baada ya kuingia ndani ya mfumo wa hewa virusi hushambulia seli za utando wa nje wa njia ya hewa (respiratory tract epithelium) na kuingia katika mzunguko wa wa limfu na kufika kwenye tezi zilizo karibu. Katika tezi huzaliana zaidi na kusambaa mwilini.
 
Muonekano wa mgonjwa
Kawaida dalili za mwanzo zinaanza kuonekana baada ya siku 8 ya kupata uambukizi. Mgonjwa huwa na mafua mepesi, homa, kukohoa na macho kuwa mekundu.

Baada ya siku 2-4 tangu kuanza kuonekana kwa dalili za awali, ukichunguza mdomo wa mtoto, na kama utamchunguza pembeni (ndani ya shavu) utaona vidonda vyeupe kwenye utando mwekundu wa ndani ya mdomo. Vidonda hivi huonekana kama chumvi iliyomwagwa kwenye zulia jekundu. Hali hii huitwa Koplik spots. Hii ni dalili tosha ya kuthibitisha uwepo wa surua.

Lakini vilevile mgonjwa anaweza kuwa na vipele vidogo sana ambavyo inaweza kukuwia vigumu kutambua. Vipele hivi huweza kuonekana vizuri siku mbili baadaye. Kwa kawaida, vipele hivi huanzia usoni au nyuma ya sikio na kushuka chini kabla ya kutapakaa mwili mzima siku zinazofuata. Vipele huongezeka na kuwa vingi kadiri siku zinavyopita. Kawaida hali hii ya vipele inaweza kuchukua kati ya wiki 1-2. Vipele hupotea baada ya siku 7 na kuacha ngozi iliyobabuka. Hata hivyo, kukohoa kunaweza kuendelea zaidi ya siku 10.
 
Athari za Surua ni zipi?
Ingawa baadhi ya wagonjwa hupona katika kipindi cha siku 10 mpaka 14, baadhi hupata matatizo zaidi yanayoweza kuwa ya muda mrefu kama;

    1.Maambukizi njia ya masikio (Otitis media)
    2.Maambukizi njia ya chini ya mfumo wa hewa kama vile
  1. Uambukizi kwenye mirija ya hewa ya koo (bronchitis) maambukizi kwenye njia ya sauti (laryngitis) na croup. Surua inaweza kusababisha kuvimba katika sehemu ya sauti na kuathiri uwezo wa kutoa sauti lakini vilevile inaweza kusababisha uvimbe katika kuta za utando wa njia ya hewa.
  2.  Homa ya mapafu (pneumonia) ambayo ni sababu kuu inayosababisha vifo vinavyotokana na surua. Mgonjwa wa surua ni rahisi kupata homa ya mapafu kwa sababu kinga ya mwili wake huwa imepungua. Homa hii ya mapafu yaweza kusababishwa na aina nyingine ya virusi kama adenovirus, herpes simplex au bakteria kama Staphylococcus aureus, Streptococcus pneumonia, Haemophillus influenza, Klebsiella pneumonia. Lakini vilevile Kifua kikuu kinaweza kutokea kwa kusababishwa na upungufu huu wa kinga mwilini.
  3.Surua pia inahusishwa na aina mbalimbali ya mashambulizi kwenye ubongo kama vile
    4.Acute encephalitis ambayo hutokea wakati au ndani ya wiki chache baada ya maambukizi.
   5.Progressive encephalitis ambayo hutokea kwa wagonjwa walio na upungufu wa kinga mwilini unaotokana na sababu yeyote ile ikiwemo wale anaopata tiba ya kemikali (Chemotherapy) au kwa sababu ya VVU. Hali hii hutokea miezi 6 baada ya maambukizi, na inaweza kusababisha mgonjwa kufa.
6.Subacute sclerosing panencephalitis (SSPE) ni nadra sana kutokea. Mara nyingi kama likitokea, basi humpata mgonjwa baada ya mwaka mmoja wa ugonjwa wa surua. Sifa mojawapo ya hili tatizo ni kupungukiwa kwa uwezo wa kufikiri na akili kuzorota na hatimaye mgonjwa kufariki dunia.

7.Surua inaweza kusababisha utapiamlo kwa sababu ya ukali wake hasa kwa watoto ambao hawapati lishe nzuri. Inahusishwa pia na kuharisha na kutapika na kusababisha upungufu wa maji mwilini.
8.Surua husababisha upungufu wa Vitamini A na kusababisha tatizo la kutoona vizuri ambalo hijulikana pia kama Keratitis. Kwa mtoto ambaye ana upungufu wa Vitamini A tatizo la macho huwa kubwa zaidi na kwa kitaalamu hujulikana kama Keratomalacia ambapo sehemu nyeupe ya jicho hutoboka.
 9.Maambukizi katika misuli ya moyo (Myocarditis)
10.Upungufu wa chembe sahani kwenye damu (Thrombocytopenia)

Utambuzi wa surua
Utambuzi wa surua inajumuisha historia ya mgonjwa kuwa na homa kwa angalau siku 3 na kuwepo kwa mojawapo ya dalili za mwanzo za surua ambazo ni kukohoa, kuwa na mafua mepesi, macho kuwa mekundu na upele mwilini. Aidha ikithibitika mgonjwa ana Koplik spots baada ya uchunguzi ndani ya mdomo ni utambuzi tosha wa surua.

Vilevile vipimo vya kimaabara ni pamoja na uthibitisho chanya wa antibodi dhidi ya surua (measles IgM antibodies) na uwezekano wa kuwapata virus wa surua kutoka katika mfumo wa hewa, damu au mkojo wa mgonjwa (isolation of measles virus RNA) au kwa njia ya kuoteshwa maabara (culture).
 
Kinga
Surua huzuiwa kwa urahisi kwa njia ya chanjo. Watoto ambao hawajapata chanjo ya surua wapo katika hatari kubwa sana ya kupata surua.
 
Kumbuka
Surua ni ugonjwa hatari. Unaweza kuua au kusababisha madhara ya muda mrefu lakini chanjo dhidi yake inazuia hatari hiyo. Kwa hiyo pale unapohisi mtoto wako ana dalili za surua mpeleke haraka hospitali ili kujithibitisha na kupata matibabu yanayofaa.

Waziri Mkuu kuanza ziara ya siku nne Kigoma

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuwasili mkoani Kigoma Februari 16, 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku nne.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga amesema Majaliwa atatembelea wilaya ya Kigoma, Uvinza, Kibondo na Kakonko.

Amesema lengo la ziara yake hiyo ni kuweka mkazo na msisitizo katika ufufuaji na uendelezaji wa zao la chikichi ikiwa ni pamoja na  kukagua vitalu, mashamba, lengo likiwa ni uboreshaji wa zao hilo.

Amesema akiwa mkoani humo Waziri Mkuu atatembelea kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo na kuzungumza na wakimbizi.

Amebainisha kuwa pamoja na mambo mengine ataangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ya CCM na kukagua miradi mbalimbali pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo atakayokuwa anakutana nao.

CHADEMA Kufungua Kesi Mahakamani Kuipinga Sheria ya Vyama vya Siasa

0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitafungua kesi mahakamani kupinga sheria ya vyama vya siasa ambayo sasa inasubiri kusainiwa na Rais  John Magufuli ili kuanza kutumika.

Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari amesema chama hicho kilipinga muswada huo lakini kesi yake ya kuupinga haikusajiliwa mahakamani.

"Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa (wa mwaka 2018) unakuja kunyonga demokrasia, tulishirikiana na wadau kuupinga lakini hatukufanikiwa sasa tutafungua kesi ya kupinga sheria yenyewe itakapoanza kutumika,” amesema Profesa Safari.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amesema chama hicho kinasubiri sheria hiyo itangazwe katika gazeti la Serikali (GN) ili kupeleka mahakamani vipengele ambavyo hawajaridhishwa navyo.

"Mahakama ina mamlaka ya kuondoa vipengele vyote ambavyo vinaminya haki za binadamu lakini pia vinavyokiuka katiba ya nchi. Hata tulipokwenda kusajili kesi ya kupinga muswada tuliambiwa tusubiri iwe sheria," amesema Dr Mashinji.

Ujenzi Wa Reli Ya Kimataifa Dar Es Salaamhadi Morogoro Washika Kasi, Wafikia Asilimia 42

0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imedhamiria kwa dhati kukamilisha mradi mkubwa wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ambapo tayari kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 2 kimetolewa mpaka sasa kwa ajili ya ujenzi huo.

Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi eneo la Soga, umbali wa kilometa 53, na kujionea maendeleo makubwa ya ujenzi wa reli hiyo.

Ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wake na kumpongeza mkandarasi anaye jenga reli hiyo, Kampuni ya Yapi Merkezi, kwa kutekeleza ujenzi huo kwa viwango vya hali ya juu ambapo ameelezwa kuwa, treni ya kwanza kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro inatarajia kuanza safari zake Mwezi Novemba mwaka huu kama kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.

"Ninampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake kubwa na kuamua kwa dhati kutekeleza mradi huu mkubwa na miradi mingine, ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, ambayo kukamilika kwake kutachochea uchumi wa viwanda" alisema Dkt. Kijaji

"Tunakwenda kwenye Tanzania ya viwanda, tutakuwa na viwanda kila mahali, tumeanza ujenzi wa mradi wa umeme wa megawat 2,115, viwanda vitazalisha bidhaa ambazo zitahitaji miundombinu ya usafirishaji, reli hii itatumika na tunatarajia ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa ni nchi yenye kipato cha kati"  aliongeza Dkt. Kijaji

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha  kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, Mhandisi Machibya Masanja, amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo umekamilika kwa asilimia 42.

"Mradi wetu unaenda vizuri na kwa wakati, zoezi la ujenzi na utandikaji reli tumeanza katika Jijini la Dar es Salaam umeanza na unaendelea vizuri ambapo ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 55 na utandikaji wa reli katika Jiji hili utafikia kilometa 10 mwishoni mwa mwezi Februari" alifafanua Mhandisi Masanja.

na nguvu kubwa imeelekezwa katika ujenzi wa tuta na madaraja, zezi ambalo limefikia asilimia 55 hivi sasa" alifafanua Mhandisi Masanja

Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Mwanza, na baadae kuunganisha mtandao wake na nchi jirani za Kongo, Uganda, Burundi na Rwanda, unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi trilioni 7.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezungumza na wakazi wa eneo la Guluka Kwalala, Gongo la Mboto, waliokuwa wakiendelea na taratibu zao za kulipwa fidia ambapo amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaletea maendeleo.

Baadhi ya wakazi hao, pamoja na kuiomba Wizara ya Ardhi na Makazi iwasaidie kupata viwanja kwa ajili ya kujenga makazi yao baada ya kulipwa fidia kupisha ujenzi wa mradi huo wa Reli ya Kisasa, wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusimamia ustawi na maendeleo ya nchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono.

Mwisho

Mwigulu Nchemba Aruhusiwa Kutoka Hospitali

0
0
Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) Dk Mwigulu Nchemba aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Dk Mwiguli alipata ajali Februari 13, 2019 katika eneo la Migori mkoani Iringa akitokea mkoani humo kwenda mkoani Singida baada ya gari lake kugonga punda waliokuwa wanakatisha barabara.

Katika ajali hiyo Dk Mwigulu, aliumia maeneo ya kifua, nyonga na kwenye mguu lakini dereva wake ambaye ni mtu pekee aliyekuwa naye kwenye gari hilo hakuumia mahali popote.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk Alphonce Chandika amesema waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani ameruhusiwa hospitalini hapo baada ya afya yake kuimarika.

“Mheshimiwa Mwigulu anaendelea vizuri na sasa tumemruhusu kurejea nyumbani baada ya afya yake kuimarika,” amesema Dk Chandika.

 Katika ukurasa wake wa Istagram, Mwigulu Nchemba ameandika ujumbe wa kumshukuru Mungu, Rais Magufuli na viongozi wengine na wananchi kwa maombi yao,

Hiki Ndicho Wanacho Kiwaza Wanaume Wengi Kuhusu Kuingia Katika Mahusiano /ndoa Na Single Mothers

0
0
Wewe  ni  Single  Mother ?  Upo  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  na  mwanaume ? Au  unataka  kuingia  katika  mahusiano ya  kimapenzi/uchumba/ndoa  na  mwanaume  ambae  si  baba  wa  mtoto  wako?

Basi  kabla  ya  kufanya  hivyo,unatakiwa  kujua  kitu  gani  wanacho  kiwaza  wanaume  wanao  ingia  katika  mahusiano  na  single  mothers.

Pia  unatakiwa  kuyafahamu  mambo  wanayo  yawaza wanaume  wengi  kabla  ya  kuingia katika  ndoa  na  single  mothers.

Mahusiano  mengi ya  single  mothers  yanashindwa kufika  mbali  kwa  sababu  single  mothers  wengi  huwa  wanaingia  katika  mahusiano  na  wanaume  bila  kuyafanyia   analysis  mambo  haya  muhimu  kabisa  kwa  kila  single  mother kuyafahamu.

AFRICANDADAZ ime kusanya maoni  kutoka  kwa  wanaume  mbalimbali kuhusu  uzoefu  wao  na  mtazamo  wao  kuhusu  kuingia  katika  mahusiano  ya kimapenzi  au ndoa  na  single  mothers.  

Maoni  haya  yamechukuliwa  kutoka  kwa  wanaume  mbalimbali  wa  hapa    Tanzania  na  waliopo  nje  ya  Tanzania.  Baadhi  ya  mambo  yanayo semwa  na  wanaume  hawa  kuhusu  kuingia  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  au  ndoa na  single  mothers  yanatisha  na  kuogopesha   sana. 

 Ni  vyema  kila  single  mother ambae  anafikiria  kuingia  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  au  kuingia  katika  ndoa  na  mwanaume  ambae  si  baba  wa  mtoto  wake  ayafahamu  mambo  haya.

Kusoma  zaidi  makala  haya tembelea Kwa kubofya hapo chini :

Serikali Yakabidhi Eneo La Mradi Wa Umeme Wa Maji Mto Rufiji Kwa Mkandarasi Tayari Kwa Kazi Kuanza

0
0
SERIKALI imekabidhi rasmi eneo la mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP),  kwa mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors kwa pamoja na ile ya Elsewedy  Electric zote kutoka nchini Misri.

Hatua hiyo sasa inaashiria kuanza kwa kazi ya ujenzi wa mradi huo wa umeme ambao utazalisha Megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye dridi ya Taifa na kuifanya Tanzania kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alikabidhi mradi huo jana katika eneo la Hifadhi Matambwe lililopo mpakani mwa mikoa ya Pwani na Morogoro, akisema faida nyingine ya mradi huo utakapokamilika bei ya umeme itashuka kwa kiwango kikubwa na utasaidia nchini kutekeleza rasilimali muhimu za Taifa.

Alisema mradi huo utajenga bwawa kubwa, lenye mita za ujazo bilioni 34 na kituo cha kufua umeme, kitakachokuwa na mashine tisa za kuzalisha umeme zenye uwezo wa megawati 2,115.

Aidha, alisema pindi mradi huo ukikamilika, utasaidia kushusha gharama za umeme kutokana na uzalishaji wa umeme huo wa kutumia maji kuwa nafuu, tofauti na nishati nyingine kama mafuta, gesi, upepo na jua.

Aliwataka wakandarasi hao, kukamilisha mradi huo kwa muda waliokubaliana, huku akiwapongeza wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuchangia utekelezaji wa mradi huo kwa hatua za awali. 

Aliwataka wakandarasi watakaotekeleza ujenzi huo, kujenga kwa ufanisi mkubwa na kwa viwango vinavyotakiwa na muda uliopangwa na utakaondoa shaka kwa wale wasioutakia mema mradi huo.

Dk Kalemani alimpongeza Rais John Magufuli kwa jinsi ambavyo amechukua ujasiri wa kuamua kutekeleza ndoto za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye mwaka 1958 alikuwa na mpango wa kujenga bwawa hilo, lakini ikashindikana kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo za kifedha. 

Hivyo aliwataka wakandarasi wa kampuni hizo na timu ya wataalamu wa Tanesco, kutoondoka eneo la mradi baada ya kukabidhiwa eneo, kwa kuwa hadi sasa kila kitu kipo kuanzia nyumba za kuishi, umeme na maji. Aliwataka wajenge wakati wote wa mvua na jua.

“Hatutaki kugeuka nyuma kuanzia sasa, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco ushiriki kikamilifu ili mradi huu uweze kukamilika kwa wakati uliopangwa,” alisema Dk Kalemani. 

Aliongeza, “Mimi na Naibu Waziri na hata Rais tutakuwa bega kwa bega usiku na mchana kuona mradi unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa viwango na ubora wa kimataifa wa mabwawa ya kufua umeme.”

Alisema kukamilika kwa mradi huo, kutaleta tija katika kujenga uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda. Alisema mahitaji ya umeme nchini kwa sasa ni makubwa kwani nchi inatekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda, hivyo huduma za umeme wa uhakika inahitajika zaidi. 

Dk Kalemani alisema ujenzi wa mradi huo, unajumuisha ujenzi wa bwawa kuu lenye uwezo wa kutunza maji takribani mita za ujazo bilioni 34, kituo cha kufua umeme kitakachokuwa na mashine tisa za kuzalisha umeme zenye uwezo wa megawati 235 kila moja, hivyo kufanya uwezo kuzalisha umeme wa mradi megawati 2,115.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema mradi huo wa kihistoria, uliosainiwa kati ya Tanesco na Kampuni ya Ubia Arab Contractors (Osman A. Osman Co na Elsewedy Electric), utakuwa na mkataba wa miezi 42. 

Msimamizi Mkuu wa kampuni mbili zilizopewa kandarasi hiyo, Makamu wa Rais wa kampuni hizo kutoka Serikali ya Misri, Wael Handy alisema mradi huo si wa Watanzania pekee, bali ni faida kwa wananchi wa Afrika yote.

Alisema mradi huo umeshirikisha timu mbalimbali za wataalamu wa sekta mbalimbali na katika kutekeleza mradi huo, Serikali ya Misri haitawaangusha na itahakikisha unatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

Airbus kusitisha uzalishaji wa ndege zake aina ya A380

0
0
Shirika la Airbus limetangaza kwamba ifikapo mwaka 2021 litasitisha uzalishaji wa ndege zake aina ya A380 superjumbo kutokana na kukosekana kwa soko.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika hilo ifikapo mwaka 2021 oda zilizokuwepo za ndege aina ya A380 zitakabidhiwa kwa wanunuzi na uzalishaji wa ndege hizo utasimamishwa.

Katika taarifa hiyo mkurugenzi mkuu wa Airbus Tom Enders alisema, wanatoa tangazo hilo huku wao na wanahisa wengine wa A380 wakiwa na uchungu.

Mteja mkuu wa ndege hizo aina A380 shirika la ndege la Emirates limepunguza kiasi cha manunuzi ya ndege hizo kutoka ndege 162 hadi 123 imefahamishwa katika taarifa hiyo.

Emirates imeingia mkataba mpya wa kununua ndege 70 aina ya A330-900s na a350-900s mbadala wa A380. Mkataba huo mpya una thamani ya dola bilioni 21.4.

Ndege hizo za Airbus A380 zenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 800 ziliazalishwa kutoa ushindani kwa ndege aina ya Boeing 747 za shirika la uzalishaji ndege la Marekani.

Baraza la Wawakilishi Marekani lasitisha msaada kwa Saudi Arabia

0
0
Baraza la Wawakilishi la Marekani lenye Wademokrat waliowengi limemkosoa Rais Donald Trump Jumatano na kupiga kura kusitisha msaada wa kijeshi unaotolewa na Marekani kwa majeshi ya ushirika yanayoongozwa na Saudi Arabia yanayo fanya mashambulizi nchini Yemen.

Kura zilikuwa 248 kwa 177 na ni mara ya kwanza kwa baraza hilo kutumia sheria ya War Powers Act.

Uamuzi huo sasa utapelekwa Baraza la Seneti ambalo lilipitisha hatua kama hiyo mwishoni mwa mwaka 2018, na kuwepo uwezekano wa kuzuka mvutano na White House.

Marekani imekuwa ikitoa msaada wa kipelelezi na vifaa kwa ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia unaopigana na waasi wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen.

Vita hiyo imeuwa maelfu ya raia tangu mwaka 2014 na tayari imesababisha janga kubwa la kibinadamu katika moja ya mataifa maskini sana duniani na kufanya hali kuwa mbaya zaidi nchini humo.

Mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Saudi Arabia yanayowalenga waasi yameharibu maeneo ya shule na mahospitali.

Wakimbizi 500 watoroka machafuko DRC na kuingia Uganda

0
0
Mapigano ya ukabila yaliyotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wiki iliyopita yamesababisha zaidi ya watu 500 kukimbilia Uganda.

Wakimbizi hao wamewafahamisha maofisa wa Uganda   na Shirika la Umoja Mataifa linalowahudumia Wakimbizi (UNHCR) kuwa mapigano hayo kati ya jamii za Lendu na Bagerere yamelitumbukiza eneo la mashariki mwa Congo katika hali ya sintofahamu.

Makundi hayo ya wakimbizi kutoka jimbo la Ituri mashariki mwa nchi, yanafanya safari za hatari kuvuka Ziwa Albert lililoko mpakani mwa nchi hizo mbili wakitumia mitumbwi isiyo na ubora.

Wengi wao  ambao ni wanawake na watoto, wameshuhudiwa wakiwa na mizigo yao hususan magodoro.

Kinachowatia hofu na wasiwasi viongozi wa wilaya za Hoima na Kikuube ni uwezekano wa kuzorota  hali ya usalama.

Inahofiwa huenda kuna uwezekano wa wakimbizi kuingia Uganda wakiwa wamejihami kwa silaha.

Shaka nyingine ambayo wimbi hilo jipya la wakimbizi kutoka DRC ni namna watu hao wanavyowasili bila kupitia njia rasmi za mipakani ambako wangepimwa kabla ya kutangamana na jamii za Uganda.

Wakazi wana wasiwasi kuwa kuna uwezekano wa milipuko ya magonjwa ya Ebola na kipindupindu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya February 16

Wadau wa madini kuandamana kumpongeza Rais Magufuli

0
0
Wadau wa madini na wachimbaji wa mkoa wa Manyara, wanatarajia 
kuandamana Jumamosi ijayo, kwa lengo la kumshukuru Rais John Magufuli 
kwa kukubali kutia saini muswaada wa dharura wa marekebisho ya sheria za
fedha, kupunguza na kufuta kodi zilizolalamikiwa.

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara
(Marema), Tawi la Mirerani, Shwaibu Mushi, alisema jana kuwa
 maandalizi ya maandamano hayo yatakayopokelewa na Mkuu wa Mkoa huo,
Alexander Mnyeti, yanaendelea vizuri.

Alisema maandamano yatafanyika umbali wa kilomita tatu na yataanzia 
kwenye lango la Magufuli la kuingia ndani ya ukuta saa 2:00 asubuhi
na kumalizika Saa 4:00 asubuhi.

Baada ya hapo, alisema itasomwa risala ya kumpongeza
Rais Magufuli kudhibiti utoroshwaji madini, ulipaji kodi na kumuunga
mkono.



“Waandamanaji watazunguka migodi ya madini ya Tanzanite hadi kwenye
uwanja wa barafu wa CCM Mji Mdogo wa Mirerani ndipo 
watakapoishia,”alisema.



Mushi alisema maandamano hayo yatawahusisha wachimbaji wote wa madini
 wa mkoa huo kutoka wilaya zote za Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang'
na Mbulu.

Alisema lengo kubwa ni kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwakubalia
 ombi lao, hadi wabunge wakapitisha sheria hiyo baada ya mkutano wa
kisekta wa wadau wa madini uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam.

 

Alisema kaulimbiu ya maandamano hayo ni “Rais Wetu, Madini Yetu,
Uchumi Wetu” na wadau mbalimbali wa madini wakiwamo wachimbaji,
wamiliki wa migodi na wazamiaji (na Apolo) watashiriki.

"Pia wadau wengine wanaonufaika na madini wakiwamo wafanyabiashara,
madalali na wanunuzi wa madini, watashiriki maandamano hayo
ya kumpongeza Rais Magufuli wetu," alisema Mushi.

Alisema wanaandamana kumpongeza Rais Magufuli, baada ya kupita siku 17
tangu mkutano wake na wadau wa madini kufanyika na kisha kupitishwa
kuwa sheria na bunge.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Agustino Senga
 alisema maandamano kama hayo yanaruhusiwa kufanyika mradi
 wahusika wawe na kibali kutoka kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya husika.

Kamanda Senga alisema hivi karibuni yalifanyika maandamano kama hayo
 ya wafugaji na wakulima kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwatetea, hivyo 
hata hayo ya wadau wa madini watayaruhusu wakiomba kibali.

Wilaya Ya Mufindi Imeanza Kupiga Kura Kuwabaini Wabakaji Na Walawiti

0
0
Na.Amiri kilagalila
Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imeanza kupiga kura ya maoni ya siri katika vijiji vyote vya tarafa tano za wilaya hiyo ili kuwabaini waharifu wa matukio ya ubakaji na ulawiti ambayo yanaonekana kukithiri katika wilaya hiyo na kuifanya wilaya hiyo kuwa ya kwanza kati ya wilaya tatu za mkoa huo kwa ukatili huo.

Kaimu katibu tawala wa wilaya ya mufindi Joseph Mchina amesema kuwa kura ya siri ya maoni imeanza tangu januri katika vijiji na mitaa na baadae litafanyika katika taasisi za elimu zikiwemo shule za sekondari , msingi na vyuo ili kuwabaini watu wanaohusika na matukio hayo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga mh Charles makoga amesema kuwa sababu za matukio ya kikatili ya ubakaji na ulawiti katika mkoa wa iringa zinachagizwa na imani za kishirikina mambo ambayo yanatokana na ukosefu wa elimu.

Badhi ya wananchi waliozungumza na mtandao huu wamesema utaratibu wa serikali kupiga kura ya maoni ya siri uende sambamba na uandaaji wa takwimu sahihi kwa kuwa bado kunataarifa zilizipo hazina uhalisia na matukio.

TANTRADE Yamwaga Fursa Kwa Wazalishaji Wa Kahawa,viungo,chai, Ufuta Na Matunda

Waziri Wa Mambo Ya Ndani Kangi Lugola Apokea Gari,akemea Polisi Kusindikiza Bangi

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amekemea matumizi yasiyofaa ya magari ya Jeshi la Polisi ikiwamo kubeba au kutumika kusindikiza magari yaliyopakia bangi na mirungi.

Ametoa kauli hiyo jana Ijumaa Februari 15, 2019 jijini Arusha wakati akipokea gari la Polisi lililokarabatiwa na taasisi ya Fredkin Conservation Fund kwa gharama ya Sh15 milioni.

"Mkuu wa Polisi wa wilaya sitaki kusikia hii tabia ya magari yetu kuhusika kwenye vitendo viovu, akabidhiwe dereva aliyehitimu vyema na mwenye maadili," alisema Lugola.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameishukuru taasisi hiyo kwa kuchangia shughuli za ulinzi na kuwa tayari wamejitokeza wadau watakaokarabati magari yote mabovu ya polisi wilayani humo.

Waziri Mkuu Akaribisha Wawekezaji Nchini......Awahakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi za India, Misri na Falme za Kiarabu waje wawekeze nchini na Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.

Ameyasema hayo jana (Ijumaa, Februari 16, 2019) wakati alipokutana kwa nyakati tofauti na mabalozi wa India, Misri na Falme za Kiarabu wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania.

Mabalozi aliokutana nao ni  Balozi Sandeep Arya (India), Balozi Mohamed Abulwafa (Misri) na Balozi Mohammad Albahri (Kaimu Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania).Akizungumza na Mabalozi hao Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni, Dar es salam, Waziri Mkuu amesema Tanzania ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka kwenye nchi hizo.

Amesema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini ili kukuza uchumi na kufikia wa kati ifikapo 2025, hivyo amewakaribisha wafanyabiashara waje wawekeze.Amesema Ofisi yake kupitia Waziri mwenye dhamana ya Uwekezaji, Bibi Angela Kairuki iko tayari kuwasikiliza na kuwasaidia wawekezaji wote wanaokusudia kuwekeza nchini.

“Tanzania iko tayari wakati  wote kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wawekezaji watakaojitokeza kuwekeza nchini wanafanikiwa ili mataifa yote yaweze kufaidika.”Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Tanzania ina vivutio vingi vya utalii ikiwa ni pamoja na uwepo wa mlima Kilimanjaro, mbunga zenye wanyama wa aina mbalimbali na fukwe nzuri.
 
Hivyo, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watalii kutoka mataifa mablimbali yakiwemo yaIndia, Misri na Falme za Kiarabu waje nchini na kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo.

Kwa upande wao,Mabalozi hao wameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na nchi zao, hivyo wamemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza.

Wamesema wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati kupitia sekta ya viwanda unafanikiwa. 

Pia Mabalozi hao wameahidi kushirikiana na Serikali Tanzania kuhakikisha inaboresha sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Sekta Ya Afya Isiwe Kikwazo Kwa Wananchi Kupata Matangazo Yao Mapema.

0
0
Na WAMJW - DSM
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameagiza Sekta ya Afya kutokuwa kikwazo kwa wananchi kupata Matangazo ya kuzaliwa kwa watoto kwa ajili ya kupata cheti cha kuzaliwa kwa muda mfupi.

Ameyasema hayo jana, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala jijini Dar ea salaam.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Hospitali hiyo ni lazima ichukue juhudi za makusudi, ikiwemo kuongeza wafanya kazi ili kuhakikisha kwamba Watoto wote wanaweza kupata matangazo yao ndani ya Wiki moja, jambo litaloepusha usumbufu kwa Mwananchi ambao unaweza kuepukika.

" Sisi kama sekta ya Afya, tusiwe kikwazo, vya Mwananchi kupata haya matangazo, na hili nimeliona nimeshatoa maelekezo juu ya hili, na ndani ya wiki moja nategemea kwamba tatizo hili litakuwa limetatuliwa" Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile akiongeza kuwa Matangazo haya ni ya muhinu sana katika mchakato wa kupata vyeti vya kuzaliwa, hivyo Mganga Mfawidhi ni lazima aweke mikakati thabiti ikiwemo kuongeza watu ili kuhakikisha kuanzia sasa matangazo yawe yanatoka ndani ya masaa 24.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupambana na changamoto ya msongamano wa watu katika Hospitali hiyo, Serikali imeboresha zaidi ya vituo vya Afya 350, huku zikijengwa Hospitali za Wilaya 67, na Hospitali za mikoa 2, ili wananchi waweze kupata huduma katika ngazi ya chini kabla yakufikia katika Hospitali za Rufaa.

"Kama Serikali tunachofanya ni kuboresha vituo vya Afya karibia 350, tunajenga Hospitali za Wilaya 67, na Hospitali za Rufaa za Mikoa 2, hivyo tunatarajia hizi Hospitali zinkianza kufanya kazi na huduma za upasuaji zikianza kupatikana kule, huu msongamano utaamia kule" alisema Dkt. Ndugulile

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amewapongeza watu wote wenye VVU kujitokeza kupata matibabu, huku lengo la Serikali ni kufikia 909090, yaani 90 watu wote walio na Virusi vya Ukimwi waweze kufikiwa na kupimwa, 90 ya pili ni kuhakikisha waliopimwa waweze kuanzishiwa dawa papo kwa papo, na 90 ya tatu ya walioanzishiwa dawa waweze kufubaza virusi vyao vya Ukimwi, yote ni kuhakikisha ifikapo 2030 pasiwe na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dkt. Mkungu Daniel mesema kuwa Hospitali hiyo inapokea Mwananchi zaidi ya 2000, huku akisisitiza kuwa Hospitali hiyo ipo katika hatua yakujenga jengo ambalo litabeba jumla ya vitanda 150 kwaajili ya mama na mtoto ili kupambana na changamoto hiyo ya msongamano.

Mgimwa: Sheria Za Kilimo Zilizopo Kwa Sasa Hapa Tanzania Ni Za Tangu Ukoloni Na Za Unyonyaji Kwa Wakulima

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati za kudumu za bunge ,kamati ya kilimo ,Mifugo na Maji Mhe.Mahamoud Mgimwa amesema kuwa sheria za kilimo  zilizopo kwa sasa  hapa Tanzania ni za  tangu ukoloni na hazina tija yoyote kwa mkulima wa kawaida bali zipo kwa ajili ya kumwumiza na kunufaisha watu wa tabaka  la juu.

Mgimwa ameyasema hayo  Februari 15 jijini Dodoma wakati akifunga mkutano  mkuu wa tano wa wadau wa Sekta  ya  kilimo hapa nchini ambapo amezitolea  mfano baadhi ya sheria ambazo serikali imezikuta kutoka kwa wakoloni ni pamoja na sheria   ya bodi ya korosho,sheria ya bodi ya pamba na sheria ya tumbaku hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kutunga sheria zitakazoleta tija kwa wakulima.
 
“Sheria nyingi  ukiangalia ni za kikoloni hatujazitunga sisi,kuna sheria ya bodi ya korosho,sheria ya bodi ya tumbaku,sheria ya bodi ya Pamba nakadharika,angalia hazikuwa zinamfever mkulima zilikuwa zinamfever mkoloni kwa hiyo tunahitaji kuwa na sheria yetu watanzania,sheria zinatungwa nje ya bunge na ndani ya bunge kwa hiyo anzeni mchakato mkiona kuna ukakasi tunashirikiana ili mkulima wa chini anufaike na yeye”
 
Mhe.Mgimwa amefafanua mkulima wa chini amekuwa akihangaika kulima yeye mwenyewe bila usaidizi wowote  lakini inapofika wakati wa mavuno  serikali inamwingilia na kumpangia namna ya kuuza au kutouza mazao Yake  kutokana na mfumo mbovu na kandamizi wa sheria zilizopo za tangu ukoloni .
 
“Mkulima anapokwenda kulima shamba hana confilict na mtu yeyote  aidha akodi shamba au alime shamba lake,ikifika wakati wa kuvuna anataka kuuza serikali inakuja kumwambia hakuna kuuza nje ya nchi,sawa si sawa.

"Kwa  hiyo  hakuna sheria yoyote inayomlinda mkulima zaidi ya kumnyonya na kumgandamiza,hivyo kuna uhitaji mkubwa wa marekebisho ya sheria wadau wa kwanza wa kuangalia mapendekezo ya sheria ni ninyi wadau na wataalam  wa kilimo pekee sisi bunge ni kupokea mapendekezo,kujadili na kutunga sheria”
 
Katika hatua nyingine Mgimwa amemtaka mwandaaji na mratibu wa kongamano hilo la wakulima  ,Mshauri wa Masuala ya kilimo Tanzania, Profesa David Nyange kuwa na utaratibu wa kuwashirikisha  wakulima wenyewe wa hali ya chini  na si kama ilivyo  kwa sasa  ambapo wamekuwa wakishiriki wasomi pekee  huku pia  akitaka mpango wa program wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili[Agricultural Sector Program ][ASDP-2] kuwa na mpango wa kuweka ripoti kwamba imefikia wapi katika utekelezaji wake huku serikali ikiwa na mpango wa kuwekeza  Sh.Trilioni 14 .
 
“Wataalam mpo wengi sana kuliko hata watu waliokusudiwa.mkutano huu ungependeza ungekuwa na wakulima wengi,wavuvi wengi,pamoja na wafugaji.Lakini liangalieni nanyi watu wanaobadilishana mawazo sio tunaowalenga”.
 
Kwa upande wake Mshauri wa Masuala ya Kilimo hapa nchini Prof.David Nyange amesema maazimio ya mkutano huo watayachambua zaidi na kuyafikisha katika sehemu husika huku Mtaalam mwingine wa masuala ya kilimo ambaye kwa sasa ni Katibu tawala mkoa wa Kagera Prof.Faustine Kamzora akisema kuwa  Tanzania haiwezi kuondokana na umasikini bila kuongeza tija.

Mkutano huo wa siku tatu umehudhuriwa na wataalam na viongozi mbalimbali wa asasi za kiraia na kiserikali miongoni mwao ni pamoja na makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge,kilimo,mifugo na maji Dokta  Christopher Ishengoma,Mhadhiri chuo kikuu cha kilimo-SUA Dokta Sizya Lugeye ,mkurugenzi wa mradi SOYA NI PESA kupitia taasisi ya CATHORIC RELIEF SERVICE Bi.Neema Mrema  na wengine wengi na kaulimbiu ni mchango wa sekta ya kilimo katika kuhamasisha kukuza viwanda.
 
MWISHO.

Uchaguzi wa rais, wabunge Nigeria waahirishwa

0
0
Uchaguzi mkuu wa urais na wabunge nchini Nigeria umeahirishwa ambapo utafanyika baada ya wiki moja.

Tume huru ya kitaifa ya uchaguzi (INEC) ilitangaza hatua hiyo saa tano  kabla ya wapiga kura kuelekea katika vituo vya upigaji kura leo Jumamosi.

“Haiwezekani kuendelea na zoezi la uchaguzi kama ilivyopangwa,” mwenyekiti wa tume hiyo, Mahmood Yakubu, amesema, akitaja hitilafu za kimipango.

Amesema uamuzi huo mgumu umehitajika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki. Uchaguzi wa urais na ubunge umepangwa kufanyika Jumamosi ijayo Februari 23.

Uchaguzi wa magavana, wawakilishi wa majimbo na mabaraza ya manispaa umepangwa kufanyika Jumamosi Machi 9 mwaka huu.  Uamuzi huo umetolewa baada ya mkutano wa dharura katika makao makuu ya tume hiyo ya uchaguzi katika mji mkuu Abuja.

Yakubu amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya ‘ukaguzi wa makini’ wa ‘mpango wa namna uchaguzi utakavyofanyika’, akiongeza kwamba kuna ‘jitihada kubwa za kuhakikisha kuna uchaguzi  huru, wa haki na wa kuaminika’.

Amesema ni muhimu kuchelewesha uchaguzi huo kuipa tume nafasi ya kukabiliana na masuala muhimu na pia “kusalia na hadhi katika uchaguzi”, lakini hakutoa ufafanuzi zaidi.

Katika wiki mbili zilizopita ofisi kadhaa za tume hiyo ya uchaguzi ziliteketezwa moto, huku maelfu ya vifaa vya kunakili kadi , na kadi za upigaji kura zikiharibiwa.

Pia kumekuwa na taarifa ya uhaba wa vifaa vya upigaji kura katika baadhi ya majimbo 36 ya nchi hiyo. Nigeria imelazimika kushinikiza usalama wake kuelekea katika uchaguzi huu uliokumbwa na ghasia.

Siku ya Ijumaa, maofisa katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria wameripoti kugundua miili ya watu 66, ambapo 22 kati yao ni ya watoto, na 12 ya wanawake waliouawa na ‘wahalifu’.

Je Unaupungufu Wa Nguvu Za Kiume au Maumbile Mafupi na Membamba...Suluhu iko hapa

0
0
Acha kusubilia mpaka mke au mpenzi wako akwambie Mme wangu wewe ni dhaifu tuwepo kitandani,unatakiwa ujitambue mapema ,kwa mwanaume aliyekamilika  na mwenye nguvu za kutosha  ili kumridhisha mke au mpenzi wake anatakiwa awe na uwezo wa kurudia zaidi ya Mara mbili lakini kama unakomea moja au mbili hapo ujue umejilidhisha wewe tu sio na yeye, ili uwe mwanaume mwenye uwezo kamili tumia dawa yako hii hapa

 SUPER MAJINJAS MIX; dawa hii ni tofauti na ambazo uliwai kutumia inamichanganyo ya miti na matunda zaidi ya saba ndio maana inakupa uwezo wa ,KURUDIA TENDO ZAIDI YA MARA TATU,NA ITAKUFANYA UCHELEWE KUFIKA KILELENI DAKIKA 10-15 KWA TENDO LA KWANZA,NA PIA HUIMALISHA MISULI ILIYOLEGEA NA KUSINYAA KWA WALE AMBAO WALIPIGA SANA PUNYETO,dawa hii ni ya vidonge na unga na haina madhara yoyote

MAKAKANUA NO 5 MPYA; dawa hii uboresha uume saizi upendayo UREFU WA INCHI 5,6,7,NA 8 NA UPANA WA CM 2,3,4 NA 5 dawa hii ipo ya kunywa na kupaka  na pia usahidia zaidi kwa mwanaume aliyefanyia tohara ukubwani,

ISENYE NO 3; hii ni dawa kwa wenye kisukari dozi siku 21 tatizo la kisukari na ndio chazo kikubwa cha kuishia nguvu za kiume,

NGWALUSA ; hii ni dawa ya uzazi ambayo ufungua milija ya uzazi ata kwa wale walifungwa uzazi,zipo dawa za busha,vidonda vya tumbo,miguu au viungo kufa gazi kupungza kitambi,minyama uzembe,na matiti makubwa 

FIKA NTUNZU HEBRISTI CLINIC ILIYOPO MBAGALA ZAKHEMU Njoo mpaka ulipo ukumbi wa DAR LIV ni dakika tano tu kufika ofisi ilipo. MOROGORO,MWANZA,NA KAHAMA WAPO MAWAKALA

 Kwa mawasiliano zaidi piga simu 0744040721, 0683645920 DR BRUNO pia unaweza ukaletewa popote ulipo
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images