Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili, Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa sababu shahidi aliyetakiwa kuanzakutoa ushahidi wake Leo amepata dharura.
Kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi lakini Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ameiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine Kwani shahidi amepata dharura.
Kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi lakini Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ameiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine Kwani shahidi amepata dharura.
“Kwa jinsi upande wa mashtaka tulivyokuwa tumejipanga tulitaka tuanze na ushahidi leo na shahidi tuliyekuwa tumemuandaa amepata matatizo ya kifamilia tunaomba kuahirishwa kwa muda,” amesema Katuga.
Wakili wa utetezi, Jebra Kambole amedai mshtakiwa alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini pia ana majukumu mengine kuomba tarehe za mwishoni.
Hakimu Shahidi baada ya kusikiliza maelezo hayo ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 27, 2019 kwaajili ya kuanza kusikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka.
Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa kutenda makosa hayo Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.
Alifikishwa katika mahakama hiyo na kushtakiwa kwa mashtaka matatu ya uchochezi.