Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

KCMC Yasitisha Kutoa Huduma ya Bima Kwa Makampuni Haya

$
0
0
Hospitali  ya Rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro imesitisha kutoa huduma kwa wafanyakazi wa makampuni saba yanayotumia bima za afya kutokana makapuni hayo kudaiwa zaidi ya shilingi bilioni 2.2.
 
Kwa mujibu wa Ofisa Habari na Mahusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo, hospitali hiyo imelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya makampuni hayo kushindwa kulipa madeni yake  yanayokadiliwa kufikia Sh. Bilioni 2.2.
 
Chisseo ameyataja Makampuni hayo kuwa  ni NSSF, AAR, Jubilee, Strategies, Ngorongoro, TPC na TANESCO ambapo amesema  baadhi yake yanadaiwa fedha za tangu mwaka 2016.
 
“Tuna mkataba na hizi taasisi, ule mkataba unaonyesha baada ya mwezi mmoja wawe wametulipa baada ya kutoa huduma kwa wanufaika wao, hadi sasa tuna madai ya tangu mwaka 2016 mpaka sasa.
 
“Kwa hiyo kwetu sisi tunapata mzigo mkubwa na wakumbuke
tumekuwa tuna jukumu la kutibu watanzania ambao hawana uwezo kupitia hiki hiki kiasi kidogo ambacho wananchi wamekuwa wanachangia,” alisema Chiseo.
 
Alisema uongozi wa hospitali umeshatoa taarifa kwa njia mbalimbali, hivyo ni wajibu wa wanufaika hao kwenda moja kwa moja katika taasisi na mashirika hayo kuwaeleza namna ambavyo wataweza kuhudumiwa baada ya huduma kusitishwa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya January 22

Kamati Ya Bunge Yaishauri Serikali Kuweka Mkazo Katika Kampeni Ya Upandaji Miti

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira imeishauri Serikali kuona namna bora ya kuendeleza kampeni ya upandaji miti kwa mafanikio zaidi katika ngazi zote.

Ushauri huo umetolewa katika kikao  baina ya Kamati hiyo na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa kipindi cha miezi sita yaani (Julai 2018 – Desemba 2018).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Waheshimiwa Wabunge wameishauri Serikali kuhuisha kampeni ya upandaji miti katika Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Vikuu ili kasi ya upandaji miti iendane na kasi ya ukuaji wake, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kwa vitendo mpango wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

“Wekeni utaratibu wa kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi katika kupanda na kutunza miti” alisisitiza Mhe. Dotto Gimbi Mjumbe wa Kamati hiyo

Akitoa ufafanuzi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amesema katika kipindi cha miezi sita, Ofisi ya Makamu wa Rais imepata mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kutimiza malengo waliojiwekea na kuahidi kuendelea kuzipatia ufafanuzi changamoto nyingine zilizoibuliwa na wajumbe wa Kamati likiwemo suala la utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi kwa upande wa pili wa Muungano.

Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vinaendelea katika kumbi za Bunge Jijini Dodoma na siku ya kesho Kamati hii itapokea taarifa ya Usimamizi na Matumizi salama ya Bioteknolojia ya Kisasa na Maandalizi ya Mpango wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji wadogo wa dhahabu chini ya Mkataba wa Minamata.

Je, Dada unataka kuwa mrembo? Na kaka unataka kuwa mtanashati??....Tumia bidhaa za NATURAL BEAUTY

$
0
0
Je, Dada unataka kuwa mrembo? Na kaka unataka kuwa mtanashati??

Tumia bidhaa za NATURAL BEAUTY ni bidhaa zenye matokeo ya uhakika na kwa haraka zaidi.

Bidhaa hizi ni salama kabisa zimetengenezwa kwa mimea na matunda hazina kemiko wala madhara yoyote.

 🍉🥑🍇🍒🍑🍐

1. BOTCHO MULT PLUS- Hii ni dawa ya kuongeza ( Hips mapaja na makalio) inapatikana kwa @250,000/=

2. BOTCHO HOLOGRAM CREAM-Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza hips na makalio inapatikana kwa@220,000/=

3. HANDSOME UP ORIGINAL-- Hichi ni kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo pamoja na kuimalisha misuli kifaa hichi  kinapatikana kwa @250,000/=

4. LEG  BOOSTER- Dawa ya kupaka ya kuongeza miguu kuwa ( Chupa ya bia) @170,000/=

5. MAXMAN 2 CAPSULE-Hii ni dawa ya vidonge ya kuongeza uume urefu na upana pamoja na kuongeza nguvu za kiume kwa wiki mbili  inapatikana kwa @250,000/=

6. VIG RX- Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 11.5 inapatikana kwa @220,000/=

7. BODY BOOSTER- Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri  @150,000/=

8. WHITE COLLECTION---- Ni vidonge vya kuwa mweupe mwili mzima pamoja na kuwa soft  vinapatikana kwa @170,000/=

9. SHARK SUPER POWER-Ni dawa ya kuongeza maumbile mpaka nchi 7.5 ndani ya wiki tatu tu @200,000/=

10. YODI PILLS-- Ni vidonge vya kuongeza (hips mapaja na makalio) vinapatikana kwa @250,000/=.      N.K

Wasiliana nasi kwa simu
NO. +255 75902996
                   AU
          +255 659618585

Popote ulipo utapata huduma zetu.
Pia hakikisha unapatiwa risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY PROD ununuapo bidhaa kampuni hii.

                         WELCOME ALL

Taasisi Ya Moyo Ya Jakaya Kikwete Yawa Ya Kwanza Afrika Mashariki Na Kati Kuwa Na Wodi Ya Watoto Wenye Magonjwa Ya Moyo

$
0
0
Na: Genofeva Matemu – JKCI
Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI) imekuwa   taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na wodi pekee ya kuwahudumia watoto wenye magonjwa ya moyo bila kuwachanganya na watu wazima.

Eneo la wodi hiyo lilitolewa mwaka 2017 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli alipokua akizindua Hospitali ya Mloganzila na kuiagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoa sehemu ya jengo linalohudumia watoto kwa JKCI ili watoto wenye magonjwa ya moyo waweze kuwa na wodi yao katika kuleta ufanisi wa matibabu ya moyo kwa watoto hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi hiyo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamaii, Jinsi, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alisema upatikanaji wa wodi hiyo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha utolewaji wa matibabu ya moyo kwa watoto ya kibingwa yanaendelea kuboreshwa hapa nchini.

“Kwa wodi za watoto wenye magonjwa ya moyo peke yake kwa hapa Afrika Mashariki na kati hii ndio itakua wodi ya kwanza inayowahudumia watoto bila kuwachanganya na watu wazima na hii italeta ufanisi zaidi kwani nafasi ya kufanya makosa haitakuwepo kwasababu kutakuwa na wataalamu wanaohudumia watoto tu” alisema Waziri Ummy

Waziri Ummy, alisema  wodi hiyo ambayo ukarabati wake umekamilika inatarajiwa kuwa  na vitanda 32 na chumba cha uangalizi maalum (ICU) kitakachokuwa na vitanda 15 jambo ambalo litasaidia kuwafanyia upasuaji watoto wengi zaidi waliopo katika foleni ya upasuaji na kuokoa maisha yao.

“Serikali ilitoa milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa wodi hii na sasa kwa mara nyingine tena serikali imetoa milioni 500 kukamilisha miundombinu ya ukarabati wa wodi hii. Nawashukuru sana taasisi ya Baps Charity ambao nao wamewekeza  milioni 800 katika kuhakikisha kuwa wodi hii inakarabatiwa, serikali tutazidi kuunga mkono juhudi hizi ”  alisema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prf. Mohamed, Janabi alisema kwa shifti mbili za kliniki ya watoto zilizopo JKCI inaona wagonjwa wa moyo hadi sitini kwa siku thelathini wakiwa ni watoto, hivyo kulikuwa na umuhimu wa kuongeza wodi hiyo ya watoto.

Akizungumzia upasuaji wa magonjwa ya moyo prof. Janabi amesema kuwa jumla ya wangonjwa 1356 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa mwaka 2018, hii kwa mwaka jana ukiondoa Afrika kusini JKCI ndio hospitali iliyofanya upasuaji kwa wangonjwa wa moyo wengi zaidi kuliko nchi yoyote ya Afrika.

“Wodi hii mpya ni kwaajili ya watoto chini ya miaka 13 pekee na hii itatufanya kuwa taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuwa na jengo lenye kuhudumia watoto bila kuwanchanganya na watu wazima “alisema prof. Janabi

Umehangaika na Tatizo la Nguvu za Kiume,Tezi Dume, Miguu Kuvimba Bila Mafanikio?? Suluhisho Ni Dr.Ngaru

$
0
0
Kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume usiopungua nchi 5_6 mpaka 7,vinginevyo mtu huyo anamatatizo,zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo Hilo baadhi Ni upungufu wa vichocheo vya HORMONES ZA CETROGEN.

IGWATA,Ni dawa inayozalisha Hormones za CETROGEN na kufanya uume kukuwa   na kuongezeka size uitakayo na kuzibua mirija iliyosinyaa.

NGUMO MIX 4 POWER,dawa Bora ya kurudisha Nguvu za kiume kwa kutibu kabisa tatizo hilo na kukupa hamu ya kurudia tendo zaidi ya Mara nne bila kuchoka.

SALIUNGU,Ni dawa inayotibu magonjwa sugu Kama kisukari,Tezi dume,Presha ya kupanda na kushuka pamoja na stroke (kupalaizi) na Busha bila kufanyiwa operation..Tumia SALIONGO kwa kutatua tatizo lako kabisa.

NTUNDWA,Ni dawa Bora kabisa inayotibu uvimbe tumboni na kwa wale wakina mama wasiopata hedhi kwa wakati pia hupanga mayai ya Uzazi kwa mtumiaji na kufanya mimba zisiharibike  pia kwa wale wasiopata watoto kwa mda mrefu hii Ni kiboko kabisa wahi Sasa.

TALIGURA,Ni dawa ya kumvuta mpenzi,hawara, mchumba,mke au mume aliekuacha kwa muda wa siku 4.

IDACHAMWA, Hutibu miguu kuwaka moto, Miguu kuvimba, magoti, kiuno,na  mgongo Ni ya kunywa na kupata  dozi siku 8.

HUDUMA ZANGU NGARU NI ZA HARAKA ZAIDI NA MAFANIKIO MAFUPI,UNAWEZA KUFIKA NILIPO AU KUSAFIRISHIWA POPOTE ULIPO., NAPATIKANA DAR ES SALAAM NA KAHAMA USISITE KUULIZA WASILIANA NAMI KWA NAMBA

  0753 928 576.

Wagonjwa MOI Kufanyiwa Upasuaji Bila Nusu Kaputi

$
0
0
Na Andrew Chale
TAASISI ya tiba ya Mifupa MOI imeanzisha huduma ya kutoa dawa za usingizi (Reginal block Anaesthesia) ambapo eneo husika linalofanyiwa upasuaji ndilo litakolo husika kwa kuzuia mishipa ya fahamu na hivyo mgonjwa kuwa macho na kuzungumza au hata kusoma gazeti

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface katika hafla ya kuwapokea wakufunzi wawili kutoka Chuo kikuu cha Latvia cha nchini Latvia ambao watatoa mafunzo hayo ya kibingwa ya kuzuia mishipa ya fahamu katika eneo linalofanyiwa upasuaji badala ya kumlaza mgonjwa usingizi (Nusu kaputi) kwa zaidi ya siku kumi kwa madaktari bingwa wa MOI na madaktari walio mafunzoni

“Huu ni muendelezo wa mafunzo ambayo tulishayaanzisha kwa mdakatari wetu , lengo kubwa la mafunzo haya na ujio wa wakufunzi hawa ni kuhakikisha huduma hii inaendlea kutolewa hapa MOI. Ni mbinu bora na salama ya kumlaza mgonjwa kwaajili ya upasuaji ambapo mgonjwa anaweza kufanyiwa upasuaji huku anasoma kitabu (Novel) ambapo baada ya upasuaji mgonjwa hapati maumivu makali na anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani siku hiyohiyo” Alisema Dkt Boniface

Dkt Boniface amesema pamoja na wakufunzi hawa kutoa mafunzo , Taasisi ya MOI itasiani mkataba wa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Latvia lengo kuu ikiwa ni kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma za kibingwa za Usingizi (Anaesthesia)

“Kwa kuanza tutasaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu ambapo watalaamu kutoka hapa watapata fursa ya kujifunza kwenye Chuo chao lakini pia watakuja hapa kutoa mafunzo ya muda mfupi kama ambavyo hawa wamekuja” Alisema Dkt Boniface

Dkt Boniface ameongeza kwamba kwa sasa Taasisi ya MOI imeanzisha huduma ya kulazwa na kufanyiwa upasuaji siku hiyohiyo yaani (Same day Surgery) hivyo huduma hii itatumika katika wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji na kuruhusiwa kwani wagonjwa hawapati maumivu makali baada ya upasuaji na hakuna masharti magumu baada kufanyiwa upasuaji

Kwa upande wake Profesa Alex Miscuks kutoka Chuo Kikuu cha Latvia amesema ni heshma kubwa kupata fursa ya kuja kubadilishana uzoefu hapa Tanzania kwani pamoja na kutoa mafunzo atapata fursa ya kujifunza mambo mengi.

“Nashukuru sana kwa kunialika, nimefurahi kukutana na madaktari wazuri na wazoefu hapa MOI, naamimi mimi pia nitajifunza mambo mengi kwenu, ahsnteni sana” alisema Prof Miscuks

Kwa upande wake Dkt Iveta Gobovska ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha wagonja mahututi katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Latvia amesema amefarijika kupata fursa ya kuja kubadilishana uzoefu na madaktari wa Tanzania na anamini pande zote mbili zitanufaika na mafunzo haya.

DRC: Polisi yamzuia Fayulu kuhutubia wafuasi wake....Bado Anasisitiza Yeye Ndo Mshindi Halali wa Urais

$
0
0
Polisi wamezuia wafuasi wa Martin Fayulu kukusanyika kwenye makao makuu ya chama chake alitakorajiwa kuwahutubia. Ingawa Korti ya Katiba imethibitisha ushindi wa Felix Tshisekedi, Fayulu anadai ameibiwa ushindi wake.

Msemaji wa Martin Fayulu Eve Bazaiba amesema polisi walivamia mahali ambako Fayulu alikusudia kuwahutubia wafuasi wake, na kulibeba jukwaa na vipazasauti vilivyokuwa vimeandaliwa.

''Wamevikamata vyombo vyote na kuwakamata pia watu, na sijui wamewapeleka wapi.'' amelalamika Bazaiba na kuongeza, ''nilipouliza kinachoendelea, nimeambiwa polisi wanacho kibali cha kuwazuia watu kuingia na kutoka.''

Licha ya kutawanywa na polisi baadhi ya wafuasi wa vuguvugu la upinzani la LAMUKA linalomuunga mkono Fayulu waliendelea kusubiri kuwasili kwa kiongozi wao kwenye makao makuu ya chama cha MLC.

Fayulu na wafuasi wake ambao wamepinga matokeo yaliotolewa na tume ya uchaguzi na kujitangaza kuwa mshindi wa uchaguzi huo amesema kwamba ni lazima raia wa kongo wapewe haki zao.

''Tunachotaka ni kupata haki kulingana na matokeo ya uchaguzi, kwa sababu tuna uhakika kwamba tulishinda,'' amesema msemaji wa Fayulu Eve Bazaiba, na alipoulizwa watafanya nini kuhakikisha wanafanikiwa, amesema watazidi kukazana kwa sababu 'sheria iko upande wetu.''

Wakati huohuo, mandalizi kwa ajili ya kuapishwa kwa rais mteule Felix Tshisekedi yanaendelea mjini Kinshasa. Sherehe hiyo iliotarajiwa kufanyika Jumanne imeahirishwa hadi Alhamisi, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa Lambert Mende msemaji wa serikali inayoondoka madarakani.

Mahali patakapofanyika sherehe hiyo bado kufahamika, lakini wafuasi wa chama cha UDPS cha Tshisekedi waliomba kiongozi wao aapishwe kwenye uwanja wa kandanda wa Kinshasa ilikuwaruhusu washiriki pia.

Ni kwa mara a kwanza Kongo itashuhudia kuapishwa kwa rais mpya kufuatia kuchukuwa madaraka kwa njia ya amani kutoka kwa rais mwingine.

Credit:DW

Wahamiaji 81 Wanaswa Dar es Salaam......Msako Bado Unaendelea

$
0
0
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, imeanza kusaka wahamiaji haramu kwenye makazi na sehemu za kazi, ikiwamo kuwachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa, Kamishna Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiani, Novaita Mroso, alisema operesheni maalum imefanyika na inaendelea.

Alisema wameamua kuwasaka wahamiaji haramu kwenye mitaa, ili kuweza kuwadhibiti zaidi.

“Tukishindwa kukupata eneo la kazi tutakufuata nyumbani, kwa utaratibu tuliojiwekea Dar es Salaam, siyo sehemu salama kuwa maficho kwa wahamiaji haramu. Yeyote anayeajiri raia wa kigeni ahakikishe ana vibali vyote vya kuishi nchini,” alisema.

Alisema ilianza Januari 17 mwaka huu, na hadi jana ilikuwa na siku tano na jumla ya wahamiaji 81, ambao wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali walitiwa mbaroni.

“Kati yao tumebaini 35 wanatoka nchini Burundi, waliobaki wanatoka Somalia na Congo, wengine 46 wanaendelea kuchunguzwa na baada ya kukamilika tutabaini uhalali wao wa kuwapo nchini,” alisema.

Mroso alisema waliobainika kuwa ni wahamiaji haramu watachukuliwa hatua za kuwafikisha mahakamani na kuwafukuza nchini.

“Operesheni maalum ni sehemu ya jukumu letu la udhibiti wa wahamiaji haramu. Pia tumekuwa tukifanya uhakiki wa taarifa za wageni waliopo Mkoa wa Dar es Salaam ambao wamejiajiri au kuajiriwa,” alisema.

Waziri Mkuu Majaliwa Kufungua Mkutano Wa Maafisa Ustawi Wa Jamii

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kufungua mkutano wa siku tatu wa maafisa ustawi wa jamii mikoa 26 na halmashauri zote nchini wenye lengo la kujadili utendaji kazi, utoaji huduma za ustawi wa jamii na mifumo ya utendaji kazi.

Akizungumza na mwandishi wa habari jana jijini hapa, Mkurugenzi Msaidizi  wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi, Rashid Maftaha, alisema kuwa  mkutano huo unatarajia kuanza Januri 29 hadi 31 mwaka huu jijini Dodoma.

Alisema kuwa  mkutano huo unatarajia kushirikisha washiri takribani 370 ikiwamo maafisa ustawi wa jamii wa mikao 26, halmashauri 184, wadau wa maendeleo, na wizara za kisekta ambazo zinahusiana na utoaji wa huduma za ustawiwa jamii, kama wizara ya elimu, afya, Katiba na Sheria, Viwanda na Biashara, madini na kilimo.

“ Unaweza jiuliza, Wizara ya Madini inahusikajie na huduma za ustawi wa jamii, hawa ni wadau muhimu, kwani kwenye migodi kuna utumikishwaji wa watoto, na hata watumishi wake wanakuwa wako mbali hivyo ni lazima wafikiwe na huduma za jamii, halii hii pia iko kwenye viwanda.

“Pia unaweza kujiuliza kwa nini wizara ya kilimo, lakini ukweli ni kuwa asimia 80 ya watanzania wanafanya shughuli za kilimo na asilimia 70 yao wako vijijini, na takwimu zetu zinaonesha kuwa watoto wengi walio katika mazingia hatarishi wanatoka vijijini ambaochanzo kikubwa na umasikini na jangwa la Ukwimi.

Maftaha aliongeza :” Tunashukuru wenzetu wa kilimo katika Mpango wa Maendeleo ya Kilimo kwa kwanza na huu wa pili ni jumuishi kwani kuna dirisha maalumu kwa ajili ya watu walio katika mazingira hatarishi wakiwemo, wenye ulemavu, wajane, wazee ambao wanapata pembejeo na wana uwakilishi katika kamati za ugawaji pembejeo

Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Weledi, uadilifu, uwajibikaji ni nguzo ya msingi katika kuleta usatawi wa makundi maalumu kuelekea katika uchumi wa kati wa viwanda.”

Maftah alisema kuwa : “ Tunaamini watendaji wetu kwenye halmashauri na mikoa wakifanya kazi zao kwa kuzingatia uadilifu, weledi, wakifuata sheria, kanuni na taratibu tunaamini makundi yenye uhitaji maalumu wanaweza kufikiwa inavyotakiwa hivyo mchango wao ukaongezeka katika uchumi wa viwanda,

Mkutano huu ni wa kwanza ikiwa ni takribani miaka 15 baada ya kutokea mabadiliko ya kimuundo kwa kuiondoa Idara ya Ustawi wa Jamii kutoka Serikali kuu kwenda Serikali za Mitaa.

Akifafanua zaidi, Maftaha alisema serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikifanya kwa vitendo katika kuwahudumia wananchi hususani wale wanyonge ikiwamo wazee, wenye ulemavu, watoto wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu, wanawake wenye mahitaji maalumu kama wajane, wenye magonjwa sugu na walio katika kaya masikini.

Hata hivyo alisema kuwa  lengo la mkutano ni kuwakutanisha watendaji hao na kutoa mrejesho wa utekelezaji wa huduma za jamii katika maeneo ya serikali za mitaa, utendaji kazi na namna mfumo inavyofanya kazi.

“ Pia tutaangalia mafanikio na changamoto na kwa upamoja na kuja na mapendekezo ya kutatua changamoto stahiki za za kiutendaji na mfumo ili kusogeza na kuimarisha zaidi hudumua za ustawi wa jamii kwenye mamlaka ya serikali za mitaa. Kama kuna yale ambayo yatataka kuwepo mabadilko ya kisera basi tutafikisha katika mamlaka husika.

Aidha, Maftah alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kuendelea kuwalinda watoto kwa kutoa taarifa haraka kwa mamlaka pale panapokuwa na viiashiria ay dalili au kitendo cha ukatili kwa mtoto.

Alisema kuwa pamoja na pamekuwa na changamoto ya ushahidi pale kesi zinapofika mahakamani au wahanga na mashahidi kubadili taarifa walizotoa awali, lakini ni vyama jamii ikaungana kutakabiliana na ukatili kwa watoto.

“Hatuwezi kukubali vitendo vya ukatili anavyofanyiwa mtoto alafu tuambiwe kuwa wamekubaliana pembeni hilo hatulikubali mpaka sheria ichukue mkondo wake.

Serikali Yapokea vifaa vya Dola za Marekani 30,000 kudhibiti uhamiaji haramu Nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, amepokea vifaa vya kudhibiti uhamiaji haramu katika mipaka mbalimbali nchini vyenye thamani ya Dola za Marekani 30,000 (sawa na Sh. mil. 68.7)
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, wakati wa kupokea vifaa hivyo, Masauni alisema vifaa hivyo vitasaidia kwa kiwango kikubwa kudhibiti mipakani ambako hutumika kama mwanya wa kuingilia wahamiaji haramu na kwamba lengo ni kuhakikisha wanakomesha kabisa wahamiaji haramu ikiwamo vitendo vyote vya uhalifu katika mipaka ya nchi.

"Vifaa hivi ni kama sehemu ya kuongeza nguvu katika mipaka yetu ya nchi katika udhibiti wa wahamiaji haramu na vitendo vyote vya uhalifu katika mipaka yetu yote nchini," alisema Masauni na kuongeza:

"Tunataka kuhakikisha tunakomesha vitendo vyote katika mipaka yote, wahamiaji haramu, bidhaa haramu zinazopita katika mipaka yetu na mambo mengine yote."

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wahamiaji (IOM), Dk. Qasim Sufi, alisema wametoa vifaa hivyo kama mchango wao katika kupambana na vitendo vya uhamiaji haramu Tanzania.

Alisema wataendelea kusaidia katika nyanja hiyo, ili kuhakikisha tatizo hilo hasa katika sehemu za mipaka ya nchi linakomeshwa.

"Tunaamini kwamba kwa vifaa hivi kidogo tulivyotoa kwa Serikali ya Tanzania itasaidia kupambana na vitendo vya uhamiaji haramu kama siyo kumaliza kabisa tatizo hili, lakini tunaahidi kwamba kwa ushirikiano mzuri tulionao na nchi hii, tutaendelea kutoa mchango wetu pale tunapoweza," alisema Dk. Sufi.

Watalii 61 Wawasili Nchini Kwa Treni

$
0
0
Na Paschal Dotto-MAELEZO.
Watilii 61 kutoka nchi mbalimbali wamewasili Jijini Dar es Salaam leo kutoka Afrika ya kusini kwa kutumia treni ya kifahari ya Rovos,kwa nia ya kuja kuangalia vivutio vya kitalii vinavyopatikana hapa nchini.

Akizungumza katika mapokezi hayo Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii nchini Geofrey Tengeneza amesema kuwa kupokelewa kwa wageni hao ni fahari kwa Bodi ya Utalii  kwani ni mwanzo mzuri wa kupata mabalozi wa kuitangaza Tanzania katika sekta ya utalii duniani.

“Tupo hapa kuwapokea watalii hawa 61 kutoka nchi mbalimbali duniani wakitokea Afrika ya Kusini wakitumia Treni hii ya kifahari (ROVOS) Pride of Afrika iliyosafiri kwa siku 15 ikitokea Cape Town mpaka Dar es Salaam ikiwa ni mara ya kwanza kuwasili nchini  kwa mwaka huu wa 2019.”, Alisema Bw.Tengeneza.

Alisema kuwa katika kundi hilo la watalii wapo Waingereza, Wajerumani, Waholanzi, Wasweden, Waitaliano pamoja na watalii kutoka Afrika ya Kusini, treni hiyo imekua ikija nchini mara tano kwa mwaka.

“Nifahari kwa Bodi ya Utalii na Sekta ya Utalii kwa ujumla nchini kwani itaongeza idadi ya watalii wanaowasili nchini kwakutumia hawa 61 kusambaza mema na vivutio vilivyoko Tanzania, lakini pia imeweka uhusino mzuri na watu wa ROVOS kufanya safari zao Dar es Salaam Tanzania mpaka Cape Town Afrika ya Kusini”, alisema.

Tengeneza alisema kuwa katika kundi la watalii hao 61 watagawanyika na kwenda sehemu mbalimbali za kitalii zikiwemo Zanzibar, Serengeti, Ngorongoro pamoja na sehemu nyingine za utalii hasa zinazopatikana Dar es Salaam na Maeneo ya Jirani kama vile Bagamoyo na Saadani.

Treni hii ambayo imekuwa na utamaduni wa kuwasili nchini kupitia reli ya TAZARA imekuwa na ratiba ya kuja nchini mara 5 kwa mwaka huku ikipita katika nchi mbalimbali kama vile  Zimbabwe, Botswana na Zambia na kuingia Tanzania kupitia mpaka wa Tunduma na kupita maeneo mbalimbali ya kitalii ikiwemo Selous.

Watalii hawa watakaa nchini kwa siku 7 huku Treni ikitarajia kuondoka tarehe 24 Januari 2019 ikiwa na watalii wengine ambao walikuja mapema kwa kutumia usafiri wa ndege.

Jeshi la Polisi: Matukio ya mauaji ya ulevi , Watoto Kuibiwa Yamepungua

$
0
0
Jeshi la Polisi limesema matukio ya mauaji yatokanayo na ulevi nchini yamepungua kutoka makosa 129 yaliyoripotiwa mwaka 2017 hadi makosa 118 mwaka jana, ambayo ni sawa na upungufu wa asilimia 8.8.

Pia, matukio ya kupotea ama kuibiwa kwa watoto yamepungua kutoka matukio 134 yaliyoripotiwa mwaka 2017 hadi makosa 116 yaliyotokea mwaka jana, ikiwa ni upungufu wa asilimia 13.4.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali.

“Takwimu zinaonyesha kuwa matukio ya mauaji yanayotokana na ulevi yamepungua. Kwa kipindi cha Januari hadi Desemba matukio hayo yamepungua, ambapo kwa mwaka 2018 yalikuwa matukio 118, ukilinganisha na mwaka 2017 yaliripotiwa matukio 129, ikiwa ni upungufu wa mkosa 11 sawa na asilimia 8.8,” alisema Msangi.

Msangi alisema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watumiaji wa kilevi kunywa kwa kiasi na kujiepusha na matukio ya ugomvi pindi wanapokuwa wamelewa.

Kuhusu matukio ya kupotea kwa watoto, Msangi alisema mwaka 2017 kuliibuka vitendo vya kuibiwa kwa watoto ama kupotea hali iliyosababisha hofu kwa jamii hususani kwa wazazi na walezi.

“Kuhusu matukio ya kupotea au kuibiwa kwa watoto nayo yamepungua, kwa mwaka 2017 matukio yaliyoripotiwa yalikuwa 134, lakini mwaka 2018 yalipungua hadi kufikia matukio 116 ikiwa ni upungufu wa matukio 18 sawa na asilimia 13,” alisema Msangi.

Alisema licha ya kupungua kwa matukio hayo, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wazazi kutowaacha watoto kutembea peke yao, pamoja na kuwa makini na watu wasiowafahamu kuwaachia watoto.

Kuhusu matukio ya usalama barabarani, Msangi alisema matukio hayo nayo yamepungua ambapo kwa mwaka 2017 yalitokea matukio 6,022 kulinganisha na mwaka jana, ambapo yalitokea makosa 3,988 ikiwa ni pungufu ya matukio 2,034 sawa na asilimia 33.8

“Kupungua kwa matukio hayo kumeonyesha kuwa kuna juhudi za Jeshi la Polisi kupambana na matukio hayo,” alisema Msangi.

Alisema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa taasisi mbalimbali zikiwamo za serikali, vyama vya siasa, asasi za kiraia, asasi za kidini na Watanzania wote kuendelea kutoa taarifa za kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini.

Rudisha heshima yako Kwa Mpenzi Wako, Mke Wako...Tumia Tiba Hii ya Asili

$
0
0
Rudisha heshima yako sasa kwa kutumia Dawa hii iitwayo SUPER GAFINA, kwa ajili ya nguvu za kiume na NKOLOMIJE ni kwaajili ya kuongeza maumbile.

Kwa mwanaume aliye kamilika anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara mbili ,ila ukiwa unapiga moja tena kwa shida wewe ujue  unamatatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

TIBA YA TATIZO LAKO NI; Dawa iitwayo SUPER GAFINA, dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge na unga wa asili ambavyo havina madhara kwa mtumiaji ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja;-

1).itakufanya urudie tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuchoka.

2).ltakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dk.15 hadi 20 kwa tendo la kwanza.

3).lnaimarisha uume uliolegea na uliosinyaa na kuupa nguvu maradufu.

Je unamaumbile madogo pamoja na uume mfupi? NKOLOMIJE ni suluisho la tatizo lako. Na ni dawa inayoboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi kuanzia inch. 5 hadi 8 kwa muda mfupi sana .Dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk.30 ukisha tumia guarantee miaka 50  ikishakutibu.

Pia ninatibu;- KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU, MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE ,BP, NK.

IGULYATI, ni dawa ya mvuto wa biashara, kazi,kupandishwa cheo na humfanya mfanyakazi kupendwa na mwajiri wake. Pia humvuta mke,Mme,hawara ,mchumba unae muitaji utampata kwa dk.30 tu na atatulia na kumfunga asitoke nje ya ndoa, Pia natoa Pete za bahati ambazo zimetajirisha wengi.

Pia ipo dawa ya kupunguza matiti,unene ,tumbo,na kitambi ,hupunguza mafuta ,kuondoa makovu,chunusi,michilizi mwilini na kuongeza hipsi, makalio na mguu wa bia nk. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na DR,HOSUTWA .Anapatikana Mbagara

Simu no, 0756241666 na 0672186977.

       Huduma hii utaipata popote ulipo

Spika Ndugai, Tundu Lissu Waendelea Kunyukana Kwa Maneno....Hatima ya Ubunge Wa Lissu Kujulikana Baada ya Siku 7

$
0
0
Hatma ya ubunge wa Tundu Lissu itajulikana kuanzia Januari 29 wakati Job Ndugai atakapovaa “joho” la uspika kuongoza Mkutano wa 14 wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Ndugai amemtaka Lissu arejee nyumbani kuendelea na majukumu yake ya kuwawakilisha wananchi wa Singida Mashariki, akisema hana kibali baada ya mbunge huyo kutoa tamko mwishoni mwa wiki akituhumu kuwepo na mpango wa kumvua ubunge.

Lissu yuko nchini Ubelgiji kumalizia matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa ndani ya gari, nje ya makazi yake Area D mjini Dodoma, ikiwa ni saa chache baada ya kuhudhuria kikao cha Bunge.

Baada ya shambulio hilo la Septemba 7, mwaka juzi alipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kusafirishwa kwa ndege kwenda Nairobi, Kenya usiku wa siku hiyo.

Mkutano huo wa 14 wa Bunge la Kumi na Moja utaanza Januari 29, siku saba kuanzia leo, pamoja na mambo mengine unatarajiwa kupokea ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), aliyehojiwa jana na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.

Majibizano kati ya Lissu na Spika Ndugai yamekuwa yakipamba moto siku hadi siku tangu alipotoa waraka alioupa jina la “Baada ya Risasi Kushindwa, Sasa Wanataka Kunivua Ubunge”. Katika waraka huo, Lissu anatuhumu uongozi wa Bunge na Serikali kuandaa mpango huo, jambo ambalo Ndugai amesema “ni uzushi”.

Akiongea katika Mahojiano na Gazeti la Mwananchi jana, Spika Ndugai alisema ; “Alipopata matatizo wote tulishuhudia na Bunge lilitimiza wajibu wake katika zile saa chache ambazo ni muhimu katika kuokoa maisha yake. Na hilo lilifanikiwa. Tunatambua kwamba mwenzetu aliumizwa na alikuwa hospitalini.

“Ila sasa hivi tunavyoongea ametoka hospitali yuko huko aliko. Inaelekea ameruhusiwa. Amekuwa akitumia mwanya huo kuzunguka na kuchafua sifa ya nchi yetu. Kwani nani amempa ruhusa?

“Sasa nimwambie tu kwamba sisi tunamuhitaji maana mpaka sasa hajawahi kuniandikia chochote mimi kama kiongozi wake bungeni na wala daktari wake hajasema kitu. Kwa maana hiyo, mimi namuhesabu kama ni mtoro.”

Alipoulizwa sababu za muhimili huo kushindwa kumuhudumia Lissu licha ya familia yake kuandika barua mara nne, Ndugai alijibu kwa kifupi: “Hayo ya nyuma tuyaache. Atakapokuja mwenyewe tutayazungumza.”

Lakini Lissu, ambaye alihojiwa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC) katika kipindi cha Hard Talk kilichorushwa jana alikuwa na majibu ya hoja za Spika.

Alisema kama Spika anataka kujua vizuri hali yake, hahitaji kwenda Ubelgiji bali wapo madaktari ambao Ndugai aliahidi kuwapeleka Nairobi kumuona, lakini hajafanya hivyo.

“(Madaktari) Wakifika Ubelgiji, hawahitaji hata kuzungumza na mimi, wataonana na madaktari wangu na kuzungumza hali yangu na hapo Spika atakuwa na nafasi ya kusema nimepona au la,” alisema mwanasheria huyo.

“Mimi niliumizwa mguu na kiunoni, sikupigwa risasi kichwani, kwa hiyo naweza kuzungumza. Nilikwenda BBC nikitokea hospitalini na nikarudi hospitalini mpaka sasa. Kwa hiyo asiseme nimepona wakati yeye si daktari,”alisema Lissu.

Credit: Mwananchi

Je Unaupungufu Wa Nguvu Za Kiume au Maumbile Mafupi na Membamba...Suluhu iko hapa

$
0
0
Acha kusubilia mpaka mke au mpenzi wako akwambie Mme wangu wewe ni dhaifu tuwepo kitandani,unatakiwa ujitambue mapema ,kwa mwanaume aliyekamilika  na mwenye nguvu za kutosha  ili kumridhisha mke au mpenzi wake anatakiwa awe na uwezo wa kurudia zaidi ya Mara mbili lakini kama unakomea moja au mbili hapo ujue umejilidhisha wewe tu sio na yeye, ili uwe mwanaume mwenye uwezo kamili tumia dawa yako hii hapa

 SUPER MAJINJAS MIX; dawa hii ni tofauti na ambazo uliwai kutumia inamichanganyo ya miti na matunda zaidi ya saba ndio maana inakupa uwezo wa ,KURUDIA TENDO ZAIDI YA MARA TATU,NA ITAKUFANYA UCHELEWE KUFIKA KILELENI DAKIKA 10-15 KWA TENDO LA KWANZA,NA PIA HUIMALISHA MISULI ILIYOLEGEA NA KUSINYAA KWA WALE AMBAO WALIPIGA SANA PUNYETO,dawa hii ni ya vidonge na unga na haina madhara yoyote

MAKAKANUA NO 5 MPYA; dawa hii uboresha uume saizi upendayo UREFU WA INCHI 5,6,7,NA 8 NA UPANA WA CM 2,3,4 NA 5 dawa hii ipo ya kunywa na kupaka  na pia usahidia zaidi kwa mwanaume aliyefanyia tohara ukubwani,

ISENYE NO 3; hii ni dawa kwa wenye kisukari dozi siku 21 tatizo la kisukari na ndio chazo kikubwa cha kuishia nguvu za kiume,

NGWALUSA ; hii ni dawa ya uzazi ambayo ufungua milija ya uzazi ata kwa wale walifungwa uzazi,zipo dawa za busha,vidonda vya tumbo,miguu au viungo kufa gazi kupungza kitambi,minyama uzembe,na matiti makubwa 

TUNAPATIKANA DARES SALAAMU buguruni na MOROGORO YUPO WAKALA na MWANZA YUPO MTAA WA BIZA C, NA KAHAMA MJINI kwa mawasiliano zaidi piga simu 0744040721, 0683645920 DR BRUNO pia unaweza ukaletewa popote ulipo

Super Mkongo: Kiboko ya Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
********************************
SUPER MKONGO MPYA,
_______________________________
********************************
Ni dawa bora ya kutibu na kumaliza matatizo yote ya nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile,

- kuwahi kufika kileleni dakika moja ushakojoa
- maumbile kusinyaa na kulegea wakati wa tendo
- kukosa hamu ya tendo la ndoa
- kushindwa kurudia tendo la ndoa
- uume kusimama kwa kulegea
- uume kulegea katikati ya tendo
- kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu
- kuishiwa nguvu kutokana na punyeto.

Epuka aibu hii leo kwa kutumia SUPER MCONGO MPYA, kiboko ya matatizo haya.
_______________________________
Pia kuna MCONGO POWER Kiboko ya uume mdogo inaboresha maumbile ya uume kwa kurefusha na kunenepesha kwa saizi uipendayo haijalishi umri hata kwa walioathirika na upigaji punyeto.
_______________________________
Kwanza fahamu sababu zinazopelekea kuwa na upungufu wa nguvu za kiume na uume mdogo.
_______________________________
(1) kujichua (punyeto) kwa muda mrefu maana hupelekea misuli ya uume kulegea.
(2) ngiri
(3) kuugua chango la uzazi kwa muda mrefu.
(4) kupungukiwa hormone za testosterone.
(5) ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho  vya kutosha.
(6) kutokufanya mazoezi na mwenendo wa maisha.
(7) kisukari.
(8) tumbo kuunguruma na kujaa gesi.
(9) maumivu ya kiuno nk.
_______________________________
Kwanini uhangaike? Kwanini uhuzunike?
Hii ni spesho kwa waliotumia madawa mengi bila kufanikiwa hakika hautajuta kuitumia. _______________________________
WASILIANA NA:
DR. MCONGOMANI
SIMU NO:
📞0658816558
📞0682323682
Popote ulipo huduma hii inakufikia
_______________________________
********************************

Mtumishi wa TANROADS kizimbani kwa tuhuma za Rushwa

$
0
0
Na Emanuel Madafa, Mbeya
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Mkoa wa Mbeya, imemfikisha Mahakamani mtumishi wa Wakala wa Barabarani(TANROADS) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya shilingi 597,000.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Kiyano, alisema mtumishi huyo akiwa msimamizi wa mzani wa kupima magari uliopo eneo la Uyole Jijini Mbeya, alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mtumishi wa Kampuni ya Kichina iitwayo Chongqing Foreign Trade Economic Corporation.

Alisema Kesi hiyo namba CC. 189/ 2018 imefunguliwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya, chini ya kifungu cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 dhidi ya mtumishi huyo wa umma Zabron Zebeda Kenan.

Alieeleza kuwa mtumishi huyo wa Kampuni ya Kichina, Onesphory Ngonyani, inasemekana alitoa kiasi hicho cha fedha ili gari aina ya Howo lenye namba za usajili T 755BZC na Tela namba T587BPY lililokuwa halina kibali cha mzigo wenye upana usio wa kawaida(Abnomal Wide Loard) lipite kwenye mzani huo bila ya kukamatwa.

Aidha,Mkuu huyo alisema , Taasisi hiyo inaendelea kumtafuta mtumishi wa Kampuni ya Kichina, Onesphory Ngonyani kwani alifanikiwa kutoroka baada ya kutoa hongo hiyo, huku gari yake aina ya Toyota Carina lenye namba  T108 BQH likishikiliwa na ofisi hiyo ya TAKUKURU.

"Baada ya kutoa fedha hiyo Ngonyani alitoweka na kukimbilia Mahali pasipo julikana ambapo tulifanikiwa kumamata gari anayo tumia hivyo tunamtaka afike na achukue gari lake "Alisema Kiyabo.

Hata hivyo, alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa gari hiyo, iliponunuliwa haikubadilishwa umiliki wake hivyo kuna fedha ya serikali inatakiwa kulipwa kama ada ya kuhamisha umiliki na endapo ataendelea kujificha chombo hicho cha moto kitapigwa mnada ili kufidia gharama za serikali.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Takukuru Mbeya alisema katika roho ya Tatu ya mwaka 2018/2019 taasisi hiyo imeendelea kuchambua mifumo katika utendaji wa serikali ,mashirika ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kuzuia mianya ya rushwa .

Watu Wawili Wapandishwa Kizimbani Kwa Kukutwa na Kilo 14 za Bangi

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam imewapandisha kizimbani watu wawili kwa shtaka la kukutwa
na dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa kilo 14.07.
 
Waliopandisha kizimbani ni Musa Amos (19) mkazi wa Tandale Sokoni na Anas Swalehe (18) mkazi wa Magomeni Kagera.
 
Wakisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa, Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Grace Lwila, alidai Novemba 26 mwaka jana, eneo la Tandale kwa Mtogole, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, washtakiwa walikutwa na dawa hizo huku wakijua ni kinyume cha sheria.
 
Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo na Hakimu Kiliwa alisema dhamana iko wazi kwa wadhamini kutoa bondi ya Sh 100,000 kwa kila mmoja.
 
Hata hivyo walishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yao itakaposomwa tena Januari 30.

Jeshi la Polisi Lazungumzia Ma RPC Watatu Waliotumbuliwa na Waziri Lugola

$
0
0
Msemaji wa Jeshi la  polisi, DCP Ahmed Msangi, amesema suala la makamanda watatu wa polisi ambao Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, alitangaza kuwavua nyadhifa zao lipo mezani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, likisubiri utatuzi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Msangi alisema kwa nafasi yake hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa tayari liko mezani kwa IGP ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kulizungumzia na kulisimamia.
 
“Mimi nikiwa msemaji wa polisi siwezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa liko mezani kwa IGP,” alisema alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa agizo la Lugola.
 
Wiki iliyopita, Lugola alitangaza kutengua uteuzi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Ilala, Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi. 

Licha ya agizo hilo la Lugola, makamanda hao waliendela kubaki ofisini.
 
Siku chache baadaye Lugola alipoulizwa juu ya agizo lake kutotekelezwa, alisema: “Sina taarifa kwamba agizo langu halijatekelezwa, lakini nilimpa IGP muda wa utekelezaji, kwa hiyo naamini litatekelezwa. Saa nyingine watu hawajui kutengua mtu ni mamlaka, na mimi ninayo. Utekelezaji unaendelea.” 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images