Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Bodi ya mikopo ya wanafunzi yatangaza utaratibu mpya wa Kulipa Mikopo

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, HESLB imekuja na mfumo mpya wa kielektoniki wa ulipaji madeni ya waliyokuwa wanufaika wa mikopo, ambapo mfumo huo utajulikana kwa jina la 'Goverment Electronic Payment Getway' (GEGP).

Akitagaza mfumo huo, Mkurugenzi wa bodi ya mikopo nchini, Abdulrazack Badru amesema mfumo utarahisisha uwazi wa kwenye ukusanyaji wa fedha hizo, utamfanya mdaiwa kulipa mahali popote alipo pamoja na kutoa fursa ya kuongezeka kwa mapato ya bodi hiyo.

"Tumekamilisha utaratibu mfumo wa serikali wa kukusanya mapato (GEPG), mwajiri na wanufaika watatakiwa kujiunga kwenye mfumo huu mpya wa GEPG ili kulipa madeni wanayodaiwa na serikali," amesema Badru

Aidha amesema, "waajiri ambao watashindwa kulipa madeni ya wafanyakazi ambao walikuwa ni wanufaika, tutawaanzishia operesheni maalumu ya kupitia maofisini kwao ili kuwabaini wasiolipa mikopo ya bodi".

Akifafanua mfumo huo mpya mtaalamu wa GEPG, Baziri Bajunia  amesema, "mfumo huu umekuwa ukitumika sasa hivi na taasisi nyingi ambazo zinafanya malipo kwa taasisi za serikali, ni utaratibu ambao hata taasisi nyingine za kifedha wanautumia".

BREAKING: Rais Magufuli Asitisha Zoezi La Kuondoa Vijiji Na Vitongoji Vilivyopo Ndani Ya Maeneo Ya Hifadhi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kusitishwa mara moja kwa zoezi la kuviondoa vijiji na vitongoji vinavyodaiwa kuwepo katika maeneo ya hifadhi na amewataka viongozi wa wizara zote zinazohusika kukutana ili kubainisha na kuanza mchakato wa kurasimisha maeneo ya vijiji na vitongoji hivyo.

Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Januari, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangallah, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Bi. Dorothy Mwanyika.

Pamoja na agizo hilo Mhe. Rais Magufuli ametaka viongozi wa wizara husika kubainisha maeneo ya hifadhi za wanyamapori na misitu ambayo hayana wanyamapori ama misitu ili yagawiwe kwa wafugaji na wakulima ambao kwa sasa wanataabika kupata maeneo ya kufugia wanyama na kuzalisha mazao.

Mhe. Rais Magufuli pia ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia upya zoezi la uwekaji wa mipaka ya hifadhi na makazi, na kutumia busara katika uwekaji wa mawe ya mipaka hiyo ili kutowaondoa wananchi katika maeneo ambayo hayana ulazima wa kuwaondoa.

“Mimi sifurahii kuona wafugaji kila mahali wanafukuzwa, kama kuna eneo ambalo tunafikiri lilikuwa hifadhi ya wanyama lakini halitumiki, tutabadilisha sheria, tunalimega na tunaligawa kwa wafugaji, vivyo hivyo hata kwa wakulima kama kuna eneo tunaona ni hifadhi lakini halina msitu wala wanyamapori, na lina rutuba, na wakulima wanataka kulima nalo tunalimega tunawapa wakulima.

Baadaye tutajua kabisa eneo hili ni la hifadhi, hili ni la mifugo, hili ni la wakulima, hili ni la makazi. Kwa hiyo nyinyi Mawaziri na Makatibu Wakuu mkakae mkatangulize maslahi ya hawa tunaowaongoza ambao ni wakulima, wafugaji, wavuvi nakadhalika, lakini pia tunahitaji wanyamapori, sijasema sasa hifadhi zote za wanyama tunazimaliza, hapana, hifadhi za wanyama lazima tuzihifadhi” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ameagiza vijiji vyote 366 vilivyoainishwa kuwepo ndani ya maeneo ya hifadhi hapa nchini visiondolewe katika maeneo hayo na badala yake ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa wizara zote zinazohusika kubainisha maeneo ya vijiji hivyo na kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya sheria ili yawasilishwe katika kikao kijacho cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amefafanua kuwa ni lazima Serikali ifanye maamuzi haya sasa kwa kuwa idadi ya Watanzania imeongezeka hadi kufikia Milioni 55, idadi ya mifugo imeongeza hadi kufikia Milioni 35 na hivyo kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya maeneo ya ardhi ikilinganishwa na wakati nchi inapata uhuru ambapo Watanzania walikuwa Milioni 9 na mifugo ilikuwa Milioni 10.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameagiza sheria ya vyanzo vya maji pia iangaliwe upya ili kutowazuia Watanzania wanaozalisha mazao kandokando mwa mito na ameelezea kutofurahishwa kwake na vitendo vya kufyeka mazao ya wakulima kwa madai kuwa wamelima ndani ya mita 60.

Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwasilisha kwake mapendekezo ya kufutwa kwa mashamba ambayo hayajaendelezwa na ameagiza wizara hiyo iendelee kumpelekea mapendekezo ya mashamba yote yaliyotelekezwa ili ayafute na wananchi wagawiwe kwa ajili ya kuyatumia kwa uzalishaji wa mazao na mifugo.

Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli amesema maagizo hayo hayana maana kuwa sasa wananchi waruhusiwe kuvamia maeneo ya hifadhi, na ametaka zoezi la uwekaji wa mipaka lifanyike haraka na kwa uwazi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
15 Januari, 2019 .a

Mtoto Wa Tembo Aliyetumbukia Shimoni Aokolewa Pori La Akiba Lwafi

$
0
0
Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori Tanzania, inapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa mnamo tarehe 11/01/2019 majira ya saa kumi kamili jioni (10:00) Ungozi wa Pori la Akiba Lwafi Mkoani Katavi walipokea taarifa kutoka kwa Bw.Salum Summy ambaye ni  mmiliki wa shamba la Msipazi linalopakana na pori hilo kuhusu kunasa kwa mtoto wa tembo kwenye tope  aliyetumbukia ndani ya chimo eneo la china ndani ya pori hilo.

Bw. Salum alipata taarifa hizo kutoka kwa wafanyakazi wake waliyokuwa jirani baada ya kusikia tembo wakipiga kelele kwa sauti zaidi ya saa moja, na baada ya kufuatilia wakaona kundi kubwa la tembo wakijitahidi kumtoa mtoto wao kwenye shimo. Kwa vile tembo walikuwa wengi watu hao hawakuweza kuwasogelea, hivyo waliamua kuwasiliana na uongozi wa Pori la Lwafi kuhusu tukio hilo . Waliwasiliana na  Mkuu wa Kanda ya Lwafi Bw. Asubuhi T. Kasunga,na kumueleza taarifa hiyo, Bw. Asubuhi bila kuchelewa aliondoka akiongozana na askari  4 wakiwa na siraha na mahema kuelekea eneo la tukio, walifika majira ya saa 5:00 usiku na kupata taarifa ya awali toka kwa mashuhuda  wa tukio hilo,

 Kwa vile ilikuwa usiku sana  na kuhofia kuwepo kwa tembo wengine jirani  walisubiri hadi kupambazuke hadi tarehe 12/1/2019 majira ya saa 12:00 asubuhi walifuatana na wafanyakazi wa shamba pamoja na  wanakijiji jumla walikuwa 11 walifika  eneo la tukio na kumkuta mtoto wa tembo mwenye umri chini ya wa mwaka mmoja  akiangaika kutoka shimoni. Jitihada za kumuokoa zilifanyika baada ya kupanga mawe ndani ya shimo bila kumdhuru mtoto,na hatimaye walimtoa mtoto.

Baada ya kumtoa walimpelea hadi kambi ya Shamba la Msipazi. Waliwahoji wafanyakazi kujua  tembo wanaonekana muda gani kusudi waweze kumrudisha mtoto kwenye kundi, walidai kawaida wanapita majira ya saa nne usiku walisubiri siku nzima hadi muda huo lakini  hawakuonekana.  Tembo hao.

Muda wote  walikuwa wakiwasiliana na Dakitari wa tiba za wanyamapori toka Shirika la Uhifadhi liitwalo (Wildlife Conservation Society-WCS) Bi. Elizabert Stigmaier  kutoa ushauri wa chakula cha kumlisha mtoto huyo maana alionekana amechoka. Wakaelezwa wampatie Glucose aina ya DNS na aliwaeleza jinsi ya kumpa ilia pate nguvu.

Tarehe 13/1/2019  Ofisi yangu iliwasiliana na wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa wanyamapori (TAWIRI ). Idara ya wanyamapori,na WCS na kufikia uamuzi wa  tumsafirishe kwa ndege ya kampuni ya Northen Air Transport No. 5G-DEB  ambayo ilitolewa na Rusell Hastings wa Shirika la Uhifadhi liitwalo ‘ Freidkin Conservation’ hadi Arusha majira ya saa 10: 00 jioni na kupelekwa kwenye kituo cha kupokea Wanyamapori yatima kiitwacho ‘ Makoa farm Vertinary Clinic’ iliyopo Machame Wilaya ya Hai.Mtoto huyo wa tembo anaendelea vizuri.

LIMETOLEWA NA
Dkt. JAMES WAKIBARA  (KAMISHNA MHIFADHI-TAWA)

Mahakama ya ICC Yamwachia huru Gbagbo

$
0
0
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), imemwachia huru rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake.

Gbagbo alifikishwa mbele ya mahakama hiyo mwaka 2011 kutokana na vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambao ulishuhudia akishindwa mbele ya mpinzani wake, Alassane Ouattara.

Katika uamuzi wao, majaji wa ICC, waliamuru Rais Gbagbo kuachiwa huru kwa kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha shitaka hata moja kati ya yale aliyoshitakiwa mbele ya mahakama hiyo.
Gbagbo alishitakiwa kwa madai ya kuhusika na vurugu zilizosababisha mauaji ya watu 3,000 huku wengine 500,000 wakiyakimbia makazi yao.

Kwa mujibu wa rekodi za ICC, Gbagbo ni kiongozi mkuu wa kwanza wa zamani wa nchi kupandishwa mbele ya mahakama hiyo. Kukamatwa kwake kulitekelezwa na vikosi vilivyokuwa vikiungwa mkono na Umoja wa Mataifa (UN) na Ufaransa.

Mbali na Gbagbo, mke wake Simone Gbagbo, naye alitiwa hatiani na mahakama za nchi hiyo kwa kuhusika na makossa mbalimbali ikiwemo kuratibu makundi ya ujambazi.

Serikali ya Ivory Coast ilikataa kumkabidhi Simone kwa ICC ikisema itamshitaki na kumhukumu katika mahakama za ndani.

Alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa makossa mbalimbali ikiwamo ya uvunjifu wa sheria za nchi, kuvuruga usalama wa nchi na makossa dhidi ya ubinadamu.
Simone alinufaika na msamaha wa Rais Ouattara mwaka jana ambaye alisema ameamua kumsamehe ili kufungua milango ya majadiliano na maridhiano kwa mustakbali wa taifa hilo linaloongoza kwa kilimo cha kakao duniani.

BREAKING: Kenya Yashambuliwa Tena na Magaidi

$
0
0
Milipuko na Milio ya risasi vimesikika kwenye eneo la Riverside Nairobi, Kenya ambalo linazungukwa na Ofisi mbalimbali na Hoteli  ya DusitD2 ambapo Citizen TV wametipoti kwamba inahisiwa linaweza kuwa shambulio la Kigaidi.

Mkuu wa polisi wa uchunguzi wa jinai Bw George Kinoti ni miongoni mwa maafisa wakuu wa polisi waliofika kuratibu operesheni ya kuokoa watu waliokwama ndani.

 Tunaendelea kufatilia zaidi.

Maafisa watano wa TFDA kizimbani kwa tuhuma za kuisababishia Mamlaka hiyo hasara ya sh. milioni 58

$
0
0
Maofisa wanne wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la kusababisha hasara ya Sh58,390,000 kwa kuidhinisha malipo mara mbili kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Waliosomewa hati ya mashtaka ni Raymond Wigenge, Ezekiel Mubito, Adelard Mtenga, Abdalah Juma na mshtakiwa wa kwanza, Chary Ugullum ambaye hata hivyo hajafikishwa mahakamani.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Takukuru, Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwezile alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja wanashtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi.

Wakili Swai alidai kuwa kati ya Mei na Desemba mwaka 2016 washtakiwa hao wakiwa katika ofisi ya TFDA kwa uzembe waliisababishia hasara ya kiasi cha Sh58,390,000 kwa kuidhinisha posho maalumu kwa wafanyakazi ambao walishalipwa na kufanya walipwe mara mbili jambo ambalo ni kosa la kisheria.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana shtaka hilo na upande wa Jamhuri walidai kuwa upelelezi umekamilika na waliomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea hoja za awali.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rwezile alisema dhamana kwa washtakiwa hao ipo wazi hivyo wanatakiwa wadhamini wawili wawe na kitambulisho cha Taifa (Nida) na barua za utambulisho.

Pia kati yao mmoja awasilishe fedha taslimu Sh5.8 milioni au hati yenye thamani ya Sh5.8 milioni.

Hata hivyo washtakiwa walishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo wote wamerudishwa mahabusu.

Hakimu Rwezile aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 28, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali.

Naibu Waziri Masauni Ayaonya Makampuni Binafsi Ya Ulinzi Kujihusisha Na Uhalifu

$
0
0
Serikali imeziasa Kampuni Binafsi za Ulinzi kutoshiriki katika matukio ya uhalifu baada ya kuripotiwa mara kwa mara kwa walinzi wa kampuni hizo kupatikana na hatia ya uhalifu katika mahala pao pa kazi ikiwemo kuwaazima silaha wahalifu kwenda kufanya matukio ya uhalifu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania (TSIA), uliofanyika leo jijini Dodoma.

Amesema kampuni zinatakiwa kuongea na walinzi wao sambamba na kuongeza maslahi kwa walinzi hao ili wasiingie katika vishawishi hali itakayopelekea kutoshiriki katika matukio ya uhalifu sehemu zao za kazi.

“Baadhi ya walinzi wa kampuni mnazozisimamia wamekua wakishiriki katika uhalifu, wengine wameenda mbali zaidi kwa kuwaazima silaha wahalifu kwenda kufanyia uhalifu, jambo hili halikubaliki, sasa naziagiza kampuni zenye walinzi wa namna hii kuhakikisha vitendo hivi vinakoma mara moja,” alisema Masauni

Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Narcis Misama alisema wao kama jeshi wanawahakikishia wanachama hao wa sekta ya ulinzi ushirikiano utakaowasaidia kutimiza majukumu yao huku akiweka wazi jeshi kama jeshi haliwezi kuyafikia maeneo yote kwa wakati

“Nawashukuru sana kwani mmekua msaada muhimu kwa jeshi la polisi hasa pale uhalifu unapotokea maeneo mnayolinda, tumeweza kuwapata watuhumiwa wa matukio mbalimbali kupitia taarifa zenu pindi tu uhalifu unapotokea, nawaahidi ushirikiano kwa siku zijazo  zaidi ya mnaoupata kutoka kwa jeshi,” alisema SACP Misama

Akizungumza kwa niaba ya wanachama Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania, Felix Kagisa aliiomba serikali ipitishe sharia zinazoongoza sekta ya ulinzi binafsi ili waweze kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na taratibu  za nchi.

TFDA yaimarisha udhibiti wa bidhaa katika vituo vya forodha

$
0
0
NA WAMJW-ARUSHA
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kaskazini imeeleza kuwa, itaendelea kulinda soko la ndani la bidhaa za vyakula ,dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa kuimarisha huduma kwenye mipaka yote nchini ikiwemo mpaka wa Namanga, Mkoani Arusha.

Udhibiti katika mipaka hiyo ni unalenga kuhakikisha kuwa bidhaa bora, salama na zenye ufanisi pekee ndiyo zinaingia nchini ili kulinda afya ya wananchi.

Hayo yamebainishwa katika kituo cha TFDA kilichopo Mpaka wa Namanga mkoani hapa wakati wa Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo walipotembelea Kituo hicho cha ukaguzi ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Maafisa ukaguzi wa Mpaka wa Namanga ambao unatenganisha nchi za Tanzania na Kenya walieleza mikakati ya utoaji wa huduma za ukaguzi kutokana na Serikali kuwekeza rasimali watu pamoja vitendea kazi katika kurahisisha utoaji wa huduma katika Mpaka huo.

Kaimu Meneja TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John amesema ofisi ya Kanda imeendelea kutekeleza majukumu yake mbalimbali ikiwemo udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa vipodozi, vifaa Tiba na vitendanishi kwa kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata kanuni na sheria zilizowekwa katika kuhakikisha wanalinda maslahi mapana ya kulinda afya ya wananchi.

“Udhibiti wa bidhaa zinazoingia nchini umeongezeka kwa wafanyabiashara kulipa ada na tozo za Serikali na hivyo kuongeza pato la Taifa” alisema Kaimu Meneja huyo.

Nae Mkaguzi wa Dawa wa TFDA Mpaka wa Namanga, Bw. Elia Nyeura amesema takwimu za uingizaji wa mizigo katika kituo cha Namanga zimeongezeka kutoka shehena 724 mwaka 2015/16 hadi kufikia 1,223 kwa mwaka 2016/2018.

“Kwa sera ya awamu ya tano ya kuwa na Tanzania ya viwanda, bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA na kuruhusiwa kwenda nje ya nchi hususani zilizosindikwa kwa kipindi cha miaka mitatu zimeongezeka kutoka shehena 429 hadi kufikia 640 kwa 2017/18 ” amesema Nyeura na kuongeza kuwa, mamlaka imepunguza upotevu wa mapato kutokana na bidhaa zisizofaa kwa kuimarisha ukaguzi”. Alisema.

Hata hivyo amebainisha kuwa thamani ya bidhaa zilizokamatwa kwa kuingizwa nchini bila kufuata utaratibu zimepungua kutoka Milioni 630.3 hadi kufikia Milioni 24.7 kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018.

Aidha, maafisa Uhusiano hao wameweza kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho ikiwemo chumba maalum cha Maabara na kujionea namna bidhaa za dawa zinavyochunguzwa katika kuangalia ubora wake kabla hazijaingizwa Nchini.

Mpaka wa Namanga ni moja ya mipaka ambayo tayari imeanza kufanya kazi kwa kufanya ukaguzi wa bidhaa kwa upande mmoja tu wa Nchi (One Stop Boder Post-OSBP) ambapo bidhaa inaingia na kukaguliwa kwa pamoja na wakaguzi wa nchi mbili (Tanzania na Kenya) ili kupunguza muda wa wadau kukaa mpakani kwa muda mrefu kwa ukaguzi.

Dereva Aliyepambana na Trafiki Watatu Mahakamani

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoani Songwe limemfikisha mahakamani dereva Mawazo Jairos (29) kwa kosa la kupigana na askari watatu wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
 
Licha ya dereva huyo kufikishwa mahakamani, amelalamikia kitendo cha kung’atwa eneo la shingoni na mgongoni na mmoja wa askari wakati wakipambana naye kwa madai alishindwa kutii amri bila shuruti.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Yusuf Sarungi jana alisema tukio la dereva na askari hao lilitokea Januari 12, mwaka huu saa 2:30 asubuhi Mtaa wa Transfoma mjini Tunduma.
 
Kamanda Sarungi alisema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la kuzuia askari kufanya kazi yao na shambulio la kudhuru mwili.
 
Alidai siku ya tukio, askari hao walikuwa na maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) ambao walikuwa na operesheni ya ukaguzi wa magari.
 
Kamanda Sarungi alidai katika ukaguzi huo walisimamisha gari lenye namba za usajili T 842 AAC aina ya Mistubishi Fuso, likiendeshwa na Jairos mkazi wa Mbeya.
 
Alisema baada ya kusimamishwa Jairos anadaiwa kutoa lugha chafu za kashfa na matusi kwa askari na maofisa wa Sumatra.
 
Alidai kuwa dereva huyo akiwa kwenye njia ya vumbi kutoka eneo la Mwaka kwenda Songea, aliondoa gari hilo bila kuruhusiwa kitendo kilichowalazimu maofisa hao kulikimbiza na walipofika eneo la Makambini walifanikiwa kumkamata.
 
Kamanda Sarungi alidai kuwa baada ya gari hilo kukamatwa, Jairos alishuka akiwa amehamaki na kuanza kutoa lugha za matusi kwa maofisa.
 
Alidai kuwa dereva huyo ghafla alianza kuwashambulia askari, lakini wakafanikiwa kumdhibiti.
 
Kamanda Sarungi alidai kuwa dereva huyo alianza kupiga kelele kuwa askari hao wanamuua na wananchi wakajaa na kuwazuia askari wasiendele kumpiga.
 
Alidai kuwa baada ya askari hao kumwachia, alipata upenyo na kuingia katika gari, kisha kutoka na panga akaanza kuwatishia baadaye alifanikiwa kuondoka na gari hilo kabla ya kukamatwa katika mji wa Vwawa wilayani Mbozi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya January 16

Tanzania Kunufaika Mkataba Mpya na Airtel....Kila Mwezi Kulipwa Bilioni 1 Kwa Miaka Mitano

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 15 Januari, 2019 ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel ya India juu ya umiliki wa hisa za kampuni Airtel Tanzania na maslahi mengine ya Tanzania kutokana na biashara ya kampuni hiyo.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ametia saini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunil Mittal ametia saini kwa niaba ya kampuni ya Bharti Aitel.

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi amesema katika makubaliano hayo kampuni ya Bharti Airtel imekubali kupunguza umiliki wa hisa zake za kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kutoka asilimia 60 hadi 51 na hivyo kuongeza hisa za Serikali kutoka asilimia 40 hadi 49 bila malipo yoyote kutoka Serikalini.

Prof. Kabudi amebainisha maeneo mengine ya makubaliano kuwa ni Serikali kupata gawio la kila mwaka kutokana na umiliki wake wa asilimia 49 ambapo inakadiriwa itakuwa ikipata shilingi Bilioni 10, kufutwa kwa madeni yote ya kampuni ya Airtel yaliyokuwa yamefikia shilingi Trilioni 1, Bharti Airtel itatoa shilingi Bilioni 1 kila mwezi kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia Aprili 2019 ili kuonesha nia njema na Bharti Airtel itatoa shilingi Bilioni 2.3 kwa ajili ya kuchangia huduma za kijamii.

Maeneo mengine ya makubaliano ni Bodi ya Wakurugenzi wa Airtel Tanzania kuundwa na wajumbe 7 ambapo Serikali ya Tanzania itawakilishwa na wajumbe 3 (akiwemo Mwenyekiti atakayeteuliwa na Serikali) na Bharti Airtel itawakilishwa na wajumbe 4, Menejimenti ya Airtel Tanzania itaongozwa na Bharti Airtel lakini Afisa Mkuu wa Ufundi atateuliwa na Serikali ya Tanzania, pande zote mbili zitashirikiana kuandaa upya nyaraka muhimu za kusaidia uendeshaji wa kampuni, pande zote mbili zitashirikiana kuongeza tija na ufanisi wa Airtel Tanzania na pande zote mbili zitashirikiana kutumia miundombinu ya Shirika la Simu Tanzania (TTCL) ikiwa kuna hoja za kibiashara.

Kwa upande wake Bw. Sunil Mittal amesema amefurahishwa na kufikiwa kwa makubaliano katika mazungumzo hayo na amebainisha kuwa awali aliona kuna ugumu wa kufikia makubaliano lakini baadaye alielewa kuwa lengo la Mhe. Rais Magufuli ni kuhakikisha anaweka mwelekeo mzuri wenye manufaa kwa Tanzania.

Bw. Mittal ameongeza kuwa makubaliano hayo yameandika historia mpya kwa hisa nyingi kumilikiwa na Watanzania katika kampuni ya Airtel Tanzania na kwamba anatarajia kuwa Airtel Tanzania itaendelea kufanya vizuri katika soko la Tanzania ambayo ni nchi yenye uwekezaji mkubwa wa Bharti Airtel Barani Afrika.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano hayo Mhe. Rais Magufuli ameipongeza timu iliyoiwakilisha Serikali ya Tanzania chini ya Prof. Kabudi na timu ya Bw. Mittal kwa kufikia makubaliano hayo yaliyochukua muda wa miezi 8 na ameelezea furaha yake kuwa sasa Airtel Tanzania itaanza kutoa manufaa kwa Serikali ikiwemo gawio na maslahi mengine yanayostahili, mambo ambayo hayakufanyika kwa miaka zaidi ya 8 tangu kampuni hiyo ianzishwe hapa nchini.

Amempongeza Bw. Mittal kwa kuridhia kuongeza hisa za Serikali, kutoa shilingi Bilioni 1 kila mwezi kwa miaka 5 na kutoa mchango wa Shilingi Bilioni 2.3 ambazo ameagiza ziungane na shilingi Bilioni 1 iliyotengwa kwa ajili ya sherehe za siku ya Uhuru za mwaka 2018 (na kufanya jumla shilingi Bilioni 3.3) kwenda kujenga hospitali katika makao makuu ya nchi Jijini Dodoma.

“Huu ndio uwekezaji ninaoutaka, uwekezaji ambao tuna faida nao, Airtel ilikuwepo tangu miaka 8, 9 iliyopita lakini tulikuwa hatupati kitu, sasa tutapata fedha, na hili liwe somo kwetu Watanzania wote kuwa Serikali inapotetea maslahi ya Watanzania haizungumzi kutoka hewani, tujifunze kuwaheshimu watalaamu wetu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia Bw. Mittal na wawekezaji wote hapa nchini kuwa Tanzania ni nchi nzuri ya kuwekeza na itadumisha utamaduni wa kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kutambua kuwa uwekezaji huo unasaidia kuzalisha ajira na kuiwezesha Serikali kupata mapato.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
15 Januari, 2019

Aliyekuwa Ofisa Tra Kortini Kujibu Tuhuma Za Kumiliki Mali Za Milioni 720/- Isiyolingana Na Kipato Chake

$
0
0
Aliyekuwa Ofisa Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Godfrey Mapuga amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kumiliki mali ya zaidi ya Sh.milioni 720 ambayo hailingani na kipato chake cha sasa wala cha zamani.

Akisoma hati ya mashtaka jana Januari 19, 2019 ,Wakili wa Serikali Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Vitalis Peter akisaidiana na Lilian William amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Salim Ally kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo  kati ya Aprili Mosi mwaka 2011 na Julia 19,2016 huko wilyani Ubungo mkoani Dar es Salaam.

Imedaiwa mshtakiwa akiwa ameajiriwa kwa nafasi ya Ofisa Msaidizi wa forodha wa TRA alikutwa akimiliki mali isiyolingana na kipato chake ambapo, alikutwa anamiliki nyumba ya gorofa moja yenye thamani ya Sh. 698,921,217, kiwanja ambacho hakijasaliwa kilichopo eneo Mbezi Juu,

Ubungo chenye thamani ya Sh. Milioni 7, Kiwanja kingine ambacho hakijasajiliwa chenye thamani ya Sh. 9,500, 000 kilichopo eneo La Goba.Mali nyingine ni kiwanja ambacho hakijasajiliwa chenye katika eneo la Kigamboni Wilayani Temeke chenye thamani ya Sh.milioni sita.

Imedaiwa kuwa mali yote hiyo ina thamani ya Sh. 721,421,217 mali ambayo hailingani na kipato chake cha sasa wala cha zamani. Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hata hivyo Mahakama imemtaka mshtakiwa kuweka fedha taslimu Sh. 360,710,608 au kuweka mali isiyohamishika yenye thamani ya kiwango hicho cha fedha, pia mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja anatakiwa kusaini bondi ya milioni 360.

Aidha mshtakiwa ametakiwa kuwasilisha hati zake za kusafiri mahakamani hapo na Pia haruhusiwi kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salama bila ya kuwa na kibali.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika na imeahirishwa hadi Januari 29,2018 kwa ajili ya mshtakiwa kuja kusomewa maelezo ya awali (PH).

Vyama 8 vya Upinzani Vyafurahia Kesi ya Zitto Kabwe Kufutwa

$
0
0
Vyama vinane visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimepongeza uamuzi wa Mahakama Kuu kulifuta shauri lililofunguliwa na baadhi ya wanasiasa kupinga Bunge kujadili muswada wa marekebisho wa sheria ya vyama vya siasa wa mwaka 2018.

Tamko la vyama hivyo lililotolewa  jana Jumatatu Januari 15, 2019 limeeleza uamuzi huo wa Mahakama ni mzuri na umetenda haki kwa vyama vya siasa ambavyo vilidai sheria hiyo.

Vilevile vyama hivyo ambavyo ni DP, AAFP, Demokrasia makini, SAU, TLP, UDP, NRA, UMD vimempongeza Spika Job Ndugai kwa kualika kila chama kwa ajili ya kutoa maoni yao kuhusu muswada huo mbele ya kamati.

Akisoma tamko hilo, Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya alisema kwa upande wao maboresho ya sheria hiyo wanayaunga mkono kwa asilimia 100 kwa kile alichodai ndio hitaji lao.

“Spika amefanya jambo jema sana kutuhusisha vyama katika hilo na tutakwenda kupeleka maoni yetu kadri tutakavyoona inafaa,” alisema Mluya.

“Tunaamini kamati iko vizuri itayachambua yote maana tutaeleza hata yale yanayoonekana hayafai,” alisema Mluya.

Mluya alisema suala kubwa ambalo wamelifurahia katika muswada huo ni kuondolewa kwa vikundi vya ulinzi na usalama ndani ya vyama na jukumu hilo kubaki mikononi mwa Serikali.

Naye Katibu Mkuu wa NRA, Hassan Almas aliyeeleza kufurahishwa kwake na kifungu hicho alisema, “Sheria imetutendea haki sisi ambao vyama vyetu havikuwa na uwezo wa kumiliki jeshi au vikundi vya ulinzi. Kuna watu wanajiita makamanda na wana vyeo baada ya kupewa mafunzo ya kijeshi hii ilikuwa hatari.”

“Kwani kuna haja gani ya chama kuwa na jeshi au kikundi cha ulinzi wakati wote tunatakiwa kuwania dola itakayotuwezesha kuongoza majeshi yote. Uchaguzi ukiisha aliyeshinda ndiye anakuwa kiongozi wa majeshi yote yaliyo chini ya Serikali,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa (AAFP) Rashid Rai alisema fursa hiyo waliyopewa na Spika wataitumia vizuri na kushiriki kutoa maoni kuhusu muswada huo.

“Spika amefanya jambo jema sana kutuhusisha vyama katika hilo na tutakwenda kupeleka maoni yetu kadri tutakavyoona inafaa. Tunaamini kamati iko vizuri itayachambua yote maana tutaeleza hata yale yanayoonekana hayafai,”

Bodi ya mikopo yakusanya TZS 94.01 bilioni kati ya Julai – Desemba, 2018

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imekusanya jumla ya TZS 94.01 bilioni kutoka kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu katika kipindi cha Julai – Desemba, 2018 na kuvuka lengo lake la kukusanya TZS 71.4 bilioni katika kipindi hicho.

 Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema jana jijini Dar es salaam kuwa makusanyo hayo yametoka kwa jumla ya wanufaika zaidi 198,659 ambao wamejiari au kuajiriwa katika sekta binafsi na umma.

 Wanufaika waliobainika na kuanza kulipa kati ya Julai – Disemba 2018
 “Katika kipindi hicho cha Julai – Desemba pia tumefanikiwa kuwabaini wanufaika wapya zaidi 12,600 ambao walikua hawajaanza kurejesha mikopo yao na sasa wameanza na hivyo kufanya wateja wanaorejesha kufikia 198,656 hivi sasa,” amesema Badru wakati akiongea na wanahabari katika ofisi za HESLB na kuongeza:

 “Makusanyo haya ya TZS 94.01 bilioni ni sawa na ongezeko la asilimia 8.7 ikilinganishwa na TZS 85.88 bilioni zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka uliopita yaani, Julai – Disemba, 2017,” amesema.

Badru alikua akieleza hali ya ukusanyaji wa mikopo katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha wa 2018/2019 utakaomalizika mwezi Juni mwaka huu ambao lengo kwa mwaka mzima ni kukusanya TZS 150 bilioni.

Kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha HESLB, waajiri wanapaswa kukata asilimia 15 ya mshahara ghafi (basic salary) wa mnufaika na kuwasilisha makato hayo kwa HESLB ndani ya siku 14 baada ya tarehe ya mwisho wa mwezi wa makato.

Kujiunga na GePG
Katika mkutano huo, HESLB pia ilitangaza rasmi kujiunga na Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato yaani (Government e-Payment Gateway - GePG) na kusisitiza kuwa kuanzia sasa, malipo yote kwenda HESLB yatapokelewa kwa mfumo huo unaofuatwa na taasisi mbalimbali za Serikali.

Mwajiri au mnufaika anatakiwa kunakiri ‘Namba ya Kumbukumbu’ Control Number) iliyopo kwenye ankara (Loan Statements) zao na kufanya malipo kwa njia ya benki au simu. Maelezo ya kina yapo kwenye tovuti hii.

Namba za simu kwa wateja wenye maswali
Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza kuwa kuanzia sasa, hakuna malipo yoyote yatakayopokelewa bila kufuata mfumo huo na kwamba wateja wenye maswali wapige kwa namba 0659 748 536; 0621 870 172; 0620 714 421; na 0621 870 173).

HESLB ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2005 ili kutekeleza majukumu makuu mawili. Mosi, kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa kitanzania ambao ni wahitaji na pili kukusanya fedha za mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika waliokopeshwa na Serikali tangu mwaka 1994/1995.

Mwisho.
Jumanne, Januari 15, 2019

Super Mkongo: Kiboko ya Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
********************************
SUPER MKONGO MPYA,
_______________________________
********************************
Ni dawa bora ya kutibu na kumaliza matatizo yote ya nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile,

- kuwahi kufika kileleni dakika moja ushakojoa
- maumbile kusinyaa na kulegea wakati wa tendo
- kukosa hamu ya tendo la ndoa
- kushindwa kurudia tendo la ndoa
- uume kusimama kwa kulegea
- uume kulegea katikati ya tendo
- kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu
- kuishiwa nguvu kutokana na punyeto.

Epuka aibu hii leo kwa kutumia SUPER MCONGO MPYA, kiboko ya matatizo haya.
_______________________________
Pia kuna MCONGO POWER Kiboko ya uume mdogo inaboresha maumbile ya uume kwa kurefusha na kunenepesha kwa saizi uipendayo haijalishi umri hata kwa walioathirika na upigaji punyeto.
_______________________________
Kwanza fahamu sababu zinazopelekea kuwa na upungufu wa nguvu za kiume na uume mdogo.
_______________________________
(1) kujichua (punyeto) kwa muda mrefu maana hupelekea misuli ya uume kulegea.
(2) ngiri
(3) kuugua chango la uzazi kwa muda mrefu.
(4) kupungukiwa hormone za testosterone.
(5) ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho  vya kutosha.
(6) kutokufanya mazoezi na mwenendo wa maisha.
(7) kisukari.
(8) tumbo kuunguruma na kujaa gesi.
(9) maumivu ya kiuno nk.
_______________________________
Kwanini uhangaike? Kwanini uhuzunike?
Hii ni spesho kwa waliotumia madawa mengi bila kufanikiwa hakika hautajuta kuitumia. _______________________________
WASILIANA NA:
DR. MCONGOMANI
SIMU NO:
📞0658816558
📞0682323682
Popote ulipo huduma hii inakufikia
_______________________________
********************************

Dr Hindu: Bingwa Wa Tiba Asili .....Hutibu Matatizo Yafuatayo

$
0
0
NKURURU:-ni dawa inayotibu miguu kuwaka moto, kiuno tumbo kupooza kupoteza fahamu 

MALABALA; hutibu kisukari , uti wa mgogo, Change, pumu, busha, kaswende, kifua kikuu, muwasho sehemu ya siri 

NKURUNGU,: Ni dawa kutibu  N, B, G, POWER :-ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume ni vidonge 20 

MPERAMPERA:- ni dawa ya kurudisha Mke, mme, mpenzi,mchumba aliyekuacha /kuteseka, ni kwa mda wa siku 2 tu kusafisha , pia kuna dawa za kupunguza vitambi(nyama uzembe), maziwa makubwa,michirizi, mikovu makubwa, chunusi sugu. 

NR SIX POWER:-inatibu upungufu wa nguvu za kiume kwa wasio weza kumudu tendo la ndoa itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 4 bila hamu Kuisha, inaboresha maumbile madogo na inaimarisha misuri iliyo legea na kusinyaa una pona kabisa, ndani ya siku 4 tu 

GASELA:-ni dawa ya maajabu (9) yaliyoshindikana. (1)-Kisukari, vidonda vya tumbo, tezi dume,walioshindikanika kupata watoto(ugumba),busha bila oparesheni, (2)zindiko Kali Katika biashara yako (chuma ulete) ndo kiboko yao kumkamata mwizi aliye kuibia vitu vyako pikipiki, gari, n, k( 2)zindiko la nyumba, mashamba, viwanja,.(4)kukutolea sumu uliyo ikanyaga (Mtego) (5)ujiamini kutumia dawa ya maajabu Saba (6)kutoa mikafara mfano ugomvi ndani ya nyumba kufukuzwa kazini bila sababu (7)kutabiri nyota na kung'arisha (8)kurudisha Mali iliyo potea mazingira ya kutatanisha, kushinda kesi uliyo sumbuka nayo mda mrefu. (9)kufukuza majini wachafu ndani ya mji,.

Haya yote yanawezekana kwa DR HINDU popote ulipo . Muone  DR HINDU,anatibu nguvu za kiume anarefusha na kunenepesha uume kwa saizi uipendayo kwa muda mfupi sana, pamoja na kuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa mara 4 bila hamu kuisha Na utachelewa kufika kileleni kwa muda wa dakika 40 bila kuchoka .

Angalizo usitume meseji wala kubipu..
 
You can get it in all East African countries,,our service is fast and easy... contact Whatsapp 0784,47,59,46. Dar es salaam, Mbagala Tanzania. ,..Dr. HINDU 0744,92,29,82 / 0716608959...You are welcome. Yuko pia Khahama Mjini

Mkuu wa Kikosi kazi cha Kupambana na Ujangili Kanda ya Ziwa Adai Kuibiwa Milioni 9 Hotelini

$
0
0
Mkuu wa Kikosi kazi cha Kupambana na Ujangili Kanda ya Ziwa ambaye pia ni Mhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanapa, Richard Shilunga inadaiwa kuwa ameibiwa Shilingi Milioni 9.4 akiwa katika nyumba za kulala wageni Bariadi mkoani Simiyu.

Ilidaiwa kuwa Shilunga aliwasilia kwenye nyumba moja inayofahamika kwa jina la Sumaye 'Lodge' iliyopo katikati ya mji wa Bariadi, Janauri 13, 2019 majira ya saa 10 jioni akitokea Tarangire Mkoani Manyara.

Kwa mujibu wa moja ya chanzo cha taarifa hiyo, kilieleza kwamba Shilunga alifika katika nyumba hiyo, akiwa na begi dogo ambalo linadaiwa kuwa na kiasi hicho cha fedha ambazo bado haijafahamika kama zilikuwa za matumizi ya kitu gani.

Aidha, Shilunga baada ya kuwasili alipewa chumba herufi T, ambacho gharama yake ni Shilingi 20,000, na kuhifadhi begi lake kisha akatoka na kwenda kutazama mchezo wa mpira wa mguu wa ligi Kuu ya Uingereza kati Manchester United na Tottenham.

Baada mchezo huo kuisha, majira ya 2:45 usiku Shilunga alirejea katika nyumba hiyo na kuingia kwenye chumba chake,na baadaye kabla ya kulala aligundua kupotea kwa kiasi hicho cha fedha na kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Bariadi.

Hata hivyo haikujulikana fedha hizo kama zilikuwa mali ya serikali au zake binafsi, huku ikidaiwa kuwa hakuweza kutoa taarifa kwa wahudumu wa nyumba hiyo kama ana kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari  jana ambao walifika katika kituo kikuu cha polisi, baada ya kupata taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Deustedith Nsimeki alikiri kuwepo kwa tukio hilo, na uchunguzi unaendelea.

Kamanda Nsimeki amesema mpaka sasa wanawashikilia watu ambao ni wahudumu wa nyumba hiyo, ambao hata hivyo hakutaka kuwataja majina yao kwa sababubu za kiupelelezi.

“Tukio kweli yupo mtu anaedai kupotelewa na fedha hizo mtumishi wa Tanapa kituo cha Tarangire mkoani Manyara. Bado tunaendelea na uchunguzi ili kubaini kama fedha zilizoibiwa ni mali ya Serikali, Kama tutabaini ni kweli mali ya serikali watamfungulia mashitaka kwa mwendesha mashitaka wa serikali kwa sababu ya uzembe, kuna taratibu za kubeba pesa kiasi kikubwa ziwe za Serikali au mtu binafsi,”alisema Nsimeki.

Amesema kuwa bado wana mashaka juu ya kuibiwa kwa pesa hizo kama ni kweli au hapana, kutokana na taarifa za awali zikieleza kuwa mlalamikaji hakutotoa taarifa za mdomo au maandishi kwa wahudumu kama ana kiasi hicho cha pesa.

Amesema kuwa taarifa za awali zinaeleza kuwa Shilunga alikuja na pesa hizo kwa ajili kuwalipa baadhi ya watu walioko kwenye kikosi kazi maalumu kanda ya ziwa.

“Kwa kawaida pesa za serikali huziendi hivyo wala huwezi kubeba  kwa njia hiyo kuna mifumo yake hata kama ni ulipaji bado kuna mifumo yake, hata fedha binafsi kuna taratibu, lakini huyu hakuna sehemu ambayo ametoa taarifa kama ana kiasi hicho cha fedha,” Nsimeki.

Aidha Kamanda Nsimeki amesema kuwa mbali na kuwashikilia wafanyakazi hao kwa ajili ya uchunguzi, bado kuna wasiwasi kama kweli ameibiwa fedha hizo kutokana na taarifa za awali.

Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Yafutwa

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni amesema Baraza la Taifa la Usalama Barabarani limeifuta wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyokuwa ikifanyika kila mwaka kwa madai imekuwa ikitumia gharama kubwa huku ajali zikiendelea kuwepo.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo Jijini Dodoma wakiwemo wakuu wa vikosi vya Usalama Barabarani wa Mikoa yote bara na Visiwani, ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo amesema baraza limefikia uamuzi huo kutokana na kushindwa kufikia malengo pamoja na kumvua madaraka mwenyekiti wa baraza hilo mkoa wa Mbeya Chacha Mugaka.

Naye mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini, Fortunatus Muslim amesema kutokana na oparesheni nyakuanyakua iliyofanyika kwa madereva wa magari kufanikiwa wanapanga kuihamishia kwa madereva wa bodaboda  na kudai wamekuwa kikwazo kikubwa na kusababisha ajali nchini.

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliamo, Elias Kwandikwa amesema wizara hiyo imejipanga katika kuhakikisha inaondoa changamoto za sekta ya usafiri ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara.

Umoja wa Afrika, Marekani Walaani Shambulio la Al Shabaab Kenya

$
0
0
Mwenyekiti  wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amelaani vikali shambulio lililofanywa katika hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi, Kenya.

Katika taarifa yake, Faki amevisifu vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa kuchukua hatua za kuwahudumia haraka watu walioathirika na tukio hilo na kupambana na wahalifu mapema iwezekanavyo. 

Pia amesema tukio hilo linaonyesha umuhimu wa kupitia upya mipango ya kuongeza nguvu ya kupambana na vikundi vya kigaidi barani Afrika.

“Mwenyekiti wa Tume anathibitisha utayari wa AU kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na nchi wanachama katika kupambana na ugaidi na harakati za kuleta amani nchini Somalia, na kuzidisha mapambano dhidi ya kundi al-Shabaab kupitia vikosi vyake vya AMISOM.

Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake nchini Kenya, Bw Robert Godec, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Marekani inashutumu vikali shambulio hilo.

Amesema maofisa wote wa ubalozi wa Marekani wako salama na kwamba Marekani iko tayari kusaidia iwapo itahitajika kufanya hivyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa raia wake mmoja ni kati ya watu waliopoteza maisha kwenye mkasa huo.

Kuna ripoti kuwa mpaka sasa watu sita wamethibitishwa kupoteza maisha, watano kati yao walifariki wakiwa ndani ya mgahawa mmoja ulio ndani ya viunga hivyo na mwingine alipoteza maisha baada ya kufikishwa hospitali.

Bado idadi rasmi ya watu waliofariki haijatolewa na mamlaka husika, hata hivyo, mfanyakazi mmoja wa chumba cha  kuhifadhi maiti jijini humo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa kuna miili 15 iliyohifadhiwa kutokana na shambulio hilo.

Kundi la al-Shabab ambalo linadai kutekeleza shambulio hilo limetoa taarifa kuwa watu 47 wameuawa.

Wakenya Wakerwa na Gazeti la New York Times kwa Kuchapisha Picha za Maiti Waliouawa na Alshabaab Jana

$
0
0
Gazeti la New York Times limeshutumiwa vikali na Wakenya  kwa kuchapisha picha za miili ya watu waliopoteza maisha katika shambulio la hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi.

Wahalifu wenye silaha za moto na mabomu walivamia viunga vya hoteli hiyo jana Jumanne saa 9 alasiri.

Gazeti hilo lenye makao makuu yake nchini Marekani limechapisha picha za marehemu wakionekana dhairi kuwa na matundu ya risasi kwenye miili yao na kulowa damu.
 
Baada ya shutuma hizo kushika kasi, uongozi wa gazeti hilo ulitoa taarifa ya kujitetea wakisema lengo lao ni "kuonesha uhalisia wa tukio zima japo picha zinaweza kuwa za kuogofya."

Maelezo hayo pia yamepingwa, huku Mhariri wa Biashara wa BBC kanda ya Afrika, Larry Madowo akilitaka gazeti hilo kuonesha mifano ya picha za marehemu walizozichapisha kwenye shambulio lolote lililotokea nchini Marekani.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images