Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

LIVE: Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar

0
0
LEO ni kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, maadhimisho hayo yanafanyika katika uwanja wa Gombani Pemba.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein.

Tazama hapo chini

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Tiba Asilia ya Tatizo la Nguvu za Kiume

0
0
Kifaru vidonge asilia hurefusha maumbile ya kiume nchi 6-8 dk 60 garantii mika 30- 40 .itakupa nahamu ya kufanya tendo la ndoa mara 4- 5 bila kuchoka au hamu kuisha, ina imalisha misuri  ya uume  na haina madhara kwa mtuaji

Malelemba; inatibu presha kisukari, ngili, busha bila uperesheni, kiuno, kutopata choo vizuri, vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto, kisosono

Jirumba; kumvuta mume mke mpenzi mchumba kwa masaa 3 yoyote unae mtaka  uta mpata ..acha kuumiza roho bure hatakama una fanya nae kazi sehemu moja ila unaogopa kumuanza au muone mzee jirumba atakusaidia

Fika mbagara kwa wa mikoani shinyanga kahama mwanza kwa mawasiano piga 0713560943 /0762540447 dr jirumba

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Wimbo Mpya wa Enock Bella - I Swear

0
0
Wimbo Mpya wa   Enock Bella - I Swear

Video Mpya:ngel GoodLuck - NISHIKE

0
0
Video Mpya:ngel GoodLuck - NISHIKE

Wanafunzi 30 Wanusurika Kifo Dereva Akichat na Simu

0
0
Jumla ya wanafunzi 30 wa shule ya msingi binafsi ya Little Treasure, iliyoko Manispaa ya Shinyanga, wamenusurika kifo baada ya kupata ajali wakirejea nyumbani kuto shule.

Chanzo cha ajali ni dereva wa basi hilo, Emmanuel Faustine (32), ambaye alikuwa akichati na simu ya mkononi huku akiendesha, Januari 10 majira ya ya saa 9 alasiri katika eneo la Kalogo mjini humo.

Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, Kamishina Msaidizi (ACP) Simon Haule, amesema wanafunzi 30 walikuwa wamesalia kwenye basi hilo na hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya kupata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva ambaye alikuwa akichati na simu wakati akiendesha hatua ambayo ilisababisha kutumbukia mtaroni na kusababisha ajali na mwenyewe kukimbilia kusikojulikana.

“Jeshi la Polisi linamsaka dereva wa basi hili ambaye alikimbia mara baada ya kusababisha ajali, ili achukuliwe hatua kali za kisheria na liwe fundisho kwa madereva wengine ambao wamekuwa wakisababisha ajali za lazima na kugharimu maisha ya watu pamoja na kuwapatia ulemavu”, amesema Haule.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa, Dk. Albert Masigati amesema alipokea wanafunzi 30 na baada ya kuwapatia matibabu, 26 waliruhusiwa na kubakia wanne wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Aliyedaiwa kuiba Sh mil saba kila dakika Asomewa Mashitaka Mapya 39

0
0
Mfanyabiashara aliyedaiwa kuiibia Serikali Sh milioni saba kwa kila dakika moja, Mohamed Yusufali na wenzake wanne walifutiwa kesi hiyo iliyowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kisha wakakamatwa tena jana na kusomewa upya mashtaka 39 likiwamo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni mbili.

Washtakiwa hao walifutiwa kesi hiyo  baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuomba kuondoa shtaka hilo mahakamani hapo na hawana nia ya kuendelea nalo.

Maombi hayo yaliwasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Hashimu Ngole, kisha mahakama hiyo ikayakubali na washtakiwa wakafutiwa mashtaka yao yaliyowakabili.

Washtakiwa hao walifutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Ngole alidai mahakamani hapo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini DPP hana nia ya kuendelea nalo dhidi ya washtakiwa hao.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Augustina Mmbando, alisema shauri hilo lilikuja chini ya kifungu namba 91(1) cha CPA, sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 ila kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo.

Hata hivyo, baada ya Hakimu Mmbando kufuta kesi hiyo, washtakiwa hao  walikamatwa tena na kuwekwa mahabusu na kisha baadaye kupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka 39.

Mbali na Yusufali, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Alloyscious Mandago, Isaack Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif.

Wakili Ngole akisoma hati ya mashtaka hayo mapya mbele ya Hakimu Mmbando, alidai kuwa kati ya Machi 2, 2010 na Aprili 26, 2016 katika maeneo tofauti ndani ya Dar es Salaam, washtakiwa hao walikula njama kwa kughushi, kukwepa kulipa kodi na kutakatisha fedha.

Katika shtaka la pili linalomkabili mshtakiwa wa tatu Kasaga, Wakili Ngole alidai kuwa kati ya Mei 9, katika ofisi za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) zilizoko Manispaa ya Ilala, aliwasilisha nyaraka za uongo yenye fomu namba 128 ya Mei 2, 2016 akionyesha kuwa Machi 4, 2012 wakurugenzi wa Kampuni ya Superior Financing Solution Limited ni Yusufali, Kassanga na Maria.

Katika shtaka jingine la utakatishaji fedha kinyume na sheria linalowakabili washtakiwa wote,  inadaiwa kati ya Machi 4, 2011 na Aprili 13, 2016 katika maeneo tofauti ndani ya Dar es Salaam akiwa mmiliki na mkurugenzi wa kampuni hiyo walijihusisha na muamala wa kiasi cha Sh 2,967,959,554 wakijua fedha hizo zinatokana na zao la fedha haramu.

Baada yakusomewa mashtaka hayo, Ngole, alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na wanaandaa maelezo ya mashahidi kwa ajili ya kupelekwa Mahakama Kuu.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote, Hakimu Mmbando, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 24, mwaka huu.

Lugola awashukia wanaoponda ujio wa ndege mpya

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuwa ujio wa ndege mpya za kisasa utaongeza hali ya amani na usalama katika viwanja vya ndege kwa kuimarisha mifumo mbalimbali ya usalama.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam jana mara baada ya kuwasili kwa ndege mpya, ambapo amesema kuwa ujio wa ndege hizo utaimarisha huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya nchi, kitu ambacho kilikosekana kwa muda mrefu.

”Ujio wa ndege hizi kwanza kabisa utakuwa kivutio kwa watalii, ambapo naimani kabisa idadi yao itaongezeka baada ya kuwa na usafiri wenye uhakika, hivyo kulingana na ongezeko hilo, tutaweza kuongeza uimarishaji maradufu wa usalama katika viwanja vya ndege,”amesema Lugola

Hata hivyo, Lugola amewataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu ambao wamekuwa wakibeza jitihada za rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuiletea nchi maendeleo na kusema kuwa waachwe kama walivyo.

Katika kusherehekea sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, kanisa la Shekinah Presbyterian Madale Lajitolea kufanya usafi katika jiji la Dar es Salaam

0
0
Waumini wa kanisa la Shekinah Presbyterian Tanzania wamezindua rasmi zoezi la kufanya usafi kwa kujitolea katika mtaa wa Madale mahali kanisa lilipo. 

Katika kusherehekea sikukuu ya Mapinduzi, walizindua zoezi hili katika serikali ya mtaa wa Madale. Wakiongozwa na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Mch. Daniel John Seni asubuhi na mapema walianza usafi katika kituo cha daladala cha Madale mwisho, baadaye Kisauke shule, na kisha Madale sokoni.

 Baada ya kusafisha katika maeneo hayo waliondoka moja kwa moja mpaka kwenye serikali ya mtaa wa Madale ambapo katibu/Msaidizi wa kanisa ndugu George Shiganga alitoa maelezo kwa mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo.

Wakiongozwa na Kauli mbiu ya  “USAFI WA MAZINGIRA NI SEHEMU YA UTAKATIFU,” mchungaji Daniel alifafanua kwamba “hakuna kitu ambacho kilianzia kwenye imani kikashindikana.” 

Mchungaji huyu alielezea kuwa “Siyo kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ndugu Makonda ameshindwa kwenye zoezi la usafi, tatizo ni wapi alianzia.” Alikaza kwamba “sisi katika kumuunga mkono mkuu wetu wa mkoa; tumekuja na mbinu mpya ambayo tunapenda watu wa dini zote katika Mkoa wa Dar es salaam waige, na mbinu hiyo ni kuwafundisha waumini wetu kwa vitendo na kuwabadilisha katika mawazo.” 

Aliendelea kusema kuwa “Katika kuhakikisha tunaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanya na serikali ya awamu wa tano, tunapaswa kupunguza maneno na tuongeze kwenye vitendo zaidi, ifike mahali wachungaji tuwaambie wazi waumini wetu kwamba uchafu ni dhambi! Na kama uchafu ni dhambi, maana yake wakristo wote wanapaswa kuwa wasafi kuanzia rohoni hadi nje (mazingira). 

Alisisitiza kwamba kanisa lazima liwe na athari chanya katika jamii. Kazi ya mchungaji siyo kukemea pepo tu, bali ni kuwafundisha waumini pia waweze kujitolea kwenye jamii inayowazunguka. 

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Madale bwana Mberwa aliwashukuru sana waumini hawa, na kuomba watu wa dini zote kuhubiri habari za usafi katika makanisa na misikiti yao, ili kujenga fikra mpya kwao. Katika kuhakikisha kwamba zoezi hili linakuwa ni endelevu, waumini hawa wamekubaliana kwamba watakuwa wanafanya usafi mara moja kwa mwezi kwa kujitolea.

Mchungaji Daniel aliwakaribisha watu wa Madale ambao wangependa kuunga mkono zoezi hili la usafi kuwasiliana naye kwa 0769080629 ili kupata ratiba kamili ya zoezi zima.

Imetolewa na ofisi ya kanisa la Shekinah Presbyterian Church
Madale Dar es salaam.

Rais Magufuli Akwama Kuhudhuria Sherehe za Mapinduzi Zanzibar....Dr Shein Ataja Sababu

0
0
Rais wa Tanzania, John Magufuli ameshindwa kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika leo Jumamosi Januari 12, 2019 katika Uwanja wa Gombani, Pemba visiwani humo.

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali waliojitokeza uwanja hapo amesema Rais Magufuli amesema hajaudhuria sherehe hizo kwa sababu amepata dharura.

Viongozi wengine waliohudhuria ni; Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, marais wastaafu wa Tanzania,  Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete.

Wanafunzi Kidato Cha Kwanza Kondoa Wapata Neema

0
0
Na Peter Haule, WFM, Kondoa
WANAFUNZI wote 3,287 waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma, wanatarajia kuanza masomo baada ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, kutoa msaada wa mabati 1080 ya kuezekea vyumba 20 vya madarasa.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa kipaumbele chake kikubwa ni elimu na anataka kila mwanafunzi aliyefaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo anapata fursa hiyo ya kusoma.

"Tumeamua kutumia mfuko wa Jimbo, zaidi ya sh. 20m zimetumika kununulia mabati haya na niombe Mkurugenzi wewe ndiye mwenye watendaji mpaka ngazi ya vijiji na vitongoji ambako shule zetu zipo, mabati haya yafikishwe kwenye kila shule ili inapofika mwisho wa mwezi Februari, 2019, watoto wote waanze kusoma" alisema Dkt. Kijaji

Aidha, Dkt. Kijaji amewapongeza viongozi na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa jitihada zao za kukuza elimu na kufanikisha Wilaya hiyo kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2018 ambapo shule nane kati ya kumi zilizofanya vizuri katika Mkoa wa Dodoma, zinatoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

"Tunakwenda kwenye Tanzania ya Viwanda, hatuwezi kuwapeleka wanaKondoa wasio na elimu ndio maana tumefanya mapinduzi makubwa katika wilaya yetu kutoka kuwa ya mwisho kielimu katika Mkoa wa Dodoma miaka mitatu iliyopita hadi kuwa na shule 8 zilizofanya vizuri kati ya 10, kimkoa" aliongeza Dkt. Kijaji

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bi. Hildegard Saganda, wamesema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka baada ya kuwa na wasiwasi wa namna ya kuwawezesha zaidi ya wanafunzi elfu 3 kupata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa uliokuwa ukiikabili Halmashauri ya Wilaya hiyo.

"Mbati haya yatapelekwa kwenye shule ambazo wananchi wamejenga maboma na zimefikia hatua ya lenta ambazo ni Busi, Kikore, Changaa, Kalamba, Itaswi, Kwadelo, Hondomairo na Loo" alifafanua Bi. Hildegard Saganda

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa, ameelezea kuridhishwa kwake na namna Ilani ya CCM inavyotekelezwa katika wilaya yake katika nyanja mbalimbali na kumpongeza Dkt. Ashatu Kijaji kwa jitihada zake za kuiletea Maendeleo wilaya hiyo.

MWISHO

Rais Magufuli Aagiza Ndege za Rais Zianze Kubeba Abiria

0
0
Rais Dkt. Magufuli ameagiza kwamba ndege 2 kati ya ndege 3 za Rais, zipakwe rangi ya Air Tanzania na zianze kutumika kusafirisha abiria.

Ametoa agizo hilo leo Ijumaa Januari 11, 2019 wakati wa mapokezi ya ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyowasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.


“Kwa kuwa rais mwenyewe hasafiri hovyo sasa zinakaa kufanya nini na moja ina uwezo wa kubeba watu 50. Hii haitabeba abiria pale tu ambako itakuwa inatumika,” amesema Rais Magufuliu.

Akijibu ombi la Askofu mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship (FGBF) Zachary Kakobe aliyemuomba kuwa na desturi ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kama ilivyo kwa viongozi wa dini, Magufuli amesema anaogopa kukutana na watu ambao wanatukana na kutishia kumkatakata.

“Huwezi kukutana na mtu anayekuambia akikushika atakukata halafu ukutane naye kumbe ndiyo siku yako ya kuchinjwa hivyo ni bora umuache akae mwenyewe huko,” amesema Rais Magufuli


Aidha Rais Magufuli ameshwashukuru wabunge wa Chama cha Mapinduzi kwa kuwezesha maendelo hayo kupitia kuunga kwao mkono bajeti inapopelekwa bungeni.

Airbus 220-300 imekuwa ni ndege ya 6 kuwasili nchini miongoni mwa 7 zilizonunuliwa na Serikali huku nyingine moja ikisubiriwa ambapo leo Rais amethibitisha kuwa ndege nyingine ya 8 inanunuliwa.

Makonda: Naomba Mniombee Niwe Kama Rais Magufuli

0
0
Mkuu wa Mko wa Dar es salaam, Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini waweze kumuombea ili atimize ndoto ya kuwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Muda mfupi uliopita akizungumza katika mapokezi ya ndege aina ya Airbus A220-300 uwanja wa ndege, Makonda amewataka viongozi wa Dini kumuombea juu ya ndoto yake ya kuwa kama Rais Magufuli kwa kuwa ni mtu wa kutekeleza.

"Viongozi wa dini naomba mniombee, nataka nikikua niwe kama Rais Magufuli, haya ni maombi yangu kabisa, kwa sababu ni mtu wa kutekeleza, usiyeyumbishwa,umehakiksha Mungu kwanza na unaipenda Tanzania kuliko hata familia yako"- Paul Makonda.

Makonda ameongeza, "hivi ulivyo Rais wetu angekuwa mwingine Watoto wake tungekuwa tunagombana nao mtaani lakini Wewe umehakikisha hakuna anayeingilia jukumu lako kama Baba wa familia" Makonda

Pamoja na hayo Makonda amemwambia Rais Magufuli, yeye na wakazi wa Dar es salaam wamekwenda kumuunga mkono kwa kuwa alitoa ahadi kutoka kwenye ilani ya CCM na anatekeleza ikiwemo elimu bure

"Nilipotoa tangazo la kuja hapa nilisema waje wale waliowahi kutoa ahadi na wakatekeleza" Ma

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya January 12


Ndege Nyingine Mpya Dreamliner kutua nchini Novemba Mwaka Huu

0
0
Serikali imesema inatarajia kupokea ndege nyingine aina ya Boeing Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 iliyotengenezwa nchini Marekani.

Dreamliner hiyo  itakuwa ni ya pili baada ya ile ya kwanza ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyotua hapa nchini Julai 8, mwaka jana amabyo hadi sasa inafanya safari zake Entebbe nchini Uganda, Bujumbura nchini Burundi na Visiwa vya Comoro.

Akizungumza jana  katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Airbus 220-300 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema Serikali ilipanga kulifufua Shirika la Ndege nchini (ATCL) kwa kununua ndege mpya Saba.

“Rais Magufuli alipoingia madarakani aliahidi kuifufua ATCL kwa kununua ndege saba lakini juzi kanipigia simu kuniagiza tununue nyingine ziwe nane kabisa, ”alisema Waziri Kamwelwe.

Naye Rais Magufuli alisema pamoja na kuwa aliahidi kununia ndege saba na nyingine zimeshawasili lakini huo si mwisho kwani ana mpango wa kuagiza ndege nyingi zaidi.

“Nataka mjue kuwa ndege hii tunayopokea leo sio ya mwisho nataka kununua ndege nyingine zaidi ambazo zitakuwa zinapishana katika masafa ndani na nje ya Afrika,” alisema Rais Magufuli.

Hadi sasa ndege sita zilizonunuliwa na Serikali zimeshawasili hapa nchini ukiachana na hizo za Airbus 220-300 na Dreamliner nyingine ni Bombadier Dash 8 Q400 tatu zenye uwezo wa kubeba airia 76 kila moja.

Rais Magufuli Ammwagia Sifa Katibu Mkuu CCM....."Moto Wake Hata Mimi Siufikii"

0
0
Rais John Magufuli  ameweka wazi kuwa hotuba za Katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally huwa zinamshangaza kwa namna ambavyo anazitoa bila uoga jambo ambalo humfanya yeye ajione ni mpole.
 
Mwenyekiti huyo wa CCM alieleza hilo jana kwenye hotuba yake wakati wa mapokezi ya ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyowasili nchini jana mchana Januari 11, 2019 kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

''Dkt. Bashiru amekuwa muwazi, huwa namuangalia kwenye hotuba zake saa nyingine nasema kumbe mimi nafuu bwana kuliko huyu jamaa'', alisema.

Rais alieleza kuwa Katibu wake huyo amekuwa akikemea ufisadi ambao ulikuwa ukishamili siku hadi siku lakini sasa yeye anapingana nao hadharani bila kujali.

Magufuli amewataka viongozi wote wa chama na Serikali kuendelea kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja ili kusaidia maendeleo na siku moja Tanzania itakuwa kama Ulaya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya January 13

Waziri Ummy Awaonya Madaktari Nchini, Awataka Kuacha Kuwa Madalali Wa Maduka Ya Dawa

0
0
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaonya madaktari nchini kuacha tabia za kuwa madalali wa maduka ya dawa kwa kuwaandikia wagonjwa dawa mara mbili mbili huku akiwaambia kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali.

Huku akiagiza hospitali za Rufaa kote nchini kuhakikisha zinakuwa na maduka ya dawa litakalokuwa  na uhakika wa dawa zote muhimu ili kuondosha kero hiyo na kuondoa mianya ya madaktari kudalalia dawa kwenye maduka binafsi.

Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani wa Tanga aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na kauli hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walimsimamisha nje ya hospitali hiyo kabla ya kukutana nao.

Wananchi hao ambao walikuwa wakisubiri kuingia hospitalini hapa walimueleza kero hiyo ambapo alisema mbali na kero hiyo aliwaagiza madaktari nchi nzima kuhakikisha wanazingatia mwongozo wa kutoa dawa au matibabu ili kuepusha lawama kwa wagonjwa wa kubadilishiwa dawa na kila daktari.

Akiwa kwenye eneo hilo ambalo ni maalumu kwa ajili ya kupumzikia wananchi ambao wanakwenda kuwatazama wagonjwa wao kabla ya kuingia hospitalini hapo ndipo wananchi hao walipoamua kumueleza kilio hicho ambacho kimekuwa kikiwaumiza muda mrefu sana na kumuomba akishughulikie.

“Kwa kweli hii sio sawa kabla ya hapa nimepata wasaa wa kuzungumza na wananchi nje ya geti lakini kilio chao kikubwa ni kutokuridishwa na huduma tunazozitoa likiwemo suala la mgonjwa kuandikiwa dawa na kila daktari hii sio sawa naaagiza madaktari acheni kuwa madalali wa maduka ya dawa na sitaki kusikia hili siku nyengine “Alisema Waziri Ummy

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya waziri huyo Mmoja wa wananchi Mussa Jangwa alisema kwamba kwenye hospitali hiyo kumekuwa na changamoto kubwa ambazo wanakumbana nazo ni kila daktari anayeingia wodini anaandika dawa zake.

Alisema kwamba hatua hiyo imepelekea kuingi gharama kubwa huduma bado ni changamoto kutokana na kutumia fedha nyingi kutokana na kuwepo kuandikiwa dawa kila wakati na kulazimika kwenda kununua

“Mh Waziri tunashukuru kwa kuja na tungeomba viongozi wengine waige mfano wako hapa hospitali ya Bombo kuna tatizo kubwa sana unapo na mgonjwa wodini unapokuja daktari wa kwanza naandika dawa na mwengine akipita anaandika dawa kwenye zamu yake sasa mgonjwa hajui anunue zipo na ghamara zinakwenda “Alisema Mussa.

Alisema wakati wanapoandikiwa dawa hizo wanaelekezwa duka la kwenda kununulia huku wakitumia fedha nyingi ndani ya siku nne jambo ambalo limechangia kujikuta wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kubaki kuingia gharama zisizokuwa za msingi huku mgonjwa akiwa bado hajatumia akizoandikiwa na hali yake ni mbaya.

“Unapozungumzia jambo la afya ni uhai wa binadahamu nichukue fursa hii kukupongeza kutembelea hospitali hii isiwe ni wewe tu viongozi wote wafanye ziara kama wewe huduma za afya bombo bado changamoto kubwa sana “Alisema

Naye kwa upande wake Pili Nzoya Alisema wakati mwengine daktari anaweza kupita wodini na kumuandikia mgonjwa dawa nyingi wakati ni za kununua na kila wakati wamekuwa wakifanya hivyo na kupelekea kuwepo kwa usumbufu mkubwa kwao.

Awali naye mkazi mwengine Amina Mrisho alimueleza Waziri Ummy kwamba wamekuwa wakiandikiwa dawa wakati bado nyengine walizokuwa nazo hawajazimaliza kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu na kujikuta wakiingia hasara.

Alisema kwamba jambo ambalo limekuwa likiwashangaza ni kuandikiwa dawa na daktari halafu wanabadilishiwa dawa nyengine jambo ambalo ni hasara kwao huku wagonjwa wao wakiwa kwenye hali mbaya na baadae mgonjwa anafariki.

“Kwa mfano Mh Waziri umeandikiwa dawa leo za sh.40,000 kabla haujazimaliza unaandikiwa nyengine hili ni tatizo ambalo limekuwa likituumiza sisi wananchi tunaomba utusaidie “Alisema.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo lakini walikuwa wanafanya kwa nia njema lakini kama tukiwabaini ambao walikuwa wanafanya kwa nia binafsi tutawachukulia hatua.

Mnyika Amvaa Spika Ndugai, Adai Bunge la Sasa ni Dhaifu

0
0

Zikiwa zimesalia siku nane kabla ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa kwamba Bunge ni dhaifu, Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika, naye amekoleza moto kwa  kusema Bunge la sasa ni dhaifu.

Mnyika alitoa kauli hiyo jana wakati wa mjadala ulioshirikisha vyama vya siasa kuhusu Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa ulioandaliwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), ulioongozwa na Rais wa chama hicho, Fatma Karume.

Alipoanza kuchangia, Mnyika aliwashukuru TLS kwa kuandaa mjadala huo na kuahidi kuwa maoni mbalimbali yaliyotolewa washiriki wa mkutano huo, Chadema itayachukua kwa ajili ya kusukuma mabadiliko ili hatimaye wahakikishe ile nia mbaya ya muswada huo haitimii.

“Nianze kwa kuwaeleza waziwazi na kuwaomba sana kwamba kwa muundo wa Bunge letu lilivyo sasa na kwa namna Bunge lilivyo dhaifu, tukifikiria kuwaachia wabunge na kuwaachia mchakato wa kibunge uendelee mpaka mwisho tukitarajia kwamba mambo mabovu yaliyoelezwa kwenye muswada yatabadilika, tutakuwa tunafikiria vibaya,” alisema Mnyika.

Mnyika aliwaomba washiriki wa mjadala huo wasiishie kutoa maoni yao hapo bali washirikishe taasisi za kidini na za kiraia ziende kwa wingi mbele ya Kamati Dodoma kufikisha ujumbe kwamba muswada huo usiende mbele ya Bunge badala yake uondolewe kabisa.

Januari 7, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka CAG afike mbele ya Kamati hiyo, Januari 21 kujieleza kutokana na kauli yake aliyoitoa Marekani wakati akihojiwa na redio moja nchini humo kuhusu Bunge linavyotekeleza mapendekezo ya ripoti zake.

Mbali na kumtaka Profesa Assad kufika mbele ya Kamati, Ndugai pia alimtaka Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, kuripoti mbele ya kamati hiyo, Januari 22, mwaka huu, kuthibitisha madai yake aliyoyatoa kupitia mitandao ya kijamiii kuwa Bunge ni dhaifu.


Aidha, Spika Ndugai aliongeza kuwa CAG na maofisa wake wanaingia kwenye Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).


Spika alifafanua kuwa ripoti hizo zikifika kwenye kamati hizo ambazo zinaongozwa na upinzani, muda wote maofisa wa CAG wanakuwapo kueleza upungufu waliobaini na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Ndugai alisisitiza kuwa tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani, imekuwa ikipambana dhidi ya matumizi mbaya ya fedha za umma na hatua zimekuwa zikichukuliwa.

Kadhalika, Ndugai alibainisha Bunge lilivyofanya kazi kubwa katika kipindi cha miaka mitatu tangu serikali ya Rais John Magufuli, ilipoingia madarakani mwaka 2015.



Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa (CCM), alisema mabadiliko makubwa kwenye usimamizi wa fedha za umma yamefanyika kwa ushauri wa Bunge na CAG, hivyo alishangazwa na hatua zipi ambazo CAG alitaka zichukuliwe.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images