Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tatizo la Maji Lamuibua Waziri Mabula Ilemela, Mwanza

$
0
0
Na Munir Shemweta, ILEMELA
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea miradi ya Maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa jitihada za kuwapatia wananchi wa jimbo hilo huduma ya maji safi na salama.

Katika ziara hiyo Aweso alijionea changamoto mbalimbali zinazoikabili miradi ya maji katika manispaa hiyo pamoja na kero ya maji wanayoipata wananchi wa Kata ya Bugogwa yenye mitaa kumi na tano na wakazi wapatao 32,000 ambao kwa muda mrefu hawana huduma ya maji licha ya juhudi za mbunge wa jimbo la Ilemela Dk Mabula kuwachimbia visima.

Mbunge wa Jimbo hilo Dk Mabula ameiomba Wizara ya Maji kuwapatia wananchi wa kata ya Bugogwa huduma ya maji katika mradi wa maji vijijini kutokana na chanzo cha maji cha mradi huo kupitia eneo lao.

Kwa Mujibu wa Dk Mabula, pamoja na chanzo cha mradi wa maji vijijini kuwa katika kata ya Bugogwa jimboni humo lakini wananchi wake hawajajumuishwa kwenye mradi jambo linaloleta sintofahamu kwa wakazi hao ambao sasa wanaona kutengwa na serikali  jambo alilolieleza kuwa linaweza hata kutishia usalama wa mradi.

Alisema, njia pekee ya kuwafanya wananchi wa kata ya Bugogwa kufurahia matunda ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ni kuwapatia huduma ya maji safi na salama kitendo kinachotafsiriwa kama kumtua ndoo mama kichwani.

Kufuatia ombi hilo, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alimuagiza Mhandisi wa Maji katika Manispaa ya Ilemela Anna Mawala pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Mwanza (MWAUWASA) Injinia Anthony Sanga  kushirikiana kuandaa mpango mdogo utakaowezesha wakazi wa kata nao kufaidika na mradi na mapendekezo hayo yawasilishwe wizarani mapema ili kufanyiwa kazi.

Aweso alisema kuwa, Wizara ya Maji haiwezi kuwa kikwazo kwa wananchi kupata huduma ya maji kwa kuwa huduma hiyo haina mbadala hivyo Serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha wananchi hao wanapata huduma ya maji safi na salama ili kuondokana na kero ya muda mrefu.

Mtendaji wa Kata ya Bugogwa Manispaa ya Ilemelea mkoa wa Mwanza Rashid Sukwa alisema kata yake imekuwa na tatizo la maji kwa muda mrefu pamoja na juhudi za mbunge wa jimbo hilo Dk Mabula kusaidia kuchimba visima lakini baadhi ya wananchi wanatumia visima vya asili.

Ameitaja baadhi ya mitaa yenye changamoto kubwa ya maji katika kata hiyo kuwa ni pamoja na Lugezi, Igombe A na B, Bugogwa, Kigote, Bugigwa, Kabaganja, Kasamwa, Kayenza Ndogo, Kisonde, Kilabela, Isanzo, Igogwe pamoja na Nkoronto.

Mmoja wa wakazi wa Bugogwa Janet Lusia alimshukuru Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa kuona umuhimu wa wananchi wa kata hiyo nao kufikiriwa kupata maji katika mradi huo kwa kuwa wametaabika kwa muda mrefu pamoja na jitihada za mbunge wao kuwachimbia visima.

Bobaboda Auawa kwa Kupigwa na Abiria Wake

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamsaka mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi kwa tuhuma za kumuua dereva bodaboda Salumu Ramadhan (40).

Tukio hilo lilitokea Jumatatu ya Januari 7, 2019 majira ya saa nne usiku eneo la Foren Pub - Mawenzi katika Manispaa ya Morogoro ambapo mtuhumiwa alimpiga bodaboda huyo kichwani baada ya kukataa kumpakia mwanamke  aliyekuwa naye kwenye pikipiki kwa nauli ya Sh500. 

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wilbrod Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo bado hajakamatwa huku akiwataka watu wenye taarifa zake kuzitoa kwa Jeshi la Polisi ili waweze kumkamata na kumchukulia hatua za kisheria.

Nguo zinazofanana na sare za JWTZ zanaswa kambi ya wakimbizi Kigoma

$
0
0
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, imekamata nguo zinazofanana za sare za kijeshi katika makambi ya wakimbizi.
 
Akizungumza na waandishi na kamati hiyo mjini hapa jana Alhamisi Januari 10, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Samson Hanga, alisema nguo hizo zilikamatwa Desemba 31 mwaka jana kati ya saa tano asubuhi hadi sita mchana kwenye  makambi ya wakimbizi.

“Jumla ya nguo zinazofanana na sare za kijeshi 1,947 zilikamatwa katika kambi ya wakimbizi ya Mtendeli na Nduta zote za hapa hapa Kigoma.

“Katika Kambi ya Nduta zilikamatwa sare 1,325 na Mtendeli 622,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaini walioingiza sare hizo na lengo lao.

Kilichoendelea Mahakamani Asubuhi ya Leo Katika Kesi ya Kupinga Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa

$
0
0
Shauri la kupinga muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ambalo lilipangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu leo Ijumaa saa tatu, limehamishiwa kwa Jaji mmoja.

Shauri hili lilipangwa kusikilizwa na jopo linaloundwa na Jaji Barke Sehel (kiongozi wa jopo), Benhajo Masoud na Salma Maghimbi, lakini usikilizwaji huo umekwama baada ya wajibu maombi (Serikali) kuwasilisha pingamizi la awali wakiitaka Mahakama hiyo ilitupilie mbali.

Kutokana na pingamizi hilo, Mahakama ilisitisha usikilizwaji wa shauri la msingi na badala yake ikaamua kuanza kusikiliza pingamizi na ikapanga pingamizi hilo lisikilizwe na jaji Masoud katika chemba kuanzia saa 4:00 asubuhi

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Wahukumiwa Miaka 7 Jela Kwa Kuchezesha Upatu na utakatishaji fedha.

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Jones Moshi na James Gatuni, kulipa faini ya Sh milioni 204 au kwenda jela miaka saba kwa kosa la kuendesha biashara ya upatu na utakatishaji fedha.

Waliohukumiwa ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Rifaro Africa Ltd, Jones Moshi (42) mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam na Mkurugenzi mwenza wa Kampuni hiyo, James Gatuni (35) raia wa Kenya.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, alisema katika kosa la kwanza la utakatoshaji fedha watu kila mmoja anatakiwa kulipa faini ya Sh milioni mbili na endapo watashindwa kufanya hivyo watatakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani.

Mashauri alisema katika shtaka la pili linalohusu utakatishaji fedha haramu kila mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 100 na endapo atashiwa kufanya hivyo atalazimika kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

“Lakini wakishindwa kulipa faini za makosa yote watatakiwa kutumikia kwenda gerezani kama adhabu kwa makosa yote mawili” alisema Mashauri.

Awali Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro, akisaidiana na Wakili Esther Martine na Neema Mbwana alidai mahakamani hapo kuwa wawili hao walitenda kosa hilo kati ya Julai 14 mwaka 2014 na March 31 mwaka 2016, jijini Dar es Salaam na maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kanisa Katoliki lapinga matokeo ya uchaguzi DRC

$
0
0
Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) limesema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Taifa Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) hayaakisi taarifa zilizokusanywa na waangalizi wake.

Jana alfajiri, CENI ilitangaza matokeo ya uchaguzi ya urais ambayo yalimtangaza Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa asilimia 38.5, akiwazidi Emmanuel Shadary wa chama tawala na Martin Fayulu aliyekuwa anaungwa mkono na vyama kadhaa vya upinzani.

“Tunaona matokeo ya urais yaliyotangazwa na CENI kuwa hayaendani na takwimu zilizokusanywa na waangalizi wetu katika vituo vyote vya kupigia kura nchini,” amesema Padri Donatien Nshole ambaye ni msemaji wa Baraza la Maaskofu nchini humo.

Wiki iliyopita, Kanisa hilo lilisambaza waangalizi 40,000 kwenye vituo vya kupigia kura nchini humo. Baada ya kukusanya takwimu zake, ilieleza kuwa inafahamu mshindi wa uchaguzi huo lakini ikaitaka CENI kuhakikisha inamtangaza mshindi kwa haki.

Mwanadiplomasia Mwandamizi wa Ufaransa, Nshole alieleza jana kuwa takwimu za Kanisa Katoliki zimeonesha kuwa Martin Fayulu ndiye aliyeshinda uchaguzi huo na sio Tshisekedi.

Takwimu za CENI zinaonesha kuwa Tshisekedi alipata kura Milioni 7 na Fayulu akimfuatia kwa kura Milioni 6.4 huku mgombea wa chama tawala, Emmanuel Shadary akiambulia kura Milioni 4.4.

Tshisekedi anatarajiwa kuapishwa Januari 25 mwaka huu kuwa Rais wa Tano wa DRC akihitimisha utawala wa miaka 18 wa Rais Joseph Kabila. Anaandika historia mpya ya kuwa rais wa kwanza aliyekabidhiwa madaraka kwa njia ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura.

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 49

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
“Ethan kumbe bado hujaondoka?”
Biyanka alizungumza huku akiingia ofisini kwangu. Nikamsindikiza kwa macho hadi kwenye kiti alicho kikalia. Taratibu nikasimama na kuzunguka kwenye meza hii kubwa ya hapa ofisini kwangu, nikakaa juu ya meza huku nikimtazama Biyanka kwa macho makali, taratibu nikamshika kidevu chake kwa kiganja cha mkono wangu wa kulia kisha nikamnyanyua uso wake na tukatazama. Biyanka akasimama taratibu akasimama na mikono yake akaiweka juu ya mapaja yangu huku tukitazamana na midomo yake akianza kuing’ata ng’ata akiashiria kwamba ana haja ya kuhitaji kile nilicho kikusudia kumfanyia na sasa ndege niliye mtega anaanza kuingia kwenye tundu bovu.

ENDELEA           
Nikaushusha mkono wangu mmoja hadi kiunoni mwake na kumsogeza karibu yangu na tukaendelea kutazamana kwa sekunde kadhaa. Biyanka akayafumba macho yake ikiwa ni ishara ya kuhitaji kupokea lipsi zangu. Taratibu nikazisogeza lipsi zangu hadi kwenye midomo yake, tukazikutanisha ndimi zetu kwa mara ya kwanza na kumfanya Biyanka kusisimka mwili mzima. Japo moyo wangu na hisia zangu zote zipo juu  ya Camila ila hapa nipo kazini. Hisia za Biyanka zikazidi kupamba moto na akaanza kufungua vifungo vya shati langu, kabla hajafika kifungo cha tatu kutoka juu nikamshika mkono wake.
“Sehemu  hii sio salama, si unajua kuna baadhi ya wafanyakazi wapo bado ofisini”
“Ndio Ethan”
“Tutafute sehemu nyingine ambayo tunaweza kufanya hili jambo”
 
“Tunaweza kwenda kwangu?”
“Mmmm unaishi na nani?”
“Na dada wa kazi, ila hana shida sana”
“Mmmm ngoja nizungumze na mlinzi wangu akiniruhusu basi nitaweza kuondoka nawe akikataa basi tutafanya siku nyingine”
“Mmm….jamani Ethan nina hamu sana na wewe mpenzi wangu. Usinifanyie hivyo jamani?”
“Ngoja niwasiliane naye mara moja”
Nikamuachia Biyanka na kuzunguka hadi kwenye kiti changu, nikaingiza mkono wangu mmoja kwenye mfuko wa koti la suti yangu ambalo nimeliweka kwenye suti yangu na kutoa simu yangu na kumpigia Jojo.
 
“Ndio Ethan”
“Upo wapi?”
“Nipo hoteli kuna mambo nayashuhulikia, vipi nije kukuchukua?”
“Hapana, nahitaji kwenda nyumbani kwa Biyanka naamini nitalala huko”
“Mmmmm wewe mtoto, usitake kuniambia kwamba kila jambo ulilo likusudia limekwenda kama vile ulivyo panga”
“Ndio maana yake”
“Duuuu, kuwa makini”
“Nipo makini kuliko unavyo dhania”
“Sawa ujtanijulisha kila jambo na utakapo patwa na tatizo nifahamishe”
“Sawa”
 
Nikakata simu na kumtazama Biyanka usoni mwake.
“Tunaweza kwenda sasa”
“Kweli?”
“Ndio”
Biyanka kwa haraka akazunguka kwenye hii meza kubwa kiasi, akanikumbatia kwa furaha sana huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Unataka nikupikie nini?”
“Chohote”
“Sawa baba”
Biyanka akaninyonya midomo yangu kwa sekunde kadhaa kisha akabeba koti langu, akanisaidia kupanga vitu juu ya meza yangu kisha tukaondoka katika eneo hili. Tukaelekea katika eneo la maegesho ya magari na kuwakuta walinzi wake wakitusubiria. Tukaondoka eneo hili na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwake.
“Ethan yaani sijui niseme nini?”
“Kivipi?”
 
“Yaani nashindwa hata kuzielezea hisia zangu juu yako. Unajua toka siku ile tulipo kutana pale Mlimani City nilihisi jambo fulani katika moyo wangu. Ila sikuhitaji kujiaminisha kwa haraka na nikajua ni mambo ya kupita. Sasa siku nilipo kuona kwenye kikao cha kununua hisa, hapo ndipo nilipo ishiwa nguvu kabisa. Yaani haijawahi kutokea kwa mwanaume yoyote ile kuwa naye na hisia kama jinsi nilivyo patwa na hisia kwako”
“Hahaaa usijali nilikupenda nilipo kuona kwenye picha”
“Kwenye picha?”
“Ndio, kumbuka kwamba baba yako ni maarufu sana na nyinyi familia yenu ni maarufu, ila nilipata mashaka kwamba nitakupataje, ikiwa unalindwa namna hii”
“Hahaa jamania, ila unajua ni nini Ethan?”
“Ni nini?”
 
“Kila jambo kwenye haya maisha linatokea kwa makusudi ya Mungu.  Sikutarajia kw kipindi kama hichi kama ninaweza kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote”
Biyanka alizungumza kwa furaha sana, tukaendelea na safari yetu hadi tukadika kwenye nyumba yake nzuri iliyo tengenezwa kwa mtindo mmoja mzuri sana wa gorofa pacha zinazo fanana katika muonekano wa nje.
Tukaingia ndani na kukaribisha na msichana mmoja mzuri.
“Fatuma, huyu ni Ethan. Ethan huyu ni Fatuma, ukiachilia kama mfanyakazi wangu, ila ni mdogo wangu kwa maana nimeishi naye kwa miaka mingi sasa”
 
“Ohoo nashukuru kukufahamu Fatuma”
“Hata mimi nashukuru kukufahamu Ethan”
“Fatu huyu ni shemeji yako”
Nikamuona Fatuma akistuka kidogo, kisha akatabasamu.
“Ndio ni shemeji yako acha kushangaa”
“Jamani dada kwani nimeshangaa”
“Nakuona macho yamekutoka. Umepika nini?”
“Kama kawaida?”
“Mpenzi amepika kuku na chipsi vipi utakula au niingie jikoni mwenyewe?”
 
“Hapana, usisumbuke hicho hicho chakula kina tosha”
Fatuma akatukaribisha mezani, Biyanka akapata jukumu la kunihudumia chakula hichi na taratibu tukaanza kula huku tukiwa tumejawa na furaha. Kwa haraka haraka mtu akitutazama anaweza kuhisi tumejuana siku nyingi sana, ila ukweli ni kwamba tumejuana leo na katika mahusiano yetu hatujamaliza hata masaa matano. Matukio yote ya kulishana mimi na Biyanka kwa fatuma yakawa ni mshangao mkubwa sana.
 
“Shem”
“Bee”
“Mbona una tushangaa sana vipi?”
“Unajua sijawahi kumuona dada yangu akiwa katika hali ya furaha kama leo, ndio maana nina shangaa shemeji yangu”
“Ohoo hajawahi kuleta mchepuko humu ndani?”
“Hata siku moja. Huu unakwenda mwaka wa sita sijawahi kumuona akiwa na mwanaume aliye nitambulisha kwamba ni mpenzi wake”
“Basi mimi ni mwenye bahati”
“Kweli shemeji una bahati kubwa sana”
“Mpenzi wangu twende ndani bwana”
 
Biyanka alizungumza huku akinishika mkono. Tukanyanyuka kwenye kiti hichi nilicho kalia na tukaanza kuongozana kupandisha gorofani. Tukaingia kwenye moja ya chumba kizuri na kilicho pangiliwa vizuri. Biyanka hakuhitaji  hata kunipa sekunde za kujifikiria hichi ninacho kwenda kukifanya, ambacho kwa namna moja ama nyingine ni usaliti kwa Camila.
Akaanza kuninyonya lipsi zangu huku akinivua nguo zangu, nilipo salia na boksa mwilini mwangu, akanisukumia kitandani, kisha naye akaanza kuvua nguo zake. Akapanda kitandani akiwa na bikini tu, kwa jinsi alivyo nona, nikajukuta nikimeza fumba zito la mate.
 
“Ethan”
“Mmmmm”
“Nakupa usichana wangu, nakuomba usije ukanichezea”
“Unataka kuniambia kwamba wewe ni bikra?”
“Ndio”
Nikashusha pumzi taratibu kwani hichi ninacho kwenda kukifanya ni ukatili mkubwa sana kwake, kwani kusema kweli Biyanka ni daraja la mimi kuweza kufanikisha kile kitu ambacho nimekikusudia kukifanya juu ya baba yake.
“Mbona huna raha?”
Swali la Biyanka, likanitoa kwenye msongamano wa mawazo ulio anza kukishika kichwa changu.
 
“Hapana nipo sawa”
“Una uhakika Ethan”
“Yaa nina uhakika, unajua sikuwahi kufikiria siku hata moja kama nitakuja kupata msichana ambaye amejitunza. Nakuahidi Biyanka wewe ndio mke wangu, nitafanya kila jambo ili mradi uweze kujawa na furaha kwenye maisha yako”
“Nashukuru sana mpenzi wangu”

Hadi tunafika tamati Biyanka hakulalamika sana mwishoni kama ilivyokuwa mwanzoni. Biyanka akanikumbatia kwa nguvu sana hukua akilia.
“Siamini Ethan”
“Kwa nini?”
“Sijui mpenzi wangu, yaani siamini kama kweli leo usichana wangu umeweza kuondoka jamani”
 
“Amini tu mpenzi wangu”
Biyanka akanitazama usoni mwangu kwa sekunde kadhaa.
“Ethan”
“Mmmm”
“Ukiniacha haki ya Mungu nitajiua mpenzi wangu”
“Siwezi kufanya kitu kama hicho niamini. Sitaki kufanya dhambi kubwa kama hiyo”
“Hivi Ethan huna mwanamke kweli?”
Nikaka kimya huku nikifikiria nini cha kuzungumza
“Nilikuwa naye, ila kwa sasa hatuna mahusiano kabisa”
“Ulikuwa naye hapa Tanzania?”
 
“Hapana ni Ujerumani ninapo ishi”
“Ahaa kwa hiyo kwa Tanzania, mimi ni mwanamke wako wa kwanza?”
“Ndio”
“Ohoo asante Mungu kwa kweli”
Biyanka alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Biyanka akaniaga na kuelekea bafuni, gafla nikamuona Ethan akiwa amesimama pembeni ya kitanda hichi.
“Nakuona una kula bata wajina”
“Aisee imenistua sana”
“Pole sana rafiki yangu, kitu ambacho nimekuja kukusisitizia hakikisha kwamba humsahau Camila, unakumbuka maagano ambayo nilikueleza huko nyuma?”
“Ndio, tambua kwamba nipo  kazini hata mimi mwenyewe sipendi kumsaliti mpenzi wangu”
 
“Sawa, zoezi lako lifanye ndani ya muda mchache na uhakikishe kwamba likiisha unamrudia binti wa watu kwa maana kitu ninacho kifanya hivi asa ni kumpa moyo wa uvumilivu na kuto kuwa na wivu mkubwa sana na wewe”
“Nashukuru kwa hilo. Vipi Mery mumefikia wapi?”
“Tunaendelea vizuri”
“Mwanasheria na mke wake, wamefikia wapi?”
“Mmmmm nitakueleza kesho, sasa hivi acha niondoke eneo hili”
Ethan akaondoka eneo hili na kuniacha peke yangu. Biyanka akarudi huku akwia na furaha sana. Akapanda kitandani na akanikumbatia kwa furaha sana.
                                                                                                                      ***
    Asubuhi na mapema tukajiandaa na kuelekea kwenye hoteli ambayo ninaishi. Tukaingia katika chumba ninacho ishi na Jojo huku nikiwa nimeongozana na Biyanka. Tukasalimiana na Jojo ambaye tayari tumemkuta akiwa amesha jiandaa kwa kunipeleka ofisini kwa siku ya leo. 
 
“Tayari nguo nimesha kuandalia”
“Sawa sawa nashukuru”
Nikabeba nguo zangu na kuingia bafuni, nikabadilisha nguo na tukaiza safari ya kuelekea ofisini kwangu, huku tukiwa tumepanda gari moja na Biyanka huku gari mbili za walinzi wake zikitutangulia kwa mbele. Tukafika ofisini na kila mmoja akaendele ana majukumu yake. Kitu cha kwanza nilicho anza kukifanya ni kuhakikisha kwamba kila mkataba wa mfanyakazi  katika kampuni yangu nina upitia kwa umakini wa hali ya juu. 

Nilipo maliza kuipitia mikataba yote, nikafanya kikao na wakurugenzi wa vitengo vyote katika hii kampuni na tukapanga mikakati ya jinsi gani tunaweza kuikuza kampuni yetu ndani ya wiki mbili tu. Mikakati niliyo weza kuwapatia kila mmoja aliweza kuridhinika naye na kuamini kwamba kwa muda huo nilio weza kuwapatia basi tunaweza kufanikiwa kwa asilimia kubwa sana. Nikarudi ofisini kwangu huku kichwa changu kikiwa kimechoka kwa kweli kwani kazi niliyo ifanya kwa siku ya leo ni kubwa kuliko kawaida.
“Pole mpenzi wangu kwa kuchoka”
Biyanka alizungumza huku akizunguka meza yangu na kusimama nyuma ya kiti changu na kuanza kuniminya minya mgongoni mwangu.
 
“Nashukuru mpenzi wangu”   
“Nimezungumza na baba leo na nimemueleza juu ya mahusiano yetu na sifa zako zote, ameniomba leo usiku twende nyumbani kwake tukajumuike chakula cha usiku.”
Habari hii kidogo ikanistua sana, kwani sikutarajia kwa haraka hivi ninaweza kukutana na adui yangu ambaye nimejiapiza moyoni mwangu kwamba ni lazima niweze kumfanyia kitu ambacho hakuwahi kufanyiwa kwenye maisha yake yote.

==>>ITAENDELEA KESHO

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 182 na 183 )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
"Carin hakikisheni mkuu anakuwa salama”
Ester alizungumza huku akiwa ameishika vizuri earphone aliyo ivaa sikioni mwake.
“Muweke loudspeaker”
Ester akafanya hivyo, akaminya moja ya simu za mezani na tukaanza kusikia milio ya risasi jinsi inavyo endelea kurindima katika eneo hilo. Wanajeshi wa Marekani wakazidi kuongezeka jambo ambalo ni hatari sana kwa vijana Livna.
“Mkuu tumezidiwa tunaomba msaada, narudia tena tumezidiwa tunaomba msaada”
Tuliisikia sauti ya Carin alizungumza jambo lililo tufanya sote kutazamana, kwani hata tukituma wasichana wengine ili kuweza kufika eneo hilo watachukua muda mrefu njiani na wanaweza kukuta kila kitu kimekwisha, jambo ambalo ni hatari sana kwetu.

ENDELEA
“Tunatuma kikosi sasa hivi”
Ester alizungumza kisha akazima simu hii na kuvua earphone aliyo ivaa sikioni mwake.
“Tunafanya nini kwa maana hata tukitoa timu ikaenda kwa njia ya angani kwa kutumia helicopter hatutoweza kufika”
“Kuna mbinu yoyote ambayo tunaweza kumtishia Mmarekani?”
Kila mtu akaka kimya huku akifikiria ni kitu gani anaweza kunijibu.
 
“Mbinu ya mwisho iliyo baki  ni ile ya kuzipambanisha Marekani na Korea Kusini”
“Haito chelewa kutimia?”
“Hapo ni kumuomba Mungu, pia tunaweza kufanya mashambulizi makubwa sana kwa Korea Kaskazini na tutamfanya apatwe na hasira ya kuhakikisha kwamba anajibu mashambulizi”
“Kazi ianze mara moja”
Ester na wezake wakaka kwenye viti kila mmoja akiwa na laptop yake, nikaendelea kutazama mapambano ya wasichana hawa na jeshi la Marekani.
“Mungu wangu risasi zimewaishia”
Nilizungumza huku nikiwatazama wasichana hawa wakiwa wamejificha sehemu walipo huku kila mmoja akiwa hana silaha kabisa.
 
“Nina wazo pia?”
Msicha mwengine ambaye bado sijamfahamu jina lake alizungumza na kutufanya sote kumgeukia.
“Ndio”
“Kuna ndege ya kivita ambayo tunaweza kuitumia kwa kuwashambulia hao wanajeshi”
“Ipo wapi hiyo ndege?”
“Ipo chini kabisa ya hii meli, ndege hii mkuu alinionyesha na hiyo ndio silaha ya haraka kwa sisi kujilinda pale tunapo shindwa”
“Nani anayeweza kuiendesha?”
“Uzuri hiyo ndege haitumii rubani, unaweza kuiendesha kupitia hata hii laptop”
Sote tukabaki tukimtazama msichana huyu huku tukiwa na mshangao.
 
“Itachukua muda gani kufika eneo la tukio?”
“Dakika kumi hadi saba hivi”
“Anza kuiendesha sasa”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama msicha huyu ambaye kwa muonekano wake ni mpole sana, ila kichwa chake kina akili na kinaweza kufanya mambo mengi sana makubwa.
“Ukiendesha hiyo ndege naomba video uitume kwenye video hii”
Nilizungumza huku nikimuonyesha tv ya kwanza, akatingisha kichwa huku akiendelea kuminya minya batani zake kwa kasi kubwa sana. Tukaanza kuiona ndege hii ambayo sio kubwa sana ikianza kutoka chini kanisa ya meli hii kwa kasi ya ajabu ikaanza kuelekea angani, binti huyu mwenye utalamu wa hii kazi akazidi kuiendesha ndege hii ambayo kusema kweli hata mimi leo ndio mara yangu ya kwanza kuiona. 

Kwa jinsi binti huyu anavyo endesha ndege hiyo kwa kutumia laptop yake, hadi jasho usoni mwake likaanza kumwagika, ndani ya dakika sita ndege ikafika eneo la kisiwa, shambulizi la kustukiza kwa wanajeshi wa marekani likaanza, cha kumshukuru Mungu wasichana hao bado hawakuwa wamekamatwa, ikamuwia urahisi msichana huyu kushambulia kisawa sawa wanajeshi hawa, na kila aliye bahatika kupigwa risasi japo ya mguu, basi mguu wake uliweza kukatika kabisa, na inaonyesha ndege hii ina risasi kubwa na zenye uwezo wa kutoboa hata ukuta.
 
“Wasichana hawa walivyo ona wamepata msaada nao hawakuwa wanyonge, wakanza kuchukua bundiki za wanajeshi walio kufa na kuendelea kujibu mashambulizi kwa wanajeshi wanao jihahidi kushambili hiyo. Ester akavaa tena earphone sikioni mwake na kiiwasha simu iliyopo mezani.
“Songeni mbele hamuwezi kuudhurika sawa”
Ester alizungumza kwa msisitizo.
“Sawa mkuu”
Wasichana hawa wakaanza kukimbilia ndani ya hospitali alipo Sara na wagonjwa. 
 
“Wanasarenda masikini ya Mungu weee”
Logate alizungumza huku akiwaona wanajeshi wa Marekani wanao kimbialia baharini ambapo ndipo walipo ziacha boti.
“Kumbe walikuja na meli?”
Nilizungumza huku nikiitazama meli hiyo kubwa ya Wamarekani
“Ndio hiyo”
“Tuishambulie?”
“Ishambuli tu, usiiche”
Msicha huyu akapelekea mashambulizi kwenye meli hiyo, na safari hii mashambulizi ni ya mabomu makubwa makubwa na kuifanya meli hiyo kuanza kuteketea kwa moto na mwishowe ikaanza kuzama ndani ya maji ya bahari.
 
“Kazi imekwisha”
“Ngoja kwanza usiirudishe, hembu wasiliana na hao mabinti waulize wamewaona kina Livna”
“Carin mume wapata wagonjwa?”
“Ndio tumewapata na wapo salama kabisa na japa nao walikuwa wakisaidiana na dada Sara kuhakikisha wana wazuia wamarekani hawa kuingia ndani ya hospitali.”
Maeno ya Carini yakazidi kunipa faraja moyoni mwangu.
“Mtoto wa K2 je?”
“Pia yupo”
 
“Basi  hakikisheni muna rudi naye hapa”
“Sawa mkuu”
Tukajikuta tukishangulia kwa furaha, Logate pasipo kujali akajikuta akinikumbatia kwa nguvu, kitendo hichi kikanifanya nisisimke sana na kumuachia Logate haraka sana kwani sikuwahi kukumbatiana na mwanamke na damu yangu kunisisimka haraka kama hivi.
“Kazi nzuri, unaotwa nani?”
“Ritha”
“Oohoo hongera sana, kusema kweli ni kazi nzuri iliyo tukuka”
“Shukrani, ila nitawaomba munilinde kwa mkuu kwani ndege hii hakuihitaji watu waifahamu na wala hakihitaji itumike pasipo  idhini yake”
“Usijali nitazungumza na Livna akija sawa Ritha”
“Shukrani kaka Dany”
 
Carin na wezake wakafanikiwa kuwachukua Livna na wezake na kuanza safari ya kurudi huku tulipo huku wakiwa wameongozana na Sara pamoja mtoto wa K2. Sura za furaha zikazidi kutawala ndani ya chumba hichi. Livna na wezake walipo fika karibu na hii meli sote tukatoka ndani ya chumba hichi na kuelekea sehemu ambayo boti hiyo inasimama. Livna akashuka kwenye boti na kwaharaka akanfwata na kunikumbatia kwa nguvu huku machozi yakimwagika.
“Nimerudi”
Livna alizungumza huku akizidi kunikumbatia kwa nguvu.
“Shiiii usilie”
Taratibu nikamuachia Livna kifuani mwangu na kumtazama usoni mwake. Tukaondoka eneo hili huku nikimtazama mtoto huyu wa K2 .
 
“Kama sijakufa leo, basi siwezi kufa siku  nyingine kwa kushambuliwa kama leo”
Livna alizungumza huku tukiingia kwenye ofisi ya ambayo tulikuwepo.
“Sara asante, sikutegemea kama unaweza kuwa na akili kaama hiyo uliyo itumi. Logate, Ester asanteni, ilifikia hatu ya sote tulikata tamaaa kwani tulisha shindwa kabisa na mashambulizi”
Livna alizungumza kwa sauti ya upole na unyonge sana.
“Dany nina imani na wewe mchango wako umeonekena ninakushukuru sana kwa kweli”
“Usijali tupo pamoja”
 
“Tumekueletea uliye hitaji kumuona, sasa kazi ni kwako”
Nikamtazama mtoto wa K2 ambaye anaonekana amelia sana hadi amechoka, taratibu nikamsogelea na kuchuchumaa mbele yake.
“Unanikumbuka?”
“Mmmmmm”
Alijibu kwa kutingisha kichwa akimaanisha kwamba ananikumbuka.
“Ninaitwa nani?”
“Dokta Lameck”
Jina la dokta Lameck likawafanya watu wote kunishangaa.
“Sawa utazungumza na mama yako muda si mrefu”
“Sawa, kwa nini umenichukua?”
“Utajua baada ya muda ni kwa nini nimekuchukua. Kampeni chakula”
 
“Sawa”
Pacha mmoja akamchukua mtoto wa K2 na kutoka naye humu chumbani.
“Sara nina imani kwamba umemsikia Dany, sasa huyu ni Dany”
“Kweli anafaa kuwa gaidi, nashukuru kukufahamu Dany”
“Nashukuru nawe pia kwa hili ulilo nifanya, ila ni kwa nini unasema kwamba ninafaa kuwa gaidi?”
“Muonekano wako japo ni mzuri ila kwa watu kama sisi tunaweza kuona ni kitu gani ambacho kipo ndani yako”
“Samahani jamani kuna simu inaingia”
Ester alizungumza huku akitutazama.
 
“Kutoka wapi?”
“Hii kwa sasa inatokea Iraque na anaye piga ni Osama Bin Laden”
“Ngojeni kwanza mumesema Osama!!?”
“Ndio rafiki yangu, Osama yupo hai na nimarafiki wazuri na Dany”
Nikasimama mbele ya Tv ambayo ninawasilianana Osama, nikavaa eaphone aliyo nikabidhi Ester.
“Asallam Alghaikum?”
“Salama, nina imani umepata sehemu sahii ya kujificha?”
“Ninashukuru sana Dany kwa maana kuna mmoja wa watu wangu ndio alikuwa anavujisha signal ndio maana wamarekani waliweza kufanikiwa kuyanasa mawasiliano yetu”
 
“Sawa ninaimani hilo umelishuhulikia?”
“Ndio nimelishuhulikia kabisa kabisa. Ila sijasikia mashambulizi yoyote kutoka sehemu ambayo ilikuwa maficho yangu?”
“Niliweza kuziteketeza ndege zote hewani, kwa hiyo hapakuwa na ndege moja iliyo weza kufika nchini Pakistani”
“Ohoo Allah akuzidishie”
 
“Shukrani”
“Sasa tunaweza kuonana, kwa maana kuna mengi sana ninahitaji kuzungumza nawe”
“Hilo halina kipingamiza, ila kuna jambo moja ninahitaji unisaide”
“Zungumza”
“Wamarekani wamamkamata mke wangu ambaye ni mjamzito kwa sasa, wanamtumia yeye kuhitaji nijisalimishe mikononi mwao, ninakuomba sana uweze kuniasidia katika kumuokoa kutoka mikoni mwao, na siku tukionana basi itakuwa ni siku nzuri ya urafiki wetu”
 
“Usijali katika hilo, nitahakikisha kwamba wapelelezi wangu wanafanya kazi usiku na mchana kufahamu ni wapi alipo mke wako kisha tutamchukua tu. Nipatie picha yake ili iwe raisi kuweza kumpata”
“Utatumia muda wowote kuanzia hivi sasa”
“Tayari”
Ester aliziungumza
“Nimeipata, ninakuahidi rafiki yangu nilazima mke wako tumpate”
 
“Ninashukuru”
“Basi nikimpata nitakuambia ni wapi tuonane ili tuweze kukabidhiana”
“Sawa sawa”
Mazungumzo kati yangu na Osma yakaishia hapa na kunifanya niwageukie Livna na Sara walio simama pembeni yangu.
“Sara nina imani kwamba umeamini”
“Jamani huyu baba tuliambiwa ni marehemu kabisa”
“Yupo hai na taafira zilikuwa ni za uongo”
“Mmmm makubwa basi”
“Martin pole sana mdogo wangu”
“Usijali mkuu  ni jukumu langu”
“Usiku huu ninahitaji tufanye sherehe na wasichana wangu wote, kwa maana leo nimepata nafasi nyingine ya kuishi. Ninakuomba Ester ulisimamie hilo, pia tutamkaribisha Sara nyumbani sasa”
“Sawa mkuu”
 
“Jamani ninaomba nikapumzike kidogo”
Martin alizungumza kwa sauti ya upole kidogo nikamtazama kwa sekunde kadhaa kisha nikatingisha kichwa kumkubalia kwamba aende akapumzike.
“Unaonaje ukawasiliana na K2 sasa hivi ili kumpa presha?”
“Hapana ngoja siku ya leo ipite, tunahitaji kupumzika, kwani tumefanya kazi kubwa sana”
“Sawa ni wewe tu Dany”
Maandalizi ya sherehe yakaanza kufanyika, Livna akaanza kunitembeza katika meneo ambayo sikuwahi kuingia ndani ya hii meli kubwa sana.
“Dany”
“Naam”
“Ninakupenda”
Livna alizungumza huku tukiendelea kutembea taartibu tukielekea katika eneo jengine ambalo ameniambia linatatumika kwa kuzalishia mazoa mbali mbali yanayo tumika ndani ya hii meli.
“Ninakupenda pia”
“Kweli Dany, yaani leo nilipo zimia pale, picha ambayo inijia akilini mwangu ni yako, nilihisi ninakwenda kufa kusema kweli nilimuomba Mungu kwa mara yangu ya kwanza kunipa nafasi ya kiishi ili nije kuishi kama mama sasa”
 
“Unahitaji kuzaa na wewe?”
“Ndio, Dany umri wangu unakwenda sasa, na mimi siku nahitaji kuwa mama ninahitaji kuwa mama. Wewe ndio mwanaume sahihi wa kunipatia ujauzito sihitaji kufa nikiwa sina mtoto japo kwa mara ya kwanza niliapa kutokuwa na mtoto ila sasa ninahitaji”
Tukaingia katika eneo hili ambalo ni kubwa kama hekari kumi, limejaa udogo mwishi pamoja na mazoa ya kila aina, nikajikuta nikiwa ninashangaa kwani utaalamu huu sijajua wameutolea wapi.
“Mumefanyaje fanyaje hadi kuwa hivi?”
“Mimi mwenyewe kusema kweli nimekuta hili shamba kutoka kwa waanzilishi, na mimi nikaliendeleza kulilima na vijana wanaendelea kupata matunda ya kila aina”
 
“Kusema kweli sijapata ona kitu kama hichi”
Tukaanza kutembea ndani ya hili eneo ambalo kwa pembeni limezingushiwa vioo.
“Haya mazao yanakua kwa mionzi ya jua inayo ingia, seme sasa hivi ni jioni kama tungefika mchana basi tungeweza kuona jinsi mionzi ya juu jinsi inavyo ingia ndani ya hili eneo”
“Inashangaza kusema kweli daaaa”
Niliendelea kuzungumza huku nikiwa nimejawa na furaha kubwa kwani hili eneo unaweza kusmea ni shamba ambalo lipo nchi kavu kumbe ni ndani ya meli hii kubwa ambayo imeundwa kwa utaalamu mkubwa ambao unaweza kuwafanya watu kuishi miaka kwa miaka. Simu ya Livna ikaita, akaitoa mfukoni mwake na kuipokea. Akasikiliza kwa sekunde kadhaa akionekana anakabidhiwa maeleo fulani.
“Tunakuja sasa hivi”
Livna akakata simu na kuiridisha mfukoni mwake.
“Kuna nini?”
“Martin”
Livna alijibu huku akianza kukimbia, tukazidi kukimbia kuelekea ndani. Tukafika katika chumba cha Martin na kukuta madaktari wawili wa kike wakiwa wamemvua shati lake huku pembeni ya tumbo lake upande wa kulia kukiwa na damu nyingi.
 
“Amefanyaje?”
“Amepigwa risasi iliyo zama ndani na imeharibu sehemu kubwa sana ya vitu vya ndani, jambo linalo weza kupelekea kufa muda wowote kuanzia hivi sasa”
Maneno ya msichan huyu ambaye ni daktari yakanifanya nibaki na mshangaoo huku machozi yakinilenge lenga, hapa ndio nikakumbuka jinsi nilivyo mtazama Martin usoni mwake kipindi alipo aga anakwenda kupumzika, alikuwa ni mnyonge sana kupita siku zote nilizo wahi kumfahamu na kufanya naye kazi.    
 
AISIIIII……….U KILL ME 183 

“Apegiwa risasi saa ngapi jamani?”
Livna alizungumza huku machozi yakimlenga lenga  usoni mwake.
“Hili jeraha alikuja nalo na mimi ndio mtu wa kwanza kumuona”
Daktari alizungumza huku wakiendelea kujaribu kuitoa risasi iliyopo tumboni mwa Martin.
“Martin, Martin, Martin?”
Niliita huku niwa nimechumaa pembeni yake. Martina hakuitika wala kuyafumbua macho yake zaidi ya kukaa chini.
“Tunahitaji damu ya mtu mwenye group A plus”
Nesi alizungumza huku akiweka kifaa maalumu cha kupumulia pauni mwa Martin.
 
“Nitoeni mimi”
“Inabidi kukupima kwanza, tufahamu kwamba ni group O plus kwa maana Martin kundi lake la damu ndio hilo”
“Nipimeni tu”
Nilizungumza huku nikikunja mikono ya shati hili la jeshi nililo vaa, nikatoka chumbani humu na daktari mmoja na kuelekea hadi maabara. Akatoa damu yangu kiasi na kuipima.
“Damu yako ipo safi, na ni group A plus, inabidi utoe japo chupa mbili za damu”
“Sawa dokta fanya haraka haraka basi”
“Sawa”
 
Dokta akaufunga mkono wangu na mpira unao vutika kisha akanichoma sindano iliyo anza kupeleka damu kwenye dripu.
“Itachukua muda kidogo hadi kujaza chupa moja”
“Sawa, hivi ulimuonea wapi Martin kama amepigwa risasi?”
“Nilimkuta karibu na mlango wake akiwa ameegemea ukutani huku ameshika tumbo lake, nilipo mchunguza nikaona kiganja chake kimelowana damu, ikanibidi kumdadisi sana japo alikuwa anaficha mtu asione, katika kuminyana minya ili nione, akaanguka chini na kupoteza fahamu. Nikamuingiza chumbani kwake na tukaanza kumshuhulikia, na katika semehu ya jeraha tuliona amejifunga kitambaa kikubwa ambacho kilizuia kuonekana kwa damu yake”
 
“Daaa”
Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na majonzo mengi sana. Ikamalizika chupa moja, dokta akaitoa na kuweka chupa nyingine, kisha akatoka na chipa hii na kuniacha mimi nikiendelea kutoa damu hii.
‘Mungu ni mwema kwa kweli, kugongana kote huku sijapata Ukimwi mmmmmm’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kutazama damu hii jinsi inavyo ingia kwenye dripu. Nesi akaingia ndani ya chumba hichi huku akiwa ameshika dripu alilo toka nalo.
“Vipi?”   
Nilimuuliza huku macho yakiwa yamenitoka sana.
“Martin amekufaa”
 
Nikahisi kama nipo ndotoni, nikajaribu kuyafumbua macho yangu zaidi na zaidi ila hakuna kilicho badilika mbele yangu kwani, daktari ninaye muona na mandhari ninayo yaona ni yale yake. Kwa haraka nikachomo sindani niliyo chomwa kwenye mkono wangu, nikafungua mpira huu na kutoka chumbani humu nikikimbia kuelekea katika chumba cha Martin. Nikiwa ninakaribia mlangoni nikaisikia sauti ya Winy akilia kwa uchungu, nikaingia ndani na kumkuta Winy akiwa amelaza kichwa chake kifuani mwa Martin, Livna amesimama pembeni yake huku naye machozi yakiwa yanabubujika usoni mwake. Daktari amesimama pembeni Livna akiwa ametulia kimya.
 
“Hapana Martin huwezi kufa kizembe hivi”
Nilizungumza huku nikisegelea kitanda cha Martin, nikakaka pembeni ya kitanda hichi na kumtazama usoni mwake.
“Martin acha ujinga basi kuigiza vipi hivi rafiki yangu eheeee”
Niliendelea kuzungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu. Hawa na Babyanka nao wakafika ndani ya hichi chumba kila mtu aliye muona Martina akiwa amelala hapa kitandani na ameyafumba macho yake kusema kweli roho yake iliweza kumuua kwa staili yake.
 
“Martin si umetoka kuniaga kwamba unakwenda kumchukau mtoto wa K2 jamani mbona umeondoka mapema jamani, ikiwa penzi letu ndio kwanza limeanza jamaniii Martinnnnnnn”
Winy aliendelea kuzungumza machozi yakizidi kumwagika. Nikanyanyuka kiitandani humu na kumshika mkono Livna na kutoka naye.
“Dany tunaelekea wapi jamaani”
Livna alizungumza huku akijaribu kusimama ila nikamshika kwa nguvu na kuendelea kumvuta.
“Mtoto wa K2 na Wamarekani ni lazima walipe kwa hili walilo lifanya, siwezi kumpoteza mtu ninaye mpenda. Martin ni sawa na mdogo wangu”
 
Niliendelea kuzungumza kwa jazba kubwa. Tukaingia katika chumba cha mawasiliano na kukuta kukiwa hakuna mtu.
“Niitie Ester na Logate, waje na huyo kibonge”
Livna akabaki akabaki na bumbuwazi, nikamgeukia na kumtazama kwa macho makali sana, akatoka chumbani humu yeye mwenyewe. Baada ya dakika mbili akarudi akiwa ameongozana na Ester pamoja na Logate.
“Yupo wapi kibonge?”
“Amelala”
“Kamlete, analala hapa kwao. Fanya fasta sawa”
Nilizungumza kwa ukali, Logate akatoka kwa haraka humu ndani kwani kila mmoja nina imani leo hii ndio ananiona nikiwa nimekasirika kwa kiwango hichi.
“Wasiliana na LIVNA”
“Livna!!?”
“K2”
 
Ester akati kufanya kile nilicho muagiaza, haikuisha hata dakika moja nikamuona K2 mbele ya hii video.
“Mbona macho mekundu hivyo unavuta bangi siku hizi?”
Swali la kejeli la K2 likanifanya nizidi kupandwa na hasira, mtto wake akaingizwa humu ndani, alipo muona mama yake kwenye hii tv akakimbilia sehemu nilipo simama.
“Mamaaaa”
K2 akastuka sana kumuoan mtoto wake mikononi mwangu.
“U…..uu….umefikaje huk…..”
K2 alizungumza kwa kigugumizi kikali sana, nikamuona jinsi jasho likimwagika usoni mwake.
“Nipatie bastola”
Nilizungumza huku nikimshika mtoto wa K2 na kumuweka mbele yangu.
 
Livna akanirushia bastola yake, nikaidaka vizuri, nikaikokoki na kuiweka kichwani mwa mtoto wa K2 aliye anza kutetemeka mwili mzima.
“Mtu wangu mmoja amekufa. Martin amekufa kwa ajili yako wewe malaya, pamoja na huyu nguruwe wako. Umemuua Lucy sasa shuhudia ninavyo mfumua ubongo sawa”
Nilizungumza kwa ukali sana.
“Mamamaaaaaaa”
“Dany, Dany ninakuomba, ninakuomba sana nipo chini ya mguu yako, nipo tayari kufanya chochote unacho niagiza hivi sasa”
K2 alizungumza huku machozi uakiendelea kumwagika usoni mwake.
“Dany vita yako ni mimi na wewe, mwanangu hana hatia yoyote katika hii vita…ha……”
“Hana nini mpuuzi wewe, ulivyo muua malaika wangu ambaye hata raha ya dunia hakuwahi kuiona. Hadi leo sitambuu ni wapi walipo zikwa, alafu unaniambia kwamba hana hatia”
“Dady nimekosa, shetani shetani alini……”
Nikampiga risasi ya bega mtoto wa K2 na kumfanya aanguke chini na kuangua kiliok ikali sana. Nikamnyanuyua huku nikimtazama K2. 
 
“Ulihisi nitakushindwa, ulihisi kumuweka mwanao mbali na Afrika, nitashindwa kumuangamiza eheeee”
Niliendelea kufoka, K2 machozi  yaliyo ambatana na makamasi yakazidi kutiririka usoni mwa K2.
“Dany nipo tayari kufa, nipo tayari uniue na mkono wako”
Kilio cha mamuvu cha mtoto wa K2 pamoja na mama yake vikaendelea kutawala hapa. Nikamtazama K2 kwa muda wa dakika moja, kisha nikamsukumia mtoto wake pembeni.
“Unamasaa kumi na mbili hakikisha unajisalimisha kwa mtu nitakaye kuambia”
 
“Niambie tu Dany, niambie mimi nipo tayari kujisalimisha”
“Kwanza kiri dhambi zako kupitia vyombo vya habari, nitakatishe na useme kwamba mimi sina hatia na ugaidi wote huo. Wewe ndio gaidi japo itakuwa ni ngumu kwa watu kunielewa, ila hakikisha kwamba unanisafisha mimi sawa”
“Nitafanya hilo”
“Pili ukimaliza jisalimishe mikononi mwa OSAMA Bin Ladane”
“Osama!!?”
“Fanya hivyo, sihitaji maswali mengi na sihitaji kuwasiliana nawe, nikiwasiliana nawe masaa kumi na mbili yajayo uwe mikononi mwa Osama sawa”
“Sawa nimekuelewa, nimekuelewa Dany”
Nikazima Tv na kumtazama mtoto wa K2 anye endelea kulia hapa chini huku bega lake likiendelea kuvujika damu.
“Mtoeni hapa nisije nikamuua”
Logate kwa haraka akamnyanyua mtoto huyo na kuondoka  naye. 
 
“Dany”
Livna aliniita huku akinisogelea pembeni yangu, akanishika mkono wangu wa kulia na kuichukua bastola yake na kuichomeka kiunoni mwake. Taratibu akanikumbatia huku machozi yakiendelea kumwagika.
“Naogopa Dany, Martin amechukua kifo changu. Yote ni makosa yangu Dany”
“Shiiii…..sio makosa yako, usijilaumu katika hili”
“Kwa nini jamani nisinge mzuia, kwanini eheeeee?”
Nikazidi kumkumbatia Livna. Baada ya dakika kama kumi nikamuachia na kumkalisha kwenye kiti.
“Ester sherehe zote zikatishe, watu wote wavae nguo nyeusi. Tupo kwenye msiba”
Livna alizungumza kwa sauti ya ungonge huku akimtazama Ester usoni mwake.
 
“Sawa mkuu”
“Muje kusafisha hii damu hapa sawa”
“Sawa mkuu”
Masaa yakazidi kusonga mbele huku nikiwa siamini kabisa kwamba Martina amekufa, kwa mara kadhaa nikajikuta nikienda kwenye sehemu maalumu alipo hifadhiwa, kumuangalia kama atanyanyuka kutoka katika usingizi ila ndio hiyo hata kufumbua macho yake hawezi. Uhodari wake na kujitoa kwake kote kumeishia hapa.
“Samahani kwa kukusumbua”
Daktari aliye muhudumia alizungumza huku akiingia akirudishia mlango wa chumba hichi maalumu cha kuhidadhia maiti.
 
“Kwenye nguo za Martin tumeikuta hii karatasi, nina imani kwamba ni ujumbe wako”
Daktari akanikabidhi karatasi hii iliyo kunjwa vizuri, kisha akatoka chumbani humu. Taratibu nikaifungua na kuanza kuisoma humu ndani.
{Dany kaka, ninajua utaumia sana kuona siku moja nikiwa nimeondoka duniani. Ninautambua upendo wako mkubwa unao zidi kuuonyesha kwangu mimi. Leo hii roho yangu imekuwa ni nzito sana, sijui kama siku ya leo kama nitaimaliza. Ninawaona rafiki zangu wa boko haramu wakiniita niwafwate kule walipo, natamani kubaki na wewe, ila muito wao ni mkubwa sana……}
Nikajikuta nikimwagikwa na machozi yaliyo anza kuidondokea karatasi hii, nikajifuta kisha nikaendelea kuisoma.
 
{……Sina jinsi kaka itabidi niondoke nikuache peke yako. Sijui ni kwa nini ninajikuta ninaandika maneno haya ila moyo na hisia zangu zinanisukuma kuandika hivi. Sijawahi kufanya kazi na mtu cheshi kama wewe, japo watu wa nje wanakuchukualia wewe vibaya, ila kusema kweli nimefurahi sana kufanya kazi kwako. Umenifanya niwe mahiri, japo ilikuwa ni hatari ila hukusita kunitetea na kunielekeza nini cha kufanya pale nilipo hitajika kufanya hivyo. Bro walinde watu wako, hakikisha maadui zako unawamaliza wote na baada ya hapo kaka mrudie Mungu wako, kwani yeye ndio atakuwa muamuzi wa mwisho pale siku ya mwisho itakapo wadia. Ninakuependa sana kaka Dany na Mungu azidi kukulinda. Amen}
 
Kijikatuni kidogo alicho kichora Martin hapa chini ya barua yake kinachomuonyesha amenipigia saluti kikanifanya nizidi kulia kwa uchungi tena kwa sauti ya juu sana. Kusema kweli kutoka moyoni mwangu, kifo cha Martin kinaniuma sana. 
 
Hadi kunapambazuka sijapata hata lepe la usingiza zaidi ya kukaa pembeni ya mwili wa Martin ambao umechomwa sindao maalimu ya zuia kuto kuoza. Nikasimama wima, kisha nikapiga saluti huku machozi yakiendelea kunitiririka usoni mwangu. 

Nikatoka katika chumba hichi, kila msichana ninaye muona amevaa nguo nyeusi ikiashiria kwamba msiba huu umewagusa wote japo wengine. Nikaelekea chumbani mwa Livna na kumkuta akiwa amekaa kitandani, machozi uyamemjaa mwilini mwake na mkononi mwake ameshika pete ya ndoa.
 
“Japo nilichukulia ni jambo la kupita, ila pete hii inanikumbusha tabasamu lake. Kusema kweli Martin alikuwa ni mcheshi sana. Alijitoa kwa ajili yangu, japo nilimuumiza moyo wake na nikashindwa kujali hisia zake, ila bado aliona umuhimu wangu kwake.”
 
Livna alizungumza kwa sauti ya upole sana huku macho yake yote ameyaelekezea kwenye pete hii ya dahabu anayo endelea kuizungusha zungusha taratibu.
 
“Martin kusema kweli sipati mfano wake, jana aliweza kunilinda kwa kila namna kwa maana yeye ndio alikuwa mtu wa kwanza kuzinduka baada kuzima. Kusema kweli alijikaza, kupigwa risasi na kutembea nayo pasipo kuonyesha dalili yoyote ya maumivu, kusema kweli amejikaza”
 
Livna aliendelea kuzungumza, mlango ukagongwa.
“Nimesema sihitaji kusumbuliwa leo nahitaji kichwa changu kutulia”
Mlango ukafunguliwa akaingia Ester na kusimama mbele yetu.
“Kuna nini tena Ester, hujasikia nilicho kuambia?”
“Samahani mkuu ila hili swala ni muhimu sana. Ninawaomba mukaone”
“Ni nini?”
Nilimuuliza Ester huku nikinyanyuka kitandani na kusimama.
“Ni vyema tukaenda kujionea”
Hatukuwa na namna zaidi ya kutoka humu ndani, moja kwa moja tukaeleka hadi chumba cha mawasiliano. Tukamkuta K2 akiwa amesimama kwenye Tv hii, usoni mwake amejawa na tabasamu pana sana. 
 
“Nashukuru kwa kuja pole kwa msiba Dany wa huyu nguruwe wako. Ninahitaji tufanye biashara ya amani, niachie mwanangu nikupatie huyu”
K2 akamsogeza Yemi mbele yake, akamkaba kabali ya shingo na kumuweka bastola begani mwake.
“Ninawashukuru Wamarekani kwa kuniletea hii zawadi nono. Sasa ni kidonda kwa kidonda”
K2 akafyatua risasi iliyo toboa bega la Yemi na kumfanya alie kwa uchungu sana hadi nikabaki nikitetemeka mwili mzima kwa hasira kali sana.

ITAENDELEA
‘Haya sasa K2 amekabidhiwa Yemi kutoka mikononi mwa Wamarekani ikiwa ni njia ya pekee itakayo mfanya Dany kutoka mafichoni mwake... je Dany atakubali kumuachia mtoto wa K2? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
 

Rais Magufuli Akutana Na Sunil Mittal Mwenyekiti Wa Bharti Airtel Ikulu Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel  ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya kuwasili kwaajili ya mazungumzo , Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel  ( kampuni ya Simu ya Airtel ) Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Mwaluko pamoja na mwakilishi kutoka kampuni ya Bharti Airtel. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel aliyeambatana na ujumbe wake kutoka kampuni ya Simu ya Airtel pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Kabudi, Gavana wa BOT Profesa Luoga, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Mtendaji mkuu wa kituo cha Uwekezaji (TIC ) Geoffrey Mwambe  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL  Mhandisi Omary Nundu. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma taarifa ya majadiliano kutoka kwa mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya Mazungumzo yao . Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel aliyeambatana na ujumbe wake kutoka kampuni ya Simu ya Airtel pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Kabudi, Gavana wa BOT Profesa Luoga, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Mtendaji mkuu wa kituo cha Uwekezaji (TIC) Geoffrey Mwambe  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL  Mhandisi Omary Nundu, Mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Mwenyekiti wa Bharti Airtel (kampuni ya Simu ya Airtel) Bw. Sunil Mittal akizungumza na Wana habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo  yao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wana habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo  yao na Mwenyekiti wa Bharti Airtel (kampuni ya Simu ya Airtel) Bw. Sunil Mittal, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.

PICHA NA IKULU

Mahakama Yawafutia Kesi aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya na wenzake

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya na mwenzake wawili ambao ni maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon.

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo ya kutakatisha fedha.

Wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Uamuzi huo imefikiwa leo Januari 11 na Hakimu Mkazi, Salum Ally baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kueleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole akisaidia na wenzake Pendo Mangole na Patrick Mwida, amedai mahakamani hapo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.

"Taarifa hii ya kutokuendelea na shauri hili mbele ya mahakama yako, imeletwa chini kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002," amesema Ngole.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Ally alisema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo, wamekamatwa tena na kuwekwa mahabusu.

Mawakili wa Serikali Wadai Mahakama haina mamlaka kusikiliza Kesi ya muswada wa sheria ya vyama vya siasa

$
0
0
Serikali imedai Mahakama Kuu ya Tanzania haina mamlaka ya kusikiliza shauri la kupinga muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Vyama vya Siasa.

Hoja hiyo imetolewa leo Ijumaa Januari 11, 2019 na kiongozi wa jopo la mawakili wa Serikali, Wakili wa Serikali Mkuu, Mark Mulwambo, wakati akiwasilisha hoja za pingamizi la Serikali dhidi ya usikilizwaji wa shauri hilo.

Wakili Mulwambo amedai katika dhana ya mgawanyo wa mamlaka katika mihimili mitatu ya dola kila mhimili uko huru kufanya shughuli zake bila kuingiliwa na mhimili mwingine.

Amedai Katiba inalipa Bunge mamlaka ya kutunga sheria kwa mujibu wa Ibara za 63 na 64 na kwamba pia katika hiyo Ibara ya 100 inalipa Bunge kinga ya kutokuingiliwa katika utekelezaji wa shughuli zake.

Amedai  Katiba inatoa uhuru wa maoni, uhuru wa mjadala wakati wa shughuli za Bunge na kinga ya kutoingiliwa katika utekelezaji wa majukumu yake.

Pia, Wakili Mulwambo amedai kifungu cha 8(3) Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi za Binadamu na Wajibu kinaizuia Mahakama kuingilia mjadala wa muswada.

Wakili Mulwambo amedai sheria na Katiba inatoa haki kila mtu kwenda mahakamani kupinga sheria anayoona inaathiri haki zake na si muswada kwani muswada si sheria hivyo hauwezi kumwathiri mtu kwa namna yoyote ile.

"Waombaji wameleta maombi haya chini ya Ibara ya 30 ya Katiba, lakini ibara hiyo inazungumzia sheria na si muswada. Hivyo Mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza shauri Hilo.

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali, Abubakar Murisha amedai mmoja wa waombaji katika shauri hilo, Zitto Kabwe ni mbunge tena mzoefu anayezijua kanuni za Bunge.

Amedai kanuni ya 88 inampa haki mbunge kuomba muswada kusitishwa kwa muda mpaka atakapowasilisha mapendekezo yake, lakini hakuitumia fursa hiyo.

Amedai ingawa wadai wengine, Joran Bashange na Salim Bimani si wabunge lakini kanuni za Bunge zinawapa nafasi ya kutoa maoni yao.

Upande wa Serikali bado unaendelea kutoa hoja zake huku mawakili hao wakipeana zamu, kabla ya mawakili wa waombaji kijibu hoja hizo.

Breaking News: Bharti Airtel waongeza hisa za Serikali katika Airtel Tanzania kutoka 40% hadi 49%.

$
0
0
Kampuni ya Bharti Airtel imekubali kuongeza hisa zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania katika kampuni ya Airtel Tanzania kutoka asilimia 40 hadi 49.

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa Januari 11, 2019 katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa baada ya mazungumzo kati ya Rais John Magufuli na mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel Sunil Mittal, waliokutaka Ikulu Dar es Salaam.

Wawili hao wamezungumzia maendeleo ya mazungumzo ya umiliki wa hisa za kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya mazungumzo hayo Mittal amesema kampuni yake imekubali kuongeza hisa zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania katika kampuni ya Airtel Tanzania kutoka asilimia 40 hadi asilimia 49.

Kwa uamuzi huo umepunguza  hisa zilizokuwa zikimilikiwa na Bharti Airtel kutoka asilimia 60 hadi asilimia 51.

Kwa upande Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika mazungumzo hayo pamoja na kuongeza hisa za Serikali katika umiliki wa Airtel Tanzania.

Kampuni hiyo imekubali kutoa gawio kwa Serikali ya Tanzania mara baada ya mazungumzo hayo kukamilika hivi karibuni.

“Masuala mengine ya kumalizia mazungumzo haya yataendelea leo ili kumalizia, lakini jambo zuri ni kuwa sasa wamekubali kutoa gawio kwa Serikali ambapo kwa muda wa miaka minane hadi kumi tulikuwa hatujapata gawio,” amesema Magufuli.

“Kiasi cha asilimia za gawio nacho watajadili leo, kwa hiyo mimi naona huu ni mwanga mzuri wa kwenda mbele kati ya kampuni ya Bharti Airtel na Serikali ya Tanzania pamoja na kampuni zingine.”

Timu ya majadiliano na kampuni ya Bharti Airtel inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa  Palamagamba Kabudi.

LIVE: Rais Magufuli akiipokea ndege mpya Airbus A220- 300. Tazama Hapa

$
0
0
LIVE: Rais Magufuli akiipokea ndege mpya Airbus A220- 300. Tazama Hapa

Askofu Zakary Kakobe Ammwagia SIFA Rais Magufuli Ujio wa Ndege Mpya

$
0
0
Askofu Mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship (FGBF), Zakary Kakobe, ameweka wazi kukoshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kwa kuweza kuingiza ndege nyingine ya Air Bus 220-300.

Askofu Kakobe ameyasema hayo leo katika mapokezi ya ndege ya sita zilizoingizwa nchini katika awamu ya uongozi wa Rais Magufuli.

Kakobe ametumia nafasi yake ya kuliombea taifa kutoa maneno hayo. 

“Mheshimiwa Rais mimi huwa ni mbishi kidogo na ukiniona nimekanyaga mahali kama hapa ujue umenikosha na sijui kama kuna watu wengine wamekoshwa kama Kakobe kwa ajili ya haya yanayotendeka,” amesema Askofu Kakobe huku akishangiliwa na umati wa watu waliojitokeza

“Na wengine wanasema mnamwabudu na kumsifu wakati hata Biblia inasema anayestahili heshima apewe heshima, hivyo unastahili zote.”

Askofu Kakobe amesema suala la kuwakusanya watu wote bila kujali itikadi huo ndio uzalendo unaotakiwa.

Amesema, “Ukiona hizi shangwe na vigelegele japo sio wote wanaokusifu ujue kuna watu wanashangilia kazi zako na leo tunakusihi ujipongeze, ulale na ujue wapo watu wanakushangilia kwa kazi zako.”

CHADEMA Watoa taarifa 'kupotea' kwa kiongozi wa BAVICHA

$
0
0
Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa chama hicho (BAVICHA) Wilaya ya Ilala, Michael Kapama hajulikani alipo.

Chadema wameeleza mara ya mwisho Kapama kuonekana ni Januari 6 mwaka huu.

Polepole: "Ni dhambi kuchukua sifa isiyo yako, Aliyesimamia Swala la Kikokotoo ni Rais Magufuli na Siyo Bulaya"

$
0
0
Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi -CCM Humphrey Polepole  amepinga suala la Mbunge wa Bunda Mjini kutambuliwa na kupewa sifa kwamba aliwatetea wafanyakazi juu ya mafao kwa kipinga hadharani kikokotoo kipya na badala yake itambuliwe serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli.

Polepole amesema kwamba aliyesimama na jambo la kikokotoo tangu mwanzo ni serikali ya CCM na aliyehitimisha jambo hilo ni Rais Magufuli mwenyewe.

Ameongeza kwamba Rais Magufuli baada ya kusikiliza maoni ya wawakilishi na baadhi ya viongozi wa wafanyakazi akaamua kufanya maamuzi ambapo pia aliweka utaratibu na utaratibu huo umeshaanza kufanya kazi.

"Ni dhambi kuchukua sifa ambayo si yakwako. Siyo kweli kwamba ni yeye, aliyesimama na jambo hili, tangu mwanzo ni serikali ya CCM na aliyehitimisha jambo hilo ni Rais Magufuli mwenyewe. Maoni na mitazo ilikuwa mingi, ni haki ya kila mtanzania kila mmoja ana uhuru wa maoni. CCM inaheshimu uhuru hatutashangaa kila mtu akiweka maoni hadharani.

Mwezi Novemba mwaka uliopita, Spika wa bunge alimsifu Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA), Ester Bulaya, ambaye pia ni Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), aliyeibua suala kutumika kwa kanuni mpya kwenye mafao ya wastaafu.

Bulaya aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kikokotoo hicho kipya kilichotungwa na serikali ni kitanzi kwa wastaafu kwa kuwa hawatanufaika na fedha zao ambazo wamezitolea jasho kwa miaka mingi.

Baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi, Rais Magufuli alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), vyama shiriki, watendaji wakuu wa mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PSSSF na NSSF na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) Desemba 28, aliagiza kikokotoo kilichokuwa kikitumika awali kieendelee katika kipindi cha mpito mpaka mwaka 2023.

Mwanaume Aliyempa Mimba Binti wa Mtoto Aliyefungiwa Kabatini Atiwa Mbaroni

$
0
0
Kijana anayedaiwa kuzaa na msichana wa kazi aliyedai mwanaye wa miezi mitano alikuwa akifungiwa kabatini na mwajiri wake tangu alipozaliwa, amekamatwa na polisi mkoani Dodoma.

Kijana huyo, Salum Waziri, amekamatwa baada ya agizo lililotolewa na mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.

Katambi alisema Waziri amekamatwa kwa tuhuma za kumpa ujauzito Neema Matimbe ambaye ana miaka 15, ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani wa mwalimu, Anitha Kimako.

Alisema pamoja na tuhuma zinazomkabili Anitha kuwa alimfungia kabatini mtoto wa binti huyo, kulikuwa na ulazima wa kumsaka kwanza baba mzazi wa mtoto yuko kwa sababu alifanya kitendo hicho kwa binti mwenye umri chini ya miaka 18.

Katambi alisema kijana huyo ni mkazi wa Area C alikataa mimba ya mtoto huyo.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa, William Mkonda alisema kijana huyo atafikishwa mahakamani muda wowote uchunguzi utakapokamilika.

Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Dakika Afutiwa Mashitaka

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi imewafutia mashtaka mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake wanne.

Mfanyabiashara huyo na wenzake Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif wanakabiliwa na mashtaka 198 ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni.

Washtakiwa hao wamefutiwa kesi hiyo, chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Wakili Mkuu wa Serikali, Hashim Ngole amedai mahakamani hapo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea nalo dhidi ya washtakiwa hao.

Hakimu Augustina Mmbando amesema shauri hilo lilikuja chini ya kifungu namba 91(1) cha CPA, sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Hakimu Mmbando amesema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo, wamekamatwa tena na kuwekwa mahabusu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images