Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Video: Damian Soul & Barnaba - Asante

0
0
Msanii wa muziki Bongo, Damian Soul kwa kushirikiana na Barnaba wanakukaribisha kutasikiliza wimbo wao uitwao Asante. Usikilize hapa.

Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power

0
0
Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power Kwaajili Ya Nguvu Za Kiuume Na Promix Kwaajili Ya Kuongeza Maumbile;

Kwa mwanaume aliyekamilika na mwenye Afya njema ili kumridhisha mke au mpenzi anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya Mara mbili hapo utamridhisha mpenzi wako ila ukiwa unapiga moja au mbili hapo ujue umejilidhisha wewe 

Tiba Ya Tatizo Lako Ni Dawa Hiitwayo Simpo Power No, 1; dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge vya miti shamba na unga ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja :-1 itakufanya urudie tendo zaidi ya mara tatu 
2 itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-20 kwa tendo la Kwanza 
3 huimarisha uume uliolegea na kusinyaa 

Je Una Mke Au Mpenzi Aliyebalikiwa Kuwa Na Kario Kubwa Au Mwili Mnene Na Wewe Mume Wake Una   Maumbile Mafupu?; tumia sasa dawa ya PROMIX dawa itakufanya umfikishe shemu nyeti maana inaboresha maumbile saizi upendayo.

Dawa zangu haziina madhara yoyote kwa mtumiaji 

MARKSU; ni dawa ya kisukari dozi siku 21 
MWARU; ni dawa ya uzazi,hufungua milija ya uzazi ata kwa Wale waliofungiwa uzazi  
MTUNDUU; ni dawa ya busha bila kupasua 
MAZANZA; ni dawa ya kisukar zipo dawa za miguu Kuuma,tumbo,kupunguza Matiti,kutoa minyama uzembe ngiri,vidondo vya tumbo  

FIKA OFISINI KWANGU BUGURUNI MALAPA KARIBU NA KOTA ZA POLISI AU PIGA  SIMU ULETEWE MAHALI ULIPO SIMU NO : 0783185060 au 0752348593  -DR AGU

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaagiza Vicoba, Saccos kuwasilisha taarifa wiki ijayo

0
0
Waendeshaji wote wa taasisi ndogo za fedha nchini vikiwamo Vicoba na Saccos, sasa watakuwa wakifanya shughuli zao chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuanzia wiki ijayo, watatakiwa kuwasilisha baadhi ya nyaraka.

Novemba 16, mwaka jana, Bunge lilipitisha Sheria ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 kwa lengo la kusaidia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya 2017.

Desemba 31, mwaka jana, BoT ilitoa taarifa kwa umma ikiwataka watu wote wanaofanya biashara ya huduma ndogo za kifedha kuwasilisha taarifa zao za uendeshaji na wasimamizi wa taasisi hizo kwa chombo hicho cha juu katika usimamizi wa sekta ya fedha kabla ya Januari 11.

“Watu wote wanaofanya biashara hiyo katika sekta ndogo ya fedha wanapaswa kuwasilisha cheti cha kutambuliwa kama wamiliki, leseni ya biashara iliyotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara (Brela), leseni na anuani ya mahali biashara ilipo na mawasiliano,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Pia, iliyataja mambo mengine yanayopaswa kuwasilishwa kuwa ni ya aina ya huduma zinazotolewa na taarifa endapo kuna ukaguzi wa hesabu unaofanyika kila mwaka sambamba na orodha ya wamiliki wa biashara, bodi ya wakurugenzi, mtendaji mkuu wa taasisi na uraia wao.

Kadhalika, taarifa kuhusu mfumo unaotumika katika uhifadhi wa fedha na teknolojia ya mawasiliano pamoja na taarifa za vitega uchumi, madeni na thamani ya hisa za kila mmiliki.

Aidha, katika sheria hiyo mpya katika kifungu chake cha 12 pamoja na mambo mengine, imeipa mamlaka BoT kutoa leseni, kusimamia na kudhibiti sekta ya taasisi ndogo za fedha na kifungu cha 16 kimezuia mtu ambaye hana leseni kujihusisha na biashara hiyo.

Ofisi ya TRA Kigoma Yamchefua Waziri Jafo

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amefadhaishwa kwa kukosekana kwa afisa wa TRA katika Kituo cha Kibiashara cha Pamoja ambacho lengo lake ni kurahisisha shughuli za kibiashara kwa wananchi wa Wilaya ya Kigoma kwa kupata huduma zote za uwezeshaji wa biashara katika eneo moja.

Licha ya kuwepo kwa kituo hicho kilichojengwa na kukamilika tangu miezi sita iliyopita lakini afisa kutoka TRA anakosekana licha ya ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Ujiji kufanya mawasiliano na TRA kwa miezi sita hadi sasa.

Kituo hicho ni miongoni mwa miradi kadhaa iliyo chini ya mradi wa Local Investment Climate(LIC) unao ratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Kutokana na hali hiyo waziri Jafo ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Kigoma kufanya ufuatiliaji wa haraka ndani ya siku nne ili kituo hicho kiweze kuwa na Wadau wote wa kutoa huduma na wananchi waweze kupata huduma ya kuanzisha na kuratibu biashara zao kwa haraka.

Inadaiwa kwamba TRA walishafika kituoni hapo na kuahidi kuleta Afisa mmoja lakini hadi leo bado jambo hilo halijafanyika hivyo kuleta usumbufu kwa wafanya biashara wanaohitaji huduma kutoka katika kituo hicho.

Diamond Asogeza Mbele Siku ya Ndoa Yake

0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka kuhusu mipango yake ya kuoa.

Diamond akizungumza na Wasafi TV amesema kuwa tarehe waliyopanga awali kwa ajili ya ndoa wameisogeza mbele kutokana anataka harusi yake iwe nzuri na kuhudhuriwa na watu wengi.

"Ndoa yangu ilitakiwa iwe siku ya Valentine tarehe 14 lakini tumeipeleka mbele. Watu wengi wanatakiwa kuja kuhudhuria kwa sababu ndoa yangu watakuja kina Rick Ross," amesema Diamond.

Kwa sasa Diamond Platnumz yupo mapenzini na mrembo Tanasha kutoka nchini Kenya, bado haijajulikana iwapo atamuoa mrembo huyo.

Waziri Mkuu Majaliwa apiga marufuku kusafirisha kahawa ya maganda Nje ya Nchi.....Minada ya kahawa sasa kufanywa kikanda

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema hakuna kahawa itakayoruhusiwa kuuzwa nje ya nchi kabla ya kukobolewa, kwa lengo la kuiongezea thamani kabla ya  kuingizwa sokoni.

Pia, Waziri Mkuu ameziagiza halmashauri zinazolima kahawa nchini kuwa na kitalu chenye miche zaidi ya laki mbili ifikapo mwisho wa mwezi wa pili mwaka huu.“Wakati utakapofika uongozi wa Wizara ya Kilimo utakwenda kukagua iwapo agizo hili limetekelezwa’’.

Aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akizungumza na wadau wa kahawa wa mkoa wa Ruvuma kwenye ukumbi wa Jimboni wilayani Mbinga.

Waziri Mkuu alisema kuanzia sasa kahawa yote itakayozalishwa nchini ni lazima iongezewe thamani na hakuna kahawa yenye maganda itakayoruhusiwa kuuzwa nje ya nchi.

“Hairuhusiwi kutoa kahawa nchini na kuiuza nje ya nchi ikiwa bado na maganda, ni lazima iongezewe thamani ndipo ipelekwe katika masoko ya nje ya nchi ili iuzwe kwa bei nzuri.

Hatua hii itasaidia kuongeza mnyororo wa thamani na kusaidia kulinda uwekezaji wa viwanda uliofanyika nchini’’

Akizungumzia kuhusu madeni ya wakulima, aliagiza watendaji wote wa AMCOS waliohusika watafutwe na walipe deni. 

“Kwa sasa Serikali haina taratibu za kununua madeni ya chama chochote cha ushirika. Kuendelea na utaratibu huo kunachochea viongozi wa ushirika kufuja mali za ushirika. Lazima watambue ukifuja fedha za wanaushirika , Serikali iko na wewe.”

Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitorudi nyuma katika msimamo wake wa kuwasimamia wakulima nchini ili nao waweze kunufaika na kazi kubwa wanazofanya.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaagiza viongozi wa AMCOS wahakikishe wakulima wote wanasajiliwa na taarifa zao ikiwemo ukubwa wa mashamba,kiasi cha uzalishaji na mahali walipo zinatunzwa vizuri katika kompyuta.

Pia, Waziri Mkuu alimuagiza Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Ruvuma akague AMCOS zote na kujiridhisha kama ziko hai na kwenye tatizo la uongozi aitishe uchaguzi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema minada yote ya kahawa itafanyika kwenye maeneo yanayolima ambayo yamegawanywa kwa kanda 1.Moshi (Kilimanjaro,Arusha,Tanga,Manyara) 2. Kagera ( Kigoma, Geita, Kagera, Mara) 3. Songwe ( Rukwa,Mbeya,Iringa,Katavi), na Mkoa wa Ruvuma utafanyika Mbinga

Alisema lengo ya kufanya minada hiyo katika maeneo yanayolima kahawa ni kuongeza uwazi katika biashara hiyo na kuwawezesha wakulima kujua bei ya mnada na kulipwa kwa wakati. Mkulima anaruhusiwa  kupeleka kahawa katika mnada wowote nchini ilimradi azingatie sheria na taratibu husika

“Kila kanda inayolima kahawa nchini itakuwa na maeneo yake ya kuuzia kahawa na kahawa ya Mbinga itauzwa katika minada itakayofanyika Mbinga na bei kila mtu ataijua siku hiyo.”

Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuimarisha kilimo cha zao la kahawa ili kila mmoja anayehusika na zao hilo akiwemo mkulima aweze kunufaika na kuongeza tija.

Kwa upande wao, wadau walifurahishwa na uamuzi wa Serikali wa kulisimamia zao kwa ukaribu na hasa baada ya kutangaza minada yote ya kahawa kufanyika katika maeneo yao na kwa uwazi.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Jux Na Mbosso Wasikilizwa Zaidi 2018.

0
0
Application ya Boomplay inafahamika kuwa chanzo kikubwa cha ukuaji wa muziki katika bara la Afrika na mnamo mwaka 2017 boomplay app iliweza kujinyakulia tuzo ya application bora ya muziki barani Afrika kupitia kipengele cha “App Afrika award” ikiwa imewafikia watu million 38 ulimwenguni kote na million 3 kwa Tanzania tu.

Kwa wapenzi wa muziki Application ya boomplay inapatikana kiuraisi ikiwa imepakuliwa katika simu za Android kama vile TECNO, Infinix na itel au unaweza kupakua kupitia google play store.
Application ya boomplay imeweza kusaidia wapenzi wa muziki kupakua/kusikiliza nyimbo mpya kwa wepesi zaidi lakini pia imeweza kulinda masilahi ya wasanii wetu kwa kuweza kutambua kiasi cha fedha msanii alichoingiza kupitia mauzo ya nyimbo katika kipindi Fulani.

Na kwa mwaka 2018 boompay imezalisha nyimbo million 833 na takribani nyimbo 30,000 zikiwa mbioni kuingia katika application ya boomplay kutoka kwa wasanii mbalimbali na kupitia takwimu za boomplay inaonyesha wasanii kama Vanessa Mdee, Nandy, Jux, Aslay, Mbosso, rayvanny, Harmonize kuwa miongoni mwa wasanii waliosikilizwa zaidi barani Afrika.

Boomplay mpaka sasa imefanikiwa kufanya kazi na makampuni mengine kama vile Universal music, Kudos, Tunicore na Africori na iko mbioni kuzindua application ya iOS.



Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) lawafutia matokeo wanafunzi kwa kuandika matusi

0
0
Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), limetangaza matokeo ya mitihani ya taifa ya darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika kuanzia Novemba 23, mwaka jana na limewafutia matokeo wanafunzi tisa baada ya kuandika matusi.

Akizungumza jijini hapa jana, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, alisema ufaulu wa watahiniwa umeongezeka kulinganisha na mwaka juzi.

Pia alisema katika matokeo hayo hakuna shule ya Serikali iliyojitokeza katika shule 10 bora zilizofanya vizuri.

Huku katika matokeo ya kidato cha pili, jumla ya wanafunzi 47 walifutiwa matokeo yao yote kutokana na udanganyifu, kati yao tisa kutokana na kuandika matusi katika karatasi zao za majibu.

“Kwa hawa wanafunzi tisa walioandika matusi kwenye skripti zao tumeziagiza bodi za shule wanakotoka wawachukulie hatua za kinidhamu ili tukio hilo lisijirudie tena kwa sababu bodi za shule ndizo zenye mamlaka ya kutoa adhabu kwa wanafunzi,” alisema Msonde.

Pia alisema limewafutia matokeo kwa mujibu wa kifungu cha 17(1) kinachokataza mwanafunzi kuandika matusi katika karatasi yake ya majibu.

Alisema jumla ya watahiniwa 506,235 wa kidato cha pili walisajiliwa kufanya mtihani sawa na asilimia 92.87 huku wanafunzi 38,842 sawa na asilimia 7.13 hawakufanya mtihani kutokana na ugonjwa na utoro.

Alisema matokeo ya mtihani huo yanaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 452,273 sawa na asilimia 89.68 wamepata alama za ufaulu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu huku 52,073 sawa na asilimia 10.32 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

“Mwaka 2017 wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 89.32 walipata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu, hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.36,” alisema.

Alizitaja shule kumi zilizofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili kuwa ni St Francis Girls ya Mbeya, Thomas More Machrina ya Dar es Salaam, Bright Future Girls ya Dar es Salaam, St. Monica Moshono Girls ya Arusha, Bethel Sabs Girls ya Iringa, Centennial ya Pwani, St. Augustine-Tagaste ya Dar es Salaam, Anwarite Girls ya Kilimanjaro, St. Mary’s Ulete ya Iringa na St. Aloysius Girls ya Pwani.

Huku shule 10 za mwisho kitaifa kuwa ni Ocean ya Mtwara, Mdando ya Tanga, Kwashemshi ya Tanga, Miteja ya Lindi, Thaqalain ya Dar es Salaam, Korona ya Arusha, Imbafi ya Dodoma, Magindu ya Pwani, Mashindei ya Tanga na Luagala ya Mtwara.

Katika matokeo ya darasa la nne, alisema kati ya watahiniwa 1,302,461 sawa na asilimia 95.58 waliofanya mtihani huo na kufaulu kwa kupata daraja A, B, C, na D ni 1,213,132 sawa na asilimia 93.16 huku 89,093 sawa na asilimia 6.84 wamepata daraja E lenye ufaulu usioridhisha.

“Hata hivyo, jumla ya watahiniwa 151 wamefutiwa matokeo yao yote baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika upimaji wa kitaifa kwa mujibu wa kifungu 32 (2) (b) cha kanuni za mitihani.

“Baraza limezishauri mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kusababisha kutokea kwa udanganyifu katika upimaji wa darasa la nne kwa mujibu wa kanuni za utumishi na sheria za nchi,” alisema.

Pia alisema ufaulu umeongezeka kulinganisha na mwaka 2017 kwa kuwa matokeo ya jumla ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kwa mwaka 2018, yanaonyesha wanafunzi wamefanya vizuri kutokana na takwimu za matokeo zinaonyesha kuwa ufaulu wa watahiniwa kwa masomo yote uko juu ya wastani.

Pia alisema ubora wa ufaulu umezidi kuimarika kwa kuwa watahiniwa waliofaulu kwa daraja la A, B, na C wameongezeka kwa asilimia 0.03 ukilinganisha na mwaka 2017.

Huna Sababu ya Kuabika Tena, Jipatie Dawa Bora ya Nguvu za Kiume, Maumbile Madogo na Mvuto wa Mapenzi

0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiathiri watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine ....kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapungufu katika mwili wake.

Kuna sababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huathiri misuli ya uume, 


Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0620510598  / 0743543944

Kanisa Katoliki lafichua jina la mshindi wa urais DRC

0
0
Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Cenco), lenye ushawishi mkubwa  nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limesema linafahamu aliyeshinda uchaguzi wa rais ambao ulifanyika Desemba 30 mwaka jana na kuomba Tume ya Uchaguzi (CENI) kutangaza matokeo katika mazingira huru, haki na ukweli.

Baraza hilo limetoa baada ya tume ya uchaguzi kutangaza kwamba italazimika kuchelewa kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita kutokana na hitilafu za kimitambo.

Kanisa hilo limesema sampuli ya wawakilishi ilichapishwa katika vituo vya kupigia kura ambavyo vinawaruhusu kujua jina la rais aliyechaguliwa. Sampuli hiyo ni ya vituo zaidi ya 23,000 kati ya vituo 70,000 vilivyowekwa na Ceni nchini humo.

Akizungumza na vyombo vya habari nchini humo, msemaji wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Padri Donatien Nshole, amesema si jukumu lao kutangaza matokeo, bali wao ni waangalizi lakini wanafahamu nani aliyechaguliwa na wananchi.

“Ni muhimu kusisitiza kuwa kasoro zilizojitokeza haziwezi kuathiri kwa kiwango kikubwa chaguo la wananchi wa DRC walioonyesha wazi katika uchaguzi wa urais wa Desemba 30. Cenco imeitaka Tume ya Uchaguzi (Ceni) kama taasisi inayounga mkono demokrasia kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa heshima ya ukweli na haki,” amesema Padri Nshole.

Msemaji huyo amekuwa anawasilisha ripoti ya awali ya ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi wa Tume ya Haki na Amani ya Cenco, ambayo inasema kuwa ilikuwa na waangalizi 40,000 siku ya uchaguzi mkuu.

Uchaguzi huo utapelekea kumpata mrithi wa Rais Joseph Kabila, ambaye hakuruhusiwa kuwania muhula wa tatu kulingana na Katiba.

Mwanzoni mwa wiki hii Tume ya Uchaguzi, Ceni ilisema itatangaza matokeo ya awali Januari 6, mwaka huu, kabla ya siku chache baadaye kubadili kauli kuwa huenda zoezi hilo litaahirishwa.

Raia nchini DRC bado wanasubiri kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo. Hali ya wasiwasi bado inaendelea, huku huduma ya intaneti ikiendelea kufungwa na mitambo ya radio ya kimataifa ikizimwa. Wakati huo Ceni imesema tayari imehesabu asilimia 20 tu ya kura zilizopigwa.

Kwa upande wake Serikali ya Marekani imeiomba Ceni kutangaza matokeo sahihi na kusema yeyote atakayekwenda kinyume na demokrasia ya nchi hiyo atawekewa vikwazo. Marekani pia imeitaka Serikali ya Congo kufungua mtandao wa intaneti na kuondoa vikwazo kwa vyombo vya habari.

Shirika la utangazaji la Ufaransa, RFI, ambalo lina wasikilizaji wengi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, linasema mwandishi wake, Florence Morice, alilazimika kuondoka nchini humo baada ya kibali chake cha kufanya kazi kufutiliwa mbali.

Uongozi wa DRC kupitia Waziri wa mawasiliano, Lambert Mende, unalituhumu shirika hilo kwa kuleta utata baada ya kutangaza matokeo yasiyo rasmi madai ambayo shirika lenyewe limekanusha.

“Ni muhimu kufahamu kwamba chini ya sheria za Congo, ni Ceni pekee yenye mamlaka ya kuandaa uchaguzi na kutangaza matokeo,” alisema Mende.

Nalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilitarajiwa kufanya mkutano wa faragha kujadili uchaguzi wa DRC. Mkutano huo umeitishwa na Serikali ya Ufaransa, wakati ambapo mataifa yenye nguvu duniani yanasubiri matokeo ya uchaguzi huo.

Tume ya uchaguzi imepanga kutangaza matokeo kamili Januari 15 na rais aliyechaguliwa ataapishwa siku tatu baadaye.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Wenzake Wamchukiza Waziri Mkuu.....Awataka Waripoti Ofisini Kwake Tarehe 7 Asubuhi

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote zinazozalisha nguzo za umeme katika mkoa huo kufika ofisini kwake ili waeleze sababu za kuzuia nguzo hizo zisitoke.

“Wanieleze kwa nini wanazuia nguzo,Wakati wananchi wanasubiri kuunganishiwa huduma ya nishati ya umeme wao wanazuia nguzo wanasubiri posho, Wanaidai Serikali wakati ni wao ni sehemu ya Serikali Tutakutana ofisini kwangu Januari 7, saa tano kamili asubuhi.”

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji Nyoni, wilayani Mbinga akiwa katika siku ya tatu za ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma. Alisema jambo hilo linakwamisha zoezi la usambazaji umeme.

Aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walilalamikia kitendo cha kutofikishiwa huduma ya umeme katika maeneo yao kutokana na kukosekana kwa nguzo ambazo zimezuiwa kwa sababu ya wahusika wanaidai Serikali posho.

Waziri Mkuu alisema viongozi wengine watakaokuwepo kwenye kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, Wenyeviti wa halmashauri hizo zilizozuia nguzo ili wamueleze sababu za kuzuia nguzo hizo.

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli iAlisema Serikali imedhamiria kusambaza huduma ya nishati ya umeme katika vijiji vyote nchini vikiwemo na wananchi hao wataunganishiwa umeme huo kwa gharama ya sh. 27,000 tu.

Pia Serikali imeondoa gharama za kulipia nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali na kwa vijiji ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo linalenga kufungua fursa za ajira na kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa.

Serikali imefanya maamuzi hayo kwa sababu huduma hiyo ya umeme ni muhimu kwani mbali ya kutumika katika matumizi ya majumbani, pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni itawezesha zahanati, shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JANUARI 5, 2019.

Waziri Mkuu Anusa Ufisadi Ukarabati Wa Jengo Songea.....Ni La Wajawazito Wanaosubiri Kujifungua, Limegharimu Sh. Milioni 129

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amenusa harufu ya ufisadi katika mradi wa ukarabati wa jengo la mama na mtoto  katika Hospitali ya Rufaa  ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO) na amesema kwamba hajaridhishwa na kiasi ya sh. milioni 129 zilizotumika.

Hivyo, amemuagiza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile afuatilie suala hilo ili kumbaini mtu ambaye amehusika katika kupitisha zabuni ya ukarabati wa jengo hilo na kisha kumpelekea taarifa.

Waziri Mkuu amenusa harufu ya ufisadi katika mradi huo leo (Jumamosi, Januari 5, 2019) wakati alipotembelea hospitali hiyo na kukagua ukarabati wa jengo la akinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua (mama ngojea) ambalo umegharimu sh. milioni 129.

“Sijaridhishwa na gharama za ukarabati wa jengo hilo kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika kwani Serikali inajenga vituo vya afya vyenye jengo la maabara, jengo la kujifungulia, wodi ya mama na mtoto, chumba cha upasuaji, nyumba ya watumishi kwa gharama za sh. milioni 400 hadi 500 sasa inawezekajane jengo moja linalokarabatiwa ligharimu kiasi hicho.”

Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma lazima azingatie maadili ya kiutumishi na kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na Serikali. Amesema Serikali imeagiza miradi ijengwe kwa kutumia force accountna kuhakikisha miradi inalingana na thamani ya fedha.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu utoaji wa huduma ya watoto waliochini ya miaka mitano zinazotolewa katika hospitali kwani baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa wakiwatoza gharama za dawa wakati wanatakiwa watibiwe bure.

Waziri Mkuu amesema hayo baada ya Kanisia Fusi ambaye amelazwa na mtoto wake katika hospitali hiyo kumueleza kwamba ameandikiwa dawa na kuambia akanunue wakati mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatakiwa atibiwe bure.

Pia baada ya Dkt. Ndungulile kuangalia cheti cha mtoto huyo alisema dawa aliyoandikiwa ipo hospitalini hapo jambo ambalo lilithibitishwa na Mganga Mfawidhi wa hopitali hiyo Dkt. Majura Magafu, hivyo Waziri Mkuu amemuagiza mganga huyo amtafute mtendaji aliyemuambia mama huyo akanunue.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezindua mpango wa usambazaji wa x-ray za kidigitali ambazo zitazambazwa kwenye hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa ili kuboresha utoaji wa huduma zinazotolewa kwa njia ya mionzi.

Waziri Mkuu amesema kwa kuanzia x-ray hizo zitasambazwa kwenye hospitali za rufani katika mikoa 11 na kisha baadae zitasambazwa kwenye hospitali zingine 20, lengo ni kuhakikisha hospitali zote za rufaa za mikoa zinakuwa na x-ray hizo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Ndungulile amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za nchini.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma za afya zinawafikia Watanzania wote karibu na maeneo yao ya makazi tena kwa gharama nafuu. ”Katika kufikia azma hii moja wapo ya kipaumbele ni kununua vifaa vya kisasa vinavyoendana na teknolojia iliyopo.”

Amesema kwa sasa wizara hiyo imenunua mashine 11 za x-ray za kidigitali zenye thamani ya zaidi ya shilingi 2,027,029,794.60 ambazo zimekusudiwa kupelekwa kwenye hospitali 11 zenye x-ray za zamani. Hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi, Morogoro, Njombe, Ruvuma, Simiyu, Singida na zingine tatu zitafungwa katika hospitali za wilaya za Chato, Magu na Nzega. 


 (mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Lugola Ampa Wiki Mbili Bosi Wa Uhamiaji Nchini Aende Mikoa Ya Kagera Na Kigoma Kufanya Operesheni Kubwa Kuwaondoa Wahamiaji Haramu Kabla Ya Uchaguzi Serikali Za Mitaa Haujanza

0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Karagwe.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa wiki mbili  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt Anna Makakara, awe amefika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Karagwe katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Changarawe mjini humo, Lugola alisema kuna idadi kubwa ya wahamiaji haramu katika mikoa hiyo, hivyo CGI na Maafisa wake wahakikishe wanawaondoa wahamiaji wote haramu kupitia operesheni kubwa niliyoitangaza.

“Nimepata taarifa na ndani zaidi na pia nyie wananchi hapa mmesema leo kuhusu uwepo wa wahamiaji haramu, ndio mana nimekuja hapa kwa ajili ya kuhakikisha wahamiaji hao wanaondolewa haraka iwezekanavyo hapa Kagera na Mkoa wa Kigoma,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, licha ya kutangaza operesheni hiyo, lakini viongozi wa uhamiaji katika mikoa hiyo wawe makini mara kwa mara kuhakikisha wanawafuatilia wahamiaji hao kwa kuwashirikisha wananchi waaminifu ili waweze kutoa taarfia sahihi za wahamiaji hao.

“Tunatarajia kufanya uchaguzi hivi karibuni mwaka huu, hivyo mnapaswa kuhakikisha watakaopiga kura ni Watanzania na sio wenginevyo ili kuepusha usumbufu mkubwa katika jamii,” alisema Lugola.

Lugola aliwataka wananchi wa mikoa hiyo watoe ushirikiano na wasiwafiche wahamiaji hao kwasababu kumuhifadhi ni kosa kisheria, hivyo wanapaswa kuhakikisjha wanatoa taarifa za wahamiaji hao kwa maafisa uhamiaji ili waweze kukamatwa.

Waziri Lugola katika mkutano huo alijibu maswali mbalimbali ya wananchi wa Karagwe yakiwemo kuhusu uwepo wa wahamiaji hao haramu ambao pia wanalalamikiwa kuwa wanatumia nguvu ya fedha kuwanyanyasa Watanzania wenye kipato kidogo.

“Pia nina taarifa za kutosha kuwa, baadhi ya maafisa uhamiaji wanapewa fedha na wahamiaji hao ili wasiweze kuwakamata, sasa ole wenu, katika Serikali hii ya Magufuli haichezewi na haijaribiwi, ole wako wewe afisa uhamiaji uingie mikononi mwangu, sitakuonea huruma na hakika nitakuondoa kazini,” alisema Lugola.

Lugola alisema wahamiaji haramu sio wakuchekewa hivyo amemtaka CGI ahakikishe anawapanga vizuri nmaafisa wake kwa kutembnea nyumba kwa nyumba kuwasaka na kuhakikisha wote wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Lugola alisema alifanya ziara katika Mkoa wa Kigoma kwa kutembelea Wilaya zote kama anavyofanya Mkoa wa Kagera, anapewa kero hiyo katika ziara hiyo, hivyo anataka Uhamiaji wawaondoa wahamiaji wote ndani ya mikoa hiyo ili Watanzania waweze kuishi kwa amani wakiendelea kujionea maendeleo ya uongozi wa Rais Dkt. Magufuli.

Waziri Lugola amemaliza ziara yake Wilaya Karagwe na Wilaya inafuata ni Kyerwa, Ngara, Biharamulo na Muleba, ambapo akiwa ziara hiyo, pia uzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara pia ukutana na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya January 6


Mbunge CHADEMA Amwangukia Rais Magufuli Kuhusu Korosho

0
0
Ndugu wanahabari nawatumia taarifa hii, kwa nia ya kufikisha kilio cha wakulima wa korosho kwa *Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk,John Pombe Magufuli* kwasababu ndio zao tegemeo la kiuchumi kwa sasa.

Kama mnavyojua mkoa wa Mtwara umekuwa ukiongoza kwa kuzalisha korosho nyingi ikifuatiwa na mkoa wa Lindi,Ruvuma na Pwani pamoja na mikoa mingine mipya ambayo inaongezeka siku hadi siku.

Mtakumbuka baada ya mvutano kati ya serikali na wafanya biashara (wanunuzi wa korosho) baadae serikali iliamua kutangaza kuzinunua korosho zote kwa Tsh.3,300/-kwa kilo.

Zoezi hili lilifanyika kwa maamuzi ya haraka kabla ya kupata ushauri wa kitaalamu lakini pia utafiti wa kina wa namna ya kufanikisha zoezi hili la ununuzi wa korosho ikiwa ni pamoja na kupata uhakika wa soko la korosho na taratibu zingine.

Hata hivyo, itakumbukwa wakati huo wanunuzi na makundi yao walishauri namna bora ya kutekeleza maelekezo hayo bila mafanikio.
 
Wakati wa kikao cha mashauriano cha Mkoa wa Mtwara (RCC) tulipokea taarifa kwamba kwa mwaka  nchi ina uwezo wa kubangua tani 20,000 tu kati tani 270,000 zinazotarajiwa kukusanywa.

Taarifa hii inapingana na taarifa ya Waziri wa viwanda  kwamba tani 100,000 zitabanguliwa na hivyo serikali sasa inatafuta wadau ili wawezi kununua ziada ya tani 150,000.

Hivyo ndugu wanahabari, nawaanfikia leo ili kutoa mrejesho wa yanayoendelea katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani kwa wakulima baada ya kufanya uchunguzi wangu binafsi kama *Mwakilishi wa Wananchi wa Jimbo la Ndanda* ambao na wao wako katika Kilio cha kutolipwa.

Ifahamike kwamba, baadhi ya wakulima wanalipwa, wale wanaizalisha zaidi ya tani 1.5 wao hawalipwi, wakiwemo makundi ya *Wazee, wajane na warithi* Ivi kuwaongezea uchungu wa maisha kwa kisingizio cha uhakiki,

*Yafuatayo ni matatizo yaliyopo kwenye tasnia ya Korosho kwa sasa*

1. Utaratibu wa malipo umekuwa wa kusuasua sana tofauti na taarifa alizopewa *Mheshimiwa Rais na Waziri Mkuu*

2. Wakati kinachodaiwa kuwa zoezi la *uhakiki* kikiendelea kuna *viashiria vya rushwa* kutoka kwa wahakiki.

3. Wakulima wamegawanywa kwa makundi makundi na hivyo kuwafanya wawe wanyonge zaidi

4. Taarifa za malipo zimekuwa za siri kiasi kwamba  hata viongozi wa vyama vya msingi hawana taarifa wala kufahamu kinachoendelea juu ya wakulima waliokusanya korosho maghalani, ivyo kuhatarisha uhai wa vyama ambavyo vitakumbwa na madeni makubwa, yakiwemo ya wabebaji na wasafirishaji.

5. Matumizi makubwa ya nguvu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama, jambo hili liko maeneo mengi, kubwa zaidi ni tukio lililotokea Nachingwea, viongozi wa vyama vya msingi wamepigwa na wanajeshi kwa kushirikiana na polisi ofisini kwa Katibu tawala (DAS), ushahidi upo na waliofanya tukio hilo wanafahamika kwa majina

6. Uwezo mdogo wa wahakiki na ujuzi kuhusiana na zao la korosho, wahakiki nao wako mafunzoni, badala ya kutekeleza wajibu

7. Malalamiko yanayotolewa chinichini kutoka kwa wasimamizi wa zoezi la uhakiki, kuhusu posho zao na stahiki nyingine, ivyo kuongeza gharama za uendeshaji, overhead cost

8.Kuna dalili zote za kutokea kwa utaifishaji wa mali za wananchi kwa kisingizio cha kukomesha biashara ya kangomba.

Swali la kujiuliza kama wauzaji wa korosho hizo hawatalipwa na korosho zao zimechukuliwa na serikali, je hii tunaita nini?
Ni kweli kwamba hakuna wachuuzi wa mazao mengine zaidi ya korosho.

Hivyo ndugu waandishi, kutokana na masuala ya msingi niliyoyataja yanaweza kuwa na athari kubwa sana kwa mwananchi mmoja mmoja lakini athari kubwa iko kwa Taifa.

*Naomba niwatajie athari chache zinazoweza kujitokeza sasa hivi na baadae....*

1. Halmashauri zetu zitashindwa kujiendesha kwa sababu zinategemea kwa kiasi kikubwa mapato yatokanayo na mazao ikiwemo korosho, mtakumbuka kwamba mbaazi haikuwa na soko zuri msimu uliopita.

2. Kuharibika kwa korosho zilizoko maghalani kwa kunyeshewa na mvua, hasa zile zilizoko mikononi mwa wakulima, na hivyo kupoteza ubora wake ambao ndio sifa kuu ya korosho ya nchi yetu.

3. Wakulima kushindwa kujimudu maisha yao ya kawaida mfano kulipia ada za watoto (private schools) na michango mbalimbali hii pia itasababisha kushuka kwa elimu,  lakini pia wakulima hawa hawa wanashindwa kuandaa mashamba yao kwa ajili ya msimu ujao, ivyo kupunguza uzalishaji, na baadae kipato kuendelea kushuka

4. Kupoteza mapato kwa serikali kwa maana ya *Export Levy na Export Revenue* hivyo kushusha thamani ya shillingi, na pia kupoteza imani kwa wafanya biashara wa nnje na wa ndani wa mazao.

5. Bidhaa kudorora madukani, hasa maduka ya vifaa vya ujenzi na vyakula kwasababu wafanyabiashara wakishajua ni wakati gani wakulima wanahitaji biadhaa fulani fulani.

7.Kujengeka kwa chuki  kati ya wananchi na serikali hasa kwa wale ambao watadhulumiwa korosho zao.

8. Kudorora kwa shughuli za maendeleo katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ambao kipindi kama hiki wananchi wanakuwa na kazi nyingi za maendeleo yao hasa ujenzi na uboreshaji wa makazi, na miundombinu mingine yakiwemo madarasa zahanati nk

Ni wakati sasa wa *Mh Rais* kutembelea mikoa ya Kusini na kuwapa wananchi nafasi ya kuzungumza ili ajionee mwenyewe ni kitu gani kinaendelea kwa lengo la kumsaidia mkulima na si vinginevyo
 
Imeandaliwa na;

*Cecil David Mwambe*(Mb)
*Mbunge Jimbo la Ndanda*

IGP Sirro Awapongeza Wastaafu Kumaliza Bila Kashfa

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amewapongeza Wastaafu wa Jeshi hilo kwa kumaliza utumishi wa umma wakiwa hawana kashfa yoyote ambayo ingelichafua jeshi hilo na kufanya lipoteze uhalali mbele ya wananchi.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Kuwaaga Askari na Wastaafu wa Jeshi na Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

“Nawapongeza kwa kumaliza salama naomba mkawe na nidhamu ya fedha mtakayolipwa kama kiinua mgongo na mtumie kiasi hicho cha pesa kwa manufaa ya familia na jamii inayowazunguka” alisema IGP Sirro

Akizungumza katika Sherehe hizo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo amewataka Wastaafu wa Jeshi la Polisi kuhakikisha wanakuwa raia wema na kudumisha amani katika maisha yao mapya baada ya kulitumikia Taifa kwa manufaa,ameongeza kuwa Upendo waliouonesha kwa wafanyakazi wenzao wakati wakiwa kazini wakauonyeshe huko wanakoenda.

“Mmekuwa mfano wa kuigwa kipindi chote mlichokua kazini, tunaomba mkawe raia wema huko kwa kuendelea kusimamia matukio ya uhalifu katika maeneo mtakayokua mnaishi, tunaamini nyie bado askari na mnafahamu mbinu zote za kupambana na uhalifu hivyo fahamuni tunawategemea bado,” alisema Jenerali Mabeyo.

Maafisa na Askari Wastaafu wa Jeshi la Polisi walioagwa katika sherehe hizo walilishukuru Jeshi la Polisi kwa upendo walioupata katika kipindi cha utumishi kwa umma na kuwaasa maafisa na askari walipo kazini kulitumikia jeshi kwa uaminifu mkubwa.

Marekani Yapeleka Wanajeshi Gabon ili Kukabiliana na Machafuko yoyote yanayoweza Kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

0
0
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema nchi yake imewapeleka wanajeshi 80 mjini Libreville, Gabon kuwalinda raia wa Marekani na ubalozi wa Marekani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Katika barua aliyowasilisha Bungeni jana, Trump alisema wanajeshi Zaidi huenda wakapelekwa katika eneo hilo kutokana na uwezekano wa kuzuka maandamano yenye ghasia.
 
Barua ya Trump imesema wanajeshi hao: “watabaki katika eneo hilo hadi hali ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utakapokuwa imara na uwepo wao usihitajike tena.”
 
Mwishoni mwa wiki Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni ya Marekani ilitoa wito kwa Tume ya Uchaguzi – CENI kuhakikisha kuwa kura zinahesabiwa kwa umakini na kutishia kuwawekea vikwazo watakaohujumu mchakato huo au kutishia Amani na utulivu wa nchi hiyo.
 
Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika ziliiongezea mbinyo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zikiitaka iheshimu matakwa ya wapiga kura wakati muda wa mwisho wa kutoa matokeo ukikaribia.
 
Kuna ongezeko la matarajio kuwa wasimamizi wa uchaguzi watachelewesha matokeo ya mwanzo yanayotarajiwa Jumapili – hatua inayoweza kuongeza hofu katika nchi hiyo isiyokuwa na utulivu.
 
“Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iko katika wakati wa kihistoria kuelekea mpito wa kidemokrasia,” umesema Umoja wa Ulaya. 
 
Umetoa wito kwa maofisa kuhakikisha mat okeo yananayosubiriwa yatatimiza matakwa ya wapiga kura. 

Ombi sawa na hilo limetolewa na Umoja wa Afrika – AU baada ya kupewa tathmini kutoka kwa mkuu wa timu ya uangalizi wa uchaguzi yenye wanachama 80.

“Ni muhimu kuheshimu matokeo ya uchaguzi,” amesema mkuu wa AU Faki Mahamat kwenye Twitter.
 
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana katika kikao cha faragha kuujadili uchaguzi huo, lakini baada ya masaa mawili ya mkutano likashindwa kukubaliana kuhusu taarifa kwa vyombo vya habari. 

Wanadiplomasia wamesema nchi kadhaa yakiwemo mataifa ya Kiafrika yalisema hatua ya aina hiyo itakuwa ya mapema mno.

RC Makonda Ataka Watendaji Kuongeza Kasi Ya Makusanyo Ya Kodi Pasipo Kuwasumbua Wananchi

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makusanyo ya kodo ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mpya na rafiki za ukusanyaji pasipo kuwatisha wala kuwabugudhi wananchi.

RC Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa kikao mkakati baina yake ya mamlaka za ukusanyaji wa kodi ambapo amesema mwaka huu jiji hilo limedhamiria kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ili kuendelea kuwa kinara.

Aidha RC Makonda amewataka watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuongeza idadi ya walipa kodi, kufanya mabadiliko ya sheria kandamizi zilizopitwa na wakati pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo kwa kadi Kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Pamoja na hayo RC Makonda ameshauri kuanzisha kwa kitengo cha ushauri kwa wafanyabiashara jambo litakalowajengea wananchi hamasa ya kulipa kodi na kuondoa dhana ya kuonekana ni watu wa kukusanya mapato pekee.

RC Makonda anaamini kuwa wananchi wapo tayari kulipa kodi serikalini endepo watawekewa mazingira rafiki ya kuwawezesha kulipia ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kuwekwa katika data base moja.

Kikao hicho kimehusisha wakuu wa wilaya, makatibu tawala, TRA, BOT, TIC, NBS, Wizara ya fedha na kamati za ulinzi na usalama.

Jipatie Dawa ya Asili ya Kupunguza Maziwa, Kupunguza Tumbo,Kuongeza Unene, Kuongeza Maumbile ya Kiume na Kuondoa Chunusi

0
0
Anza mwaka 2019 na mambo mapya kutoka kampuni ile ile inayofanya vizuri TANZANIA na nchi za NJE ambayo ni @natural_beauty_prod.

           BADO TUNATOA OFFA KAMA IVI👇👇👇
1. SHARK POWER--Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 7.5 ilikua inapatikana kwa @170,000/= sasa ni @160,000/= tu

2.VIGA 84000---Hii dawa ya kuspray yenye uwezo mkubwa wa kuchelewesha wakati wa tendo la ndoa ilikua ni  @160,000/=. Sasa ni 150,000/= tu

3. HANDSOME UP ORIGINAL-- Hichi ni kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo wewe pamoja na kuimalisha misuli kifaa hichi kilikua kinapatikana kwa @230,000/=. Sasa ni 210,000/= tu

4. MAXMAN CAPSULE--- Hii ni dawa ya vidonge ya kuongeza uume urefu na upana pamoja na kuongeza nguvu za kiume kwa wiki mbili ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/= tu

5. VIG RX---- Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 10 ilikua inapatikana kwa @190,000/=. Bei ya sasa ni 170,000/=

6. BODY BOOSTER---Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri ilikua inapatikana kwa @150,000/=. Sasa ni 140,000/=

7. BOTCHO MULT PLUS-- Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza (hips mapaja na makalio) kwa size uipendayo ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/=

8. WHITE COLLECTION---- Ni vidonge vya kuwa mweupe mwili mzima pamoja na kuwa soft ilikua inapatikana kwa @150,000/= Sasa ni @140,000/= tu

9. BOTCHO HOLOGRAM CREAM--- Hii ni dawa ya kuongeza hips na makalio ilikua inapatikana kwa@180,000/= Sasa ni@160,000/=       

N.K

Wasiliana nasi kwa simu
NO:. +255 759029968  AU +255 659618585
Popote ulipo utapata huduma zetu.

Pia hakikisha unapatiwa risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY PROD ununuapo bidhaa kampuni hii.
               WELCOME ALL
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images