Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazetiu Ya Leo Jumanne ya January 1 2019


Waziri Mkuu: CRDB kuhamasisha ukuaji wa uchumi

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua tawi la benki ya CRDB wilayani Ruangwa na kuushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kuwa tawi hilo litahamasisha ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi kujua umuhimu wa kuhifadhi fedha zao benki.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema ni vema kwa benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Jumatatu, Desemba 31, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuzindua tawi la benki ya CRDB, ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamisha wananchi kutumia benki kwa kuhifadhi fedha zao.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwa sasa benki hiyo inatakiwa itoe mikopo midogo, ya kati na mikubwa  kulingana na uhitaji wa wajasiriamali ndani ya wilaya hiyo kwa sababu mikopo itawawezesha wananchi waweze kukuza mitaji na kujikwamua kiuchumi.

Pia Waziri Mkuu ameipongeza benki ya CRDB kwa kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo za afya pamoja na elimu kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na benki hiyo nchini.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki ya CRDB imekua na kupanua wigo wake wa kufikisha huduma kwa wateja na kuunga mkono sera ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za fedha.

Alisema tawi hilo ni la sita katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania, kwani tayari wanamatawi mengine manne ambayo ni Lindi mjini, Mtwara, Masasi, Tandahimba na tawi  linayotembea katika Wilaya ya Newala. Pia wapo katika hatua za mwisho za ujenzi wa tawi Nachingwea.

“Wilaya hii ya Ruangwa ni kiungo muhimu sana katika uchumi wa mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla, hivyo uwepo wa mfumo rasmi wa kibenki,  kupitia  tawi hili la Benki ya CRDB, utasaidia sana kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kufungua fursa mpya.”

Mkurugenzi huyo alisema CRDB wanajivunia utendaji mzuri wa tawi hilo, kwani katika kipindicha mwaka mmoja toka limeanza kazi, limeweza kupata matokeo makubwa ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa amana ambazo zimefikia kiasi cha shilingi bilioni 1.5.

Pia jumla ya AMCOS 12 wanachama 4,600 zimejiunga na kufungua akaunti zao hivyo kuongeza usalama wa fedha zao. Pia  jumla ya mikopo ya shilingi bilioni 1.2 imeshatolewa kwa wateja wa wilaya hiyo, ambapo shilingi milioni 409 zilitolewa katika kilimo cha korosho na ufuta, wakati shilingi milioni 790 zilitolewa kama mikopo kwa wafanyakazi na wafanyabiashara.

Moto wa Gesi Waua Mama na Watoto wake Wawili

$
0
0
Mwanamke mmoja aliyetambuliwa  jina la Pendo Adolph Manyama (29) na watoto wake wawili, wakazi wa Kola katika Manispaa ya Morogoro, wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuungua na moto uliyosababishwa na kulipuka kwa jiko la gesi.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Wilbrod Mutafungwa, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 26, mwaka jana, saa 10:30 jioni , maeneo ya Kola, Manispaa ya Morogoro.
  
Mutafungwa alisema siku hiyo mtoto wa mama huyo aliyejulikana kwa jina la Angela Baltazar (4) alifungua mtungi wa gesi na kusababisha gesi kujaa ndani ya nyumba hiyo.
 
“Wakati mtoto akifungua mtungu huo, mama yake ambaye alikuwa Mwalimu wa shule ya Msingi Forest, bila kujua aliingia ndani na jiko la mkaa na kusababisha moto kulipuka na kumuunguza yeye na watoto wake wawili, jambo lilosababisha vifo vyao,” alisema.
 
Aidha, Kamanda Mutafungwa aliwataka wananchi kuwa waangalifu wakati wote wanapokuwa wanatumia vyombo hivyo vya majumbani, ili kuepusha ajali mbalimbali za moto kutokea.
 
Mmoja wa jamaa wa karibu na familia hiyo, alielezea tukio hilo lilitokea Jumatano iliyopita wakati mume wa mama huyo, Baltazar Kineneko (37) akiwa mkoani Arusha kikazi.
 
“Ilikuwa majira ya usiku mama akiwa anapika kibarazani kwenye jiko la mkaa mtoto wa miaka minne aliingia ndani na kuchezea jiko la gesi, gesi ikawa inavuja.

"Mtoto alipofungua mlango kutoka nje mvutano wa gesi na mkaa ulisababisha mtungi wa gesi kulipuka hadi juu na kutoboa gypsum.
 
“Mama aliingia ndani kumuokoa mtoto, lakini alitoka akiwa anaungua mwili mzima. Mtoto wake mwingine wa miaka sita
aliyekuwa nje anacheza alipoona mamaye anatoka ndani na mdogo wake huku wakiwa wanaungua moto alikimbia kumkumbatia mama yake naye akaanza kuungua,” alieleza jamaa huyo.
 
Ndugu huyo alisema mama na mtoto mdogo walikufa papo hapo, mtoto mkubwa alisafirishwa kwa ndege kwenda Nairobi nchini Kenya kwa matibabu baada ya hali yake kuonekana mbaya.
 
Hata hivyo, jamaa huyo alisema baba wa mwanamke aliposikia kuwa mwanaye na mjukuu wamekufa alipata mshtuko naye akafa hapo hapo, alizikwa jana mkoani Morogoro.
 
“Baba wa mtoto yaani mume wake yule mama katoka leo (jana) Nairobi, ili kesho (leo) amzike mke na mwanaye kisha arudi Nairobi kumuuguza mwanaye aliyebaki, lakini usiku wake akiwa safarini alipigiwa simu kuwa mtoto aliyemwacha
Nairobi naye kafariki,” alieleza mtu huyo.

Wanne Watiwa Mbaroni na Mifuko 50 ya Simenti Iliyoibiwa Eneo la Ujenzi wa Majengo ya Serikali Dodoma

$
0
0
Jeshi la Polisi Jijini Dodoma  linawashikilia watu wanne kwa kudaiwa kuiba saruji mifuko 50 katika eneo la ujenzi wa majengo ya serikali Chamwino Ikulu mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, jiijini hapo jana.

Alisema watuhumiwa walikamatwa jana Disemba 31, 2018 wakiwa wamepakia mifuko hiyo ya saruji kwenye lori.

Kamanda Muroto alisema watuhumiwa wanasadikiwa kuvunja stoo na kufanikiwa kuiba mifuko hiyo 50 ya saruji kwa lengo la kwenda kuiuza.  Alisema upelelezi ukikamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani

Atiwa Mbaroni Kwa Kumuua Mama Yake Mzazi kwa Kisu

$
0
0
Jeshi  la Polisi linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Moleti Wilaya ya Kongwa, mkoani hapo, Peter Mgomba (26), kwa madai ya kumuua mama yake mzazi kwa kumchoma kisu tumboni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, jiijini hapo jana.
 
Kamanda Muroto alisema tukio hilo lilitokea Desemba 29, katika Kijiji cha Moleti, Tarafa Mlali, Wilaya ya Kongwa.

Alisema tukio la mauaji linadaiwa kufanyika wakati Mgomba alipomchoma kisu tumboni mama yake mzazi, Anita Mgomba (61) na kusababisha kifo.

Alisema chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika, lakini wanaendelea na uchunguzi na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Hata hivyo, Kamanda Muroto alisema mtuhumiwa anasadikiwa kuwa ni mgonjwa wa tatizo la akili na baada ya kufanya tukio alitoroka, lakini jeshi hilo lilimtafuta na kumtia nguvuni.

Alisema siku ya tukio, Anita alijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini, lakini akiwa kwenye matibabu Desemba 30, alifariki dunia.

Mwanamke Avamiwa na Simba na Kung'atwa Kalio Moja

$
0
0
Mkazi wa Kijiji cha Kata ya Ngwala, wilayani Songwe, Susan James, amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na simba na kutafunwa kalio lake la kushoto wakati akimpeleka mtoto wake hospitali.
 
Diwani wa kata hiyo, Donald Maganga, alithibitisha mwanamke huyo kunusurika kifo baada ya kuvamiwa na simba huyo.

Alisema baada ya simba huyo kumjeruhi mwanamke huyo, aliondoka na kuwaacha mama huyo na mtoto wake na kwamba ni kitendo cha kumshukuru Mungu kwa kuwa mnyama huyo anapomvamia mtu anakula kila kitu na kubakiza kichwa na viganja vya mikono.

Alisema, wananchi kwa kushirikiana walimchukua mama huyo na kumpeleka zahanati ya kijiji ambako alipatiwa matibabu na baadaye walimpeleka hospitali teule ya Mwambani, iliyopo makao makuu ya wilaya kilometa 120 kutoka kwenye kata hiyo.

Alisema mbali na tukio hilo, pia kulikuwapo na tukio la mke na mume wakiwa na mtoto wao kuvamiwa na simba ambaye alimtafuna mtoto wao na wao kunusurika.

Alisema kupitia tukio hilo, anatoa rai kwa wananchi hasa wageni wanaoingia kwenye maeneo hayo kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo kuwa makini na wanyama waliopo mbugani.

Aliwaomba watu wa maliasili kuwa waangalifu kwa kuwanusuru wananchi wanaoishi karibu na mbuga hiyo kuwaepusha na majanga ya kuvamiwa na wanyama.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwambani, Dk. Kusenge Benangode, alithibitisha kumpokea mwanamke huyo ambaye amepatiwa matibabu na hali yake ikiendelea vizuri.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH....Anatoa Pete za Bahati, Anasafisha Nyota, Anazuia Chuma Ulete na Mengine

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam Shariff,  Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
 
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
 
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Adam Shariff Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. 

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Mawasiliaono: +255715971688  au +255756914036
 
Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power

$
0
0
Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power Kwaajili Ya Nguvu Za Kiuume Na Promix Kwaajili Ya Kuongeza Maumbile;

Kwa mwanaume aliyekamilika na mwenye Afya njema ili kumridhisha mke au mpenzi anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya Mara mbili hapo utamridhisha mpenzi wako ila ukiwa unapiga moja au mbili hapo ujue umejilidhisha wewe 

Tiba Ya Tatizo Lako Ni Dawa Hiitwayo Simpo Power No, 1; dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge vya miti shamba na unga ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja :-1 itakufanya urudie tendo zaidi ya mara tatu 
2 itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-20 kwa tendo la Kwanza 
3 huimarisha uume uliolegea na kusinyaa 

Je Una Mke Au Mpenzi Aliyebalikiwa Kuwa Na Kario Kubwa Au Mwili Mnene Na Wewe Mume Wake Una   Maumbile Mafupu?; tumia sasa dawa ya PROMIX dawa itakufanya umfikishe shemu nyeti maana inaboresha maumbile saizi upendayo.

Dawa zangu haziina madhara yoyote kwa mtumiaji 

MARKSU; ni dawa ya kisukari dozi siku 21 
MWARU; ni dawa ya uzazi,hufungua milija ya uzazi ata kwa Wale waliofungiwa uzazi  
MTUNDUU; ni dawa ya busha bila kupasua 
MAZANZA; ni dawa ya kisukar zipo dawa za miguu Kuuma,tumbo,kupunguza Matiti,kutoa minyama uzembe ngiri,vidondo vya tumbo  

FIKA OFISINI KWANGU BUGURUNI MALAPA KARIBU NA KOTA ZA POLISI AU PIGA  SIMU ULETEWE MAHALI ULIPO SIMU NO : 0783185060 au 0752348593  -DR AGU

Rais Magufuli awatakia heri ya mwaka mpya 2019 Watanzania wote

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri ya Mwaka Mpya wa 2019 Watanzania wote na kuwaomba wadumishe umoja, amani na upendo waliouonesha katika mwaka 2018.

Akizungumza kutoka nyumbani kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Magufuli amesema mwaka 2018 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Watanzania na anatarajia kuwa mwaka 2019 utakuwa wa mafanikio zaidi kulingana na mipango ambayo nchi imejipangia kuitekeleza.

Mhe. Rais Magufuli amewataka watumishi wa umma, viongozi, wakulima, wafanyabiashara, wavuvi na wafugaji kuongeza juhudi za uzalishaji mali katika mwaka 2019 huku wakipiga vita rushwa, wizi, ufisadi, ubadhilifu na kwamba anaamini kuwa uchumi wa Tanzania utazidi kupanda katika mwaka 2019.

“Ujumbe wangu kwa watumishi wa umma, ni kama nilivyotoa ujumbe kwa Watanzania wengine, wachape kazi, wajiamini, waachane na utamaduni wa kila kitu wanachokifanya kudai ni maagizo kutoka juu, huo ni ugonjwa ambao umeanza kuwapata watumishi wa umma ambapo kila wanalolifanya hata kama ni kwa mujibu wa sheria hawataki kujiamini, na wanasema hili ni maagizo kutoka juu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Amemalizia kwa kusema; “Ninaanza kuiona Tanzania mpya inakuja, tusiiachie Tanzania mpya, tuifike, tuikae na tuiishi kwa sababu huu ndio wakati wa kuijenga Tanzania mpya, nina imani kubwa sana Mungu wetu atatusaidia, mwaka 2019 mengi mazuri yatafanyika, kikubwa ni mshikamano wetu sote Watanzania, niwaombe Watanzania wote wa rika zote, wa dini zote, wa makabila yote, mshikamano waliouonesha kwa mwaka 2018 katika Serikali, wauoneshe tena mwaka 2019, na ikiwezekana wauoneshe zaidi na zaidi kwa kutanguliza zaidi uzalendo na Utanzania wetu, tutafanikiwa, Mungu ni mwema, Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki Watanzania wote na Mungu ubariki mwaka 2019.

Habari Njema Kwa Wenye Matatizo Ya Nguvu za Kiume, vitambi, nyama uzembe

$
0
0
NAUHABARISHA ULIMWENGU TIBA BORA YA MITI SHAMBA..

  Ninatibu magonjwa 1-100 dawa ninazo Sasa.

KOLA; ni dawa ya kisukari dozi siku 14 ata kama unajihisi itumie kwa kinga zaidi

  THREE(3) POWER MIX,inatibu Nguvu za kiume Ni dawa iliyo Bora na Humfanya mume kuchelewa kufika kileleni dkk 40_47 bila kuchoka.Inaanza kufanya kazi ndani ya door 80 na inatibu kabisa ndani ya siku 6 tu,hutatumia Tena dawa ya Nguvu za kiume three power mix Ni kiboko kabisa,hata Kama unahisi una tatizo unaruhusiwa kutumia kwa ajili ya Kinga baadae.

 DUDUMA MIX 4 POWER,hunenepesha na kurefusha uume na kukomaza uume uliosinyaa kwa mda mfupi,tumia siku 4 na kupona kabisa.

  SHOOLA,Ni dawa ya kutibu tezi dume na kupona kabisa ni ya miti shamba hutumika kwa kunywa bila upasuaji ndani ya siku 14 haina madhara.

 NENGONENGO,dawa ya kutibu Uzazi kwa akina mama walioshindwa kubeba mimba kwa mda mrefu ukitumia utaweza kupata mimba na kujifungua salama.

  KAMINGO,Ni dawa inayotibu Busha bila kufanyiwa operation na aliyevimba korodani inatibu kabisa dozi Ni siku 7 na inaubora wa Hali ya just na unapona kabisa.

  IKUMBIJA,Ni dawa ya kumvuta mpenzi aliekuacha na mwenye ahadi za uongo kukutimizia,na kumkomesha mtu asiwe na mtu mwingine pia atakurudia ndani ya masaa 6.

   MALAMALA,Ni dawa ya vidonda vya tumbo na tumbo kujaa gesi, kilungulia na inafanya kazi kwa haraka zaidi na kupona kabisa ndani ya siku 6.
 

SAALA,Ni dawa inayotibu miguu kuwaka moto,kiuno,mgongo,magoti na viungo vyote mwilini na joints,Sasa tiba yake Ipo kwangu.

   HALALA MIX,Ni dawa mix ya miti 100 inayotibu matatizo yote,Kama majini,kesi,biashara,kazi,mitego na kupoteza kumbukumbu. no

TUNAFANYA KAZI SIKU ZOTE PIA NAKUFIKIA POPOTE ULIPO KWA HARAKA,NAPATIKANA DAR ES SALAAM NA KAHAMA,PIA NINA MAWAKALA MIKOANI SIMIYU,SHINYANGA,MOSHI NA MBEYA.


     KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA: 0784 475946
           0744 922982
    DR,SANDALA.

Waziri Mkuu Apokea Vyumba Vya Madarasa

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amepokea msaada wa vyumba viwili vya madarasa vikiwa na  madawati vyenye thamani ya sh. milioni 80 kutoka kwa bank ya CRDB.

Alipokea madarasa hayo jana (Jumatatu, Desemba 31, 2018) katika shule ya Sekondari  Kassim Majaliwa iliyopo Kata ya Nachingwea katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi

Waziri Mkuu aliushukuru uongozi wa benki ya CRDB kwa msaada hu ambao umesaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa unaoikabili wilaya hiyo.

Kadhalika, Waziri Mkuu alizitaka taasisi nyingine ziige mfano wa bank ya CRDB kwani imekuwa bega kwa bega na Serikali katika kuchangia shughuli za kimaendeleo nchini.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alitoa wito kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kassim Majaliwa kutumia vizuri madarasa hayo na kutunza mali zilizopo shuleni hapo.

Alisema ujenzi wa shule hiyo ni mradi uliobuniwa na wakazi wa kata ya Nachingwea ili kuwawezesha watoto wao kupata elimu katika eneo lililo karibu na makazi yao.

Waziri Mkuu alisema awali wanafunzi wa kata hiyo walikuwa wanatembea umbali mrefu hadi shule ya sekondari ya Ruangwa jambo ambalo lilikuwa ni changamoto kwao.

“Nawaomba wananchi wenzangu tuendelee kushirikiana katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo kwenye kata yetu ya Nachingwea.”

Pia Waziri Mkuu alikabidhi kompyuta 20 kwa shule za sekondari tano ambazo ni Kassim Majaliwa, Likunja, Mnacho, Hawa Mchopa na Ruangwa.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki yao inathamini elimu na imekuwa ikirudisha kwa jamii faida wanayoipata kwa kuchangia shughuli za maendeleo.

Alisema mbali na msaada huo wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na madawati yake, pia aliahidi kutoa sh. milioni 20 ili zitumike kununulia madawati yatakayosaidia kupunguza changamoto ya madawati wilayani Ruangwa.

Kwa upande wao, wakazi wa kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa waliishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono katika mradi wa ujenzi wa shule hiyo ya sekondari ambayo imewawezesha watoto wao kusoma karibu na maeneo yao ya makazi yao.

Mmoja wa wakazi hao Omari Losi alisema ujenzi wa shule hiyo utawarahisishia wanafunzi kwenda shule na kuwaondolea shida ya kutembea umbali mrefu kwenda shule ya sekondari ya Ruangwa walikokuwa wakisoma awali.

Naye, mkazi mwingine wa kata hiyo ya Nachingwea, Mariam Kingamkono alisema uwepo wa shule ya sekondari katika kata yao kumeongeza hamasa ya wanafunzi kupenda kusoma kwa sababu wameondolea shida ya kutembea umbali mrefu.

Alisema shule hiyo inawalimu wazuri na wa kutosha na ina mazingira mazuri ya kujifunzia, hivyo aliwaomba wazazi wenzake waendelee kushirikiana na Serikali katika kuboresha maendeleo kwenye kata yao hususan ujenzi wa shule.


 (mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

Mwanamke Auawa Kikatili......Mwili wake wafungiwa ndani ya banda la ng'ombe

$
0
0
Mkazi wa  Kijiji cha Luhega, Wilaya ya Tanganyika, Milembe  Manoni (22), amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kisu kifuani, kisha mwili wake kufungiwa ndani banda ng’ombe.

Akizungumzia tukio hilo jana,  kaka wa  marehemu, Nestory Malongo  alisema lilitokea  juzi usiku nyumbani kwa marehemu.

Alisema taarifa ya kuuawa kwa  Milembe aliipata  saa tatu  asubuhi na wasamalia wema,

Baada ya kapata taarifa hizo, alikwenda eneo la tukoo na kukuta watu wengi wakiwa wamekusanyika nje ya nyumba.

Alisema baada ya kuona mwili hiyo, waliona majereha sehemu za kifuani ambayo inaonyesha alichowa na kisu.

Alisema polisi  walifika eneo hilo, kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya kwenda kuufanyia uchunguzi Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa  Katavi .

Mama wa marehemu,  Tuma Matine alisema alipigiwa simu na mkwe wake na kusisitiza kitendo hicho ni cha kikatili mno.

 Alisema  katika  nyumba hiyo, binti yake alikuwa kuwa akiishi na mfanyakazi mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi ya kuchunga  mifugo ya ng’ombe.

“Nasikitika baada ya tukio hili huyu mfanyakazi hajaonekana nyumbani…inawezekana wazi ndiye aliyehusika na kifo hiki,”alisema.

Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa mifugo wa  Mkoa wa  Katavi, Mussa Kabushi  alisema kumekuwapo na mauaji ya mara kwa mara ya kuuawa kwa wafugaji.

Alisema mauaji hayo, yamekuwa yakisababishwa kutokana na tabia ya wafugaji kukaa kwenye maeneo ya kujitenga na kutokuwa na ulinzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas  Nyanda alithibitisha kutokea kwa mauaji  hayo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.

Credit: mtanzania

Gigy Money afunguka kurudiana na MO J

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo na Video Vixen, Gigy Money amejibu iwapo amerudiana  na mpenzi wake Mo J baada ya hivi karibuni kuonekana pamoja na mtoto wao.

Mwanadada huyo maarufu mtandaoni akizungumza na Wasafi TV amesema ni kweli kwa sasa wapo pamoja na hawajawahi kuachana.

"Unajua kuachana ni maneno tu tunakuwa tunaongea, halafu tukiachana sisi kwa ajili tayari ni wazazi kimaadili yetu tutakuja kukutanishwa tu na yule mtoto pale ndani, angalieni tu vitendo (tumerudiana)," amesema Gigy Money.

Utakumbuka baada ya Gigy Money kujifungua kuliibuka mvutano kati yake na Mo J ambaye ni Mtangazaji wa Choice FM kwa madai kuwa mtoto si wake baadaye zikaibuka tuhuma nyingine kuwa hatoi matunzo kwa mtoto lakini sasa wameonekana pamoja na wenye furaha.

Rudisha heshima yako Kwa Mpenzi Wako, Mke Wako...Tumia Tiba Hii ya Asili

$
0
0
Rudisha heshima yako sasa kwa kutumia Dawa hii iitwayo SUPER GAFINA, kwa ajili ya nguvu za kiume na NKOLOMIJE ni kwaajili ya kuongeza maumbile.

Kwa mwanaume aliye kamilika anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara mbili ,ila ukiwa unapiga moja tena kwa shida wewe ujue  unamatatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

TIBA YA TATIZO LAKO NI; Dawa iitwayo SUPER GAFINA, dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge na unga wa asili ambavyo havina madhara kwa mtumiaji ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja;-

1).itakufanya urudie tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuchoka.

2).ltakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dk.15 hadi 20 kwa tendo la kwanza.

3).lnaimarisha uume uliolegea na uliosinyaa na kuupa nguvu maradufu.

Je unamaumbile madogo pamoja na uume mfupi? NKOLOMIJE ni suluisho la tatizo lako. Na ni dawa inayoboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi kuanzia inch. 5 hadi 8 kwa muda mfupi sana .Dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk.30 ukisha tumia guarantee miaka 50  ikishakutibu.

Pia ninatibu;- KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU, MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE ,BP, NK.

IGULYATI, ni dawa ya mvuto wa biashara, kazi,kupandishwa cheo na humfanya mfanyakazi kupendwa na mwajiri wake. Pia humvuta mke,Mme,hawara ,mchumba unae muitaji utampata kwa dk.30 tu na atatulia na kumfunga asitoke nje ya ndoa, Pia natoa Pete za bahati ambazo zimetajirisha wengi.

Pia ipo dawa ya kupunguza matiti,unene ,tumbo,na kitambi ,hupunguza mafuta ,kuondoa makovu,chunusi,michilizi mwilini na kuongeza hipsi, makalio na mguu wa bia nk. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na DR,HOSUTWA .Anapatikana Mbagara

Simu no, 0756241666 na 0672186977.

       Huduma hii utaipata popote ulipo

TFDA Yaongoza Afrika kwa kuwa na Mfumo Bora wa Udhibiti wa Dawa

$
0
0
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mafanikio hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Adam Fimbo, alisema kuwa TFDA imepata mafanikio hayo makubwa  kutokana na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, ambapo Desemba mwaka huu, imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imesaidia  Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia  hatua hiyo muhimu.

“Hii ni hatua kubwa kwa kuwa taasisi ya mfano barani Afrika katika udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi  na hivyo kuvutia nchi mbalimbali kuja TFDA  kujifunza mifumo iliyopo  na kwenda kuitekeleza nchini mwao na sasa mifumo yetu imetambulika na kujulikana na nchi nyingi kwa mfano Zimbabwe, Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini, Botswana, Mauritius, Lesotho na Bangladesh” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA

Sambamba na hilo, Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA,  aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo idadi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi vilizosajiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka,

Akitolea mfano katika kipindi cha 2015/16 hadi 2017/18, TFDA imesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la 62%. Ikiwa ni kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA, alifafanua kuwa tathmini na usajili wa bidhaa hufanyika kwa lengo la kuhakiki endapo bidhaa zinakidhi vigezo vya usalama, ubora na ufanisi kabla ya kuruhusiwa katika soko. Kuwepo kwa bidhaa nyingi zilizosajiliwa katika soko ni uthibitisho kuwa walaji wanapata bidhaa zilizo salama, zenye ubora na ufanisi.

Kuhusu udhibiti wa uingizaji na usafirishaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi, alisema kuwa  katika kutekeleza hilo ambalo ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, la mwezi Mei, 2017, TFDA  imeweka wakaguzi wake ambao hufanya kazi masaa 24 kwa siku zote za juma, pamoja na mfumo wa kieletroniki wa utoaji vibali vya kuingiza na kutoa nchini bidhaa unaomwezesha mteja kutuma maombi, kufanya malipo popote alipo na hatimaye kupata kibali ndani ya masaa 24.

Aidha, kwa kutumia mifumo hiyo, mwenendo wa utoaji wa vibali vya uingizaji na utoaji wa bidhaa nje ya nchi umeongezeka ambapo katika mwaka 2017/18, jumla ya vibali 11,866 sawa na ongezeko la 91% ukilinganisha na 13,018 mwaka 2016/17 vilitolewa.

Vilevile, katika jitihada za kujenga Tanzania ya viwanda ifikapo 2025, TFDA imeendelea kutoa msaada wa kiufundi na kuwajengea uwezo wenye  viwanda vya dawa nchini na kushawishi wawekezaji kujenga viwanda vya dawa, chakula, vipodozi na vifaa tiba. Ambapo hadi sasa jumla ya wawekezaji 70 wameonesha nia ya kuanzisha viwanda vya dawa huku viwanda vinne vikiwa vimeanza kujengwa katika maeneo ya Morogoro na Kibaha.

Sambamba na hilo, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema  kuwa, mafanikio mengine ya TFDA yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatau ya Serikali ya Awamu ya Tano ni pamoja na kuweka mifumo madhubuti ya ufuatiliaji wa madhara yatokanayo na matumizi ya chakula, dawa na vifaa tiba ili kuweza kutambua, kutathmini na kuzuia madhara yasiyovumilika yasitokee kwa wananchi.

Pia, kwa kipindi cha mwaka 2015/16 hadi 2017/18, matokeo ya uchunguzi wa sampuli yanaonesha kuwa bidhaa zilizochunguzwa zimekidhi viwango vya ubora na usalama kwa wastani wa 88%.

Alifafanua kuwa maabara ya uchunguzi wa dawa imekidhi vigezo vya kimataifa na kutambuliwa rasmi na Shirika la Afya Duniani (prequalification), maabara ya uchunguzi wa chakula na ile ya maikrobiolojia zimepata ithibati kwa kiwango cha kimataifa cha ISO/IEC 17025:2005. Hii inafanya majibu ya uchunguzi yanayotolewa na maabara kuaminika na hivyo kutambulika kitaifa na kimataifa, hali ambayo inamuhakikishia mwananchi uhakika wa maamuzi ya mamlaka kuhusiana na ubora wa bidhaa.

TFDA imefanikiwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika utekelezaji wa mipango kazi yake, ambapo katika kipindi cha mwaka  2017/18 itaendelea kutoa kipaumbele katika utekelezaji kwa ufanisi wa malengo mahususi nane (8) yaliyomo katika Mpango Mkakati mpya wa miaka mitano (5) yaani 2017/18 – 2021/22, ili kulinda afya ya jamii.

Ujenzi wa Kituo cha Afya Hamai wamchefua Jafo

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, Chemba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amechukizwa na kusuasua kwa ujenzi wa kituo cha Afya Hamai kilichopo katika Wilaya ya Chemba ambacho hakijakamilika ujenzi wa miundombinu ya Afya ilihali fedha za ujenzi zikiwa zimefikishwa kituoni hapo miezi kumi iliyopita.

Mhe. Jafo ameonyesha kuchukizwa kwake  wakati wa ziara  ya kukagua miradi ya Afya inayoendelea kujengwa katika Halmashauri hiyo mapema leo hii.

Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Jafo amesema Kituo cha Hamai kimepokea fedha tangu Januari 2018 lakin mpaka sasa ujenzi haujakamilika wakati vituo vingine vyenye mazingira magumu zaidi vimekwishakamilisha ujenzi tena kwa ubora wa hali ya juu.

Mhe Jafo aliongeza  kuwa fedha zilizoletwa hapa ni sh milioni 400 nimeambiwa kuwa zimekwishatumika zote na inahitajika tsh mil 29 zaidi ili kukamilisha majengo haya; Nashindwa kuelewa ni kitu gani cha gharama kilichowekwa katika kituo hiki ambacho kimepelekea fedha hizo kwisha kabla ya ujenzi kukamilika.

“Inakuwaje halmashauri zingine wametumia kiasi hicho cha fedha kukamilisha miundombinu yao lakini kwa chemba fedha hizo  zisitoshe kukamilisha kituo kuna tatizo gani hapa” alihoji Jafo

Hakuna fedha itakayoongezwa katika kituo hiki cha Hamai nataka majengo yote yaliyojengwa hapa yakamilike haraka iwezekenavyo  na kwa ubora unaotakiwa bila kuwa na sababu zingine zozote mkatafute fedha popote mkamilishe kituo hiki aliongeza Jafo.

Akizungumza na wananchi wa Hamai Mhe. Jafo aliwajulisha kuwa Halmashauri ya Chemba ni miongoni mwa Halmashauri zilizopata fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya vitatu na Hospital ya Wilaya kwa hiyo hatavumilia kuona fedha hizo zikitumika vibaya atasimamia sharia na atakayekwenda kinyume na maelekezo atachkuliwa hatua kali.

Sambamba na kumuagiza Mkurugenzi kutaftua fedha za kukamilisha ujenzi huo Waziri Jafo ametoa muda wa wiki mbili kukamilisha ujenzi huo na ameahidi kurejea tena Hamai mnapo Januri 15,2019 kuja kukagua maendeleo ya ujenzi huo.

Naye Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia amesema kuwa kumekua na kusuasua kwa ujenzi wa kituo cha Afya Hamai umetokana na ujanja ujanja wa baadhi ya watumishi kutaka kufanya vitu wenyewe bila kushirikisha kamati za ujenzi na mara nyingi wanaposhauriwa hawakutaka kusikiliza ushauri huo ndio baadhi ya sababu zilizochangia kutokamilika kwa ujenzi huo kwa wakati.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chemba Dkt. Semistatus Mashimba amesema changamoto zilizojitokeza katika ujenzi wa kituo cha Afya Hamai zimetokana na uhaba wa watumishi hususan  katika idara ya ujenzi na manunuzi ndio ndio muhimu katika kusimamia shughuli zote za ujenzi wa vituo vya Afya.

Vituo vya Afya vilivyopokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Wilaya ya Chemba ni vitatu ambavyo ni Hamai, Mrijo na Kwamkoro ambapo kila kimoja kimepata sh mil 400 huku hospital ya Wilaya ikipatiwa kiasi cha sh Bil 1.5.

Waziri Lugola Kuanza Ziara Mkoani Kagera Kesho...... Awataka Wananchi Kumletea Kero Katika Mikutano Yake Ya Hadhara

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Bukoba.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili mjini Bukoba Mkoani Kagera leo, kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku nane kwa kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.

Waziri Lugola anatarajia kuanza ziara hiyo rasmi kesho Januari 2, 2019 mjini Bukoba kwa kukutana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kupokea taarifa ya Kamati hiyo, kabla ya kuanza kuzungumza na Wakuu wa vyombo vyake na baadaye kuzungumza na Baraza la Askari na Watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo mjini humo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, leo, Lugola amesema baada ya kuzungumza na Askari na Watumishi wa Wizara yake pamoja na kupokea changamoto zao, atafanya mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi utakaofanyika uwanja wa uhuru mjini humo ili aweze kusikiliza na kuzitatua kero mbalimbali zinazowakabili.

“Nitafanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru eneo la Mayunga hapa mjini Bukoba, ambapo utaanza saa 10:00 hadi 12:00 jioni, hivyo nawaomba wananchi wa mji huu wajitokeze kwa wingi kunisikiliza kile ambacho nimepanga kuwaambia na pia nitawapa nafasi wananchi waulize maswali bila woga, waniambie kero zao nami nitazitatua katika mkutano huo,” alisema Lugola.

Pia Lugola alisema lengo la ziara hiyo ni kufuatilia maagizo yake mbalimbali ambayo aliyatoa mwaka jana 2018 katika mikutano yake kama yalifanyiwa kazi na viongozi wa Taasisi anazoziongoza au yalipuuzwa, yakiwemo ya dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe.

Lugola alisema katika ziara yake aliyoifanya mwaka jana Mkoani Kigoma aligundua wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo hawezi kulala akiwa ofisini, lazima afanye ziara nchi nzima kuwasaidia wananchi kutatua kero zao ambapo wengi wao wakiwalalamikia Polisi wakiwaonea.

Waziri Lugola ameongeza kuwa, kupitia mikutano yake ya wananchi mkoani Kigoma ndipo ameamua kufanya ziara ya pili kwa kuutembelea Mkoa wa Kagera ambao changamoto zake zinafanana kwa sehemu kubwa kwa kuwa mikoa hiyo ni ya mipakani na changamoto kubwa ni uwepo wa wahamiaji haramu pamoja na matukio kadhaa ya ujambazi ambayo kwa kiasi kikubwa Serikali inaendelea kuyadhibiti.

“Wananchi wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kusikiliza matatizo yao yanayowakabili, ndio mana nimepanga kufanya ziara kama hizi nchi nzima, hii inasaidia sana kujua matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuangalia utendaji kazi wa Taasisi zangu zilizopo ndani ya Wizara hii, na hakika Serikali ya Dokta Magufuli inawajali wananchi wake ndio mana inawafuata mahali walipo, ili wazungumze na Serikali yao uso kwa uso,” Alisema Lugola.

Waziri Lugola baada ya kumaliza ziara yake mjini Bukoba, ataenda Wilaya za Misenyi, Karagwe, Kyerwa, Ngara, Biharamulo na Januari 8, 2019 atamalizia ziara yake Wilaya ya Muleba ambapo katika Wilaya hizo pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.

Waziri Kalemani Awanyooshea Kidole VISHOKA

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa onyo kali kwa watu wenye tabia ya kuhujumu miundombinu ya umeme pamoja na vishoka.
 
Waziri Kalemani alitoa kauli juzi akiwa katika ziara wilayani Kwimba, Mwanza na kuzungumza kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Ngulla na Ibindo, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme, kuwasha umeme na kuzungumza na wananchi.
 
“Mtu atakayebainika akikata nguzo, akiiba nyaya, akichezea transfoma kiasi cha kukosesha umeme wananchi, Mkuu wa Wilaya wa eneo husika atamweka korokoroni,” alisema.
 
Aidha, alisema kwa wale vishoka, wanaounganisha umeme kwenye nyumba za wananchi bila kuwa na taaluma hiyo, vilevile watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.
 
“Ikitokea tumekukamata, hatutajali wewe ni kibarua wa mkandarasi anayetekeleza miradi yetu ya umeme sehemu yoyote, utakamatwa na kuwekwa ndani,” alisisitiza Waziri.
 
Waziri Kalemani aliwaasa wananchi kuendelea kuwa makini kwa kujiepusha kuwatumia vishoka kwa kazi ya kufunga nyaya za umeme katika nyumba zao.
 
Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi kuutumia umeme kwa kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na hata vikubwa ili uwe na tija kwao na taifa kwa ujumla.
 
Naye Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa, pamoja na kuishukuru serikali kwa kuwapelekea wananchi wa jimbo lake umeme; aliwahamasisha kujitokeza kwa wingi kulipia, ili waunganishiwe huduma hiyo.
 
“Umeme huu unapokuja unahitaji watumiaji na watumiaji ni ninyi. Gharama za kupeleka umeme ni kubwa. Ni vizuri muwe mnajitokeza kwa wingi kuwasilisha maombi Tanesco, ili muunganishiwe na kuanza kuutumia kuboresha maisha yenu,” alisema.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Senyi Ngaga aliipongeza serikali kuwapelekea wananchi umeme na kuomba vijiji vichache ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo vipelekewe, ili nao wautumie katika shughuli za kujiongezea kipato na kuboresha hali zao za maisha.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya TANESCO, Wilaya ya Kwimba ina jumla ya vijiji 119 ambapo mpaka kufikia Julai 2020, vijiji 78 vitakuwa vimepatiwa umeme, sawa na asilimia 66 ya vijiji vyote vya wilaya hiyo.

Zitto Kabwe: Mwaka 2018 Nimesoma Vitabu 49

$
0
0
Tangu Mwaka 2012 nimekuwa naorodhesha vitabu nilivyosoma katika mwaka. Si vitabu vyote huviweka hapa kwani vingine huwa nasoma na kuviacha njiani ama kutopendezwa navyo au kwa kusahau tu.

Vitabu vingine huwa vitabu rejea na huvirudia kwa ajili ya mafunzo ili kufanya maamuzi Fulani Fulani au kwa ajili ya ibada (kwa mfano Quran) au kwa sababu nyenginezo. Nafurahi kuwa hivi sasa kwenye mitandao duniani kote watu wamekuwa wakiorodhesha vitabu ili kujengana katika utamaduni wa kusoma. Barack Obama yeye alianza kuweka orodha yake mwaka 2015 na tayari ameshaweka orodha ya mwaka huu. Obama pia huweka orodha ya muziki aliyopenda mwaka huo. Inavutia.

Mwaka huu nimesoma vitabu 49 (kutoka vitabu 36 + 3 vya mwaka 2017). Wakati natoa orodha yangu 23/12/2017 nilikuwa bado nasoma riwaya za Jumba Maro ya Ally Saleh na The Feast of the Goat cha Mario Vargos Llosa ambazo nilizimaliza nikiwa Maputo, Msumbiji. 

Pia niliweza kuongeza Simulizi iitwayo Zeitoun ya Dave Eggers kuhusu kimbunga cha Katrina huko New Orleans, Marekani. Hii ni simulizi ya wahamiaji kutoka Syria walivyoshiriki kuokoa makumi ya watu kutoka kwenye maafa ya Hurricane Katrina.

Mwaka 2018 nimesoma mchanyato kidogo kuliko mwaka 2017 ambapo dhima (themes) kadhaa ziliniongoza. Hata hivyo bado njaa yangu ya kuwasoma madikteta duniani iliendelea kuniongoza kwa lengo la kupata ufahamu na maarifa ya namna ya kuchangia katika kuzuia nchi yetu kuangukia kwenye utawala wa Imla. Pia nilijaribu kutafuta majawabu ya changamoto hizo. Kwenye dhima hiyo nilisoma:

- The Death of Democracy: Hitler’s Rise to Power
Benjamin C Hett

- The Plots Against Hitler
Danny Orbach

- Franco: Anatomy of a Dictator
Enrique Moradiellos

1 The New Sultan: Erdogan and the Crisis of Modern Turkey
Oner Cagaptey

- How Democracies Die
D Ziblatt and S Levitsky

Kama nilivyopata kusema, ninapenda na kujivunia sana historia ya ukombozi dhidi ya ukoloni barani Afrika na haswa Ukombozi wa Kusini mwa Afrika. 

Mwaka huu niliongeza maarifa katika eneo hilo kwa kusoma sio tu habari nzuri za vyama vya ukombozi bali pia baadhi ya makosa waliyofanya viongozi wetu. SWAPO Captive kilichoandikwa na Bwana Angula ni simulizi muhimu sana kusoma ili kuona namna baadhi ya watu walivyoonewa kwenye harakati za ukombozi. Kwa jina la ukombozi watu huonewa, huteswa na hata huuwawa. Pia nilisoma kuhusu mashujaa wa ukombozi na athari kwa familia zao. Katika dhima hii ya Ukombozi nilisoma:

- Cuito Cuanavale: 12 Months of War That Transformed a Continent
Fred Bridgland

- Africa Tomorrow
Edem Kadjo

- Umkontho we Sizwe: The ANC Armed Struggle
Thula Simpson

- Mozambique: Sowing the Seeds of Revolution
Samora Machel

- 491 Days
Winnie Mandela

- Thabo Mbeki
Adekeye Adebajo

- Umkontho we Sizwe
Janet Cherry

- Chris Hani
Hugh Macmillan

- Being Chris Hani’s Daughter
Lindiwe Hani and Melinda Ferguson

- SWAPO Captive: A Comrade’s Experience of Betrayal and Torture
Oiva Angula

Pia nilisoma vitabu vya hali ya sasa ya Afrika Kusini baada ya ukombozi:

- No Longer Whispering to Power: The Story of Thuli Madonsela
Thandine Gqubule

- How to Steal A City: The Battle for Nelson Mandela Bay, An Inside Account
Crispian Olver

- How to Steal A Country? State Capture and Hope for the Future in South Africa
Robin Renwick

- Coalition Country: South Africa After the ANC
Leon Schreiber

Kama Mtanzania ninayejiandaa kwa majukumu muhimu ya kitaifa nimekuwa nikipenda kupata maarifa Zaidi kuhusu Historia ya Zanzibar. Mwaka 2018 niliongeza maarifa kwa kusoma vitabu kadhaa ikiwemo:

- The Threat of Liberation: Imperialism and Revolution in Zanzibar
Amrit Wilson

- Social Memory, Silenced Voices and Political Struggle: Remembering the Revolution in Zanzibar.
(Ed) W. Cunningham and M. Fouere

Vitabu vinavyofuata ni mchanyato wa riwaya, historia za watu na mataifa mengine, mafunzo ya uchumi na kadhalika. Vitabu vinavyohusu Marekani na utawala wao mpya chini ya Trump ni kwa lengo la kujifunza nini kinaendelea huko. Kitabu cha Deng Xiaoping nilipewa na ndugu yangu Harith Ghassany katika mjadala wa kisomi wa kutafuta modeli sahihi ya kimaendeleo kwa nchi zetu za Afrika.

- Pakistan: Personal Story
Imran Khan

- Making Africa Work: A Handbook for Economic Success
Gregg Mills, O Obasanjo, et al

- Sidetracked
Henning Mankell

- In Praise of Blood: The Crimes of Rwandan Patriotic Front
Judi Rever

- Thomas Sankara Speaks
Thomas Sankara

- A Higher Loyalty
James Comey

- State Secrets: Deathly High Stakes in the Corridors of Power
Quintin Jardine

- Deng Xiaoping and The Transformation of China
Ezra F Vogel

- Gorbachev: His Life and Times
William Taubman

- Tell Tale
Jeffrey Archer

- The Growth Delusion
David Pilling

- CTRL ALT DELETE: How Politics and The Media Crashed Our Democracy
Tom Baldwin

- Unhinged: An Insider’s Account of The Trump White House
Omarosa Manigault

- Fire and Fury: Inside The Trump White House
Michael Wolf

- Why The Dutch are Different
Ben Coates

- The French Revolution: What Went Wrong
Stephen Clarke

- An Extra Ordinary Life: A Passion for Service
V J Mwanga

- Uwajibikaji Ndani ya Kalamu Isiyokuwa na Wino
Ludovich Utouh

- Betting the House: Inside Story of the 2017 Elections
Tim Ross and Tom McTaguwe

- In Defence of Bolsheviks
Max Shachtman

- The Future That Works: Selected Writings of A M Babu
(Ed) Salma Babu and Amrit Wilson

- Our Commonwealth: The Return of Public Ownership in USA
Thomas Hanna

- Democracy, Direct Action and Socialism: A Debate of Fundamentals
Michael Foot and Sean M

Mwaka huu ukiwa unaelekea ukingoni, Wachapishaji wa Vitabu Mkuki na Nyota Publishers walichapisha upya vitabu vya harakati za Willy Gamba, mpelelezi maarufu barani Afrika. Rafiki yangu katika kusoma vitabu Fadhy Mtanga (ambaye pia ni adui yangu kwenye soka – maana yeye ni shabiki mandazi wa Manchester United FC na mimi shabiki wa mabingwa watarajiwa Liverpool FC) alininunulia vitabu vyote 4 vya Mzee Elvis Musiba. Nilikuwa na muda wa kutosha na kuvisoma vyote bila kuweka chini. Namshukuru sana Fadhy kwa zawadi yake murua kabisa. Vitabu hivi ni:

- Kikosi Cha Kisasi
A E Musiba

- Njama
A E Musiba

- Kufa na Kupona
A E Musiba

- Hofu
A E Musiba

Kitabu changu cha mwisho mwaka 2018 ni :

- Dear Ijeawele OR A Feminist Manifesto in 15 Suggestions
Chimamanda Adichie

Vitabu 3 vilivyonigusa sana
The Death of Democracy
: Hitler’s rise to power cha Benjamin Hett kilinigusa sana kutokana na namna wanasiasa wanavyoweza kufanya makosa yenye kudidimiza nchi kwa sababu tu ya kulinda madaraka. Katika kitabu hiki somo kubwa ni namna Wabunge wa vyama vyote vya Siasa walivyomruhusu Adolf Hitler kutunga sheria inayompa mamlaka makubwa wakiamini kuwa Hitler ana nia njema na atawalinda. 


Wabunge wa Chama cha SDP ndio pekee walikataa, walizomewa, kuzodolewa na hata kuuwawa. Wengine walikimbilia uhamishoni. Ndani ya miezi michache, hata wale waliomwunga mkono Hitler walishughulikiwa na Taifa la Ujerumani likaingia kwenye taharuki kubwa na hatimaye vita vya pili vya dunia. 

Waliompa madaraka Hitler waliamini kuwa watamdhibiti. Hawakuweza. Historia kama hii ipo lakini wanaadam hatujifunzi tunarudia makossa hayo kila wakati katika nchi mbalimbali duniani.

How Democracies Die cha Ziblatt na Levitsky kilinigusa sana kwa kuwa kinatoa majawabu ya changamoto za demokrasia kuanguka. Licha ya kwamba ni kitabu maalumu kwa muktadha wa nchi ya Marekani, kitabu hiki nilicholetewa na rafiki yangu Rakesh Rajani, kinatazama mifano ya nchi mbalimbali duniani kama Colombia na njia walizotumia kuhami demokrasia (walitumia sana Bunge na Mahakama), Venezuela (jinsi mgomo wa vyama vya upinzani kutoshiriki chaguzi ulivyotoa nafasi ubwete kwa chama tawala) na hata Ujerumani ambayo hali yake nimeeleza hapo awali. 

Somo kubwa kabisa kutoka kitabu hiki ni kwamba ni lazima wadau wote wa demokrasia kushirikiana pamoja kupambana na udikteta bila kujali tofauti ndogo ndogo au kubwa kubwa miongoni mwao. Bila ushirikiano dikteta husaga saga kila mmoja. Ni Kitabu nashauri kila mwana demokrasia akisome.

Dear Ijeawele Or A Feminist Manifesto in 15 Suggestions cha Chimamanda Adichie ni kitabu kidogo sana kwa idadi ya kurasa. Kwa hakika ni barua ambayo Chimamanda kamwandikia rafikiye ambaye amepata mtoto wa kike na anamshauri amkuze vipi mtoto huyu. Kijitabu hiki kimenigusa kwa sababu kinatoa changamoto kadhaa kwa sisi wanaume katika malezi. 

Kuna mambo ambayo tunafanya tunaona kama ni msaada kumbe inapaswa kuwa wajibu kwa familia. Kwa mfano, mara nyingi husikia wanaume tukisema ‘leo nafanya kazi ya kulea mke wangu kasafiri’ ama kwa kimombo ‘baby-sitting’. Chimamanda anatuambia hapa, Baba mtoto hafanyi ‘baby-sitting’ bali anatimiza wajibu wake kama baba. Pia kinachoitwa ‘gender roles’ kwenye nyumba zetu kiasi kwamba tunazuia watoto wa kike kukua na kukuza vipawa vyao vyote. 

Nashauri wenye watoto wa kike wasome kijitabu hiki, wababa na wamama kwani kinaweza kuchangia kubadili mtazamo wako wa namna tunalea watoto wetu wa kike. Mapendekezo 15 ya Chimamanda unaweza usiyakubali yote lakini yana mafunzo mengi ambayo yanaweza kukufaa kwenye malezi ya mabinti zetu.

Heri ya Mwaka mpya 2019

Zitto Kabwe
Dar es Salaam
30/12/2018

Bwana harusi afariki dunia akisubiri kufunga ndoa kanisani

$
0
0
Sherehe ya harusi iliyokuwa ifanyike juzi jioni katika Kanisa la Nabii wa Utukufu wa Bwana lilipo Olmatejoo, Kata ya Sakina jijini Arusha  kwenye ukumbi wa Sariko Olasiti Garden, iligeuka msiba baada ya bwana harusi kufariki dunia ghafla akiwa kanisani.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 11 jioni katika kanisa hilo ambapo bwana harusi huyo, Heaven Makupa (47) alikuwa kanisani tangu saa saba mchana akisubiri kufunga ndoa na Jane Kimaro.

Hata hivyo, wakati sherehe, nderemo na vifijo vikiendelea vikiongozwa na kikundi cha matarumbeta nje ya kanisa huku bibi harusi akiingia kanisani, Heaven alianza kujisikia vibaya na kupoteza fahamu.

Kutokana na hali hiyo alikimbizwa Hospitali ya St Elizabeth, lakini alifikishwa akiwa tayari amefariki na mwili wake kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

Mhudumu wa chumba hicho, Fransis Costa jana alikiri kuwa wanaendelea kuuhifadhi mwili wa bwana harusi huyo.

Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe na kiongozi wa kanisa hilo, Nabii Peter Alayce na tayari taratibu zote zilikuwa zimekamilika tangu mchana alipofika bwana harusi na ujumbe wake.

Wakati kifo hicho kinatokea mamia ya watu walikuwa tayari wamefika katika ukumbi wa Sariko Olasiti Garden kuwasubiri maharusi hao ili kuendelea na sherehe.

Kutokana na tukio hilo, bibi harusi, Jane, alipatwa na mshtuko ambapo hadi jana baadhi ya ndugu zake ambao hawakupenda kuzungumzia msiba huo walisema alikuwa amepumzishwa.

Credit:Mwananchi
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images