Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yakusanya Trilioni 7.37 Ndani ya Miezi Mitano (Julai – Novemba)

$
0
0
Serikali imekusanya makusanyo ya ndani katika kipindi cha miezi mitano ya kwanza (Julai – Novemba), 2018 Sh. trilioni 7.37 sawa na asilimia 88.9 ya makadirio ya Sh. trilioni 8.30 katika kipindi hicho.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema hayo jana wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa taifa na utekelezaji wa bajeti ya serikali, mjini Dodoma.

Alisema katika kipindi hicho, mapato ya kodi yalifikia Sh. trilioni 6.23 ikiwa ni asilimia 88 ya lengo la kukusanya Sh. trilioni 7.04 kwa kipindi hicho.

Aidha, alisema mapato yasiyo ya kodi yalifikia Sh. bilioni 936.03 sawa na asilimia 21 zaidi ya lengo la Sh. bilioni 775.36 na mapato ya halmashauri yalifikia Sh. bilioni 203.8 sawa na asilimia 61 ya lengo.

Dk. Mpango alisema ongezeko la mapato yasiyo ya kodi limetokana na kuimarishwa kwa ufuatiliaji kwenye taasisi, mashirika na kampuni kulikoiwezesha serikali kupata michango na gawio stahiki kutoka kwenye uwekezaji wake; kuimarika kwa matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji wa maduhuli kwenye wizara na idara zinazojitegemea kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato uitwao Government Electronic Payment Gateway (GePG) na kati ya Julai 2017 hadi Novemba 2018, jumla ya taasisi za serikali 325 zimetumia mfumo huo kukusanya maduhuli.

Akizungumzia jitihada za kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara, alisema serikali kupitia Sheria ya Fedha 2018/19 ilipunguza ada na tozo mbalimbali ambazo zilikuwa kero kwa wananchi. Miongoni mwa ada na tozo zilizopunguzwa ni pamoja na za mazingira, OSHA, FIRE, TBS, TFDA na tozo kwenye madini ya chumvi.

Kuhusu changamoto ya ukusanyaji wa mapato, alisema ni pamoja na ukwepaji wa kodi; mwamko mdogo wa wananchi kudai risiti pale wanapofanya manunuzi na wafanyabiashara kutoa risiti pale wanapofanya mauzo; na wigo mdogo wa kodi.

Tiba Hii Ya Asili Inatibu Na Kuponyesha Kabisa Tatizo La Low Sperm Count Pamoja Na Tatizo La Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu Za Kiume.

$
0
0
Unasumbuliwa  na  tatizo  la  low  sperm count ? Umejaribu  tiba  nyingi  bila  kupata  nafuu  ? Kama  jibu  lako  ni NDIO  basi  HII  NI  HABARI NJEMA  SANA  KWAKO.  Neema   Herbalist  ni  duka  la  kuuza  dawa  mbalimbali  za  asili.  Tunapenda  kukufahamisha  kuwa  tunayo  dawa  ya  asli   ambayo  INATIBU  na  KUPONYESHA  KABISA tatizo  la  LOW  SPERM COUNT pamoja  na  tatizo  la  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

 MAELEZO  YA  PICHA  YA  TIBA  HII  NI  KAMA  IFUATAVYO :
No. 1 :   Katika  tiba  hii  dawa  hii  inafanya  kazi  ya  kuongeza  kiwango  cha sperms.   Mtu  alie  tumia  dawa   hii  hutoa  sperms  nyingi  na  pia  wale   wanao   lalamika  kwamba  wakiwa  wanatoa  sperms zinakuwa  hazi  shoot  basi  hii  ni  tiba  sahihi kabisa  kwao kwani  mwanaume  akitumia  dawa  hii  basi  wakati  wa  kutoa  sperms  zinakuwa  zinatoka  kwa  mtindo wa  kushoot.

Mbali  na   kutibu  tatizo  la  low  sperms  count  dawa  hii  pia  inatumika  kuongeza  ute  ute  kwenye  joint  mbalimbali  mwilini  kama  vile  kwenye  magoti, viwiko  nakadhalika.  Ni tiba  nzuri  sana  kwa  mtu  aliye  vunjika  mifupa.  Kama  mtu  amevunjika  mifupa   akitumia   dawa  hii  itamfanyia  wepesi  sana  katika  tiba  yake  kwani    husaidia  sana  kuongeza uteute  kwenye  joints.

Dawa  hii  pia  husaidia  katika  kuipa nguvu  misuli ya  uume.
Jinsi  ya  kutayarisha  dawa  hii. Unamenya  kisha  una  I chip ( una  kata  kata  )  vipande  halafu  unavitia  ndani  ya  chupa  yenye  maji  au  chombo  chochote  chenye  maji.   Baada  ya  lisaa  limoja    ute  ute wa  dawa  hii  unakuwa  tayari  umefyonzwa  kwenye  maji  na  maji  yanabadilika  rangi  ya damu yam zee.

Na  jinsi  ya  kutumia  unakuwa  unatumia  kunywa  glasi  moja  asubuhi  na  glasi  moja  usiku  kwa  muda  wa  siku  thelathini.  Utaona  maajabu  makubwa  sana  katika suala  zima  la  kutoa  sperms  nyingi,  kushoot  sperms na nguvu  za  kiume  kuimarika

No.2  ; Haya  ni  mafuta  ya  asili  yenye  faida  nyingi sana katika  tiba . Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kisayansi  mafuta  haya   ya  asili  ndio  mafuta  yenye  nguvu  kuliko  mafuta  mengine  yoyote  yale  yatokanayo  na  miti au  mimea.  Hata  mafuta   ya  Mzeituni   pamoja  na  mafuta  ya  Habbat  Sawda  yanaachwa  mbali  kabisa  katika  ufanisi  wa  kitiba  na  mafuta  haya.  Kwa  lugha  nyingine  mafuta  haya  yana  nguvu  kubwa  kuliko  hata  mafuta ya  Habbat  sawda  na  mafuta  ya Mzeituni.

Tafiti  mbalimbali  za  kisayansi  zinaeleza  kuwa  mafuta  haya  yana  uwezo wa  kutibu  magonjwa  na  matatizo  ya  kiafya  karibu  yote  yanayo  msumbua  mwanadamu.

Mbali  na  kutumika  katika  tiba  dhidi  ya  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, mafuta  haya   yanatumika  pia  katika  tiba  ya  kupunguza  uzito  na  unene , kuondoa  manyama  uzembe  pamoja  na  kuondoa  mafuta  yasiyo hitajika  mwilini  yani  “  bad  cholesterol “

Vile  vile  mafuta  haya  yana  tajwa  na  wanasayansi  kuwa  na  uwezo  mkubwa  sana  wa  kutibu  tatizo  la  sukari  ya  kupanda  na kusawazisha  kiwango  cha  sukari  kwenye  damu.

Katika  tiba  dhidi  ya  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, mafuta  haya  husaidia kusafisha  mishipa  ya  damu  mwilini , kusafisha  mishipa  inayo  peleka  damu  kwenye  misuli  ya  uume,  kusawazisha  kiwango  cha  sukari  kwenye  damu,  kuondoa  mafuta  mabaya    kwenye  damu “ “bad cholesterol “ au   lehemu  mbaya  kwa  jina  lingine  pamoja  na  kubalance  homoni.

 Jinsi  ya  kutumia  mafuta  haya  katika  tiba  hii, mtumiaji  anatakiwa  kutumia  kichupa  kimoja  kila  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini. Kwa  hiyo  kila  siku  atakuwa anatumia  kichupa  kimoja kula  mafuta  haya  na  atakuwa  anakula  vifuniko  viwili  vya  mafuta  hayo  mara  tatu  kwa  siku  yani  asubuhi anakula  vifuniko  viwili, mchana  vifuniko  viwili  na  usiku  vifuniko  viwili. Atafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini.  Mteja wetu  atakae  hitaji   tiba  yetu  hii, atapatiwa  vichupa  vyote  thelathini  pamoja  dawa  namba  moja  na  namba  tatu.   Na  baada  ya  siku  hizo  thelathini  za  tiba  hii, basi mgonjwa  atakuwa  amepona  kabisa  tatizo  la  ukosefu  bna  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  pamoja  na  tatizo  la  low  sperm count.

No. 3.  Hii ni  dawa  yetu  ya  asili  iitwayo  Jiko  ambayo  inatokana  na  miti  na  mimea  mbalimbali. Dawa  hii  inafanya mambo mengi  sana  katika  tiba  ya  tatizo  la  ukosefu na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume. Baadhi  ya  mambo  hayo   ni pamoja  na  kuimarisha  mishipa na misuli   ya  uume, kutibu  uume  ulio legea  na kusinyaa  kwa  sababu  ya  punyeto, kukupa  wuezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  muda  mrefu  pamoja  na  uwezo  wa  kurudia tendo  la  ndoa   bila  kuchoka.  Dawa  hii  imeelezewa  zaidi  kupitia  makala  yetu  nyingine  ambayo    uanweza  kuisoma  hapa  chini:

http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/uhusiano-kati-ya-damu-na-tatizo-la.html?showComment=1531548155915#c4496211800795986975

JINSI  YA  KUPATA  TIBA  HII : Fika  katika  duka  letu. Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONA  HOUSING  nyuma  ya  jingo  la  UBUNGO  PLAZA.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba     0693   005  189.

Kwa  wateja  wetu  waliopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali popote  walipo  ndani  ya  jiji  la  Dar  Es Salaam ( HOME AND OFFICE  DELIVERY )

Na  kwa  wateja  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabus mbalimbali  na  wale  waliopo  Zanzibar  tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  boti . Pia  tunatuma  dawa   kwa  wateja w etu  waliopo  NAIROBI, MOMBASA, KAMPALA, KIGALI , BUJUMBURA  na  LUSAKA.

Kwa  taarifa   zaidi  kuhusu  huduma  zetu  tutembelee  kila  siku  kupitia  blogu  yetu :

www.neemaherbalist.blogspot.com

Mama Mjamzito na Mwanae Wafariki Dunia kwa Uzembe wa Muuguzi...Mkuu wa Wilaya Atoa Siku Tatu

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo
**
 Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo, ametoa saa 72 sawa na siku tatu kwa uongozi wa hospitali ya wilaya, kuwachukulia hatua kali watumishi wanaodaiwa kusababisha
kifo cha mjamzito.
 
Milo Peter (29), mkazi wa mtaa wa Masanga, Igunga, alifariki Desemba 29, mwaka huu na kuzikwa katika makaburi ya Masanga.
 
Baadhi ya wajawazito waliolazwa katika hospitali hiyo, waliwalalamikia watumishi wawili kufanya kazi kizembe, hali inayodaiwa kusababisha kifo cha Milo na mtoto.
 
Mbele ya diwani wa kata ya Igunga Charles Bomani, wajawazito hao, walidai mwenzao hakupata matibabu yanayostahili mapema, licha ya kuomba msaada kwa wauguzi waliokuwa zamu.
 
Kwa nyakati tofauti Blandina Enock, Rahel John, Rusia Ramadhani na Sikudhani Mrisho, walidai mwenzao alifikishwa hospitalini hapo Desemba 27, mwaka huu saa mbili usiku kwa ajili ya kujifungua.
 
Walisema kuwa, Milo alipofika alipewa kitanda huku ndugu zake waliomfikisha hospitalini, wakipewa ruhusa kuondoka.
 
"Jamani mnajua ufike wakati tuseme ukweli kwani kifo cha mama mwenzetu, kinaonekana kabisa uzembe umechangia.

"Sisi wenyewe tumeshuhudia kabisa namna ambavyo alikuwa akiomba msaada kwa wauguzi," alidai Rahel kwa niaba ya wenzake.
 
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Amada Kasigwa, alikiri kutokea kwa kifo hicho cha mjamzito na mtoto mchanga mwenye uzito wa kilogramu 3.8.
 
Alisema kuwa vifo hivyo vilitokea Desemba 28, mwaka huu na kudai hali hiyo imetokana na uzembe wa muuguzi wa zamu, Matinde Muhonye. 

Kwa mujibu wa Amada, mtumishi huyo alionywa kuhusu madai hayo ya ufanyaji kazi kizembe.

Bodi ya Pamba kuwaondolea machungu wakulima......RC Aggrey Mwanri Atoa Maagizo

$
0
0
Na Tiganya Vincet
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeagiza Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kuhakikisha inanunua pamba iliyobaki Daraja B (fifi) ya wakulima wa Urambo ili kutowakatisha tamaa ya kuendelea na kilimo hicho.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kufuatia malalamiko kutoka kwa wakulima wa zao hilo katika Kijiji cha Itengamatwi wilayani Urambo juu ya uwepo wa pamba ambao hadi hivi sasa iko katika maghala na wakulima hawajalipwa fedha.

Aliwataka wakulima kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa jitihada zinaendelea ili kuhakikisha pamba yao fifi(daraja B) ambayo hadi hivi sasa bado iko katika maghali ya kuhifadhi mazao inanunuliwa na Bodi ya Pamba Tanzana baada ya wanunuzi wa awali kusimamisha ununuzi na kuzima mashine.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wakulima kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha zao hilo ili kuepuka kuzalisha pamba Daraja B ambalo ndio wakati mwingine linakuwa kigezo cha wanunuzi kuwapa bei mbaya na wakati mwingine kukataa kununua pamba yao.

Alisema azimo la Mkoa wa Tabora katika msimu wa kilimo cha zao ujao ni  kila mkulima ni lazima azingatite kanuni kumi za zao hilo ikiwemo kuvuna kwa wakati na kuhifadhi katika hali ya usafi.

Mwanri alisema hatua hiyo itasaidia kulinda ubora wa zao hilo na kumsaidia mkulima kupata Daraja A na kulipwa bei ya juu itakayompa fedha nyingi ambazo zitasaidia kuboresha maisha yake.

Kwa upande wa Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Modest Kaijage aliwahakikishia wakulima wa pamba wilayani  Urambo ambao wana pamba fifi(Daraja B) kuwa Bodi imeamua kuinunua  na itawalipa malipo yao.

Alisema Mkurugenzi Mkuu wa TCB amesema kuwa wanafanya utaratibu ili waweze kununua pamba iliyobaki ambapo wao ndio wataifanyia uchambuzi kwa ajili ya msimu ujao.

Awali baadhi ya wakulima walisema kuwa walipokuwa wakihamasishwa kulima  pamba na wakati wa ununuzi waliambiwa kuwa pamba ina madaraja mawili lakini wakati wa mauzo pamba yao daraja B haikununuliwa na bado ipo katika maghali jambo linalowakatisha tamaa kuendelea na kilimo hicho.

Huna Sababu ya Kuabika Tena, Jipatie Dawa Bora ya Nguvu za Kiume, Maumbile Madogo na Mvuto wa Mapenzi

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiathiri watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine ....kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapungufu katika mwili wake.

Kuna sababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huathiri misuli ya uume, 


Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0620510598  / 0743543944

Ujenzi wa Mji wa serikali Dodoma wazidi kuwanyima usingizi mawaziri....Biteko Atoa Maagizo Mazito

$
0
0
Ujenzi wa Mji wa serikali kumeendelea kuwanyima usingizi viongozi na watendaji mbalimbali wakiwemo mawaziri.
 
Pia, serikali imetishia kuwanyang’anya zabuni ya upelekaji kokoto kwenye mji wa serikali Ihumwa baadhi ya kampuni za uzalishaji kutokana na kusimamisha uzalishaji kwa madai kuwa watendaji wake wapo likizo.
 
Uamuzi huo ulitolewa jijini hapa jana na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye viwanda vya kuzalisha kokoto vya kampuni ya Laroy Aggregates na WADI akiwa ameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde.
 
Katika ziara hiyo, viongozi hao walikuta viwanda hivyo havizalishi kokoto licha ya kuwa na zabuni ya kupeleka kwenye kandarasi zinazojenga majengo ya Wizara mbalimbali kwenye mji huo.
 
Hatua hiyo ilisababisha mawaziri hao kuwasiliana kwa simu na wamiliki wa kampuni hizo na kuwapatia maelekezo kuhakikisha ifi kapo Januari 3, mwakani wawe wameanza uzalishaji ili kuharakisha ujenzi wa mji huo.
 
Katika hatua nyingine, serikali imewataka watu wote wenye leseni za uchimbaji wa kokoto katika eneo la Chigongwe jijini Dodoma kuhakikisha wanafanya uzalishaji kwa kuwa serikali haitasita kuzichukua leseni hizo.
 
Naibu Waziri Biteko alisema wametembelea wazalishaji hao kutokana na ziara iliyofanywa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mji huo ambapo aliagiza ujenzi uende kwa kasi.
 
Alifafanua kwamba wakandarasi wanaofanya ujenzi katika mji wa serikali wanalalamika wazalishaji kokoto hawapeleki za kutosha na kusababisha ujenzi kutokwenda kwa kasi inayotakiwa, hivyo wameamua kutembelea ili washuhudie, ambapo wamekuta wengi wameenda kwenye mapumziko.
 
“Viwanda hivyo vimechukua zabuni Shirika la nyumba(NHC),
Shirika la Mzinga na kandarasi nyingine zinadai kokoto kwa ajili ya ujenzi huo. Cha kushangaza hawa ambao tumewapatia oda wameenda likizo wakati wajenzi wapo ‘site’ wanasubiri kokoto, tumeenda kwingine tumekuta mitambo ni mibovu inahitaji matengenezo,”alisema.
 
Biteko aliagiza wale wote waliopewa leseni za uchimbaji wafanye kwa weledi mkubwa na wale ambao hadi kufi kia tarehe hiyo watakuwa hawajaanza uzalishaji wa kokoto na kupeleka mchanga zabuni zao zitachukuliwa na kupewa kampuni nyingine nje ya Dodoma yatakayokuwa tayari kupeleka kokoto.
 
Alisema ujenzi huu unatakiwa kufanyika kwa kasi na kuwataka watu wote ambao hawafanyi vizuri watawafutia zabuni na kuwapatia watu wa Lugoba na Chalinze ambao wana uwezo wa kuzalisha na kukidhi mahitaji ya wakandarasi.
 
Naye, Naibu Waziri Mavunde alitoa rai kwa wazalishaji kuhakikisha wanakidhi matarajio ya ujenzi wa mji huo kwa kuwa ni fursa kwa watu wa Dodoma.
 
“Watu wa Dodoma tufanye kazi kwa weledi ili fursa tuliyokuwa tunaililia iweze kukidhi mahitaji kwa kuwa kuna mahitaji makubwa ya kokoto,” alisema.
 
Ofisa Madini Mkoa wa Dodoma, Jonas Mwano alisema atahakikisha anafuatilia kila siku kwa viwanda hivyo ili kukidhi
mahitaji ya ujenzi wa mji huo.
 
“Ofi si yangu imetoa leseni 75 za uchimbaji kokoto katika eneo la Chigongwe, nawataka wale wenye leseni waanze kuchimba ili kuongeza uzalishaji na wale ambao hawataweza
tutazichukua na kuwapa watu ambao wapo tayari kuanza uzalishaji,”alisema.
 
Alisema awali walisingizia soko lakini hivi sasa soko ni kubwa Dodoma kutokana na miradi mbalimbali ya ujenzi inayofanyika.
 
Ziara hiyo ilikuja siku chache baada ya Waziri Mkuu kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali na kukuta ujenzi ukisuasua.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika machimbo ya kokoto ya kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd, Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde na kushoto ni msaidizi wake Kungulu K. Masakala
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko, akitoa tamko la Serikali kwa wachimbaji wa kokoto alipofanya ziara kujionea kinachoendelea katika machimbo hayo baada ya kubainika uhaba wa kokoto katika eneo la ujenzi wa ofisi za Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto)  pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde (Kulia) wakiangalia moja ya kifaa kinachotumika katika kuchoronga mawe kwa ajili ya kokoto ambacho kwa sasa hakifanyi kazi kutokana na kuharibika. Katikati ni Fundi wa mashine katika mgodi wa WADI Gao Peng

Wenye mizani FEKI wazidi kubanwa

$
0
0
Katika kuhakikisha kwamba mnunuzi wa bidhaa hapunjwi, Wakala wa Vipimo Nchini (WMA), wameendelea kufanya ukaguzi wa mizani zinazotumika sehemu tofauti hasa kwa wauzaji wa zao la korosho.
 
Lengo la kufanya hivyo ni kutaka kubaini mizani zisizo na viwango ambazo hazitoi kipimo kinachostahili.
 
WMA ilitembelea baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika ili kushuhudia hali halisi ya upimaji korosho za wakulima.
 
Meneja wa WMA, mkoa wa Pwani, Evarist Masengo, alisema katika kuhakikisha wakulima wanauza mazao yao kwa kutumia mizani sahihi iliyohakikiwa na wakala huo, mizani 109 zimehakikiwa na kupigwa chapa ya Serikali.
 
Alisema mkoa wa Pwani una jumla ya vyama vya msingi (AMCOS) 95, ambavyo vinapatikana katika wilaya saba.
 
Wilaya na idadi ya vyama kwenye mabano ni Mkuranga (39), Kibaha (8), Bagamoyo (3), Chalinze (3), Kisarawe (2), Mafia (1), Rufi ji (13) na Kibiti (26).
 
Masengo alisema kutokana na elimu ambayo hutolewa na WMA kwa wakulima wa korosho na viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) kabla ya msimu, imesaidia kujua matumizi sahihi ya mizani.
 
Hatua hiyo imesaidia kupungua kwa tofauti ya uzito wa korosho unaotoka katika chama cha msingi na uzito unaopimwa kwenye ghala.
 
Pia, Masengo aliongeza kuwa hivi sasa wakala wa vipimo katika mkoa wa Pwani, unafanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye mizani inayopatikana kwenye vyama vya msingi na ile ya maghala makuu ili kujiridhisha kama walivyohakiki na kuziruhusu, zinapima kwa usahihi.
 
“Nawapongeza vyama vya msingi, wamejitahidi mizani nyingi tunakopita tunakuta ni sahihi na pale tunapogundua dosari ndogo ndogo zinafanyiwa marekebisho mara moja ili mkulima aendelee kupata faida ya jasho lake la kulima korosho,”alisema Masengo.
 
Kwa Mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura 340, Wakala wa Vipimo ndiyo yenye jukumu la kusimamia usahihi wa vipimo vinavyotumika au vinavyotarajiwa kutumika kufanyia biashara kwa lengo la kumlinda muuzaji na mnunuzi.
 
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi, Stella Kahwa kutoka WMA Makao Makuu, alipongeza juhudi zinazofanywa na ofi si ya wakala wa vipimo mkoa wa Pwani.

Waziri Kalemani Awanyooshea Kidole VISHOKA

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa onyo kali kwa watu wenye tabia ya kuhujumu miundombinu ya umeme pamoja na vishoka.
 
Waziri Kalemani alitoa kauli juzi akiwa katika ziara wilayani Kwimba, Mwanza na kuzungumza kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Ngulla na Ibindo, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme, kuwasha umeme na kuzungumza na wananchi.
 
“Mtu atakayebainika akikata nguzo, akiiba nyaya, akichezea transfoma kiasi cha kukosesha umeme wananchi, Mkuu wa Wilaya wa eneo husika atamweka korokoroni,” alisema.
 
Aidha, alisema kwa wale vishoka, wanaounganisha umeme kwenye nyumba za wananchi bila kuwa na taaluma hiyo, vilevile watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.
 
“Ikitokea tumekukamata, hatutajali wewe ni kibarua wa mkandarasi anayetekeleza miradi yetu ya umeme sehemu yoyote, utakamatwa na kuwekwa ndani,” alisisitiza Waziri.
 
Waziri Kalemani aliwaasa wananchi kuendelea kuwa makini kwa kujiepusha kuwatumia vishoka kwa kazi ya kufunga nyaya za umeme katika nyumba zao.
 
Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi kuutumia umeme kwa kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na hata vikubwa ili uwe na tija kwao na taifa kwa ujumla.
 
Naye Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa, pamoja na kuishukuru serikali kwa kuwapelekea wananchi wa jimbo lake umeme; aliwahamasisha kujitokeza kwa wingi kulipia, ili waunganishiwe huduma hiyo.
 
“Umeme huu unapokuja unahitaji watumiaji na watumiaji ni ninyi. Gharama za kupeleka umeme ni kubwa. Ni vizuri muwe mnajitokeza kwa wingi kuwasilisha maombi Tanesco, ili muunganishiwe na kuanza kuutumia kuboresha maisha yenu,” alisema.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Senyi Ngaga aliipongeza serikali kuwapelekea wananchi umeme na kuomba vijiji vichache ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo vipelekewe, ili nao wautumie katika shughuli za kujiongezea kipato na kuboresha hali zao za maisha.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya TANESCO, Wilaya ya Kwimba ina jumla ya vijiji 119 ambapo mpaka kufikia Julai 2020, vijiji 78 vitakuwa vimepatiwa umeme, sawa na asilimia 66 ya vijiji vyote vya wilaya hiyo.

Zitto Kabwe: Mwaka 2018 Nimesoma Vitabu 49

$
0
0
Tangu Mwaka 2012 nimekuwa naorodhesha vitabu nilivyosoma katika mwaka. Si vitabu vyote huviweka hapa kwani vingine huwa nasoma na kuviacha njiani ama kutopendezwa navyo au kwa kusahau tu.

Vitabu vingine huwa vitabu rejea na huvirudia kwa ajili ya mafunzo ili kufanya maamuzi Fulani Fulani au kwa ajili ya ibada (kwa mfano Quran) au kwa sababu nyenginezo. Nafurahi kuwa hivi sasa kwenye mitandao duniani kote watu wamekuwa wakiorodhesha vitabu ili kujengana katika utamaduni wa kusoma. Barack Obama yeye alianza kuweka orodha yake mwaka 2015 na tayari ameshaweka orodha ya mwaka huu. Obama pia huweka orodha ya muziki aliyopenda mwaka huo. Inavutia.

Mwaka huu nimesoma vitabu 49 (kutoka vitabu 36 + 3 vya mwaka 2017). Wakati natoa orodha yangu 23/12/2017 nilikuwa bado nasoma riwaya za Jumba Maro ya Ally Saleh na The Feast of the Goat cha Mario Vargos Llosa ambazo nilizimaliza nikiwa Maputo, Msumbiji. 

Pia niliweza kuongeza Simulizi iitwayo Zeitoun ya Dave Eggers kuhusu kimbunga cha Katrina huko New Orleans, Marekani. Hii ni simulizi ya wahamiaji kutoka Syria walivyoshiriki kuokoa makumi ya watu kutoka kwenye maafa ya Hurricane Katrina.

Mwaka 2018 nimesoma mchanyato kidogo kuliko mwaka 2017 ambapo dhima (themes) kadhaa ziliniongoza. Hata hivyo bado njaa yangu ya kuwasoma madikteta duniani iliendelea kuniongoza kwa lengo la kupata ufahamu na maarifa ya namna ya kuchangia katika kuzuia nchi yetu kuangukia kwenye utawala wa Imla. Pia nilijaribu kutafuta majawabu ya changamoto hizo. Kwenye dhima hiyo nilisoma:

- The Death of Democracy: Hitler’s Rise to Power
Benjamin C Hett

- The Plots Against Hitler
Danny Orbach

- Franco: Anatomy of a Dictator
Enrique Moradiellos

1 The New Sultan: Erdogan and the Crisis of Modern Turkey
Oner Cagaptey

- How Democracies Die
D Ziblatt and S Levitsky

Kama nilivyopata kusema, ninapenda na kujivunia sana historia ya ukombozi dhidi ya ukoloni barani Afrika na haswa Ukombozi wa Kusini mwa Afrika. 

Mwaka huu niliongeza maarifa katika eneo hilo kwa kusoma sio tu habari nzuri za vyama vya ukombozi bali pia baadhi ya makosa waliyofanya viongozi wetu. SWAPO Captive kilichoandikwa na Bwana Angula ni simulizi muhimu sana kusoma ili kuona namna baadhi ya watu walivyoonewa kwenye harakati za ukombozi. Kwa jina la ukombozi watu huonewa, huteswa na hata huuwawa. Pia nilisoma kuhusu mashujaa wa ukombozi na athari kwa familia zao. Katika dhima hii ya Ukombozi nilisoma:

- Cuito Cuanavale: 12 Months of War That Transformed a Continent
Fred Bridgland

- Africa Tomorrow
Edem Kadjo

- Umkontho we Sizwe: The ANC Armed Struggle
Thula Simpson

- Mozambique: Sowing the Seeds of Revolution
Samora Machel

- 491 Days
Winnie Mandela

- Thabo Mbeki
Adekeye Adebajo

- Umkontho we Sizwe
Janet Cherry

- Chris Hani
Hugh Macmillan

- Being Chris Hani’s Daughter
Lindiwe Hani and Melinda Ferguson

- SWAPO Captive: A Comrade’s Experience of Betrayal and Torture
Oiva Angula

Pia nilisoma vitabu vya hali ya sasa ya Afrika Kusini baada ya ukombozi:

- No Longer Whispering to Power: The Story of Thuli Madonsela
Thandine Gqubule

- How to Steal A City: The Battle for Nelson Mandela Bay, An Inside Account
Crispian Olver

- How to Steal A Country? State Capture and Hope for the Future in South Africa
Robin Renwick

- Coalition Country: South Africa After the ANC
Leon Schreiber

Kama Mtanzania ninayejiandaa kwa majukumu muhimu ya kitaifa nimekuwa nikipenda kupata maarifa Zaidi kuhusu Historia ya Zanzibar. Mwaka 2018 niliongeza maarifa kwa kusoma vitabu kadhaa ikiwemo:

- The Threat of Liberation: Imperialism and Revolution in Zanzibar
Amrit Wilson

- Social Memory, Silenced Voices and Political Struggle: Remembering the Revolution in Zanzibar.
(Ed) W. Cunningham and M. Fouere

Vitabu vinavyofuata ni mchanyato wa riwaya, historia za watu na mataifa mengine, mafunzo ya uchumi na kadhalika. Vitabu vinavyohusu Marekani na utawala wao mpya chini ya Trump ni kwa lengo la kujifunza nini kinaendelea huko. Kitabu cha Deng Xiaoping nilipewa na ndugu yangu Harith Ghassany katika mjadala wa kisomi wa kutafuta modeli sahihi ya kimaendeleo kwa nchi zetu za Afrika.

- Pakistan: Personal Story
Imran Khan

- Making Africa Work: A Handbook for Economic Success
Gregg Mills, O Obasanjo, et al

- Sidetracked
Henning Mankell

- In Praise of Blood: The Crimes of Rwandan Patriotic Front
Judi Rever

- Thomas Sankara Speaks
Thomas Sankara

- A Higher Loyalty
James Comey

- State Secrets: Deathly High Stakes in the Corridors of Power
Quintin Jardine

- Deng Xiaoping and The Transformation of China
Ezra F Vogel

- Gorbachev: His Life and Times
William Taubman

- Tell Tale
Jeffrey Archer

- The Growth Delusion
David Pilling

- CTRL ALT DELETE: How Politics and The Media Crashed Our Democracy
Tom Baldwin

- Unhinged: An Insider’s Account of The Trump White House
Omarosa Manigault

- Fire and Fury: Inside The Trump White House
Michael Wolf

- Why The Dutch are Different
Ben Coates

- The French Revolution: What Went Wrong
Stephen Clarke

- An Extra Ordinary Life: A Passion for Service
V J Mwanga

- Uwajibikaji Ndani ya Kalamu Isiyokuwa na Wino
Ludovich Utouh

- Betting the House: Inside Story of the 2017 Elections
Tim Ross and Tom McTaguwe

- In Defence of Bolsheviks
Max Shachtman

- The Future That Works: Selected Writings of A M Babu
(Ed) Salma Babu and Amrit Wilson

- Our Commonwealth: The Return of Public Ownership in USA
Thomas Hanna

- Democracy, Direct Action and Socialism: A Debate of Fundamentals
Michael Foot and Sean M

Mwaka huu ukiwa unaelekea ukingoni, Wachapishaji wa Vitabu Mkuki na Nyota Publishers walichapisha upya vitabu vya harakati za Willy Gamba, mpelelezi maarufu barani Afrika. Rafiki yangu katika kusoma vitabu Fadhy Mtanga (ambaye pia ni adui yangu kwenye soka – maana yeye ni shabiki mandazi wa Manchester United FC na mimi shabiki wa mabingwa watarajiwa Liverpool FC) alininunulia vitabu vyote 4 vya Mzee Elvis Musiba. Nilikuwa na muda wa kutosha na kuvisoma vyote bila kuweka chini. Namshukuru sana Fadhy kwa zawadi yake murua kabisa. Vitabu hivi ni:

- Kikosi Cha Kisasi
A E Musiba

- Njama
A E Musiba

- Kufa na Kupona
A E Musiba

- Hofu
A E Musiba

Kitabu changu cha mwisho mwaka 2018 ni :

- Dear Ijeawele OR A Feminist Manifesto in 15 Suggestions
Chimamanda Adichie

Vitabu 3 vilivyonigusa sana
The Death of Democracy
: Hitler’s rise to power cha Benjamin Hett kilinigusa sana kutokana na namna wanasiasa wanavyoweza kufanya makosa yenye kudidimiza nchi kwa sababu tu ya kulinda madaraka. Katika kitabu hiki somo kubwa ni namna Wabunge wa vyama vyote vya Siasa walivyomruhusu Adolf Hitler kutunga sheria inayompa mamlaka makubwa wakiamini kuwa Hitler ana nia njema na atawalinda. 


Wabunge wa Chama cha SDP ndio pekee walikataa, walizomewa, kuzodolewa na hata kuuwawa. Wengine walikimbilia uhamishoni. Ndani ya miezi michache, hata wale waliomwunga mkono Hitler walishughulikiwa na Taifa la Ujerumani likaingia kwenye taharuki kubwa na hatimaye vita vya pili vya dunia. 

Waliompa madaraka Hitler waliamini kuwa watamdhibiti. Hawakuweza. Historia kama hii ipo lakini wanaadam hatujifunzi tunarudia makossa hayo kila wakati katika nchi mbalimbali duniani.

How Democracies Die cha Ziblatt na Levitsky kilinigusa sana kwa kuwa kinatoa majawabu ya changamoto za demokrasia kuanguka. Licha ya kwamba ni kitabu maalumu kwa muktadha wa nchi ya Marekani, kitabu hiki nilicholetewa na rafiki yangu Rakesh Rajani, kinatazama mifano ya nchi mbalimbali duniani kama Colombia na njia walizotumia kuhami demokrasia (walitumia sana Bunge na Mahakama), Venezuela (jinsi mgomo wa vyama vya upinzani kutoshiriki chaguzi ulivyotoa nafasi ubwete kwa chama tawala) na hata Ujerumani ambayo hali yake nimeeleza hapo awali. 

Somo kubwa kabisa kutoka kitabu hiki ni kwamba ni lazima wadau wote wa demokrasia kushirikiana pamoja kupambana na udikteta bila kujali tofauti ndogo ndogo au kubwa kubwa miongoni mwao. Bila ushirikiano dikteta husaga saga kila mmoja. Ni Kitabu nashauri kila mwana demokrasia akisome.

Dear Ijeawele Or A Feminist Manifesto in 15 Suggestions cha Chimamanda Adichie ni kitabu kidogo sana kwa idadi ya kurasa. Kwa hakika ni barua ambayo Chimamanda kamwandikia rafikiye ambaye amepata mtoto wa kike na anamshauri amkuze vipi mtoto huyu. Kijitabu hiki kimenigusa kwa sababu kinatoa changamoto kadhaa kwa sisi wanaume katika malezi. 

Kuna mambo ambayo tunafanya tunaona kama ni msaada kumbe inapaswa kuwa wajibu kwa familia. Kwa mfano, mara nyingi husikia wanaume tukisema ‘leo nafanya kazi ya kulea mke wangu kasafiri’ ama kwa kimombo ‘baby-sitting’. Chimamanda anatuambia hapa, Baba mtoto hafanyi ‘baby-sitting’ bali anatimiza wajibu wake kama baba. Pia kinachoitwa ‘gender roles’ kwenye nyumba zetu kiasi kwamba tunazuia watoto wa kike kukua na kukuza vipawa vyao vyote. 

Nashauri wenye watoto wa kike wasome kijitabu hiki, wababa na wamama kwani kinaweza kuchangia kubadili mtazamo wako wa namna tunalea watoto wetu wa kike. Mapendekezo 15 ya Chimamanda unaweza usiyakubali yote lakini yana mafunzo mengi ambayo yanaweza kukufaa kwenye malezi ya mabinti zetu.

Heri ya Mwaka mpya 2019

Zitto Kabwe
Dar es Salaam
30/12/2018

Habari Njema Kwa Wenye Matatizo Ya Nguvu za Kiume, vitambi, nyama uzembe

$
0
0
NAUHABARISHA ULIMWENGU TIBA BORA YA MITI SHAMBA..

  Ninatibu magonjwa 1-100 dawa ninazo Sasa.

KOLA; ni dawa ya kisukari dozi siku 14 ata kama unajihisi itumie kwa kinga zaidi

  THREE(3) POWER MIX,inatibu Nguvu za kiume Ni dawa iliyo Bora na Humfanya mume kuchelewa kufika kileleni dkk 40_47 bila kuchoka.Inaanza kufanya kazi ndani ya door 80 na inatibu kabisa ndani ya siku 6 tu,hutatumia Tena dawa ya Nguvu za kiume three power mix Ni kiboko kabisa,hata Kama unahisi una tatizo unaruhusiwa kutumia kwa ajili ya Kinga baadae.

 DUDUMA MIX 4 POWER,hunenepesha na kurefusha uume na kukomaza uume uliosinyaa kwa mda mfupi,tumia siku 4 na kupona kabisa.

  SHOOLA,Ni dawa ya kutibu tezi dume na kupona kabisa ni ya miti shamba hutumika kwa kunywa bila upasuaji ndani ya siku 14 haina madhara.

 NENGONENGO,dawa ya kutibu Uzazi kwa akina mama walioshindwa kubeba mimba kwa mda mrefu ukitumia utaweza kupata mimba na kujifungua salama.

  KAMINGO,Ni dawa inayotibu Busha bila kufanyiwa operation na aliyevimba korodani inatibu kabisa dozi Ni siku 7 na inaubora wa Hali ya just na unapona kabisa.

  IKUMBIJA,Ni dawa ya kumvuta mpenzi aliekuacha na mwenye ahadi za uongo kukutimizia,na kumkomesha mtu asiwe na mtu mwingine pia atakurudia ndani ya masaa 6.

   MALAMALA,Ni dawa ya vidonda vya tumbo na tumbo kujaa gesi, kilungulia na inafanya kazi kwa haraka zaidi na kupona kabisa ndani ya siku 6.
 

SAALA,Ni dawa inayotibu miguu kuwaka moto,kiuno,mgongo,magoti na viungo vyote mwilini na joints,Sasa tiba yake Ipo kwangu.

   HALALA MIX,Ni dawa mix ya miti 100 inayotibu matatizo yote,Kama majini,kesi,biashara,kazi,mitego na kupoteza kumbukumbu. no

TUNAFANYA KAZI SIKU ZOTE PIA NAKUFIKIA POPOTE ULIPO KWA HARAKA,NAPATIKANA DAR ES SALAAM NA KAHAMA,PIA NINA MAWAKALA MIKOANI SIMIYU,SHINYANGA,MOSHI NA MBEYA.


     KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA: 0784 475946
           0744 922982
    DR,SANDALA.

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Bwana harusi afariki dunia akisubiri kufunga ndoa kanisani

$
0
0
Sherehe ya harusi iliyokuwa ifanyike juzi jioni katika Kanisa la Nabii wa Utukufu wa Bwana lilipo Olmatejoo, Kata ya Sakina jijini Arusha  kwenye ukumbi wa Sariko Olasiti Garden, iligeuka msiba baada ya bwana harusi kufariki dunia ghafla akiwa kanisani.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 11 jioni katika kanisa hilo ambapo bwana harusi huyo, Heaven Makupa (47) alikuwa kanisani tangu saa saba mchana akisubiri kufunga ndoa na Jane Kimaro.

Hata hivyo, wakati sherehe, nderemo na vifijo vikiendelea vikiongozwa na kikundi cha matarumbeta nje ya kanisa huku bibi harusi akiingia kanisani, Heaven alianza kujisikia vibaya na kupoteza fahamu.

Kutokana na hali hiyo alikimbizwa Hospitali ya St Elizabeth, lakini alifikishwa akiwa tayari amefariki na mwili wake kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

Mhudumu wa chumba hicho, Fransis Costa jana alikiri kuwa wanaendelea kuuhifadhi mwili wa bwana harusi huyo.

Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe na kiongozi wa kanisa hilo, Nabii Peter Alayce na tayari taratibu zote zilikuwa zimekamilika tangu mchana alipofika bwana harusi na ujumbe wake.

Wakati kifo hicho kinatokea mamia ya watu walikuwa tayari wamefika katika ukumbi wa Sariko Olasiti Garden kuwasubiri maharusi hao ili kuendelea na sherehe.

Kutokana na tukio hilo, bibi harusi, Jane, alipatwa na mshtuko ambapo hadi jana baadhi ya ndugu zake ambao hawakupenda kuzungumzia msiba huo walisema alikuwa amepumzishwa.

Credit:Mwananchi

Picha: Fid Q amvisha pete ya uchumba mpenzi wake

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake.

Rapper huyo ame-share picha kadhaa kwenye ukurasa wake wa Instagram zikionyesha hatua hiyo muhimu kuelekea kwenye maisha ya ndoa.
 
Utakumbuka December 08 mwaka huu rapper kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili naye pia alimvisha pete ya uchumba mpenzi wake.

Rudisha heshima yako Kwa Mpenzi Wako, Mke Wako...Tumia Tiba Hii ya Asili

$
0
0
Rudisha heshima yako sasa kwa kutumia Dawa hii iitwayo SUPER GAFINA, kwa ajili ya nguvu za kiume na NKOLOMIJE ni kwaajili ya kuongeza maumbile.

Kwa mwanaume aliye kamilika anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara mbili ,ila ukiwa unapiga moja tena kwa shida wewe ujue  unamatatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

TIBA YA TATIZO LAKO NI; Dawa iitwayo SUPER GAFINA, dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge na unga wa asili ambavyo havina madhara kwa mtumiaji ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja;-

1).itakufanya urudie tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuchoka.

2).ltakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dk.15 hadi 20 kwa tendo la kwanza.

3).lnaimarisha uume uliolegea na uliosinyaa na kuupa nguvu maradufu.

Je unamaumbile madogo pamoja na uume mfupi? NKOLOMIJE ni suluisho la tatizo lako. Na ni dawa inayoboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi kuanzia inch. 5 hadi 8 kwa muda mfupi sana .Dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk.30 ukisha tumia guarantee miaka 50  ikishakutibu.

Pia ninatibu;- KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU, MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE ,BP, NK.

IGULYATI, ni dawa ya mvuto wa biashara, kazi,kupandishwa cheo na humfanya mfanyakazi kupendwa na mwajiri wake. Pia humvuta mke,Mme,hawara ,mchumba unae muitaji utampata kwa dk.30 tu na atatulia na kumfunga asitoke nje ya ndoa, Pia natoa Pete za bahati ambazo zimetajirisha wengi.

Pia ipo dawa ya kupunguza matiti,unene ,tumbo,na kitambi ,hupunguza mafuta ,kuondoa makovu,chunusi,michilizi mwilini na kuongeza hipsi, makalio na mguu wa bia nk. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na DR,HOSUTWA .Anapatikana Mbagara

Simu no, 0756241666 na 0672186977.

       Huduma hii utaipata popote ulipo

Mwendokasi Yatoa Taarifa ya Basi Lake Lililoungua

$
0
0
Kampuni  inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (UDA-RT) imeeleza chanzo cha ajali iliyoyokea mchana Desemba 25, mwaka huu eneo la Ubungo Maji ilitokana na hitilafu ya mfumo wa umeme.

Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa UDART,  John Nguya kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 155 ,lilikuwa likitokea Kimara kwenda Gerezani lilishika moto kwenye injini na kuwatia hofu abiria na wananchi wengine.

Alisema kuwa moto huo ulidhibitiwa kwa ushirikiano wa wananchi waliokuwa eneo hilo,Jeshi la Zima Moto na Uokoaji , Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa UDART kwa kutumia vifaa vya kuzima moto vilivyomo kwenye magari hayo.

“Tungependa wananchi wafahamu kwamba usalama wa mabasi yote ya UDA -RT umedhibitiwa kwa asilimia 100 kuwa matengenezo take yanafanyika kwa umahiri ,viwango vya kimataifa  kwa wasimamizi na watalaam kutoka kampuni ya Xiamen Golden Dragon ya China, Cummings ya Marekani ya kimataifa na Voith ya Ujerumani.

“Ndani ya mabasi hayo eneo la injini vipo vizimia koto vitatu vilivyotengenezwa humor na kuzima moto baada ya koto kuzidi na ndivyo ilivyokuwa wakati wa tukio na pia mabasi makubea kuna vizimia moto vinne vyenye ujazo wa kilogramu tatu katika kila mlango mikubwa ya pande zote mbili kwa akili ya dharura,” alisema Nguya.

Nguya alisema kuwa kwa mujibu wa sheria katika mabasi yote  makubwa vipo vizimia moto vine vyenye ujazo wa kilogramu tatu kila kimoja na milango mikubwa pande zorte mbili kwa ajili ya dharura na matumizi ya kawaida.

Serikali Kuwachukulia Hatua Kali Wamiliki wa Maabara Binafsi Wasiofuata Taratibu

$
0
0

Wamiliki wa maabara na vituo vya afya nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao mara moja bila shurti kabla ya Januari 15 2019 kwa kuhakikisha wanakamilisha vigezo vyote vya umiliki maabara hizo kwa kuwa muda wa kutoa elimu umepita na sasa ni muda wa kazi tu.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa  Tiba wa Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto na Mkurugenzi wa bodi ya usajili wa maabara Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa hadi kufikia Septemba 2018 bodi ya usimamizi wa maabara binafsi ilitambua jumla ya maabara 641 zinazojitegemea na maabara 719 zilizoshikizwa kwenye vituo vya tiba vya watu binafsi vya ngazi mbalimbali.

Amesema kuwa kutokana na baadhi ya wamiliki wa maabara binafsi hasa zilizoshikizwa kutofuata maadili ya uwajibikaji kisheria kufikia Septemba 20, bodi kupitia ziara yake imebaini kuwa kati ya vituo vya tiba 1731vya  watu binafsi vyenye maabara ndani ni maabara 1012 sawa na asilimia 58 pekee ndizo zilizotimiza wajibu wake wa kujiandikisha kwenye bodi ya usimamizi wa maabara binafsi na kutekeleza matakwa ya kisheria.

Amesema kuwa wamiliki ambao hawatatekeleza wajibu wao wa kumiliki maabara hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kifungo pamoja na faini au vyote kwa pamoja.

Amewataka wamiliki hao kuhakikisha kuwa kila mmoja awe amekidhi vigezo vyote vya umiliki wa maabara ikiwa ni pamoja na kulipa ada zote stahiki zikiwemo malimbukizo ya nyuma na faini stahiki pamoja na kuwa na risiti halali za malipo hayo. Pia amewataka wamiliki wa maabara hizo kulipa tozo stahiki kila mwaka ili kuwezesha bodi kufanya uhakiki wa kudumu wa huduma zitolewazo katika maabara hizo.

Vilevile amesema kuwa katika kutekeleza hilo watatoa orodha za zahanati katika gazeti la Serikali na zahanati isiyokuwapo kwenye orodha hiyo haitatakiwa kutoa huduma yoyote na watakaokiuka watakutana na mkono wa dola. Gwajima ametoa mwito kwa serikali katika ngazi zote  kushirikiana na kutoa taarifa  dhidi ya wavunja sheria na kufanikisha  kuipeleka mbele sekta hiyo.

Akieleza kuhusiana na faini zitakazotolewa Kaimu Afisa msajili wa bodi ya usimamizi ya maabara binafsi Neema Halliye amesema kuwa kwa mujibu wa sheria watakaokiuka sheria hiyo watapigwa faini ya kulipa kiasi cha shilingi laki mbili au kufungwa miaka miwili au vyote kwa pamoja na bado maboresho ya sheria hiyo yanafanyiwa kazi ili kuweza kutoa kibano zaidi.

Polisi Dodoma Wakanusha Mtoto Kufungiwa Kabatini

$
0
0
Wakati binti wa kazi akieleza jinsi mwanaye mwenye umri wa miezi mitano alivyofungiwa kabatini na  mwajiri wake mkoani Dodoma kwa muda wa miezi sita, Jeshi la Polisi mkoani humo limekanusha madai ya mtoto huyo kufungiwa kabatini.

Binti huyo wa miaka 15, jana Desemba 30, 2018 akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alidai kufanyiwa ukatili kwa kupigwa na kufanyishwa kazi hadi usiku wa manane  na bosi wake anayedaiwa kuwa ni mwalimu na kwamba amekuwa akimwambia amfungie hadi usiku mtoto wake na kila alipovunja masharti alikumbana na kipigo.

Leo Desemba 31, 2018 polisi mkoani Dodoma imekanusha madai ya mtoto  huyo kufungiwa kabatini kama inavyodaiwa, lakini wamekiri binti huyo kushambuliwa na mwajiri wake.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema polisi wamefanya upekuzi katika nyumba ya mwajiri wa binti huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu, Anitha Kimako na kubaini hakuwa na kabati nyumbani kwake.

"Kesi ya shambulio ipo na ameshambuliwa kweli na ndiyo maana tunamshikilia. Anashikiliwa kutokana na usalama wake kwani kelele za watu ni nyingi, ila hili suala la kuwekwa mtoto kabatini halipo," amesema Muroto.

Amesema uchunguzi wa kina unafanyika na kwamba lazima mwalimu huyo wa Shule ya Msingi Medali afikishwe mahakamani.

Nandy Awapa Wazazi Wake Zawadi ya Nyumba ya Mamilioni

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy alimaarufu The African Princess, ameamua kuweka wazi nyumba aliyowajengea wazazi wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nandy ameandika haya:- ”
A small gift for my parent this year 2018…🏠
Zawadi ndogo ya wazazi wangu mwaka huu 2018..
.
WISDOM IS POWER”

“Nilikuwa na furaha sana wakati na shoot hii nyumba!!! So so so happy for 2018…🏠...”

“Mungu wangu na Baba yangu najua nakukosea sana kama binadamu na kama kijana ila nikipiga goti unajua namaanisha kutoka moyoni mwangu na unajua hakuna ninaye mtegemea zaidi yako… Asante kwakunipa uvumilivu, unyenyekevu, katika maisha yangu hasa kipindi hiki cha mwaka 2018!! Asante kwa hii zawadi ndogo ya wazazi wangu najua hii ni ndoto ya kila kijana mwenye kutafuta!!! Ni kila ndoto ya mwanadamu yoyote duniani kuona wazazi wake wako na furaha na ndiyo baraka zenyewe . Nashukuru media zote , blogs zote, ma producers wote, ma promoters wote, familia yangu ya THT, familia yangu ya clouds ,management yangu, Team yangu, marafiki zangu, Baba yangu wa kiroho Mtumishi MWAMPOSA , na mafans wangu wote ,bila kusahau na hatters wote kwa kunipa nguvuu na supports kwa namna moja au nyingine uwepo wenu ndio mafanikio yangu……..
Nili jipa nguvu kabla sijapewa
Nilijipa moyo kabla sijapewa
Nilijiamini kabla yakuaminika
Nilijikubali kabla yakukubalika
Popote ulipo kijana mwenye ndoto yoyote ile jua inawezekana ukiweka nia ukikubali mazuri na mabaya yote yakufikie sababu ni daraja na nguzo ya mafanikio yako bila kusahau MUNGU ndio kila kitu. Nawapenda
HAPPY NEW YEAR IN ADVANCE 👑
#DADAMWENYENYUMBA”
 

Jeshi la Polisi Dar Latoa Dakika Tano za Kuoiga Fataki Mwaka....Latoa Onyo Utapeli Unaoendelea Nchini

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam Lazaro Mambosasa amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja Jeshi hilo limefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 29, zilizotokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani ambayo watuhumiwa wake walikiri kufanya.

Mambosasa ameyasema hayo leo Desemba 31, 2018, Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa jeshi hilo na mafanikio yake katika kipindi cha mwaka mmoja.

"Kipindi cha mwaka mmoja fedha tulizofanikiwa kukusanya ni bilioni 29, kwa watuhumiwa wa makosa ya kukamatwa kwa vyombo vya usafiri na wenyewe wakakiri kufanya makosa hayo".

Aidha Kamanda Mambosasa ameogeza, "naomba wadau tushirikiane kwa pamoja kuhusu wahamiaji haramu, kwa hapa DSM kuna wimbi kubwa la matapeli ambao ni raia wa kigeni na wanafanya uhalifu, hili eneo si la kufumbiwa macho, unakuta mstaafu katoka kuchukua kiinua mgongo, anatapeliwa".

"Wanachi wanaumizwa kweli mmoja hapo chini kuna mstaafu ametapeliwa milioni 120, na mnigeria ambaye ameingia nchini na anaishi bila kibali."

Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amewaonya wananchi watakaosherehekea mkesha wa mwaka mpya kwa kufyatua mafataki badala yake ametoa dakika 5 kwa watakaotaka kufanya tukio hilo kuanzia saa 6 kamili usiku hadi saa 6.05 usiku.

“Milipuko yoyote hatutaruhusu isipokuwa kwa wale waliopewa kibali hasa kwenye mahoteli ya nyota tano. Hawa ndio watakaofyatua fataki tena ziwe nyepesi na si nzito,” amesema Mambosasa.

“Wakati wakiendelea na ufyatuaji, polisi watakuwepo eneo husika na atakayekwenda kinyume na maagizo atachukuliwa hatua.”

Mambosasa amewaonya wananchi kutochoma matairi kwenye barabara, watakaobainika watakamatwa.

Mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini Pancras Ndejembi Kuzikwa Kesho

$
0
0
Mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini Pancras Ndejembi unatarajia kuzikwa kesho Jumanne Januari Mosi, 2019 katika  kitongoji cha Chizomoche kijiji cha Bihawana Jijini Dodoma.

Ndejembi (90) alifariki dunia Jumamosi Desemba 29, 2018 saa 2  asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Mweyekiti wa kamati ya mazishi, David Mzuri amesema leo Jumatatu Desemba 31, 2018 kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo watoto wa marehemu ambao walikuwa wanasubiriwa kutoka nje ya nchi.

Mzuri amesema mwili wa marehemu ulitarajia kuchukuliwa hospitali leo na kulala nyumbani kwake mtaa wa Uzunguni kata ya Kilimani.

“Kesho  saa sita mchana tutapeleka mwili wa mpendwa wetu Kanisa la Mtakatifu Paul wa Msalaba na ibada itafanyika pale kisha msafara utaelekea Chizomoche kwa ajili ya mazishi,” amesema.

Baadhi ya viongozi waliofika nyumbani kwa marehemu ni mawaziri wakuu wastaafu Mizengo Pinda na John Malecela. Viongozi wengine wastaafu ni Balozi Job Lusinde, Joseph Butiku, William Kusila na Hezekia Chibulunje.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images