Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH....Anatoa Pete za Bahati, Anasafisha Nyota, Anazuia Chuma Ulete na Mengine

0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam Shariff,  Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
 
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
 
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Adam Shariff Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. 

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Mawasiliaono: +255715971688  au +255756914036
 
Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

Huna Sababu ya Kuabika Tena, Jipatie Dawa Bora ya Nguvu za Kiume, Maumbile Madogo na Mvuto wa Mapenzi

0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiathiri watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine ....kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapungufu katika mwili wake.

Kuna sababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huathiri misuli ya uume, 


Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0620510598  / 0743543944

Waziri wa Kilimo aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote hapa nchini

0
0
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amewaagiza Wakurugenzi wa Bodi za Mazao kuanza mara moja zoezi la kuwatambua na kuwasajili wakulima wa mazao yote nchini lengo likiwa kuwatambua ili kupanga mipango sahihi yenye kuongeza tija na uzalishaji katika mazao yote.

Ametoa agizo hilo jana tarehe 29 Disemba 2018 wakati akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.

Mhe. Hasunga amesema ili kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya kilimo na kuandaa mipango madhubuti ya kuendeleza mazao yote ni vyema kuwatambua Wakulima wote nchini na kuongeza kuwa Wakulima wa zao la korosho wametoa funzo kubwa kwa Wizara yake kufanya jambo kama hili katika mazao mengine hapa nchini.

Itakumbukwa kuwa wiki tatu zilizopita, Waziri Hasunga alitoa agizo kwa Bodi ya Korosho agizo kuandaa daftali maalumu la kuwatambua Wakulima wa korosho kote nchi ambapo moja ya taarifa ambazo zitajumuishwa katika daftali hilo ni pamoja na Jina Kamili la Mkulima, Mkoa, Wilaya, Kata na Tarafa anayotoka.Mambo mengine ni pamoja na Kitongoji, Mtaa au Jina la Kijijini anapotoka, mahali lilipo shamba pamoja na ukubwa wa shamba lake.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa mipango sahihi ya kuwaendeleza Wakulima kuanzia kwenye kilimo chenyewe hadi kufikia katika hatua ya kuvuna, kuhifadhi na kulifikia soko ni vyema kuwa na mfumo maalumu wa kanzi data (Database) ya kuwafahamu ili kushughulikia mahitaji yao kisasa na kwa haraka zaidi.

Waziri Hasunga alienda mbali na kushauri matumizi ya TEHAMA na ya Mfumo wa GPS ili kuboresha daftari hilo kwa lengo la kuboresha uwekaji wa taarifa za Wakulima na maeneo wanayotoka Wakulima kwa usahihi zaidi.

“Tumepata changamoto kadhaa wakati wa kuwahakiki Wakulima wa korosho katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Ruvuma na kama Bodi ya Korosho ingekuwa makini kuandaa daftari la Wakulima zoezi la uhakiki lingekuwa rahisi, kwa ajili hiyo niliwaagiza Bodi ya Korosho kukamilisha zoezi hili mpaka Mwezi Machi, 2019 na Bodi za Mazao zilizobaki ukiacha Bodi ya Tumbaku ambao wao tayari walishafanya hivyo, kukamilisha Mwezi June, 2019”. Amekaririwa Mhe. Hasunga.

Waziri ameitisha kikao maalumu na Viongozi wa Bodi za Mazao, Wakala na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo kwa lengo la kuboresha mikakati na kuongeza ufanisi katika utendaji wa Wizara pamoja na kujitathmini kabla ya kufikia nusu mwaka wa utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti ya Wizara ya mwaka 2018/2019 ili kujipanga kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya kilimo ya mwaka ujao wa 2019/2020.

Bodi za Mazao zilizoshiriki mkutano huo ni pamoja na Bodi ya Korosho, Bodi ya Pamba, Bodi ya Mkonge, Bodi ya Pareto, Bodi ya Chai, Bodi ya Kahawa, Bodi ya Tumbaku, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na Bodi ya Sukari.Wakala zilizoshiriki ni pamoja na Wakala wa Taifa wa Mbolea (ASA) Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai (TSHTDA).

Taasisi nyengine za Wizara ya Kilimo zilizoshiriki ni pamoja na Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu (TOSCI), Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF), Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA), Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) na Bodi ya Leseni za Maghala.

Stempu Za Kielektroniki Za Ushuru Wa Bidhaa Kuanza Kutumika Januari, 2019

0
0
Na Veronica Kazimoto
Bidhaa zinazostahili kutozwa ushuru wa bidhaa kama vile sigara, mvinyo, pombe kali pamoja na bia zitaanza kutumia rasmi stempu za kielektroniki Januari, 2019 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga na Mbeya ambapo mfumo wa stempu hizo umeshafungwa kwenye mitambo ya uzalishaji.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua ufungaji wa mfumo huo katika Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na Kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema kuwa mfumo huo mpya unaondoa mfumo wa zamani wa stempu za karatasi.

“Nimekuja kufanya ziara katika viwanda hivi ili kujiridhisha kama kweli mfumo huu wa stepu za kielektroniki umefungwa na nimejionea mwenyewe mfumo tayari umefungwa katika viwanda vyote nilivyotembelea. Hivyo, tunaachana na mfumo wa zamani wa stempu za karatasi na kwa sasa tunaendelea kufunga mfumo huu mpya wa stempu za kielektroniki kwenye mikoa mingine ambayo haitaanza katika awamu hii”, alisema Kichere.

Kichere alisema kuwa lengo la kuweka stempu za kielektroniki kwenye bidhaa hizo ni kupata idadi halisi ya uzalishaji wa bidhaa ili kutoza kodi stahiki na kuondoa dhana ya kusema kwamba TRA inawaonea wafanyabiashara wanaozalisha bidhaa hizo kwa kutoza kodi isiyoendana na uzalishaji.

“Lengo la kuweka stempu hizi za kielektroniki ni kupata kiasi halisi cha uzalishaji wa bidhaa hizi ili kila upande uridhike yaani mzalishaji alipe kodi sahihi na sisi TRA tutoze kodi stahiki bila kupingana wala kugombana na wateja wetu”, alisema Kichere.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania Rupa Suchak amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha serikali kufunga mfumo huo wa stempu za kielektroniki kwa sababu serikali itaongeza mapato na wafanyabiashara wataongeza uhiari wa kulipa kodi.

“Ninaishukuru sana serikali yetu kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuleta mfumo huu mpya ambao utaongeza mapato na kupanua wigo wa kodi lakini pia kwetu sisi wafanyabiashara tutaongeza uhiari wa kulipa kodi”, alisema Rupa.

Uwekwaji wa stempu za kielektroniki katika bidhaa nyingine kama vile juisi, maji ya chupa, bidhaa za muziki na filamu (CD\DVD\Tape) zitafuata kwa tarehe ambayo itatangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania hapo badae.

Mwisho.

CHADEMA Yapigwa 'Marufuku' Jimboni Kwa Mbowe

0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezuiwa kufanya mkutano pamoja na ziara ya viongozi wa chama hicho kitaifa, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Hayo yamebainishwa kupitia barua iliyotumwa kwa Katibu wa CHADEMA wilayani Hai, ambayo imesainiwa na Katibu tawala wa wilaya hiyo, Said Omary iliyoelekeza kusitisha kibali cha kufanya mkutano wilayani humo.

"Nimeagizwa na Mkuu wa Wilaya ambae ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ya Hai. Nikuandikie kukutaka kusitisha mkutano na ziara ya viongozi wako kitaifa, tarehe 29/12/2018 na kuendelea", imesema barua hiyo.

Baada ya zuio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya jana  aliamuru kukamatwa kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji pamoja na viongozi wengine kwa makosa ya kufanya kusanyiko bila kibali.

Wema Sepetu Apewa Masharti Na Familia

0
0
Baada ya kuanzisha biashara yake ya duka la nguo za watoto liitwalo 'Little Sweetheart', staa wa kike wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amepewa masharti na familia yake namna ya kuliendesha duka hilo, pamoja na kuachana na baadhi ya marafiki wasiokuwa na faida kwake.
 
Miongoni mwa masharti aliyowekewa Wema na familia yake ni kuwa chini ya dada yake aitwaye Nuru Sepetu. Nuru ndiye meneja wa Wema kwa sasa hivyo ili kumfikia staa huyo lazima upite kwake.

“Nuru ndiye anayesimamia kila kitu dukani hapo kuliko kumwachia Wema mwenyewe ambaye wanamjua ana mambo mengi hivyo usimamizi unaweza kumshinda na hata huyo Wema mwenyewe lazima afuate maelekezo ya Nuru", kimesema chanzo hicho na kuongeza;

“Wema anatakiwa kujilinda na skendo kwani kadiri atakavyokuwa akichafuka ndivyo atakavyokuwa akiharibu taswira ya biashara kwa maana ya jina la duka na ameambiwa kama akileta mambo yake ya skendo za kila kukicha, basi atapoteza hata wateja hivyo lazima ajilinde na alinde jina lake kubwa ambalo amekuwa akishindwa kulitumia kwa muda mrefu kumwingizia pesa".

Mbali na hayo, Wema pia amepigwa marufuku kufanya mahojiano ya mara kwa mara na vyombo vya habari ambavyo vingine vimelenga kumharibia badala ya kumjenga. 

“Sasa hivi hatakiwi kabisa kuzungumza na waandishi wa habari, badala yake anayetakiwa kuzungumza kwa niaba yake ni Nuru ambaye ndiye msemaji wake".

Duka hilo la Wema lililopo Kinondoni jijini Dar es salaam, ni la pili baada ya lile la kwanza lililomshinda, ambalo lilikuwa likiuza lipstick zake za 'Kiss by Wema' lililokuwa maeneo ya Mwenge, jijini humo.

Serikali Kuendelea Kuyafutia Usajili Maduka ya Kubadilishia Fedha Yasiyokidhi Vigezo

0
0
Serikali imesema ni maduka 109 nchini ya kubadilisha fedha ndiyo yaliyokidhi vigezo vya sheria mpya kwa biashara hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango, DK Philip Mpango ametoa kauli hiyo leo Jumapili Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya hali ya uchumi wa taifa na utekelezaji wa bajeti ya Serikali katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/19.

DK Mpango amesema kabla ya kufanya usajili mpya, kulikuwa na jumla ya maduka ya kubadilisha fedha 297 nchi nzima.

Amesema jumla ya maduka 188 yalishindwa kutimiza masharti na hivyo kupelekea kufutiwa usajili wao huku akiahidi kuendeleza msako zaidi kwenye maduka yote nchini.

"Serikali kupitia (Benki Kuu ya Tanzania) BOT imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha biashara ya kubadilisha fedha za kigeni ili kuondoa uwezekano wa maduka makubwa haya kufanya biashara isiyo halali ambayo ni pamoja na utakatishaji wa fedha haramu," amesema Mpango

Ametaja baadhi masharti yaliyowaondolea leseni ni kuwekwa kwa sharti la kiwango cha chini kwa maduka yaliyo katika daraja A kuwa ni mtaji wake uwe Sh100 milioni hadi Sh300 milioni wakati daraja B iwe Sh250 milioni hadi Sh1 bilioni.

Serikali Yatoa Ufafanuzi Sakata la Mwananchi Aliyekamatwa Akisafirisha Vitanda Viwil

0
0
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii na wadau mbalimbali zinazohusisha namna Afisa Misitu wa Wilaya ya Korogwe alivyokuwa akitekeleza majukumu ya kusimamia Sheria ya Misitu Na. 14 ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni zake za Mwaka 2004. Afisa huyo alikuwa akitekeleza majukumu hayo kwa mujibu wa kifungu cha 93 (Powers of officers with respect to offences) inayompa mamlaka Afisa Misitu au Afisa wa Jeshi la Polisi kukagua, kukamata na kuzuia mazao yanayodhaniwa kupatikana kinyume na sheria.

Kufuatia taarifa hizo, uongozi wa TFS umefanya uchunguzi wa haraka na kubaini kuwa abiria mmoja alikuwa akisafirisha vitanda viwili (2) vipya kwa basi. Vitanda hivyo vililipiwa ushuru wa Serikali kupitia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) na kupewa stakabadhi halali ya tarehe 26 Disemba, 2018 katika kituo cha Mkata, Handeni Mkoani Tanga.

Katika kutekeleza majukumu yake, Afisa wetu alimtaka abiria huyo kuonesha Hati ya Kusafirishia (Transit Pass) bidhaa hizo kwa mujibu wa Kanuni ya 13(4) ambayo inakataza mwenye chombo chochote cha usafiri kusafirisha mazao ya misitu ambayo hayana hati ya usafirishaji ambapo abiria huyo hakuwa nayo. Hata hivyo, Afisa wetu alishindwa kutafsiri masharti ya kifungu hiki na mahitaji ya utoaji wa Hati ya Usafirishaji kwani kama msafirishaji binafsi kwa matumizi ya nyumbani asingeweza kukidhi vigezo vya kuwa na hati hiyo. Hati ya Usafirishaji huhitaji msafirishaji kuonesha usajili, leseni ya biashara, utambulisho wa mlipa kodi na namba ya usajili wa chombo kinachotumika kusafirisha mazao hayo pamoja na kuonesha vituo atakavyopaswa kukaguliwa.

Kufutia tukio hilo, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unamwomba radhi abiria huyo na umma wa watanzania kwa tukio hilo na usumbufu uliojitokeza. Wakala unaendelea kufuatilia suala hili, na utahakikisha kuwa tukio kama hili halijirudii tena. Aidha, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za utumishi wa umma dhidi ya mtumishi aliyehusika na utoaji wa lugha isiyo na staha wakati akitekeleza sheria ya misitu ambapo alitegemewa kutoa elimu stahiki kwa umma. Hivyo, TFS inapenda kufafanua mambo yafuatayo:- 2

1. Kwamba ikiwa mwananchi yeyote amenunua samani mpya kutoka kwa watengenezaji au wauzaji mahali popote kuhakikisha anapatiwa risiti halali kwa malipo aliyofanya. Hivyo, mmiliki wa samani mpya kwa matumizi binafsi halazimiki kuwa na Hati ya Usafirishaji anaposafirisha toka eneo moja kwenda jingine isipokuwa awe tayari kuonesha uthibitisho wa nyaraka za malipo halali ya samani hizo kwa ukaguzi pale itakapohitajika.

2. Mwananchi yeyote anayesafirisha samani zilizotumika kutoka eneo moja hadi jingine halazimiki kuwa hati za malipo wala kuwa na hati ya kusafirishia samani hizo.

3. Serikali itaendelea kufanya mapitio ya Sheria ya Misitu na Kanuni zake ili kuepuka mkanganyiko wowote wa tafsiri ya sheria unaoweza kujitokeza na kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unapenda kutoa rai kwa wananchi wote kuendelea kuzingatia Sheria za uhifadhi wa misitu. Aidha, Wakala hauna nia ya kuzuia utengenezaji, usafirishaji na matumizi ya samani za mbao mahali popote nchini ilimradi tu upatikanaji wa malighafi zake uwe umefuata utaratibu. Lengo ni kuhakikisha kuwa rasilimali za misitu zinatunzwa na kutumika kwa njia endelevu kwa maendeleo ya Taifa. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania utaendelea kutoa elimu kwa umma pamoja na watumishi wake kuhusu taratibu za uvunaji, usafirishaji na biashara ya mazao ya misitu nchini kupitia njia mbalimbali na kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.

IMETOLEWA NA
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO KWA UMMA
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS)

Katibu Mkuu CCM Atoa ONYO Kwa Wagombea Wanaotoa Rushwa

0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema atakayejihusisha na vitendo vya rushwa katika mchakato wa chama hicho tawala kusaka wagombea wake katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, atapoteza sifa za kugombea.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Desemba 30, 2018 alipokutana na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya za Muleba na Biharamulo mkoani Kagera.

Amesema kila kiongozi wa CCM atakayejitokeza kugombea uenyekiti wa kijiji au mtaa, lazima awe mwadilifu na mwaminifu.

Amebainisha kuwa baadhi ya wagombea wanatumia majukwaa kupinga rushwa licha ya kuwa wanajihusisha nayo, ikiwa ni pamoja na kukiuka maadili ndani ya chama.

"Makatibu wa CCM kila ngazi hata nyie msiwe wa kupokea rushwa kupitisha majina ya wagombea wasiokuwa na sifa lazima kiongozi afuate miiko na ahadi za mwanachama,” amesema Bashiru.

Alitumia nafasi hiyo kuzungumzia migogoro ya ardhi, kuziagiza halmashauri za wilaya hizo na nyingine nchini Tanzania kutatua migogoro ya ardhi kati ya wananchi na taasisi mbalimbali.

Mwenyekiti wa CCM mkoani Kagera Costansia Buhiye ameahidi kusimamia kanuni na sheria za chama hicho tawala kuhakikisha viongozi watakaojitokeza kuwania nafasi wanakuwa waadilifu na waaminifu.

Waziri Mkuu: Shilingi Bil. 222 Zimelipwa Kwa Wakulima Wa Korosho

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema jumla ya shilingi bilioni 222 zimelipwa na Serikali kwa wakulima wa zao la korosho na kuwataka wakulima wawe na subira.

Amesema wakulima walioanza kulipwa ni wale wenye kilo zisizozidi kilo 1,500 na wale wenye kilo zaidi ya 1,500 na kuendelea Serikali inaendelea na uhakiki kisha watalipwa.

”Fedha zipo, hakuna mkulima ambaye atapoteza haki yake wote watalipwa. Tunaendelea na uhakiki kwa wale wenye korosho nyingi ili kubaini kama hawajanunua kangomba.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Desemba 30, 2018) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Nandagala ‘A’ baada ya kufungua ofisi ya CCM kata ya Nandagala.

Amesema baadhi ya watu wamekutwa na kilo zaidi ya 1,500 na wameshindwa kuonesha mashamba yao ya mikorosho, hali inayodhihirisha kwamba amenunua kupitia kangomba.

Waziri Mkuu amesema baadhi ya waliokutwa na korosho nyingi ni vijana wadogo ambao hawana hata uwezo kifedha hivyo Serikali itahakikisha inawakamata watu wanaowatuma.

Amesema lengo la Serikali inayoongizwa na Rais Dkt. John Magufuli ni kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao, hivyo biashara ya kangomba lazima lidhibitiwe.

Waziri Mkuu ambaye leo ameanza ziara yake kwa kikazi wilayani Ruangwa, Mkoani Lindi amesema zoezi la ulipaji kwa wakulima wa korosho linaendelea, wakulima wawe na subira.

Serikali iliamua kununua korosho zote za mwaka huu baada ya kubaini wafanyabiashara wamepanga kuwadhulumu wakulima kwa kupanga kununua kwa bei ndogo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametembelea eneo la ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Matambalale wilayani Ruangwa ambapo amewataka wahakikishe ujenzi unakamilika.

Amewataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na kuhakikisha wanachangia nguvu kazi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ili mwakani wanafunzi waanze kusoma.

”Tunataka tuondoe dhiki ya watoto wetu kutembea umbali mrefu hadi Namichiga kutafuta elimu, tunataka watoto wetu wote wasome katika maeneo yaliyo karibu na makazi yao.”

Amesema wanafunzi zaidi ya 200 wamefaulu na hawana pa kwenda hivyo ni lazima ujenzi wa shule zote za sekondari za Matambalale, Chibura na Ruchelegwa ukamilike.

Waziri Mkuu amesema hadi Januari 10, 2019 shule hizo zote lazima ujenzi wake ukamilike ili wanafunzi waanze kusoma, hivyo viongozi washirikiane na wananchi kukamilisha ujenzi.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri wa Fedha atoa sababu za wahisani kutokutoa fedha walizoahidi

0
0
Hadi kufikia Novemba 2018 washirika wa maendeleo walikuwa wamechangia Sh498.5 bilioni ambayo ni asilimia 54 ya kiasi walichotakiwa kuwa wamechangia katika kipindi hicho.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema katika kipindi cha Julai hadi Novemba 2018, wadau hao walipaswa kuwa wamechangia Sh928.7 bilioni kutokana na ahadi yao kwa Serikali kwamba mwaka wa fedha 2018/19 wangechangia Sh2.67 trilioni.

Akizungumza leo Jumapili Desemba 30, 2018 jijini Dodoma, Waziri Mpango ametaja baadhi ya sababu za kutochangia ni kutokana na masharti na vigezo vinavyowekwa na wadau hao ikiwemo kasi ndogo ya utekelezaji wa miradi.

Waziri amesema Serikali imeliona jambo hilo na imejipanga katika kukabiliana na hali hiyo ikiwemo kubana matumizi na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato.

Wakati huo huo Waziri Mpango amesema deni la Serikali la Sh49.37 trilioni bado ni himilivu hivyo Watanzania hawapaswi kuwa na hofu kwani halizuii Serikali kukopa.

Mtoto afichwa kabatini kwa miezi mitano Dodoma

0
0
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi mitano, jijini Dodoma amefungiwa kabatini na mwajiri wa mama mzazi wa mtoto huyo ambaye alikuwa akifanya kazi za ndani.

Akithibitisha kupokelewa kwa mtoto huyo katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Ibenzi amesema kuwa mtoto amefikishwa hospitali siku tatu zilizopita na kwamba atatibiwa kwanza tatizo la ukosefu wa lishe (utapiamlo).

Dkt. Ibenzi amesema kuwa mama wa mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa hajitambui kwa kile kilichodaiwa kupigwa na mwajiri wake hadi kupoteza fahamu.

"Mtoto anaendelea na matibabu kwakuwa bado tunamfanyia uchunguzi zaidi ikiwemo kufuatilia kama alipatiwa chanjo zote stahiki, na sisi tunatibu wagonjwa tu, mambo mengine watayafuatilia wahusika", amesema Dkt. Ibenzi.

Taarifa za awali zinadai kuwa binti huyo alipata ujauzito akiwa nyumbani kwa mwajiri wake anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi jijini humo ambaye alimtaka kufanya siri ili majirani wasifahamu kama yeye ni mjamzito.

Baadaye alifanikiwa kujifungua na kuendelea kufanya siri na mtoto kuhifadhiwa kabatini, hadi hapo juzi ambapo inadaiwa alimpiga binti huyo hadi kupoteza fahamu ndipo majirani walipofika eneo la tukio na kugundua kulikuwa na mtoto mchanga ndani ya kabati.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya January 31

Tanzania Miongoni mwa Nchi Tano Zinazoongoza Katika Ukuaji wa Uchumi Barani Afrika

0
0


1.   Pato la Taifa (kwa bei za 2007)
·         Uchumi wa Taifa umeendelea kuwa imara, ukikua kwa 7.1% (2017) ikilinganishwa  na wastani wa ukuaji wa 7.0% kwa miaka miwili iliyopita (2015-2016).

·         Kwa nchi za EAC, uchumi wa Tanzania ulikua kwa kasi zaidi (7.1%) mwaka 2017 ukilinganisha na Rwanda (6.1%), Uganda (5.1%), Kenya (4.9%), na Burundi (0.0%). Vilevile, Tanzania iliongoza katika ukuaji wa uchumi kwenye nchi za SADC.

·         Katika kipindi cha Januari hadi Juni 2018, Pato la Taifa lilikua kwa 7.0% ikilinganishwa na 6.3% katika kipindi kama hicho mwaka 2017. Sekta zilizokua kwa kasi zaidi ni: ujenzi (15.7%), Uzalishaji viwandani (12.0%), habari na mawasiliano (11.2), na uchukuzi & uhifadhi mizigo (8.2%).

·         Aidha, Tanzania imeendelea kuwa miongoni mwa nchi 5 bora kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika bara la Afrika katika nusu ya kwanza ya 2018, ikijumuisha: Ethiopia (8.5%), Ivory Coast (7.4%), Rwanda (7.2), Tanzania (7.0%), na Senegal (7.0%).

·         Sekta zilizoendelea kutoa mchango mkubwa katika Pato la Taifa (Januari - Juni 2018) ni Kilimo (34.5%), Ujenzi (16.8%) na Biashara (10.1%). Aidha, sekta ya kilimo ilikua kwa 3.6% kwa kipindi hicho. Napenda kwa niaba ya Serikali kuwapongeza wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mchango wao mkubwa katika uchumi wa Taifa.

2.   Mfumuko wa Bei
·         Mfumuko wa bei umeendelea kupungua kutoka wastani wa 4.3% mwaka 2017/18 hadi kufikia kiwango cha chini kabisa kuwahi kutokea katika miaka ya karibuni cha 3.0% mwezi Novemba 2018. Lengo la kipindi cha muda wa kati ni 5%.

·         Kati ya Julai hadi Novemba 2018, Tanzania ilikuwa na kiwango kidogo zaidi cha mfumuko wa bei ikilinganishwa na Uganda (3.3%) na Kenya (4.8%).

·         Sababu zilizochangia mfumuko wa bei kuwa chini ni pamoja na:
ü  Upatikanaji mzuri wa chakula katika masoko ya ndani na nchi jirani, ambapo uzalishaji wa chakula nchini ulifikia tani 15.9m ikilinganishwa na mahitaji ya tani 13.3m kwa kipindi hicho, hivyo kuwa na utoshelevu wa chakula kwa 120%. Mfumuko wa bei ya chakula ulifikia 2.0% Novemba 2018 ikilinganishwa na 7.9% katika kipindi kama hicho mwaka 2017;
ü  Kutengamaa kwa bei za mafuta katika soko la dunia; na
ü  Utekelezaji madhubuti wa sera za fedha na za bajeti.


3.   Hali ya maisha ya mwananchi
·         Kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi imepelekea kuimarika kwa hali ya maisha ya wananchi hasa wale waliopata fursa za ajira (na kipato) katika shughuli za kiuchumi zinazokua haraka, kama vile ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara, reli, upanuzi wa bandari na viwanja vya ndege, mauzo ya mazao ya kilimo, ujenzi wa viwanda na utoaji wa huduma za fedha na mawasiliano. Kuongezeka kwa ujenzi wa nyumba bora za kuishi, umiliki wa mali zisizohamishika na vyombo vya usafiri, na vifaa vya kudumu vya majumbani (consumer durables) vinaashiria kuimarika kwa hali ya maisha ya wananchi.

·         Aidha, ukuaji mzuri wa uchumi umeiwezesha Serikali kuongeza ukusanyaji wa mapato na kugharamia uboreshaji wa huduma za jamii hususan elimu (ikwemo elimu-msingi bila ada), afya (hospitali, vituo vya afya, zahanati, madawa, vifaa-tiba, vitendanishi), maji na kuimarisha uzalishaji wa umeme na kuusambaza vijijini.

·         Kutokana na kiwango kidogo cha mfumuko wa bei, uwezo wa shilingi kununua vitu ni mkubwa (Nguvu ya buku 10 acha kabisa!). Aidha, gharama za maisha kwa mwananchi kwa ujumla, zimeongezeka kwa kasi ndogo.

4.   Thamani ya Shilingi
·         Thamani ya shilingi ya Tanzania imeendelea kuwa tulivu. Katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2018, dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa shilingi 2,276, ikilinganishwa na shilingi 2,235 katika kipindi cha Julai hadi Novemba 2017. Hivyo, shilingi ilipungua thamani dhidi ya dola (depreciation) kwa asilimia 1.8,  kiwango ambacho ni kidogo na hakikuathiri utulivu wa thamani ya shilingi ya Tanzania ikizingatiwa kuwa mfumuko wa bei wa wastani katika nchi washirika wakuu wa biashara na Tanzania ni asilimia 3.0. 

·         Utulivu wa thamani ya shilingi umetokana na utekelezaji wa sera ya fedha, usimamizi thabiti wa mapato na matumizi ya Serikali, kutumia gesi asilia katika kuzalisha umeme, na baadhi ya viwanda kuzalisha bidhaa ambazo awali zilikuwa zikiagizwa kwa wingi kutoka nje, mfano, vigae.

5.   Utekelezaji wa Sera ya Fedha
·         Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2018/19, Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania ilichukua hatua mbalimbali kuongeza ukwasi kwenye uchumi ili kuziwezesha benki za biashara kuongeza utoaji wa mikopo kwa sekta binafsi. Miongoni mwa hatua hizo ni:
ü  Kutoa mikopo ya muda mfupi kwa mabenki;
ü  Kushusha riba ya mikopo kwa mabenki kutoka 9.0% hadi 7.0% Agosti 2018; na
ü  Kununua fedha za kigeni kutoka katika benki za biashara & taasisi za Serikali;
·         Kutokana na hatua hizo, ukwasi kwenye mabenki ya biashara uliongezeka na riba katika masoko ya fedha zilipungua.
ü  Riba ya siku moja katika soko la fedha baina ya mabenki ilishuka kutoka 3.72% Oktoba 2017 hadi wastani wa 2.29% Oktoba 2018.
ü  Riba za dhamana za Serikali zilipungua kutoka 9.41% hadi kufikia wastani wa 7.40% Oktoba 2017.
ü  Riba za mikopo inayotolewa na mabenki ilipungua kwa kiasi kidogo kutoka wastani wa 18.1% kati ya Julai na Oktoba 2017 hadi 17.3% katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

·         Ukuaji wa ujazi wa fedha (M3) uliimarika na kuwa wastani wa 6.1% (Julai - Oktoba 2018) ukilinganisha na 5.0% katika kipindi kama hicho 2017. Ukuaji huu uliendana na mahitaji ya uchumi.

·         Ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi uliongezeka kwa wastani wa 4.6% (Julai hadi Oktoba 2018) ukilinganisha na wastani wa 0.2% kwa kipindi kama hicho mwaka 2017.

6.   Akiba ya Fedha za Kigeni
·         Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kutosheleza mahitaji ya kuiwezesha Tanzania kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje na pia kujenga imani ya wawekezaji.

·         Akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani milioni 5,079.0 mwezi Novemba 2018, kiasi ambacho kinatosha kugharamia uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha takriban miezi 5.

·         Kiwango hiki cha akiba ya fedha za kigeni ni zaidi ya lengo la Serikali kuwa na akiba ya fedha za kigeni inayokidhi uagizaji wa bidhaa na huduma kwa miezi 4. Pia ni zaidi ya lengo la miezi 4.5 lililowekwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

7.   Mwenendo wa Sekta ya Kibenki.
·         Sekta ya kibenki imeendelea kuwa imara, salama na yenye kutengeneza faida, ikiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha zaidi ya kiwango kinachotakiwa kisheria.

·         Uwiano wa mitaji ya mabenki ikilinganishwa na rasilimali zao ulikuwa 16.3%, ikiwa juu ya kiwango kinachohitajika kisheria cha 10.0%.

·         Kiwango cha mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu ikilinganishwa na kiwango cha amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi kilifikia 36% ikilinganishwa na kiwango cha chini kinachohitajika kisheria cha 20%.

Hii inaashiria kuwa mabenki yana ukwasi wa kutosha kwa ajili ya shughuli zake za kila siku ikiwemo kulipa madeni pamoja na kutoa mikopo.

·         Katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2018, sekta ya kibenki ilipata faida ya shilingi bilioni 285.4 (ikilinganishwa na shilingi bilioni 317.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2017). Kupungua kwa faida kulitokana na kuongezeka kwa tengo la hasara kufuatia kuanza kutumika kwa Kanuni za Kimataifa za Utoaji Taarifa za Fedha (International Financial Reporting Standard 9 - IFRS9) mwezi Januari 2018.

·         Mikopo chechefu iliendelea kushuka hadi kufikia 9.7% ya mikopo yote Septemba 2018 kutoka 12.5% iliyorekodiwa mwishoni mwa Disemba 2017.

·         Kuendelea kupungua kwa mikopo chechefu kulitokana na hatua zilizochukuliwa na BoT   ikiwa pamoja na:
ü  Kuzitaka benki zote kutekeleza mikakati ya kuboresha utoaji na usimamizi wa mikopo, ikiwemo uchambuzi wa maombi ya mikopo, na kutumia kwa lazima taarifa ya historia za wakopaji kabla ya kutoa mkopo; na
ü  Benki zote kutakiwa kuazisha idara maalum kwa ajili ya kufuatilia ukusanyaji wa madeni chechefu.

·         Sekta ya kibenki pia imeendelea kukua. Hadi Septemba 2018, kulikuwa na jumla ya Benki na Taasisi za fedha zinazosimamiwa na BOT zipatazo 61. Kati ya hizo, mabenki yalikuwa 52 yenye matawi 884 nchini kote na zingine zilikuwa taasisi zinazotoa huduma za kifedha.

8.   Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni
·         Serikali kupitia BoT imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ili kuondoa uwezekano wa maduka haya kufanya biashara isiyo halali ambayo ni pamoja na utakatishaji wa fedha haramu.

·         Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na BoT kufanya msako wa kukagua maduka haya Arusha na kubaini baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanafanywa na maduka haya kinyume na leseni zao. Zoezi hili litakuwa endelevu ili kuhakikisha kwamba mwenendo wa maduka haya unaridhisha.

·         Mwezi Juni 2017, BOT ilifanya mabadiliko ya Kanuni za Biashara ya Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni ya mwaka 2015 kwa lengo la kuboresha usimamizi na kudhibiti matumizi mabaya ya maduka haya. Hivyo, kiwango cha chini cha mtaji wa maduka yaliyoko katika Daraja A kiliongezwa kutoka Tshs. 100mn hadi Tshs. 300mn na Daraja B kutoka Tshs. 250m hadi Tshs. 1bn.

·         Kabla ya zoezi la usajili upya wa maduka hayo, kulikuwa na maduka 297 nchi nzima. Baada ya zoezi la usajili, maduka 109 tu ndio yalikidhi vigezo husika na kupewa leseni mpya. Jumla ya maduka 188 yalishindwa kutimiza masharti na hivyo kupelekea kufutiwa leseni.

9.   Mwenendo wa Sekta ya Biashara Nje (Julai - Nov 2018)
·         Thamani ya mauzo nje (traditional & non traditional exports) ilifikia USD 1,939.2mn (Julai - November 2018) ikilinganishwa na USD 2,194.4mn katika kipindi kama hicho mwaka 2017.

·         Thamani ya bidhaa zilizonunuliwa kutoka nje (Capital, intermediate & consumer goods f.o.b.) iliongezeka kutoka USD 3,310.1mn (Julai - Novemba 2017) hadi USD 3,483.4mn (Julai - Novemba 2018).

·         Nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho mali nchi za nje (current account deficit) iliongezeka na kufikia USD 701.0mn ikilinganishwa na nakisi ya USD 580.4mn katika kipindi kama hicho mwaka 2017/18.

·         Kuongezeka kwa nakisi kulitokana na:
ü  Kuongezeka kwa thamani ya bidhaa za mitaji zilizoagizwa kutoka nje ya nchi (kutoka USD 1,097mn hadi USD 1,408.8mn) kwa ajili ya miradi mikubwa ya maendeleo, hasa ile ya ujenzi wa reli ya kisasa na barabara.
ü  Kupungua kwa mapato yatokanayo na bidhaa zilizouzwa nje ya nchi kulikochangiwa na sababu mbalimbali, hasa ile ya kushuka kwa bei za mazao mengi katika soko la dunia.

10.        Mwenendo wa Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali
(a)        Mapatoya Serikali
·         Katika kipindi cha miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2018/19 (Julai - Novemba), makusanyo ya ndani (ikijumuisha mapato ya Halmashauri) yalifikia Ths. 7.37tn sawa na 88.9% ya makadirio ya Tshs. 8.30tn katika kipindi hicho.
·         Mapato ya kodi yalifikia Tshs. 6.23tn ikiwa ni 88% ya lengo la kukusanya Tshs.7.04tn kwa kipindi hicho.
·         Mapato yasiyo ya kodi yalifikia Ths. 936.03bn sawa na 21% zaidi ya lengo la Tshs.775.36bn
·         Mapato ya Halmashauri yalifikia Tshs. 203.8bn sawa na 61% ya lengo.

·         Ongezeko la mapato yasiyo ya kodi limetokana na kuimarishwa kwa ufuatiliaji kwenye Taasisi, Mashirika na Kampuni kulikoiwezesha Serikali kupata michango na gawio stahiki kutoka kwenye uwekezaji wake; Kuimarika kwa matumizi ya Technolojia katika ukusanyaji wa maduhuli kwenye Wizara na Idara zinazojitegemea kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato uitwao Government Electronic Payment Gateway (GePG) ambapo kati ya Julai 2017 hadi Novemba 2018, jumla ya Taasisi za Serikali 325 zinatumia mfumo huu kukusanya maduhuli.

·         Jitihada za kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara: Serikali kupitia Sheria ya Fedha 2018/19 Serikali ilipunguza ada na tozo mbalimbali ambazo zilikuwa kero kwa wananchi. Miongoni mwa ada na tozo zilizopunguzwa ni pamoja na tozo za mazingira, OSHA, FIRE, TBS, TFDA na tozo kwenye madini ya chumvi.

·         Changamoto za ukusanyaji wa mapato ni pamoja na ukwepaji wa kodi; mwamko mdogo wa wananchi kudai risiti pale wanapofanya manunuzi na wafanyabiashara kutoa risiti pale wanapofanya mauzo; na wigo mdogo wa kodi.

(b)        Misaada na Mikopo Nafuu
·         Washirika wa Maendeleo wameendelea kusaidia bajeti ya Serikali kupitia miradi na programu mbalimbali. 2017/18, Washirika wa Maendeleo waliahidi kuchangia Bajeti ya Serikali kiasi cha Tshs. 3.97tn. Hadi kufikia Juni 2018, Washirika wa maendeleo walitoa Tshs. 2.46tn ambazo ni sawa na asilimia 62 ya ahadi.

·         Katika mwaka 2018/19, Washirika wa Maendeleo wameahidi kuchangia bajeti ya Serikali kiasi cha Tshs. 2.67tn. Hadi kufikia Novemba, 2018, kiasi cha Tshs. 498.5bn kimepokelewa, sawa na asilimia 54 ya kiasi cha Tshs 928.7bn kilichotarajiwa katika kipindi cha Julai hadi Novemba 2018.

·         Kasi ndogo ya utoaji fedha inatokana na:
ü  Masharti magumu ya wafadhili na majadiliano kuchukua muda mrefu.
ü  Kasi ndogo ya utekelezaji wa baadhi ya miradi katika sekta na hivyo kusababisha fedha za awamu zinazofuata kuchelewa kutolewa;

(c)          Matumizi ya Serikali
·         Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa mwaka 2018/19 ni Tshs. 32.47tn ikijumuisha Tshs. 20.46tn za matumizi ya kawaida na Tshs. 12.00tn matumizi ya maendeleo.

·         Kati ya Julai hadi Novemba, 2018, Serikali imetumia jumla ya Tshs.10.41tn, sawa na asilimia 79 ya lengo la Tshs. 13.22tn kwa kipindi hicho.

·         Kati ya kiasi hicho, Tshs. 8.29tn ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida (bila kujumuisha makusanyo ya Halmashauri) sawa na 99% ya lengo la Tshs. 8.36tn.
ü  Tshs. 2.86tn zilikuwa za mishahara, sawa na asilimia 93 ya lengo la Tshs. 3.08tn; na fedha za matumizi mengineyo (OC) zilikuwa Tshs. 5.42tn sawa na 103% ya lengo la Tshs. 5.27tn.
·         Fedha za maendeleo zilikuwa Tshs. 2.12tn

·         Katika Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kipaumbele kilitolewa katika maeneo yafuatayo:
ü  Utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya barabara, reli na viwanja vya ndege (Tshs. 638.23bn);
ü  Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu, uimarishaji wa vyuo vya VETA na kukuza ujuzi kwa vijana Tshs. 226.76bn);
ü  Utekelezaji wa miradi ya maji na umeme vijijini (Tshs. 185.68bn);
ü  Miradi ya afya, ununuzi wa dawa, chanjo, viatilifu na vitendanishi na ujenzi/ukarabati wa hospitali (Tshs. 179.86bn);
ü  Kukamilisha malipo ya ndege mpya mbili aina ya Airbus A220 – 300 ambapo moja imewasili nchini tarehe 24 Disemba (Tshs. 152.1bn); na
ü  Kugharamia Elimu-msingi bila malipo (Tshs. 104.03bn).

·         Serikali iliendelea kulipa madai mbalimbali jumla ya Tshs 331.79bn kama ifuatavyo:
ü  Wazabuni Tshs. 132.72bn; Wakandarasi Tshs. 175.37bn; na Watumishi Tshs. 23.7bn.

11.        Deni la Serikali
·         Kufikia Sept. 2018 deni la Serikali lilifikia Tshs. 49.37tn (sawa na ongezeko la 3.2%) ikilinganishwa na Tshs. 47.82tn Sept.  2017
ü  Deni la ndani lilikuwa Tshs. 13.64tn (27.6%)
ü  Deni la nje Tshs. 35.72tn (72.4%)

·         Mikopo hii imetumika kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo:
ü  Ujenzi wa bomba la gesi Mtwara – Dar es Salaam;
ü  Ujenzi na ukarabati wa miondombinu ya barabara, madaraja, reli na bandari;
ü  Ujenzi wa mitambo ya kufua umeme (Ubungo, Mwanza na Kinyerezi II);
ü  Miradi ya maji, (ikijumuisha mradi wa Maji ziwa Victoria);
ü  Miradi ya TASAF;
ü  Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; na
ü  Mradi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

·         Nchi kuwa na deni sio dhambi, jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa fedha tulizokopa zinatumika kujenga rasilimali ambazo ni msingi wa kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha mali na kulipa mikopo hiyo.

12.        Uhimilivu wa Deni
·         Kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo Dhamana na Misaada Sura 134, Serikali inawajibu wa kufanya tathmini ya uhimilivu wa deni (DSA) kila mwaka ili kupima mwenendo wa deni  na uhimilivu wake.
·         Matokeo ya awali ya tathmini iliyofanywa Desemba 2018 inaonesha kuwa deni ni himilivu kwa muda mfupi, wa kati na mrefu. Matokeo haya yanafanana na tathmini iliyofanywa na IMF. Deni la umma limeendelea kuwa himilivu.

·         Katika tathmini hiyo, viashiria vinaonesha uwiano ufuatao kwa thamani ya sasa (Present Value Terms):
ü  Deni la Serikali kwa GDP 27.2% ikilinganishwa na ukomo wa 70%; 
ü  Uwiano wa deni la nje kwa GDP (22.2%) ikilinganishwa na ukomo wa 55%;
ü  Deni la nje kwa mauzo nje 157.3% ikilinganishwaa na ukomo wa 240%;
ü  Ulipaji wa deni la nje kwa kutumia mauzo ya bidhaa nje 15.2% ikilinganishwa na ukomo wa 23%; na
ü  Ulipaji wa deni kwa mapato ya ndani 49.6%.

·         Viashiria vyote vinaonesha kuwa Serikali ina uwezo wa kuendelea kukopa na kulipa pale mikopo inapoiva.

·         Serikali itaendelea kusimamia deni na kuhakikisha kuwa linaendelea kuwa himilivu:
ü  Mikopo itaelekezwa kugharamia miradi ya maendeleo yenye tija kwa Taifa na ambayo inachochea ukuaji wa uchumi;
ü  Kuweka kipaumbele kukopa mikopo yenye masharti nafuu na kuhakikisha mikopo ya masharti ya kibiashara inakopwa kwa uangalifu mkubwa na kwamba inatumika kwenye maeneo ambayo yanachochea ukuaji wa uchumi;
ü  Kuboresha ukusanyaji wa mapato (ya kodi na yasiyo ya kodi), hususan kwa kuziba mianya ya uvujaji wa mapato na kupanua wigo ili kuhakikisha sehemu kubwa ya bajeti inagharamiwa na mapato ya ndani pamoja na kupunguza matumizi yanayoweza kuepukika; na
ü  Kusimamisha utoaji wa Dhamana za Serikali kwa Taasisi za Serikali ambazo zinategemea ruzuku kujiendesha.

13.        Matarajio Hadi Juni 2019
Uchumi unatarajiwa kuendelea kukua kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kwenye miundombinu wezeshi ya uzalishaji mali kama vile barabara, madaraja, bomba la mafuta, ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa na viwanja vya ndege; Ujenzi wa kituo cha kufua umeme utokanao na nguvu za maji katika mto Rufiji chenye uwezo wa kuzalisha 2,100MW  kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani; na Maboresho katika sekta ya madini na kilimo; na uanzishwaji wa kanda maalum za kiuchumi (EPZ/SEZ).

Tunatarajia pia kuwa viwanda vilivyojengwa na vitakavyojengwa vitachangia zaidi Pato la Taifa kwa kuchochea uzalishaji mali hasa bidhaa za kilimo na kuongeza thamani ya bidhaa. Aidha, mapato ya ndani yanatarajiwa kuongezeka kutokana na hatua mbalimbali za Serikali kukuza uchumi na kupanua wigo wa mapato.
Pia, maboresho ya mazingira ya biashara na uwekezaji yanayoendelea kutekelezwa na Serikali yanatarajiwa kushawishi na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi.

Mfumuko wa bei unatarajia kuendelea kubakia katika wigo wa tarakimu moja isiyozidi asilimia 5.0 katika kipindi cha muda wa kati. Thamani ya shilingi ya Tanzania inatarajiwa pia kubaki kuwa imara.

Nakisi ya urari wa biashara ya nje inatarajiwa kupungua kufuatia mikakati ya kuongeza thamani na mauzo ya mazao ya kilimo na madini kwa kutumia viwanda vya ndani, na kuimarika kwa shughuli za utalii na huduma za usafirishaji kwenda nchi jirani.

Akiba ya fedha za kigeni itaendelea kuwa ya kuridhisha na kutosheleza mahitaji ya fedha za kigeni na kwa kiwango cha kutosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kwa miezi 4.5 kilichowekwa kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sekta ya kibenki unatarajiwa kuendelea kuwa imara ikiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha. Aidha, ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi unatarajiwa kuendelea kuongezeka kufuatia hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na BoT na Serikali ikiwamo kuboresha masoko ya fedha, usimamizi wa karibu wa utendaji wa mabenki, na kuboresha mazingira ya kufanya biashara.

14.        Changamoto Katika Nusu ya Pili ya 2018/19
Pamoja na kukua kwa uchumi na matarajio ya kuimarika kwa ukuaji, zipo changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kuathiri mwenendo wa Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa bajeti ya 2018/19 kama ifuatavyo:

       i.        Kuongezeka kwa gharama za mikopo kwenye masoko ya fedha duniani kutokana na mabadiliko ya sera za fedha katika nchi kubwa kiuchumi (hususan Marekani na nchi za Ulaya) na kupungua kwa misaada ya kibajeti na fedha za washirika wa maendeleo za kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo:Katika kukabiliana na changamoto hii, Serikali inaongeza nguvukuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kupanua wigo na vilevile kuimarisha usimamizi wa matumizi ya Serikali. Aidha, Serikali inatafutavyanzo vingine vya mikopo ya nje vyenye masharti nafuu katika nchi za Mashariki ya Kati na Mashariki ya mbali.

     ii.        Mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuathiri uzalishaji hususan katikasekta mama ya kilimo ambapo sehemu kubwa bado tunategemea mvua. Mkakati wa Serikali ni kuongeza nguvu kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, kuhifadhi vyanzo vya maji, kuhimiza matumizi ya mbegu bora za mazao ikiwa pamoja na yanayohimili ukame, na kuongeza jitihada za kutafuta masoko ya uhakika ya mazao.
    iii.        Mvutano wa kiuchumi baina ya Marekani na China unaopelekea nchi hizo kuwekeana kodi za kulipizana kisasi (retaliatory tariffs)unaweza kuathiribiashara kati ya Tanzania na China kutokana na uwezekano wa kuongezeka kwa bei ya bidhaa tunazoagiza kutoka China. Ili kujihami, Serikali imejielekeza kupanuawigo wa bidhaa na huduma tunazouza nje (hasa utalii) na nchi washirika wa biashara.

    iv.        Uwezekano wa kupanda kwa bei za mafuta kwenye soko la dunia kutokana na Marekani kuiwekea tena vikwazo nchi ya Iran na vita vinavyoendelea Syria, na Yemen. Mkakati wa Serikali kukabiliana na changamoto hiyo ni kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na gesi asilia na vyanzo vingine mbadala, pamoja na ujenzi wa bwawa na mtambo wa kufua umeme Mto Rufiji.

15.        Hitimisho
Watanzania tumeshuhudia mafanikio makubwa sana katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa Mhe. Dkt. John P.J. Magufuli. Naungana na Rais wetu kuwashukuru wananchi wote wazalendo ambao wametekeleza wajibu wao wa msingi wa kulipa kodi na kuiwezesha Serikali kugharamia miradi ya maendeleo na kupata mafanikio ya kishindo! Hakika Watanzania tunaweza.

Hata hivyo, ni dhahiri pia kuwa tumeingia katika vita kubwa ya kiuchumi (ndani na nje ya nchi). Marekebisho ya sheria na mapitio ya mikataba mbalimbali ambayo yamefanyika chini ya uongozi shupavu wa Rais Magufuli kwa lengo la kuhakikisha kuwa Watanzania wote wananufaika na rasilimali za Taifa, na pia hatua za kijasiri za kupambana na rushwa, kukusanya mapato ya Serikali na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, yamewaumiza wachache waliokuwa wananufaika na mfumo uliokuwepo juu ya migongo wa wananchi wanyonge.

Ninawasihi sana Watanzania wenzangu tusimame pamoja katika vita hii. Mambo matatu muhimu sana ni kuwa: (i) kila mmoja wetu awajibike kufanya kazi kwa bidii (yaani shughuli yoyote halali katika kilimo, ufugaji, uvuvi, viwandani, biashara, huduma, utumishi wa umma, na masomoni) ili kujipatia kipato au ujuzi kuwezesha kuboresha maisha yake na familia yake na pia kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa; (ii) kila Mtanzania mwenye kipato, awajibike na aone fahari kulipa kodi inayowiana na kipato chake ili kujijengea uhalali wa kuidai Serikali nayo kutoa huduma bora kwa wananchi. Wakati umefika kwa Tanzania kuachana na bajeti tegemezi, maana utegemezi unadhalilisha na pia unahatarisha uhuru wa kweli wa Taifa letu; na (iii) wale waliokuwa wanafaidi juu ya migongo ya Watanzania masikini, wabadilike (waokoke!) maana Watanzania wengi hawako tayari kurudi nyuma!

Kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) napenda kuwasisitiza tena watumishi wote wa TRA kutoza kodi kwa mujibu wa sheria za kodi na kanuni zake. Kama maandiko matakatifu yanavyoelekeza: “Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa” (Luka 3:11-16). Makadirio ya kodi yasiwe kandamizi. Aidha, ninaukumbusha uongozi wa TRA utekeleze maagizo ya Mheshimiwa Rais aliyoyatoa katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha TRA kilichofanyika Mwalimu Nyerere Convention Centre tarehe 10 Disemba 2018. Utaratibu wa kumfungia mfanyabiashara biashara yake ili kushinikiza alipe kodi anayodaiwa, sasa usitishwe isipokuwa kwa mkwepa kodi sugu na kwa kibali cha Kamishna Mkuu wa TRA! Badala yake, TRA ijikite zaidi kutoa elimu kwa mlipa kodi juu ya utunzaji wa vitabu vya hesabu za biashara, na kumpa fursa ya kufanya naye majadiliano kuhusu mpangilio bora wa kulipa malimbikizo ya kodi kwa mkupuo au kwa awamu pamoja na adhabu stahiki kama zilivyobainishwa kwenye Sheria ya Usimamizi wa Kodi 2015. Matumizi ya lugha mbaya, vitisho na ubabe dhidi ya walipa kodi wenye historia nzuri ya kulipa kodi stahiki yasipewe nafasi kabisa, na pale inapothibitika kwenda kinyume na maadili mema basi mtumishi husika awajibishwe mara moja kwa kuzingatia taratibu za kiutumishi. Vilevile, mtumishi wa TRA yeyote anayetuhumiwa kupokea au kudai rushwa asimamishwe kazi mara moja kupisha uchunguzi wa vyombo husika (TAKUKURU na Jeshi la Polisi). Aidha ninaiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania kuongeza jitihada za kudhibiti biashara ya magendo inayoendeshwa na wafanyabiashara wanaopitisha mizigo bandari bubu kwa nia ya kukwepa kodi hususan eneo la mwambao wa bahari ya Hindi na sehemu zote za mipakani na kuhakikisha kodi stahiki inalipwa mara moja na bidhaa zilizokamatwa kutaifishwa.

Kwa upande wa mabenki, Serikali inayataka mabenki yote ya biashara nchini yaongeze jitihada za kupeleka huduma za kibenki vijijini katika mwaka ujao 2019, kwa kuanza na shughuli na maeneo ambayo yana fursa za kupanua wigo wa huduma za kibenki kama vile minada ya mifugo, masoko makubwa mipakani na miji midogo na ile inayoibukia kibiashara.

Napenda kuwahakikishia tena wafanyabiasharakuwa Serikali inathamini sana mchango adhimu wa wafanyabiashara katika maendeleo ya Taifa hili. Serikali imedhamiria kuongeza jitihada kurahisisha mazingira ya kufanya biashara nchini na hususan kwa kupitia tena mfumo wa kodi na tozo mbalimbali zinazowakwaza. Aidha, katika kipindi kilichobaki cha mwaka wa fedha 2018/19, Serikali itaongeza kasi ya kulipa madeni na madai mbalimbali kwa serikali yaliyohakikiwa. Lengo letu ni kumaliza kulipa madai mbalimbali kwa muda tuliojiwekea kwenye mkakati wa kulipa madai halali na kudhibiti malimbikizo mapya. Hata hivyo, Serikali inaendelea kuwakumbusha wafanyabiashara wema kulipa kodi kwa mujibu wa sheria ili kuchangia ujenzi wa nchi yao. Ukwepaji kodi hauna nafasi chini ya Serikali ya awamu ya tano.

Kwa mara nyingine napenda, kwa niaba ya Serikali, kuwapongeza sana wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyakazi viwandani, sekta binafsi kwa ujumla, watoa huduma na watumishi wa umma waliofanya kazi kwa bidii katika nusu ya kwanza ya 2018/19 na kuufanya uchumi wetu kuendelee kukua kwa kasi na pia kwa kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi. Aidha, ninawakumbusha wananchi wote agizo la Mheshimiwa Rais kwamba "UKIUZA, TOA RISITI. UKINUNUA DAI RISITI"

Mwisho kabisa ninawaalika wadau wote wa kodi na wananchi kwa ujumla kutuletea kwa maandishi mapendekezo na ushauri kuhusu vyanzo vipya vya mapato ya Serikali na marekebisho ya viwango vya kodi kwa ajili ya bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2019/20 na ninaomba mapendekezo hayo yawasilishwe kwa maandishi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kabla ya tarehe 10 Februari 2019.

Nawatakia Wazalendo wote wa Watanzania HERI YA MWAKA MPYA 2019.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yapigwa Marufuku Kufungia Maduka ya Wasiolipa Kodi

0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepigwa marufuku kufunga maduka na biashara za watu kwa kisingizio cha kutolipa kodi, badala yake imetakiwa kukaa meza moja na wafanyabiashara ili kujadiliana nao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alitoa agizo hilo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa na utekelezaji wa bajeti ya Serikali katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2018/19.

“Utaratibu wa kumfungia biashara mfanyabiashara anayedaiwa kodi ili kumshinikiza alipe sasa usitishwe mara moja, isipokuwa kwa wakwepa kodi sugu na hapo lazima kuwe na kibali cha kamishna wa mkuu wa TRA, nataka mjikite katika kutoa elimu siyo vitisho,” alisema Dk Mpango.

Waziri huyo alikemea matumizi mabaya ya lugha, vitisho na ubabe dhidi ya walipakodi wenye historia nzuri akitaka yasipewe nafasi na itakapothibitika mtumishi wa TRA amekwenda kinyume awajibishwe kwa kuzingatia tararibu za kiutumishi.

Dk Mpango alisema hata Rais John Magufuli amekwishaagiza utaratibu wa kufungia maduka usitishwe alipofungua kikao kazi cha TRA Desemba 10, hivyo amri hiyo inapaswa kutekelezwa.

Kiongozi huyo aliagiza TRA kujikita katika kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili waone faida na thamani ya kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yao na akawataka kupambana na wakwepa kodi hasa katika maeneo ya bandari bubu ambako alisema dawa yao ni kuwalipisha kodi na kutaifisha bidhaa zilizokwepa kulipiwa.

Dk Mpango alisema hali ya maisha ya Watanzania imeendelea kuimarika hasa waliopata ajira na katika shughuli za uchumi zinazokua kwa haraka kama ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, upanuzi wa bandari na viwanja vya ndege ambao wengi wamejenga nyumba bora.

Alisema ukuaji mzuri wa uchumi uliisaidia Serikali kuongeza ukusanyaji wa mapato na kugharamia uboreshaji wa huduma za jamii katika zahanati, elimu, dawa, maji na kuimarisha uzalishaji wa umeme na kuusambaza vijijini.

Dk Mpango alisema mabadiliko yaliyofanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Juni 2017 yaliweka masharti ya uendeshaji wa maduka ya kubadilishia fedha ambapo yamesababisha zaidi ya nusu ya maduka hayo kufutwa kwa kutokidhi vigezo.

“Tuliweka masharti kuwa kiwango cha chini cha mtaji wa maduka yaliyoko daraja A kiongezeke kutoka Sh100 milioni hadi 300 milioni na daraja B kutoka Sh250 milioni hadi 1 bilioni, hivyo zoezi la usajili limeendeshwa na tulikuwa na maduka 297, lakini tumetoa leseni kwa maduka 109 ndiyo yamekidhi vigezo,” alisema

Waziri Mpango alisema sekta ya benki imeendelea kuimarika na kutengemaa ikiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha zaidi ya kiwango kunachotakiwa kisheria ambapo mitaji ya benki ukilinganishwa na rasilimali zao ni asilimia 16.3 wakati kiwango kinachotakiwa ni asilimia 10.

Waziri alisema katika kipindi cha Januari hadi Novemba, sekta hiyo ilipata faida ya Sh285.4 bilioni ikilinganishwa na Sh317 bilioni katika kipindi kama hicho mwaka jana wakati mikopo chechefu iliendelea kushuka hadi kufikia asilimia 9.7 ya mikopo yote mwezi Septemba 2018 kutoka asilimia 12.8 iliyorekodiwa Desemba 2017.

Waziri Mpango alisema shilingi ya Tanzania imeendelea kuwa tulivu katika kipindi cha Julai hadi Novemba ambapo Dola ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa Sh2,276 ikilinganishwa na Sh2,235 katika kipindi kama hicho 2017.

Mvua Kubwa Yaua Mmoja Kwa RADI Akiwa na Mtoto Mgongoni.....Nyumba 250 Zaezuliwa na Kubomoka

0
0
Mkazi wa Kijiji cha Nambalapi mashambani, Kata ya Masonya, wilayani Tunduru, Awetu Adam (33), amefariki dunia baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na upepo mkali akiwa shambani.

Mvua hiyo iliyonyesha Desemba 29, mwaka huu kwa saa nne kuanzia saa 9 hadi 12 jioni imeripotiwa pia kuezua na kubomoa zaidi ya nyumba 250 za wananchi wa tarafa hiyo.

Pia imeharibu na kuvunja miundombinu ya Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kung`oa baadhi ya nguzo na kusababisha ukosefu wa nishati hiyo katika baadhi ya maeneo ya mji huo.

Mbali na tukio la kifo, mtoto wa miaka miwili Bakari Said, alijeruhiwa kwa kupigwa na radi wakati akiwa amebebwa mgongoni na mama yake ambaye alikufa kwa kupigwa na radi.

Diwani wa Kata ya Mchangani, Haillu Hemed Mussa, alisema jumla ya nyumba 141, madarasa matano na ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Mchangani, zimezuliwa.

Alifafanua kuwa pamoja na uharibifu huo pia kata yake iliripoti kujeruhiwa wananchi watatu waliotambuliwa kama, Kawale Bakari, Alli Ambe na Shekhe Mohamed Salum, ambao walikimbizwa Hospitali ya Serikali ya Wilaya kwa ajili ya matibabu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Majengo, Abdalah Rajabu, alisema kuwa tukio la mvua hiyo limesababisha kuezuliwa kwa mapaa ya maghala mawili ya kuhifadhia korosho mali ya Chama Kikuu cha Wakulima (TAMCU) na kulowesha tani 536 za korosho, mali ya serikali.

Alisema pamoja na madhara hayo pia upepo na mvua hizo ziliezua nyumba 13 mali ya wakazi wa eneo la kata yake.

Diwani Rashid Mkwawa kutoka Kata ya Nanjoka, alisema kuwa jumla ya wakazi 11 walikosa makazi kutokana na nyumba zao kuezuliwa na mvua hizo.

Taarifa zilizotolewa na maofisa tabibu katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, zinaeleza kuwa majeruhi wote wanaendelea vizuri baada ya kuanza kupatiwa matibabu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na tayari amewaagiza viongozi wa serikali za vijiji kuzunguka katika maeneo yao na kufanya tathmini ili kubaini hali halisi ya uharibifu huo.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH....Anatoa Pete za Bahati, Anasafisha Nyota, Anazuia Chuma Ulete na Mengine

0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam Shariff,  Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
 
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
 
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Adam Shariff Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. 

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Mawasiliaono: +255715971688  au +255756914036
 
Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power

0
0
Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power Kwaajili Ya Nguvu Za Kiuume Na Promix Kwaajili Ya Kuongeza Maumbile;

Kwa mwanaume aliyekamilika na mwenye Afya njema ili kumridhisha mke au mpenzi anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya Mara mbili hapo utamridhisha mpenzi wako ila ukiwa unapiga moja au mbili hapo ujue umejilidhisha wewe 

Tiba Ya Tatizo Lako Ni Dawa Hiitwayo Simpo Power No, 1; dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge vya miti shamba na unga ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja :-1 itakufanya urudie tendo zaidi ya mara tatu 
2 itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-20 kwa tendo la Kwanza 
3 huimarisha uume uliolegea na kusinyaa 

Je Una Mke Au Mpenzi Aliyebalikiwa Kuwa Na Kario Kubwa Au Mwili Mnene Na Wewe Mume Wake Una   Maumbile Mafupu?; tumia sasa dawa ya PROMIX dawa itakufanya umfikishe shemu nyeti maana inaboresha maumbile saizi upendayo.

Dawa zangu haziina madhara yoyote kwa mtumiaji 

MARKSU; ni dawa ya kisukari dozi siku 21 
MWARU; ni dawa ya uzazi,hufungua milija ya uzazi ata kwa Wale waliofungiwa uzazi  
MTUNDUU; ni dawa ya busha bila kupasua 
MAZANZA; ni dawa ya kisukar zipo dawa za miguu Kuuma,tumbo,kupunguza Matiti,kutoa minyama uzembe ngiri,vidondo vya tumbo  

FIKA OFISINI KWANGU BUGURUNI MALAPA KARIBU NA KOTA ZA POLISI AU PIGA  SIMU ULETEWE MAHALI ULIPO SIMU NO : 0783185060 au 0752348593  -DR AGU

Deni la taifa Laongezeka Hadi Trilioni 49.37 kwa Mwaka 2018

0
0
Serikali  imesema deni la taifa limefikia Sh. trilioni 49.37 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na Septemba 2017, lililokuwa Sh. trilioni 47.82 sawa na ongezeko la asilimia 3.2.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema hayo jana, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya fedha ya hali ya uchumi wa taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya nusu mwaka ya 2018/2019 iliyotolewa, jijini Dodoma.

"Nchi kuwa na deni sio dhambi, jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa fedha tulizokopa zinatumika kujenga rasilimali ambazo ni msingi wa kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha mali na kulipa mikopo hiyo," alisema Dk. Mpango.

Dk. Mpango alisema, kufikia Septemba 2018, deni la taifa lilifikia kiasi cha Sh. trilioni 49.37, ikilinganishwa na deni hilo Septemba 2017, lililokuwa Sh. trilioni 47.82 sawa na ongezeko la asilimia 3.2.

Waziri Mpango alisema katika deni hilo, la ndani ni Sh. trilioni 13.64 sawa na asilimia 27.6 na la nje ni Sh. trilioni 35.72, sawa na asilimia 72.4.

Alitaja sababu za ndeni hilo kuwa ni mikopo ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, madaraja na bandari.

Sababu nyingine aliitaja kuwa ni ujenzi wa mitambo ya kufua umeme ya Ubungo, Mwanza na Kinyerezi II, miradi ya maji ikijumuisha wa maji wa Ziwa Victoria.

Alitaja sababu zingine kuwa ni miradi ya Tasaf, Mkongo wa Taifa wa mawasiliano na mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).

Hata hivyo, Dk. Mpango alisema matokeo ya awali ya tathmini iliyofanywa Desemba 2018, inaonyesha kuwa deni ni himilivu kwa muda mfupi na mrefu.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya mikopo, dhamana na misaada sura 134, serikali ina wajibu wa kufanya tathmini ya uhimilivu wa deni (DSA) kila mwaka ili kupima mwenendo wa deni na uhimilivu wake.

Katika tathmini hiyo viashiria vinaonyesha uwiano ufuatao: Deni la serikali kwa GDP asilimia 27.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 70.

Kwa uwiano wa deni la nje kwa GDP asilimia 22.2 ikilinganishwa na ukomo wasilimia 55, kwa deni hilo la nje mauzo nje asilimia 157.3, ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 240 , ulipaji wa deni la nje kwa kutumia mauzo ya bidhaa za nje asilimia 15.2 ikilinganishwa na ukomo asilimia 23 na ulipaji wa deni kwa mapato ya ndani ni asilimia 49.6.

Alisema viashiria vyote vinaonyesha kuwa serikali ina uwezo wa kuendelea kukopa na kulipa pale mikopo inapoiva.

Dk. Mpango alisema serikali itaendelea kusimamia deni na kuhakikisha kuwa linaendelea kuwa himilivu, mikopo itaelekezwa kugharamia miradi ya maendeleo yenye tija kwa taifa na ambayo inachochochea ukuaji wa uchumi.

Aliongeza kuwa serikali itaweka kipaumbele kukopa mikopo yenye masharti nafuu na kuhakikisha ya masharti ya kibiashara inakopwa kwa uangalifu mkubwa na inatumika kwenye maeneo yanayochochea ukuaji wa uchumi.

Aidha, alisema matarajio ya serikali ni kuwa viwanda vilivyojengwa na vitakavyojengwa vitachangia zaidi pato la taifa kwa kuchochea uzalishaji mali hasa bidhaa za kilimo.

Wahamiaji haramu 13 wafariki baada ya Kutupwa Barabarani Morogoro

0
0
Wahamiaji 13 kati ya 26 raia wa Ethiopia wamefariki dunia baada ya kutupwa eneo la Sangasanga mkoani Morogoro Barabara Kuu ya Iringa- Morogoro na gari aina ya lori ambalo halijajulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumapili Desemba 30, 2018, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema tukio hilo liliripotiwa saa 9 alasiri jana na Vyombo vya usalama kwenda eneo la tukio na kukuta raia 26 kati yao 13 wakiwa wamepoteza maisha.

Mutafungwa  amesema watumiaji wa barabara hiyo waliiona miili ya raia hao pembeni mwa barabara na kutoa taarifa kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani eneo la Sangasanga.

Kamanda huyo amesema kati ya raia hao yumo mtoto wa miaka minane na polisi wanaendelea na uchunguzi ili kulibaini lori na wahusika wa tukio hilo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images