Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tazama Hapa LIVE: Rais Magufuli akutana na Vigogo wa TUCTA, NSSF, PSSSF na SSRA

$
0
0
Tazama Hapa LIVE: Rais Magufuli akutana na Vigogo wa TUCTA, NSSF, PSSSF na SSRA

Picha Ya Lemutuz Akiwa na Gari la Serikali Yaibua Gumzo Mtandaoni

$
0
0
Picha aliyoipiga Wiliam Malecela maarufu kama Lemutuz na kuposti katika mtandao wake wa kijamii ikimuonesha ameegemea gari la Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro na kuandika maneno ya kumshukuru kwa kumpatia usafiri huo, imeibua mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii.
 
Jana Lemutuz aliposti picha mbili tofauti katika ukurasa wake
wa kijamii wa Instagram, moja ikimuonyesha akiwa amesimama na mdada aliyevaa koti la rangi ya kaki na nyingine ikimuonesha ameegemea gari la DC Muro.

Baada ya kuposti picha hiyo ambayo ilikuwa na maneno yafuatayo; “Thanks to God hatimaye nimefika salama at Masailand Safari Lodge...downtown Sakina/Arusha...I mean thank u ndugu yangu sana DC wa Arumeru JerryMuro kwa
kunipatia usafiri toka nilipofika mpaka hapa...I mean I am Super Humbled u know,” aliandika Lemutuz.
 Aidha baada ya picha hiyo na maneno hayo uliibuka mjadala katika mitandao ya kijamii ambapo watu mbalimbali walihoji sababu ya Lemutuz kuumia gari la Serikali kwa safari zake binafsi.
 
Hata hivyo muda mfupi baada ya kuibuka kwa mjadala huo, Lemutuz alidaiwa kubadilisha picha hiyo na kuweka picha ile ile lakini ikiwa na maneno mengine tofauti.
 
Katika posti ya pili Lemutuz aliandika;  “Thank God hatimaye
nimefika at Masailand Safariandlodge...I mean happy to meet you bro Jerrymuro1980...na thank u Masailand Safariandlodge kwa ukarimu wa ajabu sana...I am home here u know and I lov it,” aliandika.
Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Muro alisema Lemutuz ni rafiki yake aliyekwenda jijini Arusha kwa ajili ya kutalii na yeye kama mwenyeji wake alikwenda hoteli aliyofikia kumsalimia.

“Masailand Hotel iko Sakina, Ngaramtoni ambayo ni wilaya yangu ya Arumeru na alikuja kwa ajili ya kutalii kama mtalii wa ndani na mimi nilikwenda pale kumsalimia na alipiga picha kwenye gari la umma yeye ni mwananchi na ana haki ya kupiga picha nalo,” alisema.

“Msifuate yanayoandikwa kwenye mitandao, wale ni wageni wangu nilikwenda kuwatembelea hotelini wakapiga picha na gari la serikali sasa si mali ya Muro. Lile ni gari la umma ni mali ya wananchi wanahaki nalo,” alisema.

Baadhi ya wachangiaji kwenye mitandao hiyo ya kijamii walihoji kubadilishwa maneno na picha ya awali iliyokuwa ikionyesha namba za STK na bendera ya taifa na kuwekwa picha mpya.

“Yaani unapata ujasiri wa kumpa rafiki yako gari la serikali tena bendera inapepea duu,” alihoji mmoja wa wachangiaji kwenye picha hiyo.

Mapendekezo Yaliyotolewa na THTU kwa Rais Magufuli kuhusu kikokotoo

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU), Paul Loisulie ametoa pendekezo la kuundwa kwa  kamati shirikishi kwa ajili ya kujadili na kusikiliza hoja kuhusu kikokotoo.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Desemba 28, 2018 mbele ya Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam katika mkutano unaoendelea hivi sasa uliowakutanisha viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), mifuko ya hifadhi za jamii ya PSSSF na NSSF na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA).

Hivi karibuni umeibuka mjadala kuhusu mafao baada ya kanuni  za Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuondoa mfumo wa zamani wa kulipa asilimia 50 ya mafao ya mkupuo na badala yake mstaafu kuruhusiwa kuchukua asilimia 25 kwa mkupuo na asilimia 75 igawanywe ili ilipwe kama pensheni kwa kila mwezi kwa kipindi chote cha maisha ya mstaafu.

Katika maelezo yake Loisulie amesema kamati hiyo itakwenda kufanya hesabu ya kusikiliza hoja za wafanyakazi na mwelekeo bora zaidi kuhusu suala hilo ili waende kisayansi.

“Ninaamini tukikaa pamoja na kuangalia msingi wa  kikotoo hiki tutapata mwafaka ambao hautaumiza mifuko wala wafanyakazi,”  amesema.

Amesema moja ya madai ya wafanyakazi baada ya mifuko kunganishwa ni kupata mafao madogo tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Amesema mbali na hilo, wafanyakazi wanataka itumike fomula ya mwanzo ilivyokuwa mifuko mbalimbali lakini msimamizi hataki kwa madai ya kuwa mifuko itakufa badala yake itumike mpya.

Kikao hicho kinaongozwa na Rais Magufuli ambaye huenda akaweka msimamo wake kuhusu sakata hilo.

Breaking News: Rais Magufuli aamuru Kikokotoo cha zamani kiendelee hadi 2023

$
0
0
Rais Magufuli ametangaza kuwa kikokotoo kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya Mifuko ya Hifadhi za jamii kuunganishwa kiendelee katika kipindi cha mpito hadi mwaka 2023, ambapo wanachama 58,000 ndio Watastaafu katika kipindi hicho.


==>>Tazama hapo chini nukuu ya maneno yote aliyoyasema leo

1. Nimewasikiliza, kimsingi lina umuhimu, na ndio maana nimeona niwaite, na hasa kwa sababu nimekuwa nikisikiliza maelezo hata ya regulator, yanakuwa too academic. 

2.Ukishatoa maelezo ambayo ni too academic, unaelezea wastaafu, na kustaafu ni sifa na heshima, ulifanya kazi yako kwa uadilifu mkubwa, umesacrafice maisha yako kwa ajili ya kazi.  

3. Unapoona hiyo heshima inakuwa karaha, mateso, inafrustrate kwa mfanyakazi yoyote, sasa mimi siko hapa kumfrustrate mtu, kwani hata mimi nilikuwa mfanyakazi.  

4.Tuliamua kuunganisha mifuko, tulikubaliana NSSF ufanyiwe marekebisho, hatua hii ilitokana na ombi la muda mrefu la vyama vya wafanyakazi waliotaka hii mifuko iunganishwe.  

5.Mifuko ya jamii yote ilikuwa na hali mbaya, kwa sababu haikuwa coordinated, waendesha mifuko wote walikuwa wanapigana vita, wanagombania wanachama, walikuwa hawapendani.  

6.Mingine ilikuwa ikiendeshwa kiajabu, pakawa panaanzishwa miradi ya kiajabu, na miradi mingi ilikuwa ya majengo, nenda Kigamboni kaangalie yale majengo ya ndege vilaje, its a huge thing'. 

7.Tulipongia madarakani tulikuta deni trilion 1.2, serikali yenyewe haijachangia hii mifuko, waliostaafu kwa wakati ule ilikuwa ni shida, kwani hata ile michango ya serikali haitekelezwi. 

8.Tukaanza kulipa madeni, mpaka mwezi Machi mwaka huu madeni yote yalikuwa yamemalizika kulipwa. 

9.Matatizo yapo lazima tuende kwenye solution, kile kikokotoo angalau imefika 50%, lakini pia hata hawa walioko chini ilifaa ipande, hata hiyo formula inachanganya zaidi.

10.Mishahara mingi ya wafanyakzi serikalini si mizuri, anapofika mwisho unampa kidogo kidogo haingii, si unipe tu yote nikafie mbali, nilipokuwa nachangia hukuniambia, leo nachukua unaniambia nachukua kidogo, hata logic haingii. 

11.hata hawa Mawaziri, wabunge wanachukua hela yao yote, halafu uwaambie utachukua kidogo kidogo kila ukija, hawatakubali, kwenye reality, hata mimi hainingii.  

12.Tunahitaji watu wetu wapate fedha nyingi walipwe, lakini pia tunahitaji huu mfuko usife, hii formula haipo duniani, mtu anamaliza halafu kiwango chake unakizidisha mara 4, haipo.

13. Walioweka formula hii ni makatibu wakuu wa wakati ule, wa wakati wangu hawawezi, kwa sababu kwenye ile mifuko wengine ni beneficiary, ni kosa walifanya.  

14. Hifadhi za jamii zipunguze matumizi ya hovyo, kama mtu anastahili kulipwa 60% hatuwezi kumlipa kwa sababu hifadhi zinafanya matumizi ya hovyo.  

15. Kwa mfano kuna mfuko mmoja unachapisha kalenda kwa 1.3 bilion, hiyo hiyo imeajiri walinzi ambao ni very expensive, wanawalipa bilioni 2 kwa mwaka, wakati wangeajiri SUMA JKT wangewalipa chini ya bilioni 1 kwa mwaka.  

16. Uwekezaji kama ule wa Dege Heko village haufai, ukatumia fedha za wanachama bila ridhaa zao, halafu leo wastaafu uwaambie hamna hela formula imekataa.  

17. Mifuko muweke utaratibu mzuri, ni suala ambalo haliingii akilini nikasubiri mpaka nitakapofika miaka 60 ndio nipate mafao yangu, nimetoa michango yangu, kwanza hayupo atakaye nikumbuka kama nilifanya kazi, hata contructor atakuwa kashakwenda kwao.  

18. Kustaafu sio dhambi, kustaafu ni heshima, lazima awe respected, mwalimu amefundisha ameharibu na macho kutokana na chaki, halafu umpe condition.  

19.Mazungumzo yenu yote nimeyasikia, mimi nimeamua, angalau tuwe na kipindi cha mpito, kikokotoo kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya mifuko kuunganishwa, tuendelee katika kipindi cha miaka ya mpito. 


20. Mtu anayestaafu anatakiwa kuheshimiwa, amelitumia taifa hili, amesacrafice, ni shujaa, kustaafu bila kufukuzwa ni heshima, hatakiwi kupata shida, nimeamua kikokotoo kiendelee katika kipindi hiki cha mpito, ambapo ni hadi mwaka 2023.  

21. Mifuko hiyo itakuwa imetengamaa, ni matumaini yangu, nitaichungulia kweli kweli hiyo mifuko, na Waziri natoa maagizo yake, wachungulie kweli, ili kusudi watu wasitumie hovyo hovyo, hii ni mifuko ya wanachama. 

22.Formula nzuri ni zile zinazo wapromote wafanyakazi, ndio ninazozitaka mimi, formula zinazowanyima haki wafanyakazi sio formula nzuri, ninashukuru katika kipindi hiki kifupi cha kuunganisha mifuko tumeanza kuona matokeo.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Huna Sababu ya Kuabika Tena, Jipatie Dawa Bora ya Nguvu za Kiume, Maumbile Madogo na Mvuto wa Mapenzi

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiathiri watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine ....kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapungufu katika mwili wake.

Kuna sababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huathiri misuli ya uume, 


Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0620510598  / 0743543944

Mrema Aiangukia Serikali Ruzuku Vyama vya Siasa .....Aiomba Iruhusu Mikutano ya Hadhara

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema, ameitaka serikali inapofanya marekebisho ya vyama vya siasa kuangalia umuhimu wa kuvipatia vyama vidogo vya siasa ruzuku, ili navyo viweze kujiendesha.
 
Mbali na kutaka marekebisho hayo kuruhusu vyama vya siasa ambavyo havina wabunge wala madiwani kupewa ruzuku, pia ametaka sheria iruhusu kufanyika kwa mikutano ya siasa ili kuweza kujenga vyama hivyo.
 
Mrema alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana na kusema yapo mambo ambayo katika marekebisho ya siasa lazima yaingizwe na kutoa nafasi sawa kwa vyama vya siasa vidogo na vikubwa, kwani
vyote vinafanya siasa za kulijenga taifa kwa misingi ya utaifa.
 
Katika hatua nyingine Marema alivitaka vyama vya siasa vya
upinzani kuangalia uwezekano kwa kuunganisha nguvu kwa ajili ya kuusoma vema muswada wa vyama vya sheria na kuona ni wapi kuna mapungufu, ili yaweze kurekebishwa na yale mazuri yakubaliwe.
 
Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, alisema
licha ya kuwa yeye ni mtumishi wa serikali kwa sasa, hawezi kufumbia macho mambo maovu ambayo yanafanywa na serikali na kama yatakuwepo atayasema.
 
“Mimi pamoja na kuwa mtumishi wa serikali ikumbukwe nimeitumikia nchi hii kwa nafasi mbalimbali, hivyo siwezi kunyamaza pale ninapoona mambo yanaenda vibaya, lakini pia ninapoona mambo yanaenda vizuri nitasema ukweli,”alisema Mrema.
 
Mrema alikana kuwa kibaraka wa serikal, ila  akasema anapenda kusimamiaukweli. 

“Siyo kweli kuwa mimi ni kibaraka wa serikali ya CCM ila nataka kufanya siasa ambayo inaweza kuwa na tija. Haiwezekani nikaona serikali inafanya vibaya nikanyamaza, lazima nitasema na kuikosoa serikali,” alisema na kuongeza:
 
“Kwa mfano nataka serikali iruhusu mikutano ya kisiasa kwa
vyama vyote vya siasa kwani vyama vyote vinajenga nchi, lakini pia ikumbukwe kuwa vyama vyote vinatakiwa kupewa ruzuku ili viweze kujiendesha,” alisema Mrema.

Mzazi Mwenza wa Msanii Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’’ Afunguka Maneno MAZITO Akijiandaa Kuupokea Mwaka Mpya 2019

$
0
0
Mzazi mwenzie wa msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’’, amesema kuwa yuko tayari kuupokea mwaka 2019, kutokana na miaka miwili 2017 na 2018, alipitia matatizo makubwa ikiwamo la kuondokewa na maama yake mzazi.
 
Kupitia ukurasa wake wa Instagraam, Zari, alisema kuwa mwaka 2017 alipitia katika kipindi kigumu cha koondokewa na Mama yake mzazi pamoja na aliyekuwa mume wake Ivan.

Pia, alieleza namna alivyoutumia mwaka 2018 katika kujemga na kuyarekebisha baadhi ya makosa yake na matatizo aliyopitia, kujijenga zaidi baada ya kuondokewa na wapendwa wake hao wawili na kuahidi kuwa yuko tayari kwa mwaka 2019.
 
“Mwaka 2019, niko tayari kwa mwanzo mpya… Katika maisha, sisi huumiza, tunafanya makosa, tunasamehe, tunaendelea. Lakini, zaidi ya yote  tunajifunza. Asante 2018, bado nina pumua.Asante, Nishirikishe hadithi yako ya maisha kwa mwaka 2018,” aliandia Zari.

“2017 i was shattered in ways i could never explain, 2 major deaths of my loved ones, infidelity and other things. 2018 was all about picking up my broken pieces and rebuilding. 2019 am simply ready for a new beginning….

"In life, we hurt, we make mistakes, we forgive, we move on. But, most of all & through it all we learn. Thank You 2018, i still have my breath. #Grateful #Blessed #Thankful Share with me your life story of 2018….,”
-ZARI


Waziri wa Kilimo: Rais Magufuli ni Nyerere kwa maneno na matendo

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga amesema namna ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Joseph Magufuli anavyoongea na kutenda ni sawa Mwasisi wa  Taifa la Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mhe. Hasunga ameyasema hayo leo alipotembelea eneo la Ihumwa ambapo ujenzi wa ofisi mpya za Wizara ya Kilimo zimeanzwa, Jijini Dodoma.

Mhe. Hasunga amesema Baba wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere ndiye aliyetoa wazo la Dodoma kuwa makao ya Chama Tawala pamoja na Serikali lakini kwa miaka kadhaa wazo hilo lilikuwa halijawahi kutekelezwa na kuongeza kuwa Rais Magufuli ndiye amelitekeleza kwa vitendo.

Waziri wa Kilimo ameongeza kuwa baada ya utekelezaji wa wazo hilo la kuhamia Dodoma kwa Serikali, Rais Magufuli aliagiza Wizara zote zijenge ofisi katika eneo moja na kwa kulitekeleza jambo hilo, Wizara zilipewa mgao maalum wa fedha kwa ajili ya kujenga ofisi za kudumu katika eneo la Ihumwa.

“Napenda nimpongeze Mhe. Rais wetu kwa kulisimamia wazo hili la kuwa na eneo maalum na rasmi la kuwa ofisi kwa Wizara zote na moja kati ya faida ni kuwa Wananchi ambao wamekuwa wakisafiri kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata huduma katika ofisi za umma, sasa watapata unafuu wa kuhudumiwa katika eneo moja kama hapa, ambapo kila Wizara itapatikana.” Amekaririwa Mhe. Hasunga.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa, jambo hili ni sawa na utekelezaji wa Oparesheni Sogeza ambapo, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alianzisha katika mwaka 1974 lengo likiwa ni kuhakikisha Wananchi wanakaa pamoja ili Serikali iwahudumie kwa haraka zaidi na kwa ufanisi zaidi.

“Wazo la Mhe. Rais John Pombe Magufuli kuhamia Dodoma na Ofisi za Serikali kukaa pamoja hivi, jambo hili linafanana na wazo la Baba wa Taifa kupitia Oparesheni Sogezaambapo Wananchi wanawekwa pamoja ili Serikali iwajibike sawasawa kwa Wananchi”. Amekaririwa Mhe. Hasunga.

Mhe. Hasunga amefanya ziara ya kushtukiza kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Kilimo ambapo kwa kuanzia Wizara inajenga ofisi za Wakuu wa Idara na Vitengo na baadae zitajengwa ofisi wa Watumishi wengine wa Wizara katika eneo hilo la pamoja.

Akizungumza kuhusu kukamilika kwa ujenzi huo, Waziri Hasunga amesema Mkandalasi alipewa lengo la kukamilisha ujenzi huo tarehe 31/12/2018 lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake, kazi hiyo inataraji kukamilika tarehe 12 Februari, 2019.

Naye Fundi Mkuu wa majengo ya Wizara ya Kilimo, Mhandisi Meja Onesmo Njau amesema kama ambavyo Mpango kazi wao unavyooshesha kazi kuanza rasmi tarehe 10 Disemba, 2018 na kwamba wanataraji kukamilisha na kukabidhi rasmi tarehe 12 Februari, 2019 na kuongeza kuwa Tasisi yao ya SUMA JKT imepewa jukumu muhim na la heshima na kwamba watamaliza kwa wakati.

MWISHO

Askofu aonya misaada ya Wazungu Inayotaka Tukubaliane na USHOGA

$
0
0
Askofu Alinikisa Cheyo wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi amewataka watanzania kuepukana na misaada inayotokana na ushoga kutoka mataifa ya nje.
 
Aidha, amewataka kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ikiwemo adhabu ya viboko kuanzia nyumbani hadi shule hali inayowafanya kujengeka kikatili kwenye makuzi.
 
Cheyo ametoa wito huo katika Kanisa la Mabatini Kata ya Mbalizi Road Jijini Mbeya katika ibada ya mbaraka kwa wanandoa kumi ibada iliyovuta hisia za watu wengi Jijini Mbeya.
 
Hata hivyo ameiasa serikali na jamii kwa ujumla kupinga vitendo vya ushoga kwani ni kinyume na maadili ya Kikristo.
 
“Taifa liepukane na misaada inayotokana na ushoga kutoka mataifa ya nje kuwakuwa ni kinyume na maadili ya dini ya kikristo, hivyo tuupinge kwa nguvu zote,”alisema.
 
Hata hivyo, Askofu Cheyo alisema vitendo vya ukatili vimekuwa vikiongezeka katika jamii vikiwemo vya ubakaji na ulawiti katokana na watoto kufanyiwa ukatili wangali wadogo.
 
Aidha alipendekeza kuondoolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kwani hali hiyo inawafanya watoto kuwa wakatili hata ukubwani.
 
“Ndugu zangu Watanzania sasa hivi tumeshuhudia vitendo vya kikatili dhidi ya watoto kutokana jamii kushindwa kutoa malezi bora kwa watoto wetu”alisema Cheyo.
 
Pia Cheyo amesikitishwa na wanandoa kushindwa kuvumiliana katika ndoa na baadhi ya jamii kuingilia migogoro ya ndoa, amesema migogoro hiyo inapaswa kumalizwa na wanandoa wenyewe na si vinginevyo.

Ameiasa jamii kuheshimu ndoa kwani ndoa ni taasisi huru inayopaswa kujiendesha yenyewe badala ya watu kutoka nje.
 
Akitolea mfano amesema hata migogoro ya ndoa kupelekwa kwa wachungaji au mabalozi si sahihi kwani hata wao wana matatizo yao kwa kuwa nao ni binadamu.
 
Aliwahimiza wanawake kuwa wasafi na kuwataka wanaume kuwaheshimu wanawake.

Mtumishi benki ya NMB Ajeruhiwa Jijini Mbeya....Watu 9 Watiwa Mbaroni

$
0
0
Watu tisa wamekamatwa Mkoani Mbeya kwa tuhuma za uhalifu wa kuvunja, kuiba na kujeruhi likiwemo tukio la mtumishi wa benki ya NMB Kasumulu Kyela na mkazi wa Iwambi Jijini Mbeya Habib Juma.
 
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ulrich Matei amewataja watuhumiwa wawili waliomjeruhi mtumishi wa NMB ni Richard Jackson fundi ujenzi mkazi wa DDC Mbalizi na David Labi (32) ambao walikamatwa Disemba 9 mwaka huu majira ya saa nane mchana wakiwa na nguo za majeruhi, TV, Simu aina ya Tecno na vifaa vilivyotumika kumshambulia majeruhi.
 
Matei alisema watuhumiwa wamekiri kutenda uhalifu huo na kuonesha vitu vilivyoibiwa pamoja na bomba lililotumika kumpigia kichwani ambapo hivi sasa majeruhi anapatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam.
 
Aidha Kamanda Matei alisema Disemba 13 mwaka huu Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watu sita kwa tuhuma za kuwavamia watu usiku wakijifanya sungusungu hususani maeneo ya TEKU, Ilomba,Ituha na VETA.
 
Matei alisema kinara wa tukio hilo ni Pascally Aron (18)dereva wa Bajaj na mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya. Wengine ni Justin Laurence(18) fundi ujenzi mkazi wa Ilemi, Allen Daud(19)mkulima mkazi wa Ilemi, Yassin Naso(19) mkazi wa Ilemi, Hamza Charle (22)mkazi wa Ilemi na Anthony Elias (32)mkazi wa Ilemi. 

Pascally alikiri kujihusisha na uhalifu kwa kujifanya sungusungu ambapo hutishia kwa kutumia mapanga na kuwapora watu vitu vya thamani.
 
Hata hivyo alisema baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
 
Alitoa wito kwa yeyote mwenye kufahamu makundi yanayojihusisha na uhalifu kuwasiliana na jeshi la pilisi kupitia ulinzi shirikishi.

Alichokisema Sumaye, Zitto Kabwe Baada ya Tundu Lissu Kusema Yupo Tayari Kugombea Urais 2020

$
0
0
Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamesema wanamsubiri kwa hamu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu apitishwe na chama chake kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Lissu anayetibiwa nchini Ubelgiji baada ya shambulio la risasi zaidi ya 30 lililotokea Septemba 7, mwaka jana akiwa Dodoma, juzi aliliambia gazeti la Mwananchi kwamba hatakuwa na kipingamizi ikiwa chama chake kitampitisha kuwania nafasi hiyo.

Kauli ya Lissu ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya CCM, imepokewa kwa furaha na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakiamini anaweza kutoa ushindani mkubwa kwa mgombea wa chama tawala.

Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe alisema Lissu atavifaa vyama hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
 
Maoni ya Rungwe yaliungwa mkono na Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye alisema hana shida na kauli ya Lissu.

“Jambo la muhimu kuliko yote ni kuwa mwaka 2019, kwetu ni mwaka wa kudai demokrasia. Azimio la Zanzibar limeweka mpango maalumu wa kukabiliana na ukandamizaji wa demokrasia. Tundu Lissu ni kiongozi muhimu katika harakati hizo,” alisema Zitto.
 
Pia, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema Lissu hajafanya kosa kutoa kauli hiyo kwa sababu mwanachama yeyote anaweza kueleza nia yake.

“Sijamsikia, lakini kama atapitishwa na chama sioni tatizo, kwa sababu kila chama kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea na ni lazima ufuatwe,” alisema Sumaye.

Sumaye ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mwenyekiti wa Kanda ya Pwani wa chama hicho alisema Lissu si wa kwanza, “Nimemsikia hata mheshimiwa (Edward) Lowassa, mimi sioni tatizo kama mtu anafuata utaratibu wa chama.”

Credit:Mwananchi

Askari Magereza Ajiua kwa Kujipiga Risasi Kidevuni

$
0
0
Askari Magereza katika Gereza la Kilimo Kitai wilayani Mbinga, Ruvuma, Adamu Kulwa Mgaga (24), amejiua kwa kujipiga risasi.
 
Askari hiyo mwenye namba B:8400 WDR, amejiua akiwa lindo la mifigo kwa kujipiga risasi eneo la kidevu na kusababisha kichwa kupasuka
 
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma, Arekizanda Nyifwa, alithibitisha kutokea kwa tuko hilo Desemba 25, mwaka huu, saa 2:30 usiku katika gereza la Kitai-Mbinga.
 
Alisema askari huyo alipokuwa lindo ilipofika saa 2:30 usiku alichukua bunduki aliyokuwanayo aina ya SAR na kuelekeza bomba kwenye kidevu chake kisha kuhesabu moja hadi tatu na kufyatu risasi ambazo zilifumua kichwa chake na kufariki dunia papo hapo. 

Alisema askari huyo alifanya hivyo akiwa katika sare za jeshi hilo na kwamba chanzo cha kujiua bado hakijafahamika kwa kuwa hakuacha ujumbe wowote.Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Maagizo Yaliyotolewa na Waziri Mkuu Majaliwa Baada ya Kufanya Kikao na Mawaziri Leo

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la tenki la maji la kutolea huduma katika ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba badala ya ukumbi wa Hazina kama alivyokuwa amepanga awali.

Akiwa Ihumwa, Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri wafike kwenye maeneo ya ujenzi wa ofisi zao, watathmini uwezo wa wakandarasi wanaojenga majengo ya wizara na pale watakapojiridhisha kuwa uwezo wao ni mdogo, wawabadilishe mara moja.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Desemba 28, 2018) akiwa kwenye kikao cha kazi (site meeting) na mawaziri 15 na manaibu mawaziri katika eneo la Ihumwa lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.

“Mawaziri mliopo na makatibu wakuu wote kaeni na wakandarasi wenu hapa site ili waeleze kazi hii itakamilishwa lini. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kazi hii inakamilishwa kwa wakati,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa mrejesho Mawaziri juu ya changamoto alizokutana nazo jana alipofanya ukaguzi wa ujenzi kwa kila wizara. “Nataka Mawaziri ambao ofisi zao zinajengwa wa watu wa Mzinga, wakae nao na kutathmini uwezo wao na kama mtaona hawawezi, mkabidhi kwa mkandarasi mwingine,” amesema Waziri Mkuu.

Amewataka wakandarasi wahakikishe wanaongeza idadi ya vibarua ili kazi hiyo iweze kwenda haraka. “Wizara iliyofanya vizuri kuliko zote ni ya Utumishi, wao wako hatua nzuri. Kwa maana ya uchapaji kazi, eneo nililokuta lina wafanyakazi wengi ni magereza,” amesema.

Wakati huohuo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi alimweleza Waziri Mkuu kwamba kuna wagongaji wa kokoto ambao wamepokea fedha lakini wakaamua kufunga machimbo yao kwa sababu ya sikukuu.

“Waziri wa Madini aongee nao hawa watu ili warejee na kufanya kazi kwa sababu baadhi yao wameshapokea fedha na mahitaji ya kokoto hapa ni makubwa na aliyebakia akifanya kazi ni Nyanza Road Works peke yake,” alisema.

Naye Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alimweleza Waziri Mkuu kwamba wizara yake imetoa transforma tisa za kusaidia kupoza umeme lakini ni wizara nne ambazo zimejitokeza na kulipia line za transforma hizo.

“Wizara yetu tumetoa transforma tisa za kusaidia umeme upatikane eneo la ujenzi. Niwaombe mawaziri waliopo, walipie service line tu ambazo gharama yake ni sh. 921,000 ili wafungiwe transforma na kazi iweze kufanyika mchana na usiku. Hadi sasa, tumeshapokea maombi kutoka  wizara nne tu za Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Elimu na Nishati ili kazi imalizike ndani ya muda mfupi,” alisema.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Kikao Cha Baraza La Vyama Vya Siasa Kufanyika Januari 10 Na 11, 2019 Zanzibar


Polisi Atiwa Mbaroni kwa Kumuunguza Pasi Kijana aliyekuwa Anamvixia Binti Yake Kimapenzi

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikikia askari  E.9301 Koplo Almas kwa tuhuma za kumuunguza kwa pasi mwanafunzi shule ya sekondari Cheyo, Jumanne Hussein (17).

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 28, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ,Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea Desemba 25, 2018.

Amesema mwanafunzi huyo alituhumiwa na Almas kuwa anataka kufanya mapenzi na binti yake.

Amebainisha kuwa baada ya askari huyo kumhisi mwanafunzi huyo alianza kumpiga na kumuunguza na pasi sehemu mbalimbali mwilini.

Kamanda Nley amesema tayari  polisi imechukua hatua za kinidhamu kwa askari huyo ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kijeshi na atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Wasafi Festival kufanya makubwa Dar, Diamond aeleza Itavyokuwa

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz amesema Wasafi Festival itafanya mambo makubwa Dar es Salaam.

Muimbaji huyo kutoka WCB ameeleza hayo baada ya tamasha hilo kumalizika nchini Kenya hapo juzi.

"Dar es Salaam Mwenyez Mungu akijaalia, Nawahidi kwa pamoja tutaandika Kumbukumbu ambayo itaiweka Bongo Fleva yetu kwenye kumbukumbu ya dunia," ameandika Diamond Instagram.

Hadi sasa Wasafi Festival imepita kwenye mikoa ya Mtwara, Morogoro, Iringa, Mwanza, Sumbawanga na visiwani Zanzibar.

Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Rais Magufuli Kuamuru Kikokotoo cha Zamani Kitumike Mafao ya Wastaafu

$
0
0
Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe  amempongeza Rais John Magufuli kwa kukubali ushauri walioutoa na kuacha upande wa waziri, washauri wake na watendaji wa Serikali yake.

Maoni ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini ameyatoa leo baada ya Rais Magufuli kurejesha utaratibu wa awali wa kikokotoo cha asilimia 50 kwa watumishi wa Serikali na asilimia 25 kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.

“Kufuatia uamuzi wa Rais Magufuli kuhusu kikokotoo cha mafao ya pensheni kwa wastaafu , sisi ACT Wazalendo na vyama vya upinzani kwa ujumla tumesimama na wafanyakazi toka mwanzo wa sakata hili, wakati sheria ikiwa muswada na hata baada ya kanuni kutungwa,” amesema 

“Kwetu, jambo lolote linaloongeza maslahi na ustawi wa wafanyakazi ni jambo jema na muhimu. Tunashukuru kuwa Mheshimiwa Rais ametuelewa na amekuja upande wetu na na kuacha upande wa waziri wake, washauri wake na watendaji wa Serikali yake,” ameongeza.

 “Tunapoelekea mbele, tunamuomba asiwe na aibu kutusikiliza na mengine mengi kwa kuwa  nia yetu  ni njema tunajenga nchi moja. Atusikilize na kuhusu mishahara ya watumishi wa umma atusikilize kuhusu mateso  ya wakulima wa korosho na atusikilize kuhusu sheria ya vyama vya siasa.”

“Kama hili la wafanyakazi hatukutumwa na mabeberu, basi na mengine pia hatutumwi na mabeberu,” amesema Zitto

BREAKING NEWS: Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka

$
0
0
Rais Magufuli leo Disemba 28 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka

Taarifa ya Ikulu usiku huu imeeleza kuwa Dkt. Irene Isaka atapangiwa kazi nyingine.

Baada ya Rais Magufuli Kufanya Maamuzi MAGUMU Leo, Mbunge CHADEMA Ataka Waziri Mhagama Ajiuzulu

$
0
0
Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA), Ester Bulaya ambaye pia ni Waziri Kivuli (Ofisi ya Waziri Mkuu) wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, amewataka Waziri Jenista na Mkurugenzi wa SSRA kujiuzulu, baada ya Rais Magufuli kuufuta mswada wa mabadiliko ya sheria ya utoaji mafao kwa kwa wastaafu.

Tayari uteuzi wa   Mkurugenzi wa SSRA umeshatenguliwa na Rais Magufuli Usiku huu.

Bulaya amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter ambapo amesema kuwa Waziri Mhagama na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) wajiuzulu kwa kuwa wameshindwa kuwatetea wafanyakazi.

"Mh Jenista, na Mkurugenzi wa SSRA, mjiuzulu nimewashinda, hamkuwatetea wafanyakazi", ameandika Bulaya.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images