Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Mstaafu wa Marekani, George H. W. Bush kuzikiwa kwa heshima za Kitaifa

$
0
0
Wizara  ya Ulinzi   imesema  maelezo zaidi juu ya mipango ya maziko ya Rais Mstaafu, George H. W. Bush, ambaye alifariki  dunia mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 94, yanaandaliwa na familia yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na wizara hiyo, Rais Bush ambaye alitumikia nafasi ya urais tangu mwaka 1989-1993, ataagwa kwa heshima zote za taifa kesho  katika Kanisa   Kuu la  Washington na kuzikwa Alhamisi katika makazi  yake   katika Jimbo la   Texas.

Ilieleza baada ya jana maandalizi hayo kuwa tayari, mwili wake ungewekwa katika ukumbi wa Rotunda ndani ya bunge la hapa  kwa ajili ya wananchi   kuuaga mpaka kesho  asubuhi, wakati utaratibu wa kupewa heshima zote za taifa uliondaliwa jana.

Tarifa hiyo ilieleza zaidi kwamba umma wa Wamarekani utaweza kuendelea kutoa heshima   za mwisho wakati mwili wa Rais Bush ukiwa katika jeneza kuanzia jana  saa 1:30  asubuhi     hadi Jumatano majira kama hayo.

Ikulu   ilitangaza juzi kuwa Rais Donald Trump  atahudhuria shughuli za kuuaga mwili wa wa kiongozi huyo.

Msemaji wa Ikulu, Sarah Sanders alisema  kesho  imepangwa kuwa siku ya  taifa ya maombolezi  na bendera ndani ya Ikulu tayari zimeshushwa nusu mlingoti kumuenzi kiongozi huyo.

Katika hatua nyingine, mbwa ambaye alikuwa akimuhudumia kiongozi huyo amepigwa picha akiwa amelala kando ya jeneza kama sehemu ya kutoa heshima zake za mwisho.

Mbwa huyo anayeitwa Sully, jana alitarajiwa kusafiri kwa ndege pamoja na jeneza lenye mwili huo kutoka mjini Texas hadi hapa ambako  ulitarajiwa kuanza kuagwa.

Picha iliyotumwa kwa njia ya mtandao wa Twitter na msemaji wa Rais  Bush, Jim McGrath,inamuonyesha  mbwa Sully akiwa kando ya jeneza ikiwa na ujumbe unaosema ‘Mipango imekamilika’.

Afisa Uvuvi Ilemela Mbaroni Kwa Rushwa Ya Mil.1.5

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza inamshikilia ofisa uvuvi wa manispaa ya Ilemela, Williadius Buberwa (33) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. milioni 1.5.

Imeelezwa kuwa kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha 15(1) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba 4, 2018 naibu mkuu wa Takukuru mkoani Mwanza, Emmanuel Stenga amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani muda wowote leo.

Stenga amesema  mtuhumiwa huyo alifanya doria isiyo rasmi katika eneo la Tunza wilayani Ilemela Oktoba 25, 2018 kwenye boti ya mfanyabiashara huyo na kukuta ana vibali vyote.

Stenga amesema mtuhumiwa aliweka kikwazo, kuzuia samaki kushushwa na kutishia kuwataifisha endapo asingepewa fedha.

“Aliomba rushwa ya Sh 2milioni ila mfanyabiashara huyo aliomba kiwango kipungue na kufika  Sh1.5milioni. Alipopewa fedha ndio akaruhusu mzigo kupakiwa kwenye gari,” amesema Stenga.

Ukaribu wa Rais Magufuli, Lowassa Waibua Minong'ono

$
0
0
Mjumbe wa Kamati ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Edward Lowasa ameonekana kutafsiriwa kwa sura mbili tofauti mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kipindi cha siku 6.

Rais Magufuli na Lowasa wamekuwa wakikutana mara kwa mara na kutoleana sifa za kiutendaji jambo ambalo limeonekana kutokuwa la kawaida kutokana upinzani mkali uliokuwepo baina yao kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, lakini pia msimamo wa viongozi wengine wa upinzani nchini dhidi ya serikali ya Rais Magufuli.

Novemba 27 mwaka huu wakati Rais Magufuli, akifungua maktaba mpya ya chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Rais Magufuli alimtolea sifa Waziri Mkuu huyo wa zamani kwa kujitokeza kushiriki kwenye matukio mengi kama hayo.

"Kwenye uchaguzi huwa kuna kushinda na kushindwa, mimi nakupongeza kwa moyo wa kweli na uzalendo kwa Tanzania, na mimi nasema kwa dhati tunahitaji watu waliokomaa kutoka kwenye vyama mbalimbali, kama wewe Mzee Lowassa , wewe ni 'Super man'," alisema Rais Magufuli.

"Maendeleo hayana chama, ndiyo maana Mzee Lowassa yupo hapa, nikushukuru kwa utulivu wako nilipokutupa chini baada ya uchaguzi ulikaa kimya, maana tuligombea mimi na wewe lakini wengine wanapiga kelele tu, kwakweli nikupongeze kwa uzalendo," aliongeza.

Tukio hilo lilikuwa ni la pili kwa Rais Magufuli kukutana na Mgombea huyo wa Urais mwaka 2015 kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ambapo Januari mwaka huu viongozi hao walikutana Ikulu Jijini Dar es salaam, na Rais Magufuli alimpongeza Lowassa juu ya uvumilivu wake kwenye siasa.

Desemba 02 mwaka huu akiwa ziarani Jijini Arusha, Rais Magufuli alitaja sura ya pili ya Edward Lowassa baada ya kupokea malalamiko ya maji, kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga.

"Kalanga, Mbunge wa Monduli aliwahi kuniomba maji akiwa CHADEMA, lakini amesahau kuwa Lowassa amewahi kuwa Waziri wa Maji, simsemi mzee wangu namaanisha kuwa uzalendo unaanzia nyumbani, nikupongeze Kalanga kwa ujasiri wako wa kurudi huku, maji utapata," alisema Rais Magufuli.

Mbali na sura mbili za Lowassa kwa Rais Magufuli, lakini kiongozi huyo amekuwa akisifiwa mara kwa mara na baadhi ya viongozi wa serikali na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Katibu Mkuu CCM, Dkt Bashiru Ally kwa siasa zake.

Huna Sababu Ya Kuaibika tena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0620510598  / 0743543944

Tigo Fiesta kufanyika tena Dar Kabla mwaka huu Haujaisha

$
0
0
Uongozi wa Clouds Media Group, umetangaza kuwa tamasha la Fiesta ambalo liliahirishwa kufanyika Dar Es Salaam mwishoni mwa mwezi Oktoba, litarudiwa tena mwezi huu.

Taarifa hizo za kurudiwa kwa tamasha hilo, zimethibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga kupitia kipindi cha Clouds 360.

Novemba 24, 2018 manispaa ya Kinondoni ilieleza kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa walio karibu na eneo la Leaders Club lilipopangwa kufanyika Fiesta, kuwataka waandaaji kulihamishia tamasha hilo viwanja vya Tanganyika Peakers.

Baada ya uamuzi huo wa manispaa, waandaaji wa tamasha hilo walitangaza kuwa halitafanyika tena.

“Wakati mwingine matatizo huibua fursa kubwa na bora zaidi. Tamasha lijalo litakuwa kubwa kuliko lile la awali, wale ambao walikuja kutoka mikoani kwa ajili ya kuhudhuria shoo hiyo tutaangalia namna ya kuwapunguzia machungu kwenye tamasha hilo,” amesema Kusaga.

Amesema kutokana na kutofanyika kwa tamasha hilo amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuangalia namna bora ya kulifanya tamasha hilo.

Bulaya kuwasilisha muswada binafsi bungeni kuhusu vikokotoo vya mafao

$
0
0
Mbunge wa Bunda Mjini, Eser Bulaya (Chadema), amesema anakusudia kuwasilisha muswada binafsi bungeni kupinga matumizi ya vikokotoo vya pensheni kwa madai kuwa vinamnyonya mfanyakazi.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 4, Bulaya amemtaka waziri husika kujitokeza na kusema kwanini mchakato wa uandaaji vikokotoo hivyo haukuzingatia ushirikishwaji wa wadau.

“Kwanini kumekuwa na malalamiko mengi… waache kutoa majibu mepesi kwenye hoja nzito. Mimi nikishikilia jambo huwa lina ukweli na nilikaa muda mrefu sijaongea nikifanya utafiti wa kina,” amesema Bulaya.

Kuhusu pongezi za Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema zimemuongezea nguvu ya kulishughulikia suala hilo.

“Pongezi za Spika nimezipokea na zimeniongezea kasi ya kukomaa na suala hili hadi dakika ya mwisho… na kufukuzwa bungeni nimezoea,” amesema Bulaya.

Kusaga Azungumzia Taarifa za Kumiliki Wasafi TV na Wasafi FM

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amejibu tetesi zinasombaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kumiliki vituo viwili vya runinga na radio, Wasafi TV na Wasafi FM.
 
Akizungumza katika Kipindi cha Clouds 360, Kusaga amesema;  “Namiliki Redio zote za vijana kwa namna moja au nyingine. Naamini kwenye ushirika na hivyo kuna biashara nyingi pamoja na Redio nitaendelea kuzianzisha kwa kushirikiana na vijana kwa sababu hilo lilikuwa lengo la Clouds tangu zamani”

Kusaga amesema kuwa anashirikiana na radio nyingine za mikoani kama Safari FM ya Mtwara na Jembe FM ya Mwanza

Pia Kusaga amesema ; “Utake usitake bila Clouds hakuna Staa yeyote angetokea, hata watukane waseme nini ila bila Clouds wasingekuwa walipokuwa”

Kabla ya kutoa tamko hilo, kulikuwa na maneno kuwa Kusaga ndiye mmiliki wa vituo vya Wasafi TV na Wasafi FM.

Wizara Ya Fedha Na Mipango Yaanza Ujenzi Wa Ofisi Zake Za Kudumu Kwenye Mji Wa Serikali Ihumwa-dodoma

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amelitaka Shirika la Nyumba na Taifa, NHC, lililopewa kandarasi ya kujenga ofisi za Hazina katika eneo la Mji wa Serikali-Ihumwa mkoani Dodoma, kuhakikisha kuwa inajenga ofisi hizo kwa umakini, umahiri na viwango vya ubora wa vya juu vinavyokwenda sambamba na hadhi ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Dkt. Kijaji ametoa rai hiyo kwa uongozi wa Kampuni ya Ujenzi ya Shirika la Nyumba Tanzania-NHC, baada ya kutembelea eneo zitakapojengwa Ofisi za kudumu za Wizara hiyo katika mji huo wa Serikali ambapo jengo la kwanza litakalo gharimu shilingi bilioni moja, linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2018.

Aidha, Dkt. Kijaji ameielekeza NHC kuhakikisha kuwa inajenga jengo kubwa la Wizara kwa kuzingatia teknolojia inayo hifadhi mazingira ikiwemo kuweka miundombinu ya kuwezesha kupatikana kwa nishati mbadala ya umeme katika jengo hilo.

Waziri Mkuu Atembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Kutoa Maagizo

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimalize urasimu ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kadhalika, ameuagiza uongozi wa TIC uweke kipaumbele cha kwanza katika kulinda rasilimali za nchi na maliasili zake ikiwemo ardhi, mazao ya uvuvi, misitu, madini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jioni (Jumanne, Desemba 4, 2018) alipozungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa TIC na Menejimenti, jijini Dar es Salaam.

“Katika kuvutia wawekezaji hasa wa nje ni lazima tuweke kipaumbe katika kulinda rasilimali zetu kama ardhi, madini fukwe ili zisiporwe kwa kisingizio cha uwekezaji.”

Amesema eneo hilo linahitaji umakini na uadilifu mkubwa, hivyo ni muhimu kwa kituo hicho kuhakikisha kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

Amesema ili kupata matokeo mazuri ni lazima waimarishe mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.

“Serikali imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025, TIC inatakiwa iongoze kwa kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa wawekezaji ambao TIC inatakiwa ivutie ni walio mahiri wenye nia thabiti ya kutufikisha huko na siyo wachuuzi au madalali.

Kadhalika,Waziri Mkuu amesema Serikali  ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka TIC iwe kioo cha nchi ambacho kitavutia wawekezaji.

Amesema Serikali inataka TIC mpya ambayo itakuwa kimbilio la wawekezaji wengi wa ndani na nje, badala ya kuwa kikwazo na kusababisha wawekezaji wakija kukimbilia.

Hivyo, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa kituo hicho ubadilishe muundo wa kuwapokea wawekezaji, wawapokee vizuri na wawaeleze fursa za uwekezaji zilizopo.

“ Pia, TIC iweke mazingira rafiki ya kuwawezesha Watanzania wengi kumiliki uchumi kwa kuanzisha miradi mipya wao wenyewe au miradi ya ubia kati ya wawekezaji.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma ni lazima afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu, uadilifu, weledi, uaminifu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

Waziri Mkuu amesema ni lazima wahakikishe vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma vinaepukwa na kila mtumishi.” Serikali haivumii watumishi wa aina hiyo.”

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe amemuomba Waziri Mkuu awasaidie kwa kuwapatia ofisi kwa kuwa eneo wanalofanyia kazi kwa sasa halitoshi.

Pia amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa rasilimali watu, sasa wanahitaji watumishi 31 wakiwemo mameneja 11.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea eneo la kutolea huduma za pamoja zilizopo ndani ya Kituo hicho cha Uwekezaji Tanzania na kusema kwamba ameridhishwa na utendaji.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri wa Kilimo Amuagiza Katibu Mkuu Wizara Ya Kilimo Kumsimamisha Kazi Mtumishi Mmoja Kwenye Timu Ya Opareshini Korosho

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe kumsimamisha kazi mtumishi George Mboje na kumuondoa kwenye timu ya Operesheni Korosho.

Pamoja na kumundoa kwenye timu hiyo pia Katibu Mkuu ametakiwa kumuondoa kwenye Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko.

"Katibu Mkuu, nataka umuondoe huyu George kwenye hii timu na pia sitaki kumuona kwenye Bodi na Taasisi yoyote katika Wizara ya Kilimo" Alisisitiza Mhe Hasunga awali wakati akizungumza

Mhe Hasunga ametoa agizo hilo leo tarehe 4 Disemba 2018 wakati akizungumza  kwenye kikao kazi cha Watendaji wa timu ya Oparesheni korosho kilichofanyika katika ukumbi wa CBT Mkoani Lindi na wakati wa kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018.

George Mboja ambaye yupo kwenye timu ya Oparesheni Korosho akiwakilisha Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko anatuhumiwa kwa Utovu wa nidhamu sambamba na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wa Oparesheni Korosho inayoendelea nchini.

Aidha, Waziri Hasunga amewahakikishia watendaji hao kuwa serikali ina fedha za kutosha kuwalipa wakulima wa Korosho lakini lazima wakulima wote wahakikiwe ili kujiridhisha kwamba anayelipwa ni mkulima wa mwisho na sio wafanyabiashara maarufu kama Kangomba.

Akizungumzia hatua iliyofikiwa na serikali kuhusu malipo ya wakulima wa korosho, alisema hadi kufikia Jana tarehe 3 Disemba 2018 uhakiki ulikwishafanyika kwenye vyama 220 kati ya vyama 504 vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara, Lindi na Ruvuma na kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na Korosho nchini.

Alisema kati ya vyama hivyo vilivyokwisha hakikiwa ni vyama 181 ndivyo ambavyo tayari vimelipwa fedha zao huku Bilioni 41.8 zikiwa zimelipwa.

Aliongeza kuwa wakati zoezi hilo linaanza serikali ilikuwa inalipa Bilioni Moja kwa siku lakini kwa sasa utaratibu uliowekwa ni kulipa kati ya Bilioni 5 mpaka 10 kwa siku.

Katika taarifa yake Waziri Hasunga amesema kuwa jumla ya wakulima 40,208 wamekwishalipwa fedha zao.

Mhe Hasunga aliongeza kuwa serikali imeamua kuwalipa wabebaji na wapakiaji wa mizigo kwenye maghala sambamba na kuanza kuwalipa malipo ya awali wasafirishaji kutoka kwenye vyama vya msingi kwenda kwenye vyama vikuu.

Kuhusu swala la magunia Waziri Hasunga alisema kuwa serikali imeamua kuyalipa magunia yote ili kurahisisha uhifadhi wa Korosho.

MWISHO.

Uteuzi Mpya Uliofanywa Leo na Rais Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jaji Mstaafu Steven Bwana kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha miaka 3.

Pamoja na kumteua Mwenyekiti wa Tume, Rais Magufuli amewateua Makamishna 5 wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Walioteuliwa ni George D. Yambesi, Balozi Mstaafu John Michael Haule, Immaculate P. Ngwale, Yahaya F. Mbila, Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay.

Uteuzi huu wa Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma umeanza tarehe 22 Novemba, 2018.

Katibu Mkuu CCM Dk Bashiru Ally Akana Kumjibu Bernard Membe Mitandaoni

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,  Dk Bashiru Ally amelikana andiko  linalosambaa mtandaoni likionyesha kuwa amemjibu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Dk Bashiru amesema andiko hilo si lake na hayupo katika mfumo wowote unaomuwezesha kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii zaidi ya kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno.

Sehemu ya andiko hilo linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii linasema, “Zipo taarifa kwamba yupo kiongozi mmoja aliyewahi kuwa mwandamizi wa Taifa hili eti kanikosoa kuhusu utaratibu niliotumia kumwita ndugu Membe, mimi niombe hawa wastaafu watulie ili tukiweke chama sawa.”

“Na nirudie tu kusema ndugu Membe kama atakuwa hajafika ofisini kabla ya tarehe 17 na 18, 2018 nitakiomba kikao cha kamati kuu ya NEC kimwazimie.”

Dk Bashiru amesema waliofanya hivyo ni wale waliozoea kuendesha nchi kiholela na bado watazua mengi.

 “Watu wanaonijua wanafahamu jinsi ninavyotumia simu, sipo huko na  sina Instagram, Twitter, WhatsApp, Facebook wala mfumo wa barua pepe kwenye simu yangu, ni wazushi hao puuzeni hizo habari, ”amesisitiza.

==>> Hili ndo andiko linalosambaa mitandaoni

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Disemba 5

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Shirika la Nyumbu na Kamishna wa Fedha na Utawala wa Zimamoto

$
0
0
Uteuzi wa Mwenyekiti wa Shirika la Nyumbu na Kamishna wa Fedha na Utawala wa Zimamoto

Kisima Cha Gesi Mtwara Hatarini Kumezwa na Bahari

$
0
0
Kutokana na kina cha bahari ya Hindi katika eneo la Mnazi Bay Msimbati mkoani Mtwara kuendelea kumomonyoka siku hadi siku kuelekea nchi kavu,  huenda nchi ikajikuta gizani kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Hayo yamesemwa jana Jumatatu Desemba 4, 2018 na Naibu mkurugenzi wa Kampuni ya Maurel & Prom Tanzania inayohusika na kuchimba gesi, Elias Kilembe kwa Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alipotembelea visima hivyo vya  gesi.

Kilembe alisema  siku hadi siku bahari inasogea nchi kavu kuelekea kilipo moja ya kisima cha gesi na mitambo hali inayowapa wasiwasi.

“Hata mwaka jana ulitokea mmomonyoko lakini haukuwa tishio kama wa mwaka 2015, lakini ukija hapa baharini unakuta mchanga umeondoka wote na kupotea, kweli ni tishio kwa kambi hii,” alisema Kilembe.

Waziri wa nishati, Dk Kalemani amesema hali halisi inaonekana na hakuna haja ya utafiti, bali kinachotakiwa kufanyika ni kujengwa kwa ukuta haraka ambao utatenganisha kisima  kilipo na bahari ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

“Kuanzia sasa anzeni kufanya utaratibu wa kujenga ukuta kwa sababu mtafika mahala mtakosa hata pa kuweka ukuta maji yakishafika huku, ni vizuri kuanza sasa ili msije kukumbwa na dhoruba kubwa, haya ni maagizo ya haraka haraka wala si jambo la kufanya utafiti,” amesema Dk Kalemani.

Harmonize Aweka Wazi Mahusiano Yake Na Jackline Wolper

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Harmonize amefunguka kuhusu yeye na Jackline  Wolper. Muimbaji huyo ameiambia Wasafi TV kuwa kwa sasa wao ni marafiki tu wa kawaida.

'Nikimtaja Wolper au nikimpandisha kwenye jukwaa ni Malkia wangu," amesema Harmonize.

Utakumbuka mapenzi ya wawili hao yalivunjika na Harmonize kuwa mapenzini na mrembo Sarah, licha ya kuachana mara kadhaa walijikuta wakirushiana maneno mtandaoni. 

Kwa sasa wameanza kuonekana pamoja tena kwenye show za Wasafi Festival.

Msikilize hapo chini

Video Mpya: Sister Fay Ft Hollystar – Wasinichapie

$
0
0
Video Mpya ya Sister Fay Ft Hollystar – Wasinichapie . Itazame hapa

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Disemba 4

Waziri Mkuchika Akerwa na Wakuu wa Mikoa, Wilaya Wanaowaeka Watu Rumande Bila Sababu za Msingi

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Kapteni mstaafu George Mkuchika, amewashangaa wakuu wa mikoa na wilaya wanaoweka watu ndani saa 48 na kusema katika kipindi chake cha miaka 22 alichokuwa mkuu wa mkoa na wilaya hajawahi kumweka mtu ndani.
 
Aidha, alisema anajivunia kuwa Mtanzania aliyeteuliwa na marais watano nchini kushika nyadhifa mbalimbali ikiwamo za ukuu wa mkoa na wilaya.

Mkuchika alitoa kauli hiyo jana kwenye mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanzania Bara yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi, jijini hapa.

Akielezea jinsi alivyoteuliwa katika vipindi vya marais watano, alisema hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere, alimteua kuwa mkuu wa wilaya akiwa na umri wa miaka 35, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, alimteua kuwa mkuu wa wilaya na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alimteua kuwa mkuu wa mkoa.

"Rais mstaafu Jakaya Kikwete yeye alinipa uwaziri, Rais John Magufuli amenipa uwaziri sasa namngoja Rais wa awamu ya sita," alisema.

Aliongeza: "Mimi naitwa Waziri wa Utawala Bora sina mipaka, wewe mkuu wa wilaya umepewa mamlaka ya kumweka mtu saa 24 au 48, napiga simu kwa bosi wako kwa kuwa umetumia madaraka yako vibaya akikupeleka mahakamani unashtakiwa."

Alisema serikali inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, hakuna mtu anayeweza kuendesha bila kujua hizo sheria zinasemaje.

Alisema baada ya wakuu wa wilaya kupata mafunzo, figisu figisu za kuweka watu ndani zimepungua.

"Mimi nimekuwa DC (Mkuu wa Wilaya) miaka 14, nimekuwa mkuu wa mkoa miaka minane, sijawahi kuweka mtu ndani hata siku moja."

"Sheria inasema unamuweka mtu ndani kwa usalama wake kama ameua, ndugu wa marehemu wanataka kulipiza kisasi unaenda kumficha ndani, sasa mtu kachelewa kwenye mkutano wa DC au RC unamuweka ndani wakati zipo taratibu za kushughulika naye," alihoji.

Alisisitiza serikali kuendeshwa kwa kutumia sheria, taratibu na kanuni.

"Nataka kusisitiza muendesha serikali kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni," alisema.

Aidha, alisema waziri kufunga safari bila kutoa taarifa kwa mkuu wa mkoa mahali anapokwenda ni kosa.

"Ningekuwa mimi mkuu wa mkoa ningepeleka polisi kwenda kublock kwa kuwa mimi sina taarifa na ugeni huu, lakini na mimi nimefanya hiyo kazi kuna wengine wagumu, taratibu za kiserikali zinataka waziri unapokwenda kutembelea kwenye mkoa unatuma taarifa," alisema.

Jinsi Ya Kuandaa Na Kutayarisha Lishe Maalumu Ya Kuongeza Na Lunenepesha Mwili

$
0
0
LISHE hii ni maalumu kwa watu walio Linda na kudhoofika kwa sababu ya kuugua matatizo mbalimbali ya kiafya .

Pia inawasaidia na wale walio konda kwa sababu ya msongo wa mawazo.

MAHITAJI
1. Dawa LISHE ya kunenepesha mwili ( Hii ni dawa ya asili ambayo kazi yake ni KUONGEZA na kunenepesha mwili ulio dhoofika kwa kuugua.

2. Karoti 2
3 . Pilipili mbuzi 2
4. Chumvi kijiko kidogo kimoja.
5. Ndimu fresh moja.
6. Nanasi robo  kilo
7. Njegere robo kilo.
8. Kunde mbichi robo  kilo.
9. Papai bichi 1.
10. Embe kubwa moja
11. Parachichi moja.

MATAYARISHO NA MATUMIZI.
1. Chukua vijiko vidogo viwili vya dawa LISHE kisha changanya  kwenye kikombe chenye maji ya moto au vugu vugu  koroga na unywe. Utafanya hivyo Mara mbili kwa siku asubuhi jioni kwa muda wa siku thelathini.

2. Chukua vitu vyote vilivyo orodheshwa hapo juu yani karoti, ndizi mbivu, chumvi,ndimu,nanasi,njegere,kunde mbichi,papai bichi,karanga,embe na parachichi kisha visage  kwenye blends kupata juisi yake.

MATUMIZI: Utakuwa unatumia kunywa glasi moja asubuhi na glasi nyingine utakuwa unatumia kunywa usiku.

Utakuwa unaweka interval ya dakika tano tangu unywe dawa LISHE yani ukisha kunywa dawa LISHE unakaa dakika tano kisha unakunywa juisi yako.

Unaweza KUONGEZA vipimo vyako kwa kutengeneza kiasi cha juisi ambayo unaweza kutumia kwa muda wiki nzima ili usisumbuke kutengeneza kila siku na utakuwa unahifadhi juisi yako kwenye friji.

Hii ni Tiba sahihi kabisa kwa MTU ambae amekonda na anataka kurejesha afya yake.

KUPATA DAWA LISHE YAKO FIKA KATIKA DUKA KA KUUZA DAWA ZA ASILI LA NEEMA HERBALIST. TUNAPATIKANA UBUNGO  JIJINI DAR ES SALAAM JIRANI NA SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING NYUMA YA JENGO LA UBUNGO PLAZA.

WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0693 005 189
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images