Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Miili ya askari Watatu wa JWTZ waliofariki dunia wakilinda amani yaagwa

$
0
0
Askari watatu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia wakati wakiwa kwenye operesheni za amani za Umoja wa Mataifa (UN) wameagwa leo Lugalo huku vilio na hali ya kuzimia ni baadhi ya mambo yaliyotawala wakati waombolezaji walipoishuhudia miili ya wapendwa wao.

Askari hao waliuawa wakiwa kwenye majukumu ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)  ni Praiveti Mussa Shija Machibya na Koplo Mohammed Mussa  wakati  Koplo Erick Masauri John alipoteza maisha akiwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Askari wote waliuawa baada ya kushambuliwa na vikosi vya waasi vinavyoendesha mapigano katika maeneo ya msituni.

Shughuli za kuagwa askari hao zimefanyika katika viwanja vya hospitali ya Lugalo na kuhudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussen Mwinyi, vikosi vya ulinzi na usalama na ndugu na jamaa.

Waziri Mwinyi ndiye aliyeanza kutoa heshima za mwisho na baadaye kufuatiwa na maofisa wa jeshi kabla ya ndugu kumalizia.

Wakati wakitoa heshima zao baadhi ya ndugu walionekana kuzidiwa kiasi cha wengine kuzimia hali iliyofanya watoa huduma ya kwanza kuwasaidia.

Miili ya askari hao iliyowasili jana imesafirishwa katika mikoa ya Mara, Mwanza na Zanzibar ambako itazikwa.

Tanzania Tunazidi Kuchanja Mbuga: Tazama Hapa Ndege Yetu Mpya Ambayo Kwa Afrika Sisi Ndo Wakwanza Kuitumia

$
0
0
Rais Magufuli  aliahidi kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania kukidhi safari za ndani na pia kupata Watalii wengi kwa Nchi kuwa na Ndege zinazofanya safari zake moja kwa moja kutoka mataifa mengine.

Alinunua Bombadier kisha akanunua nyingine kubwa ya Dreamliner na sasa kachukua nyingine ambapo kampuni ya kutengeneza Ndege ya Canada ya Airbus imeitambulisha Ndege hiyo mpya ambayo ni A220.

Kampuni hiyo ya Airbus imesema Ndege hiyo inaelezwa kuwa ndio itakuwa Ndege ya kwanza ya aina hiyo kufanyia safari zake kwenye Bara la Afrika.

Rudisha Heshima ya Ndoa Yako.....Pata Tiba Bora ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Wanaume wengi hawawaridhishi wake au wapenzi wao kwa kutokuwa na nguvu za kiume au uume mdogo? 

Kawaida mwanamke huwa anachukua dakika saba 7 adi kumi 10 ili aweze kufika kileleni na wakati wanaume wengi kwa sasa hutumia dakika tatu 3 hadi tano 5 ameshafika kileleni , hapo utagundua kabisa mke au mpenzi wako hujamtendea haki yake. Dr Nyalobi  anakuletea dawa imara na yenye nguvu tatu?

Simpo power; Hutibu matatizo yafatayo;

1.itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-20 kwa tendo la kwanza

 2. itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi mara nne 

3 Huimalisha misuli iliyolegea na kusinyaa 

4 Hutoa uchovu pale umalizapo kufanya tendo

 Je kwa nini uzidi kuona aibu pale ukutanapo na mpenzi wako kwa sabubu uume wako mdogo na mwembamba? 

Promix; hii ni dawa ya kuongeza uume saizi upendayo.Dawa zetu ni za mitishamba na hazina madhara yoyote na ni tofauti na ulizowai kutumia ata wazee hutumia 

Mkuya; hii ni dawa ya kisukari dozi siku 21 

Mwaru; hii ni dawa ya uzazi hufungua mirija ya uzazi ata kama uzazi umefungwa

Markusi; ni dawa ya presha zipo dwa za korodani kuvimba,, vindonda vya tumbo, kupunguza kitambi, na minyama uzembe 

Fika ofisini kwetu Buguruni Malapa na Mwanza yupo wakala wetu au piga simu 0752348593 -Dokta Nyalobi

Upelelezi Kesi Ya Mfanyabiashara Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Dakika Bado Haujakamilika

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa  kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara, Mohamed Mustafa Yusufali aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika pamoja na wenzake wanne.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Novemba 23, 2018  na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa Serikali, Tulia Holela  kueleza kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya  kutajwa.

“Kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika naomba mahakama kuipangia kesi tarehe nyingine ya kutajwa,” amesema Holela.

Baada ya kusikiliza hoja hizo Hakimu Shaidi ameutaka upande wa mashtaka kufanya bidii katika jambo hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 7, 2018.

Mbali na Yusufali ambaye anakabiliwa na mashtaka 198 peke yake,  washtakiwa wengine wanaokabiliwa na shtaka moja la utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni ni Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif.

Hapana Kuteseka Tena ....... Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume Na Kurudisha Mali Zako Pamoja Na Magonjwa Sugu Yaliyoshindikana

$
0
0
Ninauwezo wa kumrudisha mume, mke, mchumba, hawara au unaempenda kwa mda mfupi sana na kumfunga asiwe na mtu mwingine zaidi yako na kumfanya akutimizie kirakitu unachokihitaji kutoka kwake hata km yuko mbali na atatulia kabisa.

GALIMBO 3 POWER; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa utabibu na uimara wa hali ya juu sana kwa afya ya binadam, Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimarisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bira ham kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwamda wa dk (18- 35 ) kwa tendo moja.

SUNU EXTRA :- hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa inch (6-7) no unene wa sm (3-4) .  
Yote hayo yanasababishwa na ngili busha, kisukali ,kaswende, punyeto, presha,  korodani moja kuvimba ama kuingia ndani, tumbo kuunguluma na kujaa ges,  vidonda vya tumbo nk .

SUPER MORISISI :- nidawa bora inayoponesha tatizo la kisukali na kuifanya afya yako iwe imara hatakama sukaliyako imekusumbua kwa mda mrefu inatibika

Pia ninadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyama uzembe ) matiti makubwa kuwa madogo, makovu mwilini, kuzuia mimba kuhalibika, uzazi kwa akina mama na akina baba, kusafisha nyota, kuzuia majini wachafu, pesa nyingi (utajili)  kurudisha mali iliyo potea au kuibiwa, kuuzavitu bila kununuliwa, vilevile ninadawa za biashara kwa wafanya biashara, wachimba madini, kushinda kesi, kurudishwa kazini, kupandishwa cheo nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR MALUPA SM.     0653182109    /0744391089 

Kwawale walioko mikoani hudumahii inakufikia popote ulipo

Wafanyabiashara Wa Uturuki Waonesha Nia Ya Kuwekeza Katika Kiwanda Cha Nguo Simiyu

$
0
0
 Na Stella Kalinga, Simiyu
Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki wameonesha nia na dhamira ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza nguo mkoani Simiyu ambacho kitakuwa na uwezo wa kuajiri watu zaidi ya 4000.

 Hayo yamebainishwa katika kikao kati ya Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo ambaye aliambatana na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara wa Uturuki kutoka makampuni saba ya nchi hiyo, katika kikao maalum na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali na jumuiya ya wafanyabiashara ya mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.

Balozi Kiondo amesema Wafanyabiashara hao wanayo azma ya kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza nguo katika mnyororo mzima wa utengenezaji kutoka bidhaa ya awali ya pamba mpaka bidhaa ya mwisho kabisa, ambayo ni nguo kwa ubia(partineship) na Watanzania.

Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS amesema  mpaka sasa ni makampuni sita kutoka nchini humo yameonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha nguo mkoani Simiyu na akaahidi kwenda kuwashawishi wafanyabiashara wenzake hivyo watakaporudi kwa mara nyingine  makapuni mengi yatakuja kuwekeza katika viwanda vya nguo.

“Nikirudi nyumbani kama kiongozi wa wafanyabiashara nitawashawishi wengine pia waje wawekeze katika viwanda vya nguo,ombi langu kwenu ni kwamba ninahitaji Mfanyabiashara Mtanzania ambaye tutashirikiana naye katika uwekezaji huu(partinership), lakini niwahakikishie tu kuwa katika kiwanda tutakachojenga mashine na vifaa vyote vipo tayari kule Uturuki” alisema  Cengiz.

 Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia wafanyabiashara hao upatikanaji wa soko la uhakika la nguo zitakazotengenezwa, pamoja na upatikanaji wa malighafi kwa kuwa Simiyu ndiyo mkoa unaozalisha zaidi ya asilimia 55 ya pamba yote nchini, ambapo kwa  mwaka 2018 Simiyu imezalisha takribani kilo milioni 131.

Ameongeza kuwa pamoja na uhakika wa soko na malighafi  Simiyu ina viwanda vingi  vya kuchambua pamba, ardhi itatolewa bure, miundombinu muhimu yote ipo, utashi wa kisiasa kwa viongozi wa wilaya upo, hivyo akawatoa hofu wawekezaji hao na kuwaeleza kuwa mkoa utashirikiana nao, huku akiomba waone uwezekano wa kuwekeza katika uongezaji thamani wa mazao ya mifugo kama ngozi na nyama

Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola amesema wako tayari kushirikiana na mwekezaji huyo, huku akibainisha kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho kitawasaidia wanaochambua pamba na wakulima kupata faida ikilinganishwa na sasa ambapo zaidi ya asilimia 75 ya pamba inasafirishwa nje ya nchi.

Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Mhe. Najlu Silanga ameahidi ushirikiano kwa wawekezaji aho kutoka Uturuki na kuiomba Wizara ya Viwanda, Baiashara na Uwekezaji kuzitambu na kusughuliakia changamoto mbalimbali za wafanyabiashara hapa nchini .

Wakati huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda  (TIRDO) Prof. Mkumbukwa Mtambo amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuzingatia Utafiti na maendeleo katika Viwanda, huku akisisitiza kuwa ili viwanda vinavyoanzishwa viweze kuwa endelevu ipo haja ya kufanya utafiti na maendeleo na akaahidi kuwa Taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Simiyu katika tafiti mbalimbali  za  maendeleo ya viwanda.

Waziri Apiga Marufuku Kununua Vifaa Vya Ujenzi Nje Ya Nchio

$
0
0
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jafo amepiga marufuku kununua vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi kwaajili ya ujenzi wa hospitali za ndani kwa kile alichokidai kufanya hivyo ni kuvihujumu viwanda vya ndani.
 
Waziri Jafo ametoa maagizo hayo akiwa wilayani Kilolo mkoani Iringa wakati akikagua ujenzi wa Hosiptali ya Wilaya hiyo ambapo alibaini kuwepo kwa baadhi ya vifaa vianvyoagizwa kutoka Hispania jambo linaloenda kinyume na adhma ya serikali katika kuendeleza viwanda vya ndani.

“Nimetoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa yote Tanzania tena kwa barua wanunue vifaa vyote vya ujenzi wa hospitali vitoke hapa nchini ni marufuku kununua vifaa kutoka nje, kama TBS wamethibtisha kuwa vina ubora.”

Katika hatua nyingine Waziri Jafo ametoa siku nane kwa mkandarasi anayefanya Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Kidabaga wilayani humo kuhakikisha anakamilisha ukarabati huo huku akiwataka watumishi kufanya kazi kwa weledi ili wananchi waweza kupata huduma bora za afya.

Zaidi ya wananchi laki mbili wanatarajiwa kunufaika na ujenzi huo wa hospitali kutokana na adha waliyoipata kwa muda mrefu ambapo walilazimika kutembea zaidi ya kilometa 100 kufuata huduma za afya katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

Jeshi la Polsi Dar Lapiga Marufuku Maandamano Yasio na Vibali

$
0
0
Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano yasiyokuwa na vibali badala yake wamezitaka taasisi au watu ambao watahitaji kufanya hivyo kuomba kibali maalum kwa ajili ya kupatiwa ulinzi pindi watakapohitaji kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema ;“Jeshi la polisi linatoa onyo kwa wanaodamana bila kibali ikiwemo wizara, idara za serikali, NG’O na taasisi zozote zilizosajiliwa kisheria kuacha kufanya maandamano bila kutoa taarifa ili jeshi la polisi liweze kutoa ulinzi.”

“Maandamano yanafanywa bila jeshi la polisi kuambiwa, yanawanyima haki ya msingi watumiaji wengine wa barabara wa taifa, si hilo tu pia wale wanaofanya mashindano ya kukimbiza upepo  (marathoni) lazima watoe taarifa, na  yeyote atakayefanya maandamano bila kupewa ulinzi atazuiwa.”

Aidha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amebainisha polisi imewakamata watu watatu kwa makosa ya kukutwa na vipande vya meno ya tembo.

Watu hao walikamatwa eneo la Yombo Makangarawe wakiwa wameficha vipande hivyo kwenye mabegi mawili.

Waziri Mkuu Aagiza Vyoo Na Mifumo Ya Maji Viwandani Ikaguliwe....Asisitiza Vitakavyobainika Kuwa Na Makosa Hatua Kali Zichukuliwe

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ikishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira ifanye ukaguzi wa vyoo na mifumo ya kutiririsha maji katika viwanda vyote na vitakavyobainika na makosa hatua kali zichukuliwe.

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza maafisa afya na mazingira katika mikoa yote nchini badala ya kuzingatia maeneo ya hoteli, mabucha na migahawa waende kwa jamii na kutoa elimu ya matumizi ya vyoo bora pamoja na umuhimu wa usafi wa mazingira, hivyo watakuwa wameiepusha na maradhi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Novemba 23, 2018) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Usafi wa Mazingira Kitaifa na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa, Halmashauri na Wadau wa Afya Mazingira Tanzania, uliofanyika jijini Dodoma.

Amesema viwanda vina jukumu la kuhakikisha vinatunza afya za wafanyakazi wake kwa kufuata taratibu na sheria za afya kazini. “Ni jukumu la kila kiwanda kuhakikisha kwamba kinadhibiti uchafuzi wa hewa ili tuweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.”

Amesema kwamba hivi sasa, madhara ya mabadiliko ya tabianchi yameanza kushuhudiwa  nchini na endapo jitihada za makusudi zisipochukuliwa ipo hatari ya kufifisha matarajio ya kesho na kesho ya watoto.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mkuu ametoa rai kwa wakuu wote wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na maafisa watendaji wa kata, mitaa na vijiji nchini kwamba wasimamie vizuri na kwa ukaribu kampeni ya usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.

“Hakikisheni kuwa lengo la kila kaya nchini kupata choo bora kabla ya tarehe 31 Desemba, 2018 linafikiwa. Waziri mwenye dhamana, tambua kwamba baada ya tarehe husika kupita nitahitaji kupata taarifa kuhusu utekelezaji wa agizo hilo kutoka kwa kila mkoa na halmashauri nchini.”

Waziri Mkuu amesema ameelezwa kwamba, hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2018 kaya zenye vyoo bora zimefikia asilimia 51.4 kutoka asilimia 46.6 Julai, 2017 na katika kipindi hicho kaya zisizokuwa na vyoo kabisa imepungua kutoa asilimia 5.4 hadi asilimia 3.8.

Amesema iwapo watazidisha kasi katika utoaji wa elimu, usimamizi wa sheria na kuongeza ufuatiliaji, kaya zote zitakuwa na vyoo bora ndani ya muda mfupi ujao. “Nimedokezwa hapa kwamba, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika hilo. Sasa nitashangaa sana kwa nini wengine mshindwe?

Sambamba na suala hilo la ujenzi na matumizi ya vyoo bora katika kaya, pia Waziri Mkuu amesisitiza uwepo wa huduma za vyoo bora kwa taasisi zote za umma na binafsi. “Ninaagiza shule zote, vituo vyote vya tiba, vituo vya abiria, masoko na nyumba zote za ibada ziwe na miundombinu bora ya vyoo na sehemu za kunawa mikono.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amewagiza wakurugenzi wa halmashauri wahakikishe maeneo yote hayo yanakuwa na huduma hizo muhimu kabla ya tarehe 30 Aprili, 2019 ili itasaidia sana kuondokana na aibu ya kukosa miundombinu ya usafi katika taasisi zao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameonya jamii dhidi ya tabia ya ya kuchimba dawa wakati wa safari. “Tabia hii imeota mizizi, imekuwa kama ni desturi ya baadhi ya watu licha ya Serikali pamoja na sekta binafsi imeweza kuweka huduma za vyoo kwenye stendi za mabasi, vituo vya kuuzia mafuta, pamoja na hoteli zinazotumiwa na wasafiri.”

Amesema haiingii akilini kuona basi la abiria linasimama porini ili watu wajisaidie wakati muda mfupi uliopita basi hilo lilisimama kwenye kituo kikubwa cha abiria au sehemu zinazotoa huduma ya chakula.

“Katika kudhibiti hali hii ninaagiza Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani, SUMATRA na TABOA kuandaa mikakati ya kuondokana kabisa na tabia hii hatarishi kiafya. “

Waziri Mkuu amewaagiza maafisa afya mazingira kote nchini watekeleze wajibu wao kwa kuwachukulia hatua za kisheria madereva na makondakta wote watakaobainika kusimamisha magari porini kwa lengo la kuchimba dawa.

Katika mkutano huo halmashauri ya wilaya ya Njombe imeibuka kidedea kwenye kundi la utekelezaji wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira, ambapo imepewa zawadi ya gari aina ya ford ranger lenye thamani ya Dola za Marekani 35,700.

Mbali na halmashauri hiyo kuibuka mshindi na kupata zawadi ya gari jipya pamoja na tuzo, ndiyo Halmashauri pekee nchini ambayo kaya zake zote zina vyoo bora na kwamba hakuna kabisa tabia ya kujisaidia vichakani.

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa halmashauri nyingine nazo ziige mfano huo wa Njombe. “Ni dhahiri kuwa endapo halmashauri zote zitafikia hadhi ya Njombe tutaokoa fedha nyingi ambazo zinatumika kugharamia matibabu ya wagonjwa pamoja na kuokoa muda mwingi unaohitajika kwenye shughuli za uzalishaji ambao unapotea kila siku kwa kuuguza watu wanaopata magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya uchafu.”

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 36

$
0
0

ILIPOISHIA
Inadi ya wachezaji wanao nikaba kwa timu pinzani ikaongezeka, wakaanza kunikaba wachezaji wanne wanne jambo lililo nifanya nianze kuuona mchezo mgumu kwa upande wangu, kwani kila mpira ambao ninaletewa na wachezaji wezangu, siumiliki hata kwa sekunde nyingi wanakuwa wananipokonya. Kipindi cha kwanza kikaisha pasipo kufungana
“Pole mume wangu”
Camila alizungumza huku akitembea pembeni yangu.
“Ndio mpira mpenzi wangu”   
Nilizungumza huku tukiingia ndani ya chumba chetu. Kila mchezaji uso wake umetawaliwa na kuchoka, kwani mtandange huu ni wa kukata na shoka, yaani ni bora hata na mechi ya kwanza tulo cheza kwani tulifungwa na tulikuwa na hamasa ya kutafuta goli, ila mechi hii, karibia wachezaji wa timu pinzani wanakaba na wanaonekana hawana hata hamu ya kutafuta goli na itakuwa ni furaha yao wakiona tunagawana pointi.
                   
ENDELEA   
“Mumecheza vizuri. Ila wapinzani wetu hawajaweza kutupa nafasi ya kufunga. Munachotakiwa kufanya hivi sana ni kuhakikisha kwamba viungo wa katikati munapanda na nyinyi wafungaji, wakipanda viungo kwenda kushambulia nyinyi munarudi kuwa viongo”
 
Kocha alizungumza huku akitutazama.
“Ndio mfumo gani tena huo kocha?”
Mchezaji mmoja aliuliza huku akimtazama kocha usoni mwake.
“Ni ZigZag. Wapinzani wote macho yao yapo kwa Ethan na Pinto. Wanawafanya wanashindwa kumiliki mpira. Mawinga wa pembeni, hakikisheni sasa hivi nyinyi ndio munakuwa munaongoza jaramba za kufunga. Safu ya mabeki, nanyi hakikisheni kwamba hapiti mshambiliaji yoyote wa upinzani. Mumenielewa?”
 
“Tumekupata kocha”
Baada ya kumaliza kutibiwa majeraha madogo madogo yakiwemo kubwanwa na misuli, tukaanza kurudi uwanjani.
“Mume wangu leo umeshikika”
Camila alizungumza kwa sauti ya chini huku tukitembea kwa pamoja.
“Yaani wee acha tu, wanakaba kama nyuki. Tena mtazame yule mchezaji namba sita uwanjani. Yaani kama nimepokonya mwanamke. Yaani nikigusa mpira tu huyu hapa miguuni”
“Hahaaaa acha hizo mume wangu. Nenda kanifungie goli bwana nifurahie”
“Sawa mke wangu”
“Nitakunyima na leo pia”
 
Maneno ya Camila yakanifanya nitabasamu tu huku nikiingia uwanjani na yeye akielekea kwenye eneo la benchi la ufundi. Wachezaji wote tukakamilika uwanjani, refaa akaanzisha mpira, huku wachezaji wa timu zote mbili tukionyesha haya ya kuhitaji kufunga goli. Kama vile kocha alivyo tuelekeza ndivyo tulivyo anza kucheza na kuwachanganya wapinzani wetu ambao muda wote macho yao yalikuwa kwangu na Pinto. Kazi yetu ikawa ni kuwakusanya upande mmoja wapinzani wetu, kisha mipira tunawapasia Alex na Lukas. 
 
Ndani ya dakika kumi na tano za kwanza tukafanikiwa kupata goli la kuongoza ambalo amelifunga Lukasa, kwa kuunganisha pasi nzuri aliyo pewa na Rodguize kiungo wetu wa katikati. Furaha ikatawala uwanja mzima huku kila mtu akiwa amejawa na furaha kubwa sana.
“Wamachanganyikiwa, ni mwendo wa kuongeza kasi ya mashambulizi”
 
Niliwaambiwa wachezaji wezangu, huku tukiwa tumekusanyika duara moja, muda wa kushangilia. Tukatawanyika na mpira ukaanza tena, wapinzani wetu wakaanza kuelewa mfumo wetu, wakapunguza mazoea ya kutukaba mimi na Pinto na walicho kifanya ni kunza kujigawa mmoja mmoja kwa kila mchezaji wa timu yetu.
“Kampeni mchezo umebadilika tunafanyaje?”
Alex aliniuliza huku tukisubiria beki wetu apige mpira mbele.
“Turudini kwenye mfumo watu wa kawaida”
“Utasaidia?”
“Hatuna jinsi, hakikisha munalinda goli”
“Sawa”
 
Maagizo niliyo yatoa yakaanza kumfikia mchezaji mmoja baada ya mwengine, nikafanikiwa kupata mpira, nikautuliza chini, mchezaji ambaye leo amenikamia kuhakikisha sing’ari uwanjani, akanifwata kwa kasi, nikamtazama kwa macho yakumkazia, akajaribu kunyosha mguu ili kuuchukua mpira, nikauvuta mpira kwa nyum kidogo na kuufanya mguu wake upoteze muelekeo, nikaupitosha mpira katikati ya miguu yake, japo alijaribu kuibana ila akashindwa. 

Akajaribu kunipiga kikumbo nisimpite, ila nikamkwepa kisha nikaanza kukimbia na mpira pembezoni mwa chaki nyepe. Wakaongezeka na kuwa wachezaji wa nne huku wote wanaonekana kujawa na uchu wa kunipokonya mpira.
 
Nikaubana mpira katikati ya miguu yangu, nikaurusha juu kidogo na ukampita beki mmoja, nikauwahi kabla ya mchezaji mwengine kuuchukua, naye nikamfanya kama mwenzie. 

Nikatika kama ninaupiga mpura, ila nikausogeza kidogo pembeni na kumfanya beki mmoja kupitiliza huku akiserereka kana kwamba ameanguka na pikipiki. Nikaanza kuichezesha miguu yangu huku nikimtazama beki aliye salia, nikaukanyaga mpira na mguu wangu mmoja kisha nikazunguka nao na nikampita beki huyu akiwa amesimama pasipo hata kuthubutu kunyoosha mkono wake. Uwanja mzima ukafurika kwa shangwe, nikalitazama goli na kumuna kipa akiwa amesimama upande huu ninao tokea. 

Nikausogeza mpira kwa mbele kidogo kisha nikaachia shuti moja kali sana na kuufanya mpira uzunguke zunguke hewani, na ukaingia katika kona ya juu ya goli, japo kipa alijaribu kwa kadri awezavyo kuruka ili autoe ila akashindwa kabisa. Shangwe zikafumuka uwanja msimza. Nikaanza kukimbia kuelekea katika benchi la ufundi huku nikimyooshea Camila kidole. Nilipo mkaribia Camila akanikumabia kwa furaha huku kocha na wachezaji wengine wote nao wakinikumbatia.
“Kwa ajili yako mke wangu”
Nilizungumza kwa sauti huku nikiendelea kukumbatiwa. Camila akashindwa hata kuzungumza kitu na kubaki akimwagikwa na machozi tu.
 
Tukarudi unawanjani huku jina langu likiibwa na mashabiki wote. Mpira ukaanza tena huku wapinzani wetu wakiwa wamechanganyikiwa kabisa, kwani goli nililo lifunga hakika limeingia kwenye rekodi ya magoli bora katika michuano hii.
Hadi tunafika dakika ya mwisho, goli ni mbili bila. Tukaanza kuepeana mikono na wapinzai wetu, japo tumewafunga ila kwenye kundi letu wao ndio wanatufwatiwa nyuma tetu. Tukawaaga mashabiki wetu huku waandishi wa habari wakiwa makini katika kuniwinda ili kunihoji maswali mawili matatu. Nikaitwa na waandishi wa habari wawili na nikasimama katika eneo maalumu ya kuhojiwa huku nikiwa na Frendando.
 
“Kwanza hongereni sana kwa ushindi huu mzuri”
“Tunashukuru sana”
“Ethan unajisikiaje kufunga goli moja zuri sana ambali hakika hadi sasa hivi sijapata la kufananisha nalo?”
“Ahaa….ni furaha kwa kweli, unajua wapinzani wetu ni wazuri sana. Kipindi cha pili hawakunipa nafasi ya kufunga basi kipindi cha pili nikaapiza kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba ninafunga na kweli nimefunga. Ninamshukuru sana Mungu kwa hilo”
 
“Hongera sana hii ni zawadi ya goli bora kwa mechi ya leo”
Muandishi huyu alinipa kiboksi ambacho ndani kina kiatu kidogo cha dhahabu.
“Nashukuru sana”
“Frenando Alemedo, hongera sana kwa kuto ruhusu goli kuingia nyavuni kwako”
“Nashukuru”
“Nini siri yako ya kunyaka kila mkwaju ambao walikuwa wakiutuma wapinzani wako na isitoshe ndio umerudi kutoka kwenye majareha?”
“Kila kitu ni kijituma na mazoezi, nilijitahidi kuhakikisha kwamba ninakuwa kipa bora na basi nitakuwa kipa bora kwenye hii michuano”
“Hongera sana na wewe umepata zawadi yako ya mchezaji bora wa mechi kutoka SuperSport”
 
“Tunashukuru”
“Hata tutwatakie siku njema”
“Asanteni”
Tukaondoka katika eneo hili na nikamkuta Camila akinisubiria, akanipoke zawadi yangu niliyo pesa kisha akanipiga busu la mdomoni na kuwafanya wa wapiga picha kila mmoja kujitahidi kupiga picha kadri ya uwezo wake. Tukarudi katika vyumba vya kubadilishia nguo. Kila mmchezaji hakusita kunipongea kwa juhudi niliyo ionyesha.
“Unajua nini Ethan”
“Mmmm….”
Muna ule yule beki alivyo kwua akiserereka, nilifumba macho kwa kweki, kwa maana ile miguu laiti kama ingekupata basi sasa hivi tungekuwa tunazungumza mambo mengine kwa kweli”
 
“Yaa na nilijua tu kwamba akili zake zitaishia pale, unajua ameserereka hadi ameacha alama uwanjani, kang’oa kabisa nyasi”
“Hahaaaaa…..”
Furaha ikazidi kutawala ndani ya chumba chetu hichi. Tukavaa track suit zeu kisha tukaelekea eneo lilipo basi letu tukapanda na kuanza safari ya kurudi kambini.
“Mume wangu ona ona”
Camil alizungumza huku akionionyesha jinsi goli langu linavyo rudiwa kurushwa kwenye kituo cha SuperSport 3. Nikaendelea kujitazama kwenye simu hii ya Camila, hakika kitu nilicho kifanya kwa mabeki hawa kitaandika histori kubwa sana kwenye maisha yangu.
“Wanalifananisha goli langu na Ronaldinho yule wa Braziel”
Nilizungumza huku nikimuonyesha kocha matangazo haya ya moja kwamoja tunayo yatazama kupitia simu ya Camila.
“Duu, na wanasema kwamba ni zaidi ya goli lake”
Nilizungumza kwa furaha.
 
“Ni historia umeandika, sasa usivimbe kichwa. Hakikisha kwamba unazidi kuishangaza dunia kwa mambo mengine mengi sana.  Sawa”
“Sawa kocha”
Tukafanikiwa kufika hotelini salama salmin. Tukaingia kwenye vyumba vyetu. Mimi na Camila tukaanza kuoga kwa pamoja. Kutokana na hisia kali zilizopo kati yetu, tukashindwa kujizuia hisia zetu na kujikuta tukizama kwenye mahaba mazito ambayo kila mmoja alijitahidi kuhakikisha kwamba ana mridhisha mwenzake kwa kiwango cha juu. Tukamaliza mzunguko huu na tukajilza kwenye sinki hili la kuogea.
“Baby”       
“Mmmmm”
“Una mpango gani na maisha yako ya mpira ya baadae?”
“Nitainia kwenye timu yoyote kubwa ambayo itanihitaji”
“Kama?”
 
“Liverpool, Real Madrid”
“Unaipenda sana Liverpool?”
“Yaa nina ipenda, ila kama watanihitaji kwa dau kubwa basi nitakubali kuungana nao?”
“Inabidi unifanye niwe wakala wako”
“Haahaaa”
“Ndio mume wangu, kila kitu kiwe kwa ajili ya familia yetu. Lazima nikusimamie kwenye kila jambo zuri ambalo badae litatufanya tuishi maisha mazuri”
“Usijali mke wangu, nina imani kwamba kuna mawakala wengi watajitokeza. Mbaya sina msimamizi, baba alisha fariki na aliniacha katika wakati mgumu kiasi wa kusimamia kampuni zake. Kwa hiyo nahitaji mtu makini katika maisha yangu ya soka”
“Sawa mume wangu, kama utapenda utaniweka mimi?”
“Nitalifikiria hilo, il aje siku ukiwa mjamzito kweli utaweza kusafiria masafa ya mbali kuingia mikataba na timu kubwa kubwa?”
 
“Kwani mume wangu mimba nina ibeba mwaka mzima. Tutapanga mpango madhubuti na tena mume wangu, tufanye jambo juu ya hili sawa. Maliza masomo yako nami nimalize yangu kisha tutaendelea na biashara yetu ya mpira huu wa miguu”
“Sawa tuombe Mungu”
“Timu ambayo itataka kukunununua, ni lazima ikulipe paund dola laki tano mshabara wa wiki”
“Mmmm mke wangu, unataka nikawe mbuzi wa albadili huko kwenye timu za watu?”
“Kwa nini?”
“Msaada wangu kwenye timu ni lazima uwe mkubwa kutokana kile wanacho nilipa”
“Mungu atakujalia Mume wangu”
“Kweli na utafanikiwa tu mume wangu”
“Haya”
 
Tukamaliza kuoga, tuvaa nguo za kushindia kwa usiku huu. Tukajumuika na wachezaji wezangu katika kupata chakula cha usiku. Tukiwa katika eneo hili tukaanza kuwaona walinzi wa baba Camila wakiingizana humu ndani jambo lililo tufanya watu wote humu kupatwa na mshangao. Tukawaona wazazi wa Camila ambao kwa kipindi hichi ni maarufu sana hapa Ujerumani, hii ni kutokana na nafasi ya kiti cha uraisi anacho kigombania baba yake.
Mimi na Camila tukanyanyuka na kuwakaribisha kwa furaha sana.
“Tumewafanyia suprize”   
Baba Camila alizungumza huku akinisalimia kwa kunipa mkono.

“Tunashukuru sana, karibuni sana wazazi wetu”
“Asanteni”
Tukakaa nao katika meza tuliyo kuwa tumeketi.
“Kwa goli ambalo Ethan umefunga leo, yaani nilisime hapana. Nilazima nije nikuangalie vizuri mwanangu. Heee hapana kwa kweli”
Mama Camila alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.
“Nashukuru sana mama. Kumbe mama na wewe huwa unatazama mpira ehee?”
“Yaani toka ulipo anaza kucheza wewe, nikaanza kupenda mpira. Unakumbuka ile siku ambayo Camila alitaka kujirusha gorofani?”
 
“Ndio ndio nakumbuka mama?”
“Sasa siku ile ndio nilipenda kutazama mpira, hakika nina mkwe ambaye anatufanya kila muda tujisikie amani katika mioyo yetu”
“Nashukuru sana mama”
“Kocha wenu yupo wapi?”
“Yule kule”
Nikamuita kocha kwa ishara, akasimama na kutufwata eneo hili tulio kaa.
“Hongera sana kwa wachezaji wako ulivyo waanda. Yaani wanatupa buruni moja nzuri sana”
“Nashukuru sana mkuu”
“Nikipata nafasi, nitapendekeza uinoe timu ya taifa na hii mashine yako hapa nayo iwepo katika timu yako ya Taifa”
Maneno ya baba Camila yakanistua kidoo, kwani katika maisha yangu yote ya kuishia hapa Ujerumani, sijawahi kufikiria kuichezea timu ya taifa ya nchi hii japo nina uraia wa hapa Ujerumani. Nchi yangu mimi ni Tanzania na mimi ni Mtanzania na kamwe sinto isaliti Tanzania hususani katika maswala ya mpira ninao cheza.

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 158 na 159 )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
               
“Nimewapakiza ndege mbili tofauti na Yemi. Yemi amapenda katika ndege yangu binafsi na mwili  wa mwanaye, jamaa na watu wake nao wamependa kwenye ndege nyingine na wale wajinga wake watatu. Kwenye ndege waliyo panda, kuna bomu liliko tengwa, na nitahitaji maamuzi yako kwamba tuwalipue wafie hewani au tuwaache waendelea na maisha yao?”
Swali la meja likanifanya nitazamane na Martin, taratibu nikamtazama meja usoni mwake, huku nikikumbuka uwenda wazimu ulio nipata jana usiku kutokana na ukweli walio uzungumza mume mwenzangu kwa Yemi na kujikuta nikisikia sauti moyoni mwangu ikihitaji niweze kumuangamizaa jamaa huyu kwani amenipotezea mwanamke aliye nipa furaha maishani mwangu.

ENDELEA   
 Taratibu nikajiku nikiyang’ata meno yangu kwa hasira huku sauti ninayo isikia moyoni mwangu ikiendelea kunipa uchochezi wa kufanya mauaji haya.
“Dany nasubiria jibu lako?”   
“Samahani meja kama ninawaingilia, ila ninaomba nishauri katika hilo”
 
Sote tukamtazama Martin aliye zungumza kwa sauti ya upole.
“Kwa jinsi nilivyo agana na Yemi leo asubuhi, aliniomba nimlinde Dany hadi mwisho wa maisha yangu. Sikuhitaji kulizungumza hapo awali kwako mkuu, ila ukweli ni kwamba Yemi bado anakupenda. Tukimuua mume wake huyu ni lazima atajawa na chuki ambayo itapaelekea yeye kulipiza kisasi kwako jambo ambalo litakuzidishia maadui hapa duniani ikiwa hawa maadui waliopo mbele yetu hatujawamaliza”
 
Martina alizunguzma kwa upole na usikivu mkubwa sana, taratibu nikajikuta moyo wangu ukianza kutulia.
“Sasa hivi tunatakiwa kuwaangalia maadui hawa watatu walipo mbele yetu, inabidi kuwazuia kwa manaa hao wana nguvu ya kiserikali, wana nguvu ya kuendelea kukutangaza Dany wewe kama gaidi, hembu tuangalie hili sasa”
“Kwa hiyo Martin unapendekeza bosi wako amuachilie mbali mwanaume aliye mpokonya mke?”
 
“Mimi ndio nilimpokonya mke wake”
Nilizungumza kwa sauti ya upole huku nikimtazama meja usoni mwake na kumfanya anishangae.
“Nilimpokonya jamaa mke wake kwa kumpiga na pia nimepelekea mtoto wao kufa, yote ni kwa ajili yangu. Nina hisi hata nikimuua jamaa damu yake itenililia maishani mwangu na pia inaweza kupeleka kuto kukamilisha hili zoezi la kulipiza kisasi”
Nilizidi kuzungumza kwa upole huku n ikijitahidi hasira na sauti ya uchochozi inayo endelea moyoni kuipinga ili kutoa maamuzi mazuri kwa ajili ya maisha yangu ya baadaye kwa maana Yemi hajanifanyia jambo lolote bada.
 
“Sawa kama umeridhia rafiki yangu siwezi kuendana kinyume na makubaliano yako, ngoja nimpigie simu rubabi niliye mpa jukumu la kujitoa muhanga kwa ajili hili”
“Kumbe ulikuwa umemtoa mtu muhanga?”
“Ndio nimemkabidhi kiasi kikubwa cha pesa kitakacho isaidia familia yake kwa miaka mingi tu baada ya kifo chake”
“Mmmmmmm”
Nilijikuta nikihema kwani maamuzi aliyo kuwa ameyachukua meja katika kunisaidia ni magumu sana. Meja akatoa simu yake mfukoni akaminya minya juu ya kioo kisha akaiweka sikioni.
“Zoezi nimelisitisha”
“Sawa”
Meja akakata simu huku akitabasamu.
“Jaamaa ameshusha pumzi sana, masikini wee”
“Nani?”
 
“Rubani, emeshusha pumzi nina imani hapo alikuwa anaomba zoezi lisikamilike”
“Hivi kumbe kuna watu wanaweza kujitoa muhanga kwa ajili ya pesa?”
“Ohoo rafiki yanu umasikini mbaya sana, kwa maana nimemlipa jamaa pesa ya mshahara wake kwa mawaka mara mbili nikazidisha kwa miaka kumi mbele”
“Ni sawa na kiasi gani?”
“Dola milioni tano, ni utajiri mkubwa sana”
“Pesa yote hio utamuacha ande nayo?”
“Yaa ni dili, wewe ndio umemuakoa, itabidi nije kumuambia kwamba wewe ndio umeweza kuyaokoa maosha iyake atajua ni jinsi gani atakushukuru”
“Usimuambie bwana kwa maana sijafahamu anaweza kunichukulia vipi, isitoshe nina imani atakuwa amesikia habari zangu”
“Sidhani, unajua huku Madagasca watu sio wafwatiliaji sana wa mambo, ndio  maana juzi tuliweza kutembea barabani kwa kujiamini na wala hakuna hata polisi aliye weza kukutilia mashaka”
 
“Kweli. Sasa ni muda wa kujua tunaanzai katika hii kazi iliyo bakia mbale yetu”
Nilizungumza huku nikimtazama meja usoni mwake.
“Jambo la kwanza ambalo tunatakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba unaingia nchini Tanzania pasipo mtu yoyote kuweza kukufahamu, kwani nina imani kwa sasa ulinzi nchini Tanzania utakuwa ni mkali sana kutokana na ujio wa raisi Donald Bush”
“Tutatumia ndege au?”
“Hatuwezi kutumia ndege kwa maana kila ndege inayo ingia katika angala la Tanzania ni lazima ikaguliwe na wewe nina imani picha yako itakuwa imesambazwa kwenye vituo vyote vya usifiri.
 
Meja aliendelea kusisitiza huku akitutazama.
“Njia  ya usalama itakayo kuwezesha wewe kufika nchini Tanzania ni kutumia bahari?”
“Unahitaji tutumie meli?”
“Hapana nina boti za mwendo kasi ambazo zinaweza kuwafikisha Tanzania katika masaa machache sana ila itabidi kuwaacha japo maili moja kabla ya kuingia Tanzania, na mutazamia majini hadi kufika Tanzania.”
Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi huku nikimtazama meja usoni mwake.
 
“Hapo ni lazima kuogela rafiki yangu, pasipo kufanya hivyo unakwenda kuingia mikononi mwa Wamarekani na wakikukamata ndugu yangu kwa sasa hawato kuacha na watakuua haya kwa kukuchoma sindano ya sumu”
“Hilo halita weza kutokea”
 Martin alizungumza kwa kujiamini.
“Yaa mukiwa makini nina imani kwamba hilo halito weza kutokea”
“Mukiwa makini basi halito weza kutokea. Tanzania mutakwenda kukutana na kijana wangu anaotwa Godlove, atawapokea katika fukwe ambayo mutatokea”
“Kwa Dar es Salaam ni fukwe gani ambayo haina ulinzi sana?”
 
Nilizungumza huku nikikmtazama meja.
“Wewe ndio mwenyeji mwenzetu unatuuliza na sisi tena?”
“Nimeondoka muda sana Tanzania kwa hiyo siwezi kuelewa kama mambo yamebadilika au laa”
“Ngona nimpigie Godlov”   
Meja akampigia kijana wake baada ya sekunde kadhaa akaiweka simu mezani huku akiwa ameweka loudspeaker.
“Mkuu habari yako?”
“Salama meja”
“Hii laini yako ina usalama wa kuweza kuzungumza?”
“Ndio mkuu hakuna anaye weza kupata mawasiliano yetu”
“Sawa ni bichi gani kwa jijini Dar es Salaam hapo mulipo ina ulinzi dhaifu?”
 
“Koko bichi ipo dhaifu, japo kwa wiki hii umeimarishwa ulinzi kwa ajili ya ujio wa raisi wetu ila bado ulinzi wake ni wa kusua sua”
“Sasa Dany na mwenzake watakuja Tanzania nina imani watakuwepo huko majira ya saa tisa usiku nina imani kwamba ume waandalia mazingira mazuri?”
“Hilo usijali mkuu nimeanda kila kitu kipo sawa, na nitawasubiria katika ufukwe huo hadi wafike”
“Itakuwa vizuri, nina imani utawapa ratiba nzima ya shereha na ziara za Donald pamoja na K2”
“Ndio mkuu”
 
“Basi nikutakie asubuhi njema”
“Nashukuru mkuu”
Meja akakata simu na kututazama usoni mwangu.
“Kazi ni raisi sana kilicho baki ni nyinyi kuanza safari muda wowote mukiwa tayari”
“Shukrani sana meja sijajua hata nikulipe kitu gani kwani kwa msaada wako ulio nipatia sijawahi kuupata kutoka kwa mtu yoyote duniani”
“Usijali Dany haya ni maisha na pesa inatafutwa, kikubwa ni wewe kuwa makini katika hilli”
“Kitu kingine ninakuomba umlinde Yemi, ninajua baada ya haya matukio ambayo nitakwenda kuyafanya nina imani kwamba kuna watu watakao mfwatilia na kumuua”
“Unampenda?”
 
Meja aliniuliza kwa sauti ya upole huku akinikazia macho.
“Ndio nina mpenda, upendo hauwezi kufutika kwa siku moja na…..”
“Usijali Dany huna jaya ya kujieleza sana katika hilo ikiwa hata mii ninazielewa hisia zako”
“Shurkani meja kwa kuweza kinielewa”
“Sawa ngoja niwaache muzungumze mawili matatu, niandae mpango mzima wa safari”
“Sawa meja”
Meja akasimama na kuondoka katika eneo hili na kuniacha na Martin.
“Mkuu isije ikatokea siku ukamkosea huyu mzee”
“Kwa nini?”
“Amekusaidia kwa asilimia kubwa sana na pasipo yeye nina imani kwamba tungekuwa tumesha kufa ile siku tuliyo tekwa na Wamarekani”
 
“Yaa ni mtu mwenye thamani kubwa kwangu nina mthamini sana. Sasa jiandae kama kuna cha kuchukua chukua safari itaanza asubuhi hii”
“Sawa mkuu”
Nikanayuka na kuelekea chumbani kwangu kwangu, nikaingia bafuni na kuaoga, japo ninayakumbuka matukio machache niliyo yafanya humu bafuni na Yemi ila sina jinsi zaidi ya kuvumilia na kuweka hisia za mapenzi pembeni na kuimalizia kazi iliyopo mbele yangu.
Nikava jinsi, tisheti na raba, nilipo hakikisha kwamba nimekamilika, nikachukua  pete ya Yemi na kuivaa katika kidole changu cha mwisho cha mkono wangu wa kushoto kisha nikatoka humu chumbani. Nikamkita Martin akiwa amesimama sebleni na meja.
 
“Boti ipo tayari kwa ajili ya safari”
“Sawa meja”
Tukaanza kutoka na kuelekea katika kingo za fukwe ya bahari iliyopo pembezoni mwa jumba la meja.
“Hakikisheni kazi munaifanya kikamilifu na safari hii Dany usifanye makosa yoyote ambayo yatakugarimu”
“Usijali meja, nikishindwa kufanya sasa hivi nina imani kwamba sinto weza kufanya tena hii kazi”
“Sawa sawa nakuamini katika hili”
“Pia meja nina shukuru sana kwa kila kitu ulicho nifanyia na unacho endele kunisaidia”
 
“Usijali rafiki yangu, niwatakie safari njema”
“Asante”
Tukaingia kwneye boti moja kubwa ya kifahari.
“Mukifika Tanzania, Godlove atawaeleza jinsi ya kuwasiliana nami”
“Sawa meja”
Taratibu boti hii ikaanza kuondoka eneo hili huku tukiwa tumekabidhiwa vijana wawili wa meja pamoja na nahodha wa hii boti. Safari ikazidi kusonga mbele huku boti hii ikienda kwa mwendo kasi sana.
“Mkuu unahitaji tuwaue vipi maadui  zako?”
“Hilo tutalijua tukifika nchini Tanzania kwa sasa ni vigumu kulizungumzia kwani bado hatujajua wamejipanga vipi katika hilli swala”
“Sawa”
Nahodha wahii boti kusema kweli ni mtaalamu kwania kasi anayo kwenda nayo ni kibwa na muda mwengine tunakutana na mawimbi makubwa ya maji ila tunafanikiwa kupita. Masaa yakazidi kwenda hadi giza likaingia.
 
“Tuna masaa kadhaa mbele, kuna maelezo tunatakiwa kuwapatia”
Kijana mmoja wa meja alizungumza huku akitutazama kwenye siti tulizo kaa. Nikanyanyuka na kumsogelea.
“Sawa”
“Kuna nguo maalumu za kuzamia kwenye maji pamoja na mitungi maalumu nina imani kwamba munaweza kuitumia?”
“Kwa mimi ninaweza, Martin unaweza?”
“Ndio ninaweza mkuu”
“Basi hii mitungi inagesi itakayo wawezesha kukaa chini ya maji kwa masaa zaidi ya kumi. Pia kuna hii simu haiingii maji na inatumika hata ukiwa ndani ya bahari. Itawasaidia katika swala zima la kutazama muelekeo wa wapi munakwenda, kwani tumeambiwa kuwaacha maili moja kutoka Tanzania ilipo”
 
“Sawa”
Kijana huyu akanikabidhi simu hii nikaitazama vizuri, kisha nikamkabidhi Martin.
“Kuna swali munahitaji kuniuliza?”
“Hapana”
“Basi niwatakie kazi njema na karibuni Madagascar”
“Asante”
“Tukiwa tunakaribi kufika basi tutawaambia muweze kuvaa mavazi hayo?”
“Tunaweza kuvaa juu ya hizi nguo zetu?”
“Hapana labda muziweke kwenye begi maalumu ambalo lipo hapa na haliingii maji?”
“Sawa sawa na sehemu ambayo munatuacha haina samaki wakali?”
“Hapana samaki wake ni wa kawaida. Na kuna tochi maalimu mutazitumia mikiwa chini ya maji ila munatakiwa kuwa makini sana”
 
“Shukrani kaka”
“Niite Michael”
“Sawa asante sana Michael”
Nikarudi kwenye siti yangu baada ya kupata maelekezo hayo, huku kichwani mwangu nikifikiria jinsi nilivyo poteza uhuru katika nchi yangu na nina rudi kama mvamizi ambaye endapo nitaonekana basi ninaweza kupoteza maisha yangu.
‘Mungu nisaidie katika hili’
Nilijikuta nikizungumza maneno hayo huku nikiwa nimeyafumba macho yangu. Baada ya masaa mawili, Michael akaingia tena kwenye hichi chumba tulipo kaa huku akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana.
 
“Vipi?”
“Tumepata tatizo”
“Tatizo gani?”
Boti yetu inafukuziwa na boti za jeshi la majini na wanamlazimisha nahodha kusimamisha boti la sivyo wanakwenda kutulipua na hadi sasa wametupa onyo la pili tunasubiria amri yako tusimamishe boti au tusonge mbele ili tulipuliwe”
Michael alizungumza haraka haraka na kunifanya ninyanyuke kwa haraka hukun ikiwa nimejawa na wasiwasi mwingi, kwani hili ni tatizo jengine ambalo sikulitarajia litokee kwenye safari yangu hii.

AISIIIII……….U KILL ME 159  

“Boti zipo ngapi za hao wanajeshi?”
“Zipo boti nne”
“Muambie nadhodha asimamishe boti”
“Sawa mkuu”
Michael akatoka katika chumba hichi, na kutuacha mimi na Martin tukiwa tumesimama huku wasiwasi mwingi ukiwa umetutawala. 
 
“Tutafanyaje mkuu wakitukuta humu ndani?”
“Ni lazima tufanye jambo”
Nilizungumza huku nikitoka ndani ya hichi chumba, nikawakutua Michael na wezake wakiwa wamesimama wakitazama jinsi boti hizi za jeshi zikiizunguka boti hii tuliyo panda.
“Michael njoo”
Michael akanifwata sehemu nilipo jibanza.
“Kuna silaha humu ndani ya hili boti”
“Ndio mkuu”
“Zipo wapi?”
Tukarudi kwenye chumba tulichopo, Michael akafungua moja ya kabati lililomo humu ndani akasogeza nguo zilizopo kwenye hili eneo, akaanza kutoa bunduki moja baada ya nyingine na kutukabidhi. Nikachukua bunduki moja iliyo jaa risasi za kutosha.
 
“Wanajeshi wakileta shida tutawashambulia”
“Sawa mkuu”
Michael akatoka ndani humu na kutuacha mimi na Martin kila mmoja akiwa na bunduki yake na tumejibanza kwenye sehemu ambayo si rahisi kwa mtu wa nje kuwea kutuona ila sisi ni rahisi kuweza kumuona mtu wa nje hii ni kutokana na vioo vigumu viliyomo kwenye kuta za hichi chumba.
Tukawashuhudia wanajeshi watatu wakiingia kwenye boti hii huku wakiwa wameshika bunduki zao, ila katika kuwatazama sare zao sio za wanajeshi wa jeshi la maji Tanzania.
 
“Hawa wanajeshi ni wa wapi?”
Nilimuuliza Martin huku nikiendela kuwatazama wanajeshi hawa.
“Ni wanajeshi wa Msumbiji”
“Ina maana bado hatujaingia Tanzania?”
“Yaa”
Tukaendelea kuwatazama wanajeshi hawa walio anza kugaua vibali vya hii boti huku wakiwatazama Michael na mwenzake, wakazungumza nao kwa dakika kadhaa, Michael akatoa kibunda cha dola za kimarekani na kumkabidhi mwanajeshi mmoja aliye anza kuhesabu pesahii haraka haraka kisha akamtazama Michael huku akitingisha kichwa. Taratibu nikawaona wakishuka kwenye boti kisha wakaruhusu boti yetu kuondoka. Nikajikuta nikishusha pumzi nyijngi kisha nikarudi kukaa kwenye siti yangu. Michael akaingia kwenye chumba chetu.
 
“Walihitaji nini hao wanajeshi?”
“Walikuwa wanafoka foka tu kwa nini tumepita kweney ukanda wa nchi yao, pasipo kuw ana kibali”
“Wana vichaa kweli”
“Nimewapa dola elfu tano, ndio maana wametuachia”
“Sawa tumebakisha muda gani hadi kufika nchini Tanzania?”
“Tumesha ingia kwenye ukanda wa nchi ya Tanzania, hapa tutatumia muda mchache kufika usawa wa Dar es Salaam”
“Sawa sawa”
 
Michael akaanza kurudisha silaha ndani ya kabati hili huku akisaidia na Martin. Baada ya muda wa kama dakika aroboini na tano Michael akatuommba tuweze kuvaa nguo maalumu za kuogelea kwani muda kuzama baharini umefika.
Tukaanza kujiandaa mimi na Martina hatukuchukau muda mrefu tukawa tumefanikiwa kuvaa nguo hizi pamoja na mitungi maalimu ya gesi ya oksijeni tuliyo ivaa mgononi. Tukavaa miwani maalimu, kisha Michaela katukabidhi tochi.
“Niwatakie kazi njema”
 
“Shukrani na murudi salama. Martin mbona umemeba begi?”
“Nimeweka nguo zetu na vifaa vichache”
“Sawa”
Nikampa mkono wa shukrani Michael na mwenzake kisha taratibu tukajitosha kwenye maji. Tukaanza kushuka chini huku tukiwa tumewasha tochi zetu. Tulipo fika katika usawa ambao tunaamini hata mmtu awe kwa juu hatoweza kuona mwanga wa tochi tulizo ziwasha, tukaanza kuogelea kwenda mbele huku Martin akiongoza kwa kufwata malekezo kwenye simu aliyo ishika, tukazidi kusonga mbele huku tukiwa makini sana hadi tukafanikiwa kufika kwenye moja ya nyavu kubwa ya chuma. Martin akanikabidhi simu aliyo ishika kisha akavua begi na kutoa koleo kubwa la kukatia njavu hii. Taratibu akaanza kukata njavu hii huku mimi nikiwa makini kutazama tunapo toka na tuendapo. 
 
Alipo maliza kukata taratibu tukaanza kuingia kwenye uwazi alio kata na tukaendelea na safari yetu. Hadi inatimu saa tisa usiku tukafanikiwa kufika katika ufukwe wa koko bichi huku tukiwa tumechoka sana. Tukatoka ndani ya maji na kukaa chini ya mwamba mmoja ulipo hapa pembezoni.
“Ohooo kukaa kwenye maji ni kazi kweli kweli”
Nilizungumza huku nikihema sana.
“Yaani wee acha tu”
“Huyu jamaa sijui atakuwa amesha fika”
“Ngoja nikamtazame”
Martib alizungumza huku akinyyanyuka, akavua viatu maalumu vya kuvulia, akaivua na tochi na kuizima, akatoka kwenye mwamba huu ambao umeingia ndani, hata hazikupita dakika mbili nikiaiskia milio ya risasi iliyo nistua sana, kwa haraka nikachungulia kwenye mwamba huu, nikamuona Martin akiwa amezungukwa na watu walio valia nguo nyeusi.
 
Nikatamani kujitokea ila sina silaha amabayo itawezesha kushambuliana na watu hawa. Nikamuona Martin akipigishwa magoti chini huku mikono yake akiweka nyuma na kufungwa pingu. Akanyanyuliwa kwa haraka na watu hawa wakaondoka naye katika hili eneo.
“Shitiii”
Nilizungumza huku nikiwa nimekasirika sana kwani sijajua mpango huu umevurugwa na nani na mtu ambaye tumeambia kwamba atakuja katika hili eneo ni Godlove ambaye hata sura yake siifahamu. Nikafungua begi lenye nguo, kwa haraka nikaanza kubadilisha nguo nilizo zivaa na kuvaa nguo za kawaida, nilizo kuwa nimezivaa nilipo toka katika kisiwa cha Madagasca.
 
Nikachunguza hili eneo kwa umakini na nikaanza kutoka katika huu mwamba sikuelekea katika usawa alio kuwa amekwenda Martin. Nikaanza kutembea huku nikiwa makini sana katika kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaye weza kunifwatilia au kuniona. Nikiwa katika moja ya barabara iliyo tulia nikaona gari aina ya Toyota Mark X ikiwa imefunuliwa boneti ya mbele huku ikitoa moshi mwingi na mlango wa dereva nao umefunguliwa. 
 
Nikataza hili eneo nikagundua kwamba hakuna sehemua mbayo askari wanaweza kujificha na ikawa ni mtego kwangu. Nikaanza kulisogelea hili gari hadi nikanikiwa kufika, nikamkuta msichachan mmoja akiwa amejilaza kwenye siti yake akionekana kuchoka sana na kwenye zake zimefunika sehemu ya uso wake. Mkononi ameshika chupa ya wyne na inaonyesha amelewa sana.
“Hei”
Nilimuita huku nikiendeleak kutazama eneo hili kwa umakini sana. Binti huyu akakurupuka na kunitazama huku akiziweka nywele zake sawa. Sote tukabaki tukishangaana kwani huyu binti ninamfahamu sana.
“Dany!!”
“Lucy!!”
Nilimuita huku sote tukishangaana. Lucy akatoka kwenye siti aliyo kaa na kusimama, akanikumbatia kwa haraka, tukajikuta tukiwa tumejawa na furaha.
“Oohoo Dany ni miaka mimi sasa hatujaonana, upo wapi wewe?”
 
Lucy alizungumza huku akiwa ametanasamu.
“Maisha tu, gari lako lina tatizo gani?”
“Sijui ninaona limenizimia tu hapa”
Nikamuachia Lucy huku nikitembea hadi mbele ya hili gari, nikaanza kutazama tazama tatizo la hili gari, mwanga mkali wa gari inayo kuja nyuma yetu ukanifanya nisigeuke na kujifanya nipo bize ninaendela kutengeneza hili gari. Gari hili likasimama karibu kabisa na gari hili, taa za gari hilo zikazimwa na kunipa nafasi ya kugeka kidogo, nikajikuta nikistuka baada ya kuona platenamba za hili gari inaonyesha ni gari ya polisi.
‘Nitawaua’   
Nilijikuta nikiapia huku nikiendelea kuinama kugusa gusa baadhi ya vitu viluyopo kwenye hii bonet.
“Mbona mumechelewa?”
Nilisikia sauti ya Lucy akizungumza na polisi hawa, jambo lililo nifanya moyo wangu kunistuka sana na kuhisi kwamba Lucy ameniuza kwa askari hawa. Nikataka kugeka ila nikajikuta nikiwa mvumilivu nikisikilizia kauli ya askari yoyote atakaye jibu swalli la Lucy mtoto wa Mzee Jogoo, niliye wahi kumsaidia mikaa mingi katika ajali ya moto kipindi nilipo kuwa ninaishi Sinza.
 
“Kidogo tulikuwa kwenye patroo Ubungo ndio maana tumechelewa samahani”
“Ahaa gari limenibumia hapa”
“Huyo anaye kusaidia ni nani?”
Kwa jicho la kona nikamuona Lucy akigeuka na kunitazama, akatabasamu na kunisogela nilipo simama na kuendelea kujifanya nina tengeneza gari hili.
“Ni mpenzi  wangu”
Nikashusha pumzi kidogo kwani tayari nilisha anza kujiandaa kiakili jinsi ya kupambana na askari hawa wanne.
“Ingia ndani ya gari ujaribu kuwasha”
Nilizungumza huku nikaza moja ya nati ambayo nimeikuta imelegea. Lucy akatembea kwa madoido hadi ndani ya gari akajaribu kuwasha na gari ikawaka.
“Waooooooooooo”
Lucy alishangilia huku akishuka kwenye gari.
“Asante mpenzi wangu”
Lucy alizungumza huku akinifwata na kunikumbatia, sikutaka kabisa kuigeuza sura yangu kuwatazama hawa askari kwani nina imani wataingia kwenye msiba ambao sihitaji niwe chanzo cha vifo vyao.
 
“Ngoda mumaweza kuondoka tu gari langu tayari”
“Mkuu ametuagiza tukusindikize hadi nyumbani”
“Mumbieni baba kwamba mimi ninaendelea kula bata weekend ndio imeanza hivi”
“Ila ni kwa ajili ya usalama wako”
“Nipo salama si munamuona shemeji yenu hapa”
“Mbona shemeji haitaji kututazama”
“Eheee kwani ni lazima jamani. Ngoda ondoka na watu wako bwana”
“Sawa”
Askari hawa wakarudi kwenye gari lao, wakapanda na kuondoka eneo hili na kutuacha tukiwa tumesimama tukisindikza gari lao kwa macho.
“Asante”   
Nilizungumza huku nikielekea katika mlango wa pili wa hili gari, Lucy akazunguka hadi katika mlango wa dereva na sote tukaingia ndani, tukafunga milango na kuanza kuondoka eneo hili.
 
“Dany ni kwa nini wewe?”
Lucy alizungumza kwa sauti ya chini huku akinitazama.
“Tunaelekea wapi kwanza?”
“Jibu swali langu kwanza”
“Unahisi ni kweli ni mimi?”
“Ndio maana nina hitaji kujua ukweli kuhusu wewe kwa kipindi chote ambacho unatafutwa na kutangazwa kama Gaidi tena wa kimataifa?”
“Mimi sio gaidi ila hao wanao watangazia wao ndio magaidi”
“Nitakuamini vipi ikiwa nimesikia umeua watu wengi sana na hapa Tanzania unatafutwa kama shahabu na endapo mtu atafanikishwa kukamatwa kwako basi yeye na umaiskini ndio kwaheri”
 
“Lucy”
“Beee”
“Una niamini?”
“Ndio ninakuamini, ndio maana sikuhitaji kukuchomesha kwa wale askari pale kwani bado sijakaa na wewe kufahamu ukweli ulio pelekea kuitwa gaidi na kuwindwa sana”
“Nashukuru, baba yako yupo wapi?”
“Baba ni waziri mkuu”
“Ananizungumziaje mimi katika hili swala”
“Baba yangu nina imani amejazwa chuki kubwa na anakuchukia sana na anatamani hata leo akukamate na kukuadhibu kwa makosa yako yote uliyo yafanya”
“Asijaribu kufanya hivyo kwani na yeye nitamua”
Gafla nikastukia Lucy akifunga breki za gari lake huku akinitazama kwa macho makali akionekana kushangaa kauli yangu niliyo itoa kwani ni kauli ambayo nina amini kwamba ni mbaya sana kwake ila ndio ukweli kutoka moyoni mwangu.
 
ITAENDELEA
“Haya sasa Lucy ameweza kukutana na Dany ambaye ameahidi kumuua baba yake endapo ataamua kuingia kwenye kumi na nane zake na Lucy ndio mtu wa pekee anaye tambua kwamba Dany yupo nchini Tanzania, je ni kitu gani kitakcho endelea. Usikose sehemu inayo fwata ya kisa hichi cha kusisimua

Alichokisema Freeman Mbowe Kabla ya Kupelekwa Gerezani

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho kuwa “imara na kutoogopa” akisema kesho ni “nzuri kuliko jana” baada ya kufutiwa dhamana yake.

Mbowe ametoa kauli hiyo, akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, baada ya mahakama hiyo kumfutia dhamana na mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana hiyo.

Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alitumia kizimba cha mahakama hiyo kusalimiana na viongozi wengine wa Chadema na wafuasi pamoja na kutoa ujumbe wake wa kuwatia moyo.

 “Naomba muwe stable (imara), msiogope. Kesho ni nzuri kuliko jana,” alisema Mbowe kisha akamalizia na salamu ya chama hicho ya “peoples” na wafuasi kuitikia “power”.

Kabla ya kutoa ujumbe huo, askari walitaka kumuondoa katika kizimba, lakini akawasihi akisema “kwanza nizungumze na watu wangu”.

Uamuzi wa kuwafutia wawili hao dhamana ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri akisema kitendo kilichofanywa na washtakiwa hao ni kudharau amri za mahakama kwa makusudi.

Waziri Lugola ataka polisi walioua majambazi Jijini Mwanza wapandishwe vyeo

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema askari wote walioshiriki katika mapambano na kuwaua watu wanaosadikika kuwa majambazi saba Novemba 15, 2018 jijini Mwanza watapandishwa vyeo.

Tukio hilo lililotumia takribani dakika 45 lilitokea katika Kata ya Kishili jijini hapa saa tano usiku.

Akizungumza na maofisa wa polisi na baadhi ya askari wa vikosi vyote vya polisi jijini hapa leo Ijumaa Novemba 23,2018 katika viwanja vya polisi Mabatini, Waziri Lugola amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuwapongeza askari hao.

"Askari hawa wamefanya jambo la kizalendo kupambana na majambazi hao wanaosumbua raia wetu, kwa hiyo inapotokea askari wanatutoa kimasomaso lazima tuna kila sababu ya kuwafanyia jambo la kuwafurahisha, hivyo na hawa tunawapandisha vyeo wote," amesema Lugola.

Hata hivyo, amesema bado majambazi wapo na ni wajibu wa askari kuhakikisha wananchi na mali zao wanakuwa salama kwa kupambana nao.

"Ni kosa kwa askari kuwa mwoga hupaswi kukimbia tukio, lazima ukabiliane nalo maana ndio dhamana tuliyokabidhiwa," amesema.

Ligola ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi wapo salama na kuwatumia salamu wanaofanya uhalifu kwamba bora wajisalimishe na kuacha mara moja vitendo hivyo vinginevyo watashughulikiwa popote watakapokuwa hata kama ni mapangoni maana Serikali ina mkono mrefu.

Awali, Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana amesema mkoa huo upo shwari licha ya kuwapo matukio kadhaa ya wahalifu lakini wamekuwa wakiwadhibiti kabla ya kutekeleza azma yao.

"Mkoa upo shwari, vikosi vyetu vimejipanga kuwashughulikia wanaoleta ujuaji kufanya uhalifu kwenye mkoa wetu, nikuhakikishie tupo vizuri,” amesema

Hatimaye Mbunge Bwege na Wenzake Waachiwa kwa Dhamana

$
0
0
Viongozi watatu wa Chama cha Wananchi (CUF) leo Ijumaa, Novemba 23, 2018 wameachiwa, baada ya kukamilisha masharti ya dhamana, yaliyowekwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi.

Walioachiwa ni pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Habari na uwenezi Taifa, Mbalala Abdallah Maharagande,M’bunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Selemani Said Bungala (Bwege) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Abuu Mussa Mjaka.

Viongozi hao walilazimika kurejeshwa mahabusu jana kufuatia baadhi ya barua za wadhamini kukosew majina na muda wa kazi za ofisi kumalizika wakati hawajakamilisha taratibu za dhamana zao.

Hata hivyo dhamana ya viongozi hao, ilitaka kuingia dosari kwani hadi saa 5:16 asubuhi, walikuwa bado hawajafikishwa Mahakamani kwa madai mbalimbali, ikiwemo kukosekana kwa askari wa kuwafuata gerezani, na kufanikiwa kuletwa saa 7:45 na kukamilika kwa taratibu ndogondogo za ki-Ofisi, ambapo wameachiwa saa 9:30 Alasiri.
 
Viongozi hao wanakabiliwa na mashitaka matano, yakiwemo mawili ya kuuwa, pamoja na kutoa lugha ya uchochezi na matusi, wakati wa mkutano wa uzinduzi wa uchaguzi mdogo wa udiwani, uliokuwa umefanyika viwanja vya Maalimu Seif Gurden uliopo mji mkongwe wa Kivinje.

Wakili anayewatetea viongozi hao, Rainery Songea, akizungumza mara baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, alisema uwepo wa kesi hiyo haitawazuia kujihusisha na shughuli zozote zinazohusiana na kampeni inayoendelea hivi sasa.

Aidha, Wakili Songea ameendelea kuwasisitiza wateja wake, kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya uchaguzi wanapoendesha mikutano yao ya kampeni.

Shauri la washitakiwa hao namba 10 na 11/2018, limepangwa kufikishwa tena mbele ya Mahakama hiyo, Decemba 3, mwaka huu.

CHADEMA Watoa Tamko Zito Baada ya Freeman Mbowe Kupelekwa Gerezani

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimewataka wanachama wake nchi nzima kufika mahakamani wakati kesi inayowakabili viongozi wake watano itakapounguruma ili wajionee uendeshwaji wa kesi na kuamua kwa pamaoja nini cha kufanya.

Wito huo wa CHADEMA umekuja saa chache baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu kuamua kufuta dhamana ya viongozi wawili wa chama hicho, Mwenyekiti wa chama taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Tarime mjini, Ester Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Akizungumza na wanahabari, makao makuu ya chama hicho yaliyopo mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji amesema, "wanachama wa CHADEMA nchi nzima, suala hili ni zito, ni nyeti na linahusu mustakabali wa nchi yetu, usisubiri kusimuliwa njoo uone mwenyewe kinachoendelea mahakamani kwasababu kumekuwa na upotoshaji mkubwa".

"Tunaomba tuje tusikilize wenyewe mahakamani na baada ya hapo tuamue ni hatua gani tutachukua sisi kama watetea haki wa watu wote katika taifa hili," ameongeza.

Aidha katika hatua nyingine, chama hicho kimeazimia kukata rufaa katika Mahakama Kuu kwa kile ilichokidai ni kupinga juu ya hatua ya kufuta dhamana ya viongozi wake iliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi.

"Tumeamua kukata rufaa kwenda Mahakama Kuu na tumeshawasilisha barua yetu, bado tunasubiria watupe namna. Na katika barua yetu tumeeleza haya mashaka yetu yote juu ya mwenendo wa hii kesi

Waziri Mkuu: Tutaendelea Kushirikiana na Vyuo Vikuu Vyote Nchini

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano na miongozo kwa vyuo vikuu vyote nchini, vya binafsi na vya umma ili viendelee kutoa elimu ya juu yenye ubora na viwango vinavyotakiwa kwa lengo la kukidhi matakwa na ushindani kwenye soko la kitaifa na kimataifa.

Amesema suala hilo ni muhimu likapewa uzito unaostahili kwani wahitimu hao wakitoka vyuoni wanakwenda kutoa huduma katika jamii ya Watanzania na pia ya kimataifa, hivyo ni muhimu elimu inayotolewa ikazingatia ubora na viwango vinavyostahiki.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Novemba 23,2018) kwenye mahafali ya tisa ya chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania Kampasi ya Chifu Mazengo, Dodoma yaliyofanyika kwenye ukumbi wa CCM.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, inatambua na kuthamini mchango wa Sekta Binafsi hususan wa vyuo vikuu binafsi kama Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania, katika maendeleo ya elimu ya juu.

“Serikali inatambua mchango wa vyuo hivyo katika kupanua fursa kwa Watanzania wengi kupata elimu ya juu, ambapo hadi sasa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu kwenye vyuo vikuu binafsi nchini ni takriban asilimia 25 ya wanafunzi wote.”

Amesema Serikali inatambua mchango wa chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania katika kutayarisha watalaamu wa fani mbalimbali. Aidha, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007, chuo hicho kimetoa wahitimu zaidi ya 10,000.

Amesema kati ya wahitimu hao wapo Wafamasia, Wauguzi, Walimu wa Sayansi, Walimu wa Sanaa, Wataalamu wa Maabara, na Wasimamizi na Waendeshaji wa fani mbalimbali kama Utawala, Masoko na Wahasibu, mchango ambao unahitajika kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa uchumi wa Taifa katika nyanja tajwa.

Waziri Mkuu amesema baadhi ya wahitimu watapata ajira lakini si kila mhitimu atapata fursa ya kuajiriwa, hivyo Serikali itaendelea kuunga mkono azma yao kama chuo kikuu ya kutoa wahitimu wenye tabia, utashi na uwezo wa kutengeneza kazi na siyo watafuta kazi tu.


Akizungumzia kuhusuchangamoto zinazokabili sekta ya elimu ya juu, amesema baadhi ya changamoto zinafanana katika vyuo vikuu vyote nchini na pia zipo changamoto zinazokabili vyuo vikuu binafsi na wakati mwingine zipo changamoto zinazohusu chuo kikuu kimoja kimoja.

Amesema moja ya changamoto kubwa katika elimu ya Juu ni uhaba wa Wahadhiri wenye sifa stahiki ili kuendana na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na vyuo vyao. “Nafahamu jitihada ambazo vyuo vikuu binafsi vinafanya katika kuendeleza Rasilimali Watu wao na hasa katika eneo la taaluma ili viwe na Wahadhiri na Maprofesa wa kutosha.”

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito vyuo vingine binafsi nchini viwekeze katika eneo la kuendeleza Rasilimali Watu kwa bidii zaidi na kwa upande wa Serikali, ipo mikakati mbali mbali ya kuajiri lakini pia kusomesha wale waliopo kazini ili kufikia viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa.

Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine inayovikabili vyuo vikuu ni miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kama vile mabweni na nyumba za watumishi, hivyo kusababisha baadhi ya vyuo  kushindwa kukidhi matakwa ya ithibati zao na kuzuiwa kufanya udahili au kufungiwa kabisa.

“Ni kweli tunahitaji Watanzania wengi wapate elimu ya juu kwenye vyuo vyetu vikuu. Hata ninyi wanafunzi, mngependa kupata elimu iliyo bora itakayoweza kuwasaidia maishani na itakayowakomboa kifikra, itakayowapa ujuzi na maarifa ya kupambana na changamoto za maendeleo. Kila mmoja anataka elimu bora na si bora elimu.”

Waziri Mkuu amesema kuwa dhamira hiyo ndiyo inayoifanya Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu kuhakikisha kuwa vyuo vyote visivyokidhi matakwa ya ithibati yao haviendelei kutoa mafunzo ya aina yoyote. “Nitoe rai kwa vyuo vikuu vyote vizingatie matakwa ya ithibati zao ili viweze kutoa elimu iliyo bora itakayokidhi matamanio ya Watanzania na ushindani wa soko la ndani na nje.”

Kuhusu Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania ambacho kimeomba kuruhusiwa kufanya udahili baada ya kufungiwa, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kujiridhisha iwapo chuo hicho kimekidhi vigezo kabla ya kukipa kibali cha kudahili wanafunzi wapya.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Septemba 24

Waziri Dkt.kigwangalla Atembelea Eneo Alilopata Ajali,Atoa Shukrani

$
0
0
Na Andrew Chale, Manyara
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla jana Novemba 23, 2018 ametembealea kituo cha Afya Magugu, pamoja na eneo alilopatia ajali katikati ya Mdori na Minjingu, Mkoani Manyara.

Dkt.Kigwangalla ameweza kutembelea maeneo hayo, hii ni baada ya zaidi ya siku 100 tokea apate ajali hiyo alipokuwa katika majukumu ya kiofisi kutokea Mkoani Arusha kurejea Dodoma.

Akiwa katika kituo hicho cha Afya Magugu, aliweza kuonana na wafanyakazi wakiwemo Madaktari, Waguzi na Wasamalia wema walioshughulika wakati wa tukio la ajali ambapo ametoa shukrani zake kwa namna walivyomsaidia yeye na majeruhi wengine kabla ya kuhamishiwa Arusha na baadae Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Akitoa neno la shukrani, Waziri Dk Hamisi Kigwangalla alisema:

“Ninawashukuru sana ndugu zangu kwa kutuhudumia vizuri siku ya ajali, Mungu alipenda tupatie ajali Karibu ya kituo chenu ili mtuokoe…hatuna cha kuwalipa, zaidi ya maneno Ahsante na kuwaombea dua, Mungu awanusuru na kila shari na awajaze kheir tele katika maisha yenu” alisema Dkt. Kigwangalla wakati wa shukrani zake hizo

Mbali na kutembelea kituo hicho cha Afya Magugu, pia ameweza kutembelea eneo alilopata ajali katikati ya Minjingu na Mdori ambapo pia ameweza kwenda kushuhudia gari alilopatia nalo ajali lililohifadhiwa katika kalakana ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dk Hamisi Kigwangalla  akikagua eneo la nyuma ya gari alilopatia nalo ajali mnamo Agosti 4,mwaka huu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dk Hamisi Kigwangalla  akiangalia kitanda alichopatiwa huduma wakati wa ajali hiyo katika kituo Cha Afya Magugu. Dk. Kigwangalla alipata ajali mnamo Agosti 4,mwaka huu

Serikali Yafafanua Utolewaji Wa Vibali Kwa Ajili Ya Uchimbaji Visima Nchini

$
0
0
Serikali imewatoa hofu wananchi kuhusu utaratibu ulioanzishwa kwa wenye visima kuanza kuvilipia na kueleza kuwa haina nia ya kuwakomoa wananchi bali sheria inawataka kufanya hivyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa, Kitilia Mkumbo, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa masuala ya maji pamoja na visima.

Prof. Mkumbo alikuwa anatoa ufafanuzi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliyetaka kujua ni visima gani hasa ambavyo vinalengwa na serikali.

"Mkoa wangu una visima vingi moja wapo ni hivi ambavyo wananchi wangu wamejichimbia maji nyumbani mita 12 na wengine kwa sababu hatujawafikishia maji asilimia 100 waliona wana uwezo wa kuchimba visima na kuwasambazia wenzao," alisema na kuongeza:

"Sasa juzi nimesikia kauli ambayo kidogo imeleta taharuki na kuna visima zaidi ya 3,000 naomba na hili utupe kauli yako na Sheria inasema nini maana wanaona kama serikali inawatisha," alisema Makonda.

Mkumbo alisema visima hivyo vimegawanywa katika makundi matatu, la kwanza ni la visima ambavyo havihitaji kibali wala mhusika halipii chochote, la pili vinavyohitaji kibali na kulipa wakati cha tatu ni kile cha kiwango cha kufanya biashara kama viwanda.

Alisema wenye viwanda wote wanafahamu taratibu za kumiliki visima, namna ya kutumia maji na wakulima wakubwa kwa kuwa kila mwaka wanaomba vibali lakini changamoto inakuwa katika kundi la kwanza na pili.

Alisema kwa kundi la kwanza kwa mujibu wa sheria, kama mtu anachimba maji nyumbani chini ya mita 15 kwa ajili ya kwa matumizi ya nyumbani na hajaweka miundombinu yoyote, hahitaji kibali wala kulipia.

"Lakini kama utatengeneza mita 15 au zaidi, ukaweka miundombinu kama mashine za kusukuma maji, hapa utahitaji kibali na ukifuata maji zaidi ya mita 15 utalipia ada fulani kutokana na kiwango cha maji. Hizi ndizo taratibu za msingi," alisema.

Mkumbo alisema suala hilo limewekwa hivyo kwa makusudi ili mhusika atumie maji katika hali ambayo haitaathiri watu wengine, atumie katika hali isiyoathiri mazingira na atumie maji hayo katika hali ambayo itawezesha kutumika na vizazi vijavyo.

"Lengo la kufanya hivyo si kumkomoa mwananchi hata kidogo. Serikali inatambua ni lazima upate maji na imeweka utaratibu wa kawaida wa kurahisisha kupata maji," alisema.

Katibu Mkuu alisema kwa bahati mbaya sheria hizo zilikuwa hazifuatwi na kwa sasa wameanza kufuatilia visima ingawa kumekuwa na changamoto.

Alisema wanatoa elimu kwa wananchi ili waelewe hizo taratibu na kuzizingatia na anaamini kwamba watanzania ni watu wanaofuata taratibu baada ya kuzielewa sheria.

"Katika mchakato huu wa kutekeleza sheria hiyo kama kutajitokeza changamoto za kisheria ndio maana kuna Bunge, wananchi watatoa malalamiko yao na Bunge letu watalichukua na kulifanyia kazi lakini kwa sasa utaratibu ndio huo," alisema.

Aidha, Mkumbo alisema maji ni rasilima ya nchi hivyo mtu binafsi hawezi kusema anamiliki maji yake.

Alisema kwa sababu maji ni rasilimia ya taifa ni lazima kuwepo na utaratibu wa kuipata na Rais ndiye aliyekabidhiwa kuisimamia.

"Wapo wananchi na wafanyabiashara wamechimba visima kwa bahati mbaya bado hatujavitambua vyote kwa sababu hatujapata taarifa kutoka kwa wananchi. Tumeagiza maofisa wetu katika mikoa yote kuanza kufanya kazi ya kuvitambua," alisema

Mkumbo alisema Sheria ya mwaka 2009 na 2011 ya rasilimali za maji imeweka taratibu zake kuhusu namna wananchi wanavyoweza kujishughulisha katika kupata maji.

Aidha, alisema wanaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji na ifikapo 2020 wana uhakika wa kupunguza tatizo la maji kwa asilimia kubwa.

Treni Ya Serikali Ilivyotumika Kusafirisha Mizigo ya Magendo

$
0
0
Shehena ya mbao imekamatwa katika stesheni ya Shinyanga ikisafirishwa kimagendo katika treni ya mizigo kutoka mkoani Tabora kuelekea Mwanza.

Shehena hiyo imekamatwa baada ya kuwekwa mtego na wakala wa huduma za misitu wakishirikiana na Jeshi la Polisi.

Akizungumza jana Ijumaa Novemba 23, 2018 ofisa misitu Wilaya ya Kahama mkoani humo, Mohamed Dossa alisema mbao hizo zimekamatwa wakati mabehewa hayo yakiwa katika kituo cha bandari kavu cha Isaka.

Alisema baada ya kupata wasiwasi waliwasiliana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) mkoani humo  pamoja na polisi na kufanikiwa kukamata mabehewa mawili yakiwa na mbao hizo.

Treni hiyo ya mizigo baada ya kukaguliwa  mabehewa mawili yalibainika kuwa na  shehena ya mazao ya misitu ikiwemo mbao, asali na milango.

Alisema vitu hivyo huenda vimevunwa na kusafirishwa kinyume cha sheria,  bila kulipiwa ushuru   wa Serikali.

Alisema kukamatwa kwa mabehewa hayo kulitokana na taarifa zilizotolewa na wasamaria wema wa wakala wa misitu mkoani Tabora na hivyo treni hiyo kuzuiwa baada ya kufika mjini Shinyanga.

“Treni hiyo ya mizigo ilikuwa ikitoka mkoa wa Tabora, walianza kuishtukia katika kituo cha bandari kavu cha Isaka na askari wa TFS aliyejulikana kwa jina la Leonard Maguta alipopanda katika treni hiyo kufuatilia alipigwa na askari waliokuwemo ndani na kushushwa njiani,” alisema Dossa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule akizungumza na waandishi wa habari alisema katika tukio hilo wanawashikilia watu wanne ambao majina yao yamehifadhiwa hadi uchunguzi utakapokamilika.

Alisema mbao zilizokamatwa ni zile ambazo haziruhusiwi kuvunwa mpaka kwa kibali maalumu na zilikuwa zikisafirishwa bila kuwa na kibali.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amewataka watumishi kuwa waadilifu na kuacha kusafirisha vitu haramu ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kuwataka kufuata taratibu na sheria.

“Usafirishaji wa magendo kwa njia ya reli umekithiri sana na mizigo mingi ya aina hiyo imebainika na kukamatwa ambapo amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa wanapoona hali kama hiyo ili kuchukua hatua kabla ya tukio kumalizika kutendeka” alisema mkuu wa wilaya .
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images